Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

MIMI NI MWENYE DHAMBI NISAMEHE MUNGU - 5

 





    Simulizi : Mimi Ni Mwenye Dhambi Nisamehe Mungu

    Sehemu Ya Tano (5)



    Joram na Ignas bado walikuwa wakiendelea kufanya kazi zao za kusafirisha madawa kama kawaida. Katika kipindi hiki biashara ile ilionekana kusafirishwa kwa njia nyingine kabisa, njia ambayo ilianza kuingia miaka hiyo, kusafirisha madawa kwa kutumia maiti. Maiti zilikuwa zikisafirishwa huku tumboni kukiwa na madawa ya kulevya. Usafirishaji ule ulikuwa ni wa kisasa zaidi ambao walikuwa wameugundua na hakukuwa na mtu yeyote ambaye alikuwa akiufahamu.

    Kila walipokuwa nchini Tanzania, Ignas na Joram walikuwa na kazi ya kutafuta maiti na mwisho wa siku kuzisafirisha sehemu husika na huko ndipo ambapo walikuwa wakizipasua maiti zile na kisha kuchukua madawa ambayo yalikuwa yamesafirishwa kwa njia hizo. Ignas na Joram hawakuonekana kuwa na wasiwasi kabisa, kiasi cha fedha ambacho walikuwa wakilipwa walikiona ni kikubwa sana jambo ambalo liliwafanya kufanya kazi ile kwa moyo mkunjufu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mwisho wa Ignas na Joram kusafirisha madawa ilikuwa mwaka 2009, mwaka ambao walikamatwa nchini Thailand na hivyo kusafirishwa mpaka Tanzania na kufungwa jela kwa miaka kumi. Hilo likaonekana kuwa kama pigo kubwa kwa Samuel na Sadiki ambao walikuwa wakiwategemea sana vijana wale ambao walikuwa wamekwishapelekwa gerezani na kutumikia adhabu ya kifungo hicho.

    Samuel na Sadiki hawakutaka kuangaika sana, walichokifanya hapo ni kuanza kusafirhsa madawa wao wenyewe kwa staili ya kumeza vidonge kadhaa mpaka katika nchi husika. Japokuwa ilikuwa ni jambo hatari lakini katika kipindi hicho hawakuonekana kuwa na jinsi, ilikuwa ni lazima wafanye jambo hilo hili biashara ile isiweze kusimama huku wakiendelea kutafuta vijana wengine.

    Kazi ya kusafirisha madawa kuelekea katika nchi mbalimbali kwa njia ya kuyameza ikaonekana kuwa njia rahisi ambayo wala haikuweza kugundulika hata mara moja. Huo ndio ulikuwa mchezo ambao walikuwa wakiucheza, mchezo ambao ulidumu kwa muda wa miezi sita, kipindi ambacho Sadiki akawa na safari ya kutaka kuelekea nchini Ujerumani ndani ya jiji la Munchen kwa ajili ya kupeleka mzigo mkubwa wa madawa ya kulevya ambayo yalikuwa katika kete arobainii ambazo alikuwa amezimeza.

    “Huku nitapiga mpunga mkubwa sana kaka. Nikitoka huko, nitakuwa nimeingiza zaidi ya milioni mia nne” Sadiki alimwambia samuel.

    “Nakutakia kila la Kheri, fanikisha mpango huo. Ukirudi, na mimi nitaelekea Sweden, kuna mzigo nitatakiwa kupeleka huko. Nadhani hata kazi ya kuwaajiri vijana kwa sasa tupunguze wasije wakatufanyia kama tulivyomfanyia Khaled” Samuel alimwambia Sadiki.

    “Hakuna tatizo. Nadhani nikitoka Ujerumani nitaelekea nchini Brazil kuchukua mzigo mwingine na kuupeleka Malyasia na kisha kurudi nchini Tanzania” Sadiki alimwambia Samuel.

    “Hakuna tatizo” Samuel alimwambia sadiki.

    Siku tatu zilizofuata, Sadiki akaanza safari yake ya kuelekea nchini Ujerumani huku tumboni akiwa amemeza kete arobaini ambazo zilikuwa katika mfumo wa vidonge, kete ambazo zilikuwa na madawa ya kulevya ambayo yalitakiwa kufikishwa nchini Ujerumani.

    Ndani ya ndege muda wote Sadiki hakuonekana kuwa na wasiwasi, alikuwa amekwishazoea kumeza kete za madawa ya kulevya na kisha kuzisafirisha barani Ulaya kwa ajili ya kufanya biashara. Hiyo ndio ilikuwa kazi yake, hakutaka kumgawia kijana yeyote kupeleka madawa yale kwa kuamini kwamba vijana wengine wasingeweza kuwa waaminifu kama ambavyo walivyokuwa Ignas na Joram ambao walikuwa gerezani wakati huo.

    Sadiki hakula chakula kigumu kwa kuhofia kuleta matatizo tumboni mwake, matatizo ambayo yangesababisha kete zile kupasuka na hatimae madawa yale ya kulevya kutapakaa tumboni mwake na kufa papo hapo. Chakula cha kikubwa kilikuwa ni biskuti chache sana ambazo alikuwa akinywa na maji ili kusaidia kete zile zisiweze kupasuka tumboni mwake.

    ****

    Mwezi wa kumi na mbili kilikuwa ni kipindi kilichokuwa na baridi kali sana katika nchi za Ulaya kiasi ambacho muda mwingi theluji ilikuwa ikionekana mitaani jambo ambalo lilisababisha theluji ile kufunika barabara nzima na hivyo magari maalumu ya kuondoa theluji kupita katika bharabara nzima ili ziweze kuonekana na magari yaweze kupita.

    Katika kipindi hicho cha baridi ndicho kilikuwa kipindi ambacho ndege ya shirika la ndege la Fly Emirates ilikuwa ikitua katika jiji kubwa la Munich, jiji lililokuwa Kusini mwa nchi ya ujerumani. Katika kipindi chote hicho ndani ya ndege Sadiki hakuonekana kuwa na wasiwasi hata kidogo, alikuwa na uhakika wa kupita salama kama ambavyo alivyokuwa akipita katika sehemu nyingine.

    Baada ya ndege kusimama, abiria wakatakiwa kuteremka na Sadiki pamoja na abiria wengine kufanya hivyo. Koti kubwa lilikuwa mwilini mwake, japokuwa alikuwa akipigwa na baridi lakini wakati mwingine koti lile lilikuwa likimsaidia sana kumkinga na baridi hilo ambalo lilionekana kuwa kali sana katika nchi za Ulaya hasa katika kipindi hicho cha mwezi wa kumi na mbili.

    Mara baada ya mizigo kukaguliwa, akaanza kupiga hatua. Kitendo cha Sadiki kuwaona wanaume saba ambao walikuwa wamevaa suti huku wakiwa na hearphone masikioni mwao na maiki ndogo karibu na midomo yao, Sadiki akaonekana kuwa na wasiwasi, hofu ikaanza kumuingia japokuwa hakujua hofu ile ilikuwa imesababishwa na nini.

    Akaanza kupiga hatua za kujishtukia kuufuata mlango wa kuelekea nje. Huku akiwa amebakiza hatua ishirini kabla ya kuufikia mlango, akashangaa kumuona mwanaume mmoja ambaye alivaa suti akimfuata na kisha kumsimamisha. Sadiki akaonekana kuhofia kupita kawaida, mwanaume yule alionekana kugundua kitu fulani, alichokifanya mara baada ya kuona Sadiki kasimama, hapo hapo akawaita wenzake wawili na kisha kumchukua Sadiki na kumpeleka katika chumba kimoja kilichokuwa maalumu kwa kufanyia mahojiano na wasafiri ambao walikuwa wakionekana kuwa si watu wa kawaida.

    Ndani ya chumba kile kulikuwa na meza moja ambayo wala haikuwa na viti vingi huku juu ya meza ile kukiwa na televisheni pamoja na deki na pembeni kukiwa na baadhi ya mikanda. Kitu walichokifanya watu wale ni kumuondoa wasiwasi Sadiki ambaye wala hakuonekana kuondokewa na wasiwasi ambao alikuwa nao moyoni mwake. Ndani ya chumba kile, akatakiwa kukaa katika kiti kimoja huku wanaume wanne wakikaa katika viti vya tofauti.

    Maswali kibao yakaanza kumiminika kichwani mwa Sadiki juu ya sababu ya watu wale kumhitaji ndani ya chumba kile huku wakionekana kumtilia mashaka kupita kawaida. Alichokifanya Sadiki ni kubaki kimya huku akitaka kuona ni kitu gani kingetokea kwani kila alipokumbuka kwamba sehemu alipoyaweka madawa yasingeweza kuonekana, akajipa imani ya kushinda kila kitu mahali pale.

    “Samahani. Tunaweza kuangalia passpoti yako?” Mwanaume mmoja alimuuliza Sadiki ambaye akaichukua pasipoti yake kutoka kwenye begi na kisha kumpa mwanaume yule aliyeihitaji, akaanza kuiangalia, alipoona amemaliza, akawapa wenzake ambao wakaiangalia na kisha kumwangalia Sadiki usoni huku tayari wakionekana kumtilia mashaka.

    “Umetembea nchi nyingi sana, tena nchi ambazo zimekuwa maarufu katika usafirishaji wa madawa ya kulevya. Wewe ni mmoja wao?” Mwanaume huyo ambaye alijitambulisha kwa jina moja ya Kurt alimuuliza Sadiki.

    “Madawa! Hapana. Mimi ni raia safi kabisa. Sijasafirisha madawa yoyote yale” Sadiki aliwajibu huku akijaribu kuitoa hofu usoni mwake.

    “Sawa. Ila umetembea nchi nyingi sana Sadiki” Kurt alimwambia Sadiki huku akichukua pasipoti ile na kisha kumrudishia.

    “Kawaida tu. Mimi ni mfanyabiashara wa kujitegemea” Sadiki aliwaambia.

    “Ok! Hakuna tatizo. Tumekuelewa. Ningependa kukwambia kitu kimoja” Kurt alimwambia Sadiki.

    “Kitu gani?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Subiri kwanza” Kurt alisema na hapo hapo kuinuka na kutoka ndani ya chumba kile. Wanaume wengine ambao walikuwa ndani ya chumba kile wakaonekana kuwa bize wakipiga stori huku wakitaka kumuonyeshea Sadiki kwamba hawakuwa wakijali sana uwepo wake mahali pale na wakati kwa macho ya wizi walikuwa wakimfuatilia vizuri sana. Kurt alichukua dakika mbili tu, akarudi mahali hapo huku akiwa na jagi lililokuwa na maji pamoja na glasi na kisha kutulia kitini.

    “Haya unayoyaona si maji kama maji bali ni dawa iitwa Methrophesium, dawa maalumu kwa ajili ya kupasua kete za madawa ya kulevya ambayo yapo tumboni mwa mtu yeyote” Kurt alimwambia Sadiki maneno ambayo yalionekana kumshtua kupita kawaida na kisha kuendelea.

    “Subiri kwanza” Kurt alimwambia Sadiki na kisha kuchukua rimoti na kuiwasha televisheni ile ambayo ilikuwa mezani na kisha kuweka mkanda mmoja katika deki.

    “Huu mkanda utakaouona ni wa watu ambao tuliwashuku kuwa wana madawa tumboni na kisha kuwaambia wanywe maji haya yenye dawa hiyo. Kwa hapa ngoja nikwambie kitu kimoja. Kama kweli hauna kete za madawa ya kulevya tumboni mwako, maji haya yenye dawa hayatokuwa na madhara yoyote yale ila kama una madawa tumboni, kete zitakwenda kupasuka na hatimae madawa kumwagika tumboni mwako na kufa huku ukijiona” Kurt alimwambia Sadiki ambaye alionekana kuwa na wasiwasi mwingi.

    “Kuna watu walikuwa na madawa ya kulevya ila wakasema hawana, wakanywa na matokeo yake ndani ya sekunde kumi baada ya maji kugusa kete zile, zikapasuka na hatimae madawa kumwagika tumboni na kufa ila kuna wengine ambao walisema hawana, na kweli wakanywa, hakukuwa na kilichotokea na hivyo kuwalipa dola mia tano kwa kila mmoja kutokana na usumbufu ambao waliupata kutoka kwetu. Ngoja nikuonyeshee video kidogo” Kurt alimwambia Sadiki maneno mengi na kisha kumuwekea video ile.

    Sadiki akayatuliza macho yake katika televisheni ile na kuwaona watu wakiwa katika chumba kile kile huku wakifanya mahojiano na mwisho wa siku kupewa glasi moja ya maji yale na kunywa. Kuna wengine walikuwa wakitoka salama lakini kulikuwa na wengine ambao walionekana kuangaika huku wakiyashika matumbo yao na hatimae kufa kwa maumivu makali.

    “Hao ni baadhi ya watu. Ukinywa maji haya na kuwa mzima, basi tutakulipa dola mia tano kama usumbufu ila kama ukisema hauna, na ukanywa kisha kufa, hiyo utakuwa umejiua kwa uzembe wako. Chaguo ni lako” Kurt alimwambia Sadiki huku akiyamimina maji katika glasi na kisha kumuwekea glasi ile ya maji Sadiki.

    Muda wote Sadiki alikuwa akitetemeka tu, kijasho chembamba kikaanza kumtoka kwa kuona kwamba siku hiyo alikuwa amepatikana. Alibaki kwa dakika kadhaa huku akiiangalia glasi ile iliyokuwa na maji. Kila alipokuwa akiyapeleka macho yake katika televisheni ile, watu wengi walionekana kufa mara baada ya kuyanywa maji yale, watu ambao walikuwa na madawa ya kulevya tumboni mwao.

    Bila kupenda na bila kushinikizwa, Sadiki akaamua kuiweka mikono yake juu ya meza katika staili iliyoonyesha kwamba alikuwa tayari kufungwa pingu lakini si kuyanywa maji yale, hiyo ilimaanisha kwamba alikuwa na madawa ya kulevya tumboni mwake.

    “Uamuzi mzuri” Kurt alimwambia sadiki na kisha kumfunga pingu.

    Katika safari zaidi ya hamsini ambazo alikuwa amezifanya katika nchi mbalimbali safari hiyo ndio ambayo ilionekana kuwa mbaya sana kwake, hakuamini kwamba kwa mafanikio makubwa ambayo alikuwa ameyapata siku hiyo alikuwa amekamatwa kilaini sana jambo ambalo alijua fika kwamba kulikuwa na mtu ambaye aliwambia polisi wale kwa ajili ya kumkamata, alijua fika kwamba mtu huyo alikuwa mzee Bill Brug, mzee wa kijerumani ambaye alikuwa akifanya nae biashara ile lakini mara kwa mara alikuwa na wasiwasi nae.



    Katika kipindi ambacho alikuwa amekamatwa Sadiki akaanza kujutia kile ambacho alikuwa akikifanya, kuuza madawa ya kulevya. Moyo wake uliumia kupita kawaida kila alipokuwa akiyakumbuka maneno ya baba yake, mzee Hamidu ambaye kila siku alikuwa akimtaka kumrudia Mungu. Utajiri mkubwa ambao alikuwa nao katika kipindi hicho akauona ukianza kupotea kwa kuamini kwamba ilikuwa ni lazima afungwe jela miaka kadhaa nchini Ujerumani.

    Kutokana na tetesi ambazo zilikuwa zikisikika jijini Munich kwamba kulikuwa na Mtanzania ambaye alikamatwa na madawa ya kulevya, balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Emmanuel Kihampa ikambidi kuingilia kati kwa kutaka mtuhumiwa asafirishwe mpaka nchini Tanzania kwa ajili ya kuhukumiwa kwa kosa la usafirishaji wa madawa ya kulevya ambao alikuwa amelifanya.

    Haikuwa kazi nyepesi hata mara moja, ilichukua takribani wiki tatu na ndipo kila kitu kilipokamilika na hivyo Sadiki kuanza kurudishwa nchini Tanzania kwa ajili ya kuhukumiwa kwa kile alichokuwa amekifanya. Ndani ya ndege, alionekana kutia huruma, pingu zilikuwa zimefunga mikoni yake huku maneno ya baba yake ambayo yalikuwa yakimtaka kumrudia Mungu yakiwa yanajirudia kichwani mwake.

    “Hii laana. Maneno ya baba ndio yamesababisha nikamatwe” Sadiki alijisemea katika kipindi ambacho safari ya kurudi nchini Tanzania ikiendelea kama kawaida.

    “Bora niachane na kazi hii kwa sasa” Sadiki alijisemea huku akionekana kumaanisha kile alichokuwa akikisema.

    Hicho ndicho kilikuwa kipindi maalumu cha kuyakumbuka maneno ya busara ambayo walikuwa wakiyaongea wazazi wake na kisha kuyapuuzia. Katika kipindi hicho alikuwa akikumbuka kila neno ambalo wazazi wake walikuwa wakimwambia katika kipindi cha nyuma. Alijuta, moyo wake ulijuta kupita kiasi kutokana na kile ambacho kilikuwa kimetokea huku akiona kwamba kulikuwa na kila sababu za kuachana na biashara ile ya madawa ya kulevya.

    Mpaka katika kipindi hicho alikuwa amechelewa mno, kama kuachana na biashara ile alitakiwa kuachana nayo toka katika kipindi cha nyuma lakini si katika kipindi hicho kwani tayari alikuwa amekamatwa na ilikuwa ni lazima afikishwe mahakamani na kuhukumiwa.

    Nchini Tanzania Samuel hakutulia, mara baada ya kupata taarifa kwamba rafiki yake ambaye alimchukulia kama ndugu yake, Sadiki alikuwa amekamatwa alionekana kuchanganyikiwa. Kitu cha kwanza ambacho alikifanya ni kuanza kuwasiliana na watu waliokuwa na vyeo vikubwa ambao alikuwa akishirikiana nao katika uuzaji wa madawa ya kulevya na kuwataka wafanye kila linalowezekana kuhakikisha kwamba Sadiki anatoka na kuwa huru tena.

    “Itawezekana ila ina mlolongo mrefu sana” Bwana Marko alimwambia Samuel.

    “Inaweza kuchukua muda gani mpaka kukamilika?” Samuel alimuuliza.

    “Kama mwezi mzima tena hapo tukiwa tumetoa kiasi kikubwa cha fedha” Bwana Marko alimwambia Samuel.

    “Kuhusu fedha si tatizo, ishu iliyokuwepo ni yeye kuwa uraiani kwa mara nyingine tena” Samuel alimwambia Bwana Marko.

    “Hakuna tatizo. Ila siku nyingine msijali kusafirisha madawa kwenda Ujerumani”

    “Kwa nini?”

    “Kule ni nuksi sana, watu wa kule hawatupendi watu wenye ngozi nyeusi na ndio maana huwa hatuendi kufanya biashara kule, sijui imekuwaje mpaka Sadiki kwenda kule” Bwana Marko alimwambia Samuel.

    “Cha kwanza tuhakikishe huyu mtu anakuwa huru na hayo mengine yatafuata” Samuel alimwambia Bwana Marko.

    Mishemishe zao zikaanza mahali hapo, Samuel hakuweza kutulia, alikuwa akiangaika huku na kule ili tu akamilishe kile ambacho kilitakiwa kukamilishwa muda huo. Bwana Marko alikuwa pamoja nae katika kila hatua ambayo alikuwa akiifanya kuhakikisha kwamba Sadiki anaachiwa huru. Kazi haikuwa nyepesi hata mara moja kutokana na polisi kulishikilia sana suala lake.

    “Kazi itafanyika. Mna milioni sabini?” Mwanaume mmoja alimuuliza Bwana Marko na Samuel.

    “Fedha si tatizo”

    “Basi niachieni mimi. Nyie nendeni nyumbani kanyweni kahawa tu” Mwanaume yule alimwambia.

    Hapo ndipo kazi ilipoanza, mwanaume yule ambaye hakutaka kujitambulisha jina lake akaingia kazini. Japokuwa kazi kwa wengine ilionekana kuwa kubwa lakini kwake kazi ile ikaonekana kuwa nyepesi sana na ndani ya wiki tatu tu kila kitu kilikuwa tayari na Sadiki kuwa huru kwa masharti mawili tu, asikae ndani ya nyumba yake mpaka miezi sita itakapokwisha na pia asisafiri kwenda nchi yoyote ya Ulaya mpaka miezi hiyo itimie kitu ambacho wala hakikuonekana kuwa tatizo kwake.

    “Nashukuru kwa kila kitu. Nilikuwa napotea hivi hivi” Sadiki aliwaambia Samuel na Bwana Marko.

    “Kuwa makini siku nyingine” Samuel alimwambia Sadiki.

    “Na kitu kingine ni kwamba usijaribu kwenda Ujerumani, kule utapotezwa” Bwana Marko alimwambia Sadiki.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nafikiri huu ulikuwa ni mpango ambao ulipangwa. Sirudi kule tena” Sadiki aliwaambia.

    Muda wa majuto ukaonekana kupotea tena. Katika kipindi ambacho alikuwa amekamatwa alitamanai kubadilika na kuwa mtu wa dini kutokana na kipindi cha matatizo ambacho alikuwa nacho lakini kwa wakati huo ambao alikuwa ameachiwa huru, akaonekana kusahau kila kitu. Hakurudi nyumbani kwake, kitu ambacho aliambiwa akifanye ndicho alikitekeleza. Hakwenda kuishi hotelini, akaamua kuishi pamoja na Samuel ndani ya nyumba ya Samuel.

    Ndani ya nyumba kubwa wakawa wakiishi watu watatu, Samuel, Catherine na Sadiki tu. Tabia yake ya kuchukua wanawake haikuisha, kila siku Sadiki alikuwa mtu wa kubadilisha wanawake kama nguo kitu ambacho kilimkasirisha sana Samuel lakini hakuwa na la kufanya kwani kama kuongea nae alifanya hivyo mara nyingi sana lakini hakukuwa na mabadiliko yoyote yale.

    Leo alikuwa akiingia na wanawake wa vyuo, kesho alikuwa akiingia na wafanyakazi na kesho wahudumu wa bar. Sadiki hakutaka kuelewa hata mara moja, alionekana kama mtu ambaye alikuwa akitafuta kitu fulani kutoka kwa wanawake kwani mara baada ya kumpa Zubeda, msichana wa kitanga, Sadiki akatulia, hakutaka tena wanawake.

    Hiyo ikaonekana kuwa nafuu sana, mchezo wake wa kuchukua wanawake ukaonekana kuanza kuisha kabisa. Samuel hakujua Zubeda alikuwa akimfanya nini Sadiki mpaka kutulia namna ile, hiyo ilikuwa ni siri ya watu wawili, Sadiki na Zubeda tu.

    “Huyu demu noma kaka” Sadiki alimwambia Samuel.

    “Kivipi?”

    “Kuwa mtoto wa mjini. Nikisema noma najua unajua namaanisha nini” Sadiki alimwambia Samuel na wote kuanza kucheka.

    Hiyo ndio ilikuwa siri ambayo alikuwa nayo Zubeda. Kitandani alikuwa mtundu kupita kawaida kitendo ambacho kilionekana kumchanganya sana Sadiki. Mapenzi motomoto ambayo alikuwa akipewa na Zubeda ndio ambayo yakamfanya kuwasahau wanawake wengine. Zubeda alikuwa akiujua vilivyo mchezo ule kiasi ambacho akili ya Sadiki ikaonekana kuchanganyikiwa kupita kawaida.

    Ni kweli alikuwa ametembea na wanawake wengi katika maisha yake lakini kwa msichana Zubeda akaonekana kuchanganyikiwa kupita kawaida. Kitandani, Zubeda alikuwa na uwezo wa kila kitu, alikuwa akiweza kukipeleka kiuno chake huku na kukipeleka kule, alipokuwa akitulia, Sadiki alikuwa akihema juu juu kana kwamba alikuwa akitaka kukata roho. Huyo ndiye alikuwa Zubeda, msichana kutoka Tanga barabara ya tisa,msichana ambaye alikuwa akijua hasa kucheza na mwanaume kitandani.

    “Umejifunzia wapi mchezo huu?” Sadiki alimuuliza Zubeda.

    “Kwa nini umeuliza?”

    “Hapana aisee. Yaani kama una mota kiunoni” Sadiki alimwambia Zubeda.

    “Usijali. Nilifundishwa sana nyumbani” Zubeda alimwambia Sadiki.

    “Kuna siku utaniua, haiwezekani uwe unakwenda huku na kule kama nyigu” Sadiki alimwambia Zubeda.

    Hayo ndio yalikuwa maisha yao, kila siku walikuwa wakifanya ngono tu kitu ambacho kiliwafanya kujiona kama walikuwa katika ulimwengu mwingine, ulimwengu ambao uliwafanya kuwa huru kabisa. Sadiki akaonekana kuridhika, hakuwa na haja ya kuwatafuta wanawake wengine na wakati Zubeda alikuwa amejitosheleza kwa kila kitu.

    Hiyo ikaonekana kuwa nafuu kwa Samuel, zile mishemishe za wanawake kuingia na kutoka zikawa zimekwisha kwani tayari Sadiki alikuwa amempata mwanamke ambaye alikuwa akimridhisha kwa kila kitu. Japokuwa alikuwa akimuona Zubeda kuwa mwanamke mzuri aliyekuwa na uwezo wa kila kitu lakini nyuma ya pazia Zubeda hakuwa msichana mzuri, alikuwa ni msichana ambaye alivaa sura ya bandia.

    Kwa Sadiki, akaonekana kupata lakini ukweli ni kwamba alikuwa amepatwa kwani maisha ya nyuma ya pazia ambayo alikuwa akiishi Zubeda yalikuwa ni balaa, hayo maisha ndio ambayo yalimfanya Zubeda kubadilika kwani afya yake haikuwa sawa, alikuwa ameathirika na kitu ambacho alikuwa akikifanya ni kuusambaza ugonjwa wa UKIMWI kwa wanaume waliokuwa na fedha tu akiwepo Sadiki kwa kuamini kwamba kupitia watu hao, wanawake wengi wangeteketea kama ilivyokuwa kwake.

    ****

    Samuel hakutaka kuachana na biashara zake, mara kwa mara alikuwa akitoka na kuelekea katika nchi nyingine kwa ajili ya kuuza madawa ya kulevya ambayo bado yalikuwa yakimuingizia fedha kupita kawaida. Kila kitu ambacho kilikuwa kikiendelea Catherine hakuwa akikifahamu japokuwa mara kwa mara mpenzi wake huyo alikuwa akimuaga kwamba alikuwa akisafiri kuelekea nje ya nchi.

    Mapenzi yao hayakupungua, kila siku walikuwa wakizidi kupendana kupita kawaida. Catherine hakutaka kuwaambia wazazi wake kwamba aliamua kuwa na Samuel, mwanaume wake ambaye alimtoa usichana katika kipindi ambacho walikuwa shuleni Kilimanjaro. Mapenzi yao yakaonekana kuwa siri kwa wazazi wao, hawakutaka wazazi hao wafahamu kile ambacho kilikuwa kikiendelea kwao.

    Muda mwingi ambao Samuel alikuwa nchini Tanzania walikuwa pamoja huku wakiyaurahia maisha yao kama kawaida. Catherine hakuonekana kuambiwa chochote kwa mapenzi ambayo alikuwa nayo kwa Samuel, alikuwa akimpenda kupita kawaida. Akamtambulisha Samuel kwa marafiki zake, Catherine bado alionekana kuwa mwanamke aliyekuwa na bahati kwa kumpata mwanaume ambaye alikuwa na fedha nyingi katika maisha yake.

    Wivu wa wanawake bado ulikuwa ukiendelea, kila siku walikuwa wakimuonea wivu Catherine ambaye wala hakuonekana kujali. Catherine akapewa gari la kutembelea huku akaunti yake ya benki ikijazwa pesa jambo ambalo liliendelea kuyafanya mapenzi yake juu ya Samuel kuzidi kuongezeka zaidi na zaidi.

    Katika kipindi ambacho Samuel aliamua kuelekea nchini Australia kwa ajili ya kupeleka mzigo wa madawa ya kulevya, hali nyumbani ikaonekana kubadilika. Sadiki ambaye alikuwa pamoja na Zubeda akaonekana kuanza kuingiwa na tamaa hasa mara baada ya kumuona Catherine akiwa amevaa kanga moja tu na kuja sebuleni katika kipindi ambacho ulikuwa ni usiku wa saa tano.

    Sadiki akabaki akimwangalia Catherine kwa macho ya matamanio, ni kweli kwamba alikuwa akimfahamu vilivyo Catherine lakini kitendo cha kumuona akiwa amevaa kanga moja kukaonekana kumpagawisha kupita kawaida. Catherine alionekana kuumbika kupita kawaida, hipsi zake zilikuwa tofauti na jinsi ambavyo Sadiki alivyokuwa akifikiria kabla. Kitendo cha kumuona Catherine akiwa na kanga moja tayari kikaanza kutengeneza kitu fulani moyoni mwake.

    Tamaa ikamuingia na kuuhisi mwili wake kuwa na hamu ya kufanya mapenzi na Catherine. Sadiki hakuonekana kujali kwamba angeonekana vipi kwa Samuel kitu ambacho alikuwa akikitaka ni kufanya ngono na Catherine tu. Kuhusu wasichana, Sadiki hakuonekana kuwa na wasiwasi nao kabisa, alijua fika kwamba hata kama msichana alikuwa akimpenda mwanaume wake kwa kiasi gani lakini kuna mambo ambayo kama ungefanikiwa kumfanyia basi ungeweza kumteka na kisha kufanikisha lengo lako.

    Huo ndio ulikuwa udhaifu wa wanawake ambao ulikuwa ukijulikana moyoni mwake. Alijua fika kwamba kama angekaza basi ilikuwa ni lazima kutembea na Catherine katika kipindi hicho ambacho Samuel alikuwa nchini Australia. Sadiki hakuonekana kuujali urafiki wake uliokuwa kama ndugu baina yake na Samuel, tamaa ambayo ilikuwa imemuingia ilikuwa imebadilisha kila kitu moyoni mwake na kumsahaulisha ukaribu ambao alikuwa nao na Samuel.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hakujua ni kipi kingetokea endapo angemwambia Catherine na kisha mwanamke huyo kukataa na kumwambia Samuel katika kipindi ambacho angerudi nchini Tanzania. Sadiki akaupiga moyo konde, kitu ambacho alikuwa akikitaka ni kufanya mapenzi na Catherine tu kwani tayari akili yake ilikuwa imekwishachanganyikiwa.

    Katika kipindi ambacho Catherine alikuwa akikaa na kanga moja sebuleni Sadiki alionekana kubadilika, kila wakati alikuwa akimwangalia Catherine ambaye alichukulia kila kitu kawaida sana. Sadiki alikuwa na kazi kubwa ya kubadilisha mikao, mara akae hivi, mara akunje nne, yaani kila mkao ambao alikuwa akikaa aliuona kutokufaa.

    Tabia ile ya Catherine kuvaa kanga moja na kuja sebuleni iliendelea zaidi na zaidi huku kila siku Sadiki akionekana kuumia kupita kawaida. Kila alipokuwa akikaa sebuleni hakuonekana kuwa huru, suruali yake maeneo ya zipu ilikuwa ikija mbele kana kwamba zipu ilitaka kutobolewa. Maisha yakawa kama mateso, alipokuwa akilala chumbani kichwa chake kilikuwa kikimfikia Catherine tu huku wakati mwingine akitamani kumfuata chumbani na kulala nae.

    “Hatuwezi kwenda kuangalia muvi leo” Sadiki alimwambia Catherine ambaye alikuwa sebuleni hapo, kama kawaida alikuwa na kanga moja.

    “Hapana. Leo najisikia nimechoka sana” Catherine alimwambia Sadiki.

    “Sawa. Usijali. Na vipi kuhusu pombe. Hatuwezi kwenda kununua pombe?” Sadiki alimuuliza Catherine.

    “Usiku wote huu?”

    “Ndio kwanza saa tano. Kwanza hatutakiwi kuhofia kwa sababu tuna usafiri wa kuturahisishia” Sadiki alimwambia Catherine.

    “Ngoja nikavae” Catherine alimwambia Sadiki.

    “Hakuna noma” Sadiki alimuitikia.

    Tayari akili yake ikazidi kufikiria ngono, kitu ambacho alikuwa akikitaka mahali hapo ni kwenda kununua pombe, amnyweshe sana Catherine na kisha kufanya nae mapenzi. Mpango wake huo ukaonekana kufaa sana. Baada ya dakika kadhaa, Catherine akatoka chumbani huku akiwa amevaa sketi fupi ambayo iliyaacha mapaja yake wazi. Kwa nguo ile tu tayari ikaonekana kumpagawisha Sadiki.

    “Umependeza sana” Sadiki alimwambia Catherine ambaye akaanza kujiangalia.

    “Asante” Catherine alimwambia Sadiki na kisha kuanza kutoka mpaka katika eneo lililokuwa na magari na kisha kuingia ndani ya Prado na kuondoka mahali hapo.

    Kichwa cha Sadiki katika kipindi hicho kilikuwa kikifikiria ngono tu. Kila alipokuwa akiyaangalia mapaja ya Caterine pake ndani ya gari alionekana kuchanganyikiwa kupita kawaida. Akili yake haikutulia, mawazo yake yakaanza kumuonyeshea akiwa chumbani pamoja na Catherine, akaanza kumvua nguo na kisha kuanza kufanya nae mapenzi.

    “Simuachi leo. Hata kama urafiki na Samuel bora ufe tu” Sadiki alijisemea kila alipokuwa akiyaangalia mapaja ya Catherine kiwizi..

    Ndani ya dakika kumi gari likasimama nje ya duka moja la pombe kali lililokuwa Mwenge na kisha kuteremka. Sadiki akaanza kuangalia ndani ya duka lile, chupa nyingi zilizokuwa na pombe kali zilikuwepo mahali hapo. Sadiki akachukua zile pombe ambazo aliziamini kwamba zilikuwa kali sana na kisha kuondoka mahali hapo.

    Lengo lake ambalo alikuwa amelipanga lilikuwa ni kumlewesha sana Catherine na mwisho wa siku afanye nae mapenzi bila kipingamizi chochote kile. Kwa kuwa alielewa kwamba Catherine alikuwa mtu wa pombe sana, hakuona kama kulikuwa na dalili za mwanaumke huyo kukataa kunywa pombe.

    Walipofika nyumbani moja kwa moja Sadiki akalisimamisha gari na kulipaki, akamfungulia Catherine mlango na kisha kuelekea ndani huku wakiwa wameshika mfuko ambao ulikuwa na pombe kali. Walipofika ndani, moja kwa moja wakazifungua na kuanza kuzinywa huku wakipiga stori za hapa na pale.

    Sadiki alikuwa ametuliza kichwa chake kwa wakati huo, hakuwa akinywa mara kwa mara kama ambavyo Catherine alivyokuwa akinywa pombe zile. Alipoona kwamba ukimya ulikuwa haufai mahali hapo, akasimama na kisha kuwasha muziki. Ni ndani ya dakika thelathini tu pombe zikaonekana kuanza kumchukua Catherine, akasimama na kisha kuanza kucheza muziki huku akiwa anayumbayumba kama kwamba angeweza kuanguka muda wowote ule.

    Sadiki hakutaka kumuacha peke yake, nae akasimama na kisha kuanza kucheza nae huku Catherine akiendelea kunywa pombe. Kichwa cha Catherine hakikuwa na uwezo wa kuhimili pombe zilizokuwa na ulevi mkubwa namna ile, pombe ambazo alikuwa akizipenda zilikuwa ni Kilimanjaro tu na ndio maana ndani ya muda mchache alikuwa hoi.

    Catherine akaonekana kuchoka, akajilalia juu ya kochi huku hata chupa ambayo alikuwa ameishika ikiwa pembeni yake, pombe ilionekana kumchukua kupita kawaida. Hiyo hali ndio ambayo Sadiki alikuwa akitaka kuiona, akamsogelea Catherine mahali pale na kisha kuanza kumuasha. Catherine alikuwa aking’ang’ania kuachwa mahali pale, alichokifanya Sadiki ni kumbeba na kisha kumpeleka chumbani.

    “Kiulainiiiiiii najilia mambo” Sadiki alisema katika kipindi ambacho alimlaza Catherine kitandani.

    Catherine alikuwa amelala chali, miguu ameitanua na hivyo kuyafanya mapaja yake kuwa wazi. Uchu wa kufanya ngono ukazidi kumpata Sadiki, akaona kwamba lilikuwa ni kosa la jinai kumuacha Catherine mahali hapo bila kufanya nae ngono, alichokifanya ni kuanza kumchojoa nguo zake, Catherine hakuwa na kipingamizi kwani pombe zilikuwa zimemchukua sana.

    Siku hiyo ndio ilikuwa siku ya kwanza kwa Sadiki kufanya mapenzi na Catherine. Hata Catherine alipoamka asubuhi na kujikuta yupo chumbani kwa Sadiki akajua kwamba Sadiki alikuwa amefanya nae mapenzi kutokana na kutokuwa hata na nguo moja mwilini mwake. Catherine akaonekana kukasirika, akasimama kitandani pale na kisha kuanza kuvaa nguo zake huku akimwangalia Sadiki kwa hasira kitandani pale.

    “Sadiki....Sadiki....” Catherine alimwambisha Sadiki ambaye akaamka huku nae akiwa mtupu.

    “Ndio umenifanya nini?” Catherine aliuliza huku akionekana kuwa na hasira.

    “Samahani Catherine. Tulilewa sana na ndio maana kitu hiki kilitokea” Sadiki alimwambia Catherine.

    “Kwa hiyo umenibaka?”

    “Hapana”

    “Kumbe umefanyaje?”

    “Ni pombe zilituchukua sana” Sadiki alimwambia Catherine ambaye akatoka chumbani hapo kwa hasira.

    Hapo ndipo ambapo Sadiki akaanza kujutia kile ambacho alikuwa amekifanya kwa Catherine, moyo wake ukanyong’onyea na hatimae kuanza kuufikiria ukaribu ambao alikuwa nao na Samuel, akajiona kuwa msaliti mkubwa katika maisha yake. Hakutaka kuendelea kubaki katika hali hiyo, akatoka chumbani kwake na kisha kuanza kumfuata Catherine chumbani kwake, alipoufikia mlango akaufungua na kisha kuingia ndani.

    Catherine alikuwa amekaa kitandani akilia, kitendo ambacho alikuwa amefanyiwa na Sadiki kilionekana kumuumiza kupita kawaida, machozi yalikuwa yakitiririka shavuni kwake. Akilini mwake alikuwa akimfikiria mpenzi wake, Samuel ambaye alikuwa amesafiri kuelekea nchini Australia.

    Sadiki akaanza kupiga hatua, alipokifikia kitanda nae akakaa kitandani na kisha kumsogelea Catherine na kisha kumvutia kwake na kisha kumkumbatia. Sadiki akatumia nafasi hiyo kumuomba msamaha Catherine ambaye alionekana kuwa kwenye majonzi makubwa.

    “Naomba unisamehe” Sadiki alimwambia Catherine ambaye bado alikuwa akiendelea kulia tu.

    “Naomba unisamehe Catherine” Sadiki alimuomba msamaha Catherine kwa mara nyingine tena.

    Sadiki hakujua ni kitu gani kilichokuwa kikiendelea mwilini mwake, kwa sababu Catherine alikuwa bado amevaa kisketi chake kifupi huku kifuani akiwa na sidiria tu, akauhisi mwili wake ukianza kushikwa na hisia za kutaka kufanya mapenzi. Sadiki alijitahidi kwa nguvu zote kuzizuia hisia hizo lakini akajikuta akishindwa kabisa hali iliyompelekea kuanza kuyashikashika mapaja ya Catherine.

    Catherine hakuwa na ujanja tena, hakuonekana kuwa mgumu kwani hata kama angejifanya kuwa mgumu tayari alikuwa amekwishatembea na Sadiki, tayari alikuwa amekwisauona mwili wake wote. Catherine akajikuta akijifuta machozi, Sadiki alipousogeza mdomo wake, wakajikuta wakianza kubadilishana mate na kisha kuanza kufanya ngono kwa mara nyingine tena.

    Usaliti ukaendelea kama kawaida, mchezo ule ukaonekana kushamiri ndani ya nyumba ile. Kila siku wakawa watu wa kufanya ngono tu jambo ambalo liliwafanya kuwa huru kupita kawaida. Hapo ndipo ambapo Sadiki akaamua kuachana na Zubeda bila kuwa na sababu yoyote ile. Japokuwa Zubeda alikuwa ameumia sana lakini wala hakuwa na wasiwasi kwani lengo lake tayari alikuwa amelikamilisha, kumuambukiza UKIMWI Sadiki.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Siku Samuel akija kujua....” Catherine alimwambia Sadiki huku akiwa amemuegemea kifuani.

    “Uzuri ni kwamba hakuna atakayemwambia, kwa hiyo hatoweza kujua” Sadiki alimwambia Catherine.

    “Hahah! Yeah! Tuombe Mungu asije kujua kwani akijua itakuwa ni balaa mpenzi” Sadiki alimwambia Samuel.

    “Niamini, hatokuja kujua” Sadiki alimwambia Catherine na kisha kukumbatiana, kilichofuata, kama kawaida yao, wakaanza kufanya ngono tena.





    Nchini Australia Samuel hakuonekana kuwa na furaha hata mara moja, muda mwingi alikuwa akimfikiria mpenzi wake Catherine ambaye alikuwa amemuacha nchini Tanzania. Katika safari hii, Samuel hakuonekana kuwa na amani kabisa, muda mwingi alikuwa akionekana kuwa mnyonge kupita kawaida kiasi ambacho alijua kwamba kulikuwa na tatizo sehemu.
    Wasiwasi ukaanza kumkamata kwamba ingewezekana kuwa nae alikuwa akienda kukamatwa katika kipindi hiki kutokana na madawa ya kulevya ambayo alitakiwa kuyasafirisha kuelekea katika nchi nyingine za barani Asia. Mara kwa mara Samuel alikuwa akiongea na mpenzi wake, Catherine simuni, alikuwa akimpenda sana na kumhitaji na ndio maana kila alipokuwa akielekea ilikuwa ni lazima aongee nae na kumjulia hali.
    Moyoni mwake bado alionekana kuwa tofauti kabisa, hakujua sababu ambayo ilimfanya kuwa namna ile, ni kweli kila siku mapenzi yake yalikuwa juu ya mpenzi wake lakini katika kipindi hicho akaonekana kuwa na wasiwasi kupita kawaida.
    Samuel alikaa nchini Australia kwa siku sita na ndipo alipoelekea nchini Thailand na kisha Mongolia na kurudi nchini Tanzania. Samuel alirudi huku akiwa ameingiza zaidi ya milioni mia tano kwa safari zake ambazo alikuwa amezifanya za kwenda katika nchi hizo kwa ajili ya kusafirisha madawa ya kulevya tu.
    Utajiri wake haukukoma, kila siku alikuwa akiendelea kuingiza fedha kiasi ambacho mpaka yeye mwenyewe alikuwa akijishangaa. Fedha hazikukoma, alijiona kama mtu ambaye alimiliki kisima kikubwa cha mafuta na hivyo alitakiwa kuingiza fedha kila siku katika maisha yake. 
    Alipofika nchini Tanzania akaonekana kuwa na amani, kitendo cha kumuona mpenzi wake kwa mara nyingine kilionekana kumpa furaha kupita kawaida. Kila alipokuwa akikaa nae, alikuwa akimmwagia mabusu mfululizo. Samuel hakuonekana kufahamu kitu chochote kile ambacho kilikuwa kikiedelea kwa wakati huo, kwake, aliamini kwamba Catherine alikuwa msichana muaminifu ambaye alikuwa akilitunza penzi lake katika kipindi ambacho alikuwa safarini.
    Wote wawili walikuwa wakimuonyeshea unafiki mbele yake jambo ambalo linamfanya Samuel kutokufahamu kitu chochote kabisa, upofu mkubwa ukatawala machoni mwake, uaminifu mkubwa ambao alikuwa amemuwekea Catherine ulikuwa ni kazi bure kwani Sadiki alikuwa amekwishatembea nae na hivyo kumwambukiza ugonjwa wa UKIMWI.
    Ndani ya nyumba hiyo walikuwa wakipokezana kufanya mapenzi na Catherine. Katika kipindi ambacho Samuel hakuwepo nyumbani hapo, Sadiki alikuwa huru kufanya mapenzi na Catherine huku milango ikiwa imefungwa. Katika kipindi ambacho Samuel alikuwa akirudi nyumbani, alikuwa akilala nae chumbani kama kawaida. 
    Maisha hayo yaliendelea kila siku mpaka kufikia kipindi ambacho Sadiki akaona kwamba ilitosha na hivyo alitaka kuondoka mahali hapo kwani kwa jinsi hali ilivyokuwa ikienda aliona kwamba Samuel alikuwa njiani kugundua kila kitu ambacho kilikuwa kikiendelea kwao.
    “Kwa nini unataka kuondoka mahali hapa?” Samuel alimuuliza Sadiki.
    “Maamuzi, nimekaa sana hapa”
    “Sasa unataka kwenda wapi? Nyumbani kwa wazazi wako uanze kwenda msikitini?” Samuel alimuuliza Sadiki.
    “Hapana. Nataka kwenda kuishi hotelini” Sadiki alimwambia samuel.
    “Hapana Sadiki. Mbona unakuwa hivi? Kuna nini ndani ya nyumba yangu mpaka unataka kuondoka kwenda kujiingizia gharama zisizokuwa na msingi?” Samuel alimuuliza Sadiki.
    “Basi tu. Wakati mwingine najiona kutamani kubadilisha mazingira” 
    “Au shemeji yako kaanza chokochoko? Manake wanawake nao wakati mwingine wanakuwa wajinga sana” Samuel alimuuliza Sadiki.
    “Hapana. Shemeji yupo peace sana ila nadhani natakiwa kubadilisha mazingira” Sadiki alimwambia Samuel.
    Samuel hakuwa na jinsi, alichokifanya ni kukubaliana na Sadiki kwamba alikuwa akitaka kuondoka nyumbani hapo na kwenda kuishi sehemu nyingine tena. Alichokifanya Samuel ni kumchukua na kisha kuelekea nae katika hoteli ya New Africa iliyokuwa Posta na maisha yake kuanza huko.
    Hiyo ikaonekana kuwa njia nyingine nzuri ambayo ilimfanya Sadiki kutanua sana na Catherine. Mara kwa mara Catherine aliposema kwamba alikuwa akienda chuoni wala hakuwa akifika huko na matokeo yake kwenda katika hoteli ya Kilimanjaro ambapo Sadiki alikuwa akitoka katika hoteli ya New Africa na kisha kukutana huko na kufanya mapenzi.
    Hiyo ndio ilikuwa tabia ya Catherine, maisha yale yaliendelea zaidi na zaidi huku Samuel akiwa hafahamu kitu chochote kile kilichokuwa kikiendelea nyuma ya pazia. Kwake, kila siku aliona kwamba Catherine alikuwa na mapenzi ya dhati na wala hakuwa radhi kumtilia mashaka kwa kumuona kwamba alikuwa akitembea na mwanaume mwingine.
    “Naona leo umekuja hotelini. Kuna demu mpya nini upo nae?” Ilikuwa ni meseji iliyotoka kwa rafiki yake, Issa, meseji iliyoingia katika kipindi ambacho alikuwa akitaka kuelekea bafuni kuoga.
    Samuel akaiangalia meseji ile mara mbili mbili, akataka kuijibu lakini akaona kama angechelewa, alichokifanya ni kumpigia simu Issa ambaye akaipokea na kisha kuanza kuongea huku Issa akionekana kuwa na furaha.
    “Unasema nimekuja hotelini! Hoteli gani?” Lilikuwa swali la kwanza ambalo aliuliza Samuel katika kipindi ambacho simu ilipokelewa na Issa.
    “Ninaliona gari lako hapa nje ya hoteli ya Kilimanjaro, nikafikiri upo ndani. Au uliliuza?” Issa alimwambia Samuel na kisha kumuuliza.
    “Gari gani?”
    “Ile Prado yako ya bluu” Issa alimjibu.
    “Ile gari nilimpa mpenzi wangu na anaitumia kwa sasa” 
    “Kwa hiyo ndio umekuja nae hotelini?”
    “Hoteli gani? Mimi mbona nipo nyumbani na sijatoka toka asubuhi”
    “Mbona naliona gari lako hapa”
    “Gari gani?”
    “Hiyo Prado”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    “Mmmh! Nadhani umeichanganya kwani Catherine yupo chuoni kwa sasa” Samuel alimwambia issa.
    “Mmmh! Ila ni gari lako bwana”
    “Hebu angalia namba zake”
    “Nimeziona. Ni T 2674 TUN. Au sio zenyewe” Issa alisikika.
    Samuel akaonekana kushtuka, ni kweli maneno aliyoyaongea Issa yakaonekana kuwa na ukweli, namba za gari ambazo alikuwa amezitaja zilikuwa ni namba za gari lake ambalo alikuwa amempaka Catherine. Hapo ndipo maswali mengi yakaanza kumiminika kichwani kwake juu ya sababu iliyomfanya Catherine kuwa katika hoteli hiyo na wakati ulikuwa ni muda ambao alitakiwa kuwa chuoni.
    Japokuwa alikuwa akitaka kuoga, akaamua kuahirisha na kisha kuvaa nguo zake na kuondoka chumbani. Moja kwa moja akalifuata gari lake na kuondoka mahali hapo. Akili yake ikawa imechanganyikiwa, kila alipojaribu kujiuliza swali, hakuwa na jibu lolote lile. Tayari akahisi kwamba kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea kwa wakati huo, alitaka kuwahi hapo hotelini hata kabla Catherine hakuondoka kwani kitu ambacho alikuwa akitaka kukifahamu ni kuona Catherine alikuwa na nani katika hoteli hiyo.
    “Kwanza ngoja nimpitie Sadiki niende nae, na kama tukimkuta na mwanaume, atanitambua” Samuel alisema huku akiwa amekwishafika Jangwani, alikuwa akiendesha gari kwa mwendo wa kasi kuelekea katika hoteli ya Kilimanjro iliyokuwa Posta.
    Bado Samuel alionekana kama kuchanganyikiwa juu ya kile ambacho alikuwa ameambiwa na rafiki yake, Issa. Hakuamini kama kweli msichana wake, Catherine angeweza kwenda katika hoteli ya Kilimanjaro na wakati alimuaga vizuri kwamba alikuwa akielekea chuoni. Kadri ambavyo Samuel alivyokuwa akimfikiria Catherine na ndivyo ambavyo alishikwa na hasira zaidi na zaidi kiasi ambacho akaona kweli msichana hakutakiwa kuwekewa dhamana hata mara moja.
    Ndani ya dakika kadhaa Samuel akawa amekwishafika ndani ya eneo la hoteli ya New Africa ambapo akateremka na kisha kuanza kuelekea ndani. Kwa wakati huo mwendo wake ulikuwa ni wa haraka haraka, hakutaka kwenda katika hoteli ya Kilimanjaro akiwa peke yake, alikuwa akitaka kwenda na swahiba wake, Sadiki ili aweze kumfumania vizuri Catherine huku shahidi akiwepo pembeni.
    Alipofika mapokezi, akamuulizia Sadiki, mhudumu wa pale mapokezini akamwambia kwamba mtu huyo alikuwa ametoka kama dakika arobaini zilizopita. Samuel akaonekana kuchanganyikiwa, tayari shahidi hakuwepo, alichokifanya ni kuchukua simu yake na kisha kuanza kumpigia. Simu ya Sadiki haikuwa ikipatikana kabisa jambo ambalo lilionekana kumtia hasira zaidi.
    Alichokifanya Samuel ni kuondoka mahali hapo na kuelekea katika hoteli ya Kilimanjaro. Kichwa chake hakikuweza kufikiria kwamba Sadiki ndiye ambaye alikuwa amesababisha Catherine kuwa ndani ya hoteli ile. Samuel hakuacha kumtafuta Sadiki simuni, alikuwa akiendelea kumtafuta zaidi na zaidi lakini majibu yalikuwa ni yale yale, simu haikupatikana.
    Samuel hakutaka kwenda kuliegesha gari lake katika eneo la hoteli ya Kilimanjaro kwa kuona kwamba Catherine angeweza kuliona na kulijua, alichokifanya ni kwenda kuliegesha nyuma ya hoteli ile na kisha kuingia ndani ya eneo la hoteli ile. Kitu cha kwanza alichokifanya ni kuanza kuangalia ndani ya eneo la kuegeshea magari ndani ya hoteli ile, macho yake yakatua katika gari aina ya Prado ambayo alikuwa amemnunulia mpenzi wake kama zawadi.
    “Upo wapi?” Samuel alimuuliza Issa simuni.
    “Huku kwenye hiki kimghahawa” Sauti ya Issa ilisikika hali iliyomfanya samuel kukata simu na kuelekea huko ambapo akamkuta Issa akimsubiria.
    “Umeliona?” Issa alimuuliza samuel.
    “Nimeliona ila yeye mwenyewe simuoni” Samuel alimwambia Issa.
    “Umemtafuta simuni?” Issa alimuuliza.
    “Hapana. Tena umeongea jambo la maana sana. Ngoja nimcheki” Samuel alimwambia Issa na kisha kuchukua simu yake na kumpigia.
    Simu ya Catherine ikaanza kuita. Kwanza iliita sana mpaka ikakata. Samuel hakuishia hapo, akarudia kupiga tena, simu ile ikaita na baada ya muda fulani simu kupokelewa na sauti nyembamba ya Catherine kusikika simuni.
    “Halllow mpenzi” Sauti ya Catherine ilisikika.
    “Hallow baby! Upo wapi?” Samuel alimuuliza Catherine kwa sauti ya upole, hakutaka kumuonyeshea kwamba alikuwa na wasiwasi.
    “Nipo chuo”
    “Utatoka saa ngapi?”
    “Mmmh! Bado sijajua. Nafikiri mpaka saa kumi na mbili jioni” Sauti ya Catherine ilisikika.
    “Sawa. Hakuna tatizo. Ukimaliza hakikisha unakuja mpenzi. Nimekwishakumiss mpaka nahisi kufa” Samuel alimwambia Catherine.
    “Usijali” Catherine alimwambia Samuel ambaye akakata simu.
    Samuel akaonekana kuvimba kwa hasira, hakuamini kama kweli mpenzi wake, Catherine alikuwa amefikia hatua ya kumdanganya namna ile. Akapiga ngumi mezani huku akionekna kuwa na hasira zaidi kiasi ambacho mpaka mishipa ikaanza kumsimama.
    “Nikimkuta na mwanaume. Namuua” Samuel alimwambia Issa.
    “Ngoja kwanza. Punguza hasira” Issa alimwambia Samuel.
    “Nakwambiaje Issa, huyu malaya nitamuua. Nitamuua” Samuel alimwambia Issa.
    “Ngoja tusubirie tuone nini kitatokea. Inawezekana kaja kunywa mara moja au kuonana na marafiki zake” Issa alimwambia Samuel.
    “Haiwezekani. Atakuwa na mwanaume tu. Atakuwa na mwanaume tu huyu malaya” Samuel alimwambia Issa huku akionekana kuwa na hasira zaidi.
    Samuel na Issa wakaendelea kusubiri mahali pale. Kuanzia saa nane mchana mpaka saa kumi na moja bado Catherine hakuonekana kutokea mahali hapo. Ilipofika saa 12:05, Catherine akaonekana akitoka ndani ya hoteli ile, Samuel akasimama na kisha kuanza kumwangalia, alikuwa ndiye yeye. 
    “Ngoja nimfuate” Samuel alimwambia Issa. 
    “Hapana. Ngoja kwanza” Issa alimwambia Samuel hali ambayo ilimfanya Samuel kutulia.
    Walimuona Catherine akiingia ndani ya gari lake na kisha kuanza kuondoka mahali hapo. Samuel akashikwa na hasira zaidi, akawa katika hali ya kutaka kufanya mauaji tu kwa wakati huo. Kitendo cha Catherine kutoka ndani ya hoteli ile kilimuonyesha kabisa kwamba alikuwa na mwanaume ndani.
    Issa bado alikuwa akimsisitiza Samuel kuendelea kusubiri na wala hakutakiwa kuchukua uamuzi wa haraka mpaka pale ambapo angefanikiwa kumjua mtu ambaye alikuwa nae ndani ya hoteli ile. Wala hazikupita dakika nyingi, Sadiki akaonekana akitoka ndani ya hoteli ile. Kwanza Samuel hakuonekana kuamini kile ambacho alikuwa akikiona, akaangalia vizuri, alikuwa Sadiki.
    Hapo ndipo ambapo picha ikaanza kumjia kichwani kwake, akaonekana kugundua kwamba Sadiki aliomba kuondoka ndani ya nyumba yake kwa kuwa alikuwa akihitaji muda zaidi wa kuendelea kutanua na msichana huyo kwani kama angeendelea kuwepo ndani ya nyumba ile wala asingeweza kupata uhuru.
    Samuel hakuishia hapo, aliendelea kufikiria mambo mengi hata juu ya wasiwasi ambao alikuwa nao mara kwa mara alipokuwa nchini Australia juu ya mpenzi wake, Samuel alionekana kukasirika kupita kawaida.
    “Sadiki anatembea na Catherine.....Sadiki anatembea na Catherine! Nitawaua!” Samuel alisema huku akionekana kutokuamini.
    “Subiri kwanza Samuel. Hautakiwi kuwa na haraka ya kufanya maamuzi” Issa alimwambia samuel.
    “Haiwezekani. Ni LAZIMA NIWAUE” Samuel alimwambia Issa huku akionekana kuwa na hasira.
    “Sasa ukichukulia uamuzi wa haraka hautoweza kufanikiwa. Pata ushahidi kwanza”
    “Ushahidi gani ambao wewe unataka mimi niupate zaidi ya huu? Unataka nipate ushahidi gani tena Issa?” Samuel alimuuliza issa.
    Samuel hakutaka kuendelea kubaki mahali hapo, alichokifanya ni kuondoka huku akiwa na hasira kupita kawaida. Chuki ikaonekana kuanza kuchipukia moyoni mwake, alimchukia Sadiki na kumchukia Catherine pia. Upendo wote ambao alikuwa nao juu ya watu hao ukaonekana kupungua na mwisho wa siku kupotea kabisa. 
    Samuel akaingia ndani ya gari lake, kichwa chake kilikuwa kimechanganyikiwa kupita kawaida. Hakuonekana kuamini kile ambacho alikuwa amekiona hotelini. Hakuamini kama urafiki wake pamoja na Sadiki, urafiki mkubwa ambao ulianzia shuleni ungeweza kuleta yale, hakuamini kama urafiki ule ungeishia kwa yeye kuwa na hasira na Sadiki na kutaka kumuua.
    Samuel akaondoka moja kwa moja mpaka nyumbani kwake na kisha kutulia chumbani. Akajilaza kitandani, machozi yakaanza kumtoka. Moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makali mno, wakati mwingine alijiona kuwa katika njozi na baada ya muda angeamka lakini ukweli ni kwamba ile haikuwa njozi bali tukio halisi ambalo lilikuwa limetokea katika maisha halisi.
    Katika kipindi hicho ndipo ambapo mawazo yake yalipomrudisha nyuma kabisa katika kipindi ambacho alikuwa shuleni, kipindi ambacho alikuwa na urafiki mkubwa na Sadiki, siku ambazo alikuwa na uhusiano wa mapenzi na msichana Catherine ambaye alimfanya kumuacha Mungu na kuingia katika maisha ya kumtumikia shetani.
    Katika kila kitu ambacho alikuwa akikifikiria mahali hapo kilionekana kumuumiza kupita kawaida, hakuamini kama matokeo ya urafiki wake na Sadiki, uhusiano wake na Catherine ungeishia namna ile. Samuel akaonekana kujuta, akajutia sababu ambazo zilimpelekea kuanzisha mahusiano na Catherine. Ukiachana na hilo, alijutia uamuzi wake wa kuachana na Mungu na wakati alikuwa na nafasi kubwa ya kubadilisha maisha yake. 
    Huku akiendelea kuwa katika lindi la mawazo, mara simu yake ikaanza kuita, alipoichukua na kuangalia namba, alikuwa Catherine. Kwanza hasira zilizidi kumkamata zaidi na zaidi, hakuamini kama Catherine angeweza kumpigia simu katika kipindi kama hicho. Kitendo cha kuliona jina lake tu kikamfanya kukumbuka kila kitu kilichotokea hotelini. Alichokifanya Samuel ni kujaribu kuzishusha hasira zake na kisha kuipokea.
    “Upo nyumbani mpenzi?” Sauti ya Catherine ilisikika.
    “Yeah! Umekwishatoka darasani?”
    “Ndio. Leo tulikuwa tumebanwa sana na ndio maana nimechelewa kidogo kutoka. Ila usijali, nakuja” Catherine alimwambia Samuel.
    “Usijali. Karibu sana laazizi” Samuel alimwambia Catherine na kisha kukata simu.
    Samuel akaonekana kukasirika zaidi na zaidi, hasira ambazo alikuwa nazo zikaongezeka maradufu, hakuamini kama Catherine alikuwa akimwambia maneno ya uongo na wakati ukweli wote alikuwa akiufahamu. Alichokifanya Samuel ni kuchukua bunduki yake iliyokuwa kabatini na kisha kuanza kuiangalia.
    Siku hiyo hakutaka kuchelewa wala kujiuliza, kitu ambacho alikuwa ameamua ni kumuua Catherine tu. Alitaka kuanza kumuua yeye na mwisho wa yote kuanza upya na Sadiki. Maumivu ambayo alikuwa nayo katika kipindi hicho yakamfanya kuwa na kiu ya kutaka kuua tu, hakutaka kumuacha Catherine aendelee kuishi na wakati alikuwa amemfanyia upuuzi wa kutembea na rafiki yake kipenzi, Sadiki.
    Ndani ya dakika thelathini, Catherine akafika ndani ya nyumba hiyo. Kwa kitendo cha Samuel kumuona Catherine ndani ya nyumba yake akaonekana kupandwa na hasira zaidi lakini hakutaka kumuonyeshea dhahiri kwamba alikuwa amekasirika. Alichokifanya ni kumfuata Catherine na kisha kumkumbatia.
    Ni kweli moyoni mwake alikuwa na hasira sana lakini ili apate kumuua vizuri Catherine hakutaka kuonyesha hasira zozote zile zaidi ya kumfanyia unafiki wa kumuonyeshea mapenzi ya dhati. Unafiki ambao alikuwa akimuonyeshea Catherine ukamfanya kutokugundua kile ambacho kilikuwa kikiendelea moyoni mwake.
    “Ni lazima nikuue” Samuel alikuwa akijisemea kila alipokuwa akimwangalia Catherine ambaye hakuwa akifahamu kitu chochote kile.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Kama kawaida yake Catherine akaingia jikoni kwa lengo la kupika chakula cha usiku lakini Samuel akamkataza, hakutaka apike chakula chochote kile kitu ambacho kilionekana kuwa kigeni kwake.
    “Vipi tena?” Catherine alimuuliza Samuel.
    “Leo nataka tukale nje ya nyumba hii. Unapenda twende wapi?” Samuel alimuuliza Catherine huku akimsogelea na kisha kumkumbatia kwa nyuma huku mabusu mfululizo yakimtoka mdomoni mwake.
    “Popote mpenzi”
    “Chagua mpenzi”
    “Popote pale. Utakapopapenda wewe basi na mimi nitapapenda” Catherine alimwambia samuel.
    Katika kipindi chote hicho uso wa Samuel ulikuwa ukionekana kujawa na tabasamu pana alakini moyo wake ulikuwa tofauti sana. Moyo ulikuwa na maumivu makali sana, kila alipokuwa akimwangalia Catherine alionekana kukasirika kupita kawaida. Alikuwa na kila sababu za kumuua msichana huyo ambaye alionekana kuwa msaliti mkubwa sana katika maisha yake ya mahusiano.
    Japokuwa kwa asilimia mia moja alikuwa akitaka kumuua msichana huyo lakini kwa upande mwingine moyo wake ulikuwa ukimkataza kufanya jambo lile kwa sababu lilikuwa na madhara makubwa zaidi. Japokuwa upande huo ulikuwa ukimpa ushauri mzuri lakini kwake ukaonekana kuwa ushauri mbaya sana ambao wala haukutakiwa kufuatwa.
    “Kama upo tayari twende” Catherine alimwambia Samuel.
    “Nisubiri” Samuel alimwambia Catherine na kisha kuelekea chumbani.
    Alipofika chumbani, Samuel akakaa kitandani kwa muda, mawazo yakaanza kumjaa tena kichwani mwake, pande mbili moyoni mwake zikaonekana kushindana kwa wakati huo, Upande mmoja ulikuwa ukimtaka kumuua Catherine siku hiyo lakini upande mwingine wa moyo wake ulikuwa ukimkataza kufanya hivyo. Samuel akaonekana kupuuzia, alichokifanya ni kuchukua bunduki yake ambayo ilikuwa katika kdroo cha kabati lake na kisha kuondoka chumbani hapo.
    “Hapana. Hebu ngoja” Samuel alisema mara baada ya kufungua mlango wa chumbani kwake kwa nia ya kutoka, akarudi tena.
    “Kumuua kwa risasi noma. Ngoja nimuue kwa sumu” Samuel alijisemea.
    Akarudi tena kitandani na kisha kufungua kidroo kile na kisha kutoa sumu aina ya Smothropheum, sumu kali ambayo ilikuwa ikitumika kuulia wadudu, sumu ambayo haikutakiwa kuguswa kwa mikono. Alichokifanya Samuel ni kuitoboa chupa ile na kisha kuimimina sumu ile katika kichupa kidogo, akakifunga na kisha kukiweka mfukoni.
    Huo ndio uamuzi ambao aliuwa ameuchukua katika kipindi hicho, kumuua Catherine kwa sumu ile kali ambayo aliamini kwamba isingemchukua hata dakika kumi kupumua. Alipoona kwamba tayari ilikuwa katika kichupa kile, akatoka chumbani mule na kuelekea sebuleni.Catherine alikuwa sebuleni hapo, uso wake ulionekana kuwa na tabasamu kubwa kila alipokuwa akimwangalia Samuel ambaye nae alikuwa akimrudishia tabasamu pana ambalo lilificha hali ambayo alikuwa nayo moyoni mwake.
    “Kama kunywa ngoja tuanze kunywa hapa nyumbani. Kule ni kwenda kula tu” Samuel alimwambia Catherine na kumtaka kuelekea jikoni kwa ajili ya kuchukua glasi. 
    Kitendo cha Catherine kuondoka sebuleni pale na kuelekea chumbani kilionekana kuwa kosa kubwa sana kwani hapo ndipo Samuel alipopata mwanya wa kuweza kuimiminia sumu ile katika chupa moja ya pombe ambayo alitaka kumpa Catherine anywe. Mpaka Catherine anarudi sebuleni pale, tayari Samuel alikuwa amekwishafanya kile ambacho alikuwa akitaka kukifanya.
    Unafiki haukumuisha usoni mwake, bado alikuwa akiendelea kutoa tabasamu mbele ya Catherine ambaye alionekana kutokuwa na wasiwasi wowote ule. Alichokifanya Samuel ni kummiminia Catherine pombe iliyokuwa katika chupa ile na kisha yeye kuchukua chupa nyingine ambayo ilikuwa na pombe nyingine.
    “Mbona hautaki kunywa pombe hii?” Catherine alimuuliza Samuel mara baada ya kuona anamimina pombe kutoka katika chupa nyingine.
    “Hii yako nikinywa silewi. Hiyo kwa ajili ya wanawake kama nyie” Samuel alimwambia Catherine huku akimimina pombe ile katika glasi ile.
    Catherine hakujua ni kitu gani kilichokuwa kikiendelea, kitu ambacho alikuwa akikifikiria ni kwamba bado Samuel alikuwa na mapenzi nae na bado alikuwa akiendelea kumuamini kama zamani na wakati mtu huyo kwa wakati huo alikuwa amebadilika kabisa, mapenzi ambayo alikuwa nayo juu yake yalikuwa yamekwishapotea kabisa ndani ya muda mchache kabisa. Catherine akanywa pombe ile.
    “Bora ufe, haya ndio malipo yako malaya mkubwa” Samuel alijisemea moyoni huku akimwangalia Catherine ambaye alikuwa akinywa pombe ile.
    Wala haukuchukua muda mrefu, Catherine akaanza kusikia kizunguzungu, akalishika tumbo lake na kulalamikia maumivu makali. Katika kipindi ambacho Cathereine alikuwa akilalamika kwa maumivu makali huku akimuomba msaada Samuel, ndio kwanza Samuel alikuwa amekaa katika kochi jingine, kakunja nne huku akiendelea kunywa pombe.
    “Nisaidie mpenzi.....tumbo linaumaaaa....nakufa mpenziiiii.....” Catherine alilalamika kwa maumivu makali huku akijaribu kumsogelea Samuel kochini pale.
    “Wewe kufa tu. Kila nafsi itaonja mauti” Samuel alimwambia Catherine.
    “Nisaidieeeeeee....” Catherine alimwambia Samuel kwa maumivu makali lakini hakuonekana kujali kabisa zaidi ya kuendelea kunywa pombe yake.
    “Nani akusaidie malaya mkubwa wewe. Hivi haukujua unacheza na mtu wa aina gani? Wewe kufa tu, yaani hapa wala sijuti kukupoteza mpumbavu mkubwa wewe” Samuel alimwambia Catherine huku akimtoa mkono ambao alikuwa amemshika pajani. 
    Catherine alikuwa akiendelea kulia kwa maumivu makali, mwili wake ukakosa nguvu na kisha kulala chali chini. Mapovu yaliyochanganyikana na damu yakaanza kutoka mdomoni huku akikipandisha kifua chake juu na chini na baada ya sekunde kadhaa kutulia tuli, alikuwa amekwishakata roho.
    Samuel akaonekana kuridhika, tayari mtu ambaye alikuwa akitaka kumuua akawa amekwishamuua. Alichokifanya ni kusimama na kisha kumuwekea kidole Catherine puani kuona kama alikuwa akipumua, hakuwa akipumua. Huku akiwa amesimama na kujifikiria nini alitakiwa kukifanya, ghafla akashtukia honi ikipigwa getini. Kwanza akasimama na kisha kuangalia getini kupitia dirishani, mlinzi akafungua geti na kisha gari kuingia, alipoliangalia, lilikuwa gari la Sadiki.
    Samuel hakuonekana kuamini kama alikuwa amerahisishiwa kazi namna ile, alichokifanya ni kuelekea chumbani kwake na kisha kuchukua bunduki yake, akaiweka kiunoni na kisha kurudi sebuleni. Kitu ambacho alikuwa akikitaka mahali hapo kilikuwa ni kumuua Sadiki tu kwani kazi ya kumuua Catherine ilikuwa imekwishafanyika na alikuwa amebakia Sadiki tu.
    Samuel akasikia mlango wa gari ukifungwa na baada ya muda Sadiki kuingia sebuleni hapo. Kitu ambacho alikutana nacho ni mdomo wa bunduki ambayo aliishika Samuel. Sadiki akaonekana kushtuka kupita kawaida, hakuamini kama Samuel alikuwa amemuwekea bunduki bila kujua sababu yoyote ile.
    “Ingia ndani kimya kimya mpuuzi mkubwa” Samuel alimwambia Sadiki ambaye akaanza kuingia ndani huku akionekana kushangaa.
    “Kuna nini tena Samuel? “ Sadiki alimuuliza Samuel ambaye alikuwa nyuma yake huku mdomo wa bunduki ukiwa kichwani mwake.
    “Mungu wangu! Samuel umemuua Catherine?” Sadiki alimuuliza Samuel kwa mshtuko mara baada ya kuuona mwili wa Catherine pale chini.
    “Ndio nimemuua. Na baada ya dakika chache nakuua na wewe pia” Samuel alimwambia Sadiki ambaye akaonekana kuchanganyikiwa na kugundua kwamba Samuel alikuwa amejua kila kilichokuwa kimeendelea nyuma ya pazia.


    Sadiki alikuwa akitoka kwa machale ndani ya hoteli ya Kilimanjaro. Macho yake yalikuwa yakiangalia huku na kule kwani hakutaka mtu yeyote amuone katika kipindi hicho. Kama kufanya mapenzi na Catherine alikuwa amekwishafanya nae sana na wala moyo wake haukuwa na majuto juu ya kumsaliti rafiki yake mkubwa, Samuel.
    Tamaa ya mwili wake juu ya Catherine ilikuwa kubwa sana kiasi ambacho aliona hata kwa namna gani asingeweza kupigana nayo na kuishinda. Kama kumvua sketi Catherine alikuwa amekwishamvua sana na aliamini kwamba angeendelea kumvua hata kama ingetokea siku Samuel angemuona Catherine bado alikuwa na uhakika kwamba angeendelea kumvua sketi msichana huyo.
    Akaondoka hotelini hapo na kuelekea New Africa ambapo moja kwa moja akaelekea katika chumba chake na kutulia. Muda wote Sadiki alionekana kuwa na furaha, hakuamini kama alikuwa na uwezo wa kumshawishi msichana ambaye alikuwa na jamaa yake mwenye pesa na kuwa nae. Kwake yeye, Catherine alionekana kuwa msichana mjinga kwa sababu alikubali kutembea nae na wakati alikuwa akifahamu fika urafiki ambao alikuwa nao kwa Samuel.
    Kitandani pale alikuwa amejiachia huku uso wake ukiwa na tabasamu pana. Alikaa katika hali hiyo kwa dakika kadhaa, akainuka na kisha kuelekea bafuni ambapo akaoga na kisha kurudi chumbani pale. Baada ya hapo, akaiwasha televisheni iliyokuwa chumbani mule na kisha kuanza kuangalia filamu. Sadiki aliangalia filamu ile mpaka saa moja, akapata wazo ambalo kwake likaonekana kufaa sana.
    Akasimama na kisha kuanza kuelekea kabatini, akachukua nguo zake nadhifu na kisha kuzivaa. Kitu ambacho alikuwa akikifikiria mahali hapo kilikuwa ni kumwambia Samuel kwamba walitakiwa waende sehemu kupata chakula usiku huo. Japokuwa alikuwa amemsaliti kwa mpenzi wake lakini Sadiki alikuwa akipenda sana kuwa karibu na rafiki yake huyo ambaye alikuwa akisaidiana nae kwa mambo mengi.
    “Daah! Ila moyo unanisuta sana utafikiri mimi ndiye mtu wa kwanza na wa mwisho kufanya haya” Sadiki alijisemea huku akiwa amekwishavaa nguo zake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Saa moja na dakika ishirini akatoka chumbani mule na kisha kuelekea nje ambapo akachukua gari lake na safari kuelekea Mbezi Beach kuanza. Hakutaka kumpa taarifa Samuel kwa kuona kwamba iwe isiwe ni lazima akubaliane nae na kuelekea sehemu fulani kwa ajili ya kupata chakula cha usiku. Moyo wake bado uliendelea kumsuta kiasi ambacho akaanza kujisikia aibu yeye mwenyewe.
    “Ikitokea siku akajua sijui itakuwaje! Nadhani hata urafiki wenyewe utakwisha siku hiyo hiyo” Sadiki alisema katika kipindi ambacho alikuwa akiendelea na safari yake huku akiwa amekwishafika Mbezi Beach.
    Safari iliendelea zaidi na zaidi mpaka alipofika Africana ambapo akakata kona na kuanza kuingia ndani. Wala hakuchukua muda mrefu akawa amekwishafika katika eneo lililokuwa na nyumba ya Samuel na kisha kupiga honi ambapo mlinzi akatoka, alipoona kwamba lilikuwa gari la Sadiki, akalifungua geti na kuliingiza gari ndani.
    “Kumbe yupo na mke wetu” Sadiki alijisemea mara baada ya kuliona gari la Catherine katika eneo la nyumba ile.
    Sadiki akalipaki gari lile na kisha kuteremka na kuanza kupiga hatua kuelekea ndani. Kwa sababu alikuwa amekwishaizoea sana nyumba ile na kujiona kama kwake, wala hakupiga hodi, alipoufikia mlango, akaufungua na kuingia ndani. Sadiki akaonekana kushtuka kupita kawaida mara baada ya kuingia ndani na uso wake kukutana na mdomo wa bunduki ambayo alikuwa ameishika Samuel.
    “Ingia ndani kimya kimya mpuuzi mkubwa” Samuel alimwambia Sadiki huku akionekana kuwa na hasira. 
    “Kuna nini tena Samuel?” Sadiki alimuuliza samuel huku akiendelea kuwa na mshangao wa kile kilichokuwa kikiendelea kutokea.
    Sadiki hakuwa na jinsi, alionekana kushangaa sana lakini akaamua kufanya kama ambavyo Samuel alivyotaka afanye. Alipopiga hatua mbele zaidi na ndipo macho yake yakatua katika mwili wa Catherine ambaye alikuwa ametokwa na mapovu mdomoni, mapovu ambayo yalikuwa yamechanganyikana na damu.
    “Mungu wangu! Samuel umemuua Catherine!” Sadiki alimuuliza samuel kwa mshtuko.
    “Ndio nimemuua. Na baada ya dakika chache nakuua na wewe pia” Samuel alimwambia sadiki ambaye akabaki akitetemeka tu.
    Samuel akamuamuru Sadiki kukaa kochini, Sadiki akafanya hivyo. Tayari uso wa Samuel ulionekana dhahiri kufahamu kila kilichokuwa kikiendelea, Sadiki alionekana kuchanganyikiwa, tayari alikiona kifo chake kikiwa kimekaribia. Hapo ndipo majuto yalipoanza kumuingia moyoni mwake, hakuamini kama urafiki wake na Samuel leo hii ungekuwa namna hii.
    Samuel alionekana kuwa na hasira zaidi. Muda wote alikuwa akimwangalia Sadiki kwa macho yaliyojaa chuki kubwa, kwa jinsi alivyoonekana, kulikuwa na uwezekano wa kumfyatulia risasi muda wowote ule.
    “Kwa nini umenifanyia haya?” Samuel alimuuliza Sadiki huku wakiwa wamekaa makochi tofauti.
    “Nimefanya nini tena Samuel?” Sadiki aliuliza huku akijua dhahiri Samuel alimaanisha nini.
    “Nisikilize Sadiki. Usitake kunifanya mimi mtoto. Najua unajua kabisa jinsi nilivyo, ninapoamua kuua huwa sijifikirii mara mbili mbili” Samuel alimwambia Sadiki.
    “Samu........”
    “Nadhani tunataniana na haujui kama nipo serious” Samuel alimwambia Sadiki na kisha kuikoki bunduki yake tayari kwa kumfyatulia risasi.
    “No..no usifanye hivyo samuel. Ngoja nikueleze ukweli” Sadiki alimwambia Samuel huku akionekana kuwa na hofu.
    “Ukweli gani unataka niufahamu? Nimekwishajua ukweli, kuna lipi jipya ambalo unataka nilifahamu? Umetembea na Catherine toka nilipokuwa nchini Australia, ukatembea nae ulivyojisikia, sasa unataka kuniambia ukweli upi? Au unataka kuniambia kwamba leo mlikuwa pamoja pale Kilimanjaro Hotel? Sema unataka kuniambia ukweli upi nisioujua?” Samuel alimuuliza sadiki kwa sauti ya juu huku akiwa ameanza kubadilika.
    “Naomba unisamehe Samuel, ni shetani tu ndiye aliyenipitia kufanya haya ila kiukweli kwa jinsi tulivyo sikutakiwa kufanya haya” Sadiki alimwambia Samuel.
    “Sadiki..Sadiki...yaani wewe ndiye wa kunifanyia haya? Urafiki wote tuliokuwa nao, mambo mengi tuliyofanya pamoja leo hii umekwenda kunifanyia haya? Nimekufanya nini Sadiki mpaka umeamua kuniumiza namna hii? Urafiki wetu wote tuliokuwa nao, ukaribu wote tuliokuwa nao umekwenda kunifanyia haya...kweli wewe wa kunifanyia haya Sadiki?” Samuel alimuuliza Sadiki kwa uchungu huku akianza kulia.
    “Naomba unisamehe Samuel” Sadiki alimwambia Samuel huku akianza kupiga magoti.
    “Sadiki, nimeangaika nawe katika mambo mengi mno. Ulipokamatwa nikafanya kila lililowezekana tena kwa kutumia fedha zangu mpaka wewe kuwa huru na wakati ulikuwa unakwenda kupotea. Eti vyote hivyo...yaani vyote hivyo haya ndio malipo yake? Yaani umeamua kunilipa kwa kuniumiza namna hii? Hebu jifikirie hata wazazi wetu wakijua kilichotokea watakuchukuliaje? Au nilifanya makosa kukukaribisha nyumbani kwangu? Au nilifanya makosa kukutoa katika mdomo wa serikali? Hebu niambie nilifanya makosa wapi?” Samuel alimuuliza Sadiki.
    “Naomba unisamehe Samuel”
    “Unafikiri msamaha unaweza kubadilisha kitu chochote kile? Unafikiri msamaha unaweza kunifanya niwe na furaha tena? Hapana Sadiki. Msamaha hautoweza kubadilisha kitu chochote kile, msamaha hautoweza kuniletea furaha wala kunifariji” Samuel alimwambia Sadiki.
    “Naomba unisamehe Samuel. Hapa unavyoniona mimi ni mfu ninayetembea. Nimeathirika Samuel. Naomba unisamehe kwa sababu mimi tayari ni mfu” Sadiki alimwambia Samuel.
    “Unasemaje? Umeathirika?”
    “Ndio Samuel”
    “Kwa hiyo ulitaka na mimi kuniangamiza? Umefanikiwa Sadiki. Hebu niambie, kuna sababu gani ambayo itanifanya mimi nikuache hai, hebu niambie, kuna sababu gani”
    “Wewe ni rafiki yangu Samuel”
    “Hapana. Rafiki yangu wa dhati hawezi kutembea na mpenzi wangu. Niambie kuna sababu gani ya kukuacha hai. Umetembea na mpenzi wangu, umemwambukiza UKIMWI na mimi pia nimeupata, hebu niambie kuna sababu gani ya kukuacha hai mtu kama wewe?” Samuel alimuuliza Sadiki.
    “Naomba unisamehe Samuel” Sadiki alisema huku nae akianza kulia.
    Bado Samuel alikuwa na hasira kupita kawaida. Alijua fika kwamba Sadiki alikuwa amemkasirisha sana lakini kila alipokuwa akimwangalia, kumbukumbu za urafiki wao zikawa zinamjia kichwani mwake, akajikuta akiingiwa na roho ya huruma kitu ambacho hakukitegemea.
    “Nimekuelewa. Nimekusamehe ila nataka ufanye kitu kimoja” Samuel alimwambia Sadiki.
    “kitu gani?”
    “Ondoka na mwili wa mpenzi wako. Uchukue mwili huo uondoke nao. Utakapoondoka nyumbani hapa, usirudi tena. Huu ndio uwe mwanzo na mwisho kukanyaga mahali hapa, na kama iktokea siku umekanyaga hapa, nitakuua” Samuel alimwambia Sadiki.
    “Nimekuelewa”
    “Ukitoka nje, usiondoke na gari lako, tumia gari lake. Umenielewa?” Samuel alimwambia Sadiki.
    “Nimekuelewa” Sadiki alimwambia Samuel.
    Kitu alichokitaka Samuel kifanyike ndicho ambacho kikafanyika kama kuepuka kesi kwake. Sadiki akaubeba mwili wa Catherine na kisha kutoka nao nje na kuupakiza ndani ya gari la Catherine na kuondoka mahali hapo huku akiwa hajui ni kitu alitakiwa kukifanya juu ya mwili ule.
    ****


    Samuel hakuonekana kuwa na furaha hata mara moja, mawazo yalikuwa yamemkamata kupita kawaida, kila alichokuwa akikifikiria kwa wakati huo kilikuwa kikimuumiza kupita kawaida. Kichwa chake kilikuwa kikimfikiria Catherine, alikumbuka mambo mengi ambayo alifanya nae mpaka katika kipindi ambacho alikutana nae kwa mara ya pili, hakuamini kama angeweza kumsaliti kirahisi namna ile na wakati alikuwa akimpa kila kitu alichokuwa akikihitaji.
    Ukiachana na Catherine akaanza kumkumbuka rafiki yake ambaye alimchukulia kama ndugu yake, Sadiki. Moyo wake ukaumia zaidi, kitendo alichokuwa amekifanya Sadiki cha kutembea na msichana wake ambaye alitarajia kuwa mke wake kilimuumiza zaidi. Aliufikiria ukaribu ambao alikuwa nao pamoja na Sadiki, akafikiria mambo mengi ambayo alifanya na Sadiki, akabaki akiwa haamini kama mwisho wa kila kitu ungekuwa namna ile.
    Hapo ndipo alipoanza kujuta, maumivu ambayo alikuwa akiyasikia moyoni mwake yakamfanya kukumbuka katika kipindi ambacho alikuwa akimtumikia Mungu. Katika kipindi kile alikuwa na amani, alikuwa na furaha lakini mara baada ya kuingilia mambo ya kidunia kila kitu kikaonekana kubadilika. 
    Maneno mengi ya nyuma ya wazazi wake yalikuwa yakijirudia kichwani mwake, katika kipindi hicho ndicho ambacho aliyaona maneno yale kuwa ya maana sana tofauti na kipindi kile. Hakujua afanye nini, alijiona kuwa katika wakati mgumu kupita kawaida.
    Samuel akabaki katika hali ya mawazo kwa dakika kadhaa, akasimama na kisha kuanza kuzungukazunguka chumbani kule huku akionekana kuwa na mawazo kupita kawaida. Bunduki yake ilikuwa mkononi mwake huku akionekana kuwa na hasira. Ni kweli kwamba hata Sadiki alikuwa ameuumiza sana moyo wake lakini hakuona kama kulikuwa na sababu ya kumuua mtu huyo kwani walikuwa wametoka mbali na walifanya mambo mengi pamoja.
    Ukiachana na mambo mengi, tayari Samuel akajijua kwamba alikuwa ameathirika na UKIMWI, ugonjwa ambao hakuwa akiupenda hata mara moja kwa sababu haukuwa na dawa hospitalini. Kwa wakati huo alikuwa akijiona mfu, alijua fika kwamba kulikuwa na siku ambayo angekufa kitandani, tena kifo kibaya ambacho kingempa sana mateso.
    “Nisamehe Mungu” Samuel alijikuta akiongea na kisha kutoka nje huku akiwa na bunduki yake mkononi.
    Akamuamuru mlinzi afungue geti na kisha kuondoka na gari lake, katika kipindi hicho, safari ilikuwa ni kuelekea nyumbani kwa wazazi wake. Hakuona kama kulikuwa na sababu ya kuendelea kubaki nyumbani kwake na wakati alikuwa katika hali hiyo ya mawazo, alijiona kuhitaji maneno ya faraja, maneno ambayo aliamini yangeweza kumpa nguvu tena.
    Kutokana na foleni za hapa na pale, Samuel alichukua dakika arobaini mpaka kufika katika mtaa wa nyumbani kwao, Mwenge. Hata kabla ya kwenda katika eneo lililokuwa na nyumba ya wazazi wake, akalisimamisha gari lake na kuuegemea usukani wa gari lake na kisha kuanza kukumbuka mambo mengi ya nyuma.
    Kila kitu alichokuwa akikifikiria mahali hapo kilionekana kumuumiza kupita kawaida. Nyakati za majuto zikafika maishani mwake, alikuwa akijutia kila sababu ambayo ilimfanya kumuacha Mungu na kuishi maisha ya dhambi. Katika kipindi hicho alikuwa akisikia msukumo mkubwa moyoni mwake ukimtaka kutubu juu ya kila kitu kibaya ambacho alikuwa amekifanya, amani ikatoweka moyoni mwake, alijiona kuwa mtu mwenye dhambi kuu ambayo haikuwa ikisamehekea.
    “Nimekuja” Samuel aliwaambia wazazi wake mara baada ya kufika ndani ya nyumba hiyo, uso wake haukuonekana kuwa na amani, alionekana kuwa na wasiwasi sana.
    “Mbona usiku hivi?” Mchungaji Mpelele aliuliza huku akishangaa, Samuel akaangalia saa yake, ilikuwa saa tatu na nusu usiku.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    “Nimemtenda Mungu dhambi” Samuel aliwaambia wazazi wake ambao walikuwa wamekaa kimya.
    “Kuna nini Samuel?” Bi Magreth aliuliza.
    “Nimemtenda Mungu dhambi mama. Nimekuwa nikiyadharau maneno yenu ambayo mmekuwa mkiniambia katika maisha yangu. Nimekuwa nikiishi katika ulimwengu wa dhambi kipindi chote” Samuel aliwaambia wazazi wake na kuanza kulia.
    Hicho ndicho kilikuwa kipindi cha majuto, katika kila chozi ambalo alikuwa akilimwaga mbele ya wazazi wake lilikuwa ni chozi la majuto, chozi ambalo lilisababishwa na mambo mengi ambayo alikuwa ameyafanya katika kipindi cha nyuma.
    “Hebu tueleze kwanza, kuna nini?”
    Hapo ndipo ambapo Samuel akaanza kuelezea kila kitu ambacho kilitokea katika maisha yake ya nyuma toka pale ambapo aliamua kwenda kuishi hosteli pamoja na Sadiki. Historia ya maisha yake ilionekana kumuumiza kila mmoja, Bi Magreth akashindwa kuvumilia, akabaki akilia tu kwani Samuel alionekana kupotea katika ulimwengu wa dhambi.
    “Mungu anaweza kila kitu. Yakupasa kumrudia sasa” Mchungaji Mpelele alimwambia Samuel.
    “Hapana baba. Acha niendelee na maisha yangu” Samuel alimwambia baba yake.
    “Unayafurahia maisha ya huko?”
    “Hapana”
    “Unatamani kubaki huko?”
    “Hapana”
    “Sasa kwa nini usimrudie Mungu?”
    “Ni ngumu baba”
    “Hapana. Si ngumu kama ukiamua kurudi tena” Mchungaji Mpelele alimwambia Samuel.
    Siku hiyo ilikuwa ni siku ya huzuni katia familia hiyo, historia ya maisha ya Samuel ilionekana kuwaumiza kupita kawaida. Mtoto wao ambaye alikuwa amepotea katika maisha ya dhambi akaonekana kupata ugonjwa hatari wa UKIMWI ambao uliendelea kuwa gumzo duniani. Ugonjwa ule ukaonekana kuwa malipo ya kila dhambi ambayo alikuwa ameifanya.
    “Acha niendelee kuishi maisha yangu baba. Dhambi zangu zimekuwa nyingi mno” Samuel alimwambia baba yake huku akisimama na kuanza kuondoka mahali hapo.
    “Sikiliza Samuel. Neno la Mungu linasema kwamba Hata kama damu zetu zitakuwa nyekundu kama bendera, Yeye atazisafisha na kuwa nyeupe kama sufi” Mchungaji Mpelele alimwambia Samuel ambaye alisimama na kisha kuondoka mahali hapo.
    Samuel akaonekana kukata tamaa ya kuendelea kuishi maisha ya kumcha Mungu. Alijua fika kwamba endapo angeokoka na kumrudia Mungu basi biashara yake ya madawa ya kulevya alitakiwa kuachana nayo kwa sababu angekuwa mtu mpya kabisa. Samuel hakuonekana kuwa radhi kuiachia biashara ile ambayo ilikuwa ikimuingizia fedha kila siku, alionekana kuwa bora kufanya jambo lolote lile lakini si kucha kufanya biashara ile ambayo ilimpa fedha ambazo zilimfanya kuwa juu nchini Tanzania.
    “Kama kufa acha nife tu” Samuel alijisemea katika kipindi ambacho alikuwa akiingia ndani ya gari na kuondoka mahali hapo huku ikiwa ni saa tano kasoro usiku.
    ****
    Sadiki alionekana kuwa na wasiwasi, kila alipokuwa akiuangalia mwili wa Catherine alikuwa akiogopa kupita kawaida. Katika kipindi hicho alikiona kichwa chake kutokuwa sawa kabisa, usaliti ambao alikuwa ameufanya kwa rafiki yake ukaonekana kumuumiza kupita kawaida. Japokuwa katika kipindi cha nyuma alikuwa akikiona kila kitu kuwa kawaida lakini katika kipindi hicho alikuwa akiona mambo kumbadilikia.
    Kama ilivyokuwa kwa Samuel, nae Sadiki akaanza kujutia kwa kila kitu ambacho alikuwa amekifanya katika maisha yake. Kwanza akaanza kukumbuka katika kipindi cha nyuma ambacho alikuwa akimtumikia sana Mungu, alipojitoa katika kila siku maishani mwake kuswali kwa kwenda msikitini na muda mwingi akiutumia kusoma Qur-an kitu ambacho kilikuwa kikimpa nguvu kusimama kwa Mungu na kupata nguvu za kupinga dhambi maishani mwake.
    Hakuishia kuyafikiria mambo hayo tu, akaanza kukumbuka katika kipindi ambacho alikuwa akimuona baba yake akisimama mbele ya msikiti na kisha kuswalisha, mawazo yale yalimpa uchungu mkubwa moyoni, alijua fika kwamba baba yake alikuwa na ndoto nyingi za kumtaka yeye kuwa kama alivyokuwa katika maisha ya baadae, alijua fika kwamba baba yake alikuwa akijitahidi kufanya kila liwezekanalo ili aweze kuwa imamu kama ambavyo alivyokuwa lakini ndoto za baba yake zikaonekana kufutika mara baada ya kuangukia katika mapenzi ya Mariamu.
    Mapenzi yakamfanya kumsahau Mungu, mapenzi yakamfanya kucha kabisa kuswali na kwenda msikitini, mapenzi yale yakamfanya kutokusoma kitabu kitakatifu cha Qur-an , mapenzi yakaonekana kumpoteza kabisa maishani mwake. Katika kipindi cha nyuma alikuwa akiona faida nyingi za kumtumikia Mungu, alijua kabisa kwamba moyoni mwake alikuwa na amani tele, moyoni mwake alikuwa huru bila ya kuwa na kifungo chochote kile lakini mara baada ya kuchagua kumtumikia shetani, kila kitu kikaonekana kubadilika, kuanzia mwilini mpaka moyoni.
    Aliishi maisha ya kuteseka, bangi zikaonekana kumsumbua kupita kawaida, bila bangi hakuwa akijisikia amani moyoni mwake, bila kuvuta bangi hakuwa akijisikia kuwa mtu sawa. Kitendo cha kuangukia katika mapenzi ya Mariamu ndicho ambacho kikamfanya mpaka kuupata ugonjwa wa UKIMWI kutoka kwa msichana Zubeda ambaye alikuwa amefanya nae ngono sana, ugonjwa ambao alimwambukiza Catherine na Catherine kumwambukiza Samuel.
    Kila kitu katika kipindi hicho kikawa kimebadilika, uamuzi mmoja wa kumuacha Mungu ukaonekana kumgharimu kupita kawaida. Machozi yalikuwa yakimtoka katika kipindi hicho, alikuwa akitamani sana kuwa na uwezo wa kuzirudisha siku nyuma ili aweze kuyabadilisha maisha yake lakini katika kipindi hicho alionekana kuchelewa mno.
    “Nisamehe Allah!” Sadiki alisema huku akilia.
    Kwa wakati huo alikuwa akielekea katika ufukwe wa Coco huku lengo lake likiwa moja tu, kuutelekeza mwili wa Catherine pamoja na lile gari. Aliona fika kwamba alitakiwa kufanya jambo lile kwani kwa kitendo cha Samuel kumuacha hai kililimfanya kumuona mtu huyo kuuthamini sana urafiki ambao walikuwa nao na ndio maana hakutaka kumuua kama alivyofanya kwa Catherine.
    Alitumia dakika kadhaa mpaka kufika katika ufukwe wa Coco. Alichokifanya ni kuvua fulana aliyokuwa ameivaa na kisha kuanza kufuta alama zote za vidole katika kila sehemu ambayo alikuwa ameishika kwa mikono yake. Alipofuta garini akaanza kuufuta mwili wa Catherine, alipoona ameridhika, akaondoka zake huku akiendelea kulia kama mtoto.
    Kila kitu kikaonekana kubadilika, hatua moja tu ya kuingia katika mahusiano ya kimapenzi na Mariamu ikaonekana kubadilisha kila kitu maishani mwake mpaka kumfikisha katika hali hiyo kwa wakati huo. Moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makali kupita kawaida, kitu ambacho alikuwa akikitaka katika kipindi hicho ni kuwafuata wazazi wake na kuongea nao kwani hakuona kama kulikuwa na sehemu nyingine ambayo angeweza kupata maneno ya Mungu zaidi ya wazazi wake.
    Kutoka Msasani mpaka Magomeni hakukuwa mbali sana, akafika nyumbani kwao na kisha kuingia ndani. Kitendo cha mama yake, Bi Asha kumuona tayari akajua kwamba kulikuwa na kitu ambacho kiliendelea kwa wakati huo. Sadiki hakuonekana kuwa mtu wa kawaida, Bi Aisha hakuzoea kumuona mtoto wake akiwa katika hali ile hata mara moja, alikuwa akilia huku macho yake yakiwa yamevimba sana.
    “Kuna nini?” Bi Aisha alimuuliza huku akionekana kuwa na wasiwasi.
    “Nimekosa mama. Nimemkosea Allah” Sadiki alimwambia mama yake, Bi Asha ambaye akatoka mahali hapo na kuelekea chumbani, akamuita mume wake, Ustaadhi Hamidu na kuja sebuleni hapo. 
    Kitendo cha Sadiki kumuona baba yake, maneno mengi ya hekima kama ambayo alikuwa akiambiwa katika kipindi cha nyuma na baba yake yakaanza kujirudia kichwani mwake kama kanda ya redio. Yalikuwa ni maneno makali ambayo yalikuwa yakimuumiza sana kwa wakati huo, maneno yale yalikuwa yakimfanya kujutia sana kila kitu ambacho alikuwa amekifanya katika maisha yake. Sadiki akapiga magoti na kuanza kuomba msamaha.
    “Tumekwishakusamehe Sadiki, tumekusamehe kwa kila kitu. Ila kuna nini kimetokea?” Ustadhi Hamidu alimuuliza Sadiki huku akimnyanyua, Sadiki akaishika kanzu ya baba yake na kuinuka.
    “Nimemkosea Allah, niliacha kuyafuata maneno ya Mtume Muhammad S.A.W na kufanya mambo ya kishetani” Sadiki alimwaambia baba yake huku akimwangalia usoni na kuendelea kulia zaidi na zaidi.
    Muda wote Sadiki alionekana kuumia kupita kawaida. Maisha yake ambayo alikuwa ameishi mara baada ya kujiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi yakaonekana kuharibu kila kitu na ndio ambayo yalimfanya kuwa katika hali hiyo kipindi hicho. Sadiki alijiona kuwa mkosaji mkubwa katika maisha yake, alichokifanya ni kuanza kuwaambia wazazi wake kila kitu ambacho alikuwa amekifanya toka aondoke nyumbani pale.
    Historia ya maisha yake ya nyuma ikaonekana kumuumiza kila aliyekuwa akiisikia, kila mmoja akawa na huzuni kupita kawaida. Sadiki akaonekana kupitia katika maisha yaliyojaa dhambi, maisha ambayo yalionekana kumuabudu shetani usiku na mchana. Sadiki hakujiona kama alikuwa na nafasi ya kubadilisha kila kitu maishani mwake na kumrudia Mungu.
    “Yakupasa kumrudia Allah” Ustaadhi Hamidu alimwambia mtoto wake.
    “Unafikiri nitaweza baba? Kumbukumbu za maisha yangu ya nyuma zitakuwa zikiniumiza sana” Sadiki alimwambia baba yake.
    “Unaweza. Allah si kama binadamu, unapomkosea na kuamua kumrudia, anakusamehe na kuwa mtu mpya maishani mwako” Ustaadhi Hamidu alimwambia Sadiki.
    “Ila biashara ya madawa ya kulevya itakuwaje?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    “Achana nayo. Hizo ni kazi za ibilisi ambazo amekuwa akikutumikisha bila kujijua. Mrudie Allah nae atakupa biashara nyingi za halali za kufanya” Ustaadhi Hamidu alimwambi Sadiki.
    Kwa Sadiki ikawa tofauti na Samuel. Kwake, kila kitu alikiona kikiwa kimebadilika katika maisha yake. Ni kweli kwamba alikuwa amefanya mambo mengi sana ambayo kwake aliyaona kutokustahili kusamehewa hata mara moja, mambo ambayo yalimuumiza kila mtu ambaye angediriki kumwadithia. Katika kipindi hicho alitaka kurudi tena kwa Mungu wake, alitaka kurudi tena na kuomba msamaha kwa kila alichokuwa amekifanya.
    “Ukiamua kwa moyo mmoja kumtumikia Allah, atakusamehe dhambi zako na kukufanya mpya” Ustadhi Hamidu alimwambia mtoto wake.
    Sadiki akakubali kubadilika, kwa sababu alikuwa amezuiliwa kujihusisha na uuzaji wa madawa ya kulevya kwa miezi sita hilo wala halikuonekana kuwa tatizo, akaamua kuachana na kila kitu kuhusiana na madawa ya kulevya. Akaanza tena kuvaa kanzu kama zamani, akaachana na mambo ya wanawake, akaanza kuswali huku kila siku akilia kila alipokuwa akikumbuka maisha ya nyuma ambayo alikuwa amepitia.
    Sadiki alitamani kuoa lakini kila alipokuwa akikumbuka kwamba alikuwa ameathirika hakuonekana kuwa na nguvu za kutafuta mke wa kuoa. Wazazi wake hawakujua hilo, wao walichokuwa wakifahamu ni kuhusiana na uuzaji wa madawa ya kulevya lakini hakutaka kuwaambia kuhusiana na ugonjwa wa UKIMWI ambao alikuwa ameambukizwa na msichana Zubeda.
    Maisha yake yakawa yamebadilika, biashara ya madawa ya kulevya akawa ameiacha jumla na kushughulikia biashara nyingine ambazo zilikuwa na uhalali katika uso wa binadamu na mbele za Mungu pia. Sadiki akajitahidi kutoa misaada mbalimbali kwa watu waliokuwa na uhitaji wa kifedha au vyakula.
    Huyo ndiye alikuwa Sadiki, akayabadilisha maisha yake kwa ujumla, hakutaka kumkaribisha shetani katika maisha yake, akawa mtu wa kuswali, mtu wa kuhudhuria msikitini na mtu ambaye alitamani sana kuwaambia watu kuhusiana na maisha yake mpaka kufikia kipindi hicho. Japokuwa alikuwa akimtumikia Mungu na kujitoa kwa kuwasaidia watu wengi lakini ukweli ukabaki vile vile kwamba alikuwa ameathirika kwa ugonjwa wa UKIMWI.
    ****
    Watu walionekana kushtushwa na taarifa ambayo ilisema kulikuwa na maiti ya msichana ambayo ilikuwa imetelekezwa katika ufukwe wa Coco huku ikiwa ndani ya gari aina ya Prado. Taarifa zile ziliwashtua watu wengi ndani ya jiji la Dar es Salaam na kadri muda ulivyozidi kwenda taarifa ile ilizidi kuvuma sana.
    Nchi ya Tanzania ikaonekana kuingiwa na mambo ambayo mara nyingi yalikuwa yakisikika katika nchi za Ulaya au Marekani. Wasichana wakaonekana kuwa na hofu kwa kuamini kwamba inawezekana muuaji alikuwa ameamua kuwauwa wanawake katika kipindi hicho.
    Polisi wakafanya kazi yao kama inavyotakiwa kufanywa na kisha mwili kupelekwa Muhimbili. Simu yake ilipotumika kuwapigia marafiki wachache, ikagundulika kwamba hiyo ilikuwa maiti ya Catherine ambapo wazazi wake, Bwana Mushi na Bi Maria wakapigiwa simu na kutakiwa kufika katika kituo cha polisi.
    Hiyo ikaonekana kuwa taarifa mbaya na nzito katika maisha yao, hawakutarajia kupokea taarifa kama hiyo, taarifa ya kifo cha binti yao waliyekuwa wakimpenda sana. Polisi walipochukua maelezo yake, wakamtaka mpenzi wake ambaye alikuwa akijulikana nyumbani, Edmund afike jijini Dar es salaam kwa sababu walikuwa wakitaka kumuuliza maswali kadhaa.
    Katika kipindi ambacho Edmund alipewa taarifa juu ya kifo cha mpenzi wake, Catherine akaanza kulia kama mtoto, hakuamini kwamba msichana ambaye alikuwa akitaka kufunga nae ndoa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja ndiye ambaye alikuwa ameuawa kinyama.
    Alijua fika kwamba uhusiano wake na Catherine haukuwa mzuri lakini hiyo haikuwa sababu ya kumfanya kufikiria kwa Catherine hakuwa mpenzi wake, bado alikuwa akimpenda na kumthamini kama kawaida yake. Ndani ya basi Edmund hakuonekana kuwa na furaha hata kidogo, kifo cha mpenzi wake, Catherine kilikuwa kimegusa kupita kawaida.
    “Kipindi cha mwisho kabla ya mahusiano yenu ilikuwaje?” Lilikuwa swali la kwanza ambalo aliuliza polisi huku akimwangalia Edmund machoni mwake.
    “Mpenzi wangu alibadilika, alikuwa na mabadiliko ambayo yalitushangaza sisi sote” Edmund alimwambia.
    “Unaposema sisi sote unamaanisha nani na nani?”
    “Mimi, wazazi wangu na wazazi wake” Edmund alijibu.
    “Yaliwashangaza kivipi?”
    “Hakuwa akinijali kama ilivyokuwa zamani, hatukuwa tukiwasiliana kama ilivyokuwa zamani, alikuwa amebadilika sana” Edmund alimwambia polisi.
    “Ulihisi nini kwa wakati huo?”
    “Kiukweli kabisa nilihisi kwamba alikuwa na mwanaume mwingine, mwanaume aliyetokea kuuteka moyo wake zaidi yangu” Edmund alijibu.
    “Mara yako ya mwisho kuwasiliana na marehemu ilikuwa lini?”
    “Ilikuwa wiki mbili zilizopita”
    “Mbona kipindi kirefu hivyo?”
    “Kila nilipompigia simu hakuwa akiipokea. Jana tu nilimpigia sana simu, ila mara ya mwisho kuongea nae ilikuwa wiki mbili zilizopita lakini kuhusu kumpigia simu, nimekuwa nikifanya hivyo kila siku” Edmund alimwambia polisi yule ambaye aliandika kila kitu alichoona kustahili kuandikwa.
    “Na vipi kuhusu gari?”
    “Mmh! Sijui. Ninachokifahamu ni kwamba wazazi wake walimnunulia” Edmund alimwambia polisi yule.
    “Hapana. Wazazi wake wamekataa kumnunulia. Haukumnunulia wewe?”
    “Hapana. Sijawahi kumnunulia gari” Edmund alijibu.
    Polisi walionekana kuchanganyikiwa, swali ambalo walikuwa wakijiuliza ni kuhusiana na gari ambayo alikuwa akiitumia Catherine ambayo alikutwa ndani akiwa ameuawa kwa kunyweshwa sumu. Kilichofanyika ni kwenda mpaka chuoni na kisha kuongea na marafiki zake ambao alikuwa akiishi nao ndani ya chumba chake na ndipo walipomtaja Samuel.
    “Alikuwa mpenzi wangu na gari nilimnunulia mimi” Samuel aliwaambia polisi.
    “Ok! Ulikwishawahi kugombana nae?” 
    “Hapana. Alikuwa ni msichana ambaye anajiheshimu na kujua kupenda sana. Ila katika siku za karibuni hakuonekana kuwa na furaha. Mimi kama mpenzi wake nilijaribu kumuuliza kuhusiana na hali yake lakini hakuniambia kitu. Nikaona bora niache tu kwani kuna siku niliamini angeniambia” Samuel aliwaambia polisi.
    “Uhusiano wenu ulikuwa ukijulikana nyumbani?”
    “Hapana ila ndio tulikuwa tukijiandaa kwenda kujitambulisha kwani mwaka kesho ilitakiwa tuoane” Samuel aliwaambia polisi.
    “Ok! Bado tunaendelea na uchunguzi. Tutapakokuhitaji tutakuita” Polisi mmoja alimwambia Samuel ambaye akaingia ndani ya gari lake na kuondoka mahali hapo huku kwa muonekano akionekana kuwa na huzuni sana.
    ****
    Siku zikaendelea kukatika, wiki zikasonga mbele kama kawaida, wote wawili waliendelea kuishi maisha ya kitajiri huku Sadiki akiwa amebadilika kabisa na kumrudia Mungu. Kwa Samuel, hakutaka kumrudia Mungu, kwake, alijiona kuwa na wakati mgumu sana kama angeamua kuachana na biashara ya madawa ya kulevya,. Bado alihitaji kuwa na fedha zaidi na zaidi.
    Baada ya miezi kumi toka Sadiki amrudie Mungu, dalili za ugonjwa wa UKIMWI ukaanza kuonekana mwilini mwake. Alianza kwa kutapika na mwili kupungua. Japokuwa alikuwa na fedha lakini kamwe hakutaka kwenda kubadilisha damu Ulaya kama matajiri wengine walivyokuwa wakifanya. Kitu ambacho alikuwa akikisubiria kwa wakati huo kilikuwa ni kifo tu.
    Alijua kwamba maisha yake hayakuwa maisha ya mtu mwenye dhambi tena, alijua fika kwamba alikuwa akiishi katika maisha matakatifu kwa wakati huo, alijiandaa kwa kila kitu, hakuonekana kuogopa kifo hata mara moja. Sadiki hakutaka kumficha mtu yeyote, alijua fika kwamba kuna watu wengi wangebadilika endapo wangemuona jinsi alivyokuwa akipungua.
    Kwa wazazi wake ilikuwa ni kilio kila siku, hawakuamini kama katika kipindi hicho kijana wao, Sadiki alikuwa katika hali hiyo baada ya kuamua kumrudia Mungu na kuishi kama alivyokuwa akiishi zamani. Kila walipokuwa wakimwangalia, alionekana kuwa katika hali ya majuto mazito, alionekana kuumizwa na maisha yake ya nyuma ambayo alikuwa ameyaishi.
    “Huu ndio mwisho wa kila kitu ila ninamshukuru Allah kwa kuweza kunirudisha na kuwa kama nilivyokuwa zamani” Sadiki aliwaambia wazazi wake katika kipindi ambacho alikuwa kitandani.
    “Allah ndiye kila kitu, amini kwamba utakapofariki utakuwa umekwenda kupumzika sehemu salama” Ustadhi Hamidu alimwambia mtoto wake huku akionekana kuwa na uso uliokuwa na majonzi tele.
    Hakukuonekana kubadilika kitu chochote, ugonjwa wa UKIMWI ulianza kumtafuna pale kitandani. Watu ambao walikuwa wakimfahamu walikuwa wakifika hospitalini pale na kumuangalia, Sadiki alionekana kuwa mifupa mitupu. 
    Japokuwa alikuwa katika hali hiyo lakini kila siku kitabu cha Qur-an kilikuwa pembeni mwake. Bado tegemeo lake lilikuwa kwa Mungu, bado alikuwa akijiona kufa na kuamini kwamba Mungu alikuwa amepanga kila kitu katika maisha yake.
    Tarehe 13/4/2011 ndio ilikuwa siku ambayo Sadiki akafariki kitandani. Alifariki huku akiwa mifupa mitupu, UKIMWI ulikuwa umemtafuna kupita kiasi. 
    Kwa sababu alikuwa amejitengenezea marafiki wengi Tanzania, watu wengi wakajitokeza kumzika katika makaburi ya Kinondoni, mali zote pamoja na fedha zote ambazo alikuwa nazo akawaachia wazazi wake huku akiwataka kujenga vyuo vya madrasa pamoja na misikiti ambayo itatumika kumwabudu Mungu.
    “Mungu akulaze Pahali Pema peponi” Ustaadhi Hamidu alisema katika kaburi la mtoto wake, Sadiki.
    ****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Ugonjwa wa UKIMWI ukaonekana kuwa kama malipo juu ya kila kitu alichokuwa amekifanya katika maisha ya dhambi, ugonjwa ule ukaonekana kama mshahara wa dhambi zake alizokuwa amezifanya katika kipindi cha nyuma. Mwili ukaanza kupungua, vipele vikaanza kuota huku nywele zikianza kunyonyoka kama kuku aliyewekwa kwenye maji ya moto.
    Kila kitu katika maisha yake kikaonekana kubadilika mpaka kikafika kipindi ambacho alikiona ni bora kutengeneza maisha yake na Mungu. Alichokiamua Samuel ni kuwaita wazazi wake na kisha kumuongoza sala ya toba huku akiomba msamaha kwa kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea.
    Alikuwa na utajiri mkubwa lakini katika kipindi hicho alikuwa akiuacha mikononi mwa watu wengine. Alikuwa na biashara nyingi lakini nazo alikuwa akiziacha. Watu walibaki wakishangaa, kifo cha sadiki kilikuwa kimetokea siku chache zilizopita na leo alikuwa akiumwa Samuel ambaye nae alionekana kukonda kupita kawaida.
    “Huu ni mshahara wa dhambi baba” Samuel alimwambia baba yake.
    “Tunajua. Ila kwa sababu umeyakabidhi maisha yako kwa Mungu hakuna tatizo” Mchungaji Mpelele alimwambia mtoto wake, Samuel.
    “Nimekuwa nikijuta sana katika maisha yangu, mapenzi yakaonekana kuniweka mbali na Mungu, nilianguka dhambini na hatimae nimekuwa hivi. Ni bora ningeendelea kuwa hata masikini lakini moyoni niwe na Mungu kuliko kuwa na mali halafu moyoni uwe na shetani. Inanuma sana baba kupoteza muda wangu kumtumikia shetani” Samuel alimwambia baba yake.
    “Mungu anaweza, Mungu ameyabadilisha maisha yako, damu ya Yesu Kristo imeusafisha moyo wako” Mchungaji Mpelele alimwambia Samuel.
    “Najua baba lakini najutia maisha yangu, najutia kila kitu kilichotokea katika maisha yangu ya nyuma. Haikutakiwa kuwa hivi” Samuel alimwambia baba yake.
    Huo ndio ulikuwa muda wa kujutia kila kitu kilichopita. Baada ya Sadiki kufariki, baada ya mwezi mmoja nae Samuel alikuwa hoi kitandani. Biblia haikumtoka pembeni mwake, akawa mtu wa kusali kila wakati huku akiendelea kuomba msamaha kwa kila alichokuwa amekifanya.
    “MIMI NI MWENYE DHAMBI NISAMEHE MUNGU” Samuel alisema huku akiwa ameikumbatia Biblia yake kifuani mwake.
    Tarehe 27/6/2011 ndio ilikuwa siku ambayo Samuel akafariki katika kitanda ndani ya hospitali ya Muhimbili. Mauti ilimkuta huku akiwa amekumbatia Biblia kifuani mwake. 
    Mwili wake ulikuwa umekonda sana, vipele vilikuwa sehemu kubwa ya mwili wake, nywele zake zilikuwa zimenyonyoka kupita kawaida. Katika mazishi yake, wauzaji wengi wa madawa ya kulevya walikuwa wamekusanyika kumzika. Mama yake alikuwa mtu wa kulia tu, hakuamini kama angeweza kumpoteza mtoto wake katika umri mdogo ambao alikuwa nao.
    Kila kitu katika maisha yao kikaonekana kufungwa, mali walizokuwa wamezipata zikawa mikononi mwa wazazi wao ambao walizitumia kuwasaidia watu pamoja na kufanya mambo mengine ya maendeleo. Majina yao yalikuwa makubwa nchini Tanzania, historia zao zikabakia kuwa miongoni mwa watu waliokuwa wamefanya biashara ya madawa ya kulevya kwa nguvu zote. Vifo vyao vilieleza kila kitu kwamba ‘MSHAHARA WA DHAMBI NI MAUTI’. 
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    MWISHO.




0 comments:

Post a Comment

Blog