Simulizi : Miss Tanzania
Sehemu Ya Tatu (3)
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Happy akaikata simu na kumpa Patrick ambaye aliizima kabisa.Patrick alikwisha ng’amua kuwa mambo katu hayakuwa mazuri kwa Happy .
“Happy my baby” Akasema Patrick huku amemshika Happy mkono
“Calm down my sweet love.This is just the beginning .You have to be strong”
Kikapita kimya kifupi halafu Patrick akauliza
“Mama alikuwa anasemaje?
“Alihitaji kufahamu nitarudi lini na ni kwa nini siwasiliani na Mike.Patrick nilikubali kumpa moyo wangu Mike kwa sababu kwa wakati huo nilijua tayari umeshafariki.Laiti ningelijua kuwa badio upo hai nisingempa moyo wangu Mike.Lakini kwa vile tumeshaonana na wewe ndie mwanaume pekee nikupendaye duniani,basi sina budi kuwa wazi kwa Mike.It hurts lakini sina jinsi ni lazima nimweleze ukweli.Patrick ulinipotea mara ya kwanza lakini safari hii hutaweza kunipotea tena.I’ll fight for you”
ENDELEA........................
“MISS TANZANIA ATOWEKA NYUMBANI,MREMBO WA TANZANIA ATOROKA,HAPPY KIBAHO HAJULIKANI ALIPO,WASI WASI WATANDA JUU YA MAISHA YA HAPPY KIBAHO,MASKINI MISS TANZANIA…Hivi ni baadhi tu ya vichwa vya habari ambayo vilikuwa vikipamba kurasa za mbele za magazeti hasa yale ya udaku.Magazeti mengi yaliandika habari nyingi zinazohusiana na kutoonekana hadharani kwa mrembo mpya wa Tanzania,Happy kibaho lakini karibu magazeti yote hakuna hata moja ambalo lilikuwa na taarifa za ukweli juu ya wapi alipo Happy kibaho.
Wakiwa bado Arusha Patrick na Happy waliyasoma magazeti yote na kila kilichoandikwa ,wakacheka sana.
“Umekuwa maarufu sana kwa sasa” Patrick akasema
“mhh yaani wanavyonifuatilia !!’
“Na huu ni mwanzo tu Happy bado watakufuatilia sana katika kila jambo unalolifanya.Kila utakachokifanya itakuwa ni biashara kwao.Unatakiwa uwe jasiri sana na hasa katika hiki kizungumkuti kilichoko mbele yetu,mengi yatasemwa na mengi yataandikwa.Ningependa sana uwe mrembo mwenye sifa nzuri kama Nancy sumari,kama Hoyce Temu.Katika vipindi vyao vya kuvaa taji la miss Tanzania hawakuwa na kashfa yoyote ile iliyoyachafua majina yao.Nitafurahi ikiwa utafuata nyendo zao.”
“Nakuunga mkono Patrick ,unajua Nancy ndiye aliyenivutia mimi mpaka nikaingia katika fani hii ya urembo.Nampenda na nitafurahi sana kama nitafanikiwa kuwa kama yeye yaani kumaliza kipindi cha kulivaa taji hili bila kuwa na skendo yoyote mbaya katika jamii”
Wakakumbatiana na kucheka.
“Happy darl kuwa nawe hapa najiona ni kama vile ninaishi mbingu ya saba mbali na matatizo lukukiya dunia hii.Ninasikitika sana kwamba inatubidi turejee Dar.Nina imani kila mmoja wetu anafurahia sana kuwepo hapa lakini hatwezi kukaa hapa kwa muda mrefu kwa sababu bado tuna majukumu mengine ya kufanya huko tulikotoka na kubwa zaidi ni hili suala letu.Kikao cha mwisho cha harusi yangu kinakaribia hivyo inanibidi niwepo kabla ya kikao hicho na kuweka kila kitu bayana na hatimaye kuuvunja rasmi uchumba wangu na Vero kisha niufungue ukurasa mpya wa maisha yangu ya furaha.Halikadhalika wewe pia unatakiwa uende nyumbani kabla Mike hajaondoka na kufanya kama tulivyokubaliana.”
“ Kweli kabisa Patrick hata mimi nilikuwa na wazo hilo hilo.Hatuwezi kukaa hapa kwa muda mrefu sana wakati kuna jukumu zito linatukabili mbeleni.Ni wazi tunatakiwa kurudi dar”
“Ouh Gosh! Kumbe tulikuwa na wazo moja? Kwa nini sasa hukunieleza kama na wewe ulikuwa ukiwaza hivyo hivyo?Kuhusu usafiri usihofu,nitaongea na Andrew atatutumia gari la kuja kutuchukua hapo kesho.”
***************************CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Saa kumi na dakika saba gari aina ya Toyota Surf yenye vioo vyeusi ilifunga breki mbele ya lango la nyumba ya akina Happy .Mlango wa kulia ukafunguliwa akashuka Patrick kijana mtanashati akazunguka na kuufungua mlango mwingine akashuka mrembo mpya wa Tanzania Happy kibaho,tayari walikwisha fika Dar wakitokea Arusha.Kwa takribani dakika tano hivi walizitumia kuagana kisha Patrick akaingia garini na kuondoka.Happy alibaki amesimama pale huku mkono wake ukiwa katika hali ya kupungwa,hadi gari lilipopotea kabisa machoni pake
“I looo…..oove…uuuuuu….Pa…aaa.tri…ck…..”Alisema Happy huku machozi yakimlenga ,mara geti likafunguliwa akatoka mtumishi wa ndani.
“wow! Dada Happy !!!!!!!!!!!!!!”
Happy akastuliwa na sauti ile kugeuka akakuta ni Christina .
‘wow Tina”
Wakakumbatiana kwa furaha .Tina akamshika Happy mkono na kumuongoza mpaka ndani.Huko ndani ilikuwa ni furaha isiyo na kifani ,kila mtu aliruka ruka na kushangilia kwa nguvu Happy kurudi tena.
“Karibu sana mwanangu”Akasema mama yake
“Ahsante mama nimeshakaribia”
“habari za huko utokako”
“huko kwema mama,sijui nyie hapa”
“Sie huku wote wazima kabisa ila hofu yetu kubwa ilikuwa kwako.Tunashukuru Mungu umerudi salama.”
“Hata mimi nashukuru sana mama kama nyote mu wazima.I missed you so much”
Kisha salimiana Happy akaenda kuoga halafu akajifungia chumbani kwake akaanza kutafakari jinsi atakavyoweza kuutekeleza mpango wake wa kuachana na mchumba wake Mike cambell.kabla hajaanza kuwazua ni nini afanye simu yake inalia.Akaichukua na kuangalia ni nani mpigaji akakuta ni Patrick,Happy akatabasamu .
“Haloo my sweet love”
“Haloo darling vipi umepumzika?
“Yes Patrick nimejipumzisha kitandani”
“Ouh I’ve already missed you”
“mhh Patrick jamani hata masaa mawili hayajapita!!!
“Yeah I miss u a lot already.I miss you each second Happy ”
“Hahahahahaa….Mwaaaaaaa.I love you Patrick”
“I love you too Happy ”
“Ok my baby boy ngoja mi nipumzike tutawasiliana baadae.”
“Ok Happy hata mimi ndo najiandaa niende kwa andrew kisha nitapita nyumbani nikamuone mama”
“Ok bye love”
Baada ya kukata simu Happy akaendelea kuitazama simu ile huku akitabasamu.
“Mhh ! kila ninapoisikia sauti ya Patrick nahisi mwili wote unanichemka.I love him so much,and I’ll do anything for him”
Wakati akimuwaza Patrick mara sura ya Mike ikamjia akilini Happy akashindwa kujizuia akaangusha machozi.
“I’m sorry Mike but I have to do this.”
Akachukua simu yake tena na kuzitafuta namba ambazo Mike huwa anazitumia pindi awapo Tanzania akapiga.
“Hallow baby”ilikuwa ni sauti ya upole ya Mike cambell.
“Hallow Mike how are you”
“wow Happy unajisikiaje sasa hivi?
“Najisikia vizuri Mike,nashukuru sana kwa kuja kunitazama”
“Nashukuru hata mimi kama umerudi salama.Nilipata taarifa za ushindi wako na ghafla nikapata taarifa nyingine kuwa ulipoteza fahamu baada ya kutangazwa mshindi.Pole sana haya ni mambo ya kawaida.Nililazimika kuomba dharura ya wiki mbili ili nije kukaa nawe kwa kipindi hiki ambacho najua unanihitaji sana,lakini nilipofika mama akaniambia kuwa haupo umesafiri kidogo nje ya Dar es salaam .Sikutaka kukusumbua kwani nilijua unahitaji kuwa peke yako kwa kipindi hicho.Nafurahi umerudi salama” Mike akasema
“Mike naomba unisamehe kwa kutowasiliana nawe .Mambo mengi yalinitokea hapa kati kati hivyo nlihitaji kuwa peke yangu.Samahani sana kwa hilo”
“Usijali Happy nalitambua hilo na kuyaheshimu maamuzi yako.dont worry I’ll always be there for you my sweet baby.All I want is you to be happy.Happy I want to remind you that anytime you need a shoulder to cry on just count on me.I’m here for you”
Maneno haya yanamchoma sana Happy na kujikuta akitokwa na machozi ,alishindwa ajibu nini ,mara akastuliwa na sauti ya Mike.
“Happy niko njiani nakuja nina hamu sana ya kukuona na kukupa pongezi zangu na kama utakuwa unajisikia vizuri basi tunaweza kutoka out kwa ajili ya dinner.
“Thanx Mike,nashukuru sana lakini najisikia kichwa kinaniuma mno.Nadhani nahitaji kupumzika Hivi kwa nini tusionane kesho?
“Ok Happy kama umeamua hivyo basi vizuri.Jiandae kesho tutoke kwa chakula cha mchana .”Mike alisema kwa sauti ambayo ilionyesha dhahiri kuwa hakuwa ameridhika na maamuzi yale ya Happy .
“sawa Mike nashukuru sana ,tuonane hiyo kesho”
“Ok Happy have a nice rest.I love you………………..”
Happy akashindwa atamke nini ,midomo ikawa mizito machozi yakimtoka.Akakata simu na kujitupa kitandani.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mike I’m sorry I didn’t want this to happen to our relation but its already happened.I’m sorry……….”
*****************
“Hello Komrade” Andrew akasema huku akimkumbatIa rafikiye Patrick kwa furaha mara baada ya kufungua mlango na kumkuta amesimama mlangoni
“Hello Andrew” Patick akasema huku akitabasamu
Andrew akaushika mkono wa patrick akauinua kidogo na kuuminya halafu akacheka kicheko kikubwa.
“Brother naona mambo ya Arusha hayakuwa madogo.Siku hizi chache tu naona hata mwili umeongezeka. “
Wote wakacheka kicheko kikubwa na kuketi sofani.Andrew ambaye ndiyo kwanza alikuwa amerejea toka katika shughuli zake,akaelekea chumba cha chakula kisha akarejea sebuileni na chupa kubwa ya mvinyo.
“Nashukuru umerudi salama.Hamkupata tatizo lolote njiani?”
Akasema Andrew huku akiweka chupa ile mezani na kuumimina mvinyo katika glasi akampatia Patrick glasi moja.
“hatukupata tatizo lolote njiani.Nashukur yule dereva uliyemtuna ni mahiri mno.” Patrick akasema
“Kaka nipe habari za Arusha.Mambo yamekwendaje? Happy hajambo? Andrew akauliza huku akitabasamu baada ya kupiga funda la mvinyo.Patrick naye akainua glasi yake akapiga funda moja halafu akalegeza tai yake na kusema
“Andrew namshukuru Mungu kwa sababu mambo yaliyotokea Arusha sikuyategemea kabisa.Ndugu yangu sikufichi nilikuwa najihisi kama niko peponi kwa raha nilizokuwa napata .Kama isingekuwa ni masuala haya ya harusi nisingerejea mapema hivi.” Patrick akanyamaza na kunywa tena funda la mvinyo halafu akaendelea
“Happy alifika Arusha kama tulivyokuwa tumepanga.Mara tulipokutanisha macho nilihisi kama ninapaa kwa furaha niliyoipata.Sikuwa nimetegemea kama ningekuja kuonana tena na Happy maishani.Tulikuwa na maongezi marefu sana siku hiyo.Tulikumbushana toka siku ya kwanza tulipokutana ,mambo yote yaliyotokea hadi siku niliyoingia gerezani.Happy alilia sana.Tulikumbuka mambo mengi mno.Tulikumbuka nyakati zetu za furaha na hata nyakati zile tulizokuwa katika wakati mgumu na hasa wakati ule tuliposimamishwa shule kwa kosa la kupigana darasani halafu tukaenda kujificha Bagamoyo ambako ndiko penzi letu lilikoanzia.” Patrick akanyamaza akanywa tena funda la mvinyo halafu akaendelea na maongezi.Andrew alikuwa kimya akimsikiliza.
“Andrew mambo yaliyotokea huko ni makubwa na ya kushangaza sana”
“Patrick hebu niambie ,mambo gani hayo yaliyotokea huko? Nina hamu ya kutaka kufahamu kilichoendelea huko Arusha” Andrew akasema huku akiifungua tai yake na kuitupa pembeni.
“we real had a great time”
“Usiku wa siku ile ya kwanza happy aliniuliza kitu ambacho kilinistua na kunishangaza sana.Aliniuliza eti ni kwa nini niliamua kumdanganya kwamba nimefariki dunia wakati ningali hai? “
“Etu ulifanya nini? Andrew akauliza kwa mshangao
“Anadai nilidanganya kwamba nimefariki dunia”
“Enhee wewe ukamjibuje?
“Kwanza swali lile lilinistua sana japokuwa hata Margreth alikwisha nidokeza kuhusu kuwepo kwa jambo hilo la mimi kudai nimefariki dunia.Nilimtuliza na taratibu nikamuomba anielezee kwa undani kuhusiana na mkasa ule kwa sababu mimi ndiyo kwanza niliusikia.Alianza kunieleza kwamba akiwa chuoni alipokea barua toka kwa mtu ambaye alijitambulisha kwamba ni mtu anayenifahamu mimi na familia yangu na kwa kuwa anaufahamu uhasiano wetu aliamua kumpa taarifa ambazo hazikuwa nzuri hata kidogo.Mtu huyo aliyemuandikia barua hiyo alidai kwamba Patrick yaani mimi ,nilifariki kwa ugonjwa wa kuhara nikiwa gerezani.Nikinukuu maelezo yake anasema kwamba almanusura ajitoe uhaibaada ya kuipata taarifa ile kwa sababu hakuona ni namna gani angeweza kuishi bila mimi.Ilimchukua muda mrefu sana kuja kukubaliana na ukweli kwamba nimefariki.Baada tu ya kumaliza masomo yake alirudi nchini na kitu cha kwanza alichokifanya ni kuanza kutafuta mahala nilipokuwa nimezikwa.Alikwenda hadi Sumbawanga ,mahala tulikokuwa tukiishi kabla ya baba hajastaafu utumishi serikalini akambiwa kwamba familia yangu ilihama kitambo baada ya baba kustaafu kazi.Toka Sumbawanga akaenda hadi Iringa katika gereza nililoanza kutumikia kifungo akaambiwa kwamba nilihamishwa pale gerezani na kwenda Songea nikiwa mzima wa afya.Hakukata tamaa akaenda tena hadi Songea ambako taarifa aliyoipata ilisema kwamba nilimaliza kifungo changu na kufanikiwa kutoka gerezani salama salimini.Majibu haya yalimpa wakati mgumu sana na kumfanya azidi kuchanganyikiwa kwani aligundua sikuwa nimekufa.Kwa mujibu wa maelezo yake,siku ile aliposhinda taji la Miss tanzania alipoteza fahamu baada ya kuiona sura yangu.Hakuamini kama kweli ni mimi au ni mzuka anaouona” Patrick akanyamaza ,akamtazama rafiki yake aliyekuwa kimya akimsikiliza
“Enhee ikawaje baada ya hapo? Andrew akauliza
“baada ya hapo ikanibidi na mimi nimweleze ukweli kwamba nilipokea taarifa toka kwa Vero niliyekuwa nikimtumia kama kiungo cha mawasiliano baina yangu na Happy .Taarifa hiyo ilisema kwamba yeye Happy amepata mchumba wa kizungu na tayari ana ujauzito na kwa sasa wanaishi pamoja kama mume na mke.Nilimweleza ni jinsi gani nilivyoumizwa na taarifa ile.Happy alilia sana hadi nikamuonea huruma.Alinilaumu sana kwa kuwa mwepesi wa kuamini taarifa kama ile hali nikijua kwamba alikuwa akinipenda kwa moyo wake wote.” Patrick akatulia akanywa tena mvinyo halafu akakohoa kidogo.Andrew akainuka na kuwasha feni alianza kuhisi joto.
“Enhee ikawaje tena? Akauliza Andrew huku akiongeza mvinyo katika glasi yake.
“Kilichofuata ikatubidi tukae kwa pamoja na kutafakari ni kwa nini mambo haya yalitokea.Tuligundua kwamba taarifa zile mbili zilikuwa na lengo la kuuvunja kabisa uhusiano wetu.Swali likaja ni nani ambaye aliamua kutufanyia ukatili wa namna ile? Ni nani ambaye alihitaji mimi na Happy tutengane? Happy akanionyesha ile barua aliyotumiwa ambayo ameitunza hadi hivi sasa.Nilistuka mno baada ya kuutambua mwandiko .Ulikuwa ni mwandiko wa Vero.Andrew nilihisi kuishiwa nguvu baada ya kuligundua hilo” Patrick akatulia kidogo na kuinama chini.Andrew akastuka na kusema kwa sauti ndogo
“Ouh My God ! ..Hii sasa ni hadithi mpya”
Pamoja na feni iliyokuwa ikipuliza mle sebuleni na kuipooza hali ya hwea iliyokuwa ya joto,Andrew alikuwa akitoka jasho jingi.
“Pat..patri..Patrick ngoja nikachukue barafu katika friji naona imeisha hapa” Andrew akasema kwa sauti yenye kitetemeshi huku akiinuka na kuelekea chumba cha kulia chakula.Alipofika katika friji akahisi kama mikono yake imeisha nguvu ,akaeliegemea friji.
“Ee Mungu naomba unipe nguvu ya kustahimii kipindi kigumu kinachokwenda kuanza muda si mrefu.” Andrew akaomba kimoyo moyo akiwa bado ameliinamia kabati.
“Nimestuka sana kusikia kwamba Vero ndiye aliyewatenganisha Patrick na Happy.Pamoja na kwamba ni muda mrefu wametengana na Patrick kwa sasa anakamilisha maandalizi ya harusi yake na Vero lakini bado hajaacha kumzungumzia Happy.Kila tukikaa huwa anamkumbuka .Kwa jinsi Patrick anavyompenda Happy ,sina haja ya kuuliza kwani jibu liko wazi,hapa hakuna ndoa tena.Nahisi kuishiwa nguvu…….”
Andrew akachukua barafu na kurejea sebuleni.Patrick alikuwa ameegemeza kichwa katika ukingo wa sofa huku mkono wake mmoja ukiwa umelishika shavu lake.
“Enhee endelea kunipa michapo ya Arusha.Ikawaje baada ya kugundua kwamba ni Veronika ndiye aliyesababisha mambo haya yote? Andrew akauliza
“kwanza Happy alilia sana.Mimi kwa upande wangu nilipandwa na hasira za ajabu .Sikuamini kama Vero anaweza akafanya kitendo cha namna ile.Niliumia sana Andrew.”
“Du ! haya mambo ni makubwa sasa” Andrew akasema
“Ilituchukua muda mrefu sana kuliongelea jambo hilo lakini kuna kitu kiliibuka ambacho kiliniuma sana”
“Kitu gani hicho?
“Happy alikuwa na pete ya uchumba kidoleni”
“Ina maana tayari Happy ana mchumba? Andrew akauliza huku akishusha pumzi
“kweli Andrew.Tayari Happy ana mchumba.Baada ya kukaa muda mrefu bila kuniona aliamua kumpa nafasi mtu mwingine.”
“Too bad.” Andrew akasikitika
“Na wewe ulimweleza kuhusu harusi yako na Vero? Andrew akauliza tena
“Ndiyo Andrew.Hatukutaka kufichana chochote.Tuliweka bayana kila kitu bila kuficha chochote” Patrick akasema
“Baada ya hapo nini kiliendelea? Andrew akauliza huku akitabasamu
“Kilichofuata baada ya hapo tuliiweka dunia yote na matatizo yake kando, tukaingia katika ulimwengu mwingine kabisa wenye raha zisizoelezeka.Andrew nilihisi raha ambayo sijawahi kuipata toka nimezaliwa.Nilijiona ni mwenye bahati kubwa kuwa na mrembo kama yule”
“wow ! maelezo yako yananifanya nijenge picha ya jinsi mambo yalivyokuwa.Tell me about that first night ? Akasema Andrew
“Andrew ,ule ulikuwa ni usiku wangu wa kwanza kuhisi kama niko peponi.Nilihisi kama siko katika dunia hii iliyojaa shida na mahangaiko.Sijawahi kuwa na usiku kama ule.Sikufichi Andrew,Happy ni msichana aliyebarikiwa mno.She’s so sweet” Patrick akasema na kumfanaya Andrew acheke wakagonganisha mikono.
“You had sex with her? Andrew akauliza.Huku akicheka Patrick akasema
“Yes we had .and one thing that you cant agree is that she was still a virgin.I was her first man” Patrick akasema na kumfanya Andrew asimame huku akiwa na tabasamu la mshangao.
“ wuuuh ! Its unbelievable “ Andrew akashangaa
“Yes Andrew.hata mimi nilishangaa sana .Kwa mujibu w a maelezo yake anasema kwamba japokuwa aliamua kuwa na mpenzi mwingne lakini bado moyo wake ulikuwa kwangu.Aliamini siku zote kwamba mimi ndiye mwanaume wake a pekee kwa hiyo alikuwa mzito sana kumpa mwili wake huyo mpenzi wake mpya”
Andrew akamimina mvinyo katika glasi yake akaiinua juu,wakagonganisha glasi
“Patrick nakupa hongera zako” Andrew akasema huku akitabasamu halafu wote wakacheka kwa nguvu.
“Andrew kwa siku hizi chace nilizokaa na Happy kule Arusha nimeonja utamu wa maisha.Sikujua hapo awali kama kuna nyakati maisha huwa matamu namna ile.Kila nikiamka niko na malaika wangu pembeni ilimradi raha na furaha kila wakati.”
Patrick akasema na kuchukua glasi yake ya mvinyo akapiga funda kubwa.Andrew akamtazama na kusema
“Patrick naomba nikuulize jambo moja”
“Uliza Andrew”
“Ni muda mrefu hamjaonana na happy .baada ya kukutana naye safari hii umeuonaje mtazamo wake kuhusu mahusiano yenu?
“Andrew wewe ni mtu wangu wa karibu na siwezi kukuficha kitu.Pamoja na yote yaliyotokea lakini bado mimi ni mtu wa pekee kwake.Bado nafasi yangu iko pale pale ndani ya moyo wake.”
“na vipi kuhusu wewe? Pamoja na yote yaliyotokea,bado unaamini kwamba Happy ana nafasi moyoni mwako? Andrew akaulizaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Swali lile likamfanya Parick anyamaze kidogo ,akachukua glasi ya mvinyo na kupiga funda moja,akakohoa kidogo na kusema
“Andrew ,pamoja na yote yaliyotokea bado Happy ndiye namba moja wangu .Yeye ndiye furaha yangu.Samahani Andrew kama kwa kusema hivi nimekukera.”
“hapana hujanikera Patrick.Nafurahi kwa sababu siku zote umekuwa mkweli kuhusu hisia zako.Kwa hiyo baada hisia za kila mmoja wenu kuwa wazi kwamba bado mnapendana nini kilifuata?
“Tulikuwa na wakati mgumu mno kwa sababu sote tayari tuko katika mahusiano mapya ambayo yamekwisha piga hatua kubwa,lakini hii haikuwa sababu ya kutufanya tusiendelee na urafiki wetu hata kama tuko katika mahusiano mengine.Tulikubaliana kuendelea na urafiki wetu wa kawaida lakini tukajiuliza tena,sisi tunapendana kwa dhati,je tutakuwa tunajitendea haki sisi wenyewe ? Huko tuliko tutakuwa na furaha? Majibu ya maswali haya yote yalikuwa ni hapana.Hatutakuwa tumejitendea haki sisi wenyewe ,vile vile huko tuliko hatutaweza kuishi kwa furaha na amani.Tukajiuliza tena tufanye nini basi? Jibu likawa kwamba tunalazimika kuifanya maamuzi magumu.”
“maamuzi magumu yapi tena? Andrew akauliza
“Kuachana na wapenzi wetu wa sasa ! Patrick akasema na kumfanya Andrew asimame
“No ! you are kidding me” Akasema Andrew
“Andrew,Happy ndiye furaha ya maisha yangu.Nilimpenda Happy muda mrefu na hata nikafungwa kwa ajili yake.Pamoja na yote yaliyotokea lakini bado Happy amekuwa ni mtu wa pekee kabisa ndani ya moyo wangu .Ninampenda na nitaendelea kumpenda hadi kufa kwangu.Kwa sababu ya upendo huo mkubwa nilionao kwa Happy ,nimeamua kuachana na Vero.Nimeona uwe mtu wa kwanza kufahamu kabla sijaliweka wazi jambo hili kwa ndugu .Ndoa kati yangu na Vero haipo tena.Its over.Happy naye ameamua kuachana na mpenzi wake ili tuweze kuwa pamoja.Nafahamu si jambo rahisi lakini siku zote nguvu ya penzi ni kubwa na hushinda kila kikwazo“ Patrick akasema na kumfanya Andrew ainame na kuzama katika mawazo ghafla.
“Nilijua tu ,hapa hakuna ndoa tena.Masikini Vero” Andrew akawaza.
“Andrew nafahamu umekuwa mtu wangu wa karibu mno na umenisaidia katika mambo mengi lakini tafadhali naomba usinishauri chochote kuhusu jambo hili.Nimekwisha fanya maamuzi na siwezi kurudi nyuma tena.Kwa ajili ya Happy nitafanya kila kitu ili niwe naye maishani..Ahsante sana Andrew kwa kunisaidia katika mambo mengi lakini nakuomba katika suala hili usijihusishe kwa sababu ninafahamu kinachokwenda kutokea si kitu kizuri.Please don’t be part of this” Patrick akasisitiza.Andrew akamtazama na kusema
“Patrick wewe ni zaidi ya rafiki yangu.Tumeshauriana na tumesaidiana katika kila jambo.Mpaka sasa hivi kati ya ndugu zako wote hakuna mtu yeyote anayefahamu kitu gani kinaendelea zaidi yangu.Kusema kwamba nisikushauri au nisijihusishe kwa namna yoyote na suala hili ni jambo lisilowezekana kwa sababu I’m too involved now.Tumetoka mbali na jambo hili kwa hiyo siwezi kuishia hapa.Kama nilikubali toka mwanzo kwamba nitakuwa nawe,siwezi kamwe kukuacha peke yako hasa katika kipindi hiki kitakachokuwa kigumu zaidi kwako.Patrick utake usitake mimi nitakuwa pamoja nawe katika suala hili hata kama umekataa nisikushauri chochote lakini nitakuwa nawe hatua kwa hatua na hata ikibidi kukushauri pale itakaponilazimu japokuwa sintakushauri ubadili mawazo yako kuhusu yupi ni msichana unayemtaka maishani.”
Patrick akamtazama Andrew na kusema
“Andrew narudia tena ,kinachokwenda kutokea si kitu kizuri.Ninaomba kila kitu nikibebe mimi mwenyewe.Umenisaidia sana lakini kwa hili naomba uniache mwenyewe.Nimekwisha jitolea kuubeba mzigo huu mkubwa ,ninajua nitaumia na wengi pia wataumia lakini sina namna nyingine ya kufanya .Lazima nifanye hivyo.Lazima niachane na Vero”
“Patrik nimekuelewa vizuri naomba ufahamu kwamba hata kama hupendi bado nitaendelea kuwa nyuma yako.Naomba tafadhali tusiongelee suala hili tena.Fahamu kwamba tuko pamoja na siku zote tutaendelea kuwa pamoja.” Andrew akasema huku akimpa Patrick mkono.
“Andrew nashukuru kama kwa moyo wako umekubali kuungana nami katika suala hili.Nitakuja kukuona kesho asubuhi na kukufahamisha kwa kina mpango mzima .Naomba nikuache na tuonane kesho.”
Wakaagana na Patrick akaondoka zake na kumuacha Andrew akiwa na mawazo mengi
“Du ! mambo yanazidi kujikoroga.Sipati piha ni kitu gani kitakachotokea baada ya Patrick kutamka kwamba amevunja mahusiano yake na Vero.Sikutegemea kama suala hili lingefika hapa lilipofika.Hatua waliyokwishaifikia ni kubwa sana na umebaki muda mchache tu wafunge ndoa.Kitendo cha kusitisha masuala ya ndoa yao kimeniumiza sana japokuwa sina uwezo wa kulizuia jambo hilo lisitokee, kwani tayari Patrick amekwisha fanya maamuzi na hakuna mtu anayeweza kuyabadili.Ninamfahamu Patrick vizuri akisha amua kitu huwa hapendi kupingwa Nimemuona machoni ,alikuwa akimaanisha kile alichokisema.Sijui Happy amempa kitu gani Patrick mpaka ameshindwa kumsahau hata baada ya miaka mingi kupita.Hadi kufikia hatua ya kusitisha mipango ya harusi yake kwa ajili tu ya Happy basi hakuna kitu ninachoweza kukifanya kwa ajili ya kuinusuru ndoa hii ya Patrick na Vero.Patrick na Happy wanapendana na hilo halina ubishi.Ukijiuliza ni kwa nini Happy ajitokeze katika kipindi hiki baada ya kupotea kwa miaka hii yote utapata jibu kwamba ilipangwa wawe pamoja.Nakubaliana na ukweli huo japokuwa ninamuhurumia sana Vero kwa jinsi anavyompenda Patrick.Kosa moja ambalo alilifanya ni kutumia uongo kuwatenganisha wawili hawa.Uongo wake leo hii umekuja kujulikana na hivyo kumgharimu .Kama walivyoumia wenzake kipindi kile alipowatumia taarifa za uongo zilizowafanya wakatengana basi hata yeye atasikia uchungu kama walioupata wenzake kwa miaka hii yote.Roho inaniuma sana lakini sina namna nyingine ya kuweza kumsaidia..Kingine kinachoniumiza ni gharama kubwa tuliyoitumia katika maandalizi ya harusi hii.Nimetumia fedha zangu nyingi kama mchango kwa rafiki yangu katika kuiandaa harusi hii lakini kila kitu kimepotea bure……” Andrew akawaza huku akiketi sofani akakishika kichwa chake alikuwa na mwazo mengi.
“Ngoja nimpigie mama yake Patrick ili afahamu kama mwanae amesharudi.Kwa jinsi Patrick alivyochanganyikiwa na Happy sidhani kama amekumbuka hata kumtaarifu mama yake kama amesharudi Dar es salaam.” Akawaza Andrew huku akichukua simu na kuzitafuta namba za mama yake Patrick.
“Lakini simlaumu sana Patrick kwa sababu kwa uzuri wa Happy hata mimi ningechanganyikiwa.Mtoto ameumbika mithili ya malaika.Mtoto anastahili kabisa kutwaa taji la mrembo wa dunia” Akawaza Andrew wakati akisubiri simu yake ipokelewe na mama Patrick.
“Hallo Andrew habari yako mwanangu” Akasema mama Patrick baada ya kupokea simu
“Habari nzuri mama ,pole na mihangaiko ya kutwa nzima ” Andrew akasema
“Tumeshapoa baba yangu.Kutwa nzima tumekuwa tukizunguka hapa na pale katika kuhakikisha maandalizi yanakamilika.Japokuwa kuna kamati inayoshughulikia kila kitu lakini hata mimi kuna mambo ambayo inanilazimu kuyafuatilia na kuhakikisha yamekaa sawa.Si unajua siku zimebaki kidogo sana na jiji hili lina sherehe nyingi kwa hiyo inabidi kufanya maandalizi ya mapema.”
“ Pole sana .Mama nimekupigia kukufahamisha kwamba Patick amerejea Dar es salaam jioni ya leo .Umefanikiwa kuonana naye?
“Hapana Andrew.Habari hizi wewe ndiyo wa kwanza kuniambia.Hajanitaarifu kama amerejea japokuwa alinipigia simu jana akaniambia kwamba atarejea Dar es salaam siku yoyote.Andrew huyu mwenzio amepatwa na kitu gani ? mbona amebadilika namna hii?Nimeona kuna mabadiliko makubwa sana katika siku hizi chache toka apatwe na yale matatizo ya kupoteza fahamu.Kitu gani kinamsumbua mwenzio? Mama yake Patrick akauliza
“mama siwezi kujua kitu gani kinamsumbua ,japokuwa mimi na yeye ni marafiki wakubwa lakini kuna masuala ya ndani kabisa ambayo hatuwezi kuambiana.Mimi naona tumpe muda wa kutosha ili atulie kwa sababu ninahisi hali hi inaweza kuwa inachangiwa na mambo mengi aliyonayo na hasa hili suala la harusi yake”
“Sawa Andrew.nashukuru kwa kunifahamisha kwa sababu rafiki yako haoni hata umuhimu wa kuwataarifu wazazi wake kama amerejea salama.Tena imekuwa vizuri amerejea kwa sababu mwenzake alinipigia simu kunitaarifu kwamba atarejea leo saa nane za usiku.Kwa hiyo itakuwa vizuri kama atakuwepo uwanja wa ndege na kumpokea mwenzake kwani aliondoka akiwa hana amani kwa hiyo litakuwa jambo la faraja kama akimkuta Patrick uwanjani akimsubiri .Ngoja nimpigie simu nimfahamishe kuhusu hilo.”
“Ok Ahsante mama.Usiku mwema” Andrew akasema na kukata simu kisha akaitupa sofani.
“Damn you Patrick!! Kila siku nimekuwa nikidanganya watu wazima.Umeniweka katika matatizo makubwa sana na siku mama yako akigundua kama mambo yote niliyokuwa nikimwambia yalikuwa ya uongo atatamani hata kunitoa roho.Hatatamani anione tena katika macho yake…” Andrew akatikisa kichwa kwa masikitiko.
“masikini Vero leo usiku anarejea akiwa na matumaini kwamba ndani ya wiki chache zijazo atakuwa mwanamke mwenye furaha kwani atakuwa ameolewa na mwanaume anayempenda sana.laiti angejua ..nadhani asngekubali kurudi tena Tanzania.Namuonea huruma lakini yote haya aliyataka mwenyewe.Palipo na penzi la kweli hakuna awezaye kulitenganisha.Na tusubiri tuone kitakachotokea….” Andrew akawaza akachukua glasi yake iliyokuwa na mvinyo akapiga funda kubwa.
**********************
Akiwa katika kona ya kuingilia nyumbani kwake smu yake inaita.Akapunguza mwendo wa gari na kutazama mpigaji.Alikuwa ni mama yake.Akasita kuipokea simu ile.
“Ukiona hivi ujue tayari amekwisha pata taarifa kuwa nimerudi.” Akawaza Patrick
“Hallo mama shikamoo” Akasema Patrick baada ya kuipokea simu ile.
“Marahaba hujambo? “ Akaitika mama yake. Patrick akaguna kidogo kwa muitikio ule kwa sababu kuna kitu alihisi hakikuwa sawa katika sauti ya mama yake.Anamfahamu mama yake vyema.
“Sijambo mama.habari za hapo nyumbani? Patrick akauliza
“Hivi wewe mwanangu naomba nikuulize kitu.Sisi wazazi wako unatuweka katika kundi gani? Mama yake akauliza kwa sauti yenye ukali.
“Kazi imeanza” akawaza Patrick
“mama samahani naomba nikupigie baada ya muda mfupi .Nataka kupaki gari.”Akasema Patrick na mama yake akakata simu bila kusema chochote.Baada ya kuliingiza gari ndani akaelekea sebuleni kisha akaketi sofani akaishika simu yake na kumpigia mama yake.
“Samahani mama kwa kukatisha maongezi yetu mida ile.”
“hakuna hata haja ya samahani kwa sababu siku hizi sisi wazazi wako hatuna tena thamani kwako.”
“kwa nini uansema hivyo mama?
“Kwani si kitu kilicho wazi.Hutaki kutusikiliza chochote tunachokwambia.Hutaki ushauri wetu tena.”
“ Si kweli mama.” Patick akajibu
“Kama si kweli unawezaje kurudi bila kututaarifu kwamba umerudi salama?
“Mama ni kweli nimerudi jioni hii na nilikuwa na mpango wa kuja hapo nyumbani lakini nikiwa njiani nilijsikia hali kubadilika ghafla ikanibidi nirudi nyumbani mara moja.Nimetumia dawa na ninajisikia safi kwa sasa.”
“Mh ! Haya bwana.Sasa sikiliza.Mwenzako alinipigia simu na kunitaarifu kwamba anarudi leo saa nane za usiku.”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mwenzangu !! Patrick akauliza
“Ndiyo mwenzako.Kwani una wenzako wangapi? Ina maana Vero si mwenzako?
“Ouh kumbe unasema Vero”
“Ndiyo anarejea leo saa nane za usiku akitokea London alikoenda kwa ajili ya kufanya manunuzi ya harusi yenu.Kwa kuwa umerudi,litakuwa jembo kama ukienda kumpokea uwanja wa ndege.Patrick mwenzako aliondoka hapa akilia machozi na alikubali kwenda London baada ya mimi kumbembeleza afanye hivyo.Tafadhali mfurahishe mwenzako.Nenda ukampokee usiku huu arudipo.Atajiskia mwenye furaha sana pindi akishuka ndegeni na kukuona pale ukimsubiri.Atasahau kila kitu kilichopita” mama yake akasema .
Patrick akafikiri kidogo na kusema
“Sawa mama nitajitahidi kwenda huko uwanjani.Vipi kuhusu kile kikao?
“Kikao kitafannyika kesho na kila mwanamakati ana taarifa.Katika kikao cha kesho tutafanya majumuisho ya kila kitu na kuangalia kama kuna kitu kilichobaki na kisha jumatatu ndoa ikaandikishwe na kuanza kutangazwa kanisani.Kwa ujumla kila kitu kipo tayari.”
“Sawa mama .Nitafika katika kikao hicho Kuna mambo nataka kuongea na wanakamati wote kwa ndugu wa karibu kwa ujumla.Jitahidi wewe na baba muwepo na umtaarifu pia mama yake Vero naye awepo.Ni muhimu sana..”
“Patrick unataka kutueleza kitu gani? Mama yake akauliza
“Ni masuala madogo madogo tu ya kuwekana sawa kuhusu mambo haya ya harusi” Patrick akasema kisha akaagana na mama yake akaegemeza kichwa sofani na kuvuta pumzi ndefu.
“ Hatua kubwa imeshapigwa mpaka sasa.Kila kitu kiko tayari .Fedha nyingi imeshatumika katika maandalizi ya harusi hii.Ndugu jamaa na marafiki wote wana taarifa juu ya harusi yangu na wanaisubiri kwa hamu kubwa na wengi wametoa michango yao kwa ajili ya maandalizi ya harusi hii.Mambo hayatakuwa rahisi kama nilivyotegemea.Hakuna atakayekubali uhusiano huu uvunjike.hakuna atakayekubali ndoa hii isitishwe.Hakuna atakayenielewa.Hawatanielewa kwa sababu hakuna anayefahamu wapi nimetoka na Happy zaidi ya Andrew .Wazazi wangu walimchukia Happy hasa kwa kitendo chake cha kwenda kusoma Ulaya na kuniacha gerezani.Sipati picha nini kitatokea wakisikia kwamba ninaachana na Vero kwa ajili ya kuwa na Happy.Nafahamu sintaeleweka katika jamii lakini siwezi kurudi nyuma.Lazima niachane na Vero.Nafahamu ni jisni gani Vero anavyonipenda lakini alifanya kosa kubwa sana kuamua kunitenganisha na furaha ya moyo wangu.namuonea huruma sana.Atateseka sana lakini sina namna nyingine ya kufanya .Kwa ajili ya Happy chochote kile nitafanya.Kwa upande wa Happy jambo hili linaweza kumletea picha mbaya katika jamii.Ninafahamu kwa sasa yeye ni mrembo wa Tanzania na ni mtu maarufu.Kila akifanyacho kinatengeneza kichwa cha habari.Kama waandishi wa habari wakilipata jambo hili litasababisha heshima ya Happy kuporomoka ghafla.Nitakuwa nimemsababishia matatizo makubwa mtoto mzuri kama huyu ambaye taifa linamtazama kama mrembo ambaye anaweza akaliletea taifa hili sifa kubwa sana kupitia taji lake hili” Akawaza Patrick akiwa ameketi sofani.Akainuka akawasha luninga akarudi tena kuketi sofani.
“Nilimuahidi mama kwamba nitakwenda kumpokea Vero usiku huu.No ! siwezi kufanya hivyo.Sijisikii kuonana na Vero kwa sasa.Ninaweza nikajaribu mambo bado mapema.Nataka kila kitu kiishe kesho mbele ya ndugu na jamaa.Nataka kila mmoja afahamu nini Vero alinifanyia.Kwa sababu nilikwisha muahidi mama kwamba nitakwenda kumpokea Vero,ngoja niwasiliane na Andrew ili nimuombe akampokee Vero uwanja wa ndege.”
**********************
Honi ya gari ikamstua Andrew akiwa jikoni akijiandalia chakula cha jioni.Akazima jiko na kutoka mle jikoni akaelekea getini .Akafungua na kukutana na gari jipya kabisa aina ya BMW jeusi.Akastuka na kujiuliza ni nani yule kwa sababu hajawahi kuliona gari lile pale kwake.Akalisogelea na mara kioo cha gari kikashushwa taratibu akakutana na sura yenye tabasamu ya mpenzi wake Vick.
“wow ! Vicky” Andrew akasema kwa mshangao huku akilifungua geti lote na gari likaingia ndani.
“Naona kama ndoto .Ni wewe kweli? Andrew akauliza
“Ni mimi Andrew.Kwani kuna kitu gani cha ajabu? Vick akauliza huku akishuka garini.
“wow ! umeazima wapi gari la thamani kubwa namna hii?
“Ina maana mimi siwezi kumiliki gari la namna hii?” Vick akauliza
“Kwa maana hiyo gari hili ni lako? Andrew akauliza
“Ndiyo ni gari langu.Kuna tatizo lolote mimi kuwa na gari kama hili?
“hakuna tatizo lakini unapokuwa na kitu cha thamanai kama hiki,kuna tatizo gani mwenzio akifahamu umekipataje pataje? Andrew akauliza
“Kwa maana hiyo unahofia kwamba ninaweza kuwa nimenunuliwa na mwanaume mwingine? Vick akauliza huku akimkazia macho Andrew
“Hata kama umenunuliwa na mwanaume mwingine unaweza ukaniambia?
“Hakuna kitu nilichowahi kukuficha mpenzi wangu na kwa hili ninataka kukueleza ukweli kwamba nimenunuliwa na bosi wangu ambaye mimi ni kimada wake.” Vick akasema na ghafla Andrew akageuza macho akaanguka chini
Vick akamuinamia akambusu na wote wakaangua kicheko kikubwa.
“Usirudie tena kusema hivyo.Unajua sisi wengine hatukawii kuanguka kwa presha” Andrew akasema huku akicheka
“kama ingekuwa ni kweli ningemkata kichwa huyo bosi wako” Andrew akasema na kumfanya Vick acheke kwa nguvu.
“Kweli Andrew unaweza ukakata mtu kichwa kwa ajili yangu?
“Nakwambia ukweli Vick.Niko tayari kukata mtu kichwa kwa ajili yako” Akasema Andrew na kumfanya Vick aendelee kucheka.
“Inuka twende ndani darling.Hili ni gari la mama ametumiwa na dada kwa hiyo ameniachia nilitumie” Vick akasema wakati wakiinuka na kuelekea ndani.
Mara tu baada ya kuingia sebuleni simu yake inaita.Akaichukua na kuangalia mpigaji.Alikuwa ni Patrick.
“halo Patrick” akasema Andrew baada ya kuipokea simu ile.Vick ambaye alikuwa karibu akastuka na kugeuka.
“Patrick ! ina maana Parick amerudi? Akauliza na Andrew akamfanyia ishara kwamba anyamaze
“Andrew kuna jambo limejitokeza ninaomba msaada wako” Akasema Patrick
“jambo gani hilo? Andrew akauliza
“Nimeongea na mama muda mfupi uliopita.Amenitaarifu kwamba Vero anarejea leo saa nane za usiku na akanitaka kwenda kumpokea uwanja wa ndege.Kwa kuwa sikutaka mabishano na mama ikanilazimu kumkubalia kwamba nitakwenda huko uwanja wa ndege kumpokea Vero.Andrew sikufichi kwamba pamoja na kumkubalia mama lakini siko tayari bado kuonana na Vero kwa sasa.Ninaogopa mambo yanaweza yakaharibika mapema.kwa hiyo ninaomba kama hutajali unisaidie kwenda kumpokea Vero.Najua hili ni suala gumu kwako lakini sina mwingine ambaye ninaweza nikamkimbilia kwa msaada.naomba unisaidie kwa hilo” Patrick akasema na kumfanya Andrew akae kimya kwa muda.
“Andrew upo? Akauliza
“Nipo Patrick nilikuwa natafakari kidogo.Anyway nitakwenda huko uwanjani.Nitumie namba ya ndege atakayopanda.”
“nashukuru sana Andrew .Umenisaidia sana ndugu yangu.Hilo ni deni kubwa kwangu.Ngoja niwasiliane na mama anipe namba ya ndege atakayokuja nayo Vero” Patrick akasema na kukata simu.Andrew akabaki katika mawazo mengi,na mara akastuliwa na Vick
“Andrew hebu nieleze.Patrick amerudi?
“Ndiyo amerudi jioni ya leo”
“Alikuwa amekwenda wapi?
“Hakuniambia alikuwa wapi ila alichoniambia ni kwamba alikuwa nje ya mkoa kwa dharura”
“Nimesikia mkiongea kuhusu namba ya ndege.Nani anakuja na dege? Vick akauliza na kumfanya Andrew asite kujibu.
“Andrew niambie tafahdali nani anayekuja na ndege?
“Vero anarudi leo toka London kwa hiyo Patrick ameniomba niende nikampokee badala yake” Andrew akasema
“ Andrew are you out of your mind? Kwa nini yeye ambaye ndiye mpenzi wake asiende na akutume wewe? Vick akauliza
“Patrick hajisikii vizuri na ndiyo maana ameniomba nikampokee Vero badala yake.”
“No Andrew you are not going “ Vick akasema uso wake ukiwa umebadilika
“Unasemaje? Andrew akauliza
“You are not going. Andrew wakati umefika sasa wa kuyaacha mambo ya Patrick na Vero na kuangalia mambo yetu. Sisi tuna mambo mengi ya kukaa na kuongea kuhusu maisha yetu ya baadae. Leo hii nimekuja ili niwe na mpenzi wangu na mimi nifurahi lakini badala yake the whole night unakwenda kumpokea mpenzi wa rafiki yako.Is that fair? Vick akauliza. Andrew akamtazama mpenzi wake halafu akamsogelea karibu akamshika mabegani.
“Vick nimekuelewa. Hata mimi si kwamba ninapenda kuwa mstari wa mbele katika masuala ya Patrick na Vero na kusahau mambo yetu. You are always my everything. You are my breath and my life. Ninamshukuru Mungu kila siku kwa zawadi hii kubwa aliyonipa ya kuwa nawe.Nakupenda sana malaika wangu na niko tayari kufanya chochote kile kwa ajili ya kukufanya uwe ni mwenye furaha daima.Nafahamu umuhimu wako kwangu lakini Patrick he is my best friend.Mimi ni rafiki yake pekee anayeniamini kwa sasa.Sina namna ya kuweza kumkatalia kwa jambo aliloniomba kwa sababu yuko katika wakati mgumu mno kwa sasa na anahitaji msaada.Please let me do this for him and after this, I’m done.Mambo yake atayafanya yeye mwenyewe lakini kwa usiku wa leo naomba uniruhusu niende nikampokee Vero.”
Vick akamtazama Andrew kwa makini akasogea karibu akamkumbatia na kumbusu kisha akasema
“Usihofu baby nimekuelewa. Nitakusindikiza huko uwanja wa ndege siwezi kukuacha uende huko peke yako.lakini naomba uniahidi kwamba baada ya hili utaachana na mambo ya Patrick na kuelekeza nguvu katika mipango yetu”
Huku akitabasamu Andrew akasema
“I promise “
Vick akambusu tena na kusema
“Ok kabla hatujakwenda huko uwanja wa ndege twende kwanza chumbani.Nafasi yangu mimi ni ya kwanza kabla ya hao rafiki zako.” Vick akasema na taratibu wakaelekea chumbani
******************
Ni saa tano za usiku sasa lakini hakuhisi dalili zozote za kuonyesha kupata usingizi.Kila alipojaribu kufumba macho ni picha moja tu iliyokuwa ikimjia .Picha ya Patrick.Happy alishindwa kulala akaamka na kuketi kitandani.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Am I going crazy? Mbona najihisi kama vile siko kawaida? Patrick amenipa nini hadi nishindwe kupata usingizi kwa ajili yake? Kwa siku hizi chache nilizokaa naye Arusha amenifanya niwe kama chizi kwa ajili yake.Siku hizi chache nilizokuwa naye Arusha ndizo zilikuwa siku pekee zenye furaha katika maisha yangu.I lived my whole life in those few days.Sidhani kama nitarudi katika hali yangu ya kawaida bila ya kuwa na Patrick.Ni yeye tu ndiye atakayeweza kuniondolea uchizi huu ulionipanda kichwani .This is too much .This is beyond love.Nitafanya kila kitu kwa ajili ya kuwa naye.I swear I’m going to do anything to get him.He’s all mine.” Akawaza Happy ,akainuka akachukua glasi ya maji akanywa,akaichukua picha ya Patrick akaitazama akaibusu .
“Siwezi kupata usingizi bila kuisikia sauti ya Patrick.Sielewi ni kitu gani kimemfanya asinipigie simu wakati aliniahidi kwamba atanipigia usiku..” akawaza Happy huku akichukua simu na kupiga
“Hallo my angel” akasema Patrick
“Patrick my love, nimeshindwa kulala bila kuisikia sauti yako. Tafadhali usichelewe tena kunipigia simu mpenzi wangu. Kwa sasa siwezi kukaa muda mrefu bila kukuona na kuisikia sauti yako tamu.Its shame to say this but I’m crazy for you Patrick.” Happy akasema
“Ouh my angel,samahani sana kwa kuchelewa kukupigia simu hata hivyo nilikuwa katika maandalizi ya kukupigia simu muda si mrefu.Toka nimefika hapa nilikuwa katika shughuli za usafi kuiweka nyumba katika hali nzuri.”
“Pole sana Patrick.Kuanzia sasa fahamu kwamba siwezi kumaliza siku moja bila kukuona au kuisikia sauti yako nzuri.” Happy akasema
“nalifahamu hilo Happy na ndiyo maana nimekuahidi kufanya kila niwezalo ili kuhakikisha kwamba tunakuwa pamoja daima.Ni wewe tu ambaye unanifanya nijione kama malaika wa peponi.Ni wewe tu uliyeibeba furaha ya moyo wangu” Akasema Patrick
“ Vipi umeshaongea na Vero? Happy akauliza
“Vero alikuwa safarini ulaya na anarejea usiku wa leo.Nimeitisha kikao kesho na katika kikao hicho nitawaeleza kila kitu na kuuvunjilia mbali uchumba wangu na Vero.Nafahamu halitakuwa jambo rahisi lakini nimekwisha jiandaa kukabiliana nalolote litakalojitokeza.Usiumize kichwa kuhusu hilo.Muda si mrefu ile ndoto yetu itatimia”
“nafurahi kusikia hivyo Patick.Hata mimi kesho ndiyo nitaonana na Mike na nitamueleza ukweli.Mike ananipenda kwa hilo siwezi kuficha lakini sina namna nyingine yua kufanya zaidi ya kuachana naye.Ni mtu mwelewa na ninatumai atanielewa “ Happy akasema.
“Kwa hiyo mpaka kesho jioni tutakuwa na jibu lenye uhakika zaidi kuhusiana na suala hili gumu.Happy naomba uwe jasiri kwa sababu hii ni kwa ajili ya maisha yetu,kwa ajili ya furaha yetu.Kwa lolote litakalotokea,naomba uniahidi kwamba hautarudi nyuma.Tutashikamana pamoja hadi mwisho.”
“Kwa penzi zito nililonalo kwako ambalo haliwezi kulinganishwa na kitu chochote,kwa kuwa wewe ndiye mwanaume pekee niliyekukabidhi moyo wangu uutunze hadi mwisho wa maisha yangu,ninakuahidi kwamba sintarudi nyuma.Niko tayari kukabiliana na lolote lile ambalo linaweza kuwa kikwazo cha sisi kutimiza ndoto yetu ya kuwa pamoja.”
Happy akasema huku macho yake yakilengwa na machozi
“Nimekuelewa mpenzi wangu.naomba sasa ulale tutaonana kesho.Nitakupigia simu kesho asubuhi na mapema kukupa busu la asubuhi” Patrick akasema
“nashukuru sana malaika wangu .Sasa ninaweza kulala baada ya kuisikia sauti yako.Ah kabla sijasahu naomba uniimbie ule wimbo uliopenda kuniimbia kila siku kule Arusha” Happy akasema
“Wimbo upi? Patrick akauliza
“Ule wa Diamond Platinum..Lala salama”
Patrick akacheka na kuanza kumuimbia Happy wimbo ule mzuri luiomfanya Happy ahisi kama vile yuko na Patrick karibu yake..
Mlio wa simu ulimstua Patrick toka usingizini.Kitu cha kwanza alichokiangalia ni saa yake ya ukutani ambayo ilimuonyesha kwamba ilipata saa tisa na dakika nane za usiku.Akafikicha macho na kunyoosha mkono akaichukua simu yake iliyokuwa juu ya droo ya kitanda akatazama ni nani aliyempigia simu usiku ule mkubwa .Ilikuwa ni namba ya simu ya Vero.Patrick akakunja uso
“tayari ameshafika.Sijui anataka kuniambia kitu gani.Ngoja nipokee nimsikilize”
“Hallo “ akaita Patrick baada ya kubonyeza sehemu ya kupokelea
“Hallo my love.Unaendeleaje? Vero akauliza
“Naendelea vizuri Vero.Umeshatua?
“Nimeshatua niko kitandani hapa” akasema Vero kwa sauti laini
“Pole na safari” akasema Patrick
“Nimekwishapoa mpenzi wangu.Pole sana kwa kutojisikia vizuri.Nilitegemea kukuona uwanja wa ndege lakini nikamkuta Andrew na Vick peke yao nikaambiwa kwamba umeshindwa kufika kunipokea kwa sababu hukuwa unajisikia vizuri.Vipi maendeleo yako kwa sasa? Vero akauliza
“Naendelea vizuri Vero.” Patrick akajibu.
“nashukuru kama unaendelea vizuri.safari yangu ilikuwa nzuri.Dada na shemeji wanakupa salamu nyingi na wanakutakia uponaji wa haraka.Wameahidi watakuwepo siku ya harusi yetu.”
“Ahsante sana” Patick akajibu kwa ufupi
“Darling are you ok? Vero akauliza
“I’m ok Vero.Kwani vipi? Patrick akajibu
“Ninaona sauti yako haiko kawaida.Naona kama bado hauko sawa.Nini kinakusumbua mpenzi wangu? Nilitaka nije moja kwa moja kwako ili niwe nawe usiku huu lakini Andrew akanikataza akaniambia nikuache upumzike.Baby najisikia vibaya sana kuwa mbali nawe hasa katika kipindi hiki ambacho haujisikii vyema” akasema Vero
Patrick akavuta pumzi akafikir kidogo na kusema
“Usjali Vero.Mimi ninaendelea vizuri .Usihofu kitu”
“najua unaniambia hivyo ili kunitoa wasi wasi .Ngoja nikuache ulale upumzike.Nilitaka kukufahamisha kwamba tayari nimesharudi .Nitakuja kukuona kesho asubuhi kabla sijafanya kitu chochote kile.Sintakuwa na amani ya moyo bila kukuona.Niliondoka bila kukuona na siku zote nimekuwa roho juu juu nikikuwaza wewe mpenzi wangu.Patrick nakupenda sana na sintaweza kuishi bila kuwa nawe.Usiku mwema mpenzi.I love you”Vero akasema
“Bye baby” akajibu Patrick na kuitupa simu pembeni.
“Laiti angejua ninavyomchukia asingethubutu hata kunipigia simu.Angeniogopa kama ziraeli.” Akawaza Patrick wakati akijifunika vizuri
“vero ni mwanamke mzuri,ana roho nzuri ya ukarimu, ni mrembo,msomi na ana kila sifa ya kuwa mke.Sikutegemea kama kuna siku itanitokea nikamchukia kama ilivyonitokea sasa.Kitendo cha kunitenganisha na mtu niliyeyatoa maisha yangu kwake kimeniuma sana.Maumivu niliyoyapata wakati ule sitaki kuyakumbuka.Niliumia sana.Niliteseka kupita kiasi kwa kuamini kwamba ni kweli Happy amenisaliti.Ilinichukua muda mrefu maumivu yale kunitoka moyoni mwangu .Happy naye aliteseka kiasi kikubwa sana baada ya kusikia kwamba mtu pekee ambaye alikuwa akimpenda amefariki dunia.Mateso na maumivu aliyotusababishia Vero ni makubwa sana na kwa hili sidhani kama nitamsamehe.Dunia nzima haitanielewa ni kwa nini nimechukua maamuzi haya lakini sintajali mtu yeyote.Maamuzi niliyoyachukua hakuna mtu anayeweza kuyabadili.Lazima niachane na Vero na kuendelea na mtu ninayempenda maishani.Happy ndiye mwaname pekee mabaye nimepangiwa niwe naye katika maisha yangu na si huyu mlaghai Vero.” Patrick akawaza akiwa amejilaza pale kitandani.Akasikia hasira nyingi akaamka na kwenda kuchukua glasi ya maji akanywa na kurudi tena kitandani.
*********************CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kengele ya mlangoni ndiyo iliyomstua Patrick toka usingizini.Akaangalia saa ya ukutani ilioyesha ni saa tatu za asubuhi.Akajinyoosha na kwa uchovu akatoka mle chumbani na kuelekea mlangoni.Akafungua mlango mdogo wa geti na kukutana na sura yenye tabasamu pana sana ya Vero ambaye alimrukia na kumpa mabusu mengi
“Ouh my love nimefurahi sana kukuona tena mpenzi wangu” akasema Vero kwa furaha huku akimkumbatia Patrick kwa nguvu.
“karibu sana Vero” Patrick akasema .Akalifungua geti na Vero akaingiza gari lake. Na kisha akatoa begi kubwa na kulivuta kuelekea ndani.
“Darling hizi zote ni zawadi nilizokuletea toka uingereza.” Akasema Vero na kumfanya Patrick atabasamu
“nashukuru sana Vero” Patrick akajibu na kwenda kukaa pembeni ya Vero.Wakatazamana kwa sekunde kadhaa.
“Unajisikiaje leo mpenzi wangu? Vero akauliza akiwa ameiweka mikono yake shingoni kwa Patrick
“Najisikia vizuri sana leo.Unajua wewe ndiye dawa yangu.Umekuja na nimepona kabisa” akasema Patrick na kumfanya vero atabasamu na kumkumbatia kwa nguvu.
“Nimekwambia hivyo kukupa moyo tu lakini siku ya leo haitaisha kabla hujalia machozi ya damu” akawaza Patrick.
Wakiwa bado wamekumbatiana ,simu ya Patrick ikaita.Akaichukua na kutazama mpigaji.Alikuwa ni mama yake.
“mama shikamoo”
“marahaba mwanangu hujambo?
“sijambo mama”
“Unaendeleaje? ” akauliza mama Patrick kwa sauti ya upole isivyo kawaida yake.
“mama ninaendelea vizuri sana”
“sasa mwanangu mbona jana hukwenda kumpokea mwenzio? Kwa nini unamfanyia hivyo mwenzako?
“mama nilishindwa kwenda kule uwanjani kwa sababu sikuwa najisikia vyema na ndiyo maana nikamuomba Andrew aende akampokee Vero badala yangu”
“yaani kwenda kumpokea mwenzako hapo uwanjani hujisikii vizuri .mbona kwenye dharura zako husemei kwamba hujisikii vizuri? Mama Patrick akauliza huku sauti ikianza kubadilika na kuwa ile ya ukali iliyozoeleka.
“mama si kwamba nilifanya makusudi kutokwenda kumpokea Vero.Nilikuwa naumwa na ndiyo maana nikamuomba Andrew aende badala yangu.” Patrick akajibu
“Sawa baba nimeshakuelwa manake ukiendelea utaanza kuzungumza vingereza vyako halafu tukashindwa kuelewana.Usichelewe leo kwenye kikao .Tayari kila mtu nimeshampa taarifa na nimewasisitiza kwamba wasikose.”
“haya mama tutaonana mida hiyo.Msalimu baba” Patrick akasema na kukata simu
Wakati Patrick akiongea na mama yake vero alikuwa ameingia bafuni.Aliposikia tayari Patrick amemaliza kuzungumza na simu akatoka mle bafuni akiwa amejifunga taulo na kumfuata Patick pale kitandani akaanza kumtoa zile nguo za kulalia ambazo bado Patrick alikuwa amezivaa.
“Ratiba ya leo itakuwa kama ifuatavyo.Kitu cha kwanza tunatakiwa tukaoge pamoja halafu tupate stafstahi halafu tutajifungia chumbani kwetu siku nzima ya leo” akasema vero akilivua shati la Patrick na kuliweka pembeni.
“Ulimtaarifu mama kwamba sikufika kukupokea uwanja wa ndege? Patrick akauliza
“Nilimpigia simu usiku kumtaarifu kwamba nimeshatua kwa sababu aliniomba nikishafika salama nimfahamishe.Aliniuliza kama ulikuwepo uwanjani nikamwambia kwamba hukuweza kufika kutokana na kutokujisikia vizuri.Samahani kama nilikosea kwa hilo” Akasema Vero huku akimshika Patrick mkono na kumuongza kuelekea bafuni.
“Patrick nilipokuwa safari nilikuwa nikiweweseka kila usiku nikilitaja jina lako mpaka watu wakashangaa umenipa kitu gani cha kunifanya nikupende kiasi kikubwa namna hii.Naomba nikiri kwamba sintaweza kuishi bila kuwa nawe.Wewe ndiye pumzi yangu,wewe ndiye maisha yangu,wewe ndiye kila kitu kwangu.Bila wewe siwezi kitu.” Akasema Vero huku akiutembeza mkono wake taratibu katika kifua cha Patrick wakiwa katika jakuzi.Patrick akamuangalia Vero kwa sekunde kadhaa akataka kusema kitu lakini Vero akamuwahi na kumuwekea kidole mdomoni.
“shhhhhhhh…..Don’t say anything” akasema vero na kutoa kidola kile na taratibu akakisogeza kichwa chake karibu na kuigusanisha midomo na kutoa busu moja zito ,halafu akatoa ulimi na kuilamba midomo ya Patrick.Wakari akifanya hivyo alikuwa akilisugua sikio la kushoto kwa mkono wake wa kulia kwa ufundi mkubwa.Sehemu hii ndiyo ambayo huwa inayaamsha mashetani ya Patrick.Kama Vero alivyokuwa amekusudia Patrick akaanza kuhema mfululizo huku akitoa mguno Fulani kwa raha aliyokuwa akiisikia.Akashindwa kuvumilia na kumvuta Vero karibu zaidi.Wakati wakiendelea kunyonyana ndimi simu ya Patrick ikaanza kuita kule chumbani.Mlango wa bafuni haukuwa umefungwa hivyo aliweza kuisikia simu yake vizuri ikiita
“Vero ngoja kwanza nikapokee simu.Anaweza akawa ni mtu muhimu ananipigia”
“No Patrick.No phone calls at this time.Its only me and you” akasema Vero huku akiendelea na mautundu juu ya mwili wa Patrick.
“Anaweza akawa ni Happy ndiye anapiga.Nisipoipokea simu yake atajiuliza maswali mengi “ akawaza Patrick.
Simu ile ikaita na kukata.Ikaita na kukata tena .Ikaanza kuita kwa mara ya tatu.Patrick akamsukuma Vero pembeni akainuka na kukimbia huku akichuruzika maji kuelekea chumbani .Kabla hajaifikia simu ikakatika.Akachuka na kutazama mpigaji alikuwa ni Happy.Akaishikilia simu ile kwa dakika nzima akijiuliza kama ampigie Happy ama la.
“Nitampigia baadae.Siwezi kumpigia wakati Vero yupo.Hii inaweza ikaharibu kila kitu.Nataka nikamalize mambo yote mbele ya wazee” akawaza Patrick na kuiweka simu yake mezani akarudi bafuni.
“Nani aliyekusumbua namna hiyo kwa kukupigia simu wakati kama huu na kuharibu starehe zetu? Akauliza Vero
“Foregt about it…Kuna jamaa mmoja nilikuwa na miadi ya kuonana naye leo jioni lakini sintaweza kuonana naye kutokana na kikao tutakachokihudhuria ”
“Kikao !! “ Vero akauliza kwa mshangao
“Ina maana hauna taarifa kwamba kikao cha mwisho kinakaa leo ? Saa tisa za alasiri itatubidi tuelekee sote katika kikaohiki.Taarifa zimekwisha sambazwa kwa kila mhusika awepo katika sherehe hii”
“Ouh basi hiyo ni habari nzuri .Hakuna shaka tutahudhuria ili tuweze kuona mpaka sasa maandalizi ya harusi yamefikia wapi.” Akaseam Vero huku akimshika mkono Patrick na kuimvutia katika jakuzi ili waendelee kuoga.
“Vero No! Siwezi kufanya hivyo tena.Sina hamu tena.Tumalizie kuoga tukapate kifungua kinywa.”
Vero akamuangalai Patrick kwa jicho kali lakini hakuwa na la kufanya.wakamaliza kuoga na kuelekea chumbani .
***************************
Mlango wa chumba cha Happy ukagongwa na kumfanya astuke toka usingizini.Akajiinua kitandani na kutembea taratibu huku akifikicha macho na kwenda kuufungua.Alikuwa ni mdogo wake Margreth.
“Wow ! Margreth “ Happy akasema huku akitabasamu
“Ouh Happy…” Magreth akaruka ruka kwa furaha na kumkumbatia dada yake.
“habari za Arusha? Yaani Happy unarudi hutaki hata kunijulisha kama umesharudi” akasema Margreth
“Samahani kwa hilo mdogo wangu.Nilirudi jana jioni na mama akanieleza kwamba umepata kazi katika kampuni ya mtandao wa simu na umeingia zamu ya usiku.Sikutaka kukusumbua kwa sababu nilifahamu lazima tutaonana asubuhi..Kwanza hongera kwa kupata kazi nzuri “ Happy akamwambia mdogo wake.
“nashukuru Happy.Niko upande wa huduma kwa wateja.kazi yangu ni kupokea simu za wateja,kupokea malalamiko ya wateja na kuyawasilisha sehemu husika.Nipe habari za Arusha..naona mambo yalikwenda vizuri kiasi kwamba ukasahau hata kunitaarifu kinachoendelea”
“Margeth ,kwanza kabisa napenda nikushukuru sana kwa kazi kubwa uliyoifanya ya kuniunganisha tena na Patrick.Sikutegema kama ningeweza kumuona tena Patrick maishani mwangu .Mara tu nilipofika katika hoteli ile ya Kobe Village nilikuta tayari Patrick amekwisha fika muda mrefu akinisubiri.Nilipomtia machoni sikuamini kama kweli ni yeye.Nilishindwa kujizuia nikaanza kulia.Nililia sana kwa sababu tayari nilikwisha poteza matumaini ya kuonana naye tena.Kwangu mimi ilikuwa ni kama muujiza mkubwa .Kwa ufupi kwa siku hizi chache nilizokaa na Patrick Arusha nilihisi kama niko peponi kwa raha ya ajabu niliyokuwa nayo.”
Margreth akamtazama dada yake huku akitabasamu na kisha akasema
“Ulimuuliza ni kwa nini aliamua kutangaza amekufa kumbe sivyo?
“Ndiyo nilimuuliza kuhusu jambo hilo na akashangaa sana kwani hakuwahi kufanya jambo kama hilo.Yeye pia aliniuliza ni kwani nini niliamua kumuacha gerezani na kuolewa na mzungu ambaye nilizaa naye mtoto mmoja.Nilistuka sana baada ya kusikia kitu kama hiki.Nilimuuliza alipata wapi taarifa kama hizo.Nilimuonyesha barua niliyotumiwa ikinieleza kwamba amefariki dunia.Akaisoma barua ile na kwa bahati nzuri akafanikiwa kuutambua mwandiko wa mtu aliyetuma ile barua.Kwa mujibu wa maelezo yake ni kwamba baada ya kuhamishwa gereza alikutana na dada mmoja aitwaye Vero ambaye alifika hapo gerezani kumsalimu mjomba wake aliyekuwa mkuu wa gereza jipya alilohamishiwa Patrick.Kwa kuwa kila siku Patrick alipangiwa kwenda kufanya shughuli za usafi nyumbani kwa mkuu wa gereza alijikuta akizoeana na Verona wakawa marafki.Muda wa Vero kuwepo pale ulipokwisha ilimlazimu kurejea jijini Dar es salaam na hivyo Patrick akamuomba amtumie kama kiungo baina yangu na yeye.Vero akakubali lakini kumbe alikuwana lake moyoni.Akatunga uongo ule kwa kunitaarifu kwamba Patrick amefariki dunia na halafu akamweleza Patrick kwamba mimi nimemsaliti kwa kuamua kuolewa na mzungu na kumuacha yeye akiozea gerezani.Margreth niliumia sana baada ya kusikia hivyo. Siwezi kuelezea ni maumivu gani aliyoyapata Patrick baada ya kusikia eti nimemsaliti na kuolewa na mwanaume mwingine.Patrick alifungwa gerezani kwa sababu ya upendo wake kwangu.Alifungwa baada ya kuua bila kukusudia kwa kuniokoa mimi nisidhalilishwe na wale wahuni sasa iweje leo niamue kumtelekeza gerezani na kuolewa na mwanaume mwingine? Ni jambo ambalo haliingii akilini lakini Vero alilifanya likaonekana ni kweli “ Happy akasema na kumtazama mdogo wake.
“Pole sana Happy.Kumbe hivyo ndivyo mambo yalivyokuwa !! “ Margreth akashangaa.
“Siamini kama dunia hii kuna watu wenye ukatili wa namna hii.Jambo alilolifanya huyu Vero ni baya sana ambalo lingeweza kusababiosha hata mmoja wenu akajitoa uhai.Hebu niambie Vero alifanya ubaya huu kwa sababu ya nini? manake hata mimi nimesikia uchungu sana kwa ukatili huu alioufanya Vero.” Margerth akaulizaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ sababu kubwa ni kwamba alimpenda Patrick na akautumia umbali uliokuwepo baina yetu kututenganisha.Kweli alifanikiwa alichokuwa akikihitaji.Amefanikiwa kuwa na Patrick na kikubwa ni kwamba mwezi ujao wanafunga ndoa.” Happy akasema na kumfanya Margerth astuke.
“Ama kweli siku hizi binadamu ni wakatili kuliko hata wanyama.Kumbe uongo wote huu mkubwa ni kwa ajili ya kumpata Patrick ! loh ! “ margerth akasikitika sana.
“lakini siku zote kitu alichokipanga Mungu binadamu hawezi kukipangua.” Happy akasema
“kwa nini unasema hivyo Happy? Margreth akauliza
“Si unaona mambo yalivyojitokeza. Nimekutana na Patrick katika mazingira ambayo sikutegemea.Uongo wa Vero umegundulika muda mfupi kabla ya ndoa yake.Hii ina maana kwamba Mungu hakupendezwa na kitu alichokifanya Vero.Baada ya kuonana na Patrick kwa mara nyingine tena imenibidi nikubaliane na ukweli kwamba sina uwezo wa kumtoa Patrick moyoni mwangu.Yeye ndiye mwanaume pekee anayestahili nafasi katika moyo huu”
“Happy unamaanisha nini unaposema hivyo? Margreth akauliza. Happy akamshika bega na kumtazama machoni kwa makini.
“Nimeamua kuachana na Mike.”
“What !! Margreth akastuka
“Toka moyoni mwangu nimeamua kuachana na Mike na kuendelea na Patrick.”
“Happy sidhani kama inawezekana.Mike tayari amekwisha kuvisha pete ya uchumba.Itawezekana vipi umwambie kwamba umekusudia kuachana naye? Kingine kinacholifanya suala hili kuwa gumu zaidi ni kama ulivyosema kwamba Patrick na Vero wako katika maandalizi ya mwisho ya kufunga ndoa.Unadhani itawezekana vipi kuwatenganisha ?
Happy akatabasamu na kusema
“Itawezekana Margreth.Baada ya kugundua kilichotokea tulijadili suala hii kwa undani na kufikia uamuzi mmoja kwamba hakuna kitu cha kuweza kututenganisha,tukaamua kwa kauli moja kwamba tunaachana na wapenzi wetu wa sasa na kuurudisha uhusiano wetu wa awali.Nitamueleza Mike na nina imani atanielewa.Patrick naye atafanya hivyo hivyo na ataachana na Vero.” Happy akasema na kuichukua simu yake akazitafuta namba za Patrick na kupiga .
“Unampigia nani simu? Margreth akauliza
“Ninampigia Patrick.nataka kufahamu maendeleo yake” akajibu Happy
Simu ikaita na kukata,ikaita tena mara ya pili bila kupokelewa,hakukata tamaa akapiga tena mara ya tatu lakini bado simu haikupokelewa.
“Hapokei simu nadhani atakuwa yuko mbali na simu yake” akasema Happy
“Happy mimi sina tatizo na maamuzi yoyote utakayoyachukua .Najua unahitaji kuwa na furaha maishani na kama Patick ndiye mtu pekee ambaye unaamini atakupa furaha ya maisha ,sina kipingamizi na hilo.lakini ninachokihofia ni kwamba katika maamuzi haya mliyoyachukua watu wengi wataumia.Nina wasi wasi mkuwa na hilo.Mwezi mmoja umebaki Patrick na Vero wafunge ndoa kwa maana hiyo maandalizi yatakuwa yameshafanyika ya kutosha.Kitendo cha Patrick kutangaza kuivunja ndoa kati yake na Vero kitawaumia watu wengi na wengi watakuchukia kwa kuamini kwamba wewe ndiye chanzo cha haya yote.Sitaki uingie katika mtafaruku mwingine dada yangu.Sipendi kukuona ukiw akatika mateso na maumivu.Umekwisha lia kiasi cha kutosha dada yangu” Akasema Margreth.
“Margreth nakubaliana nawe kwamba suala hili ni gumu na litawaumiza watu wengi sana lakini tayari tumeshafanya maamuzi na hakuna kurudi nyuma .Niko tayari kukabiliana na chochote kile .Mambo mengi yatajitokeza lakini nitakabiliana nayo” akasema Happy kwa kujiamini
“Nitakutana na Mike baadae na nitaitumia nafasi hiyo kumweleza ukweli na nina imani atanielewa na kuniacha huru ili niweze kuwa na mtu ninayempenda kuliko wote katika maisha yangu” Happy akasema na Margreth akamtazama dada yake kwa huruma.
Saa sita za mchana gari ndogo nyeupe yenye namna za ubalozi wa Marekani ilisimama mbele ya nyumba ya akina Happy na kijana mmoja mtanashati aliyevalia suti nzuri nyeusi iliyomkaa vyema akashuka.Alikuwa ni kijana mwenye sura nzuri sana na ambaye ni wazi alikuwa akiwasisimua mabinti kila apitapo.Huyu alikuwa ni Mike mchumba wa Happy.kwa uzuri aliokuwa nao happy alistahili kuwa na kijana kama huyu
Margreth ambaye alikuwa amekaa sebuleni akatoka kwa kasi na kwenda kumpokea shemeji yake na kumkaribisha ndani.Mike akasalimiana na familia yote kisha akaletewa kinywaji na kuanza kunywa taratibu wakati akimsubiri Happy aliyekuwa chumbani kwake akijipamba.
“ Mike amekuja yuko sebuleni anakusubiri” Margreth akamwambia Happy baada ya kumfuata chumbani kwake.
Baada ya kupokea taarifa ile toka kwa Margreth Happy akakaa kitandani na kupumua kwa nguvu.Akauweka mkono wake mahala unapokaa moyo .Alipatwa na mawazo mengi ya ghafla.
“happy kulikoni? Margreth akamuuliza dada yake baada ya kuona namna alivyonyong’onyea ghafla
“Maggy nahisi miguu mizito sana kwenda kuonana na Mike.nashindwa nitaanzaje kumweleza kuhusiana na suala la kuachana.Nina wasi wasi mkubwa”
Margreth akamtazama dada yake na kusema
“happy huna sababu ya kuogopa.Hii ni kwa ajili ya furaha ya maisha yako.Kama kweli una nia ya dhati ya kuachana na Mike ili uwe na Patrick usisite kufanya hivyo.Huu ndio wakati wako.Umeipata nafasi naomba uitumie.Usisubri nafasi nyingine ijitokeze.Mueleze Mike ukweli na nina imani ni mtu mwelewa sana na atakuelewa vizuri.Najua ugumu uliopo katika kufanya hivyo hasa kwa mtu ambaye tayari mmeshakuwa wapenzi kwa muda wa miaka mingi na tayari mmeshaingia katika uchumba lakini kama ulivyosema kwamba chaguo lako ni Patrick basi huna budi kuachana na Mike.kwa maana hiyo basi vuta pumzi ndefu inuka hapo kitandani nenda kaonane na Mike,mtoke kwa chakula cha mchana na uitumie nafasi hiyo kumueleza Mike ukweli kuhusiana na msimamo wako huo.Kama kutakuwa na tatizo lolote lile nipigie simu nitakufuata haraka sana.”
Maneno yale ay Margreth yanamfanya Happy atabasamu na kisha akamkumbatia mdogo wake.
“nashukuru sana Maggy kwa kunipa moyo.Ninakwenda kuonana na Mike.” Akasema Happy huku akiichukua pochi yake nogo na kujiangalia kwa mara ya mwisho katika kioo.Akaufungua mlango wa chumba chake akatoka na kuelekea sebuleni.Mara tu alipotokeza sebuleni Mike alishindwa kuvumilia na kwa kasi akainuka na kumkumbatia Happy kwa nguvu.
“Ouh malaika wangu. Nafurahi nimekuona tena.Ningeingiwa na uchizi kama siku aya leo ingekwisha bila kuitia machoni sura yako nzuri” akasema Mike huku akimshika mkono Happy na kumketisha sofani
“habari yako Mike.habari za Marekani? Hajambo Michelle? Happy akauliza
“habari za Marekani ni nzuri.Michelle ni mzima ila mimi ndiye nilikuwa mgonjwa.Nilikuwa nikiumwa ugonjwa wa kutoiona sura yako lakini kwa sasa nimepona baada ya kukutia machoni.” Akasema Mike na wote mle sebuleni wakacheka.Mama yake Happy akainuka na kuondoka kuelekea chumbani kwake na kuwaacha vijana wake pale sebuleni.
“Happy mpenzi wangu vipi maendeleo yako? Mike akauliza huku ameushikilia mkono wa happy
“namshukuru Mungu ninaendelea vizuri sana” Hapy akajibu
“Nashukuru kama unaendelea vizuri.Nilipata taarifa kwamba ulipatwa na maradhi ya ghafla baada ya kulitwaa taji la Miss Tanzania.Niliogopa sana ikanilazimu kuchukua likizo ya ghafla na kuja hapa kuungana nawe katika kipindi hiki ambacho nina imani ulihitaji sana uwepo wangu.Hongera sana kwa kufanikiwa kulitwaa taji hili kubwa la urembo.Nina zawadi nzuri sana kwa ajili ya ushindi wako huo” akasema Mike na kumfanya Happy atabasamu
“ahsante sana Mike kwa kuja kunifariji.Ni kweli nilipata kitu kama mstuko Fulani baada ya kutangazwa mshindi wa taji lile la Miss Tanzania.Sikuwa nimetegemea kama ningeweza kulitwaa taji lile kutokana na ushindani mkubwa uliokuwepo baina ya washiriki.Baada ya hali ile kunitokea ilinilazimu kuchukua siku kadhaa za mapumziko na kuwa mwenyewe kwa ajili ya kuweza kutafakari na kujipanga namna nitakavyoweza kuishi maisha mapya na namna nitakavyoweza kulibeba jukumu hili kubwa nikiwa kama mrembo wa Tanzania.Nashukuru kwamba ninaendelea vizuri kwa sasa .ahsante kwa zawadi yako” Happy akasema na kisha kikapita kimya kifupi
“vipi uko tayari kwa kutoka? Tulikubaliana kwamba leo tutatoka kwa ajili ya chakula cha mchana .” Mike aksema
“Niko tayari Mike tunaweza kutoka” Happy akajibu na kisha Mike akamshika mkono Hapyy wakatoka wakaingia garini na kuelekea mahala ambako Mike alitaka waende wakapate chakula
“Happy nimefurahi sana kwa kukuona tena.Huwezi kujua ni furaha ya namna gani ambayo ninayo kwa kuwa nawe tena .Kwa mahala nilipofika sasa sintaweza kuishi bila kuwa nawe.Niko tayari kufanya kila kitu ili mradi niwe nawe.Niko tayari kuacha hata kazi ninayoifanya kule Marekani kwa ajili ya kuwa nawe .Ninakupenda sana Happy “ Mike akasema wakiwa garini kuelekea hotelini.Happy akatoa kitambaa katika mkoba wake akafuta jasho lililokuwa likimtoka.Alikuwa akitokwa jasho kutokana na mtihani mgumu aliokuwa nao juu ya kuusitisha uhusiano kati yake na Mike.
“Mungu nisaidie.Niko katika mtihani mgumu sana wa kumueleza Mike ukweli kwamba nimekutana na Patrick na nimeamua kurudiana naye.Mike ananipenda sana na sijui nitaanzaje kumueleza ukweli kwamba hatutaweza kuendelea tena na uhusiano wetu.” Happy alizama katika mawazo na ghafla akastuliwa na sauti ya Mike
“Unawaza nini mpenzi wangu? Halafu mbona jasho linakutoka sana?
“ Ni hili joto la Dar “ happy akasema
“Ni kweli hata mimi ninalisikia joto kali sana.Ningejua ningechukua gari la wazi “ akasema Mike Happy hakujibu kitu akatabasamu.
Walifika hotelini ambako tayari Mike alikwisha weka oda ya meza moja maalum kwa ajili yake na Happy.Wakaonyeshwa meza yao na kwenda kukaa na kisha wakaagiza chakula .Wakati wakisubiri chakula kiwe tayari,walikuwa wakiendela kuburudika kwa vinywaji
“Happy bado naendela kukupa hongera zangu kwa kushinda taji la mrembo wa Tanzania.Siku zote nilikuwa nikiamini kwamba una vigezo vyote ya kuwa mrembo mwenye jina kubwa lakini niliogopa kukwambia kuhusiana na masuala ya urembo kwa sababu toka nimekufahamu sijawahi kusikia hata mara moja ukigusia kwamba unapenda mambo ya urembo.” Akasema Mike
“Mike ni kweli sijawahi kukutamkia kwamba ninapenda urembo lakini toka siku nyingi nilikuwa nipenda sana mambo haya ya urembo japokuwa nilikuwa bado sijaamua kujiingiza rasmi katika fani hii.Kuna mtu aliniona akanishauri nijaribu kushiriki mashindano ya miss Tanzania na kweli nikajaribu na nikashinda.” Happy akasema huku akitabasamu.
Chakula kikaletwa wakala na baada ya kula wakaendelea na maongezi mengine.kadiri muda ulivyokuwa ukisonga na ndivyo Happy alivyozidi kuwa na wasi wasi mwingi hali iliyomfanya Mike kugundua kwamba kuna jambo ambalo haliko sawa.Akamuuliza kama kuna jambo linamsumbua.
“hapana Mike hakuna jambo linalonisumbua.Unajua kwa sasa kila nionekanapo ninakuwa nikipigwa picha na waandishi wa habari.Ndiyo maana ninakuwa sina imani kila mahala ninapokuwa” Happy akajibu
“Suala hilo lisikuumize kichwa mpenzi wangu.Kwa sasa wewe ni mrembo wa taifa na ni kioo cha jamii.Hutakiwi kujificha.Unatakiwa kutoka na kuchangamana na jamii inayokuzunguka.usiwe na wasi wasi kuhusu jambo la kupigwa picha ni suala la kawaida” Mike akasema na kisha wakaendelea na maongezi mengine.
*****************************
Saa tisa za alasiri tayari viti vyote vilivyokuwa vimeandaliwa kwa ajili ya wale wote waliokuwa wamealikwa kuhudhuria kikao hiki cha mwisho cha maandalizi ya harusi.ya Patick na Vero vilikuwa vimejaa.Kikao hiki kilichojumuisha kamati nzima ya maandalizi ya harusi hii pamoja na ndugu wengine muhimu ambao Patrick alikuwa amependekeza wawepo katika hiki kikao ambacho yeye alikiita ni muhimu sana .
Saa tisa na dakika ishirini gari la Patrick likawasili katika nyumba ya wazazi wake ambako ndiko kikao hiki cha leo kilikuwa kikifanyikia.Toka ndani ya ile gari wakashuka Patrick na Veronika na kuanza kupiga hatua kuelekea ndani.Ni wao pekee waliokuwa wakisubiriwa.katika kikao kile.
Mara tu walipoingia bustanini ambako ndiko kikao kilikuwa kifanyikia vikasikika vigere gere vingi na watu wakaanza kushangilia.Wote waliamini kwamba muda si mrefu tayari familia hizi mbili zingeungana na kuwa kitu kimoja.Akina mama walipiga vigere gere na kushangilia kwa nguvu baada ya kuwaona Patrick na Vero pamoja.
Moja kwa moja Patrick akaanza kwanza kusalimiana na baba yake ambaye hakuwa ameonana naye kwa muda mrefu kidogo na kisha akamsalimu mama yake Vero na ndugu wengine na baada ya zoezi hilo wakachukua nafasi zao.
Mwenyekiti wa kikao kile ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati ya maandalizi akafungua kikao kwa sala fupi na kisha akawakaribisha wote katika kikao kile.Baada ya kufungua kikao kile akatoa taarifa ya kamati kuhusiana na maaandalizi yote ya harusi ile kwa ujumla.Baada ya kuisoma taarifa ile ya jumla ,mwenyekiti akawakaribisha wenyekiti wa kamati ndogo ndogo ili nao waweze kutoa ripoti zao na kisha wote kwa pamoja waweze kuangalia kama kuna sehemu yoyote yenye mapungufu ili waweze kuyafanyia kazi.Kabla hajasimama mtu yeyote kuongea Patrick akasimama na kuomba kuongea machache.
“ Wapendwa sana wazazi wetu,ndugu wote mliohudhuria kikao hiki,ndugu wanakamati wote mabibi na mabwana nilikuwa nimeomba nafasi ya kusema machache katika kikao hiki hivyo kabla mambo mengine hayajaendelea naomba niitumie nafasi hii niseme mambo machache sana kwenu nyie ndugu zangu.Kwanza nawashukuru sana kwa namna mlivyojitolea kwa kila hali kuhakikisha kwamba maandalizi ya harusi yangu yanakamilika.Nawashukuru sana kwa jitihada zenu na ushirikiano wa kila mmoja wenu.Sina kitu chochote cha kuwalipa ni mwenyezi Mungu pekee atakayewalipa.Jambo la pili ninalotaka kulisema hapa ni jambo ambalo linahusu historia yangu kwa ujumla.Ni jambo linalonihusu mimi na maisha yangu.Wengi bado hamjafahamu historiia yangu ,wapi nimetoka hadi leo hii tuko hapa pamoja mkinisaidia kuandaa harusi yangu.Sitaki kuchukua muda mrefu sana ila naomba nitumie dakika chache kuwakumbusha japo kwa muhtasari nimetoka wapi hadi nilipo hivi sasa.” Patrick akasema na kuwafanya watu wote wajiulize nini anataka kuwaambia.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Historia ambayo katu haitaweza kufutika maishani na itaendelea kuwapo kichwani mwangu daima ni siku ile ambayo nilihamia katika shule ya sekondari Malangali Iringa nikitokea shule ya Mazwi sekondari Sumbawanga ambako wazazi wangu walikuwa wakiishi na kufanyakazi kule kama watumishi wa umma.Nakumbuka nikiwa katika kituo cha magari yaendeayo katika kijiji cha malangali nilikutana na msichana mmoja ambaye naye alikuwa akielekea huko.Msichana huyu ambaye kwa jina aliitwa Happy baadae alikuwa rafiki yangu mkubwa sana.”
Wazazi wa Patrick wakatazamana.Kila mmoja alikumbuka mbali sana .Vero alionyesha mstuko wa dhahiri.Patrick akaendelea
“ msichana huyu alitokea kuwa rafiki yangu mkubwa kwa sababu ni mimi pekee ambaye nilimuelewa na kumuamini.Happy alikuwa akisemekana kwamba ni muathirika wa virusi vya ukimwi na hivyo wanafunzi wote wakamtenga.Kati ya wanafuni wote ni mimi pekee ambaye nilimuamini aliyonieleza kwamba hakuwa muathirika kama alivyokuwa amezushiwa bali alikuwa na matatizo ya kiafya.Nilifanya kila nilivyoweza na nikafanikiwa kumfanya Happy asikate tamaa na hivyo akaanza kusoma tena kwa bidii na kuanza kushika nafasi za juu kimasomo.Kitendo hiki hakikuwafurahisha wanafuni wengi na hivyo kuzidisha chuki na uhasama.Sitaki kueleza kila jambo kwa sababu ni mambo mengi yalitokea lakini katika kila jambo nilisimama imara kumtetea na sikuwa tayari kuona Happy akinyanyaswa.” Patrick akanyamaza akameza mate .Kila mtu alikuwa akaishangaa ni kitu gani alichokuwa akikiongea Patrick.
“ Ilitokea siku moja kulikuwa na muziki wa disko pale shuleni.Nikiwa sina hili wala lile kumbe kuna baadhi ya wanafunzi watukutu walikuwa wameunda mpango wa kutaka kumdhalilisha Happy.Tukiwa tumekaa peke yetu tulivamiwa ,nikapigwa na kitu kizito kichwani nikapoteza fahamu baada ya hapo Happy akapelekwa katika kichaka na wahuni wale wakaanza kujiandaa kumfanyia vitendo vya udhalilishaji.kwa bahati nzuri nilipata fahamu haraka na kuwafuata wale jamaa kule kichakani nikampiga kiongozi wao na chuma kichwani akaanguka na kufariki dunia.Baada ya hapo nilikamatwa na kufungwa gerezani “ Patrick akanyamaza tena na mara watu wakaanza kusemezana wao kwa wao.Wengi hawakuwa wakifahamu historia ya Patrick.Vero alikuwa amejikunyata akiwa na mawazo mengi sana.
“Nikiwa gerezani bado Happy ambaye kwa kipindi hicho tayari nilikuwa na mahusiano naye ya kimapenzi aliendelea kuwa nami hadi pale wazazi wake walipomtaka akaendelee na masomo yake nchini marekani.Alikataa kwenda huko na kuniacha peke yangu lakini ni mimi ndiye niliye msisitiza kwamba akubali kwenda huko .Hata baada ya kwenda huko bado tuliendelea kuwasiliana kila mara .Matatizo yalianza baada ya mimi kuhamishwa gereza.Nilihamishiwa katika gereza jipya huko Songea na baada ya hapo mawasilano kati yangu na Happy yakawa magumu sana.Siku moja nilikutana na mtu ambaye baadae nilimtambua kwamba ni Veronika ambaye yeye pamoja na mimi tumewakutanisha nyote hapa leo .Nilimweleza historia yangu na nikamuomba Veronika ili aweze kunisaidia katika kufanya mawasiliano kati yangu na Happy.” Patrick akanyamaza tena.Vero alikuwa akimuangalia kwa macho makali .Watu woe walikuwa kimya wakisikiliza
“Siku moja Vero alikuja na taarifa ambayo ilinitesa kwa miaka mingi.Alinieleza kwamba mpenzi wangu Happy ameamua kuolewa huko Marekani na tayari ni mjamzito.Sitaki kukumbuka mateso na maumivu nililyoyapata siku ile.Niliumia mno .Baada ya miaka mingi kupita niliamini kwamba nikweli Happy aliamua kunisaliti.Niliamua kuendelea na maisha yangu na hivyo mimi na Vero tukawa wapenzi.Siku moja tukiwa nyumbani nilitazama katika luninga na mara nikamuona Happy nikapatwa na mstuko na kuzimia.Sikumueleza mtu yeyote yule sababu ya kuzimia kwangu.Siku ya kinyang’anyiro chakumtafuta mrembo wa Tanzania Happy akafanikiwa kunyakua taji la Miss Tanzania na nilipomkaribia alinitambua na yeye akapoteza fahamu.Baada ya hapo nilifanya juhudi mpaka nikafanikiwa kuonana naye.Nilishangaa sana aliponiuliza ni kwa nini niliamua kudanganya kwamba nimekufa hali niko mzima.Nilishangaa sana na sikuamini hadi aliponikabidhi barua aliyoandikiwa na mtu ambaye alimtaarifu kwamba nimefariki nikiwa gerezani.Niliisoma barua ile nikatoa machozi baada ya kugundua kwamba ilikuwa imeandikwa na Vero.Baua yenyewe hii hapa” Patrick akasema huku akimkabidhi baba yake ile barua ili aisome. Watu wote walibaki vinywa wazi.Vero alikuwa ameinama akilia kwa kwikwi.
“ Ndugu zangu nimewaeleza haya yote ili mtambue ni kwa jinsi gani Vero alivyonifanyia ukatili mkubwa.Ni wazazi wangu pekee ambao wanafahamu ni mateso gani niliyoyapata wakati ule.Nimeumia sana baada ya kuufahamu uongo huu mkubwa alioutunga Vero na kusababisha mimi na Happy tukasambaratika.Mbele yenu wazazi na ndugu wengine wote naomba mnisamehe sana kwa haya nitakayoyasema lakini huu ni uamuzi wangu kutoka moyoni….” Patick akanyamaza kidogo na kisha akasema
“Nimeamua kuachana na Vero na kusitisha kila kitu kuhusiana na ndoa yetu. kuan…………….” Patrick hakumaliza kauli yake mara akina mama watatu akiwemo mama yake na mama yake Vero wakaanguka na kuzirai.Kizaa zaa kikaibuka.Baba yake jasho lilianza kumtiririka ,shinikizo la damu lilimuanza.Kila mtu alihisi kuishiwa nguvu.
Eneo ambalo saa chache zilizopita watu walikuwa wakifurahi na kupongezana , akina mama wakipiga vigere gere kwa furaha kubwa waliyokuwa nayo wakiamini kwamba hakuna kipingamizi chochote cha kuwazuia kuziunganisha familia zao kupitia kwa watoto wao wawili Patrick na Veronika , kwa sasa liligeuka sehemu yenye vilio na mstuko mkubwa sana.Kila mtu aliyekuwepo eneo lile alikuwa amestushwa mno na kilichotokea.Hakuna aliyekuwa ametegemea kama Patrick angeweza kuongea kitu kama kile alichokiongea.Hakuna aliyeota kama ingetokea siku Patrick angeweza kusitisha mipango ya ndoa yake na mchumba wake Veronika.Kila mtu aliona hii ni kama ndoto na si kitu cha kweli..
Haraka haraka wale wote waliozirai kutokana na mstuko walioupata wakaanza kusaidiwa kwa kupatiwa huduma ya kwanza ili waweze kurejewa na fahamu zao .Mahala hapa palionekana kama vile kumetokea msiba.Watu waliokuwa wakiishi jirani na eneo lile wakaanza kujaa katika nyumba hii wakiamnini kuna tatizo limetokea baada ya kusikia vilio vya akina mama.Baba yake Patrick alikuwa katika hali mbaya kutokana na shinikizo la damu .Hali ilikuwa ya kuogopesha sana na kwa haraka Patrick akalisogeza gari na kisha baba yake akapakiwa na kumuomba mtu mwingine aendeshe gari kwa kuwa hakuwa na nguvu za kuweza kulimudu gari kwa wakati huo .Baba yake akakimbizwa hospitali.Patrick jasho lilikuwa likimtoka.Alionekana kama ni mtu aliyechanganyikiwa kutokana na alichokishuhudia kikitokea.
“Ee Mungu naomba unisaidie katika suala hili ambalo limeanza kuwa gumu sana” akaomba kimya kimya wakati wakiwa garini wakimkimbiza baba yake hospitali.Patrick hakuwa akiongea kitu alikuwa ameinamisha kichwa chini akitafakari.
“Sikutegemea kama mambo yangeweza kufika hapa yalipofika .Nilitegemea kungekuwa na ugumu na upinzani mkubwa katika jambo hili lakini sikuwa nimetegemea kama jambo la namna hii lingetokea.Imekuwa ni zaidi ya msiba.Hakuna aliyekuwa ametegemea kama ningeweza kuachana na Vero na hasa katika kipindi hiki cha mwisho cha maandalizi ya harusi yetu.Nimewaumiza watu wengi sana .Kila mtu atakayesikia kuhusu suala hili atanilaani na kuniona mkatili mkubwa.Lakini ni kwa nini basi hakuna hata mtu mmoja ambaye yuko tayari kunisikiliza na kunielewa? Kwa nini hawataki kuupa uzito upande wangu pia? Nimejaribu kuwaelezea kwa ufasaha mkubwa sana ili wanielewe lakini hakuna hata mmoja anayeonekana kunielewa.Hakuna hata mmoja ambaye ameguswa na machungu niliyoyapata kwa uongo huu mkubwa wa Vero“ akawaza Patrick halafu akatoa kitambaa na kujifuta jasho lililokuwa likimtiririka kama maji..
“Litakalo tokea na litokee .Sintaweza kurudi nyuma kamwe.Nilimuahidi Happy kufanya kila niwezalo kwa ajili ya kuwa naye tena.Siwezi kubadili maamuzi yangu.Hata kama nitakabiliana na magumu ya kiasi gani lakini sintarudi nyuma katika azma yangu ya kutaka kuachana na Vero.Kwa sababu ya Happy nitafanya kila litakalowezekana hata kama nikilazimika kuutoa uhai wangu.” Patrick bado alizidi kusongwa na mawazo mengi.
* * * *
“Kitu gani cha kwanza umepanga kukifanya ukiwa kama mrembo wa Tanzania? Mike akamuuliza Happy huku wakiendelea kupata vinywaji.Happy akamtazama Mike kisha akatabasamu na kusema
“Kama mrembo wa Tanzania nitakuwa nikipangiwa majukumu ya kufanya na ofisi maalum inayohusika na kuratibu mambo yote ya Miss Tanzania.Lakini pamoja na kufanya kazi hizo nitakazokuwa nikipangiwa ambazo ni kazi za kujitolea katika jamii ninafikiria kuanzisha umoja au taasisi itakayowawezesha watu mbali mbali kuweza kujitolea katika jamii.”
Mike akatabasamu na kuuliza
“Sijakuelewa vizuri mpenzi wangu kuhusiana na taasisi hiyo unayotaka kuianzisha”
Happy akatabasamu kama kawaida yake,tabasamu ambalo linamfanya Mike naye atabasamu.
“Umoja huu ninaotaka kuuanzisha lengo lake ni kujenga ule moyo wa kujitolea miongoni mwa wanajamii.Kila mtu ataruhusiwa kujiunga na umoja huu na kila mwisho wa wiki tutakuwa tukitembea katika sehemu mbali mbali kama vile mahospitali,magerezani ,mashuleni,katika vituo vya kulelelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu na hata kuwatembelea wale watu walioko majumbani wasiojiweza na kisha kila mtu akatoa msaada wake.Sitaki kujikita katika sehemu moja tu kama ilivyozoelekea katika jamii yetu kwamba kila mrembo wa Tanzania malengo na mtazamo wake ni kusaidia mayatima.Mtazamo wangu mimi utakuwa tofauti kidogo na wengine kwa sababu mimi ninataka kuisaidia jamii masikini na yenye uhitaji kwa ujumla wake bila kubagua.Katika suala hili sintahitaji mfadhili bali nitaitumia kofia ya Miss Tanzania kupita kila kona ya nchi hii kutoa elimu na kuwafundisha watu maana ya kujitolea .Kila mtu atakayeguswa atakuwa akijitolea kile kitu alichokuwa nacho kwa ajili ya watu wenye uhitaji.Kama atatokea mtu mwenye ufadhili nitashukuru na tutauelekeza ufadhili wake katika kada maalum yenye uhitaji mkubwa.” Happy akasema na kumtazama Mike ambaye alikuwa kimya akisikiliza.
Mike akatabasamu baada ya kuisikia mipango ile ya mchumba wake Happy.
“Happy siku zote ninamshukuru sana Mungu kwa kunipa mchumba mwenye akili nyingi na mwenye roho ya huruma sana.Nina kila sababu ya kujivuna kuwa nawe na siku zote za maisha yangu nitahakikisha kwamba unakuwa ni mwanamke mwenye furaha kubwa.Ninakuahidi msaada wangu mkubwa katika jambo hili unalolifikiria.Siku zote nitakuwa nyuma yako ili kukupa ushirikiano wangu.Nikiwa Marekani nitakuwa nikifanya kazi ya kuwakusanya watu wenye asili ya afrika na kuwaomba tuuchangie mfuko huu kwa ajili ya maendeleo ya jamii zetu huku afrika.Natumai baada ya muda mfupi mfuko huu utakuwa mkubwa na kuwasaidia watu wengi sana.” Mike akasema na kumfanya Happy atabasamu halafu akainama chini.
“Kila nikimuangalia Mike nashindwa nitaanzaje kumueleza kwamba uhusiano wetu umefikia mwisho.Siwezi kuishi bila Patrick lakini kumweleza Mike ukweli ninashindwa.Nitafanya nini sasa? Happy akawaza.Mike akagundua kwamba mchumba wake Happy alikuwa katika mawazo mengi.
“Happy malaika wangu una matatizo gani? Naona kama bado hauko sawa sawa.Kuna jambo gani linalokusumbua akili yako? Ninakufahamu vizuri sana na ninafahamu kuna kitu kinakuumiza kichwa chako.tafadhali naomba unieleze nini kinakusumbua akili yako.Niko hapa kwa ajili yako Happy” Mike akamweleza HappyCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mike ni kweli nina tatizo kubwa na sijui hata nianzie wapi kukueleza” Happy akasema huku moyo wake ukimuenda mbio sana
Mike akalegeza tai yake na kumsogelea karibu zaidi Happy ili aweze kusikia ni tatizo gani hilo alilonalo Happy
“Happy niambie una tatizo gani? Mimi niko hapa kwa ajili yako.Nitakwenda hadi mwisho wa dunia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba unakuwa na uso wenye tabasamu daima.Niambie tafadhali una tatizo gani? Mike akasema huku akiupeleka mkono wake katika bega la Happy
Happy akakosa la kusema.Kila alipojitahidi kufumbua midomo yake iligoma kufunguka na kubaki ikicheza.Alikuwa akiogopa.Mara simu yake ikalia.Kwa haraka akafungua mkoba wake akaichukua na kuangalia mpigaji ambaye jina lake lilisomeka kama “My everything”.Hili ni jina alilotaka lisomeke katika namba ya Patrick.Moyo ukamuenda mbio.
“Excuse me “ akasema Happy huku akiinuka na kusogea pembeni akabonyeza kitufe cha kupokelea simu.
“Hallo Patrick “ akasema Happy kwa sauti ndogo
“Happy uko wapi sasa hivi? Patrick akauliza na kumfanya Happy astuke kidogo kutokana na sauti ya Patrick kuwa na mabadiliko
“Patrick mbona sauti yako haiko kawaida? Whats wrong? Happy akauliza kwa sauti na kumfanya Mike astuke baada ya kusikia Happy akitamka jina la Patrick.
“Happy matatizo makubwa yametokea.” Patrick akasema
“Matatizo gani Patrick ? Happy akauliza
“Happy nashindwa hata nianzie wapi kukueleza kwa sababu hapa nilipo nahisi kuchanganyikiwa kutokana na mambo yaliyojitokeza. Kwa sasa niko hapa hospitali kuu ya magonjwa ya moyo kama unaweza ukapata nafasi njoo ili niweze kukueleza kwa undani kilichotokea”
“Patrick umenistua sana nieleze ni kitu gani kimetokea? Happy akauliza kwa wasi wasi
“ Baba amepatwa na shinikizo la damu na tumemleta hapa hospitali hali yake si nzuri hata kidogo”
“Ok Patrick nakuja sasa hivi” akasema Happy huku sura yake ikiwa imebadilika na alionekana kuchanganyikiwa ghafla.
“Happy nini kimetokea mbona umebadilika ghafla? “ Mike akauliza baada ya kugundua mabadiliko katika sura ya Happy
“Mike…it.s….uuhhmm...Its nothing “ Happy akasema kwa kubabaika.
“Niambie ukweli Happy nini kimetokea? Mbona umestuka na kubadilika ghafla? Mike akauliza akiwa amemshika Happy mkono
“Mike its nothing.take me back home” Happy akasema huku akiutoa mkono wake toka katika mkono wa Mike
“Happy don’t say its nothing wakati nafahamu kabisa kwamba kuna kitu umeambiwa na mtu aliyekupigia simu kilichokustua na kukufanya uwe katika hali hii.Halafu nimesikia ukimtaja Patrick..Ni nani huyo Patrick ? Mike akauliza na kumfanya Happy amtazame kwa mshangao uliochanganyika na uoga ndani yake.
“Niambie happy ,Patrick ni nani ? kwa sababu amekufanya ubadilike ghafla “Mike akauliza hali uso wake ukionyesha wasi wasi mkubwa.
“Mike please take me back home” Happy akasema kwa sauti kali.
Mike akamtazama Happy kwa makini halafu akamsogelea akamshika mabega yake kwa mikono yake na kusema
“happy wewe ni mchumba wangu na unafahamu kwamba ninakupenda na siwezi kuishi bila kuwa na wewe.tafadhali naomba uniangalie machoni na uniambie huyo Patrick ni nani? Mike akauliza
Happy akashindwa kumuangalia Mike usoni akainama chini huku machozi yakimdondoka.
“take me home Mike” happy akasisitiza
“happy hapa hatutaondoka mpaka unieleze huyo Patrick uliyekuwa ukiongea naye simuni ni nani? Na amekupa habari gani ambayo imekufanya ustuke namna hii? Mike akauliza na uso wake ulionesha kwamba hakuwa akifanya masihara.
“Mike please..not now…kama hutaki kunirudisha nyumbani I’ll take a taxi” Happy akasema akiwa ameanza kupiga hatua kuondoka.Mike akamkimbilia.
“happy samahani.Sikuwa na nia mbaya kukuuliza vile.Yote hii ni kwa sababu ninakupenda na sipendi kukuona ukiwa katika hali hiyo na ndiyo maana nilihitaji kufahamu kilichokusibu .Naomba unisamehe mpenzi wangu” akasema Mike kwa unyenyekevu.Toka wameanza mapenzi yao haijawahi kutokea hata siku moja wakawa katika hali hii. Mike akamfungulia mlango Happy akaingia garini na kisha wakaondoka kurudi nyumbani.
“Kuna jambo ambalo linamsumbua Happy.Nimeanza kuwa na wasi wasi mwingi kuhusiana na mwenendo wake.Naona kuna mabadiliko makubwa sana.Happy niliyemzoea hakuwa namna hii.Amekuwa ni mwingi wa mawazo na si mchangamfu kama nilivyomzoea.Kuna kitu gani kinachoendelea? Halafu nilisikia akiongea na mtu akamtaja jina la Patrick.Ni nani huyo mtu ? Nakumbuka aliwahi kunisimulia kwamba aliwahi kuwa na mpenzi wake aliyeitwa Patrick ambaye alifariki dunia na ndiyo maana akaamua kunipa mimi nafasi ndani ya moyo wake.Huyu Patrick mwingine ambaye kwa maongezi ya dakika chache ameweza kuibadilisha hali ya Happy ni nani? Kitu gani kimetokea kiasi cha kumfanya Happy astuke namna ile na ghafla tu anaamua kurejea nyumbani? Lazima nifahamu kitu gani kinaendelea.Lazima nifahamu jambo gani lialomsumbua Happy.” Mike alikuwa katika mawazo mengi sana
Baada ya kufika nyumbani kwao Happy akashuka ndani ya gari la Mike na kwa haraka akaingia chumbani kwake,akachukua ufunguo wa gari lake na kutoka kwa kasi.
Mike alikuwa amesimama na Margreth wakijadili jambo wakati Happy alipotoka ndani kwa kasi na kuingia katika gari lake.Margreth akamsogelea na kugonga kioo cha gari kwa mkono wake .Taratibu Happy akashusha kioo na kumtazama
“happy nini kimetokea? Margreth akauliza
“Maggy tutaongea baadae.I need to see Patrick now.Kuna tatizo kubwa limetokea.” Akasema happy huku akiwasha gari na kumfanya mdogo wake azidi kushangaa.
“Happy nini kimetokea? Magreth akajaribu kuuliza lakini tayari Happy alikwisha liwasha gari lake na kuondoka kwa kasi.
“Mike nini kimetokea? Mbona Happy amebadilika ghafla hivi? Margreth akamuuliza Mike ambaye bado alikuwa amesimama asiamini kilichotokea
“hata mimi nilitaka kukuuliza swali kama hilo kwa sababu nimegundua kuna mabadiliko makubwa sana kwa Happy.Si Happy yule niliyemzoea.Kitu gani kinamsumbua? “ Mike akauliza
“Hakuna jambo lolote amekueleza huko mlikokuwa? Margreth akauliza
“hapana Margreth.Happy hajanieleza jambo lolote lile.Kwani kuna nini? Mike akauliza.Margreth akainama chini.
“Ninachokikumbuka ni kwamba kuna wakati nilimuona amezama katika mawazo mengi ikanilazimu kumuuliza ni kitu gani kinachomsumbua .Akaniambia kwamba kuna jambo ambalo limekuwa likimuumiza kichwa na alipotaka kunieleza simu yake ikaita na sielewi aliambiwa kitu gani na huyo aliyempigia simu kwa sababu alibadilika ghafla sana na akaniomba nimrudishe nyumbani.” Mike akasema na kumtazama Margreth.
“Margreth ,kuna jambo ambalo hata mimi limekuwa likiniumiza kichwa sana.” Mike aksema
“Jambo gani hilo Mike? Margreth akauliza
“Happy alipopigiwa simu alisogea pembeni na kwenda kuongelea huko kitu ambacho haikuwa kawaida yake.Wakati akiongea nilisikia akilitaja jina la Patrick,nikastuka sana.Unaweza ukamfahamu huyo Patrick? Mike akauliza na kumfanya Margreth astuke kidogo halafu akatabasamu na kusema .
“…unajua Mike kwa sasa Happy ni mrembo wa Tanzania kwa hiyo atakuwa akipigiwa simu na watu mbali mbali.Usihofu kuhusu huyo Patrick.Huyo ndiye mbunifu wake wa mavazi na ndiye aliyemsaidia sana happy hadi akashinda taji la Miss Tanzania.” Magreth akadanganya huku akitabasamu na kumfanya Mike naye atabasamu.
“Nashukuru sana Margreth kwa kuniondolea huu mzigo niliokuwa nao kichwani kwangu.Tayari nilikwisha anza kuwa na wasi wasi mwingi labda Happy amekutana na Patrick aliyekwisha fariki kwa sababu nakumbuka jinsi Happy alivyokuwa akimpenda.” Mike akasema
“Usiwe na wasi wasi Mike.Jisikie amani.halafu kitu kingine unachotakiwa kukifahamu kwa sasa ni kwamba happy anahitaji kuvumiliwa kwa sababu hakuzoea kuishi maisha haya ya kufuatiliwa kila siku mara na waandishi wa habari n.k.Anahitaji muda ili kuweza kuiweka akili yake sawa sawa kwahiyo kuna mambo ambayo anaweza akayafanya ambayo yanaweza yakakuudhi lakini naomba usichukie na uendelee kumvumilia” Margreth akamweleza Mike
“Nakusukuru sana Margreth nimekuelewa vizuri”Mike akasema huku akitabasamu.
“Happy amekwambia anakwenda wapi? Mike akauliza
“hapana hajanieleza ni wapi anaelekea.Karibu ndani upumzike wakati ukimsubiri”
“Nashukuru sana margreth lakini kwa kuwa sina uhakika kwamba atarudi saa ngapi mimi naona itakuwa vyema kama nikiondoka nitaonana naye kesho” Mike akasema na kuingia katika gari lake akaondoka.
“Nilimuonya Happy kuhusiana na mpango wake wa kuachana na Mike.Inavyoonekana hajamweleza kitu chochote Mike na hivyo kuzidi kumfanya awe na mawazo mengi sana.Happy Anasema Patrick amepatwa na matatizo,ni matatizo gani hayo? Nahisi yanaweza yakawa yanahusiana na huu mpango wao wa kuachana na wapenzi wao wa sasa ili waweze kurudiana.Namuonea huruma sana dada yangu ,yuko katika wakati mgumu.” Akawaza Margreth akitembea taratibu kuingia ndani.
* * * *
“Nimeamua kuachana na Vero na kusitisha kila kitu kuhusiana na ndoa yetu”
Ni maneno ambayo yalikuwa yakijirudia kichwani kwa Veronika ambaye alikuwa akiendesha gari la mama yake hukua akilia.Baada tu ya mama yake kuanguka na kuzirai kutokana na maneno aliyoyatamka Patrick kwamba hakutakuwa na harusi tena,Veronika akainuka kwa kasi kitini akamwendea mama yake pale alipokuwa ameanguka na kwa haraka akaunyakua ufunguo ambao ulikuwa umeanguka pembeni baada ya mama yake kuanguka akaingia katika gari la mama yake na kuondoka kwa kasi kurudi nyumbani kwao.
Machozi yalikuwa yakimtiririka na kulilowanisha shati lake kama vile amemwagiwa maji.Kuna wakati ilimbidi asimamishe gari pembeni ya bara bara akainamia usukani akalia na kisha akaendelea na safari.
“Siamini kama jambo hili ni kweli au niko ndotoni.Patrick huyu huyu ninayempenda kupita kitu chochote katika dunia hii ndiye huyu leo amenifanyia jambo kama hili !! Hapana si kweli.Hii si kweli” Happy akaupiga usukani kwa mikono yake miwili
“That’s not Patrick.Kile ni kivuli chake tu.Patrick ninayemfahamu hawezi kamwe kutamka maneno kama yale.Patrick ananipenda na katu hawezi kufanya vile alivyofanya” Vero akauma meno kwa hasira.Bado machozi yaliendelea kumchuruzika
“My God ! show me that this isn’t true,Im just dreaming, because if its true I don’t know whats going to happen….” Vero akaomba kimya kimya huku akifuta machozi
Alipofika nyumbani kwao akashuka garini na kukimbia kwa kasi kuelekea chumbani kwake akajitupa kitandani na kuanza kulia kwa nguvu huku akitupa mashka na mito chni kwa hasira
“Ouh Patrick! Patrcik!! Kwa nini lakini umenifanya hivi? Kwa nini ?? Sikutegemea katu kama siku moja ungeweza kunifanyia kitendo cha kikatili kama hiki.Sioni tena thamani ya maisha yangu bila wewe.Patrick umeniua…Umeniua Patrick…” Vero akalia kwa uchungu mkubwa.
Sura ya Patrick amesimama akiongea ikamjia tena na kumfanya ainuke na kuzidi kulia.
“Its true…Its not a dream….”
“Kwa sasa nimepata picha kamili .Kumbe siku zote hizi Patrick amekuwa akiteseka kumbe amemuona Happy !! Why this time Happy? Kwa nini umetokea wakati huu na kuja kuyaharibu maisha yangu? Patrick ndiye maisha yangu,ndiye pumzi yangu,ndiye kila kitu kwangu.Kwa nini umekuja wakati huu ? Bastard ! “ Vero akaendelea kulia
“Ninamfahamu Patrick lazima atakuwa amerogwa na mchawi hapa ni huyu huyu Happy ambaye amesababisha Patrick ashindwe kumsahau hata bada ya miaka hii yote kupita.He still loves her…he loves her….” Vero akaendelea kulia
“Nimeumia sana.Umeniumiza sana Patrick na huyo Malaya wako Happy.Kwa sasa kuna kitu kimoja tu ninachotakiwa kukifanya.Only one thing” Vero akasema kwa hasira huku akiigonga meza kwa mkono wake wa kulia.Kwa kasi akatoka mle chumbani na kuelekea katika chumba cha mama yake.Akalifungua kabati kubwa la nguo na kuvuta droo ndogo akachomoa kiboksi kidogo na kukiweka kitandani.Akakiangalia na kukifungua.Ndani yake kulikuwa na bastora nyeusi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Akiwa na mpira wa maji mkononi Andrew alikuwa nyumbani kwake akiosha gari lake ,mara simu yake ikaita.Akauweka chini mpira ule wa maji na kuifuta mikono yake halafu akaichukua simu .Mpigaji alikuwa ni Patrick
“Hello Patrick” akasema Andrew
“Andrew uko wapi ? Akauliza Patrick kwa sauti ambayo kidogo ikamfanya Andrew astuke.
“Niko nyumbani ninaosha gari .Patrick.you sound so strange.” akasema Andrew.
Patrick akavuta pumzi ndefu na kusema
“Andrew kuna matatizo yametokea”
“Matatizo ? Andrew akauliza
“Ndiyo Andrew.Niko hapa hospitali kuu ya moyo.Mzee amepatwa na shinikizo la damu kwa hiyo tumemleta hapa hospitali”
“Ok nakuja hapo sasa hivi”
Andrew akasema na kukata simu akabaki amesimama mahala pale kwa muda wa kama dakika mbili akiwaza
“kazi imeanza.Nilijua toka mwanzo lazima mambo kama haya yatajitokeza tu pindi Patrick atakapotangaza kusitisha ndoa yake na Vero.Nina amini kabisa kwamba shinikizo la damu alilolipata mzee wake linatokana na jambo hili.Pamoja na kwamba Patrick ni rafiki yangu mkubwa lakini jambo alilokuwa amekusudia kulifanya mimi siliafiki kabisa na nilimweleza ukweli kwamba anavyofikiria kufanya si sawa lakini akakataa kunielewa.Nilikwisha ona mbali kuhusu mambo yatakayokwenda kutokea Ngoja niende huko hospitali nikajue kinachoendelea lakini tayari Patrick amekwisha tuingiza katika matatizo makubwa”
Andrew akaingia ndani kwa haraka ili avae nguo na kuelekea hospiotali kuu ya magonjwa ya moyo ambako ndiko baba yake Patrick alikuwa amepelekwa.Wakati akiwa chumbani kwake akijiandaa simu yake ikaita.Akaichukua na kutazama mpigaji.Alikuwa ni Vero.Akasita kuipokea
“Ninayo kazi kubwa siku ya leo.Sijui Vero anataka kunieleza kitu gani” akawaza Andrew na kisha akabonyeza kitufe cha kupokelea simu
“Hallo Vero habari yako? Akasema Andrew
“habari mbaya Andrew” akasema Vero
“habari mbaya ? unaumwa?
“Ina maana hujui kilichotokea? Vero akauliza kwa ukali
“kwani kumetokea nini Vero? Mimi sielewi chochote” akasema Andrew.
“Andrew usinifanye mimi mtoto mdogo ambaye mnaweza mkanichezea akili wewe na rafikiyo.Wewe na Patrick lenu moja na unafahamu kabisa nini ambacho kimekuwa kikiendelea kwa sababu wewe ndiye mshenga wake.Nimekupigia simu kukueleza kwamba ninashukuru kwa mambo mliyonifanyia.Sikutegemea kama iko siku mngeamua kunifanyia mambo kama haya”
“Vero unaposema hivyo unakuwa unanichanganya.Mimi sielewi jambo lolote lile.Naomba tafadhali unieleze nini kimetokea kwa sababu Patrick naye amenipigia simu muda si mrefu na akaniambia kwamba yuko hospitali kuu ya moyo lakini hajanieleza kimetokea nini.” Akasema Andrew
“ Andrew kama unaelekea hospitali,basi tutakutana huko huko.hata mimi naelekea huko sasa hivi” akasema Vero na kukata simu
Andrew akabaki ameishikilia simu ile akiwa na mawazo mengi .
“Kumekucha.Mambo yameanza kupamba moto.Patrick ameniingiza katika matatizo makubwa.Kwa sauti aliyokuwa akiongea Vero inaonekana huko hospitali anakoenda anakwenda kwa shari.Itanilazimu kuwahi ili kuepusha shari inayoweza kutokea.Nilimuonya Patrick toka mapema kwamba suala lile lingeweza kusababisha matatizo makubwa lakini hakutaka kunisikia na haya ndiyo matokeo yake.Mambo yameshaharibika na sijui nini kitatokea huko mbele.Ngoja niwahi hospitali” akawaza Andrew huku jasho likimtoka kwa wingi.Haraka haraka akatoka na kuingia katika gari lake na kueleka hospitali.
****************************
“Huyu shetani Happy ni kwa nini ameibuka katika wakati huu ? Laiti ningelijua mapema kama yangekuja kunitokea mambo kama haya ningelihakikisha ninammaliza Happy angali bado mapema.Nilifanya kosa kubwa sana kumuacha hai wakati ule.Sikutegemea kama baada ya miaka mingi kupita mpaka leo Patrick bado moyo wake uko kwa Happy.This devil must have done something to him because I know Patrick loves me with his life so why he changed all over sudden?? Lakini ni kwa nini Patrick anitende hivi? Alitakiwa anieleze na tulijadili suala hili kabla ya kufikia maamuzi aliyoyafikia .Kama bado anampenda Happy mimi nisingemzuia na kwa namna ninavyompenda ningekubali hata kuwa mke mwenza ili mradi niwe katika ndoa na mtu ninayempenda kuliko watu wote hapa duniani.You’ve killed me Patrick..you’ve killed me…” Akawaza Vero akiwa katika gari kuelekea katika hospitali ya moyo ambako baba yake Patrick alikuwa amelazwa.Michirizi ya machozi ilionekana mashavuni mwake.
“Patrick nimetoka naye mbali sana.Ni mimi ndiye niliyemtoa ukiwa aliokuwa nao gerezani na kumrejeshea tena furaha aliyokuwa ameipoteza.Nimefanya kila nililoweza kumfanya asahau maisha yake ya nyuma na kumrejesha tena katika maisha yenye furaha tele.Toka siku ya kwanza niliyomuona Patrick pale gerezani nilimpenda na kuamini kwamba ndiye furaha ya moyo wangu na hii ndiyo sababu iliyonifanya nitunge uongo ule ili niweze kuwa naye.Ninampenda Patrick toka moyoni na yeye analifahamu hilo.Haikuwa kazi rahisi kuweza kuufanya moyo wa Patrick ukubali kupenda tena.Ilikuwa ni kazi ngumu lakini nilifanikiwa na Patrick akazama katika mapenzi na mimi.Baada ya kazi hii ngumu niliyoifanya kwa miaka mingi ambayo bado muda kidogo tu matunda yake yaonekane kwa mimi kufunga ndoa na yeye,lakini anatokea huyu shetani Happy… a stupid girl from nowhere and try to undo all that I’ve done for Patrick.I cant let that happen…I swear I cant let that happen..!! Vero akasema kwa hasira huku akipiga ukukani kwa nguvu kwa mikono yake na ghafla gari ikaserereka na mara sauti za matairi yaliyojiburuza katika barabara kutokana na breki za ghafla zikasikika .Vero akawahi kukanyaga breki.Huku moyo ukimuenda mbio akauninamia usukani wa gari na kuanza kulia kwa kwikwi.
“Binti una matatizo gani? Akauliza mzee mmoja aliyekuwa amesimama dirishani.
“Siku nyingine kama una matatizo yanayokusumbua tafadhali naomba usiendeshe gari.Umetaka kusababisha ajali mbaya sana “ akasema kwa ukali mzee yule huku akirejea katika gari lake.Vero aliendelea kuuinamia usukani wa gari lake akiendelea kulia.
“ Ni bora hata kama ningekufa katika ajali kuliko kuishi bila ya Patrick.Mateso haya sintaweza kuyavumilia kamwe..” akawaza na mara mlango wa gari lake ukagongwa kwa nguvu.Akainua kichwa kwa hasira na kutazama ni nani aliyekuwa akigonga mlango
“mwanangu una matatizo gani? Eneo hili si zuri kwa kuegesha gari.Eneo hili lina vibaka wengi sana na wamekwisha anza kukuzungukia.tafadhali ondoka eneo hili na ukaegeshe sehemu nyingine yenye usalama mkubwa.” Alisema mama mmoja mnene .
“Nashukuru mama” akajibu kwa ufupi Vero na kuliwasha gari na kisha akaingia barabarani na kuondoka eneo lile.
***********************
“Lolote litakalotokea na litokee tu lakini sintabadili msimamo wangu.Nimekwisha fanya maamuzi na hakuna mtu yeyote ambaye atanifanya nibadili maamuzi yangu.Niko tayari kwa lolote lile ili mradi niweze kuwa na Happy.Nilifungwa gerezani kwa ajili yake na kwa maana hiyo siogopi lolote lile litakalotokea.Ninajua ni mambo mengi sana yanakwenda kutokea ikiwamo kutengwa na familia lakini sintajali .Happy ni mwanamke pekee ambaye nimempenda na ambaye ninataka kuwa naye katika siku zote za maisha yangu yaliyobaki hapa duniani.Ni Mungu pekee ambaye ana uwezo wa kunizuia nisiweze kuwa na Happy katika maisha yangu.” Patrick alikuwa akiwaza huku akitembea tembea nje ya chumba cha wagonjwa mahututi ambamo baba yake alikuwa amelazwa akipatiwa huduma..
“Nafahamu kwamba hakuna mtu yeyote atakayenielewa ni kwa nini nimefanya hivi kwa sababu hakuna anayefahamu nini maana ya penzi la kweli japokuwa nilijaribu kuwapa historia ya maisha yangu na bni kwa nini Happy ni mtu muhimu sana katioka maisha yangu .Wote wananihukumu mimi na kuniona ni mtu mkatili sana kwa kitendo nilichokifanya.hakuna hata mtu mmoja wa kukaa upande wangu.Hakuna hata mtu mmoja ambaye anaonekana kunielewa ni kwa nini nimeamua kufanya maamuzi haya…Pamoja na hayo …….” Ghafla akiwa katikati ya mawazo mengi mara akasikia sauti ikimuita nyuma yake .kwa haraka akageuka kumtazama mtu aliyemuita.Alikuwa ni Happy.
“ Happy !! akasema Patrick na mara Happy akamkumbatia kwa nguvu.
“Ouh Patrick…”akasema Happy huku amemkubatia Patrick .
Watu wote waliokuwepo pale wakageuza vichwa vyao na kuwaangalia na kuanza kusemezana wao kwa wao.Patrick aliliona hilo akamshika mkono Happy na kisha wakapanda katika ghorofa ya juu
“nini kimetokea? Akauliza Happy wakiwa katika ghorofa ya juu.
“Tell me my love what happened” akauliza tena Happy kwa wasi wasi
“baba amepatwa na shinikizo la damu ghafla ikatulazimu kumkikmbiza hapa hospitali.” Akasema Patrick
“Hali yake inaendelea vipi?
“Mpaka sasa bado hali yake si nzuri .Yuko katika chumba cha wagonjwa mahututi madkatari wanajaribu kumpatia huduma .”
“Ouh my love…Pole sana Patrick” akasema Happy akiwa na sura yenye huzuni.
“Ahsante Happy.” Akajibu Patrick na kutazama chini
“ Tell me Patick…nini kimesababisha hali hii kutokea? Akauliza Happy kwa wasi wasi.Patrick akageuka na kutazama chini katika mlango wa kuingilia chumba alimokuwa amelazwa baba yake idadi ya watu ilikuwa ikiongezeka.
“Tulikuwa katika kikao kile nilichokwambia kwamba kinafanyika leo.Nimewaeleza ukweli bila kuficha hata neno moja na mwisho nikatangaza kwamba mimi na Vero basi na nimesitisha kila kitu kuhusu mipangilio ya harusi.Hapo ndipo kizaa zaa kilipoibuka.Watu wamezimia na wengine kuangua vilio kama vile kuna msiba umetokea.Kitu cha ajabu ni kwamba hakuna hata mmoja ambaye amejaribu kuwa upande wangu.Kila mmoja ananiona kama shetani kwa kitendo nilichoifanya…” akasema Patrick na kuinama chini.Happy akatoa kitambaa katika mkoba wake akavua miwani yake na kuyapangusa macho yake yaliyojaa machozi.
“Patrick..nasikitika sana kwa mambo haya yote kutokea.Sikutegemea kama mambo yangekuwa namna hii….” Akasema happy na kabla hajamaliza Patrick akasema
“Happy naomba tafadhali usijilaumu hata kidogo kwa yote yaliyotokea.kwa sasa tunapigna vita na katika vita lolote linaweza kutokea kwa maana hiyo hatuna budi kujiandaa kwa kila litakalotokea.Katika vita tunawapoteza makamanda hodari na shupavu lakini bado vita inaendelea kupiganwa hadi mwisho.Huu ni mwanzo tu na hatupaswi kukata tamaa.Mimi sikati tamaa na sijutii hata kidogo maneno niliyoyasema leo kwani nimeeleza ukweli na kuuanika ubaya na ukatili wa Vero lakini hakuna hata mmoja ambaye anaonekana kunielewa.Hakuna hata moja anayeonekana kujali furaha ya maisha yangu.Kitu muhimu kwao ni kula na kunywa katika harusi na kisha baada ya hapo hakuna mwenye muda wa kufahamu kama maisha unayoishi yana furaha na amani.Mimi nayajali maisha yangu na ninafahamu ni kitu gani ninakitaka maishani.Ninahitaji furaha na furaha hiyo nitaipata ikiwa nitakuwa na wewe pekee katika maisha yangu.Kwa maana hiyo niko tayari kwa lolote lile litakalotokea” Patrick akamwambia Happy ambaye alikuwa ameinama machozi yakimchuruzika.
“Patrick nakupenda sana na nitakupenda mpaka siku naingia kaburini.hata baada ya kupata taaria kwamba umekufa sikuacha kukupenda.Nakubaliana nawe kwamba tunatakiwa tuwe jasiri na kusimama imara katika maamuzi yetu..Lakini mpenzi wangu nina wasi wasi kwamba maamuzi haya yatawaumiza watu wengi sana.So many people will get hurt ..kwa nini tusia……………….” Happy akataka kusema kitu lakini akakatishwa na sauti ya Andrew aliyetokeza ghafla
“Patrick….” Akasema Andrew
“Andrew !! karibu sana ..kutana na Happy..Happy kutana na Andrew my best friend” akafanya utambulisho mfupi Patrick.Andrew na Happy wakashikana mikono
“Nafurahi kukufahamu” akasema Andrew
“Vipi hali ya mzee inaendeleaje? Akauliza Andrew
“anaendelea kupatiwa huduma na madaktari ili kuhakikisha shinikizo linashuka na kuwa la kawaida.Tumuombee Mungu.Mbona unaonekana umeloa maji namna hiyo?
“Nilikuwa naosha gari uliponipigia simu.Niliogopa sana ikanibidi kuondoka kwa kasi ili kuwahi hapa hospitali.Vipi hali ya nyumbani ikoje na mbona mmejitenga huku peke yenu?
“Nimeamua kukaa huku kwa sababu kila mtu ananiona mimi kama shetani .Ninaonekana kama mtu mbaya sana ,binadamu nisiye na roho.Kuhusu nyumbani sifahamu hali ikoje kwa muda huu kwa sababu wakati ninaondoka kuja hapa hospitali hali ilikuwa ni ya vilio na watu walikuwa wameanguka wamezirai.Sijapata taarifa nini kinaendelea hko nyumbani na sina haja ya kufahamu.” Akasema Patrick.
“Ok Patrick ngoja nijaribu kufuatilia hali ya nyumbani ikoje.Kuna watu nimewaona wamekuja muda huu ngoja nikajaribu kuwauliza hali ikoje huko nyumbani ili tujue nini cha kufanya.I’ll be back” akasema Andrew na kushuka ngazi kwa haraka.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Happy wakati huu ni mgumu sana kwetu na tunatakiwa tushikamane more than ever.Tafadhali naomba uwe jasiri na tusimamie maamuzi yetu.Mengi yatasemwa na hata kutokea lakini mwisho wa siku tutashinda na tutakuwa pamoja katika maisha.Tutaishi raha mustarehe” akasema Patrick akiwa amemshika happy mikono.
“Patrick mimi niko tayari kwa lolote lile na sintaweza kurudi nyuma katika maamuzi yetu.Pamoja na hayo Patrick ndugu ,jamaa na rafiki zako watanichukuliaje mimi? Wataniona kama Malaya ,muhuni niliyeuvunja uchumba wa watu,Sidhani kama nitakubalika katika familia yako” Happy akasema kwa wasi wasi.Patrick akamvuta kwake na kumkumbatia.
“Nisikilize Happy.Wewe ndiye mboni ya jicho langu.wewe ndiye pumzi yangu.Yeyote atakayekupenda nitampenda kwa sababu atakuwa ameipenda mboni yangu ya jicho amayo ni kitu muhimu sana .yeyote atakayekuchukia nitamchukia pia.Niko tayari kutengwa na familia,ndugu jamaa na marafiki kwa sababu yako.You are my family,you are my friend,you are my every thing.Siku moja dunia nzima itaufahamu ukweli na wale wanaofahamu nini maana ya penzi la kweli watauona ubaya na ukatili aliotufanyia Vero na watasimama upande wetu wakituunga mkono lakini wale waliokuwa wamejiandaa kwa kula na kunywa katika sherehe watabaki wakisema na kutoa kila aina ya laana hadi siku wanaingia kaburini.Nakuomba tafadhali usiwaze lolote kuhusiana na suala hili..one more thing that you have to know is hata kama dunia nzima itakutenga I’ll be the only person standing by your side.I’ll always be there for you my angel till my last breath…..” Patrick akamwambia Happy maneno yale ambayo yalimuongezea faraja na matumaini.
“Patrick !! “ Ilikuwa ni sauti kali ya Andrew iliyowastua Patrick na Happy waliokuwa wamekumbatiana wakipeana faraja.Patrick akainua kichwa na ghafla akakutananna kitu ambacho hakukitarajia.
“Vero !! Patrick akasema kwa mshangao…
Vero alikuwa amesimama mita kadhaa toka mahala alipokuwa amesimama Patrick na Happy na mkononi alikuwa ameshika bastora.Nyuma yake alikuwepo Andrew ambaye alionekana kama vile alikuwa akitetemeka kwa woga.
“Vero tafadhali punguza hasira na tukae chini tuongee mambo haya ili tuyaweke vizuri.Kila kitu kinawezekana iwapo tutakaa a kuzungumza” akasema Andrew aliyekuwa amesimama mita kadhaa nyuma ya Vero
“Shut up Andrew…usinieleze upumbavu wako wowote la sivyo nitaanza na wewe” akasema Vero kwa ukali
“Vero please acha utani na silaha za moto” akasema taratibu Patrick akimsihi Vero
“Nakufahamu vizuri Vero ,wewe si muuaji and you are not going to shoot me.tafadhali weka bastora chini” akaendelea kusisitiza Patrick
“You know me ? You don’t know the second side of me..and today I’m going to show you my second side..How I look like …” akasema Vero kwa hasira huku midomo ikimtetemeka
“vero tafadhali acha utani na silaha za moto”akasema Patrick
“Utani ! Patrick uaniona kama ninafanya utani ? Unaniona kama ninakutania Patrick ? Akasema Vero kwa ukali na mara akaielekeza bastora kwa Happy na mlipuko mkubwa ukasikika.Happy akaanguka chini.
Eneo lote la hospitali likawa kimya baada ya kusikika mlio ule wa risasi iliyotoka katika bastora aliyokuwa ameishika Veronika.Baada ya dakika kama mbili hivi za ukimya na taharuki iliyowapata watu kutokana na mstuko wa mlio wa risasi ,watu wakaanza kuulizana juu ya kilichotokea.Taratibu Patick akainua kichwa na kumtazama Veronika ambaye alikuwa amesimama machozi yakimtoka akiwa anatetemeka kwa hasira na bastora yake ikiwa inafuka moshi.Akageuza shingo yake na kumuona Happy akiwa amelala chini na kwa kasi akainuka na kumuendea
“Happy….Happy my dear ….amka…amka Happy my love..” Patrick akasema huku akimgeuza Happy.Happy akafumbua macho.Hakuwa amepigwa risasi kama wote walivyokuwa wamedhani.Veronika alipiga risasi nguzo ambayo Happy alikuwa amesimama .
“Ouh Happy my love..you are ok…thanx God..I love you” akasema Patrick huku akimkumbatia na kumbusu Happy baada ya kuhakikisha kwamba yuko salama.Happy machozi yalikuwa yakimtoka..Hakuamini kama alinusurika kifo .
Andrew ambaye alikuwa amesimama mita kadhaa nyuma ya Veronika akapiga hatua na kutaka kumuendea Patrick na Happy pale chini walipokuwa wamekaa wamekumbatiana.
“Stay where you are Andrew..or I will shoot you..” Akasema kwa ukali Veronika na Andrew akapiga hatua kurudi nyuma.
Eneo lote la hospitali likawa katika taharuki baada ya kusikika kwamba kuna mtu ana bastora na anataka kufanya mauaji. Watu waliokuwa maeneo yale ya hospitali wakaanza kukimbia kuelekea juu ya ghorofa ambako Veronika na akina Patrick walikuwepo.
Taratibu Patrick akainuka mahala pale alipokuwa na kumtazama Vero kwa macho makali sana.
“ Vero tafadhali naomba uweke silaha chini…tafadhali naomba uache mchezo na silaha za moto” akasema Patrick kwa ukali.
“Patrick umenifanyia kitu kibaya sana na sintaweza kuvumilia.After all these years..leo unakuja kuniacha namna hii? Sintaweza kuvumilia unitende namna hii Patrick..so today its me ,you na huyo Malaya wako..” akasema Veronika kwa ukali mdomo ukiwa unamtetemeka kwa hasira.
“Vero tafadhali naomba upunguze hasira..Hasira zako zinakupelekea ufanye kitendo ambacho utakijutia maishani mwako..tafadhali Vero punguza hasira na uiweke chini bastora yako then tutaongea..” akasema Patrick.
“Hakuna kitu cha kuongea mimi na wewe tena Patrick.Umekwisha weka wazi kwamba mimi na wewe tumefikia mwisho kwa hiyo hakuna kitu tunachoweza tukaongea tena.Its over Patrick..its over…Una roho ya kikatili Patrick..you are so cruel..sikutegemea kama mtu niliyempenda kwa moyo wote ,nikajitoa mwili na roho kwa ajili yako leo hii umenigeuka na kunitupa kama taka taka…I loved you Patrick ..I loved you sooo much..and I still do…lakini kitendo ulichokifanya leo kimenifanya nigeuke mnyama.Nimeumia sana.Umeniumiza kiasi ambacho sikutegemea..Maisha yangu yote niliyakabidhi kwako na sioni kama kuna sababu ya kuendelea kuishi hapa duniani bila ya kuwa na wewe.Wewe ulikuwa ni kila kitu kwangu lakini sasa nakuona kama ni kiumbe usiye na roho..so today its our end..me and you..” akasema Vero huku machozi yakimtoka.Ni wazi alikuwa ameumia sana moyoni.Machozi yalikuwa yakimtiririka.Patrick alikuwa akipiga hatua za taratibu kumkaribia Vero.
“Patrick..usijaribu kunikaribia..nitakupiga risasi kabla ya wakati niliopanga kukuua kufika ” akasema Vero kwa ukali na kumfanya Patrick asimame.
* * * *
Katika mlango wa kuingilia sehemu ile ya ghorofa waliyokuwapo akina Patrick Andrew alikuwa na kazi ngumu ya kuwazuia watu waliokuwa wakijaribu kutaka kushuhudia kilichokuwa kikiendelea na wengine walitaka kumkamata Vero ili asiweze kufanya jambo baya.
“Jamani hali iliyoko huku juu si nzuri hata kidogo..tafadhali msijaribu kutaka kuingia kwa kasi huku juu kwa sababu mtaifanya hali kuzidi kuwa mbaya.Kinachotakiwa kutumika hapa ni busara ya hali ya juu sana ili kumshawishi huyu mwanadadda aweke silaha chini.Lakini iwapo mtajaribu kutaka kutumia nguvu ya aina yoyote ile mtaifanya hali kuwa mbaya.Huyu dada mwenye silaha ana hasira sana na kutokana na jinsi alivyoumizwa moyo,yuko tayari kufanya jambo lolote lile kwa hiyo nawaomba ndugu zanguni msijaribu kutaka kuingia kwa kasi huku juu..tujaribu kuwa watulivu ili tuone nini tufanye kuepusha maafa yanayoweza kujitokeza.Ninamfahamu Patrick vizuri atamtuliza na kila kitu kitakuwa shwari..Naomba tuvute subira kidogo ndugu zangu .” akasisitiza Andrew akiwazuia baadhi ya ndugu na jamaa ambao walitaka kwenda kumzuia Vero asiweze kufanya jambo lolote baya.
“Unashauri tufanye nini? Kwa sababu tunavyozidi kuchelewa huyu mwanamke anaweza akasababisha maafa.” Akauliza mzee mmoja ambaye ni mmoja wa ndugu za Patrick na alikuwepo katika kikao kilichosababisha mambo haya yote kutokea.
“Ninachoweza kushauri kwa sasa hebu tusijaribu kuingilia mambo haya kwa sababu haya ni masuala ya kihisia zaidi na wanaogombana ni watu walioishi kama wapenzi kwa muda mrefu kwa hiyo kuna kila dalili kwamba wanaweza wakafikia muafaka na wakamaliza haya matatizo.Tusubiri tuone mwisho wake utakuwaje..” akasema Andrew na kuwafanya watu wale watulie
“Lakini kwa nini tusiwataarifu polisi kwamba kuna mtu mwenye silaha na anatishia usalama wa raia? Tutakuwa tunafanya jambo la kijinga kuendelea kukaa hapa na kumuangalia msichana huyu ana silaha na anatishia kuwaua wenzake.Tayari amekwisha piga risasi moja na hatujui ni kitu gani amedhamiria kukifanya.Tuwataarifuni polisi haraka kuhusiana na tukio hili ili waweze kufika haraka na kumdhibiti huyu msichana” akasema mmoja wa madaktari ambaye naye alikuwa amesimama pale mlangoni.
“Hapana daktari..naomba msifanye hivyo kwanza kwa sababu kuwaleta polisi mapema kunaweza kukampandisha hasira Vero ambaye anaweza akafanya jambo lolote baya.Tafadhali naomba msifanye hivyo kwanza hadi tutakapohakikisha kwamba hali inazidi kuwa mbaya .” akasisitiza Andrew.
* * * *
“Simama hapo hapo Patrick na usitembee hata hatua moja…ama la nitakupiga risasi Patrick..” akasema kwa ukali Vero baada ya Patrick kutaka kupuuza onyo alilompa awali la kutaka kumkaribia.
“Vero nakufahamu vizuri..huwezi kunipiga risasi…mambo yote haya umeyataka wewe mwenyewe.Ulifanya jambo baya sana ulipofanya ule udanganyifu mkubwa na kusema kwamba eti nimekufa.na eti Happy ameolewa na mzungu na kuniacha peke yangu gerezani.Huwezi kujua ni kwa kiasi gani niliumia kwa udanganyifu ule..Niliumia sana ..hakuna mtu anayeweza kufahamu kiwango gani niliumizwa..Vero wewe ni mkatili na mnyama mkubwa tofauti na muonekano wako.Hauna mapenzi na mimi hata kidogo na kama ungekuwa na mapenzi ya kweli na mimi usingethubutu kutunga uongo ule mkubwa na kusababisha mimi kupata uchungu mkubwa sana moyoni.You are selfish..you only care for yourself.Hukujali kama mimi na Happy tulikuwa na mapenzi mazito,ulitunga uongo mkubwa kututengenisha mimi na Happy wakati ukifahamu fika kwamba nilikuwa pale gerezani nikitumikia kifungo kwa sababu ya kumlinda Happy asidhalilishwe kwa sababu ni mwanamke pekee ninayeweza kufanya jambo lolote kwa ajili yake.Kwa roho yako mbaya ya kikatili na kinyma hukulijali hilo na ukawa tayari kusababisha maumivu makubwa kati yetu sisi ili kutimiza lengo lako.Ndiyo, ulitimiza lengo lako kwa kuwa na mimi kama ulivyokuwa ukihitaji lakini napenda kukueleza wazi kwamba pamoja na kuwa nawe lakini moyo wangu siku zote ulikuwa kwa Happy.Sikuacha hata mara moja kumpenda Happy..not for one second.kwa sababu ni yeye pekee niliyepangiwa niwe naye hapa duniani.Namshukuru Mungu kwa sababu amekuumbua ,uongo wako umejulikana na leo hii unayasikia machungu kama niliyoyasikia mimi siku ile uliponidanganya kwamba Happy amenikimbia na kuolewa na mzungu..Machungu kama aliyoyasikia Happy siku alipopata taarifa kwamba mwanaume aliyempenda kupita kitu chochote kile amefariki dunia..Kama kweli unafahamu kama ulitenda kosa kubwa kutunga uongo na kunitenganisha na Happy ,weka silaha chini na mambo haya yaishe kwa amani.Hata ufanye ufanyavyo mimi sitishiki Vero..hata ukitaka kuniua..niko tayari kwa hilo lakini utambue kwamba nitakufa nikilitamka jina la Happy mwanamke pekee ninayempenda katika dunia hii.Now if you want to shoot me..go ahead..shoot me now…” akasema Patrick huku akitembea taratibu kumuendea Vero pale alipokuwa amesimama.Bado mkono wa Vero uliokuwa na Bastora uliendelea kumuelekea Patrick
“Patrick tafadhali usinisogelee..don’t come near me !! akasema kwa ukali Vero.Patrick akampuuza na kuendelea kutembea taratibu kumuendea Vero.
“Patrick usimkaribie Vero tafadhali…!! Alipaaza sauti Andrew ambaye alikuwa ameiweka mikono yake kifuani kwake kwa uoga mkubwa baada ya kumshuhudia Patrick akitembea taratibu kumuendea Vero bila kuijali silaha aliyokuwa ameishika mkononi.
“My God Patrick !! Unataka kufanya nini? Akasema Andrew kwa sauti ndogo akiwa ni mwingi wa wasi wasi.
“Shoot me now..” akasema Patrick akiwa karibu kabisa na Vero..Vero alikuwa akitetemeka kwa hasira akamsogelea Patrick na kumuwekea bastora kichwani.
“I did all that because I love you…Nilifanya kila nililoweza kukusahaulisha huyu Malaya wako Happy lakini hukuweza kumsahau…You are good for nothing Patrick..you are idiot…you are stupid….you don’t deserve to live in this world….Kwa mambo uliyonifanyia nasema hivi leo nakuua wewe na Malaya wako..ni bora wote tukakosa.” Akasema Vero kwa hasira
“Vero tafadhali usifanye hivyo..tafadhali Vero naomba tukae tuyaongee masula haya ili yaishe bila madhara yoyote.” Akapaaza sauti Andrew lakini kabla hajamaliza kauli yake akakatishwa na sauti kali ya Vero aliyegeuka ghafla na kumuelekezea bastora .
“shut up you fool..!! ..kuwadi mkubwa wewe.. you’ll have to pay for th…….” Kabla hajamalizia sentensi yake Vero akastukia mkono wake uliokuwa na bastora umeshikwa kwa nguvu na Patrick.
“Patrick nakwambia niachie !! …” akapiga kelele Vero.Happy ambaye alikuwa amekaa ameinama akilia akastushwa na ukelele ule alioupiga Vero.Akageuza shingo na kuangalia kilichokuwa kinaendelea.Akastuka baada ya kuona Patrick na Vero wakigombania bastora iliyokuwa katika mkono wa Vero.
“Ouh My God !! akasema Happy kwa mstukoCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mwanamke huyu anaweza akasababisha mauaji.Dhamira yake si nzuri hata kidogo..amekwisha nikosa kwa risasi..si wa kumuachia aendelee kuimiliki ile silaha.” Akawaza Happy huku akijiinua toka pale sakafuni.
Kukurukakara ikaendela kati ya Patrick na Vero na bila kutazamia Patrick ajikuta akizidiwa nguvu na Vero na kugandamizwa ukutani na kumuwekea bastora kichwani
“Nimesema leo lazima nikuue mwanaharamu wewe..” akasema Vero kwa hasira.
“You want to kill me? ..kill me now…!! Akasema kwa ukali Patrick
“Ouh No ! .Happy akasema kwa mstuko huku akiushika mdomo wake kwa uoga .
“Andrew do something !! …..” akapiga ukelele Happy akimuamuru Andrew ambaye alikuwa amesimama asijue la kufanya.
“Waiteni polisi haraka..hali ya hapa si nzuri hata kidogo” akapiga kelele Andrew baada ya kuona hali imebadilika na sura ya Vero ilionyesha kila dalili za mauaji.
Ghafla bila kutazamia Happy akavua viatu vyake virefu alivyokuwa amevaa na kukimbia kwa kasi na kwa nguvu zake zote akamsukuma Vero ambaye alijibamiza ukutani kwa kishindo kikubwa na kuanguka chini.Damu zikaanza kumtoka mdomoni na hakufurukuta tena.
“Are you ok Patrick “ akauliza Happy na kumkumbatia Patrick
“Thank you my angel..umeyaokoa maisha yangu.” Akasema Patrick na kukumbatiana na Happy.Mara Patrick akastuliwa na sauti ya Andrew aliyekuwa ameinama pale chini mahala alipolala Vero .
“Patrick !!…..”
Patrick akageuka na kukutanisha macho yake na macho yaliyojaa hasira na machozi ya rafikiye mkubwa Andrew aliyekuwa pembeni ya daktari aliyekuwa akimpima Vero.
“Patrick umefanya nini sasa ? kwa nini umemuua Vero ? Andrew akauliza na akashindwa kujizuia kuangusha machozi
“Unasemaje?? ..Vero amekufa ? akauliza Patrick kwa mstuko.. na wakati huo huo watumishi wa hospitali ile wakiwa na machela wakafika na kumchukua Vero na kuondoka naye kwa kasi .Happy akaishiwa nguvu akakaa chini akainama.
“Patrick nimeua…nimeua Patrick !! Happy akalia kwa sauti ndogo….
Patrick ambaye naye miguu ilikuwa ikimtetemeka akamuinamia Happy pale chini
“Shhhhhhh…Happy nyamaza kulia.Hujaua mtu yeyote.Vero bado hajafa..amezirai tu. Tusubiri taarifa ya daktari inasemaje.” Akasema Patrick na kumkumbatia Happy.Mara polisi waliokuwa wamejiandaa kwa ajili ya kumdhibiti mtu waliyetaarifiwa kwamba ana silaha silaha wakaingia kwa kasi .Happy alipowaona akazidi kulia.
" Patrick please dont leave me.I'm so scared" akasema Happy.Patrick ambaye naye alijawa na hofu kubwa akawatazama maaskari wale ambao walianza kuwatawanya watu wote waliokuwa kule ghorofani.
" Patrick nimeua...Nimeua Patrick.." akazidi kulia Happy.Patrick akamkumbatia na kukilaza kichwa cha Happy kifuani pake.
" Happy tafadhali usilie my love...tafadhali usilie mpenzi wangu" Patrick akambembeleza happy lakini bado aliendelea kulia.
" Patrick please dont leave me..dont leave me Patrick" Happy akasisitiza
" Happy my love I'm here..I'll never leave your side." akasema Patrick akimpiga piga Happy mgongoni.
Askari mmoja ambaye alikuwa na cheo cha mkaguzi aliyeonekana kama mkuu wa kikosi kile kilichofika pale kwa dhumuni la kutuliza fujo akawasogelea Patrick na Happy pale chini walipokuwa wamekaa.
" Ndugu zangu kuna usalama hapa? akauliza yule askari.
" Tuko salama afande" akajibu Patrick
" Hakuna mtu yeyote aliyedhurika? akauliza tena
" hakuna afande wote tuko salama." akajibu Patrick.
" Ndugu unaweza ukatueleza ni kitu gani kimetokea hapa ? akauliza yule askari
Patrick akajaribu kufungua mdomo wake ili aweze kuongea lakini akashindwa .Midomo ilikuwa ikimtetemeka.
" Jitahidi ndugu yangu utueleze ni nini chanzo cha vurugu hii iliyotokea hapa muda mfupi uliopita mpaka ikafikia hatua ya kutishiana silaha? akauliza tena yule mkaguzi wa polisi.
Patrick akajitahidi na kusema
" Afande nashindwa nikueleze vipi................." akasema Patrick kisha akamkumbatia Happy zaidi.
"Ni nani aliyewatishia wenzake kwa silaha? akauliza askari.
" Afande kilichotokea hapa kinahitaji maelezo marefu lakini nitajaribu kukueleza kwa ufupi.Ugomvi uliotokea hapa unanihusisha mimi na mpenzi wangu wa zamani aitwaye Veronika ambaye tumeachana muda si mrefu .Mpenzi wangu yule hakuridhika na kitendo cha kuachana naye hivyo akanitafuta mahala nilipo akagundua kwamba nimekuja hapa hospitali na yeye akaja na kwa bahati mbaya akanikuta niko na huyu hapa mpenzi wangu wa sasa " akasema Parick na kutulia baada ya kumuona askari yule akimtazama sana Happy.
" Huyu si yule msichana aliyeshinda taji la Miss Tanzania juzi juzi? akauliza yule askari
"Ndiye huyu "akajibu Patrick
" Huyu ni mpenzi wako? akauliza tena askari.
" Ndiyo ni mpenzi wangu." akajibu Patrick.
" Ouh My God sijui ni kwa nini wasichana wengi wanaposhinda taji hili hujikuta wakiingia katika migogoro hasa ya kimapenzi.Huyu amechaguliwa juzi tu lakini tayari amekwisha anza kutengeneza vichwa vya habari." akawaza askari yule.
" Kwa hiyo nini kilisababisha ugomvi kutokea?
" Kilichotokea ni kwamba mimi na huyu mpenzi wangu tukiwa huku juu ghrofani akatokea Vero akiwa na bastora mkononi na akaanza kututisha kwamba leo ama zetu ama zake.Baada ya majibizano ya maneo ya muda mfupi nikajaribu kumsihi apunguze hasira na tuweze kukaa tukayaongea masuala haya yakaisha.Badala ya kutuliza hasira vero akapandisha zadi na kuachia risasi iliyomkosa Happy.baada ya kitendo kile ikanilazimu kumsogelea karibu ili niweze kumzuia asiweze kuleta madhara." Patrick akanyamaza na kumtazama Happy ambaye bado aliendelea kufuta machozi.
" Nini kilifuata baada ya hapo? akauliza mkaguzi wa polisi
Happy akauinua uso wake na kumtazama Patrick.
"Nini kilitokea ? akauliza tena
" I must save her..This is the time I have to show her how important she is to me.I must prove my love now.I cant let anything happen to a woman I love..I cant let her suffer" akawaza Patrick kisha akasema
" Veronika alishindwa kunipiga risasi mkono wake ulikuwa ukitetemeka.Nikamsogelea karibu zaidi nikataka kumnyang'aya silaha na hapo ndipo vurugu ilipoibuka .Tukaanza kusukumana na ......." Kabla Patrick hajaendelea kumueleza mkaguzi wa polisi nini kilitokea mara akatokea daktari akamuita yule askari mkaguzi pembeni na kuanza kuongea naye.Katika maongezi yao alikuwa akimuelekezea kidole Happy ambaye alipoona daktari akimuelekezea yeye kidole akapatwa wasi wasi mwingi akaanza kulia.
" Patrick ninaogopa sana.Please dont leave me" akasema Happy huku akilia kwa uoga
Patrick akauweka mkono wake wa kulia kichwani kwa Happy na kumgeuza kichwa ili aseweze kuwaona daktari na yule askari.
" Usiogope Happy,hakuna jambo lolote baya lililotokea"
" Nina wasi wasi mwingi Patrick..itakuwaje kama ni kweli nitakuwa nimemua Vero? Akasema Happy kwa uoga.Patrick akamuwekea kidole mdomoni
" Shhhhhhhhhhhhhh.!!!!!!......
" Usiwaze kitu kama hicho Happy.Hujaua mtu and you'll never kill anyone.Whatever happened here my love you havent done anything..you understand me ? Patrick akamwambia Happy ambaye bado alikuwa akifuta machozi
" Umenielewa Mpenzi? akauliza Patrick baada ya kuona Happy hamjibu
"Do you understand me ? akauliza kwa mara nyingine kisha akaigeuza shingo ya Happy na kumuangalia usoni.
" What? akauliza Happy
" we have to do something ...first swear to me that you'll do as I tell you to do."
Huku akifuta machozi Happy akasema
" I swear ..."
" Good.." akasema Patrick kisha akayashika mabega ya Happy.
" What happened here you are not involved in anything..I am the one who did everything here"
" Patrick No ! Please dont do that...." akasema Happy
" Happy naomba unisikilize kwa makini sana.Nimeanza kuhisi kitu kibaya kinaweza kutokea kwa maana hiyo lazima nichukue hatua za kukulinda na kila kitu kwa sababu wewe ni mwanamke pekee ambaye niko tayari hata kuyatoa maisha yangu kwa ajili yake.Kwa maana hiyo mimi ndiye nitakayekuwa muongeaji mkubwa na hata kama ukiulizwa kana kila kitu na useme mimi ndiye niliyehusika na vurugu yote.Please do that for me Happy." Patrick akasema.Kabla Happy hajajibu kitu daktari na askari mkaguzi wakawasogelea Happy na Patrick.
" Kijana na mchumba wako kuanzia sasa inatulazimu kuwashikilia kwa mahojiano zaidi .Kwa mujibu wa maelezo ya daktari ambaye amekuwa shuhuda wa vurugu hizi toka mwanzo na hadi kilipotokea kifo cha Veronika." akasema askari mkaguzi na kuwafanyia ishara askari watatu waliokuwa wamesimama pembeni wafike pale haraka .Baada ya kauli ile ya askari happy nguvu zikamuisha akataka kuanguka chini Patrick akamdaka.
" be strong Happy..be strong my love" Akasema Patrick halafu akamgeukia daktari
" Daktari ni kweli vero amefariki dunia?
" Ndiyo..Baada ya kwenda kumpima tuligundua kwamba alikwisha fariki kitambo"akasema daktari.
Patrick akakishika kichwa kwa mikono yake miwili.
" Ouh My God,..why this is happening to me ?
" Daktari hebu nieleze nielewe mazingira ya kifo chake.." akasema tena Patrick
"Alisukumwa na kujigonga ukutani kwa nguvu na tunahisi ubongo wake ulitikisika na kusababisha kifo chake.Lakini tutapata majibu yenye uhakika baada ya mwili wa vero kufanyiwa uchunguzi wa kina katika hosptali ya Muhimbili"
Patrick akainama akifikiri.Alihisi kuchanganyikiwa.Mwili ulikuwa ukimtetemeka.Hakutegemea kama tukio lile lingeweza kujitokeza.
" Mungu wangu sikutegema kama mambo yangekuwa hivi..Kila kitu sasa kimeharibika.Nimepoteza kila kitu.Ouh My God Please help me.." akawaza Patrick halafu akainua uso wake akamuangalia yule askari mkaguzi.
"Afande naomba tafadhali mumuache huyu mchumba wangu aende zake.Yeye hahusiki na kitu chochote kilichotokea hapa.Mimi ndiye niliyemsukuma Vero akajigonga ukutani na hivyo kusababisha kifo chake.Nichukueni mimi na mumuache Happy aende zake" Patrick akamwambia yule askari mkaguzi.
" Kijana kwa taratibu za kipolisi ninyi nyote mtachukuliwa na kupelekwa kituoni na mtachukuliwa maelezo yenu na baadae kama ikionekana huyu mchumba wako hahusiki na suala hili basi ataachiwa huru.Kwa sasa nyote mtashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi"
" Afande ninafahamu hivyo lakini nakuomba tafadhali mumuache huru Happy.Nichukueni mimi ambaye ndiye muhusika wa tukio hili .Happy hajajihusisha na jambo lolote lile..." akasema Patrick na mara daktari aliyekuwa amesimama pembeni ya askari akasema kwa hasira
" Afande huyu kijana anakudanganya kwa sababu mimi nilikuwapo hapa wakati mambo yote yanatokea na nimemshuhudia kwa macho yangu huyu msichana akimsukuma mwenzake ambaye alijigonga ukutani na kufariki dunia." Patrick akapandwa na hasira akataka kumvamia daktari yule askari wakamzuia.
" Kijana tafadhali usijaribu kuleta vurugu .mfungeni pingu mpelekeni katika gari." akaamuru mkaguzi
" No ! Hamuwezi kumfunga pingu mpenzi wangu.Leave her alone" akasema kwa ukali Patrick.Happy aliyekuwa amekaa chini akitoa machozi akasimama akamuendea Patrick na kumshika usoni kwa mikono yake akamwambia
" Patrick usibishane nao.Please let me go with them."
" No ! Happy you cant go with them." akasema Patrick huku akiruka ruka .Tayari mikono yake ilikwisha fungwa pingu.Mkaguzi wa polisi akamfuata Happy.
" Samahani Binti..nafahamu mchumba wako hataki uongozane na sisi k wenda kituoni lakini kwa taratibu za kipolisi ni lazima tuwashikilie ninyi nyote ili tuweze kufanya uchunguzi na baada ya uchunguzi kukamilika basi tutamuachia huru ambaye ataonekana hahusiki na tukio hili.Nafahamu wewe ni mrembo wa Tanzania na ninakupa heshima yako.Sitaku ufungwe pingu ila nakuomba ukubali kuongozana nasi kuelekea kituoni.Uko tayari kuongozana nasi kwa amani? akauliza mkaguzi
" Niko tayari afande.Nitaongozana nanyi kwenda kituoni.." akasema Happy.
Sauti za vilio toka kwa akina mama waliokuwa wamekuja kufuatilia maendeleo ya baba yake Patrick zikaanza kusikika mara tu iliposikika taarifa kwamba Vero amefariki dunia.Ilikuwa vigumu kuamini kama ni kweli vero amefariki dunia. Patrick na Happy wakapakiwa katika gari la polisi .
" Dont worry my love..everything will be ok..we'll be ok" akasema Patrick akimpa moyo Happy aliyeonekana kukata tamaa.
" No matter what happens you have to say as I told you to say " akasema Patrick.Happy hakujibu kitu aliendelea kumwaga machozi.
Japokuwa alijitahidi kuonyesha ujasiri mkubwa kwa nje lakini kwa ndani Patrick alikuwa akitetemeka ..aliogopa sana kwa tukio lililotokea.Kwake aliona tukio lile ni kama ndoto.Hakuamini moja kwa moja kama ni kweli Vero amefariki dunia.
" Its hard to believe..vero amekufa ? ...No this cant happen..." akawaza
Picha ya vero akiwa ndani ya tabasamu pana sana ikamjia akilini.Akajikuta akiuma meno kwa uchungu.
" Ouh Vero.....!! " akawaza Patrick na kushindwa kuyazuia machozi kumtoka.
" She loved me... Alikuwa ni msichana mzuri sana ,mwenye kila sifa ya uzuri.Masikini Vero..why I did this for you?`..Patrick akasikia uchungu mkubwa moyoni.Kifo cha Vero kilimuumiza sana.
Picha ya yeye na vero wakiwa bafuni asubuhi ikamjia kichwani akazidi kuumia moyo.Akainama chini akafikiri kwa muda halafu akageuza shingo na kumuangalia Happy aliyekuwa ameinama akilia.
" masikini Happy..hakufanya vile kwa kupenda..hakukusudia kufanya vile.hakuna aliyetegemea lingetokea jambo kama hili.hakuna aliyetegemea Vero angefariki dunia.Happy ana wakati mgumu sana.Siwezi kukubali Happy akaingia gerezani.She's the woman I love and I'll do everything to protect her..." akawaza Patrick.
Kitanda cha magurudumu kikatolewa ndani ya chumba kikisukumwa na wauguzi wawili na nyuma yao walifuata wauguzi wengine wanne na madaktari wawili pamoja na askari polisi wanne.Wote walionekana na nyuso zilizojaa simanzi.Juu ya kitanda kile kilichokuwa kikisukumwa,kulikuwa na mwili wa mtu uliokuwa umefunikwa shuka jeupe.gari la kubebea wagonjwa la hospitali likasogea taratibu karibu na mlango ,wauguzi wakafungua milango yake ya nyuma halafu shuka lililokuwa limeufunika ule mwili likaondolewa na sura ya mtu aliyekuwa juu ya kile kitanda ikaonekana wazi.Ilikuwa ni sura ya msichana mrembo aliyekuwa amefumba macho kana kwamba amesinzia.Ulikuwa ni mwili wa Veronika.Alikuwa amelala usingizi wa milele na hatoweza kuamka tena.Alikuwa amefariki dunia.Taratibu wauguzi wakauingiza mwili ule katika gari tayari kwa kuupeleka katika hospitali ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi wa sababu ya kifo chake.
Wakiwa chini ya ulinzi mkali ,ndani ya gari la polisi ambalo halikuwa mbali sana na lile gari la wagonjwa ,Happy na Patrick waliushuhudia mwili wa Veronika ukipakiwa garini.Happy akashindwa kuvumilia akaanza kulia
" Ouh ! Patrick why I did that ?.....
Patrick akamvuta kwake akamkumbatia na kumziba mdomo wake kwa kiganja cha mkono.
" Shhhhhhhhhh......!!!!!!!!!." Patrick akamwambia Happy kwa sauti ndogo
" Stop crying Happy..you are going to be fine..trust me"
" It hurt me Patrick..It hurt so much ..I didnt mean to k.................." Kabla hajamaliza sentensi yake akastuka ghafla na kumtazama Patrick usoni kwa sekunde kadhaa kisha akamkumbatia Patrick kwa nguvu.
" Don't leave me Patrick..dont let me die" akasema Happy kwa sauti ndogo.Patrick akainama kidogo akambusu katika paji la uso na kumwambiaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" Sintakuacha Happy..I will always be here for you" akasema Patrick na kumkumbatia zaidi Happy halafu akaigeuka shingo yake na kuwatazama wauguzi wakiifunga milango ya ile gari iliyoubeba mwili wa Veronika na taratibu gari lile likaanza kuondoka huku likisindikizwa na gari moja la polisi.Patrick akasikia uchungu mkubwa.Machozi yakamdondoka lakini akawahi kuyafuta ili Happy asigundue kama alikuwa akilia.
" Ouh Vero....masikini Vero..sikutegema kama yangetokea haya.Sikufikiria kabisa kama suala hili lingetufikisha hapa lilipofika na kupeleka mauti yako..Bado siamini kama umekufa Vero..Its so hard to believe.Ni asubuhi ya leo tulipokuwa tukiongea na kucheka kwa furaha lakini jioni hii eti umefariki.!! .Ouh Jamani Vero it hurt so much" akawaza Patrick.Michirizi ya machozi ikaonekana katika mashavu yake.
" Nasikia uchungu mkubwa mno kwa tukio hili.Nimemuweka Happy katika wakati mgumu sana ..Hakuwahi kutegemea kama angeua mtu katika maisha yake.Mimi ndiye niliyemsababishia dhambi hii kubwa.Najua moyoni mwake ameumia mno .I must save her..Yes I must save Happy.." akawaza Patrick.
Picha ya Veronika akiwa katika tabasamu ikaendelea kumjia kichwani na kumuumiza sana.
" Forgive me Vero...Nisamehe Veronika." akawaza Patrick akiwa amefumba macho yake na kuuma meno kwa uchungu.Picha ya Vero akiwa amesima ameshika bastora ikamjia tena kichwani.Akakumbuka uoga aliokuwa nao pale Vero alipoachia risasi moja iliyomkosa Happy. Akaukunja uso wake.
"Haya yote umeyataka wewe mwenyewe Vero..Nilikupenda sana lakini sikuwa nimefahamu ukatili uliotufanyia mimi na Happy.Ulitunga uongo na kututenganisha hali ukijua fika kwamba Happy ndiye mwanamke pekee ambaye moyo wangu unampenda kuliko wanawake wote.Ninaumia ninapokumbuka nyakati zile za furaha tulizokuwa nazo,tulipendana sana hadi kufikia mamuzi ya kufunga ndoa .Lakini Inaniuma zaidi kila nikifikiria mateso na maumivu uliyotusababishia mimi na Happy kwa uongo ulioutunga .Niliumia mno nikijua ni kweli Happy amenisaliti .Ni Mungu wangu pekee ndiye anayefahamu maumivu niliyoyapata wakati ule.Maumivu yale niliyoyapata yameendelea kwa miaka hata miaka hadi nilipokutana na Happy na tukaufahamu ukweli.Sifurahii kifo chako lakini ukweli utasimama pale pale kwamba wewe ndiye chanzo cha haya yote na hili ni fundisho kwa wengine kwamba alichokipanga Mungu siku zote binadamu hawezi kukipangua. Najua bado nina safari ndefu na ngumu katika mapenzi yangu na Happy lakini niko tayari kwa lolote lile litakalotokea kwa sababu Happy ndiye mwanamke pekee ambaye ninaamini amezaliwa kwa ajili yangu " Patrick akastuliwa kutoka katika mawazo baada ya watu wengine wanne kupandishwa ndani ya ile gari.Mmoja wa watu wale alikuwa ni Andrew.Patrick akaonyesha mshangao lakini Andrew akamsogelea karibu na kumnong'oneza sikioni.
" Tumechukuliwa kama mashuhuda wa tukio .Tunakwenda kutoa maelezo yetu jinsi tukio lilivyokuwa" akasema Andrew.Patrick akamfanyia ishara kwamba asogeze sikio lake karibu ili aweze kumweleza jambo.
" Andrew ulikuwepo eneo la tukio na kuona kila kilichotokea ,katika maelezo yako andika kwamba Happy hakuhusika na kitu chochote kilichotokea hapa na kusababisha kifo cha Vero.Tuhuma zote zielekeze kwangu kwamba mimi ndiye niliyesababisha kila kitu.Eleza kwamba mimi ndiye niliyemsukuma Vero akagongesha kichwa chake ukutani na kufariki dunia.Umenielewa? akauliza Patrick.Andrew hakumjibu kitu akabaki akimtazama kwa mshangao
" Patrick.............." Andrew akataka kusema jambo lakini Patrick akamzuia.
" Do as I say Andrew" Akasema Patrick kwa ukali na kuwafanya wale askari waliokuwa wakiwalinda kugeuka ghafla.Andrew akainamsha kichwa
" Sasa nimeamini Kweli Patrick anampenda Happy.Hata baada ya kitendo alichokifanya cha kusababisha kifo cha Vero bado Patrick anathubutu kusimama na kumtetea? Its hard to believe this is happening.....yaani Patrick anataka kujitwisha yeye mzigo huu wa mauaji?...This is insane.." akawaza Andrew huku akimuangalia Happy kwa macho makali .
" Msichana huyu ndiye chanzo cha haya matatizo yote yaliyotokea.Toka ameonana tena na Patrick nimekuwa nikihisi lazima kuna jambo baya linaweza likatokea na nikamuonya Patrick kwamba aachane na huyu mwanamke lakini hakutaka kunisikia.Tayari yeye na Vero walikwisha kuwa na maisha mazuri yenye furaha.Walikuwa wanapendana sana na tayari maandalizi yote ya ndoa yalikwisha fanyika.Zilibaki siku chache sana wafunge ndoa .Masikini Patrick namuonea huruma sana rafiki yangu ana wakati mgumu mno.Amemkosa Vero na sasa anataka kwenda gerezani kwa kosa ambalo hajalifanya.Hili ni kosa la mauaji na linaweza kupelekea akapata adhabu ya kunyongwa au hata kifungo cha maisha gerezani.No ! I cant let that happen..I cant let my friend go to jail just because of this good for nothing woman..Haiwezekani hata kidogo Patrick afungwe au anyongwe kwa sababu ya mwanamke huyu..This woman must pay for what she has done.."Andrew akazidi kuwaza na kumuangalia Happy aliyekuwa amekilaza kichwa chake kifuani kwa Patrick kwa jicho la chuki.Akamtazama tena rafiki yake na kumkuta ameinama akiwaza.
" Sijui mwanamke huyu amempa nini Patrick hadi akampenda kiasi hiki.Upendo huu umepitiliza.Pamoja na kupita miaka mingi hawajaonana na kila mmoja kuendelea na maisha yake lakini baada tu ya kuonana kila kitu kimebadilika.Penzi lao limerudi kwa kasi ya ajabu sana na kusababisha madhara makubwa si kwao tu bali hata kwetu sisi tunaowazunguka.Nashindwa nifanye nini..Je nisimame katika ukweli halisi kwamba Happy ndiye aliyemuua Vero? au nifuate maelekezo ya Patrick kwamba yeye ndiye aliyesababisha kifo cha Vero?..Patrick ni rafiki yangu mkubwa na ni zaidi ya rafiki itakuwaje kama nikienda kinyume na matakwa yake na kusimama katika ukweli? Mhhh Hapana ! ..Ninamfahamu vizuri Patrick ,kama nikienda tofauti na anavyotaka yeye basi kuna hatari hata urafiki wetu unaweza ukafikia mwisho.Ouh God help me to decide whats best for my friend" akawaza Andrew.Akainua kichwa akawatazama tena Patrick na Happy.Mikono ya Patrick ikiwa imefungwa pingu mikononi.
" Masikini Patrick anatia huruma sana .Mara ya kwanza kukutana naye ilikuwa ni gerezani ambako alikuwa amefungwa kwa kosa la mauaji na aliua kwa ajili ya kumtetea huyu huyu Happy.Kuna hatari kubwa akarejea tena gerezani kwa mara ya pili kwa kosa lile lile la mauaji.Kama kungekuwa na mashindano ya mapenzi ya kweli basi Patrick na Happy wangechukua ushindi kwa sababu inaonekana wanapendana kweli.Nimeamini katika penzi la kweli chochote kinawezekana.Sipati picha huyo mchumba wa Happy akisikia juu ya tukio hili ataamua nini.." Andrew akastuliwa toka mawazoni na gari moja lililoingia kwa kasi eneo lile.Alilifahamu gari lile.
Gari lile aina ya rav 4 likasimama na kwa haraka akashuka mwanadada mmoja mrefu ,mwembamba mwenye nywele ndefu alizozifunga kwa nyuma.Kwa mtazamo wa haraka haraka ungedhani kwamba mwanadada yule alikuwa akjishughulisha na masuala ya urembo kutokana na umbo lake . Alikuwa amevaa suti nyeupe iliyo mkaa vyema na kuzidi kumfanya apendeze zaidi.Sauti ya mlango wa gari ukifungwa ikamfanya Patrick ainue kichwa chake na mara akamuona mwanadada yule aliyeshuka katika ile gari, akatabasamu.
" Savana ! " Patrick akatamka kimoyo moyo.
Savana alikuwa ni wakili wa kujitegema na alikuwa na kampuni yake ya uwakili iitwayo Savana & Company Advocates moja ya kampuni za uwakili zinazosifika kwa kuwa na wanasheria mahiri sana.Savana anasifika kwa umahiri wake katika kusimamia kesi na amekuwa akisimamia kesi mbali mbali kubwa na kati ya hizo nyingi amekuwa akishinda na kumfanya aingie katika orodha ya mawakili maarufu nchini.
" Nilimpigia simu Savana nikamwambia aje mara moja" Andrew akamwambia Patrick ambaye hakujibu kitu.
Toka ameshuka garini Savana amekuwa akiongea na simu.
" Ok nashukuru,nitakupigia tena simu baadae,kuna jambo ninalifuatilia " akasema Savana akikatisha maongezi na mtu aliyekuwa akiongea naye simuni kisha akaiweka simu mfukoni na kumuendea askari polisi mmoja aliyekuwa amesimama karibu kabisa na gari lile walilokuwa wamepakiwa akina Patrick.Akasalimiana na yule askari polisi akamuuliza jambo na askari yule akamuelekeza katika jengo la utawala la hospitali ile.Kwa haraka Savana akapiga hatua kuingia ndani ya lile jengo aliloelekezwa. Ndani ya jengo lile akawakuta askari polisi watatu na madakatari wawili akawasalimu kwa ujumla na kuomba kuonana na Meja Simoni Mkerege .Meja mkerege akamuomba amsuburi nje kwa kama dakika tano hivi ili weze kumaliza maongezi muhimu na madaktari.
Dakika kumi baadae Meja Simon akatoka nje ya lile jengo na kumkuta Savana akimsubiri.Akamsogelea na kumuuliza
" Nkusaidie nini?
" Ninaitwa Savana Pius Nkere.Ni wakili wa kujitegemea toka katika kampuni ya Savana & company Advocates.Nimetaarifiwa kwamba mteja wangu aitwaye Patrick anashikiliwa kwa kosa la kusababisha mauaji.Nimekuja hapa kama mwanasheria wake ili kufuatilia na kuhakikisha kwamba mteja wangu anapata haki zote anazostahili kama mtuhumiwa kwa mujibu wa sheria." akasema Savana.
" Ouh kumbe wewe ndiye Savana ! Nimekuwa nikikusikia sana .Wakili maarufu sana hapa mjini.Nashukuru kukufahamu.Mteja wako ni kweli tunamshikilia kwa tuhuma za kusababisa kifo cha msichana aitwaye Veronica.Tunamshikilia yeye na msichana mwingine aitwaye Happy ambaye inasemekana ni mpenzi wake.Taarifa za awali zinaonyesha kwamba kulitokea ugomvi kati ya Patrick na Veronika ambao ulisababishwa na wivu wa kimapenzi.Inasemekana kwamba Veronika alikuwa ni mpenzi wa Patrick na kukatokea matatizo katika mahusiano yao na hivyo Patrick akaamua kumuacha na kuwa na huyu mpenzi wake mpya Happy.KItendo hicho hakikumpendeza Vero ambaye aliwafuata akiwa na silaha na kuanza kutishia kuwatoa uhai na ndipo vurugu kubwa ikaibuka na hatimaye kusababisha kifo chake.hayo ndiyo machache tunayoyafahamu kwa sasa ." akasema Meja Simon.
" Ahsante kwa taarifa Afande..je naweza kuruhusiwa kuonana na mteja wangu japo kwa muda mfupi? " akasema Savana.
" Kwa sasa yuko ndani ya gari,tunawapeleka kituoni yeye na mwenzake Happy pamoja na watu kadhaa ambao ni mashuhuda wa tukio hili watakaotoa maelezo yao.Nakushauri uvute subira tufike kwanza kituoni na pale nitakusaidia ili uweze kuongea na mteja wako kwa uhuru zaidi." akashauri Meja Simon.
" Sawa afande." akasema Savana.
Hatimaye Patrick na Happy wakafikishwa kituo cha polisi chini ya ulinzi mkali.Andrew na wale watu wengine wanne wakachukuliwa maelezo yao kama mashuhuda wa tukio lile wakaruhusiwa kurejea majumbani kwao.Patrick na Happy wakawekwa katika mahabusu za hapo kituoni kwa ajili ya kuchukuliwa maelezo yao siku itakayofuata.
Jitihada za Savana za kutaka kuonana na mteja wake zikazaa matunda na hatimaye ikaruhusiwa kuonana na Patrick ambaye alitolewa mahabusu na kupelekwa katika chumba kimoja kilichokuwa na mafaili mengi ambamo ndimo Savana alikuwamo.
" Pole sana Patrick" akasema Savana baada ya kubaki wao wawili peke mle chumbani.Savana alikuwa ameomba apewe uhuru wa kuweza kuongea na mteja wake na hivyo askari wakatoka nje na kuwaacha wao peke yao chumbani.
" Ahsante Savana." akasema Patrick kwa unyonge
" usijali Patrick,jipe moyo mambo haya yatakwisha.Hebu nieleze tukio hili lilitokeaje? Nilistuka sana nilipopigiwa simu na rafiki yako Andrew akanifahamisha kwamba unashikiliwa kwa mauaji ikanilazimu kuacha kila nilichokuwa nakifanya nikaja mara moja" akasema Savana.Patrick akavuta pumzi ndefu kisha akaanza kumsimulia Savana kila kitu kilichotokea.
" Pole sana Patrick...Ni mkasa mzito sana lakini usijali mambo haya yatakwisha...Pamoja na hayo kuna jambo moja ambalo nataka unihakikishie Patrick " akasema Savana
" Jambo gani hilo Savana?
"Patrick una uhakika kwamba ni Happy ndiye aliyemsukuma Vero na kusababisha kifo chake? akauliza Savana huku akimuangalia Patrick kwa umakini mkubwa.
" Savana wewe ni rafiki yangu na ni mwanasheria wangu vile vile kwa hiyo siwezi kukudanganya.Ni kweli Happy ndiye aliyemsukuma Vero na kusababisha ajigonge ukutani na kupoteza maisha.Lakini hakukusudia kufanya vile bali alikuwa katika harakati za kuniokoa mimi kwa sababu wakati ule mimi na Vero tulikuwa tuking'ang'ania silaha aliyokuwa ameishika Vero mkononi.Kwa maana hiyo Savana nakuomba ufanye kitu kimoja"
" Kitu gani Patrick" akauliza Savana
" Nataka Happy asihusishwe kabisa katika kesi hii.Kila kilichotokea katika tukio lile na kusababisha kifo cha Vero nataka nikibebe mimi.Happy is innocent..Umenielewa Savana? akauliza Patrick.Savana akamuangalia kwa makini kisha akamuuliza
" Patrick are you out of your mind? How could you do such a thing? Happy ndiye anayetakiwa kubeba mzigo wote wa kesi hii na si wewe.." akasema Savana
" Naomba unisikilize vizuri Savana..Sitaki Happy ahusishwe katika jambo lolote lile kuhusiana na kesi hii.Nataka aachiwe huru.Nina sababu zangu za msingi kutaka iwe hivyo na niko tayari kubeba adhabu zote kuhusiana na kesi hii kwa hiyo nakuomba Savana ufanye hivyo ninavyokutaka ufanye.Nitakulipa kiasi chochote kile cha pesa unachokitaka kwa ajili ya kufanikisha suala hili." akasema Patrick.Savana akainama akafikiri kisha akasema
" Patrick niko hapa si kwa ajili ya kutafuta fedha.Niko hapa kwa ajili yako kama mtu wangu wa karibu ,kama rafiki yangu.Niko hapa kwa ajili ya kutaka kukutoa katika kesi hii ya muaji lakini mambo unayoniambia niyafanye yamenistua sana .Kwa nini ubebe mzigo wa mtu mwingine? Na vipi kama utakutwa na hatia na kuhukumiwa kunyongwa?Uko tayari kunyongwa kwa kosa ambalo hukulitenda? Akauliza Savana.
" Savana naomba ufanye ninavyokuomba ufanye.If you cant do that for money then do it as my friend." akasema Patrick.
" Savana nafahamu kwamba nimekushangaza sana kwa maamuzi haya lakini naomba ufahamu kwamba haya ni maamuzi magumu niliyoyachukua kwa ajili ya kumuepusha Happy na kifungo.She didnt kill on purpose.She was trying to help me..She was helping me..you understand? Kama nikifungwa basi nitafungwa badala yake..Niliweza kufungwa mara ya kwanza kwa ajili yake na safari hii niko tayari tena kufungwa kwa ajili yake pekee kwa sababau ninampenda na sitaki aingie gerezani.Tafadhali Savana fanya kila uwezalo ili uweze kunisaidia katika suala hili." akasema Patrick.
" Patrick nadhani unahitaji muda wa kufikiri zaidi kuhusu maamuzi haya unayoyafanya .Nakuomba tuzungumze tena ukisha tulia ." akasema Savana
" No Savana..Akili yangu iko sawa.Nakuomba tafadhali ufanye hivyo.Ninafahamu uwezo wa kufanya hivyo unao kwa hiyo nakuomba usiniangushe Savana.Najua hupendi kufanya hivyo lakini nakuomba usinihofie mimi.I'll be fine." akasema Patrick.Savana akainama akafikiri kisha akasema.
" Ok Patrick I'm going to do it.I'll do what you want but in record I dont like this.I real dont like doing this to my friend lakini kwa kuwa umeniomba na kunisisitiza sana sina budi kufanya kadiri ya matakwa yako.Nitahakikisha Happy anatoka lakini nakuomba baada ya kesi hii kufika mwisho na matokeo yoyote yatakavyokuwa itakubidi utafute mwanasheria mwingine kwa sababau sintaendelea tena kuwa mwanasheria wako.Moyo wangu utakuwa unaumia sana." akasema Savana kwa masikitiko.
" Nashukuru sana Savana kwa kukubali kunisaidia katika suala hili.Umenifanyia jambo kubwa mno na nitakushukuru katika uhai wangu wote uliobaki" akasema Patrick.
" Happy umekwisha muelekeza namna atakavyotoa maelezo yake? Akauliza Savana.
" Nilijaribu kumweleza na akaonyesha kukubali"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" Good.Sasa hivi ndivyo utakavyoandika katika maelezo yako na huo ndio utabaki msimamo wako.Nitaonana na Happy pia naye nitamuelekeza namna ya kuandika maelezo yake."
Savana akampa Patrick maelekezo ya namna atakavyo andika maelezo yake halafu wakaagana.
Baada ya kumaliza kuongea na Patrick Savana akafanya juhudi za kuonana na Happy akafanikiwa.
Happy hakuwahi kuonana wala kufahamiana na Savana .Akapelekwa katika kile kile chumba alichotoka Patrick .Savana alipomuona Happy akastuka.Akamuangalia tena kwa makini kisha akasema
" Pole sana Happy"
" Ahsante sana dada" akajibu Happy
" Mimi naitwa Savana ni mwanasheria wa Patrick .Nina kampuni yangu ya uwakili inaitwa Savana & Company advocates.Mimi nikishirikiana na mawakili wenzangu ndiyo tutakaowatetea katika kesi hii inayowakabili.Patrick ni rafiki yangu mkubwa na ndiyo maana baada ya kupata taarifa za tukio hili nilifika haraka sana eneo la tukio.Pole sana Happy matatizo ni sehemu ya maisha na huja bila ya kutazamia."
" Ahsante sana Savana.." akasema Happy na kutoa machozi
" Usilie Happy..Naomba kuanzia sasa uwe jasiri.Ni ujasiri pekee ambao utakuwezesha kusimama imara na hatimaye kushinda kesi hii.Kuanguka ni jambo la kawaida na ni sehemu ya maisha ya mwanadamu.Sote tunaanguka lakini tuangukapo hatupaswi kukaa chini na kulia.Tunatakiwa kuinuka na kusonga mbele.Kwa hiyo hata wewe hutakiwi kuangusha chozi hata kidogo. Halafu wewe ni mrembo wa Taifa.Kama msichana ambaye ulifanikiwa kutwaa taji kubwa kama lile ni lazima ulikuwa ukijiamini kwa hiyo ujasiri ule uliokuwa nao wakati ukishindania taji lile ulete hapa na usimame imara katika suala hili.Tumeelewana Happy?
" Tumeelewana" akasema Happy huku akifuta machozi
" Ok vizuri..Sasa Happy nimekuita hapa usiku huu kuna mambo mawili matatu ambayo kama wakili ninayekwenda kuwatetea ningependa kuyafahamu.Ninakuomba uwe muwazi katika kila nitakachokuuliza .Kwanza kabisa naomba unieleze japo kwa ufupi tukio hili la leo lilitokeaje? akasema Savana.Happy akainama akafikiri kidogo halafu akaanza kumsimulia Savana kila kitu anachokifahamu kuhusiana na tukio lile.
" Ok nashukuru sana Happy kwa kuwa muwazi.Lakini kuna jambo ambalo ningependa unihakikishie.Naomba unihakikishuie kwamba wewe ndiye uliyemsukuma vero akajigonga ukutani na kupoteza maisha"
" Ni kweli mimi ndiye niliyemsukuma Vero akajigonga ukutani" akasema Happy
" Lakini sikufanya vile kwa kukusudia.Nilikuwa nikijaribu kumzuia Vero asiweze kufanya madhara kwa sababu wakati huo alikuwa ameshika bastora mkononi na tayari alikwisha nikosa na risasi ."
" Sawa Happy nimekuelewa pole sana kwa mkasa huu. Patrick amenieleza jambo moja ambao lilinistua kidogo lakini akasisitiza kwamba ni lazima nilifanye.Ameniambia kwamba wewe usihusiswe na jambo lolote kuhusiana na kesi hii.Anataka tukutoe kabisa na mzigo wote aubebe yeye.Je alikudokeza jambo kama hili?
" Ndiyo alinidokeza jambo hilo"
" wewe ukaamua nini?
" Alinisisitiza sana ikanibidi nimkubalie anavyotaka iwe." akajibu Happy.
" Je unafahamu kwamba Patrick anakupenda sana kiasi cha kuamua kujitwisha yeye mzigo wote wa mauaji?
Huku akitoa machozi Happy akajibu
" Ninafahamu ..Ninafahamu jinsi gani Patrick ananipenda ..Hata mimi ninampenda sana .."
Savana akamuangalia Happy kwa makini kisha akasema
" Happy naomba ufahamu kwamba Patrick ni rafiki yangu mkubwa sana na sikuwa tayari kufanya hivyo anavyotaka lakini baada ya kunisisitiza sana na kuonyesha wazi ni kwa namna gani anavyokupenda na hataki uguswe kabisa na mkondo wa sheria nikakubaliana naye.Nitakutoa katika kesi hii ila nakuomba Happy sadaka hii kubwa aliyoitoa Patrick isiende bure.Siku zote nakuomba uwe karibu naye na kumpa moyo na faraja.Endapo nitasikia kwamba unaponda raha na wanaume wengine wakati Patrick yuko gerezani kwa sababu yako naapa mbele za Mungu kwamba nitayafaya maisha yako yawe magumu sana na utatamani hata kufa.Umenielewa Happy"
Happy akafuta machozi kisha akasema
" Nimekuelewa Savana..Patrick ndiye maisha yangu na siku zote nitakuwa upande wake" akasema Happy
" Vizuri..sasa maelezo yako utakayoyatoa yatakuwa namna hii." akasema Savana na kumwelekeza Happy maelezo ya kutoa kisha wakaagana na Happy akarudishwa mahabusu
Mrembo wa Tanzania Happy Kibaho kuhusishwa katika tukio la mauaji ndiyo habari kuu iliyokuwa ikiongelewa kila mahali nchini. Tukio hili liliwastua sana watu.Vyombo vya habari hususan magazeti yalipamba kurasa zao kwa habari hii ya kustusha.Nje ya kituo cha polisi ambacho Happy na Patrick walikuwa wakishikiliwa kwa siku ya tatu sasa kulijaa waandishi wa habari wakijaribu kupata habari ya kuandika kuhusiana na tukio lile lililogusa hisia za watu wengi..Eneo la kituo liligeuka kuwa eneo lenye pilika pilika nyingi tofauti na ilivyozoeleka.
Saa nane na dakika ishirini za mchana ,katika mlango mkubwa wa kuingilia kituoni kilitokea kitu ambacho hakuna aliyekuwa amekitazamia. Miss Tanzania Happy kibaho akiwa ameongozana na familia yake yaani baba na mama yake mzazi na mdogo wake Isabella wakajitokeza.Pamoja nao walikuwepo wakili Savana,mkurugenzi wa Miss Tanzania,msemaji wa Miss Tanzania pamoja na watu wengine wanne.Kitendo cha sura ya Happy kuonekana akitoka mlangoni kundi kubwa la wapiga picha na waandishi waliokuwa wamepiga kambi pale kituoni wakisubiri taarifa ya kamanda wa polisi kuhusiana na tukio lile likasogea karibu na kuanza kumpiga picha.Happy hakuwajali akaendelea kupiga hatua japo miguu ilikuwa mizito kutembea.Baadhi ya waandishi wa habari wakajaribu kumuhoji maswali lakini Happy hakuwa tayari kuongea lolote.
" samahani ndugu waandishi ,Happy kwa sasa hayuko tayari kwa kujibu maswali yenu.Nawaomba ndugu zangu mumuache akapumzike kwa sasa na akili yake ikishatulia atawajibu maswali yenu yote." Msemaji wa Miss Tanzania Abdool azizi Sharrif akawaambia waandishi wa bahari huku akijaribu kuwazuia kutomsonga zaidi Happy.
" Tunaomba basi utueleze nini kimetokea? Mbona miss Tanzania ameachiwa huru wakati anahusishwa na tuhuma za mauaji? mmoja wa waandishi wa habari akamuuliza Abdoolaziz.
" Kwa ufupi ni kwamba Happy ameachiwa huru baada ya kuonekana hahusiki na jambo lolote lililosabisha kifo." Akasema Abdoolazizi kwa ufupi .
Happy akaongozwa kuelekea katika gari moja aina ya Noah yenye rangi nyeupe.Ndugu jamaa na marafiki ambao walikuwepo pale kituoni,walimpa pole na kumfanya ashindwe kuzuia hisia zake na kudondokwa na machozi.Hatua chache kabla ya kulifikia lile gari,kijana mmoja mtanashati aliyevalia nadhifu akajitokeza toka katika gari moja dogo lenye namba za kibalozi.Kijana yule mwenye umbo lililojengeka vyema akatabasamu huku akimuendea Happy.Happy ambaye alikuwa akitembea huku ameinamisha kichwa akaguswa bega na mdogo wake akageuka.
" Mike huyu hapa" akasema Margreth na kumfanya Happy astuke ghafla kana kwamba ameona kitu cha kutisha.Happy akasimama halikadhalika Mike naye akasimama wakaangaliana kwa sekunde kadhaa kisha bila kujali kamera za waandishi wa habari na wapiga picha Mike akamwendea na kumkumbatia Happy kwa furaha akambusu lakini Happy hakuonyesha furaha wala kuongea kitu chochote.Mike akaishika mikono ya Happy na kutaka kusema neno lakini Happy akajitoa katika mikono ile na kutembea kwa kasi kuliendea lile gari ambalo tayari mlango wake ulikwisha funguliwa.Mike akabaki ameduwaa.Hakuelewa sababu ya happy kumfanyia vile.
" Usikasirike Mike ..give her sometime." Margreth akamnong'oneza Mike aliyekuwa amesimama akimshangaa Happy.
Waandishi wa habari ambao waliokuwa makini kufuatilia kila hatua anayopiga happy wakaliona tukio lile na kumzunguka na kuanza kumuhoji ili wafahamu nini kilitokea.Mike hakujibu swali lolote la waandishi wa habari.Taratibu akaelekea liliko gari lake lenye namba za kibalozi akafunguliwa mlango akaingia garini kisha gari ikaondoka pale kituoni.
Familia yote ya Happy ikaingia garini tayari kwa kuondoka .
" Happy jitahidi upate mapumziko marefu ili uweze kutuliza akili.Pamoja na hayo usisahau tuliyoongea juzi" akasema Savana .Happy bado machozi yaliendelea kumtiririka.
" Ahsante sana Savana kwa msaada wako.Siwezi kusahau" akasema Happy.
" Stop crying Happy..usilie tena.you have to be strong..be strong for you and Patrick..." akasema Savana huku akimfuta Happy machozi kwa kitambaa..Mama yake Happy ambaye alikuwa ameketi mbele akiongea na simu aliposikia jina patrick linatajwa akastuka na kugeuka ghafla akamuangalia Savana kwa macho makali.Savana akaufunga mlango na taratibu gari ile ikaondoka maeneo ya kituoni ikiongozana na gari nyingine nne.
Baada ya kuhakikisha Happy ameondoka kituoni,waandishi wa habari hawakuondoka waliendelea kusubiri taarifa toka kwa kamanda wa polisi ambaye alikuwa ameahidi kulitolea ufafanuzi suala lile ambalo lilikuwa limeteka hisia za watu wengi na kugubikwa na upotoshwaji mkubwa hususan toka katika vyombo vya habari.
Saa tisa za alasiri waandishi wa habari wakaitwa ofisini kwa kamanda wa polisi .Bila kupoteza muda kamanda wa polisi akawaambia.
" Ndugu zangu wanahabari nimewaiteni hapa ili kuweza kuwapeni taarifa kadhaa za kipolisi na vile vile kutolea ufafanuzi kuhusu suala linalomuhusu Miss Tanzania ambaye alikuwa akishikiliwa kwa tuhuma za kusababisha mauaji"
Kamanda James fungakata akatoa taarifa mbalimbali kuhusiana na matukio mbali mbali ya kiuhalifu yaliyotokea halafu akasema
" Katika wiki hii pia kumetokea tukio ambalo limezua gumzo kubwa katika kila kona ya nchi.Kumekuwa na upotoshwaji mkubwa sana kuhusiana na tukio hili.Tukio hili linamuhusu mrembo wetu wa Tanzania Happy Kibaho.Taarifa sahihi ni kwamba kulitokea ugomvi uliosababisha kifo cha mwanamke aitwaye Veronika.Sababu kuu ya ugomvi huo inasemekana ni wivu wa kimapenzi.Kijana mmoja aitwaye Patrick alikuwa na mahusino ya muda mrefu na marehemu Veronika na tayari walikuwa katika maandalizi ya kufunga ndoa.Wakiwa katika maandalizi hayo ya harusi,ukaibuka mgogoro mzito kati yao uliomsababisha Patrick kuamua kusitisha kila kitu kuhusiana na ndoa na kuvunja kabisa mahusiano yao ya kimapenzi.Kitendo kile kilimchukiza sana Veronika na hasa baada ya kugundua kwamba Patrick alikuwa tayari na mahusiano ya kimapenzi na msichana mwingine aitwaye Happy kibaho .Veronika alipata taarifa kwamba Patrick na Happy walikuwa pamoja katika hospitali kuu ya moyo.Akawafuata pale akiwa na silaha mkononi na kuanza kutoa vitisho vya kuwaua wote .Silaha aliyokuwa nayo Veronika ni hii hapa" Kamanda akaiinua bastora ile juu akawaonyesha waandishi wa habari.
" Msichana huyo Veronika " akaendelea kamanda James
" Alikuwa na lengo la kulipa kisasi kwa Patrick kwa kitendo chake cha kuamua kumuacha na hasa katika hatua za mwisho za maandalizi ya ndoa yao.Ili kuthibitisha kwamba alikuwa amedhamiria kuwadhuru Patrick na mpenzi wake akaachia risasi ambayo ilimkosa Happy.Kitendo kile cha kumkosa Happy kwa risasi kilimkasirisha Patrick ,akamfuata na kutaka kumny'ang'anya ile silaha na hapo ndipo ikaibuka purukushani ya kugombea silaha ile.Katika purukushani hiyo Veronika akajigonga ukutani na kufariki papo hapo. Jeshi la polisi lilikuwa likiwashikilia Patrick na Happy lakini baada ya mahojiano tumeamua kumuachia huru Happy baada ya kuthibitika kwamba hakuhusika na ugomvi ule uliosababisha kifo cha Veronika.Kwa sasa bado tunaendelea kumshikila kijana Patrick ambaye amekiri kugombana na Veronika na kusababisha kifo chake.Kwa sasa tunaandaa mashitaka na muda wowote atapelekea mahakamani kusomewa shitaka la mauaji. Kwa ufupi huo ndio ukweli halisi kuhusiana na tukio hili" akamaliza kamanda James .Kwa kuwa muda ulikuwa umekwenda sana hakukuwa na nafasi ya kuuliza maswali.
Safari ya kuelekea nyumbani ilikuwa ya kimya kimya.Happy hakutaka kuongea na mtu yeyote.Macho yake hayakukauka machozi. Baada ya kufika nyumbani Happy akashuka garini na kuelekea moja kwa moja chumbani kwake akifuatana na mdogo wake Margreth.Kabla hajafunga mlango wake akamgeukia mdogo wake na kumwambia
" Margreth sihitaji kuona na mtu yeyote leo..I need to be alone...." akasema Happy.Margreth akamwangalia akamwambia
" kweli happy suala hili ni zito sana...you need more time to rest...nitahakikisha hakuna mtu atakayekusumbua.." akasema Margreth..
" Ahsante sana Margreth..." akasema Happy kisha akaufunga mlango wake akalala.Margreth akabaki amesimma pale mlangoni kwa Happy akiwa na mawazo mengi mara akatokea mama yake..
" Mbona umesimama hapa nje peke yako? Happy amekuzuia kuingia ndani? akauliza mama yake
" Happy anahitaji kuwa mwenyewe kwa sasa..Hataki kuonana na mtu yeyote" akajibu Margreth
" Kwa hiyo amekuweka wewe askari wake? akauliza mama yake kwa ukali huku akikishika kitasa cha mlango wa Happy.
" Mama please !!!..Happy anahitaji kuwa mwenyewe kwa sasa...naomba tafadhali usimsumbue hadi kichwa chake kitakapotulia.." akaomba Margreth . Mama yake akamuangalia kisha akasema.
" Nahitaji kuongea na happy...Jambo lililotokea ni zito sana .Sikutegemea kama siku moja Happy angeweza kuwa na tuhuma kama hizi..Halafu nataka kufahamu huyu Patrick ni yule yule aliyekuwa amefariki au ni Patrick yupi? Mambo haya yametuchanganya akili zetu mno...." akasema mama yake akiwa amesimama pale mlangoni akimuangalia Margreth..
" Mama nakuomba tafadhali mpe Happy nafasi ya kuweza kutuliza kichwa chake kwa sababu jambo hili ni zito sana..Baada ya kutulia atatupa majibu ..." akajibu Margreth..
" Ulikuwa unafahamu kwamba Happy ana mahusiano na huyo Patrick? Mama yake Happy akamuuliza Margerth huku amemkazia macho.Margreth akashindwa kujibu akabaki ameinama chini.
" Naomba unijibu Margreth..Ulikuwa ukifahamu kwamba Happy ana mahusiano na Patrick? Umewahi kuonana na huyo Patrick? Naomba unijibu tafadhali"
"Mama suala hili ni gumu sana .Ni Happy pekee ambaye anaweza akakueleza na si mimi" akajibu Margreth kisha akaondoka kwa kasi akaelekea chumbani kwake akajifungia.
" Masikini Happy..kwa nini lakini yamemtokea haya? Namuonea huruma dada yangu.Anateseka sana kwa sasa..Hakujua kama mambo yangekuwa hivi.." akawaza Margreth..."
" hata mimi sikutegemea kabisa kama mambo yangekuwa namna hii japokuwa nilikwisha hisi toka mwanzo kwamba suala lile halitakuwa na mwisho mzuri.Maamuzi haya waliyoyachukua Patrick na Happy ya kutaka kurejesha mahusiano yao ya kimapenzi lazima yangekuwa na madhara.Tayari wote wana wapenzi na mahusiano yao yamekwisha piga hatua kubwa .Patrick alikuwa katika maandalizi ya kufunga ndoa na Vero.Happy nae tayari amekwisha vishwa pete ya uchumba na Mike.Du ! nashindwa kupata jibu ..Jambo hili limekuwa gumu tofauti na tulivyotazamia." akawaza Margreth akiwa ameka kitandani .
"masikini Patrick harakati zake zote za kutaka kurudiana na Happy zimemfanya aishie gerezani.Itamchukua muda mrefu sana kutoka gerezani na kuna uwezekano asiweze kutoka kabisa kama atahukumiwa kunyongwa.MasikiniPatrick kwa nini kila mara akiwa na Happy yanamkuta haya? Why always you Patrick? namuonea huruma sana kwa sababu mara ya kwanza alifungwa kwa kosa kama hili la mauaji na alifanya mauaji yale akiwa katika harakati za kumuokoa Happy. Safari hii anarejea gerezani kwa kosa kama .lile la mwanzo la mauaji .Ouh Patrick ! nashindwa kuelewa ni kwa nini mambo haya yanakutokea......" Margreth akafuta machozi yaliyokuwa yakimtoka.
"Ni ukweli ulio wazi kwamba Patrick na Happy wanapendana sana Sina shaka kabisa na hilo kwa sababu hata baada ya kutengana kwa miaka mingi na kila mmoja akalazimika kuendelea na maisha yake ikiwa ni pamoja na kuanzisha mahusiano mapya lakini mara tu walipokutana tena ile mbegu ya mapenzi yao ya dhati ambayo bado iko mioyoni mwao imechipua kwa kasi kubwa na kuwafanya watake kurudisha tena mahusiano yao na kuamua kuachana na wapenzi wao wa sasa" akawaza margreth na mara simu yake ikaita.Akaichukua na kuangalia mpigaji.Alikuwa ni Mike.Margreth akavuta pumzi ndefu na kuangalia simu ile ikiita na kukatika.Ikaita kwa mara ya pili na kukatika.Ikaanza kuita tena kwa mara ya tatu ,akapiga moyo konde na kuipokea.
" hallow Mike" akasema Margreth.Mike akasikika akivuta pumzi ndefu na kusema
" Margreth sifahamu nianzie wapi kwa mambo haya yaliyojitokeza. Nahisi kichwa changu kinaweza kupasuka kwa mawazo mazito niliyonayo.Margreth naomba tafadhali unifafanulie juu ya mambo haya yaliyotokea ili niweze kufahamu tukio lile limetokeaje tokeaje." akauliza Mike.Margreth akanyamaza akafikiri kidogo kisha akasemaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mike nasikitika kwamba sina lolote la kuweza kukwambia kwa sasa.Mambo haya hata mimi yamenistua sana .Tafadhali Mike naomba uniache kwanza ili niweze kulifahamu suala hili kwa undani wake " akasema Margreth.
" Margreth tafadhali naomba unieleze hata kile kidogo unachokifahamu kuhusiana na tukio hili.Najua lazima kuna jambo unalifahamu.Niambie kuhusu huyu kijana Patrick ambaye anasemekana alikuwa na Happy usiku wa tukio.Niambie Margreth huyu Patrick na Happy wana mahusiano yoyote? Walikuwa wanafanya nini usiku huo walipokutwa na msichana aliyefariki?" akauliza Mike.Margreth akaanza kuhisi kijasho kwa mbali.
" Mike kama nilivyokwambia awali kwamba suala hili limetustua sana hata sisi na mpaka sasa hivi hakuna yeyote mwenye kufahamu undani wa jambo hili.Ni Happy pekee ndiye mwenye kufahamu.Ni yeye pekee ndiye mwenye kuweza kukueleza ukweli halisi." akasema Margreth.
" Unaweza ukanisaidia ili niweze kuongea naye? akasema Mike.
" hapana Mike..Kwa sasa Happy amepumzika .Jambo hili lililomtokea ni jambo kubwa na zito kwa maana hiyo anahitaji kupewa muda wa kutosha ili aweze kutuliza kichwa chake...." akasema Margreth.
" Margreth naelewa kuna kitu unakifahamu lakini hutaki kuniambia.Kuna jambo gani linaendelea kimya kimya ?Na kwa nini hutaki kunieleza? Nimeyaona macho ya Happy pale kituo cha polisi na nimehisi kuna jambo amb........." Mike akakatishwa ghafla na Margreth.
" Mike tafadhali naomba uniache nipumzike.Nipigie baadae" Margreth akakakata simu.
" Jamani mbona happy ameleta mambo ! Mike anateseka sana kijana wa watu.Amekuja toka Marekani kwa lengo la kukaa na kufurahi na Happy lakini badala ya furaha imekuwa ni majonzi .Happy kwa nini umewatesa watu wengi namna hii? Kwa mara ya kwanza ninaona ingekuwa vyema kama wewe na Patrick msingekutana kabisa katika maisha yenu yaliyobakia" akawaza Margreth
* * * *
Ni saa mbili za usiku bado Happy amejifungia chumbani kwake.Toka amerejea nyumbani hajatoka chumbani kwake na hajataka kuonana na mtu yeyote yule.usiku huu familia yake yote ilikuwa imekaa mezani ikijiandaa kwa ajili ya chakula cha usiku.
" Happy amekwisha taarifiwa kuja hapa mezani? akauliza mzee Kibaho baba yake Happy
" Nimejaribu kugonga mlango wake lakini amekataa kunifungulia.Nilipomgusia kuhusu suala la chakula amesema kwamba hasikii njaa.Nina wasi wasi sana na happy kwa sababu toka amerejea hapa nyumbani hajatia kitu chochote tumboni." akasema margreth.
" Ngoja nikamtoe huko chumbani.Asituumize vichwa huyu mtoto." akasema mama yake Happy akionekana kukasirika.
" hapana usiende..Ntakwenda mimi" akasema mzee Kibaho akainuka na kuelekea katika mlango wa chumba cha Happy akagonga mlango na kusema taratibu
" Happy mwanangu naomba unifungulie mlango nataka kuongea nawe." akasema mzee Kibaho.Happy hakujibu kitu.Mzee Kibaho akagonga tena mlango.
" Happy !! fungua mwanangu.."
Toka ndani ya chumba ikasikika sauti dhaifu ya Happy
" Daddy I want to be alone...I'm sorry"
" Happy nafahamu kwamba unahitaji nafasi ya kuwa peke yako lakini naomba niongee nawe dakika tatu tu"
Kikapita kimya kifupi mlango ukafunguliwa.Sura ya Happy ilikuwa imesawajika.Macho yake mazuri yalivimba na kuwa mekundu kwa kulia.Baba yake akashikwa na uchungu mwingi kwa hali ile aliyomkuta nayo mwanae akamkumbatia na kumfariji.
" Be strong my dear,you are going to be fine...you'll be ok" akasema mzee Kibaho huku akimpiga piga mwanae mgongoni .Kitendo kile kikaamsha tena kilio kwa Happy.Baba yake akamketisha katika sofa lililokuwamo mle chumbani na kumfuta machozi.
" Daddy why always me? akauliza Happy huku akilia.
" Happy mwanangu usilie ,usisikitike na wala kuhuzunika na kujiuliza kwa nini wewe? Nafahamu moyo unauma sana lakini naomba ufahamu kwamba matatizo tumeumbiwa sisi wanadamu na matatizo huja pasi na taarifa.Matatizo yanatukomaza na kutufanya tuwe majasiri hivyo kaza moyo mwanangu na yote yatakwisha.Sisi sote tuko pamoja nawe katika kipindi hiki kigumu kwako..we love you and we support you..."
Maneno yale ya mzee Kibaho yakamfariji sana Happy akafuta machozi .Mara akaingia mama yake akiwa na sahani iliyojaa chakula akaiweka mezani halafu akaenda kukaa pembeni ya Happy.
" Pole sana mwanangu.Huyu baradhuli anataka kukuharibia maisha yako..Kila nikikuona ninapatwa na hasira kali.Kwa nini atake kukusababishia matatizo makubwa namna hii? Ouh Happy mwanangu naomba umuogope kabisa kijana huyo..achana naye kabisa huyo shetani......."
Happy akayafikicha macho yake , akamtazama mama yake na kusema
" Mama tafadhali naomba usirudie tena kumtukana Patrick na kumuita shetani " akasema happy akionyesha kukerwa na kauli ile ya mama yake.
" Mwanangu ninaumia sana kukuona ukiwa katika hali hii.Nina hasira sana na huyo kijana ambaye ninamfananisha na shetani kwa sababu ametaka kukuingiza katika matatizo makubwa.Amesababisha ukalala polisi.Ameliharibu jina lako zuri.Happy mwanangu nakuomba uvunje kabisa urafiki na huyo kijana ..."
" Mom thats enough !!!..tafadhali naomba usiongee kitu ambacho hukifahamu..Naomba niwafahamishe wazazi wangu kwamba Patrick huyu ambaye mnasikia nilikuwa naye wakati tukio hilo linatokea ni yule yule ambaye alifungwa jela kwa ajili yangu.Patrick hakufa kama ilivyokuwa imezushwa."
Wazazi wake wakastuka sana kwa taarifa ile .Wakatazamana usoni. Happy akaendelea
"Katika tukio hilo naomba mfahamu kwamba ni mimi ndiye niliyemsukuma Veronika akajigonga ukutani na kupoteza maisha na wala si Patrick kama watu wanavyofahamu.Kwa kuniepusha mimi na adhabu ya kufungwa,kunyongwa au kifungo cha maisha jela,Patrick ameamua kuubeba yeye mzigo wote wa kesi hii na yeye kuonekana ndiye muuaji.Amefanya yote haya ili kuniweka mimi huru.I'm free now because of him..so this man doesnt deserve to be called a devil. Akasema Happy machozi yakaanza kumtiririka upya.
Hakuna aliyeongea tena wote wakaa kimya.Mzee Kibaho akambembeleza Happy ale chakula japo kidogo Happy akakubali akala chakula.Mama yake alikuwa ameshika tama akimtazama mwanae.
Ni saa tatu kasoro za usiku Savana alikuwa ndani ya chumba kimoja katika kituo cha polisi akizungumza na Patrick.
" Patrick kesho utapandishwa mahakamani kwa mara ya kwanza kusomewa shitaka halafu utapelekwa mahabusu katika gereza la Uwangwa. Hautaweza kupatiwa dhamana kutokana na uzito wa kosa lenyewe. Nasikitika sana Patrick kwa kupandishwa kizimbani lakini yote haya ni matakwa yako ...Lakini usijali nitatumia kila uwezo nilionao kuhakikisha kwamba unashinda kesi hii.." akasema Savana .Patrick akainama akafikiri kisha akasema
"Nashukuru sana Savana kwa msaada wako mkubwa.Jambo ulilonifanyia ni kubwa sana .Kuhakikisha kwamba Happy anaachiwa huru ni jambo kubwa sana kwangu." akasema Patrick huku akitabasamu
" Patrick mimi siwezi kupingana nawe katika maamuzi yako lakini bado nina mashaka sana na maamuzi uliyoyafanya ya kuamua kuubeba mzigo wa Happy..unafikiri yeye anakupenda kiasi cha kuweza kufanya kama ulivyofanya wewe?..anaweza kuyatoa maisha yake kwa ajili yako? akauliza Savana
" Ninamuamini Happy ananipenda na kwa hilo sina shaka naye.." akasema Patrick..
" Ndiyo unamuamini lakini una hakika kwamba anakupenda kiasi cha kuweza kuyatoa maisha yake kwa ajili yako? akauliza Savana.Patrick akanyamaza kimya.
" Patrick nimekuuliza makusudi swali hili kwa sababu wewe ni rafiki yangu,ninakujali na kukuthamini na ndiyo maana sitaki sadaka hii ya maisha yako uliyoitoa kwa ajili ya Happy iende bure..Nina wasi wasi sana lakini sitaki kuingilia masuala ya ndani ya moyo wako.Wewe ndiye mwamuzi wa maisha yako. Ninachotaka kukuhakikishia kwamba mimi na timu yangu tutasimama kidete na kwa uwezo wetu wote tulionao tutajitahidi kwa kila tuwezavyo kukutetea katika kesi hii..." akasema Savana na kuagana na Patrick akaondoka.Kichwa chake bado kilikuwa kizito mno kuhusiana na kesi hii ya Patrick.
" Patrick ananisikitisha sana .kila nikimuona ninaumia mno..kwa nini ayaweke maisha yake katika hatari kwa kosa la mtu mwingine? ..Patrick ni mtu wangu muhimu sana na nitafanya kila niwezalo ili kumsaidia ." akawaza Savana.
Saa tano za usiku Savana akawasili nyumbani kwake.Akashuka garini na kuelekea ndani.Msichana wake wa kazi alikuwepo sebuleni akimsubiri.Savana akasalimiana naye na kuelekea moja kwa moja chumbani kwake.Mumewe george tayari alikuwa amejilaza kitandani .Mara tu Savana alipoingia akamuendea George akamtikisa na George ambaye alikuwa ameanza kupitiwa na usingizi akaamka.Savana akambusu mumewe halafu akaelekea bafuni kaoga na kurejea kitandani.Akambusu mumewe na kugeukia upande wa pili tayari kwa kulala.
" Savana kuna jambo gani limekutokea katika siku hizi tatu? Nakuona umebadilika sana..Unachelewa kurudi na ukirudi unakuwa umechoka na hutaki hata kuongea na mimi tena.Una matatizo gani? George mume wa Savana akauliza
" George naomba uniache kwa sasa kichwa changu kina mambo mengi mazito" akasema Savana
" Savana naomba unisikilize.Mimi ni mumeo na nina haki ya kukuuliza .Siwezi kukuona ukichelewa kurudi nyumbani na hunielezi chochote .Huna tena muda na mimi mumeo.Unanipa wasi wasi sana Savana.Hebu angaliani hii ni saa ngapi unarejea nyumbani kama mke wa mtu? akauliza George ambaye alionekana kuanza kukasirika.
" George nina kesi ngumu ninayoisimamia kwa sasa .Patrick anashikiliwa kwa kosa la mauaji.." akasema Savana.
" Patrick !! akauliza George kwa mshangao.
" Ndiyo..Patrick..Ina maana hujasikia tukio lililotokea siku tatu zilizopita likimuhusisha Patrick na mauaji? akauliza Savana
" Patrick huyu ambaye aliwahi kuwa mpenzi wako? akauliza George
" Ndiye huyo...." akasema Savana.George akainuka na kumuangalia Savana usoni.
" Sasa nimepata picha halisi.Kumbe kuchelewa kote huku ni kwa ajili ya kesi ya aliyowahi kuwa mpenzi wako..Kwa maana hiyo yeye ni muhimu sana kuliko mimi mumeo ? akauliza George
" George tafadhali usiseme maneno hayo.Patrick ni rafiki yangu na mteja wangu vile vile kwa hiyo sina budi kuishughulikia kesi yake..Kuna tatizo gani kuisimamia kesi yake ? akasema Savana.
" Tatizo lipo..tena tatizo kubwa..Unasimamia kesi nyingi lakini hakuna hata siku moja umewahi kurejea nyumbani usiku kama huu..Yaani unamthamini Patrick ambaye ni muuaji kuliko hata mumeo? Lakini sioni kama ni jambo la ajabu kwa sababu nilihisi lazima jambo hili litatokea siku moja.Bado hujaweza kumtoa Patrick moyoni mwako.Pamoja na miaka hii yote kupita lakini bado hujafanikiwa kumtoa Patrick moyoni mwako..You still love him ...I'm so stupid" akasema George.Savana akainuka na kumtazama George kwa hasira
" George tafadhali naomba usiseme hivyo..Ndiyo niliwahi kuwa mpenzi wa Patrick lakini baada ya kukupata wewe nikaachana naye kwa sababu tayari yeye alikuwa na mpenzi wake Veronika.I'm with you now and not Patrick." akasema SavanaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" Yes you are with me ..but am I in your heart? akauliza George
" george mambo gani hayo unayaongea leo? akauliza Savana.
" Savana nafahamu kabisa kwamba hujawahi kumsahau Patrick. Nimekununulia vito vingi vya thamani lakini mbona huvivai na unaendela kuvaa vile alivyokununulia Patrick? You still love him isnt it? akauliza George ambaye tayari alipandwa na hasira
" George ...!! akasema Savana.George akamkaribia Savana na kumuangalia usoni.
" Savana naomba uniangalie machoni na uniambie kwamba unanipenda na unanipenda mimi peke yangu.." akasema George.
" George mambo gani haya unayafanya? ...akauliza Savana
" Savana nimekuuliza swali mbona hunijibu? Huna jibu la kunipa?
Savana akabaki kimya akimtazama George huku akihema kwa nguvu.
" Nilijua tu.You never loved me.All this long you still love Patrick..." akasema George
" George hebu achana na hayo mawazo yako ya kijinga..You know I've always loved you..." akasema Savana.
" Do you love me Savana? Una hakika kwamba unanipenda? akauliza George
"yes I love you and you kow that" akajibu Savana
" Vizuri..sasa kama kweli unanipenda naomba ufanye yafuatayo..Nataka uachane kabisa na kusimamia kesi ya Patrick..Kama kweli mimi ni mumeo na unanipenda nataka uachane na ukae mbali kabisa na kesi hii" akasema George.Savana akainama akafikiri kisha akainua uso wake.macho yake yalijaa machozi.Akamuangalia George usoni kisha akatikisa kichwa.
"I'm sorry George I cant do that..siwezi kufanya hivyo unavyotaka nifanye...Patrick is my friend and he needs me now more than ever..siwezi kuacha kumtetea hata iweje.akasema Savana.George akamuangalia kwa makini usoni kisha akasema.
" Vizuri..huwezi kuacha kumtetea kwa sababu unampenda .Kama hivyo ndivyo naona ni bora nikuache huru uendelee kumtetea Patrick ashinde kesi na uje uishi naye hapa.Mimi nimechoshwa na vituko vyako Savana.Toka tumeanza kuishi pamoja mpaka leo hii ni vituko kila siku..Ni miaka mingapi mpaka leo na hutaki hata kusikia suala la mtoto? Nimechoka Savana.Nakuacha uendelee na huyo Patrick." akasema George huku akivaa nguo zake.Savana akasimama na kumuangalia George kwa macho makali.
" Mimi naondoka Savana..nitakuja kuchukua vitu vyangu kesho..Siwezi kuendelea kuishi nawe wakati moyo wako unampenda mtu mwingine..Siwezi kuendelea kugombania nafasi katika moyo wako..nafasi ambayo tayari amekwisha pewa mtu mwingine.Nimevumilia mengi na ninashukuru kwa kupata jibu leo kwamba chanzo cha haya yote ni Patrick..Nakutakia maisha mema na huyo mhalifu wako...." akasema George
" Dont you dare insult Patrick again infront of me...kwa taarifa yako ninampenda Patrick na nitafanya kila niwezalo niwe naye tena..You are nothing compared to him." akasema Savana kwa hasira..George akakasirika na kutaka kumnasa Savana kibao
" ukijaribu kunigusa nitahakikisha unaozea gerezani...." Savana akamtisha George ambaye alimuangalia kwa hasira kisha akaanza kuondoka.Savana machozi yakamtoka akajitupa kitandani kwa hasira
" Patrick siwezi kukuacha hasa kwa kipindi hiki..Niko tayari kwa lolote lile lakini si kuacha kukutetea..Hakuna mtu yeyote ambaye atanizuia nisikutetee ..Nitasimama nawe hadi dakika ya mwisho .That bastard George is right.sijaweza kukutoa katika moyo wangu hadi leo hii..I still love you so much Patrick.I'll make you love me Patrick and when this is over you'll be mine" akawaza Savana
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment