Simulizi : Miss Tanzania
Sehemu Ya Nne (4)
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
" Mimi naondoka Savana..nitakuja kuchukua vitu vyangu kesho..Siwezi kuendelea kuishi nawe wakati moyo wako unampenda mtu mwingine..Siwezi kuendelea kugombania nafasi katika moyo wako..nafasi ambayo tayari amekwisha pewa mtu mwingine.Nimevumilia mengi na ninashukuru kwa kupata jibu leo kwamba chanzo cha haya yote ni Patrick..Nakutakia maisha mema na huyo mhalifu wako...." akasema George
" Dont you dare insult Patrick again infront of me...kwa taarifa yako ninampenda Patrick na nitafanya kila niwezalo niwe naye tena..You are nothing compared to him." akasema Savana kwa hasira..George akakasirika na kutaka kumnasa Savana kibao
" ukijaribu kunigusa nitahakikisha unaozea gerezani...." Savana akamtisha George ambaye alimuangalia kwa hasira kisha akaanza kuondoka.Savana machozi yakamtoka akajitupa kitandani kwa hasira
" Patrick siwezi kukuacha hasa kwa kipindi hiki..Niko tayari kwa lolote lile lakini si kuacha kukutetea..Hakuna mtu yeyote ambaye atanizuia nisikutetee ..Nitasimama nawe hadi dakika ya mwisho .That bastard George is right.sijaweza kukutoa katika moyo wangu hadi leo hii..I still love you so much Patrick.I'll make you love me Patrick and when this is over you'll be mine" akawaza Savana
ENDELEA................
Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu ilifurika watu waliokuja kufuatilia kesi ya mauaji inayomkabili Patrick.Taarifa za Patrick kupandishwa kizimbani na kusomewa shitaka la mauaji zilisambaa kwa kasi na kupelekea idadi kubwa ya watu kujaa mahakamani .Patrick hakuwa mtu anayefahamika sana lakini kutokana na vyombo vya habari hususani magazeti kuandika habari ya tukio lile la kusababisha kifo watu wengi walitaka kumfahamu na hasa baada ya kuandikwa kwamba alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mrembo aliyeitikisa nchi kwa uzuri wake Miss Tanzania Happy kibaho.
Saa tano za asubuhi gari mbili za polisi zikawasili katika mahakama ya kisutu.Patrick akashushwa garini na kuingizwa mahakamani chini ya ulinzi mkali.Savana na jopo la mawakili wanaomtetea Patrick tayari walikwisha fika mahakamani kuanzia asubuhi .Siku hii Savana alionekana mkimya na mwenye mawazo mengi.
" Happy amekuja leo? Patrick akamuuliza Savana wakati wakisubiri kesi yake itajwe.
" Mpaka mida hii sijamuona bado .Inawezekana amefika lakini amejificha mahala akiogopa waandishi wa habari " akasema Savana.
"Ukifanikiwa kuonana naye mpe salamu zangu" akasema Patrick.
" masikini Patrick amejibebebsha mzigo mzito ambao si wake.Sina hakika kama happy anafahamu uzito wa mzigo huu alioubeba Patrick kwa ajili yake." akawaza Savana.
" Savana umefuatilia maendeleo ya baba yangu kule hospitali na kujua anaendeleaje? akauliza Patrick
" Hapana Patrick bado sijafuatilia lakini leo nikitoka hapa nitaelekea hospitali kwenda kumjulia hali baba yako": akasema Savana.
" Nimesababisha matatizo kwa watu wengi . Vero amefariki,baba yangu amelazwa hospitali ,na wengine wengi wameumia sana kwa ajili ya maamuzi yangu. I deserve this..ninastahili adhabu hii ya kukaa gerezani" akasema Patrick kwa sauti ndogo.Savana hakumjibu kitu bali akachukua faili lake na kuanza kumuelekeza Patrick jambo fulani.
Hatimaye kesi ya kusababisha kifo inayomkabili Patrick ikatajwa kwa mara ya kwanza .Mshitakiwa katika kesi hiyo ambaye ni Patrick akasomewa shitaka la kusababisha kifo cha Veronika na hakutakiwa kujibu chochote.Kesi ikapangwa kutajwa tena baada ya wiki tatu na mshitakiwa akaamriwa kupelekwa mahabusu katika gereza jipya la Uwangwa kigamboni.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" Usihofu Patrick .Kesi hii tunaifuatilia kwa umakini mkubwa .Niko pamoja nawe katika kila dakika.Naomba uondoe hofu na uniamini " .Akasema Savana akimpa moyo Patrick wakati akisubiri kupanda katika basi maalum la kubebea mahabusu na kupelekwa gerezani.
" Nakuamini Savana na sina shaka hata kidogo na wewe.Ulifanikiwa kuonana na Happy? akauliza Patrick
" happy sijaonana naye .Nadhani hajafika mahakamani siku ya leo" akasema Savana.
" Una mawasiliano yake" akauliza Patrick
" Nina namba za simu za mdogo wake Margreth.Nitampigia baadae nifahamu maendeleo yake" akasema Savana .Muda huo huo akaingia mmoja wa mawakili wanaounda jopo la kumteta Patrick akamuomba Savana waongozane kuna suala la kisheria linalohitaji ufumbuzi wa haraka.Savana akaagana na Patrick kwa ahadi ya kwenda kumtembelea gerezani kesho yake.
" kwa nini Happy hajafika mahakamani? Ana matatizo gani?Pengine ameshindwa kufika akiogopa macho ya watu " akawaza Patrick baada ya Savana kuondoka.
" Mama ,ndugu zangu na marafiki nimewaona mahakamani .Wote wamekuja kunifariji na kunipa moyo.Japokuwa nimewaudhi na kuwaumiza sana kwa mambo niliyoyafanya lakini bado wananipenda na wamekuja kunionyesha kwamba bado tuko pamoja.Ni familia ya Happy pekee ambayo haijafika mahakamani.Napatwa na wasi wasi nini kimetokea? I love Happy and I trust her with my life.." akawaza Patrick na mara sura ya Veronika ikamjia kichwani akafumba macho na kuuma meno.
" masikini Veronika sina taarifa atazikwa lini.Laiti nigekuwa na uwezo ningehudhuria mazishi yake lakini siwezi tena.Niko mikononi mwa sheria.Pumzika kwa amani vero.Utabaki ndani ya moyo wangu daima.Nitazikumbuka zile nyakati zote za furaha tulizowahi kuwa nazo katika mapenzi yetu. Daima nitaukumbuka upendo wako,ukarimu na ucheshi wako.Natambua ulinipenda kwa moyo wako wote.Kama siku moja nitabahatika kutoka gerezani nitalitafuta kaburi lako na kuweka maua meupe uliyokuwa unayapenda sana enzi za uhai wako,lakini kama nitahukumiwa kunyongwa au kufungwa maisha basi tutakutana mbinguni kwa baba.Pumzika kwa amani Veronika sikutegema kabisa kama mambo yangekuwa namna hii." akawaza Patrick huku akijizuia asidondoshe machozi.
Saa nane za mchana Patrick akapakiwa katika basi maalum la kubebea mahabusu na safari ya kuelekea gereza la Uwangwa ikaanza.Taratibu basi likaanza kuondoka.Kupitia dirishani Patrick akaweza kumuona mama yake ambaye alikuwa amekaa chini kutokana na kuishiwa nguvu,kaka yake Alois akiwa na mkewe,rafiki yake Andrew akiwa na mchumba wake Vick pamoja na ndugu wengine,na marafiki.Wengi walikuwa na nyuso za huzuni kubwa na wengie walishindwa kujizuia kutokwa na machozi.
Patrick akawapungia mkono na taratibu basi likaondoka maeneo ya mahakama kuelekea mahabusu katika gereza la Uwangwa ambako anakwenda kuanza maisha mapya.
Gari moja aina ya Lexus lenye rangi nyeusi lilikuwa limeegeshwa katika mahakama ya kisutu.Hakuna mtu aliyekuwa ameitilia maanani gari ile wala kuifuatilia.Ndani ya gari ile yenye vioo vyeusi walikuwemo wasichana wawili waliokuwa wamekaa kimya.Mmoja wao alikuwa akitokwa na machozi
“Happy nyamaza kulia.You have to remain strong.Kulia hakutakusaidia chochote na wala hakutabadili hali halisi ya mambo.Ukumbuke vile vile kwamba tears is the sign of defeat.Usikubali kushindwa Happy.Simama imara na kumpa nguvu Patrick .Simama katika maamuzi yako.” Margreth akampa dada yake maneno ya faraja.
“Margreth najitahidi sana kujipa moyo na ujasiri lakini najikuta nikishindwa.Kila nikifikiria kuhusu tukio lile najikuta nikiangusha machozi.Nasikia uchungu mkubwa moyoni.namuonea huruma Patrick na wakati huo huo sijui nifanye kitu gani..ouh Patrick..!!!!..Amebeba jukumu zito sana .Amejitwisha mzigo wangu.Ni mimi ndiye niliyestahili kuwepo mahakamaini mida hii na si yeye lakini kwa upendo wake usio na kifani amejitolea kuubeba mzigo huu nilioustahili.Sijui nitaulipaje upendo huu mkubwa alionionyesha Patrick.I’m confused !!” akasema Happy.Margreth akamtazama halafu akamshika bega
“Happy huna haja ya kuendelea kulia .Unachotakiwa kufanya kwa sasa ni kukubaliana na kilichotokea na kujipanga kuikabili hali hii na kuona namna tutakavyoweza kumsaidia Patrick ambaye amefanya kitendo ambacho mimi nakiita ni cha kijasiri sana na ameyatoa maisha yake kwa ajili yako.Jukumu lako kwa sasa ni kumpa kila aina ya ushirikiano unaohitajika na kuhakikisha kwamba anashinda kesi.Kwa hiyo Happy nakushauri uwe jasiri sana na ujasiri wako ndicho kitu pekee cha kumpa Patrick nguvu ya kuhimili kukaa gerezani.” Akasema Margreth
“Margreth, si kwamba nashindwa kuwa jasiri ,lakini kuna nyakati ninajikuta nikiwa dhaifu sana hasa kila nikikumbuka mambo yaliyotokea.Things happened so fast.Sikutegemea kama mambo yangefika hapa yalipofika.”
“Huna haja ya kujilaumu Happy.Yaliyotokea yametokea na na kuna usemi usemao kwamba kila jambo hutokea kwa sababu.Ninaamini hata suala hili limetokea kwa sababu maalum pia.Jiulize ni kwa nini jambo hili limetokea sasa? Muda ambao zilibaki siku chache Patrick afunge ndoa na Vero? Huoni kwamba hapa kuna sababu kubwa ya nyie kukutana tena na mambo yakawa hivi yalivyokuwa ?.Happy kama kweli moyo wako unampenda Patrick na kama ndiye mwanaume wa maisha yako tafadhali simama imara katika msimamo wako huo.This is for your own life and your own happiness.” Akasema Margreth
“Nimekuelewa Maggy.Naomba nikuhakikishie kwamba ninampenda Patrick na ndiye mwanaume pekee wa maisha yangu .Sintaubadili msimamo wangu,I’ll fight for him.Nitas………..” Happy akanyamaza ghafla akaelekeza macho yake nje.Gari mbili za polisi zilikuwa zinaingia pale mahakamani na nyuma yake kulikuwa na basi la kijani ambalo ni maalum kwa kubebea mahabusu na kuwaleta mahakamani.Happy alibaki ameyakodolea macho magari yale.Alikosa neno la kusema.
“Nadhani mahabusu ndio wanaletwa mahakamani” akasema Margreth.
Happy bado aliendelea kuyakodolea macho magari yale hadi yaliposimama.Mapigo ya moyo wake yalibadilika na kuanza kwenda kwa kasi kubwa na machozi yakamtoka.
“Usilie Happy.Nilifahamu kwamba utaumia sana na ndiyo maana nikakuzuia usije mahakamani siku ya leo.Twende tuondoke maeneo haya.Turudi nyumbani ukapumzike” akasema Margreth
“No Maggy,let me stay here.I need to be here .I’m supposed to be here” akasema Happy.Katika mashavu yake ilionekana michirizi ya machozi yakitiririka.Baada ya dakika kama mbili hivi akainamisha kichwa
“I’m so stupid !!!..so stupid !!!!....” akasema Happy kwa uchungu huku akikipiga piga kichwa chake.
“Calm down Happy…..!!!!” akasema Margreth
“Maggy,I’m so stupid” akasema tena Happy kwa sauti ya masikitiko
“I’m so stupid Margreth..Mtu aliyeyatoa maisha yake kwa ajili yangu yuko mahakamani lakini ninashindwa kuingia mle ndani na kumuonyesha kwamba niko pamoja naye katika kipindi hiki kigumu kwake.Nashindwa kuonyesha ushirikiano.I’m real so stupid.” Akasema Happy
“You are not stupid Happy.Nakufahamu vizuri dada yangu.You are strong woman.You’ve been and you are always so strong so don’t become weak now.Huu ni wakati unaotakiwa kuwa na ujasiri wa hali ya juu sana.” Akasema Margreth.Happy akafuta machozi akauangalia mlango wa kuingilia mahakamani akakishika kitasa cha mlango wa gari.
“Maggy,I cant be such a stupid.Happy isn’t that coward.Naingia mahakamani” akasema Happy huku akiufungua mlango wa gari tayari kwa kushuka.Margreth akamzuia.
“Hapana Happy huwezi kushuka.”
“Kwa nini Maggy? Kwa nini nisiingie mahakamani? Patrick atajisikiaje asiponiona mahakamani leo? Please Maggy let me go”
“Happy,nafahamu umuhimu na ulazima wa wewe kuwepo mahakamani lakini siku ya leo sidhani kama itakuwa vyema uingie mle ndani.Kuna watu wengi leo na hasa waandishi wa habari ambao wanategemea kukuona mahakamani ili wakupige picha na kuzipamba kurasa zao za mbele.Nakushauri siku ya leo usiingie mahakamani badala yake unatakiwa kwenda kumtembelea Patrick gerezani kila mara na hapo ndipo utakapopata nguvu na ujasiri wa kuweza kuikabili hali hii na ndipo utakapoweza hata kuhudhuria mahakamani.Endapo utaingia mle ndani utashindwa kujizuia na utaangua kilio.Utazidi kuumia”
Happy akabaki kimya kwa muda wa kama dakika tatu hivi akitafakari
“Nahisi kuchanganyikiwa Margreth.Sijui nifanye nini “ akasema Happy
“twende tuondoke hapa.Twende turudi nyumbani ukapumzike”
“Nadhani hilo ni jambo la msingi kwa sasa.Nirudishe nyumbani nikapumzishe kichwa changu” akasema Happy na Margreth akawasha gari wakaondoka kurejea nyumbani.
“Usife moyo Happy ,mambo haya yatakwisha.Tuzidi kumuomba Mungu” Margreth akampa moyo dada yake wakiwa njiani kurejea nyumbani.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hii ni mara ya pili sasa Patrick anaingia gerezani kwa ajili yangu.Mara ya kwanza aliua bila kukusudia wakati akiniokoa nisidhalilishwe na genge la wahuni.Safari hii ni mimi ndiye niliyesababisha kifo lakini bado ameamua kuubeba mzigo huu wote wa mauaji na sijui hatima yake itakuwa nini.Huu ni upendo wa ajabu sana ambao sijawahi kuuona katika zama hizi.Sielewi ni kwa nini Patrick ananipenda namna hii kiasi cha kufanya haya anayoyafanya .Huu ni zaidi ya upendo ambao hauelezeki kwa maneno.Huyu ndiye mwanaume wa maisha yangu Nitampenda hadi mwisho wa uhai wangu.” Akawaza Happy akiwa amejiinamia.
“Nina deni kubwa sana kwa Patrick.Nimefanya kosa kubwa kutokuoenekana mahakamani siku ya leo.Sijui atakuwa amejisikiaje kwa kutoniona mahakamani .Najua alitegemea sana kuniona na ingemfariji sana kuona kwamba tuko pamoja katika wakati huu mgumu.Sintakubali suala kama hili lijitokeze tena.Kuanzia sasa sintaogopa mtu yeyote Yule.Nitasimama imara na Patrick hadi dakika ya mwisho.” Bado Happy aliendelea kuwa na mawazo mengi sana.Safari yao ilikuwa inaendelea kimya kimya.
Hatimaye wakafika nyumbani .Mtumishi wa ndani akawafungulia geti wakaingia.Mara tu walipoingia ndani Happy akapatwa na mstuko mwingine baada ya kuliona gari moja dogo jeupe lenye namba za kibalozi likiwa limeegeshwa mle ndani.Mapigo ya moyo yakabadilika na kuanza kumwenda mbio .
“Ouh Gosh ! Its Mike.” Akasema Happy huku uso wake ukiwa umebadilika.
“Sitaki kuonana na naye kwa sasa.Nitafanya nini Margreth?
“Usiogope Happy.Huna haja ya kumkimbia Mike.Onana naye ana kwa ana.” Akasema Margreth.
“I’m not ready Margreth .I’m not ready to face him yet” ( siko tayari Margreth.Siko tayari kuonana naye ana kwa ana”
“Hakuna namna nyingine ya kufanya Happy zaidi ya kuonana na Mike.Nadhani ni wakati muafaka sasa kwa Mike kuufahamu ukweli halisi.He loves you and he deserve to know the truth”( anakupenda na ana haki ya kuufahamu ukweli”
“Not now Margreth.Siko tayari kuongea lolote na Mike kwa sasa”
“Ok Happy kama kama hauko tayari kuongea naye lolote kwa saa siwezi kukulazimisha kufanya hivyo lakini hata hivyo twende ndani ukasalimiane naye halafu uende chumbani kwako.Mimi nitaongea naye na kumuelewesha kwamba akusubiri hadi hapo utakapokuwa tayari kuzungumza naye” akasema Margreth.Happy akavuta pumzi ndefu na kuufungua mlango wa gari akashuka.
Margreth ndiye aliyekuwa wa kwanza kuingia sebuleni akifuatiwa na Happy.Pale sebuleni alikuwepo mama yao pamoja na Mike.Mara tu Margreth na Happy walipoingia Mike akasimama na sura yake ikaonyesha tabasamu kwa mbali.
“Hallo Happy” Mike akamsalimu.
“Hallo Mike” Happy akajibu huku akiwa amekiinamisha kichwa chake chini.Mike akamsogelea na kutaka kumshika mkono lakini Happy akausogeza mkono wake ili Mike asiushike.
“Unajisikiaje Happy.” Akauliza Mike
“Naendelea vizuri .” akajibu Happy
“Nafurahi kusikia hivyo.Nimekuwa na wasi wasi mwingi sana juu ya maendeleo yako Happy.Nashindw…” Mike hakumaliza alichotaka kukisema Happy akamkatisha
“Mike tutaongea siku nyingine.Nimechoka sana naomba uniruhusu nikapumzike.tafadhali sana naomba unisamehe Mike” akaomba Happy halafu akaanza kutembea kuelekea chumbani kwake.
“Happy !!!....akaita Mike.Sura yake ilionyesha huzuni kubwa.
“Mike let her go.She need some rest” akasema Margreth.
“Margreth ninaumia sana nikimuona Happy akiwa katika hali hii.Sijawahi kumuona hata mara moja Happy akiwa hivi”
“Mike !“ akaita Margreth halafu akamsogelea karibu.Mike akageuka na kumtazama
“Happy anapita katika kipindi kigumu sana hivi sasa.Ni kipindi kigumu kupita vyote alivyowahi kupitia.Anahitaji kupewa muda wa kutosha wa kutuliza akili yake.Kwa muda huu hataweza kuongea lolote.Nakushauri Mike vuta subira hadi hapo atakapokuwa tayari ametulia na mtakaa mtaongea” akasema Margreth.Mama yake aliyekuwa amesimama karibu yao akakohoa kidogo na kusema
“Mike maneno ya Margreth ni ya msingi sana.Happy anahitaji muda wa kupumzisha akili yake.Mambo mengi mazito yamemtokea katika kipindi kifupi kwa hiyo bado anahitaji kuirejesha akili yake katika hali ya kawaida.Nakuomba Mike umvumilie mwenzio hadi hapo atakapokuwa tayari”
Mike akainama chini akafikiri kwa muda kisha akasema
“Nimesafiri toka Marekani mpaka hapa kwa lengo moja tu la kuwa karibu na Happy katika wakati ambao niliamini alikuwa ananihitaji sana.Nafahamu katika wakati mgumu kama huu Happy anahitaji mtu wa karibu wa kumfariji na kumfanya awe na furaha ndani ya moyo wake.Nashangaa sana kwa Happy kutokuonyesha dalili za kunihitaji katika wakati huu wa matatizo.Inaonekana kama vile ananikwepa” Akasema Mike kwa sauti ya masikitiko.
“Mike ninafahamu kwamba unampenda sana Happy na ndiyo maana umesafiri safari hii ndefu kwa lengo la kuwa naye katika matatizo yaliyompata.Ushauri wangu kwako ni kwamba muache Happy apumzike kwa siku ya leo na kesho kama atakuwa yuko vizuri basi mtakaa na kuongea kuhusiana na kinachoendelea hivi sasa.” Akasema mama yake Happy.Mike akainamisha kichwa akafikiri kwa muda halafu akainua kichwa na kusema
“Nimekuelewa mama.Nitamuacha Happy apumzike.Nitakuja tena kesho kumtembelea na kujua maendeleo yake.Naomba endapo kutatokea mabadiliko yoyote katika hali yake basi mnitaarifu mara moja ili kwa pamoja tusaidiane namna ya kufanya” Akasema Mike kisha wakaagana akaondoka Margreth akamsindikiza
“Margreth,moyo wangu umeumia sana kwa hali ya Happy.Mpaka hapa niko gizani na sielewi chochote kuhusiana na kilichotokea na kumpelekea Happy awe katika hali hii.Margreth unaweza ukanifahamisha japo kwa muhtasari ni kitu gani kilichotokea na kumfanya Happy awe katika hali hii? Kuna huyu mtu aitwaye Patrick ambaye Happy aliwasiliana naye tukiwa kule hotelini tukipata chakula cha mchana na Happy akabadilika ghafla ni nani? Akauliza Mike
“Mike sina maelezo yoyote ambayo yanaweza kukutosheleza kwa sasa.Kama mama alivyokushauri msubiri Happy atulize akili yake na atakueleza kila kitu kilichomsibu yeye mwenyewe.”akasema Margreth.Mike akamtazama usoni kwa makini na kumuuliza tena
“Kitu gani kinaendelea hapa Margreth? Kuna jambo naona unalifahamu lakini hutaki kunieleza.Unazidi kunipa wasi wasi.Naomba kama kuna kitu unakifahamu kinachomsumbua Happy nieleze ili kwa pamoja tuweze kukitafutia ufumbuzi.”
“Mike kama nilivyokwambia kwamba sina chochote cha kukwambia.Mwenye maelezo yote na anayeweza kukueleza kwa ufasasa na kwa kina juu ya kilichompata na kinachomsumbua ni Happy mwenyewe.Kwa hiyo naomba umsubiri yeye mwenyewe hadi hapo atakapokuwa tayari” akasema Margreth.
“Nimekuelewa Margreth.Nitakuja tena kesho kumuangalia Happy” akasema Mike na kuingia garini akaondoka.
*********************
Basi la kubeba mahabusu likiwa linaongozwa na magari mawili ya polisi liliendelea kuikata mitaa ya jiji hili la Dar es salaam likielekea maeneo ya Kigamboni.Patrick alikuwa mmoja wa mahabusu kumi waliokuwamo katika basi hili,wote walikabiliwa na kesi za mauaji.Wakati wote wa safari macho yake yalikuwa nje akitazama majengo mazuri ya jiji hili pamoja na pilika mbali mbali za kila siku
“ Patrick gerezani tena “ akasema kwa sauti ndogo na kisha akainama chini
“Sikutegemea kama mambo yangekuwa namna hii.Sikutegemea kama suala hili lingenirejesha tena gerezani” akaendelea kuwaza Patrick huku gari likienda kwa kasi.
“Kuna nyakati najiuliza ni kwa nini Happy ametokea tena kwa wakati huu? Baada ya kupita kwa miaka mingi iweje ajitokeze sasa? Yote haya yaliyotokea yametokea kwa sababu ya kuonekana kwake tena.Endapo asingetokea kwa wakati huu yasingetokea haya yote” Akawaza Patrick halafu akainua kichwa akatazama nje
“Kuna kitu kimoja ambacho kinanifanya niamini kwamba kutokea kwa Happy katika wakati huu ni kwa sababu maalum.Ilipangwa iwe hivi.Japokuwa vikwazo ni vingi lakini ni ukweli usiopingika kwamba mimi na Happy tumepangiwa tuwe pamoja na kamwe hatuwezi kutenganishwa.Vero hakuwa amepaumbwa kwa ajili yangu na ndiyo maana yametokea haya yaliyotokea.Ninaamini hivyo kwa sababu ya upendo mkubwa uliopo kati yangu na Happy.Licha ya kutengana kwa miaka mingi lakini tumeonana tena na kujikuta tukiwa bado tunapendana tena kwa kiwango kikubwa sana na ndiyo maana kwa pamoja mioyo yetu ilikuwa tayari hata kuachana na wapenzi wetu wa sasa kwa lengo moja tu la kuwa pamoja tena.Lakini pamoja na hayo yote bado kuna kitu kinachotutenganisha mimi na Happy.Hata hivyo kwa vyovyote vile itakavyokuwa sintabadili msimamo wangu.Nitasimama katika maamuzi yangu.Happy ndiye mwanamke pekee ambaye ninamuhitaji katika maisha yangu.Niko tayari kwa lolote lile hata kama ni kuhatarisha maisha yangu kwa ajili yake.Sitaki kuuficha ulimwengu juu ya mapenzi yangu mazito kwa Happy.Kwa wale wanaofahamu nini maana ya mapenzi ya kweli wataungana nami na kusimama upande wangu lakini wale wasioelewa maana ya penzi la kweli watanichukia ,watanibeza na kunilaani.Nitaubeba mzigo wa lawama ,chuki na laana zote nitakazopewa kwa sababu ya upendo wangu kwa Happy ulionipelekea nikafanya maamuzi haya niliyoyafanya.” Akawaza Patrick na mara sura ya Happy ikamjia kichwani, akatabasamu
“ I love you Happy and I will always love you my angel”( Nakupenda Happy na nitakupenda daima malaika wangu) akasema kimoyomoyo.Kwa sasa gari lilikuwa linalivuka daraja kuelekea Kigamboni liliko gereza kubwa la Uwangwa gereza ambalo hutumika kuwahifadhi watu wenye kesi kubwa kubwa hasa za mauaji.Kupitia dirishani Patrick aliweza kushuhudia namna watu walivyokuwa wakiendelea na shughuli zao za kiuchumi baharini.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mida hii nilipaswa niwe kazini nikiendelea na shughuli zangu kama watu wengine lakini niko garini naelekea gerezani.Mipango na malengo yangu yote ya maisha vimepotea.Sijilaumu kwa kilichotokea kwa sababu naamini ilipangwa iwe hivi.Nimefanya haya yote kwa sababu ya mwanamke ninayempenda kuliko wote duniani” akawaza Patrick na kuendelea kutazama nje huku gari likiendelea na safari yake kwa kasi.
“Nasikitika sana kwa kifo cha Vero.Sikutegemea kama suala hili lingesababisha Vero apoteze uhai wake.Inauma sana lakini sikuwa na namna nyingine ya kufanya zaidi ya kuusikia moyo wangu na kuufuata.Moyo wangu umeniambia kwamba Happy ndiye mwanamke wa maisha yangu na siku zote moyo wangu huwa haunidanganyi.Hata hivyo kifo cha Vero kimeniumiza sana.Tukio hili ni moja kati ya matukio ambayo hayatafutika katika historia ya maisha yangu hadi naingia kaburini.” Akawaza Patrick.Sura ya Vero ikamjia akainamana na kufuta machozi.
“Bado nazikumbuka zile nyakati zetu za furaha enzi za uhai wake.Tulipendana sana na sikutegemea hata kidogo kwamba mwisho wetu ungekuwa namna hii.Inaniuma sana na siku zote nitaendelea kumkumbuika .Vero ni mwanamke ambaye nimetoka naye mbali toka nikiwa gerezani Songea.Alinisaidia sana wakati ule nikiwa gerezani .Alinifanya nisiyaone magumu maisha ya gereza.Hata wakati ule nilipoamini kwamba Happy amenisaliti bado Vero alisimama nami ,akanifariji na kunifanya nitake kuishi tena.Baada ya kutoka gerezani alijitahdi kwa kila alivyoweza kuhakikisha kwamba ninayaanza upya maisha yangu.Amekuwa na mchango mkubwa sana katika kuyajenga upya maisha yangu na ninaweza kusema kwamba ni mmoja kati ya watu waliochangia sana mimi kufika hapa nilipofika.Siku zote yeye ndiye alikuwa mfariji wangu,mshauri wangu na msimamizi wangu katika kila jambo ninalolifanya.Sina shaka na upendo wake kwangu.Vero alinipenda kwa moyo wake wote na alikuwa tayari kufanya lolote na kwa wakati wowote kwa ajili yangu.Nini kimetokea hadi yakatokea haya yaliyotokea?!!!...” Patrick akainama chini kichwa chake kilijaa mawazo na macho yake yalikuwa na machozi.
“ Nilimpenda sana Vero lakini Kosa moja tu alilolifanya ni kutunga ule uongo na kunitenganisha na Happy.Alifanya hivi bila kufahamu kwamba mimi na Happy ni watu ambao hakuna awezaye kututenganisha zaidi ya Mungu pekee.Tunapendana kwa dhati ya mioyo yetu na tayari mioyo yetu imekwisha ungana.Ouh Vero …..!!!!!” Patrick alisikia maumivu ya moyo kana kwamba kuna kisu kikali kinaukata.Wakati huo gari lilikuwa linamalizia kulivuka daraja la Kigamboni.
“Kwa nini Happy hajatokea mahakamani leo? Nilitegemea kumuona akiwa miongoni mwa watu waliokuja kusikiliza kesi yangu ikitajwa.Ningefarijika sana kama ningeiona sura yake.Inawezekana hakutokea mahakamani kwa sababu kuna jambo limemsibu.Inawezekana akawa ni mgonjwa.Ninamfahamu vizuri Happy asingeweza kukosa mahakamani leo lazima kuna jambo linamsumbua .Au inawezekana akawa anakwepa macho ya watu na waandishi wa habari ambao wengi walitegemea kumuona mahakamani leo.Maskini Happy ameingia katika matatizo makubwa.Tayari alikuwa na maisha yake mazuri yaliyotulia,alikuwa na machumba wake anayempenda, alikuwa na ndoto nyingi za maisha yake lakini baada tu ya kukutana na mimi ndoto zake zote zimepotea.Nasikitika sana kwa jambo hili.Hana muda mrefu toka amelitwaa taji la Miss Tanzania lakini katika kipindi hiki kifupi tayari amekwisha tengeneza vichwa vya habari kwa kuhusika kwake na tukio la kifo cha Vero.Sifa yake kama mrembo wa Taifa imepotea na kwa mara nyingine historia imejirudia kwa warembo wanaovishwa taji hili la kuingia katika kashfa .Simlaumu Happy kwa alichokifanya .Alikuwa akilipigania penzi lake la kweli .Alimsukuma Vero kwa lengo la kuniokoa mimi kwani ni wazi Vero alikuwa na kila dalili za kufanya tukio baya” Bado Patrick aliendelea kuwaza mambo mengi kuhusiana na tukio lile lililopelekea kifo cha Vero na yeye kukabiliwa na kesi ile ya kusababisha kifo.Kwa sasa gari lile la mahabusu lilikwisha ishika njia ya kuelekea gerezani.
“Japokuwa kuna watu ambao hawakubaliani moja kwa moja na maamuzi yangu ya kumtoa Happy katika kesi hii ambayo ilikuwa imkabili yeye na mzigo wote kuubeba mimi,bado sijutii kufanya hivyo hata kidogo kwa sababu hata siku moja sintakubali mwanamke nimpendaye aingie gerezani.Niko tayari kwa adhabu ya aina yoyote ile lakini si kumuona Happy akiteseka gerezani.Nitaipokea adhabu hiyo kwa mikono miwili kwa sababu nitakuwa nimeibeba adhabu ambayo alistahili kuibeba mwanamke ninayempenda kuliko wanawake wote duniani.”
Gari lilipunguza mwendo na kusimama.Akachungulia nje walikuwa wamesimama katika geti la kwanza la kuingilia hapo gerezani.
“Nakumbuka Savanna hakukubaliana nami kabisa katika uamuzi wangu huu wa kumtoa Happy katika kesi hii na jukumu lote kulibeba mimi.Nalikumbuka swali aliloniuliza kama je Happy naye yuko tayari kuyatoa maisha yake kwa ajili yangu kama mimi nilivyofanya kwake? Patrick akanyanyua kichwa akatazama nje.Gari liliruhusiwa kupita na kuendelea na safari ya kuelekea gerezani.
“Swali kama Happy yuko tayari kufanya kama nilivyofanya mimi ni swali gumu sana kulipatia jawabu lakini sina shaka na Happy.Japokuwa siwezi kuusemea moyo wake lakini nina uhakika kwamba anaweza akafanya lolote kwa ajili yangu kama alivyokubali kuuvunja uhusiano wake na mchumba wake kwa lengo moja tu la kuwa nami.Ninaamini ananipenda kwa dhati ya moyo wake .Patrick akawaza,akainua kichwa akatazama juu halafu akaninama tena chini.
“Sijui hali ya baba ikoje huko hospitali.Nimewaumiza watu wengi kwa maamuzi yangu.Kwanza ni familia yangu.Baba hali yake si nzuri hata kidogo.Ndugu zangu,marafiki wameumizwa sana na kitendo hiki cha kuuvunja uchumba wangu na Vero.Familia ya vero nayo imeumizwa sana kwanza kwa kuuvunja uchumba na mtoto wao na pili kwa kusababisha kifo cha binti yao.Ninaamini kamwe hawataweza kunisamehe kwa jambo hili.Familia ya Happy pia imeumizwa sana na jambo hili.Mtoto wao ameingia katika kashfa nzito ya kusababisha mauaji wakati wa ugomvi wa kimapenzi.Jina lake limechafuka.Hawakutegemea hata siku moja mtoto wao waliyemlea katika maadili aingie katika kashfa kubwa kama hii.Yote haya yamesababishwa na mimi.Mchumba wa Happy aitwaye Mike sifahamu atakuwa katika hali gani akiufahamu ukweli kwani sina hakika kama tayari Happy amekwisha muweka wazi kwamba uhusiano kati yao umefika mwisho.kwa ujumla nimeumiza watu wengi sana.Rafiki zangu walijitolea michango mingi mikubwa ili kuhakikisha kwamba harusi yangu inakuwa ya kihistoria .Wote hawa wameumizwa kwa kiwango cha juu kabisa na nina hakika itawachukua muda mrefu sana kunisamehe lakini pamoja na hayo sikuwa na namna nyingine ya kufanya zaidi ya kuchukua maamuzi haya magumu niliyoyachukua kwa ajili ya kuipigania furaha ya maisha yangu.Siku zote yanapofanyika maamuzi magumu lazima wawepo watu watakaoathirika na maamuzi hayo na ndiyo maana yakaitwa ni maamuzi magumu.Natakiwa nisimame katika maamuzi yangu na nionyeshe msimamo japokuwa si kazi rahisi hata kidogo na inahitaji ujasiri mkubwa sana lakini hata hivyo lazima nifanye hivyo.Haya ni maisha yangu na ninachokipigania hapa ni furaha ya maisha yangu.Pumzika kwa amani Vero.Nitakukumbuka siku zote za maisha yangu na nina hakika huko uliko utanisamehe” Akawaza Patrick na kuyafuta machozi. Tayari gari lilikwisha fika gerezani.Mlango ukafunguliwa na mahabusu wote wakashushwa garini na kuingizwa gerezani
Akionekana ni mwenye haraka Savanna akawaaga mawakili wenzake ambao kwa pamoja wanamtetea Patrick kisha akaingia katika gari lake ,akaliweka lundo la vitabu na nyaraka katika kiti cha pembeni akaufunga mkanda akawasha gari na kuondoka maeneo ya mahakamani.
“Nitaisimamia kesi hii hadi nihakikishe Patrick anashinda.Ni kesi ambayo haiwezi kunisumbua hata kidogo.Nitafanya kila niwezalo kuhakikisha kwamba Patrick hafungwi.Patrick ni mtu wa muhimu sana kwangu .Nakumbuka wakati tukiwa bado na mahusiano ya kimapenzi alinipa penzi la kiwango cha juu mno na kumfanya awe ni mwanaume wa pekee kabisa kwangu.Anajua kupenda ,anajali,na anafahamu mwanamke anahitaji nini toka kwa mwanaume.Nathubutu kusema kwamba sijaona wa mfano wake.Japokuwa tulisitisha mahusiano yetu baada ya mimi kumpata George lakini mpaka leo hii sijaweza kumsahau hata kidogo.Kuna nyakati nikiwa nafanya mapenzi na George ninahisi kama ninaiona sura ya Patrick na mara kadhaa nimewahi kujisahau na kulitamka jina la Patrick kutokana na kuhisi uwepo wake karibu yangu.Wakati mwingine ili nipate hisia za kimapenzi lazima niivute taswira ya Patrick ndipo ninasisimka.Bado nampenda na sijafanikiwa kumtoa moyoni mwangu.Huu ni wakati wangu wa kumrudisha Patrick kwangu na kitu kikubwa kitakachonifanya nimrejeshe kwangu ni namna nitakavyomjali na kumpigania katika wakati huu mgumu .Anahitaji mtu wa kuwa naye karibu katika kipindi hiki na mtu huyo lazima niwe mimi.Nitakuwa naye karibu nitamfariji,na mwishowe atakuwa wangu tena.” Akawaza Savanna akiwa garini.
“Kwa nini Happy hajatokea mahakamani leo? Sina hakika kama anampenda Patrick kiasi cha kuweza kuyatoa maisha yake kama Patrick alivyofanya..Nikitoka hospitali nitakwenda kujua nini kimemsibu na kwa nini hakufika mahakamani siku ya leo.Nimeanza kuwa na wasi wasi sana na huyu Happy na nina imani baada ya muda si mrefu Patrick atakijutia kitendo chake cha kuubeba mzigo alioustahili Happy ambaye ameshindwa hata kufika mahakamani kuonyesha kwamba anajali.” Akawaza Savanna
Ilimchukua Savanna takribani saa moja kufika katika hospitali kuu ya magonjwa ya moyo alikolazwa baba yake Patrick.Akashuka garini na kutembea kwa kasi kuelekea katika vyumba vya wagonjwa walio katika uangalizi maalum.Kwa mbali akamuona Alois kaka yake Patrick akiwa nje akamsogelea.Alois alipomuona Savanna akakatisha maongezi na mtu aliyekuwa akiongea naye simuni.
“Hallo mheshimiwa “ Alois akamsalimu Savanna.Huku akitabasamu Savanna akasema
“Ouh Alois niite Savanna inatosha sana.”akasema Savanna
“Karibu sana Savanna.”
“Ahsante Alois” akajibu Savanna halafu kikapita kimya kifupi
“Alois tulionana kule mahakamani lakini hatukupata wasaa wa kuzungumza lolote .Pilika pilika zilikuwa nyingi sana.” Akasema savanna.
“Usijali Savanna,hata mimi niliona namna ulivyokuwa na shughuli nyingi.Ninafahamu ugumu uliopo katika kusimamia kesi kubwa kama hizi na ndiyo maana sikutaka kukusumbua.Hata hivyo Savanna naomba nikushukuru sana kwa kuamua kulibeba jukumu hili la kumtetea Patrick katika kesi hii ngumu” akasema Alois
“Ahsante Alois.Kesi inayomkabili Patrick ni kesi ngumu sana ,ni kesi ya mauaji lakini nitajitahidi kufanya kila niwezalo kuhakikisha kwamba Patrick anashinda kesi hii”
“Savanna,sisi kama familia tuko pamoja nawe na tuko tayari kulipa gharama zozote zile zinazohitajika katika kesi hii.”
“Patrick ni mtu wangu wa karibu sana na nimeamua kuifanya kazi hii bila malipo yoyote yale.Kitu pekee nitakachokihitaji toka kwenu kama familia ni kumpa Patrick ushirikiano mkubwa katika wakati huu.Mambo yote yaliyotokea na kusababisha tofauti katika familia naomba muyaweke pembeni kwa wakati huu.Kwa pamoja tutashinda jambo hili” akasema Savanna
“Usihofu kuhusu hilo Savanna.Patrick ni ndugu yetu na pamoja na yote aliyoyafanya lakini hatutaweza kumuacha.Tutatoa kila aina ya ushirikiano unaohitajika .Vipi kuhusu Yule binti Happy,mbona sijamuona mahakamani leo? Akauliza AloisCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hata mimi sifahamu ni kwa nini hajatokea mahakamani leo”
“Savanna,sielewi ni kwa nini kila mara Patrick anapokuwa na huyu Happy lazima jambo baya limfike.Mara ya kwanza aliwahi kufungwa gerezani kwa kosa la kuua bila kukusudia akiwa na huyu huyu Happy.Safari hii amefanya tena kosa lile lile la mauaji akiwa na huyu huyu Happy.Ninahisi msichana huyu ana mkosi na ndiyo maana kila mara lazima mambo mabaya yamfike Patrick.Kitu kingine,sielewi ni kwa nini ameibuka katika wakati huu ambao tayari maisha ya Patrick yametulia na alikuwa anakaribia kufunga ndoa na Vero.Kuibuka kwake kumeharibu kila kitu ikiwamo na maisha ya Patrick.Vero amefariki na Patrick anakabiliwa na mashtaka ya mauaji..Ninamchukia sana Happy na sitaki hata kuonana naye uso kwa uso kwani ninaweza kughafirika na kufanya jambo baya linaloweza kuniletea matatizo.Naomba Mungu aniepushe kabisa nisikutane na Yule mwanamke uso kwa uso na hasa katika siku hizi za karibuni.” Akasema Alois kwa hasira.
“Alois,mambo haya yamekwisha tokea na hatupaswi kulaumiana kwa sasa.Tunachotakiwa kukifanya ni kukabiliana na hali halisi iliyojitokeza.Si Patrick wala Happy aliyetegemea wala kupanga kwamba kingetokea kifo cha Vero.Hakuna aliyejua kama mambo haya yangefika hapa yalipofika.”
“Nakubaliana nawe Savanna lakini moyo wangu unauma sana kwa jinsi huyu Happy alivyomuweka ndugu yangu katika matatizo makubwa.Sina hakika kama nitaweza kumsamehe .Si mimi tu bali hata familia yote kwa ujumla.Yeye ndiye chanzo cha haya yote.Ametusababishia jeraha kubwa ambalo litachukua muda sana kupona” akasema Alois
“Alois huna haja ya kumchukia Happy.Kama nilivyokueleza kwamba si Patrick wala Happy aliyetegemea kama jambo kama hili litatokea na kufika hapa yalipofika.Tuachane na hayo,nimekuja kujua hali ya mzee anaendeleaje?
“Hali ya mzee si nzuri hata kidogo.Baada tu ya kutoka mahakamani tulitaarifiwa kwamba hali yake ilikuwa inazidi kuwa mbaya.Muda mfupi uliopita amehamishiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.Kwa ufupi hali yake bado si nzuri hata kidogo.Hapa tunasubiri madaktari watueleze nini kinaendelea.Tunafikiria hata kufanya mpango wa kumpeleka nje ya nchi lakini endapo italazimika kufanya hivyo.Mama na ndugu wengine wako kule ndani mimi nimechomoka mara moja kwa ajili ya kuja kupiga simu.” Akasema Alois
“Dah ! Poleni sana Alois.” Akasema Savanna halafu kikapita kimya kifupi Savanna akasema
“Alois kwa kuwa kinachosubiriwa kwa sasa ni taarifa ya madaktari kuhusiana na maendeleo ya mzee,mimi naona niondoke nikaendelee na shughuli nyingine.Utanifahamisha kuhusu maendeleo yake” Akasema Savanna na kubadilisha namba za simu na alois.
“Usihofu Savanna,lolote litakalotokea nitakutaarifu mara moja” akasema Alois kisha wakaagana na Savanna akaondoka.
“Kwa namna nilivyoiona sura ya Alois ,inaonyesha hali ya baba yake katu si nzuri.Mungu amsaidie mzee Yule apone haraka kwa sababu endapo ikatokea akafariki dunia mambo yatazidi kuwa mabaya sana kwa Patrick.” Akawaza Savanna wakati akiligeuza gari lake na kuondoka maeneo ya hospitali.
“Kwa sasa ngoja nikaonane na Happy nifahamu nini sababu iliyomfanya ashindwe kufika mahakamani siku ya leo.Nilikuwa namtazama Alois machoni wakati akiongea kuhusiana na namna anavyomchukia Happy,hakuwa akitania hata kidogo.Ni wazi anamchukia mno Happy toka moyoni.Suala hili linazidi kuchukua sura mpya kila uchao.Kwa hivi sasa mambo haya yatahamia katika famila.Chuki kubwa itajengeka baina ya familia hizi .Familia ya Happy katu haitaweza kutazamana na familia ya Patrick na ile ya Vero katu hawatakuja kuelewana na ile ya Patrick.Dah.!!....” akawaza Savanna na mara simu yake ikaita.Akatazama mpigaji alikuwa ni George
“I’m sorry George,siwezi kupokea simu yako kwa sasa.” Akasema Savanna na kuirusha simu pembeni.Simu ikaendelea kuita lakini hakusumbuka hata kuitazama tena.
“George aliniudhi sana kiasi kwamba sihitaji hata kuiona sura yake tena .Kwa sasa akili yangu yote nimeielekeza katika kitu kimoja tu.Kumsaidia Patrick ashinde kesi.Pamoja na kushinda kesi hii lakini nina kazi nyingine ngumu ya kumrudisha Patrick katika himaya yangu tena.Yeye ni mwanaume pekee ambaye aliwahi kunifikisha mawinguni kwa raha alizokuwa akinipa.Naapa pamoja na ugumu wote uliopo nitamrejesha kwangu.Najua moyo wake umekufa ukaoza kwa Happy lakini hii hainipi shida hata kidogo.Nitafanya kila niwezalo kumrejesha kwangu tena” akawaza Savanna
* * *
Mlio wa kengere ya getini ulimfanya Margreth ainuke sofani na kwenda kuangalia mtu aliyekuwa akigonga.Hakuamini alipokutana na msichana mmoja mrembo na wakili maarufu,Savanna
“Dada Savanna !!..shikamoo” akasema Margreth
“Marahaba Margreth.Habari yako?
“Habari yangu nzuri dada ” Akasema Margreth huku akilifungua geti na Savanna akaingiza gari ndani
“Karibu sana dada Savanna,karibu ndani” akasema Margreth akimuongoza Savanna kuelekea ndani
“Pole na matatizo dada ” akasema Margreth huku akimuwekea Savanna kinywaji mezani
“Nimekwisha poa Margreth.Poleni nanyi pia.Matatizo haya ni yetu sote.”
“Ahsante dada Savanna.” Akajibu Margreth halafu kikapita kimya kifupi.Savanna akasema
“Happy anaendeleaje? Sijamuona leo mahakamani.Patrick alipatwa na wasi wasi sana na akaniomba nifike nijue kilichomsibu” akasema Savanna
“Dada Savanna hali ya Happy si nzuri hata kidogo na ndiyo maana hata leo alishindwa kuingia mahakamani japokuwa alikuwepo pale mahakamani.Nadhani itakuwa vyema kama nitakupeleka chumbani kwake ukaongee naye wewe mwenyewe.” Akasema Margreth na kumuongoza Savanna kuelekea chumbani kwa Happy
“Karibu sana Savanna” akasema Happy akiwa amekaa kitandani.Macho yake yalikuwa mekundu na yamevimba kwa kulia.Nywele zake ndefu na nzuri zilikuwa zimetawanyika.Kwa ujumla alitia huruma sana mnyange huyu wa Taifa.
“Pole sana Happy” akasema Savanna
“Nimekwisha poa Savanna”
“Happy mimi si mkaaji sana,nimepita mara moja kujua hali yako baada ya kutokuona mahakani leo .Patrick alipatwa na wasi wasi mwingi na akanituma nifike nijue hali yako na kama kuna jambo limekusibu” akasema Savanna
“Savanna nilifika mahakamani leo lakini nilishindwa kuingia ndani ya mahakama” akasema Happy
“Kwa nini Happy? Akauliza Savanna
“Niliogopa kukutana na macho ya watu pamoja na waandishi wa habari.Niliogopa vile vile kukutana na ndugu za Patrick ambao sijui wangenitazamaje kwani moja kwa moja wanafahamu kwamba mimi ndiye chanzo cha matatizo yote yanayomkuta mtoto wao.Najua Patrick atakuwa na mawazo mengi sana kwa kutoniona mahakamani leo .I’m so stupid Savanna….I’m so stupid “ akasema Happy kwa masikitiko.Savanna akamtazama kwa makini na kusema
“Sikiliza Happy,huu si wakati wa kujilaumu kwa kilichotokea.Si wewe wala Patrick aliyetegemea mambo haya kufika hapa yalipofika.Yaliyotokea yameshatokea na hatupaswi kushughulika nayo ila tunachopaswa kushughulika nacho kwa sasa ni athari zilizotokana na kilichotokea.Patrick kwa upande wake tayari amekubaliana na kilichotokea na ndiyo maana ameamua kulibeba jukumu zima ambalo ulistahili ulibebe wewe,kwa hiyo basi nakushauri na wewe usimame imara na usimamie kile kilichowapelekea mkafika hapa mlipofika kwa ujasiri mkubwa.Ikabili jamii na usiogope kitu chochote kile.Usiogope kwamba utaonekanaje kwa kuivaa kofia hii ya Miss Tanzania.Kofia hii ni ya kupita tu kwa maana hiyo usiogope kupigwa picha ukiwa mahakamani ukisikiliza kesi ya Patrick.Kuanzia sasa futa machozi na usimame imara.Kumbuka utakuwa ni mmoja wa watu watakaosimama mahakamani kutoa ushahidi wao kwa hiyo jitahidi kuanzia sasa uwe jasiri”
Maneno yale ya Savanna yalimuingia Happy vilivyo.Akainama akatafakari
“Tumeelewana Happy ? akauliza Savanna
“Savanna nakushukuru sana kwanza kwa kuja kunitembelea.Ujio wako na maneno yako machache yenye nguvu vimenifanya nipate nguvu mpya.Nakuahidi sintalia tena.Nitasimama imara kumtetea Patrick.Siku zote nitakuwa karibu yake na kumpa moyo kwa sababu ameubeba mzigo mzito ulionistahili mimi.Nimefanya kosa kubwa sana kutokuingia mahamani leo .Savanna naomba uniombee msamaha kwa Patrick kwa kitendo hiki.Nilikuwa dhaifu sana kukabiliana na hali halisi” akasema Happy huku kwa mbali machozi yakimlenga.
“Usijali Happy,nitamuelewesha Patrick na atakuelewa ,ila kumbuka kuyafanyia kazi hayo niliyokwambia..Patrick needs you now more than ever.Anahitaji ushirikiano wetu sote kwa wakati huu .Kila mmoja kwa upande wake anatakiwa aonyeshe ushir…………………….” Savanna akanyamaza ghafla kutokana na mlio wa simu yake.Akaitoa na kutazama mpigaji alikuwa ni Alois kaka yake Patrick.Savanna akamtazama Happy usoni huku simu yake ikiendelea kuita.
“It’s Alois “ akasema Savanna kwa sauti ndogo
“Pokea usikie anataka kukueleza kitu gani.” Akasema Happy.Savanna akavuta pumzi ndefu halafu akabonyeza kitufe cha kupokelea simu.
“Hallo Alois “ akasema Savanna baada ya kupokea simu.Baada ya sekunde kadhaa taratibu Savanna akajikuta akishusha mkono wenye simu chini.Sura yake ilikuwa imebadilika ghafla.
“Ouh My God !! “ akasema Savanna na kuzidi kumuogopesha Happy
“Savanna kuna tatizo gani? Akauliza Happy ambaye alistushwa sana na mabadiliko yale ya ghafla ya Savanna aliyekuwa amesimama huku mkono wake wa kulia ukiwa kifuani .
“Savanna kuna tatizo gani? Mbona umebadilika ghafla.Kuna taarifa gani toka kwa Alois? Is Patrick ok? Akauliza Happy.
“Baba yake Patrick amefariki” akasema Savanna.Happy akaishiwa nguvu akajikuta akikaa kitandani.
“Ouh Mungu wangu ,mambo haya yanazidi kuwa makubwa kila siku” akasema Happy kwa wasi wasi
Savanna akiwa bado chumbani kwa Happy simu yake ikaita tena.Safari hii alikuwa ni Andrew.
“Hallo Andrew..!!” akasema Savanna baada ya kupokea simu
“Savanna kuna taarifa mbaya imenifikia sasa hivi.baba yake Patrick amefariki dunia.” Akasema Andrew.
“Hata mimi nimezipata taarifa hizo muda si mrefu .Alois amenipigia kunitaarifu kuhusu msiba huo.kwa sasa uko wapi?
“Niko ofisini kwangu lakini baada ya kupata taarifa hizi ninaelekea hospitali kupata uhakika zaidi na kujua nini kinachoendelea”
“Sawa Andrew hata mimi nakuja huko hospitali” akasema Savanna na kukata simu halafu akamfuata Happy pale kitandani.
“Happy naomba tafadhali usihuzunike sana wala kupata mstuko kwa jambo hili.Tulia na muombe Mungu akupe nguvu ya kuweza kuhimili mambo haya na yote yatakayokuja kwani hatujui nini kitatokea huko mbeleni.Hiki ni kipindi kigumu sana kwako ,kwa Patrick na kwetu sote.Endapo utakuwa na tatizo lolote lile nipigie simu haraka sana nitakusaidia.Kwa sasa ngoja nielekee hospitali ili kujua kinachoendelea huko.Akasema Savanna.
“Ahsante sana Savanna.Nashukuru kwa kuja kunitembelea na kunipa moyo.Nitazidi kumuomba Mungu anipe nguvu na kwa pamoja tuweze kukipita kipindi hiki kigumu sana.Kuhusu kifo hiki cha baba yake Patrick nimeshindwa nifanye nini,siwezi kulia wala kufanya lolote.Yote namuachia Mungu” akasema Happy kwa majonzi
“Usilie tena Happy.Kuwa jasiri .Mkabidhi Mungu matatizo yako yote naye atakushindia” akasema Savanna
“Savanna siwezi kukusindikiza.Miguu yangu haina nguvu hata ya kuinuka “Akasema Happy ,akaagana na Savanna akatoka mle chumbani akaelekea sebuleni ambako alimkuta Margreth
“Margreth ,tafadhali naomba uwe karibu sana na Happy ,anapitia kipindi kigumu sana hivi sasa na anahitaji uangalizi wa karibu mno.Tumepata taarifa mpya muda si mrefu baba yake Patrick amefariki dunia kwa shinikizo la damu.Taarifa hii imemstua sana Happy kwa hiyo naomba uwe karibu naye sana kumpa moyo.” Akasema Savanna.Margreth naye alistushwa sana na taarifa ile ya kifo cha baba yake Patrick.Baada ya maongezi mafupi na Margreth,Savanna akaondoka kuelekea hospitali.
“mambo yanazidi kuwa mambo.Suala hili limewaumiza watu wengi hadi hivi sasa.Sifahamu hatima yake ni nini kwani nina hakika chuki inazidi kuongezeka miongoni mwa familia hizi hasa baada ya kifo cha baba yake Patrick leo.Familia ya Patrick itaongeza chuki dhidi ya Happy kwa madai kwamba yeye ndiye chanzo cha haya yote yaliyotokea..Namuonea huruma sana Happy,yuko katika wakati mgumu mno.Patrick naye sijui atazipokeaje taarifa hizi za kifo cha baba yake.Najua ataumia mno” Akawaza Savanna akiwa njiani kuelekea hospitali kuu ya magonjwa ya moyo ili kukutana na ndugu za Patrick
“Bado sijapata taarifa zozote kuhusiana na msiba wa Veronika.Najua Patrick angependa afahamu kinachoendelea kule.Kuna wakati hata mimi najikuta nikiogopa kila nikifikiria jinsi Patrick, Happy pamoja na familia zao walivyo katika wakati mgumu.” Akawaza Savanna
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nilimuonya Patrick mapema sana kuhusiana na athari za jambo hili lakini alinipuuza na akaendelea na harakati zake za kuurejesha uhusiano wake na Happy.Nilifahamu mambo kama haya yangeweza kujitokeza kwa sababu uhusiano wake na Vero tayari ulikwisha kuwa mkubwa na kuota mizizi.Patrick hakutaka kunisikiliza.Laiti angenisikia mambo haya yote yasingetokea” akasema Andrew kwa masikitiko akiwa amesimama na Savanna pale katika hospitali kuu ya moyo.Vilio vya akina mama vilitawala eneo hili.Ilikuwa ni hali ya simanzi kubwa.
“Andrew huu si wakati wa kulaumiana kwa kilichotokea.Hakuna kati yao aliyefahamu kama mambo haya yangefika hapa yalipofika.” Akasema savanna
“ Savanna sikufichi mimi ni mmoja wa watu walioumizwa sana na kitendo hiki alichokifanya Patrick cha kuachana na Vero.Siwezi kuelezea nimeumia kiasi gani lakini naomba ufahamu kwamba nimeumizwa mno.Patrick ni rafiki yangu mkubwa sana lakini kwa hili alilolifanya nitazidi kumlaumu kila siku na pengine baada ya mambo haya kumalizika itanilazimu kuangalia upya kama nitaweza tena kuendelea na urafiki naye.Amekuwa ni mtu asiyetaka ushauri wa mtu yeyote yule .Nilimshauri sana na kumuonya kuhusiana na Yule mwanamke Happy lakini hakunisikia.Yote haya yamesababishwa na Happy. Kama asingejitokeza kwa wakati huu tusingekuwa katika matatizo haya tuliyomo sasa hivi.Namchukia sana Happy.Ninamchukia sana..!!!” akasema Andrew.
“Andrew,sote tumeumizwa na kitendo cha Patrick kuachana na Vero lakini hatupaswi kuelekeza lawama zote kwa Patrick au kwa Happy.Sote tunafanya makosa hapa duniani na sioni sababu ya kila mmoja kuelekeza chuki zake kwa Happy.Kila mtu ninayekutana naye anasema anamchukia Happy nani atakayesimama na kumtetea ? Nani yuko tayari kumsikiliza? Tusiwe wepesi wa kuhukumu namna hii.Hata yeye hakujua kama mambo haya yangetokea.Nawaombeni msimchukie Happy” Akasema Savanna halafu kikapita kimya kifupi
“Vipi una taarifa zozote kuhusiana na msiba wa Vero?
“Nilipanga niende leo ili kujua taratibu za mazishi zikoje.Nilitegemea pengine kungekuwa na ujumbe wa watu toka kwa familia ya akina Patrick kwenda kuwakilisha katika mazishi na kupeleka salamu za pole lakini kutokana na jambo lililojitokeza la kifo cha mzee sidhani kama hilo litawezekana tena.” Akasema Andrew
“Andrew kuna ulazima wa kutuma wajumbe kwenda kwa akina Vero kwani tayari familia hizi zilikwisha unganishwa na upendo uliokuwepo baina ya watoto wao.Hivi sasa kumetokea aina fulani ya chuki iliyoanza kujengeka miongoni mwa familia hizi mbili.Tusiache hilo litokee Andrew.We have to do something” akasema Savanna
“Tutafanya nini Savanna? Mambo haya ni ya kifamilia na hatupaswi kuingilia ugomvi wa familia hizi mbili.”
“Andrew,Patrick ni mtu wetu wa karibu kwa maana hiyo hatupaswi kuwa waoga ,tunachotakiwa kufanya ni kuishawishi familia yake wakubali kutuma ujumbe kwa akina Happy ili kwenda kuwaunga mkono na kupeleka salamu za pole,hii itasaidia sana katika kupunguza chuki na uhasama vilivyoanza kujengeka kutokana na tukio hili .Alois yuko wapi? Akauliza Savanna.Andrew akayaelekeza macho yake katika kundi la akina mama waliokuwa wakilia huku madaktari na wauguzi wakiendelea na jitihada za kuwanyamazisha kwani eneo lile halikuhitaji kelele.
“Inasikitisha sana “ akasema Savanna
“Inauma Savanna.Bado nitaendelea kumlaumu sana Patrick kwani yeye ndiye chanzo cha haya yote.Amesababisha maumivu kwa watu wengi.” Akasema Andrew.Magari matatu yakasogezwa karibu na akina mama wale waliokuwa wakilia,wakaombwa waingie katika magari yale na kuondolewa pale hospitali.Alois ambaye alikuwapo karibu na magari yale aliwaona Andrew na Savanna akawafuata
“Pole sana Alois “ wakasema kwa pamoja
“Ahsanteni sana.Ni kazi ya Mungu ambayo hakuna mwanadamu anayeweza kuipinga.Tunapaswa kushukuru kwa kila jambo kwani yeye ndiye mwenye kutoa na kutwaa” akasema Alois
“kwa kweli hali ya mzee haikuwa nzuri hata kidogo .Tulikuwa na mpango wa kumpeleka nje ya nchi kwa matibabu zaidi lakini madaktari walinihakikishia kwamba hali ya mzee haikuwa na tumaini la kupona kwani hata kama angepelekwa nje ya nchi uwezekano wa kupona ulikuwa mdogo sana.” Akasema Alois
“Poleni sana Alois.Inauma sana jamani.” Akasema Savanna kwa huzuni.Kikapita kimya cha muda mfupi
“Kwa hiyo nini kinaendelea hapa kwa sasa? Akauliza Andrew
“Kwa sasa kinachoendelea ni maandalizi ya shughuli za msiba pale nyumbani kwa mzee.Tunasubiri baada ya ndugu kukusanyika wote tutakaa na kupanga taratibu zote za mazishi .Mpaka sasa bado tunaendelea kusambaza taarifa hizi kwa ndugu jamaa na marafiki walioko hapa jijini na walio nje ya Dar es salaam.” Akasema Alois
“Alois kuna jambo nilitaka kulifahamu .Vipi kuhusiana na msiba wa Vero kuna taarifa zozote mmezipata? Kuna mtu yeyote ambaye ataiwakilisha familia yenu kule? Akauliza Savanna
“Kusema kweli bado sina taarifa zozote kuhusiana na kinachoendelea katika msiba wa Vero na wala bado hatujatuma mtu yeyote kwenda kutuwakilisha kule.Toka lilipotokea tukio hili kumekuwa na mvurugano mkubwa sana.Ahsante sana kwa kunikumbusha kuhusu jambo hili Savanna kwani japokuwa hata sisi tumefiwa na mzee lakini kuna ulazima mkubwa wa kutuma uwakilishi katika msiba wa Vero kwani halitakuwa jambo la busara endapo hatutatuma mtu yeyote kwenda kutuwakilisha.” Akasema Alois
*****************************
Saa moja za jioni dege la shirika la ndege la British airways likatua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.Tayari kiza kimekwisha lifunika anga la jiji hili kuu la kiuchumi nchini Tanzania.
Dege lilisimama,mlango ukafunguliwa na abiria wakaanza kushuka .Miongoni mwa abiria walioshuka ndegeni alikuwa ni mwanamke mmoja aliyekuwa amevaa suti nyeusi.Macho yake yalikuwa mekundu na yamevimba.Alikuwa ameongozana na mwanaume mmoja wa kizungu na watoto wawili.Huyu alikuwa ni Loniki dada yake Vero aliyekuwa akiishi na kufanya kazi nchini Uingereza.Alikuwa amekuja nyumbani Tanzania kuhudhuria msiba wa mdogo wake akiwa ameongozana na mumewe na watoto wao wawili mapacha Patricia na Paula.
Loniki alionekana dhaifu na alikuwa anatembea taratibu.Pale uwanjani walipokelewa na ndugu waliokuwa wakiwasubiri na kuanza safari ya moja kwa moja kuelekea msibani.Hakukuwa na maongezi mengi katika gari watu wote walikuwa katika hali ya majonzi makubwa.
Hatimaye waliwasili nyumbani na vilio vikaamka upya.Loniki akapoteza fahamu kabla hata hajashuka garini.Akabebwa na kupelekwa sehemu yenye uwazi na kuanza kupatiwa msaada .Alipozinduka akapelekwa katika chumba alichokuwamo mama yake pamoja na akina mama kadhaa ambao walikuwa wakimsaidia.Alimkumbatia mama yake na wote wakaanza kulia kwa nguvu.Ilikuwa ni hali ya simanzi kubwa.
“Loniki mdogo wako amekwenda kama upepo.Bado siamini kama ni kweli Vero amekufa.Siamini kama mwanangu amefariki dunia.” Akasema mama yake Loniki huku akilia
“Mama inauma sana.Ni siku chache tu nimeagana naye akirejea Tanzania baada ya kufanya manunuzi ya vitu alivyohitaji kwa harusi yake.Sikujua kumbe ndiyo nilikuwa namuaga.Ilikuwa ni mara yangu ya mwisho kuongea naye.Masikini mdogo wangu ,nitampata wapi tena kama yeye? Loniki naye aliendelea kulia kwa nguvu
Sarah ambaye ndiye anayemfuata Loniki kwa kuzaliwa naye akawasili , akasalimiana na dada yake pamoja na familia yake .Baada ya kusalimiana,Loniki na Saraha wakaelekea bustanini kwa maongezi.
“Sarah moyo wangu umeumia sana kwa kifo cha Vero.Ninahisi ni kama vile roho yangu inataka kutoka.Vero alikuwa ni kila kitu kwangu.Nilimpenda mno kiasi kwamba nashindwa hata nifanye nini.Kama ningekuwa na uwezo wa kumrudisha hai ningefanya hivyo.Hebu nieleze Sarah ili nifahamu namna kifo cha Vero kilivyotokea kwa sababu najiona kama vile bado niko ndotoni.” Akasema Loniki
“Loniki kifo cha Vero kimetokea ghafla sana na hakuna aliyetegemea kama ingekuwa hivi.Nilipigiwa simu na mama siku moja kabla ya Vero kufariki akinitaka kama nina nafasi basi tuongozane kuelekea katika kikao kilichokuwa kimeitishwa nyumbani kwa wazazi wa Patrick kikao ambacho kilikuwa ni maalum kwa ajili ya kuongelea maandalizi ya mwisho ya harusi ya Vero na Patrick.Sikuwa na nafasi ya kuhudhuria kikao hicho hivyo nikamuomba shangazi aongozane na mama .Walifika kikaoni lakini mambo yakawa tofauti na walivyokuwa wametegemea.Wakati kikao kikiendelea Patrick alisimama na kuomba aongee machache.Wote walitarajia labda angeweza kuongelea kuhusiana na harusi yake lakini hakufanya hivyo na badala yake akaanza kutoa historia yake wapi alipotoka na katika historia hiyo alimtaja msichana mmoja aitwaye Happy kwamba aliwahi kuwa mpenzi wake wakati wakisoma na ndiye alikuwa sababu ya yeye kufungwa gerezani mara ya kwanza.Wakati Patrick akiwa gerezani kwa kosa la kuua bila kukusudia wakati akimuokoa Happy asibakwe na kundi la wahuni,Happy alihamia nchini Marekani kwa ajili ya masomo na hapo ndipo Patrick alipokutana na Vero alipokwenda kumtembelea mjomba kule gerezani Songea.Vero alitokea kumpenda Patrick na kama unavyojua Vero huwa akipenda anapenda kupita kiasi.Kwa kuwa alimpenda Patrick alifanya kila lillilowezekana na kujenga urafiki kati yao.Alipoondoka kule Songea kurejea Dar es salaam Patrick alimpatia barua ili aitume kwa Happy.Kwa kuwa tayari alikwisha mpenda Patrick na alikuwa akihitaji awe wake ,Vero hakuituma ile barua na badala yake aliandika barua nyingine ikimtaarifu Happy kamba Patrick amefariki dunia kwa ugonjwa wa kuhara akiwa gerezani.Baadae alikwenda tena kwa Patrick na kumtaarifu kwamba alipata taarifa kwamba Happy tayari ameamua kuolewa na mzungu na tayari ana ujauzito .Huo ukawa ni mwanzo wa Patrick na Happy kutengana na hivyo kumpelekea Patrick kumpa Vero nafasi moyoni mwake wakawa wapenzi na hatimaye uchumba na maandalizi ya ndoa yakaanza.” Sarah akatulia akamuangalia dada yake aliyekuwa amekaa kimya akimsikiliza kwa makini.
“Siku moja tulipata taarifa kwamba Patrick amepoteza fahamu kwa mstuko.Hakuna aliyefahamu sababu ya mstuko ule alioupata uliopelekea apoteze fahamu.Ukweli ni kwamba alipatwa na mstuko baada ya kumuona Happy mpenzi wake wa zamani katika runinga akishiriki kinyang’anyiro cha Miss Tanzania .Baadae Happy na Patrick walionana na ndipo ukweli ulipodhihirika kwamba ni Vero ndiye aliyewatenganisha kwa kutunga uongo.Kitendo hiki kilimchukiza sana Patrick na hivyo mbele ya wazazi ndugu na jamaa akatangaza kuuvunja uchumba kati yake na Vero.Baada ya kauli ile ya Patrick iliyopelekea watu kadhaa kupoteza fahamu,Vero aliondoka na kuelekea nyumbani halafu akachukua bastora ile iliyokuwa ya baba akamfuata Patrick hospitali.Hatujui alikuwa na lengo gani lakini kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwepo eneo la tukio wanadai kwamba Vero alikuwa amedhamiria kuua kwani alikuwa amemuelekezea Patrick bastora na aliachia risasi moja iliyomkosa Happy.Baada ya tukio hilo Patrick na Vero walianza kupambana akiwa na lengo la kumnyang’anya silaha ile lakini katika purukushani hiyo Vero akajigonga ukutani na kufariki hapo hapo.Kwa hivi sasa Patrick anashikiliwa katika mahabusu ya gereza la Uwangwa na kesi yake tayari imekwisha tajwa mahakamani.Yule miss Tanzania Happy ameachiwa huru baada ya kuonekana hahusiki na tukio lile.Kwa ufupi hicho ndicho kilichotokea.Nimeumia sana Loniki.Nimelia mno hadi machozi yamekauka kabisa lakini hakuna namna nyingine ya kufanya zaidi ya kumuombea mdogo wetu apumzike kwa amani “ akasema Sarah.Loniki akainama na kufuta machozi.
“Sarah naomba uende chumbani kwangu katika kibegi kidogo cheusi utakuta kuna mkebe mdogo naomba uniletee” akasema Loniki ambaye machozi bado yaliendelea kumtoka.
Sarah akaenda chumbani na kurejea na mkebe ule mdogo alioutaka Loniki,akaufungua na kutoa sigara akawasha na kuanza kuvuta.Akapiga mikupuo kadhaa na kupuliza moshi mwingi hewani
“Sikutegemea kama Patrick angeweza kumfanyia Vero kitendo kama hiki.Wiki tatu tu kabla ya ndoa anavunja uchumba? Tena kwa sababu ya msichana ambaye ni Miss Tanzania? This is unfair.Hakumtendea haki Vero hata kidogo.Alimfanyia kitendo cha kinyama na kikatili sana.Ameniumiza mno na kwa maumivu haya ninayoyasikia sasa hivi sintaweza kumsamehe hadi siku naingia kaburini.Ameiondoa furaha na pambo la familia yetu.Tulimpenda mno Vero na tulimtunza zaidi ya tulivyojitunza wenyewe,iweje leo atokee Patrick na amtende Vero namna hii??? Patrick must pay for this..I swear in heaven and earth Patrick must pay..!!!!!.” Loniki akasema kwa hasira huku akipuliza moshi mwingi hewani.
“Tayari yuko mikononi mwa sheria na ninafahamu lazima sheria ichukue mkondo wake na haki itendeke” akasema Sarah.
“That’s not enough…,lazima yeye na yeyote aliyeshirikiana naye katika kumkatili uhai mdogo wangu vero ,walipe uovu walioutenda.Damu ya mdogo wangu haiwezi kupotea hivi hivi.They must pay.Sintaondoa mguu wangu Tanzania hadi pale nitakapohakikisha kwamba wote wamelipa.” Akasema Loniki kwa hasira huku machozi yakimtoka na mara akatokea shangazi yao.
“Loniki pole sana ,huu ni wakati mgumu sana.Tunatakiwa tumuombe Mungu atupe uvumilivu wa hali ya juu sana.Mambo haya haujui yataisha vipi kwa sababu tumepokea taarifa sasa hivi kwamba baba yake Patrick naye amefariki dunia kwa shinikizo la damu .” akasema shangazi yao
“What !!!!!!!.....baba yake Patrick naye amefariki dunia ? !! akauliza Sarah kwa mshangao
“Ndiyo Sarah ,amefariki dunia.Sijui Yule kijana alikuwa anafikiria nini hadi akafanya maamuzi haya ambayo yanaathiri maisha ya watu wengi?
“Ouh my God !! “ akasema Sarah huku akivuta pumzi ndefu.
“Hilo ni pigo kwa Patrick na bado yatakuja mengine makubwa zaidi” akasema Loniki
“Loniki usiseme hivyo.Tunatakiwa tumuombe sana Mungu atuepushe na mabalaa mengine yanayoweza kujitokeza kwa sababu jambo hili linaonekana ni kama limekuwa na mkosi Fulani.” Akasema Sarah ambaye kwa haiba yake ni mpole na huongea taratibu
“Sarah huna haja ya kumuonea huruma huyu shetani asiyekuwa na huruma hata kidogo.Amesababisha kifo cha mdogo wetu .Kama asingeuvunja uchumba wake na Vero basi ndugu yetu angekuwa hai hadi hivi sasa.Mimi simuonei huruma hata kidogo na ninaapa kwa miungu yote kwamba Patrick na huyo kahaba wake Happy watanitambua.They must pay “ akasema Loniki kwa ukali.
“Sarah naomba umtume mtu akanitafutie mvinyo mkali ,pengine unaweza kunisaidia kuyapunguza machungu haya ninayoyasikia.” Akasema Loniki.Sarah akainuka na kuondoka pale bustanini akamuacha Loniki na shangazi yake.
“Shangazi nimeumia sana lakini kwa sasa sintasema lolote kwa sababu bado tuko katika majonzi makubwa .Nitaongea baada ya kumaliza msiba huu.Ila naomba mtambue kwamba sijawahi kuumia moyo katika maisha yangu kama nilivyoumizwa na kifo cha Vero.Nimeumia sana.Nimelia sana na nitaendelea kulia kwa miaka mingi ijayo.Laiti uhai ungeweza kununuliwa basi ningetumia fedha zangu zote kuununua uhai wa Vero.” Akasema LonikiCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kwa kweli bado siamini kama Yule kijana Patrick amefanya jambo kama hili alilolifanya.Siku zote nilimuona ni kijana mtaratibu na mwenye roho nzuri ya huruma na anayempenda Vero lakini kumbe ni kijana mwenye roho mbaya ya kishetani.” Akasema shangazi yake Loniki.
“Shangazi nina hakika kabisa kwamba haikuwa akili yake ya kawaida iliyomfanya Patrick akafanya alilolifanya.Japokuwa sijawahi kukaa naye kwa muda mrefu nikamfahamu vizuri lakini kwa kipindi kifupi nilichowahi kuonana naye nilimuona ni kijana mtaratibu sana na mwenye utu.Ninashawishika kuamini kwamba yule mwanamke Happy lazima atakuwa ametumia hata dawa ili kumvuruga Patrick akili na asijue jambo analolifanya.Hainiingii akilini hata kidogo kuamini eti kwamba Patrick aliamua kumuacha Vero kwa akili yake timamu tena wiki kadhaa kabla ya ndoa yao.Ninaapa kwenda hadi mwisho wa dunia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Patrick na Happy wamelipa kwa kitendo cha kumuua Vero.” Akasema kwa uchungu Loniki bado machozi yaliendelea kumtoka.Mkononi alikuwa na sigara yake akiivuta na kupuliza moshi hewani.
“Narudia tena kwamba sintaondoa mguu wangu Tanzania hadi nitakapohakikisha kwamba wote waliohusika na kifo cha mdogo wangu wamelipa nikianzia na Patrick na Happy.”
“Umefikiria kufanya nini Loniki” akauliza shangazi yake
“Shangazi ni mapema sana kusema nitafanya nini lakini nitakachokifanya kitakuwa ni fundisho kwao na familia zao.Tusubiri kwanza tumzike Veronika na halafu mtajua nitakachokifanya.” Akasema Loniki na muda huo huo Sarah akarejea akiwa na chupa ya mvinyo.Loniki akaipokea na kuinywa kwa pupa.
“Sarah nasikia uchungu mwingi ambao siwezi kuuelezea.Angekuwa ni mtu ambaye si jasiri tayari angekwisha kufa kwa uchungu huu ninaousikia.Uchungu huu na maumivu haya hayawezi kwenda bure bila ya kulipwa.Patrick amenifanya nijifunze ukatili na nitakuwa mkatili kama anavyotaka niwe ” Akasema Loniki.Sarah akaumuangalia dada yake na kusema
“Loniki naomba utulize moyo wako na usiwe na hasira namna hiyo.Sote tulimpenda sana Vero lakini hata kama ukiwaua wahusika ili kulipiza kisasi Vero hatarudi tena.Kilichobaki ni kusameheana ili maisha yaweze kuendelea .Tukumbuke kwamba hata Vero naye alifanya makosa.Alitunga uongo na kuwatenganisha Patrick na Happy.Hili ni jambo baya sana alifanya na ambalo limekuja kumgharimu maisha yake.Nakushauri dada yangu tuachane na haya mambo ya kulipiza visasi kwani hayatatusaidia kitu badala yake yatazidi kututia matatizoni.” Akasema sarah
“Maneno gani hayo unayaongea Sarah? Unaonekana umefurahishwa na kifo cha Vero .Sikuombi ushirikiano wako na wala sihitaji kushirikiana na mtu na hakuna mtu yeyote atakayenizuia wala kuyabadili mawazo yangu.Lazima wote waliohusika na kifo cha Vero walipe.” Akasema Loniki kwa ukali kisha akainuka na kuondoka.
“Shangazi mimi siafikiani kabisa na mawazo ya Lonny ya kulipiza kisasi kwa Patrick na Happy.Tukio limekwisha tokea ,tuliache lipite na maisha yaendelee kama kawaida.Aliyesababisha kifo hicho cha Vero tayari anashikiliwa na vyombo vya sheria ,kwa nini basi tuviingilie vyombo vya kutoa haki ? Sioni sababu yeyote ya kuendeleza uhasama baina ya familia zetu kwani tayari tulikwisha kuwa kama ndugu na hatupaswi kutengana kwa sababu ya tukio hili.Wa kulaumiwa hapa si Patrick na Happy pekee bali hata Vero naye alifanya makosa tena makubwa ya kuwatenganisha watu wawili waliopendana kwa dhati.Ukumbuke Patrick aliwahi kufungwa gerezani kwa ajili ya Happy , kwa maana hiyo aliumia sana alipotenganishwa na mtu aliyempenda kwa uongo wa Vero.Pamoja na kosa hilo alilolifanya lakini bado Vero alidhamiria kufanya mauaji.Kama asingefariki yeye basi angeweza kuwaua Patrick na Happy kwani tayari alikwisha dhamiria kufanya hivyo.Naomba shangazi mshawishi Loniki asituingize katika matatizo mengine zaidi“ akasema Sarah.Shangazi yake akamuangalia na kubetua midomo akasema
“Sarah wewe ni mtu wa ajabu sana na kama alivyosema Loniki unaonekana umefurahi kwa kifo cha mdogo wako.Kama kweli ungeumizwa na kifo cha Vero basi ungeweza kusimama na kumtetea kwa kuungana na Loniki kulipa kisasi kwa wale waliohusika na kusababisha kifo hicho.Umenishangaza sana hata mimi sikutegemea kabisa kusikia ukiongea maneno hayo” akasema shangazi
“Shangazi …..” akaita Sarah lakini tayari shangazi yake alikwisha inuka na kuanza kuondoka.
“Sihitaji kusikia upuuzi wowote toka kwako .Umenisikitisha sana Sarah” akasema shangazi yake huku akiondoka.
“wananishangaza sana hawa ndugu zangu kwa maamuzi yao na kutokuona mbali.Kisasi hakitatusaidia chochote na badala yake tutazidi kuongeza matatizo zaidi.Kama watalipiza kisasi wafanye wao ,mimi wasinishirikishe kabisa.Nahitaji kuishi kwa amani na sitaki kugombana na mtu yeyote.Sijui kwa nini wanashindwa kuona kwamba ni Vero ndiye chanzo cha haya yote” akawaza Sarah kisha naye akaondoka pale bustanini
Baada ya kurejea toka katika mishughuliko yake ya siku ,mzee Raymond Kibaho baba mzazi wa Happy kibaho alitaka kufahamu kuhusiana na maendeleo ya mwanae.
“kama kawaida bado hakuna mabadiliko yoyote .Leo alikwenda mahakamani lakini hakuweza kuingia ndani ya mahakama na toka amerudi amejifungia chumbani kwake na hataki kuonana na mtu yeyote .Mtu pekee ambaye amekubali kuonana ni yule wakili wa Patrick” akasema mama Happy.Mzee Raymond akainama chini akafikiri kisha akasema
“Happy anahitaji msaada mkubwa sana wa kisaikolojia.Ngoja nikaonane naye” akasema mzee Raymond huku akitembea taratibu hadi katika mlango wa Happy akagonga lakini hakujibiwa.
“Happy my dear its me your father” akasema mzee Raymond na baada ya dakika mbili mlango ukafunguliwa.Happy alikuwa katika sura yenye majonzi makubwa sana.Baba alipomuona akastuka na kuogopa .Akamsogelea pale sofani alipokuwa amekaa akaketi pembeni yake.
“Happy mwanangu ni kwa nini unakuwa katika hali hiyo? Kwa nini unateseka kiasi hicho? Mimi baba yako na familia yote tunaumia sana tukikuona ukiwa katika hali hii.Wewe ndiye furaha yetu ,wewe ndiye mwanga wa nyumba yetu.Ukififia fahamu kwamba nyumba yetu haina mwanga tena.Tazama sasa nyumba iliyokuwa imetawaliwa na vicheko na furaha kubwa leo hii imekuwa ni nyumba ya simanzi na vilio kila kukicha.Happy wewe ndiye furaha yetu,ukilia nasi tunalia,ukicheka nasi tunacheka,,ukifurahi nasi tunafurahi pia.Tafadhali Happy nakuomba usiendelee kuumia moyo wako.You have to let it go.You have to live your life like it was before.Tuko nyumna yako na tutafanya kila tuwezalo kuhakikisha kwamba unarejea katika maisha yako ya kawaida.” Akasema mzee Kibaho
“Baba nakushukuru sana na nitaendelea kukushukuru siku zote kwa ushirikiano wako mkubwa unaonipa.Pamoja na upendo mkubwa toka kwa familia yangu lakini bado najikuta nikishindwa kuvumilia kila nikikumbuka kilichotokea.Picha ya tukio ilie imekuwa inanitesa usiku na mchana.Sikutegemea kamwe katika maisha yangu kama nitakuja kuua mtu.Kila nikifikiria kuhusu jambo hilo naumia sana.Kingine ambacho kinaniumiza akili yangu ni kila nimuwazapo Patrick.Sijui hatima yake itakuwa nini ,sifahamu atapata adhabu gani.Naumia sana dady” akasema Happy na kuanza kulia.
“Nyamaza kulia Happy.Be strong my daughter.You are always strong.Happy unahitaji ujasiri mkubwa sana na ili uwe na ujasiri unahitaji nguvu.Nguvu inakuja kwa kula chakula kwa hiyo naomba kuanzia sasa usizembee tena kula chakula.Ni chakula pekee ndicho kitakachokupa nguvu zitakokufanya uwe jasiri na kusimama imara kumtetea Patrick.He needs you now.He needs your support.So you cant support him while you are weak.Naomba inuka sasa twende mezani ukapate chakula “ akasema mzee Kibaho na kumshika Happy mkono wakaelekea katika chumba cha kulia chakula ambako Happy alijitahidi akala chakula
“Baba nakushukuru sana kwa kunipa moyo.Maneno yako uliyoniambia usiku huu na yale aliyonieleza Savanna yamenifanya nitambue nini natakiwa kufanya.Ninatakiwa kukabiliana na hali hii bila woga.Natakiwa kusimama na Patrick katika suala hili hadi mwisho.Amenionyesha upendo wa kweli kwa kukubali kuubeba mzigo mzito ambao hakuustahili.Ili kuweza kulifanikisha hilo nimewaza na kufikia maamuzi” Happy akanyamza akawatazama baba na mama yake waliokuwa kimya wakimsikiliza .Kila mtu alitaka kuyafahamu maamuzi anayotaka kuyachukua Happy.
“Nimeamua kulivua taji la Miss Tanzania.” Akasema Happy na kuwastua wote.Kila mmoja alimwangalia kwa mshangao mkubwa.Hakuna aliyetegemea kama Happy angefikiria kufanya jambo kama lile
“Nafahamu ni namna gani mlivyostushwa na maamuzi haya.Nimeamua kuchukua maamuzi haya magumu baada ya tafakari ya kina.Kwa kuhusika na tukio hili lililotokea tayari nimelitia doa taji la miss Tanzania.Kila siku magazeti na vyombo vya habari vinaripoti tukio hili kwa kutumia jina la Miss Tanzania badala ya Happy.Ili kuilinda heshima ya taji hili sina budi kulivua .Vile vile nimefikia maamuzi haya kwa ajili ya kupata muda zaidi wa kuwa na Patrick katika wakati huu mgumu tulionao.Nafahamu maamuzi haya yatawaumiza wengi lakini sina namna nyingine ya kufanya.Ninafanya hivi kwa ajili yangu mimi na nitawaomba Watanzania wanisamehe katika hili kwani nimewaangusha.Walikuwa na matarajio makubwa sana toka kwangu” akasema Happy.Bado wazazi wake waliendelea kumshangaa.
“Mwanangu Happy una hakika na maamuzi yako? Akauliza mama yake ambaye alikuwa anamtazama kwa macho makali.
“Ndiyo mama,nina hakika na maamuzi yangu.Ninafanya hivi kwa ajili yangu mimi na si kwa ajili ya mtu mwingine yeyote.Wapo watakaonibeza kwa maamuzi haya lakini sintabadili maamuzi yangu.Niko tayari kukabiliana na chochote kitakachojitokeza kutokana na maamuzi haya.” Akasema Happy
“Happy hata mimi bado nina wasi wasi sana kuhusiana na maamuzi haya.Naona kama umefanya maamuzi ya haraka sana.Kwa nini usisubiri kwanza kichwa chako kitulie ndipo ufanye maamuzi yenye kufaa? Akasema Margreth
“Hapana Margreth,sijafanya maamuzi ya haraka kwa kukurupuka kama unavyodhani.Nimefanya maamuzi haya nikiwa na akili zangu timamu na hii ni kwa faida yangu na Patrick.”
“Nimekusikia katika kila maongezi yako unamtaja Patrick.Vipi kuhusu Mike? Yeye mbona humpi nafasi ? Mike amekuwa nawe kwa miaka mingi sasa na tayari mmekwisha kuwa wachumba.Ametoka Marekani kwa ajili ya kuja kuungana nawe lakini hauonyeshi kufurahishwa na ujio wake hata kidogo.Kwwa nini unamfanyia hivyo mwenzio? Akauliza mama yake Happy.Bila kukwama kwama Happy akajibu.
“Mama na familia nzima kwa ujumla kuna jambo ambalo sikuwa nimeliweka wazi kwenu na ninaomba nitumie fursa hii kuliweka wazi mbele yenu.Nimeamua kuachana na Mike” akasema Happy.
“Unasema ?????!!!!....” mama yake akauliza kwa hamaki huku akisimama na kusababisha glasi kuanguka na kuvunjika.
“Unasemaje Happy ???? akauliza tena mama yake Happy
“Nimeamua kuachana na Mike” akasema Happy.Baba yake akatoa kitambaa na kujifuta jasho lililoanza kumchuruzika.
“Happy sikutegemea kama siku moja ungekuja kufanya maamuzi ya kipuuzi namna hii.Umenisikitisha sana mwanangu.Bado siamini kama maneno haya unayoyazungumza yametoka mdomoni mwako.Baada ya miaka hii yote kupita ukiwa na Mike leo hii unadiriki kusimama na kusema kamba Mike humtaki tena? Mike ambaye amekuwa nawe katika nyakati zote za shida na raha leo hii hana thamani tena kwako? Happy ni kitu gani kimekubadilisha namna hii? Huyo Patrick ambaye hakauki mdomoni mwako amekupa kitu gani cha kukufanya ubadilike namna hi??? “ akasema kwa ukali mama yake Happy
“Happy mimi sikubaliani kabisa na hicho unachotaka kukifanya.Ninakuapia iwapo utaachana na Mike basi tambua kwamba mimi si mama yako tena.” Akaendelea kufoka mama yake
“Mama haya ni maamuzi yangu mimi, kwa manufaa ya maisha yangu mimi mwenyewe.Mimi ndiye mwenye kufanya maamuzi ya nini nifanye na nani niwe naye katika maisha yangu.Nimemchagua Patrick na nitahakikisha ninafanya kila linalowezekana ili kuwa naye maishani.Mike ananipenda na hata mimi nampenda pia lakini moyo wangu hauko radhi kuendelea kuwa naye.Moyo wangu unamuhitaji Patrick pekee.Tafadhali mama naomba tusiyafanye mambo haya yawe magumu zaidi.Naomba nyote mkubaliane na maamuzi yangu” akasema Happy
“Happy usisikitike mwanangu.Mimi kama baba yako ninasema kwamba ninakubaliana na mawazo yako.Haya ni maisha yako na wewe ndiye mwamuzi wa nani ambaye unahitaji kuwa naye katika maisha yako.Kama kiongozi wa nyumba hii ,ninasema kwamba maamuzi ya Happy ndiyo ya mwisho na hakuna wa kuyapinga.Happy ninakuunga mkono na nitakuwa pamoja nawe katika kila maamuzi unayoyachukua kwa faida yako” akasema mzee KIbaho na kumfanya mke wake amuangalie kwa macho makali asiamini kile alichokisikia
“Ahsante sana baba .Nashukuru kwa kuniunga mkono.Nahitaji sana uungwaji mkono katika maamuzi magumu ninayoyafanya kwa ajili ya mustakabali mzima wa maisha yangu” akasema Happy
“Usijali mwanangu,tuko pamoja nawe katika kila jambo.Tunakuunga mkono katika maamuzi yote yenye faida katika maisha yako” akasema mzee Kibaho
“Baba ahsante sana” akasema Happy
“Happy wewe ni mwanetu na tuna kila sababu ya kuhakikisha kwamba unakuwa na furaha siku zote za maisha yako na ni wajibu wetu kuungana nawe katika kila nyakati unazohitaji msaada wetu.Siku zote kumbuka kwamba wewe ndiye mwenye uamuzi na maisha yako.Kama Patrick ndiye mwanaume wa maisha yako na ambaye unahisi atakupa furaha katika maisha yako ,sisi hatuna kipingamizi hata kidogo.Kwa mara ya kwanza hata mimi naomba nikiri kwamba nimevutiwa na huyu kijana Patrick.Anaonekana ni kijana ambaye ana upendo wa dhati kwako .Kitendo cha kukubali kubeba dhamana yako ni kikubwa sana na ni watu wachache mno katika dunia ya sasa wanaoweza kufanya kitendo kama hiki.Ni kijana wa aina yake anayehitaji kuungwa mkono na kupewa moyo.Natamani nimuone tena huyu kijana kwani nakumbuka nilimuona miaka mingi iliyopita kipidi kile akiwa na kesi kule Iringa.” Akasema mzee Raymond Kibaho huku akiangaliwa kwa jicho kali na mke wake.
“Margreth say something !!!!!..Wewe umekaa kimya tu na hauchangii chochote.Au na wewe unakubaliana na maamuzi ya dada yako? Akauliza kwa ukali mama yake
“Mama ,mimi sina la kusema.Haya ni maamuzi yake binafsi na kama baba alivyosema kwamba Happy ndiye mwenye mamuzi na maisha yake.Mimi ninakubaliana na maamuzi anayoyachukua” akasema Margreth.
“Stupid !!!!!!!....” akasema mama Happy kwa ukali akainuka na kuondoka kuelekea chumbani huku akiongea peke yake.Alikuwa amekasirika mno
“Naomba msimjali mama yenu wanangu.Ninyi sasa hivi ni watu wazima na mnajua mnachokifanya katika maisha yenu.Mimi niko nyuma yenu na nitashirikiana nanyi katika kila hatua.Nataka binti zangu muishi maisha ya furaha na wala sintawapangia nani anawafaa katika maisha yenu.Kumbukeni hatima ya maisha yenu iko mikononi mwenu.Ninawapa uhuru wa kufanya machaguo yenye kufaa ili msije kujilaumu siku za usoni” akasema mzee Kibaho
“baba kuna taarifa nyingine ya kuhuzunisha” akasema Happy
“Taarifa gani hiyo?
“Baba yake Patrick amefariki dunia jioni ya leo”
“Unasema …….!!??” Mzee Kibaho akastuka
“Baba yake Patrick amefariki dunia .Nimeumizwa sana na taarifa hizi.Baba sikutegemea kama mambo haya yangefika hapa yalipofika.Sikujua kama maamuzi yetu yangetufikisha katika hali hii na kusababisha kupotelewa na wapendwa wetu.Kwanza alikuwa ni Vero na sasa ni baba mzazi wa Patrick na sijui ni nani atakayefuata kwa sababu suala hili kila uchao linachukua sura mpya” akasema Happy
“Nimestushwa sana na taarifa hii.Nini kimesababisha kifo chake? Akauliza mzee Kibaho
“ni shinikizo la damu”
“Ouh Mungu wangu ! Apumzike kwa amani mzee mwenzangu.Namkumbuka sana hasa wakati ule wa kesi ya Patrick wakati mnasoma alikuwa ni mtu mwenye ushirikiano mkubwa .Tulishirikiana vizuri sana” akasema mzee Raymond halafu kikapita kimya kifupi
“Happy nakuomba usihuzunike sana mwanangu na wala matukio haya yasikurudishe nyuma katika maamuzi yako.Najua mliamua kuchukua maamuzi haya wewe na Patrick kwa ajili ya furaha ya maisha yenu kwa hiyo usikatishwe tamaa na magumu yatakayotokana na maamuzi yenu.Mengi yatasemwa na mengi yatajitokeza ya kukatisha tamaa lakini ninachoweza kukushauri ni kwamba hata likitokea suala gumu kiasi gani simama imara katika maamuzi yako” akasema mzee Kibaho.
“Nitafanya hivyo baba” akasema Happy
“Kuhusu huyu kijana Mike,umekwisha muweka wazi kuhusu mpango wa kuachana naye? Akauliza mzee Kibaho
“Hapana baba ,bado sijamueleza chochote.Kila nikitaka kumweleza nashindwa”
“Ouh My dear,usiogope kufanya hivyo.Kuwa jasiri na umweleze ukweli ili afahamu angali bado mapema.Tafuta namna nzuri ya kumweleza ili aelewe.Najua si suala rahisi kumwambia lakini hakuna namna nyingine ya kufanya zaidi ya kumueleza ukweli.Patrick yeye amekwisha maliza sehemu yake na yametokea haya yaliyotokea .Wewe pia inakubidi ufanye upande wako.Mwambie ukweli wala usiogope kitakachotokea.Kuhusu hili suala la kulivua taji la Miss Tanzania umejipanga vipi?
“Nimekwisha wasiliana na mkurugenzi wangu na nimemweleza aniandalie mkutano na wandishi wa habari kesho saa nne asubuhi,kwa hiyo kesho nitalitangazia taifa azma yangu ya kulivua taji la Miss Tanzania.Baada ya hapo nitaonana na Mike na kumweleza ukweli.Kesho itakuwa ni siku yangu ngumu sana,sifahamu nini kitatokea hiyo kesho lakini lazima niyafanye haya yote” akasema Happy.Baba yake akamuangalia kisha akasema
“I’ll be with you”
“me too” akasema Margreth.Happy akatabasamu lile tabasamu lake adimu sana.
“Nashukuruni sana.I love you my family” akasema Happy.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
* * *`
Taarifa za kifo cha baba yake Patrick zilisambaa kwa kasi kubwa.Watu walifika kwa wingi msibani nyumbani kwa Marehemu baada ya kuzipata taarifa hizi za kustusha.Wengi hawakuamini taarifa hizi na kuwafanya wafike wenyewe kuthibitisha kama ni kweli.Mtaa huu walioishi wazazi wa Patrick ulijaa watu na kutawaliwa na vilio.
Saa tatu za usiku gari moja lenye rangi ya fedha aina ya BMW likasimama nje ya nyumba ya wazazi wa Patrick na mwanadada aliyekuwa amejitanda mavazi meusi akashuka .Aliangaza angaza huku na huko kana kwamba kuna mtu alikuwa anamtafuta lakini hakujua aanzie wapi kutokana na idadi kubwa ya watu waliouwepo hapo msibani.Akachukua simu yake akazitafuta namba Fulani na kupiga
“Hallo Alois habari yako? Pole sana na matatizo.Mimi niko hapa nje ya nyumba nashindwa kuingia ndani kutokana na idadi kubwa ya watu” akasema mwanadada Yule .Baada ya kama dakika mbili akatokea Alois na kumfuata Yule dada
“Ouh Sarah !!!!..karibu sana” akasema Alois huku akikumbatiana na Sarah dada yake Vero.
“Pole sana Aloisi.Nimepata taarifa za msiba wa baba usiku huu .Nimestuka sana nikaona siwezi kulala bila kuja kutoa pole.” Akasema Sarah
“Ahsante sana kwa kufika Sarah.Mtatusamehe sana kwa kutoweza kufika katika msiba wa Vero wala kutuma mwakilishi.Toka matatizo haya yalipotokea tumekuwa na wakati mgumu sana kumuuguza mzee na leo jioni ametutoka” akasema Alois
“Poleni sana Alois na wala usijali kuhusu kutokufika msibani kwani bado zilikuwa zinaandaliwa taratibu ikiwa ni pamoja na kuwasubiri baadhi ya ndugu walioko nje ya nchi wafike .” akasema Sarah
“Hii ni kazi ya Mungu na siku zote haina makosa.” Akasema Alois
“Alois mimi si mkaaji sana ,nimepita tu kutoa pole kwa msiba huu .Naomba yaliyotokea yasiweze kutugawa na kutufanya tuwe na uhasama au visasi kwani sisi tayari ni ndugu na tutaendelea kuwa hivyo siku zote.Tusikubali kugawanywa kwa mambo haya waliyoyafanya wadogo zetu.” Akasema sarah
“Nakushukuru sana Sarah kwa kulitambua hilo.Ni kweli hayo usemayo kwamba hatupaswi kutenganishwa na tukio hili lililofanywa na wadogo zetu.Umoja na mshikamano wetu lazima vidumishwe siku zote”
“Kweli kabisa Alois.Hatupaswi kufikia hatua ya kuchukiana na kumtafuta mchawi ni nani.Wote tunasikitika kwa yaliyotokea lakini hatuna budi kuyasahau yote na kusonga mbele na maisha yetu.Alois ninaweza kupata nafasi ya kuonana na mama nimpe pole kwa usiku huu?
“Bado hayuko katika hali nzuri lakini twende tukamuone” akasema Alois na kumuongoza Sarah hadi ndani aliko mama yake.
“Mama, Sarah amekuja kukupa pole” Alois akamwambia mama yake
“Mama pole sana” akasema Sarah akiwa amepiga magoti na kumkumbatia mama yake Patrick.
“Ni kazi ya Mungu mwanangu haina makosa .Tunashukuru kwa yote” akasema mama yake Patrick huku machozi yakimtoka
Sarah alikaa mle chumbani kwa takribani dakika kumi na tano halafu akaaga
“Nashukuru sana mwanangu kwa kuja kunitazama.Mungu akubariki sana” akasema mama yake Patrick.
“Mama tuko pamoja katika wakati huu mgumu” akajibu Sarah na kutoka mle chumbani,akampigia simu Alois aliyekuwa na pilika nyingi usiku huu ambaye alifika mara moja.Wakati Alois akimsindikikiza Sarah wakapita karibu na mahala walipokuwa wamekaa Andrew na Savanna.
“Andrew huyu ni Sarah dada yake Vero.Amekuja kutupa pole baada ya kupata taarifa za kifo cha mzee.” Akasema Alois halafu akamgeukia Sarah
“Sarah hawa ni marafiki wakubwa wa Patrick.Huyu anaitwa Andrew na Yule pale anaitwa Savanna.”
“Poleni sana jamani,tuko pamoja katika matatizo haya yaliyotufika” akasema Sarah huku akipeana mikono na akina Andrew.
“Mpangilio mzima wa mazishi ya Vero ukoje? Akauliza Savanna
“Kilichokuwa kinasubiriwa ni ndugu waliokuwa mbali nje ya nchi wafike ili tuweze kupanga ratiba kamili ya mazishi.Dada Loniki tayari amekwisha fika na aliyebaki ni mjomba ambaye anaishi Urusi .Yeye tunamtegemea usiku wa leo lakini kwa mujibu wa kamati ya maandalizi imeamuliwa kwamba mazishi yatafanyika kesho kutwa katika makaburi ya kinondoni.Nadhani mpaka kesho tutapata ratiba kamili ya mazishi.Nitawafahamisheni kila kitu baada ya kuipata ratiba kamili” akasema Sarah halafu akaagana na akina Andrew akaelekea katika gari lake.
“Sarah tutatuma ujumbe wa watu wachache kuja kuungana nanyi katika mazishi .Sisi bado hatujapanga tarehe kamili ya mazishi ya mzee bado kuna ndugu wa muhimu tunawasubiri toka mikoani.Watakapofika wote ndipo itakapopangwa siku ya mazishi.Nitakutaarfu juu ya tarehe ya kuzika” akasema Alois
“Sawa Alois tutaendelea kutaarifiana na kujulishana kinachoendelea” akasema Sarah halafu akaingia katika gari lake na kuondoka
“Sasa moyo wangu una amani.Nimefarijika sana kwa kuwapa pole familia ya Patrick.Sitaki kuishi kwa visasi na hasama kama anavyotaka Loniki.Ninafikiria pia baada ya mazishi ya Vero nikaonane na Happy nimfariji na kumpa moyo kwani kwa muda huu nina imani atakuwa katika wakati mgumu sana .Palipo na ukweli lazima tuuseme,Vero alifanya kosa kubwa sana kutunga uongo na kuwatenganisha Patrick na Happy.Hawa walikuwa wanapendana na wana historia ndefu katika mapenzi yao.Simlaumu Patrick kwa maamuzi aliyoyafanya kwani alifanya vile kwa ajili ya kuitafuta furaha ya moyo wake ambayo nina hakika anaipata akiwa na Happy na ndiyo sababu hata baada ya kupita miaka mingi bado hajaweza kumsahau” akawaza Sarah wakati akirejea nyumbani kwako kutokea nyumbani kwa wazazi wa Patrick alikoenda kutoa pole.
“Nimefurahishwa na kufarijika sana na ujio wa Sarah.Sikuwa nimetegemea kabisa kama kuna ndugu yeyote wa Vero angeweza kuungana nasi katika kipindi hiki kigumu.” Akasema Alois baada ya Sarah kuondoka.
“Sarah ni mtu mwelewa sana.Ameonyesha moyo wa uungwana “ akasema Savanna
“Tutatuma ujumbe wa watu wachache ukatuwakilishe siku ya mazishi ili tusije onekana kwamba hatukushirikiana nao katika mazishi ya mtoto wao.” Akasema Alois
Saa tano na dakika kumi na tisa za usiku kwa mujibu wa saa aliyokuwa ameivaa mkononi,Savanna akawasili nyumbani kwake.Alistuka sana baada ya kukuta taa za ndani zinawaka.
“Ouh Gosh ! nani kawasha taa za ndani? Ina maana niliondoka asubuhi bila kuzima taa? Akajiuliza
“ Inawezekana ni kweli niliondoka bila kuzima taa kwa sababu kichwa changu kwa sasa kina mambo mengi mazito.Kesi hii ya Patrick imenifanya nisahau kila kitu.” Akawaza Savanna huku akishuka garini na kuelekea getini.Alistuka baada ya kutoliona kufuli ambalo hutumia kufungia geti.
“Gosh ! kufuli liko wapi? Akajiuliza Savanna huku moyo ukimuenda mbio.
“Kuna wezi wamevunja,wameingia ndani wakaiba?!!..Savanna akaogopa sana
“Ngoja nimpigie simu Kamanda Zuberi anitumie askari.Lazima ndani kwangu nitakuwa nimeibiwa.” akawaza Savanna huku akirudi garini na kuchukua simu .Alizitafuta namba za Zuberi lakini akasita kupiga
“Kwa nini niogope? Hii ni nyumba yangu na sioni sababu ya kuogopa.Ngoja niingie ndani nikatazame kama kumeibwa au vipi ndipo nimpigie simu afande Zuberi.Naweza kuwasumbua askari kumbe ni mimi nilisahau hata kufunga geti.” Akawaza Savanna halafu akashuka garini akalifungua geti.Bila kuogopa akaliingiza ndani gari halafu akafunga geti.Alijaribu kuusukuma mlango wa kuingilia sebuleni lakini ulikuwa wazi na kwa ndani sauti ya muziki ikasikika.Akaingia sebuleni kwa tahadhari.Akapatwa na mshangao mkubwa uliochanganyika na hasira baada ya kumkuta George amejilaza katika sofa pale sebuleni.
“Its’ you again !!!!!......” akasema Savanna kwa hamaki.George hakujibu kitu akabaki akitabasamu.
“Nini kimekurudisha humu kwangu George? Nani kakupa ruhusa ya kuingia humu wakati mimi sipo? Akauliza Savanna kwa ukali.George akatabasamu ,akacheka kidogo na kusema
“Nimerudi kwangu mpenzi..Aren’t you Happy that I‘m back? You didn’t miss me? Akasema George halafu akainuka pale sofani na kumuendea Savanna akataka kumkumbatia.Savanna akamsukuma kwa hasira
“George please get out of here now !!!!” akafoka Savanna
“George sitaki tena kukuona ndani ya nyumba yangu.Uliondoka hapa kwa kashfa na matusi .Nimekwisha choka nawe George naomba uondoke haraka sana.Sikuhitaji hapa kwangu na katika maisha yangu pia.” Akafoka Savanna
“Savanna tafadhali nakuomba upunguze hasira na tukae tuongee tuyamalize mambo haya.I love you Savanna and I cant live without you.Please my love forgive me.Najua nilikosea sana naomba unisamehe” akasema George
“George kichwa changu kina mambo mengi sana kwa sasa na sitaki uwe ni moja ya matatizo yangu.Naomba uondoke uende zako.Sina chochote cha kuongea nawe George.Please go !” akasema Savanna kwa hasira
“Savanna leo hii unadiriki kunitamkia maneno hayo? Muda huu wote tumeishi pamoja kwa amani na upendo leo hii unanitamkia maneno hayo?
“George tafadhali nimechoka sana nahitaji kupumzika.Please go..!!!!!!!” akasema Savanna huku akiufungua mlango na kumfanyia George ishara atoke nje.
“Savanna kweli umeamua kunifukuza?
“ George please go !!..naomba uende”
“ Najua haya yote ni kwa sababu ya Patrick”
“ Vyovyote utakavyofikiria George lakini sihitaji tena kuwa nawe.Tafadhali ondoka”
“Nashukuru sana Savanna kwa mambo uliyonifanyia.Nakutakia maisha mema na huyo Patrick.Akasema George huku akitoka taratibu.Savanna akamfungulia geti akaenda zake.
“ Kesho nitaajiri walinzi wa kampuni binafsi ya ulinzi waanze kuilinda nyumba yangu.Sitaki huyu mtu awe anakuja hapa kwangu.Vile vile nitabadilisha vitasa vyote vya nyumba nzima kwani tayari anazo funguo zote za nyumba yangu kitu ambacho ni hatari sana.Sihitaji kabisa mawasiliano yoyote naye.Simuhitaji katika maisha yangu.Akili yangu yote kwa sasa inamuwaza Patrick pekee” akawaza Savanna huku akielekea chumbani kwake baada ya George kuondoka.Aliingia bafuni akajimwagia maji halafu akajilaza kitandani.Kichwa chake kilitawaliwa na picha moja tu,picha ya Patrick.
“I’ll get you out Patrick.Nitafanya kila niwezalo kukakikisha kwamba unashinda kesi.Hii ni nafasi yangu nyingine ya kumpata Patrick na safari hii atakuwa wangu peke yangu” akawaza Savanna kisha taratibu usingizi ukamchukua akalala.
* * * *
Saa tatu za asubuhi Patrick macho yake yalikuwa mekundu na kichwa kilimuuma sana kwa mawazo mengi aliyokuwa akiwaza.Hakuweza kupata usingizi usiku alikesha akiwaza hatima ya maisha yake .
Mlango wa chumba chake kilichokuwa na watu wanne ukafunguliwa na akaitwa,akatoka akaongozana na askari magereza wawili akapelekwa katika chumba kimoja kilichokuwa na meza ndogo na viti viwili .Ndani ya chumba kile akakutana na sura ya Savanna.Akafarijika sana kwa kuonana na Savanna ambaye aliinuka na kumkumbatia.
“Pole sana Patrick.” Akasema Savanna
“Ahsante sana Savanna.Nimefurahi umekuja.Nimefarijika sana.Nilikuwa na usiku mrefu mno na sijaweza kupata usingizi kabisa.”
“Pole Patrick.Jitahidi usiwaze sana kuhusu suala hili.Sisi tupo na tunalishughulikia hadi mwisho wake.Habari za toka jana?
“Habari ni kama hivyo nilivyokueleza,mawazo mengi nasikia kama kichwa kinataka kupasuka.Namshukuru Mungu kumekucha salama.”
“Patrick,naomba usijisikie vibaya na wala usithubutu kuyaruhusu mawazo mengi kiasi cha kukukosesha usingizi. Suala hili liko mikononi mwangu ninalishughulikia kwa nguvu na uwezo wangu wote na ninakuahidi kwamba tutashinda.Naomba uniamini kwamba tutashinda kesi hii” akasema Savanna
“Ninakuamini sana Savanna.Moyo wangu hauna wasi wasi hata chembe kuhusu wewe,lakini mawazo mengi yanakuja kila nikikumbuka mambo haya namna yalivyotokea na nini itakuwa hatima yake.Sura ya Vero inanijia kila dakika.Nashindwa kabisa kuitoa kichwani kwangu.Sikutegemea kama angeweza kufikwa na umauti .It looks like she’s haunting me.Ninamfikiria pia Happy.Alikuwa na maisha yake mazuri tu na mpenzi wake lakini alipokutana na mimi ameingia katika matatizo makubwa.Namfikiria baba yangu hospitali.Nawafikiria ndugu zangu,ninafikiria mambo mengi sana na ndiyo maana siwezi kabisa kupata usingizi.” Akasema Patrick.Savanna akamtazama usoni kwa muda kisha akasema
“Patrick kuanzia sasa naomba usifikirie tena kuhusu mambo haya.Kifanye kichwa chako kiwe huru na usikubali kufungwa na mawazo yoyote yale.Yaliyotokea yamekwisha tokea na tuangalie ya mbele.”
“Nakuelewa Savanna hata mimi sitaki kuumiza kichwa changu kwa mawazo mengi lakini nashindwa kabisa kuyaepuka mawazo haya.Anyway tuachane na hayo,vipi ulifanikiwa kupita hospitali na kujua maendeleo ya baba yangu? Ulifanikiwa kuonana na Happy? Vipi kuhusu Vero una taarifa zozote kuhusiana na kinachoendelea kwao? Patrick akauliza maswali mfululizo.
“Happy nilifanikiwa kuonana naye jana.Nilimfuata nyumbani kwao.Anaendelea vizuri.Jana alikuwepo katika viwanja vya mahakama lakini hakuweza kuingia ndani ya mahakama .Bado ana mstuko kwa mambo yaliyotokea na bado inamuwia ugumu kukabiliana na hali halisi.Nimeongea naye kwa kirefu nikamuelewesha kwamba anatakiwa asimame imara kuikabili hali halisi.Nashukuru alinielewa na ameahidi kutokuogopa kitu chochote tena.Ameahidi kukutembelea mara kwa mara hapa gerezani .” Savanna akamuangalia Patrick kwa muda kisha akaendelea.
“Kuhusu Vero ni kwamba atazikwa kesho kutwa katika makaburi ya Kinondoni.Hii ni kwa mujibu wa dada yake Sarah.”
“Ulifanikiwa kuonana na Sarah? Ulienda nyumbani kwao? Akauliza Patrick.
“Hapana sikwenda nyumbani kwao.Alikuja pale nyumbani jana usiku kutoa pole ya msiba….. akasema Savanna na kustuka.
“Mbona umestuka Savanna? Saraha alikuja kutoa pole ya msiba wa nani nyumbani kwetu? Akauliza Patrick huku akimtazama Savanna kwa wasi wasi.Savanna hakujibu kitu akabaki anamuangalia.
“Nijibu Savanna,msiba wa nani ambao Sarah alikuja kutoa pole?
“Patrick !!!.. akaita Savanna
“Naomba uwe mvumilivu sana”
“Savanna mbona unaniogopesha? Nini kimetokea” Nani kafariki tena?Akauliza Patrick huku akimtazama Savanna kwa wasi wasi.
“Patrick ,baba yako amefariki dunia jana jioni.” Akasema Savanna.
Patrick akaishiwa nguvu akabaki anamuangalia Savanna.Alishindwa aseme nini.Savanna akaogopa kwani aliwahi kusikia kwamba Patrick aliwahi kupatwa na matatizo ya mstuko wa moyo
Dakika zaidi ya tatu zilikatika bila ya Patrick kuongea lolote.Alikuwa katika mawazo mazito.
“Are you ok Patrick? Akauliza Savanna
“I’m ok Savanna though I’m deeply hurt.Nashindwa niseme nini,nashindwa nilie au vipi.Tayari nimelia machozi mengi sana na sitaki kulia tena.Hata kama nikilia kwa sauti kama ya radi my dady wont come back.He’s gone.He’s dead.Ninachotakiwa kufanya ni kuwa jasiri na kukabiliana na kila kitakachokuja mbele yangu.Huu ni mwanzo tu nina imani mengi bado yatakuja huko mbeleni.” Akasema Patrick kwa sauti ya upole.Savanna akainuka na kusimama nyuma yake akamshika mabega
“Patrick tuko pamoja katika mambo haya na kamwe usijihisi mpweke.Any time you need someone by your side I’ll be right there for you”
“Ahsante sana Savanna .Sina cha kukulipa kwa wema wako huu mkubwa.Umenionyesha ni namna gani rafiki wa kweli anapaswa kuwa.Wewe ni rafiki wa kweli.Umeweza kusimama nami hata katika nyakati zile ngumu zaidi ambazo wengine wameshindwa.Ahsante sana Savanna siku zote utakuwa hapa moyoni mwangu” akasema Patrick maneno ambayo yalimfariji sana Savanna.
“Usihofu Patrick wewe ni mtu muhimu sana kwangu.Tatizo lako ni langu .Na kwa maana hiyo basi nitafanya kila niwezalo hadi nihakikishe kwamba unakuwa huru.Sintalala usingizi hadi nihakikishe kwamba umekuwa huru” akasema SavannaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Savanna ,ujio wako umenipa faraja sana japokuwa kidonda cha moyo kimezidi kuongezeka kwa taarifa ya kifo cha baba.Naomba ufanye kila linalowezekana ili niweze kutoka humu ndani.Nina ndoto nyingi sana ambazo zote zitapotea iwapo nitaendelea kukaa gerezani”
“Patrick nimekwisha kuahidi kwamba nitafanya kila linalowezekana ili ushinde hii kesi.Naomba uniamini”
Maongezi kati ya Savanna na Patrick yalichukua zaidi ya nusu saa halafu Patrick akarejeshwa tena mahabusu.Savanna akaondoka .
****************************
Ukumbi mdogo wa mikutano wa Korongo hoteli ulifurika waandishi wa habari wakisubiri kusikia kile walichoitiwa na mkurugenzi wa Miss Tanzania.Waandishi wa habari toka vyombo mbali mbali vya habari walikuwepo hapa ukumbini kuanzia saa mbili za asubuhi.Hii ilionyesha ni kwa jinsi gani walivyokuwa na hamu ya kusikia kile walichoitiwa.Kwa takribani siku kadhaa sasa mrembo mpya wa Tanzania Happy Kibaho amekuwa akitawala vyombo vya habari ,kuhusiana na kuhusika kwake katika ugomvi uliosababisha kifo cha Veronika Rugi aliyekuwa mchumba wa Patrick.Mengi yalikuwa yameandikwa kuhusiana na na tukio hili lakini si miss Tanzania Happy kibaho wala mkurugenzi wake au mtu yeyote toka katika kamati ya Miss Tanzania aliyejitokeza katika vyombo vya habari na kuongea lolote kuhusiana na jambo hili.
Maongezi ya hapa na pale yalitawala miongoni mwa waandishi wa habari wakati wakimsubiri mkurugenzi wa Miss Tanzania.Saa nne kamili za asubuhi juu ya alama ,gari la mkurugenzi wa miss Tanzania likawasili pale hotelini.Akiwa ameongozana na wajumbe watatu wa kamati ya miss Tanzania wakashuka na kuelekea moja kwa moja katika ukumbi wa mikutano kulikokuwa kumejaa waandishi wa habari.Kama ilivyo kawaida yake mkurugenzi huyu akataniana na waandishi wa habari kadhaa .Alikuwa akifahamiana na waandishi wengi wa habari.
Saa nne na nusu akaingia ukumbini mrembo wa Tanzania Happy kibaho akiwa ameongozana na mdogo wake Margreth pamoja na baba yake mzee Raymond Kibaho.Happy aliyekuwa amevaa suruali ya jeans nyeusi ,shati dogo jeusi na miwani mikubwa myeusi iliyoyafunika kabisa macho yake ,alikuwa aking’aa kwa mianga ya kamera za waandishi wa habari waliokuwa wakimpiga picha katika kila hatua aliyopiga.Alisalimiana na na mkurugenzi wake kisha akaelekezwa sehemu ya kuketi.Sura yake haikuwa na lile tabasamu lake lililozoeleka .Picha nyingi ziliendelea kupigwa wakati akiwa amekaa.
“Ndugu waandishi wa habari toka katika vyombo mbali mbali vya habari” alifungua mkutano mkurugenzi wa miss Tanzania.Ukumbi wote ukawa kimya ukimsikiliza.
“Awali ya yote napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru sana nyote kwa kuitika mwito na kufika kwa wingi.Sikutegemea kama kungekuwa na idadi kubwa namna hii ya waandishi.Papo hapo napenda kuwaomba radhi kwa kuchelewa kidogo kuanza mkutano wetu kutokana na sababu zisizoweza kuzuilika.” Akanyamaza kidogo na kuendelea.
“Ndugu zangu waandishi wa habari ,tumewaiteni hapa asubuhi ya leo kwa ajili ya kuweka sawa baadhi ya mambo.Kama mnavyofahamu kwamba kwa siku chache zilizopita mrembo wetu mpya wa Taifa Happy kibaho amekuwa akiandikwa sana katika vyombo vya habari kuhusiana na tukio Fulani ambalo nisingependa kuliongelea hapa lakini naamini nyote mnalifahamu.Kwa muda huu wote amekuwa kimya na hajaongea lolote na hata sisi kama kamati ya Miss Tanzania hatujasema lolote kwani suala lililotokea halihusiani na miss Tanzania bali ni suala binafsi la Happy Kibaho .Kwa hiyo basi mkutano huu wa siku ya leo ni wa Happy Kibaho ambaye ana jambo la kuongea nanyi wanahabari na watanzania wote hususani wale mashabiki wake.Bila kupoteza wakati naomba nimkaribishe Miss Tanzania Happy Kibaho aweze kuzungumza nanyi.Karibu Happy” Akasema mkurugenzi wa miss Tanzania akamsogezea kipaza sauti Happy aliyekuwa amekaa pembeni yake.Akakohoa kidogo kurekebisha koo lake kisha akasema.
“Ndugu zangu waandishi wa habari awali ya yote na mimi ningependa kwanza kuwashukuru kwa kufika kwenu kwa wingi ili kusikia ni kitu gani nimewaitia hapa siku ya leo.” Akanyamaza kidogo halafu akaendelea.
“Kwa siku kadhaa zilizopita kulitokea tukio ambalo mimi nilihusishwa nalo.Ni tukio la ugomvi lililosababisha kifo cha msichana mmoja aitwaye Veronika.Mengi yameandikwa na kusemwa kuhusiana na tukio lile .Kwa kuwa suala hili liko mahakamani ninaomba niliongelee kwa ufupi sana.Ukweli halisi ni kwamba mimi na Patrick ni marafiki na wapenzi wa muda mrefu sana.Urafiki wetu ulianza toka tukiwa shuleni.Tulikutana,tukapendana na kuwa wapenzi.
Lilitokea tukio baya ambalo lilipelekea Patick kufungwa gerezani baada ya kusababisha kifo wakati akipambana na genge la wahuni waliokuwa wakitaka kunidhalilisha kijinsia.Wakati akiwa gerezani nilipata nafasi ya masomo nchini Marekani na hapo ndipo yalipotokea ya kutokea ambayo nisingependa kuyaongelea hapa na nikapotezana na Patrick kwa kipindi kirefu hadi tulipokutana tena hivi karibuni ambapo tulibaini kitu kilichotutenganisha .Naomba nikiri kwenu waandishiwa habari na watanzania kwamba mimi na Patrick tunapenda kwa dhati ya mioyo yetu na ndiyo maana hata baada ya kutengana kwa muda mrefu lakini bado tumejikuta tukiendelea kupendana zaidi na zaidi na hii ndiyo sababu iliyosababisha ugomvi uliopelekea kutokea haya yaliyotokea.” Happy akanyamaza kidogo akameza mate na kuendelea
“Kuhusika kwangu katika tukio hili kumeniathiri kwa kiasi kikubwa kisaikolojia mimi binafsi na kumelitia doa taji la miss Tanzania nililolivaa kwa sababu katika kila habari inayoandikwa kuhusiana na tukio hili inaandikwa kama Miss Tanzania na si kama Happy Kibaho.Familia yangu pia imekuwa na wakati mgumu sana toka tukio hili limetokea na ninawashukuru kwa sababu wamekuwa nami katika kila dakika na wamekuwa wakinipa ushirikiano mkubwa sana.” akanyamaza kidogo na kuendelea.
“Ndugu waadishi wa habari ,tukio hili lilinihusu mimi kama Happy Kibaho na si kama miss Tanzania.Kuendelea kuandika habari kwa kutumia kichwa cha miss Tanzania ,hakutendei haki taji hili kubwa la urembo hapa nchini,waandaji na kamati nzima ya miss Tanzania.Kwa hali hiyo nimekaa ,nikatafakari na familia yangu nikafikia maamuzi ambayo ninataka kuyaweka wazi kwa watanzania.” Happy akanyamaza akawatazama waandishi wa habari ambao walikuwa kimya wakimsikiliza.
“Baada ya tafakari nzito nimeamua kuchukua maamuzi magumu ili kuilinda heshima ya taji hili kubwa la miss Tanzania na tasnia nzima ya urembo hapa nchini.Nimeamua kulivua taji la miss Tanzania” Happy akanyamaza na kuwatazama waandishi wa habari ambao walionyesha mshangao mkubwa na minong’ono ikasikika kati yao.
“Ndugu zangu waandishi wa habari na watanzania ,najua mmestushwa sana na maamuzi haya hasa ikizingatiwa kwamba sina muda mrefu toka nimelivaa taji hili.Nimechukua maamuzi haya ili kuilinda heshima ya taji hili kubwa kabisa la urembo hapa nchini.Nawaomba watanzania wenzangu walioniamini na kuniona ninafaa kulibeba taji hili wanisamehe sana kwa kuwaangusha.Waliniamini sana na kunipatia taji hili na ndiyo maana kwa heshima yao nimeamua kulivua taji hili ili hata kama ni kuendelea kuandikwa basi niandikwe kama Happy Kibaho na si kama miss Tanzania.Asubuhi ya leo nimewasilisha barua ya kulivua taji langu kwa mkurugenzi mkuu wa Miss Tanzania na ninasubiri hatua itakayofuata.Ndugu zangu waandishi wa habari ni hilo tu ambao nimewaitieni hapa siku ya leo.” Akasema Happy na kisha mkurugenzi wake akachukua kipaza sauti.
“Ndugu zangu waandishi wa habari,nadhani nyote mmesikia alichokisema Happy.Hii ni taarifa ya kustusha mno na hata sisi kama kamati tumestushwa sana na taarifa hii.Kitu ninachotaka mkifahamu ni kwamba haya ni maamuzi binafsi ya Happy na sisi kama viongozi wake tutayaheshimu na kuyapa uzito unaostahili na baada ya kuyatafakari tutatoa taarifa kamili.Kwa kuwa bado tuko katika mstuko kutokana na maamuzi haya ya Happy ,nawaombeni ndugu zangu waandishi wa habari mkutano wetu uishie hapa siku ya leo.Hakutakuwa na maswali yoyote kwa Happy kwa sababu hayuko katika wakati mzuri wa kujibu swali lolote .Tumuache akapumzike na ninawaahidi kufanya tena mkutano mwingine na nitawaalikeni nyote na mtapata fursa ya kuuliza maswali mengi mtakavyo.” Akasema mkurugenzi wa miss Tanzania huku akisimama halafu Happy naye akasimama na kuondoka mle ukumbini kwa kupitia mlango wa nyuma kwa lengo la kukwepa kuonana na waandishi wa habari.
“mkurugenzi nashukuru sana .Tutazidi kuwasiliana” akasema Happy akimpa mkono mkurugenzi wake wa Miss Tanzania.
“Happy pole sana.Ninakuomba usihofu chochote ,leo hii hii tunaanza kulifanyia kazi suala lako na tutakutaarifu maamuzi ya kamati lakini nakuhakikishia kamba tutayaheshimu mawazo yako” akasema mkurugenzi
Happy akiongozana na baba yake pamoja na mdogo wake Margreth wakatembea kwa haraka kuelekea katika gari lao huku wakipigwa picha na waandishi wa habari .
“Thank you guys for your support” akasema Happy akiwaambia baba yake na Margreth wakati wakiondoka pale hotelini.
“ Uwepo wenu umenipa nguvu sana leo.”
“Happy sisi kama familia tutasimama pamoja nawe katika kipindi hiki kigumu na hatutakuacha hata sekunde moja.” Akasema mzee Raymond,Happy akatabasamu na kumgeukia mdogo ake aliyekuwa amekaa kiti cha nyuma
“Margreth ahsante sana kwa ushirikiano wako.”
“Usijali Happy.Siku zote tuko pamoja nawe .Ni jukumu letu kama familia kusimama pamoja nawe “Happy akainama chini akazama ghafla katika mawazo.
“Unawaza nini Happy? Akauliza mzee Raymond
“Bado kuna suala linaniumiza kichwa sana.Suala la kukutana na Mike linanitatiza ninashindwa namna nitakavyomtamkia kwamba mimi na yeye basi .Inauma sana baba Mike ananipenda kwa moyo wake wote.Naogopa sana kuumiza moyo wake” akasema Happy
“Happy my dear,usiogope.Nafahamu ugumu uliopo lakini hakuna njia nyingine ya kufanya,you have to do it.Unatakiwa uwe jasiri ili uweze kukabiliana na masuala mazito kama haya.Mweleze Mike ukweli wa moyo wako na ninakuhakikishia kwamba utakapomueleza utajisikia huru .Utaumia moyo lakini hii ni kwa faida yako mwenyewe kwa furaha ya moyo wako.Kumbuka hapa unaitafuta furaha ya maisha yako ambayo ni Patrick kwa hiyo usiogope hata kidogo kusimama imara katika suala lolote linalohusiana na mustakabali mzima wa maisha yako na Patrick.” akasema mzee Kibaho .
“Ahsante sana baba kwa kunipa moyo.” Akasema Happy kisha akachukua simu yake na kuzitafuta namba za simu atumiazo Mike akiwa Tanzania akapiga
“Hallo Happy unaendeleaje malaika wangu? Akasema Mike kwa furaha baada ya kupokea simu.
“Naendelea vizuri sana Mike.Tayari umeshafika hapo hotelini kama tulivyokubaliana?
“Ndiyo Happy.Nimekwisha fika muda mrefu ninakusubiri wewe mpenzi wangu.Nina hamu sana ya kuongea nawe” akasema Mike
“Niko njiani nakuja Mike.Naomba uendelee kunisubiri” akasema Happy na kukata simu akainama na kuvuta pumzi ndefu.
“Be strong Happy.You can do it” akasema mzee Kibaho
Saa saba na robo za mchana Happy na familia yake waliwasili Nady Villa Park moja kati ya hoteli maarufu jijini Dar es salaam.Wote watatu wakashuka garini na kuingia hotelini
“Usiogope Happy.Just be strong” akasema mzee Raymond akizidi kumpa moyo binti yake.Waliingia hotelini hadi katika meza aliyokuwa amekaa Mike wakasalimiana halafu Rayomond na Margreth wakaenda kuketi katika meza zilizokuwa nje ya hoteli na kuwaacha Happy na Mike peke yao
“Baba nina wasi wasi na Happy .Sijui kama ataweza kumweleza ukweli Mike” akasema Margreth.
“Usiwe na wasi wasi Margreth.Ninamfahamu Happy,she’s a strong woman.I know she can handle this” akasema mzee Kibaho huku akiyafuta macho yake baada ya kuvua miwani
“Sikutegemea kama siku moja Happy angeweza kuwa katika wakati mgumu kama huu alionao sasa hivi.Hata hivyo ninamshukuru sana huyo kijana Patrick kwa moyo wake wa upendo wa kuamua kuubeba yeye mzigo huu mzito alioustahili Happy.Ninaamini Patrick ana mapenzi ya dhati kwa Happy kwa sababu katika dunia ya sasa ni watu wachache sana wenye kuweza kufanya kitendo kama alichokifanya yeye. Na ndiyo maana ninaona kuna kila sababu ya kuwasaidia ili waweze kuwa pamoja.Patrick ni kijana sahihi kwa Happy.” akasema mzee Raymond.
“Baba ,Patrick na Happy wanapendana mno na hakuna mtu au kitu chochote zaidi ya kifo kitakachoweza kuwatenganisha.Mapenzi yao yalianza miaka mingi iliyopita na hata ilipotokea wakatenganishwa kwa uongo wa Vero ,hakuna aliyeweza kumsahau mwenzake.Nakumbuka Happy hakukaukiwa machozi kila siku akimlilia Patrick na ndiyo maana siku ile alipotwaa taji la mss Tanzania alipoteza fahamu baada ya kumuona Patrick” akasema Margreth.
“Hii ndiyo ilikuwa sababu ya Happy kupoteza fahamu siku ile?? Akauliza mzee Kibaho huku akishangaa.
“Ndiyo baba.Hii ndiyo sababu pekee ya Happy kupoteza fahamu siku ile.Mapenzi ya Patrick na Happy ni mazito sana na ndiyo maana haikumuwia ugumu Patrick kuubeba mzigo wote wa kesi aliyoistahili Happy.Ninachosikitika ni kwamba hata Mike anampenda sana Happy na ndiyo maana amesafiri kutoka marekani na kuja hapa kuungana naye katika matatizo.” Akasema Margreth.Mzee Kibaho akavuta pumzi ndefu na kusema
“Ni wakati mgumu sana kwa Happy lakini ni vyema kumuacha yeye mwenyewe afanye maamuzi yenye kufaa kwa mustakabali mzima wa maisha yake na tayari amekwisha amua kuwa na Patrick”
Ukimya mkubwa ulikuwa umetawala meza waliyokuwa wamekaa Mike na Happy.Ilionekana kana kamba walikuwa wakitegeana kuongea.Ni Mike ndiye aliyeanzisha maongezi.
“Happy nimefurahi sana kupata nafasi hii kukutana nawe leo hii kwa chakula cha mchana” akaanzisha mazungumzo Mike.Happy akajilazimisha kutabasamu na kusema
“Hata mimi nimefurahi sana Mike kwa kupata wasaa huu wa kukaa pamoja nawe.Ni muda mrefu umepita toka tulipokaa pamoja kama hivi.Nimekuwa nikitamani sana kuipata nafasi hii lakini toka ulipokuja nimekuwa nikikabiliwa na mfululizo wa matukio kiasi cha kushindwa kabisa kupata nafasi kama hii.Utanisamehe sana Mike” akasema Happy
“Happy kwanza kabisa napenda nikupe pole nyingi kwa matatizo na hongera nyingi kwa kushinda taji kubwa la urembo nchini.Haikuwa kazi rahisi kuwashinda warembo wote uliochuana nao.Hongera sana Happy.Michelle pamoja na wazazi wangu wanakupa hongera nyingi sana.” Akasema Mike
“Ahsante sana Mike”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Vile vile nakupa pole sana kwa mfululizo wa matukio yaliyoambatana na ushindi wako huu.Nilipata taarifa kwamba ulipoteza fahamu ukumbini .Niliogopa sana ikanilazimu nifanye safari ya dharura kwani nilijua kwa nyakati kama hizi unanihitaji sana.Nimekuja ili niwe karibu nawe Happy kama mpenzi wako ,nikufariji na kukuonyesha upendo.” Akasema Mike
“Nashukuru sana Mike” Happy akajibu kwa ufupi
“Happy ni wajibu wangu kufanya hivi .Nina imani hata wewe ungefanya hivi endapo ungesikia kwamba kuna jambo limenitokea.Naamini ungekuja marekani mara moja” Akasema Mike na mara muhudumu akafika na kuanza kuandaa meza.Baada ya meza kuandaliwa wakaanza kula
“Pole sana kwa matatizo Happy.Ninaumia sana kila nikuonapo ukiwa katika mawazo mengi na machozi yasiyokauka.Ile sura yako ya kimalaika yenye tabasamu lisilofutika imetoweka ghafla.Happy ni kitu gani hasa kilichotokea na kupelekea uwe katika hali hii? Niko gizani sielewi nini kimekupata malaika wangu.Moyo wangu unaumia,natamani nifanye kitu kukurejesha katika hali yako ya kawaida lakini sielewi nianzie wapi.Happy mpenzi wangu naomba tafadhali unifahamishe nini hasa kimekusibu? Niko tayari kukusikiliza na niko tayari kwenda hadi mwisho wa dunia hii ili kuirejesha tena furaha ya maisha yako.” Akasema Mike.Happy akakiweka kijiko mezani halafu akamtazama Mike usoni
“Mike nashindwa nianzie wapi .Mambo mengi yametokea katika kipindi kifupi sana”
“Jitahidi Happy na unipe walau picha ya kilichotokea na kinachoendelea hivi sasa na kwa pamoja tutafute namna ya kuweza kuyatatua.” Akasema Mike.Happy akainama
“Help me Lord.This is so difficult but I have to do it” akawaza Happy halafu akainua kichwa.
“Mike matatizo yalianza usiku ule niliposhinda taji la miss Tanzania.Mara tu nilipotangazwa mshindi watu wengi walikuja kunipongeza kwa ushindi wangu lakini miongoni mwa waliokuja kunipongeza nilimuona mtu ambaye alinipelekea nikapatwa na mstuko na kupoteza fahamu” akasema Happy.
“Ulimuona mtu ambaye alikustua hadi ukapoteza fahamu? !!!! ..mtu wa namna gani huyo aliyekustua na kukusababishia matatizo haya makubwa? Was it a ghost? Akasema Mike na kumfanya Happy atabasamu kwa mbali.
“It wasn’t a ghost.I saw a human being” akasema Happy.Mike naye akaweka kijiko chake mezani na kuendelea kumtazama Happy.
“Mike I saw a person whom I believed he is dead” akasema Happy( Mike nilimuona mtu niliyeamini alikwishafariki)
“What ?!!!!..You saw a dead person? That’s a ghost Happy !! You saw a ghost” akasema Mike.(Nini ?!!!!..Ulimuona mtu aliyekwishafariki? Uo ni mzimu Happy)
“Mike sikuona mzimu.NIlimuona binadamu ambaye nilidhani kwamba amefariki miaka mingi iliyopita” Happy akasisitiza
“Ni nani huyo ambaye ulimuona?Hili ni jambo la kushangaza sana”
“I saw Patrick”(Nilimuona Patrick) akasema Happy .Sura ya Mike ikaonyesha mstuko wa dhahiri.Midomo ilikuwa inamtetemeka na kushindwa kuongea.Baada ya dakika moja Mike akasema
“Ulimuona Patrick!!! Ni Patrick yupi huyo uliyemuona Happy?
Happy akakohoa kidogo na kusema
“Kama utakumbuka kwamba niliwahi kuwa na mpenzi wangu ambaye alikuwa ni kila kitu kwangu na ambaye niliamini alifariki dunia akiwa gerezani.Huyo ndiye niliyemuona.” Akasema Happy na kuzidi kumchanganya Mike
“No ! Happy you must be mistaken.Patrick is dead and there is no way he can come back.What you saw must be a ghost” akasema Mike( Hapana ! Happy ulikosea.Patrick amekwishafariki na hakuna namna anayoweza kurejea.Ulichokiona ni mzimu)
“Mike,Patrick ni mzima hajafa na hakufa kama taarifa ile niliyoipata ilivyokuwa inasema.Ilikuwa ni taarifa ya uongo iliyoandikwa na mtu ambaye lengo lake lilikuwa ni kunitenganisha naye.Baada ya kurudi toka marekani nililazimika kutafuta mahala alipozikwa ili na mimi nikaweke shada la maua kama ishara ya upendo wangu kwake lakini taarifa nilizozipata toka katika magereza aliyokuwa amefungwa ni kwamba Patrick hakufariki akiwa gerezani bali alimaliza kifungo chake akiwa mzima wa afya.Hapo ndipo nilipoamini kwamba Patrick alikuwa mzima.Kwa bahati nzuri siku ile ya fainali alijitokeza mbele yangu.” Akasema Happy
“Happy bado siamini kama ni kweli hayo unayoniambia.Inawezekana akawa ni mtu ambaye amefanana na Patrick na anataka kukudanganya kwamba yeye ni Patrick.” Akasema Mike kwa sauti ya juu.Happy akaendelea kumtazama .Mike akachukua glasi ya mvinyo akagugumia mvinyo wote na kusema
“Happy my love nakuomba utulize mawazo .Achana kabisa na huyo mtu anayejiita yeye ni Patrick.Patrick halisi alikwisha kufa na hatarudi tena duniani.”
“Mike naomba uniamini kwamba mtu nilimuona
Patrick halisi na nilifanikiwa kuonana naye,nikaongea naye”
“What !! ..Mike akashtuka
“Nilikutana na Patrick na nikathibitisha kwamba ni yeye kweli na si mzimu wake”
“Ulikutana naye wapi? Mliongea nini? Mike akauliza maswali mfululizo
“Siwezi kukwambia kila kitu kwamba nilikutana naye vipi na wapi lakini naomba ufahamu kwamba nilikutana naye na ni mzima na hakufa kama ilivyokuwa imedaiwa”
“Jesus Christ !!!!!!....” akasema Mike huku mikono yake akiwa ameikunja na kuiweka kifuani
“Happy una hakika kweli kwamba mtu uliyeonana naye ni Patrick? Mike akauliza tena
“Ndiyo Mike.Mtu niliyeonana naye ni Patrick” akajibu Happy halafu kikapita kimya kifupi.
“Huyo mtu aliyekuandikia ujumbe ule kwamba Patrick amefariki dunia ni nani? Umekwisha mfahamu?
“Ndiyo Mike,tumekwisha mjua mtu huyo.Ni Vero ambaye alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Patrick”
“Ouh Gosh !! ..where is she? She’s a monster..Anatakiwa akamatwe akashtakiwe kwa kosa alilolifanya ambalo lingeweza kupelekea hata kupoteza uhai wa mtu.Nilikuwepo wakati ule ulipopata taarifa hizi za kifo cha Patrick na niliyashuhudia mateso uliyoyapata.That woman must pay.Show me where she is and I can make her pay” akasema Mike kwa ukali
“There is no need Mike..She’s gone now.She’s dead” akasema Happy na Mike akashusha pumzi kikapita kimya kifupi Happy akasema
“Mike ni kweli kwamba nilipata mateso makubwa sana wakati ule nilipopata taarifa za kifo cha Patrick,wewe ulikuwepo na uliyashuhudia mateso niliyoyapata.Ni wewe na Michelle mliokuwa wafariji wangu.Mateso yote yale yalitokana na upendo wangu mkubwa kwa Patrick na ndiyo maana kuna nyakati sikuona hata faida ya kuendelea kuishi tena duniani kwa sababu sikuamini kama kuna maisha bila ya Patrick.” Happy akanyamaza akamtazama Mike ambaye uso wake ulianza kuloa jasho
“Its hard but I have to do it” akawaza Happy
“Mike naomba niwe wazi kwako kwamba baada tu ya kukutana na Patrick kumbu kumbu zangu zote za nyuma zimerudi ghafla .Understad that I’m a human being and sometimes I’m weak.” Akasema Happy
“Whats that suppose to mean Happy ? (Hiyo inamaanisha nini Happy? akauliza Mike kwa wasi wasi huku akimtazama Happy usoni
“Mike I’m so sorry to tell you this but me and Patrick we’re back together” ( Mike samahani kwa kukueleza hili lakini mimi na Patrick tumerejesha mahusiano yetu)
Mike akastuka mno kwa maneno yale .
“Happy sijakusikia vizuri umesema nini? !!
“Nimesema kwamba mimi na Patrick tumerejesha mahusiano yetu ya awali” akasema Happy.Mike akaonekana kuchanganyikiwa ghafla
“Happy !!!..bado siamini..Kwa nini umefanya hivi? Kwa nini umenifanyia hivi? Siamini Happy kama ni wewe kweli ambaye unaweza ukanifanyia mambo haya.How can you do that to me????!!!!.. Mike aliongea kwa masikitiko makubwa sana na macho yake yalilengwa na machozi.
“Happy naamini unanitania na si kweli hayo unayoniambia..Huwezi kunifanyia hivi Happy.Ninakufahamu vizuri hauwezi kufanya kitu kama hicho.Ninakupenda zaidi ya nafsi yangu Happy tafadhali naomba uniambie kwamba unanitania” akasema Mike huku machozi yakianza kumtoka katika macho yake.
“Mike mimi ni binadamu na ninahitaji moyo wangu uwe na furaha siku zote.Mike nafahamu unanipenda tena kwa moyo wako wote na hata mimi ninakupenda vile vile.Umekuwa na mimi kwa kipindi kirefu sasa.Umenijali na kunionyesha mapenzi ya hali ya juu sana.Siku zote niliamini kwamba baada ya Patrick kufariki wewe ndiye mwanaume wa maisha yangu lakini baada ya kukutana na Patrick tena nimejikuta nikiwa dhaifu kwake.Patrick ndiye alikuwa mwanaume wangu wa kwanza kumpenda na kumkabidhi moyo wangu na ndiyo maana hadi leo hii sijaweza kumtoa moyoni mwangu.Mike naomba ufahamu kwamba si rahisi kufanya mamuzi magumu kama haya hasa kwa mtu anayekupenda lakini nimeamua kuusikia na kuufuata moyo wangu unavyonituma.Moyo wangu unamtaka Patrick.Mike this is for the best of me.Naomba Mike kama unanipenda na unanitaka niwe na furaha naomba unielewe na uniruhusu niwe na Patrick” akasema Happy.
“ No ! No ! No Happy you cant do this to me.Huwezi kuniacha kamwe Happy.Ninakupenda na wewe ni wangu peke yangu.Sintakubali kamwe mtu yeyote Yule anitenganishe na wewe.” Akasema Mike huku akiinuka na kumshika Happy mikono.
“Mike ..!!” Happy akataka kusema jambo lakini Mike akamzuia
“Happy naomba naomba usiseme chochote kwa sababu kila neno utakaloendelea kuliongea hapa linazidi kuniumiza.Mimi na wewe kamwe hatutaweza kuachana” akasema Mike huku akiwa ameing’ang’ania mikono ya Happy.
“Mike naomba utulie na unisikilize “ akaomba Happy
“Happy nitakusikilizza kama una jambo lingine la kuniambia lakini si kuachana na mimi.Ninakupenda Happy ,wewe ni zaidi ya maisha yangu.Sikutegemea hata siku moja kama ungenitamkia maneno kama haya.” Akasema Mike.
“Baada ya miaka hii yote ya kuwa pamoja na kufikia hatua ya kukuvalisha pete ya uchumba iweje leo Happy uamue kuniacha ? You want to leave me just because of a man who rose from death? No Happy !! That wont happen.You cant leave me because of good for nothing ghost” (Unataka kuniacha kwa sababu ya mtu aliyeibuka toka kifoni? Hapana Happy !! hilo haliwezi kutokea.Huwezi kuniacha kwa sababu ya mzimu “ akasema Mike kwa ukali.Maneno yale yalimchoma sana Happy akasimama kwa hasira.
“Mike naomba iwe ni mara ya kwanza na ya mwisho kutoa maneno machafu na ya kejeli kwa Patrick.Yeye ndiye aliyeushika moyo wangu na sintakubali mtu yeyote Yule atoe matamshi ya kumkosea heshima.Kama unanipenda nadhani utakuwa unaijali pia furaha ya moyo wangu ambayo ninaipata nikiwa na Patrick.” Akasema Happy kwa ukali.Mike naye akasimama kwa jazba
“You are selfish Happy.You never thought about me at all.What about my happiness? You are my happiness.How could you be so cruel? ( Wewe ni mbinafsi Happy.Hufikiri kabisa kuhusu mimi.Vipi kuhusu furaha yangu na mimi? Wewe ndiye furaha yangu.Mbona unakuwa mkatili hivyo? Akafoka Mike.
“Mike naomba unielewe kwamba moyo wangu umefanya maamuzi magumu sana ya kuamua kuuvunja uhusiano wetu ambao umedumu kwa muda mrefu.Naomba unisamehe sana Mike kwani sintaweza kuyabadili maamuzi yangu .I’m sorry Mike that we have to end up this way.Nitakurejeshea gharama zote ulizotumia katika safari yako ya kuja Tanzania.” Akasema Happy
“Utanirudishia pesa lakini vipi kuhusu moyo wangu ambao hauwezi kuishi bila ya wewe? Hakuna pesa inayoweza kufikia thamani ya penzi langu kwako.Sihitaji pesa au kitu kingine chochote kile.Nakuhitaji wewe tu.My life is nothing without you.” Akasema Mike
“Mike ,please don’t make this too hard for me.Nina matatizo makubwa kwa sasa na ninaomba tafadhali usilifanye suala hili likawa tatizo.Kama kweli unanipenda Mike naomba uniruhusu nifanye kila ninachokihitaji kwa moyo wangu.Ninampenda Patrick na ninamuhitaji katika maisha yangu.Mimi na wewe tutaendelea kuwa marafiki” Akasema Happy
“Happy sitaki kuwa rafiki yako.Nataka kuwa mwanaume wa maisha yako.Tafadhali niambie ni kitu gani umekikosa toka kwangu? Kuna jambo lolote baya nimewahi kukufanyia? Au niambie nikufanyie kitu gani ili uwe na furaha na uendelee kuwa na mimi? Niambie Happy niko tayari kufanya chochote kile kwa ajili yako.” Akasema Mike.Happy machozi yalikuwa yanamtoka.Alikuwa na wakati mgumu sana.
“Mike umenipa kila kitu nilichokihitaji katika maisha yangu.Umekuwa pembeni yangu na kusimama pamoja nami hata katika nyakati zile ngumu kabisa.Thamani yako kwangu na katika maisha yangu ni kubwa sana lakini pamoja na hayo Mike naomba uniamini kwamba Patrick ndiyo furaha yangu.Ndiye maisha yangu ,ndiye kila kitu kwangu.” Akasema Happy.Mike akamtazama kwa macho ya huruma .
“Sasa ndiyo natambua kwamba kwa muda huu wote umekuwa ukinidanganya kwamba unanipenda kumbe hukuwa na hata chembe ya upendo kwangu.Ulinidanganya.Nilikuwa kipofu,nilipofushwa na uzuri wako wa tausi kumbe ndani ni kahaba na shetani usiye na hata chembe ya huruma.Hakukuw……” kabla hajamaliza sentensi yake Happy akamnasa kibao kikali
“Naomba usirudie tena kutamka maneno hayo uliyoyatamka.Usinifananishe mimi na shetani au kuniita kahaba.Nilikupenda Mike na nilikuwa tayari kuwa nawe katika maisha yangu yote na wala sijawahi kukudanganya hata mara moja.” Akasema Mike na mara Mike akagonga meza kwa hasira
“You lied to me Happy all this long and all its because of this stupid ghost.” Mike akaongea kwa sauti kubwa .Macho yake yalikuwa yamebadilika na kuwa mekundu.Alikuwa na hasira zisizomithilika.Wateja waliokuwa wakiendelea kupata chakula katika meza za pembeni wakageuza vichwa vyao kuangalia kilichokuwa kinaendelea kati ya Mike na Happy.
Happy naye alipandwa na hasira baada ya maneno yale ya kejeli toka kwa Mike.Machozi yalikuwa yanamtoka.Taratibu akatoa katika mkoba wake pete ya uchumba aliyovishwa na Mike na kuiweka mezani.
“Mike nakurudishia pete yako ya uchumba uliyonivisha.Ahsante sana kwa yote.Utanisamehe kwa maamuzi haya magumu.This is for the best of me” akasema Happy na kuchukua mkoba wake.Mike akamshika mkono akamzuia asiondoke.
“Huwezi kwenda Happy.Huwezi kuondoka na kuniacha hapa.You’ll never leave me Happy.You’ll always be mine” akasema MikeCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/-
“Mike let me go !!!!....” Akasema Happy kwa sauti huku akiuvuta kwa nguvu mkono wake ili kujinasua toka katika mikono ya Mike. Alitumia nguvu nyingi kujivuta na kujinasua toka katika mikono ya mike na kumpelekea kukosa mhimili akaangukia meza ya jirani na kumwaga vinywaji.Watu wote mle hotelini wakasimama kuangalia kilichokuwa kinaendelea.Happy akasimama na kwa haraka wahudumu wa hoteli wakafika na kumshika Mike.Happy akatoka kwa kasi huku akilia.Mzee Raymond na Margreth walistuka sana baada ya kumuona Happy anatoka mle hotelini huku analia.Kwa haraka wakamfuata
“Happy kumetokea nini? Mike amekupiga? Akauliza mzee Raymond.Happy hakujibu kitu akaendelea kulia.Baba yake akamshika mkono na kumuongoza hadi katika gari.
“Nyamaza kulia Happy.” Akasema mzee Kibaho.Happy akanyamaza kulia akafuta machozi.
“Tuondoke dady” akasema Happy
Mzee Raymond akawasha gari na kuondoka pale hotelini.
“Nini kimetokea mle hotelini? Ulifanikiwa kumweleza Mike ukweli? akauliza mzee Raymond baada ya kusimama katika foleni.
“I did it dady.Its over now” akasema Happy.Baba yake akamuangalia na kusema
“Pole sana Happy.Najua haikuwa kazi rahisi lakini umeweza kuifanya.Endelea kuwa na ujasiri huo katika kuipigania furaha ya moyo wako.Wakati mwingine tunapoitafuta furaha ya mioyo yetu inatulazimu kuchukua maamuzi magumu kama uliyoyachukua na siku zote katika maamuzi magumu lazima wawepo watu watakaoathiriwa na maamuzi hayo.Mike alikuelewa? Amekubali kwa moyo mmoja muachane?” Akasema mzee Raymond.
“It was painful dady.So painful.Sikutegemea kumuumiza Mike kiasi kile.He loves me so much .” Happy akashindwa kujizuia akaanza kulia.
“Nyamaza kulia Happy.Its over now.Yes its painfull but you did the right thing.Hupaswi kulia kabisa kama moyoni mwako una nia ya dhati na Patrick ambaye naye alifanya kama ulivyofanya wewe na kupelekea mwenzake kupoteza maisha.Mnapita katika kipindi kigumu sana lakini haya yote yana mwisho na yatakwisha tu” akasema mzee Raymond.
“Happy ,kama anavyosema baba ,vumilia katika kipindi hiki kigumu cha mpito na mambo haya yatakwisha tu.” Akasema Margreth ambaye muda mwingi alikuwa kimya
“Margreth najitahidi sana kuvumilia lakini kuna nyakati najikuta nikishidwa kuvumilia hasa kila nikikumbuka ugumu uliopo mbele yetu.Hata hivyo I’m still strong “ akasema Happy.Magari yaliyokuwa yamesimama katika foleni yakaanza kwenda safari ikaendelea.walifika nyumbani Happy akaomba aachwe peke yake akajifungia chumbani kwake.
Mike alicharuka na kuanza kupambana na wahudumu wa hoteli akiwataka wamuachie ili amfuate mchumba wake Happy.Walinzi wa hoteli wakafika haraka baada ya vurugu kuwa kubwa na kumkamata Mike ambaye alikuwa katika hali ya kuchanganyikiwa kwani alikuwa anaongea mfululizo maneno yasiyoeleweka.
Ili asiendelee kuwabugudhi wateja wengine waliokuwa wakijipatia mlo,Mike akapelekwa hadi katika chumba kimojawapo cha hoteli ile kwa lengo la kumpumzisha.Jasho jingi lilikuwa linamtoka hali iliyowafanya viongozi wa hoteli wamuite daktari haraka ili amfanyie uchunguzi Mike kuona kama ana tatizo lolote baya.
Daktari alifika haraka na kumpima Mike lakini hakukuwa na tatizo lolote la kiafya, akapendekeza ingekuwa vyema kama angendelea kupatiwa mapumziko kwani tatizo alilokuwa nalo lilionekana ni hasira za kupita kiasi.Mike aliendelea kuwa mbishi na hakutaka kuendelea kukaa pale hotelini.Akaomba apatiwe hesabu ya hasara iliyopatikana kwa vyombo mbali mbali kuvunjika wakati wa vurugu ile ili alipe.Baada ya kulipa,Mike akaruhusiwa kuondoka.Aliingia katika gari lake akakaa kama dakika mbili hivi akitafakari halafu akaliwasha na kuondoka kwa kasi.
“ Sikutegemea hata kidogo kama Happy angeweza kunifanyia kitu cha namna hii.Mpaka hivi sasa ninaona ni kama ndoto na si kitu cha kweli.Happy huyu niliyemfahamu na kumpenda kwa moyo wangu wote leo amenifanyia kitu cha namna hii??!!!!!..baso siamini.Pengine baada ya akili yangu kukaa na kutulia nitapata jibu nini cha kufanya.Pengine labda alikuwa ananitania ili kunipima kama nina mapenzi ya kweli kwake.” Akawaza Mike
“ Kwa nini Happy amekuwa mkatili namna hii? Kwa nini amesahau ni namna gani ninampenda .Kwa miaka hii yote niliyokuwa naye,nimemuonyesha mapenzi ya kiwango cha juu sana nikitazamia kwamba yeye ndiye mwanamke wa maisha yangu lakini kumbe nilikuwa najidanganya.Inaniuma sana….” Akawaza Mike huku akiendesha gari lake na mara kikasikika kishindo na gari lake likasimama ghafla.Akastuka kama mtu aliyekuwa usingizini na kuangalia kilichokuwa kimetokea.Ilikuwa ni ajali.Alikuwa ameligonga kwa nyuma gari lililokuwa mbele yake.
“ Ouh my God ….!!!!!!..” akasema Mike akiwa hajui la kufanya.Watu tayari walikwisha fika kwa wingi katika eneo la tukio ili kuishuhudia ajali ile.Bado Mike alikuwa garini na hakuthubutu kushuka.Alikuwa amechanganyikiwa na mikono yake ilikuwa inamtetemeka.
Askari wa kikosi cha usalama barabarani waliokuwepo karibu na eneo lile wakafika mara moja.Jamaa aliyegongewa gari lake na Mike akatoa maelezo ya namna ajali ile ilivyotokea halafu mmoja wa polisi akamfuata Mike katika gari lake na kugonga katika kioo akamtaka afungue mlango na ashuke garini.Bado Mike aligoma kushuka garini hali iliyomlazimu askari Yule kugonga kwa nguvu zaidi ili kumstua Mike aliyekuwa ameinamia usukani.
Ghafla kikatokea kitendo ambacho kiliwashangaza watu wote waliokuwepo eneo la tukio.Mike alifungua mlango akashuka akiwa na hasira kama mbogo na kuanza kumvurumishia makonde askari Yule wa usalama barabarani.Iliwalazimu raia waliokuwa wamesimama pembeni kuingilia kati na kumdhibiti Mike asiendelee kufanya kitendo kile .Mike akawekwa chini ya ulinzi.Akili yake haikuwa sawa sawa na hakujua alichokuwa anakifanya.Askari polisi waliokuwa doria walitaarifiwa kuhusu tukio lile na wakafika mara moja.Jitihada za kumuhoji Mike zikashindikana baada ya kushindwa kutoa ushirikiano.Kila alichoulizwa hakuwa tayari kujibu.Polisi wakalazimika kumpakia katika gari lao na kuondoka naye kuelekea kituoni.
Baada ya masaa mawili Mike alitulia na kurejea katika hali ya kawaida na hivyo kuwapa polisi fursa ya kumuhoji na ndipo walipogundua kwamba Mike alikuwa ni raia wa Marekani hivyo wakapiga simu katika ubalozi wa marekani ambao walikiri kumfahamu Mike na wakafika pale kituoni mara moja ili kutafuta namna ya kuweza kulimaliza suala lile lililokuwa linamkabili.
* * *
Kikao cha mwisho cha maandalizi ya mazishi ya Veronika kilikuwa kinaendelea nyumbani kwao.Wakati wakiendelea na upangaji wa ratiba nzima ya mazishi ,akaingia mmoja kati ya ndugu na kumuita Sarah pembeni.
“Sarah kuna wageni wamekuja wamesema kwamba wametoka kwa akina Patrick wamekuja kutoa pole,wanahitaji kukuona”
Sarah akamfuata dada yake Loniki aliyekuwa anamuangalia kwa jicho kali akamvuta pembeni.
“Loniki kuna ujumbe wa watu umekuja toka kwa akina Patrick wamekuja kutoa pole” akasema Sarah na mara sura ya Loniki ikabadilika ghafla.
“Wako wapi? Akauliza Loniki kwa ukali
“Sikiliza Loniki,hakuna sababu ya kukasirika kwa ujio wa watu hawa.Wamekuja kwa nia njema ya kuungana nasi katika wakati huu mgumu kwani tayari wao na sisi tulikwisha kuwa kama ndugu.Kukataa kuwapokea au kuwatendea kitendo chochote kile kisichokuwa cha kistaarabu kutajenga picha ambayo si nzuri na inaweza ikawa ni mwanzo wa chuki na uhasama baina yetu.Hata wao pia wameumizwa na kilichotokea kwani nao pia wamempoteza mzee wao.”
“Sarah sikuelewi kabisa ni kwa nini umekuwa ukimtetea sana Patrick na familia yake? Hutaki kabisa kusikia lolote likiongelewa kuhusiana na Patrick.Inaonekana hujaguswa kabisa na kifo cha Vero” akasema Loniki kwa ukali
“Loniki unakosea unaposema kwamba sijaguswa na kifo cha Vero.Nimeguswa sana lakini sioni sababu yoyote ya kumchukia Patrick au familia yake.Ni kweli amesababisha kifo cha mdogo wetu lakini tayari anashikiliwa na vyombo vya dola ili haki itendeke.Kwa kuwa tunasubiri maamuzi ya vyombo vyenye kutoa haki hatuna sababu ya kuendeleza chuki na uhasama baina ya familia zetu kwani hazitatusaidia kitu na hata tukichukiana hatutaweza kuwarejeshea watu wetu waliopoteza uhai” akasema Sarah
Loniki akaonekana kuchukizwa na kauli ile ya Sarah .Hakutaka tena kuendelea na maongezi akamfuata shangazi yake.
“Shangazi wako wapi wageni waliotoka kwa akina Patrick?
Shangazi yake ambaye amekuwa akikubaliana na kila anachokisema Loniki akamuongoza hadi nje walikokuwa wamekaa wajumbe toka kwa akina Patrick.Walikuwepo wanaume watatu na wanawake watatu na wote alikuwa wanaongozwa na Andrew rafiki mkubwa wa Patrick
“Wageni ni hawa hapa” akasema shangazi yake Loniki.
“Habari zenu? Loniki akawasalmu akina Andrew huku akiwaangalia kwa jicho la chuki
“Habari zetu nzuri ,poleni sana” wakajibu
“Tumekwisha poa” akajibu Loniki halafu kikapita kimya cha sekunde kadhaa akasema.
“Ninyi ndio mliotoka kwa akina Patrick? i
“Ndiyo sisi” akajibu mmoja wa wazee
“Tunashukuru mmefika lakini kwa bahati mbaya hatuhitaji mtu au muwakilishi yeyote toka katika familia ile.Uhusiano baina yetu na ninyi ulikwisha pale mtoto wenu alipomuua ndugu yetu kwa makusudi.Naombeni mkawaambie kwamba hatuna haja na pole zenu na wala hatuhitaji kufarijiwa nanyi.Tuacheni na msiba wetu” akasema Loniki.Kila mtu alibaki amepigwa na butwaa
“Sikiliza dada” akasema Andrew
“Tumekuja hapa kwa lengo zuri la kuungana nanyi katika msiba.Hata sisi tumeguswa na kuumia kama mlivyoumia ninyi.Tunaomba tafadhali mtupokee na mzipokee salamu zetu za pole.” akasema Andrew
“Hatuhitaji salamu zenu za pole.Mmetuulia mwanetu tuacheni tulie wenyewe,Nendeni nanyi mkalie na mzee wenu” akasema Loniki
“Bado mnaendelea kushangaa hapa? Nimesema ondokeni hatuwataki hapa msibani.” Akasema Loniki kwa ukali na mara akatokea Sarah
“Andrew nawashukuru sana kwa kufika kwenu ,lakini nawaomba tu muondoke ili kuepusha matatizo.Loniki bado ana hasira nyingi ,nadhani baada ya shughuli za mazishi kuna ulazima wa kukaa na kuliangalia sula hili kwa undani ili lisije likaleta uhasama baina ya familia zetu.Samahani sana jamani.” Akasema Sarah
“Ahsante sana Sarah.Tumekuelewa ,tunaondoka lakini naomba umfahamishe dada yako kwamba kitendo alichokifanya si cha kiungwana hata kidogo” akasema Andrew halafu wakapanda gari na kuondoka.
“Sarah unaonekana kifo cha Vero hakuijakuumiza kabisa.Umenisikitisha mno .Naumia kila wakati unapochagua kukaa upande wa akina Patrick.Who’s Patrick to you? Loniki akamwambia Sarah kwa ukali baada ya akina Andrew kuondoka.Sarah akaonekana kukerwa sana na maneno yale ya dada yake.
“Loniki naomba ufahamu kwamba sisi sote tulimpenda sana Vero na tuna uchungu mkubwa kwa kifo chake.Usitake uonekane kwamba una uchungu zaidi kupita watu wote hapa.Kitendo ulichokifanya si cha kiungwana hata kidogo.Watu wale wamekuja kwa nia njema tu ya kuungana nasi katika msiba lakini umewatimua bila sababu ya msingi.Mimi sintakubaliana hata kidogo na mambo kama haya ya kuendeleza chuki na uhasama baina yetu.”
“Sarah mimi na wewe tutaongea baada ya kumalizika kwa msiba” akasema Loniki na kuondoka akiwa amefura kwa hasira.
“Kama tusipokuwa makini tunaweza kujikuta tukiwa katika uadui mkubwa baina ya familia zetu.Hata kama tukiwachukia familia ya Patrick lakini hii haitatusaidia kumrejesha Vero.Nitapambana na Loniki katika suala hili na wala sintamuogopa kwa sababu endapo tutamuacha afanye anavyotaka kufanya anaweza akatupeleka mahala tusikotaka kwenda.” Akawaza Sarah
Baada ya kuachana na Sarah ,Loniki akaenda moja kwa moja hadi katika chumba alichokuwamo mama yake.
“Mama kuna watu wamekuja toka katika familia ya akina Patrick wanasema eti wamekuja kutupa pole.”
“Wako wapi ? Mmewakaribisha?
“Mimi nimewafukuza”
“Umefanya vizuri sana Loniki.” Akasema mama yake kwa sauti ndogo.Sauti yake ilikuwa inakwama kwama kutokana na kulia kwa muda mrefu.
“Mtoto wao amenisababishia kidonda ambacho hakitapona kamwe.Nilimpenda sana Vero na siku zote nilimtunza na kumlinda kama mboni ya jicho langu.Vero alikuwa ni mshauri wangu,furaha yangu,alikuwa ni kila kitu kwangu na sikutegemea kama angeondoka mapema namna hii .Ninamchukia sana yule kijana.Ameyafanya maisha yangu yote yaliyobaki hapa duniani yawe magumu na ya mateso makubwa.Nitamchukia hadi siku ninaingia kaburini na sitaki hata kuiona familia yake,Umefanya vizuri kuwatimua” akasema mama yake Loniki.
“Basi mama imetosha usiwaze sana ,nakuahidi Patrick lazima atalipa uovu wake.Siku hizi malipo ni hapa hapa duniani.Mtenda ubaya hulipwa kwa ubaya.” Akasema Loniki na kumkumbatia mama yake.
Andrew pamoja na ujumbe wote uliotumwa kupeleka salamu za pole kwa akina Vero walirejea nyumbani kwa wazazi wa Patrick kulikokuwa na umati mkubwa wa watu.Baada tu ya kushuka garini Andrew akamfuata Alois
“Mbona mmerejea mapema namna hii? Akauliza Alois
“Mambo yamekwenda tofauti kabisa na matarajio yetu”
“Nini kimetokea?
“Tumefukuzwa”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mmefukuzwa ?!!..” akauliza Alois
“Ndiyo Alois ,tumefukuzwa na dada mkubwa wa Vero.Amesema hataki kumuona mtu yeyote anayehusiana na Patrick katika msiba wa mdogo wake.Namshukuru sana Sarah kwa sababu ndiye aliyetokea na kutuomba tuondoke ili kuepusha shari kwa sababu Yule dada yake alikuwa tayari kufanya lolote ili kutuondoa pale.” Taarifa ile ilimstua sana Alois akasimama na kushika kiuno.
“Dah !! haya mambo yanazidi kuchukua sura mpa kila siku.Lakini nilitegemea jambo kama hili lingeweza kutokea.Poleni sana.Tuendeleeni na taratibu za kushughulikia msiba wa baba na tusiumize vichwa vyetu kwa yaliyotokea huko kwa akina Vero.” Akasema Alois
* * *
Saa ya ukutani ilionyesha ilikwisha timu saa mbili za usiku.Margreth alikuwa ameketi sebuleni akisubiri kutazama taarifa ya habari.Pamoja naye alikuwepo baba yake mzee Raymond Kibaho na mama yake. Happy alikuwa amejifungia chumbani kwake.
“Mtu mmoja afikishwa kituo cha polisi kwa tuhuma za kumshambulia askari wa usalama barabarani” Hii ilikuwa ni moja ya taarifa zilizokuwemo katika muhtasari wa habari.Margreth akastuka mno baada ya kuitazama habari ile.
“Mike..!!!! Baba ni Mike..Ouh My God !!!!” akapiga kelele Margreth.Mzee Raymond naye alistuka baada ya kuiona picha ya Mike akiwa anashushwa katika gari la polisi.Kwa haraka Margreth akainuka pale sofani na kukimbia kuelekea chumbani kwa Happy
“Happy twende ukamuone Mike.” Akasema Margreth
“Mike kafanya nini? Akauliza Happy kwa wasi wasi
“Amefikishwa kituo cha polisi” akasema Margreth
“Ouh My God !!!! akasema Happy huku akiinuka kitandani na kukimbia kuelekea sebuleni
“Mtu mmoja ambaye ni raia wa Marekani amefikishwa katika kituo cha polisi kwa kosa la kumshambulia na kumjeruhi askari wa kikosi cha usalama barabarani.” Ilisema taarifa ile na kuendelea
“Mtu huyo aliyefahamika kama Mike Cambell ambaye ni raia wa Marekani ,alitenda kosa hilo baada ya kusababisha ajali na alipotaka kuhojiwa na askari huyo wa usalama barabarani alimvamia na kuanza kumshambulia.” Wakati taarifa ile ikiendelea kusomwa,picha zilikuwa zinamuonyesha Mike akishushwa toka katika gari la polisi na kuingizwa kituoni.
“Mungu wangu.!! Yote haya yamesababishwa na mimi” akasema Happy na kuondoka kwa kasi kurejea chumbani kwake.Macho yake yalijaa machozi.Margreth akainuka na kutaka kumfuata lakini baba yake akamzuia.
“Let her cry all out..Let her be alone for now” akasema mzee Kibaho.
“Namuonea huruma Happy ana wakati mgumu sana” akasema Margreth
“Naomba ufahamu Margreth kwamba furaha ya maisha siku zote ina gharama zake.Happy anaipigania furaha ya maisha yake kwa hiyo anapaswa kuwa na ujasiri wa hali ya juu sana.Kwa sasa muache aendelee kulia na atakapoamka asubuhi atakuwa katika hali nzuri” akasema mzee Kibaho
“Baba nina wasi wasi anaweza hata akajidhuru.mambo yaliyoko kichwani kwake kwa sasa ni mengi “
“Hapana Margreth,Happy hawezi kufanya jambo kama hilo la kipuuzi.Anampenda Patrick kwa hiyo hawezi katu kufanya kitu kama hicho.”
Baada ya kuingia chumbani Happy alijitupa kitandani na kuanza kulia.
“Ouh Mungu wangu mambo haya yatakwisha lini? Nini itakuwa hatima ya mambo haya? Kila uchao kuna jambo jipya linaibuka.Ni kwa sababu ya suala hili tumekwishawapoteza watu wawili hadi hivi sasa na bado hatujui nini kitakachokuja mbele yetu.Leo Mike amekamatwa kwa kumshambulia polisi.Kesho kitatokea kitu gani?Najua Mike alifanya kitendo kile kutokana na hasira alizokuwa nazo baada ya kusitisha uhusiano baina yetu.Hakutegemea kama siku moja mimi naye tungefika mwisho.” Akawaza Happy huku akiendelea kulia.
“Sikuwahi kuota kama siku moja ningekuwa katika wakati huu mgumu.Sikutegemea kama siku moja ningeua mtu.Ouh My God please forgive me..This is getting too much for me.Naona kama akili yangu haifanyi kazi tena.Naona kama uwezo wake wa kufikiri umefika mwisho.I’m confused and I don’t know what to do any more.” akawaza Happy halafu akatoka na kuelekea jikoni akamkuta Pendo mfanyakazi wao wa ndani akiendelea na shughuli zake za usafi.
“Pendo baba huwa anaweka wapi chupa zake za pombe? Akauliza Happy huku akiyafungua makabati ya jikoni.
“Huwa zinakaa kule katika chumba cha kulia chakula” akasema Pendo, Happy akatoka kwa haraka akaeleka katika ukumbi wa chakula akalifungua kabati kubwa na kutoa chupa ya mvinyo akaenda nayo chumbani kwake.Hali aliyokuwa nayo Happy ilimstua sana Pendo hakuwahi kumuona hata siku moja akiwa katika hali ile na hakuwahi kumuona Happy akinywa pombe kali.Aliogopa sana akaacha kazi zote alizokuwa anafanya na kuelekea sebuleni.
“Pendo kuna nini ? Mbona umekuja kwa kasi namna hiyo? Akauliza mzee Raymond.
“Baba ni dada Happy” akasema Pendo akiwa na wasi wasi.
“Happy kafanya nini?
“Amekuja jikoni akiwa analia akachukua chupa moja ya pombe na kwenda nayo chumbani kwake.” Akasema Pendo.
“Ouh My God !!!..” akasema mzee Raymond na kuinuka akaeleka chumbani kwa Happy
Happy alimimina mvinyo ule mkali katika glasi na kuishika mkononi.Akaitazama glasi ile huku akitoa machozi
“Pengine hii inaweza kunisaidia kuniondolea mzigo huu wa mawazo.” Akawaza Happy na kabla hajaipeleka glasi ile mdomoni akaingia baba yake na kumshika mkono akamnyang’anya ile glani na kuiweka mezani
“Happy unafanya nini??
“Daddy niache ninywe.Nahisi kama akili yangu imefika mwisho wake wa kufikiri.I don’t know what to do anymore” akasema Happy.Mzee Raymond akaketi pembeni yake
“Happy please don’t do this.Hii si njia sahihi ya suluhisho la matatizo yote yanayokukabili kwa sasa.Kunywa pombe kunaongeza matatizo na si kuyapunguza.Happy unatakiwa usimame imara na ukabiliane na kila jambo linalotokea.To win this you have to be strong.Nakuomba usife moyo Happy.Inuka ,simama na upambane hadi mwisho.” Akaseme amzee Kibaho
“Dady ,najitahidi sana lakini nashindwa.I’ve been so strong but not anymore.I’m so weak now.I cant fight, I cant do anything,I’m confused” akasema Happy
“Happy mwanangu naomba ujitahidi na usimame imara na hasa katika wakati huu.Patrick yuko gerezani .He’s alone and lonely.He neesds you.He needs your support.If you cant be strong for yourself then be strong for Patrick” akasema mzee Raymond
Kauli ile ya mzee Raymond ikamchoma sana Happy aliyekuwa ameinama akilia akainua uso wake na kufuta machozi.
“Happy umenielewa?
“Nimekuelewa baba.Samahani kwa kitu nilichotaka kukifanya.Nilidhani kutumia pombe kungekuwa ni suluhisho la kuniondolea mawazo mazito niliyonayo.I wont do that again dady.I promise..” akasema Happy
“Nafurahi kusikia hivyo Happy.tafadhali jipe moyo ,simama imara na sisi tuko nyuma yako katika kila hatua.Tutakupa kila aina ya ushirikiano unaouhitaji toka kwetu”
“Ahsante sana baba .Japokuwa suala hili ni gumu lakini nitajitahidi kwa kadiri niwezavyo kukabiliana nalo hadi dakika ya mwisho.Sikushawishiwa na mtu kufanya maamuzi haya .Niliamua mimi mwenyewe kwa hiari yangu kuachana na Mike na kurudiana na Patrick kwa hiyo inanilazimu nisimame imara katika kukipigania kile kilichonifanya nikachukua maamuzi haya..Najua Mike ameumia sana na yote aliyofanya leo ni kwa sababu yangu.Hakutegemea kama mimi naye tungeachana.Atanisamehe kwa maamuzi haya .” akasema Happy
“Nimefurahishwa na kauli yako Happy.kama nilivyokwambia mchana wa leo kwamba kuna wakati katika maisha yetu tunalazimika kufanya maamuzi magumu na maamuzi hayo magumu siku zote huwa yana athari zake.Lazima wawepo watu watakaoathirika na maamuzi hayo na ndiyo mana yakaitwa ni maamuzi magumu.Ninachokushauri kwa sasa achana na mambo yote yanayojitokeza au yatakayojitokeza na badala yake akili yako ielekeze katika jambo moja tu kulipigania penzi lako na Patrick.Pambana kila uwezavyo kuhakikisha kwamba Patrick anakuwa huru na hatimaye muishi maisha yenye furaha kubwa .Dont ever give up fighting.Mengi yametokea na mengi yatatokea lakini usiyape uzito bali macho na akili yako vielekeze kwa Patrick ambaye anateseka gerezani” akasema mzee Raymond.
“Baba nimekuelewa na ninakuahidi kwamba kuanzia sasa sintalia tena.I’ll be strong.Nimekwisha lia vya kutosha.Ahsante sana kwa kunifanya nitambue kwamba kulia hakutanisaidia lolote zaidi ya kuniongezea maumivu ya moyo” akasema Happy
“kesho tunakwenda kumuona Patrick gerezani,uko tayari kuonana naye? Akauliza mzee Raymond
“Niko tayari baba.Niko tayari kuonana na mtu ambaye ameushika moyo wangu.Nina imani hata haya mateso na maumivu ya moyo niliyonayo sasa yatapungua kama si kuisha kabisa nitakapomuona Patrick”
“Ok Happy kesho nitakupeleka Uwangwa Prison kuonana na Patrick.Nina imani hata naye pia ana hamu kubwa ya kuonana nawe.Margreth utapenda kuongozana nasi?
“Hapana baba kwa siku ya kesho nitakuwa kazini.Nitakwenda kumtembelea siku nyingine”akajibu Margreth.
Baada ya maongezi yaliyochukua zaidi ya saa moja,Happy akajikuta akitabasamu tena.Mzee Raymond akaichukua ile chupa ya mvinyo na kutoka mle chumbani akamuacha Happy akiwa na mdogo wake Margreth
Saa ya ukutani ilionyesha ni saa tatu za asubuhi.Happy Kibaho alikuwa mbele ya kioo kikubwa akijitazama.Siku hii ya leo alikuwa ameamka asubuhi sana na kuanza kujiandaa kwa ajili ya safari ya kuelekea katika gereza la Uwangwa kuonana na Patrick
“Moyo wangu una furaha sana na wasi wasi pia.Sijui Patrick atakuwa katika hali gani.Sijui itakuwaje nitakapomuona “ akawaza Happy akiwa amesimama mbele ya kioo kikubwa.
Wakiwa bado wanajiandaa ,ikasikika kengele ya getini.Pendo mfanyakazi wa ndani akaenda kufungua geti akakutana na gari lenye namba za kibalozi likiambatana na gari moja la polisi..Aliogopa na kutaka kufunga geti na kurudi ndani lakini toka katika gari lile lenye namba za kibalozi akashuka Mike.
“Maafisa naomba dakika tano tu niagane na mtu wangu wa muhimu sana” akasema Mike akiwaomba maafisa wa polisi alioambatana nao halafu akamfuata Pendo
“Happy yuko wapi? Akauliza Mike
“Yuko chumbani kwake” akajibu Pendo kwa wasi wasi
“Naomba ukamuite” akasema Mike huku akiingia ndani.Mara tu alipoingia sebuleni akakutana na mzee Raymond wakasalimiana.
“Pole sana Mike kwa yaliyotokea.”
“Nashukuru sana mzee” akajibu Mike.Hakutaka maongezi mengi na mzee Kibaho.
“Mzee nimepita mara moja kuonana na Happy na kumuaga……….” Kabla hajaendelea Happy akatokea pale sebuleni.Alikuwa na uso wenye wasi wasi mwingi.Akamtazama Mike na macho yake yakalengwa na machozi.Akamfuata na kumkumbatia.
“Mike I’m sorry……” akasema Happy
“You don’t have to be sorry Happy “ akajibu Mike.Wakatazamana kwa muda halafu Mike akasema
“Happy sina muda mrefu wa kukaa hapa.Nimekuja mara moja kukuaga.Ninaondoka kurejea Marekani sasa hivi.”
“Ouh Mike I’m sorry..!!!!.” akasema Happy huku machozi yakimtoka.
“Tafadhali usilie Happy.I’m ok now” akasema Mike
“Mike jambo gani hasa lilitokea? Niliona katika taarifa ya habari jana usiku kwamba ulipatwa na matatizo ukapelekwa polisi.Niliumia sana Mike.”
“Jana uliponiacha pale hotelini nilikuwa katika hali ya kuchanganyikiwa.Sikutambua nilichokuwa nakifanya.Nilishikiliwa kwa muda pale hotelini na waliponiachia niliondoka nikiwa na mawazo mengi sana na nilipokuwa barabarani nilisababisha ajali.Sifahamu ilitokeaje lakini nilijikuta nikimshambulia afisa wa usalama barabarani na kumsababishia majeraha.Nilikamatwa na kupelekwa polisi.Nawashukuru viongozi wangu wa ubalozi wa Marekani kwa jitihada zao za kunisaidia katika tatizo hili.Baada ya jitihada kubwa za kidiplomasia hatimaye serikali ya Tanzania imeamua kuniachia huru lakini imeniamuru niondoke nchini haraka sana na nisirejee tena hapa Tanzania.Nimeona nisiondoke bila ya kuja kukuona na kukuaga Happy.Utanisamehe sana kwani sikutegemea kama ningeweza kufanya kitendo kama kile cha uvunjifu wa sheria.Unanifahamu vizuri mimi si mtu wa vurugu na hii ilitokea kutokana na kughafirika tu.” akasema Mike
“Ouh Mike nisamehe sana mimi kwani ndiye chanzo cha haya yote.Bila mimi yasingekukuta mambo haya .” akasema Happy
“Usijilaumu Happy.Ni ujinga wangu ndio uliopelekea nikafanya kitendo cha kijinga namna ile.I shouldn’t ‘ve done that.Anyway sitaki kuliongelea sana hilo .Yameshatokea na tuyaache yapite.Happy nimekuja kukuaga.Nilikuja hapa Tanzania kwa ajili yako kwa hiyo siwezi kuondoka bila ya kuja kukuaga hata kama yametokea haya yaliyotokea.Nadhani hii itakuwa ni mara yetu ya mwisho kuoanana kwani nimepigwa marufuku kurejea Tanzania tena.Pamoja na kuondoka kwangu lakini naomba ufahamu kwamba moyo wangu bado unakupenda sana na nitaendelea kukupenda siku zote na kwa sababu ya upendo wangu kwako nayakubali maamuzi yako.Nakuacha uwe na Patrick kama ulivyoomba.Japokuwa nimeumizwa sana na suala hili lakini sina namna nyingine ya kuweza kuyabadili mawazo yako.Kitu kimoja tu ambacho naomba ukifahamu ni kwamba siku zote utaendelea kuwepo moyoni mwangu na unakaribishwa muda wowote kama una hitaji kuongea nami au aina yoyote ya msaada toka kwangu.I’ll always be there for you Happy because I love you” akasema Mike akiwa ameishika mikono ya Happy ambaye machozi yalikuwa yanamchuruzika.Mike akamfuta Happy machozi kwa mikono yake halafu akainama na kumbusu shavuni.
“Kwa heri Happy.” Akasema Mike na kugeuka akaanza kuondoka..Kabla hajafika mlangoni Happy akaita
“Mike !!!.” Mike akageuka
“Hutajali kama nikikusindikiza uwanjani? ..akasema Happy Mike akatabasamu na kusema
“Sintajali Happy” akajibu Mike Happy akakimbia chumbani kwake akachukua funguo ya gari lake
“I’ll go with you” akasema mzee Raymond.Happy akatabasamu.Wakaingia garini na safari ya kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere ikaanza.
“Nasikitika sana baba kwa mambo haya yaliyomkuta Mike.Am……………….” akasema Happy lakini kabla hajaendelea mbele baba yake ambaye alikuwa anaendesha gari ile akasema
“Usisikitike Happy.Kama nilivyokueleza jana usiku kwamba kwa sasa elekeza akili yako katika jambo moja tu nalo ni Patrick.Haya mambo mengine usiyape nafasi ya kukuumiza kichwa chako..Mike ni kijana mzuri ambaye ninaamini atapata mwanamke mwingine .Usiwaze sana kuhusu Mike.” Akasema mzee Raymond.
“Hata hivyo namshukuru Mike amenielewa na ameahidi hatanisumbua tena.Amebariki uhusiano wangu na Patrick.” Akasema Happy huku akitabasamu .baba yake naye akatabasamu
“Siamini kama leo hii ninaondolewa nchini Tanzania nikiwa chini ya ulinzi wa polisi.Nakijutia kitendo nilichokifanya.Nilifanya kitendo cha kijinga sana ambacho nitaendelea kukijutia katika maisha yangu yote.Lakini yote haya yamesababishwa na Happy.Wakati ninafanya kitendo kile sikuwa katika akili yangu ya kawaida.maamuzi yale ya Happy yalikuwa yameichanganya sana akili yangu .Sikutegemea kama mapenzi yangu na Happy yangetufikisha katika hatua hii.Sikutegemea kama siku moja tungeachana kirahisi rahisi namna hii.Bado naona ni kama ndoto kutokana na jinsi tulivyokuwa tunapendana.Nilimpenda Happy kwa moyo wangu wote na nilikuwa tayari kufanya jambo lolote lile kwa ajili yake.Kwa upande mwingine simlaumu sana kwa maamuzi haya kwa sababu ameufuata moyo wake.Kama alivyosema yeye mwenyewe kwamba Patrick ndiye furaha ya maisha yake kwa hiyo sina budi kuyaheshimu maamuzi yake.Lakini sintamsahau hata kidogo.Itanichukua miaka mingi kumtoa Happy moyoni mwangu na ninaamini siku moja nitamsahau na nitampata mwanamke ambaye ameumbwa kwa ajili yangu.” Mike alikuwa akiwaza wakati wakielekea uwanja wa ndege.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Walifika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere na baada ya kushuka garini Mike akamfuata Happy akamshika mikono
“Happy nashukuru sana kwa kunisindikiza.You can go home now.I’ll be fine” akasema Mike.Macho ya Happy yalilengwa na machozi.
“Mike naomba unisamehe sana kwa yote yaliyotokea.Sik…………………………” akasema Happy lakini Mike akamzuia asiendelee.
“Shhhhhhhhhhh…!!!!...Usisikitike Happy kuhusu kilichotokea.Nimetafakari kwa kina na kukuelewa kwamba unaitafuta furaha ya moyo wako ambayo ni Patrick na kwa hilo mimi sina tatizo .Ninaamini kwamba wewe na Patrick hakuna kitakachoweza kuwatenganisha tena.Kitu pekee ninachokuomba Happy ni kwamba mpende Patrick kwa moyo wako wote. You’ ve made a huge sacrifice so don’t you ever let it be for nothing.Fight till the end” akasema Mike.
Happy hakusema kitu alikuwa anatokwa na machozi.
“Happy usijali kuhusu mimi.Japokuwa moyo wangu umevunjika vipande lakini nitajitahidi kwa kadiri niwezavyo ili kulitibu jeraha hili litakalochukua muda mrefu kupona.Ninachokushauri kwa sasa ,mpiganie Patrick ili aweze kutoka gerezani.” Akasema Mike na kugeuka baada ya ofisa mmoja wa ubalozi kumsogelea na kumfanyia ishara kwamba muda unakwenda.
“Happy muda wangu umekwisha,natakiwa kuondoka sasa lakini kabla sijandoka kuna kitu ambacho nataka kukuomba”
“Omba chochote Mike” akasema Happy
“Ninaomba niendelee kuwa rafiki yako”
“Mike siku zote utabaki kuwa rafiki na mtu wa karibu sana kwangu.” Happy akashindwa kuendelea akaanza kulia
“Nashukuru sana Happy.Muda wowote ukinihitaji unafahamu namna ya kunipata.Ubaki salama Happy.” Akasema Mike halafu akamkumbatia Happy na kumbusu shavuni na kuondoka.Happy akamtazama Mike hadi alipopotea kabisa katika macho yake.Bado machozi yaliendelea kumtoka.
“ It’s ok ..!! let him go “ akasema mzee Kibaho.
“ Inatosha sasa.Nyamaza kulia.” Mzee Kibaho akamshika mkono Happy na kumfungulia mlango wa gari akaingia kisha wakaondoka pale uwanjani.
“Tunaelekea Uwangwa Prison.Uko tayari kuonana na Patrick? Akuliza mzee Kibaho.
“Niko tayari baba” akajibu Happy
************************
Ni siku ya mazishi ya Veronika.Toka alfajiri nyumbani kwao kumekuwa ni sehemu yenye pilika nyingi.Kila kitu kilikwisha tayarishwa na kilichokuwa kinasubiriwa na muda tu wa kuanza shughuli hii.Ndugu ,jama na marafki waliokuwa wakisubiriwa tayari walikwisha fika wote.
Saa tatu za asubuhi ,Sarah akampigia simu Alois kaka yake Patrick
“ Hallow Sarah” akasema Alois baada ya kupokea simu
“Alois nimekupigia kukutaarifu kwamba leo tunamzika Vero.Atazikwa katika makaburi ya kinondoni.Ratiba inaonyesha kwamba baada ya mwili kuchukuliwa toka hospitali ya muhimbili , utaletwa hapa nyumbani kwa ajili ya kuagwa na baadaye utapelekwa kanisani kwa ajili ya ibada ya misa na kisha tutaelekea makaburini.Nilitaka kujua kama kuna mtu yeyote ambaye atatumwa kuja kuwakilisha ..” akasema Sarah
“Sarah ningependa sana kutuma uwakilishi lakini ninasita kufanya hivyo kutokana na kilichotokea jana.Wajumbe tuliowatuma kuja kutuwakilisha walifukuzwa na Loniki na kuambiwa kwamba hatutakiwi kabisa kuonekana katika msiba wa Vero kwani mwanetu amemuua ndugu yenu makusudi.Sarah nasikitika sana kwa jambo hili.”
“Alois samahani sana kwa kilichotokea jana.Hata mimi siafiki jambo kama lile na sikulipenda hata kidogo.Hatupaswi kujenga chuki na uhasama baina yetu.Sote tumeumizwa na jambo hili kwa hiyo kuna kila ulazima wa kushirikiana katika kipindi hiki kigumu.Alois naomba usikate tamaa ,sisi tayari tulikwisha kuwa ndugu kwa hiyo nakuomba ufanye juu chini utume watu ambao watakuja kumuwakilisha Patrick katika mazishi ya mchumba wake.Watakapofika wanitafute mimi na si mtu mwingine yeyote” akasema Sarah.
“Nimekuelewa Sarah nitatuma ujumbe wa watu kuja kutuwakilisha na kumuwakilisha Patrick .Ningeweza kuja hata mimi mwenyewe lakini bado naendelea kupokea wageni mbali mbali kwa sababu mimi ndiye mtoto mkubwa wa mzee..”
“Usijali Alois .Kwa sasa tunaelekea hospitali ya Muhimbili kuuchukua mwili na kisha tutarejea hapa nyumbani kwa ajili ya taratibu za kuuaga.” Akasema Sarah akaagana na Alois na kukata simu.
Baada ya kumaliza kuongea na Sarah,Alois akampigia simu Andrew ambaye alikuwa katika majukumu mengine pale msibani na kumtaka waonane mara moja
“Andrew nimetoka kuongea na Sarah muda si mrefu ,leo ndiyo siku ya mazishi ya Vero .Ameniomba nitume ujumbe wa watu kwenda kutuwakilisha..Una mawazo gani kuhusu hilo?
Andrew akainama akafikiri kidogo na kusema
“Ni wazo zuri lakini bado nina wasi wasi na kilichotokea jana.Loniki dada mkubwa wa Vero alitufukuza na kutuonya kwamba tusikanyage tena pale msibani.Lakini kama Sarah amesisitiza kwamba utume ujumbe ,basi fanya hivyo.Teua ujumbe wa watu wachache na uwatume kutuwakilisha katika mazishi”
Alois akainama na kufikiri kidogo halafu akasema
“Andrew itabidi uongoze ujumbe utakaokwenda kutuwakilisha huko.” Akasema Alois
“Sawa Alois.Sina tatizo na hilo.” akasema Andrew na muda huo huo akaingia Savanna.Wakasalimiana na kumfahamisha kilichokuwa knaendelea.
“Ninaomba na mimi niungane na ujumbe huo utakaokwenda nyumbani kwa akina Vero katika mazishi.” Akasema Savanna
“Usijali Savanna tutakuwa sote” akasema Andrew huku akiitoa simu yake iliyokuwa inaita na kusogea pembeni
“Savanna,Patrick alikuwa katika hali gani ulipompa taarifa za kifo cha mzee? Akauliza alois
“Alistuka sana.Japokuwa alijaribu kujikaza lakini aliumia mno moyoni.Vifo viwili vya watu wake muhimu vimetokea kwa haraka sana lazima atakuwa na maumivu makubwa moyoni.” Akasema Savanna.
“Namuonea huruma sana mdogo wangu.Tayari alikuwa na maisha yake mazuri na yenye furaha akiwa na Vero lakini mara tu alipojitokeza huyu Happy kila kitu kimeharibika” akasema Alois kwa masikitiko.
“Usisikitike sana alois.Huwezi fahamu ni kwa nini mambo haya yametokea sasa.” Akasema Savanna
* * *
Msafara wa gari zaidi ya tano uliondoka nyumbani kwa akina Vero kuelekea hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kuuchukua mwili wa Vero.Katika msafara huo walikuwepo pia Loniki na Sarah dada zake Vero.Katika gari walilokuwa wamepanda,Loniki alikuwa na chupa ya mvinyo akiendelea kunywa.Macho yalikuwa yamemvimba kutokana na kulia.Toka asubuhi amekuwa akinywa mvinyo huu mkali ili kumsaidia kumpunguzia uchungu wa kifo cha mdogo wake.
“Loniki tafadhali naomba usiendelee kunywa huo mvinyo.” Akasema Sarah lakini Loniki akajibu kwa ukali
“Let me drink…Huwezi kujua uchungu nilionao.Nilimpenda sana Vero lakini Patrick amemkatili uhai wake.Nina uchungu mwingi sana na ambao sina hakika kama unaweza kuelezeka” akasema Loniki.Akainua chupa yake ya mvinyo akapiga funda moja na kusema
“Nina hasira sana na Patrick.Yeye ndiye aliyesababisha uchungu wote huu.Sisemi zaidi nasubiri kwanza masuala ya msiba yamalizike” akasema Loniki,Sarah akamtazama hakutaka kumsemesha tena.Safari ikaendelea.
Walifika hospitali ya Taifa ya Muhimbili .Pale walikutana na watu ambao walikwisha tangulia ili kwenda kukamilisha taratibu za kuuchukua mwili wa Vero.
Saa sita za mchana taratibu zikakamilika na mwili wa Vero ukawa tayari kwa kuchukuliwa.Ndugu jamaa na marafiki waliofika pale Muhimbili walipata nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho.Vero alikuwa amelala ndani ya jeneza lake la gharama kubwa akiwa amevalishwa gauni lake la harusi alilokuwa amelinunua uingereza kwa ajili ya kulivaa siku ya harusi yake na Patrick.Loniki alishindwa kujizuia akaanguka na kupoteza fahamu.Kwa muda wa dakika chache eneo lote la Muhimbili liligeuka sehemu ya vilio.Loniki na baadhi ya akina mama waliopoteza fahamu walipatiwa msaada na baada ya kuzinduka safari ya kuelekea nyumbani ikaanza.
Saa tano za asubuhi Happy kibaho akiwa ameongozana na baba yake mzee Raymond Kibaho wakawasili katika gereza la Uwangwa kwa lengo la kumuona Patrick.Kama zilivyo taratibu za gereza hili walijiandikisha majina yao ikiwa ni pamoja na kuchukua alama za vidole kisha wakapelekwa katika sehemu maalum kwa ajili ya kuonana na mahabusu.Happy moyo wake ulikuwa unamuenda mbio sana
“Jitahidi ujizuie usiangushe chozi.Patrick anahitaji kukuona ukiwa katika uso mkavu.” Akasema mzee Kibaho wakati wameketi wakimsubiri Patrick aletwe.Happy hakujibu kitu,alimtazama baba yake kisha akavuta pumzi ndefu.
Baada ya dakika tano akatokea Patrick akiwa ameongozana na askari magereza.Mara tu Happy alipomuona Patrick akajikuta akisimama na kutamka kwa sauti ndogo yenye mshangao ndani yake
“Patrick …..!!!!!!! akasema Happy
Patrick akaelekezwa sehemu ya kukaa na Yule askari.
“Patrick una dakika ishirini za kuongea na wageni wako” akasema Yule askari akasogea pembeni na kumpa nafasi ya kuongea na wageni wake kwa uhuru na mara Patrick na Happy wakakumbatiana kwa nguvu.
Happy alishindwa kujizuia akaangusha machozi
“Nyamaza usilie Happy.Usilie tena malaika wangu.Inatosha” akasema Patrick huku akimfuta Happy machozi kwa mikono yake.Happy akamkumbatia tena kwa nguvu.Baada ya kama dakika tatu Patrick akamshika mkono na kumketisha chini.Macho ya Happy bado yaliendelea kudondosha machozi.
“Stop crying Happy.Its enough now.Umekwisha lia vya kutosha” akasema Patrick huku akimpiga piga Happy mgongoni.Alipogeuza shingo yake akagonganisha macho na mzee Raymond Kibaho.
“Pole sana Patrick” akasema mzee Raymond huku akisogea na kumpa mkono Patrick
“Nashukuru sana mzee.Nimekwisha poa” akasema Patrick na kujilazimisha kutabasamu
“Usife moyo kijana wangu.Matatizo ni sehemu ya maisha yetu wanadamu na hatuna budi kukabiliana nayo kila yanapotokea.Tuko pamoja Patrick na wala usijali tutashirikiana katika kila jambo na mwisho kuhakikisha kwamba mambo haya yanakwisha.” Akasema mzee Raymond .
“Nashukuru sana mzee kwa ushirikiano wako.Mungu atasaidia na mambo haya yatakwisha” akasema Patrick halafu akamgeukia Happy aliyekuwa ameinama akilia kimya kimya.
“Patrick naomba niwaache wenyewe muongee nitakuwa hapo nje” akasema mzee Kibaho na kutoka nje akawapa nafasi Patrick na Happy yakuongea mambo yao kwa uhuru.
“Pole sana Patrick” akasema Happy baada ya baba yake kutoka nje.
“Ahsante sana malaika wangu.Nimefarijika sana nimekuona tena.Vipi unaendeleaje?
“Hata mimi nimefarijika sana kukuona tena Patrick.Ninashukuru Mungu ananisaidia ninaendelea vizuri japokuwa si rahisi.Nakumbana na magumu mengi sana.”
“Pole sana Happy.Ninafahamu ni namna gani ulivyo na wakati mgumu.Utanisamehe mpenzi wangu halikuwa kusudio langu kukuweka katika wakati mgumu namna hii.Sikutegemea kama maamuzi yangu yangetufikisha hapa tulipo sasa” akasema Patrick kwa uchungu.
“Usiseme hivyo Patrick.Haya hayakuwa maamuzi yako peke yako.Tulifanya maamuzi haya sote wawili kwa hiyo usijilaumu kwa kilichotokea na wala hakuna haja ya kujilaumu au kumlaumu mtu yeyote kwa maamuzi yetu.Tuachane na yaliyotokea na tuangalie namna ya kukabiliana na yale yajayo.” Akasema Happy halafu wakatazamana kwa sekunde kadhaa.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Pole sana kwa msiba wa baba “ akasema Happy
“Ahsante sana Happy nimekwisha poa.Yote haya ni mapenzi ya Mungu” akasema Patrick halafu kikapita kimya kifupi.
“Happy ninaomba uwe mvumilivu sana katika kipindi hiki .Tunapita katika kipindi kigumu mno katika maisha yetu.Nayafahamu mateso na maumivu uliyonayo ,lakini naomba nikuhakikishie kwamba siku moja mambo haya yote yatakwisha na ndoto yetu ya siku nyingi ya kuwa pamoja itatimia.Safari ya kuelekea kuitimiza ndoto yetu si rahisi hata kidogo imejaa vikwazo vingi na majaribu mengi.Tukiwa na imani na kusimama katika msimamo wetu ,tutayashinda haya yote.Yatupasa kuwa wavumilivu sana hasa katika wakati huu” akasema Patrick.
“Patrick ,naomba nikiri kamba mambo katu si rahisi hata kidogo.Haya masuala ni mazito na katika maisha yangu sikutegemea kukumbana na kipindi kigumu kama hiki.Kuna nyakati inaniwia ugumu kuyabeba mambo haya na ninajikuta nikiwa dhaifu lakini namshukuru sana Mungu kwani amekuwa ndiyo nguzo yangu na kwa sababu yake kila siku nimekuwa nikipata nguvu za kusonga mbele.Kuna nyakati ninakata tamaa lakini ninapokumbuka sura yako na upendo wako mkubwa kwangu ninapatwa na nguvu za ajabu za kupambana hadi mwisho.Patrick napenda kukuhakikishia kwamba niko imara sasa na sintalia tena na ninakuahidi kwamba nitalipigania penzi letu hadi dakika ya mwisho.Nitahakikisha kwa kila iwezekanavyo tunatimiza ndoto yetu ya kuwa pamoja.Patrick nakupenda sana na nitakupenda hadi mwisho wa uhai wangu” akasema Happy na kwa mbali sura ya Patrick ikajenga tabasamu
“Nashukuru sana Happy kwa ujasiri wako.Nitazidi kukuombea ili uweze kupata ujasiri zaidi wa kuweza kukabiliana na kila gumu linalojitokeza.” Akasema Patrick,kikapita kimya cha sekunde kadhaa wakitazamana.
“Patrick kuna mambo ambayo yametokea katika siku hizi chache ambayo nadhani ingekuwa vyema kama ungeyafahamu” akasema Happy na kukaa kimya kidogo akamtazama Patrick.
“mambo gani malaika wangu? Akauliza Patrick
“ Nimelivua taji la Miss Tanzania”
“What…..!!!!!” Patrick akashangaa
“Happy umefanya nini tena? Kwa nini umechukua maamuzi hayo? Akauliza Patrick
“Patrick si wewe peke yako uliyestushwa na maamuzi haya ya kulivua taji la Miss Tanzania .Wengi wamestushwa sana na maamuzi haya kwani haijawahi kutokea katika historia kwa mrembo kulivua taji kubwa kama hili.Sikuwa na njia nyingine ya kufanya zaidi ya kulirudisha taji lile kwa wenyewe ili kuendelea kuilinda heshima yake” akasema Happy.Patrick akamshika mkono na kumtazama usoni
“Happy kwa nini umefanya hivyo? Haikuwa rahisi kulishinda taji lile kubwa na muhimu kwako.Kwa nini umelivua haraka namna hii?
“Toka siku yalipoanza matatizo haya,nilikuwa ni kama mtu niliyechanganyikiwa.Sikujua nifanye nini ili kuweza kukabiliana na hali hii.I was so weak.Siku ile ulipopandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza nilifika mahakamani lakini sikuweza kuingia ndani .Nilibaki ndani ya gari.Nilikuwa mtu wa kujifungia ndani na kulia.Namshukuru sana Savanna kwa sababu alinitembelea nyumbani akanifariji na kuniambia maneno ambayo yalinifanya nipate nguvu na tumaini tena.Nilifikiria sana kuhusu mustakabali mzima wa maisha yangu na namna nitakavyoweza kukabiliana na suala hili lililojitokeza nikaamua kuyaweka kando mambo yote ikiwemo na taji la miss Tanzania ili nibaki naangalia suala moja tu la kesi yako.Patrick thamani yako ni kubwa sana kwangu kuliko taji la miss Tanzania au kitu chochote kile na ndiyo maana sikujuta na wala sijutii maamuzi yangu.Moyo wangu una amani kabisa kwa sababu nimefanya hivyo ili niweze kuwa na muda mwingi wa kushughulika na mtu ninayempenda kuliko wote hapa duniani.Niliwataarifu familia yangu na wakakubaliana nami.Nawashukuru sana kwani wamekuwa na mimi karibu sana na kunipa nguvu.Niliwasiliana na wakuu wangu nikawaeleza ,japokuwa ilikuwa vigumu kwao kukubali lakini waliiona hoja ya msingi katika maombi yangu na wakakubali japo kwa shingo upande.Jana nilifanya mkutano na waandishi wa habari na kutangaza rasmi kwamba nimelivua taji la miss Tanzania.” Patrick akamkumbatia Happy na kusema
“Happy,sipati neno la kusema kuelezea furaha yangu.Nilikuwa na wasi wasi mwingi baada ya kutokuona mahakamani siku ile ya kesi yangu ilipotajwa.Nilimtuma Savanna aje akuangalie .Nashukuru kukuona ukiwa unaendelea vizuri japokuwa nimeumizwa na maamuzi hayo mazito uliyoyachukua ya kulivua taji lile muhimu sana kwako” akasema Patrick.
“Patrick huna sababu ya kuhuzunika kwa maamuzi haya.Hakuna mtu yeyote aliyenishurutisha kufanya hivi .Nimefanya hivi kutokana na thamani yako kwangu,kwa sababu ninakupenda kuliko mtu yeyote duniani” akasema Happy halafu akaishika mikono ya Patrick na kuibusu
“Vipi kuhusu maendeleo ya kesi” akauliza Happy
“Bado sijapata picha halisi kuhusiana na mwenendo mzima wa kesi kwa sababu bado iko katika hatua za awali za kutajwa.Bado upande wa mashtaka wanaendelea kukusanya ushahidi wa kutosha.Savanna amenipa moyo kwamba kesi hii haina ugumu kwake.Ninamuamini Savanna ni wakili maarufu sana na hajawahi kushindwa kesi toka ameanza kazi hii ya uwakili.Nina uhakika mkubwa wa kushinda”
Happy akamtazama Patrick usoni na kuuliza
“Do you trust her ?
“Yes I do.Savanna ni mmoja wa mawakili mahiri sana hapa nchini.Amekuwa akishughulika na kesi mbali mbali kubwa kubwa na haijawahi kutokea akashindwa kesi.Kwa nini umeuliza? Una wasi wasi naye?
“Never mind….I was just curious.Nilitaka nifahamu tu uwezo wake katika kuisimamia kesi hii.Do you know each other for long ? akauliza Happy
“Yes we know each other for long.She’s my friend.Tumekuwa marafiki kwa muda mrefu sana sasa.Why do you ask? Don’t you trust her?
“Si hivyo Patrick.Nahitaji tu kumfahamu vizuri.Tunahitaji wakili mahiri katika kesi hii ambaye ataweza kuisimamia na kuhakikisha tunashinda.Savanna atahitaji shilingi ngapi katika kuisimamia kesi hii hadi mwisho? Nahitaji na mimi nitie mchango wangu katika kumlipa wakili atakaye simamia kesi hii” Akauliza Happy
“Usihofu Happy kuhusu malipo ya Savanna.Hakutakuwa na malipo yoyote kwa sababu Savanna anaifanya kazi hii bila malipo yoyote.Amejitolea yeye mwenyewe kuzibeba gharama zote za kesi hii.Huo ni mchango wake kwangu”
“Patrick..!!!..” Happy akashangaa
“Anawezaje kuisimamia kesi kubwa kama hii bila kuhitaji malipo yoyote? Happy akauliza
“Kama nilivyokwambia Happy kwamba mimi na Savanna ni marafiki wa siku nyingi na amejitolea kuifanya kazi hii bure kabisa bila malipo yoyote yale.Tunachotakiwa kufanya ni kumpa ushirikiano anaouhitaji na kwa pamoja tutashinda.” Akasema Patrick halafu akageuza shingo yake akamtazama askari magereza aliyekuwa amesimama pembeni kidogo akiangalia saa yake.
“Happy naona hatutakuwa na muda mrefu zaidi wa kuongea.Ninachokuomba usiwe na wasi wasi wowote kuhusu mimi.Niko salama na ninaendelea vizuri.Nimefarijika sana kwa kuja kunitazama.Nitafurahi zaidi kama ukija kunitazama mara kwa mara.Kuhusu kesi yangu nakuhakikishia kwa mara nyingine tena kamba usiwe na wasi wasi wowote ule.Savanna atashughulikia kila kitu.Ninachokuomba jaribu kuwa naye karibu ili aweze kukufahamisha kila kinachoendelea kuhusiana na kesi hii.”
“Ouh Patrick my angel ,natamani niendelee kukaa nawe hapa japo kwa siku nzima.Najisikia vibaya sana kuondoka na kukuacha peke yako.Ouh my darling sijui hata nifanye nini…” Happy akasema huku machozi yakimlenga lenga
“Usihofu kuhusu mimi Happy.Niko salama na ninapata kila ninachokihitaji.Savanna anafahamika sana hapa na kwa hiyo kwa heshima yake ninapata huduma nzuri tofauti na mahabusu wengine.Kwa hiyo nakuomba uwe na amani ya moyo.Kitu cha msingi ni kuongeza maombi ili mambo haya yaweze kufikia mwisho ila usisahau kuwasiliana na Savanna mara kwa mara.Kama kuna chochote ninachotaka kukwambia nitakuwa namtumia hata yeye kwa sababu yeye huja hapa gerezani kila siku na kunitazama na kuniletea taarifa mbali mbali kuhusiana na kesi yangu.”
“Patrick nitakuja mara kwa mara kukutazama.Nitashirikiana na Savanna kwa ukaribu sana kama ulivyosisitiza.” Akasema Happy halafu akamkumbatia Patrick.
“Mama,muda umekwisha.Patrick anatakiwa kurudishwa ndani” akasema Yule askari magereza aliyekuwa akimlinda Patrick.
Happy na Patrick wakabusiana na kisha akainuka na taratibu akaanza kuelekea mahabusu.Happy akamtazama huku machozi yakimtoka hadi alipopotea kabisa
“It’s ok Happy” akasema mzee Kibaho huku akimshika bega mwanae na taratibu akamshika mkono wakatoka mle ndani.
“Dady nimefarijika na kuumia pia baada ya kumuona Patrick” akasema Happy wakiwa garini wakiondoka .
“Ninaamini hata Patrick amefurahishwa na kufarijika sana baada ya kukuona.Nilimtazama machoni alishindwa kuificha furaha yake.Vipi kuhusu mwenendo wa kesi ?
“Kwa mujibu wa maelezo yake ni kwamba kesi inakwenda vizuri na amenitaka nisiwe na wasi wasi kwa sababu wakili anayemtetea ni mahiri sana katika kuzisimamia kesi kama hizi.Lakini dady bado nina wasi wasi kama kweli Savanna anaweza akaifanya kazi hii ipasavyo.Ninafikiria kumtafuta wakili mwingine ili aungane na Savanna katika kuisimamia kesi hii”
“Kwa nini unakuwa na wasi wasi kuhusiana na wakili anayemtetea Patrick? Una shaka na uwezo wake?
“Sina shaka na uwezo wake lakini nina wasi wasi kidogo kwani hahitaji hata senti moja katika kuisimamia kesi hii.Amejitolea kuifanya kazi hii bure kabisa bila malipo”
“Bila malipo??? Mzee Raymond naye akashangaa
“Ndiyo dady.Amedai kwamba hatahitaji hata senti moja na yeye ndiye atakayegharamia gharama zote za kesi hii” akasema Happy
“Kama Patrick anayoimani na huyo wakili wake basi hakuna tatizo .Kitu cha msingi ni kutoa ushirikiano kwa haraka pale utakapohitajika.Tukisema tutafute tena wakili mwingine kwa sasa inaweza ikaleta tatizo na familia ya Patrick.” Akasema mzee Kibaho.
“Nakubaliana nawe baba.Inaweza ikaleta mgongano mkubwa baina yetu.Kitu pekee ninachoona cha msingi ni kuwa karibu na Savanna kama Patrick alivyosema.” Akasema Happy halafu akachukua simu na kuzitafuta namba za simu za Savanna akapiga
“Hallo Happy !..” akasema Savanna baada ya kupokea simu
“Hallow Savanna habari yako?
“Habari yangu nzuri Happy.Unaendeleaje?
“Ninaendelea vizuri Savanna.Nimetoka kumuona Patrick”
“Vizuri sana Happy.Namna hiyo utamfanya Patrick afarijike na kupunguza mawazo”
“Savanna uko wapi mida hii? Ninaweza kupata nafasi ya kuonana nawe leo hii? Akasema Happy
“Kwa sasa niko nyumbani kwa akina vero.Mazishi yake yanafanyika leo.Na hivi sasa tunausubiri mwili wa marehemu uwasili ili tuanze zoezi la kutoa heshima za mwisho na baadae tuelekee kanisani na kisha makaburini kwenda kumpumzisha.” Akasema Savanna,kikapita kimya kifupi.Taarifa ile ilimstua sana Happy na kutonesha kidonda cha moyo,akaangusha machozi.
“Happy.!!!..akaita Savanna
“Savanna .!!!!” Happy akataka kusema kitu lakini akashindwa.
“Happy nitakutafuta baada ya mazishi.Nitakuja nyumbani kwenu kukuona.Kwa sasa vimeanza vilio ,mwili wa marehemu umewasili.” Akasema Savanna Happy hakujibu kitu akakata simu.
“Kitu gani kinakuliza Happy? Akauliza mzee Raymond.
“Vero anazikwa leo..” akasema Happy halafu akainama.Mzee Raymond akavuta pumzi ndefu ,akageuza shingo na kumtazama mwanae.
“Happy ,usiwaze sana kuhusu jambo hili.Jitahidi kusahau kuhusu hilo tukio.Kwa sasa elekeza nguvu zako katika kuhakikisha kwamba Patrick anatoka gerezani” akasema mzee Kibaho.
“Dady ,its difficult to forget about what happened that night.Mimi ndiye niliyemuua Vero.Bila mimi Vero angekuwa hai mpaka hivi sasa.” Akasema Happy huku akilia.Mzee Raymond akapunguza mwendo wa gari na kuliegesha pembeni.
“Happy tafadhali nyamaza kulia.Hukukusudia kufanya jambo lile.Ile ni ajali kama ajali nyingine.Ulimsukuma Vero kwa ajili ya kumsaidia Patrick na hukudhamiria kumuua .Usijilaumu sana kwa kilichotokea ”akasema mzee Raymond.Happy akainua kichwa chake na kufuta machozi
“Nimekusikia baba lakini moyo wangu unauma sana.” Akasema Happy.Mzee Raymond akamtazama halafu akawasha gari na safari ikaendelea.
* * *
Eneo lote liligubikwa na sauti za vilio baada ya msafara wa magari kuwasili nyumbani kwa akina Vero ukitokea
hospitali ya taifa ya Muhimbili kuchukua mwili wa Vero.Gari maalum lililokuwa na mwili wa Vero likapewa nafasi na halafu jeneza zuri jeupe lenye nakshi za kupendeza likashushwa toka garini na kuingizwa ndani.Mahala hapa hapakuwa na masikilizano tena kutokana na vilio vingi na wengine walianguka na kupoteza fahamu.Kwa wale ambao bado walikuwa hawaamini kama ni kweli Vero alikuwa amefariki dunia sasa waliamini baada ya kuliona jeneza lile na kuzidisha vilio.Ilichukua zaidi ya nusu saa kuwatuliza waombolezaji na kisha muongoza shughuli akawasomea ratiba nzima ya mazishi.
Joel Armendo mjomba wa Vero akapanda jukwaani na kusoma historia ya marehemu halafu zikafuata nyimbo za maombolezo toka katika kwaya aliyokuwa akiimbia Vero.Baada ya kwaya kumaliza wimbo wa maombolezo ,kikafuata kipindi cha kutoa salamu za rambi rambi.Watu na vikundi mbali mbali walipanda na kutoa rambi rmbi zao na kumuelezea Vero kama binti aliyekuwa mfano wa kuigwa katika jamii.Wote walielezea namna walivyokuwa wameguswa na kifo kile.Baada ya watu na vikundi mbali mbali kumaliza kutoa salamu zao za rambi rambi,mwongoza shughuli akachukua kipaza sauti na kusema
“Tunawashukuru nyote kwa salamu zenu za rambi rambi na namna mlivyoguswa na msiba huu mzito.” Akanyamaza kidogo halafu akasemaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kama mlivyosikia histora ya marehemu kwamba hadi anakutwa na mauti alikuwa na mchumba aitwaye Patrick ambaye walikuwa katika maandalizi ya mwisho ya kufunga ndoa.Kutokana na tukio hili kwa sasa Patrick anashikiliwa na vyombo vya usalama lakini pamoja na kwamba yuko gerezani ametuma salamu zake za rambi rambi kwa msiba huu mzito wa mchumba wake.Tunao hapa wawakilishi toka familia ya Patrick ambao wamekuja kuungana nasi katika mazishi ya binti yetu.Papo hapo bila kusahau ni kwamba Patrick naye amempoteza baba yake mzazi siku ya jana kwa hiyo kijana huyu amekutwa na misiba miwili hivi sasa.Kabla hatujaingia katika zoezi la kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu,naomba kwa heshima kubwa niwaite hapa jukwaani wawakilishi toka familia ya Patrick.Karibuni sana ndugu zetu” akasema muongoza shughuli na minong’ono ikaanza kusikika.
Taratibu Andrew na Savanna wakapanda jukwaani.Andrew akakabidhiwa kipaza sauti.
“Ndugu waombolezaji,tumesimama hapa mbele yenu kuwakilisha salamu nyingi za pole kwa familia hii kufuatia kifo cha mpendwa wao Veronika. Sipati neno la kusema kuelezea uchungu tulionao sisi kama familia ya Patrick kwa kifo hiki cha ghafla cha Veronika.Sote tulimpenda sana na kumjali kama ndugu yetu,shemeji yetu,mchumba wa ndugu yetu Patrick.Hakuna aliyefahamu kama yangetokea haya yaliyotoea.Naomba mfahamu kwamba tumeumizwa sana na kifo hiki.Hii ni kazi ya Mungu na siku zote haina makosa.” Akasema Andrew halafu akanyamaza kidogo akawatazama waombolezaji waliokuwa kimya wakimsikiliza.
“Wakati ,hata sisi kama familia tukiwa katika taharuki juu ya kilichotokea,hata sisi pia tumempoteza mzee wetu ,baba mzazi wa Patrick.Haya ni majonzi makubwa na familia zetu kwa sasa zinapitia kipindi kigumu sana.Hatuna cha kufanya zaidi ya kuziombea roho za wapendwa wetu zipumzike kwa amani.” Akanyamaza kwa sekunde kadhaa halafu akasema
“Baada ya tukio lile lililopelekea umauti wa Vero,Patrick anashikiliwa na vyombo vya usalama na tayari kesi yake imeanza kutajwa na tuna hakika kwamba haki itatendeka.Nawaomba ndugu zangu tuviachie vyombo vya kutoa haki vifanye kazi yake.Najua kwa tukio kama hili yataibuka mambo mengi sana,chuki,visasi,uhasama lakini nawasihi ndugu zangu tusifike huko.Sisi tayari ni ndugu kwa hiyo tusikubali hata kidogo tukio hili likatugawa na kujenga chuki miongoni mwetu.Tuendelee kushikamana katika nyakati hizi ngumu tulizonazo na tuepuke kuishi kwa hasama na kulipizana kisasi.Visasi havitaweza kuurudisha uhai wa wapendwa wetu.Binafsi nimekuwa rafiki mkubwa wa Patrick na Vero kwa muda mrefu sana na ninawafahamu kiundani.Ninayafahamu mapenzi yao pengine kuliko mtu mwingine yeyote kutokana na ukaribu wangu kwao.Kilichotokea hata mimi bado ninaona kama ndoto.” Andrew akanyamaza kisha akaendelea.
“Akiwa gerezani,Patrick ametuma salamu zake za rambi rambi kwa familia,ndugu jamaa na marafiki wa Vero.Baada ya salamu hizo za familia napenda sasa nikabidhi mchango wetu wa pole wa shilingi milioni tatu na papo hapo kuwataarifu kwamba baba mzazi wa Patrick atazikwa kesho .Kwa wale mtakaoweza kufika karibuni sana kuungana nasi katika kumpumzisha mzee wetu.” Akamaliza Andrew halafu akachukua bahasha na kumkabidhi muongoza shughuli kisha yeye na Savanna wakashuka jukwaani.Katika sehemu waliyokuwa wamekaa familia ya Vero,Loniki dada mkubwa wa Vero alikuwa amefura kwa hasira wakati Andrew akitoa salamu zile za rambi rambi.Sarah aliyekuwa amekaa pembeni yake alimtuliza na kumuomba asifanye jambo lolote la aibu mbele ya umati ule mkubwa wa watu.
Zoezi la kuuaga mwili wa marehemu likaanza na kuchukua muda mrefu zaidi ya ilivyokuwa imetazamiwa kutokana na umati mkubwa wa watu.Baada ya zoezi kukamilika ,waombolezaji wakapata chakula kisha ukaanza utaratibu wa kuelekea kanisani kwa ajili ya ibada.Magari yakapangwa vizuri na kisha jeneza lenye mwili wa Vero likatolewa ndani na kuingiza katika gari maalum na safari ya kuelekea kanisani ikaanza.Vilio viliendelea kusikika toka kwa akina mama waliokuwa wakilipungia mkono jeneza lenye mwili wa Vero wakati likiondolewa kwani ilikuwa ni mara yao ya mwisho kumuona tena mpendwa wao.Watu waliingia katika magari na safari ya kuelekea kanisani ikaanza.Ulikuwa msururu mrefu wa magari na wengine ambao hawakutaka kupanda magari walikuwa wakitembea kwa miguu kwa sababu kanisa halikuwa mbali na makazi ya akina Vero.
Hata kabla ya kuwasili kwa mwili wa marehemu kanisani,tayari kanisa lilikwisha jaa watu.Hii ilionyesha ni jinsi gani kifo cha Vero kilivyowagusa watu wengi.
Jeneza likashushwa garini na kuingizwa kanisani na kabla ya kuanza kwa ibada ikatolewa tena nafasi nyingine ya kutoa heshima za mwisho kwa wale ambao hawakuipata nafasi hiyo nyumbani.Zoezi hili lililazimika kusitishwa kutokana na idadi kubwa ya watu hivyo .Ibada ilichukua takribani saa moja halafu safari ya kuelekea makaburini kwa ajili ya kuhitimisha safari ya mwisho ya Vero ikaanza.Saa kumi za jioni waliwasili makaburini na ikafanyika ibada ya makaburini na taratibu mwili wa Vero ukashushwa kaburini.Lilikuwa ni tukio lililowafanya watu wengi wapoteze fahamu.Miongoni mwa watu waliopoteza fahamu alikuwa ni Loniki.Hii ilikuwa ni mara ya tatu katika siku hii kupoteza fahamu.Kifo hiki cha Vero kilikuwa kimemuumiza mno.
Familia na watu wa karibu wa marehemu wakatupa udongo kaburini na kisha likaanza zoezi la kulifunika kaburi.Baada ya zoezi lile lililofanywa na mafundi mahiri kukamilika ,yakawekwa mashada ya maua halafu Padre akalibariki kaburi na kisha watu wakatawanyika na kurejea msibani kwa ajili ya kuendelea na taratibu nyingine.Safari ya Vero duniani ikafikia mwisho.
“Andrew ninaondoka ,ninahitaji kuonana na Happy jioni hii” akasema Savanna muda mfupi tu baada ya kurejea nyumbani kwa akina Patrick wakitokea katika mazishi ya Vero
“Sawa Savanna.Tutaonana kesho.Patrick anafahamu kama baba yake anazikwa kesho?
“Sina hakika kama anafahamu ,lakini nitamfahamisha nitakapomtembelea kesho asubuhi.”
“Ukionana naye kesho mpe salamu zangu nyingi.Nitakwenda kumtembelea baada ya kumalizika kwa shughuli hizi za msiba wa mzee” akasema Andrew kisha Savanna akaingia garini na kuondoka kuelekea nyumbani kwa akina Happy.
“Kwa kweli hata mimi niliumia sana katika mazishi ya Vero.She was so pretty.Maskini Vero,amekufa na uzuri wake.Happy alistahili adhabu kwa kosa alilolifanya.Sielewi ni kwa nini Patrick ameamua kujitwisha yeye mzigo huu mzito ambao hakuustahili” akawaza Savanna akiwa njiani kuelekea kwa akina Happy
“Hata hivyo nitamsaidia Patrick kwa kila namna nitakavyoweza na atashinda hii kesi.Ninayafanya haya yote kwa sababu ya upendo wangu kwake.Ninampenda sana Patrick.Toka tulipoamua kusitisha mahusiano yetu baada ya mimi kumpata George ,bado sijaweza kabisa kumtoa Patrick moyoni mwangu.Hii ni nafasi yangu ya kumrudisha tena Patrick kwangu.Nitashinda hii kesi na Patrick lazima awe wangu tena.Happy hastahili kuwa na Patrick tena.” Akaendelea kuwaza Savanna.
Jua tayari lilikwisha punguza nuru yake kuashiria kwamba muda wowote litazama kulipisha giza lichukue nafasi yake.Savanna akafika nyumbani kwa akina Happy akafunguliwa geti na kuingia ndani.Akapokewa na mtumishi wa ndani
“Happy nimemkuta? Akauliza Savanna
“Ndiyo umemkuta.Karibu ndani ngoja nikamuite” akasema Yule msichana na kuelekea chumbani kwa Happy akamtaarifu kwamba Savanna amekwisha fika.Happy akatoka chumbani kwake na kuelekea sebuleni
“Karibu sana Savanna.” Akasema Happy huku akitabasamu
“Nashukuru sana Happy.Unaendeleaje?
“Ninaendelea vizuri Savanna.Namshukuru Mungu kwani ninazidi kupata nguvu kila siku”
“Nafurahi kusikia hivyo Happy.Ni jambo la faraja sana kuona hali yako inaboreka siku hadi siku” akasema Savanna.Kikapita kimya kifupi halafu Savanna akasema
“Happy ,nilisikia kwamba umelivua taji la Miss Tanzania..”
“Ndiyo Savanna.Niliamua kulivua taji lile ili kuendelea kulipa heshima yake kwa sababu kila neno baya lilikuwa linasemwa kwa kutanguliwa na miss Tanzania badala ya Happy.Nilifikiria na kuona haitakuwa busara kama taji la miss Tanzania likaendelea kuchafuliwa. Nikaona ni bora nilivue.”
“Pole Happy.Haya yalikuwa ni maamuzi magumu sana”
“Nimekwisha poa Savanna.Sikuwa na njia nyingine ya kufanya zaidi ya kulirudisha taji lile.” Akasema Happy
“Nimetoka katika mazishi ya Vero.Mimi na Andrew tuliiwakilisha familia ya Patrick katika mazishi.” Akasema Savanna.Happy hakujibu kitu akainama chini
“Happy nimepita mara moja kukuona kama ulivyokuwa umeomba.” Akasema Savanna ,Happy akainua kichwa.
“Samahani Savanna kwa kukusumbua.Ni kweli nilihitaji kuonana nawe kwa maongezi ya muhimu”
Akasema Happy
“Nakusikiliza Happy” akajibu Savanna.Happy akainama kidogo akafikiri na kusema
“Leo nimekwenda kuonana na Patrick gerezani.Tumeongea japo si kwa muda mrefu .Nilijaribu kumuuliza kuhusiana na maendeleo ya kesi na akanitoa wasi wasi na kusema kwamba mambo yote kuhusiana na kesi hii ameyaacha mikononi mwako.Amenihakikishia kwamba wewe ni wakili mahiri na kesi kama hii haiwezi kukusumbua hata kidogo.Kuna kitu aliniambia vile vile kilichonistua kidogo eti kwamba umekataa malipo yoyote na kwamba unaifanya kazi hii bure kabisa.Ni kweli?
Savanna akatabasamu kidogo na kusema
“Ni kweli Happy.Mimi ndiye ninayeisimamia kesi ya Patrick nikishirikiana na mawakili wazoefu toka katika kampuni yangu ya uwakili.Kuhusu malipo ni kweli kama alivyokwambia Patrick.Sihitaji kulipwa hata senti moja.Nimejitolea kuifanya kazi hii bure kwa sababu Patrick ni rafiki yangu mkubwa na wa siku nyingi.Kuna tatizo lolote katika suala hilo? Akauliza Savanna
“Hakuna tatizo Savanna.Nilihitaji tu kupata uhakika toka kwako kwa sababu haikuniingia akilini mtu kusitisha shughuli zake nyingine na kuisimamia kesi hii ngumu bila kuhitaji kulipwa hata shilingi moja.Labda naomba niwe wazi kwako Savanna kwamba moyo wangu hauna amani hata kidogo nikimuona Patrick gerezani.Ninataka kufanya kila linalowezekana ili Patrick ashinde kesi na atoke gerezani na ndiyo maana ninahitaji kuwa na uhakika kuhusiana na mtu anayeisimamia kesi yake.Kwa maana hiyo Savanna kama kuna kiasi chochote cha pesa ambacho ungependa kulipwa usisite kuniambia na nitakupatia.” Akasema Happy.Savanna akacheka kidogo halafu akamtazama Happy na kusema
“Happy mimi na wewe tumekutana na kufahamiana hivi karibuni baada ya kutokea tukio hili hata hivyo nadhani bado haujanifahamu vizuri.Mimi na Patrick tumekutana miaka mingi iliyopita,na tunafahamiana vyema. Sipendi kujisifu lakini mimi ni wakili mwenye uwezo mkubwa wa kusimamia kesi kubwa na karibu katika kesi zote ambazo tumewahi kusimamia mimi na kampuni yangu hatujawahi kushindwa.Ni kutokana na umahiri huo katika sheria nimeweza kukusaidia hata wewe kuondokana na kesi hii inayomkabili Patrick ambayo ulistahili uibebe wewe.Patrick ananifahamu vizuri na ndiyo maana hakusita kuiweka hatima ya kesi yake mikononi mwangu.Kuhusu malipo bado narudia tena kwamba sihitaji chochote.Ninafanya kazi hii kwa moyo kumsaidia rafiki yangu na si kwa ajili ya kutengeneza fedha.Ninazo pesa za kutosha na hata nikikwambia unilipe kama unavyotaka ,can you afford to pay me 100 millions? Akauliza Savanna akionyesha wazi kukerwa na maneno yale ya Happy.Happy akainama chini.
“Can you pay me 100 milions Happy? Akauliza tena Savanna
“Savanna samahani kama nimekuudhi ,lakini halikuwa kusudio langu kufanya hivyo.Lengo langu nilitaka niwe na uhakika kuhusu utetezi wa Patrick.” Akasema Happy
“One more thing.Who are you Happy? Akauliza Savanna huku sauti yake ikionyesha kuanza kubadilika.Happy akakaa kimya
“You are not even a member of Patrick’s family,….!!” Akasema Savanna.
“Savanna samahani kama kwa kukuuliza vile nimekukera.Niliuliza kwa lengo zuri tu” akajibu Happy
“Happy nimeshangazwa sana na namna ulivyoonyesha wasi wasi kwangu.Umesahau kwamba mimi ndiye niliyesababisha wewe uwe huru mpaka wakati huu na Patrick awe gerezani.” Akasema Savanna halafu akakaa kimya akamtazama Happy
“Kesho asubuhi,nitakwenda kumtembelea Patrick na nitamwambia kwamba najitoa katika kesi hii kwa sababu umeonyesha kutokuniamini nadhani litakuwa jambo la busara kama utaitumia nafasi hiyo kumuweka wakili unayemtaka wewe ambaye atafanya kazi hii kwa malipo tofauti na mimi ambaye sihitaji hata senti moja” akasema Savanna
“Savanna nakuomba usifanye hivyo.Usimweleze chochote Patrick.Atazidi kuumia.Nakuomba sana Savanna usimwambie Patrick chochote.” Akasema Happy
“Happy ahsante sana.Mimi naondoka.Kumbe umenipotezea muda wangu mwingi kwa kuja kunieleza mambo kama haya.!!!! Akasema Savanna huku akiinuka na kutoka mle sebuleni.Happy alikuwa ameinamisha kichwa.
“Bastard !!!..” akasema Savanna kwa hasira baada ya kuingia katika gari lake.
“Sijawahi kudharauliwa hata siku moja kuhusiana na kazi yangu na sipendi mtu aidharau taaluma yangu.Sikuwa nimetaka kukasirika lakini Happy amenikasirisha sana.Yeye ni nani hata anifanyie mahojiano na kuhoji uwezo wangu? akawaza Savanna.
“I will destroy you Happy.nitahakikisha Patrick humpati tena” Akawaza Savanna.
* * *
Baada ya kurejea nyumbani toka katika mazishi ya Vero Loniki hakutaka tena kuongea wala konana na mtu yeyote .Akajifungia chumbani kwake.
“Siyo ndoto tena kama nilivyokuwa nadhani.Ni kweli Vero amekwenda na sintamuona tena.Nilimpenda kupita kiasi na hii ni sababu inayonifaya niumie kiasi hiki.Vero amekufa , amekwenda na uzuri wake.Sintampata tena ndugu kama yeye.Patrick ameniondolea furaha ya maisha yangu na kwa hili sintamsamehe hadi siku naingia kaburini na lazima nihakikishe nimemlipia kisasi mdogo wangu.Kitendo alichofanyiwa na Yule shetani si cha kibinadamu na hakivumiliki hata kidogo na ninaapa kwa miungu yote kwamba lazima yeye na wale wote walioshiriki kumuua ndugu yangu wanalipa.Damu ya Vero haiwezi kupotea bure.They must pay ..!!!!!” akasema kwa hasira Loniki huku akigonganisha mikono yake.Akainuka kitandani akaendea kabatini akachukua pakiti la sigara akachomoa moja na kuanza kuvuta huku akipuliza moshi mwingi hewani.
“Sarah naye lazima atanieleza ni kwa nini kila mara amekuwa mtetezi mkubwa wa Patrick. Hata amediriki kuwaalika watu wake msibani.Anaonekana hana uchungu wowote na kifo cha Vero.Lazima naye nipambane naye.Zile fedha zilizotoka kwa akina Patrick nazo lazima zirudi zilikotoka .Itakuwa ni dhihaka kubwa kuzikubali pesa zilizotoka kwa watu waliomuua ndugu yetu.Sintakubali kamwe fedha zile ziendelee kukaa mikononi mwetu.Kama hawatazirejesha zilikotoka nitazirejesha mimi.” Akawaza Loniki huku akiendelea kuvuta sigara kwa fujo.
“Sintarejea London hadi nihakikishe wale wote walioshiriki katika kumuua Vero wamelipa uovu wao.Lazima walipe.Siihitaji hiyo haki ya mahakama,nitaitafuta haki kwa namna ninayojua mimi mwenyewe.” Akawaza Loniki huku akiendelea kupuliza moshi mwingi wa sigara hewani. Akafungua mlango na kutoka mle chumbani akamtafuta shangazi yake
“Shangazi naomba simu yako kuna mtu nahitaji kuwasiliana naye” akasema Loniki na shangazi yake akampa simu Loniki akarejea chumbani kwake akuchukua kitabu ambacho huandika kumbu kumbu zake mbali mbali akautafuta ukurasa ambao ameandika namba mbali mbali za simu akazipata namba alizokuwa anazitafuta akaziandika katika simu na kupiga
“Hallow Linah,Loniki hapa naongea” akasema Loniki baada ya simu kupokelewa.
“wow ! Loniki.!!....ni wewe kweli? Siamini .Umekuja lini shoga yangu.Na mbona umerudi kimya kimya? Akauliza Linah
“ Linah ina maana hujasikia matatizo yaliyonipata?
“Matatizo !!!.Linah akashangaaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ Ndiyo Linah.Ina maana huna taarifa zozote?
“Mbona unanistua Lonny? Mimi sina taarifa zozote kwa sababu nimerudi mchana wa leo toka Nairobi kuna mizigo yangu ilikwama pale kwa hiyo sifahamu chochote na wala sijajua kama umerudi.Nini kimetokea Lonny?
“Linah nilipatwa na msiba mzito”
“Msiba !!! Linah akastuka
“Pole sana Lonny.Nani kafariki?
“Vero amefariki dunia !
“Vero !? ..Vero huyu mdogo wako?
“Ndiyo.”
“Acha masihara Lonny.”
“Si masihara Linah.Ni kweli Vero amefariki dunia na ni kifo ambacho kimetangazwa sana na nchi nzima wanajua kama Vero amefariki dunia na jioni ya leo tumetoka kumzika katika makaburi ya Kinondoni.”
Kimya kifupi kikapita.Linah akavuta pumzi ndefu na kusema
“Loniki umenistua sana .Bado siamini kama uliyonieleza ni ya kweli”
“Sikudanganyi Linah.Ni kweli kabisa Vero amefariki dunia.Vero hatunaye tena.”
“Ouh my Gosh !!!”
“pole sana Lonny.Kwa kweli ni msiba mzito sana na wala sina taarifa zozote.Loniki nitajitahidi nifike hapo nyumbani kesho asubuhi kwa sababu kwa sasa niko mbali kidogo ”
“Nitashukuru sana kama ukifika Linah ninahitaji sana kukuona.Nina maongezi nawe ya muhimu sana”
“Usijali Lonny nitafika hiyo kesho bila kukosa.Mpe pole sana mama na Sarah”
“Ahsante sana Linah ,tutaonana hiyo kesho” akasema Loniki na kukata simu,akachukua sigara nyingine katika pakiti na kuiwasha akaendelea kuvuta
Kumepambazuka Dare es salaam siku mpya imeanza.Pilika pilika katika jiji hili kubwa la kiuchumi nchini Tanzania ziliendelea kama kawaida.Saa tatu za asubuhi ilimkuta Savanna katika gereza la uwangwa kwa ajili ya kuonana na Patrick.Aliwahi sana kufika siku hii ya leo.Kutokana na kufahamika kwake hupewa nafasi ya kuongea na mteja wake katika chumba maalum tofauti na watu wengine ambao hukutana na mahabusu katika sehemu yenye uwazi.
Dakika nane toka aingie mle chumbani mlango ukafunguliwa na Patrick akaingia.
“Hallo Patrick “ akasema Savanna
“mambo vipi Savanna? Akajibu Patrick huku akitabasamu
“Mambo poa Patrick.Unaendeleaje?
“Ninaendelea vizuri Savanna.Ahsante sana kwa msaada wako kwani ninapata huduma nzuri hapa gerezani tofauti na mahabusu wengine.Vipi wewe unaendeleaje?
“Mimi pia niko salama Patrick.Nafurahi kama unapatiwa huduma nzuri.Unajua mkuu wa gereza ni rafiki yangu sana na hata viongozi wengi wa gereza hili ninafahamiana nao kwa hiyo ninafurahi kama ombi langu kwao la kuwaomba wakupatie huduma nzuri linatekelezwa” akasema Savanna kikapita kimya kifupi
“Patrick.Unajisikiaje leo?
“Ninajisikia vizuri sana Savanna.Nipe habari za huko duniani” akasema Patrick na kumfanya Savanna acheke kidogo
“Jana tumemzika Veronika.Amezikwa katika makaburi ya Kinondoni.Watu walikuwa wengi mno.” Akasema Savanna halafu Patrick akainama chini.Baada ya sekunde kadhaa Savanna akasema
“Mimi na Andrew tulikuwakilisha wewe na familia nzima katika mazishi hayo ikiwa ni pamoja na kupeleka salamu za rambi rambi kwa niaba ya familia.Tulipewa nafasi ya kusema machache na Andrew akaongea machache.Alitoa salamu za pole kwa niaba yako.”
“Ndugu wa Vero mlifanikiwa kuonana nao?
“Tulionana na Sarah ambaye ndiye amekuwa akitupa ushirikiano mkubwa na alifika hadi nyumbani kwenu kumpa mama pole kwa msiba wa baba.Dada mkubwa wa Vero amekuwa mgumu sana na juzi aliwafukuza Andrew na wazee wengine walipokwenda kushiriki msiba” akasema Savanna
“Please forgive me Vero.I didn’t mean to cause your death” akasema Patrick huku ameinamisha kichwa.
“Patrick leo tunamzika baba .Nasikitika kwamba hutaweza kuhudhuria lakini usijali kwani nitakuwepo kukuwakilisha” akasema Savanna na kukaa kimya akamtazama Patrick.
“Nashukuru sana Savanna kwa taarifa.Hakuna mtu mwingine yeyote ambaye amekuja kunitembelea na kunipa taarifa kuhusiana na na kinachoendelea huko nyumbani.Bila wewe nisingefahamu chochote kuhusu mazishi ya Vero wala baba yangu.” Akasema Patrick kwa masikitiko.
“Patrick,familia yako wala ndugu zako hawajakutenga wala kukutelekeza.Wameshindwa kufika kukutazama kwa sababu wako katika majonzi makubwa hivi sasa.Baada ya kumaliza shughuli za msiba wa baba nina imani watakuwa wakifika hapa mara kwa mara kukujulia hali.” Akasema Savanna
“Anyway,I deserve to be treated this way” akasema Patrick
“Patrick we’re here for you.I’ll always be here for you.Anytime you need a friend,or a shoulder to cry on ,I’ll be here .Maumivu yako ni yangu na ndiyo maana ninakuahidi kufanya kila ninachoweza ili kuhakikisha kwamba unashinda kesi hii.Tafadhali usijihisi mpweke Patrick”
“Nashukuru sana Savanna.Toka nimepatwa na matatizo haya umekuwa ni mtu pekee ambaye uko nami kila siku.Wewe ndiye mfariji wangu .Sina cha kukulipa Savanna kwa wema huu wote ulionitendea.Mungu atakulipa.” Akasema Patrick
“Patrick ninayafanya haya yote kwa sababu wewe ni rafiki yangu na mtu wangu wa muhimu sana.Halafu kuna kitu nimekumbuka Patrick”
“Kitu gani Savanna?
“Jana nilikwenda kuonana na Happy baada ya kutoka katika mazishi ya Vero.Alinipigia simu na kunitaka nionane naye kuna jambo anataka kunieleza.Nilishangazwa sana na Happy kuonyesha wasi wasi wa mimi kuisimamia kesi yako.Anaonekana hana uhakika kama ninaweza kuisimamia kesi hii hadi mwisho.Anyway sitaki kuliongelea sana suala hili nilitaka tu ufahamu na umwambie kwamba awe mkimya na awe mfuatiliaji mzuri wa kesi na si mtoa maamuzi.” Akasema Savanna.Patrick akamtazama na kusema
“Savanna ,samahani sana kama kuna maneno yoyote aliyoyatamka Happy yakakuudhi kiasi hicho.Ni kweli jana alifika hapa na aliniuliza kuhusu mwenendo wa kesi nikamwambia kwamba mambo yote kuhusiana na kesi nimeyaacha mikononi mwako.Sikutegemea kama angekutafuta na kukuuliza kuhusu suala hili.Savanna wewe ni zaidi ya rafiki,naomba usimsikilize Happy kwa lolote.Tafadhali nakuomba usiache kunisaidia katika kesi hii.Without you I’m finished.I need you now more than ever” akasema Patrick.Savanna akaishika mikono ya Patrick.
“Patrick hakuna binadamu yeyote katika hii dunia ambaye anaweza kunizuia mimi nisikutetee katika hii kesi.I’ll get you out of here .I’ll make sure you are free.Believe me” akasema Savanna.
“Ninakuamini Savanna.” Akajibu Patrick.
“Ahsante sana Patrick.Kilichonileta hapa siku hii ya leo ni kukujulia hali na kukupa taarifa za kinachoendelea nyumbani.Nitakuja tena kesho” akasema Savanna.
“Savanna nakushukuru kwa kuja kunitembelea na kunipa taarifa za mazishi ya baba na Vero.Naomba usiache kuja kunitembelea kwani wewe ndiye mfariji wangu mkuu kwa sasa” akasema Patrick.
“Usijali Patrick,hapa ni kama nyumbani na nitakuwa nikija kila siku kujua maendeleo yako.Sintaacha kukutembelea hadi siku nitakayohakikisha kwamba umekuwa huru” akasema Savanna akaagana na Patrick na kuondoka
“Ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kumrejesha Patrick katika mikono yangu lazima kuifuta taswira ya Happy katika akili ya Patrick.Lazima niichafue picha nzuri ya Happy kichwani mwa Patrick na hapo ndipo nitakapokuwa na uhakika kwamba ninaweza kumpata Patrick tena.Najua si rahisi lakini ninatakiwa kufanya kitu kimoja tu.I have to make him hate her” akawaza Savanna na kutabasamu.
* * * *
Saa mbili na dakika ishirini za asubuhi , gari moja dogo la kifahari likawasili nyumbani kwa akina Vero na akashuka mwanamke mmoja aliyekuwa amevaa gauni refu jeusi na kichwani alijitanda mtandio mweusi na kuvaa miwani mikubwa myeusi kiasi kwamba ilikuwa vigumu kumtambua kwa haraka.Huyu alikuwa ni Linah rafiki mkubwa wa Loniki.Mara tu aliposhuka katika gari Loniki akatokea na kukumbatiana naye.Linah akashindwa kujizuia akaanza kuangua kilio kikubwa.na kumfanya Loniki naye aanze kulia.
Baada ya kulia kwa takribani dakika kumi,Loniki na Yule mwanadada ambaye ni rafiki yake kipenzi na wa siku nyingi wakanyamza kisha Linah akaitumia nafasi hiyo kuwapa pole ndugu jamaa na marafiki waliokusanyika hapo nyumbani wakiendelea na matanga.Kisha toa mkono wa pole,Loniki na Linah wakaelekea bustanini.Loniki akamuacha Linah pale bustanini ,akarejea chumbani kwake na kuchukua chupa ya mvinyo pamoja na glasi mbili bila kusahau pakiti yake ya sigara .Akarejea bustanini alikomuacha Linah na kumimina mvinyo katika glasi ,akawasha sigara na kupuliza moshi mwingi hewani.
“Bado hujaacha kuvuta sigara Lonny? Akauliza Linah.Loniki akapuliza tena moshi mwingi hewani na kusema.
“Siwezi kuacha kuvuta sigara Linah.Nimeanza kuvuta sigara nikiwa shule ya msingi na siwezi kuacha sasa hivi.Vipi wewe huvuti tena?
“Hapana Lonny,niliacha kuvuta sigara muda mrefu .nilipatwa na tatizo la kifua nikashauriwa kuachana na sigara.” Akasema Linah halafu kikapita kimya kifupi.Loniki bado aliendelea kunywa mvinyo na kuvuta sigara
“Lonny pole sana shoga yangu kwa msiba huu mkubwa.Bado siamini kama ni kweli Vero amefariki dunia.Usiku kucha nilikuwa nikitafakari kuhusu suala hili kama ni kweli au ulikuwa unanitania.Hapa nilipo mwili unanitetemeka sana,nimestuka mno” akasema Linah
“Ni vigumu kuamini Linah lakini ukweli ni kwamba Vero hatunaye tena.Jana tumempumzisha katika nyumba yake ya milele.Hata mimi bado inaniwia ugumu kuamini kwamba sintamuona tena Vero.Tabasamu lake ,ukarimu na ucheshi wake hatutaviona tena.Inauma sana Linah.Inauma sana” akasema Loniki huku akilengwa na machozi.Akachukua glasi yake ya mvinyo na kupiga funda kubwa halafu akawasha sigara nyingine.Linah ambaye naye alikuwa anafuta machozi akamtazama shoga yake na kusema
“Lakini Lonny hebu nieleze kifo cha Vero kimesababishwa na nini? Alikuwa anaumwa? Nakumbuka mara ya mwisho kuonana naye ni wiki tatu zilizopita.Nilimuomba afike dukani kwangu ili kuchukua mchango wa harusi kwa sababu nilikuwa na safari ya kwenda Dubai.Alifika dukani kwangu nikaonana naye na kumpatia mchango na akaniahidi kuniletea kadi ya harusi.Taarifa za kifo chake cha ghafla zimenistua sana” akasema LInah
“Linah dunia hii imejaa watu makatili hakuna mfano.Wamemkatili uhai mdogo wangu.Vero hakupaswa kufa mapema namna hii.” Akasema Loniki
“Ina maana Vero ameuawa? Nani hao wamefanya kitendo hicho cha kinyama?
“Ilikuwa ni siku ya pili toka aliporejea nchini akitokea London alikokuja kufanya manunuzi ya harusi yake.Kwa mujibu wa maelezo niliyopewa ni kwamba aliporejea toka London alikwenda kumtembelea mchumba wake na kushinda huko na baadae jioni wakaelekea nyumbani kwa wazazi wa Patrick kulikokuwa na kikao.Baada ya kufika huko kikaoni Patrick akasimama na kuanza kueleza mambo ambayo ni upuuzi mtupu na baadae akatangaza kwamba ameuvunja uchumba kati yake na Vero.” Akasema Loniki
“What .!!!! Linah akashangaa
“Usistuke Linah.Dunia hii imejaa watu makatili mno.Baada ya tangazo hilo la kuuvunja uchumba,watu wengi walianguka na kupoteza fahamu.Kwa mujibu wa mashuhuda ,baada ya kitendo kile Vero alipotea na haikujulikana alikwenda wapi.Baba mzazi wa Patrick ambaye naye amefariki dunia jana alikimbizwa hospitali kwa shinikizo la damu.Wakiwa hospitali walikompeleka baba yao,Patrick na kahaba wake ambaye inasemekana ndiye chanzo cha kuachana na Vero walishangaa kumuona Vero ametokea ghafla akiwa na bastora.Ulitokea ugomvi na Patrick akataka kumnyang’anya Vero bastora na aliposhindwa akaamua kumsukuma Vero akajigonga ukutani na kupoteza maisha.Wamemuua mdogo wangu ,wamemfanyia ukatili mkubwa” akasema Loniki.Linah akavuta pumzi ndefu
“Pole sana Lonny .Kwa kweli ni jambo la kuhuzunisha sana.Siamini kama ni kweli Patrick amemfanyia hivi Vero.Ni kwa nini amefanya hivi?
“Ni kwa sababu alimpata mwanamke mrembo ambaye ni miss Tanzania,akamuona Vero hafai tena.”
“Yaani Patrick aliamua kumuacha Vero kwa sababu ya Miss Tanzania? Akauliza Linah
“Huu ni ukatili mkubwa na hauvumiliki hata kidogo.” Akasema Linah kwa hasira
“Ni ukatili mkubwa sana Linah.Vero amekufa na uzuri wake.Hakuwa hata na mchubuko.” Akasema Loniki
“Patrick yuko wapi? Amekwisha kamatwa? Akauliza Linah
“Anashikiliwa na jeshi la polisi.Tayari kesi yake imekwisha tajwa mahakamani.” Akajibu Loniki
“Afadhali kama amekamatwa.Haki itatendeka kwani siku hizi mahamaka zimeboreshwa na mashauri yanaharakishwa sana.lazima ahukumiwe kutokana na kosa alilolitenda.Anastahili kifungo kirefu gerezani au ikiwezekana hata kifo” akasema Linah
“No Linah.!!....mimi sihitaji hiyo haki ya mahakama.Sina huo muda wa kusubiri haki itendeke baada ya miaka miwili.Isitoshe siviamini vyombo vya kutoa haki.Ni watu wangapi wametenda makosa makubwa na hata mauaji lakini bado tunawaona mtaani? Hakuna awezaye kuufahamu uchungu nilinao moyoni mwangu” akasema Lonny
“Kwa hiyo umepanga kufanya nini Lonny?
“Ndiyo maana nimekuita Linah.Kuna mambo nataka unisaidie”
“Sema chochote Lonny.Mimi niko tayari kukusaidia.” Akasema Linah.Lonny akanywa funda moja la mvinyo na kusema
“Linah nataka kutafuta haki kwa namna ninayojua mimi mwenyewe.Nataka wale wote waliohusika kwa namna yoyote ile na kifo cha mdogo wangu Vero walipe uovu wao kabla mdogo wangu hajaoza kaburini.They all must pay” akasema Loniki halafu akatoa sigara nyingine na kuiwasha akavuta na kumgeukia Linah
“Linah wewe ni rafiki yangu mkubwa toka shule ya msingi na hadi leo hii umeendelea kuwa mshirika wangu wa karibu.Nina imani utakuwa nami katika hili ninalotaka kulifanya kwani naamini hata wewe ulimpenda Vero kama mdogo wako pia” akasema LonikiCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Lonny wewe ni zaidi ya rafiki.Niko nawe katika kila jambo.Vero alikuwa ni mdogo wetu sote na kifo chake kimeniumiza sana kama kilivyokuumiza wewe.Niambie umefikiria kufanya nini?
“kama nilivyokueleza Linah kwamba ninataka kuitafuta haki mimi mwenyewe.Nataka unisaidie kutafuta mtu ambaye ataifanya kazi ya kulipa kisasi kwa wale wote waliohusika na kifo cha Vero.Wa kwanza kushughulika naye ni huyu msichana miss Tanzania ambaye ndiye chanzo cha Patrick kumuacha mdogo wangu na ndipo nimgeukie Patrick.” Akasema Lonny
Linah akavuta pumzi ndefu,akachukua glasi ya mvinyo akanywa kidogo halafu akasema
“Unataka huyu Happy ashughulikiwe vipi?
“Ninataka kwanza ateseke sana kabla ya kumuondoa katika uso huu wa dunia.”
“Unaposema kumuondoa duniani unamaanisha kumuua ? akauliza Linah
“Exactly..!!!!!Ninataka baada ya kupatwa na mateso makali hatimaye auawe halafu Patrick afuate.wakisha uawa watu hawa ndipo roho yangu itakapotulia.Kwa vile wao pia waliutoa uhai wa Vero basi nao hawana budi kutolewa uhai wao.Je tuko pamoja katika hili? Akauliza Loniki
“Tuko pamoja Lonny.Siwezi kukuacha katika suala hili japokuwa si suala rahisi na linahitaji umakini mkubwa sana.”
“nalifahamu hilo Linah na ndiyo maana nimekuita ili tuongee na kuweka mikakati mizito.Nina hakika suala hili haliwezi kutushinda hata kidogo.Nimekwisha weka nia ya dhati ya kuhakikisha kwamba hawa wote waliohusika na kifo cha Vero wanalipa. Damu ya mdogo wangu haiwezi kupotea bure.Lazima nimlipie kisasi” akasema Loniki
“Lonny utakuwepo hapa nchini kwa muda gani? Akuliza Linah
“Sintaondoka hapa hadi nitakapohakikisha kwamba Patrick na Happy wamelipa uovu wao”
“Basi itakuwa vyema kama utaendelea kuwepo nchini kwa muda mrefu zaidi”
“Ndiyo Linah nitakuwepo hapa nchini kwa muda mrefu tu.Ninachokihitaji ni mtu wa kuweza kuifanya kazi hii kwa umakini mkubwa na ufanisi.Ni kazi ambayo haihitaji aina yoyote ya makosa.Ninajua unafahamiana na watu wengi wa hapa mjini ambao wanaweza kuifanya kazi hii.”
“Usijali Lonny kuhusu hilo.Mimi nitalifanyia kazi hilo suala na ……………….” Kabla hajendelea zaidi mara akatokea shangazi yake Loniki.Mama huyu amekuwa rafiki mkubwa wa Loniki na amekuwa akimuunga mkono katika kila jambo ambalo Lonny analifanya.Hii imepelekea awe akipokea misaada mingi toka kwa Loniki.
“Loniki kikao cha ndugu kinataka kuanza,unaombwa uwe karibu..”
“Sawa shangazi.Ninakuja sasa hivi” akasema Loniki
“Linah twende katika kikao” akasema Loniki
“Hapana Lonny.Kikao hicho kinawahusu wanandugu pekee”
“Toka lini umeacha kuwa ndugu yangu Linah ?Twende tukahudhurie kikao halafu tutaendelea na maongezi yetu”akasema Loniki halafu wakainuka na kuelekea kikaoni.
Karibu ndugu wote walikuwa wamejikusanya kwa ajili ya kikao cha kuhitimisha shughuli za msiba na kutoa ruhusa kwa watu waliotoka mbali kuondoka.Ni mtu mmoja tu ambaye alikosekana katika kikao hiki.Ni sarah.Akatumwa mtu mmoja kwenda kumtafuta nyumba nzima lakini hakuwepo na hata gari lake halikuwepo.Shangazi yake akajaribu kumpigia simu lakini simu ilikuwa inaita bila kupokelewa.
“Simu yake inaita bila kupokelewa” akasema
“hakuna haja ya kumsubiri.Tuendeleeni na kikao” akaamuru Loniki na wote wakakubaliana naye kikao kikaanza
“Najua mahali alikoelekea Sarah.Huyu naye lazima nipambane naye.Ngoja kwanza tumalize msiba nitamfundisha adabu ” akawaza Loniki wakati kikao kikiendelea.
Sarah akiwa garini simu yake iliita akaichukua na kutazama mpigaji.Alikuwa ni shangazi yake.Hakupokea akaiweka chini.
“Najua wananitafuta kwa ajili ya hicho kikao chao.Watanisamehe kwani sintahudhuria kikao hicho.Lazima nihudhurie mazishi ya baba yake Patrick.Nataka upendo na amani vidumishwe baina yatu na si kujenga chuki na hasama.Nawashangaa sana ndugu zangu kwa kumuunga mkono Loniki kwa kila atakachokisema hata kama hakina msingi wowote.Kwa sasa karibu wote wanamuunga mkono kuhusu kulipa kisasi wa Patrick .Nafikiri ni kwa sababu anaishi ulaya na misaada anayowatumia mara kwa mara imewafanya wamsikilize na kumfuata kwa kila jambo atakaloliongea na kumfanya awe ni mtu mwenye sauti katika familia na ukoo .Mimi sintakubaliana kwa namna yoyote ile na upuuzi ambao Loniki anaufanya.Vero alikuwa ni ndugu yetu sote na sote tumeguswa na kifo chake na hapo hapo yatupaswa tukumbuke kwamba hata yeye vero alikuwa na makosa tena makubwa ,na ndiyo chanzo cha haya yote yaliyotokea.Huu ni ukweli ambao hatupaswi kuona haya kuusema.Ninapenda kuona maisha yakiendelea kama awali na sipendi kuona familia zetu zikiingia katika mzozo mwingine.Patrick anashikiliwa na vyombo vya dola na vitafanya uchunguzi na endapo atathibitika kwamba ana makosa basi atapewa adhabu kwa mujibu wa sheria za nchi” akawaza Sarah akiwa njiani kuelekea nyumbani kwa akina Patrick kuhudhuria mazishi ya baba mzazi wa Patrick.
Msafara wa magari ukitokea katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kuuchukua mwili wa baba mzazi wa Patrick ,uliwasili nyumbani kwa marehemu na kulifanya eneo lote ligubikwe na vilio.Wengi wa waombolezaji walikuwa wamevaa fulana zenye picha ya marehemu.Taratibu jeneza likashushwa toka ndani ya gari na kuingizwa ndani .
Taratibu zikafanyika na zoezi la kutoe heshima za mwisho likaanza.Watu walikuwa ni wengi sana na zoezi lilichukua muda mrefu tofauti na ilivyotazamiwa.Baada ya zoezi la kutoa heshima za mwisho kukamilika zikafuata salamu za rambi rambi toka sehemu mbali mbali,zoezi lililotanguliwa na kusomwa kwa wasifu wa marehemu.Salamu nyingi za rambi rambi zilitolewa.Toka serikalini ,watu binafsi,mashirika ya umma n,k.Wengi walionyesha kuguswa na msiba huu .Mzee huyu alikuwa ni kipenzi cha wengi na alikuwa na heshima ya kipekee katika jamii.
Salamu za rambi rambi zikamalizika na hivyo kutoa nafasi kwa ratiba nyingine kuendelea.Mwili wa marehemu ukapakiwa garini na kuelekea kanisani kwa ajili ya ibada.Kanisa lilifurika watu waliokuja kumsindikiza mzee huyu katika safari yake ya mwisho.Ibada iliyoongozwa na msaidizi wa askofu wa jimbo kuu la dare s salaam ambaye alikuwa ni rafiki mkubwa wa mzee huyu ilimalizika na msafara ukaelekea makaburini kwa ajili ya mazishi.Watu walikuwa ni wengi sana
Hatimaye ilipotimu saa kumi za jioni safari ya mwisho ya baba yake Patrick ikahitimishwa pale ambapo jeneza lililobeba mwili wake liliposhushwa kaburini.Baada ya familia,ndugu na wawakilishi wa makundi mbali mbali kutupia mchanga katika kaburi,hatimaye zoezi la kufukia likaanza.
Askofu mkuu msaidizi akalibariki kaburi na huo ukawa mwisho wa shughuli nzima ya mazishi.Waombolezaji walitawanyika na wengine wakarejea nyumbani kwa marehemu ili kuendelea na ratiba nyingine.
* * * *
Saa kumi na mbili za jioni Sarah akawasili nyumbani kwao akitokea katika mazishi ya baba mzazi wa Patrick.Mara tu alipowasili akakutana na dada yake Loniki akiwa amesimama nje ya nyumba akiwa na rafiki yake Linah.
“Linah amekuja lini? Sijamuona kitambo kirefu.Mmmhhh !!! ninaanza kupatwa na wasi wasi.Loniki akikutana na Linah.Ninamfahamu Linah ,sifa yake si nzuri hata kidogo.Imewahi kusikika kwamba anajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya.Si mtu mzuri huyu hata kidogo na kwa namna anavyoonekana akiongea na Loniki ninahisi kuna jambo wanalipanga.Kwa jinsi ninavyomfahamu Loniki najua lazima atataka kumshirikisha Linah katika mipango yake ya kulipiza kisasi.” Akawaza Sarah halafu akashuka garini na kwenda kuwasalimu.
“Sarah …Pole sana jamani .Pole sana kwa msiba.Mimi sikuwa nafahamu chochote hadi Lonny aliponipigia simu na kunifahamisha .Nimeumizwa sana na kifo hiki cha ghafla cha vero” akasema Linah
“Ahsante Linah tumekwisha poa.Ni mapenzi ya Mungu.Habari za siku nyingi?
“Habari nzuri Sarah.Nimekuwa na safari nyingi hivi sasa ndiyo maana hatuonani .”akasema Linah.Loniki ambaye alikuwa amesimama pembeni akasema
“Sarah mbona hukuhudhuria kikao cha wana ndugu? Ulikuwa wapi?
Sarah akamtazama dada yake bila kumjibu kitu halafu akamgeukia Linah.
“Linah nashukuru sana kwa kufika kwako katika msiba huu.Nikipata wasaa nitafika dukani kwako kuangalia bidhaa mpya”
“Unakaribishwa sana Sarah tena kuna mzigo mpya umewasili.”
“Ok Linah nitafika” akasema Sarah halafu akaelekea ndani akawaacha Lonny na Linah wakiendelea na mazungumzo yao
“Kwa hiyo Linah naomba ulipe uzito unaostahili suala hili.Usijali kuhusu pesa.Ukisha wapata watu wanaoweza kuifanya kazi hii naomba unifahamishe mara moja .Yule hayawani anategemea kupandishwa tena kizimbani jumatano ijayo kwa hiyo sitaki mambo haya yachukue muda mrefu”
“Usijali Loniki.Nitajitahidi kuifanya hiyo kazi .kama nilivyokwambia awali kwamba suala hili ninalipa uzito mkubwa sana na ninakuhakikishia kwamba ndani ya muda mfupi nitakuwa nimewapata watu wanaoweza kuifanya kazi hii kwa ufanisi” akasema Linah halafu wakaagana akaondoka.Baada ya kuachana na Linah,Loniki akaelekea moja kwa moja hadi katika chumba ambacho Sarah allikuwa amekaa na mama yake pamoja na akina mama kadhaa,akamuita Sarah na kumuomba wakaongee nje
“Ile ni tabia gani uliyoionyesha mbele ya Linah? Akauliza Loniki
“Tabia gani?
“Nilikuuliza ulikuwa wapi toka asubuhi,hukunijibu kitu na badala yake ukanitazama kwa dharau.”
“Sikuwa na jibu la kukupa kutokana na swali uliloniuliza.Mimi nina masuala yangu na shughuli zangu nyingi tu na anayepaswa kuniuliza swali kama lile ni mume wangu pekee na si mtu mwingine yeyote”
“Kwa maana hiyo hukuona umuhimu wa kuwepo katika kikao cha familia leo? Akauliza Loniki
“Kwani kukosekana kwangu kumeharibu kitu? Au kuwepo kwangu kungebadili kitu? Akasema sarah.Loniki akamuangalia kwa macho makali
“Kuwa makini Sarah na hayo majibu yako yaliyojaa dharau.Mimi ni dada yako na hupaswi kunijibu namna hiyo”
“Si dharau Loniki,ninakueleza ukweli kwa sababu toka umefika hapa umekuwa ndiye mwenye kutoa amri ya kufanyika kila unachopenda.Kwa taarifa yako Loniki ,mimi siko tayari kukunyenyekea eti kutokana na fedha zako au kwa sababu unaishi nje ya nchi.Nina maisha yangu mazuri tu na mume wangu na sihitaji kumsujudu mtu.Kama utaniheshimu nami nitakuheshimu pia lakini kama hutaniheshimu basi hata mimi sintakuheshimu” akasema Sarah.
Loniki akakunja uso na kumuangalia Sarah kwa hasira
“Nasikitika sana Sarah kwa namna ambavyo umeonyesha kutokuguswa na kifo cha mdogo wako.Nafahamu kabisa ulikuwa katika mazishi ya baba yake Patrick mtu ambaye alimuua mdogo wako kwa makusudi kabisa.Huna aibu hata kidogo” akafoka Loniki.
“Ni kweli nimetoka kumzika baba yake Patrick.Mimi sina roho ya kikatili kama uliyonayo wewe.Hakuna mtu anayepaswa kulaumiwa kwa kilichotokea.Hakuna mtu aliyetegemea mambo haya yangefika hapa yalipofika.nafahamu kwamba umedhamiria kulipiza kisasi kwa Patrick,nakuonya usifanye hivyo.Viachie vyombo vya dola vifanye kazi yake.” Akasema Sarah
“ Stupid !!!!!.akasema loniki kwa ukali
“Sarah wewe ni mdogo sana na huna nafasi yoyote ya kunizuia kufanya chochote.Mimi ndiye niliyeguswa na kifo cha Vero,wewe huonyeshi kuguswa hata kidogo.Kwa maana hiyo ninakuhakikishia kwamba sintafumba macho hadi nihakikishe kwamba wale wote waliohusika katika kusababisha kifo cha Vero wamelipa.Hata wewe kama utaamua kuungana na mashetani hawa,nitapambana nawe vile vile.” Akasema Loniki kwa ukali na kuondoka kwa kasi akaelekea ndani.
“Siko tayari kumtukuza Loniki na kumuacha afanye kila anachotaka kukifanya.Japokuwa ni ndugu yangu lakini niko tayari kupambana naye endapo atafanya jambo lolote lisilokuwa zuri kwa Parick,familia yake au Happy” akasema Sarah huku naye akipiga hatua kuingia ndani
* * * *
Ni saa tano za usiku bado Loniki amekaa kitandani.Juu ya meza ndogo iliyo pembeni ya kitanda kulikuwa na chupa ya mvinyo.Chumba kilikuwa kimejaa moshi wa sigara kutokana na kuvuta sigara mfululizo.
“Sarah amenichefua sana siku ya leo.Ninasema nitamuonyesha kwamba mimi ni mkubwa kwake,kiumri ,kifedha na hata kiuwezo.majibu aliyonijibu jioni ya leo yalijaa dharau kubwa sana.Hapana sintakubali kudharauliwa na mtu kama sarah.lazima nim……………………..” akakatisha mawazo yake baada ya mtu kugonga mlango wa chumba chake..Akainuka na kwenda kuufungua.Alikuwa ni shangazi yake.
“Ouh Shangazi karibu “ akasema Loniki
“Ahsante Loniki.Linah amepiga simu na anahitaji kuongea nawe.” Loniki akachukua simu na kuufunga mlango kisha akampigia Linah
“Loniki kuna habari njema nataka kukupa” akasema Linah baada ya kupokea simu.
“Habari gani hizo Linah”
“Tayari nimempata mtu ambaye unamuhitaji kwa ile kazi”
“wow !!..hizo ni habari njema sana.Hebu nipe taarifa zaidi“ akasema Loniki kwa furaha
“Mtu huyo anaitwa Khumalo.Ni mtaalamu na ana uzoefu mkubwa na shughuli hizi.Ni mtu anayeaminika kwa uwezo wake wa kufanya kazi za namna hii.Tayari nimekwisha ongea naye na amenihakikishia kwamba yuko tayari kuifanya kazi hii.Amekataa kutaja kiwango cha pesa anachokihitaji hadi hapo atakapokutana nawe na akapata maelezo ya kina toka kwako.Amenihakikishia kwamba anao uwezo wa kumshughulikia hata mtu ambaye yuko gerezani kutokana na kuwa na mtandao mpana.Kwa hiyo ametaka siku ya kesho tukutane naye ili tuweze kuangalia namna tutakavyoweza kuutekeleza mpango wenyewe” akasema Linah
“Nashukuru sana Linah kwa msaada wako huu mkubwa.Kesho tutaonana muda gani na huyo khumalo?
“Njoo saa nne ofisini kwangu halafu yeye atatuelekeza mahala pa kumkuta.Yeye si mtu wa kuonekana hovyo hovyo”
“Ok Linah.Nitakuja dukani kwako hiyo kesho saa nne” akasema Loniki halafu akaagana na Linah.
“lazima Patrick na Happy walipe damu ya ndugu yangu.Nataka wao pia wapate maumivu kama ninayoyapata mimi hivi sasa.” Akawaza Loniki huku akiuma meno kwa hasira halafu akachukua glasi ya mvinyo akapiga funda kubwa.
* * * *CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ni saa sita na dakika kumi za usiku,siku mpya imekwisha anza.Bado Savanna yuko macho .Licha ya kuhisi macho mazito na kulemewa na usingizi lakini bado alikuwa ameinamia vitabu vyake vya sheria akiendelea kupitia mambo mbali mbali ya kisheria ambayo yangeweza kumsaidia katika kesi inayomkabili Patrick
Alizidi kulemewa na usingizi,taratibu akainuka na kuelekea jikoni akatengeneza kahawa na kurejea tena katika chumba chake cha kusomea akaendelea na kazi yake.Alipokaa tu ,simu yake ikaanza kuita.Akaichukua na kutazama mpigaji ,alikuwa ni George.Akakunja uso na kuitupa simu pembeni.
“Huyu mwanaume anatafuta kitu gani kwangu? Kwa nini hataki kuelewa kwamba mimi na yeye basi? Nimekwisha mweleza kwamba sihitaji mawasiliano yoyote naye lakini hataki kunisikia.? Akawaza Savanna.Simu ikaendelea kuita akaamua kuipokea.
“Hivi wewe ni mtu gani ambaye hutaki kuelewa? Nimekwisha kuambia kwamba sitaki mawasiliano yoyote na wewe.George naomba usinisumbue tafadhali.Stay away from me and my life” akasema Savanna kwa ukali
“Ouh Savanna yaani kutengana siku hizi chache umenichukia na hutaki hata nikusalimie? Nimeshindwa kulala bila kuisikia sauti yako.Hebu niambie mpenzi wangu unaendeleaje?” akasema George kwa sauti ya taratibu na kuzidi kuchukiza Savanna
“George tafadhali naomba usiendelee kunisumbua nina kazi nyingi za maana za kufanya.Naomba hii iwe ni mara yako ya mwisho kunipigia simu.” Akasema kwa ukali Savanna
“Oooh Savanna ,naomba tafadhali usikate simu.Najua una kazi nzito ya kufanya kwa ajili ya kumsaidia Patrick ambaye ndiye mwanaume pekee unayemuota usiku na mchana.Naomba ufahamu kwamba jitihada zote unazozifanya ili uwe na Patrick ni kazi bure.Hutaipata hiyo nafasi.Unaelewa ni kwa sababu gani huwezi kuipata hiyo nafasi. Ni kwa sababu Patrick hakupendi.He’s just using you.Pamoja na hayo naomba niweke wazi kwamba mimi ndiye mwanaume wako wa pekee na hutapata mwanaume mwingine zaidi yangu.Ninakupenda kuliko wanaume wote wa dunia hii na nitahakikisha ninakuwa nawe katika maisha yangu yote.Kwa maana hiyo nitahakikisha lengo lako la kutaka kuwa na Patrick halifanikiwi hata kidogo..Nitafany………..”
“Stupid !!!!!!!!!..” Savanna akasema na kukata simu kwa hasira.
“Huyu mwanaume ana akili zote kweli? Yeye ni nani wa kuweza kunizuia mimi nisitekeleze mipango yangu? Ni Mungu pekee ambaye anaweza kunizuia mimi kuwa na Patrick.Hakuna mwanadamu anayeweza kunizuia.Nitahakikisha Patrick anakuwa huru na anakuwa wangu .” akasema Savanna halafu akainamia vitabu vyake.
* * * *
Saa sita za mchana iliwakuta Linah na Loniki katika jumba la kifahari linalomilikiwa na Khumalo.Tayari mlinzi alikwisha pewa taarifa ya ujio wao hivyo akawaruhusu kuingia ndani bila matatizo.Muhudumu aliyekuwa amevaa suti nzuri nyeusi akawapokea na kuwaongoza hadi katika sebule moja kubwa yenye nakshi na samani za kupendeza sana
“Wow !! Inaonekana huyu jamaa ni mtu mwenye kujiweza sana” akanong’ona Loniki baada ya kuviona vitu mbali mbali vya thamani ndani ya sebule lile kubwa.Linah akatabasamu hakujibu kitu.Muhudumu akawakirimu kwa vinywaji wakati wakiendelea kumsubiri Khumalo.
Baada ya dakika zipatazo kumi toka wamefika ,kijana mmoja mwembamba ,mrefu aliyevaa suti iliyomkaa vyema akaingia mle sebuleni.Mara tu alipokutanisha macho yake na Linah,kijana yule akaachia tabasamu pana sana.Linah naye akatabasamu halafu akainuka pale sofani wakakumbatiana.
“Ouh Linah..I missed you so much” akasema Yule kijana
“Its been a long time khumalo.’ Akasema Linah.Loniki akatabasamu alipogundua kwamba Yule kijana ndiye Khumalo.
“Habari yako Linah” akasema khumalo akiwa bado ameushika mkono wa Linah.
“Habari yangu nzuri khumalo.Ni muda mrefu hatujaonana. Unaendeleaje?
“Ninaendelea vizuri Linah.Umepotea siku hizi,haupatikani kabisa.Nilipita China kama wiki tatu zilizopita,nikaonana na Frank akaniambia kwamba ulikuwepo pale na uliondoka jana yake kuelekea Port Elizabeth.Nilisikitika sana kukukosa”
“Ni kweli nilipita China nikaonana na Frank lakini sikukaa sana nilikuwa nawahi shughuli muhimu Port Elizabeth.Mambo yako yanakwendaje?
“Mambo yanakwenda vizuri sana Linah.Nimefurahi sana kukuona.Naona leo umeniletea mgeni” akasema Khumalo huku akimuangalia Loniki na kutabasamu
“yah ! Samahani kwa kutokutambulisha mapema.Huyu ndiye Yule rafiki yangu anaitwa Loniki.Kwa sasa anaishi na kufanya kazi nchini Uingereza.Amekuja nyumbani mara moja kutokana na matatizo ya kifamilia.” Akasema Linah halafu akamgeukia Loniki
“Lonny,huyu ndiye Khumalo,rafiki yangu wa siku nyingi na ambaye atatusaidia katika ile kazi yetu”
“Karibu sana Loniki.Nimefurahi kukuona.Mimi ninaitwa Khumalo kama alivyokueleza Linah.Ninajishughulisha na biashara mbali mbali.Karibu sana na ujisikie nyumbani.” Akasema Khumalo huku akiinuka na kumfuata Loniki mahala alipoketi na kumpa mkono.
“Hata mimi nimefurahi sana kukuona Khumalo.” Akasema Loniki
“Linah alinieleza kwa ufupi kwamba una matatizo na unahitaji msaada.Nilitaka nionane nawe ili tuweze kuongea suala hili kwa kina.Nataka nipate picha kamili ya nini tatizo lako na nini unataka nikufanyie.” Akasema Khumalo huku akitoa sigara katika pakiti na kuiwasha.Loniki akarekebisha koo lake na kumsimulia Khumalo mkasa mzima uliohusiana na kifo cha Vero.Khumalo alikuwa kimya akimsikiliza kwa makini.Baada ya kumaliza kusimulia mkasa ule ,kimya kifupi kikatanda mle sebuleni.Khumalo akainuka na kuelekea katika friji akachukua mapande ya barafu na kurejea akiwa na chupa ya mvinyo mkononi.Akajimiminia mvinyo katika glasi na kupiga funda moja kisha akawasha sigara nyingine akavuta na kupuliza moshi hewani.
“pole sana Loniki.Nimeguswa sana na maelezo yako.Hata kama ningekuwa ni mimi ningefanya kama unavyotaka kufanya.Watu waliosababisha kifo cha mdogo wako hawastahili kuendelea kuwa hai.Mimi niko tayari kukusaidia kufanya hivyo unavyotaka lakini kabla hatujaenda huko nina ushauri mdogo.Nimekuelewa kwamba lengo lako ni kutaka wale wote waliosababisha kifo cha mdogo wako wapate mateso makali na hatimaye kuuawa.Hilo ni jambo lililo ndani ya uwezo wangu lakini kutokana na uzoefu wangu katika shughuli kama hizi ni kwamba kwa wakati huu ambao suala hili bado bichi,tukisema tumuue mmoja wapo kati ya Happy au Patrick basi inaweza ikawa mbaya kwa upande wako kwani itaonekana kabisa kwamba mauaji hayo yamefanyika kwa lengo la kulipa kisasi na familia yako inaweza ikahusishwa moja kwa moja na mauaji hayo na hii inaweza ikatuletea shida sisi sote.” Akasema Khumalo akanyamaza akamuangalia Loniki.
“kwa hiyo unashauri tufanye nini Khumalo” akauliza Linah
“Nionavyo mimi,tunachotakiwa kufanya kwanza ni kuvuruga kabisa mipango yote ya Patrick na Happy ya kuwa pamoja .Tutaanza kwanza kumshughulikia Happy.Tutamfanyia jambo ambalo litauvuruga kabisa uhusiano wake na Patrick na hata yeye mwenyewe anaweza aamue kujitoa uhai wake.Patrick anampenda Happy na endapo wakitengana Patrick atapata mateso makubwa mno.Nadhani ndivyo unavyohitaji Patrick na Happy wapate mateso makali.” Akasema Khumalo.
“Linaonekana ni wazi zuri lakini nahitaji ufafanuzi zaidi hasa namna utakavyomshughulikia Happy hadi yeye na Patrick watengane na ikiwezekana akaamua kujitoa uhai wake yeye mwenyewe” akasema Loniki.
Khumalo akachukua glasi yake ya mvinyo akanywa kidogo halafu akasema
“Tutamteka Happy.” Akanyamaza na kupuliza moshi mwingi hewani
“Nini kitafuata akishatekwa?
“Tutampeleka katika maficho yetu na halafu tutamfanyisha ngono na kundi la wanaume huku akipigwa picha na kurekodiwa katika filamu.Baada ya hapo tutachukua picha zile na kuzisambaza katika magazeti yote ya udaku na katika mitandao yote ya kijamii.Ninaamini baada ya hapo hakutakuwa tena na mahusiano kati ya Patrick na Happy.Happy tayari ana jina kubwa nchini na kwa kitendo cha picha zake za utupu kusambaa atadhalilika sana na nina hakika kama si kuikimbia nchi basi ataamua kujitoa uhai wake.Atateseka sana na hatakuwa na sehemu ya kupita kwani filamu zake tutazisambaza hadi vijijini.Mnaonaje kuhusu mpango huu? Akauliza Khumalo
Linah akatabasamu huku akimtazama Loniki na kusema
“That’s a perfect plan.Au unasemaje Lonny?
“hata mimi nakubaliana na mpango huo kwani lengo langu hasa ni watu hawa wapate mateso makubwa.Nina imani kama mpango huo utafanikiwa basi Happy atakuwa katika wakati mgumu sana.Atateseka sana kisaikolojia na kutokana na msongo wa mawazo ataona ni bora ajitoa uhai.Nadhani tukifanikiwa mpango huu kwa Happy tutakuwa tumemgusa kwa kiasi kikubwa na Patrick ambaye anampenda Happy.Wote wawili watapata mateso makali sana ya moyo na nina hakika hawatakuwa pamoja tena.Gharama nzima ya shughuli hii yote ni kiasi gani Khumalo? Akauliza Loniki.Khumalo akapuliza moshi mwingi hewani na kusema
“Kwa sababu ni wewe na umeletwa na swahiba wangu Linah basi utanipa shilingi million hamsini tu, pesa ambayo nitawapa vijana watakaonisaidia katika kuifanya hiyo kazi.Mimi sintapata chochote katika kazi hii.Nimeamua kukusaidia tu” akasema Khumalo.Loniki alistushwa sana na kiwango kile kikubwa alichokitaja Khumalo.Akainama na kufikiri.
“Ok Khumalo,pesa si tatizo.Ninachohitaji mimi ni mpango utekelezeke.Nitakupatia hizo millioni hamsini”
“Sawa Loniki.Kitu kingine ninachokihitaji toka kwako ni picha ya huyo Happy na maelezo yake kamili,mahala anapoishi au kama huna nipe picha yake na mahala anapoishi vijana wangu watamtafuta.”
“kwa sasa sina picha ya Happy lakini jumatano ijayo kesi ya Patrick itatajwa tena.Ingekuwa vyema kama ungehudhuria mahakamani wewe na vijana wako na mkamuona huyo mtu mwenyewe.”
“Hilo ni wazo zuri.Basi tutafika mahakamani siku hiyo na kumtambua huyo Happy na Patrick.” Akasema Khumalo halafu akaagana na akina Linah kwani kuna mahala alikuwa akiwahi.
“Linah umefahamiana vipi na Khumalo? Akauliza Loniki wakiwa njiani baada ya kuondoka nyumbani kwa Khumalo
“Khumalo nilifahamiana naye katika michakato yangu ya biashara.Toka wakati huo tumekuwa marafiki wakubwa sana.”
“Amenifurahisha sana kwa namna anavyojiamini na hata mpango wake ni mzuri.Ninachotaka ni Happy na Patrick waumie na endapo mpango huu utakamilika basi najua wataumia mno na ndoto yao ya kuwa pamoja itapotea” Akasema Lonny
“Khumalo ni mtu mwenye roho ya paka.Usoni anaonekana ni kijana mpole lakini awapo kazini sura yake hubadilika na kuwa ya shetani.Wewe utaona tu namna atakavyoifanya kazi hii uliyompa.”
“Nitafurahi sana sana kuona namna huyo kahaba Happy aliyevamia mapenzi ya watu atakavyodhalilika.Nataka aumie moyoni kama sisi tulivyoumia.Damu ya Vero haiwezi kupotea bure”
“Usijali Lonny.Kwa sasa unaweza kupumua baada ya kumkabishi Khumalo jukumu zima.” Akasema Linah
Mahakama ya kisutu ilifurika watu zaidi ya siku za kawaida.Kilichovutia idadi kubwa ya watu ni kesi ya kusababisha kifo inayomkabili Patrick.Kesi hii ilivuta hisia za watu wengi hasa baada ya aliyekuwa mrembo wa Tanzania ,Happy Kibaho kutajwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na kijana huyu aliyesababisha kifo cha Vero. Kwa siku ya leo kesi hii ilikuwa inatajwa kwa mara ya pili.
Waandishi wa habari toka vyombo mbalimbali vya habari walikwisha wasili mahakamani toka asubuhi ili kujiandaa kupata habari kuhusiana na kesi hii iliyoandikwa sana na magazeti mengi hapa nchini.
Saa nne kasoro dakika sita za asubuhi gari aina ya Range rover Vogue lenye rangi nyeupe ikawasili pale mahakamani.Watu wengi waligeuza shingo zao kulitazama gari lile la kifahari lililokuwa likiingia taratibu pale mahamani.Baada ya kuegeshwa mlango ukafunguliwa na mwanadada mmoja mrembo sana aliyevaa suti nyeusi akashuka na kuacha minong’ono ikiendelea midomoni mwa watu waliokuwapo pale mahakamani.Mwanadada Yule ambaye alibarikiwa uzuri,alikuwa akitembea kwa madaha kuingia katika jengo la mahakama.Huyu alikuwa ni Savanna wakili mahiri anayemtetea Patrick.Wakati akielekea katika jengo la mahakama ,mara simu yake ikaita akasimama ,akaitoa simu yake na kutazama mpigaji halafu akageuza shingo yake na na kwa mbali akamuona Andrew akitabasamu.Akatembea kumwendea.
“Habari za asubuhi Andrew.Nimechelewa kidogo na ndiyo maana sikuangalia pembeni.” Akasema Savanna huku akimpa mkono Andrew
“Usijali Savanna.Unaendeleaje? hatukuonana tena toka tulipomzika mzee”
“ Ninaendelea vizuri Andrew.Ni kweli hatujaonana tena,nilikuwa na shughuli nyingi sana kuhakikisha kwamba kila kitu kinakwenda vizuri.Alois amekwisha fika?
“Ndiyo ,familia nzima imekwisha fika ila mama bado yuko garini.”
“Nipeleke nikawasalimu” akasema Savanna kisha wakaelekea lilipo gari la akina Alois
“Mama shikamoo” Savanna akamsalimu mama yake Patrick.
“ Marahaba mwanangu.Vipi hali yako?
“ Hali yangu nzuri mama.Unaendeleaje?
“ namshukuru Mungu ninaendelea vizuri.Kila siku ninazidi kupata nguvu.”
“Hilo ni jambo la kushukuru sana mama” akasema Savanna halafu wakaendelea na maongezi mafupi kisha akawaaga na kwenda kuendelea na mambo mengine.
Saa tano na dakika kumi za asubuhi,basi linalobeba mahabusu toka katika gereza la Uwangwa likawasili likiwa chini ya ulinzi wa askari kama kawaida yake.
“Nina hakika hili ndilo basi linalotumika kuwabeba mahabusu na Patrick atakuwemo ndani ya basi hili.Jitahidi umfahamu vizuri” Mwanamke mmoja aliyekuwa ndani ya gari nyeusi aina ya Noah akamwambia kijana mtanashati aliyekuwa naye mle garini.
“Usijali Loniki,macho yangu yanaona kama tai” akasema Kijana Yule mwembamba na mwenye sura angavu.
“nakuamini Khumalo” akasema Loniki ambaye alifika mahakani hapo akiwa ameongozana na rafikiye wa karibu na wa siku nyingi sana Linah pamoja na khumalo,kijana hatari ambaye amekodishwa ili kuweza kuutekeleza mpango kabambe wa Loniki wa kulipiza kisasi kwa wale wote waliosababisha kifo cha mdogo wake Vero.
“Mbona huyo Miss Tanzania hajatokea mpaka sasa? Inawezekana asifike mahakamani? Akauliza Khumalo
“Usihofu Khumalo,lazima atafika tu.Nina hakika hawezi kukosa mahakamani.Wait…!!!” Loniki akastuka baada ya kuona kitu
“Yule si Sarah ? akauliza Loniki na kumtazama Linah
“Ni yeye.Ni nani wale anaongea nao?
“Familia ya Patrick.Nimemkumbuka mmoja wao Yule mwenye shati jekundu .Alikuja kuwawakilisha katika mazishi ya Vero.Nashindwa kumuelewa huyu mdogo wangu .Haonyeshi kuguswa kabisa na kifo cha mdogo wake.Potelea mbali mimi nitaendelea na mipango yangu na nitahakikisha wale wote waliosababisha kifo cha Vero wanalipa “akasema Loniki huku akivaa miwani yake myeusi
“Lonny wafungwa wameanza kushushwa katika basi” Linah akamstua Loniki ambaye alikuwa ameinama.Loniki akavua miwani yake na kukodolea macho mahabusu waliokuwa wakishushwa garini.
“There he is !!!!Umemuona Yule mwenye shati jeusi? That’s Patrick.” Akasema Loniki akimuelekeza Khumalo.
“Ouh.!.He’s such a handsome guy..” akasema Linah na kumfanya Loniki ageuze shingo akamtazama kwa macho makali
“Unasemaje Linah ? akauliza Loniki
“Nakutania Lony” akasema Linah huku akicheka kidogo
“Tafadhali Linah si nyakati zote huwa za utani.” Akasema Loniki halafu akamgeukia Khumalo
“Tayari nimekwishamuona Patrick.bado huyo mwanamke Miss Tanzania.” Akasema Khumalo
“She must be here..she must be somewhere around here..Let’s just wait…” akasema Loniki.
Saa sita za mchana kesi ya Patrick ikatajwa tena.Chumba kilijaa watu .Wakati mabishano ya kisheria yakiendelea kati ya mawakili wa utetezi wakiongozwa na Savanna dhidi ya wale wa serikali Loniki ambaye naye alikuwemo ndani ya chumba kile cha mahakama pamoja na rafikiye Linah na Khumalo,aliendelea kupepesa macho yake kila kona ya kile chumba akimtafuta Happy.
“Kumbe huyu mwanamke ndiye anayemtetea Patrick.!! Mnafiki mkubwa huyu.Namkumbuka sana siku ya mazishi ya Vero alikuwepo na alionekana ni mwenye huzuni nyingi sana.Anaonekana kuifahamu vizuri sheria lakini pamoja na juhudi zake zote na ufundi wake wote katika sheria hataweza kushindana nami hata kidogo.” Akawaza Loniki huku akiendelea kuyazungusha macho yake mle katika chumba cha mahakama na mara katika pembe moja ya chumba akamuona msichana mmoja aliyejifunga kitambaa kichwani pamoja na miwani myeusi.
“There she is…!!..japokuwa amejaribu kujificha ili asionekane lakini hawezi kunipotea hata kidogo.Sura yake ipo kichwani kwangu na hakuna namna anavyoweza kufanya ili kunipotea” akawaza Loniki huku akiendelea kumtazama msichana Yule kwa jicho la chuki.
“Linah nimemuona Happy.Yule pale aliyejifunga kitambaa chekundu kichwani.” Akasema Loniki na kumuelekeza Linah mahala alipokaa Happy.Linah akamnong’oneza Khumalo na kumuelekeza mahala alipokaa Happy.Wote watatu kwa pamoja wakaendelea kumuangalia Happy.
Kama ilivyokuwa kwa watu wote mle katika chumba cha mahakama,Happy naye alielekeza macho na akili yake katika malumbano ya kisheria yaliyokuwa yakiendelea baina ya wanasheria.Ghafla akageuka baada ya kuguswa begani na Pendo mfanyakazi wao wa ndani aliyekuwa ameongozana naye siku hii ya leo .
“Dada Happy kuna watu nimewaona muda mrefu wamekuwa wanakuangalia sana” akasema Pendo .Happy akageuza shingo yake katika upande alioelekezwa na Pendo na mara akakutanisha macho na sura za watu watatu zilizokuwa zikimuangalia huku zikijadili jambo.Hakuwafahamu watu wale na hawakuonekana kama waandishi wa habari.
“Twende tutoke humu ndani” akasema Happy kisha wakainuka na kutoka nje ya chumba cha mahakama huku akipigwa picha na waandishi wa habari.Baadhi ya waandishi wa habari walimfuata na kujaribu kumuuliza maswali lakini hakuwa tayari kuongea chochote na waandishi wa habari. Moja kwa moja akaenda kusimama nje ya gari lakeCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Watu wale kwa namna walivyokuwa wakiniangalia na kunong’onezana walinitoa kabisa hamu ya kukaa mle mahakamani.Yawezekana wakawa ni ndugu wa Patrick au wa Vero.Ni heri nikae tu hapa nje hadi mahakama itakapomalizika.Savanna atanieleza kitakachoendelea..Isitoshe sitaki kuonana na familia ya Patrick kwa sasa.Hawatanitazama kwa jicho zuri hata kidogo” akawaza Happy
* * * *
Mjadala mkali wa kisheria ulimalizika na hakimu akaiahirisha kesi ile na kuipangia tarehe nyingine ya kutajwa.Akiwa chini ya ulinzi Patrick akaongozwa na kutolewa nje ya mahakama.Alifarijika sana baada ya kumuona mama yake mzazi japokuwa sura yake ilikuwa imesawajika sana.Pamoja na msiba mzito wa kufiwa na mumewe kipenzi lakini bado alijitahidi na kufika mahakamani kufuatilia kesi ya mwanae.Pembeni yake alikuwa amekaa Alois pamoja na mke wake.Patrick akawapungia mkono.Walikuwepo pia ndugu mbali mbali na marafiki waliokuja kumpa moyo katika kesi hii.Mara akagonganisha macho na Sarah dada yake Vero aliyekuwa amekaa na Andrew.Patrick akawapungia mkono halafu akaangalia chini
Wakati akitoka mle chumbani,Loniki alikuwa akimtazama kwa jicho la chuki.
“Naisubiri kwa hamu siku nitakayokuona ukipata mateso na maumivu makali kama ninayoyapata mimi.Wewe na kahaba wako Happy lazima mtalipa kwa kitendo mlichokifanya.Its not a long time from now.You’ll pay dearly” akawaza Loniki huku akiuma meno kwa hasira
Baada ya Patrick kutolewa nje ya chumba cha mahakama,watu nao wakaanza kutoka.Nje ya mahakama katika gari moja lenye rangi nyeusi ,Happy alikuwa amesimama akisubiri kuonana na Savanna ili ajue kinachoendelea .Akiwa nje ya gari lake,kijana mmoja mtanashati aliyevalia nadhifu sana akajongea taratibu hadi mahala aliposimama Happy.
“Habari yako dada” akasema Yule kijana
“Nzuri habari yako” akaitika Happy huku akiendelea kuangaza macho yake katika mlango akimtafuta Savanna
“You must be Happy Kibaho” akasema Yule kijana aliyevalia nadhifu.Happy hakumjibu kitu bado aliyaelekeza macho yake mlangoni.
“By the way,I’m George….George Simkaya” akasema Yule kijana huku akimpa mkono Happy.Happy akamtazama Yule kijana usoni na kumwambia
“Tafadhali George ,sina muda wa kujibu au kuongea lolote na waandishi wa habari siku ya leo.” Akasema Happy
“Happy mimi si mwandishi wa habari.Ninafanya kazi ikulu” akasema George huku akitoa kitambulisho chake na kumuonyesha Happy
“Unataka nini toka kwangu George?
“Happy nimekuja kwako nina maongezi nawe ya muhimu sana”
“Maongezi na mimi? Yanahusu nini? Akauliza
“Yanakuhusu wewe,na hatima ya Patrick na kinachoendelea kuhusiana na kesi yake” akasema George na kumstua kidogo Happy
“Nini kuhusu hatima ya Patrick na kinaendelea katika kesi ya Patrick?
“Ni suala ambalo tunatakiwa tukae ili nikueleze kwa makini sana.Je una nafasi ya kutosha sasa hivi? Akauliza George
“Naomba unisubiri mara moja kuna mtu nahitaji kumuona” akasema Happy na mara simu yake ikaita
“Halo Savanna.” Akasema Happy baada ya kuipokea ile simu
“Happy habari yako? Nimeupata ujumbe wako sasa hivi baada ya kuwasha simu.Uko upande upi? Akauliza Savanna.Happy akamuelekeza mahala alikoegesha gari lake .Alipomaliza kuongea na Savanna simuni akageuza shingo yake lakini George hakuwepo.Happy hakujali sana mawazo yake yote hivi sasa yalikuwa kwa Savanna ambaye alimuona akipiga hatua kuelekea kule alikokuwa
“Habari yako Happy.Nafurahi kukuona leo umefika.” Akasema Savanna huku akitabasamu na kulifanya jino lake moja lililotengenezwa kwa madini ya thamani kuonekana.
“Nashukuru Mungu ninaendelea vizuri.Nilikuwamo ndani ya chumba cha mahakama lakini niliwahi kutoka.Sikutaka kuonana na ndugu za Patrick” akasema Happy
“Kwa sasa bado wana hasira kwa kilichotokea na hawatakuangalia kwa jicho zuri lakini nina imani itafika wakati ambao mambo haya yote yatapoa” akasema Savanna
“Savanna samahani sana najua una majukumu mengine lakini kitu nilichokuitia hapa ni kutaka kufahamu nini kinaendelea kuhusiana na kesi” akasema Happy
“Leo kulikuwa na mjadala mzito wa kisheria wa kutaka kesi hii ibadilishwe na kuwa kesi ya kuua bila kukusudia ili Patrick aweze kupatiwa dhamana.Japokuwa bado upande wa mashitaka unaendelea na uchunguzi lakini nina imani tutafanikiwa kuibadili kesi hii. Kwa sasa tumeiomba mahakama iwaamuru upande wa mashitaka kukamilisha upelelezi wao haraka ili tuweze kuwasilisha ombi letu la kubadili mashtaka.Bado tuna safari ndefu lakini nina uhakika mkubwa wa kusinda kesi hii.” Akasema Savanna bila ya kuwa na wasi wasi wowote.Maneno yale yakampa faraja sana Happy na uso wake ukajenga tabasamu pana.
“Nashukuru sana Savanna kwa kunipa moyo.”
“Happy usihofu kitu chochote.Kesi hii haina ugumu sana kwangu na nina imani siku moja Patrick atakuwa huru.Japokuwa inaweza ikachukua muda mrefu kidogo kutokana na upelelezi kuchukua muda mrefu lakini nakuhakikishia kwamba nitapambana hadi nihakikishe kwamba Patrick anakuwa huru.” Akasema Savanna halafu wakaagana.
Happy hakutaka tena kuendelea kukaa pale mahakamani,akaingia katika gari lake lakini kabla hajawasha gari,George akatokea na kugonga kioo cha mlangoni.Happy akaonekana kukerwa na kitendo kile akashusha kioo na kusema kwa ukali
“Its you again..Ulikuwa wapi? Mbona ulipotea ghafla?
“Sikutaka Yule wakili Savanna anione ninaongea na wewe ndiyo maana nikajificha”
“Do you know her?
“C’mon Happy,don’t ask so many questions. Are you ready to hear what I want to tell you? Akauliza George.Happy akafikiri kidogo na kusema
“Get in the car.” George akafungua mlango wa gari na kuingia ndani kisha Happy akaliondoa gari eneo lile la mahakama.
“Follow her..” akaamuru Khumalo aliyekuwamo katika gari aina ya Noah akiwa na Loniki na Linah wakimuangalia Happy.Baada ya Happy kutoka katika eneo la mahakama ,gari ya akina Loniki nayo ikatoka na kuanza kumfuatailia Happy bila ya yeye kufahamu kama alikuwa anafuatiliwa.Linah aliendesha gari lile kwa ustadi mkubwa
* * * *
“George jambo gani unalotaka kuniambia? Akuliza Happy wakiwa garini.George akamtazama Pendo aliyekuwa na Happy mle garini.
“Do you trust her? Akauliza George.
“Ofcourse I do trust her” akasema Happy
“George unataka kuniambia nini? akauliza tena Happy akiwa na wasi wasi
“Happy utanisamehe sana lakini ninachotaka kukwambia kitabaki kuwa kati yetu.Hapaswi mtu mwingine yeyote kujua.Pale mbele kuna baa,pinda kushoto ingia pale Masuke Bar,tutaongea kwa dakika chache halafu utaendelea na safari yako” akasema George.Happy akaonyesha wasi wasi kidogo
“Happy naomba uniamini.Mimi si mtu mbaya na wala hakuna jambo lolote baya litakalokupata” akasema George.Bila kusema lolote Happy akawasha taa ya kushoto kuashiria kwamba alikuwa anakata kona na kuingia Masuke Bar.Baada ya kuegesha gari akashuka yeye na George na kwenda kuketi chini ya mwavuli.Pendo alibaki garini.
“George naomba tusipoteze muda.Nieleze kile ambacho unataka kuniambia.I’m not too comfortable to be seen here” akasema Happy.George akanywa maji kidogo halafu akasema
“Kwanza kabisa naomba nikupe pole sana kwa masahibu yote yaliyokukuta”akasema George.
“Please George go direct to the point.Hatukuja hapa kupeana pole” akasema Happy huku akionekana kuanza kukasirika
“Usihofu Happy jambo kubwa nililotaka kukueleza ni kuhusiana na Yule mwanamke uliyekuwa unaongea naye pale mahakamani”.
“Savanna? Akauliza Happy
“Exactly !!!Huyo huyo Savanna” akasema George
“Savanna kafanya nini?
“Do you real know her? akauliza George
“Bado simfahamu vizuri.Tumefahamiana siku za hivi karibuni.Yeye ni wakili anayemtetea mpenzi wangu”
“Sawa Happy lakini inaonekana bado hujamfahamu Savanna ni nani.Naomba unisikilize kwa makini” akasema George
“Savanna ni mke wangu……alikuwa mke wangu”
“Savanna alikuwa mke wako? Happy akashangaa
“Ndiyo alikuwa mke wangu,lakini kwa sasa hatuko pamoja tena.Kilichosababisha mimi na yeye tukatengana ni Patrick”
“Patrick ..!!!..Happy akashangaa
“Patrick anahusika nini na kutengana kwenu wewe na Savanna? Akauliza Happy
“Kuna jambo ambalo bado hujalifahamu Happy .Ni kwamba Patrick na Savanna walikuwa na mahusiano ya siri ya kimapenzi kwa muda mrefu.”
“Mambo gani haya unanieleza George? Patrick na Savanna waliwahi kuwa wapenzi???..thats impossible.Patrick alikuwa na mpenzi wake ambaye alikuwa afunge naye ndoa na akafariki katika ugomvi na ndiyo sababu ya yeye kushikiliwa na vyombo vya usalama.”
“Niamini Happy.Mimi na Savanna tumekuwa pamoja kwa miaka mitano sasa.Kabla sijakutana na Savanna,tayari alikuwa katika mahusiano ya siri na Patrick ambaye kwa wakati huo tayari alikuwa katika mahusiano ya wazi na mchumba wake Veronika.Nilipata wakati mgumu sana kuweza kumshawishi Savanna akubali kuwa na mimi kwani walikuwa wakipendana sana na Patrick.Ilimlazimu Savanna amueleze ukweli Patrick na ndipo alipompa ruhusa ya kuwa na mimi.Pamoja na kuwa na mimi lakini mpaka leo hii akili ya Savanna bado iko kwa Patrick.Kwa kuwa ninampenda sana Savanna niliamua kuishi naye hivyo hivyo nikiamini kwamba siku moja atanipenda na kunikabidhi moyo wake lakini katika miaka hii yote niliyoishi naye sijaweza kufanikiwa kumuondoa Patrick katika akili yake.Kama huniamini ,siku ukikutana naye angalia mkufu wake anaopenda kuuvaa shingoni,una kidani kilichoandikwa P&S na hata pete yake ya dhahabu ambayo huwa haitoi kidoleni imeandikwa hivyo hvyo.Umewahi kumchunguza vizuri Patrick? Naye pia ana pete kama hii aliyonayo Savanna.” Akasema George .Happy akatoa kitambaa na kujifuta jasho lililoanza kumtoka.
“Ni kweli tukiwa Arusha nilimuona Patrick akiwa na pete kama hiyo anayoisema George na nilimuuliza kama pete ile ina maana yoyote akasema kwamba haina maana yoyote.” Akawaza Happy.George akaendelea
“Mimi na Savanna tumetengana hivi majuzi baada ya Patrick kukumbwa na masahibu.Kilichotutenganisha ni baada ya kugundua kwamba Savanna anataka kuitumia kesi hii ili aweze kuwa tena na Patrick na hasa baada ya Veronika mpenzi wa Patrick kufariki.Hii ni nafasi pekee aliyoipata ya kuurejesha uhusiano wake na Patrick na hasa baada ya mchumba wa Patrick kufariki dunia na hilo amekiri yeye mwenyewe kwa mdomo wake.Ninamfahamu Savanna,ni mwanamke ambaye akidhamiria kitu lazima atakipata.Dhamira yake ya kuitumia kesi hii kujitengenezea mazingira ya kurudiana na Patrick lazima itatimia kama asipodhibitiwa haraka” akasema George.Mapigo ya moyo wa Happy yalibadilika na kuanza kwenda mbio.
“Why are you telling me all these now? Akauliza Happy
“Happy nimekwambia kwa wakati huu ili mimi na wewe kwa pamoja tuweze kufanya kitu.Siwezi kukuficha Happy kwamba ninampenda sana Savanna na ndiyo maana ninajitahidi kufanya kila niwezalo ili niweze kurudiana naye.Sitaki kuona akiangukia tena katika mikono ya Patrick.Ninaamini vile vile kwamba Patrick ni mtu ambaye unampenda sana na hivyo hauko tayari kumuona akiangukia katika mikono ya Savanna.”
“Geoerge unataka tufanye nini” akauliza Happy.Uso wake ulikwisha badilika.Alikuwa na wasi wasi mwingi
“Nataka tufanye kila linalowezekana ili Savanna asiendelee kuisimamia kesi hii.” Akasema George.Happy akainama chini na kuzama katika mawazo.
“Ninakubaliana na Geroge kwani hata mimi nilikuwa nashangaa sana kwa nini Savanna aamue kumtetea Patrick bila malipo yoyote? Kumbe ana lake jambo.Nashukuru sana George amenifumbua macho.” Akawaza HappyCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“George umenichanganya sana akili yangu na sielewi tutafanya nini ili tuweze kumuondoa Happy katika kesi ya Patrick.Kwa uwezo wangu mimi siwezi kufanya hivyo kwa sababu sina hakika kama Patrick au ndugu zake wanaweza wakakubali.Wote kwa pamoja wana imani kubwa na Savanna” akasema Happy
“We have to do something Happy.We have to stop her.There is must be a way to stop her” akasema George.
“Ugumu uliopo hapa ni kwamba Patrick anamuamini mno Savanna na ili kuweza kumtoa Savanna ni lazima Patrick na familia yake waamue.Vinginevyo sisi wawili hatuna uwezo wowote wa kumfanya Savanna atoke katika kesi hii.Sina hakika kama Patrick anaweza akakubali kumuondoa Savanna katika kesi yake.Kitu kingine ambacho kitaleta ugumu ni kamba Savanna anaifanya kazi hii bila kudai hata senti tano. Kazi hi anaifanya bure kabisa na yeye ndiye aliyejitolea kulipa gharama zozote zitakazohitajika katika kesi hii.” Akasema Happy.Kimya kikatanda pale mezani
“ Nimekuelewa Happy lakini lazima tujaribu.Jaribu kuongea na Patrick na umshawishi kwamba Savanna hafai kuisimamia kesi yake.Mimi nitatafuta mawakili wapya na hata kuwalipa niko tayari”
Happy akafikiri kidogo na kusema
“ Nitajaribu George.” Kimya kifupi kikapita Happy akasema
“George nashukuru sana kwa taarifa uliyonipa japokuwa imenistua sana lakini nashukuru kwa kunifumbua macho kuhusiana na kile kilichokuwa kinaendelea nyuma ya pazia.Naomba niende nikapumzike nitafakari kwa kina kuhusu suala hili na endapo kutakuwa na namna yoyote ambayo nitaona tunaweza kufanya basi nitawasiliana nawe mara moja” Akasema Happy na wakabadilisha namba za simu .Happy akaondoka akaelekea garini .Kichwa chake alikiona kizito sana.Akainamia usukani
“Ouh my God ! why always me? ..Happy akasema huku akiupiga usukani kwa mikono yake.
“Dada Happy kulikoni? Akauliza Pendo
“Ouh Pendo ! Samahani kichwa changu kimetingwa na mambo mengi sana.Anyway twende tuondoke hapa” akasema Happy akawasha gari wakaondoka.
“Ninaona kama dunia inaniadhibu.Wakati bado jereha la moyo linavuja damu na sijui nitalitibu vipi ,linaibuika tena suala jingine.Ee Mungu Kwanini umeamua kuniadhibu namna hii? Akawaza Happy
“Patrick amewahi kuwa na mahusiano na Savanna…?!!!.” Kila alipowaza jambo hili aliendelea kumuumia sana kichwa.
“Ninakubaliana na maneno ya George kwa sababu Patrick huwezi kumweleza chochote kuhusu Savanna akakuelewa.Anamuamini Savanna kupita kiasi.Vile vile hainiingii akilini hata kidogo katika ulimwengu wa sasa mtu akajitolea kuifanya kazi hii ngumu ya kisheria bila kulipwa chochote.Savanna amefanya hivi kwa sababu ana agenda yake ya siri.I’m so confused” akawaza Happy
“lakini pamoja na kuwa na agenda ya siri,Patrick ataendelea kuwa wangu peke yangu.Sintamruhusu Savanna amchukue Patrick toka katika mikono yangu.I’ve sacrificed a lot for Patrick and I wont loose him this time.Nitapambana naye” akawaza Happy
“Loniki,tayari nimekwisha wafahamu wahusika wakuu wanaotakiwa kushughulikiwa.Huyu mwanamke ,Happy ndiye nitakayeanza naye na siku ya kesho lazima nimpate” akasema Khumalo huku akipuliza moshi wa sigara hewani.Walikuwa katika ofisi ya Linah baada ya kutoka mahakamani.
“Nitashukuru sana kama zoezi hili litakwenda haraka kwani itanisaidia hata mimi kurejea haraka Uingereza.Nimeapa sintaondoka Tanzania hadi Patrick na Happy na wengine wote ambao wamesababaisha kifo cha Happy wawe tayari wamekwishalipa..Jioni ya leo nitakupatia kiasi cha shilingi million arobaini na zitakazobaki kumi nitakupatia baada ya kazi hii kukamilika.Kama kazi itakwenda vizuri basi ninaweza hata kukuongeza zaidi.Kwangu mimi pesa si tatizo hata kidogo.” Akasema Loniki.Khumalo akaaga na kuondoka zake kwa miadi ya kuonana jioni ili aweze kupatiwa mzigo wake wa shilingi millioni arobaini.
“Ninamuamini sana Khumalo.Anaongea taratibu lakini siku zote huwa anamaanisha anachokisema.Kama ameahidi kwamba kesho atampata Happy basi amini atafanya hivyo” akasema Linah baada ya Khumalo kuondoka
“Nitashukuru sana .Leo roho yangu imechafuka mno baada ya kumuona Patrick mahakamani tena akitabasamu kana kwamba hana hatia.Sitaki kuisubiri haki ya mahakama ambayo pengine isipatikane.Nitamlipia Vero kwa namna ninayojua mwenyewe.Natamani hata sasa hivi nisikie kamba Patrick na Happy wamefariki dunia.Sikufichi Linah ,moyo wangu utakuwa na amani pale tu Patrick na Happy watakapoacha kuivuta hewa hii safi na sintafumba macho mpaka nitakapohakikisha kwamba wameondoka duniani” akasema Loniki halafu akaagana na Linah kwa miadi ya kukutana jioni ili wamkabidhi Khumalo mzigo wake.
Baada ya kutoka ofisini kwa Linah,Loniki akarejea nyumbani na kumkuta mdogo wake Saraha tayari amekwisha fika na anaongea na mama yake.Loniki akasalimiana na mama yake bila kumsemesha lolote Sarah
“Mbona Sarah humsalimu? Mmekwisha onana? Akauliza mama yao
“Mama sijisikii hata kumpa salamu yangu huyu mwanao.Sioni kama anastahili salamu yangu.” Akasema Loniki kwa dharau
“Sihitaji salamu yako Lonny.” Akasema Sarah huku akitabasamu
“Sarah kwa nini unamjibu hivyo dada yako? Akafoka mama yao
“Mama kamwe sintakubali au kuvumilia dharau za Loniki.Siko tayari kumnyenyekea Loniki na kumsikiliza kwa kila anachokiongea kwa sababu tu anaishi Ulaya.” Akasema Sarah na kwa hasira akaelekea katika gari lake na kuondoka akiwaacha mama yake na Loniki wakishangaa
“Mama huyu mwanao amenichefua sana .Sikutegema kabisa kumuona akiwa hivi.Haonyeshi uchungu wowote ule wa kufiwa na mdogo wake na badala yake anadiriki hata kushirikiana na wauaji wa mdogo wake.Mama siko tayari kuvumilia upuuzi kama huu anaoufanya Sarah.Ngoja nimalize mambo yangu nitamfundisha adabu” akasema Loniki
“Hata mimi sijafurahishwa kabisa na tabia ya Sarah na hasa ya kuchangamana na familia ya Patrick,ambao wametupa mateso haya yote.Kwa uchungu nilionao sijui hata nifanye nini” akasema mama yake Loniki
“Usijali mama,haki lazima ipatikane.Lazima Patrick na wale wote waliosababisha kifo cha mdogo wangu walipe.Sintarejea Uingereza hadi nihakikishe kwamba wote walimuua mdogo wangu wamelipa”
“ Kwa kweli kwa uchungu ninaousikia hata mimi natamani sana waliomuua mwanangu nao walipe uovu wao.Walitenda kitendo cha kinyama sana.Wamemuua mwanangu bila kosa lolote..Ouh Vero ..!!!!” akashindwa kuendelea akaanza kulia.Loniki ambaye naye macho yake yalijaa machozi akamkumbatia mama yake
“Basi usilie mama Haki lazima ipatikane.” Akasema Loniki
“Ahsante mwanangu ,ila naomba wewe na Sarah msigombane kwani sina uwezo wa kuhimili maumivu mengine tena .”
“Hatutagombana mama .Tutarekebishana tu “akasema Loniki
* * * *
Saa kumi na moja za jioni Happy aliamka .Toka aliporejea akitokea mahakamani alikuwa amelala.Kutokana na mawazo mengi aliyokuwa nayo aliamua kumeza vidonge vya usingizi na kulala kwa muda mrefu namna hiyo.Mambo aliyoambiwa na George yalimchanganya sana na alishindwa afanye nini.Kichwa kilikuwa kinamgonga kupita kiasi. Akainuka na kukaa kitandani.
“For the first time I feel dead.Kwa mambo aliyoniambia George ninajihisi kama mfu.Siamini kama Patrick na Savanna waliwahi kuwa wapenzi.Na ninavyohisi kuna kila dalili kwamba bado wanaendelea na mahusiano yao kwa siri kwani walikuwa na mahusiano hata kipindi kile ambacho Patrick alikuwa na Vero.Hii nina maana Patrick hakuwa mwaminifu kwa mchumba wake.Alimsaliti Vero. Na kama aliweza kumsaliti Vero hatashindwa kufanya hivyo hata kwangu.Ouh My God..why always me ? akawaza Happy halafu akaanza kuzunguka zunguka mle chumbani.
“Ninampenda Patrick na nimejitolea kila kitu kwa ajili yake.Lazima nipambane nihakikishe kwamba Savanna hapati nafasi hiyo anayoitaka.Siwezi kukubali ndoto zangu nyingi na za muda mrefu za kuwa na Patrick zipotee hivi hivi.Nilipendana na Patrick kabla hajakutana na Savanna kwa hiyo Patrick ni wangu peke yangu.I’ve made so many sacrifices just to be with him,so I cant let all that be for nothing,I must fight” akawaza Happy halafu akachukua simu na kumpigia Pendo akamuomba amtengenezee juisi ya embe.Baada ya kumaliza kuongea na Pendo akazitafuta namba za simu za Savanna akataka kumpigia lakini akasita .Akavuta pumzi ndefu na kutafakari kwa sekunde kadhaa na mwishowe akakakata shauri
“Lazima nimpigie.Siwezi kumpa Savanna nafasi ya kumpata Patrick.” Akawaza Happy halafu akabonyeza kitufe cha kupigia simu na simu ikaanza kuita.
“Hallow Happy.habari yako?” akasema Savanna baada ya kupokea simu
“Habari yangu nzuri Savanna.” Akajibu Happy
“Happy mbona sauti yako inaonyesha kama vile hauko sawa? Una tatizo lolote Happy? Akauliza Savanna
“Savanna we need to talk” akasema Happy na kumstua kidogo Savanna
“To talk?
“yes Savanna”
“Talk about what?
“About what I’ve discovered today”
“Ok Happy ngoja niegeshe gari hapa pembeni tuongee vizuri.Nitakupigia baada ya muda mfupi” akasema Savanna na kukata simu
“Leo lazima nimeueleze ukweli na utakuwa mwisho wake kuisimamia kesi ya Patrick.Niko tayari hata kukodisha mawakili kumi lakini si kuwa na wakili mmoja aliyevaa ngozi ya kondoo kumbe ndani ni simba.”Akawaza Happy huku simu yake ikiwa mkononi akisubiri Savanna ampigie.Baada ya dakika tano simu yake ikaita.Alikuwa ni Savanna
“Happy tayari nimeegesha gari.Jambo gani unalotaka kunieleza?
“Savanna kuna jambo ambalo ninataka kulifahamu toka kwako.Wewe na Patrick mlifahamiana lini?
“Kwa nini unauliza hivyo Happy ?
“Just answer my question Savanna” akajibu Happy huku sauti yake ikionyesha kutokuwa na masihara.Kimya cha sekunde kadhaa kikapita halafu Savanna akajibu
“Mimi na Patrick tulikutana miaka kadhaa iliyopita,sikumbuki ilikuwa katika mazingira gani”
“Mahusnao yenu baada ya kukutana yalikuwaje?
“Happy mbona unauliza maswali ya namna hiyo? Kuna matatizo gani?
“Savanna naomba unijibu maswali yangu” akasema Happy
“Patrick ni rafiki yangu wa muda mrefu.” Akajibu Savanna kwa ufupi
“Savanna usinidanganye.Tayari ninaufahamu ukweli halisi kuhusu wewe na Patrick.”
“Mimi na Patrick ..!!!!” Savanna akastuka
“Ndiyo.wewe na Patrick”
“Unafahamu ukweli gani kuhusu mimi na Patrick? Akauliza Savanna
“Ninafahamu kila kitu”
“Kila kitu gani Happy?CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Wewe na Patrick mliwahi kuwa wapenzi na bado mnaendelea na mahusiano yenu kwa siri na lengo la wewe kuamua kujitolea kumtetea Patrick mahakamani ni moja ya malengo yako ya kutaka kurudiana tena na Patrick “
“ouh My gosh …!!!!” Savanna akastuka
“Umezipata wapi hito taarifa? Akauliza Savanna
“Sina haja ya kukwambia nimezipata wapi .Ninachotaka kujua toka kwako je ni kweli ? akauliza Happy
“Happy nisikilize vizuri sana mdogo wangu.Tuko katika wakati mgumu wa kuhakikisha kwamba Patrick anashinda kesi kwa maana hiyo haya mambo unayoniuliza hayana msingi wowote kwa sasa.Naomba tuyaache hadi hapo tutakapomaliza haya mambo ya mahakamani na ndipo tutapata muda mzuri wa kuulizana maswali kama hayo” akasema Savanna
“Savanna mambo haya hayana umuhimu kwako lakini kwangu mimi ni muhimu sana.Tafadhali naomba unijibu” akasema Happy
“Happy kwa nini hutaki kunielewa? Nimekwisha kwambia siko tayari kukujibu maswali yako ya kipuuzi kwa muda huu” akasema Savanna kwa sauti ya ukali kidogo
“Savanna wewe ndiye hutaki kunielewa.Nimekuuliza swali rahisi sana Kwa nini hutaki kunipa jibu?
“Nenda kwa aliyekupa taarifa hizo yeye ndiye atakaye kuthibitishia kama ni kweli au si kweli.Mimi sina muda huo wa kupoteza.Tena Happy ninakuomba kama huna jambo la maana la kuongea nami,tafadhali naomba usinipigie simu.Nina mambo mengi ya kushughulikia kesi uliyoisababisha wewe mwenyewe” akasema Savanna
“Savanna hapo ulipo katika kidole chako unayo ile pete uliyopewa na Patrick? Akauliza Happy.Savanna akavuta pumzi ndefu na kusema
“Ninayo”
“kwa nini alikupa pete hiyo? Na kwa nini hujawahi kuivua kidoleni mwako? Kitu kingine ni kwa nini umekorofishana na mumeo George baada ya kuanza kujihusisha na kesi ya Patrick?” akauliza Happy.Kikapita kimya cha sekunde kadhaa,Savanna akatamani kukata simu lakini akaamua andelee kuongea na Happy
“Happy unahitaji nini toka kwangu?
“Umekubaliana nami kwamba kila nilichokiongea hapa ni ukweli mtupu? Akasema Happy.Savanna akakasirika sana.
“Unahitaji kuujua ukweli,sasa ngoja nikwambie ukweli” akasema Savanna kwa hasira
“Ni kweli mimi na Patrick ni wapenzi.Unataka ukweli gani zaidi ya huo? akasema Savanna na kumpandisha hasira Happy
“Malaya mkubwa wewe.Siku zote hizi umekuwa ukijifanya ni mtu mwema kumbe una lako jambo.Nyoka mkubwa we” akafoka Happy
“Happy naomba usinitukane.Wewe ni binti mdogo sana wa kutukanana na mimi.Tena naomba iwe ni mara yako ya mwanzo na mwisho kuniita mimi Malaya.Una jeuri ya kuufungua mdomo wako na kunitukana sasa hivi wakati kwa uwezo wangu umekuwa huru?.Hivi sasa ulitakiwa uwe gerezani na mimi na Parick tungekuwa huru tunajinafasi kwa raha zetu.Happy narudia tena kukuonya kwamba kuwa makini na kauli zako.Mimi ni mtu mzuri sana lakini hubadilika na kuwa mbaya pale ninapokorofishwa.” Akasema Savanna kwa ukali
“Savanna naomba usinitishe.Kwa taarifa yako sikuogopi hata kid……………!!!!” Happy akastuka baada ya kumuona Pendo akiwa amesimama mlangoni akiwa na sura yenye mshangao na mkononi akiwa na glasi ya juisi.
“Kwa muda gani umekuwepo mlangoni? Happy akamuuliza Pendo
“Nimefika muda huu” akajibu Pendo
“Ok weka hiyo Juisi hapo mezani na uondoke” akasema Happy na pendo akatoka mle chumbani.
“Savanna,narudia tena kukwambia kwamba usitubutu tena kunitolea vitisho.Sikuogopi na huwezi kunifanya lolote.Nakuonya kuanzia sasa achana na hiyo kesi ya Patrick.Mimi nitagharamia kumtafuta wakili mpya wa kumtetea Patrick” akasema Happy na kumfanya Savanna acheke kwa dharau.
“Happy huna uwezo wa kuniamrisha mimi nisimtetee Patrick.Wewe ni mtu mdogo sana kwa Patrick.Kama huamini basi nenda kamweleze Patrick kwamba hutaki nijihusishe tena na kesi yake na usikie jibu atakalokupa na hapo ndipo utakapoamini kwamba wewe ni mtu mdogo sana kwake na huna nguvu wala uwezo wa kuamua chochote kuhusiana na maisha yake” akasema Savanna na kuzidi kumpandisha hasira Happy
“Savanna kama hutajitoa katika kesi hii hadi kesho ba………………..” Kabla Happy hajamaliza kusema alichotaka kukisema Savanna akamzuia.
“Utanifanya nini?
“Nitapambana nawe.Sintakubali unichukulie mpenzi wangu.Nitapambana nawe hadi mwisho.Patrick nimetoka naye mbali sana na sintaruhusu fisadi kama wewe kuyaingilia mapenzi yetu.” Akasema Happy kwa ukali
“Huna lolote la kunifanya Happy.Nakuonea huruma sana Happy hujui unachokiongea.Kuwa makini na kauli zako.Kama unajiona una uwezo wa kupambana na mimi nakuruhusu ujaribu..” akasema Savanna na kukata simu.Happy jasho lilikuwa linamtiririka.Mishipa ilikuwa imemtoka usoni kwa hasira alizokuwa nazo.
“Aaaaaggggghhhh..!!!!!!!!!!!!!!!!!!” akasema Happy kwa hasira na kuanza kutupa tupa vitu hovyo mle chumbani
“Savanna siwezi kukupa nafasi,nitapambana nawe kwa kila namna nitakayoweza.Siko tayari kumpoteza Patrick” akasema Happy kwa hasira huku machozi yakimtoka
* * * *
Zaidi ya dakika tano zimekwishakwenda tangu Savanna amalize kuongea na Happy simuni.Alikuwa ameegemea kiti chake akiwa na hasira kali.
“Bastard ..!!!!!!!” akasema Kwa ghadhabu huku akiipiga mikono yake katika usukani wa gari.
“Happy mbona anataka kukivuruga kichwa changu? Amefahamuje kama nilikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Patrick?Amefahamuje kama nilikorofishana na George sababu ikiwa ni Patrick?Ameitaja hadi pete hii aliyonipa Patrick” Akawaza Savanna halafu akainua mkono wake wa kushoto akaitazama pete ya dhahabu yenye kung’aa iliyokuwa na maandishi P&S,akatabasamu
“Ni kweli pete hii tulipeana na Patrick ishara ya kupendana hadi kifo.Patrick ni kila kitu kwangu na sintamuacha kamwe” akawaza Savanna halafu akaibusu ile pete
“Nimepata jibu.taarifa hizi zote atakuwa amepewa na George.Ni yeye pekee anayefahamu kila kitu kuhusiana na kinachoendelea kati yangu na Patrick.Aliahidi kufanya kila linalowezekana ili kuhakikisha kamba mimi na Patrick hatuwi pamoja tena.Hata hivyo anajidanganya na hawezi kamwe kuizuia mipango yangu.Hata kama ikitokea bahati mbaya nikashindwa kufanikisha mipango yangu ya kuwa na Patrick tena,itakuwa vyema kama nitaishi maisha yangu yaliyobakia bila ya kuwa na mwenzi kuliko kuwa na mtu kama George.Nimekwisha mtoa katika akili yangu na juhudi zake zote za kutaka kuhakikisha kwamba anavuruga mipango yangu kwa matazamio ya kurudiana naye tena ,hazitazaa matunda.Tena ngoja nimuonye asijaribu kupambana na mimi” akawaza Savanna na kuzitafuta namba za George akapiga
“Hallow mpenzi wangu.habari yako.Missing you like crazy my angel…” akasema George mara tu alipopokea simu.Savanna akasonya kwa hasira
“Savanna my love usich………………” kabla hajaendelea Savanna akamkatisha
“Sikiliza George tena naomba unisikilize kwa makini.Sijakupigia simu kutaka kuusikiliza upuuzi wako.Ninataka kukueleza jambo moja tu.Hongera sana,juhudi zako nimeziona.Yote uliyomwambia Happy nimeyasikia.Pamoja na hayo naomba nikwambie kitu kimoja,stay away from me,far away from my life,forget that I exist.Naomba unifute kabisa katika akili yako na usitegemee kwamba siku moja mimi na wewe tutakuwa wapenzi .It’s over George.Huna nafasi tena kwangu.I don’t love you and I never loved you.Ni heri nikaolewa na shetani kuliko kuwa na mtu kama wewe” akasema Savanna
“Savanna..!!!” George akataka kutamka neno lakini Savanna akamzuia.
“Subiri nimalize George.” Akasema Savanna kwa ukali
“Ninakuonya George kwamba usijaribu kushindana na mimi .Kama unahitaji kunifahamu vizuri basi endelea kufuatilia maisha yangu.” Akafoka Savanna na kukata simu.
“Si George ,Happy wala mtu yeyote anayeweza kunizuia kuwa na Patrick.I’ll do everything ,I mean everything to be with Patrick again” akawaza Savanna na kuwasha gari akaendelea na safari yake
“Hii ni vita na inanibidi kupambana.Patrick ni mwanaume ninayempenda na nitahakikisha ninashinda vita hii ya kumgombania.Najua akili yake iko kwa Happy lakini nitafanya kila linalowezekana ili kuiharibu taswira ya Happy kichwani mwake.” Akawaza Savanna .
Mara tu alipomaliza kuongea na Savanna simuni,George akampigia simu Happy.Uso wake ulikuwa umejikunja kwa hasira.
“Hallo naongea na Happy ? akauliza George baada ya simu yake kupokelewa
“Ndiyo George.Happy hapa ninaongea’
“Happy umefanya nini? Kwa nini umemueleza Savanna yale mambo niliyokueleza? Tulikubaliana iwe ni siri yetu mimi na wewe.Kwa nini umekiuka makubaliano yetu? Akasema George kwa ukali
“George nimeshindwa kuvumilia.Patrick ni mtu wangu na nimeshindwa kuvumilia kuona kuna mtu mwingine akiwa katika jitihada za kutaka kumchukua.Nimeamua kumueleza ukweli Savanna ili aachane kabisa na mipango yake.” Akasema Happy
“Happy umekosea sana.Umefanya kosa kubwa sana.Umeharibu kila kitu.Umeniharibia kabisa mimi .Savanna ndiye mwanamke ninayempenda kuliko wote na kwa maneno uliyomwambia umezidi kumuweka mbali nami zaidi.Sikutegemea kama ungeweza kufanya jambo la kijinga kama hili…Unadhani kwa kumweleza ukweli Savanna utamzuia aachane na Patrick? Unajidanganya Happy umezidi kujiweka katika sehemu mbaya na usipoangalia hata huyo Patrick utabaki unamsikia tu.Kwa nini ukakurupuka bila kuuliza Happy???Nilikuona ni mtu mwenye akili kumbe ni mjinga kiasi hiki…..”
Happy hakumpa nafasi George ya kuendelea kuongea akakata simu.
“ Stupid !!!....” akasema kwa hasira
“Its gonna take a lot to drag me away from you.
There ‘s nothing that 100 men or more could ever do
Just like the rain down in Africa
Its gonna take some time but I know you’re worth fighting for
I’d fight for you
Eh ba bam ba eh eh ba bam baeh
I’d fight for you
Eh ba bam ba eh eh ba bam ba eh
I’ d fight for you
Let’s go
Friends are coolCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
But we both know
They don’t wanna see us together
Don’t wanna lose what I live for
I’m with willing to do whatever
Cause I don’t wanna see you cry
Give our love another chance
I bet we get it right this time
As long as youre prepared to fight,prepared to fight
I don’t wanna live another day
Without your body next to me
I’m not gonna let them break us down
Cause baby I know now,know now
If you got someone that’s worth fighting for .let no body hold you down.
Let me hear say whoa—oh – oh--oh
And if you you found someone that’s worth dying for
The one you cant live without
let me hear say whoa –oh—whoa
Wimbo huu ulioimbwa na Jason De Rulo ndio uliokuwa ukisika chumbani kwa Happy asubuhi hii..Kuonyesha ni namna gani wimbo ule ulivyokuwa umemgusa Happy alikuwa akiimba akienda sambamba na mashairi haya yenye ujumbe mzito.
Saa ya ukutani ilionyesha ni saa mbili na dakika kumi na nane za asubuhi.Happy bado alikuwa mbele ya kioo kikubwa cha meza yake iliyosheheni vipodozi vya kila aina.Siku hii ya leo alidamka mapema sana na aliutumia muda mrefu katika kujiandaa.Baada ya kuhakikisha kwamba amejipodoa vya kutosha akaenda katika kioo kikubwa cha kujitazamia mwili mzima ,akajitazama na kutabasamu
“Sipendi kujisifu lakini mimi ni mzuri.Yule Kunguru Savanna,hafikii hata robo ya uzuri wangu.” Akawaza Happy huku akiendelea kujitazama katika kioo.Siku hii ya leo alikuwa amevaa suruali ya jeans ya rangi nyeupe iliyomkaa vyema aliyoiambatanisha na shati jeupe lenye nakshi za kuvutia.Chini alivaa viatu virefu vyeupe.Hakika kama ungefanikiwa kumuona Happy siku hii ya leo ungekubali kwamba alistahili kuwa mrembo wa Taifa.
Akiwa katika harakati za kutaka kutoka mle chumbani mara mlango wa chumba chake ukafunguliwa na akaingia mama yake.
“Wow ! mama .!Shikamoo.”
“Marahaba mwanangu ,unaendeleaje?
“Ninaendelea vizuri mama”.
“Happy una haraka sana?
“Ndiyo mama..kuna tatizo lolote?
“Kuna jambo nilitaka kuongea nawe”
“Mama kuna mahala ninawahi lakini nitarejea baada ya muda mfupi. Tutakuja kuongea nikirudi mama” akasema Happy na kuchukua mkoba wake mweupe na kutoka mle chumbani akaingia katika gari lake na kuondoka.Hakutaka kumueleza mtu yeyote alikokuwa anaelekea.
“Its gonna take a lot to drag me away from you.
There‘s nothing that 100 men or more could ever do
Just like the rain down in Africa
Its gonna take some time but I know you’re worth fighting for”
Mashairi ya wimbo huu alioupenda Happy yalimfanya atikise kichwa huku akifuatilizia na kuimba taratibu.Alikuwa akiutumia mkono wake wa kushoto kuendesha gari huku mkono wake wa kulia akiwa ameuegemeza dirishani.Alikuwa analivuka daraja la kigamboni kuelekea Uwangwa prison kuonana na Patrick
“Nimewahi sana leo.Natumai muda huu Savanna bado hajafika.Naomba Mungu iwe hivyo na mimi nifike kabla yake.Nataka atakapofika akute tayari nimekwisha ongea na Patrick na kuanzia leo asimame kuisimamia kesi ya Parick.Ni Patrick pekee mwenye uwezo wa kumsimamisha Savanna asiendelee kumtetea.Nina imani atakubaliana na hoja zangu kwa sababu mimi ndiye mwanamke pekee anayenipenda na nimejaa katika akili yake.Nitakuwa tayari kulipa kiasi chochote cha pesa kwa wakili mwingine ili aendelee kumtetea Patrick mahakamani na si Savanna.” Akawaza Happy huku gari likienda kwa kasi kubwa.
Saa nne kasoro dakika saba ilimkuta Happy katika gereza la Uwangwa.Alisalimiana na askari kadhaa waliokuwepo mapokezi.Tayari walikwisha anza kumfahamu hivyo alishughulikiwa haraka haraka kukamilisha taratibu za kuonana na mahabusu wake .Siku hii ya leo alimkuta askari mmoja aliyemsaidia na kumpeleka katika sehemu ya tofauti na ile iliyozoeleka ambayo hutumiwa na kila mtu ajaye kumuona mahabusu.Sehemu hii aliyopelekwa Happy ilikuwa nzuri na ilifaa hata kwa maongezi ya faragha.Baada ya dakika kama kumi hivi Patrick akaletwa na alipogonganisha macho yake na Happy akaachia tabasamu kubwa.
“Ouh my angel..!!!” akasema Patrick
“Patrick..!!!” akasema Happy kwa furaha huku akiinuka kitini na kumkumbatia.
“Mama una dakika thelathini za kuongea na mtu wako” akasema askari aliyekuwa ameambatana na Patrick
“Ahsante sana” akasema Happy kisha akakumbatiana na Patrick.
“Nimefurahi sana kukuona malaika wangu” akasema Patrick kwa furaha halafu akaipeleka mikono yake yote miwili kichwani kwa Happy wakaangaliana kwa sekunde kadhaa halafu wakapeana busu zito na kukumbatiana tena
“Ouh my angel,I was dying to see you” akasema Patrick huku akiketi kitini.
“Patrick my love,before coming here I felt like I was dead but now I feel alive “ akasema Happy
“Ouh Happy usihofu kitu malaika wangu.Mimi ni mzima ninaendelea vizuri sana.Nitashinda hii kesi na nitakuwa huru tena” akasema Patrick
Happy akatabasamu na kuufungua mfuko aliokuwa amekuja nao uliokuwa umesheheni vitu mbali mbali alivyokuwa amemchukulia mpenzi wake.
“Ahsante sana mpenzi wangu kwa kunijali” akasema Patrick.Happy hakujibu kitu akatabasamu.Kimya kifupi kikapita wakati Patrick akiendelea kunywa juisi aliyoletewa na Happy
“Jana ulifika mahakamani? Akauliza Patrick
“Ndiyo nilifika na nilikuwamo katika chumba cha mashtaka .Usingeweza kuniona kwa sababu nilikuwa nimekaa mwisho kabisa.Hata hivyo nilitoka wakati wanasheria wakivutana baada ya kugundua kwamba kuna watu walikuwa wakinitazama vibaya sana.Nahisi watakuwa ni ndugu zako au wa Vero.Sikutaka kuwakwaza ikanilazimu kutoka nje.” Akasema Happy
“Pole sana Happy.Najua kwa wakati huu baadhi ya ndugu zangu na familia nzima hawatakuangalia kwa jicho zuri wakiamini kwamba wewe ndiye chanzo cha haya yoye.Kaza moyo na usiwajali .Elekeza akili yako katika ndoto yetu ya kuwa pamoja.Kesi hii nitashinda na nitakuwa huru na ndoto yetu ya siku nyingi ya kuwa pamoja itatimia.Ninamuamini Savanna,ana uwezo na uzoefu mkubwa katika kusimamia kesi kama hizi na amenihakikishia kwamba lazima atashinda kesi hii” akasema Patrick .Happy aliposikia jina la Savanna likitajwa na kumwagiwa sifa akabadilika ghafla na kuinama chini.Patrick akaendelea kunywa juisi .
“Patrick..!!” akaita Happy
“Yes my angel “ akaitika Patrick.Happy akamtazama usoni kwa sekunde kadhaa na kusema
“Umefahamiana lini na Savanna?
“Savanna ni rafiki yangu wa muda mrefu.Tumefahamiana miaka mingi iliyopita”
“Ouh Okk.! “ akajibu Happy.Patrick akamuangalia Happy usoni na kugundua Hakuwa sawa.
“Happy kuna kitu gani kinakusumbua leo mpenzi wangu? Nakuona kama hauko sawa.Halafu kwa nini umeniuliza kuhusiana na Savanna?
“Usihofu Patrick.Mimi niko sawa kabisa na sina tatizo lolote.Nilihitaji tu kumfahamu Savanna vizuri”
“Happy whats going on? Akauliza Patrick.Happy akainama chini kwa sekunde kadhaa na kisha akainua kichwa na kusema
“Patrick I know you love me”
“Yes I I love you so much”
“As much as you love me you’ll never lie to me” akasema Happy na kuzidi kumshangaza Patrick
“Happy una tatizo gani leo? Akauliza Patrick
“Patrick wewe na Savanna mmewahi kuwa wapenzi? Akauliza Happy.Patrick aliyekuwa ameshika boksi la juisi akastuka na kuliweka mezani akamtazama Happy
“Happy are you ok today?
“I’m ok Patrick.Just answer my question” Patrick akaendelea kumtazama Happy halafu akasema
“Hapana .Mimi na Savanna ni marafiki na hatujawahi kuwa wapenzi”.
Patrick akavuta pumzi ndefu baada ya kumpa Happy jibu lile.Kimya cha sekunde kadhaa kikapita wakabaki wanatazamana.
“Are you sure Patrick?
“Yes I’m sure.Happy kuna kitu gani kinakusumbua leo?
Happy akatoa kitambaa na kujifuta jasho.
“I know down deep in your heart you know exactly that you are lying to me.” Akasema Happy.Patrick akahisi kuchanganyikiwa.
“Happy nimekwambia ukweli mtupu na siwezi kukudanganya malaika wangu”
“Patrick muda niliopewa ni mdogo sana na si lengo langu kuanza kubishana nawe.Ninaomba tu ufahamu kwamba ninaufahamu ukweli wote kwamba wewe na Savanna mliwahi kuwa wapenzi wakati ukiwa na Veronika na mlitengana baada ya Savanna kumpata bwana aitwaye George.Is that true? Akasema Happy.Patrick midomo ilikuwa inamtetemeka.
“Unakumbuka tukiwa Arusha niliwahi kukuhoji kuhusu yale maneno P&S yaliyoko katika pete yako na ukaniambia kwamba hayana maana yoyote? Ukweli ni kwamba maneno yale yanamaanisha Patrick na Savan.Maneno haya yapo pia katika pete na mkufu wa Savanna.” Akasema Happy.Patrick jasho lilikuwa linamtoka
“Savanna bado anakupenda sana na kwa taarifa yako ana mpango wa kuitumia kesi hii kuwa chanzo cha wewe na yeye kurudiana na kuwa wapenzi tena na ndiyo maana amejitolea hata kuifanya kazi hii ya uwakili bure kabisa.Hii ni sababu iliyosababisha aachane na mumewe akiamini kwamba atarudiana na wewe”
Patrick jasho liliendelea kumtiririka.Happy akainuka ,akamfuta jasho kwa kitambaa chake.
“Happy mambo haya yote umeyatoa wapi? Nani aliy………………..” akataka kuuliza Patrick lakini Happy akamzuia
“Patrick hakuna haja ya kuanza kupoteza muda wa kuelezana mambo haya nimeyajua vipi.Kitu pekee ambacho unapaswa kukifahamu na kukizingatia ni kwamba wewe ndiye maisha yangu ,furaha yangu,pumzi yangu na kila kitu changu.Ninakupenda Patrick zaidi ya ninavyoweza kueleza.Usihofu kuhusu haya niliyokueleza,nilitaka tu ufahamu kwamba ulifanya kosa kuwa na mahusiano ya siri wakati ukiwa na Veronika.Sina hakika kama unaweza ukanifanyia mimi jambo kama hilo kwa sababu endapo nikigundua kwamba una mahusiano nje ya uhusiano wetu ,Patrick I swer I‘m gonna kill you and kill myself.You are mine alone.Anyway tuachane na hayo ni mambo yaliyopita na hayana nafasi kwa sasa.Ila kuna jambo moja ninaloliomba toka kwako”
“Jambo gani hilo Happy?
“I want Savanna out of this case.”
Patrick alihisi kama kuishiwa nguvu ,akabaki anamtazama Happy asijue aseme nini.
“Happy…..!!” Patrick akataka kusema kitu lakini Happy akamzuia
“Patrick you are my angel,my everything.Uko hapa ndani kwa sababu yangu,kwa sababu ya upendo wako kwangu.Patrick hicho ni kitu pekee ninachokuomba mpenzi wangu.Nataka Savanna aachane kabisa na kesi hii .Mimi niko tayari kumtafuta wakili mwingine mahiri ambaye ataendelea kukutetea mahakamani lakini si Savanna.Siko tayari kukupoteza Patrick.” akasema Happy.Patrick akainama akatafakari na kusema
“Happy napenda nichukue nafasi hii kwanza kukuomba msamaha kwanza kwa kusema uongo pale uliponiuliza kama niliwahi kuwa na mahusiano na Savanna.Ni kweli niliwahi kuwa na mahusiano na Savanna lakini tulisitisha mahusiano yetu pale yeye alipompata George.Toka wakati huo tumeendelea kuwa marafiki wa kawaida.Tumekuwa tukisaidiana katika mambo mengi na ndiyo maana hata katika kesi hii Savanna ananisimamia kama rafiki na mtu wake wa karibu na si kama mpenzi wake.Savanna ni mwanasheria aliyebobea na mzoefu katika kesi kubwa kama hizi.Amekuwa akisimamamia kesi kubwa kubwa na hajawahi kushindwa.Tafadhali nakuomba uniamini Happy kwamba hakuna kinachoendelea kati yangu na Savanna kwa sasa zaidi ya urafiki wa kawaida.Nakuomba Savanna uniamini kwamba ni Savanna pekee ambaye anaweza kuniweka huru.Naomba tusimuondoe katika kesi hii” akasema Patrick kwa sauti ndogo
“Patrick nakuelewa na sina tatizo na uwezo wa Savanna..Najua unamuamini sana na ni wakili mzoefu na mbobezi wa sheria.Ninachotaka kukiepuka mimi ni kupigana vita ya pili kati yangu na Savanna.Wewe ni mwanaume wangu wa pekee na niko tayari kufanya jambo lolote lile kwa ajili yako na ndiyo maana nimeamua kuachana na kila kitu kwa ajili yako kwa hiyo atakapotokea mwanamke ambaye atatishia usalama wa penzi langu nawe lazima nipambane naye.Sitaki kupambana na Savanna na ndiyo maana ninataka umuondoe katika kesi hii.Mimi niko tayari kulipa gharama za wakili hata zaidi ya mmoja.Najua Savanna anakupenda na yeye atafanya kila linalowezekana ili aweze kunitenganisha nawe.tafadhali Patrick naomba unikubalie jambo hili moja tu.” Akasema Happy
“ Happy nimekuelewa unachokisema na mimi niko radhi kufanya chochote kile kwa ajili yako na ndiyo maana niko hapa gerezani muda huu.Pamoja na yote uliyonieleza bado sijaona sababu ya msingi yakumuondoa Savanna katika kesi yangu.Naomba Happy muache Savanna aendelee kunisimamia mahakamani”
“Patrick umejitolea kuibeba adhabu yangu kwa sababu ya upendo wako mkubwa kwangu.Sina cha kuweza kukulipa kulingana na thamani ya upendo wako kwangu.Please Patrick allow me to do at least one thing for you.Allow me to hire another lawyer for you to replace Savanna.” Happy akaendelea kusisitiza
“Happy najitahidi sana kupingana na nafsi yangu kuhusiana na suala hilo unalolitaka.Najitahidi kutaka kukubaliana nawe lakini bado moyo wangu unakataa kabisa.Najua una lengo zuri la kutaka kunisaidia lakini sina hakika kama uamuzi wa kumuondoa Savanna ni uamuzi unaofaa kwa sasa.Nahitaji kutoka humu gerezani,nahitaji kushinda kesi ili niwezi kuitimiza ndoto yangu ya kuwa nawe na hilo litawezekana tu kama Savanna ataendelea kuisimamia kesi hii.Endapo tutaamua vinginevyo basi ndoto zangu zote za kuwa nawe zitapotea kwa sababu nitapotelea gerezani”
“Patrick huwezi kupotelea gerezani.I give you my word.Nitamtafuta wakili mahiri kabisa na hata zaidi ya mmoja kama itahitajika.” Happy akaendelea kuusimamia msimamo wake bila kutetereka.Patrick akainama akafikiri kidogo na kusema
“Happy hilo ni jambo lisilowezekana hata kidogo.” Happy machozi yakamlenga
“You are still in love with her,right? Akauliza Happy
“Si hivyo unavyofikiri Happy “
“Nijibu Patrick.Bado unampenda Savanna? Kwa sababu yake hauko tayari hata kunisikiliza mimi mpenzi wako” akasema Happy huku machozi yakimtoka na mara mlango ukafunguliwa na wote wakapigwa na butwaa baada ya kumuona mtu aliyesimama mlangoni.Alikuwa ni Savanna.Nyuma yake alikuwepo Andrew ,rafiki mkubwa wa Patrick ,Alois kaka wa Patrick aliyeongozana na mke wake na pamoja nao alikuwepo mama yake Patrick.
Happy akahisi mwili wote unamtetemeka.Akakosa neno la kusema.Savanna akawaongoza watu aliokuja nao wakaingia mle chumbani.Mama yake Patrick nusura aanguke kwa mstuko baada ya kuingia mle chumbani na kugonganisha macho yake na Happy
“Wewe ..!!!” akasema kwa sauti yenye mshangao.Hakuwa ametegemea kama angekutana na Happy mahala pale.Happy alikuwa anatetemeka kwa woga namna alivyokuwa anaangaliwa kwa jicho la chuki.
“Shikam…….” Happy akataka kumsalimu mama yake Patrick lakini kabla hajamaliza salamu yake akazuiwa.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Haraka sana toka nje” akasema kwa ukali mama yake Patrick.
“Mama ..!!! Patrick akataka kusema jambo lakini naye akazuiwa
Kwa Haraka Happy akauchukua mkoba wake uliokuwa kitini .Machozi yalikuwa yanamtoka akaanza kupiga hatua kuondoka.
“Na iwe ni mara ya mwanzo na ya mwisho kufika hapa.Sitaki kukuona tena karibu na mwanangu shetani wewe.Kila mara unapokaa karibu na mwanangu lazima jambo baya limfike.Una laana wewe mtoto na ndiyo maana mambo mabaya yanakukuta kila wakati.” Akasema kwa ukali mama yake Patrick
“Basi mama imetosha.Usiongee sana utasababisha matatizo mengine” akasema Alois
“Na wewe Patrick naomba ukae mbali kabisa na huyu mwanamke.Sitaki kuona ukiwa karibu naye.Yeye ndiye chanzo cha haya matatizo yote” Akaendelea kufoka mama yake Patrick.
“Patrick nimekuletea wageni” akasema Savanna baada ya hali kutulia mle chumbani
Patrick akasalimiana na mama yake pamoja na ndugu zake.Waliongea mambo mengi na kumpa moyo kuhusiana na kesi inayomkabili.Baada ya maongezi yao yaliyochukua zaidi ya nusu saa wakaaga na kuondoka.Ni Savanna pekee aliyebaki.
“Patrick unajisikiaje leo kwa kuonana tena na ndugu zako na hasa mama? Akauliza Savanna
“Nimefurahi sana kuonana nao tena,nimefarijika sana.Ahsante Savanna kwa kuwaleta.Pamoja na ujio wao lakini bado kichwa changu hakiko sawa” akasema Patrick.Savanna akamuangalia kwa makini na kusema
“Its because of her,right? Amekwambia nini Happy?
Patrick akafikiri kidogo na kusema
“Tayari anafahamu kwamba mimi na wewe tuliwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi.”
“Hata mimi alinipigia simu jana na kunieleza kuhusu suala hilo na sikuweza kukataa kwa sababu alikwisha elezwa kila kitu na George.Happy alinitukana sana na kusema kwamba atahakikisha ninaondolewa katika kesi yako.Nadhani hilo ni jambo mojawapo lililomleta kwako asubuhi hii.She wanted me out,right?
“Ni kweli Savanna.Happy alinitaka nikuondoe katika kesi yangu na nitafute mawakili wengine”
“wewe umemjibu nini?
“Siwezi kufanya jambo la kipuuzi kama hilo.” Akasema Patrick
“Kwa nini hujamsikiliza mpenzi wako Patrick.Kwa nini hujamtimizia alichokuomba? Akauliza Savanna
“kwa sababu nakuamini Savanna.Umejitolea kunitetea na ninaamini kwamba nitashinda kesi.Hakuna mtu anayeweza kunishauri nikutoe katika kesi hii.”
Savanna akatabasamu baada ya kauli ile ya Patrick.
“Nilikwambia Happy,mipango yako kamwe haitaweza kufanikiwa.Nilikuonya kwamba Patrick hawezi akakusikiliza .Na huu ni mwanzo tu.Ulitaka mapambano na mimi na sasa utaiona nguvu yangu “ akawaza Savanna
“So is that true? akauliza Patrick
“Is what true?
“kwamba umeachana na George.
“Yah..its true.” Savanna akajibu
“Samahani Patrick kwa kutokufahamisha kuhusu jambo hili kwa sababu halikuwa na umuhimu wowote”
“Sababu gani iliyopelekea mkaachana? Akauliza Patrick
“George alinitaka niachane na kesi yako.Aliogopa kwamba kesi hii ingeweza kutuweka karibu muda mwingi kwa hiyo akahofu kwamba pengine tunaweza kujikuta tukirejesha mahusiano yetu ya zamani.Sikuwa tayari kuachana na kesi yako kama alivyotaka George kwa hiyo tukaachana.Patrick niko tayari hata kutengana na dunia nzima lakini si kukuacha katika kipindi hiki kigumu.Hakuna mtu yeyote chini ya jua zaidi yako wewe mwenyewe anayeweza kunizuia nisikutetee.” Akasema Savanna
“Ahsante sana Savanna kwa kunithamini namna hii.Sina kitu cha kukulipa kwa wema wako huu mkubwa.Tafadhali fanya kila linalowezekana ili uweze kuniondoa katika kesi hii”
“Patrick usihofu.Nitafanya kila linalowezekana na kukuweka huru.naomba uniamini.I’ll fight till you get free.I give you my word” akasema Savanna na kumfanya Patrick atabasamu
“Ahsante sana Savanna” akasema Patrick
Ilimchukua Happy zaidi ya dakika kumi kutulia na kuwasha gari.Mikono yake ilikuwa inamtetemeka. Kitambaa chake cha mkononi kilikuwa kimeloa machozi.Hatimaye akawasha gari na kuondoka maeneo yale ya mahakamani.
“Na iwe ni mara ya mwanzo na ya mwisho kufika hapa.Sitaki kukuona tena karibu na mwanangu shetani wewe.Kila mara unapokaa karibu na mwanangu lazima jambo baya limfike.Una laana wewe mtoto na ndiyo maana mambo mabaya yanakukuta kila wakati”
Maneno haya ya mama yake Patrick,yalikuwa yanajirudia kichwani kwa Happy na kumfanya aangushe machozi huku akiendesha gari.
“Kwa mara ya kwanza ninajuta ni kwa nini nilionana tena na Patrick.Nadhani ingekuwa vyema kama Patrick asingejitokeza tena katika maisha yangu.Nilikuwa na maisha yangu mazuri na yenye furaha na Mike.Sikutegema hata siku moja kama siku moja ningekuja kuwa na wakati mgumu namna hii.Toka nilipoonana na Patrick maisha yangu yamebadilika ghafla.Ndoto zangu zote za maisha nilizokuwa nazo zimepotea.Mateso na maumivu ya moyo hayaishi.Nimekuwa ni mtu wa kulia kila siku.maisha yangu yamepoteza mwelekeo” akawaza Happy huku akipunguza mwendo wa gari na kufuta machozi
“Una laana wewe mtoto na ndiyo maana mambo mabaya yanakukuta kila wakati.”
Maneno ya mama yake Patrick yakazidi kujirudia kichwani mwa Happy
“Inawezekana ni kweli nina laana na ndiyo maana mambo yangu hayafanikiwa.lakini ni kwa nini hunikuta nikiwa na Patrick pekee? Miaka hii yote niliyokuwa na Mike sijawahi kuangusha hata chozi”.Happy akajiuliza na kushindwa kupata jibu.Sura ya mama yake Patrick akimtazama kwa macho makali yaliyojaa chuki ikamjia kichwani.
“Kila nikiikumbuka sura ya Yule mama mwili unatetemeka.Macho yake yalionyesha dhahiri ni namna gani anavyonichukia.Nimeogopa sana na sijui nitawezaje tena kuonana na Patrick .Kwa sasa itanibidi nijitahidi kwa kila namna nitakavyoweza kuikwepa familia ya Patrick kwani kwao mimi ni adui wao namba moja” Happy alikuwa amezama katika mawazo mazito.Alikuwa analivuka daraja la Kigamboni.
Wakati akiendelea na safari yake huku kichwa chake kikiwa kizito kwa mawazo mengi aliyokuwa nayo,mita kama mia moja hivi nyuma yake gari mbili zilikuwa zinakuja kwa kasi.Gari zile zilionekana kana kwamba zilikuwa zinafukuzana.Happy aliziangalia kupitia kioo cha pembeni lakini hakuzitilia maanani.Gari zile zikafika usawa wa gari la Happy na zote mbili zikawa kama zinataka kupishana kwa wakati mmoja.Gari lililotaka kupitwa likasogea karibu sana na gari la Happy kitendo kilichomstua na kabla hajafanya chochote gari lake likakwaruzwa ubavuni.Happy akataharuki na kufunga breki ya ghafla .Kwa bahati nzuri hakuwa katika mwendo mkali.Gari lililomkwaruza ubavuni nalo likasimama mbele yake.Happy akashuka kwa hasira na kutazama gari lake lilivyokwaruzwa.Kwa hasira akaelekea katika gari lililomkwaruza ambalo lilisimama mita chache toka aliposimamisha gari lake.Milango ya gari lile ikafunguliwa na wakashuka watu watatu mwanadada mmoja na wanaume wawili.
“You people don’t you know how to drive?? !!....” akafoka Happy
“Samahani sana dada.Hatukutegemea kama tungeweza kukukwaruza.Nilikuwa najaribu kumkwepa Yule jamaa” akasema mmoja wa wale jamaa huku akimuelekezea jamaa mmoja aliyevaa suruali nyeusi na fulana nyeupe aliyekuwa akiwaelekea
“Nasema hivi,sitaki kesi wala mjadala wowote.Nahitaji gari langu likatengenezwe.” Akaendelea kufoka Happy
“Usihofu madam,wenye makosa ni sisi na tunaomba tugharamie matengenezo ya gari lako na hata kukupatia gari lingine la kutembelea wakati gari lako linatengezwa mahala lilipokwaruzwa”
“Nimesema sihitaji kitu chochote ninachotaka ni gari langu litengenezwe haraka sana” akaendelea kufoka Happy Muda huo huo jamaa mmoja mnene akiongozana na vijana wawili akafika eneo la tukio”
“Dada samahani sana kwa tatizo lililotokea,naomba tusipoteze wakati,tuelekee gereji gari lako likatengenezwe” akasema yula jamaa mnene.Happy akaanza kupiga hatua kurejea katika gari lake lakini Yule jamaa akamzuia
“Hapana panda gari hili” Happy akageuka kwa hasira .Hakuamini macho yake kwa alichokiona.Alikuwa anatazamana na midomo miwili ya bastora.Kijasho kikamtoka,mwili mzima ukamtetemeka.
“Taratibu bila ubishi ingia ndani ya gari hili.Usitulazimishe tutumie nguvu” akaamuru Yule jamaa.Huku akitetemeka Happy akajikaza na kuuliza
“What’s going on here? What’s the meaning of this?
“Get in the car ,now !! akafoka Yule jamaa mnene.Bado miguu ya Happy ilikuwa mizito sana kunyanyuka.Hakuamini kilichotokea aliona ni kama njozi.
Kwa haraka mwanadada aliyekuwa ameongozana na watu wale akamfuata Happy na kumnong’oneza kitu sikioni halafu akamshika mkono na kumuingiza katika gari lile aliloamriwa kupanda.Haraka haraka wakarejea katika magari yao na kijana mmoja akaenda katika gari la Happy.Magari yakawashwa na kuondoka eneo lile.Kitendo kile hakikuchukua zaidi ya dakika kumi.
* * * *
Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuwaona watu wale waliokuwamo garini.Hakuwafahamu na wala hakufahamu lengo la wao kumtaka aongozane nao.Mapigo ya moyo wake yalikuwa yanaenda kwa kasi ya ajabu na jasho jingi lilimtiririka na kuloanisha shati lake jepesi.
“Mungu wangu mambo gani haya yananitokea tena ? Watu hawa ni akina nani na wanataka nini kwangu? Happy akawaza huku machozi yakimtoka.
“Jamani mnanipeleka wapi? Naombeni msinidhuru tafadhali.Nitawapa kiasi chochote cha pesa mtakachokihitaji” Akalia Happy
“Shut up !!! akafoka jamaa aliyekuwa amekaa pembeni yake.Happy alikuwa amewekwa kati kati ,mikononi alifungwa pingu.Gari lilikuwa linakwenda kwa kasi kubwa na kabla ya kulimaliza daraja la kigamboni jamaa mmoja aliyekuwa amekaa mbele pembeni ya dereva akapokea simu na kuongea kwa takribani dakika mbili halafu akawageukia wale waliokuwa wamekaa kiti cha nyuma ,akawafanyia ishara Fulani na kwa haraka wale jamaa wakamfunga Happy kitamba cheusi usoni na hakuweza kuona chochote tena.Bado aliendelea kulia akiomba aachiwe huru lakini hakuna mtu hata mmoja aliyemjali na kumsikiliza.gari lilianza kukata mitaa ya jiji .Happy hakuweza kutambua ni wapi walikokuwa wanaelekea .
Katika gari iliyokuwa imetangulia mbele,kijana mmoja mwembamba mrefu alikuwa anatabasamu kwa furaha wakati akiongea na simu.Alipomaliza kuzungumza na simu akamgeukia dereva wake
“Sasa ngoja nimpigie simu Loniki nimtaarifu kwamba mtu wake tayari tumekwisha mtia mikononi.” Akasema na kuzitafuta namba za simu la Loniki na kumpigia
“Hallow Khumalo” akasema Loniki baada ya kupokea simu
“Hallo Loniki ,habari yako.Uko wapi mida hii?
“Kwa sasa niko saluni natengeneza kucha”
“Lonny nimekupigia simu kukutaarifu kwamba Happy tayari tumemtia mikononi mwetu na hivi sasa tunaelekea mahala kazi itakapofanyikia.Nitakutaarifu baadae ni wapi tumempeleka ili ushuhudie namna atakavyofanyiwa”
“Wow !! that’s wonderful.Thats good news” akasema Loniki kwa furaha
“One more thing lonny,hatutakiwi kumuweka mafichoni kwa muda mrefu sana.Kila kitu kinatakiwa kifanyike usiku wa leo na halafu tumuache huru.Ukumbuke vile vile kuja na kiasi cha pesa kilichobakia.Jambo la mwisho vijana wanataka uwaongeze shilingi million ishirini ili waweze kuendelea kutoa ushirikiano katika kazi iliyobaki.Kwa kweli vijana wamefanya kazi kubwa na ya kitaalamu sana kiasi kwamba tumemchukua Happy bila ya rabsha wala mtu yeyote kugundua kwa maana hiyo basi vijana wanahitaji motisha ili waendelee kuwa na ari ya kazi.”
“Twenty million more …!!!!???. Loniki akastuka
“yes Lonny vijana wanataka uwaongeze kiasi hicho”
“Khumalo hatukupatana hivyo na wala hatukukubaliana kuongeza kiasi chochote cha pesa zaidi ya kile cha million hamsini tulichopatana.Hizo million ishirini unazozisema nitazipata wapi sasa hivi? Its a lot of money” akasema Loniki
“Sikiliza Lonny.tusiendelee kubishana kuhusu suala hilo.Ulitupa kazi ya kufanya tumekwisha ifanya tayari lakini kutokana na ugumu wa kazi yenyewe vijana wanataka uwaongeze kiasi hicho cha pesa ili kazi yako ikamilike.Najua hauko tayari kuona kazi hii kubwa ikiharibika,kwa hiyo jitahidi upate kiasi hicho cha pesa na tutakapoonana jioni ya leo utukabidhi.”
“Khumalo that’s unfair” akasema Loniki
“Lonny find that money.Mpaka jioni ya leo kama hutakuwa umezipata ,nitamuachia Happy” akasema Khumalo na kukata simu.Uso wake ukapambwa na tabasamu kubwa.Bado akiwa na simu yake mkononi akazitafuta namba za Linah na kumpigia
“Hallow Linah” akasema Khumalo
“Khumalo vipi maendeleo?
“Kila kitu kinakwenda vizuri.Tayari Happy tunaye na kwa sasa tunampeleka mafichoni.Nimempigia simu Lonny na kumwambia kwamba aongeze milioni ishirini na kama akishindwa kuzipata fedha hizo hadi jioni ya leo basi nitamuachia Happy.Nina uhakika atakupigia simu , na kama akifanya hivyo na wewe endelea kumsisititiza ili aweze kuzitafuta hizo fedha.”
“Good job Khumalo.Its time now to make easy money.Kama nilivyokwambia kwamba Lonny ana pesa na nina hakika mpaka jioni ya leo atakuwa amezipata hizo fedha.Hakukuwa na tatizo lolote wakati wa kumkamata Happy?
“Hapana Linah.Tulimchukua kirahisi mno na ni tukio ambalo lilichukua chini ya dakika kumi na hakuna nguvu iliyotumika zaidi ya gari lake kupata mikwaruzo kidogo”
“Vizuri sana khumalo.Nitakuja jioni na Lonny”
“Sawa Linah .Nitamtuma kijana ambaye atakuja kuwachukua jioni na kuwaleta mahala tutakapompeleka Happy”
“Ok Khumalo.Lakini naomba msimuumize Happy.Namuonea huruma sana huyo binti hana kosa lolote”
“Usijali kuhusu hilo.Hakuna mtu atakayempiga hata kofi moja.Atapatiwa kila kitu na hata mimi mwenywe sijisikii vizuri kwa kitendo hiki lakini kwa kuwa kazi hii ina hela nzuri imenilazimu kuifanya tu.See you later Linah.” Akasema Khumalo na kukata simu
“hahahaaaaa..!!! thats why I love Dar es salaam.Its easy to make money in here” akasema Khumalo nakuendelea kucheka halafu akatoa sigara yake akaiwasha na kuvuta.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
* * * *
Mara tu alipomaliza kuongea na Khumalo simuni ,Loniki alihisi kuchanganyikiwa.Haraka haraka akapanda gari na kurejea nyumbani.Alipofika nyumbani akamvuta pembeni mama yake aliyekuwa amekaa na kundi la akina mama waliokuja kumpa pole.
“ Loniki vipi,mbona uko hivyo? Akauliza mama yake
“Mama nina shida”
“Shida gani Lonny?
“Mama nina shida ya pesa”
“Pesa !! mama yake akaonyesha mshangao.Hakuwahi kumsikia hata siku moja Loniki akiwa na shida ya pesa
“Unahitaji kiasi gani cha pesa? Akauliza mama yake
“Nahitaji million ishirini”
“Millioni shirini !!!! mama yake akastuka
“Ndiyo mama”
“Pesa zote hizo za nini Loniki?
“Nina shida nazo kubwa na ya haraka kwa leo.Nimeongea na mume wangu na ameniahidi kunitumia pesa hizo kesho toka London.Kama una kiasi hicho cha pesa naomba uniazime na kesho nitakurejeshea.”
Mama yake akabaki anamuangalia loniki kwa mshangao.
“Mama mbona unanitazama hivyo?
“Nimestushwa na kiasi hicho kikubwa cha pesa.lakini hebu niambie Loniki unataka kuzipeleka wapi fedha zote hizo?
“Mama nina shida nazo sana kwa leo.” Akasema Loniki.Mama yake akafikiri kidogo na kusema
“Kwa sasa bado sijajua nina kiasi gani cha pesa ndani kwani Vero ndiye aliyekuwa meneja wangu.Twende ndani nikaangalie nina kiasi gani “ akasema mama yake na wakaelekea chumbani kwake ,akafungua kabati na kutoa vitita vya pesa wakaanza kuhesabu.
“Millioni kumi na tatu” akasema mama yake wakatazamana
“Bado million saba” akasema Loniki
“Tutatoa wapi hizo zilizobaki? Akauliza mama yake
“Mimi sijui mama.Jaribu kufanya maarifa.” Akasema Loniki
“Jaribu kuongea na mdogo wako Sarah anaweza akakupatia kiasi hicho cha pesa”
“Hapana mama siwezi kufanya hivyo.Tena ninaomba usimweleze chochote kile kuhusiana na pesa hizi.Kama unataka kuazima kwa Sarah,azima kama wewe na asifahamu kama unanipa mimi.” Akasema Lonny.mama yake akachukua simu na kumpigia Sarah.
“Hallow mama” akasema sarah
“Sarah nina shida kidogo mwanangu”
“Shida gani mama?
“Nina shida ya pesa “
Sarah akacheka kidogo aliposikia mama yake anashida ya pesa.
“Mbona unacheka Sarah?
“Ni mara yangu ya kwanza kukusikia ukisema una shida ya pesa”
“Kweli Sarah nina shida ya pesa lakini nitakurejeshea kesho”
“Unahitaji shilingi ngapi mama?
“nahitaji million saba”
“Millioni Saba? !!!!..Sarah akastuka
“Ndiyo sarah.Ninahitaji pesa hizo kwa haraka.Kama unazo naomba uniazime na kesho nitakurejeshea.”
Sarah akavuta pumzi ndefu na kimya kifupi kikapita
“Sarah unaweza ukanisaidia kiasi hicho cha pesa?
“Mama unataka kutumia kwa kazi gani fedha zote hizo?
“Nina mizigo yangu imekwama nataka nikaikomboe.Kesho nitakwenda benki na kukurejeshea pesa zako”
Sarah akafikiri kidogo na kusema
“mama naomba unipe masaa mawili,nitakuletea fedha hizo nyumbani”
“Ahsante sana Sarah” akajibu mama yake na kukata simu
“Sarah atatupatia fedha hizo.Lakini hakikisha kwamba kesho tumepata fedha za kumrudishia ndugu yako”
“Usijali mama kesho nitatumiwa fedha na tutazirejesha fedha za Sarah,ila nakuomba sana Sarah asifahamu lolote kama fedha hizo unanipa mimi.”
“Usihofu Loniki sintamwambia kitu”
“Haya ahsante mama.Niko chumbani kwangu” akasema Loniki na kuinuka akaelekea chumbani kwake.
Baada ya kuingia chumbani kwake akampigia simu Linah na kumuomba amfahamishe Khumalo kwamba tayari amekwisha pata kiasi cha pesa alichokuwa anakihitaji na atampelekea jioni ya siku hiyo kama alivyokuwa ameagiza
* * * *
Bado kitambaa kilikuwa machoni kwa Happy na hakuweza kuona chochote.Hakutambua walikuwa wapi lakini alichojua ni kwamba alikuwa wamefika mahala fulani na gari likasimama.Milango ya gari ikafunguliwa na wale watu wakashuka na kumshusha naye pia.Hakujua alikokuwa anaelekea lakini alihisi kama vile alikuwa anashushwa ngazi.Mara wakafika mahala wakasimama na watu wale wakajadili jambo halafu akasikia milango inafungwa na kitambaa kikatolewa machoni.Happy akajikuta katika chumba kikubwa chenye samani za kuvutia.Kulikuwa na kitanda kikubwa kizuri chenye nakshi,kilichotandikwa mashuka mazuri,.Kulikuwa pia na kabati kubwa la nguo na meza kubwa iliyosheheni vipodozi.Kulikuwa vile vile na runinga kubwa na sofa nzuri za kupendeza..hali ya hewa ilikuwa ni ya ubaridi uliotokana na kiyoyozi.
Happy alikitazama chumba kile halafu akageuza shingo yake na kumgeukia mwanadada aliyesimama mbele yake.
“Mmenileta wapi? Mnataka nini toka kwangu? Nani kawatuma mnilete huku? Happy akauliza maswali mfululizo.Mwanadada yule akatabasamu na kusema
“Usihofu Happy.Hapa uko salama na hakuna tatizo lolote.Jisikie huru na wala usiogope chochote.”
“mnataka nini kwangu? Nani kawatuma mnikamate na kuja kunifungia humu? Niambieni mnataka kiasi gani cha pesa? Familia yangu itatoa” akasema Happy huku machozi yakimtoka
“Relax Happy.Huna haja ya kutoa machozi.Sisi hatuna haja na pesa zako na wala hatujakuleta hapa kukudhuru au kuitaka familia yako itupe pesa” akasema Yule mwanadada
“Kama hamna shida na pesa,kwa nini basi mmeniteka nyara?
“Tumekuleta hapa ,kuna mtu anataka kuongea na wewe”
“Mtu anataka kuongea na mimi? Thats crazy.!!!! Kwa nini mtu huyo asinitafute nikaongea naye hadi awatumie ninyi mniteke na kunileta hapa?
“Happy darling,why don’t you take some rest first? Tumekuandalia kitanda kizuri.Feel at home.Anything you need let me know” akasema Yule mwanadada halafu akainuka sofani na kuufungua mlango mmoja
“Kuna bafu hapa.Ingia uoge ujisikie vizuri.Katika kabati kuna nguo nzuri utabadilisha baada ya kuoga”
“Nimesema sitaki kitu chochote,nataka mniache huru niende zangu.” Akasema Happy kwa ukali
“Huna haja ya kukasirika Happy.Mara tu mtu anayetaka kuongea nawe akifika tutakuacha huru.By the way ninaitwa Rosa” akasema Yule mwanadada.Happy akamtazama kwa hasira halafu akajitupa kitandani
“Mambo gani haya yananitokea mimi? Mbona mikosi inaniandama namna hii? Kabla ya suala moja kumalizika linaibuka lingine.why always me?” akawaza Happy huku machozi yakimtoka
“Watu hawa walionileta hapa ni akina nani ? Huyo mtu anayetaka kuongea na mimi ni nani? Anataka nini kwangu? Ouh Mungu wangu tafadhali naomba unisaidie” akawaza Happy na mara mlango ukafunguliwa na jamaa mmoja mnene akaingia akiwa na sinia la chakula.Happy akamkumbuka alikuwa ni mmoja wa watu waliomteka.Taratibu mtu yule akamsogelea Happy pale kitandani
“How do you feel Happy? Akasema Yule jamaa huku akiliweka sinia lile juu ya meza ndogo
“what do you want from me? Who are you people? Akauliza Happy kwa ukali
“Usihofu Happy.Sisi si watu wabaya na wala hatuna lengo baya nawe.Just relax and eat”
“Sintakula chochote hadi huyo mtu aliyewatuma mniteke na kunileta hapa aje anieleze sababu ya kunileta na kunifungia humu.”Yule jamaa akamtazama Happy usoni halafu akatoka nje.
Sarah aliwasili nyumbani kwako baada ya masaa mawili kama alivyokuwa ameahidi.Katika mkoba wake kulikuwa na kiasi cha shilingi millioni saba alizokuwa ameomba mama yake.Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa mama yake kumuomba msaada wa kiasi kikubwa cha pesa kwa hiyo alifanya kila aliloweza hadi akazipata fedha hizo.
Baada ya kushuka garini moja kwa moja akaelekea sehemu alikokuwa mama yake halafu wakaelekea chumbani akamkabidhi fedha zile
“Mama mzigo huu hapa.Nimelazimika kuzichukua katika akaunti ya mume wangu kwa hiyo kama ulivyoahidi kuzirejesha kesho naomba iwe hivyo” akasema Sarah
“Ahsante sana Sarah.Kesho nitakurejeshea fedha zote”
“Sawa mama,lakini mbona hujaniambia fedha hizo ni kwa ajili ya nini? Umepatwa na tatizo gani?
“Usijali sarah.Ni suala la kawaida katika biashasra zangu” akasema mama yake.Sarah hakutaka maongezi mengi akatoka mle chumbani lakini wakati akitoka akagongana na Loniki ambaye naye alikuwa anaelekea chumbani kwa mama yake.Sarah akapatwa na wasi wasi.
“Whats going on here? kuna kitu gani kinaendelea kati ya mama na Loniki.? Sarah akajiuliza maswali lakini hakutaka kuwafuatilia akaendelea na shughuli zake.Baada ya kama dakika ishirini toka Loniki aingie mle chumbani mwa mama yake mlango ukafunguliwa na wote wawili wakatoka.Sarah akamfuata mama yake
“mama kitu gani kinaendelea kati yako na Loniki?Mna mipango gani ya siri?
“Hakuna kitu chochte kibaya Sara.Kuna masuala Fulani yanayohusiana na biashara zangu ambayo Loniki anakwenda kuyashughulikia.”
“Ni masuala gani hayo mama? Naomba unieleze.”
“Ni masuala yangu ya kibiashara. Mbona maswali yanakuwa mengi Sarah?
“mama nina haki ya kufahamu tatizo lako kama mwanao.Kinachonishangaza ni kwamba miaka hii yote Loniki hakuwepo na tuliokuwa tukikusaidia katika masuala yako mbali mbali ya kibiashara ni mimi na Vero sasa iweje leo uniache mimi na umtumie Lonny?
“Sarah si kila kitu kuhusiana na biashara zangu unapaswa kukifahamu.” Akasema mama yake
“Mama nimetoa pesa zangu nyingi katika tatizo hilo kwa hiyo nina haki ya kujua zinakwenda wapi”
“Sarah inatosha sasa.Nimechoshwa na maswali yako.Umenipa pesa subiri kesho nitakurejeshea pesa zako” Akasema kwa ukali mama yake na kuanza kuondoka lakini Sarah akamuita
“Samahani mama kama nimekuudhi lakini nimekuuliza kwa nia njema tu ya kutaka kufahamu kama una tatizo lolote.Siku zote nimekuwa rafiki yako na hujawahi hata siku moja kunificha tatizo linalokusumbua.Vile vile hata siku moja hujawahi kuniomba pesa na ninafahamu unazo pesa za kutosha toka katika miradi yako .Kitendo hicho kimenistua sana na ndiyo maana nahitaji kufahamu endapo kuna matatizo katika biashara ili kwa pamoja tuone namna ya kuweza kuyaondoa”
“Sarah ahsante sana kwa msaada wako.Kwa sasa tatizo lenyewe limekwisha na endapo nitahitaji msaada zaidi nitakueleza.” Akasema mama yake na kuondoka.Hakutaka tena maongezi na Sarah
“lazima nifahamu Lonny anazipeleka wapi zile pesa.Sina hakika kama mama ana shida ya pesa.Biashara zake zinamuingizia mamilioni ya pesa na hawezi kuwa na shida na millioni saba.Lazima kuna kitu kinaendelea hapa ambacho mama hataki kukiweka wazi.Hata macho yake yanaonyesha kabisa kuna jambo analificha.Taa ya tahadhali inaanza kuwaka kichwani,inaonekana Lonny ameanza kutekeleza mpango wake wa kulipiza kisasi.” Akawaza Sarah
* * * *
Saa kumina mbili za jioni gari aina ya Toyota Surf lenye rangi nyeusi likawasili katika jumba moja la kifahari lenye rangi nyeupe lilizungukwa na miti na maua mazuri
Linah na Loniki wakashuka katika ile gari .Wakiongozwa na kijana aliyetumwa kwenda kuwachukua wakaingia ndani ya jumba lile kubwa la kifahari.Walikaribishwa katika sebule kubwa na nzuri sana na baada ya dakika tano akajitokeza Khumalo.
“Karibuni sana” akasema khumalo huku akiwapa mikono
“Hii ni moja ya makazi yangu pia na mara nyingi hupenda kuja kupumzika huku.Ni watu wachache sana wanaopafahamu mahala hapa? Akasema Khumalo huku akitabasamu na kupuliza moshi wa sigara hewani
“Hongera ,umejitahidi sana Khumalo” akasema Linah
“Ahsante sana” akajibu Khumalo halafu kikapita kimya kifupi ,Khumalo akasema
“Miss Tanzania tuko naye hapa na anaendelea vizuri”
“Kazi nzuri sana Khumalo.Hakukuwa na rabsha zozote wakati wa kumchukua? Akauliza Loniki
“Hapana Loniki.Hakukuwa na tatizo lolote.Tukio hilo limefanywa kitaalamu sana.Natumai umekuja na ule mzigo kamili kama tulivyoongea” akasema Khumalo
“Ndiyo Khumalo.Nimekuja kamili” akasema Loniki na kuufungua mkoba wake akatoa mabunda ya noti akayaweka mezani.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“million thelathini.” Akasema Loniki.Khumalo akayashika mabunda yake akatabasamu
“Mtu wangu yuko wapi? Akauliza Loniki
“Usihofu Loniki.Utamuona tu” akasema Khumalo halafu akayakusanya mabunda yale ya noti akaondoka nayo na baada ya dakika tano akarejea na kuwaomba Linah na Loniki wamfuate.Waliongozana hadi katika chumba kimoja kikubwa kilichokuwa na mitambo mingi.Kilionekana ni kama studio.Kulikuwa na kompyuta nyingi na runinga kubwa ukutani.
“Nipatie namba nane” Khumalo akamwambia kijana aliyekuwamo mle ndani na baada ya sekunde kadhaa kupitia ile runinga kubwa Happy akaonekana akiwa amekaa kitandani.Loniki akasonya na kukunja uso kwa hasira
“Unaweza kuniruhusu nikaonana naye ana kwa ana?
“Hapana Lonny.Hutakiwi kuonana naye ana kwa ana.si vizuri kwa usalama wetu.Nadhani tusiendelee kupoteza muda ni wakati wa kuianza kazi sasa”.Akasema Khumalo,Loniki akatikisa kichwa kuitikia lakini ilionyesha dhahiri kamba alikubali kwa shingo upande.Lengo lake lilikuwa ni kuonana ana kwa ana na Happy
“Ninyi mtashuhudia kila kinachoendelea kupitia hii runinga ambayo imeunganishwa na kamera zilizoko katika chumba alimo Happy.Mtashuhudia kila kitu” akasema Khumalo halafu akatoka mle chumbani.Bado Loniki aliendelea kumtazama Happy kwa hasira
Mlango wa chumba alimowekwa Happy ukafunguliwa na Khumalo akaingia.Happy ambaye alikuwa amejiinamia akainua uso wake baada ya kusikia mlango unafunguliwa.Akakutana na sura iliyomstua na kumfanya aismame
“Its you ..!!!” akasema Happy kwa mshangao
“Hallo Happy..!! akasema Khumalo huku akitabasamu.
“Kumbe ni wewe !!!.Nakukumbuka sana.Ulikuwepo mahakamani juzi na ulikuwa unaniangalia kwa jicho baya.Who are you? ..Happy akasema kwa hasira
Khumalo akatabasamu na kuizima sigara aliyokuwa anaivuta
“Calm down my love.Huna haja ya kuhamaki namna hiyo.Unajisikiaje Happy? Mbona hujala chakula? Akasema Khumalo na kuketi sofani.Happy bado aliendelea kumuangalia kwa hasira
“Niambie ni kwa nini umewatuma watu wako waniteke na kunifungia humu? Unataka nini toka kwangu?
“Happy naomba ukae,kuwa na amani na wala usiwe na hasira.Nimekuleta hapa nina maongezi nawe mafupi lakini ya muhimu sana.Baada ya kumaliza maongezi nawe nitakuruhusu uende zako” akasema Khumalo kwa upole
“Unataka kuongea nami nini na kwa nini usinitafute katika njia za kawaida hadi uniteke nyara? Akauliza Happy
“Happy ni saa moja za jioni sasa na nina imani familia yako tayari imeanza kuwa na wasi wasi juu yako kwa hiyo naomba tusipotee muda .Nisikilize kile kilichonifanya nikulete hapa halafu nitakuacha uende zako” akasema Khumalo na kauli ile ikamfanya Happy atulie.
“Naitwa Job.Mimi ni mfanya biashara wa kimataifa.Nafikiri ni mara yako ya pili kuniona.Baada ya kujitambulisha kwako ,napenda nichukue nafasi hii kukuomba samahani kwa usumbufu wote ulioupata.Nafahamu ulikuwa na shughuli zako nyingi tu na zote zimevurugika kwa kukuleta hapa.Kuna mtu ambaye alitaka uwepo hapa kwa sababu anazojua yeye mwenyewe lakini kwa bahati mbaya hutaweza kumuona mtu huyo kwani jukumu zima la kuongea nawe amenikabidhi mimi.” Akasema Khumalo na kukaa kimya akamuangalia Happy
“ Ni nani huyo aliyekutuma unikamate? Ni Savanna? Akauliza Happy kwa hasira.Khumalo hakujibu kitu akamuangalia Happy kwa makini usoni na kusema
“Happy nafahanmu uko katika wakati mgumu hivi sasa kutokana na mfululizo wa matukio lakini kuna swali moja tu ninalotaka kukuuliza.” Khumalo akatulia halafu kwa sauti ndogo akauliza
“Do you love Patrick?
Happy akamtazama Khumalo kwa mshangao na kusema
“yes I do love him”
“How much do you love him?
“More than my life” akajibu Happy kwa ufupi
“Good.Nafurahi kusikia hivyo” akasema Khumalo
“Jibu lako ninanifanya niamini kwamba uko radhi kufanya jambo lolote kwa ajili yake?
Happy akamuangalia Khumalo machoni halafu akasema
“Ndiyo .”
“nafurahi sana kusikia hivyo.Ni watu wachache sana ambao wanaweza kuyatoa maisha yao kwa ajili ya wale wawapendao.” Akasema Khumalo akakaa kimya kwa muda halafu akasema
“Patrick alikuwa na mpenzi wake aitwaye Veronika.walipendana sana na walikuwa katika hatua za mwishoni ili wafunge pingu za maisha na kuishi maisha yenye raha,lakini ulipojitokeza wewe mipango yao yote ikavurugika. Patrick alibadilika na kusitisha kila kitu kuhusiana na ndoa yake na Vero.Watu wengi sana waliumia.Vero alipatwa na uchungu mwingi na hatimaye alifariki dunia.Ni pigo kubwa kwa ndugu zake,rafiki zake na wale wote waliompenda.Matukio haya yote yaliyotokea yanadhihirisha wazi ni namna gani wewe na Patrick mnavyopendana.Ninadiriki kusema kwamba wewe na Patrick mmeumbwa ili muwe pamoja.Penzi lenu ni zito na la kweli na hakuna wa kuwatenganisha katika hii dunia” akasema Khumalo .Happy bado aliendelea kumshangaa asielewe alikuwa anamaanisha nini kwa maneno yale.Kumalo akaendelea
“Awali ulinihakikishia kwamba uko tayari kufanya jambo lolote kwa ajili ya Patrick.Vizuri sana Happy.Nitapenda nilitibitishe hilo siku ya leo” akasema Khumalo
“Sijakuelewa unamaanisha nini.Naona unaongea maneno mengi sana na sikuelewi unahitaji nini toka kwangu.Kama unahitaji pesa niambie unahitaji kiasi gani nikupatie ili niondoke zangu” akasema Happy
“Happy naomba unisikilize tena unisikilize kwa makini sana.Hatuna haja na pesa zako ,mtu aliyetutuma tukulete hapa ametupa pesa nyingi sana ,a lot of money .Kwa hiyo hatuna shida na senti yako hata moja.” Akasema Khumalo
“Hivi tunavyoongea “ akaendelea Khumalo
“Kuna mtu ambaye ni mfanyakazi wa idara ya magereza anayefanya kazi katika gereza alimo Patrick,yuko tayari na chakula chenye sumu ambacho anasubiri kumpa Patrick na baada ya dakika kumi tu atakuwa amekufa.Anachosubiri ni maelekezo yangu tu.Just one call and Patrick dies” akasema Khumalo
“whaaattt…!!!!!!!!!!.Happy akastuka na kusimama akamuangalia Khumalo kwa hasira
“Najua umestuka sana kusikia kwamba Patrick yuko hatarini kuuawa.Najua Patrick ndiye mwanaume wa maisha yako na endapo atafariki basi ndoto zako zote za kuwa na maisha yenye furaha pamoja naye zitayeyuka.Maisha yako yataharibika na juhudi zako zote ulizozifanya katika kulijenga penzi lako na Patrick zitakuwa ni kazi bure.Maisha ya Patrick ,mwanaume umpendaye yako mikononi mwako hivi sasa.Wewe ndiye utakayeamua hatima ya maisha yake kwa sasa endapo aendelee kuishi au afariki dunia kwa sumu.” Akasema Khumalo.Happy akatetetemeka .Khumalo hakuonyesha kama anafanya masihara
“Please Job,don’t ever hurt Patrick.Hakuna anayefahamu umuhimu wake kwangu.Patrick ndiye maisha yangu,ndiye furaha yangu,ndiye kila kitu kwangu.Siwezi kuishi bila yeye.Tafadhali naomba msimfanye jambo lolote la kumdhuru.Nambieni mtu aliyewatuma amewapa shilingi ngapi? Nitawapa mara mbili yake” akasema Happy huku akilia
“Happy sisi kwa maelekezo tuliyopewa na mtu aliyetutuma tukulete hapa ,hatutamgusa Patrick na wewe utaachiwa huru endapo utakubali kufanya anavyotaka yeye.”
“Huyo mtu anataka nini toka kwangu? Nimemkosea nini? Naomba niongee naye mimi mwenyewe anieleze nilichomkosea” akasema Happy
“Hapana Happy.Huwezi kuongea naye.You’ll talk to me” akasema Khumalo
“Ok Niambie unataka nini? Huyo mtu wenu anataka nini toka kwangu kama malipo ya kutomdhuru Patrick?
“Ni kitu kidogo sana ambacho kiko ndani ya uwezo wako.Kabla sijakwambia nini unatakiwa kufanya hebu kwanza angali picha hizi namna mtu aliyekula sumu hii tunayotaka kumpa Patrick anavyokufa” akasema Khumalo na kwenda katika runinga akachomeka kifaa kidogo cha kuhifadhi kumbu kumbu na kukiwasha.Picha zikaanza kuonekana
“Ukimaliza kuangalia kama utakuwa tayari kumuokoa Patrick utabonyeza kitufe hiki chekundu.Hii ni kengele ambayo itaniashiria kwamba uko tayari na mimi nitakuja mara moja.You have twenty minutes to decide” akasema Khumalo na kutoka.Happy akabaki peke yake mle chumbani akitazama picha zile za kutisha
* * * *
Baada ya kutoka katika chumba alichokuwamo Happy ,chumba ambacho kilijengwa chini ya ardhi,Khumalo akapanda moja kwa moja hadi katika chumba walimo Linah na Loniki walikokuwa wakifuatilia kila kilichokuwa kinaendelea kule chini kupitia runinga kubwa.
“Nimemuacha aangalie picha zile na nina hakika baada ya kumaliza kuzitazama lazima ataniita.Anampenda Patrick sana na hawezi kukubali Patrick adhurike.” Akasema Khumalo
“Bado roho yangu haina amani kabisa Khumalo.Nilichokuwa nakitaka ni kuona mida hii Happy akiwa katika mateso makali sana.” Akasema Loniki
“Relax Lonny.Hii ni mbinu ya kumfanya Happy akubali kufanya mapenzi yeye mwenywe kwa hiari yake na vijana wetu na ili filamu zitakapotoka isionekane kwamba kuna nguvu ilitumika.Ninakuhakikishia Lonny ,kama lengo lako ni kutaka Happy ateseke basi ndani ya muda mfupi ujao atapata mateso makali sana na kwa namna jina lale litakavyochafuka nina hakika lazima atachukua jukumu la kujimaliza .Filamu hiyo tutaisambaza katika mitandao ya ngono duniani,katika mitandano ya kijamii,katika simu na kila sehemu ambayo tutaweza kuitumia kumchafua Happy.Atateseka kwa maisha yake yote yaliyobaki hapa duniani.” Akasema Khumalo
Lonny bado aliendelea kumtazama Happy kwa hasira kupitia runinga ile.
“Usisahau vile vile kwamba picha zitakazopigwa ,Happy akifanya mapenzi na vijana wetu atafikishiwa pia Patrick gerezani.I swear to you Lonny,kwa namna Patrick anavyompenda Happy I’m sure he will drop dead” akasema Khumalo huku akicheka
“Kwa mtu mwenye jina kubwa kama la Happy kuingia katika kashfa kubwa ya ngono ni habari ambayo haitaweza kufutika kwa urahisi katika vinywa vya watanzania.Ni historia ambayo itadumu kwa vizazi hadi vizazi na atakayeteseka si Happy pekee bali hata familia yake ka ujumla na zaidi sana Patrick” Akasema Khumalo huku akipuliza moshi mwingi hewani
“Damn you Happy !!.Laiti ningekuwa na uwezo wa kufika katika chumba ulimo ,ningekuua mimi mwenyewe kwa mikono yangu.Natamani hata niutafune moyo wako.Wewe ni sababu ya mdogo wangu kufariki dunia.I swear I’ll make your life a living hell before you die” akawaza Lonny huku akiendelea kumtazama Happy kwa hasira kupitia Runinga
* * * *
Familia yote ya mzee Kibaho ilikwisha rejea nyumbani na walikuwa wanajiandaa kupata mlo wa usiku.Ni Happy pekee ambaye hakuwa ameonekana .Toka amerejea nyumbani,mzee Kibaho hakuwa ameonana na mwanae kipenzi Happy.
“Happy ameshindaje? Yuko wapi? Akauliza mzee Kibaho
“Bado hajarejea toka alipoondoka asubuhi.” Akajibu mama yake Happy
“Toka alipoondoka asubuhi?? Akashangaa mzee Kibaho
“Ndiyo.Aliondoka hapa nyumbani asubuhi na alisema kwamba hatakawia kurudi lakini nashangaa mpaka mida hii hajarajea”
“Alikuaga anakwenda wapi?
“Hakusema anakwenda wapi lakini ilionekana alikuwa na haraka na mahala alikokuwa anakwenda”
Mzee Kibaho akainuka na kwenda chumbani kwa Happy kuhakikisha kama ni kweli Happy hayupo.Akarudi sebuleni na kuchukua simu yake akapiga namba za simu za Happy lakini simu haikuwa inapatikana.
“Si kawaida ya Happy kuzima simu.” Akasema kwa wasi wasi mzee Kibaho huku akijaribu tena na tena kupiga simu ya Happy lakini jibu likawa ni lile lile namba anayopiga haipatikani.
“Margreth,Happy hakukueleza mahala anakoelekea leo? Akauliza mzee Kibaho baada ya Margreth kuingia pale sebuleni
“Hapana baba .Jana nilichelewa sana kurudi na sikuweza kuonana naye na leo asubuhi nimeondoka mapema mno na yeye akiwa bado amelala.Nilimtafuta katika simu yake mchana lakini simu yake haikuwa ikipatikana”
Mzee Kibaho akamuita Pendo mfanyakazi wa ndani
“Pendo wewe ndiye uliyekuwa na Happy jana mahakamani.Kuna jambo lolote alikueleza kuhusu mahala alikokusudia kwenda leo?
“Hapana baba hakunieleza chochote.Ninachokumbuka ni kwamba kabla hatujaondoka pale mahakamani alitokea kijana mmoja akaongea kitu na dada halafu tukaondoka naye hadi katika baa Fulani wao wakashuka mimi nikabaki ndani ya gari.Walikuwa na maongezi muhimu lakini sikujua walikuwa wanaongea nini.Baada ya muda mfupi dada akarejea garini kwa kasi akauinamia usukani akaanza kulia.Nilimuuliza alikuwa analia nini lakini hakunijibu kitu,akawasha gari tukaondoka.Jioni mida ya saa kumi na moja akanipigia simu akaniomba nimtengenezee juisi ya maembe.Nilipompelekea chumbani kwake nilimkuta akiongea na simu na kuna mtu alikuwa kama anajibizana naye.Walikuwa ni kama wanazozana.Nakumbuka nilimsikia akitaja jina la Savanna katika maongezi yao”
“ Savanna !!..akastuka mzee KibahoCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ninayo namba ya simu ya Savanna ngoja tumpigie pengine anaweza kufahamu mahala alipo Happy” akasema Margreth
“Nipe niongee naye” akasema mzee Kibaho
“hallo Margreth” akasema Savanna baada ya kupokea simu
“Hallow Savanna.Mimi ni mzee Kibaho baba yake na Happy”
“Ouh shikamoo mzee.”
“marahaba Savanna.Samahani kwa kukusumbua usiku huu.Tumekuwa na wasi wasi kuhusu Happy.Hajaonekana toka alipoondoka nyumbani asubuhi ya leo na hata katika simu hapatikani.Umeonana naye kwa siku ya leo?
“Ndiyo baba.Happy nilionana naye asubuhi .Tulikutana gerezani alikuja kumtembelea Patrick.Mimi nilimkuta tayari amekwisha fika na inaonekana aliwahi mapema sana.Hatukupata wasaa wa kuongea zaidi ya kusalimiana kwa sababu nilikuwa nimeongozana na familia ya Patrick.” Akasema Savanna.Mzee Kibaho akavuta pumzi ndefu
“Ahsante sana Savanna,.Endapo ikitokea ukawasiliana naye basi tutaarifu mara moja”
“Sawa baba nitafanya hivyo.” Akajibu Savanna na kukata simu
“Kwa mujibu wa maelezo ya Savanna,Happy alikwenda gerezani asubuhi ya leo kuonana na Patrick.” Akasema mzee Kibaho baada ya kumaliza kuongea na Savanna simuni
“Atakuwa ameelekea wapi? Akauliza mama yake
“Alipoondoka asubuhi alinihakikishia kamba hatakawia kurudi.Na hata mavazi yake hayakuonyesha kama alikuwa na safari ya kuelekea mbali.Alivaa mavazi ya kawaida”
“Kama ni hivyo atakuwa wapi? Akauliza Magreth na kisha wakaanza kupiga simu kwa watu mbalimbali kumuulizia Happy lakini hakuna hata mmoja aliyekuwa amemuona Happy
“Msiwe na wasi wasi.Happy ni mtu mzima na anafahamu kitu anachokifanya.Inawezekana amepatwa na dharura kama mnavyofahamu kwa siku za hivi karibuni amakuwa na mambo mengi .Tuendeleeni kumsubiri na nina hakika atarejea muda si mrefu” mzee Kibaho akawapa moyo familia yake lakini hata yeye alikuwa na wasi wasi mwingi moyoni kutokana na mfululizo wa matukio yaliyomuandama binti yake
Mlio wa kengele ukasikika katika chumba walichokuwamo akina Khumalo.
“kazi imeanza.” Akasema Khumalo na kuondoka kuelekea katika chumba alichokuwamo Happy
“Hallo Happy” akasema Khumalo
“Stop it..Please stop it” akalia Happy huku akiyafunika macho yake kwa viganja vya mikono ili asiendelee kuzitazama picha zile za kutisha
“Umeona Happy? Umeona namna sumu hii inavyowatesa watu kabla hawajafa?
“ Please Job ,dont do that to Patrick.I beg you don’t hurt Patrick” akalia Happy
“Kwa hiyo umeamua nini? Uko tayari kufanya kile tunachotaka kwa ajili ya kuokoa uhai wa Patrick? Akauliza Khumalo
“I’m ready.Please don’t hurt Patrick.I’m ready to do anything to save him”
“Vizuri sana.Watu kama wewe ni wachache sana.Hata mimi namuonea wivu Patrick kwani amempata mwanamke anayempenda kwa dhati.”
“Tafadhali sema mnataka niwafanyie nini? Akasema Happy huku akifuta machozi.Khumalo akainuka pale sofani alipokuwa amekaa akamsogelea Happy
“Stop crying Happy.Usilie tena.” Akasema Khumalo halafu akanyamaza kidogo akamtazama Happy usoni na kusema
“ Aliyenituma nikulete hapa alitoa sharti moja tu ambalo ukilitekeleza utaokoa maisha ya Patrick na wewe utakuwa huru.Anao vijana wake wawili wanaokupenda sana na anataka ufanye nao mapenzi.”
“ What !!!!????...Happy akastuka na kumtazama Khumalo kama ameona mzuka
“Hilo ndilo sharti pekee alilolitoa mtu aliyekuleta hapa.Ni juu yako kukubali au kukataa.Kama hautakuwa tayari sisi tutakuacha uende zako lakini nakuhakikishia kwamba wakati wewe ukitoka ndani ya jumba hili,mtu umpendaye kuliko wote duniani atakuwa atakuwa tayari amelala usingizi wa milele.” Akasema Khumalo na kuzidi kumtisha Happy.
“ Ni nani huyo shetani ambaye amenileta hapa? Ni nani huyo asiyekuwa na hata chembe ya ubinadamu? Nimemkosea kitu gani hadi aamue kunitenda namna hii ? akasema Happy huku akilia kwa uchungu
“Happy ni juu yako kuamua .Kilio na matusi kamwe havitakusaidia na muda wetu unazidi kwenda.Ninakupa tena dakika kumi nyingine za kuamua “ akasema Khumalo na kupiga hatua kutoka mle chumbani
“Ouh My God !!!! akalia Happy.Alihisi kuchanganyikiwa
“whats happening to me? Ni kweli nina laana? Kwa nini ninaandamwa na mikosi kama hii kila siku? Huyu mtu aliyenileta hapa ni nani na kwa nini atake kunidhalilisha namna hii? Happy akazidi kulia
“Huyu mtu aliyenileta hapa lengo lake ni moja tu ,kunidhalilisha. Nini kitatokea kama nitakataa kufanya anavyotaka? Je ni kweli Patrick yuko katika hatari ya kuuawa? Sina hakika kama suala hili ni la kweli.Huyu mtu lengo lake ni kuudhalilisha utu wangu.Ninaanza kuhisi mtu huyu atakuwa ni Savanna kwani ndiye mtu niliyelumbana naye jana na tukatoleana vitisho.Pengine ameamua kunionyesha uwezo wake kwa kuniteka na kunileta hapa ili nidhalilike.Siwezi kukubali hata kidogo kuwapa nafasi ya kuuchezea mwili wangu.Ni bora waniue kuliko kuwapa nafasi ya kunichezea.” Akawaza Happy lakini mara akastuka
“What if its true and Patrick is going to die? Inawezekana pengine watu hawa wakawa wanasema kweli ..Am I ready to let Patrick die? I’m confused..!!! Happy akahisi kuchanganyikiwa
“Patrick amejitolea mengi kwa ajili yangu na hata hivi sasa anasota gerezani kwa ajili yangu.Kwa nini na mimi nishindwe kusimama imara kuutetea uhai wake? Kwa maana hiyo itanilazimu kukubaliana na matakwa yao ya kufanya mapenzi na watu wawili? Ouh Jamani akili yangu naona haifanyi kazi tena.Sijui nifanye nini” akawaza Happy na mara mlango ukafunguliwa Khumalo akaingia.Safari hii macho yake yalionekana mekundu na yasiyo na masihara hata kidogo.Happy akaingiwa na woga.Mwili ukamtetemeka
Happy dakika kumi zimekwisha na ninadhani tayari umekwisha fanya maamuzi” Akasema Khumalo huku akimuangalia Happy kwa macho makali sana.
Happy mwili ulimtetemeka na hakujua aseme nini
“Inaoneka bado hujaamua lolote.I’m so sorry Happy.” Khumalo akasema kwa masikitiko halafu akatoa simu yake na akabonyeza namba na kupiga
“Hallow Josh,amekataa kutoa ushirikiano endelea na mpango wetu,mpe Patrick chakula” akasema Kumalo halafu akamuangalia Happy kwa masikitiko
“I’m so sorry Happy.Muda mfupi toka sasa Patrick hatakuwa nasi tena.”
“Stop it !!!!!..Please stop it !!!!...” akapiga kelele Happy
“Please stop it.Dont kill Patrick.Niko tayari kufanya mnavyotaka.” Akasema Happy.Khumalo akamtazama kwa makini machoni halafu akatoa simu yake na kupiga
“Hallow Josh,subiri kwanza.Sitisha kwanza hilo zoezi” akasema Khumalo na kukata simu
“Happy nadhani sasa umeamua kumuokoa Patrick”
“Niko tayari kufanya lolote ili msimdhuru Patrick”
“Vizuri sana” akasema Khumalo huku akitabasamu
“Please don’t hurt Patrick.Hastshili mateso yoyote.Kama ni mateso naomba mnitese mimi”
“Hatukutesi Happy.Fanya kama ulivyoamriwa na utakuwa huru na hakuna mtu atakayemgusa Patrick” akasema Khumalo
“Niko tayari kufanya mnavyotaka lakini kwa sharti moja tu.Mtu huyo ambaye mnataka afanye mapenzi na mimi lazima atumia kinga”
“Usihofu kuhusu hilo Happy.Tunazingatia sana usalama wa afya yako.Jiandae Happy,baada ya muda watakuja vijana wawili unachotakiwa ni kuonyesha ushirikiano na jitahidi kuwaridhisha vijana hao.Baada ya hapo tutakuruhusu uende zako” akasema Khumalo halafu akatoka mle chumbani akimuacha Happy ameinama akilia
“Mpango mzima umekamilika .Mtashuhudia kila kitu muda si mrefu.Ninawahakikishia kwamba hili ni pigo kubwa kwa Happy” akasema Khumalo baada ya kurejea katika chumba walichokuwamo akina Linah
Baada ya dakika zipatazo kumi hivi,Khumalo akiwa ameongozana na vijana wawili waliojazia miili yao na wenye vifua vipana,wakaingia katika chumba alichokuwamo Happy.Vijana wale walikuwa wamezificha nyuso zao ili wasitambulike. Happy alipowaona akaogopa na kuanza kulia.
“Naombeni mnihurumie jamani.Nimewakosea nini hadi mnifanyie hivyo? Akalia Happy lakini Khumalo wala vijana wake hawakumsikiliza
“Happy nyamaza kulia.Futa machozi yako na tukamilishe zoezi letu ili tukurejeshe nyumbani kwenu.Nina imani familia yako ina wasi wasi mwingi sana sasa hivi” akasema Khumalo huku akiwasha taa kubwa iliyokuwamo mle chumbani na kukifanya chumba kiwe na mwanga mkali
“Happy kumbuka makubaliano yetu kwamba unatakiwa uonyeshe ushirikiano na uwaridhishe vijana wangu .Tumeelewana Happy? akasema Khumalo
“Ndiyo “ akajibu Happy
“Vizuri sana” akasema Khumalo na kutoka mle chumbani .Jamaa mmoja kati ya wale vijana walioletwa na Khumalo akamfuata Happy akaketi karibu yake na kumfuta machozi
“Fanya kama alivyokuamuru mkuu wetu.Endapo utaenda kinyume na matakwa yake anaweza akabadilika na akibadilika huwa ni mtu mbaya sana” akasema yule jamaa huku akianza kumtomasa Happy
“Please don’t hurt me “ akasema Happy
“Hautaumia mrembo.You’ll feel like you are in heaven” akasema jamaa mwingine
“Ninafanya hivi kwa ajili ya Patrick, kwa ajili ya kumlinda yeye “akawaza Happy halafu kijana mmoja akaanza kufungua vifungo vya lile shati lake dogo alilokuwa amevaa
“Leave me alone…Nitafanya mwenyewe” akafoka Happy na kumsukuma Yule jamaa halafu akasimama na kuanza kufungua vifungo vya shati lake huku machozi yakimtoka
“Mtu anayenifanyia kitendo hiki ni nani? Nimemkosea kitugani? akawaza Happy
Khumalo,Linah na Loniki walikuwa wameyaelekeza macho yao katika runinga ile kubwa mbele yao wakiangalia namna zoezi linavyoendelea.Baada ya kama dakika tano za mabishano kati ya Happy na wale vijana hatimaye vijana wale wenye nguvu walifanikiwa kumuangusha Happy kitandani na kuanza kumuingilia kwa zamu.Happy alilia sana wakati vijana wale wakiendelea na udhalimu wao juu ya mwili wake.Zoezi liliendelea huku likiendelea kurekodiwa pamoja na kupigwa picha.
Zoezi lilichukua zaidi ya dakika ishirini .Vijana wale walimaliza kazi waliyopewa huku wakihema kwa nguvu sana.Taratibu waliondoka mle chumbani na kumuacha Happy akiwa analia.
“kazi tayari” akasema Khumalo huku akitabasamu
“Ina maana kazi ndo imeishia hapa? Akauliza Loniki kwa mshangao
“Pesa zote hizi nilizotoa ni kwa ajili ya kazi hii ?
“Ndiyo Loniki.Lengo lako ni kumuadhibu Happy,? Akasema Khumalo
“Ndiyo” akajibu Happy
“Kama lengo lilikuwa hilo basi kazi imekwisha kwa leo na subiri kwa hatua itakayofuata.Kesho asubuhi nchi nzima itatikisika kwa taarifa hii.Ni skendo ambayo haijawahi kutokea hapa nchini” akasema Khumalo
“Kwa hiyo nini kitafuata baada ya hapa? Akauliza Loniki
“Niachie mimi kila kitu.Kesho asubuhi usiache kufuatilia vyombo vya habari,magazeti ya udaku na mitandao ya kijamii.Taarifa itakayokuwa inatawala ni ya picha za ngono za Happy” akajibu Khumalo.
Baada ya maongezi kadhaa na Khumalo Linah akamshika mkono rafiki yake Loniki wakaelekea katika gari ambalo liliwarudisha hadi ofisini kwa Linah ambako Loniki alichukua gari lake na kurejea nyumbani
Baada ya Loniki na Linah kuondoka ,Khumalo akaelekea katika chumba alimo Happy,akaufungua mlango na kuingia ndani.Happy alikuwa amelala kitandani akilia.Khumalo akamtazama kwa sekunde kadhaa halafu akapuliza dawa ya usingizi na kutoka mle chumbani
Baada ya dakika kumi na tano kupita toka Khumalo aipulize dawa ile katika chumba alichokuwamo Happy,Khumalo akarejea akiwa na vijana wake na kumkuta tayari Happy amelala fofofo hajitambui.Wakamuinua na kumpakia katika gari lake na kuondoka naye
“Kazi ya kwanza imekwisha.Kazi iliyobaki ni kuzisambaza picha na video.Naamini hadi kesho asubuhi zoezi hili litakuwa limekamilika na hatutakuwa na deni tena kwa Loniki“ akawaza Khumalo akiwa na vijana wake wakimrejesha Happy nyumbani kwao.Khumalo ndiye aliyekuwa ametangulia mbele na gari lake halafu gari la Happy lililokuwa linaendeshwa na kijana mwingine likafuata nyuma.Tayari Khumalo alikuwa anafahamu mahala anakoishi Happy kwani alikwisha mfanyia uchunguzi wa kutosha.
Saa saba kasoro za usiku waliwasili nyumbani kwa akina Happy.Kwa haraka haraka vijana wale wa Khumalo wakashuka katika gari la Happy.Kabla ya kushuka walimuwekea kitu fulani puani na kumzindua toka usingizini .Akapiga chafya mfululizo.Kwa haraka vijana wale wakaingia katika gari la Khumalo na kuondoka kwa kasi maeneo yale.
Mlio wa magari nje ya nyumba yake,ulimstua mzee Kibaho ambaye alikuwa macho mpaka mida hii akimsubiri mwanae arejee.Akatoka chumbani kwake na kwenda getini.Mbwa walikuwa wanabweka.Akachungulia nje kupitia uwazi mdogo na kuliona gari la Happy.Haraka haraka akafungua geti na kuliendea gari.Akachungulia ndani ya gari na kumuona Happy akiwa amelala kitini.Akapigwa na butwaa kwa hali aliyokuwa nayo .Happy alikuwa amelegea na mwili wake haukuwa na nguvu hata kidogo.Kwa haraka akamtoa mwanae garini na kumpeleka ndani na familia nzima ikaamka .Kila mtu alistushwa na hali aliyokuwa nayo Happy.Haraka haraka akaanza kupatiwa huduma ya kwanza.Hakuna aliyefahamu nini kimemsibu hata akawa katika hali ile.Ilikuwa ni hali ya kusikitisha sana.Daktari wa familia aliitwa akafika kwa haraka kuja kumuangalia Happy,akampima na kisha akampatia dawa na kumtaka akapumzike hadi asubuhi atakapopata majibu ya vipimo alivyochukua.
*******************
Kumekucha Tanzania.Ni saa moja za asubuhi, jijini Dar es salaam barabara zimesheheni watu na magari wote walikuwa wanaelekea katika shughuli mbalimbali za kila siku za uzalishaji mali.Katika vibanda na katika sehemu mbali mbali za kuuzia magazeti,kulikuwa na makundi ya watu waliokuwa wakihitaji magazeti ili kufahamu kulichoandikwamo asubuhi hii.Katika baadhi ya vituo vya kuuzia magazeti kulitokea ugomvi wa watu wakigombea magazeti kitu ambacho ni nadra sana kushuhudiwa.
Gazeti lililozusha mjadala asubuhi hii na kuwafanya watu wajazane katika vibanda vya kuuzia magazeti na wengine kufikia hata hatua ya kurushiana makonde ni gazeti la Mitikisiko,gazeti maarufu kwa kuandika habari za udaku na hasa zile zinazowahusu watu maarufu ndani na nje ya nchi.Siku hii ya leo gazeti hili lilipambwa na kichwa cha habari kilichobeba habari iliyozua gumzo nchini.
“HAIJAWAHI KUTOKEA” hiki kilikuwa ni kichwa cha habari kilichoandikwa kwa maandishi makubwa na chini yake kulikuwa na vichwa vingine vidogo vidogo.
“NI VIGUMU KUAMINI LAKINI KWELI”
“HUU NDIO UCHAFU WA MISS TANZANIA”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Vichwa hivi vya habari vilisindikizwa na picha kubwa ya Happy Kibaho,akiwa mtupu huku sehemu ya kifuani na chini ya kiuno zikiwa zimezibwa kwa rangi nyeusi.Picha nyingine ilimuonyesha Happy akiwa amelala kitandani akiwa na wanaume wawili waliozifunika nyuso zao ambao ilionyesha wazi walikuwa katika harakati za kufanya mapenzi.
“Mlimbwende aliyenyakua taji kubwa la urembo hapa nchini la miss Tanzania ambaye siku chache zilizopita amelivua taji hilo kutokana na kashfa ya kujihusisha katika ugomvi wa kumgombania mwanaume,na kusababisha kifo cha msichana aitwaye Veronika ,ameingia katika aibu kubwa baada ya picha na video yake ya ngono kuvuja” Haya yalikuwa ni maelezo ya utangulizi ya habari hii kubwa na kulifanya gazeti la Mitikisiko kuongoza katika mauzo kwa siku hii.Taarifa ile iliendelea katika ukurusa wa tatu huku ikipambwa na picha zinazomuonyesha Happy akiwa mtupu huku akifanya mapenzi na wanaume wawili waliozifunika nyuso zao katika mitindo tofauti tofauti..Ilikuwa ni aibu nzito isiyoelezeka .
Katika tovuti mbali mbali na mitandao ya kijamii,tayari video na picha za Happy vilianza kusambaa kwa kasi kubwa na kuwa gumzo mtandaoni.Watu walikuwa wanatumiana video na picha hizo za Happy akifanya ngono na wanaume wawili hadi katika simu za mikononi.Kutokana na kukua kwa teknolojia ya upashanaji habari ndani ya masaa machache tayari habari kuhusu Happy ilikwisha sambaa karibu nchi nzima.
Mlango mdogo katika geti la kuingilia nyumbani kwa akina Happy ulikuwa wazi,hivyo kumfanya mama Joseph jirani wa akina Happy,apite kama mshale na kuingia ndani huku akihema akiwa na gazeti mkononi
“Mama Happy ..!!! akaita mama Joseph .Alikuwa anahema huku jasho likimtoka.Mama yake Happy ambaye alikuwa katika kazi za usafi wa nyumba asubuhi hii,akaja kwa kasi baada ya kusikia sauti ya mama Joseph.
“Mama Joseph kuna tatizo gani? akauliza mama Happy kwa mshangao
“Mama Happy njoo huku” akasema mama Joseph huku akimvuta mama Happy kuelekea sebuleni.
“Mama Happy umeshapata taarifa?
“Taarifa gani mama Joseph? Mama yake Happy akazidi kushangaa
“Ina maana hakuna hata mtu mmoja aliyekupigia simu kukueleza nini kimetokea leo?
“mama Joseph mbona unanichanganya? Nini kimetokea?
“Soma gazeti hili” akasema mama Joseph huku akimpa mama Happy gazeti lile alilokuwa amelishika mkononi.Mara tu mama Happy alipolitupia macho akaanguka na kupoteza fahamu
Mama joseph akapiga ukulele mkubwa uliomstua mzee Kibaho aliyekuwa chumbani na kumfanya atoke haraka na kuelekea sebuleni kuangalia kumetokea nini.Alistuka baada ya kumkuta mkewe akiwa ameanguka chini akiwa hana fahamu
“Nini kimetokea? Akauliza mzee Kibaho huku akimuinamia mkewe.Mama Joseph hakuweza kujibu chochote alikuwa anatetemeka huku machozi yakimtoka.Haraka haraka mzee KIbaho akaanza kumpatia mke wake huduma ya kwanza.
Kelele zile za mama Joseph,zilimstua pia Happy .Alizisikia kelele zile akiwa usingizini na mwanzoni alidhani labda alikuwa ndotoni lakini alipofumbua macho aliendelea kuzisikia.Akaogopa pengine kuna jambo baya limetokea pale nyumbani kwao. Kichwa kilikuwa kizito na mwili wake ulimuuma sana.Alisikia maumivu makali sana sehemu za kinenani lakini akajikaza na kuinuka na kukaa kitandani.Akafikiri kidogo halafu akavaa nguo na kutoka mle chumbani na kuelekea sebuleni ambako ndiko kelele zilikokuwa zinatokea.Alistuka baada ya kumuona mama yake akiwa amelala chini hana fahamu.Baba yake alikuwa anahangaika kumsaidia ili aweze kurejewa na fahamu.
Mama Joseph na mfanyakzi wa ndani Pendo walikuwa wanalia kwa uchungu.Mara tu mama Joseph alipomuona Happy ameingia pale sebuleni akazidi kulia.Happy akatamani ajue kilichokuwa kimetokea na kumpelekea mama yake apoteze fahamu,akamfuata mama Joseph na kumuomba anyamaze ili aweze kumueleza nini kilichotokea
“Mama mdogo kuna nini? Nini kimetokea hapa? ..akauliza Happy kwa sauti dhaifu lakini mama Joseph hakujibu kitu na badala yake akamuonyeshea ishara alichukue lile gazeti lilikokuwa limeanguka chini.Taratibu Happy akainama na kuliokota ,akalikodolea macho.Mwili wote ukamtetemeka alipokuwa analisoma.Alikuwa ni kama mtu aliyeliona jitu la kutisha.Mara gazeti lile likaanguka chini na uso wa Happy ukajaa machozi .Taratibu bila kuongea na mtu yeyote akageuka na kutembea kwa kasi kuelekea chumbani kwake.
Mama Joseph aliyekuwa anamuangalia Happy kwa makini ,akaogopa sana kutokana na mstuko alioupata Happy.Akamfuata mzee Kibaho na kumuomba amfuate Happy
“Kuna nini? Happy amefanya nini? Akauliza mzee Kibaho huku akiendelea na jitihada zake za kumpatia huduma ya kwanza mke wake ili aweze kurejewa na fahamu
Mama joseph akaliokota gazeti lililoanguka chini na kumpatia mzee Kibaho
“Hili ndilo chanzo cha haya yote” akasema mama Joseph
Mzee Kibaho akaanza kulipitia lile gazeti na mara akahisi mikono yake ikimtetemeka.
“Ouh My God !!!” akasema mzee Kibaho na kwa haraka akainuka na akaelekea chumbani kwa Happy.Mlango wa Chumba cha Happy ulikuwa umefungwa.Akagonga lakini hakukuwa na dalili zozote za kuwepo mtu ndani.Akachungulia katika tundu la funguo na kuiona funguo ikiwa ndani.
“Happy fungua mlango..Fungua mlango mwanangu …” akasema mzee Kibaho lakini hakusikia dalili zozote za kuwepo mtu mle chumbani.Kwa kasi akakimbia kuelekea chumbani kwake akachukua ufunguo wa akiba na kuja kuufungua mlango akaingia ndani
“Ouh Mungu wangu ..!!!!!..Mzee Kibaho nusura aanguke kwa alichokiona mle ndani.Happy alikuwa amelala kitandani huku mapovu yakimtoka mdomoni.
“Happy..!! Happy.!!! Happy.!!!!!...akapiga ukelele mzee Kibaho huku akimtikisa Happy lakini hakuwa na fahamu hata kidogo,alikuwa anakoroma.
“Ouh Mungu wangu !!” akasema mzee Kibaho baada ya kuiona chupa ndogo yenye dawa ya kuulia panya ikiwa mezani.Haraka haraka akamuinua Happy na kukimbia naye hadi garini.Mama Joseph na Pendo wakapiga ukeleel mkubwa baada ya kuishuhudia hali ile ya Happy.Mzee Kibaho hakuwajali akawasha gari lake na kwa kasi ya aina yake akaondoka pale nyumbani huku akipishana na majirani waliokuwa wakiingia kwa kasi mle ndani baada ya kusikia kilio cha mama Joseph na Pendo.
“Please God.dont let my daughter die, Please save her” mzee Kibaho ambaye kwa mbali macho yake yalilengwa na machozi ,alikuwa akiyarudia maneno haya mara kwa mara wakati akiendesha gari kwa kasi kuelekea hospitali.Kila sekunde zilivyozidi kusonga mbele ndivyo hali ya Happy ilivyozidi kubadilika na kupoteza matumaini.Alikuwa anakoroma na povu jingi likiendelea kumtoka
Geti la hospitali ya Brahmaputra inayomilikiwa na daktari bingwa Makhresh Patel lilikuwa wazi .Gari la mzee Kibaho lilikuwa likija kwa kwendo wa kazi huku likiwa limewasha taa zote.Watu waliokuwa wamesimama karibu na geti walikimbia baada ya kuliona gari lile namba lilivyokuwa likija.
Namna gari lile lilivyoingia hospitali na sauti za matairi yakilalama kutokana na breki kali aliyofungwa,iliwafanya madaktari na wauguzi watoke nje na kushuhudia nini kilichotokea.Mzee Kibaho akashuka na kukimbia na kuwataarifu wauguzi kwamba kulikuwa na mgonjwa mahututi ndani ya gari.Kwa kasi ya aina yake,wauguzi wakampakia Happy katika kitanda na kumkimbiza katika chumba cha wagonjwa mahututi.Mzee Kibaho akaombwa asubiri nje.Bado mwili wake ulikuwa unamtetemeka kupita kiasi.Aliogopa sana.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment