Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

MISS TANZANIA - 2

 





    Simulizi : Miss Tanzania

    Sehemu Ya Pili (2)



    ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA

    “Naitwa Happy ..Happy Kibaho ,natokea Tanzania”

    “Uuugh ! nafurahi sana kusikia unatoka Tanzania.I love Tanzanians.Nasikia ni watu wapole na wakarimu sana.Mama yangu amewahi kwenda Tanzania kupanda mlima Kilimanjaro na aliporudi akatuhadithia kuwa hajawahi kukutana na watu wakarimu kama watanzania.”

    Happy akatabasamu .Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Michelle kumuona happy akitabasamu.

    “Happy you are so pretty.Unajua sikuwahi kukuangalia vizuri.You are amazing” Michelle akajibu na kumfanya Happy afurahi.

    “Jina lako zuri sawa kabisa na sura yako..ukitabasamu unakuwa mzuri zaidi ya malaika..” akasema Michelle na kumfanya Happy acheke kwa nguvu.

    Huo ukawa ni mwanzo wa urafiki mkubwa kati ya Happy na Michelle.

    ENDELEA............................

    Urafiki kati ya Happy na Michelle uliendelea kuimarika siku hadi siku.Michelle alijitahidi kadiri alivyoweza kuwa karibu na Happy .Kila mwisho wa wiki walitoka na kwenda sehemu mbali mbali za starehe lengo likiwa ni kumchangamsha Happy.Pamoja na mambo hayo yote ambayo Michelle alijitahidi kufanya ili kumfanya Happy awe na furaha lakini haikuweza kumsahauliasha kuhusu Patrick hata nukta moja.Alijitahidi kila awezavyo ili asiweze kumsahahu kijana huyu mwenye upendo wa ajabu kwake.

    Ili tokea siku moja chuo kikafungwa kwa muda wa wiki mbili,Michelle akamuomba Happy wazitumie wiki mbili hizo kwa kuitembelea familia yao huko California.Happy akakubaliana na mwaliko huo na kesho yake wakapanda ndege na kuelekea California.Walipewa mapokezi mazuri na familia ya akina Michelle.Ilikuwa ni furaha iliyoje kwao kumpata mgeni aliyetoka Tanzania. .

    Siku mbili tu baada ya kuwasili kwao hapo nyumbani ,Mike naye akawasili akitokea jiji la New York anakofanya kazi.Tayari alikwisha taarifiwa na mdogo wake Michelle kuwa tayari Happy alikuwa hapo nyumbani kwao.Mike aliwasili mida ya mchana na kuwakuta familia nzima ikiwa imejipumzisha.Akasalimiana na wote kisha akaelekea chumbani kwake.Kijasho kilikuwa kikimtiririka hasa baada ya kulishuhudia kwa mara ya kwanza tabasamu pana la Happy .Alikaa kitandani na kujaribu kuwaza ni jinsi gani atakavyoweza kujiweka karibu na binti huyu mwenye urembo usioelezeka..Alishindwa kupata jibu akaamua kwenda kuoga kisha akaelekea bustanini ambako Michelle na Happy walikuwa wamepumzika kwa muda huo.

    Mara tu baada ya Mike kuwasili hapo bustanini ,Michelle akainuka na kwenda ndani kuongeza vinywaji,akawaacha Mike na Happy .Mike moyo ulikuwa ukimdunda .Ilihitaji ujasiri wa aina yake kuanzisha maongezi na binti huyu mwenye uzuri wa kimalaika.Baada ya kimya cha sekunde kadhaa toka amefika pale Mike akajikaza kiume na kuanzisha maongezi.

    “Happy unanikumbuka?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    :Happy akanyamaza kidogo kana kwamba anajaribu kukumbuka kitu kisha akajibu.

    “hapana”

    “Nilikuja siku moja chuoni kwenu nikakukuta umeiinamia kompyuta yako” akasema Mike na Happy akatabasamu

    “Ouh ! nimekukumbuka.kumbe ni wewe ! Samahani siku ile sikuwa katika hali nzuri ndio maana sikukujibu vizuri.” Akasema Happy huku akitabasamu

    “.hata mimi nilijua haukuwa katika hali nzuri kwa sababu siku hazifanani.” Mike akasema huku akatabasamu baada ya kumuona Happy akitabasamu

    “Vipi unaionaje hali ya Marekani”Mike akauliza

    “ ni nzuri,Marekani kuzuri,kila kitu kizuri ,but I miss home” akajibu Happy

    “Tanzania? Mike akauliza

    ‘Yes ! nani kakwambia kuwa natokea Tanzania?

    ‘Michelle” Mike akajibu .Happy akatabasamu

    “Hata mimi” Mike akaendelea “naipenda sana Tanzania.Nasikia ni nchi ya amani na watu wake ni wakarimu mno.” Happy akatabasamu baada ya kauli ile ya Mike

    “Nafurahi kusikia hivyo.Umekwisha wahi tembelea nchi yoyote ya Afrika? Akauliza Happy

    “Hapana bado sijatembelea nchi yoyote ya Afrika. Ila nina mpango wa kufanya ziara Afrika na nchi ya kwanza kutembelea itakuwa Tanzania.”

    “Nini kinakuvutia mpaka uifanye Tanzania kuwa nchi ya kwanza kuitembelea? Happy akauliza

    “Just to see pretty women” Mike akajibu na wote wakaangua kicheko.

    “ Nina hakika Tanzania imebarikiwa kwa kuwa na vivutio vingi vya kiasili lakini hata hivyo kuna wasichana warembo mno” akasema Mike na wote wakaendela kucheka.

    Ilikuwa ni wiki nzuri sana kwa Happy .Alifurahi kukutana na familia yenye watu wakarimu kama hii ya akina Michelle.Kwa kiasi Fulani ziara hii ya California ilisaida kumuondolea msongo wa mawazo uliokuwa ukimkabili.Mike na Michelle walijitahidi kwa kila walivyoweza kuhakikisha kuwa Happy anakuwa na furaha kwa muda wote atakaokuwa hapo kwao.

    Jumapili Mike akamuomba Happy watoke kwa ajili ya matembezi.Michelle alikuwa hajisikii kutoka.Jioni ya siku hiyo wote wawili wakiwa wamependeza vilivyo walipanda gari na kutoka.Safari iliishia katika klabu moja kubwa na maarufu .Ilikuwa ni sehemu tulivu na yenye mandhari ya kuvutia mno.Waliagiza vinywaji na kuanza kunywa taratibu huku wakiendelea na maongezi ya hapa na pale.Kisha Mike akabadili maongezi na kusema.

    “Happy leo ni siku ya furaha sana kwangu kuwa karibu nawe katika mahali tulivu kama hapa na ni siku muhimu vile vile kwa kuwa nimedhamiria kuutua mzigo mzito unaonikabili kwa muda mrefu sasa”

    Happy akastuka kidogo kwa kauli ile ya Mike lakini akamuacha Mike aendelee.

    “Happy nina furaha moyoni mwangu kukutamkia kuwa u mwanamke pekee ambaye umeweza kuuteka moyo wangu kwa kiasi ambacho siwezi elezea.Kwa ufupi Happy nakupenda sana na tafadhali ninaomba uridhie ombi langu la mimi na wewe kuwa wapenzi.Naomba unielewe Happy kuwa penzi langu kwako ni la dhati lenye lengo la kuja kuishi nawe kama mume na mke pindi utakapomaliza masomo yako.”

    Happy akaiweka glasi chini ,akamuangalia Mike kana kwamba ni mara ya kwanza anamuona.Mike naye akamuangalia Happy kwa makini Happy akatabasamu ,tabasamu ambalo kwa kiasi kikubwa linamchanganya Mike.

    “Mike you are very handsome” Happy akasema akainua glasi yake ya kinywaji akanywa funda moja

    “Oh ! thank you Happy” mike akasema huku akitababasamu na kuirekebisha tai yake aliyokuwa amevaa.Happy akaendelea

    “ Mike wewe ni kijana ambaye kila mwanamke angependa uwe naye.Una kila sifa za kijana bora.U mcheshi,mchangamfu na unayevutia.Nashukuru kwa kuwa wazi na hisia zako.Ila samahani kaka yangu mimi tayari nina mtu ambaye sijui hata nikuelezeje ili unielewe kwa jinsi ninavyompenda Kijana huyu ndiye aliyeushika moyo wangu,ameyashika maisha yangu.yeye ni kila kitu kwangu.Nampenda Patrick kuliko ninavyojipenda mimi.Kama nisingekuwa na Patrick nisingekukataa Mike.” Happy akasema kwa kujiamini.

    Mike akainama chini kwa sekunde kadhaa akiwaza.tayari alikwisha uona ugumu uliopo mbele yake.katika kumshawishi Happy akubali ombi lake la kuwa naye katika mahusiano.

    “Happy naheshimu mawazo yako na ninauheshimu sana uhusiano wa mtu.Si lengo langu kuvuruga uhusiano wako.Kwa kuwa tayari una mpenzi anayekupenda na wewe unampenda basi naomba kitu kimoja tu kutoka kwako.”

    “Kitu gani Mike?” Happy akauliza

    “ nataka tuwe marafiki wa kawaida”

    “Kwa hilo hakuna shida.Mike nashukuru sana kwa kunielewa.Nitakuombea ili uweze kumpata msichana kama mimi ambaye nina imani utampenda zaidi yangu.”

    “nafurahi kusikia hivyo Happy ” Mike akasema katika hali ya unyonge.

    Maisha yaliendelea vizuri na baada ya wiki mbili kumalizika Michelle na Happy wakarudi chuoni Mike akarejea kazini kwake New york

    ****************************

    Patrick aliendelea na maisha ya gerezani kama kawaida.Siku moja Patrick akaitwa na mkuu wa gereza na kuambiwa ajiandae kwa safari alikuwa akihamishwa gereza.Hii ilikuwa ni taarifa ambayo ilimvunja moyo sana kiasi cha kumfanya adondoshe machozi.Ni wafungwa watatu tu ndio waliokuwa wakihamishwa gereza.

    Haikuweza kufahamika mara moja sababu ya kuhamishwa kwao Wakati wakijiandaa kuondoka ,hakukuwa na mfungwa mwingine wa karibu ambaye angeweza kumwachia ujumbe wowote.Hakujua anahamishiwa gereza gani. Alizoea kila wiki kupokea barua za Happy .Hakujua angewezaje kumfahamisha juu ya uhamisho ule wa ghafla.

    Safari ilianza bila kuchelewa .Ilikuwa ni safari ndefu na yenye kuchosha.Gari walilopanda lilikuwa na madirisha madogo juu kwa ajili ya kuingiza hewa .hivyo kutokutambua ni wapi walikokuwa wakielekea.

    Wakiwa wamepitiwa na usingizi walistuliwa na sauti ya kufunguliwa kwa mlango.Walifunguliwa pingu walizokuwa wamefungwa mikononi na kuamriwa kushuka.Walikuwa wamechoka kupita kiasi.Ilikuwa ni safari ndefu na njaa ilikuwa ikiwauma kupita maelezo.Tangu wapewe chakula mchana ambacho kilikuwa ni chipsi kavu na maji ya kunywa hawakula tena chochote.

    Tayari giza lilikwisha tanda angani.Hawakujua ilikuwa ni saa ngapi mida hiyo.Hali ya mahala hapo ilikuwa ni ya baridi kali.Wote walikuwa wakitetemeka.Walisimamishwa hapo kwa takribani dakika ishirini kisha askari mmoja akatoka ndani akawaangalia na kuamuru wapelekwe ndani wakapumzike.Waliongozwa na askari wawili wenye silaha hadi ndani ya gereza.Kila mmoja akaonyeshwa chumba chake cha kulala.Hili lilikuwa ni gereza jipya kabisa na la kisasa lililokuwa limejengwa mjini songea kwa msaada wa watu wa Marekani.Lilikuwa ni gereza la kwanza la mfano nchini Tanzania kuwa na ubora wa hali ya juu afrika mashariki na kati.Patrick alishukuru Mungu kwa kuletwa hapa .Kutokana na uchovu wa safari aliokuwa nao akajitupa kitandani na kulala.

    Saa kumi na mbili asubuhi king’ora kikalia .Patrick mwili wote ulikuwa ukimuuma kwa uchovu na alihisi njaa kali.

    “Hey amka ndugu ” Akastuliwa na sauti ya mtu aliyekuwa akimtikisa.Akafumbua macho na kukutana na macho ya kijana mdogo mwenye sura ya upole.

    “Vipi husikii king’ora hicho?” Akaendelea kusema yule kijana.

    Kiuvivu Patrick akainuka na kukaa kitandani.baada ya kama dakika tatu hivi akaja askari akafungua geti la chumba chao na kumrushia Patrick nguo mpya kabisa za kifungwa.Hakusema kitu akazikunjua na kuvaa .

    “Kwa hiyo nini kinaendelea saa hizi? Utaratibu wa hapa ukoje ?” Patrick akamuuliza yule kijana waliyekuwa wakilala wote chumba kimoja.

    “huu ni muda wa kujiandaa,kunawa au kuoga kama unataka .Kitapigwa king’ora kingine tutaenda kupata mlo wa asubuhi halafu baada ya hapo tutapangiwa kazi.”

    Patrick akaonyeshwa sehemu yenye mabafu akaingia na kuoga..King’ora kingine kikalia na wote wakakusanyika katika bwalo la chakula kwa ajili ya kifungua kinywa..Walikuwa wafungwa wachache kama arobaini hivi.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baadaye kazi zikapangwa na Patrick na wenzake wakapangiwa sehemu ya kufyeka.Miongoni mwao alikuwemo yule kijana anayelala naye chumba kimoja.Walifanya usafi huku wakisimuliana mambo mengi na kupeana moyo.taratibu wakaanza kuzoeana na kujenga urafiki.

    Usiku wa siku hiyo Patrick na yule kijana ambaye alikuja kumfahamu kama Andrew waliutumia katika kusimuliana mikasa mbali mbali ya maisha yao.Andrew alimsimulia Patrick kisa cha yeye kuwapo pale gerezani.Kifungo chake kilikuwa cha miaka mitatu na kilitokana na kusababisha ajali wakati akiendesha gari akiwa amelewa.

    Patrick naye alimsimulia hadithi yake na mpaka anamaliza Andrew alishindwa kujizuia kudondokwa na mchozi.

    “Pole sana Patrick hayo yote ni majaribu katika maisha .Ni wazi Patrick una upendo wa dhati na wapekee sana kwa huyo Happy .Usikate tamaa Mungu atakusaidia utamaliza kifungo chako.”

    “Ahsante sana Andrew kwa kulitambua hilo na kunipa moyo.Lakini kitu ambacho bado kinaniumiza sana kichwa ni jinsi nitakavyoweza tena kuwasiliana na Happy .Katika gereza lile nilikotoka ,mkuu wa gereza alikuwa amejitolea kunisaidia kwa kutuma barua zangu kwenda kwa Happy na kupokea zitokazo kwa happy na kuniletea..Ningeweza kuwatumia wazazi wangu lakini bado hawajui kama nimehamishwa gereza “ akasema Patrick kwa masikitiko



    Siku moja Patrick akapangiwa kwenda kufanya usafi katika nyumba ya mkuu wa gereza.Huko alipangiwa kufyeka na kurekebisha viunga vya maua .

    Katika dirisha lililoelekea upande wa mbele ya nyumba dada mmoja mrembo alikuwa amekaa mkono shavuni kwa takribani dakika kumi na tano akimuangalia Patrick bila yeye kujua kama alikuwa akiangaliwa.Alistaajabu kwa kumuona kijana kama yule ambaye kwa mbali tu alionekana ni kijana mpole,mtaratibu na mwenye kuvutia ,akiwa gerezani.

    “ama kweli jela haina mwenyewe.How such a handsome guy be in prison?.Alifanya nini kijana yule i? Mhh ! hebu mwangalie vizuri halafu anaonekana ana mawazo mengi.Namuonea huruma ..jamani !! ..” Akawaza mwanadada yule.

    Haraka haraka dada yule akaenda jikoni na kutengeneza chai akaweka katika sinia akabeba na kuelekea mahali alipokuwa akifanya kazi Patrick.

    “kaka habari za kazi? Patrick akastushwa na sauti tamu,laini ya mwanadada.Akageuka na ghafla akajikuta akiangusha fyekeo.Macho yake yakakutana na binti ambaye uzuri wake wa asili ulikuwa unasisimua.Hakuamini kama angeweza kukutana na binti mrembo vile maeneo yale.

    “Pole na kazi “ Akasema tena binti yule baada ya kuona Patrick akimuangalia tu bila kusema kitu.

    ‘Nzu…r..rii tu dadangu” Akajibu.Patrick kwa sauti yenye kigugumizi.

    “Kaka unaweza ukapumzika walau upate kikombe cha chai kwani toka asubuhi nakuona unachapa kazi bila hata kupumzika ”Akasema yule dada akamkaribia Patrick na kuweka lile sinia chini.

    “Nashukuru sana dadangu lakini naogopa mkuu akinikuta hapa patakuwa hapatoshi”

    “Usihofu kaka yangu ,mjomba hayupo amekwenda Dar leo asubuhi na hata mkewe naye hayupo atarudi kesho”akajibu yule dada

    Patrick anamkazia macho yule dada baada ya kusikia kauli ile.

    ”Ina maana binti huyu ni mjomba wake na mkuu wa gereza? Du ! mtoto ameumbika vilivyo.Ananikumbusha sana mpenzi wangu Happy .”

    Patrick hakujivunga tena akaenda katika bomba na kunawa mikono

    “Karibu” yule dada akamkaribisha Patrick

    “Ahsante lakini mbona kikombe chenyewe ni kimoja? Patrick akauliza

    “Usijali kaka yangu hii ni kwa ajili yako”

    Patrick akanywa chai ile nzuri .Kwa muda mrefu hakuwahi kuipata chai nzito kama ile.Akamaliza kikombe cha kwanza na kuongeza tena cha pili na hatimaye cha tatu.Kimoyo moyo alimshukuru sana yule dada mrembo kwa chai ile kwani alihisi njaa kali asubuhi hiyo.

    Wakati Patrick akinywa chai ile,yule dada aliingia ndani na kwenda kukaa katika lile dirisha akiendelea kumwangalia

    “Anateseka huyu kaka .Namuonea huruma kweli.Halafu mpole.Sijui alifanya kosa gani huyu kaka manake haonekani kama mhalifu “ Akawaza yule dada

    Patrick akamaliza kunywa chai akakusanya vyombo na kwenda kugonga mlango.Yule dada akafungua mlango na kuvipokea.

    “Ahsante sana dada Mungu akubariki” Akasema Patrickkisha akaendelea na kazi yake yake ya usafi .Kila dakika taswira ya yule dada mpole mwenye roho ya huruma ilikuwa ikimjia na kumfanya atabasamu

    .”Kumbe duniani bado kuna watu wenye upendo “ Akasema taratibu huku akiendelea na kazi yake ya kurekebisha bustani ya maua.

    “Imezoeleka katika jamii yetu kila mfungwa ni mnyang’anyi,hali ambayo kufanya wafungwa kutokuthaminiwa,kutokuhurumiwa,na hata kutokusaidiwa lakini bado wako watu wachache wenye huruma na upendo kwa wafungwa kama huyu dada alivyofanya leo.Aliwaza Patrick.Wakati akiendelea na usafi dada yule akatoka tena na kisinia kilichokuwa na glasi mbili za juice.

    “Kaka karibu upumzike upate juice” akasema yule dada

    Patrick aliingiwa na wasiwasi iwapo wakuu wake wangekuja na kumkuta amekaa .

    “ahsante sana dadangu ila naogopa iwapo hawa wakuu wetu watakuja na kunikuta nimekaa nakunywa hiyo juice itakuwa ni habari nyingine” Patrick akasema huku akiwa na wasi wasi lakini moyoni alitamani sana juice ile.Huku akitabasamu dada yule akasema

    “Usihofu kaka nimekwambia mjomba wangu hayupo na hata mkewe hayupo kaenda Iringa .Hapa nipo mimi tu .Kaa upumzike kaka yangu unajua upatapo nafasi ya kufanya usafi katika nyumba hizi za wakuu ni nafasi yako ya kupumzika.Kazi zenu ni ngumu sana” Akasema dada yule

    “Ni kweli usemayo dada yangu lakini inategemea na mahali penyewe.Unajua kwa sisi wafungwa jamii inatuchukulia kama wote ni wanyang’anyi kumbe sivyo.Nimekuwa nikifanya usafi katika baadhi ya nyumba za maafisa wakubwa na wadogo lakini hakuna hata siku moja niliyowahi kupewa hata glasi ya maji.Lakini kumbe kuna watu wana roho za utofauti sana na mmoja wao ni wewe.U mkarimu sana dada yangu.”akasema Patrick

    Taratibu Patrick akajikuta akikaa chini kwenye bustani huku ameikamata glasi ya juice.Juice kama hii alizowea kuipata wakati Happy hajaondoka.Siku hii ya leo inamkumbusha mbali sana.Alishindwa kuyazuia machozi kudondoka mara alipomkumbuka Happy

    “Vipi kaka yangu mbona unalia?

    “ Juice hii imenikumbusha mbali sana” akajibu Patrick

    “Basi usilie kaka yangu Mungu yupo na atakusaidia uweze kumaliza kifungo chako”

    Kilipita kimya cha sekunde kadhaa Patrick akauliza

    “lakini dada yangu inaonyesha wewe si mwenyeji kabisa wa maeneo haya”

    Huku akitabasamu dada yule akajibu

    “kwa nini unasema hivyo”

    “Inaonyesha tu.Mwonekano wako haufanani kabisa na mazingira haya”

    Dada yule akacheka kicheko kikubwa kisha akajibu.

    “Una uwezo mkubwa wa kuweza kumsoma mtu na kumwelewa kwa haraka.Ni kweli mimi si mwenyeji wa hapa .Mimi naishi Dar es salaam.Mzee Joel mkuu wenu wa gereza ni mjomba wangu na nimekuja mara moja kumletea mizigo yake iliyotumwa na dada toka Ulaya.Ingawa sintakuwa na muda mrefu hapa lakini nimetokea kupapenda sana.Pana hewa nzuri na nimazingira tulivu sana.” Akasema yule dada

    Yule dada akatulia kidogo akanywa mafunda mawili ya Juice kisha akasema

    “ Kwa jina naitwa Veronika .Veronika Rugi sijui kaka wewe unaitwa nani?

    Patrick akanyamaza na kutafakari iwapo amweleze jina lake au vipi.Mwishowe akaamua kumtajia jina lake

    “Naitwa Patrick “CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “ nafurahi sana kukufahamu Patrick.Unajua toka nimekuona asubuhi ukifanya usafi moyo wangu haukutulia kabisa.Nilikuwa na hamu sana ya kutaka kukufahamu.U mpole sana na haufanani na wafungwa wengine”

    Patrick akacheka baada ya kauli ile ya Veronika.

    “Kweli kabisa patrick,haufanani na wafungwa tuliozoea kuwaona.Mtu yeyite akikuona mara moja atahisi kuwa uliingizwa gerezani kimakosa.Sura yako haionyeshi kuwa unaweza ukafanya kosa katika jamii ambalo lingepelekea wewe kufungwa gerezani”

    Patrick akacheka tena na safari hii kicheko kikubwa zaidi,Vero akatabasamu.

    “Patrick nitafurahi sana kama utaungana nami kwa chakula cha mchana leo hii.Niko mwenyewe hapa nyumbani na kama ujuavyo chakula cha peke yako katu hakina utamu”Akasema Vero

    “Hamna shida Veronika “Patrick akajibu .Alikwisha anza kumzoea binti yule mrembo.Veronika akamkaribisha Patrick ndani sebuleni na kumuwashia luninga kisha yeye akaelekea jikoni kuandaa chakula.Patrick alijisikia faraja kubwa kwa kukalia tena sofa nzuri kama zile baada ya muda mrefu.

    “ Veronika ni binti mzuri ,mrembo mwenye kila sifa inayohitajika kwa binti mrembo .Ni mwelewa na ana huruma sana.Nafurahi kukutana na binti huyu japo kwa muda mfupi.Nina imani vile vile anaweza kunisaidia kurejesha mawasiliano kati yangu na Happy “ akawaza Patrick mara akastuliwa toka katika mawazo na sauti ya Vero

    “Hello Patrick ,mbona unaonekana mnyonge hivyo?Usihofu kitu .Unaonekana umezama kwenye dimbwi la mawazo.Just relax.Hakuna mtu atakaye kuja kukusumbua.Pumzika mpaka muda wa kurudi ndani utakapofika.” Akasema Verokwa sautiya upole

    “Ahsante Vero,nashukuru sana dada yangu”

    Waliongea mambo mengi na kujikuta wakifahamiana na kuzoeana zaidi.Patrick alimsimulia Vero hadithi nzima ya maisha yake iliyomfanya Veronika atokwe na machozi.

    Hatimaye muda ukafika kwa wafungwa kurejea gerezani wakaagana huku Vero akiahidi kufanya kila njia ili waonane kabla hajaondoka kurudi Dar.

    * * * *

    Ulikuwa ni usiku mgumu sana kwa Vero.Hakujua ni kwa nini Patrick alikuwa ameingia moyoni mwake kwa kasi ya ajabu namna ile.

    “Sielewi ni kwa nini Patrick amenigusa ghafla hivi .Ni kijana mpole ,mtaratibu na mwenye kuvutia hata akiwa katika mavazi ya kifungwa.Namuonea huruma sana .Ameugusa sana moyo wangu.Nitajitahidi niweze kumsaidia katika kipindi chote atakachokuwepo gerezani.Toka nimezaliwa sijawahi kuguswa moyo wangu na kijana yeyote kama alivyonigusa leo Patrick na hadithi ya maisha yake.Ni mapenzi mazito aliyonayo kwa Happy ndiyo yaliyopelekea mpaka kijana wa watu anasota gerezani.Namuonea wivu huyo Happy kwa kumpata kijana mwenye upendo wa dhati kama Patrick.Natamani kama angekuwa ni mpenzi wangu.Ningejitahidi kwa kadiri niwezavyo kuweza kumfanya mwenye furaha daima.I’m dreaming for a man like Patrick.Ana karibu kila kitu ninachokihitaji kwa mwanaume wa ndoto zangu.Lakini mhh!!!… Mbona naanza tena kuwaza mambo ya ajabu ajabu?Ni kwa nini siwezi kupitisha hata dakika moja sijamuwaza Patrick ? Mhh !! nahisi tayari ameanza kuingia moyoni mwangu taratibu.Ouh My God help me with these feelings.” Veronika akajikuta akiwa katika mawazo mazito

    “Ingekuwa ni mimi ndiye niliyepelekea Patrick akafungwa nisingekubali kabisa kwenda Ulaya na kumwacha akiteseka gerezani peke yake.Stupid girl Happy . Nitafanya kila niwezalo ili kuifanya sura ya Patrick iwe na tabasamu tena.Nitahakikisha anakuwa msafi,anakula vizuri na kupata raha zote.Mkuu wa gereza ni mjomba wangu.Nitamweleza ukweli ili aweze kunisaidia.Nitamuomba kila siku Patrick awe akipangiwa kufanya kazi kwa mkuu wa gereza ili aweze kupata nafasi ya kula vizuri na kupumzika." akawaza Veronika huku akiendelea kujigeuza geuza pale kitandani akijaribu kuutafuta usingizi.

    Wakati Veronika akiwa katika wakati mgumu kwa mawazo usiku huo hali haikuwa nzuri sana kwa upande wa patrick .Mchana wa siku hiyo ulimkumbusha mbali sana.Ulimkumbusha kipindi alichokuwa katika mapenzi mazito na Happy . Alizikumbuka nyakati zile za furaha alizokuwa nazo .Alihisi kuihitaji furaha ile tena.

    Ghafla ikaja picha ya Veronika akiwa na sinia lenye chupa ya chai .Akakumbuka toka wakati akinywa chai ile na jinsi alivyokula chakula kitamu siku hiyo .

    “Mhh haya ni majaribu makubwa sana” Akawaza

    “Bado nampenda sana Happy lakini mbona Veronika naye anakuja kwa kasi sana katika mawazo yangu.Mhh ! hapana labda ni kwa ajili ya ule ukarimu wake.Tangu nimefungwa sijawahi kukutana na binadamu ambaye si mtu wangu wa karibu mwenye roho ya huruma na upendo kama Veronika.Veronika hatofautiani sana na Happy .Nahisi hii ni sababu inayonifanya niwe nikimuwaza sana kwa sababu kila nikimkumbuka Vero ananifanya nimkumbuke Happy " akawaza Patrick .



    Urafiki kati ya Patrick na Veronika ulikua kwa kasi sana.Vero kwa kupitia mjomba wake ambaye ndiye aliyekuwa mkuu wa gereza alihakikisha kuwa patrick anapangiwa kufanya kazi mbali mbali nyumbani kwa mkuu wa gereza.Bila uoga Veronika akamueleza ukweli mjomba wake Joel armendo mkuu wa gereza hilo kuhusu urafiki wake na Patrick.Alimueleza kila kitu kuhusiana na hisia zake kwa kijana huyu.Mjomba wake alimwelewa na akaahidi kumsaidia Vero lakini Ili kujiridhisha na maelezo ya Veronika mara moja akaanza kufanya uchunguzi juu ya kijana huyu ambaye jarada lake linaonyesha kuwa alihukumiwa kifungo kutokana na kesi ya kuua bila kukusudia.Hakuridhika sana na maelezo yale.Hakutaka Veronika awe na mahusiano na kijana mwenye rekodi ya uhalifu.Siku moja akamwita Patrick ofisini kwake na kuanza kumuhoji mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na kutaka kufahamu historia kamili ya Patrick.Hadithi ya Patrick ilimkuna sana Joel na kumfanya aridhike na kuoa kuna umuhimu wa kumsaidia Patrick katika maisha ya pale gerezani.Joel akajikuta akimpenda sana Patrick hasa kutokana na tabia yake nzuri na kujituma.Familia nzima ya Joel Armando ilitokea kumpenda Patrick na kadiri siku zilivyozidi kwenda taratibu wakaanza kumhesabu kama mmoja wa wanafamilia.Kila siku alipangiwa kufanya kazi nyumbani kwa mkuu wa gereza na kusaidia kazi mbali mbali mpaka muda wa kurudi gerezani ulipowadia.Hakuhitaji tena kusimamiwa .Alikuwa ni mfungwa ambaye alitokea kuaminiwa mno siyo tu na wakuu bali hata wafungwa wenzake na askari magereza wote.

    Urafiki na ukaribu baina ya Patrick na Veronika ukaongezeka maradufu.Veronika alifurahi mno kwa ukaribu ule kiasi kwamba hakuwa na hamu hata ya kurudi nyumbani kwao Dar es salaam..Mama yake akashangaa sana kwa binti yake kuchukua muda mrefu namna ile kurudi nyumbani wakati makubaliano yalikuwa atumie wiki mbili tu kwa mjomba wake lakini sasa ni wiki ya tatu hajarejea . Mama yake akaamua kumpigia simu kaka yake Joel ambaye ndiye mjomba wa Vero na kumwomba amwambie Vero arudi haraka sana Dare s salaam kwani shughuli nyingi zilikuwa zikimsubiri.Veronika alikuwa ndiye msimamizi mkuu wa miradi na shughuli zote za familia yao.Veronika alilia sana usiku huo kwa kuachana na Patrick kijana ambaye tayari alikwisha mzoea kwa kiasi kikubwa na urafiki mzito ulikwisha anza kujengeka baina yao.Alikuwa na matumaini makubwa ya kuwa urafiki ule ni lazima ungekuwa ni wa manufaa kwake..

    Siku iliyofuata alimweleza Patrick kuwa mama yake anamwitaji arudi Dar mara moja.Taarifa hii ilikuwa ni ya mstuko kwa Patrick pia kwa sababu tayari alikwisha mzoea sana Veronika.

    “Usihofu Patrick pamoja na kwamba ninaondoka lakini nitajitahidi walau kila mwisho wa mwezi niwe nakuja hapa kukutazama.Niambie kitu kimoja Patrick..”

    “kitu gani hicho Veronika ?” Patrick akauliza

    “Will u miss me ?! “

    Patrick akatabasamu ,akamshika mkono Vero na kusema.

    “ Very much.I’ll miss you very much Vero”

    Veronika akatoa tabasamu pana sana baada ya kusikia kauli ile.

    “Lakini usijali kama nilivyokwambia nitajitahidi kuja mara kwa mara kukuangalia.Isitoshe familia ya mjomba ipo nawe hivyo hutajisikia mkiwa hata kidogo na hapa kuna simu nitakuwa nakupigia kila siku tunaongea .Nadhani hutanimiss sana” akasema Veronika.

    “Vero usijali sana .Unajua toka siku ya kwanza tumeanza urafiki nilijua tu iko siku utaondoka.Tayari nilikuwa nimekwisha jiweka tayari kwa hilo.Usihofu chochote juu yangu,mimi nimekwisha zoea kuumia.Siyo siri Vero kuondoka kwako ni jeraha jingine kubwa katika moyo wangu.Umekuwa mtu wangu wa karibu sana na kunifanya nisahau mateso na mchungu yote ya gereza japo kwa muda mfupi...”Patrick akasema

    “Patrick najua una uchungu sana kwa mimi kuondoka.Hata mimi ninaumia vile vile kwa kukuacha peke yako hasa katika kipindi kama hiki ambacho ni wazi unahitaji sana mtu wa kukufariji na kukupa moyo.Lakini usijali nitarudi .”

    “Nimekuelewa Vero.Ila naomba unisaidie kitu kimoja”

    “Kitu gani hicho Patrick niambie niko tayari kukusaidia kitu chochote” akasema Vero

    “Kama unavyofahamu kuhusu kinachoendelea baina yangu na Happy .Nina imani Happy hajui kama nimehamishwa gereza na anaendelea kunitumia barua kwa kutumia anuani ya gereza la awali .Wazazi wangu pamoja na mkuu wa gereza nilikotoka ndio waliokuwa na kazi ya kuniunganisha na Happy lakini mpaka sasa hivi hawajaja kunitazama.Kwa hiyo sifahamu nini kinachoendelea.Ninachohitaji toka kwako ni msaada wako ili niweze tena kuwasiliana na Happy .Nitaandika barua na kumweleza Happy kila kitu na nitaomba ukanisaidie kuiposti kwa haraka.” Akasema Patrick.

    Akionyesha uso wa furaha Veronika akajibuCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Usihofu Patrick .Nimekwisha kueleza toka awali kuwa nipo kwa ajili yako,hivyo usisite kunituma jambo lolote lile na nitakusaidia kwa uwezo wangu wote”

    Siku hiyo Patrick akaandika barua ndefu na kumfahamisha Happy juu ya uhamisho wake na kuzidi kumsisitiza juu ya ahadi zao walizowekeana..

    “Kazi kubwa bado ninayo” Aliwaza vero usiku kabla ya siku ya kuondoka kwake.

    “Ninampenda Patrick lakini bado inaonyesha mapenzi yake yako kwa Happy .Mapenzi yao ni ya dhati kabisa.Ni ndoto yangu ya siku nyingi ya kumpata kijana mwenye mapenzi ya kweli kama Patrick.Hata hivyo bado sikati tamaa.Happy yuko mbali na mimi niko karibu na Patrick nani alisema fimbo ya mbali inaua nyoka? Kwa kuwa ninampenda Patrick nitapambana .Kwanza ni lazima niuvuruge uhusiano huu wa Patrick na Happy baada ya hapo utazaliwa uhusiano mpya kati ya Patrick na veronica.” Akawaza Veronika na kwa hasira akaifungua barua ile aliyopewa na Patrick ili akaiposti kwenda kwa Happy akaanza kuisoma.alipomaliza akairudia tena na tena.Ilikuwa ni moja kati ya barua zenye msisimko wa hali ya juu.

    “Siwezi kuituma barua hii.Maneno aliyoyaandika humu yanaweza kumfanya mgonjwa aliye mahututi kupona ghafla.Ni maneno yenye mahaba mazito.I deserve a guy like him.He must be mine.” Vero akasema mwenyewe kwa hasira huku akiichana katikati ile barua aliyopewa na patrick.

    " Nitakuwa mjinga kama nitaituma barua hii iende kwa Happy na kuzidi kuliimarisha penzi la Patrick na Happy wakati hata mimi ninamtaka Patrick..Natakiwa niuvuruge kabisa uhusiano wao ili niweze kuipata nafasi ya kuwa na Patrick..Penzi lao ni zito na kuwatenganisha si kazi rahisi lakini I will have to do something.Lazima nifanye kila linalowezekana niwatenganishe Patrick na Happy..I'll do anything I mean anything to separate them..." akazidi kuwaza Veronika.

    * * * *

    Ni siku moja tu tangu Veronika aondoke ,Patrick akatembelewa na wazazi wake.Ilikuwa ni siku ya furaha kubwa mno kuwaona tena wazazi wake .Aliruka na kufurahi,alitamani kama Vero ngekuwepo ili awafahamu wazazi wake.

    Kitu kikubwa ambacho alikitarajia na kukisubiri kwa hamu ni iwapo kulikuwa na barua yoyote toka kwa Happy .Aliamini wazazi wake watakuwa wamekuja na barua kwa sababu kimepita kipindi kirefu sasa toka alipopokea barua ya happy kabla hajahamishwa gereza..Patrick hakupoteza muda akauliza iwapo wamekuja na barua yoyote toka kwa Happy .Baba yake akajibu kwa masikitiko

    “Patrick ninasikitika kuna mambo mengi yametokea hapa kati kati na hukuwa ukifahamu..Kwa ufupi tu ni kwamba nilipata uhamisho wa ghafla kwenda Dar es salaam na ndiko tunakoishi kwa sasa.Toka tumehama hatujapata mawasiliano yoyote toka kwa Happy .Tulitaarafiwa na mkuu wa gereza ulilokuwa awali kwamba umehamishiwahuku hivyo hatukupita tena katika gereza la Iringa.Kama atakuwa ametuma barua basi zitakuwa zimetua katika mikono ya watu wengine.Nasikitika vile vile kwa kutomfahamisha juu ya kuhama kwetu ili asiendelee kutumia anwani ile tuliyokuwa tukiitumia awali “.akasema baba yake Patrick

    Patrick akainama kwa sekunde kadhaa akitafakari.

    “Oh My God” Akajikuta akitamka kwa nguvu.Kukosa mawasiliano na Happy kulimtesa sana.

    “Patrick mwanangu “Akasema mama yake baada ya kumuona mwanae amezama katika mawazo ghafla.

    “Nadhani ni wakati sasa wa kusahau yote yaliyopita na kuanza maisha mapya.Nakuomba jitahidi toka moyoni mwako uweze kumsahau Happy .Nakuomba umsahau na uuvunjilie mbali urafiki kati yako na huyo Happy .Bila Happy usingepatwa na matatizo haya mwanagu. ,Happy kakusababishia matatizo mpaka umefungwa gerezani lakini yuko wapi leo ? yuko Ulaya anasoma ! Wewe unasota gerezani,umepoteza masomo na mwelekeo mzima wa maisha .Angalia mateso unayoyapata mwanangu.Mimi na baba yako hatulali tunakuwaza wewe mwanetu.Kama ni kweli angekuwa anakupenda na kukuthamini basi asingekubali kwenda Ulaya na kukuacha peke yako hapa gerezani ukiteseka.Sisi wazazi wako tunasema hatutaki tena kuusikia urafiki kati yako na Happy .yaliyotokea yametokea tunashukuru. na tunamwachia Mungu lakini hatutaki tena kusikia wala kumwona Happy mtoto asiye na fadhila hata kidogo.’ Akasema mama yake Happy.Patrick akastuka sana.Akamtazama mama yake na kusema

    “ Hapana mama kamwe sintathubutu kufanya kitu kama hicho maishani mwangu.Siwezi kumuacha Happy hata iweje.Nilipambana kwa ajili yake na kwa ajili ya kuulinda utu na heshima yake na yote hii ni kwa sababu nampenda.Nikumuacha leo haya yote niliyoyafanya kwa ajili ya upendo wangu kwake yatakuwa ni bureWazazi wangu siwezi hata kwa sekunde moja kumsahau au kuachana na Happy..”Akasema Patrick huku machozi yakimtoka. Baba yake akamuangalia na kusema

    “Patrick sisi ni wazazi wako na ndio wenye tamko la mwisho.Kauli yetu ni hii hatutaki kumsikia Happy masikioni mwetu.Narudia tena hatutaki kabisa kumsikia binti huyo wala kusikia eti una mahusiano naye..You and her its over...” Akasema baba yake kwa hasira kisha akatoka nje.

    Hili likawa ni jaribu lingine kwa Patrick la kutenganishwa na mtu aliyempenda kupita maelezo.Alikuwa njia panda je achague kuwa na Happy au wanavyotaka wazazi wake ? Mama yake akaendelea kumbembeleza mwanae ausikie ushauri wao ili amani iweze kudumu kwani ndugu wote walikuwa wamepitisha azimio hilo kuwa hawataki kuusikia urafiki wa Happy na Patrick.Patrick hakuwa na jibu la kutoa kuhusiana na amri ile ya wazazi wake ya kumtaka atengane na Happy.Wazazi wake wakaondoka na kumuacha Patrick akiwa katika mawazo mengi mno



    Veronika alifika nyumani kwao Dar na kulakiwa na mama yake.Ilikuwa ni furaha sana kwa mama huyu kumuona tena mwanae ampendaye.Wakiwa katika mlo wa jioni mama yake Vero akaanzisha mazungumzo.

    “ Vero hebu niambie kisa cha kukaa kwa mjomba wako siku zote hizi hali makubalianao yetu yalikuwa ni wiki mbili tu.Unafahamu fika kuwa hapa niko peke yangu sina mtu mwingine wa kunisaidia katika biashara Msaidizi wangu pekee ni wewe.”

    Vero akatabasamu na kusema

    “mama samahani sana kwa kukaa siku zote hizi kwa mjomba na kukuacha peke yako.Sikuwa nimetarajia kufanya hivyo ila ilitokea dharura ikanibidi nikae.Nashukuru hata ulivyonipigia simu kwani bila hivyo nadhani ningeendelea kukaa zaidi.” Akasema Vero huku akicheka kichini chini

    “Dharura gani hizo we mtoto hebu niambie.” Akasema mama yake.Happy akala vijiko viwili vya chakula kisha akasema

    “mama wewe ni mzazi wangu lakini umekuwa ndiye mshauri wangu na zaidi ya yote umekuwa ni rafiki yangu wa karibu sana.Ni kutokana na juhudi zako wewe za kunifundisha maadili mema ndio maana leo hii nimekuwa ni binti mwenye mafanikio na kukuletea heshima kubwa.Katika mambo ambayo umekuwa ukiniusia kila siku na kunionya ni kujikita katika mahusiano ya kimapenzi.Nimekuwa nikilifuatilia hilo na ndio maana mpaka umri huu najivunia usichana wangu.Kweli mama simjui mwanaume mpaka leo hii.Lakini mama mapenzi ni kitu ambacho hakikwepeki.Mapenzi yapo na kila mtu kwa wakati wake anajikuta yu mapenzini kama nilivyojikuta mimi.”

    Alisita kidogo baada ya kumuona mama yake akimtazama kwa macho yenye udadisi .

    “Mama nikiwa kule kwa mjomba Songea nilifanikiwa kukutana na mwanaume ambaye ninaamini ndiye mwanaume wa ndoto zangu.”

    Akatulia tena na kuyaacha yale aliyoyasema yazame kabisa kwa mama yake.

    Kisha akamsimulia kisa kizima,jinsi alivyokutana na Patrick na hadithi nzima ya maisha ya Patrick .

    Mambo yalikuwa tofauti na jinsi Veronika alivyowaza.Yeye alitegemea labda mama yake angemgombeza na kumkanya juu ya jambo lile lakini ikawa tofauti.

    “Vero mwanangu nimefurahi sana kwa kuwa wazi na hisia zako.Ni wazi mapenzi hayakwepeki.Yapo na kila mtu anapenda.Mimi nafurahi kusikia kuwa kijana huyo unampenda kwa dhati.Anaonekana ni kijana mtaratibu sana na mwenye mapenzi ya kweli.Mimi nakuunga mkono na niko tayari kukusaidia kwa lolote lile ili uweze kufanikiwa kumpata kijana huyo umtakaye.Kwani lengo langu ni wewe uishi maisha ya furaha na si karaha.” Waliongea mambo mengi kisha wakaagana na kila mmoja akaenda zake kulala.

    Hakuweza kupata usingizi usiku huo.alikuwa na furaha kubwa sana baada ya mama yake kukubali kubariki harakati zake za kumpata Patrick.

    “Sasa kinachofuata ni kuharibu kabisa kila kitu baina ya Happy na Patrick.” Akasema kimoyomoyo halafu akachukua kalamu na karatasi akakaa mezani na kuanza kuandika barua ambayo alipanga aitume kwa Happy .

    Kwako dada Happy

    Ni matumaini yangu kuwa unaendelea vizuri na masomo huko uliko.

    Naomba kabla yote nijitambulishe kuwa mimi ni jirani wa akina Patrick hapa Sumbawanga.Tumeishi vizuri na familia yao na baadaye nikahamia mkoani Mbeya.Kwa jina naitwa Grace.Nilisikia matatizo yaliyomkumba Patrick.Nikasikitika sana.

    Si lengo langu kusema haya yote lakini dhumuni kuu la barua hii ni kukufahamisha kuwa Patrick mpenzio Amefariki dunia kwa ugonjwa wa kuhara akiwa gerezani.

    Kaka yake ndiye aliyenipa anwani yako na kunitaka niwasiliane nawe na kukufahamisha juu ya kifo hicho.Anadai kuwa hawawezi kukufahamisha kwa sababu familia yao haitaki kukusikia kabisa hasa baada ya kumsababishia matatizo mtoto wao na kumwacha akiteseka gerezani hali wewe ukipata maisha mazuri i na kuendelea na masomo yako huko Marekani.

    Pole sana dada ,haya ndiyo mambo ya dunia.Ulimpenda sana Patrick lakini Mungu kampenda zaidi.Jipe moyo na utampata kijana mwingine kama Patrick

    Pole sana

    Grace

    Vero Aliipitia tena na tena barua ile na kuhakikisha iko safi na siku iliyofuata akadamka na kwenda kuiposti.

    * * * *

    Akiwa katika mawazpo mengi akimuwaza mpenzi wake Patrick na maisha anayoyaishi gerezani mara mlango waq chumba chake ukagongwa .Kwa uvivu Happy akainuka na kwenda kuufungua .Alikuwa ni mtumishi wa chuo aliyekuwa na bahasha mkononi.Akamkabidhi Happy barua ile kisha akaondoka.

    Happy aliitazama barua ile kwa wasi wasi .Alitazama muhuri ulikuwa wa Tanzania.Mwandiko juu ya bahasha hakuufahamu ulikuwa ni wa nani.

    Kwa muda wa miezi miwili sasa amekuwa akiandika barua mfululizo kwa Patrick kupitia wazazi wake bila kupata majibu.Hii ilimpa wasiwasi mkubwa .aliumia sana kila alipofikiria Patrick atakuwa katika hali gani.aliujutia uamuzi wake wa kwenda Marekani na kumwacha Patrick peke yake.Alijiuliza maswali mengi juu ya ukimya huo uliotokea ghafla.

    Taratibu akakaa kitandani na kuifungua barua ile na kuanza kuisoma kwa makini.Kabla hajamaliza akapiga ukelele mkubwa sana,akaanguka chini na kupoteza fahamu.

    Ukelele ule ulikuwa mkubwa kiasi cha kuwastua wenzake waliokuwa katika vyumba vya jirani.Watu walifika hapo chumbani na kumkuta Happy amezimia.haraka haraka wakamchukua na kumkimbiza katika hospitali ya hapo chuoni kwa ajili ya huduma ya kwanza.

    Hakuna aliyeweza kufahamu mara moja sababu ya Happy kupiga ukelele ule na kupoteza fahamu.

    Saa saba za usiku Happy akazinduka na kujikuta akiwa hospitali.Michelle pamoja na wanafunzi wengine walikuwa pembeni ya kitanda.Alifumbua macho akatazama pande zote kisha akalala tena.Baada ya kama nusu saa akaamka tena na kukaa kitandani.Daktari akafika ,akampima na kumwomba aendelee kupumzika.

    Alijilaza kitandani na kuanza kukumbuka mambo yaliyotokea .Alikumbuka barua ile aliyotumiwa na kuanza kulia.Michelle ambaye kwa sasa ni rafiki mkubwa wa Happy alifanya kazi ya ziada kumbembeleza

    “ Nyamaza kulia Happy..tafadhali usilie tena..” akasema Michelle

    “siwezi kunyamaza Michelle,kilio hiki hakiishi leo,ni kilio cha milele.Nimempoteza mtu muhimu sana maishani mwangu.”akasema Happy kisha akaendelea kulia.

    “ Umempoteza nani,baba,mama au ndugu? Akauliza Michelle

    “Michelle its Patrick.Patrick is dead”

    “Whaat? Michelle naye akastuka.Aliufahamu uhusiano wa Patrick na Happy kwani kila siku Happy alikuwa akimuhadithia namna anavyompenda Patrick

    ” Yes Patrick is dead” Happy akazimia tena.

    Baada ya muda akazinduka.Safari hii aliweza kutazama lakini hakuweza kuongea .Alijaribu kufungua mdomo lakini maneno hayatoki.Ni machozi tu ndiyo yaliyokuwa yakitiririka..Iliubidi uongozi wa chuo kuwataarifu wazazi wake juu ya ugonjwa wa mtoto wao na kwa haraka ikawalazimu waende kumtazama.Ilikuwa ni siku ya sita tangu amelazwa hospitalini hapo wazazi wake walipowasili.Aliwaeleza kilichotokea wote wakastuka sana.Hawakuwa na taarifa kwamba Patrick amefariki kwa sababu toka Happy alipoondoka na kwenda Marekani kusoma hawakuwahi kumtembelea tena Patrick gerezani kwa hiyo hawakuwa na taarifa zozote juu yake.Wazazi wake wakajitahidi kwa kila namna walivyoweza kujaribu kumliwaza binti yao ili aweze kurejea katika maishaya kawaida kwani alionekana kukata kabisa tamaa ya maisha.



    * * * *

    Wiki ya kwanza ikakatika bila ya Veronika kutokea.Patrick akaanza kupatwa na wasiwasi kwani Vero alimuahidi kuwa atakuwa akimtembelea karibu kila wiki.Alikuwa na hamu sana ya kutaka kupata walau ujumbe wowote toka kwa Happy kwani Vero aliahidi kufanya kila analoweza ili kurejesha mawasiliano kati yake na .Patrick alijipa moyo na kuendelea kusubiri.Wiki ya pili ikakatika hatimaye ya tatu na ya nne Vero akarudi Songea kwenda kumjulia hali Patrick.

    Patrick alifurahi mno kumuona tena Vero.Vero naye alifurahi sana kumuona Patrick kijana ambaye amekuwa akimkosesha usingizi.Bila ya kupoteza muda Patrick akataka kufahamu kama kuna habari yoyote kutoka kwa Happy .

    Veronika akamwangalia kwa sekunde kadhaa akakohoa kidogo kisha akasema

    “Patrick nimekuja na habari Fulani ambazo si nzuri “

    Patrick akastuka na kuuliza.

    “habari gani hiyo Vero”

    Vero akatulia kidogo kisha akaendelea

    “Patrick nimechelewa kuja kukuona kama nilivyokuwa nimekuahidi lakini kilichonichelewesha ni suala hili hili la Happy .”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Happy ? Kafanya nini tena? Patrick akauliza kwa hamaki

    “Patrick you are strong I know but you need to be more stronger to hear this” Vero akasema

    “Vero sikuelewi .Mbona unanichanganya?Go straight to the point” akasema Patrick

    Vero akajiweka sawa akakaza sura ili asije onekana anadanganya

    “Patrick ! Nilipiga simu chuoni kwa Happy kama tulivyokuwa tumekubaliana na nikaambiwa kuwa Happy alikuwa amehama chuoni hapo muda mrefu.Sikuchoka nikaomba nielekezwe alihamia chuo gani nikasaidiwa nikakipata chuo alichokuwa anasoma nikapiga simu na kweli nikampata lakini nilipojitambulisha tu kuwa nina ujumbe muhimu toka kwa Patrick akakata simu.Nilistuka sana lakini sikukata tamaa.Kwa muda wa siku mbili mfululizo nikawa napiga simu lakini haipokelewi.basi nikaamua kumtumia binamu yangu mmoja ambaye naye anasoma huko huko lakini chuo kingine tofauti na hiki cha Happy .Yeye akafanya uchunguzi wake na baada ya siku kama tano hivi akaniambia kuwa amefanikiwa kumfahamu Happy lakini kwa bahati mbaya Happy amepata bwana ambaye anaishi naye na inavyosemekana tayari ana ujauzito wa mzungu huyo.Niliumia mno nikapiga tena simu kwa hasira nikaongea naye bila aibu akanijibu hivi “ sitaki kusikia habari yoyote juu ya Patrick .Kama ni gerezani alitaka kwenda mwenyewe.mwacheni akae atatoka atatafuta maisha yake.Mimi nina mtu wangu kwa sasa na sitaki usumbufu hata kidogo na wala huko Tanzania sitegemei kurudi tena ..Halafu akakata simu.Nikaj………………..” Hakumalizia sentensi yake Patrick akaanguka chini na kupoteza fahamu.Vero akapiga kelele kuomba msaada na mara wakaja askari magereza na kumbeba Patrick na kumkimbiza katika zahanati ya hapo gerezani kwa ajili ya kumpatia huduma ya kwanza.

    Veronika akachanganyikiwa na kijasho kikamtoka.Alijilaumu sana moyoni kwa kutunga uongo ule mkubwa kiasi cha kuhatarisha maisha ya wawili hawa waliopendana.Hakutegemea kama hali ingekuwa vile



    Hatimaye miezi ikatika bila ya mawasiliano yoyote baina ya Patrick na Happy .Wakati Happy akiamini kuwa Patrick ni marehemu ,Patrick kwa upande wake yeye alikuwa bado ana hasira moyoni kwa kusalitiwa na Happy .Alijiona mjinga sana kwa kuyatoa maisha yake kwa mtu asiyekuwa na thamani kwake hata chembe.Alilia usiku na mchana kwa kitendo hiki cha Happy .Happy yeye alikuwa akimlilia Patrick kila siku.Kila alipoiona picha yake machozi hayakukauka.

    Taratibu kila mmoja kwa upande wake akaanza kukubaliana na matokeo kuwa hayakuwa mapenzi ya Mungu wao kuwa pamoja.Kila mmoja akamweka mwenzie kama kumbukumbu ya pekee maishani.Pamoja na kukubali huko kuwa Patrick alikuwa amekufa lakini Happy alikuwa na dhamira moyoni ya kuja kulitafuta kaburi la Patrick na kutoa heshima zake kwa mtu pekee aliyempenda na kumthamini.

    Wakati Happy akiwa na wazo la kuja kutembelea kaburi la Patrick pindi atakaporejea nyumbani Patrick yeye aliamua kumsamehe kwa maamuzi aliyoyafanya na kuamua kusonga mbele na maisha yake.Ingawa ni kitu ambacho kilimuumiza akili kila siku lakini alijitahidi aweze kumsahanu Happy na kuanza maisha yake mapya bila ya kiumbe huyu aliyempenda zaidi .

    Ni katika wakati huu mgumu aliokuwa nao Patrick ndipo Veronika alipozidisha ukaribu wake kwa Patrick.Patrick kwa kiasi Fulani alishukuru sana kwa kufahamiana na Vero kwani yeye ndiye mfariji mkuu wake mkuu katika kipindi hiki kigumu alichokuwa nacho.Ni vero pekee ambaye anaonyesha kumuelewa na kumjali.Ukaribu wao ukaongezeka mara dufu na tayari kukaanza kuwa na kila dalili za kuibuka kwa uhusiano mzito baina yao.

    “Vero ni msichana mrembo ,ambaye ni wazi anaonyesha ana mapenzi ya kweli.Vero amekuwa ndiye mtu wangu wa karibu.Ni yeye tu ambaye anaonyesha kunielewa na kunisaidia.Ni kwa sababu ya Vero leo hii maisha yangu hapa gerezani yamekuwa mazuri kwani ninaishi kama niko nyumbani.Mjomba wake Vero mkuu wa gereza ananijali mno na kunithamini.Yote hii ni kwa sababu ya Vero.Amenifanya nisijione mkiwa tena,ameniondolea lindi la mawazo mazito niliyokuwa nayo juu ya Happy .Vero amenisaidia kurudisha tena matumaini ya ndoto zangu ambazo tayari zilikuwa zimeanza kufutika,kwa haya yote aliyoyafanya Kwa nini basi nisimpe nafasi aliyokuwa nayo Happy ? Nilitambua toka awali kuwa Vero ananipenda lakini ikawa vigumu kuipata nafasi ndani ya moyo wangu kwa sababu wakati huo funguo ya moyo wangu alikuwa nayo Happy .Ninakubaliana na hisia zangu kuwa Vero ndiye msichana pekee ambaye anaweza kuliziba pengo la Happy “

    .Patrick akawaza kwa kina sana juu ya suala hilo na akadhamiria kumtamkia wazi wazi Vero juu ya adhma yake ya kutaka wawe wapenzi.

    * * * *

    Ingawa alihuzunika sana kwa kusikia kuwa Patrick mpenzi wa Happy amefariki dunia kwa upande mwingine Mike Cambell alikuwa na furaha isiyo kifani kwani aliamini kuwa sasa ni nafasi yake ya pekee ya kuwa na Happy.Aliamini kuwa kwa sasa Happy hatakuwa tena na kisingizio cha kumkataa .Alihama toka New york city hadi Washington DC ambako Happy alikuwa akisoma.Lengo likiwa ni kujaribu kujenga ukaribu kati yake na Happy .

    Taratibu akaanza kujenga mazoea na kuwa karibu na Happy na kumfariji kwa kumnunulia maua n.k.Yeye na dada yake Michelle wakajitahidi kwa kadiri walivyoweza katika kumfariji na kumuondolea Happy majonzi yasiyokwisha.Walitoka kila mwisho wa wiki na kwenda sehemu mbali mbali za kuvutia na burudani lengo likiwa ni kujaribu kumsahaulisha juu ya msiba wa Patrick.Baada ya miezi minne kupita tayari Happy alikwisha anza kurudia hali yake ya kawaida.Tayari ukaribu mkubwa ulikwisha jengeka kati yake na Mike kiasi kwamba hakusikia raha kupitisha siku bila kumuona kijana huyu ambaye ametokea kuwa mfariji wake mkubwa hasa katika kipindi hiki cha msiba mkubwa uliompata.

    Pamoja na ukaribu huo uliojengeka baina yao bado ilikuwa ngumu kwa Happy kuitoa nafasi ya Patrick kwa mtu mwingine.Kwa mapenzi mazito aliyokuwa nayo kwa Patrick alikuwa radhi aishi peke yake kwa heshima ya kijana huyu.Suala hili liliendelea kumuumiza kichwa Mike kwa muda mrefu lakini hakukata tamaa.Alizidi kuonyesha mapenzi ya wazi na nia dhahiri ya kutaka kuwa na Happy .

    Siku moja wakiwa katika klabu ya usiku Mike akaamua tena kumkumbushia Happy juu ya ombi lake la kutaka wawe wapenzi.

    “Happy naomba kwanza nitangulize samahani kwa jambo ninalotaka kukueleza kwa sababu najua unaweza usilipende.” Akanyamaza kidogo huku Happy akimtazama kwa macho maangavu.

    “Najua bado uko katika kipindi kigumu cha kufiwa na mpenzi wako.Kusema kweli ni kipindi kigumu kwetu sote kwa sababu wewe ni rafiki yetu wa karibu na hivyo huzuni yako ni yetu pia.Pamoja na yote yaliyotokea ambayo ni kazi ya Mungu,lakini maisha hayana budi kuendelea.Ninachokusihi ni kuyasahau yote yaliyotokea na kuanza maisha mapya” Akanyamaza akamtazama Happy usoni halafu akaendelea.

    “Happy nimeona nikueleze tena kile nilichokueleza muda mrefu uliopita.Happy napenda kwa mara nyingine tena kukuhakikishia kuwa wewe ni mwanamke pekee ambaye umeweza kutua katika moyo wangu na kukataa kutoka kama vile nyuki anavyong’ang’ania ua lenye asali tamu..Toka mara ya kwanza nilipokutia machoni sura yako imejichora moyoni mwangu kiasi ambacho haitaweza kufutika kamwe.Happy nakupenda kupita ninavyojipenda mwenyewe.Naomba kwa mara nyingine tena unipe nafasi ndani ya moyo wako ya kuwa nawe.Ninaomba unipatie nafasi ya Patrick .Wewe ni mwanamke mrembo ambaye unahitaji mtu mwenye mapenzi ya dhati na ya kweli kama alivyokuwa Patrick.Siwezi kuwa kama Patrick lakini ninakuhakikishia kuwa upendo wangu kwako ni wa kweli na wa dhati .Niko tayari kufanya lolote lile katika dunia hii ilimradi tu niwe na wewe.Tafadhali Happy naomba unielewe ninaposema kuwa moyo wangu unateketea kwa penzi lako.Naomba unipe nafasi ndani ya moyo wako “

    Mike akasema na kumtazama Happy ambaye alikuwa amenyamaza huku machozi yakimtoka kwa mbali.Akatoa kitambaa katika pochi yake akajifuta uso halafu akakaa vizuri na kusema

    “Mike kwanza napenda kuchukua nafasi hii kukushukuru wewe na Michelle kwa kuwa watu wangu wa karibu.Sio siri mmenisaidia sana na hasa katika kipindi hiki kigumu nilichokuwa nacho.Bila uwepo wenu sijui ningekuwa katika hali gani.Mmekuwa na mimi katika kila hali,kila dakika.Mmefanya kila mliloweza kunifariji na mpaka leo hii ninaendelea vizuri.Sioni kitu cha kuwalipa zaidi ya maneno haya machache Ahsanteni sana.Kuhusu suala ulilonieleza ,naomba unipe muda wa kutosha wa kutafakari na kufanya maamuzi.Nitakapokuwa tayari nitakujibu”akasema Happy na Mike akamuelewa na hakutaka tena kuendelea kulionglea suala hilo.

    BAADA YA MIAKA MITANO

    Hatimaye siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu ikawadia.Ni siku ambayo Patrick alihitimisha adhabu yake ya kutumikia miaka mitano gerezani.Tangu asubuhi ya siku hiyo Patrick alikuwa ni mtu mwenye furaha sana.Aliwaaga wafungwa wenzake wote huku akiwa mwingi wa tabasamu.Wakati Patrick akiwa mwingi wa furaha kwa upande mwingine ilikuwa ni simanzi gerezani kwa kuondokewa na kijana kama huyu ambaye alipendwa karibu na kila mtu.Alikuwa mstari wa mbele katika kuwapa moyo na kuwafariji wale wenzake waliokata tamaa,vile vile alikuwa ni kiungo kikubwa katika kuwasaidia wenzake kupata vitu kama sigara,sabuni n.k kwa sababu yeye muda mwingi alikuwa akishinda nyumbani kwa mkuu wa gereza hivyo kuvipata vitu hivyo kwake ilikuwa rahisi..Kuondoka kwake lilikuwa ni pigo kubwa kwa wale wafungwa waliokuwa wakimtegemea .

    Saa tatu na nusu juu ya alama Patrick aliitwa katika ofisi ya mkuu wa gereza ambako alitaarifiwa rasmi kuwa kuanzia muda huo alikuwa huru.Aliombwa awe raia mwema huko aendako ili asije rudishwa tena gerezani.Hii ilikuwa ni kama ndoto.Hakuamini hadi pale mkuu wa gereza alipompa mkono na kumwambia kuwa yuko huru na kumtakia kila la heri katika maisha yake .

    Katika lango la kuingilia gerezani kundi kubwa la watu likongozwa na wazazi wa Patrick lilikuwa likimsubiria kwa hamu kubwa.Walikuwepo ndugu na baadhi ya rafiki zake akiwemo rafiki yake Andrew ambaye walikutana hapo hapo gerezani lakini yeye aliwahi kutoka.Alikuwepo pia binti mrembo ambaye urembo wake leo hii ulizidi mara dufu.Alikuwa amependeza zaidi ya maelezo.Huyu ni Veronika ambaye yeye pamoja na ndugu zake na mama yake waliungana na familia ya akina Patrick katika kusherehekea tukio hili kubwa .Tayari Patrick na Vero walikwisha kuwa wapenzi na urafiki wao ulikuwa na baraka ya pande zote mbili yaani upande wa akina Patrick hali kadhalika mama na ndugu zake Veronika hawakuwa na kipingamizi chochote juu ya urafiki huu.

    Taratibu lango likafunguliwa na Patrick akaruhusiwa kutoka nje akiwa huru.Alitumia sekunde kadhaa kulitazama gereza hilo ambalo amekaa takribani miaka mitatu.

    Huku akitiririkwa na machozi mama yake alikuwa mtu wa kwanza kumkumbatia mwanae,kisha wakafuata wengine wote waliokuwapo hapo .Zilikuwa ni dakika chache zenye furaha kubwa .Wote wakapanda katika magari yaliyoandaliwa na kuanza safari ya kuelekea Dar .Patrick alipanda katika gari maalum lililokuwa likiendeshwa na Andrew rafikiye mkuu pamoja na mfariji wake na hatimaye mpenzi wake ,Veronika.ambaye kwa sasa alikuwa ni kila kitu kwake .

    Ndani ya gari Patrick na Vero walikuwa wamekumbatiana wote wawili machozi yakiwatoka.Patrick alikumbuka toka alivyoonana na Vero siku ya kwanza,wakazoeana na kuwa marafiki na hatimaye kwa sasa ni wapenzi.Alimshukuru sana Mungu kwa kumrudishia furaha iliyokuwa imepotea baada ya kumpoteza Happy .Mwanzoni aliamini kuwa Happy ndiye ilikuwa furaha yake lakini baada ya Happy kuondoka akatokea Vero na kuirudisha tena furaha hiyo.Veronika alionyesha mapenzi ya kweli na uvumilivu mkubwa katika kipindi chote walichofahamiana mpaka leo.

    “Veronika nashukuru sana kwa yote uliyonifanyia.Nashukuru kwa upendo wa ajabu ulionionyesha”Akasema Patrick kwa kunong’ona.

    “ahsante pia Patrick kwa kuufungua moyo wako na kunikubali .Najiona ni mwenye bahati sana kuwa na mtu kama wewe.” Akasema Veronika.

    * * * *

    Hatimaye Happy naye baada ya kumaliza masomo yake akarejea nyumbani Tanzania.Toka akiwa safarini alikuwa na shauku moja tu ya kutaka kufahamu mahala alipozikwa Patrick .Tayari alikwisha kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Mike cambell.Alikubali kumpa nafasi Mike baada ya kuamini kwamba Patrick hatarejea tena.

    Familia yake yote ilikuwepo uwanja wa ndege kumlaki.Tayari baba yake alikwisha staafu kazi na sasa familia yote inaishi jijini Dar es salaam.Happy alipata mapokezi makubwa sana toka kwa familia yake.

    Siku tatu tu baada ya kuwasili nchini Happy akafunga safari hadi mjini Sumbawanga ambako ndiko Patrick alikuwa akiishi mwanzo.Kule alitaarifiwa kuwa familia ya akina Patrick ilikwisha hama muda mrefu na walihamia jijini Dar es salaam. Hakukata tamaa akaondoka na kuelekea Iringa katika gereza ambalo Patrick alikuwa amefungwa mwanzo.Lengo lilikuwa ni kupata ukweli juu ya kifo cha Patrick.Pale gerezani alitaarifiwa kuwa Patrick alihamishwa na kupelekwa katika gereza jipya huko Songea.Pale gerezani hawakuwa na kumbukumbu naye zozote.

    Happy hakukata tamaa akafunga safari tena hadi Songea katika gereza jipya ambako ndiko Patrick alihamishiwa.Pale akaonana na mkuu wa gereza na kumweleza kilichompeleka.Mzee Joel ambaye ni mjomba wa Veronika akamwangalia kwa mstuko .

    “wewe ndiye Happy kibaho? Akauliza baada ya kuikumbuka historia ya Patrick

    “Ndiye mimi mzee “Happy akajibu

    Mzee Joel akamtazama kwa makini na kuuliza

    “Happy nimefurahi kukuona.Niliwahi kusikia habari zako toka kwa Patrick.Nimeshangaa kwa wewe kuja kumuulizia Patrick hapa gerezani ina maana hamkuwa mkiwasiliana wakati ukiwa masomoni?

    “Tulikuwa tukiwasiliana lakini mawasiliano yakakata ghafla sana na siku moja nikapokea taarifa kuwa Patrick alifariki kwa ugonjwa wa kuhara akiwa gerezani.Baada ya kurejea nyumbani nimeona nitafute kwanza taarifa sahihi za kifo chake na nifahamu mahala alikozikwa.Nimeelekezwa kwamba alihamishiwa katika gereza hili”

    Mkuu wa gereza akstuka sana alipopata taarifa ile inayohusiana na kifo cha Patrick .Kwa kiasi fulani taarfa ile ikamchanganya kwa sababu kwa mujibu wa taarifa aliyoipata toka kwa Vero ni kwamba Happy akiwa masomoni nchini Marekani alipata bwana mwingine na kuolewa naye na kumsahau Patrick kitu kilichopelekea Patrick ampe nafasi Veronika.

    Mzee Joel akakaa kimya akitafakari kisha akasema

    “Happy kwanza nakupa pole sana kwa yote yaliyotokea kati yako na Patrick.Ni kweli Patrick alihamishiwa katika gereza hili akitokea Iringa.Patrick alikuwa ni mmoja kati ya wafungwa bora kabisa ambaye hajawahi kutokea katika gereza hili.Alipendwa na kila mtu hapa gerezani.Alikaa hapa gerezani hadi alipomaliza kifungo chake na kuachiwa huru.Hapa gerezani alitoka salama salimini .Kama ni kufariki basi atakuwa amefariki baada ya kutoka hapa kwa sababu mimi ndiye niliyeidhinisha kuachiwa huru baada ya kumaliza kifungo chake.”

    Maneno yale yakamfanya Happy atetemeke mwili .Aliinama chini akashindwa kuyazuia machozi kumtoka.Hakuyaamini maneno yale ikambidi aulize tena.

    ‘Mzee sijakuelewa vizuri.Umesema nini?

    “Nimesema kuwa Patrick alimaliza kuitumikia adhabu yake akiwa mzima wa afya na mimi kama mkuu wa gereza hili ndiye niliyemuachia huru baada ya kumaliza kifungo chake.Kama ni kufariki basi alifariki baada ya kutoka hapa gerezani.Nasikitika sana kwa kumpoteza kijana kama yule.” Akasema mkuu wa gereza.

    “mzee mbona taarifa niliyoipata mimi inasema kwamba Patrick alifariki akiwa gerezani? Tena inasema kuwa alifariki kwa maradhi ya kuhara? Happy akasema huku machozi yakimdondoka

    “Taarifa hiyo ulipewa na nani? Mkuu wa gereza akauliza

    “Taarifa hiyo nilitumiwa na mtu nisiyemfahamu akidai kuwa yeye anamfahamu Patrick kwa sababu aliishi jirani na wazazi wake kule Sumbawanga.Dada huyo alisema kwamba familia ya Patrick haikuweza kunifahamisha juu ya msiba wa mtoto wao kwa madai kwamba nilimtelekeza mtoto wao gerezani nikaenda kusoma ulaya,wakati yalikuwa ni makubaliano yetu mimi na yeye.Sikutaka kumwacha Patrick peke yake na mimi nikaenda kusoma Marekani,lakini ni Patrick huyo huyo ndiye aliyenishawishi nikubaliane na uamuzi wa baba wa kunipeleka Marekani kusoma.”akasema Happy

    “Pole sana Happy.Jipe moyo.Haya ni mambo ya kawaida Jitahidi sana uyaruhusu maisha yako yaendelee.”Mkuu wa gereza akasemaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nashukuru sana mzee kwa msaada ulionipa.Japokuwa bado kuna utata mkubwa juu ya kifo hicho lakini namuachia Mungu.Kama amekufa kweli nitamuombea kwa Mungu apumzike kwa amani lakini kama hajafa kweli huko aliko atambue kuwa maumivu anayonisababishia ni makubwa kiasi ambacho siwezi kuelezea.”

    Happy akaagana na mkuu wa gereza ,akapanda gari lake na kuondoka huku machozi yakiendelea kumtoka.Akashindwa kuendesha gari akaegesha pembeni akainamia usukani.

    “ Nina kila sababu ya kuamini kuwa Patrick hajafa.Kutokana na maelezo ya mkuu wa gereza ni kwamba Patrick alimaliza kifungo chake na kutoka gerezani salama.Na katika ile barua niliyoandikiwa ilisema kwamba Patrick alifariki akiwa gerezani.Mbona mambo haya yananichanganya? Je Patrick alinifanyia hila nijue kuwa amekufa? Kama ni kweli hajafa kwa nini basi amenifanyia hivi??”Happy akajiuliza huku akiupiga usukani kwa hasira. .

    “Nilimkosea nini Patrick hadi akaamua kunidanganya na kuniacha niteseke miaka yote hii?Moyo wangu hauna furaha hata kidogo yote hii ni kwa ajili yake .Au labda kitendo cha mimi kuondoka kwenda kusoma Marekani hakikumfurahisha?Anyway nitakutafuta Patrick hata kama itanigharimu maisha yangu I promise I’ll find you because you left me at the time I needed you most “





    Miaka sita sasa imekwisha pita toka Patrick toke gerezani na tayari Patrick amekwisha maliza shahada yake ya kwanza ya uandishi wa habari na tayari ni mwajiriwa katika kituo kimoja kikubwa cha Televisheni nchini.

    Pamoja na kwamba ni muda mrefu umepita lakini picha ya Happy bado haijafutika kabisa moyoni mwake.Huja na kufutika na wakati mwingine humuacha katika huzuni kubwa.

    Uhusiano kati yake na Vero umekomaa ukakubaliwa na ndugu wa pande zote mbili na hatimaye ukafikia hatua ya uchumba .Aliamua kumvisha pete ya uchumba Vero baada ya kuamini kuwa tayari Happy hakuwa na nafasi tena katika maisha yake.Aliamini Vero ndiye mwanamke pekee aliyepewa na Mungu ili awe mke wake.Vero ndiye aliyekuwa naye katika kipindi kirefu cha mahangaiko,Vero amemsaidia kufuta majeraha ya moyo na kuanza maisha mapya,Vero amekuw ani kila kitu kwake.

    Kwa upande mwingine baada ya Happy kugundua kuwa Patrick hakufa gerezani na kuamini kuwa bado yu hai alikumbana na shinikizo kubwa toka kwa wazazi na ndugu zake la kutaka amsahau kabisa kijana huyu na kuolewa na Mike cambell ,kijana mmarekani mweusi ambaye mapenzi yake kwa Happy hayana kifani.Mike amekuwa ndiye mfariji mkubwa wa Happy toka alipopata taarifa kuwa Patrick amefariki dunia.Ni yeye na dada yake Michelle ndio walioweza kumfuta Happy machozi aliyokuwa akilia kila uchao akimlilia Patrick.Ni Mike ndiye aliyejitolea kila alichoweza kukifanya kuhakikisha binti huyu mwenye uzuri uliotukuka anarejea katika maisha ya kawaida.Pamoja na ugumu uliokuwepo wa Happy kumsahau Patrick lakini Mike alivumilia na kuamini kuwa iko siku Happy atamsahau Patrick na yeye kupewa nafasi ndani ya moyo wa binti huyu mwenye sura ya kimalaika..Hatimaye baada ya kujishauri kwa muda mrefu akaamua kumkubali Mike awe mpenzi wake na bila kupoteza muda akakubali kuvishwa pete ya uchumba na Mike Cambell katika sherehe kubwa iliyohudhuriwa na umati wa watu.

    Pamoja na kuamini kuwa Patrick hakuwa ridhiki yake,kitu kilichompelekea akubali kuvishwa pete ya uchumba na Mike lakini bado Happy alikuwa na kitu moyoni juu ya Patrick.Kuna kitu ambacho hakuweza kukifuta moyoni mwake.Na hiki kilizidi kumtesa siku hadi siku licha ya kujitahidi kwa kadiri alivyoweza kumsahau Patrick.

    ********************

    Veronika akamtazama Patrick kwa macho makali na tayari akagundua kuna kitu kinachomsumbua mpenzi wake.Kilichomuumiza roho zaidi ni kwa nini kama Patrick ana tatizo asimwambie?

    Akapanda kitandani na kukaa karibu ya Patrick akamkumbatia .

    “Patrick mpenzi kwa siku chache sasa nimegundua mabadiliko Fulani kwako.Hauko kawaida.Kuna jambo gani linalokusumbua hebu niambie mpenzi wangu.Unajua ninapokuona katika hali hiyo hata mimi ninapata wasiwasi mwingi.Nimezoea kuiona sura yako iliyojaa tabasamu kila wakati lakini kwa sasa unajilazimisha kutabasamu na unaonekana u mwingi wa mawazo.Au kuna kitu nimekuudhi Patrick?

    Aliongea maneno haya taratibu machozi yakimlenga hali kichwa chake amekilaza kifuani kwa Patrick

    “Vero mpenzi hakuna jambo lolote linalonisumbua.Nahisi ni hizi dawa ninazotumia ndiyo zinanifanya niwe katika hali hii lakini usijali si muda mrefu nitarudia hali yangu ya kawaida.”Akasema Patrick huku akimsugua Veronika mgongoni.

    “Patrick mimi ni mchumba wako na nimekuwa karibu nawe kwa muda mrefu sasa.Sidhani kama kuna mtu mwingine anayekufahamu kiundani zaidi yangu.Nina imani kabisa kuna kitu kinakusumbua akili yako .Nina jua kabisa ni wakati gani unakuwa na furaha na ni wakati gani unakuwa na matatizo.lakini sikulazimishi kuniambia.Kama unaona tatizo hilo halina ulazima wa mimi kulijua basi hakuna neno.Ila kumbuka muda wowote utakapohitaji msaada wangu nipo tayari kukusaidia.”

    Vero akambusu Patrick kisha akatoka nje.

    Saa saba za usiku Patrick akastuka toka usingizini .Vero alikuwa pembeni yake amelala .Akamwangalia mpenzi wake kwa dakika kadhaa.akapatwa na uchungu mwingi baada ya kuyaona mapenzi makubwa aliyokuwa nayo binti huyu kwake.

    “Ni wazi vero amekuwa ni msichana wa pekee maishani mwangu ambaye ameweza kunionyesha mapenzi ya kweli na kunisaidia kupata uelekeo mpya wa maisha yangu.Nampenda Vero na nina imani ndiye mwanamke atakayenifaa maishani.lakini huyu Happy ……………mhhh …naye kajitokeza tena katika hatua za mwisho kabisa za kukamilisha ndoa yangu na Veronika.Yes ! nilimpenda Happy kuliko kitu chochote kile lakini alinitenda kitu kibaya nikamwondoa katika moyo wangu.Lakini ni kwa nini siachi kumuwaza ?Kila dakika sura yake inanijia akilini….ooh Mungu wangu nisaidie katika mtihani huu mguu nilionao.Lakini pamoja na yote yaliyotokea baina yetu lazima nimtafute Happy .Ni lazima nionane naye .Lazima nifahamu ni kwa nini alinitenda vile?

    Patrick akamtazama tena vero akamkumbatia kwa nguvu.

    Asubuhi na mapema aliamka akaoga kisha akamuaga Happy kuwa anakwenda kumuona Andrew.Vero hakuwa mbishi akamwacha aende

    Akiwa ndani ya gari Patrick alijaribu tena kupiga ile namba ya simu ambayo aliamini kabisa itakuwa na uhusiano Fulani na Happy lakini bado ikawa haipatikani.

    “Yawezekana labda alipopiga simu jana mchana ikapokelewa na Vero ,walitoleana lugha chafu .Pengine labda walitukanana ,kitendo kilichomfanya akasirike na kuizima kabisa simu yake.”

    Akawasili nyumbani kwa Andrew mishale ya saa moja na dakika ishirini hivi

    “ooh Patrick mbona asubuhi hivi.Kuna usalama kweli? Akauliza andrew kwa shauku ya kutaka kufahamu kama kulikuwa na tatizo lolote.

    “Si kwema andrew” akasema Patrick huku akiketi sofani.

    “Enhe ! kulikoni ? Akauliza tena Andrew

    Patrick akatulia kidogo akavuta pumzi kisha akasema

    “mambo katu si mazuriAndrew.Jana mchana mimi nikiwa nimelala mtu ambaye nahisi atakuwa ni Happy akalipiga simu ,basi si ikapokelewa na Vero?

    “Mhh usiniambie Patrick.Enhee ikawaje? Andrew akauliza huku akionyesha hali Fulani ya mstuko

    ‘Sasa sielewi waliongea nini kwa sababu kwa mujibu wa maelezo ya Vero ni kwamba mtu huyo hakuongea chochote.Nikajaribu kupiga mimi mwenyewe simu ikapokelewa na sauti niliyoisikia ni dhahiri ni ya Happy .Sidhani kama ninaweza kuipotea sauti yake japokuwa hatujaonana kwa kipindi kirefu.Baada tu ya kuitikia akakata simu na kuizima kabisa na hadi muda huu tunapoongea simu yake haipatikani.Nimechanganyikiwa Andrew sijui hata nifanye nini ndio maana nimekuja hapa kwako asubuhi hii ili tuone tufanye kitu gani.”

    Andrew akavuta pumzi ndefu akasimama na kuzunguka zunguka humo sebuleni kisha akasema.

    “Patrick hata mimi naanza kuhisi kuwa kuna kitu waliongea na Vero ambacho kimemfanya awe na hasira na asitake tena hata kuiwasha simu yake.lakini bado hatuna haja ya kukata tamaa,kitu tunachotakiwa kukifanya kwa sasa ni kutafuta mahala anapoishi Happy .kazi hiyo niachie mimi nitaifanya kikamilifu.Baada ya kupafahamu anapoishi itakuwa rahisi kwetu kumpata”

    ‘Ahsante sana Andrew kwa kunisaida.” Baada

    ya dakika chache za maongezi Patrick akaaga na kiondoka.

    ***************

    Happy alistuliwa toka katika usingizi mzito na hodi iliyogongwa mlangoni.Alijiinua kiuchovu na kuangalia saa.Ilikuwa ni saa nne asubuhi.

    “Mhh ! dada mbona umelala hivyo? Mi nimepatwa na wasiwasi pengine unaumwa.” Akasema Margreth.Happy hakujibu kitu akageuka na kukaa tena kitandani huku akiyafikicha macho yake ambayo kwa sasa yalionyesha hali ya kuvimba kutokana na kulia kwa muda mrefu.

    “Happy hebu niambie kitu gani tena kinakufanya uwe katika hali hiyo? Na Patrick vipi ulimpigia simu?

    “Ah ! acha tu Margreth.Nilimpigia simu lakini ikapokelewa na mwanamke.Nilishindwa kuongea jambo lolote nikakata simu.nahisi Patrick tayari atakuwa ameoa”

    Happy akashindwa kuvumilia machozi yakamtoka.

    “Hebu nisikilize dada.Hupaswi kulia.Ninaimani hizo ni hisia zako tu kwamba Patrick tayari ana mke.Huwezi jua pengine labda ni ndugu yake ,dada yake au hata katibu muhtasi wake.hata hivyo ni muda mrefu sasa umepita toka mlipopotezana na mlipotezana katika mazingira yenye kutatanisha sana huku kila mmoja akiwa bado anampenda mwenzake,nina imani kabisa kuwa pendo lile bado liko hai.Najua ndio maana unahisi kuumizwa na hisia kuwa Patrick tayari ana mke kwa sababu bado unampenda.Yawezekana labda atakuwa ameoa au pengine ana mchumba lakini hilo lisikupe shaka.Tutalifahamu muda si mrefu.”

    Maneno yale ya Margreth yanampa moyo sana Happy .

    “nashukuru sana mdogo wangu kwa kunifariji.Pamoja na hayo naomba tafadhali hii iwe ni siri yako na asijue mtu mwingine yeyote yule.”

    “Usijali Happy Hakuna mtu yeyote atakayefahamu juu ya Patrick.leo nataka nimfuate Patrick ofisini kwake kama hii kadi yake ya biashara inavyoonyesha.”

    ***************

    Saa tano na nusu ilimkuta Margreth katika jengo lenye ofisi anakofanyia kazi Patrick .Akashuka garini na na kupanda lifti kuelekea ghorofa ya saba ziliko ofisi hizo alizokuwa akizitafuta.

    Aliposhuka tu katika lifti akakutana na bango kubwa linaloelekeza zilipo ofisi hizo.Taratibu na kwa mwendo wa madaha kama ilivyokawaida yake alifika mpaka katika chumba cha mapokezi akakutana na akina dada wawili warembo,Akajitambulisha na kuoma kuonana na Patrick.

    “Patrick kwa sasa yuko mapumzikoni nyumbani kwake.Alipatwa na matatizo ya moyo hivi karibuni hivyo amepewa muda wa kupumzika .Labda tukuelekeze nyumbani kwake kama kuna ulazima wa kumuona yeye mwenyewe ”

    Margreth akaelekezwa nyumbani kwa Patrick kisha akaaga na kuondoka.

    Ilimchukua kama masaa mawili hivi kuipata nyumba ya Patrick.Kwa mujibu wa ramani aliyopewa alitumaini pale palikuwa ni penyewe kabisa.Taratibu akalisogelea geti kubwa la mbele na kubonyeza kitufe cha kengele.Baada ya kama dakika nne hivi dada mmoja mrembo ,aliyevalia nadhifu akafungua mlango.

    “Karibu dada” Yule dada akasema

    “ahsante sana” Margreth akajibu

    “sijui nikusaidie nini?

    “Samahani dada ,sijui hapa ndio nyumbani kwa Patrick?

    “Yes ndio hapa.Una shida naye ?

    “Yes nina shida naye ya kiofisi.Kuna mzigo wake ulipitia katika ofisi zetu.Baada ya kuona kimya kingi tukaona tumtafute.Nimekwenda ofisini kwake wakanieleza kuwa Patrick ni mgonjwa na wakanielekeza hapa nyumbani kwake.”

    “Kweli dada ,Patrick ni mgonjwa ana wiki ya pili sasa anamumwa.Ana matatizo ya moyo kwa hiyo amepewa muda mwingi wa kupumzika.Hivi tunavyoongea amelala lakini ninaweza kumwamsha kama kuna ulazima wa kuonana naye sasa hivi.”

    “Usijali dada ni masuala madogo tu ya kiofisi hivyo sioni kama kuna haja yoyote ya kumsumbua mgonjwa.Ila atakapoamka mwambie kuwa Margreth Kibaho alifika hapa.”

    “Sawa dada Margreth karibu sana.Mimi naitwa Veronika.karibu basi hata ndani upate walau glasi ya maji.”

    “Nashukuru sana dada Vero siku nyingine nitaingia ndani.Haya kwa heri”

    Margreth akaondoka maeneo hayo huku kichwa chake kikiwa kizito mno kwa mawazo aliyokuwa nayo.

    “Je yawezekana kweli Patrick akawa na mke?Inawezekana Vero akawa ndiye mke wa Patrick?Sasa nimepata picha kamili.Naona siku ile Happy alipopiga simu ya Patrick ikapokelewa na Vero na ndio maana akashindwa kupata kitu cha kuongea.Ok nitamshauri tujaribu tena kumpigia Patrick leo jioni.Aliwaza Margreth akiwa katika kurudi nyumbani.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Saa kumi na moja jioni Margreth akarejea nyumbani kwao na mtu wa kwanza kukutana naye alikuwa ni mama yake ambaye akamwita na kumuuliza

    “margreth ,naomba unieleze kwa undani bila kunificha ni kitu gani kinachomsumbua dada yako?Nina imani ni lazima utakuwa unafahamu kinachomsumbua dada yako.Kutwa nzima amejifungia ndani,hajala kitu na wala hataki kuonana na mtu yeyote.wakuu wake wa Miss Tanzania wamekuja kuonana naye leo hii mchana lakini ameshindwa kuonana nao.na hata waandishi wa habari wamekuja kutaka kumuhoji lakini hao ndio kabisaaa hataki hata kuwasikia.Sasa hebu niambie kitu gani kinachomsumbua mwenzio?

    “Mama hakuna jambo lolote alilonieleza mimi.Nimekuwa nikijaribu toka jana kumshawishi ili anieleze ni kitu gani kinachomsumbua lakini amekuwa mgumu kunieleza.Ni wazi hata mimi naona kuna kitu kinamtatiza .naomba uniachie kazi hiyo mama nitajitahidi kumdadisi.”

    “sawa Margreth jitahidi mwanangu.hali ya dada yako si nzuri na inatia shaka.”

    “tena mama nipeni chakula nimpelekee nitamkoroga mpaka atakula tu.”

    Haraka haraka akapewa sinia la chakula na kwenda hadi mlangoni kwa Happy .Akasimama hapo mlangoni kwa takribani dakika moja akatega sikio na kwa mbali akaisikia sauti ya Happy akilia.Aliumia sana moyoni mwake kuona jinsi dada yake anavyoteseka namna ile kwa sababu ya mapenzi.

    Akagonga mlango kisha taratibu mlango ukafunguliwa akaingia ndani.Ni wazi Happy alionyesha hali ya kukata tamaa kwa jinsi alivyosawajika.Macho yalikuwa yamemvimba kwa kulia.

    “Happy jaribu kuwa jasiri dada yangu.Unajua mambo yanaweza kuwa magumu zaidi iwapo hautaonyesha ujasiri .Hebu kwanza nyamaza kulia ule chakula.Mama anawasiwasi sana juu yako.”

    Happy akamtazama mdogo wake usoni kisha akasema

    “Najua ni rahisi kutamka hivyo kwa sababu wewe hayajakukuta.Ungekuwa katika mahala pangu , sijui ungefanya nini.Huwezi jua ni maumivu kiasi gani niliyonayo moyoni .Naumia sana Margreth.Patrick amekitonesha tena kidonda kilichokuwa kimeanza kupona.”

    “Ok Dada Happy tulia basi ule halafu nikwambie habari za leo”

    “Hebu nieleze kuna habari gani huko utokako? Akauliza Happy

    Margreth akavuta pumzi ndefu akajiweka sawa na kusema.

    “Nilipotoka hapa nikaelekea moja kwa moja katika zilizo ofisi za Patrick kwa mujibu wa wa hii businesscard inavyoonyesha.Nilifika katika ofisi hizo na nikaambiwa kuwa Patrick hayupo anaumwa .amepatwa na mstuko wa moyo na hivyo yuko nyumbani kwake anapumzika.Wakanielekeza nyumbani kwake nikaenda nikamkuta dada mmoja anaitwa Veronika .Akanikaribisha ndani na kutaka kwenda kumwamsha Patrick lakini sikuingia ndani nikamuachia ujumbe kuwa akiamka amwambie kuwa nilifika pale.Kwa ufupi ndiyo hivyo.” Akasema Margreth.

    Happy alibaki ameshika tama asiamini alichokisikia kutoka kwa Margreth.Kilichomfanya anyong’onyee ni kusikia kuwa Margreth alikuta msichana pale nyumbani kwa Patrick.

    “Najua kabisa huyu ndiye aliyeipokea simu siku ile nilipopiga.Yawezekana akawa ni mke wake? Au mchumba wake? Ni lazima nimpate Patrick ili nipate ukweli toka kwake.Yes ni muda mrefu umepita lakini…….”Alikuwa katika mawazo mazito wakati simu ya Margreth ilipolia.Alikuwa ni Mike Camble mchumba wa Happy .

    “Ni mike” Akasema Margreth huku akimtazama Happy.

    “Mwambie sipo “ Akasema Happy huku amejishika kichwa.

    Alichanganyikiwa ghafla.Tayari alikuwa amekwishaanza kukubali matokeo kuwa Mike ndiye mtu wa maisha yake lakini Ghafla sana ametokea Patrick na kumfanya Happy achanganyikiwe.Margreth akaweka sauti kubwa ili Happy asikie watakachoongea.

    “hallow Mike”

    “hallow margreth mambo vipi?

    “safi tu Mike habari ya huko?

    “Huku kwema vipi huko?

    “Huku nako kwema tu”

    “Hebu niambie Margreth mbona Happy simpati katika simu?Nimejaribu sana kuitafuta simu yake lakini haipatikani kabisa.nilipata taarifa kuwa amefanikiwa kulitwaa taji la Miss Tanzania lakini akapatwa na mstuko akaanguka na kupoteza fahamu.Mara ya mwisho alinipigia simu kabla hawajaanza mashindano toka hapo sijapata mawasiliano yoyote toka kwake.Hebu nieleze margreth nini kimetokea?

    Margreth akamtazama Happy kisha akasema

    “Happy alipatwa na mstuko kidogo baada ya kutangazwa mshindi.Lakini kwa sasa anaendelea vizuri.Kuhusu mawasiliano ni kwamba simu yake bado hata hakumbuki aliiweka wapi ngoja kwanza atulie kabisa atakupigia Mike”

    “Ok nimekuelewa margreth upo karibu naye hapo walau niongee naye kidogo?

    “Hapana niko mbali naye kwa sasa.Labda ujaribu kupiga tena baadae”

    “Ok margreth nimeomba wiki mbili za dharura ili niweze kuja Tanzania kukaa naye katika kipindi hiki kigumu alichonacho.Kesho nitaanza safari.Lakini usimwambie chochote .Nataka nimshangaze kidogo.Nitakujulisha kabla sijaanza safari yangu.

    “Ok Mike bye”Margreth akajibu na kukata simu.

    Happy alijilaza kitandani mikono ikiwa kichwani.

    “why me ?Nampenda Mike .Yes nimeshakubali kuvishwa pete ya uchumba na Mike sasa ni kwa nini Patrick ametokea na kufanya akili yangu iyumbe namna hii?

    Happy alijikuta tena katika mtihani mgumu.Ni wazi alimpenda Mike lakini baada ya kutokea Patrick taratibu ameanza kuonyesha dalili za kuanza kumsahau Mike..

    *************

    Saa kumi na moja jioni Patrick akaamka na kumkuta Veronika amekaa pembeni ya kitanda.

    “Unajisikiaje mpenzi? Vero akauliza

    “najisikia vizuri dear”

    Vero akasogeza karibu meza ndogo iliyokuwemo humo chumbani na kumuandalia Patrick kinywaji.

    “My dear wakati umelala kuna dada mmoja alikuja kukutafuta.Lakini nilimwambia kuwa umelala na hakutaka kukusumbua.Akasema kwamba nikikutajia jina lake utakuwa umemfahamu.”

    “ Alisema anaitwa nani?Patrick akauliza kwa shauku

    “Margreth kibaho”Vero akajibu

    “whaaat !!!!!!!!!!!!!....”

    “Margreth Kibaho” Vero akarudia tena

    Patrick akasimama na kujishika kiuno

    “Veronika una uhakika na unachokisema? Patrick akauliza

    “Kwani vipi Patrick mpenzi wangu kuna tatizo gani?hayo ndiyo maagizo aliyoyaacha yeye mwenyewe.” Vero akajibu kwa wasiwasi

    “Oh My god ! Margreth came here ? Alikuwa na nani? Patrick akauliza huku akiwa bado amepatwa na mshangaoCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “alikuwa peke yake”

    Patrick akakaa tena kitandani .Vero akastushwa na hali ile aliyoipata Patrick ghafla akamsogelea na kumkumbatia.

    “My dear Patrick tafadhali niambie kuna kitu gani kinachokusumbua”

    “Hakuna kitu Veronika.”Patrick akajibu

    Patrick akainuka na kumwacha Vero pale kitandani.

    “Vero naenda kwa andrew.Yeyote atakayekuja kunitafuta anisubiri sintakawia sana” Akasema Patrick huku akivaa shati lake.

    ‘Patrick ngoja basi nikusindikize kwa hali hiyo huwezi endesha mwenyewe.”Vero akasema hali machozi yakimlenga lenga

    “Vero hakuna matatizo ninaweza kuendesha”

    Haraka haraka aktoka ndani akaingia garini na kuondoka kwa kasi akimwacha Veronika amesimama mlangoni akimwangalia kwa uchungu.

    ************

    “Patrick kuna tatizo gani best? Aliuliza Andrew baada ya kumuona Patrick jinsi alivyosawajika

    “Uuuuuph ……………” Patrick akapumua kwa nguvu na kujitupa sofani

    “Mambo yanazidi kuwa magumu Andrew”

    “Kwani kumetokea nini Patrick?

    “Margreth alikuja nyumbani”Patrick akasema

    Andrew akamtazama Patrick kwa makini sana.

    “margreth amekuja nyumbani kwako? Alikuja kukueleza nini?Andrew akauliza

    “ Nilikuwa nimelala hivyo sikuweza kuonana naye.Alionana na Vero na kumwachia maagizo kuwa nikiamka aniambie kuwa alifika pale.Nahisi atakuwa alikuja na ujumbe wa muhimu sana.I’m confused”

    Kimya kizito kikatanda hapo sebuleni kila mmoja alikuwa akiwaza lake.Ghafla wote wakastushwa na mlio wa simu ya Patrick.Akaitoa mfukoni na kuangalai namba za mpigaji.Zilikuwa ni namba ngeni kabisa katika simu ya Patrick.

    “ Hallooo” Akaita Patrick.

    “Halloo naongea na nani? Ikauliza sauti ya upande wa pili ambayo ilikuwa ni sauti tamu ya kike.

    “ Patrick hapa”

    “Uuuh Patrick .margreth hapa.”

    “margreth??? Patrick akauliza kwa mstuko

    “Yes margreth Kibaho”

    “I cant believe it.magreth ni wewe kweli??

    “Yeah its me margreth”

    “ sikiliza Patrick ni hivi ,nilikuja nyumbani kwako leo mchana ulikuwa umelala nikamkuta dada mmoja anaitwa Veronika.Pole sana kwa muumwa”

    “Yah vero aliniambia kwamba ulifika nyumbani kwangu”Patrick akasema

    “Kwa ufupi shida yangu iliyonileta ni kuongea na wewe.nahitaji sana kuonana na wewe mapema iwezekanavyo.Kwa hiyo kama upo tayari nijulishe ili nikutaarifu tuonane lini na wapi”

    “Yes margreth nipo tayari,nipo tayari hata sasa hivi,we se…,” hakumaliza sentensi yake Margreth akadakia

    “Ok Patrick nitakutumia ujumbe kukufahamisha ni wapi tutaonana”

    “Sawa Margreth lakini hebu nipe habari za Hap……”Kabla hajamalizia sentensi yake margreth akasema

    “Patrick I have to go.See you ” akakata simu

    Zilipita dakika mbili toka margreth akate simu ,lakini Patrick bado alikuwa ameishikilia simu yake sikioni.

    “Hebu niambie Patrick ni nani uliyekuwa ukiongea naye?

    Sauti hiyo ya Andrew ndiyo iliyomfanya astuke

    “ni Margreth “

    “Anasemaje?

    “Anasema kuwa anahitaji sana kuonana na mimi.hakutaka maongezi mengi amesema atanitumia ujumbe kunitaarifu kuwa tonane lini na wapi.”

    Andrew akainama chini kwa sekunde kadhaa na kisha akasema

    “Mambo yanazidi kupamba moto.Inavyoonyesha kuna jambo zito anataka mkaliongee hususani kizungumkuti hiki kilichopo mbele yetu”

    “Sawa Kabisa Andrew hata mimi nadhani hivyo.”

    Andrew akaiendea friji na kujimiminia mvinyo katika glasi .mara simu ya Patrick inalia tena.Akaichukua na kuiangalia.Ilikuwa ni simu toka kwa shemeji yake yaani dada yake Veronika aishiye Uingereza.Kijasho kikaanza kumtoka.

    “Hallo shemeji” Akasema Patrick

    “ouh Shemeji habari za jioni?

    “Nzuri shemeji vipi huko wazima?

    ‘Huku wote tu wazima,Pole sana shemeji yangu nasikia ulipatwa na matatizo kidogo ya mstuko.Ilikuwa tuje kukuangalia lakini kutokana na kutingwa sana na shughuli tukashindwa”

    “Kweli shemeji nilipatwa na tatizo kidogo la mstuko lakini kwa sasa naendelea vizuri Hivi sasa niko katika mapumziko mafupi na hali yangu inaendelea vizuri.”

    ‘nafurahi sana shemeji kusikia unaendelea vizuri.Nimepiga simu kwa vero sasa hivi akaniambia umetoka kidogo hivyo nikaona ni bora nikupigie katika simu yako.sasa ni hivi pamoja na kukujulia hali nilikuwa nataka kuwataarifu kuwa zile tiketi zenu za ndege za kuja na kurudi Uingereza kwa ajili ya kufanya shopping ya harusi yenu tayari zimekwisha tumwa katika ofisi za british airways hapo dare s salaam na kwa kuwa kila kitu kuhusiana na safari hii kimekwisha tayarishwa basi safari itakuwa kesho kutwa.Mkiwa huku tutaangalia pia uwezekano wa kukupeleka katika hospitali kubwa zaidi kwa ajili ya uchunguzi wa afya yako.Msihofu shemeji hizi zote ni gharama zetu.”

    Ilimchukua Patrick sekunde kadhaa kurudisha akili na kukumbuka kuwa alikuwa akiongea na simu.Alikuwa amechanganyikiwa.

    “hallo shemeji” Aliita shemeji yake baada ya kuona muda unapita hapati jibu

    “Ouh shemeji.”Patrick akajibu

    “Vipi mbona kimya shemeji?

    “mhh shemeji nashukuru sana kwa msaada wenu shemeji yangu.Nimefurahi sana.Kesho tutafanya maandalizi ya mwisho na kesho kutwa tutaanza safari ya kuja hapo uingereza kwa ajili ya shopping ya harusi yetu.”

    “Ok shemeji tunawatakia safari njema”

    “haya shemeji bye” Akakata simu

    Kijasho chembamba kilimtiririka Patrick .Akaitupia simu yake sofani na kujishika kichwa.

    “Patrick kuna nini” Akauliza Andrew

    “Andrew I’m confused”

    “Kwa nini Patrick”

    “Si unakumbuka niliwahi kukwambia kuwa dada yake Vero yule anayekaa Uingereza alikuwa akitushughulikia safari yetu ya kwenda uingereza kufanya shopping ya harusi sasa zile tiketi za ndege za kwenda London tayari zimetumwa na safari wanataka iwe kesho kutwa.”

    “Ooh My God” Andrew akasema huku akizunguka zunguka humo sebuleni

    “Patrick” Akaita Andrew

    “Yes Andrew”

    “hata mimi nahisi kuchanganyikiwa lakini hebu amua kitu kimoja.Nini kifanyike kati ya mpango wa kumtafuta Happy au kushughulikia harusi yako na Vero?Suala la ndoa yako limepiga hatua kubwa sana kwa sasa na vile vile suala la kuonana na Happy nalo liko katika hatua nzuri.sasa chagua moja ili tushughulike nalo kwa ukamilifu”

    Patrick hakujibu kitu akaendelea kujiinamia pale sofani .Baada ya dakika kama mbili hivi akainua kichwa akasema

    “Andrew siendi London “

    “Patrick!!!!!!!! “ Andrew akahamaki

    Patrick akainuka akaichukua simu yake na kuuendea mlango

    “Tutaonana Andrew”

    “Patrick !!! Andrew akapaza sauti lakini tayari Patrick alikwisha ingia garini na kuondoka zake.

    Patrick alifika nyumbani na kumkuta Vero amekaa sofani akimsubiri.Aliinuka akamkumbatia na kumbusu.

    “Welcome back darling.” Patrick hakujibu kitu akambusu shavuni na kwenda kuketi sofani

    “Patrick mpenzi naomba kabla ya yote ule kwanza chakula.Nimekuandalia chakula kizuri sana ili ule na urejee katika hali yako ya kawaida.”

    “ahsante sana vero lakini sijisikii kula kitu chochote leo.Naomba juice baridi”

    “No Patrick lazima ule chakula “ Vero aliongea kwa msisitizo.

    Ni kweli Patrick hakuwa na hamu ya kula lakini hakutaka kumpa Vero mawazo mengi akainuka na kuelekea mezani.Vero alijitahidi kumlisha chakula na kumwonyesha mapenzi ya hali ya juu.

    Baada ya kumaliza kula wakaketi sofani wakiangalia Tv .

    “Patrick darl ,kuna habari nzuri sana nataka nikwambie “ Alisema Vero.

    Patrick akamwangalia Vero usoni kwa kituo kwani alikwishagundua kitu gani Vero alitaka kumwambia.Alitabasamu na kusema

    “jambo gani hilo Vero”

    Vero akakohoa kidogo akaendelea

    “Dada kapiga simu jioni hii na kunitaarifu kuwa tiketi zetu za kwenda na kurudi London kwa ajili ya ile shopping ya harusi zimekwisha tumwa katika ofisi za British airways na safari ni kesho kutwa.”

    Vero aliongea maneno haya huku akimsugua sugua Patrick kifuani.Patrick hakusema kitu alikaa kimya na ni wazi alionekana yuko katika mawazo mazito sana.

    “Vipi dear unawaza kitu gani?

    Patrick akamwangalia Vero usoni kwa muda mrefu kisha akasema

    “Vero dear I’m sorry .Itakubidi uende peke yako.Hali yangu kwa sasa bado si nzuri kusafiri safari ndefu kama hii.Nasikitika sana Vero”

    Vero akasimama wima akashika kiuno huku akimwangalia Patrick

    “Whaat !!!!!!!! “

    “I’m sorry Vero itakubidi uende tu mwenyewe mimi nitabaki niendelee kupumzika .Hali yangu bado si nzuri kusafiri safari ndefu kama hii”

    “No Patrick inatubidi tumuone daktari kwanza ili athibitishe kama kweli itakuwa ngumu kwa wewe kusafiri .Halafu isitoshe dada amesema kuwa watagharamia uchunguzi wa afya yako huko huko Uingereza sasa tatizo liko wapi mpenzi?

    “Veronika nimeshasema hali yangu si nzuri sasa huyo daktari wa nini tena? Ni yeye anaumwa au mimi? Tafadhali Vero hakuna mjadala katika hili” Patrick akasema kwa hali Fulani ya ukali

    Vero akaondoka sebuleni hapo kwa kasi huku akilia



    Patrick akaogopa akamfuata.Vero alikaa kitandani huku akilia kwa kwikwi.Patrick akamsogelea na kumkumbatia.

    “Vero mpenzi najua ni kwa kiasi gani kauli yangu hii imekuumiza moyo.Samahani sana kwa hilo mpenzi wangu.Wewe ndiwe kila kitu kwangu na wala sina sababu yoyote ya kukuliza.Nisamehe Vero mpenzi wangu.”

    Patrick aliingia katika kazi nzito ya kumbembeleza Vero

    “Patrick why ur doing this to me?Nimekukosea nini Patrick mbona unanifanyia hivi lakini?Patrick umebadilika ghafla.Mbona nakuwa sikuelewi ?.Hebu niambie kama kuna jambo nimelikosa niombe msamaha na nijirekebishe.”

    Maneno yale yanamwingia vilivyo Patrick anamfuta Veronika machozi

    “Veronika nyamaza mpenzi wangu.Nakupenda sana kuliko kitu chochote.Sikuwa na lengo au nia mbaya kukwambia vile ni kutokana tu na hali yangu kutokuwa nzuri bado .Hata mimi mwenyewe inaniuma sana .Lakini hakijaharibika kitu tunaweza tukapanga ukaondoka hata na Andrew akakusaidia katika shopping”

    “Shame on you Patrick.Nafunga ndoa na wewe au Andrew?Andrew ndiye mpenzi wangu au wewe?Hebu jaribu kukaa chini na kufikiri kwa makini.Dada amejitolea kugharamia uchunguzi wa afya yako katika hospitali kubwa ili kabla ya harusi yetu uwe katika hali nzuri sasa unadhani atanielewaje akisikia huendi?

    Patrick hakujibu kitu.Maneno yale ni wazi yalitoka ndani kabisa mwa moyo wa wa Vero.Alimwonea Huruma Vero kwa hali ile aliyokuwa nayo lakini ghafla sura ya Happy inamjia akilini akajikuta akitamka.

    “Vero I love you soo much.Sioni kama kuna ubaya wowote kama ukienda peke yako?Huna haja ya kuwa na wasiwasi Vero wewe ni wangu na muda si mrefu Mungu akijaalia tutafunga ndoa sasa wasiwasi wa nini mpenzi?Wewe u wangu Vero na popote nisipokuwepo wewe ni badala yangu kwa hiyo sioni bado tatizo lolote katika hili”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Vero hakujibu kitu akaendelea kulia.

    Mara ujumbe mfupi ukaingia katika simu ya Patrick .Akaufungua na kuusoma huku moyo wake ukienda kwa kasi sana..Ujumbe ule ulitoka kwa Margreth Kibaho

    ‘Kesho saa nne asubuhi Sean snacks Mbezi.margreth”

    baada ya kuusoma ujumbe ule akaufuta kabisa katika simu yake.

    ************

    Saa kumi na moja alfajiri Vero ndiye aliyekuwa wa kwanza kuamka .Hakutaka kumwamsha Patrick.Taratibu akaingia bafuni akaoga kisha akavaa nguo na kumwamsha Patrick.

    “Patrick naondoka”

    Patrick akafikicha macho yaliyojaa usingizi akasema

    “Mbona mapema hivyo kuna nini?

    “Nothing.Tutaonana”

    Ni wazi Veronika aliondoka akiwa bado na hasira na haikuhitaji akili ya ziada kung’amua kuwa dada huyu mrembo alikuwa amekasirika.Patrick hakutaka kujibizana naye ingawa aliumia sana moyoni kwa hali ile waliyoifikia katika uhusiano wao.

    Akiwa hapo kitandani Patrick akajaribu kurudisha kumbukumbu nyuma toka walivyoanza kufahamiana na Happy ,urafiki wao ulivyoanza hadi walivyokuja kutengana.Kumbukumbu zikamjia siku alipoiona suya ya Happy katika Luninga na akapoteza fahamu.Kumbukumbu zikamrudisha tena Diamond Jubilee ambako Happy alitwaa taji la miss Tanzania.

    “Ni lazima nionane na Happy .”Alitamka maneno haya kwa sauti.

    Taratibu akajiinua kitandani na kuingia bafuni kujimwagia maji.Akiwa chumbani kwake akijiandaa mara simu yake inaita.Ilikuwa ni simu toka kwa mama yake.

    “Sikamoo mama ‘

    “marahaba.Hivi wewe mtoto una matatizo gani jamani?Umepatwa na nini Patrick?Hivi ni kitu gani kinakusumbua we mtoto? Mama yake alisema kwa ukali.mama huyu ni mmoja kati ya akina mama wakali na asiyependa mchezo

    “mama kwani kuna nini mbona hivyo? Aliuliza Patrick makusudi hali akijua kuwa amekwisha likoroga.Alijua tu tayari Vero atakuwa amekwenda kushtaki nyumbani .

    “Umemfanya nini mwenzio?

    “nani Vero?

    “sasa kwani una wenzio wangapi?

    “hakuna chochote kibaya mama nilichokifanya .Ni tatizo la kupishana kauli tu”

    “sasa sikiliza Patrick nataka ufike hapa nyumbani haraka sana asubuhi hii.Mbona unaanza kutuumiza vichwa we mtoto?Alifoka mama yake

    Patrick hakujibu kitu akakaa kimya kwa sekunde kadhaa kisha akastuliwa tena

    “Umenisikia lakini?Nataka uje hapa nyumbani haraka iwezekanavyo.Na ukae ukijua kuwa kesho ni lazima usafiri vinginevyo umtafute mama yako.”

    Patrick kijasho kikamtoka.Akajikaza na kusema

    “mama huko unakofika sasa ni mbali mama yangu.Nitakuja nyumbani tuongee ila si kwa asubuhi hii.Kuna mahala natakiwa niende Nina miadi ya muhimu sana “

    “Hiyo miadi ni muhimu kushinda wito wangu mimi mama yako?

    “Nothing is important than you mother”Akajibu Patrick

    “Ah! Ah! Ah!!! Sitaki kabisa kusikia hivyo vingereza vyako.Kama unaona mimi ni muhimu njoo nyumbani haraka sana.”

    “mama samahani siwezi kuja nyumbani sasa hivi .Tayari nina miadi na mtu na ananisubiri asubuhi hii .Nitakuja baada ya kutoka huko.M…..

    Kabla hajaendelea akasikia simu ikikatwa.Patrick akabaki njia panda.Je aende kwa mama yake au aende katika miadi yake na Margreth?

    Akiwa amezama katika fikra nzito hajui nini cha kufanya mara mlango unagongwa na Andrew akaingia.

    “Hi Patrick” Andrew akasema

    “Hi” Patrick akajibu

    “Hebu niambie ndugu yangu mambo yanakwendaje kwa sababu nimepokea simu toka kwa mama asubuhi hii akilalamika sana juu yako.Anasema kuwa Vero ameenda pale alfajiri na kumweleza kuwa umebadilika mno kwa siku hizi za karibuni.Na kikubwa zaidi ni kukataa safari ya kwenda London.Hilo ndilo linawafanya wawe na hasira juu yako.Sikiliza Patrick kuna kitu kimoja ulichokosea nacho ni kuonyesha wazi wazi kuwa kuna jambo zito linakusumbua.Tayari Vero amekwisha ng’amua hilo .Na hili la kukataa kwenda safari ndio limedhihirisha wazi kuwa kuna kitu unakificha.Chonde chonde Patrick jaribu kuwa makini ili tusije haribu mambo.”

    Patrick akafikiri kidogo kisha akasema

    “ Andrew nakubali nilifanya kosa kuonyesha wazi wazi kuwa kuna suala linanisumbua.Nilishindwa kujizuia.That was a mistake.Lakini hata iweje safari hiyo ya kwenda shopping Uingereza siwezi kwenda.Leo nina miadi na Margreth na ninafikiri baada ya hapo nitaonana na Happy sasa huoni kuwa kwenda kwangu London kutaharibu kabisa mpango wangu mzima wa kuonana na Happy .Ni wazi ninahitaji kuonana na Happy .”

    “lakini Patrick mimi bado kuna kitu kimoja ninakifikiria ambacho kinaniumiza kichwa sana” Andrew akasema

    “Jambo gani hilo” Patrick akauliza huku akimkazia macho Andrew

    “Kuhusu wazazi wako pindi watakapokuja gundua kuwa unampango wa kuonana na Happy ”

    Patrick akatabasamu kidogo halafu akasema

    “Andrew masuala haya yote niachie mimi”

    “Siwezi kukuachia wewe peke yako Patrick kwa sababu mimi na wewe tunaonekana ni kitu kimoja.Chochote unachofanya wanajua na mimi nimeshiriki.Ukikosea wewe na mimi nimekosea pia.”

    “Kwa hiyo unataka kusemaje Andrew? Patrick akauliza

    “ Nafikiria kitu kimoja”

    “Kitu gani hicho?

    “Naona ni bora tu angali bado mapema uachane na suala hili la Happy .Kwa sasa uko katika maandalizi ya kumuoa Vero , huoni kuwa kuendelea kulipa kipaumbele suala hili la kuonana na Happy linapelekea hata masuala mengine ya msingi kuhusu ndoa yako kuanza kuharibika?.Naona ni bora ukaelekeza nguvu zako katika suala la ndoa yako.Suala la Happy bado halina uzito sana kwa sasa Isitoshe imekwisha pita miaka mingi na tayari Happy ana mchumba wake.Sioni sababu ya kutumia nguvu nyingi katika kumtafuta mtu ambaye alikutia matatizoni halafu baade akakuacha na kwenda zake Ulaya.Vero ndiye mwanamke pekee aliyekaa nawe katika kipindi chote hiki cha matatizo na ambaye amesimama na wewe hadi sasa ambapo maisha yako tayari yamekaa sawa.Hivi unavyofanya si vizuri na ninakwambia ukweli rafiki yangu unamuumiza Vero sana.” Andrew akasema na kumtazama Patrick usoni ambaye maneno yale yanamfanya abadilike uso wake.

    “What the hell are you talking about Andrew?. Patrick akauliza kwa ukali.

    “Andrew nimekwisha kwambia mara nyingi kwamba kama hutaki kuwa upande wangu naomba uniache.Sikulazimishi kushiriki katika masuala yangu”

    “Patrick ! huo ulikuwa ni ushauri wangu tu na si lazima uufuate.Pamoja na ushauri huo niliokupa kama rafiki yako,lakini mwisho wa siku mwenye uamuzi juu ya masuala yako ni wewe mwenyewe..Ok tufanye kama unavyotaka”

    ************

    Saa nne kamili juu ya alama ilimkuta Patrick katika maeneo ya Sean snacks.Hakutaka kupoteza hata dakika moja katika miadi hii ya muhimu.Sehemu hii ni moja kati ya sehemu tulivu sana .Ni mahali panapofaa sana hasa kwa maongezi ya faragha.

    Mara tu aliposhuka garini alitumia muda wa kama dakika kumi kuzunguka maeneo hayo kwa minajili ya kuangalia kama anaweza akamuona Margreth.Mara simu yake ikalia.Zilikuwa ni namba ngeni.

    “Halloo “ Patrick akaita

    “Margreth hapa uko wapi Patrick?

    ‘Nimeshafika kitambo ,nilikuwa najaribu kuangaza angaza kama nitakuona”

    “Mimi ndio nafika sasa hivi.Njoo basi huku nyuma kiunga L”

    Akiwa bado amesimama alijikagua kwanza na kuhakikisha yuko katika muonekano nadhifu kisha akapiga hatua kuelekea mahala alikoelekezwa.

    “Wow Patrick” Ilikuwa ni sauti ya Margreth mara tu alipomuona Patrick.Patrick hakusema kitu akamtazama Margreth kisha akamkumbatia kwa nguvu.Margreth machozi yalikuwa yakimtoka.Mtu aliyesemekana kufariki dunia leo hii wameonana.

    “Patrck siamini kama leo tumekutana tena.Siamini kwa kweli” Margreth akasema huku akifuta machozi.

    “Patrick sitaki kulia tena .Tumekwisha lia vya kutosha kwa ajili yako.Tunashukuru Mungu kwamba u mzima na ametukutanisha tena.Huu ni kama muujiza ambao hakuna aliyeutegemea.” Margreth akasema

    “sawa kabisa Margreth hata mimi sikutegemea kabisa kama nitakuja kuonana nanyi tena hasa kutokana na mambo yaliyotokea .Na ndio maana nilipatwa na mstuko wa moyo baada ya kumuona tena Happy katika Tv .Hebu kabla hatujaendelea naomba unipe japo kwa muhtasari maendeleo ya hali ya Happy .”

    “Happy anaendelea vizuri” Margreth akasema kwa ufupi huku akimtazama Patrick usoni kwa makini.

    “Really?

    “Yes .She’s fine.Tuachane na hayo.tuendelee na kilichotukutanisha hapa” Margreth akasema

    “Ok Margreth ,lakini naona tumejisahau hata kuagiza vinywaji.Sijui unatumia nini?

    “Mimi nakunywa wine.Wewe je bado unaendelea na kunywa Juice mpaka sasa?

    “Yes margreth.Patrick habadiliki.Umuonaye ndiye Patrick yule yule wa zamani..Ingawa mhh mwenzangu umebadilika sana yaani umependeza sasa hivi umekuwa msichana mrembo kama dada yako Happy .” Wote wakacheka kisha Patrick akainuka na kufuata vinywaji.

    “Patick” Alianza maongezi Margreth baada ya Patrick kurejea na vinywaji.

    “Ni mengi sana yametokea katika kipindi hiki tulichopotezana.Ni mambo mengi kiasi kwamba tukianza kukumbushana itachukua siku nzima.Kabla sijaendelea kwa niaba ya familia yetu nakupa pole nyingi sana kwa yote yaliyotokea.Sitaki kukumbusha mateso na machungu ya adhabu ile ya kifungo lakini kwa dhati kabisa naomba niweke wazi kuwa familia yetu haikukutupa na kukuacha peke yako gerezani.Baada ya Happy kuondoka alituachia jukumu la kukuangalia mara kwa mara gerezani.lakini baadae zikaja taarifa kuwa umehamishwa gereza na ndio wakati huo huo baba akawa amestaafu kazi tukahama Mbeya na kuhamia Dar es salaam.Toka hapo ndipo utengano ulipoanzia.Tulipofika Dar mdogo wetu akaanza kuumwa hivyo tukatumia muda mwingi kumuuguza kiasi cha kukusahau kabisa.Kitendo hiki cha kukusahau tayari kimetia doa kubwa sana baina yako na sisi.”

    Akanyamaza akanywa funda kadhaa za wine kisha akaendelea.

    “Patrick kitu kingine kilichotufanya tukate tama kabisa ni baada ya kupata taarifa kuwa umefariki ukiwa gerezani”

    “Nimefariki nikiwa gerezani ? Patrick akauliza kwa mstuko.

    “Yes Patrick Happy alipata taarifa kwamba umefariki ukiwa gerezani.”

    Patrick akavuta pumzi ndefu halafu akaseam kwa sauti ndogo

    “I cant believe this.Nani alimtumia taarifa hizo kwamba nimefariki dunia?

    “Siwezi kufahamu Patrick taarifa za kifo chako alizipata toka kwa nani.Suala hilo atakueleza yeye mwenyewe kwa kirefu pindi mkionana uso kwa uso” Margreth akasema

    Patrick akazama katika mawazo mengi ya ghafla.taarifa ile ya kwamba alikuwa amefariki dunia ilikuwa imemstua mno.



    Margreth akamtazama Patrick usoni halafu akaendelea.

    “ Ni vigumu mno kulezea uchungu uliotupata baada ya kupata taarifa ile.Happy alilia mno ,akawa akizimia kila siku mpaka ikabidi baba na mama wasafiri kwenda marekani kukaa naye na kumfariji.Baada ya kumaliza masomo yake Happy alirudi nyumbani na kitu cha kwanza alichokifanya ilikuwa ni kutafuta ni wapi ulikozikwa.Baada ya kufanya uchunguzi ikagundulika kuwa taarifa zile za wewe kufariki hazikuwa za kweli.Tulikaa tukimuomba Mungu kwa mapenzi yake atukutanishe siku moja.Mungu amesikia maombi yetu na hatimaye leo hii tumeonana.”

    Margreth akatulia ,akachukua glasi yake ya wine na kupiga funda kadhaa.Patrick jasho lilikuwa likimtoka.Alikosa kitu cha kuongea.Kutokana na joto kali alilokuwa akilisikia akavua koti kisha akatoa kitambaa na kujifuta jasho lililokuwa likimtiririka kwa wingi.Machozi yalimlenga lenga.

    “Patrick” Margreth akamstuaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Haikuwa dhamira yangu kuongea mambo haya ila ni katika kuweka mambo na kumbukumbu sawa. kikubwa kilichonifanya nikutafute kwa hali na mali ni suala hili lililoko mbele yetu.Patrick suala hili ni suala gumu sana.kwa taarifa yako ni kwamba Happy alipatwa na mstuko mkubwa mpaka akapoteza fahamu mara tu alipokuona.Leo hii umeniambia kuwa hata wewe ulipatwa na mstuko baada ya kumuona Happy katika Tv na wewe ukapoteza fahamu.Happy kwa sasa yuko katika wakati mgumu sana akitafuta jinsi ya kuonana na wewe na nina imani hata wewe pamoja na yote yaliyotokea utakuwa na shauku ya kutaka kuonana na Happy .”

    Margreth akanyamaza na kimya kikapita.

    “Patrick hali ya Happy si nzuri.Nasema si nzuri kimwili na hata kiakili.Tangu amekuona Diamond Jubilee Happy anashindwa hata kula.anashinda analia.Hakuna mwingine anayetaka kuongea naye zaidi yangu.Mimi peke yangu ndiye inayeweza kuongea naye tukaelewana.Ni kutokana na hali yake hii imenibidi nichukue jukumu la kukutafuta ili tuone ni jinsi gani tunaweza kulitatua tatizo hii lililoko mbele yetu.Pamoja na kwamba mmepotezana miaka mingi sasa lakini nina imani wakati mnapotezana kila mmoja alikuwa bado akimhitaji mwenzake na ndio maana baada ya kuonana kila mmoja amepatwa na mstuko wa ajabu.Kitu ninachohitaji kukifanya ni ninyi kukutana .”

    Margreth akakaa kimya na kuyaacha maneno yale yazame kabisa ndani mwa Patrick.

    “Yes ni lazima mkutane tena.Kinachomuumiza Happy kwa sasa ni jinsi gani atakavyoweza kuonana na wewe.Nina imani hata wewe utakuwa na hamu ya kuonana na Happy japokuwa miaka imeenda na kila mmoja kwa sasa ameendlea na maisha yake.Nina imani mtakapoonana mtaongea na yatakwisha.najua kila mmoja analo la kumweleza au kumuuliza mwenzake kwa hiyo mtakapokutana utakuwa ni mwanzo mpya wenye amani.Hata kama hamtarudiana tena lakini litakuwa jambo jema kama mtamaliza tofauti na kuendelea kuishi kwa amani.”

    Patrick alikuwa kimya kabisa jasho likiendelea kumtiririka.Akarekebisha koo na kusema

    “margreth uko sahihi.Ni lazima nionane na Happy .”

    Margreth akatabasamu kisha akasema.

    ‘Ok Patrick nashukuru sana kama umeridhia kuonana na Happy .Nimefurahi sana.Nina imani ni fursa hiyo ambayo hata Happy alikuwa akiingojea kwa hamu kubwa.Sasa basi kama unavyojua Happy kwa sasa ni mrembo wa Tanzania.Tayari ana jina kubwa.Kila analolifanya yeye kwa sasa linakuwa ni habari.Vyombo vya habari na hasa haya magazeti ya udaku yanamfuatilia usiku na mchana.Kwa hiyo basi hatutaki kutengeneza story na kuwafaidisha watu.Makutano haya yawe ni ya siri kubwa kiasi kwamba iwe ni siri baina ya mimi wewe na Happy .makutano yenu yafanyike nje ya dare s salaam ambako hamjulikani kabisa.Mimi napendekeza makutano yenu yawe morogoro au we unasemaje?

    Patrick akafikiri kisha akasema

    “Hapana margreth Morogoro bado ni karibu sana na Dar es salaam.Morogoro hapawazuii watu kufunga safari na kuwafuatilia hasa wakijua kuwa wanatengeneza story ambayo itawaingizia fedha.Mimi napendekeza tukakutanie Arusha.Tena nje kabisa ya mji.Pale tunaweza kukaa tukaongea na kuweka mambo sawa bila kuingiliwa na mtu yeyote yule.Au we unaonaje margreth?

    “Hilo ni wazo zuri .Tena zuri sana.Nina imani hata Happy mwenyewe hawezi kulipinga kwa sababu akili yake yote kwa sasa ni kuonana na wewe tu hata kama makutano ni Ulaya.Ok hebu nipe dakika tano hivi niongee naye nisikie anasemaje.”

    “Ok Margreth.”

    Margreth akatoa simu yake na kwenda mbali kidogo na mahali walipokuwa wamekaa akapiga simu.

    Baada ya kama dakika kumi hivi akarejea.

    “Enhee anasemaje Happy ? Patrick akauliza kwa shauku.

    Huku akitabasamu Margreth akajibu

    “Amekubali bila wasi wasi na tena amefurahi sana yaani bado haamini kama ni kweli”

    “wow ! nipe basi niongee naye mimi mwenyewe”Patrick akasema

    “No huwezi ongea naye kwa sasa.Mtaongea mkionana uso kwa uso.Kinachotakiwa kwa sasa tupange kabisa utaratibu wa safari ni lini na ni wapi mtakwenda kukutana,nina maana ni hoteli gani mtafikia.”

    Huku akichezesha mguu wake kwa furaha Patrick akasema

    “ Kuna hoteli moja mpya kabisa imefunguliwa nje kidogo ya Usa river.Ni sehemu ya kisasa na yenye utulivu wa pekee.Ninadhani inafaa sana kwani hakuna mtu atakayekuja kufuata umbea kule.Kuhusu usafiri gharama zote zitakuwa juu yangu.Wala usihofu.Community airlines wana ndege ya kwenda kaskazini kila siku saa saba na saa kumi na moja jioni.Mimi nitatangulia na ndege ya saa saba mchana na Happy itambidi aje na ndege ya saa kumi na moja jioni.Kwa hali ilivyo hatuwezi kusafiri na ndege moja.Ngoja nimpigie simu rafiki yangu Andrew afanye mpango wa tiketi hizo haraka sana.Usihofu huyu ni zaidi ya rafiki ninamwamini sana.”

    Patrick akaitoa simu yake na kumpigia Andrew.

    “Haloo Andrew”

    “Patrick vipi? Mambo yanakwendaje?

    “mambo shwari tu Andrew”

    “Sasa Andrew ni hivi,natakiwa niende Arusha leo.hapa niko na Margreth .Nimeongea naye na mwisho wa yote natakiwa nikutane na Happy Arusha.Naomba basi ufanye hima uende pale katika ofisi za community airlines na unifanyie mpango wa tiketi mbili .Ya kwangu mimi ni ya ndege ya saa saba mchana huu na nyingine ni ya Happy Kibaho ndege ya saa kumi na moja.Please Andrew its urgent.”

    “Ok Patrick tena imekuwa vizuri kwa sababu hapa nilipo sasa si mbali na ofisi zao ngoja niwahi basi.Nipe kama dakika ishirini hivi nitakupigia simu.

    “Ok Andrew”

    Patrick akakata simu na kupumua kwa nguvu

    “Everything is going to be fine.Hatimaye baada ya muda mrefu ninaenda tena kuonana tena na lulu ya thamani kubwa maishani .” Patrick alikuwa akiongea mwenyewe na kumfanya margreth atabasamu .

    Waliendelea kuongea maongezi ya hapa na pale mara simu ya Patrick inalia.

    “Ni Andtrew huyu”Patrick akasema

    “Haloo Andrew hebu nipe habari”

    “Patrick kila kitu tayari.Kuna rafiki yangu yule bwana Kimaro anafanya kazi pale pale amenisaidia sana kufanikisha zoezi hili kwa haraka.Kwa hiyo unaweza kupita ofisini kwangu kwani ndiko naelekea kwa sasa”

    “Ok Ahsante sana Andrew nitafika hapo muda si mrefu”

    Patrick akakata simu halafu akamwangalia Margreth kwa tabasamu pana sana kisha akasema

    “margreth kila kitu tayari tunaweza kwenda sasa ofisini kwa Andrew”

    “You are so fast Patrick”

    “Kwa miadi kama hii ya kukutana na Happy kila kitu lazima kiende haraka” Patrick akasema huku akitabasamu

    Walitoka hapo Sean snacks na kuelekea moja kwa moja ofisini kwa Andrew.

    Iliwachukua kama dakika arobaini hivi kuwasili zilipo ofisi za Andrew.Haraka haraka wakafululiza hadi ofisini.

    “Wow Comrade “Akasema Andrew mara tu Patrick alipoingia ofisini kwake.Wakakumbatiana kwa furaha.

    “Andrew kutana na Margreth kibaho mdogo wake Happy .Margreth kutana na Andrew,rafiki yangu mkubwa na wa pekee kabisa”

    llikuwa ni mara ya kwanza kwa Andrew kumtia machoni Margreth.Macho yake yalijikuta yameganda yakiustaajabia uzuri wa kimwana huyu.

    “Mhhhhhh !! mtoto mrembo kama malaika.Ama kweli familia hii imebarikiwa kwa kuwa na watoto warembo .Hapana I have to do something.Hii ni nafasi yangu na mimi” Andrew akawaza.

    “Hello Margreth nashukuru sana kukufahamu.Karibu sana”Andrew akasema huku akitoa rabasamu pana sana .

    “ Hata mimi nimefurahi sana kukufahamu Andrew”

    *********************

    “Patrick “ Akasema Andrew

    “Kwa kuwa muda uliopo mpaka saa saba ni mfupi sana na nina imani hautaweza kuonana na mama kama ulivyomuahidi ,unaonaje kama ukimpigia simu na kumweleza kuwa hutaweza kuonana naye leo ili asije akadhani umemdharau.”

    Patrick akatabasamu na kusema

    “Andrew una akili sana”Akasema Patrick huku akiitoa simu yake na kumpigia mama yake

    “Halloo mama”

    ”Enhe!! Unasemaje?Mbona huji we mtoto?Mwenzio yuko hapa toka asubuhi ,tunakusubiri wewe” Mama yake akasema kwa ukali

    Patrick akastuka akafikiri kidogo kisha akasema

    “Ina maana mpaka muda huu Vero yupo hapo nyumbani?

    “Vero yuko hapa akikusubiri wewe.Mbona unamtesa mwenzio namna hii Patrick”

    “mama samahani sintaweza kufika tena hapo nyumbani leo hii kama nilivyokuwa nimekuahidi.Nimepata dharura moja ya muhimu mno.Nafikiri labda kesho kutwa tutaonana”

    “Unasemaje wewe???? Mama yake akahamaki.

    “Mama nimepata udhuru wa ghafla hivyo sintaweza kufika leo mpaka kesho kutwa.”

    “Hivi Patrick una akili zote kweli?Hivi hayo masuala yako unayaona ya muhimu kuzidi ninalokuitia mimi mama yako?

    “Mama”Patrick akadakia

    “Nafahamu unaniitia jambo la msingi kabisa na siku zote siwezi kukudharau wewe mama yangu.Lakini kwa hili naomba unisamehe mama.Ni muhimu mno kwangu”

    Patrick akakata simu na kuizima kabisa.Akashusha pumzi ndefu

    “Oh My God help me.”Akasema Patrick huku akitoa kitambaa na kujifuta jasho usoni.

    Andrew na Margreth wakamuangalia usoni

    “mama anasemaje?” Andrew akauliza.

    “Hakuna muafaka .Bado ananitaka niende nyumbani kwani bado Vero yuko kule wananisubiri.Anyway ni mambo ya kawaida nimeyazoea.Ila andrew nakuomba sana rafiki yangu niko chini ya miguu yako usije ukamweleza mtu yeyote nimekwenda wapi.Najua watakusumbua sana wakiamini kuwa ni lazima utakuwa ukifahamu nimekwenda wapi.Kuonana na Happy ndilo jambo la muhimu mno kwa sasa”

    Kabla hajaendelea mbele simu ya Andrew ikaita.alikuwa ni mama yake Patrick.

    “Ni mama” Andrew akasema kwa wasi wasi

    “Ongea naye mwambie hujaniona kabisa tangu tulivyoonana asubuhi”

    ”Haloo mama “Andrew akasema baada ya kuipokea simu ile

    “Samahani Andrew ,hivi huyu mwenzio yuko wapi?Uko naye hapo?

    “Hapana mama kwani bado hajafika huko nyumbani?

    “hapana baba bado hajafika.”

    “Mimi nilimfuata nyumbani kwake asubuhi na kumweleza vile ulivyonituma nikamwacha hapo akijiandaa sasa nashangaa unaposema hajaonekana mpaka saa hizi”

    “Mimi sielewi andrew huyu mwenzio ana matatizo gani kwa sasa.Tangu apatwe na huu mstuko amebadilika sana.Mwenzake bado yuko hapa akimsubiri yeye bado haonekani.Kanipigia simu muda si mrefu na kunitaarifu kuwa ana dharura .Dharura gani hiyo ya kuushinda wito wangu mimi mama yake? Kibaya zaidi amekata simu na kuizima kabisa.Hivi kweli Patrick amefikia hatu ya kunizimia simu hata mimi?Sasa ukimuona mweleze kwamba sitaki tena aje nyumbani na hao waliompa hizo dharura ndio watakuwa wazazi wake,Ha…..”

    “Hapana Mama”Andrew akadakia

    “Samahani kwa kukukatisha mama ila huko unakofika mama ni mbali sana.Kwa jinsi ninavyoelewa mimi Patrick hawezi kukata simu na kuizima kabisa.Ni kwamba leo nilivyokwenda kwake asubuhi nimemkuta akihangaika kuikausha simu yake iliyomwagikiwa maji.Hivyo basi simu yake inatatizo hilo kwa sasa la kuwaka na kuzima.Hata mimi nimekuwa nikimtafuta kwenye simu bila mafanikio.” Andrew akadanganya huku Patrick akitabasamu.

    “Unamtetea mwenzio siyo? Haya anayoyafanya unaona ni mazuri?

    “Hapana si hivyo mama usinielewe vibaya.Wewe ni mama yetu na kamwe hatuwezi kukudanganya.Naomba mama unipe jukumu la kumtafuta Patrick na kumleta hapo nyumbani haraka iwezekanavyo.”

    “Sawa baba.Jitahidi basi umtafute umlete hapa haraka Kesho wana safari na mwenzake ya kwenda London.Atake asitake ni lazima aende na mwenzake Uingereza””

    “sawa mama” Andrew akajibu na kukata simu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wote wakajikuta wakiangaliana baada ya simu kukatwa.

    “Good.Umemjibu vizuri kiasi ambacho hata sikutegemea.Sasa hatua hiyo imekwisha.Kifuatacho sasa naona tumruhusu margreth yeye aondoke na mimi nikajiandae.Au unasemaje?

    “sawa tu Patrick .Mimi ngoja nimsindikize Margreth mpaka hapo nje nakuja sasa hivi andrew akasema Patrick akatabasamu.

    “Ok kwa heri Patrick nawatakia kila la heri.Ila please sitaki dada yangu aendelee kulia tena.Promise?

    “Happy hatalia tena ,nakuahidi ” Akasema Patrick

    Margreth na Andrew wakashuka ngazi na kumwacha Patrick katika tabasamu pana sana

    “Mhh kwa jinsi ninavyomuelewa Andrew tayari keshapenda pale”

    Baada ya dakika kama kumi hivi andrew akarejea.

    “Vipi niambie Andrew naona mzee eenh” Wote wakacheka.

    “Mhh ! Patrick hii familia ina vifaa bwana.Unajua Margreth nilikuwa namsikia tu.sasa leo ndio nimemwona Live.Wallah mtoto huyu anawapeleka puta watu wengi..Tuachane na hayo.Patrick unajua tuko matatizoni ndugu yangu.Yaani Mama kwa jinsi alivyokuwa akiongea halafu aje agundue kuwa Happy ndiye sababu ya kuifanya safari ya London isifanikiwe sijui kama patatosha.Kwa hivi sasa hata mimi haniamini tena.anajua letu moja.”

    “Andrew nilikutahadharisha kuwa mpango huu wa kuonana na Happy ni mgumu na ambao ni lazima utatufanya tukumbane na vikwazo vingi.Nina imani siku itakuja ndugu zangu wote watanichukia na kunitenga kabisa.Jipe moyo andrew haya ni mambo madogo tu yatakwisha”

    “Ok Patrick kwa sasa tuelekeze macho na akili zetu katika makutano yako na Happy huko Arusha ambako ndiko kutatoa jibu la uelekeo mzima wa suala hili.Ya hapa Dar niachie mimi nitayamaliza.Muda unakwenda sana .Sasa hautatakiwa uende nyumbani kwako.Itabidi tuende kwangu kila kitu kuhusu safari utakipanga pale.Unaweza kwenda kwako ukakutana na Vero na kila kitu kikaharibika.”

    ‘Hapo umenena ndugu yangu.Twende haraka”

    Wakaingia garini moja kwa moja hadi nyumbani kwa Andrew.Baada ya kupakia nguo na vitu kadhaa vya safari wakaingia garini na safari kuelekea airport ikaanza.

    ***************

    Baada tu ya kushuka ndani ya gari iliyomleta toka ofisini kwa Andrew,Margreth akakimbia kuelekea ndani.Wote waliokuwa sebuleni walishangaa jinsi Margreth alivyoingia kwa kasi na bila kuongea au kumsalimu mtu yeyote.Moja kwa moja alikwenda kugonga mlango wa dada yake.

    “Happy fungua I’m back”

    Mlango ukafunguliwa na kitu cha kwanza ikawa ni kukumbatiana kwa nguvu.

    Sebuleni ndugu kadhaa walikuwa wamekaa wakijadili juu ya mwenendo mzima wa hali ya Happy .Ujio wa Margreth uliwafaya wote wastuke .Mama yao ambaye naye alikuwapo sebuleni akainuka na taratibu akaelekea chumbani kwa Happy ili kujua kumetokea nini.Akakinyonga kitasa taratibu lakini kilikuwa kimefungwa kwa ndani.Akajaribu kutega sikio ili asikie ni kitu gani walikuwa wakiongea binti zake wale wawili akashindwa kusikia lolote kutokana na sauti kubwa ya muziki waliyokuwa wameifungua.Akasimama pale mlangoni kwa sekunde kadhaa ,akatikisa kichwa na kurudi tena sebuleni.

    “Watoto hawa bwana mbona nakuwa siwaelewi elewi? Lakini najua ni lazima Margreth akawa anajua kila kitu kinachoendelea kwa dada yake.Ngoja tuwaache tuone “Aliwaza mama yao huku akipiga hatua kuelekea sebuleni.

    “Happy kila kitu tayari kama nilivyokueleza katika simu.”margreth akatoa tiketi ya ndege na kumwonyesha dada yake ambaye aliruka kwa nguvu na kumkumbatia mdogo wake.

    “Margreth thank you so much.ahsante sana mdogo wangu” Happy akasema huku machozi yakimtoka

    Happy akainuka na kuikumbatia picha ya Patrick ambayo walipiga wote toka kipindi wako shuleni.

    “Ooh Patrick nuru ya maisha yangu siamini kama nimefanikiwa kukuona tena” Akasema Happy.Margreth akatabasamu na kusema

    “ Happy kama nilivyokueleza nimekutana na Patrick.Imekuwa ni siku yenye msisimko mkubwa sana hasa kwa Patrick.Sikuongea naye mambo mengi kutokana na muda na vile vile sikutaka kuingia kwa undani sana katika masuala yanayowahusu wewe na yeye.Lengo kuu lilikuwa ni kuwakutanisha nyie wawili na hapo ndipo mtakapokuwa na nafasi ya kutosha kwa kila mmoja wenu kuongea na kuweka wazi hisia zenu.Patrick alilikubali wazo la kuonana na wewe kwa furaha.Nilitaka mkakutanie Morogoro lakini Patrick akakataa na kupendekeza Arusha.Nje kidogo ya mji wa Usa river kuna hoteli mpya kabisa iitwayo Kobe village.Pale ni mahala palipotulia na hakuna bugudha yoyote.Unajua kwa sasa wewe umekwisha kuwa na jina kubwa hapa nchni.Kwa hiyo wanaokufuatilia ni wengi.Yaani haya matatizo tu ya siku mbili tayari kila siku yanazipamba kurasa za magazeti.Itakuwaje iwapo utakutwa faragha na Patrick?Kwa kuliogopa hilo ndio maana tukaona ni bora mkakutanie mbali na hawa wadaku.Kila kitu tayari kimekamilika na hiyo hapo ndiyo tiketi yako ya ndege.safari ni leo saa kumi na moja jioni.Patrick yeye anatangulia na ndege ya saa saba mchana huu.”

    Happy akamkumbatia tena mdogo wake kwa nguvu.



    “Sasa kazi inabaki jinsi ya kumkoroga mama mpaka akubali kuniachia.Hivi atanielewa kweli? Happy akauliza.

    “Fanya hivi , mwambie kwamba unaomba uende mahala ukapumzike ila usimwambie ni wapi.Mwambie unahitaji kuwa sehemu ya peke yako kwa siku kadhaa.Mama anakupenda sana na hataweza kukukatalia”

    “Ok ngoja nikamjaribu” Happy akasema huku akiinuka.

    “Wakati unaenda kuonana naye nenda na uso wa furaha ulojaa tabasamu ili asiwe na mashaka na wasi wasi wowote.” Margreth akasema

    Happy akajiweka safi akatoka chumbani na kuelekea sebuleni akiwa katika tabasamu.

    Mama yake akastuka baada ya kumuona mwanaye ghafla pale sebuleni tena akiwa katika hali ambayo hakuna aliyeitarajia.Happy alionekana mwingi wa furaha na uso mwangavu wenye nuru.

    “Ouh Happy mwanangu”mama yake akashindwa kujizuia na akainuka na kumkumbatia mwanae kwa nguvu.Watu wote pale sebuleni wakasimama na kumwangalia Happy kwa mshangao.

    “Unaendeleaje mwanangu?mama yako sili silali nakuhofia wewe”Mama yake Happy akasema.Huku akitabasamu Happy akasema

    “Naendelea vizuri sana mama.”

    “Nashukuru sana mwanangu kama unaendelea vizuri.Hapa unapotuona tuko familia nzima tukijadili juu ya hali yako na isitoshe tumekuwa katika maombi ya sala ili Mwenyezi Mungu akujalie afya njema na upone haraka.Nashukuru Mungu kwa sasa u mzima.”

    Akamwangalia tena usoni mwanae na kumpiga piga bega huku akisema

    “Mwanangu u mrembo sana”

    “Mremo kama mama yangu” Happy akajibu na wote mle sebuleni wakacheka.

    Furaha ikatawala ndani.Chakula kikaletwa watu wakala na kufurahi.Baada ya kumaliza kula Happy akamuomba mama yake waende bustanini kwa maongezi kidogo.

    “mama ninashida sana na ni wewe tu ambaye unaweza kunisaidia.”Happy akasema wakiwa bustanini yeye na mama yake

    “Kitu gani hicho mwanangu unakitaka?Sema tu kama ninacho nitakupa”

    “mama nadhani unafahamu matatizo yaliyonipata.Ni wazi yameniletea athari kubwa kisaikolojia na ndiyo maana kila siku zinavyokwenda mbele ninazidi kudhoofika.Daktari wangu ameongea na Margreth na kumwambia kwamba nina tatizo la kisaikolojia.Sikuwa nimejiandaa kulitwaa taji kubwa kama hili na hivyo akashauri nipate muda mwingi wa kupumzika bila kubugudhiwa na kitu chochote.Nimekubaliana na ushauri wake ambao nina imani kwamba utanisaidia sana.Mama nahitaji kusafiri,kuwa nje na nyumbani,nje na Dar es salaam kwa siku mbili au tatu.Nahitaji kuwa peke yangu kwa siku hizo kadhaa ili niweze kuyasahau yote yaliyotokea na niweze kujiandaa vyema jinsi ya kuweza kuishi maisha mapya nikiwa kama mrembo wa Tanzania.Mama najua siwezi kuongea na baba juu ya suala hili kwani baba hatanielewa.Please mama naomba unisaidie sana kwa hilo.Nahitaji kuwa sawa kiakili mama.taji nililonalo ni kubwa sana kwa hiyo nahitaji mandalizi ya kutosha”

    Maneno haya yanamfanya mama yake Happy akae kimya kwa sekunde kadhaa kisha akamwangalia mwanae usoni na kusema

    “Happy mwanangu,mimi mama yako kwanza nafurahi sana na kumshukuru Mungu kwa kukujalia afya njema.Huwezi kujua ni jinsi gani mimi mama yako nilivyokuwa naumia kila nikikuona ukiwa na hali ile ya majonzi mengi.Namshukuru sana Mungu kwa muujiza huu mkubwa alioitendea familia yetu.Siku zote yeye ndiye amekuwa ngao na kinga yetu.Happy nakubaliana na mawazo yako ya kwamba unataka kwenda mbali na hapa ukapumzike.Kwa jinsi ninavyokupenda mwanangu siwezi kukukatalia kwani ninataka siku zote uwe ni mwenye furaha na afya tele.Lakini kuna kitu kimoja kinanipa wasi wasi,mwanangu hauna tatizo lolote linalokusumbua akili ?naomba kama una tatizo nieleze mimi mama yako nitakusaidia.Usiponieleza mimi mama yako nani mwingine utakayemweleza akakusaidia?

    Happy akacheka kidogo kisha akasema

    “Mama nadhani unanielewa vizuri siku zote niwapo na tatizo mtu wa kwanza kumkimbilia ni wewe.Zaidi ya kupata ule mstuko na kupoteza fahamu sina tena tatizo lingine.Naomba uniamini mama ni tatizo hili la kisaikolojia ndilo inanibidi nipambane nalo kwa sasa.Ninaamini nitakaporejea nitakuwa mzima wa afya tele.”

    “Vizuri kama hayo uyasemayo ni ya kweli.Lakini Happy umenipa mtihani mgumu sana kwa baba yako.Unamfahamu baba yako alivyo mkali.Iwapo nitakupa ruhusa bila ya yeye kujua nitakuwa na wakati mgumu sana kumpa majibu yenye kueleweka.Sasa sijui nifanye nini mwanangu?

    “mama usiwe na wasi wasi wowote.naomba unipe ruhusa halafu mimi mwenyewe nitaongea naye na kumuelewesha.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mama yake happy akainama akafikiri kidogo kisha akasema

    “Unataka kwenda wapi?

    “Nje ya Dar es salaam.Sijajua bado kama niende Morogoro,Tanga .Moshi au kokote kule ili mradi iwe nje ya Dar es salaam.”

    “ Unakwenda na Mike?

    Happy anastuka kidogo kwa swali lile.

    “Mike? Happy akauliza

    “Ndiyo Mike” mama yake akajibu

    “Kwa nini umeuliza mama?Mi nitakuwa mwenyewe tu.Sintakuwa na mtu yeyote”Happy akajibu.Mama yake akamuangalia usoni halafu akasema

    “Jana Mike alipiga simu na kuniambia kuwa leo saa mbili usiku atawasili lakini alisema nisikwambie kwa sababu anataka akushangaze,ndio maana nikahisi pengine mlipanga muende wote hiyo safari”

    “Hapana mama mimi nitakuwa peke yangu.Yeye kama akija atanisubiri hapa hadi nitakaporudi.”

    “Kwa hiyo una maana unaondoka leo hii kabla mwenizo hajafika?

    “ndiyo mama.Nimekwishafanya booking ya ndege ya leo jioni inayokwenda Mwanza kupitia Morogoro na Kilimanjaro.Nitashukia Morogoro halafu toka pale nitaangalia kama nitabaki Morogoro au nitakwenda sehemu nyingine.Nianweza kwenda Iringa au Mbeya au sehemu yoyote ile.”Happy akasema huku mama yake akimkazia macho

    “Happy kwa nini umepanga safari ya ghafla namna hii? Hutaki kuonana na Mike? Unamkwepa mwenzio? Hebu niambie bila kunificha kitu kwa sababu mwenzio anakuja usiku wa leo na ameacha shughuli zake huko Marekani kwa dhumuni moja tu la kuwa na wewe .Endapo hatakukuta hapa nyumbani ni wazi atahitaji maelezo ya kina na hakuna mwingine atakayempa maelezo juu yako zaidi yangu.Naomba usinifiche kitu mwanangu.Mike anakupenda na sisi tunampenda “ Happy akakaa kimya kidogo halafu akasema

    “Mama naomba unielewe.Sifanyi hivi kwa ajili ya kumkimbia Mike.Ninampenda Mike kupita maelezo lakini ninafanya hivi kwa ajili yangu.I need to be ok mother.After all that happened I need sometime alone.Please understand me mother” Happy akasema kwa msisitizo

    Mama yake hakuona sababu ya kumkatalia binti yake.

    “Happy mwanangu mimi siwezi kukukatalia kwenda huko unakotaka kwenda.Wewe ni mtu mzima kwa sasa na nina imani kuwa kila unachokiamua hakina madhara kwako.Ila mwanangu nataka tu unihakikishie kuwa huko uendako utakuwa salama.”

    “mama nitakuwa salama na wala usihofu kitu chochote.Simu yangu itakuwa wazi muda wote”

    “Sawa mwanangu hakuna shida baba yako nitamalizana naye mimi.Kwa hiyo saa ngapi unaondoka?

    “Saa kumi na moja jioni.Sitaki kusafiri mapema sana kwa sababu watu hasa waandishi wa habari wananifuatilia na wanaweza wakaniharibia safari yangu.margreth atatumia gari lako kunipeleka uwanja wa ndege.Halafu mama naomba usimwambie mtu yeyote zaidi ya baba na Mike ni wapi nimekwenda.Kwa sasa mimi ni mtu maarufu hivyo habari zangu zinauzika sana katika vyombo vya habari.Sitaki watu waniharibie mapumziko yangu.”

    “sawa Happy .Twende ukajiandae.Nitakupeleka uwanjani mimi mwenyewe “ mama yake akasema huku akitabasamu .

    *************

    Ni kengele ya simu ya chumbani ndiyo iliyomstua Patrick toka katika jinamizi la mawazo.Tangu amefika katika hoteli hii ya Kobe Village amekuwa ni mwingi wa mawazo .Kutokana na wasi wasi mwingi aliokuwa nao aliamua kujiliwaza kwa kunywa mvinyo laini.

    Aliweka chini glasi yake ya mvinyo na kuiendea simu ile ya chumbani.

    “Haloo” Aliita kwa kitetemeshi

    “Haloo mapokezi hapa.Samahani kaka mgeni wako uliyesema atawasili tayari amefika.Je utakuja kumchukua au tumlete moja kwa moja chumbani?

    Patrick akapumua kwa nguvu ,mapigo ya moyo yakabadilika.

    “Mleteni chumbani “Patrick akasema,akaurudisha mkono wa simu kisha akapumua kwa nguvu,kijasho chembamba kilimtoka .Wakati akitafakari na kuuona huu ni kama muujiza kukutana tena na Happy mara kengele ya mlangoni inalia.Taratibu akajivuta na kwenda kuufungua.

    Kwa takribani dakika moja nzima wote wawili walipigwa na butwaa kila mmoja akimshangaa mwenzake.Halafu wakakumbatiana kwa nguvu huku wote wawili machozi yakiwatoka..Muhudumu aliyekuwa ameongozana na Happy akapigwa na mshangao kwa hali ile aliyoina.Hisia za penzi la kweli zilijidhihirisha wazi wazi baina ya wawili hawa..Tukio hili linaamsha kumbukumbu kubwa na ya pekee maishani mwao.Hakuna aliyetaka kumwachia mwenzake.

    Patrick akamshika Happy taratibu na kumkalisha katika sofa lililokuwamo humo chumbani.Uso wake wote ulikuwa umejaa machozi.

    “I cant believe this”Patrick akanong’ona.Happy hakujibu kitu midomo yake ilikuwa ikimtetemeka.Kila alilotaka kuongea lilikwama.

    “Is that you Patrick? Happy akajitahidi kusema huku akifuta machozi

    “Its me Happy.Its real me” Patrick akajibu

    “Its like I’m dreaming…Ni kama ninaota.bado siamini kama nimekuona tena” happy akalalama.

    “Ouh Patrick I real love you my angel” Aliwaza Happy huku ameikunja mikono yake kifuani kwake.Patrick alikuwa amesimama akimkodolea macho Happy asiamini alichokuwa akikiona mbele yake..

    Baada ya kama dakika kumi hivi za ukimya ,tafakari na hisia nzito kwa kila mmoja ,hatimaye Patrick akaufungua mdomo na kusema

    “Welcome back my sunshine”

    “Welcome back to my heart Patrick” Happy akanong’ona kwa sauti laini sana.

    “Huu ni muujiza mkubwa sikutegemea katika maisha yangu kama nitakuja kukuona tena.,lakini Mungu ni mkubwa na ameweza kutukutanisha tena.” Akasema patrick na kauli ile inaamsha kilio kwa Happy

    “Happy nyamaza usilie.Umelia vya kutosha uliponipoteza ,I’m here now.”

    “Patrick ninaumia sana kwa kila nikikumbuka mateso niliyoyapata kwa kukupoteza.Awali ya yote naomba unisamehe kwa yote yaliyotokea kipindi cha nyuma.Najua bado una kinyongo moyoni na hata mimi nilikuwa na fundo kubwa moyoni kwa kitendo ulichonifanyia lakini tayari nimekusamehe.Naomba na wewe utafute ndani ya moyo wako jinsi ya kunisamehe.Patrick najua ulifungwa kwa ajili yangu.Mapenzi yako makubwa kwangu ndiyo yaliyosababisha ukafungwa.Uliua kwa kuniokoa mimi nisidhalilishwe.”

    Happy akaangusha kilio tena.Patrick katoa kitambaa na kumfuta machozi .

    “Patrick halikuwa kusudio langu mimi kwenda kusoma Ulaya na kukuacha peke yako.Nilikuwa nimekataa kwenda lakini ukanishauri niende kusoma kwa ajili ya kutengeneza maisha bora kwangu na kwako.Ni…….”

    Kabla hajaendelea simu yake inalia.Akafuta machozi haraka haraka na kuitoa katika mkoba wake.mdogo.Aliangalia namba za mpigaji na kukuta ni Mike mchumba wake.Kwa hasira akakata simu na kuizima kabisa.

    Patrick akakiangalia kitendo kile lakini hakukitilia maanani .

    “Patrick”Happy aliita huku akimwangalia machoni.

    “Yes” Patrick akaitika

    “Ninajua itakuwia ngumu sana kwa wewe kama binadamu kunisamehe kwa kile kilichotokea,japokuwa tayari mimi nimekwisha kusamehe….”

    “Please Happy “Patrick akadakia.

    “Naomba usiseme maneno hayo tena.Yanaumiza sana.Ni kweli nilikuwa na hasira sana lakini huu si muda wake kuyaongelea hayo.”

    Happy akamvuta Patrick karibu akamkumbatia na kumpiga mabusu mfululizo.Patrick akahisi kitu kama chaji za umeme zimepita mwilini mwake.

    ******************

    Saa moja na nusu jioni Andrew akiwa nyumbani kwake na mpenzi wake Vick mara simu yake inalia.Akaichukua na kuangalia mpigaji ,alikuwa ni mama yake Patrick.Moyo ukaanza kuenda mbio.

    “Du! Kazi imeanza”Alisema kwa sauti ndogo ambayo Vick aliisikia.

    “Haloo mama”

    “andrew mwanangu hivi huyu mwenzako ana kitu gani jamani kinachomsumbua?Unajua mpaka sasa hivi siamuona hapa nyumbani na wala hajanipigia simu na simu yake ameizima kabisa.Nimekwenda nyumbani kwake hayupo,Veronika amekaa hapa mpaka ameamua kuondoka mtoto wa watu .Sielewi ni kwa nini anaanza kutuweka roho juu juu dakika hizi za mwisho.Maandalizi ya harusi yake yanaelekea ukingoni lakini yeye haonyeshi kujali.sasa hebu niambie baba ulifanikiwa kumuona?”

    “Mama kwa kweli nimehangaika sana na hata ofisini sijakaa kwa ajili ya kumtafuta Patrick na katu siwezi kukuficha mama Patrick sijui alipo kwa sasa.Hata mimi alinieleza kuwa ana dharura leo lakini hakunifafanulia ni dharura gani hiyo.Hata mimi nimemtafuta sana katika simu hapatikani nadhani lile tatizo la simu yake bado linaendelea” Andrew akasema

    “andrew na wewe usitake kuniudhi kama huyu mwenzio,usinieleze kabisa upuuzi huo wa simu.Patrick si mtu wa kushindwa kununua simu nyingine,angenieleza hata mimi ningemnunulia mpya.Hivi kwa nini mnataka kuzichezea akili zetu nyie watoto?

    “Mama naomba unipe muda zaidi mpaka kesho asubuhi nitakuwa nimepata jibu wapi alipo Patrick na nitakujulisha ikiwezekana nimlete nyumbani mimi mwenyewe”

    “Sawa baba jitahidi umpate kwa sababu anatuweka roho juu juu kweli huyu mwenzio.”

    “Ok mama nitajitahidi”

    “Haya Andrew usiku mwema”

    “Ahsante mama”

    Uuuuuuphhh!!!!!! Andrew alipumua kwa nguvu baada ya kumaliza kuongea na mama yake Patrick

    “:Kuna nini andrew? Vick akauliza

    “Patrick haonekani”

    “etiii!!!!!!! ???” Vick akauliza kwa mshangao,akainuka akashika kichwa kwa mikono yake yote miwili.

    “Mungu wangu ! yuko wapi sasa jamani”

    “hata mimi sielewi Vick .Mama ndio kanipigia simu sasa hivi anaulizia kama nimemuona”

    “Ina maana hujaonana naye leo?” Vick akauliza huku amemkazia macho Andrew

    “Nilionana naye asubuhi ya leo na toka hapo sijaonana naye tena na simu yake haipatikani.”

    “Hakukueleza kuwa anakwenda wapi?

    “alinidokeza kuwa ana dharura ila hakunifafanuia zaidi”

    Vick akafikiri kidogo kisha akasema

    “andrew ,wewe ndiye rafiki mkubwa wa Patrick.Hakuna kitu ambacho huwa mnafichana.Hainiingii akilini eti Patrick awe na dharura halafu ashindwe kukueleza ni dharura gani hiyo?

    “Please Vick nimesema sijui Patrick alipo!Mimi kaniambia hivyo kuwa ana dharura sasa siwezi kuingilia masuala yake binafsi.Umenielewa?

    Vick akamwangalia Andrew kwa sekunde kadhaa kisha akaketi sofani.

    Baada ya kutafakari kwa muda Andrew akaamua kumpigia simu Veronika

    “Haloo shemeji” Andrew akasema baada ya Vick kupokea simu

    “andrew I’m confused.Ni kwa nini lakini Patrick ananifanyia hivi?Nimemkosea kitu gani hadi ananitenda hivi? Vick akatamka kwa hasira

    “Vero,shemeji yangu hebu tuliza hasira kidogo.” Andrew akamsihi

    “andrew I’ll go crazy if I cant see Patrick tonight.maandalizi ya safari yamekwisha kamilika.Ni yeye tu ndiye anayesubiriwa.What am I going to do?? !!! Please Andrew help me to know where Patrick is.Hapatikani hata katika simu…”Vero akashindwa kujizuia akaangua kilio

    “Vero please naomba unisikilize.Mama naye kanipigia simu sasa hivi akimuulizia Patrick.Mimi nilionana naye asubuhi ya leo.mama alinipigia simu na kuniagiza niende kwake nikamueleze kuwa anahitajika nyumbani.Nilimkuta akijiandaa kutoka na akanieleza kuwa amepata dharura asubuhi hiyo hivyo angekuja nyumbani mchana.Toka hapo sijaonana naye tena.”

    “Oooh My God! Sasa nitafanya nini mimi? Vero akasema

    “Usijali Vero bado naendelea kumtafuta na mpaka kesho nitapata jibu yuko wapi”

    “Jitahidi Andrew “

    “Yes Vero najitahidi sana kuwasiliana na rafiki zetu mbali mbali ili nijue yuko wapi.Kama hatatokea hadi kesho kwa nini basi nisikusindikize badala yake?

    “Unasemaje????!!! Vero akauliza

    “Nasema hivi kama Patrick hajatokea mpaka kesho unaonaje kama nikakusindikiza katika safari hiyo mliyopanga kwenda wote?CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nilikuwa nakuamini sana Andrew lakini kumbe nyie wote ni kitu kimoja tu”Vero akajibu kwa hasira na kukata na kukata simu.

    Andrew alichanganyikiwa kwa kitendo cha Vero kukata simu.Ni wazi alikuwa amekasirika.Alijilaumu sana kwa kujiingiza katika matatizo makubwa kama haya.Kwa takribani dakika mbili nzima alibaki ameduwaa ameishikilia simu yake.

    “andrew kuna nini?

    Sauti ile ya Vick inamstua toka katika jinamizi la mawazo lililomkumba ghafla.

    “Hakuna kitu Vick,nilikuwa nikongea na Vero”

    “Kuhusu nini?

    “Kuhusu safari yao ya kwenda London kufanya shopping ya harusi yao”

    “Yeye anasemaje ?

    “Hana la kufanya kwani Patrick haonekani.Mimi nilijitolea kumsindikiza”

    “Yeye amejibuje?

    “Amekasirika na kukata simu halafu ameizima kabisa”

    “Huna haya Andrew,eti umsindikize mchumba wa mtu London.Hivi unatumia akili kweli Andrew?We ndie mchumba wake?Hata ningekuwa mimi nisingekujibu.Tena amekuheshimu sana hakukutukana.Hebu achana na mambo ya watu tuangalie ya kwetu.”

    Andrew hakujibu kitu.Akainamisha kichwa chini kwa sekunde kadhaa.

    “Vick I’m confused”

    “Na nini?

    “na hali nzima ya mambo jinsi yanavyokwenda”

    Vick akamsogelea Andrew akamkumbatia na kukilaza kichwa chake katika kifua kipana cha andrew .

    “Usijali Mpenzi Patrick atarejea tu muda si mrefu.”Vick akasema huku akiipitisha mikono yake laini mwilini mwa andrew kiuchokozi.Andrew alielewa alichokuwa akihitaji mpenzi wake.





    Saa kumi na moja za jioni dege la shirika la ndege la British airways lilitua katika uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere Dare s salaam.Lango la ndege lilifumguliwa na abiria wakaanza kushuka.Miongoni mwa abiria waliokuwamo katika dege hili ni Mike cambell,kijana mtanashati mwenye kila sifa ya uzuri,ambaye kila binti amuonaye angetamani awe naye.Leo hii alivaa suruali ya jeans iliyofifia na shati zuri la mikono mifupi.Kwa ujumla alikuwa amependeza vilivyo.Mike Cambell mchumba wa Happy alikuwa akitokea Marekani .Lengo kuu la safari yake hii ya tanzania lilikuwa ni kuja kumfariji mpenzi wake Happy katika maradhi yanayomsumbua pamoja na kumpongeza kwa kufanikiwa kulitwaa taji la Miss Tanzania.

    Baada ya kukamilisha taratibu za uwanjani kama uhamiaji n.k Mike akatoka na kulakiwa na dereva wake aliyetoka katika ubalozi wa Marekani.Alitegemea pengine angeweza kumuona Margreth mdogo wake Happy pale uwanjani kwa kuwa alikwisha mtaarifu juu ya ujio wake lakini mpaka anamuamuru dereva aondoe gari hakumuona mtu yeyote.

    Toka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere ,safari ilikuwa ya moja kwa moja mpaka nyumbani kwa akina Happy .Anapafahamu vizuri mahala pale kwani si mara yake ya kwanza kwenda Moyoni alikuwa akiomba Mungu amsaidie aweze kukuta hali ya Happy inaendelea vizuri.Walifika nyumbani kwa akina Happy geti likafunguliwa wakaingia ndani.baada ya kushuka ndani ya gari akakutana na mama yake Happy .

    “wow ! Mike karibu sana”

    Alimkumbatia na kumkaribisha ndani.

    Mike akaomba maji ya kunywa ya baridi sana ili aweze kulipooza joto kubwa alilokuwa analisikia.

    Baada ya kunywa glasi mbili za maji akauliza aliko Happy na Margreth.Mama yake Happy akapatwa na kigugumizi cha ghafla.

    “Margreth amekwenda katika mizunguko yake lakini Happy yeye amesafiri kidogo”

    “amesafiri?? Mike akauliza kwa mshangao

    “Ndio kasafiri” mama Happy akajibu huku akijitahidi kuuficha wasi wasi aliokuwa nao

    “Kasafiri toka lini” Mike akauliza

    “kasafiri leo mchana”

    Mike akashika kichwa akapumua kwa nguvu.

    ‘Mbona umestuka Mike Ina maana hamkuwasiliana akakwambia kuwa atasafiri” mama Happy akamuuliza Mike ambaye alionyesha kuchanganyikiwa baada ya kusikia Happy amesafiri.

    “Hapana mama sikuwasiliana naye. Kama niivyokuwa nimekueleza katika simu sikutaka afahamu kuhusu ujio wangu.Nilitaka nimfanyie mshangao.Lakini Margreth pia nilimtaarifu juu ya safari yangu.Happy alisema anakwenda wapi?” Mike akauliza

    “Hakuniambia ni wapi anakwenda .Baada ya kujisikia nafuu aliniambia kwamba amepata safari ya dharura ya kwenda nje ya Dar es salaam.Hakuniambia safarii hiyo inahusu kitu gani.Ujumbe aliouacha ni kwamba kama ukija umsubiri hadi atakaporejea nadhani mdogo wake atakuwa alimdokezea kwamba unakuja”

    Mike hakujibu kitu akatoa simu yake na na haraka haraka akazitafuta namba za Happy akapiga.Simu ilikuwa inaita ,akatabasamu.

    “Yuko hewani lakini anachelewa kupokea” alisema mike

    Simu iliita bila kupokelewa.Akapiga tena mara ya pili na ya tatu na ikakatika.Akapiga tena na mara hii ikawa haipatikani .Mike akapiga tena na tena lakini jibu likawa lile lile simu haipatikani tena.

    “amezima simu”

    Mike akaishiwa nguvu akakaa sofani.Baada ya dakika kadhaa za ukimya Mike akaomba aondoke akapumzike kwa sababu tayari kichwa chake kilikuwa kimevurugika.

    Dakika kama kumi hivi toka Mike aondoke pale nyumbani Margreth akawasili.Alimkuta mama yake akiwa amekaa sebuleni akiwa mwingi wa mawazo.

    “mama unaumwa? Margreth akauliza

    Mama yake hakujibu kitu,alimwangalia usoni kwa makini na kumuomba aketi.

    “Margreth hebu nieleze Happy kaenda wapi?Najua ni lazima unafahamu alikoenda dada yako”

    “mama mimi sijui kitu chochote.Kwani wewe alikuaga anakwenda wapi?

    “Hakutaka kuniambia anakwenda kupumzika wapi.Lakini wewe ni lazima utakuwa unajua kwa sababu toka ametoka hospitali ni wewe tu ambaye unaongea naye.”

    “Hapana mama sijui kitu chochote kile,alivyokwambia wewe na ndivyo alivyoniambia mimi”

    “Na vipi kuhuisu shemeji yako Mike?Ina maana hukujua kama anawasili leo ili uende kumpokea?

    “Du! Yaani mama nimeshasahau kabisa kama Mike anakuja leo.Vipi ameshafika?

    “Saa nyingi sana.Ila nyie watoto!!!Yaani mwenzenu anakuja hamtaki hata kwenda kumpokea.Halafu kitu kingine cha ajabu,amempigia simu Happy mbele yangu na Happy kakataa kupokea na mwishowe akazima simu kabisa.Hivi kuna kitu gani kinaendelea?

    “Mhhhh” Margreth akaguna.Akamwacha mama yake hapo sebuleni na kuingia chumbani kwake.akajifungia na kujaribu kumpigia Happy lakini simu yake ilikuwa tayari imezimwa.akajitupa kitandani.

    ****************

    Ni saa tatu za usiku katika hoteli ya Kobe Village chumba namba 68 kilikuwa na mwanga hafifu wa bluu.Sauti ya muziki laini ilisikika kwa mbali.Chumba chote kilikuwa kikinukia uturi mzuri wenye harufu ya ajabu.Chumba hiki kwa sasa kilikuwa katika mkao wa mahaba mazito.

    Juu ya kitanda kikubwa watu wawili walikuwa wamekumbatiana wakiwa katika mahaba mazito.

    “Patrick” Happy akaita kwa sauti laini,nyororo ya kimahaba huku akimchezea chezea nywele za kifuani.

    “Yes darling “ Patrick akaitikia

    Happy ambaye tayari macho yake mazuri meupe yalikuwa yamelegea kama amekula kungu akasema

    “Patrick najilaumu sana kwa kuamua kuondoka na kukuacha peke yako.Narudia tena kuomba msamaha kwa kitendo hiki cha kukuacha peke yako na wala sintachoka kufanya hivyo tena na tena kwa sababu ni kitendo ambacho kilisababisha mimi na wewe tukatengana.Kama nisingeondoka tungekuwa na maisha yetu ya raha mstarehe.Leo hii nahisi amani na raha ya ajabu.Raha ambayo nimeikosa kwa miaka mingi.Leo hii najisikia raha ya aina yake kama niliyokuwa nikiipata kipindi tukiwa shuleni.Msisimko niliokuwa nao kipindi kile pindi nikiwa karibu nawe bado haujapotea.Nikiwa nawe sihisi tatizo lolote.Nahisi raha kila mahali”

    Patrick akatabasamu akausogeza mkono wake usoni na kurudisha nyuma nywele ndefu za binti huyu mrembo ambazo tayari zilikuwa zimevurugika kutokana na kuzichezea.

    “Happy hata mimi ninajisikia hivyo hivyo.Sikutaka kuamini moja kwa moja kuwa hauko tena maishani kwangu.Nilimuomba Mungu anisaidie ili kabla siku zangu hazijaisha hapa duniani niwe nimekuona walau kwa mara ya mwisho.Mungu amesikia sala yangu na tayari amenijibu.Leo hii niko nawe tena.”

    Patrick akamvuta Happy karibu zaidi na kumpiga busu zito mdomoni.

    ‘Patrick naomba nikuulize kitu na tafadhali naomba uwe wazi kwangu.usinifiche kitu hata kidogo”

    “C’mon baby uliza chochote usihofu ,kwako hata siri za baba yangu nitakupa”

    Wote wawili wakacheka.

    “Umeshaanza utani wako nawe”

    “Usijali mama uliza”

    Happy akatulia kidogo kana kwamba anakumbuka kitu kisha akauliza.

    “Hivi Patrick ni kwa nini uliamua kunidangaya kuwa umekufa?

    Patrick akastuka,akainuka na kukaa kitandani jasho likaanza kumchuruzika.

    “What !!! ….me?…Dead?…..why ? Patrick alijikuta akitamka maneno mfululizo huku akimtazama Happy..

    “Happy nashindwa kuelewa ,eti nilifanya nini??!!……..

    Happy aliuona mstuko mkubwa wa wazi katika sura ya Patrick akaanza kuogopa kwani alisikia Patrick ana matatizo ya moyo.akamsogelea akamkumbatia na kumbusu akamsugua sugua shingo na kuhakikisha ile hamaki aliyokuwa nayo Patrick imekwisha halafu akaendelea

    “Kama unakumbuka kipindi nimeondoka kwenda kusoma tulikuwa tunawasiliana vizuri sana.Hii ilinipa faraja na kuupunguza umbali uliokuwapo kati yetu.Lakini ilitokea siku moja ambayo kwa kweli ni vigumu sana kuisahau katika maisha yangu.Ni siku hii ndiyo iliyobadili kabisa maisha yangu,siku niliyopokea barua toka kwa dada ambaye alijifahamiha kuwa alikuwa ni jirani yenu mlikokuwa mkiishi Sumbawanga.Katika barua hiyo alisema kuwa anasikitika kunitaarifu kuwa eti umefariki dunia ukiwa gerezani kwa maradhi ya kuhara”

    Patrick akasimama na kushika kiuno.

    “Happy please tell me it’s a joke”

    Happy akamtazama kisha akasema.

    “Its not a joke Patrick.Baada ya kupata taarifa ile nilipatwa na mstuko,sikutaka kusoma tena,na wala sikuona tena faida ya kushi.You were my everything.Kwa bahati nzuri baba na mama walisafiri haraka sana na kuja kunifariji na kunifanya niendelee kuishi kwani vinginevyo ningekwisha jiua muda mrefu.Patrick ,ilipita miaka mingi bila ya kuwa na furaha na amani moyoni mwangu.Furaha yangu ulikuwa ni wewe pekee.Nilikuwa nikiomba usiku na mchana kwamba taarifa ile isiwe ya kweli na kwamba siku moja ungejitokeza lakini siku zikaenda na hukutokea.Taratibu baada ya miaka kadhaa kupita nikakubaliana na matokeo kuwa tayari umekwisha fariki.Hatimaye baada ya kumaliza masomo nikarudi nyumbani na kitu chja kwanza kukifanya ilikuwa ni kutafuta mahala ulipozikwa.Nilienda mpaka Sumbawanga nikauliza nikaambiwa kuwa familia yako ilikwisha hama muda mrefu sana.Nikaenda tena kule Iringa ulikokuwa umefungwa nikaambiwa kuwa ulihamishwa gereza na kupelekwa Songea.Nikachapa mguu hadi Songea katika gereza ulilohamishiwa pale ndipo niipoufahamu ukweli.Niliwekwa wazi kuwa ulimaliza kifungo chako na ukaachiwa huru.Pale ndipo nilifahamau kwamba hukufa gerezani na kwamba kuna uwezekano mkubwa ukawa mzima.Pamoja na kuufahamu ukweli huo nilikonda kwa kujiuliza swali moja nililokosa mtu wa kunipa jibu,kwa nini unifanyie vile?.Sikujua sababu yaw ewe kuamua kunifanyia vile yaani kusingizia umekufa na kunifanya mimi niishi maisha ya kuteseka miaka yote hii.Nimekuwa nikimuomba Mungu anikutanishe nawe ili walau nifahamu sababu iliyopelekea unifanyie vile.Patrick you were the only man I real loved and trust.I gave myself to you .Please tell me why you did that ,I’ll understand.” Happy aliongea katika hali ya uchungu sana huku ameiweka mikonoyake kifuani kuonyesha machungu aliyokuwa akiyapata

    Patrick jasho lilikuwa likimtiririka kama mtu aliyemaliza mbio ndefu.Ingawa chumbani mle mlikuwa na kiyoyozi lakini hakikusaidia kulipunguza joto alilokuwa akilisikia baada ya kuipata taarifa ile.Alisimama na kuzunguka zunguka humo chumbani.

    “Happy ! sijui hata nianzie wapi.I’m confused”

    Happy akamsogelea akachukua kitambaa na kumfuta jasho lililokuwa likitiririka kwa fujo.

    “Please tell me Patrick.Tell me everything.I’ll understand” Happy akasema kwa sautiya upole sana

    “Happy sina hakika kama utaniamini na kunielewa.Ukweli ni kwamba haya yote uliyoyasema wewe kwangu mimi ni mageni kabisa.Hakuna ninachoweza kukisema au kukitolea maelezo..Niliyatoa maisha yangu kwa ajili yako ,iweje leo nijifanye nimekufa?bado hainiingii akilini . Happy kumbuka nilikuwa radhi hata kuua japo sikukusudia kwa ajili ya upendo niliokuwa nao kwako iweje leo niamue kutunga kitu ambacho kimetutenganisha?Nashindwa kupata jibu.Katika maisha yangu hakuna kitu ambacho sikupenda kukiona kama kuona ukiumia na hilo unalifahamu fika.Sasa kwa nini basi niamue kuumiza moyo ako kwa kujifanya nimekufa?

    Akatulia akafuta jasho.Happy akalifungua sanduku lake dogo akatoa bahasha ambayo ilikwisha anza kuchakaa pengine ni kutokana na kushikwa mara nyingi sana.akatoa karatasi iliyokuwamo ndani ya ile bahasha na kumkabidhi Patrick.

    “Barua yenyewe hii hapa hebu isome”

    Patrick akatumia dakika kadhaa kuisoma barua ile.Alipomaliza kuisoma akarudia tena na tena.Uso wake wote ukajaa machozi.Midomo ikawa ikimtetemeka kwa hasira,akashindwa kitu cha kuongea.

    “Umeona Patrick? Hivyo ndivyo ilivyokuwa” akasema Happy

    Kikapita kimya cha dakika kadhaa hapo ndani,kila mmoja akiwaza lake.Patrick akakumbuka toka siku ya kwanza alipokutana na Happy katika kituo cha basi Mbalamaziwa Iringa na hapo ndipo ulipoanzia urafiki wao.Picha za uhusiano wao wakiwa shuleni zikamjia mpaka siku ile alipomuokoa Happy toka katika mikono ya wabakaji .Akakumbuka pia siku alipohukumiwa kifungo cha miaka mitano gerezani na mpaka siku Happy aliyokuja kumuaga kuwa anakwenda Ulaya kusoma.Ghafla akakumbuka siku alipopata taarifa toka kwa Veronika kuwa Happy ameolewa na hatarudi tena Tanzania.Alikumbuka jinsi alivyozimia kutokana na taarifa ile.Machozi yakamtoka.

    Patrick akakohoa kidogo kisha kwa sauti yenye kitetemeshi akasema

    “Happy nimekusikia na nimekuelewa naomba sasa na mimi nikupe hadithi yangu.Naomba unisikilize kwa makini na unielewe”

    “Baada ya wewe kwenda kusoma Ulaya,huku nyuma nilihamishwa gereza na kupelekwa Songea katika gereza jipya kabisa.Siku moja nilikuwa nimepangiwa kutengeneza mazingira katika nyumba ya mkuu wa gereza.Siku hiyo mkuu wa gereza hakuwepo.Nikiwa naendelea na kazi alitokea dada mmoja ambaye alionyesha kuwa na roho ya huruma sana.Alinikaribisha chai nzuri mchana huo aaknikaribisha chakula.Ni dada mcheshi,mchangamfu,na mwenye huruma.Kwa mujibu wa maelezo yake ni kuwa pale alikuwa amekuja kumsalimu mjomba wake ambaye ndiye yule mkuu wa gereza.Baadae alijitambulisha kwangu kuwa anaitwa Veronika.Taratibu mimi na Veronika tukawa marafiki.Nilimhadithia mkasa mzima wa maisha yangu kwa sababu nilitokea kumwamini.Ukiacha wazazi wangu Veronika ndiye mtu pekee aliyekuwa akinipa moyo,kunifariji na kunipa ushirikiano wa kutosha.Muda wake ulipoisha alirudi Dar es salaam kuendelea na shughuli zake aliahidi kuwa angekuwa anakuja mara kwa mara kunitazama.Kwa hiyo nikamuomba yeye awe ni kiungo baina yetu yaani mimi na wewe.Kwa kuwa yeye aliahidi kuja mara kwa mara kuniona nikaona ni bora mawasiliano yetu yaliyokuwa yameanza kufififa yawe yakipitia kwa Veronika.Nikaandika barua na kumkabidhi ili aende akaiposti afikapo Dar es salaam.Siku moja ambayo sintakuja kuisahau alikuja Vero na kuniambia kuwa alikuwa na taarifa ambazo si njema sana.Nilijikaza kiume na kumuomba anieleze.Vero aliniambia kuwa Barua aliyokutumia imerudishwa kwa kuwa haupo tena katika chuo kile ulichokuw ukisoma.Akaendelea kusema kuwa alielekezwa mahala ulipoamia na akakupigia simu lakini ukamjibu kwa kejeli kuwa huanmuda na mimi tena, na wala huna mategemeo ya kurudi tena Tanzania.Alizidi kudai kuwa alimtumia binamu yake aishiye huko huko marekani kufanya uchunguzi na akagundua kuwa tayari ulikuwa umeolewa na tayari ulikuwa ni mjamzito.Nilianguka na kuzimia Sikutaka kuamini moja kwa moja taarifa zile lakini kwa kuwa nilikuwa kifungoni sikua na la kufanya ili kuupata ukweli.Niliwaomba wazazi wangu wanisaidie kufanya uchunguzi juu ya jambo hili lakini wao ndio hawakutaka kabisa hata kunisikia nikilitamka jina lako tena.Siku zilikwenda bila ya mawasiliano yoyote baina yetu na taratibu nikaanza kuukubali ukweli kuwa haupo tena na mimi.Mpaka siku namaliza kifungo changu sikuwa nimepata barua yoyote toka kwako.Nilimaliza kifungo na nikaanza upya tena kuyatengeneza maisha yangu.Nikasoma ,nikamaliza na hatimaye nikaanza maisha yangu ya kujitegemea.Siku moja nikiwa natazama luninga ,warembo waliokuwa wakishiriki fainali za kumtafuta mrembo wa Tanzania walikuwa wakijinadi nilikuona ukipita.Sikuamini nikaanguka na kupoteza fahamu.Na ni hapo ndipo matatizo ya moyo yalipoanza.Hakuna mtu yeyote anayefahamu nini chanzo cha maradhi yangu zaidi ya rafiki yangu wa pekee Andrew.Nilijitahidi ili niweze kukuona siku ile ya shindano lakini kwa bahati mbaya mara tu uliponiona na wewe ukapatwa na mstuko ukaanguka na kupoteza fahamu.”

    Patrick akanyamaza akamwangalia Happy usoni.Macho yake yalijaa machozi.Hadithi ya Patrick ilimchoma moyo sana.Donge kubwa likamkaba kooni.Hakuwa na la kufanya zaidi ya kulia.Patrick akamuonea huruma ,akamkaribia na kumfuta machozi kwa kitambaa chance.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “nyamaza Happy .Nyamaza mrembo wangu.Usilie tena.Hayo yameshapita”

    Ilikuwa vigumu kwa Happy kunyamaza kutokana na hasira alizokuwa nazo.

    “Nashindwa Patrick kunyamaza kutokana na ukatili niliofanyiwa .Ni bora mt aliyenifanyia hivi angeniua kabisa kuliko kuniacha nikiteseka kwa muda mrefu namna hii.”

    Kimya kikapita .Patrick akasema

    “Happy nafikiri mpaka hapa hakuna wa kumlaumu mwenzake kwa yaliyotokea.Kila mmoja amekwishapata picha halisi ya nini kilichotokea.Sisiti kusema kuwa Veronika ndiye chanzo kikubwa cha sisi kutengana.Nina imani kubwa kuwa ni yeye tu ndiye aliyeuvuruga uhusiano wetu kwa kutunga uongo huu mkubwa.Hakuna mwingine anayeweza kufanya kitu kama hiki zaidi yake.”

    Patrick akainuka na kuelekea mezani huku akiwa amefura kwa hasira.

    “I hate you Vero.I hate you..!!”

    Alitamka maneno haya kwa hasira sana huku akitokwa na machozi.Happy aliyekuwa amekaa kitandani akaogopa.Hakuwahi kumuona Patrick akiwa katika hasira namna ile.Taratibu akamsogelea na kumshika mkono.

    “Calm down Patrick.Its ok.”

    “Happy I hate this woman so much.Ametutesa kwa kwa kipindi kirefu sana.Kwa nini? she must pay for this”

    Happy akamwacha Patrick atulie kwanza na baada ya dakika kadhaa akasema.

    “Patrick”

    Patrick akastuka na kumwangalia Happy .

    “Patrick” Happy akaita tena.

    “Yes Happy nakusikiliza”

    “After all that happened do you still love me?

    Patrick akastuka kwa swali lile,akainuka na kumsogelea zaidi Happy ,akamshika mikono yake yote miwili akamtazama usoni.

    “Happy ” akatulia kidogo halafu akaendelea.

    “World do change,weather and climate do change,people do change,everything do change but Patrick never change.I’m the same Patrick you know,who loves you that much.Nothing has changed.Pamoja na yote yaliyotokea lakini I’ve never stoped loving you not for a second.Now that I’ve known the truth I love you even more.Do you still love me?

    Kauli ile inamfanya Happy atoe machozi.Midomo inamtetemeka anashindwa kuomgea.Patrick akamuangalia machoni na kumuuliza tena.

    “Happy am I still have a place in your heart ?

    Happy akajikakamua na kusema

    “Patrick you were the first man ever happened in my life.You were my first man I loved.You were the fisrt man to win my heart.I gave you my heart,my body,soul and everything.You were my angel,my Hero.No body will ever win my heart than u did.I’m everything I am because you loved me Patrick.Possibly there could be no Miss Tanzania Happy Kibaho now if its not for your love and sacrifices.Pamoja na yote yaliyotokea Patrick I still love you more and more.U still have chance in my heart,but I’m sorry Patrick….”

    Happy akashindwa kujizuia kulia kwa sauti.

    “Sorry? Sorry for what Happy ? Patrick akauliza

    “Its complicated”

    Patrick taratibu akahisi kama nguvu zinamuisha

    “Complicated?How”

    “Patrick baada ya kuamini kuwa tayari umekwisha kufa basi nikaamua kuwa na mpenzi mwingine.Mike cambell ndiye mpenzi wangu niliyenaye kwa sasa na tayari amekwisha nivisha pete ya uchumba.I’m so sorry Patrick”

    Patrick alihisi kama vile kila kitu mle ndani kilikuwa kikizunguka.hakuamini kama ni kweli anaweza kumkosa Happy kirahisi rahisi namna ile.akaunyoosha mkono wa Happy na kuangalia kidoleni.Ni kweli Happy alikuwa na pete ya uchumba kidoleni.Patrick akaingalia huku machozi yakimlenga lenga.wakati Patrick akiwa ameduwaa akiiangalia ile pete ya uchumba kidoleni mwa Happy akashangaa Happy akikinyoosha kiganja chake na kukishika kidole kilichokuwa na pete ya uchumba.

    “I’m right.Its complicated.Hata wewe hii si ni pete ya uchumba? Kila mmoja tayari amekwisha amua kuendelea na maisha yake.Kutokana na hali ilivyokuwa hakukuwa na matumaini ya kuonana tena.Hivyo hakuna mtu wa Kulaumiwa kwa maamuzi haya kati yetu sisi wawili.Kila mmoja hakuwa na njia nyingine zaidi ya kuamua kusahau yaliyopita na kusonga mbele na maisha yake.Kwa hiyo Patrick veronica ndiye mchumba wako?

    Patrick akakabwa na donge kubwa kooni.akababaika ajibu nini.

    “Happy ” Patrick akaita

    “Happy nasikitika sana.Halikuwa kusudio langu kufanya hivi lakini kwa kipindi hicho sikuwa na jinsi ya kufanya niliamini kuwa tayari ndoto yetu ya kuwa pamoja imeshapotea .Niliamini moja kwa moja taarifa za vero na nikawa na hasira sana juu yako kwa kuamini kuwa ulikuwa umevunja ahadi yetu.Kweli kwa wakati huo ni Veronika pekee ndiye aliyekuwa ni mfariji wangu mkubwa.Ukaribu wetu ukaongezeka na taratibu tukajikuta tukihama toka katika urafiki wa kawaida na kuwa wapenzi.Kwa kiasi kikubwa alinisaidia kusahau mateso na maumivu niliyoyapata juu yako.Uhusiano wetu umedumu kwa muda mrefu sasa na tukaona ni bora tufunge ndoa kabisa.Hivi sasa tunavyoongea tayari maandalizi ya harusi yetu yako katika hatua zake za mwisho.Nafikiri mwezi ujao tarehe za kati kati nitafunga ndoa na vero.”

    Happy alishindwa kujizuia kutoa kilio kikubwa.Patrick akamkumbatia.

    “Patrick my first love.Patrick my angel,siwezi kuuzuia uchungu huu mkubwa ninaousikia moyoni mwangu.Ninaumia mno kwa kitendo hiki alichonifanyia mwanamke mwenzangu.Ni bora hata angeniua kabisa kuliko kunifanyia ukatili huu mkubwa.Patrick you were my life,and my breath.Veronika has taken you from me, my breath.Sikutegemea kama mwisho wetu ungekuwa hivi”

    Happy aliongea kwa uchungu mwingi sana huku machozi mengi yakimtiririka.

    “Patrick nimefurahi kuufahamu ukweli.Sikulaumu kwa yaliyotokea.Hukuwa na kosa na wala wewe hupaswi kinilaumu mimi.Kwa kuwa kila mmoja tayari amekwisha anza maisha yake mimi naona ni bora iwe hivyo.Kila mmoja atabaki ni historia kwa mwenzake.Ninachokuomba mpende zaidi Veronika.Kamwe usimfanyie jambo lolote lililo baya.Alifanya kosa,alidanganya na hii yote ni katika kulipigania penzi lako la kweli.Nakubali kushindwa.Sitaki kushindana na Vero sipendi na yeye aje aumie kama nilivyoumia mimi.Nafikiri mateso yangu ni makubwa na sidhani kama anaweza kuyavumilia kama mimi.Mimi namwachia Mungu kwani yeye………….”

    “Happy ”Patrick akadakia

    “No Patrick don’t say anything yet.I’m hurt.”

    Chumba kilichokuwa katika hali ya mahaba mazito muda mfupi uliopita ,sasa kilikuwa ni sehemu yenye majonzi makubwa.Vilio vya chini chini ndivyo vilisikika.ILikuwa ni hali yenye kuhuzunisha sana kwa wapenzi hawa wa zamani.

    Happy akamvuta Patrick karibu yake akamkumbatia kwa nguvu.Akamwachia na kumtazama usoni.Kwa sauti yenye kukata kata Happy akaimba

    “Don’t,don’t go to your heart how feels.

    Don’t be afraid of dreams not real,

    Close ur eyes,pretend it’s just the two of us again,

    Make belief, this moment’s here to stay,

    Touch, touch me the way you used to do,

    I know, I could be lie right here with you,

    From now on ,you will be with someone else instead of me,

    So tonight, let’s feel these memories.

    So for the last, hold me now don’t cry, don’t say u were just, hold me now………

    Time, time will be kind once we’re apart,

    And ur tears, tears will no have place in ur heart.

    I wish I,I could say how much I’ll miss you when ur gone,

    All my love for yoy will go away……………

    Happy akashindwa kuvumilia akaangua kilio kikubwa.

    “No Happy !! Noo……This cant be”Patrick akasema kwa hasira.

    ***********************

    Ulikuwa ni usiku mrefu sana na mgumu kwa Mike cambell.Kitendo cha Happy kuondoka bila kumuaga anakwenda wapi kilimchanganya akili .Kilichompa wakati mgumu zaidi ni kitendo cha Happy kumkatia simu na kisha kuizima kabisa simu yake.Kitendo hiki kilimuumiza mno.Haijawahi kutokea katika uhusiano wao.

    “I real love you Happy no matter what”

    Alitamka Mike kwa sauti huku akijimiminia mvinyo katika glasi.Toka amefika chumbani kwake leo hii amekuwa akinywa pombe kali kwa dhumuni la kuupunguza mzigo wa mawazo aliokuwa nao.

    Alikaa tena sofani,akawaza,akachukua simu na kubonyeza namba za Happy lakini jibu likawa ni lile lile.Simu ya Happy haikuwa ikipatikana.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kwa jinsi ninavyomfahamu Happy lazima kutakuwa na jambo linalomsumbua akili yake.Mara nyingi akiwa na jambo linalomsumbua huwa hapendi usumbufu.Lakini ni bora basi angeongea nami japo hata kidogo tu na kunitoa wasiwasi .”

    Mike akapiga funda kadhaa za mvinyo.

    “I know u need to be alone for a while Happy .I will wait here for you till you come back.I hope you will be back soon.Be safe there my angel”

    Mike alikuwa akiongea maneno haya kwa sauti .Ni wazi alikuwa ameanza kulemewa na kilevi.

    Wakati Mike akiwa katika mtihani mgumu na kuamua kupoteza mawazo kwa kunywa mvinyo mkali,mambo yalikuwa magumu zaidi kwa Veronika.Usiku huu alikuwa katika kitanda chake akijigeuza geuza, macho yakiwa makavu na mekundu kwa kulia.Akainuka na kwenda kulifungua dirisha akachungulia nje kana kwamba kuna kitu alikuwa akitegemea kukiona.Alikaa hapo dirishani kwa muda mrefu akiziangalia nyota na mwezi.Machozi hayakuwa yakitoka tena alikuwa Amelia sana mchana kutwa.

    Ni mlio wa simu yake ndio uliomstua toka katika mawazo mazito.Taratibu akaichukua simu yake na kutazama mpigaji.Alikuwa ni mama yake Patrick.

    “Hallo mama”

    “Veronika mwanangu unaendeleaje?

    “mama naendelea hivyo hivyo tu.Vipi kuna habari yoyote mpaka sasa hivi?

    “Hapana Veronika mpaka sasa sijapata taarifa zozote kuhusu mwenzio.Ila nina wazo moja”

    “Ndiyo mama nakusikiliza”

    “Yawezekana huyu Patrick akawa katika dharura zake kama anavyodai.Mimi naona sisi kuendelea kumsubiri ni kupoteza wakati wetu.Nionavyo mimi hataki kwenda huko Uingereza ndio maana amekuwa akikimbia kimbia.Kwa hiyo basi Vero mwanangu ili tusiendelee kupoteza muda zaidi wewe itakubidi tu uende peke yako ufanye shopping .Hatuna njia nyingine ya kufanya.Vumilia Vero namfahamu Patrick vizuri atatulia tu muda si mrefu.”

    Veronika akatulia akatafakari kwa sekunde kadhaa kisha akasema

    “Ok nimekuelewa mama.Nitafanya hivyo.Safari ni kesho saa tano asubuhi.Ila sintachukua muda mrefu sana nadhani baada ya siku tatu au nne nitarejea.siwezi kukaa mbali na Patrick kwa kipindi kirefu na hasa wakati huu anaoumwa umwa”

    “Sawa Vero nashukuru sana mwanangu kwa kukubali kufanya hivyo.Nitakuja kukusindikiza kabla hujaondoka”

    *******************

    “Happy ” Patrick aliita huku akimuangalia usoni binti huyu mwenye uzuri wa kimalaika.

    “Yes Patrick”akajibu Happy kwa sauti laini sana huku naye akimwangalia Patrick usoni.

    “I can’t let you go.Ulinipotea mara ya kwanza nimefanikiwa kukupata tena.Safari hii hutanipotea tena.siwezi kukuacha kamwe upotee tena mikononi mwangu .Happy I love you so much.You are the only one I truly love.The only one.Please Happy stay with me.dont leave me again.”

    Patrick aliongea maneno haya taratibu na kwa hisia.Ni wazi maneno haya yalitoka ndani kabisa mwa moyo wake.

    “Patrick hata mimi sitaki kukupoteza tena maishani mwangu.Wewe ndiye pumzi ya maisha yangu.Wewe pekee ambaye unaweza kunifanya mimi niishi kwa furaha maisha yangu yote yaliyobakia hapa duniani.Nilikupoteza mwanzo na nimekuona tena.Nisingependa hata mimi kukupoteza tena lakini…………….”

    “Lakini?’ Patrick akadakia

    “Hakuna lakini Happy .Hata iweje siwezi kukubali upotee tena .Wewe ndiwe mwanamke pekee niliyekupa moyo wangu.Because I love you Happy , I will make a sacrifice for you.”

    “Sacrifice?? Happy akauliza kwa mshangao.

    “Yes Happy .Ninaifuta ndoa yangu na Veronika.Sintamuoa Veronika tena”

    “Patrick!!!!!!!.......

    Happy akapiga ukelele wa mshangao.

    “Patrick please usifanye hivyo.Nakuomba Patrick niko chini ya miguu yako usifanye hivyo.Najua unanipenda na penzi lako kweli ni la dhati na kweli lakini Patrick tumekwisha umia vya kutosha.Naomba tuendelee kuumia sisi wenyewe tusiwaumize tena watu wengine zaidi.Kufuta ndoa yako na Vero ni suala rahisi kwako lakini so many people will get hurt.Watu wengi wataumia sana.Vero loves you very much and Mike loves me very much.We cant hurt the people that loves us.Patri…….”

    “Happy ”Patrick akadakia.

    “Please naomba unisikilize kwa makini sana.Najua kwamba uamuzi huu utaumiza watu wengi sana.Ndiyo ni wengi wataumia na kuhuzunika lakini sina namna nyingine ya kufanya zaidi ya hivyo nilivyokwambia.Siwezi kuendelea kujidanganya kwamba nitaishi kwa furaha na amani na Veronika wakati nikijua kuwa upo na bado unanipenda.Siwezi Happy kuendelea kuwa na Veroika mtu aliyetufanyia ukatili mkubwa sana .Niko tayari kuubeba mzigo wote wa lawama na kila kitu kwa ajili ya kuitafuta furaha ya maisha yangu.Nilifungwa kwa ajili ya kuzuia usidhalilishwe kwa hiyo sioni ajabu leo hii nikivunjilia mbali ndoa yangu na vero chui mwenye ngozi ya binadamu.”

    Happy ambaye bado machozi yalikuwa yakimtoka alijikaza na kusema.

    “Patrick ninajua una nia nzuri na mimi na uamuzi huo ni wazi umetoka ndani kabisa mwa moyo wako.Hata mimi Patrick ninaumia sana tena zaidi hata ya siku ile nilipopata taarifa zile za kufariki kwako.Ninaumia kwa sababu sijui nifanyeje ili usiende mbali na mimi tena.Lakini Patrick tayari nimempa nafasi Mike .Nilifanya vile kwa sababu nilihitaji kuwa na mtu baada ya kuamini haupo tena duniani.Pamoja na nafasi hiyo lakini nafsi yangu imekuwa nzito katika kumpa moyo wangu wote aumiliki kama nilivyofanya kwako.Bado nafsi yangu inaugulia kwa ajili yako.lakini Patrick…………………”

    Happy akashindwa kuendelea kuongea akainama akilia

    Patrick akamshika shingoni na kumwambia

    “Lakini nini Happy ?

    “Patrick tayari hatua kubwa sana zimeshapigwa katika maisha yetu ya kimahusiano.Naomba Patrick tusiendelee kuwamiza watu wengine tena.naomba usimuache Vero kwa aijli yangu.Sijui kama ninatweza kuachana na Mike kwa sababu ananipenda kupita kitu chochote”

    Patrick akamtazama Happy kwa sekunde kadhaa kisha akasema

    “Happy please look at me.Look at me and tell me that U don’t lome me any more.I will understand and let you go.”

    Happy akainua uso wake na kumtazama Patrick .



    “ooh Patrick please don’t leave me.I love u so much”

    Happy akajikuta akijilaza kifuani kwa Patrick na kumkumbatia kwa nguvu.

    “patrick I love you so much.Please Patrick don’t ever leave me again.”

    “Its ok Happy it’s ok my angel. I won’t let you out of my hands again”

    Happy akamkumbatia kwa nguvu zaidi Patrick .Taratibu Patrick akaanza kuzichezea nywele nzuri na ndefu za Happy .Mkono wa kulia ukashika hadi shingoni na kuisugua taratibu kisha kwa pozi za aina yake ukashuka kuelekea mgongoni ukipita kati kati kabisa ya mgongo kana kwamba anapiga kinanda.Happy akastuka.

    “ouh Patrick I love you.”

    Wakatazamana na taratibu sana kama inavutwa na sumaku midomo ikaanza kukaribiana na mara ikakutana na zoezi tamu la kunyonyana ndimi likaanza.

    ‘ouh Patrick my baby don’t ever leave me again” alisema Happy kwa sauti ya kuhema iliyojaa raha.

    Patrick hakusema kitu taratibu akaanza kufungua vifungo vya shati alilokuwa amevaa Happy akalitoa na kulitupa pembeni.Moyo ukazidi kumwenda mbio baada ya kukutana na kifua kile cha Happy chenye kusisimua.Hakutaka kuwa na papara kwani tayari alijua kila kitu ni chake kwa usiku huo.Akampiga busu zito mdomoni kisha akaifungua sidiria nyeupe aliyokuwa ameivaa Happy akakutana na chuchu nzuri za mlimbwende huyu ambazo zinazidi kumpa wazimu Patrick.Kwa ufundi wa aina yake akaanza kuzinyonya chuchu zile huku Happy akitoa mguno kwa raha aliyoisikia.Wakati akinyonya chuchu zile mkono wake wa kulia ukawa ukiifungua zipu ya sketi fupi aliyokuwa ameivaa Happy akafanikiwa kuifungua na taratibu akaishusha chini.Happy alikuwa amezidiwa na utamu na hata maneno aliyokuwa akiyatamka yalikuwa hayasikiki vizuri.Taratibu Patrick akaanza kushuka chini mpaka maeneo ya kitovuni na halafu chini yake zaidi.Mambo aliyoyafanya hapo siwezi yaelezea.Happy alikuwa akitoa miguno kana kwamba anataka kufa.

    “Patrick I…It’s..my first…time don’t hurt me.”

    Happy akasema kwa kukata kata.Happy hakuwahi kukutana na mwanaume yeyote kabla.Patrick alistuka kusikia hivyo.Hakutegemea kama msichana mzuri kama Happy angeweza kuutunza usichana wake mpaka wakati ule.

    Kwa kuwa ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Happy ,Patrick akapunguza kasi na kwenda taratibu ili mrembo huyu asiumie.

    Happy akatoa mguno wa maumivu.Tayari usichana wake ulikuwa umeondolewa.

    *****************

    Ni saa nne asubuhi wakati Mike Cambell aliposimamisha gari nyumbani kwa akina Happy .Moja kwa moja akafululiza mpaka ndani na kumkuta mama yake Happy .

    ‘ Mike karibu baba” akasema mama yake Happy

    “Ahsante mama shikamoo”

    “Marahaba mwanangu,karibu sana”

    “Ahsante mama.Kuna taarifa zozote za Happy ?

    “Hapana baba mpaka sasa hivi hatuna taarifa zozote za Happy .Bado simu yake haipatikani.Vipi wewe una taarifa zozote ?

    “Hapana mama .Bado sijapata hata ujumbe wowote toka kwake”

    “Jamani mtoto huyu kwa nini lakini anafanya hivi?

    “Mama,nafikiri labda tuwe wavumilivu ,tumwache kidogo pengine ni wazi anahitaji kuwa peke yake kwa kipindi hiki.Nina imani huko aliko yuko salama salimini na ni lazima atarejea salama”Mike akasema lakini ni wazi moyoni alikuwa ameumia sana.

    “Nashukuru sana baba kwa kuwa mwelewa.Mimi mara tu nitakapopata taarifa yake nitakutaarifu mara moja”

    “Sawa mama nashukuru”

    Mike aliaga na kuondoka.Mama yake Happy alilisindikiza gari lile la Mike kwa macho mpaka likapotea kabisa.Alipogeuka akakutana na Margreth.

    “ Mike anasemaje? Margreth akauliza

    Mama yake akamtazama kwa sekunde kadhaa

    “Hivi nyie watoto kwa nini mnamfanyia hivi mwenzenu?

    “Mwenzetu yupi mama?

    ”Si Mike? Hivi hamuoni kuwa mnavyomfanyia si vizuri?Happy hataki kuwasiliana naye ,hata wewe unamkwepa shemeji yako.Kwa nini lakini?

    Margreth hakujibu kitu akatazama chini

    “mama mi naogopa hata kumwangalia kwa sababu atahisi ni lazima ninajua Happy yuko wapi”

    “Mhhh!!!! …….haya” Mama yake akaguna na kuondoka

    ***************

    SIKU NNE BAADAE - ARUSHA

    “Happy darl ni siku ya nne leo tangu tumefika hapa Arusha.Najua ni lazima huko tulikoondoka watakuwa na wasi wasi mwingi kwa sababu tangu tumefika hapa simu zetu zote tumezima.Nimefikiria nimeona nimpigie simu mama yangu ili nimtoe wasi wasi.’

    Happy aliyekuwa amejilaza katika kiti kilichokuwa pembezoni mwa bwawa la kuogelea ,alimtazama Patrick kwa sekunde kadhaa kisha akasema.

    “Ok baby ,ni wazo zuri ,ingawa mimi sikuhitaji kufanya hivyo kwa sasa lakini kwa vile umeomba basi sawa hata mimi itanibidi nifanye hivyo.”

    Wakainuka na kuelekea chumbani kwao.

    Patrick akaishika simu yake akaitazama kisha akaiwasha.Jumbe fupi za maneno zikaingia mfululizo .Hakusumbuika nazo moja kwa moja akaandika namba za mama yake na kumpigia.

    “Haloo mama shikamoo” Akasema Patrick baada ya mama yake kupokea simu

    “ Patrick hujambo? Uko wapi we mtoto,mbona unatuweka roho juu namna hiyo?Hatulali tunakuwaza wewe,Vero anapiga simu usiku na mchana kukuulizia,Uko wapi na unafanya nini wewe mt…..” Patrick hakutaka kumpa mama yake nafasi kubw ya kuongea,ikamlazimu kuingilia kati.

    “Mama us……………..”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kabla hajaendelea mama yake naye akadakia

    “Baba yako kawa mbogo huku ,kila siku tunakwaruzana kwamba mimi na wewe letu moja.Sasa ni lini unarudi we mtoto?

    “Mama usijali,mimi ni mtu mzima na ninajua kitu ninachokifanya.Watoe shaka watu wote mimi niko salama salimini na muda wowote ninakuja nyumbani.Ni kama nilivyokueleza nilipatwa na dharura ndo maana nikaondoka ghafla vile.”

    “lakini Patrick mwanangu hivi hizo dharura zako ni muhimu kuliko suala la ndoa yako? Hivi hizo dharura zina msaada gani katika ndoa yako?Andglia mwanangu harusi ni mwezi ujaona kikao cha mwisho ni wiki ijayo kisha ndoa ikaandikishwe kanisani na kuanza kutangazwa.Sasa huoni kuwa unahitaji kuwa karibu sana kwa wakati huu?

    “Nalielewa hilo mama na mojawapo ya mambo yaliyonileta huku ni kuhusiana moja kwa moja na hiyo harusi yangu,hivyo usijali mama,ila tafadhali naomba kikao cha mwisho kisikae kama nitakuwa sijarudi.nataka niwepo katika kikao hicho nina jambo kubwa la muhimu sana la kuongea na kamati nzima pamoja na nyie wazazi wangu”

    Mama yake Patrick akanyamaza kidogo kisha akastuliwa na Patrick.

    “Mama naomba nikate simu .wasalimu wote hapo nyumbani ila tafadhali naomba unifikishie ujumbe wangu huo kwa kamati. Bye mama.I love you.”

    Patrick akakata simu kisha akapumua kwa nguvu.

    “Darling kuna tatizo lolote? Happy akauliza baada ya kumuona Patrick akionekana kuzama katika mawazo ghafla.

    “Hapana dear hakuna tatizo lolote,ngoja kwanza niongee na Andrew”

    Patrick akazitafuta namba za Andrew na kumpigia.

    “Yes Comrade” Aliita Patrick baada ya simu yake kupokelewa na Andrew .

    “wow!Patrick how are you?

    “I’m great andrew”

    “hahahah mambo yanakwendaje hapo Arusha brother kwa sababu naona umekaa kimya kabisa ..”

    “Du ! Andrew huku ni burudani kila sekunde,.Tayari tumeshamaliza matatizo yetu na kwa sasa tumeazimia tunaanza upya.”

    “Wow! That’s great”Akasema Andrew

    “sasa andrew sina muda muda mrefu sana wa kuongea na simu hebu nipe japo kwa muhtasari juu ya hali ya mambo yanavyokwenda hapo Dar.Nimetoka kuongea na mama sasa hivi anapiga kelele huyo hadi nikakata simu”

    “Patrick huku mambo ndo yanazidi kupamba moto.maandalizi yanaendelea kwa kasi ya ajabu.Kadi ziko tayari na kinachosubiriwa ni kikao cha mwisho cha kamati ya maandalizi kikae ili kuangalia kama kuna kitu kilichobakia kabla ya kutangaza rasmi tarehe ya kufunga ndoa.Vero alienda Uingereza japo kwa shingo upande na kila siku ananipigia simu kama ninataarifa zozote.Watu wanahaha kutaka kujua uko wapi .Yaani ninapata shida sana manake kila mmoja anajua kuwa ni lazima nitakuwa ninajua mahala ulipo.”

    “du ! pole sana Andrew.I’m very sorry to involve you in this issue.Nakuomba uwe mvumilivu rafiki yangu bado yatakuja makubwa zaidi ya hayo.Mimi nitarudi muda wowote kwa sababu nataka niwepo siku kikao cha mwisho kitakapokaa.Nina mambo ya kuongea na wanakamati .Kwa sasa bado ninaendelea kula bata na mrembo wangu”

    “Sawa Patrick mimi nitafanya kila linalowezekana kufanyika.”

    “Ok andrew nitakuwa nakupigia mara kwa mara ingawa muda mwingi simu yangu itakuwa imezimwa.”

    “Ok brother take care”

    Patrick akakata simu na kumwangalia Happy .

    “Mbona Vero humpigii simu?

    “Mhh ! forget about her”Akasema Patrick huku akimpa simu Happy

    ‘Ongea na mama mtoe wasi wasi najua atakuwa na wasi wasi mwingi juu yako kwani toka umefika hapa hujawasiliana naye na kumjulisha unaendeleaje”

    Happy akaandika namba za mama yake na kupiga

    “Haloo mama shikamoo”

    “wow! Happy .Hujambo mwanangu?

    “Sijambo mama vipi hapo nyumbani wazima?

    “Huku wote wazima Happy ,roho zetu juu juu kwa sababu yako.Lini utarudi? Na mbona simu yako haipatikani?

    “Mama msiwe na wasi wasi mi ni mzima kabisa na muda wowote ninaweza kurudi nyumbani.Simu yangu kwa bahati mbaya haina chaji hata kidogo ndio maana imezima.”

    “Sawa Happy mi nafurahi kusikia uko salama.lakini ni kwa nini hutaki kumpigia simu Mike?Hivi unajua ni kwa kiasi gani unavyomtesa mwenzio?.Hebu anagali mwenzio katoka Marekani kuja kukupa hongera kwa ushindi wako lakini wewe ndio kwanza hata kumwona hutaki kwa nini lakini Happy ?

    Happy akapatwa na kigugumizi cha ghafla akashindwa ajibu nini akanyamaza kimya kwa sekunde kadhaa.

    “Happy nakuuliza kwa nini unamfanyia hivyo mchumba wako?

    Mamayake akaendelea kuhoji

    “Mom please I have to go,bye”

    Happy akaikata simu na kumpa Patrick ambaye aliizima kabisa.Patrick alikwisha ng’amua kuwa mambo katu hayakuwa mazuri kwa Happy .

    “Happy my baby” Akasema Patrick huku amemshika Happy mkono

    “Calm down my sweet love.This is just the beginning .You have to be strong”

    Kikapita kimya kifupi halafu Patrick akauliza

    “Mama alikuwa anasemaje?

    “Alihitaji kufahamu nitarudi lini na ni kwa nini siwasiliani na Mike.Patrick nilikubali kumpa moyo wangu Mike kwa sababu kwa wakati huo nilijua tayari umeshafariki.Laiti ningelijua kuwa badio upo hai nisingempa moyo wangu Mike.Lakini kwa vile tumeshaonana na wewe ndie mwanaume pekee nikupendaye duniani,basi sina budi kuwa wazi kwa Mike.It hurts lakini sina jinsi ni lazima nimweleze ukweli.Patrick ulinipotea mara ya kwanza lakini safari hii hutaweza kunipotea tena.I’ll fight for you”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ITAENDELEA



0 comments:

Post a Comment

Blog