Simulizi : Miss Tanzania
Sehemu Ya Tano (5)
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Namna gari lile lilivyoingia hospitali na sauti za matairi yakilalama kutokana na breki kali aliyofungwa,iliwafanya madaktari na wauguzi watoke nje na kushuhudia nini kilichotokea.Mzee Kibaho akashuka na kukimbia na kuwataarifu wauguzi kwamba kulikuwa na mgonjwa mahututi ndani ya gari.Kwa kasi ya aina yake,wauguzi wakampakia Happy katika kitanda na kumkimbiza katika chumba cha wagonjwa mahututi.Mzee Kibaho akaombwa asubiri nje.Bado mwili wake ulikuwa unamtetemeka kupita kiasi.Aliogopa sana.
ENDELEA…………
“Please my Lord,don’t let my daughter die” akazidi kuomba mzee Kibaho.na mara simu yake ikaita.Alikuwa ni Margreth.Mzee Kibaho akavuta pumzi ndefu kabla ya kuipokea simu ile halafu akabonyeza kitufe cha kupokelea.
“Hallo Margreth” akasema mzee Kibaho
“baba uko hospitali gani?
“ niko hapa Brahmaputra hospital.Uko wapi Margreth?
“Nimefika hapa nyumbani sasa hivi nikaambiwa kuhusu hali ya Happy.Dady tell me please how’s she? Akauliza Margreth
“Tayari amepokelewa hapa na ameingizwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.Madaktari wamesimamisha shughuli zote na wanajitahidi kuokoa maisha yake.”
“Unaonaje hali yake? Akauliza Margreth
“Margreth siwezi kusema chochote kwa sasa”
“sawa baba,nakuja sasa hivi huko hospitali” akasema Margreth
“Maggie mama yako anaendeleaje?
“Mama hali yake naye si nzuri hata kidogo.Amezinduka na kuzirai tena.Dokta Salome Yule jirani yetu yuko hapa anaendelea kumuhudumia.” Akasema Margreth.Mzee Kibaho akavuta pumzi ndefu na kukata simu
“Whats happening to my family? Ee Mungu naomba unipe nguvu ya kuweza kuyakabili matatizo haya makubwa yanayoikabili familia yangu kwa sasa.Naomba umsaidie mwanangu Happy aweze kupona” Mzee Kibaho alikuwa anaomba kimoyo moyo.Hakuweza kutulia sehemu moja.Alikuwa ni kama mtu aliyechanganyikiwa.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Margreth aliwasili Brahmaputra hospital na moja kwa moja akaelekea mahala alikokuwa baba yake.Macho yalikuwa mekundu kwa kulia
“baba kuna taarifa yoyote tayari umepata kuhusiana na Happy? akauliza Margreth
“Hakuna taarifa yoyote mpaka hivi sasa.Bado madaktari wanaendelea kumshughulikia.” Akasema mzee Kibaho.Jibu lile likazidi kumtoa machozi Margreth.Baba yake akamsogelea na kumkumbatia
“Please Margreth be strong.We need to be strong for Happy” akasema mzee Kibaho huku naye sauti yake ikionyesha kutetemeka
“Dady why could Happy do such a thing to us? Kwa nini aamue kunywa sumu? Akasema Margreth huku akilia
“I don’t know Maggie,I don’t know”
“Inauma sana baba.Sijawahi kuumia kama nilivyoumia leo.Hapa nilipo ninahisi moyo wangu unakatwa vipande vipande.Baba ninampenda sana Happy na sijui nitafanya nini kama hataweza kupona.Sijui kama nitaweza kuishi bila yeye” Margreth akaendelea kulia
“Tunatakiwa tujikite katika maombi tumuombee.Mungu atasikia vilio vyetu na atamponya Happy.I know Happy is strong and she’s going to fight this .She’ll fight for us and for all those who love her.” Akasema mzee Kibaho huku naye macho yake yakiwa na machozi.Margreth akatoa kijikaratasi toka katika mkoba wake na kumpatia baba yake
“Kikaratasi hiki kimekutwa chumbani kwa Happy.Ni ujumbe aliouacha”akasema Margreth.Mzee Kibaho akakunjua kikaratasi kile na kuanza kukisoma
“wakati mnausoma waraka huu tayari nitakuwa nimekwisha ondokewa na uhai.Nimechukua maamuzi haya magumu kutokana na kuchoshwa na aina ya maisha ninayoishi sasa.Mambo mengi yamenitokea ndani ya kipindi kifupi sana na nimeyavumilia yote lakini kwa hili lililotokea leo limenifadhaisha mno .Kwa ufupi tu ni kwamba jana nilitekwa na watu nisiowafahamu wakanipeleka mahala na wakanilazimisha kuyafanya haya mliyoyaona katika magazeti,kwa ajili ya kuokoa uhai wa Patrick.Sitaki kuliongeala sana suala hili lakini naomba mnifikishie ujumbe kwa Patrick kwamba nimekufa na yeye akiwa ni mwanaume pekee ninayempenda na sintaacha kumpenda hata huko niendako.Nilikubali kufanya haya kwa ajili ya kumuokoa yeye asiuawe.Nawapenda wote na ninawaomba mnisamehe kwa jambo hili ambalo najua litawaumiza sana lakini sina namna nyingine ya kuniondoa katika aibu hii kubwa zaidi ya kujitoa uhai…Kwa herini nyote”
Mzee Kibaho alishindwa kuyazuia machozi kumtoka baada ya kumaliza kuusoma ujumbe ule wa Happy
“Ee Mungu najua unaweza na haushindwi na lolote,nakuomba umponye binti yangu Happy.Mimi na familia yangu bado tunamuhitaji sana.Ni wewe tu ambaye unaweza kumuokoa toka kifoni kwa sasa.Naomba usikilize maombi ya familia yangu na Happy aweze kupona” Mzee Kibaho akaomba kimya kimya huku akijifuta machozi kwa kitambaa
Taarifa za Happy kutaka kukatisha uhai wake kwa kunywa sumu zilianza kusambaa kwa kasi baina ya ndugu na marafiki wa karibu wa familia.Wengi walianza kufika pale hospitali ili kujua kilichokuwa kinaendelea.
“Nilijua tu lazima kuna sababu iliyomfanya Happy afanye kitendo kile.Sikuamini kabisa kama Happy ambaye nimemlea na kumkuza katika maadili anaweza akatenda kitendo kama hiki cha kujidhalilisha kwa hiari yake.Ni nani huyo ambaye amemfanyia mwanangu unyama na udhalilishaji huu mkubwa? Huu ni udhalilishaji uliovuka mipaka.Happy ameshindwa kuvumilia na ndiyo maana akaamua kuchukua maamuzi haya aliyoyachukua.” Akawaza mzee Kibaho
“Aliyefanya jambo hili na kumdhalilisha mwanangu lazima atakuwa na lengo la kulipiza kisasi.Ninaanza kuhisi kwamba pengine jambo hili linahusiana na kifo cha Veronika kwa sababu kwa nini jambo hili litokee sasa? Lazima uchunguzi ufanyike na wale wote waliohusika na udhalilishaji huu walipe uovu wao.Lazima watu hawa wapatikane kwa namna yoyote ile.Nitahakikisha watu hawa wanakamatwa na hata kwa kuwatumia wapelelezi binafsi nitafanya hivyo.Niko tayari kutumia kiasi chochote cha fedha ili kuwasaka watu hawa waliomfanyia mwanangu jambo hili.” Akawaza mzee Kibaho.
* * * *
Mlio wa simu ukamstua Loniki toka usingizini.Akanyoosha mkono na kuichukua .Mpigaji alikuwa ni Linah
“Hallo Linah” akasema Loniki akiwa bado na usingizi
“Lonny bado umelala?
“Simu yako ndiyo iliyonistua.Jana niliporudi nilikunywa sana mvinyo na ndiyo ulionipelekea kulala namna hii” akasema Loniki
“Lonny umepata habari?
“Habari gani tena wakati wewe ndiyo mtu wa kwanza kuongea naye leo?
“Dah ! mambo tayari yameanza”
“mambo gani tena Linah?
“Leo jiji zima limeamshwa na habari moja tu.Habari ya Happy”
“Tayari habari yake imeshatoka? Akauliza Loniki na kuinuka akakaa
“Chezea Khumalo wewe .! akasema Linah huku akicheka.
“Khumalo amekwishamaliza kila kitu na hivi nikwambiavyo gazeti la Mitikisiko limekwisha na halipatikani tena mtaani.Katika mitandao ya kijami,taarifa inayozunguka hivi sasa ni hii ya Happy.Kila mtandao zimetapakaa picha na video ya Happy”
“Dah ! nashukuru sana kama kazi imekamilika.Nadhani hivi sasa kama Happy atakuwa amezipata taarifa hizi atakuwa katika maumivu makali sana kama niliyonayo mimi .Baada ya kummaliza Happy sasa tutahamia kwa Patrick” akasema Loniki.
“Lazima nihakikishe wale wote walioudhulumu uhai wa mdogo wangu wanalipa.They all must pay.This is just the beginning…” akasema Loniki
“Lonny nina imani ushauri huu alioutoa Khumalo ni wa busara sana kwani endapo Happy ataziona picha zile ni wazi ataumia mno .Ni picha zenye kudhalilisha sana.”
“Kweli kabisa Linah.Ninaanza kukubaliana na Khumalo kwamba unaweza usimuue mtu moja kwa moja lakini ukampa mateso makali ya moyo na akateseka katika maisha yake yote.Kwa mfano Happy,kwa sasa maisha yake hayatakuwa sawa tena.Tayari ameingia katika kashfa nzito na hii itamtesa katika maisha yake yote yaliyobaki.Pamoja na hayo Linah kuna jambo nataka kukuuliza”
“Uliza Lonny”
“Khumalo ni mtu wa namna gani? Anajishughulisha na nini? Na kile chumba alichowekwa Happy kina kazi gani hadi kikafungwa kamera za kisasa namna ile?
Linah akavuta pumzi ndefu halafu akasema
“Kwa kuwa wewe ni rafiki yangu nitakueleza lakini naomba mtu mwingine yeyote asifahamu.Khumalo anajishughulisha na biashara nyingi haramu ikiwamo ya madawa ya kulevya na hata shughuli kama hii uliyompa na wakati mwingine hata ujambazi wa silaha huwa anahusika pia.Kwa sasa ameamua kujikita zaidi katika biashara ya madawa ya kulevya ambayo ndiyo inayomuingizia fedha nyingi sana.Ukiacha biashara hiyo ya dawa za kulevya,hukitumia kile chumba alichowekwa Happy kwa ajili ya kurekodi filamu za ngono ambazo huziuza katika nchi za ulaya na Amerika na kujipatia fedha nyingi.Huwatafuta mabinti wazuri wa kiafrika na kuwalipa pesa nyingi halafu huwarekodi wakifanya ngono.Hii ndiyo kazi ya chumba kile.Lonny tutaongea zaidi baadae kwa sasa kuna mahala ninawahi” akasema Linah
“Ok Linah.Nitakuja ofisini kwako baadae.Ahsante kwa taarifa” akasema Lonny na kukata simu
“Ouh gosh !!Sasa moyo wangu unaanza kupata amani.I cant imagine how painfull Happy is right now.Picha ndo kwanza linaanza.Nitahakikisha wale wote waliohusika kusababisha kifo cha Vero wanalipa.Japokuwa ni gharama kubwa lakini nitajitahidi kufanya kila niwezavyo hadi nihakikishe nimemilipia kisasi mdogo wangu.” Akawaza Loniki huku akitoka mle chumbani
* * * *CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Akiwa bado katika mapumziko huku akiendelea na shughuli zake za usafi asubuhi hii,Sarah hakuwa na habari juu ya kilichokuwa kinaendelea hadi pale jirani yake alipoingia akiwa na gazeti mkononi na kumstua.
“Shoga yangu huyu si miss Tanzania aliyevunja uchumba wa Vero? Akasema shoga yake Sarah huku akimpa Sarah lile gazeti.Sarah akafuta maji mkononi na kulichukua gazeti lile
“Ouh My God ..!!! “ akasema Sarah kwa mshangao.Taarifa ile ilimstua mno.Mikono yake ilikuwa inamtetemeka.
“Hakika malipo ni hapa hapa duniani.Amemzuia mwenzake asiolewe halafu kumbe huu ndio uchafu anaoufanya.Dah ! ameumbuka sana” akasema Yule shoga yake Sarah
“Hapana..!!..Hii si sahihi.Sidhani kama Happy anaweza akafanya kitendo kama hiki.Lazima hapa kuna namna iliyofanyika ili kumzalilisha .Lazima kuna mkono wa mtu hapa na kama ndiyo hivyo mtu huyo si mwingine atakuwa ni Loniki.Ni yeye peke mwenye chuki na Happy na aliweka dhamira ya kulipiza kisasi na ninadhani hii ni moja ya mipango yake.” Akawaza Sarah.
“Mbona uko kimya Sarah? Akauliza Yule shoga yake
“Nimestushwa sana na taarifa hii.” Akasema Sarah na kuingia ndani akachukua funguo za gari lake na kuondoka kwa kasi
“Nina hakika mkubwa Loniki anahusika kwa kiasi kikubwa na jambo hili la udhalilishaji.Lazima leo hii niufahamu ukweli.Kwa nini anataka kuendeleza uhasama usiokuwa na faida yoyote kwetu? Hapana siwezi kukubali jambo hili liendelee” akawaza Linah
“Ninahisi hata zile fedha ambazo mama aliniomba jana na kisha akampatia Lonny,alikuwa anazihitaji kwa ajili ya kutekeleza mipango yake hii miovu.Ninahisi hata mama naye atakuwa anahusika kwa namna fulani na jambo hili.Kuna kitu atakuwa anafahamu kuhusiana na mipango ya Lonny ya kulipiza kisasi.Kama ni kweli Lonny atakuwa amehusika katika kumdhalilisha Happy namna hii ,kamwe sintaweza kumsamehe .” akawaza Sarah
Mama yake sarah alikuwa amekaa nje ya nyumba yake na pembeni yake kulikuwa na meza ndogo iliyokuwa na chupa kubwa ya chai.Alistuka alipomuona Sarah akiingia pale ndani akiwa na uso uliojaa hasira
“Mama shikamoo” akasema Sarah
“Marahaba Sarah.Mbona hivyo? Kwema huko utokako?
“Kwema mama” akajibu Sarah halafu akalitoa gazeti lile la mitikisiko na kumpatia mama yake
“mama hebu niambie unafahamu chochote kuhusiana na jambo hili?
Mama yake akalichukua gazeti lile akalitazama na kustuka sana
“Ouh Mungu wangu..!!
“Hii ni kashfa kubwa sana”
“kweli mama ni kashfa kubwa mno.Nina hakika Loniki anahusika na jambo hili” akasema Sarah
“Loniki .!! mama yake akashangaa
“Ndiyo mama .”akasema Sarah
“Hapana Sarah.Loniki hawezi kuhusika na jambo kama hili”
“Mama humjui vizuri Loniki.Nina hakika lazima atakuwa anahusika na jambo hili.Aliapa kwamba atalipiza kisasi kwa Happy na wale wote waliohusika na kifo cha Vero.”
“Hapana Sarah.Sikubaliani nawe kwa hilo .Ni kweli Lonny ameumizwa sana na kifo cha vero lakini sidhani kama atakuwa anahusika kwa namna yoyote na jambo hili.Hii ni tabia ya Happy mwenyewe .Amemdhulumu mwanangu na haya ndiyo yanayomkuta sasa.”
“mama pesa ulizoniomba jana zilikuwa za kazi gani?
“Sarah naomba usitake kuyafahamu mambo yangu binafsi.Kama umeifuata pesa yako nitakurejeshea baadae kama nilivyokwambia” akasema mama yake kwa ukali
“mama sijaja hapa kufuata fedha.Nimekuja kutak…………….” Sarah akastuka baada ya Loniki kutokea ghafla
“Mbona kuna mabishano hapa? Akauliza Loniki huku akiangaliana na Sarah kwa macho makali
“Niambie uhusiki katika jambo hili ?” akasema Sarah huku akimpa Loniki gazeti ambaye alilichukua akalipitia kisha akaangua kicheko kikubwa.
“Haya ndiyo malipo ya udhalimu wake.Yeye na yule mshenzi wake Patrick walimdhulumu Vero uhai wake.Ona sasa alivyoumbuliwa na magazeti..” Akasema Loniki huku akicheka.Sarah akamtazama kwa hasira
“Mbona unanitazama hivyo Sarah? Hufurahi kwa kilichompata mtu aliyemuua mdogo wako?
“Kwa nini nifurahi? Happy si adui yangu na wala sintajenga uadui naye hata mara moja.Hata kama alihusika na kifo cha vero ,lazima niuheshimu utu wake.Kitendo cha kumdhalilisha namna hii hakivumiliki hata kidogo.”
“ Nilijua tu.Huna uchungu wowote kwa kifo cha Vero na ndiyo maana kila mara umekuwa upande wa Patrick na Happy.naomba nikufahamishe kwamba Happy anastahili kudhalilika namna hii.Anastahili kuumia kama tulivyoumia sisi kwa kufiwa na mdogo wetu.Huu ni mwanzo tu na bado ataumia sana.Mengi bado yatamkuta yeye na huyo shetani mwenzake Patrick”
Sarah alishindwa kumvumilia dada yake akamsogelea karibu
“Loniki wewe ni ndugu yangu wa damu lakini ninakuonya kwamba nitafanya uchunguzi wangu na endapo nitagundua kwamba unahusika kwa namna yoyote ile na jambo hili .I swear in heaven and earth I will never forgive you.”
“Utanifanya nini? Akauliza Loniki kwa ukali
“Utafahamu wakati utakapofika.”
“Go to hell sarah.Tena nakuomba uuchunge sana mdomo wako usije ukakuponza.Mimi si mtu wa kunyooshewa kidole kama unavyofanya.Kama ni mapambano niko tayari kupambana nawe na siogopi hata kama wewe ni ndugu yangu.Ninaweza nikakufanyia kitu kibaya sana na usiamini Sarah.”
Ilimlazimu mama yao kuingilia kati na kuwaamua wanae wale ambao walikuwa wanatoleana maneno makali.Sarah hakutaka tena kukaa pale nyumbani akapanda gari na kuondoka zake kwa hasira
* * * *
Savanna hakuwa mpenzi sana wa kusoma magazeti.Hii ilitokana na kuwa na kazi nyingi kiasi cha kukosa muda wa kupitia habari magazetini.Akiwa ofisini kwake akikamilisha baadhi ya kazi zake za kila siku asubuhi kabla ya kuelekea gereza la Uwangwa kuonana na Patrick,mara mmoja wa watumishi wa ofisi yake akaingia akiwa na gazeti mkononi.
“Savanna ,najua hupendi kusoma magazeti lakini naomba uchukue dakika chache upitie gazeti hili” akasema Edson mmoja wa mawakili wanaomtetea Patrick
“Edson toka lini umeniona nikipata muda wa kusoma magazeti? Ninataka kuelekea gerezani kuonanana na Patrick halafu nije niendelee na shughuli zangu nyingine” akasema Savanna
“Naomba usome Savanna.” Akasisitiza Edson na kuliweka gazeti lile mezani.Savanna akavutiwa na kichwa cha habari akalichukua ili alisome na ghafla akalitupa mezani
“Ouh My Gosh !!!... akasema Savanna kwa mstuko
“Bado siamini.Happy anaweza akafanya uchafu wa namna hii kweli? Happy huyu ninayemfahamu mimi? No..!! thats not true..!!!” akasema Savanna
“Ni kweli Savanna.Ukiacha picha hizi kuna video yake pia ambayo imesambaa mitandaoni.” Akasema Edson huku akiisogelea kompyuta ya Savanna akaifungua video ile ya Happy .Savanna akaitazama video ile na kujikuta mdomo wazi.
“Ouh gosh !! ..Ni vigumu kuamini.Happy kweli anaweza akafanya mambo ya aibu namna hii? Akasema Savanna na kujikuta akiishiwa nguvu miguuni,akakaa kitini.
“Usishangae Savanna.Siku hizi umezuka mtindo wa mabinti hasa hawa maarufu kujirekodi wakifanya ngono au kupiga picha za utupu kisha huzihifadhi kwa ajili ya kumbu kumbu zao wenyewe lakini ikitokea zikashindwa kuhifadhiwa vizuri na zikaingia katika mikono ya watu wabaya ,huziuza kwa waandishi wa habari kwa fedha nyingi ambao hutengeneza mamilioni ya fedha katika magazeti yao kwa kuichapisha habari hiyo” akasema Edson.Savanna akainama akafikiri halafu akachukua simu yake na kumpigia Margreth.
“Hallow “ akasema Margreth baada ya kupokea simu.Savanna akastushwa kidogo na sauti ya Margreth
“Margreth,sauti yako inaonyesha kama unalia.Unaumwa? akauliza Savanna .Margreth akashindwa kukizuia kilio chake akalia kwa nguvu
“Margreth nini kimetokea? Please tell me”
“Its…..it’s….” Margregth akashindwa kuongea akaangua kilio tena
‘Margreth nini kimetokea? Tafadhali naomba unieleze”
“Its Happy….!!
“Happy kafanya nini?
“Amekunywa sumu” Margreth akajibu halafu kikapita kimya cha sekunde kadhaa.Savanna akabaki mdomo wazi akashindwa aseme nini.Akameza fundo la mate na kusema
“Margreth tafadhali naomba uniambie ukweli”
“Ni kweli Savanna.Happy amekunywa sumu “
“So how’s She? Where ae you now?
“Niko hapa Brahmaputra hospital.She’s in critical condition fighting for her life “
“Ouh gosh ! ,nakuja sasa hivi” akasema Savanna na kukata simu kisha akachukua mkoba wake na kutoka kwa kasi hadi katika gari lake na kuondoka kuelekea hospitali.
“haya mambo mbona yanazidi kuchanganya? Jana nimepigiwa simu Happy haonekani lakini leo hii amekunywa sumu.Kitu gani kinaendelea hapa? Akawaza Savanna akiwa katika mwendo mkali kueleka hospitaliCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Masikini Patrick,sipati picha atakuwa katika hali gani mara atakapozipata taarifa hizi.Sifahamu atachukua maamuzi gani lakini nafahamu lazima ataumia sana.” Akawaza Savanna
Baada ya kuwasili Brahmaputra hospital Savanna akakutana na familia ya Happy
“Shikamoo baba”
“Marahaba Savanna hujambo?
“Sijambo baba. Poleni sana” akasema Savanna halafu akamuomba mzee Kibaho wakaongee pembeni
“Nini kimetokea ? Happy anaendeleaje? Akauliza Savanna.Mzee Kibaho akakohoa kidogo halafu akasema
“Unakumbuka nilikupigia simu jana usiku nikitaka kufahamu kama unaweza ukafahamu lolote kuhusu mahala aliko Happy kwani hadi wakati ule ninakupigia hakuwa amerejea na hata simu yake haikuwa inapatikana kitu ambacho si kawaida yake.” Akasema mzee Kibaho
“Nakumbuka baba.Happy nilikutana naye jana asubuhi gerezani akiwa na Patrick.Nilipoingia nikiwa nimeongozana na familia ya Patrick yeye akaondoka na hatukupata muda wa kuongea.Nini kilitokea? Alikuwa wapi? Akauliza Savanna
“Mida ya kama saa nane hivi za usiku nilisikia muungurumo wa gari nje ya nyuma.Nilipotoka nje ya nyumba nilikuta gari la Happy na yeye akiwa ndani yake lakini akiwa hoi hajitambui.Hatukujua nini kilimpata kwa sababu alionekana ni kama mtu aliyelewa.Tulimuita dokta wa familia akaja mara moja na kumpatia huduma na alipopata nafuu akatuomba tumuache akapumzike.Hakutueleza alikuwa wapi na wala nini kilimpata.Asubuhi ya leo nilisikia mtu akilia sebuleni nikaenda kutazama nini kimetokea nikamkuta mke wangu akiwa amezirai.Wakati tukimpatia huduma ili azinduke akatokea Happy na kuliokota gazeti lililokuwa limeanguka chini.Ghafla akalitupa na kuelekea chumbani kwake.Nililitazama gazeti lile nikastuka sana.Nilimfuata Happy chumbani kwake lakini mlango ulikuwa umefungwa,ikanilazimu kuchukua ufunguo wa akiba nikaufungua mlango na kumkuta Happy akiwa hana fahamu na povu jingi likimtoka mdomoni.Alikunywa sumu ya kuulia panya.Nimemkimbiza hapa hospitali na toka nilipomfikisha hapa madaktari wanaendelea kumshughulikia.Shughuli zote hapa hospitali zimesimama kwa muda madaktari wote wanaendelea kumuhudumia Happy.Vile vile Happy aliacha ujumbe huu” mzee Kibaho akampatia Savanna ujumbe ule aliouacha Happy.Savanna akaupitia ujumbe ule na kisha akatoa kitambaa mfukoni na kuyafuta machozi
“Nilijua tu ,Happy hawezi kufanya jambo kama lile kwa hiari yake mwenyewe.Nilijua tu lazima jambo hili lina mkono wa mtu.Ni nani huyo ambaye anaweza kuwa amefanya unyama wa namna hii? Akasema Savanna
“Hakuna ajuaye ni nani muhusika wa jambo hili.Anayefahamu ni Happy pekee.Tuombe Mungu apone na atufahamishe ni nani hawa waliomfanyia kitendo hiki.Lazima wafikishwe katika mkono wa sheria“ akasema mzee Kibaho
“Ni kweli baba watu hawa waliohusika na udhalilishaji huu lazima walipe uovu wao.lazima wafikishwe katika vyombo vya sheria.” Akasema Savanna halafu kikapita kimya kifupi
“Savanna wewe ni wakili”
“Ndiyo baba”
“Naomba ushauri wako wa kisheria kuhusu kitendo hiki cha Happy.Hiki kitendo alichokifanya Happy cha kutaka kujiua ni kosa kisheria?
“Ni kweli baba,hiki ni kitendo cha kijinai.Kwa mujibu wa sheria ya kanuni za adhabu sura ya ishirini na mbili kifungu cha 217 kinachosema mtu yeyote anayejaribu kujiua ana hatia ya kosa.Iwapo suala hili litafuatiliwa na vyombo husika Happy anaweza kukabiliwa na adhabu
“Ouh My Gosh ..!!! what am I going to do ? akasema kwa masikitiko mzee Kibaho.Savanna akamtazama mzee Yule kisha akasema
“Baba kuna jambo ambalo tunatakiwa kulifanya kwa sasa”
“Jambo gani hilo savan?
“Kwanza nataka kufahamu kama suala hili limekwisha ripotiwa katika vyombo vya usalama.”
“Hapana Savanna.Suala hili halijaripotiwa sehemu yoyote ile na tunaofahamu ni sisi familia yake pamoja na ndugu wachache pamoja na majirani”
“Vizuri sana.Tunachotakiwa kufanya kwa sasa ni kulifanya suala hili kuwa siri kubwa na kuhakikisha hakuna mwandishi wa habari anayezipata taarifa hizi.Ongea na uongozi wa hospitali hii ili hata kama ikitokea watahojiwa na vyombo vya habari au usalama wasiweke wazi kwamba Happy alijaribu kujiua kwa kunywa sumu.Baada ya hapo itabidi tufanye jambo la haraka sana kwa Happy”
“Jambo gani hilo? Akauliza mzee KIbaho
“Najua hautalipenda lakini hakuna jinsi ninabidi lifanyike tu”
“Niambie Savanna.Niko tayari kufanya lolote hivi sasa kwa ajili ya Happy” akasema mzee KIbaho.Savanna akamtazama kwa sekunde kadhaa halafu akasema
“I wapo Mungu atamsaidia akapona We have to take her away from here as quick as possible”
Mzee Kibaho akastuka kwa maneno yale ya Savanna
“Baba najua umestuka sana kwa maneno haya lakini naomba uniamini haya nikwambiayo kwamba endapo Mungu atamjalia Happy uzima,tunatakiwa kumuondoa Happy hapa nchini haraka sana”
“Kwa nini unashauri hivyo ? Akauliza mzee Kibaho
“Jambo hili lililotokea si jambo dogo kama unavyoliona na hadi hivi sasa tayari limemuathiri Happy kwa kiasi kikubwa.Taswira yake katika jamii imeharibiwa na habari hii ya leo.Kwa maana hiyo basi anatakiwa kupata sehemu tulivu yenye uangalizi makini ili aweze kupatiwa msaada wa kisaikolojia na akili yake iweze kutulia.Kuendelea kumweka hapa ni kumuongezea maumivu na kutaendelea kuhatarisha usalama wake.Vile vile kumuondoa hapa kutasaidia kumuepushia mashtaka ya kijinai.Najua hili si suala jepesi lakini inatubidi tushirikiane sote kwa faida ya Happy” akasema Savanna.Mzee Kibaho akavuta pumzi ndefu .Alionekana kama amechanganyikiwa
“I don’t know what I’m going to do” akaongea peke yake.Baada ya dakika mbili za tafakari akamgeukia Savanna
“Savanna mawazo yako naona yana msingi sana.Nina mdogo wangu anaishi Mtwara.Nadhani itakuwa vyema kama nitampeleka kule akakae kwa muda”
“Hapana baba.Mtwara bado ni Tanzania.Happy anatakiwa aende mahala ambako hakuna mtu anayemfahamu mahala ambako atapata msaada wa kisaikolojia na kumsaidia kurejea katika hali yake ya kawaida.Hapa nchini Happy ana jina kubwa na anafahamika kila kona”
“Savanna suala hili linahitaji muda wa kutosha kulifanyia maandalizi.Inabidi nikae na familia yangu baada ya kujua maendeleo ya Happy na kwa pamoja tujadili suala hili ndipo tufikie maamuzi “ akasema mzee Kibaho huku akionekana ni mwenye mawazo mengi sana
“Mzee wangu nakubaliana na wazo la kukaa na kufanya maamuzi kama familia .Pamoja na hilo naomba na mimi nitoe mchango wangu.Iwapo mwenyezi Mungu atamjalia Happy uzima na iwapo mtakubaliana na mawazo yangu basi ninapendekeza Happy asafirishwe kwenda Kigali Rwanda.Mimi nitagharamia gharama zote za safari.Nitakodisha ndege binafsi hadi Kigali.Pale Kigali nina rafiki yangu aitwaye Christine umuhiza ambaye ndiye atakayemuhudumia Happy kwa kipindi chote atakachokuwa pale.Vile vile ninafahamiana na mmiliki wa hoteli moja iitwayo Reonald Hotel.Ni hoteli mpya na kubwa pale Kigali yenye hadhi ya nyota tano.Nitafanya mpango ili Happy aweze kukaa hotelini hapo kwa muda wote atakaouhitaji akiwa katika chumba chenye hadhi ya rais.Christine atamtafutia daktari ambaye atamsaidia kumtibu na vile vile tutamtafutia daktari wa masuala ya kisaikolojia “ akasema Savanna.Mzee Kibaho aliyekuwa anamsikiliza kwa makini akakohoa kidogo na kusema
“Savanna mimi binafsi nimeumizwa sana na jambo hili na kwa mantiki hiyo basi niko tayari kufanya jambo lolote lile ambalo litakuwa na msaada kwa Happy.Sipingani hata kidogo na wazo lako la kumpeleka Happy nje ya nchi.Ninachotaka kufahamu ni iwapo Happy ataondoka hapa nchini kwa ajili ya kumsaidia kwanza kumuepusha na aibu hii na pili kumuepusha na mkono wa sheria kwa kosa la kujaribu kujiua, nini itakuwa hatima ya watu waliomtenda hivi? Sitakuwa na amani hadi nihakikishe kwamba watu waliomfanyia mwanangu kitendo hiki cha kinyama wamekamatwa ,wamefikishwa katika mkono wa sheria na wameadhibiwa kutokana na kitendo walichokifanya.Lakini ninajiuliza maswali mengi hilo litawezekana vipi wakati Happy akiwa nje ya nchi? Nataka jina la mwanangu lisafishwe .Nataka umma wa watanzania wafahamu nini kilitokea na kwamba mwanangu hawezi kufanya kitendo kama kile kwa ridhaa yake.” Akasema mzee Kibaho
“Baba hayo yote unayoyasema ni ya msingi sana lakini tukumbuke kwamba ni Happy pekee ambaye anawafahamu watu hao na ambaye anaweza akatusaidia kuwatambua watu hao na anaweza akafanya hivyo pale ambapo akili yake itakuwa imetulia .Mimi binafsi nakuahidi ushirikiano wangu wa dhati katika suala hili na mara tu watakapogundulika watu hawa nakuahidi kwamba kesi hiyo nitaisimamia mimi mwenyewe na kuhakikisha kwamba wanapata adhabu kali sana”
Kabla mzee Kibaho hajasema chochote,akatokea Margreth na kumtaarifu baba yake kwamba anahitajika na daktari.Kwa haraka wote watatu wakaongozana kuelekea katika ofisi ya daktari
“karibuni sana” akasema daktari mkuu wa hospitali hii ambaye ana asili ya India lakini anakifahamu vizuri sana Kiswahili
“Poleni sana kwa matatizo” akasema daktari.Wote watatu nyoyo zao zilikuwa zinawadunda wakisubiri taarifa ya daktari
“Jamani nimewaiteni hapa ili kuwapeni taarifa kuhusiana na maendeleo ya mgonjwa wenu.Kwa ujumla ni kwamba Happy alikuwa amekunywa dawa ya kuulia wadudu ambayo ni sumu katika mwili wa binadamu.Ninakushukuru sana mzee wangu kwa jitihada zako za kumfikisha mapema hapa hospitaloi kabla sumu ile haijasababisha madhara makubwa mwilini.Tulimpokea Happy akiwa katika hali mbaya na tumefanya kila jitihada ili kumuondoa katika hali ya hatari ya kupoteza maisha.Tunapaswa kumshukuru sana Mungu kwani tumefanikiwa katika hilo.Kwetu sisi tunaona ni kama muujiza kutokana na hali aliyokuwa nayo Happy.Tumefanikiwa kuiondoa sumu iliyoko mwilini mwake kwa kutumia mtambo wetu maalum ambao ni mpya kabisa wa kuondoa sumu ya aina yoyote mwilini.Kwa sasa ninaweza kutamka kwamba Happy hayuko tena katika ile hatari ya kupoteza maisha na endapo litatokea jambo kama hilo basi itakuwa ni kwa mapenzi ya Mungu lakini napenda kuwahakikishia kwamba tumemuondoa katika hatari hiyo.” Akasema daktari na wote watatu wakashusha pumzi .Mzee Kibaho akajifuta jasho lililokuwa linamtiririka kwa wingi
“Zoezi linaloendelea kwa sasa ni kuipitisha damu yake katika mtambo maalum wa kuchuja sumu ili kuweza kujiridhisha zaidi kwamba hakuna kiasi chochote cha sumu kitakachobaki mwilini mwake.Kwa hiyo nawasihi ndugu zangu,ondoeni wasi wasi mliokuwa nao.Happy yuko salama na anaendelea vizuri.Zoezi hili litakapomalizika tutamuondoa katika chumba cha wagonjwa mahututi na kumpeleka katika sehemu ya uangalizi maalum ili kuangalia maendeleo yake.”
“Ouh Thanx God” akasema mzee Kibaho huku akiinua mikono yake juu kumshukuru Mungu
“Daktari zoezi hilo la uchujaji wa sumu litachukua muda gani? Akauliza Savanna
“Ni muda wa masaa manne”
“Mzee wangu nini hasa kilichopeleka binti mdogo kama huyu kutaka kukatisha uhai wake? Nini kimemsibu ili tuone namna ya kumpatia msaada wa kisaikolojia na asiweze kurudia tena kufanya kitendo cha hatari kama hiki? akauliza daktari.Mzee Kibaho akakohoa kidogo na kusema
“Happy ni binti yangu wa kwanza.Hivi karibuni alifanikiwa kutwaa taji la Miss Tanzania.Baada ya kulinyakua taji hilo ndipo matatizo yalipoanza.Yote haya yamesababishwa na mgogoro wa kimapenzi uliopekeka msichana aliyekuwa akizozana naye kufariki dunia.Leo asubuhi katika gazeti moja la udaku kumechanpishwa picha za Happy za faragha.Ni picha zenye kuumiza sana na zote hizi ni njama za wabaya wake za kutaka kumchafua.Jambo hilo ndilo lililopelekea aamue kujaribu kukatisha uhai wake kwa kunywa sumu.” Akasema mzee Kibaho
“Poleni sana.Hii inaonyesha ni jinsi gani dunia ilivyobadilika hivi sasa.watu wamekosa huruma na wako tayari kufanya jambo lolote lile kwa manufaa yao bila kupima athari zinazoweza kujitokeza.Poleni sana ,lakini kitu ninachoweza kuwaambia ni kwamba Happy anahitaji msaada wa kisaikolojia.Hapa tunao madaktari wazuri sana wa masuala haya ya akili.Tunacho kitengo hicho hapa cha kuasadia watu wenye matatizo kama ya Happy.Ninawashauri kwamba baadaya hali yake kuwa nzuri basi tuendelee kumpatia msaada wa kisaikolojia hapa hapa hospitalini kwetu” akasema daktari
“Nakubaliana nawe daktari kwani inaonyesha wazi kwamba binti yangu ameathirika kisaikolojia na anahitaji msaada .Lakini kuna jambo ninataka kukuomba.Kwa mujibu wa sheria ,kitendo hiki alichokifanya Happy ni kosa la kijinai kwa hiyo kuna uwezekano endapo vyombo vya kisheria vikazipata taarifa hizi vikamfungulia mashitaka,kwa hiyo tunakuomba daktari ,jambo hili libaki kuwa siri na asifahamu mtu mwingine yeyote yule awe ni mwandishi wa habari au afisa wa polisi.Unaweza ukaandika ugonjwa mwingine wowote lakini si sumu.Jambo la pili ambalo tumekusudia kulifanya kwa haraka ni kumuhamishi Happy nje ya nchi haraka iwezekanavyo.mahala ambako hakuna mtu yeyote anayemfahamu.Nadhani hii itakuwa ni njia nzuri sana ya kumsaidia kumuondoa katika mazingira haya na wakati huo huo tukiendelea kumpatia msaada wa kisaikolojia.” Akasema mzee Kibaho
“Kwanza kabisa kuhusiana na kutoa taarifa kuwa vyombo vya habari na vile vya usalama,msiwe na hofu.Nitawasaidia katika hilo.Pili kuhusiana na suala la kumpeleka Happy nje ya nchi ni suala zuri sana lakini nina wasi wasi kidogo.Happy anahitaji bado kuwa katika uangalizi wa madaktari.Kama ni kumuondoa hapa nchini basi itawabidi msubiri kidogo hadi hapo hali yake itakapoboreka kabisa.”
“Inaweza kuchukua muda gani daktari? Akauliza Savanna
“Inaweza kuchukua zaidi ya wiki moja”
“Daktari tunahitaji kumuondoa Happy nchini leo hii.”
“Kwa leo haitawezekana kumsafirisha Happy” akasema Daktari
“Daktari naomba ufanye kila linalowezekana ili tuweze kumuondoa Happy hapa nchini siku ya leo” akaendelea kusisitiza Savanna
Daktari akafikiri kidogo na kusema
“Kama mkihitaji hivyo basi ni lazima pawepo makubaliano maalum”
“makubaliano gani hayo? Akauliza Savanna
“Baada ya zoezi la kuchuja sumu kukamilika mgonjwa anatakiwa apumzike kabla ya zoezi lingine lolote kufanyika.Endapo mtahitaji kumsafirisha Happy kwa siku ya leo,itawalazimu kumsafirisha na mmoja wa madaktari wetu kitu ambacho kitawaongezea gharama zaidi kwa hiyo nawashauri mngesubiri hadi hapo Happy atakapokuwa amepata nafuu ndipo mumsafirishe”
“Daktari hilo ulilolisema si tatizo kwetu hata kidogo kwani tunatumia ndege ya kukodi.Tunaelekea jijini Kigali Rwanda.Usijali kuhusu gharama.Tutakulipa pesa zote zitakazotakiwa ikiwa ni pamoja na kumuhudumia daktari huyo hadi hapo Happy atakapopata nafuu.” Akasema Savanna
“Kama mko tayari kwa hilo mimi sina shida yoyote.Kwa sasa naombeni mnipe nafasi nikakutane na jopo la madkatari wangu ili kwa pamoja tuweze kushauriana namna bora ya kuweza kulifanikisha jambo hili” akasema daktari.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Usijali daktari.Sisi pia ngoja tukajiandae kwa safari.Naomba hesabu ya gharama zote unitumie kwa kupitia namba hizi hapa” akasema Savanna huku akimpatia daktari kadi yake yenye namba za simu halafu wakatoka mle ofisini.
“Baba mpango huu wa kumpeleka Happy Kigali umetoka wapi? Mbona hakuna aliyekuwa anafahamu kama kuna mpango kama huu? Akauliza Margreth baada ya kutoka ofisini kwa daktari
“Margreth samahani kwa kulisikia jambo hili kabla ya kutaarifiwa.Ni kwamba Savanna alikuja na wazo hili la kutaka kumuhamisha Happy na kumpeleka nje ya nchi ili kumuweka mbali na mazingira haya.Endapo ataendelea kukaa hapa wakati tayari jina lake limekwisha chafuka ataendelea kuumia zaidi.Ni bora ikiwa atakwenda kukaa mbali na hapa,mhala ambako hafahamiki kabisa.Hii itamsaidia sana kumsahaulisha kilichotokea”
“Ni mpango mzuri baba lakini maandalizi yanakwendaje manake nimemsikia Savanna akisema kamba Happy atapelekwa Kigali.Imekuwa ghafla sana na nina wasi wasi kama kuna maandalizi yoyote yaliyofanyika”
“Margreth,usihofu chochote kuhusiana na jambo hilo.Pale Kigali kuna hoteli moja kubwa ya nyota tano ambayo mmiliki wake tunafahamiana vyema na ndipo Happy atakapofikia na kukaa yeye na watu atakaoambatana nao hadi hapo hali yake itakapokuwa nzuri.Kuhusu usafiri nitagharamia mimi ,nitakodisha ndege hadi Kigali “
* * * *
Saa tano na dakika ishirini za usiku familia ya Happy ikaruhusiwa kuingia katika chumba alichokuwa amelazwa Happy.Tayari alikwisha amka toka saa mbili za usiku lakini madaktari hawakuruhusu aonane na mtu yeyote hadi hapo atakapokuwa amerejewa na fahamu zake kamili
Mara tu alipoiona familia yake ikiingia mle chumbani wakiongozwa na baba yake mzee Kibaho Happy alishindwa kujizuia akaanza kulia.
“Ouh Happy mwanangu” akasema mama yake huku akiinama na kumkumbatia wote wawili wakilia.
“Mungu ahsante kwa kumponya mwanangu” akasema mama yake Happy. Happy akasalimiana na baba yake mzee Kibaho na halafu mdogo wake Margreth na ghafla akastuka baada ya kugonganisha macho na Savanna
“Pole sana Happy” akasema Savanna.Happy akashindwa ajibu nini,donge kubwa likamkaba kooni.Savanna alilitambua hilo akatoka nje ya kile chumba.
“what is she doing here? Baba kwa nini umemleta Savanna hapa? Akauliza Happy
“Usijali Happy,Savanna tuko naye kutwa nzima ya leo tukishughulikia suala hili.Amekuwa ni msaada mkubwa kwetu katika wakati huu mgumu tulionao.Ametupa ushirikiano mkubwa sana.” Akasema mzee Kibaho
“Dady I don’t want to see her here.That woman is a devil.She’s a monster” akasema Happy kwa hasira juku akiendelea kulia.
“Its ok Happy It’s ok.Nyamaza usiendelee kulia mwanangu” akasema mzee Kibaho huku akimfuta Happy machozi
“Dady why you saved me? Akauliza Happy
“Happy naomba usahau kilichotokea.Kitu pekee kwa sasa ni kumshukuru Mungu kwa kukuponya .Sisi kama familia ni wajibu wetu kuhakikisha kwamba unakuwa salama.Tunakupenda sana na hakuna mtu yeyote anayeweza akakubali upoteze maisha” akasema mzee Kibaho halafu.Happy akainua mkono akafuta machozi.
“Baba ungeniacha nife.Nimechoka na maisha haya.I’m real tired with this kind of life.Nili……………….” kabla hajaendelea baba yake akamuwekea kidole mdomoni
“Shhhhhhhhh..!!!!..Happy usiseme hivyo.Sahau kilichotokea .Hii ni mitihani ya maisha na ambayo hatuna budi kuishinda.Happy tunakupenda sana zaidi ya unavyoweza kufikiri”
“Najua kwamba mnanipenda sana lakini kwa aibu hii niliyowapa najiona sistahili hata kuitwa mwanenu.Nime………………” Happy akashindwa kuendelea akaangua kilio
“Happy usilie mwanangu.Tunakupenda sana na siku zote tutakuwa pamoja nawe katika kila jambo.Tuko pamoja katika suala hili na ndiyo maana tumeamua kukuhamisha hapa nchini usiku huu na kukupeleka sehemu ambayo utaweza kupumzika na kusahau kilichotokea,sehemu ambayo hakuna mtu yeyote anayekufahamu”
“Mnataka kunipeleka wapi baba?
“Tumeamua kwanza uende ukapumzike Kigali Rwanda wakati tukiangalia sehemu nyingine ambayo itakufaa zaidi.Tayari kila kitu kimekwisha andaliwa kwa msaada mkubwa wa Savanna ambaye ndiye aliyefanikisha mipango yote ya safari ikiwa ni pamoja na kuandaa hoteli ambayo utafikia kule Kigali na hata kuwalipa madkatari wote watakaokuwa wakikuhudumia katika kipindi hiki chote utakachokuwa kIgali.Tumefikia uamuzi huu wa kukuondoa hapa nchini ili kukusaida usiweze kuumia zaidi kutokana na maneno ya watu na vyombo vya habari.Iwapo utaendelea kukaa hapa utakuwa ukiumia zaidi kila siku” akasema mzee Kibaho
“Please dady take me out of here right now” akasema Happy huku akitoa machozi.
“Usijali Happy.Kila kitu kimekwisha andaliwa na tuchosubiri ni taratibu za hapa hospitali .Lakini kabla hatujaondoka hapa kuna jambo ninataka kukuuliza” akasema mzee Kibaho halafu akamtazama mwanae na kusema
“Unawafahamu au kuwa na hisia ni nani aliyekufanyia hivi?
Happy akafumba macho kwa sekunde kadhaa halafu akasema
“Its not important anymore dady.Just take me out of here”
“Happy waliofanya unyama huu wanatakiwa wafikishwe katika vyombo vya sheria.Huu ni ukatili mkubwa sana ambao hauvumiliki.Tafadhali tusaidie tuweze kuwafahamu watu hao.Mimi na Savanna tutashirikiana na kuhakikisha kwamba wale wote waliotenda hivi wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria”
“Dady not now.Please take out of here” Happy akaendelea kuushikilia msimamo wake.Mzee Kibaho akatoka ndani ya kile chumba akakutana na Savanna.
“Savanna naomba usimjali Happy.Twende tukashughulikie masuala ya hapa hospitali ili tuweze kuruhusiwa kuondoka.” Akasema mzee Kibaho
“Kitu gani kinaendelea baina yako na Happy? Akauliza mzee Kibaho wakati wakishuka ngazi
“Its something stupid.Tulipishana maneno.Kuna mtu ambaye alimpelekea Happy maneno ambayo yalimfanya akasirike na kuja juu na mimi nikashindwa kudhibiti hasira zangu na tukajikuta tukitamkiana maneno makali.” Akasema Savanna
“Ninaweza kufahamu ni jambo gani hilo lililosababisha wewe na Happy mtupiane maneno? Akauliza mzee Kibaho
“Si jambo la msingi sana na sioni sababu ya kukwambia.Ni mambo ya wanawake tu na tutayamaliza” akasema savanna
Hatimaye ruhusa ya Happy kuondoka ikatolewa na akapatiwa daktari mmoja ambaye angeongozana naye kuelekea Kigali Rwanda ambaye angeendelea kumuhudumia hadi hapo hali yake itakapokuwa nzuri.Wote waliingia katika gari moja na safari ya kuelekea uwanja wa ndege ikaanza.Walikuwa makini sana kuhakikisha kwamba hawafuatiliwi na mwandishi yeyote wa habari kwani suala hili lilikuwa ni siri kubwa ya familia.Safari ilikuwa ya kimya kimya na hakuna aliyekuwa anaongea ndani ya gari.Waliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere na ,mizigo ya Happy ikashushwa garini.Kilikuwa ni kipindi kigumu sana hasa kwa mama yake Happy.Alimkumbatia mwanae huku wote machozi yakiwatoka.
“Mom I’m going to miss you” akasema Happy
“Happy sina cha kusema zaidi ya kukuombea kwa Mungu akutangulie huko uendako.Uwe salama kila siku “ akasema mama yake Happy huku machozi yakimtoka
“Nitakuwa salama mama” akasema Happy halafu akamuacha mama yake na kumfuata Margreth.
“Be safe there and get well soon” akasema Margreth
Happy hakusema kitu ,macho yake yalikuwa yamefunikwa na machozi
“Its time to go Happy” akasema mzee Kibaho kwa sauti ndogo
“Baba Happy” akaita mama yake Happy.Mzee Kibaho akageuka
“Tafadhali hakikisha Happy anakuwa salama”
Mzee Kibaho hakujibu kitu zaidi ya kutingisha kichwa ishara ya kukubaliana na kile alichokisema mke wake halafu akamshika mkono Happy na kumuomgoza kuelekea ndani ya uwanja kwa ajili ya kukamilisha taratibu za hapo uwanjani kabla ya kuruhusiwa kuondoka
Waliwaisli salama katika uwanja a ndege wa kimataifa wa Kigali.Christine Umuhiza alikuwepo uwanjani kuwapokea wageni wake na kisha wakaelekea moja kwa moja Reonaldo hotel,moja ya hoteli mpya na kubwa jijini Kigali
Tayari kila kitu kilikwisha andaliwa na Happy akapewa chumba chenye hadhi ya rais yaani presidential suit kama alivyokuwa ameahidi Savanna.Mzee Kibaho ambaye ambaye naye alikuwa ameambatana na mwanae naye alipewa chumba kizuri sana kwa ajili ya kupumzika kwa siku zote atakazokaa hapo Kigali,daktari aliyeambatana nao pia alipewa chumba cha hadhi ya juu kabisa.
“Happy,nilipendekeza ufikie katika hoteli hii kwa sababu ni nzuri na huduma zake ni nzuri na za kimataifa.Jitahidi kupumzika kwa kadiri utakavyoweza na kwa muda wowote utakaohitaji.Mmiliki wa hoteli hii ni rafiki yangu sana na anafahamu uwepo wako hapa na gharama zote ni juu yangu .Endapo kutakuwa na tatizo lolote wasiliana nami moja kwa moja.Christine atakusaidia kumpata daktari bingwa wa magonjwa ya akili ambaye atakuwa akifika hapa kila siku na atakusaidia kisaikolojia ili uweze kurejea katika hali yako ya kawaida.”Akasema Savanna halafu akamtazama Happy aliyekuwa amejilaza kitandani.
“Happy najua tulipisha kauli na kutoleana maneno makali.Tafadhali naomba tusahau yale yote yaliyopita na tuangalie mambo ya mbele.Binafsi nimeumizwa mno na jambo hili kama walivyoumia wale wote wanaokupenda na ndiyo maana nimejitolea kufanya kila lililo ndani ya uwezo wangu ili kuhakikisha unarudi katika hali yako ya kawaida na kwa pamoja tuhakikishe wale wote waliohusika na kitendo hiki wanatafutwa kwa gharama zozote na kufikishwa mbele ya sheria” akasema Savanna.Bado Happy alikuwa anamuangalia kwa macho makali yaliyojaa machozi
“Happy mimi naenda kupumzika nyumbani kwa Christine.Nitakuja kukuaga asubuhi kabla ya kurejea Dar es salaam” akasema Savanna baada ya kugundua kwamba Happy hakuwa tayari kuongea naye kwa usiku ule .Akaufungua mlango na kutoka mle chumbani
* * * *
Kumekucha Kigali,kijua tayari kimechomoza na shughuli mbali mbali za uzalishaji mali zilikuwa zinaendelea kama ilivyo ada.Saa mbili za asubuhi Chistine na Savanna wakawasili hotelini.Wa kwanza kuonana naye alikuwa ni mzee Kibaho ambaye alikwisha amka na kufanya mazoezi ya viungo katika ukumbi mkubwa wa mazoezi uliopo katika hoteli ile.
“Happy ameamkaje? Akauliza Savanna
“Nimeongea naye kwa simu asubuhi ya leo ,amesema anaendelea vizuri ,lakini kwa mujibu wa daktari ni kwamba itamchukua siku kadhaa kurejea katika hali yake ya kawaida” akajibu mzee Kibaho
“usijali baba.Nina hakika baada ya muda hali yake itakuwa nzuri na maisha yataendelea kama kawaida.” Akasema Savanna halafu akaenda kuonana na daktari aliyemuhakikishia kwamba hali ya Happy ilikuwa inaendelea vizuri.Baada ya hapo akaelekea katika chumba cha Happy akabonyeza kengele ya mlangoni.Dakika kama mbili zilipita bila majibu yoyote .Akaanza kuingiwa na wasi wasi.Akabonyeza tena kengele na baada ya kama dakika mbili tena akasikia kitasa cha mlango kikinyongwa na mlango ukafunguliwa.Akagonganisha macho na Happy ambaye bado yalikuwa yamemvimba kutokana na kulia sana.Happy hakusema kitu akarejea kitandani kwake akaketi.Savanna naye akaingia mle chumbai na kusimama pembeni ya meza kubwa ya chakula.
“Happy unaendeleaje? Akauliza Savanna lakini Happy hakumjibu kitu.
“Happy nafahamu hukupenda kuniona hapa.Nafahamu ndani ya moyo wako mimi ni mmoja wa wale watu unaowachukia sana hivi sasa.Unapaswa kunichukia hasa baada ya maneno yale makali tuliyotoleana.Sote tulitoleana maneno makali kutokana na hasira tulizokuwa nazo.Sina mengi sana ya kusema lakini naomba utambue kwamba nimeguswa sana na jambo hili na kama rafiki na mwanamke mwenzako,niko pamoja nawe katika wakati huu mgumu” akasema Savanna halafu akanyamza kidogo akamtazama Happy na kuendelea
“Happy nimekuja kukuaga.Muda mfupi ujao ninarejea Dare s salaam.Ningependa kuwa nawe hapa kwa muda mrefu zaidi lakini bado ninakabiliwa na majukumu mengine mengi.Mzee Kibaho na daktari ,wataendelea kufuatilia hali yako kwa karibu na watatufahamisha kila hatua na endapo kutakuwa na tatizo lolote basi tutasaidiana namna ya kulitatua.Kitu pekee ambacho nitaka kukushauri ni kwamba ,japokuwa ni vigumu sana lakini naomba ujaribu kusahau kilichotokea na uruhusu maisha yaendelee.Happy nakufahamu wewe ni mwanamke jasiri sana naomba tafadhali usikubali kushindwa katika hili.Usimpe nafasi mtu,au kikundi cha watu kukufanya ukate tamaa na ushindwe kutimiza ndoto zako.” Savanna akanyamaza na kumtazama Happy ambaye macho yake yalikuwa yemejaa machozi
“Hapa hotelini utaishi kwa muda wowote utakaoutaka,utapatiwa kitu chochote utakachohitaji.Endapo kutakuwa na tatizo lolote naomba unipigie simu yangu moja kwa moja.Mwisho naomba ufahamu kwamba kuna maelfu ya watu wanaokupenda na mashabiki wako wanaokusubiri upone na siku moja urejee tena Tanzania.Get well soon Happy “ akasema Savanna huku naye akilengwa na machozi halafu akageuka na kuanza kupiga hatua kuondokaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Savanna subiri kidogo” akasema Happy.Savanna ambaye alikuwa ameukaribia mlango akasimama na kugeuka.Happy akainuka pale kitandani akamfuata
“Savanna naomba unisamehe kwa yale yote niliyokutenda.Ni kweli siku ile tulipopishana maneno nilikuwa na hasira sana lakini naomba unisamehe.Kabla hujaondoka,naomba toka ndani ya moyo wangu niseme kwamba ahsante sana kwa yote.Wema huu ulionitendea ni mkubwa na sina hakika kama nitaweza kuurejesha.Pamoja na shukrani zangu kuna jambo moja nataka kukuweka wazi”akasema Happy akamtazama Savanna kwa makini halafu akasema
“Savanna sintarejea tena Tanzania.I’ve left Tanzania for good.Its my country but I hate Tanzania so much.Kwa sababu hiyo basi naomba nimkabidhi Patrick katika mikono yako.Ninamuacha mikononi mwako kwa sababu ninaamini unampenda na utahakikisha anakuwa mwenye furaha siku zote katika maisha yake.Please take good care of him .He’s all yours now.Kokote nitakakokuwa nitajua kwamba Patrick ana furaha kwa sababu yuko katika mikono salama.” Akasema Happy huku machozi yakimtoka
“Tafadhali Happy usiseme maneno hayo” akasema Savanna kwa mshangao
“Savanna naomba ufanye kama nilivyokuomba.Huu ni uamuzi wangu na nimeamua kuchukua maamuzi haya magumu kutokana na hali halisi ilivyo na ukweli ulio wazi kwamba mimi na Patrick hatutaweza kuwa pamoja japokuwa tunapendana kwa mioyo yetu yote.Pamoja na hayo naomba unihakikishie jambo moja.”
“Jambo gani Happy?
“Naomba unihakikishie kwamba Patrick atashinda kesi na atakuwa huru na kwamba hautamwambia mahala niliko.Can you promise me that?
Savanna akamwangalia Happy usoni na kusema
“Patrick will be free.I give you my word” akasema Savanna
“Thank you Savanna.Thank you so much.You can go now” akasema Happy huku uso wake ukiwa umeloa machozi
“Thank you so much Happy.” Akasema Savanna huku naye machozi yakimtoka na kumkumbatia Happy halafu akatoka mle chumbani
* * * *
“The war is over now.Patrick is mine and he’s mine alone.” Akawaza Savanna akiwa katika ndege akirejea Dar es salaam.Uso wake ulikuwa umepambwa kwa tabasamu pana
“Sijafurahia kilichomtokea Happy japokuwa sote tulikuwa katika vita ya kumgombania Patrick lakini kufa kufaana.Namuonea huruma sana Happy japokuwa kwa upande wa pili nimejawa na furaha kwa yeye kuamua kuachana na Patrick.” Akawaza Savanna
“Lakini ni nani hawa waliomfanya udhalilishaji huu mkubwa? Ninaanza kujenga picha kwamba waliofanya kitendo hiki walikuwa na lengo moja tu la kumdhalilisha Happy.Nashawishika kuamini kwamba yeyote aliyefanya jambo kama hili alikuwa na lengo la kulipiza kisasi.Ninalazimika kuamini pia kwamba lazima tukio hili litakua na uhusiano fulani na kifo cha vero.Nasikitika kwamba hatutaweza kuwapata watu hawa kwa sababu Happy hayupo tena Tanzania na hana mpango wa kurejea tena wala wa kuwatafuta watu hawa. ”
Savanna alikuwa na furaha sana kwani aliamini ile ndoto yake ya kuwa na Patrick sasa inakwenda kutimia
*****************
Saa tatu za asubuhi gari moja dogo jeupe likaingia katika gereza la Uwangwa.Kijana mmoja mfupi mnene aliyevaa suti ya kijivu iliyomkaa vyema akashuka toka ndani ya gari lile na kuelekea sehemu ya mapokezi ambako alijitambulisha kama mgeni wa Apolinary.Moja kwa moja akapelekwa katika ofisi ya Apolinary mmoja kati ya maafisa wa gereza hili
“karibu sana kijana” akasema Apolinary ,mzee mmoja mnene mweupe
“Ahsante sana mzee.” Akajibu Yule kijana huku akiketi kitini na bila kuchelewa akaitoa bahasha ya khaki toka mfukoni na kupatia mzee Apolinary ambaye aliifungua na kukutana na bunda kubwa la noti mpya kabisa nyekundu
“Sina haja ya kuhesabu,nadhani ni millioni tatu kamili.”
“Ndiyo mzee,ni tatu kamili”
“namuamini sana Khumalo.Ahadi zake huwa za kweli.” Akasema Apolinary huku akizifungia fedha zile katika kabati lake na kuchukua fimbo yake akamuomba Yule kijana amfuate.Apolinary alienda hadi katika ofisi moja inayohusiana na masuala ya mahabusu akaongea na askari mmoja aliyekuwamo mle ofisini kisha akainua simu akapiga na muda si mrefu wakatokea askari wawili ambao akaongea nao jambo fulani halafu wakaongozana na mzee Apolinary pamoja na yule kijana wake.Waliingia katika chumba kimoja kidogo kilichokuwa na viti viwili.
“Nickson, Patrick ataletwa hapa muda si mrefu na utaongea naye” akasema Apolinary halafu akawatuma wale askari wawili wakamlete Patrick.Baada ya kama dakika saba hivi Patrick akaletwa
“Patrick kuna mtu amekuja kukutembelea.” Akasema Apolinary halafu akawafanyia ishara askari wale watoke mle chumbani na kuwaacha Patrick na yule kijana Nickson
“Nickson una dakika kumi tu za kuongea na Patrick” akasema Apolinary naye akatoka nje
“Watatumia dakika kumi tu halafu mumrudishe Patrick mahabusu” Apolinary aliwaambia wale askari waliokuwa wamesimama nje ya kile chumba
“Patrick pole sana.Nadhani ni mara ya kwanza mimi na wewe tunaonana.Bila kupoteza muda naomba nijitambulishe “ akasema Nickson na kutulia kidogo halafu akaendelea
“Ninaitwa Nickson.Ni mfanyabiashara.Nimekuja hapa kukuletea taarifa ambazo si nzuri na nina imani hautazifurahia lakini kama mwanaume nakusihi ukaze moyo.” Akasema Nickson na kumfanya Patrick apatwe na wasi wasi
“Nickson sina hakika kama tumewahi kuonana mahali.Ni taarifa gani hizo ambazo si nzuri kwangu? Akauliza Patrick
“Patrick ninafahamu mahusiano yako na Happy Kibaho.Ninafahamu kwamba ulivunja mahusiano yako ya awali kwa ajili yake.Ninasikitika kukutaarifu kwamba pamoja na mapenzi yote uliyomuonyesha Happy lakini yeye ameshindwa kuwa mwaminifu kwako na hasa katika kipindi hiki ambacho uko gerezani” akasema Nickson na kumfanya Patrick azidi kuwa na wasi wasi
“Happy amefanya nini? Akauliza Patrick kwa wasi wasi.Nickson hakuongea kitu akaingiza mkono katika koti lake na kutoa bahasha akaisogeza karibu na Patrick
“Fungua uangalie” akasema Nickson.Patrick akaichukua bahasha ile na kuifungua.Ndani ya bahasha ile kulikuwa na picha akazitoa.Picha ya kwanza ikamstua na kuzifanya picha nyingine zote alizokuwa amezishika mkononi zianguke mezani.Akaitazama picha ile aliyokuwa ameishika mkononi.Mikono ilikuwa inamtetemeka huku kijasho kikianza kumchuruzika.Akaiweka picha ile chini na kuchukua picha nyingine akaiangalia.Macho yake yakaanza kutoa machozi.Akajikaza na kuanza kuzipitia picha zile moja baada ya nyingine.Kabla hajamaliza kuzitazama akamtazama Nickson kwa macho makali sana
“Nani amekutuma uniletee picha hizi? Akauliza Patrick huku machozi yakimtoka.Akainama tena akaziangalia picha zile.
“Ouh my gosh !! Happy !!!.Siamini .Siamini kama Happy anaweza akanifanyia hivi.” Akasema Patrick na kufuta machozi.Ghafla kwa nguvu akainuka ,akaisukuma ile meza na kumkaba Nickson
“Niambie nani amekutuma uniletee picha hizi?
Patashika kubwa likaibuka mle ndani na mara askari waliokuwa nje ya kile chumba wakaingia haraka na kumkamata Patrick kisha wakamuamuru Nickson aondoke haraka sana.Kwa haraka Nickson akazikusanya zile picha akaziweka mfukoni na kutoka mle chumbani huku Patrick akiwa ameshikiliwa na askari.Ghafla Patrick akamsukuma kwa nguvu askari aliyekuwa amemshikilia na kwa kasi ya aina yake akamvaa askari aliyekuwa amesimama pembeni ya mlango na kutaka kunyang’anya bunduki.Kuliibuka kizaazaa kikubwa .Patrick na Yule askari walikuwa wananyang’anyana silaha.Yule askari aliyekuwa amesukumwa na kuanguka chini akakiona kitendo kile na kuinuka haraka akamtandika teke kali la mbavuni na kumfanya Patrick aachie bunduki ile aliyokuwa akiing’ang’ania na kutoa yowe.Bila kujali maumivu aliyoyapata kwa teke lile akainuka tena kwa kasi na kutaka kumvamia askari tena yule mwenye silaha lakini askari Yule e alikiona kitendo kile na kwa nguvu akampiga na kitako cha bunduki akaanguka na kupoteza fahamu.Kwa kutumia simu ya upepo wakatoa taarifa kwa viongozi ambao walifika mara moja kushuhudia kilichotokea na kuamuru Patrick apelekwe katika hospitali ya gereza kwa matibabu wakati uchunguzi wa tukio lile ukiendelea.Patrick akatolewa mle chumbani na kukimbizwa katika hospitali ya gereza kwa ajili ya matibabu
* * * *
Savanna aliwasili salama jijini Dar es salaam,kutoka pale uwanjani alikodisha teksi iliyompeleka hadi nyumbani kwake.
“ Kitu cha kwanza ninachotakiwa kukifanya siku ya leo ni kwenda kuonana na Alois na kumuomba wasimueleze kitu chochote Patrick kuhusiana na tukio lile la Happy.Inatakiwa itafutwe namna nzuri ya kumfahamisha Patrick juu ya tukio hili kwani endapo tukikurupuka kumweleza tunaweza kusababisha mambo mengine.” Akawaza Savanna akiwa njiani kuelekea nyumbani kwake
“Namuonea huruma sana Patrick.Matatizo aliyonayo ni makubwa sana.Amempoteza Vero,baba yake na sasa amejitumbukiza katika kesi kubwa ya mauaji na kabla haijajulikana hatima yake linaibuka tena suala hili la Happy.Ninatakiwa nifanye kila niwezalo ili kuhakikisha ninamtoa Patrick gerezani “akaendelea kuwaza Savanna
Alifika nyumbani kwake akaoga na kuvaa suruali nyeupe ya jeans na shati jekundu .Alipendeza vilivyo kama ilivyo kawaida yake.Kabla hajatoka akampigia simu Alois kaka yake Patrick na kumuomba waonane,kisha akaingia katika gari lake akaondoka .
“Nayaona maisha yangu kama yamejaa nuru na furaha hivi sasa na yote hii ni kwa sababu nina uhakika wa kuishi maisha yangu yote nikiwa na mwanaume nimpendaye kuliko wote duniani.” Akawaza Savanna akiwa njiani kuelekea nyumbani kwa wazazi wa Patrick kuonana na Alois kaka wa Patrick
Alipofika alipokelewa na Alois na baada ya maongezi machache akamkaribisha sebuleni
“Unaendeleaje Alois?
“Ninaendelea vizuri Savanna.Tumekwishaizoea hali hii.Nashukuru Mungu hata mama naye anaendelea vizuri hivi sasa” Akasema Alois
“Nashukuru kusikia hivyo”
“Vipi kuhusu wewe Savanna unaendeleaje? Kesi inakwendaje?
“Mimi ninaendelea vizuri sana Alois na kuhusu kesi hakuna haja ya kuwa na wasi wasi kila kitu kinakwenda vizuri .Nawaomba muondoe shaka kabisa kuhusu kesi hii kwani ni lazima tushinde.” Akasema Savanna na kumfanya Alois atabasamu
“Ahsante sana Savanna kwa kuzidi kutupa matumaini.Umekuwa mfariji wetu na tegemeo letu katika suala hili la Patrick.Umemsaidia sana hata mama kutokuwa na wasi wasi na mwanae.Nikupe siri moja mama anampenda sana Patrick.”akasema Alois halafu kikapita kimya kifupi
“karibu sana Savanna” akasema Alois
“Alois mimi si mkaaji sana nimepita hapa mara moja ili tujadili kwa pamoja jambo hili lililotokea.” Akasema Savanna
“Jambo gani Savanna? Hili la Patrick?
“Ni kuhusu Happy.Nadhani umeisikia kashfa iliyompata”
“Ndiyo.Alinipigia simu Andrew jana na kunifahamisha.Niliitazama video yake katika mtandao sikuamini kama ni kweli Happy ameweza kufanya kitendo cha aibu kama kile.Nimefadhaika sana kwa sababu yule msichana ndiye chanzo cha Patrick kusota gerezani hivi sasa.Ni aibu kubwa mno na hata mama nimemficha sijamweleza chochote” akasema Alois
“Nakubaliana nawe Alois.Kitendo kile ni cha aibu sana na hakivumiliki.Kikubwa kilichonileta hapa ni kukuomba kwamba Patrick asifahamishwe kwa sasa.Endapo akifahamu alichokifanya Happy itamsababishia matatizo makubwa sana kwani kchwa chake kwa sasa kimebeba mambo mengi ”
“Savanna bila hata kuomba lakini naomba nikuhakikishie kwamba si mimi wala mtu yeyote katika familia yetu angeweza kumweleza Patrick kitu chochote kuhusiana na uchafu uliofanywa na Happy.Ni kitendo cha aibu sana na kisichovumilika.Moyo wangu umeumia hasa nikimuangalia mdogo wangu anavyoteseka gerezani kwa ajili ya huyu huyu msichana”
“Ahsante sana Alois kwa busara hiyo.Basi ni hilo pekee lililonileta hapa.Naomba uniruhusu niondoke nikaendelee na majukumu mengine.” Akasema Savanna
“Nashukuru sana Savanna kwa kuja kututembelea bahati mbaya mama amelala alikuwa na hamu sana ya kukuona”
“Mpe salamu zangu.Nitakuwa nikija hapa mara kwa mara kumsalimu” akasema Savanna kisha akainuka na kuondoka.
“Kwa sasa ni safari ya moja kwa moja kueleka Uwangwa .kabla sijafanya chochote lazima niaonane kwanza na Patrick.Sijamtia machoni kwa siku nzima ya jana” akawaza Savanna
* * * *
Ilimchukua dakika arobaini kuwasili katika gereza la Uwangwa.Kijua kilikuwa kikali sana siku hii.Kisha shuka garini akaelekea moja kwa moja mapokezi kama ilivyo kawaida yake na pale alipewa taarifa kwamba akaonane na mkuu wa gereza.Alistushwa sana na taarifa ile.Alijaribu kudadisi ili kufahamu nini kilichotokea hadi ikamlazimu akaonane na mkuu wa gereza kabla ya kuonana na Patrick lakini hakuna aliyekuwa tayari kumweleza chochote.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Huku akiwa na uso uliojaa wasi wasi Savanna akatembea kwa kasi kuelekea katika ofisi ya mkuu wa gereza.Alijitambulisha kwa katibu muhtasi wa mkuu wa gereza ambaye alimpigia simu mkuu wake na kisha akamruhusu Savanna aingie ofisini.
“karibu Savanna” akasema mkuu wa gereza.
“Nashukuru sana mkuu” akasema Savanna.Kikapita kimya cha sekunde kadhaa
“Mkuu nimekuja kuonana na mteja wangu lakini nimestushwa kidogo kwa kuambiwa kwamba unahitaji kuniona kabla ya kuonana na mteja wangu” akasema Savanna
“Ni kweli Savanna.Nilitoa maagizo hayo.Kuna jambo limetokea leo kuhusiana na mteja wako” akasema mkuu wa gereza na kumfanya Savanna astuke
“jambo gani limetokea tena?
“Leo asubuhi kuna mtu ambaye alikuja kuonana na Patrick.Kwa mujibu wa askari waliokuwepo eneo la tukio,mtu huyo alikuwa na bahasha yenye picha ambazo alimpa Patrick azitazame.Hatujui picha hizo ni za nani na kwa nini mtu huyo alimpa Patrick lakini inasemekana baada tu ya Patrick kuziona picha hizo alibadilika na kuwa kama mtu aliyechanganyikiwa.Alimkaba mtu Yule aliyempeleka zile picha na akazua tafrani kubwa.Askari ambao walikuwa nje waliingilia kati ugomvi huo na kumdhibiti Patrick lakini alifanya kitu cha ajabu sana kwani alimvamia askari na kutaka kumnyang’anya silaha.Hatuelewi alikusudia kufanya nini na ile bunduki lakini nina hakika angefanikiwa kuipata silaha ile angeleta maafa makubwa.Askari walifanikiwa kumdhibiti na kumsababishia jereha kidogo kichwani na hivi sasa anaendelea kupatiwa matibabu katika zahanati ya gereza”
“Ouh my gosh !! akasema Savanna huku ameshika kichwa kwa mikono.
“Kuna taarifa zozote za maendeleo yake?
“Kwa taarifa nilizozipata toka kwa madaktari muda si mrefu ni kwamba Patrick anaendelea vizuri.”
“Ouh Mungu wangu ..!!” akasema Savanna.Suala lile lilikuwa limestua sana.
“Savanna suala hili la Patrick ni suala zito sana na endapo litafika katika vyombo vya sheria litakuwa na athari kubwa sana kwa Patrick na hata kwa uongozi wa gereza.Kwa heshima yako suala hili litaishia hapa hapa na halitaenda sehemu yoyote lakini hata hivyo inabidi tuchukue hatua za kuzuia jambo kama hili lisijitokeze tena.Tumeamua kudhibiti watu wanaokuja kumtembelea Patrick.Kuanzia hivi sasa watakaoruhusiwa kuonana naye ni wewe pamoja na familia yake pekee.Hakuna mtu mwingine yeyote atakayeruhusiwa kumuona.Hii ni kwa ajili ya usalama wa Patrick vile vile kwani hatujui katika watu wanaokuja kumtazama ni yupi atakuwa adui yake”
“Nashukuru sana mkuu wa msaada wako huu mkubwa.Nitaongea na Patrick na kumsihi asithubutu kufanya kitendo cha hatari namna hiyo tena.Ninaweza kuruhusiwa kuonana naye?
“Twende tuongozane na mimi nikaangalie maendeleo yake.” Akasema mkuu wa gereza huku akiinuka akatoka mle ofisini
“Nahisi mwili wote ni kama umekufa ganzi.Ni nani huyu aliyemletea Patrick picha? Najua ni lazima zitakuwa ni picha za Happy.Ninaanza kujenga hisia kwamba jambo hili si la mtu mmoja bali linahusisha kikundi cha watu na wana ajenda yao ya siri kufanya hivi na ajenda yao kubwa ni kuuharibu uhusiano wa Patrick na Happy.Kwa mujibu wa barua ile aliyoindika Happy ni kwamba alitekwa na kundi la watu waliomlazimisha kufanya ngono na kisha kumpiga picha za utupu na kuzisambaza.Kuna ulazima wa kuwafahamu watu hawa wenye roho za kikatili namna hii” akawaza Savanna wakati wakielekea katika zahanati ya gereza kumuangalia Patrick
Mkuu wa gereza na Savanna waliingia katika ofisi ya mganga mkuu wa gereza ambaye aliwapa taarifa za maendeleo ya Patrick na kisha kuwapeleka katika chumba alichokuwa amelazwa Patrick
“Tumemchoma sindano ya usingizi nadhani baada ya masaa mawili au matatu ataamka.” Akasema daktari.Patrick alikuwa amelala usingizi mzito sana pale kitandani na sehemu ya juu ya jicho lake alikuwa na jeraha.Mkono wake wa kushoto ulikuwa umefungwa pingu.Savanna akashindwa kuvumilia kumuona Patrick katika hali ile akaangusha machozi
“Tafadhali mkuu naombeni mumfungue hiyo pingu.Hatakwenda sehemu yoyote.Hawezi kukimbia”
“Hii pingu amefungwa kwa ajili ya usalama.Alipoamka mara ya kwanza alionekana ni kama mtu aliyechanganyikiwa.Alitaka kukimbia akazuiwa hivyo tumeona ni bora kama tukimfunga pingu ili asiweze kutoka hapa kitandani akasema daktari
“Savanna wewe unaweza kwenda kupumzika.Mteja wako yuko katika uangalizi makini .Endapo kutakuwa na tatizo lolote tutakutaarifu” akasema mkuu wa gereza.
“Ahsante sana mkuu ,lakini naomba niendelee kukaa hapa hadi hapo atakapoamka ili niweze kuongea naye hata maneno mawili na nimsihi atulie asifanye jambo lolote la hatari.tafadhali mkuu naomba uniruhusu kwa hilo” akaomba Savanna
Mkuu wa gereza akainama akafikiri kwa muda kisha akasema
“Sawa Savanna,kama unahitaji kujiridhisha zaidi na maendeleo ya mteja wako basi hakuna shaka.Kuna mgahawa wa gereza unaweza kwenda kukaa pale na pindi atakapoamka tutakutaarifu.” Akasema mkuu wa gereza halafu wakatoka .Savanna akakabidhiwa askari aliyempeleka hadi katika mgahawa wa maofisa wa gereza.
“Sintawataarifu familia yake kwa sasa hadi hapo nitakapohakikisha anaendelea vizuri.Nikiwaeleza sasa hivi kwamba mtoto wao amepatwa na matatizo tena ninaweza kuwasabishia matatizo mengine katika wakati huu mgumu walionao” akawaza Savanna
Ni mtu mmoja tu aliyekuwa anasubiriwa atoke ndani ili safari ya kuelekea makaburini ianze.Siku hii ya leo familia ya Vero waliamua kwenda kulitembelea kaburi la Vero ambalo tayari lilikuwa limemalizwa kutengenezwa.Kazi iliyokuwa ikifanyika ilikuwa ni kuweka vigae pamoja na marembo mengine na kulifanya lipendeze mno
Familia yote ilikwisha kusanyika na aliyekuwa anasubiriwa ni mama yao.Wote walikuwa wamepanda katika gari moja.
“She’s taking too long” akasema Loniki
“Labda anasal…….” Shangazi yao akataka kusema kitu lakini kabla hajamaliza mtu waliyekuwa wanamsubiri akatokea na safari ikaanza
Kabla hawajafunga mlango simu ya Loniki ikaita.Akaitoa mfukoni na kutazama mpigaji alikuwa ni Linah
“Hallow Linah
“Lonny umeamkaje dear?
“Nimeamka salama Linah.”
“Uko wapi mida hii? Bado umelala?
“Hapana Linah.Niko na familia tunajiandaa kwenda kutembelea kaburi la Vero.Mafundi tayari wamemaliza matengenezo”
“Lonny kama ningekuwa na muda ningekuja kuungana nanyi lakini nimebanwa sana leo”
“usijali sana Linah.Vipi kuna habari gani mpya?
“Khumalo kanipigia simu sasa hivi na kunitaarifu kwamba tayari Patrick ameziona zile picha”
“Ouh gosh ..!! what happened? Akauliza Loniki kwa furaha huku akishuka garini ili aweze kuongea vizuri na Linah bila ya mtu kusikia maongezi yao
“kwa mujibu wa taarifa ya kijana aliyezipeleka picha hizo ni kwamba mara tu Patrick alipozitama alibadilika na kuwa kama mtu aliyepandwa na uchizi.Alimvamia kijana huyo na kutaka kufahamu aliyemtuma ampelekee picha hizo kwa bahati nzuri kulikuwa na askari karibu hivyo hakuweza kumdhuru.Baada ya askari kumshikilia Patrick asiendelee kuleta fujo ,alimrukia askari aliyekuwa na bunduki na kutaka kumnyang’anya silaha jambo lililowalazimu askari kumtembezea kipigo kikali sana.Hivi sasa nasikia hali yake ni mbaya na amelazwa katika hospitali ya gereza”
“Ouh gosh ! that’s great news to hear this morning.Sipati picha ingekuaje kama angefanikiwa kuinyakua hiyo bunduki.Nadhani lengo lake lilikuwa kujiua.Hahaha haaa I think the plan is working .Patrick and Happy are both in great pain right now” akasema Loniki huku akitabasamu kwa furaha
“Si hilo tu Lonny kuna taarifa nyingine pia imevuja kwamba Happy alitaka kujiua kwa kunywa sumu baada ya kuziona picha zile.Taarifa zinaseama kwamba baada ya kunywa sumu alikimbizwa katika hospitali ya Brahmaputra lakini uongozi wa hospitali ile umekanusha taarifa hizo.Taarifa mpya iliyopatikana toka vyanzo vya karibu vya Khumalo ni kwamba mpaka muda huu Happy hajulikani alipo.Waandishi wa wa habari wamekuwa wakimtafuta kwa mahojiano lakini hawajui yuko wapi na simu yake haipatikani tena na hata familia yake haiko tayari kusema mtoto wao yuko wapi” akasema Linah
“hahaaa aahahaa haaa!! Loniki akacheka kwa furaha na mara honi ya gari ikapigwa
“Linah wananipigia honi.Tutaongea baadae.Ahsante kwa taarifa” akasema Linah akakata simu na kukimbilia garini
“mambo ndo kwanza yanaanza Patrick.I’ll make your life a living hell.You and your girl must pay for what you did to Vero” akawaza Loniki
“Natumai kwa muda huu Patrick na Happy watakuwa katika mateso makubwa sana.Niliahidi kulipiza kisasi kwa kifo cha mdogo wangu na nitafanya hivyo.Huu ni mwanzo tu” akawaza Loniki
Safari ilikuwa ya kimya kimya hadi walipofika makaburini.Wakashuka garini na kuelekea katika kaburi la Vero.Lilikuwa kaburi linalopendeza na lililojengwa kwa ustadi mkubwa.Mama yake Vero akashindwa kuyazuia machozi kumtoka tena.Akakaa juu ya kaburi la binti yake aliyempenda sana na kuanza kulia
“Masikini binti yangu,wamekukatili uhai wako.Hukustahili kuondoka na kuniacha peke yangu mapema namna hii.Ninaomba usiku na mchana wale wote waliokukatili mwanangu na kunisababishia mateso haya makali wapate adhabu kali inayowastahili” akalia mama yake Vero.Loniki akamsogelea na kukaa pembeni yake
“Usilie mama,wote waliohusika na kifo cha Vero watapata adhabu inayowastahili na tayari yamekwisha anza kuwapata makubwa.Wataumia na kuteseka kama sisi tunavyoumia na kuteseka” akasema Loniki
Sarah ambaye anaye alikuwa amesimama karibu na kaburi akastuka baada ya kusikia maneno ya Loniki.
“mama ,kitu peke kinachoweza kukupa amani ya moyo ni kumuachia Mungu suala hili na si kuwaombea mabaya wahusika wa tukio hili.Kwa kuwaombea mabaya unakwenda kinyume na maandiko yanayotukumbusha kwamba tuwapende wabaya wetu na tuwaombee neema na Baraka .Ni Mungu pekee ndiye atakayewaadhibu” akasema Sarah
“Sarah najitahidi sana kufanya hivyo lakini ninashindwa.Kila nikifikiria namna mwanangu alivyokufa najikuta nikiwa na hasira na hamu ya kutaka kuwaona wale wote waliofanya kitendo kile wakipata adhabu kali.”
“Usiseme hivyo mama.Unat……” akasem Sarah lakini Loniki akaingilia kati
“Mama usimsikilize huyu.Siku zote yeye amekuwa upande wa Patrick.Hana uchungu wowote na kifo cha mdogo wake.Mama mimi ndio niko pamoja nawe.Wote waliosababisha kifo cha Vero lazima wapate adhabu kali”
Sarah na Loniki wakaangaliana kwa macho makali sana.Ikamlazmu mama yao kuingilia kati
“Haya inatosha sasa.Tuwekeni maua tuondoke” akasema mama yao halafu akachukua maua akayaweka juu ya kaburi na kupiga magoti,akasali kimya kimya na kusogea pembeni kuwapa nafasi wengine.Kila mmoja aliyekuja hapo aliweka shada la maua na kusali sala fupi
“Vero mdogo wangu,natumai huko uliko unaniona mida hii.Niliahidi kulipa kisasi kwa wale wote waliokufanyia unyama ule mkubwa na kukukatili maisha yako .Tayari nimeanza kuitekeleza ahadi yangu na wahusika wameanza kulipa.Si kazi rahisi lakini nakuahidi nitaifanya hadi nihakikishe Patrick na mwenzake wamelipa” akasema Loniki kwa sauti ndogo akiwa amepiga magoti katika kaburi la Vero.Zoezi lilipokamilika wakaingia garini na kuondoka kuelekea nyumbani
* * * *
Mlio wa simu ukamstua Savanna toka katika mawazo mengi.Ilikuwa ni simu toka kwa mkuu wa gereza
“hallo mkuu” akasema Savanna-
“Savanna nimetaarifiwa kwamba tayari Patrick ameamka,unaweza kwenda kumuona sasa”
“Ahsante sana mkuu” akasema Savanna huku akiinuka na kuanza kupiga hatua kuelekea katika zahanati ya gereza
“Mungu msaidie Patrick katika kipindi hiki kigumu alichonacho.” Akaomba Savanna wakati akipanda ngazi kuingia zahanati.Alionana na daktari ambaye alimpeleka moja kwa moja katika chumba alicholazwa Patrick
Mara tu Patrick alipomuona Savanna akainuka na kukaa kitandani.Savanna akamuendea na kumkumbatia
“Ouh Patrick,pole sana” akasema Savanna
“Savanna nashukuru umekuja” akasema Patrick kwa sauti ndogo yenye kukwama kwama.
“Patrick unajisikiaje sasa hivi?
“I’m dead Savanna.I feel dead” akasema Patrick
“Patrick usiseme hivyo”
“Savanna I want to die.namba uwaambie wanifungue hii pingu nife.I want to die.Sioni tena sababu ya kuendelea kuishi“CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Patrick tafadhali naomba unisikilize”
“Savanna believe me I’m dead.Ninahisi maumivu makali ya moyo.Nahisi kama kuna kitu kikali kinaukata moyo wangu vipande vipande..Ninasikia maumivu makali ambayo siwezi kuyaelezea” akasema Patrick
“Patrick nini kimetokea? Akauliza Savanna
“Savanna Happy yuko wapi? Happy ameniua.Ameniua bila kosa kama alivyomuua Vero.Nimemkosea nini mpaka anifanyie unyama wa namna hii? Upendo wote huu niliomuonyesha iweje leo hii anifanyie namna hii? It was all a lie.There was no us,there was no love ,it was all lies.Please let me die” akasema Patrick kwa uchungu
“Patrick tafad…………….” kabla Savanna hajamaliza alichotaka kukisema Patrick akapaaza sauti
“Waambie wanifungue.I want to die..!!!!!!!!!!!!!!!!”
Savanna akaogopa na kuwaita madaktari ambao walimkamata na kumchoma sindano ya usingizi
“Savanna unaweza kwenda nyumbani saas.Patrick bado akili yake haijatulia.Tutaendelea kumuangalia na kama kutakuwa na tatizo lolote tutakufahamisha” daktari akamshauri Savanna ambaye alikubali na kuondoka kuelekea nyumbani kwake.Hakutaka tena kufanya kazi yoyote kwa siku ile.kili yake yote ilikuwa inamuwaza Patrick.
* * * *
Ni siku ya pili sasa toka Parick alpolazwa katika hospitali ya gereza.Hali yake ilikuwa imeimarika tofauti na siku zilizotangulia
“Halloo Patrick “ akasema Savanna aliyekuja kumsalimu asubuhi hii
“Savanna.Karibu sana” akasema Patrick huku akijilazimisha kutabasamu
“Ahsante Patrick,unaendeleaje?
“Namshukuru Mungu leo sijambo.Naendelea vizuri sana.Madaktari wamenisaidia sana kunirejesha katika hali ya kawaida” Akajibu Patrick ambaye siku hii hakuwa amefungwa pingu kama siku zilizotangulia.
“Nashukuru sana kama unaendelea vizuri” akasema Savanna huku akiifungua chupa ya chai aliyokuja nayo na kummiminia Patrick chai katika kikombe
“mama na ndugu zangu wote hawajambo? Akauliza Patrick
“wote wazima na wanaendelea vizuri .Ninapita kila siku kuwasalimu na kumpa mama maneno ya matumaini.Mama anafarijika sana kila anionapo.Utanisamehe kwa kuwa sijawaambia chochote kuhusiana na wewe kulazwa hapa hospitali.Niliogopa kumuongezea mama matatizo hasa katika wakati huu ambao hali yake imeanza kuimarika.”
“Ulifanya vizuri sana Savanna kutokuwaeleza chochote.Wamekwisha umia vya kutoka kwa sababu yangu na sitaki waendelee kuumia zaidi.Nataka niendelee kuteseka mimi mwenyewe.” Akasema Patrick
“Savanna nakushukuru sana .Sipati nena la kuelezea shukrani zangu .You are my true friend.Umekuwa na mimi toka dakika ya kwanza na hadi leo hii haujaniacha hata siku moja.Savanna you have a special place in my heart.Sikujua kama siku moja wewe ndiye ungekuja kuwa mkombozi wangu.Watu niliowaamini na kuyatoa maisha yangu kwa ajili yao leo hii hawako tena na mimi,wamenisaliti na kuniacha peke yangu.Rafiki yangu Andrew,Happy…” Patrick akainama akazama katikam awazo halafu akainua kichwa na kusema
“Savanna naomba unisaidie ili niweze kutoka humu gerezani kwani sioni tena sababu ya mimi kuendelea kukaa humu gerezani.Nimempoteza Vero msichana aliyenipenda kwa moyo wake wote kwa ajili ya mtu ambaye haoni thamani yangu kwake.I was so wrong” Akasema Patrick kwa uchungu.
“Patrick usijilaumu sana kwani hukutegemea kama yangetokea haya yaliyotokea.Pamoja na kuondoka kwa Vero lakini kaa ukijua kwamba bado kuna watu wengi wanaokupenda na kukuombea usiku na mchana ili uweze kutoka salama gerezani na kuendelea na maisha yako.Familia yako,Happy na m………” kabla hajamaliza sentensi yake Patrick akasema kwa ukali
“Savanna tafadhali naomba usilitamke jina la huyo Malaya mbele yangu tena.Hilo ni jina ambalo sitaki kulisikia tena katika masikio yangu.Nilimpenda sana nikampa mwili na moyo wangu,nilikuwa tayari kuachana na kila kitu kwa ajili yake lakini kwa alichonifanyia sidhani kama nitakuja kumsamehe Happy.Savanna nimeumia sana.Sikuona sababu ya kuendelea tena kuishi siku ile niliponyeshwa picha za uchafu wake.” Akasema kwa uchungu Patrick
“Sijui nimweleze ukweli kuhusu suala hili? Lakini hapana,siwezi kufanya hivyo.Tayari amekwisha mtoa Happy akilini mwake na hii ni nafasi yangu sasa.Nataka Patrick awe wangu na inanibidi kuitumia vyema nafasi hii niliyoipata.Sintamweleza lolote kuhusiana na Happy” Akawaza Savanna
“Patrick pole sana.Hata mimi nilistuka sana nilipoziona picha za Happy katika gazeti na mitandao.Niliogopa sana hata kukwambia kwani nilijua ungeumia mno.” Akasema Savanna
“Usijali Savanna.Kuna watu walioguswa sana na kitendo kile na wakaniletea picha zile ili niangalie uchafu alioufanya mtu niliyemkabidhi moyo wangu.Siwafahamu watu hawa lakini nawashukuru sana kwa kunisaidia kutambua kwamba mtu niliyedhani ni kondoo ,alikuwa ni chui.Sikutegemea kama Happy angeweza kutenda kitendo kichafu na cha kujidhalilisha kama kile.Ninachoweza kukuomba kwa sasa ,nisaidie niweze kutoka humu gerezani na nianze upya maisha yangu.tafadhali Savanna usiniache nikafungwa kwa sababu ya mtu ambaye haioni thamani yangu kwake.”
“Patrick usijali kuhusu hilo.Kama nilivyokwisha kuahidi na ninavyoendelea kukuahidi ni kwamba nitafanya kila niwezalo ili uweze kushinda kesi hii.Bado hujachelewa kuyaanza upya ,maisha yako.Siku zote fahamu kwamba umezungukwa na watu wanaokupenda na kukujali kwa hiyo usijione mpweke.I’m right here for you any time you need a friend” akasema Savanna..
**********************
Dr Consolata bugama bingwa wa magonjwa ya akili,aliagana na mgonjwa wake akapanda gari lake na kuondoka pale Reonaldo hoteli.Happy alilitazama gari lile hadi lilipotoka kabisa katika lango la hoteli ile ya kifahari jijini Kigali.Akatabasamu na kuelekea katika sehemu ya kupumzikia
Ni siku ya tisa sasa toka alipokuja katika jiji hili la Kigali.Hali yake ilikuwa inaimarika siku hadi siku.Kwa msaada mkubwa anaoupata toka kwa daktari aliyeambatana naye toka Dar es salaam pamoja na Dr Consolata bingwa wa magonjwa ya akili katika hospitali kuu ya Kigali hali yake ilikuwa ya kuridhisha sana.
“Namshukuru sana Mungu kwa huruma yake hivi sasa ninaendelea vizuri.Sikutegema kama hali yangu ingekuwa namna hii.Mungu ni mwema sana na bado ananipenda na ndiyo maana hakuruhusu nife kwa sumu.Nawashukuru sana madkatari wangu kwa jitihada zao za kuhakikisha kwamba ninarejea katika hali yangu ya kawaida.Dr Consolata amejitahidi sana kuhakikisha kwamba akili yangu inarejea katika hali yake ya kawaida.Namshukuru sana pia Christine.Huyu dada amekuwa ni mtu wangu wa karibu na kila mara ninapohitaji mtu wa kuongea naye yeye amekuwa tayari kufanya hivyo.Siwezi kuusahau uongozi na wafanyakazi wa hoteli hii .They are all wonderfull people.Ni wakarimu na wote wananipenda sana.Ninahudumiwa kama mtoto wa rais.Ninapenda sana kuendelea kuishi hapa.Nimepapenda Kigali.I feel so Happy and safe around here” akawaza Happy huku akitabasamu
“Ouh gosh ! siwezi kumsahau Savanna.Japokuwa moyo wangu unastuka kila ninapoikumbuka sura yake lakini sina budi kumshukru kwa msaada mkubwa alionipatia.Najua hata wazo la kuondoka Tanzania na kuja Kigakli ni yeye ndiye aliyelitoa na kulisimamia kwa nguvu zote na likafanikiwa.Amenisaidia mno kuniondoa katika aibu na fedheha niliyoipata.Niko nje ya Tanzania sasa,ninashukru sana kwa sababu aibu niliyoipata ni kubwa na ambayo inanifanya nisitake tena kurudi Tanzania.Inaniuma sana kuiacha nchi yangu na kumuacha Patrick mwanaume wa maisha yangu niliyempigania kwa kila namna niliyoweza lakini kwa hili lililotokea nimeinua mikono.Sina namna nyingine zaidi ya kukubali kushindwa na kumuacha Patrick mikononi mwa Savanna.Najua atakuwa katika mikono salama.Mimi na Patrick hatuwezi kuwa pamoja tena.Huu ni ukweli ambao hatuwezi kuukwepa.” Akawaza Happy na sura yake ikaanza kubadilika na kuwa ya huzuni kidogo
“ Najaribu kumuhusisha Savanna na tukio lile la kutekwa kwangu lakini sioni kama ana uhusika wowote katika jambo lile.Kama si yeye nani basi anaweza kuwa nyuma ya tukio lile? Picha niliyoipata ni kwamba watu walionitenda vile lengo lao lilikuwa ni kunidhalilisha na kuhakikisha kwamba kwa namna yoyote ile ninaachana na Patrick.Laiti ningejua kwamba lengo lao ni hilo nisingekubali kufanyiwa udhalilishaji ule mkubwa.Anyway namuachia Mungu yeye ndiye atakayenilipia kwa mambo yote niliyofanyiwa.” Akaendelea kuwaza Happy
“Najua maisha yangu hayatakuwa na furaha tena na ninajua kwamba sintampata mwanaume kama Patrick katika maisha yangu yaliyobaki lakini ni vyema endapo nitakwenda kuishi mbali kabisa naye,mbali na Tanzania .Sitaki kukaa karibu naye kwani itanifanya niendelee kulipigania penzi letu na kadiri ninavyoendela kuupigania uhusiano wetu ndivyo mambo mabaya yanavyozidi kunitokea.Nimekwisha msababishia Patrick maumivu mengi ya moyo na sitaki aendelee kuumia zaidi.Nadhani uamuzi huu wa kutorejea tena Tanzania ni uamuzi wa busara sana ingawa najua Patrick ataumia mno na kunichukia.Ataniona kama ni msaliti na nilifanya kitendo kile kwa makusudi.Hakuna siri siku hizi hata kama yuko gerezani lazima atazipata taarifa zangu na nina hakika ataamini kwamba hii ndiyo tabia yangu.Ouh gosh ! ni mateso makali sana ya moyo atakayoyapata..” Akawaza Happy halafu akainuka na kuanza kuzunguka bustanini
“Dr Consolata amekuwa akijitahidi sana kuhakikisha ninasahau yaliyopita .Sipaswi kuendelea kuyafikiria yaliyopita.Ninachotakiwa kufanya kwa sasa ni kufikiri kuhusu maisha yangu ya mbele yatakuwaje.” akawaza Happy huku akiendelea kuzunguka zunguka mle bustanini
“Nimeipenda sana Rwanda .Ni nchi nzuri na ningefurahi mno kama ningeishi katika nchi hii kwa maisha yangu yote yaliyobakia.Lakini siwezi kufanya hivyo.Lazima niondoke Rwanda.Natakiwa kwenda kuishi mbali kabisa na Tanzania ikiwezekana nje kabisa ya Afrika.Nataka nikaishi mahala ambako nitaishi bila kuonana na mtu yeyote wa kutoka Tanzania.Kuna mtu mmoja tu ambaye anaweza akanisaidia katika hili. Ni Mike pekee.Najua niliutia moyo wake jeraha kubwa ambalo si rahisi kupona haraka ,niliuvunja vunja moyo wake pale nilipoamua kuachana naye na kurudiana na Patrick.Najutia nafsini kwangu kwa kitendo kile.It needs more than a man to forgive me for what I did.Japokuwa kabla hajaondoka Tanzania alinihakikishia kwamba amenisamehe lakini sina hakika kama ataweza kukisahau kitendo kile nilichomfanyia.”
Happy akasimama baada ya picha ya Mike akiondoka Tanzania chini ya ulinzi mkali kumjia kichwani.
“Ouh Gosh ! forgive me Mike” akasema Happy huku akisikia uchungu mwingi moyoni
“Sina hakika kama Mike anaweza kuwa tayari kunisaidia au hata kunisikiliza lakini sitakiwi kukata tamaa.Natakiwa kujaribu kumuomba anisaidie.Endapo atakataa kunipa msaada ninaoutaka nitatafuta namna nyingine ya kufanya.Nitamuomba hata Savanna anisaidie.Kitu pekee ninachokiami na kinachonipa msukumo wa kutaka kuwasiliana na Mike ni kwamba Mike ananipenda kwa moyo wake wote.” Akawaza Happy na kuupeleka mkono sehemu ulipo moyo wake ambao ulikuwa unadunda kwa kasi kubwa.
“lazima niwasiliane naye na nimuombe anisadie.Lazima niondoke hapa Kigali na kwenda mbali.Namuonea huruma sana baba yangu .Amekuwa nami kwa kipindi kirefu toka matatizo haya yalipoanza na yeye ndiye amekuwa msaada mkubwa kwangu.Ni wakati sasa wa yeye kupumzika na kuendelea kufanya shughuli zake za kimaendeleo.Ninajisikia furaha sana kuwa na baba kama huyu.He’s the best father in the world.” Akawaza Happy na kutabasamu
“Ngoja sasa nikampigie simu Mike.” Akawaza Happy na kuelekea chumbani kwake.Alipoingia chumbani kwake akasimama mbele ya meza iliyokuwa na simu akaitazama simu ile na kuvuta pumzi ndefu.
“I’m so scared” akasema kwa sauti ndogo.Kwa takribani dakika tatu alisimama akiitazama simu ile.Alihisi kama mikono yake ikimtetemeka kila alipojaribu kutaka kuichukua simu ile na kupiga
“Mungu wangu tafadhali naomba unisaidie.Nahitaji kufanya hivi.Nahitaji kuongea na Mike” akasema Happy kwa sauti ndogo.Baada ya tafakari akaamua kupiga.Alizifahamu namba za simu ya mkononi ya Mike na akaziandika huku mapigo ya moyo wake yakienda kwa kasi kubwa.Akauweka mkono wa simu sikioni na simu ikaanza kuita.Baada ya sekunde kadhaa akasikia sauti ikimwambia
“Mike hayuko katika nafasi ya kupokea simu kwa sasa tafadhali acha ujumbe wako baada ya mlio.” Happy akavuta pumzi ndefu na mara baada ya mlio kusikika akasema
“Hallow Mike,ni mimi Happy.Naomba upatapo uumbe huu,unipigie simu.Kwa sasa niko Kigali Rwanda,Reonaldo hoteli presidential suit number two.Please call me back Mike.I real need to talk to you” Happy aliyasema maneno haya huku machozi yakimtoka.Akauweka mkono wa simu chini ,akapangusa machozi na kwenda kuketi sofani
“Please Help me Mike” akasema kwa sauti ndogo
Baada ya dakika tano kupita simu ikaita.Akainuka na kwenda mezani akasimama na kusita kuipokea.Simu ikaendela kuita na mwishowe akaamua kuipokea.
“hallo “ akasema Happy
“Hallow Happy.Mike hapa nongea” Ikajibu sauti ya upande wa pili.Mikono ya Happy ikaloa jasho.Kwa sekunde kadhaa alihisi kama sauti yake ikigoma kutoka
“Hallow Mike” akasema Happy kwa sauti yenye kitetemeshi
“Hallow Happy.Unaendeleaje? Nimeupata ujumbe wako muda si mrefu.Habari ya Tanzania?
“habari ya Tanzania nzuri ila kwa sasa niko Kigali Rwanda”
“Sawa Happy.Nashukuru sana kwa kunikumbuka .Patrick anaendeleaje?
Swali lile likamchoma sana Happy akahisi kama miguu inaisha nguvu
“ Anaendelea vizuri” akajibu kwa ufupi
“Happy una tatizo gani? Naisikia sauti yako kama haiko sawa.Ninakufahamu vyema wakati una tatizo”
Happy akakaa kimya akahisi kama midomo yake inashindwa kufunguka
“ Happy una tatizo gani? Akauliza tena Mike
Happy akakohoa kidogo na kusema
“Mike ni kweli nina tatizo na ninahitaji msaada wako” kimya kifupi kikapita Mike akasema
“Una tatizo gani Happy?
“Mike siwezi kukueleza katika simu ni tatizo kubwa.Najua kwa sasa mimi ni mtu ambaye hupendi kuniona na hata kuisikia sauti yangu kutok…………”
“No ! No ! Happy.Usifikiri hivyo” mike akamkatisha Happy
“Ni kweli Mike.Hata mimi mwenyewe nafsi yangu inanisuta sana kwa kitendo nilichokufanyia lakini pamoja na hayo yote yaliyotokea sina mtu mwingine ninayeweza kumkimbilia kuomba msaada kwa sasa.Mike najua ndani kabisa mwa moyo wako bado nina nafasi japokuwa ndogo sana.Ninakuomba kama rafiki unisaidie” akasema Happy huku machozi yakimtoka.Kupitia spika za simu Happy akamsikia Mike akivuta pumzi ndefu na kusemaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Happy,napenda niwe wazi kwako kwamba kilichotokea baina yetu kiliniumiza sana.Nilipata jeraha ambalo halitaweza kutibika.Ulipoamua kuniacha niliumia sana.hadi hivi sasa bado ninaamini kilichotokea ni kama ndoto na ndiyo maana nilipoupata ujumbe wako nimekupigia simu mara moja.” Akasema Mike na kunyamaza .Maneno yale yakamuumiza sana Happy na kuzidi kumtoa machozi.Mike akaendelea
“Happy kama nilivyosema siku ile nilipokuja kukuaga kwamba mimi tayari nimekusamehe na wala sina kinyogo chochote nawe.Kwangu mimi ,wewe bado ni mtu muhimu sana na rafiki wa pekee kabisa. Niko tayari kukupa msaada wowote na kwa wakati wowote.Naomba unieleze unahitaji msaada gani Happy? Akasema Mike .Happy ambaye kifua chake kilikuwa kimeloa machozi akasema
“Mike kwa sasa nimekwama hapa Kigali na lengo langu kubwa ni kuondoka hapa. Nataka kuja Marekani lakini sina namna ya kuondoka hapa.Naomba unisaidie ili niondoke hapa kuja Marekani.Nahitaji kuwa mbali na Tanzania.Tafadhali Mike nahitaji sana msaada wako sasa kuliko wakati wowote katika maisha yangu.Tafadhali naomba unisaidie Mike” Happy akaomba.Sauti yake ilitia huruma sana na ilionyesha dhahiri ni jinsi gani alivyokuwa akihitaji msaada wa Mike
Mike akavuta pumzi ndefu ,kikapita kimya cha dakika moja halafu akasema
“Nimekuelewa Happy.Nitakusaidia.Siwezi kukuacha wakati wa matatizo.Nitakusaidia Happy.Ninachohitaji kufahamu ni kama nyaraka zako zote za kusafiria unazo?
“Ndiyo Mike.Nyaraka zote ninazo hapa”
“Sawa Happy.Usijali nitakusaidia .Nitakupigia simu jioni ya leo kukufahamisha mchakato mzima ulivyo”
“Ouh Mike nakushukuru sana kwa kukubali kunisaidia” akasema Happy huku uso wake ukichanua kwa tabasamu
“Ni wajibu wangu kukusaidia Happy na nitafanya hivyo.Nitaongea nawe tena jioni ya leo kwa kirefu zaidi”
“Ahsante Mike” akasema Happy na kukata simu
“Ouh Gosh ! Siamini kabisa kama Mike amekubali knisaidia. Nasikia aibu sana kumuomba msaada Mike lakini kwa wakati huu nimekwama na ni yeye pekee anayeweza kunisaidia.Ninaamini Marekani nitaweza kuishi kwa amani bila bughudha.Ouh Mungu wangu naomba unisaidie ili Mike asiweze kubadili mawazo yake.” Akawaza Happy
Wakati Happy akiwa katika lindi la mawazo lililochanganyika na furaha mara kengele ya mlangoni ikalia. Haraka akajipangusa machozi na kuelekea mlangoni.Alikuwa ni baba yake mzee Kibaho aliyetoka kuvinjari mitaa ya jiji hili la Kigali
“Ouh Dady..!!” akasema Happy na kumkumbatia baba yake.
“I missed you dady” akasema Happy.Baba yake akamtazama kwa makini usoni
“Ulikuwa unalia? akauliza mzee Kibaho .Happy akakaa kimya
“Happy una tatizo gani? Siku zote nimekuwa nikikwambia kwamba kama una tatizo lolote usisite kuniambia”
“Ni kweli baba nilikuwa nalia lakini machozi ya furaha.
“Machozi ya furaha?
“Ndiyo baba”
“Umefurahi nini leo?
“Dady kwanza kabisa napenda sana nikushukuru kwa upendo wako mkubwa kwangu.Dady umekuwa nami katika matatizo yangu.Hujawahi kuniacha hata sekunde moja toka nilipoanza kuandamwa na matatizo.You are the best dady in the whole world.I’m proud to be your daughter.” Akasema Happy na kumfanya mzee Kibaho atabasamu
“dady umekuwa nami hata katika nyakati zile ambazo hakuna mwingine aliyethubutu.Kazi uliyoifanya ni kubwa na ninadhani ni wakati wako sasa wa kupumzika”
“Happy unazidi kunichanganya.Hata siku moja sijawahi kuchoka wala sintachoka kuwa nawe kwani ni jukumu langu kuhakikisha kwamba siku zote binti zangu wanakuwa na furaha.”
“Nafahamu hilo dady na ndiyo maana nasema kwamba wewe ni baba wa kutiliwa mfano duniani.Nimesema kwamba ni wakati wako wa kupumzika kwa sababu nimeamua kuondoka Kigali
“Unaondoka Kigali? Mzee Kibaho akashangaa
“Ndiyo dady.Kigali ni mji mzuri na ninapapenda sana na ningependa kama maisha yangu yote yaliyobaki ningeishi hapa lakini kuwepo kwangu hapa kutaendelea kunikumbusha tukio lile.Baada ya kufikiri sana nimeamua ili niweze kulisahau kabisa tukio lile basi niende kuishi mbali na nyumbani,mahala ambako sifahamiki na sintaweza kukutana na mtu yeyote anayenifahamu.Nataka niyaanze maisha yangu mapya.Nataka nisahau yale yote yaliyonipata japokuwa najua si kazi rahisi lakini nitajilazimisha kufanya hivyo .Maisha yangu mapya nataka kwenda kuyaanza mbali kabisa mahala ambako ni familia yangu pekee watapafahamu”
“Happy nashukuru sana kwa maamuzi hayo.Siku zote hilo limekuwa ni wazo langu kwamba ukaanze maisha mbali kabisa na nyumbani ikiwezekana nje ya afrika.Ni wapi umefikiria kwenda ili tuanze mchakato wa Safari.?
“Ouh dady.Huna haja ya kusumbuka.Tayari nimekwisha pata msaada .Nitakwenda kuishi Marekani”
“marekani?
“Ndiyo baba”
“marekani yuko Mike na ukumbuke bado atakuwa na hasira kwa mambo yaliyomtokea Tanzania.Nina wasi wasi anaweza akakufanyia kitu kibaya cha kulipiza kisasi”
“hapana baba.Huwezi kuamini kwamba Mike ndiye anayenisaidia mimi katika mchakato huu wa kurejea Marekani”
“Happy…!!!!” akastuka mzee Kibaho
“Usiogope baba.Tayari nimekwisha ongea naye na ameniahidi kunisaidia.”
Mzee Kibaho akamtazama mwanae kwa makini na kusema
“Do you trust him?
“Yes dady ! I trust him.Mike ananipenda sana na hawezi kukataa kunisaidia”
“Najua Mike bado anakupenda na anaweza kuwa amekubali kukusaidia kwa matumaini kwamba mtarejesha mahusiano yenu.Naomba nisikie toka kwako je bado unampenda Mike na uko tayari kurudana naye?Vipi kuhusu Patrick?..akauliza mzee Kibaho.Haoppy akafikiri kidogo na kusema
“I don’t know dady… I real don’t know what going to happen there.Kuhusu Patrick I think its right time now that I let him go.Matatizo niliyoyapata katika kipindi hiki kifupi nilichokutana naye yametosha na sintaweza kuvumilia zaidi.Dady nimekuwa ni mtu wa kulia kila siku kutokana na majanga yasiyokwisha.Inauma kusema lakini ni ukweli ulio wazi kwamba mimi na Patrick hatuwezi kuwa pamoja tena.NI vyema kama tutatengana kwa sasa.Ninaumia sana kwa kuamua kuondoka na kumuacha Patrick gerezani kwa kosa nililolisababisha mimi lakini sina namna ya kufanya siwezi tena kurejea Tanzania.Nina hakika Savanna atahakikisha kamba hafungwi gerezani.Savanna amenihakikishia kwamba Patrick atakuwa huru na ataendelea na maisha yake.Patrick told me to put a trust in her and I trust her. It hurt so much dady.All these years I’ve been dreaming that some day I’ll be married to Patrick but now I have to forget him.”” akasema Happy huku machozi yakimtoka.Kikapita kimya kirefu mzee Kibaho akasema
“Nakubaliana nawe Happy ni kweli yawezekana wewe na Patrick haikupangwa muwe pamoja.Ni vyema kama utakwenda kuishi mbali naye na kujitahidi kumsahau.Vipi kuhusu wale wanaharamu waliokufanyia udhalilishaji ule? Uko tayari kuliongelea suala hilo kwa sasa?
“No dady .I’m not ready.Thats the part of my life I’m trying to forget”
“Ok Happy usijali.Utaliongelea suala hilo pale utakapokuwa tayari”
Happy akainuka pale alipokuwa amekaa akaenda dirishani akatazama nje kisha akasema
“I’ll never be ok without Patrick.But then I have to live my life without him.It hurt so much dady……” Happy akashindwa kujizuia akazidi kulia
Tayari kiza kimetanda jijini Dar es salaam,ndani ya mkahawa mmoja maarufu sana jijini Dar es salaam,watu watatu,wanawake wawili na mwanaume mmoja walikuwa wameizunguka meza iliyokuwa imesheni vinywaji vikali
Mwanamke mmoja aliyekuwa na sigara mkononi akapuliza moshi mwingi hewani na kusema
“Khumalo tumekuja kama ulivyotutaka tuonane jioni ya leo” akasema Yule mwananmke na kuchukua glasi yake ya mvingo akapiga funda kubwa.Khumalo akawatazama wanawake wale kisha akasema
“Loniki na Linah ,nimewaiteni hapa ili kuwapeni taarifa ya maendeleo kuhusiana na kazi mliyonikabidhi.Kama mnavyokumbuka ,makubaliano yetu yalikuwa ni kuwashughulikia watu wawili waliohusika katika kifo cha ndugu yenu,.Watu hawa ni Patrick na Happy.Kwa mujibu wa Loniki ulitaka watu hawa wauawe lakini nilikushauri kwamba suala la kuua mmoja wao kati ya Hapy au Patrick kwa wakati huu lingeweza kuleta utata mkubwa na lingeonekana kabisa ni tukio la kulipiza kisasi.Nashukuru mlikubaliana na ushauri wangu na na kazi ya kwanza ikafanyika. Happy alishughulikiwa na nyote mkishuhudia.Ninathubutu kusema kwamba tulifanikiwa sana lengo letu kwa Happy kwani toka picha zile na video kutolewa Happy amepotea na hajulikani alipo.Vijana wangu wamekuwa wakimtafuta lakini hakuna anayefahamu mahala alipo.Kuna tetesi vile vile kwamba alijaribu kujiua kwa kunywa sumu lakini hakuna aliyepatikana kulithibitisha hilo kwani hospitali ile aliyotibiwa wamegoma kata kata kuthibitisha taarifa hizo.Kuhusu Patrick tulifanikiwa kumpekekea picha za Happy na alipoziona nusura apandwe na uchizi.Nina hakika kwamba tumefanikiwa kuyavunja mahusiano ya watu hawa na hivi sasa watu hawa wote wawili watakuwa katika mateso makubwa sana.Happy akiteseka kwa picha zile na Patrick akiteseka kwa kumuona mpenzi wake akifanya jambo kama lile. Jana usiku nilipokea simu toka kwa Linah akiniambia kwamba Loniki bado hajaridhishwa na jambo tulilolifanya na anataka Patrick na Happy wauawe.” Khumalo akanyamaza kidogo akanywa mvinyo na kuendelea
“Loniki naomba niwe wazi kwako kwamba suala la kumuua Patrick kwa sasa limekuwa gumu kidogo kwa sababu ulinzi umeimarishwa sana pale gerezani toka alipopelekewa picha zile za Happy na akazua tafrani kubwa.Kwa sasa wanaoruhusiwa kuonana naye ni mawakili na familia yake tu.Ninashauri kwamba suala hili la kumuua Patrick au tulivutie subira kwanza ili tuweze kutafuta namna bora kabisa ya kuweza kuutekeleza mpango huu.Endapo tutataka kulazimisha jambo hili linaweza kutuletea matatizo”
Kauli ile ya Khumalo haikuonekena kumfurahisha Loniki
“Ouh gosh..!!” akasema Loniki na kukaa kimya
“Mbona umestuka Lonny? Akauliza Khumalo
“Damn you Khumalo ! laiti ungejua ni namna gani ninavyosubiri usiku na mchana kuona watu hawa wakifutika toka katika uso wa dunia usingetamka maneno hayo uliyoyatamka”
“Nahafahamu Loniki,lakini naomba ufahamu kwamba mimi ndiye uliyenikabidhi kazi na ndiye ninayefahamu ugumu wa kazi yenyewe.Hii si kazi ya kuiendea haraka.”
“Khumalo naomba usianze kuniletea hadithi zako.I’ve paid you a lot of money for this job ,so do your job..I want Patrick and Savanna dead !! ..” akasema Loniki kwa ukali.Khumalo akamtazama,akainua glasi na kupiga funda moja na kusema
“Lonny,naomba ufahamu kwamba nilikubali kuifanya kazi hii kwa heshima ya Linah.Naomba vile vile ufahamu kwamba kazi hii nimeifanya kama msaada tu kwa sababu kazi kama hii mimi huifanya kwa milioni mia mbili na zaidi.Nimekwambia haya yote ili ufahamu kwamba sijaifanya kazi hii kwa pesa. Na endapo ukihitaji fedha zako unaweza ukaniambia nikakurejeshea na ukatafuta watu wengine wa kukufanyia kazi yako” akasema Khumalo.
“Jamani naomba tusifike huko.Loniki naomba umsikilize Khumalo anavyosema.Ushauri wake mimi binafsi naona ni mzuri tu.Tujipe muda ili tuweze kujipanga vizuri zaidi kwani hata kazi iliyofanyika ni kubwa na inatia matumaini.Patrick na Happy wote kwa pamoja wameumia sana na nina hakika hawatakuwa pamoja tena “ akasema Linah
“ Linah hujui ni namna gani nilivyokuwa nahitaji kuona Patrick na Happy wameuawa kabla sijarejea London.Kamwe moyo wangu hautakuwa na amani kumuona Patrick akiendelea kuvuta hewa hii safi wakati mdogo wangu akioza kaburini”
“Usihofu Lonny.Hata kama hautakuwepo mimi nitakuwepo kuusimamia mpango huu.Unaweza ukawa Uingereza lakini tukafanya kila kitu sisi tuliobaki huku.Ninakuahidi mimi binafsi nitashirikiana na Khumalo kwamba nitahakikisha lazima Patrick na Happy wanauwa na tunalipa kisasi kwa kifo cha Vero “ akasema Linah na kauli ile ikampa moyo Loniki na kumfanya akubaliane naye japo kwa shingo upande.
MIEZI SITACHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ni siku iliyotawaliwa na kijua kikali kama ilivyo kawaida ya jiji la Dar.Pilika pilika katika jiji hili lenye shughuli nyingi ziliendelea kama kawaida.Katika mahakama ya kisutu kulikuwa na idadi kubwa ya watu tofauti na ilivyozoeleka.Ongezeko hili wa watu lilitokana na minong’ono iliyokuwa imeanza kusambaa kwamba huenda Patrick ambaye anakabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia,angepatiwa dhamana siku ya leo baada ya taratibu zote kukamilika.Kwa muda wa miezi sita sasa toka Patrick alipoanza kushikiliwa na polisi kwa tuhuma za kusababisha mauaji,kesi hii imekuwa ikipewa umuhimu mkubwa sana na vyombo vya habari na hasa kutokana na miss Tanzania Happy Kibaho kutajwa kuhusika katika ugomvi uliosababisha kifo cha Vero.Kutokana na kutangazwa sana na vyombo vya habari watu wengi walikuwa wanaifuatilia ili kujua nini hatima yake.
Wengi wa watu waliofika walitegemea kumuona miss Tanzania aliyevua taji lake Happy Kibaho akiwa mahakamani.Toka picha na video yake ya utupu kuchapishwa na kusambaa mtandaoni Happy alipotea ghafla na hakuna aliyefahamu mahala alipo hivyo wengi walitegemea pengine angeweza kuonekana mahakamani siku ya leo.
Hatimaye kama ilivyokuwa imetegemewa na wengi,saa saba za mchana Patrick alipatiwa dhamana baada ya masharti yote yanayohitajika kutimizwa.Kilikuwa ni kipindi cha furaha sana hasa kwa familia yake,ndugu jamaa na marafiki.Ilikuwa ni kama ndoto pale Patrick aliposhikwa mkono na Savanna na kuthibitishiwa kwamba yuko huru kuondoka.Hakuamini macho yake.
“Savanna thank you very much.” Hilo ndilo neno pekee aliloweza kulitamka Patrick kwa wakili huyu mahiri ambaye amekuwa akimtetea katika kesi hii.Patrick akasalimiana pia na mawakili wengine ambao kwa pamoja wanaunda jopo la mawakili wanaomtetea na kisha taratibu huku akiwa ameongozana na Savanna wakatoka nje ya jengo la mahakama ambako aliendelea kusalimiana na watu mbali mbali mbali waliofika mahakamani.Wakati akiendelea kusalimiana na watu mbali mbali ,ghafla akastuka baada ya kuiona sura yenye tabasamu ya mwanadada mrembo na kuufanya moyo wake kuanza kudunda kwa kasi.Alikuwa anatazamana na Sarah dada yake Vero.Kwa sura Sarah na Vero walikuwa wanafanana sana kiasi kwamba ungeweza kudhani ni mapacha
Sarah ambaye alikuwa anatabasamu na kumkumbusha Patrick lile tabasamu alilolizoea la Vero akamsogelea na kumkumbatia.
“Pole sana Patrick.Usijali Mungu atakusaidia na mambo haya yatakwisha.” Akasema Sarah na kumshangaza sana Patrick ambaye alikosa neno la kusema midomo yake ilikuwa inamtetemeka.Hakutegema kama Sarah angeweza kuongea naye kistaarabu namna ile hasa baada ya kusababisha kifo cha mdogo wake.
“Sarah nashukuru sana” Patrick akasema.Sarah akatabasamu na kusema
“Patrick tutaongea siku nyingine kwa sasa unahitaji mapumziko.” Akasema Sarah halafu wakaagana akaondoka zake.Baada ya Patrick kusalimiana na watu wengi waliokuja kumpa pole siku hii ya leo,Savanna akamshika mkono na kumuongoza hadi katika gari lake na ndugu wengine nao wakaingia katika magari yao na kuondoka pale mahakamani.Patrick alikuwa amegeuza shingo yake akiangalia nje na mara akavuta pumzi ndefu
“Ouh my gosh ..!!! “ akasema Patrick akionekana kustushwa na kitu Fulani
“Patrick whats wrong? Akauliza Savanna
“Bado naona ni kama muujiza vile leo nimerejea tena uraiani.Sipati neno la kukushukuru Savanna.Ni Mungu pekee ndiye atakayekulipa” akasema Patrick
“Ouh Patrick plase don’t say anything.Ni wajibu wangu kufanya hivi na huna sababu ya kunishukuru” akasema Savanna huku akitabasamu
“Unanipeleka wapi,nyumbani kwangu au kwa mama? Akauliza Parick
“Patrick ,haitakua vizuri kama ukienda nyumbani kwako kwa sasa.Nyumba ile ina kumbukumbu nyingi ambazo zitakukumbusha historia ya wewe na Vero ambayo unajitahidi kuisahau.Nyumbani kwa mama nako kuna kumbukumbu nyingi ambazo zitakukumbusha kuhusu baba.Unatakiwa kwanza kuwa tayari kukabiliana na hayo yote.Nashauri kwanza upate mapumziko halafu tutakwenda nyumbani kwa mama lakini kwa sasa utakwenda kuishi kwangu .Nimekuandalia chumba maalum.Pale utapata kila kitu unachokihitaji hadi hapo utakapojisikia kuwa tayari kurejea kwako” akasema Savanna.Patrick akatabasamu
“Nilipenda sana kufika nyumbani kwa mama siku ya leo.Najua hata yeye pia ana hamu kubwa ya kuniona”
“Nyumbani kwa mama utakwenda lakini kwanza unatakiwa ukaoge,upate chakula,upumzike kidogo halafu ndipo uwe tayari kuonana na mama”
“Ok Savanna.Wewe ndiye kiongozi wangu kwa sasa.Siwezi kukupinga kwa lolote” akasema Patrick huku akicheka na kumfanya Savanna naye acheke
“Simu hii hapa mpigie Alois na umtaarifu kwamba utakwenda nyumbani kwa mama jioni ya leo” akasema Savanna.Patrick akaichukua simu ile na kumpigia Alois akamtaarifu kwamba atakwenda kuonana nao jioni.
* * * *
Geti la rangi nyeupe likafunguliwa na gari aina ya Range rover vogue likaingia katika jumba la kifahari lenye rangi nyeupe.Milango ikafunguliwa akashuka Savanna na Patrick
“Karibu nyumbani Patrick” akasema Savanna
“Ahsante sana Savanna.Una nyumba nzuri sana” akasema Patrick huku akitabasamu.Waliingia ndani ya sebule kubwa
“Jisikie nyumbani Patrick” akasema Savanna
“Nashukuru sana Savanna.Nyumba yako nzuri mno” akasema Patrick huku akitabasamu.Mtumishi wa ndani akafika na kuwahudumia vinywaji.
Baada ya maongezi kidogo,Savanna akampeleka Patrick katika chumba maalum kilichoandaliwa kwa ajili yake
“Patrick, hiki ndicho chumba chako.Nimekiandaa maalum kwa ajili yako..Utaishi hapa hadi hapo utakapojisikia kurejea katika makazi yako.Nimejaribu kuweka karibu kila kitu unachokipenda.Katika kabati kuna nguo nilizokuandalia na sina hakika kama nimekosea vipimo” akasema Savanna na wote wakacheka halafu Savanna akamuacha Patrick na kwenda chumbani kwake .
Patrick aliingia bafuni na kabla ya kuoga akasimama kwanza na kuzama katika mawazo
“Hatimaye nimekuwa huru tena.Naona ni kama ndoto lakini huu ndio ukweli nimerudi tena nyumbani baada ya kusota gerezani kwa muda wa miezi sita.Ama kweli maisha yanaweza kubadilika ndani ya sekunde moja kama yalivyobadilika kwangu.Sikuwahi kuota kma maisha yangu yangebadilika namna hii” akawaza Patrick na mara sura ya Vero ikamjia kichwani
“Sura hii ya Vero itaendela kuniandama kwa muda mrefu sana na kuifuta sura hii kichwani kwangu itanichukau muda pia” akawaza Patrick
Baada ya kuoga akajumuika na Savanna wakapata chakula pamoja halafu akarejea chumbani kwake kupumzika.
“Ni muda mrefu sijalala katika sehemu nzuri kama hii.I missed this life a lot.Shukrani za pekee zimwendee Savanna ambaye amepambana na kuhakikisha ninapata dhamana.Savanna ni mwanamke wa shoka.Nina deni kubwa kwake.Amenionyesha kwamba yeye ni rafiki wa kweli kuliko hata wale niliowaamini kwa moyo wangu wote.Ni Mungu peke atakaye mlipa Savanna kwa wema wake huu mkubwa” akawaza Patrick
“Kwa sasa natakiwa kujipanga kwa ajili ya kuanza upya maisha yangu.Nimepoteza kila kitu.Nimepoteza kazi,nimewapoteza wapendwa wangu Vero na Happy , hata Andrew rafiki yangu mkubwa naye ameniacha na sina taarifa zake tena. Sijilaumu sana kwa kilichotokea bali napaswa kutuliza akili na kujipanga upya.Bado sijachelewa kuyapanga na kuyajenga upya maisha yangu bila ya wale niliowapenda .Tukio lililotokea limenifundisha mambo mengi sana na safari hii sitaki kurudia makosa.Nakiri nilifanya kosa kubwa kuachana na Vero.Sikupaswa kufanya vile.Vero alikuwa ni mwanamke aliyenipenda kwa moyo wake wote na siku zote alikuwa tayari kwa lolote kwa ajili yangu.Nilimpuuza,nikaupuuza upendo wake kwangu na kuamini kwamba Happy ndiye mwanamke ambaye nimepangiwa niwe naye katika maisha.Nilijidanganya sana.Mimi na Happy katu hatuwezi kuwa pamoja.Tumekwisha jaribu na imeshindikana na tayari nimemfahamu Happy ni nani.Nashukuru nimeweza kumuondoa moyoni mwangu na amebaki ni katika historia ya maisha yangu lakini moyo wangu haudundi tena kwa ajili yake.Alichokifanya kimenifanya nimvue thamani kabisa na hana nafasi tena moyoni mwangu” Akawaza Patrick halafu akafumba macho na kulala
Saa moja za jioni akiwa ameongozana na Savanna akawasili nyumbani kwa wazazi wake ambako baadhi ya ndugu walikuwa wamekusanyika ili kumpa pole kwa masahibu yaliyomkuta.Wote walijawa na furaha kubwa kwa Patrick kurejea tena nyumbani.Chakula kizuri kiliandaliwa,wakala na kunywa na ilipofika saa tano za usiku Patrick na Savanna wakaondoka kurejea nyumbani kwa Savanna ambako Patrick aliwekewa makazi yake ya muda
* * * *
Saa nne za asubuhi siku iliyofuata iliwakuta Patrick na familia yake katika kaburi la baba yao.Alois ndiye aliyeongoza sala fupi ya kumuombea marehemu baba yao halafu ukafuata wakati wa kuweka shada za maua.Patrick aliyekuwa amevalia suti nyeusi ndiye aliyekuwa wa kwanza kuweka shada la maua juu ya kaburi la baba yake.Akaliweka karibu kabisa na msalaba halafu akapiga magoti na kuliinamia kaburi
“Baba kokote uliko hivi sasa naomba unisamehe sana kwa mambo niliyoyafanya na kusababisha kifo chako.Sikutegemea kama maamuzi yangu yangetufikisha hapa.Ninasikia uchungu mkubwa sana ambao si rahisi kuuelezea.Baba nahitaji msamaha wako ili niweze kuondokana na mateso haya makubwa niliyonayo na nianze maisha mapya.Siku zote nitakuombea kwa Mungu ili aipumzishe roho yako mahala pema peponi Amina”
Baada ya kumaliza maombi yale mafupi ya kimya kimya akainuka na kuwapa nafasi ndugu zake wengine nao waweke shada zao za maua.Zoezi lile lilipokamilika Patrick na Savanna wakaingia garini na kuondoka kuendelea na ratiba nyingine ya siku hiyo.
“Kinachofuata sasa hivi kwa mujibu ratiba yetu tunaelekea katika kaburi la Vero” akasema Savanna
Walifika makaburini na Savanna akamuongoza Patrick hadi katika kaburi la Vero.
Hapa ndipo alipozikwa Vero” akasema Savanna.Patrick akaweka shada lake la maua na kuliinamia kaburi na machozi mengi yakamtoka.Savanna akasogea mbali kidogo na kumpa Patrick nafasi ya kuwa peke yake katika kaburi la aliyewahi kuwa mchumba wake.
“Anatia huruma sana Parick lakini hii ndiyo hali halisi ambayo lazima akabiliane nayo.” Akawaza Savanna
Baada ya dakika kumi za Parick kuliinamia kaburi la Vero akainuka.Macho yake yalikuwa mekundu na uso wake ulijaa machozi.Savanna akamsogelea na kumpa kitambaa
“its ok Patrick,Don’t cry anymore” akasema Savanna Patrick akafuta machozi.Akaendelea kulitazama kaburi lile kwa uchungu
“rest in peace Vero.You’ll always be in my heart” akasema Patrick halafu wakaondoka .
Toka makaburini ,Patrck na Savanna wakaendelea na safari yao hadi nyumbani kwa Patrick.Walinzi toka katika kampuni binafsi ya ulinzi ya Chem Chem security waliendelea kuilinda nyumba ya Patrick kwa kipindi chote ambacho Patrick alikuwa gerezani
“Welcome home Patrick” akasema Savanna huku akitabasamu.Patrick alishindwa kuzuia furaha yake alipoishuhudia nyumba yake namna ilivyokuwa imependeza.Ilikuwa imepakwa rangi nzuri nyeupe na kupandwa maua mengi kuizunguka.
“wow !! its incredible…!!!” akasema Patrick kwa furaha
“Nyumba yote ni salama.Imeendelea kulindwa na kampuni hii ya ulinzi kwa kipindi chote ulichokuwa gerezani.Niliingia nao mkataba wa mwaka mmoja wa kuendelea kuilinda nyumba yako na tayari fedha zote nimekwisha zilipa.Vile vile nyumba yote imepakwa rangi kwa nje.It looks beautiful,isn’t it?
“Savanna sijui hata niseme nini.Sijui nikushukuruje.The house looks so beautiful.Sikutegemea kama ningeikuta nyumba yangu katika hali hii.Ahsante sana Savanna kwa kunitunzia nyumba yangu.” Akasema kwa furaha Patrick na kuufungua mlango mkubwa akaingia ndani.Patrick alionekana kama anaiogopa nyumba yake.Hakutaka kugusa kitu chochote mle sebuleni.Walitoka sebuleni wakazunguka katika baadhi ya vyumba na hatimaye wakaingia katika chumba cha kulala cha Patrick.Mara tu walipoingia Patrick akastuka sana baada ya kuziona picha mbili kubwa zilizowekwa ukutani.Ilikuwa ni picha yake na Veronika.Alisimama kwa sekunde kadhaa akizikodolea macho picha zile kubwa
Juu ya kitanda kulikuwa na nguo za vero ambazo alizivua na kuziweka kitandani mchana wa siku ile ya kufariki kwake.Patrick akakumbuka dakika za mwisho akiwa na Vero mle chumbani.Vero alikuwa akimkumbatia kwa mahaba mazito.Alikumbuka namna walivyofanya mapenzi kwa mara ya mwisho na walipanga kuendelea tena jioni yake lakini Vero hakurejea tena katika chumba kile
“That’s the day I’ll never forget in my life.It’s the day that I made the biggest mistake of my life.Niliipoteza dhahabu ya thamani kubwa kwa mng’ao wa jiwe” akawaza Patrick huku machozi yakimlenga
“Savanna I need to be alone for a while” akasema Patrick na Savanna akatoka mle chumbani,Patrick akaufunga mlango halafu akapanda kitandani na kuzikumbatia nguo za Vero huku akilia
“Please forgive me Vero,forgive me“ akasema Patrick huku machozi yakimtoka.Alilia sana kisha akainuka na kwenda katika meza ya vipodozi iliyokuwa imesheni vipodozi vya kila aina alivyokuwa anatumia Vero.Akalifungua kabati kubwa na kuzikuta nguo nyingi za Vero ,akaanza kuitoa nguo moja baada ya nyingine na kuziweka kitandani.Kila nguo aliyoishika ilimkumbusha nyakati zile za furaha alizokuwa nazo akiwa na Vero.Alivikusanya vitu vyote vya Vero na kuviweka katika masanduku mawili makubwa
“Natakiwa kuvirudisha vitu hivi kwa ndugu zake.Kuendelea kuviweka hapa vitanifanya nishindwe kumsahau Vero na kuendelea na maisha yangu.Nitamtafuta Sarah na kumpatia vitu hivi vya mdogo wake” akawaza PatrickCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Itanichukua muda mrefu kurejea tena katika nyumba hii.Kwa sasa itanilazimu kuendelea kuishi nyumbani kwa Savanna.Ninahisi furaha na amini nikiwa pale.Savanna ananijali sana na anajitahidi kwa kila namna niweze kurejea katika maisha yangu ya kawaida.She’s a wonderfull woman” Patrick akatabasamu halafu akatoka na kuelekea sebuleni aliko Savanna.
“Savanna itanichukua muda sana kuweza kumsahau Vero .Kuna kumbu kumbu nyingi humu ndani zinazonikumbusha mbali na hasa dakika za mwisho nilizokuwa na Vero.Laiti ningejua kama ile ilikuwa ni siku ya mwisho ya Vero basi nisingefanya vile nilivyofanya.” Akasema Patrick
“Pole Patrick.Mambo haya yote yatakwisha japokuwa ni ngumu na itachukua muda kumsahau Vero lakini naomba ujitahidi kwa kila namna kuizoea hali hii na kuiona ya kawaida”
“Nitajitahidi Savanna.I’ll be ok” akasema Patrick halafu wakazungukia nyumba yake yote na walipomaliza wakaingia garini na kuondoka kurejea katika makazi ya Savanna
Siku zilizidi kusonga huku Patrick akijitahidi kujaribu kusahau mambo yote ya nyuma na kuanza maisha mapya.Bado aliendelea kuishi nyumbani kwa Savanna.Maisha ndani ya nyumba hii yalikuwa mazuri,aliishi yeye,Savanna pamoja na mtumishi wa ndani,.
Siku moja mwishoni mwa wiki Savanna alimuomba Patrick watoke kwa ajili ya matembezi.Walikwenda katika hoteli moja kubwa na tulivu iliyokuwa na ufukwe mzuri na msafi.Savanna alikuwa amejitahidi sana kwa kila namna alivyoweza ili kumsahaulisha Patrick yaliyopita na kumfanya awe na furaha lakini bado alionekana kuna jambo linamnyima raha.
“Patrick ni jambo gani hasa linalokunyima raha? Tafadhani naomba unieleze .Mimi ni rafiki yako na kama kuna jambo lolote ambalio linakufanya usie na furaha naomba unieleze mimi nitakusaidia.” Akasema Savanna wakiwa ufukweni.
“Savanna wewe ni zaidi ya rafiki yangu kwa hiyo siwezi kukuficha kitu.Kitu kinachoninyima raha ni pale ninapowaza kuhusu maisha yangu.Kama unavyojua nimepoteza kila kitu pamoja na mwelekeo mzima wa maisha yangu.Nimepoteza kazi yangu na mpaka sasa hakuna hata kampuni moja iliyoonyesha dalili za kuniajiri tena.Ninajiona kama nina laana vile lakini hata hivyo nahitaji kusahau kilichotokea na kuanza maisha mapya lakini kadiri siku zinavyozidi kwenda najikuta nikishindwa namna ya kuweza kuanza tena maisha yangu na kujitegemea mimi mwenyewe.Sijisikii vizuri ninapokutegemea wewe katika kila jambo”
Savanna akatabasamu na kusema
“Pole Patrick lakini hukupaswa kuumiza kichwa chako namna hiyo.Ulipaswa kunieleza kuhusu jambo hilo kwani tayari ninalifahamu hilo na nina mipango mizuri kwa ajili yako ila sikuweza kukueleza mapema kwa sababu nilikuwa nataka nikwambie wakati kila kitu kimekamilika.Kwa ufupi tu ni kwamba nimeanzisha kiwanda cha kusindika nyama na muda wowote kuanzia sasa kitaanza kazi.Wewe ndiye utakayekuwa meneja wa kiwanda hicho.
.majukumu yote ya uendeshaji wa kiwanda hiki yako juu yako kwa hiyo usiumize kichwa chako kuhusiana na ajira,you are a manager now.” Akasema Savanna huku akicheka.Patrick akashindwa kujizuia akasimama akamkumbatia Savanna kwa furaha.
“Savanna ni kitu gani nimekufanyia hadi ukanifanyia mambo yote haya? Nitakulipa kitu gani? Patrick akasema huku akimtazama Savanna
“Ni wajibu wangu kufanya hivi nifanyavyo Patrick na hutakiwi kunilipa chochote .Nina imani hata mimi ningekuwa katika hali kama yako ungefanya kama nifanyavyo mimi.Isnt it Patrick?
“Ndiyo Savanna .Ningefanya kama ufanyavyo.Nisingethubutu kukuona ukiwa katika hali kama yangu.Naomba nikiri kwamba ni hali ngumu sana lakini nimeweza kuvumilia na kufika hapa kutokana na jitihada za watu wachache wanaonuipenda na kunijali wakiongozwa na wewe Savanna ,watu ambao wamesimama nami toka dakika ya kwanza ya matatizo yangu na hadi leo bado wako nami.Nina deni kubwa kwako Savanna na sijui nitalilipaje.” akasema Patrick halafu akainamisha kichwa chini akazama katika mawazo ghafla.
“Patrick unawaza nini? Akauliza Savanna baada ya kumuona Patrick amebadilika ghafla
“Savanna nimekumbuka kesi yangu.Kila mara niwazapo kuhusu kesi hii ninashindwa kujizuia kuogopa.Ninafikiria itakuwaje endapo nitahukumiwa kifungo gerezani na kushindwa kutimiza malengo yangu.Sitaki kufungwa jela kwa sababu ya mtu asiyekuwa na thamani kwangu hata kidogo.”
“Patrick siku zote nimekuwa nikikwambia kwamba usiwaze chochote kuhusiana na kesi hii. Mambo yote niachie mimi na nitalishughulikia suala hili na litakwisha.I give you my word Patrick” akasema Savanna huku akitabasamu .Kikapita kimya cha dakika mbili kila mmoja akiwaza lake
“Patrick ..!! akaita Savanna.Patrick akamtazama usoni
“Kuna jambo ambalo nataka kukueleza”
“Jambo gani Savanna?
“Patrick najua ni namna gani unavyoumia kila siku moyoni kwa haya yaliyotokea.Ninayaona maumivu yako na kuyahisi na kunifanya na mimi pia niumwe kwa kukuona ukiwa katika hali hii ya mateso makubwa ya moyo.Patrick nafahamu kwamba si rahisi kuyasahau yaliyotokea na kuanza maisha mapya kwa haraka.Itachukua muda kuwasahau wapendwa wako,vero,Happy na baba yako.Hawa ni watu uliowazoea na kuwapenda lakini leo hii hawako tena nawe.Pamoja na kwamba kumbu kumbu zao bado zinakujia ,lakini ni wakati sasa wa kuwaacha waende na wewe uuruhusu moyo wako uanze maisha mapya.Its time now to let them go.Kuondoka kwao si mwisho wa maisha yako wala ndoto zako .Bado unayo maisha marefu na yenye furaha lakini pale tu utakapoufungua moyo wako na kuuruhusu uanze maisha mapya.Ufungue moyo wako sasa kwa wale wanaokupenda na kukujali na kuwa tayari kusimama nawe katika nyakati zote za shida au raha.Pamoja na yaliyotokea lakini bado unahitaji kuwa na marafiki na hata mtu ambaye unaweza tena kumwamini na kumkabidhi moyo wako.” Akasema Savanna.Patrick akamuangalia kwa makini halafu akatabasamu na kusema
“Unamaanisha nini Savanna unaposema mtu ambaye ninaweza kumwamini na kumkabidhi moyo wangu?
“Ninamaanisha kwamba you have to learn to love again.Only love can help you forget the past” Akasema Savanna na kumfanya Patrick atabasamu na kucheka kidogo
“Mbona unacheka Patrick? Ni kosa la jinai kupenda? Akauliza Savanna
“Si kosa la jinai lakini…………………………”
“ Lakini ……………? Akauliza Savanna
“Sina hakaika kama moyo wangu uko tayari kupenda tena Savanna.Kidonda nilichonacho moyoni kilichosababishwa na mapenzi kitachukua muda mrefu kupona..Nimeumizwa sana na pengine sintaweza kupenda tena.Pengine nitaishi maisha yangu yote yaliyobakia nikiwa mwenyewe.Sintavumilia tena maumivu yoyote ya kuumizwa.Kuna watu katika dunia hii hawajaumbwa ili kupenda na ninaamini mimi ni mmoja wao” akasema Patrick katika hali ya kukata tamaa kabisa
“Patrick nafahamu ni namna gani ulivyoumizwa. Sisi sote tunaumizwa na mapenzi .Lakini mimi bado nasisitiza kwamba kuuruhus moyo wako kupenda tena kutakusaidia sana katika kusahau mambo yaliyopita.Find yourself someone who truly loves you and I swear you’ll be Happy again” akasema Savanna
“Hata kama nikiamua kupenda tena ni nani nitakayempenda? Nani ambaye nitamuamini katika ulimwengu huu wa sasa na kumkabidhi moyo wangu tena? Savanna naomba niwe wazi kwako kwamba sioni sababu ya kupenda tena kwani kila mara nilipojaribu kupenda nimeishia kuumizwa moyo wangu tu.Nilimpenda mno Happy na nilikuwa tayari kufanya lolote kwa ajili yake,niliwahi hadi kuua kwa ajili yake lakini ona jeraha alilonitia moyoni..I’m hurt Savanna..’m deeply hurt.”Akasema Patrick.Savanna akamshika mikono na kumuangalia usoni.
“Patrick si wanawake wote ni wabaya na wanaweza kukuumiza kama ulivyoumizwa.Usiuamini ule msemo usemao samaki mmoja akioza na wote wameoza.Bado kuna wnawake wazuri ,wenye kukupenda ,kukujali na kukuthamini,wanawake ambao kwao una maana kubwa sana.Tafadhali usiufunge moyo wako kwa mwanamke kama huyu”
“Savanna hata wale niliokuwa nao Happy na Vero walinipenda kwa mioyo yao yote.Walinijali na kunithamini.Kwa ufupi ni kwamba sina tatizo na wanawake hata kidogo lakini sina uhakika wa kupenda tena kwa sababu niliwapenda kwa moyo wangu wote.Kuna nyakati ninahisi kama dunia inaniadhibu.The world has been so cruel to me so even if I’ll start a new relationship it wont work out and I’ll get hurt again.Sitaki kuumia tena” akaendelea kusisitiza Patrick
“Patrick,Mungu ametuleta hapa duniani tuyafurahie maisha na ndiyo maana akaumba mwanamke na mwanaume kwa hiyo si sahihi kusema au kuamini kwamba kuna watu ambao wameshushwa katika hii dunia kwa ajili ya kuishi wao wenyewe bila kuwa na mahusiano.Kama kuna watu wa namna hiyo basi Mungu angewaumba bila kuwa na jinsia” akasema Savanna halafu wote wawili wakacheka sana.Savanna akaendelea
“Ninavyoamini mimi ni kwamba kila mtu ana haki ya kuwa katika mahusiano labda upende mwenyewe kutokujihusisha na mahusiano kama vile watawa na makasisi lakini hata hao watawa wanaishi chini ya uangalizi maalum tena mkali ili kuwasaida wasiweze kuingia katika vishawishi vya kimahusiano.Tukirudi katika swala lako lingine,si kweli kwamba dunia imekuwa katili sana kwako ,dunia si mbaya hata kidogo ,dunia inatupenda wote na ndiyo maana wote tunavuta hewa sawa,inatupa mazao na kila kitu.Binadamu waishio juu ya dunia ndiyo wabaya na kwa upande wako ni kwamba you fell I love with wrong people.People whom you’re not meant to be with” akasema Savanna,Patrick akatabasamu halafu akasema
“Maneno yako yanaweza kuwa na ukweli Savanna kwa sababu kuna usemi usemao kwamba kila jambo linafanyika kwa sababu maalum.Inawezekana ni kweli nilipenda watu ambao hawakuwa sahihi kwangu.Hata hivyo nahitaji kulifikiri tena suala hili kabla ya kuamua kuingia katika mahusiano mengine na nina hakika inaweza ikanichukua muda mrefu sana.Kwa sasa nataka nielekeze nguv na akili yangu katika kazi yangu mpya” akasema Patrick
“Hilo ni jambo la msingi sana Patrick.Hutakiwi kuidhulumu nafsi yako.You need to be Happy and to be be Happy you need to love and be loved ” Akasema Savanna .Patrick hakujibu kitu
“It’s getting late Patrick.Twende tuondoke .Leo nataka tukaandae pamoja chakula cha usiku.Unakumbuka ni muda mrefu sana umepita toka tulipoandaa kwa pamoja chakula cha usiku?” Akasema Savanna
“Wow ! That’s great Idea.Ni siku nyingi sana sijaingia jikoni kupika .Nakumbuka sana nyakati zile tulizokuwa tukiandaa chakula pamoja. “ akasema Patrick huku akicheka kidogo
“Unapenda tupike nini kwa ajili ya usiku wa leo? Akauliza Savanna
“Kitu chochote utakachopenda tupike Savanna mimi niko tayari.” Akajibu Patrick na kumfanya Savanna atabasamu
“Today we’re going to have a very special dinner just for two of us.Lets make this night a wonderful and memorable one.” Akasema Savanna kisha wakaondoka.
Kabla ya kuelekea nyumbani walipita kwanza kununua vitu mbali mbali ambavyo wangependa kuvitumia kwa ajili ya usku huo.Walipofika nyumbani,waliingia jikoni na kuanza maandalizi kwa pamoja.Kitendo cha kushirikiana kuandaa chakula kile kilimpa Patrick furaha ya ajabu sana na kumkumbusha nyakati zile wakati bado alikuwa katika mahusiano ya sirina Savanna
Mpaka kufika saa mbili za usiku,chakula kilikuwa tayari.Savanna akamuomba Patrick amuachie yeye kazi zilizobakia na yeye aende akajiandae kabla ya kupata mlo huo wa usiku wazo ambalo Patrick alilikubali na kwenda kujiandaa
“Tonight is the night .I’ve been waiting for this night for so long.Leo hii Patrick lazima awe wangu tena” akawaza Savanna huku akitabasamu baada ya Patrick kuondoka mle jikoni
“Baada ya usiku wa leo nitaamka nikiwa mikononi mwa mwanaume ninayempenda sana kuliko wote.After tonight I’ll be complete and no one than death can separate us again.Patrick will be mine forever” akawaza Savanna wakati akiandaa meza
Kwa upande wake Patrick baada ya kuingia chumbani kwake,moja kwa moja aliingia bafuni akajimwagia maji
“Namshukuru sana Savanna kwani kwa sasa najisikia vizuri na nina nguvu ya kuendelea na maisha yangu mapya. Bila yeye sijui ningekuwa katika hali gani hivi sasa” akawaza Patrick halafu akaendelea kujimwagia maji .Wakati akiendelea kuoga akakumbuka kitu halafu akatabasamu
“ Katika siku zote ambazo nimekuwa na Savanna ,siku ya leo nimejikuta nikiwa na furaha sana na hasa zoezi la kupika pamoja,zoezi ambalo limenikumbusha nyakati zile nilizokuwa naye katika mahusiano ya siri .Niliwahi kuwa katika mapenzi mazito na Savanna,nakumbuka wakati ule nilikuwa na furaha sana japokuwa nilikuwa tayari katika mahusiano na Vero.Savanna alinionyesha mapenzi ya dhati na moyo wangu ulifurahi .Nilikubali kuachana naye kwa shingo upande pale alipompata George.Kama nisingekuwa katika mahusiano na Vero kwa wakati ule basi tayari ningekuwa nimekwisha funga ndoa na Savanna kwani ni mwanamke mwenye kila sifa ya kuwa mke bora .Zaidi ya yote bado ananipenda kwa dhati ya moyo wake na ndiyo maana amejitolea kwa hali na mali katika kuhakikisha kwamba suala la kesi yangu linakwisha na ninakuwa huru tena.” Akawaza Patrick na kisha akaendelea kuoga
“Hata mimi toka ndani kabisa ya moyo wangu ninakiri kwamba bado ninampenda Savanna.Ninahisi yeye anaweza kuwa ndiye mwanamke anayenifaa,lakini kutokana na msaada mkubwa alionisaidia ninasita kuziamsha tena hisia za mapenzi kati yetu” akawaza Patrick halafu akaendelea kuoga.Sura ya Savanna wakiwa jikoni wakipika pamoja ikamjia kichwani akatabasamu
“She have a pretty face,macho mazuri,shepu nzuri na sauti kama malaika.Savanna ni mwanamke bora na mzuri kupita kiasi” akawaza Patrick kisha akatoka mle bafuni
Savanna aliendelea na zoezi la kuandaa meza kwa ajili ya chakula cha usiku.Alizima taa na kuwasha mishumaa na kupafanya mahala pale pawe pa kuvutia sana.Alipohakikisha kila kitu kiko sawa akaenda chumbani kwake kujiandaa kwa ajili ya usiku huo ambao aliupanga uwe maalum kwake
* * * *
“Huu ni usiku wangu wa pekee kabisa ni usiku ambao nimekuwa nikiuota kwa muda mrefu.Ni usiku ambao nitalala nikiwa kifuani kwa Patrick.” Mawazo hayakumkauka Savanna wakati akimalizia kujipaka rangi ya mdomo halafu akajitazama katika kioo na kutabasamu.Alikuwa amependeza sana.Alivaa gauni refu jepesi la rangi jeupe ambalo lilionyesha hadi nguo ya ndani.Akageuka akajitazama na kutabasamu halafu akachukua uturi wa gharama kubwa na kujipulizia kisha akatoka mle chumbani.Patrick alikuwa bado chumbani kwake wakati Savanna alipowasili sebuleni.Savanna akampigia simu na kumtaarifu kwamba muda wa kupata chakula cha usiku umewadia.
Patrick akatoka chumbani na kuelekea sebuleni.Mara tu alipoingia ,akapigwa na mshangao kwa alichokikuta.Sebule ilikuwa imebadilika na kuwa na mandhari ya kuvutia mno.Taa zote zilikuwa zimezimwa na kilichokuwa kinawaka ni mishumaa iliyopapendezesha mahala pale na kupafanya pa pekee kabisa.
“Wow ! amazing “ akasema Patrick huku akitabasamu
“karibu Patrick” akasema Savanna kwa sauti laini huku akiinuka pale sofani alipokuwa amekaa na kwenda kumshika Patrick mkono akaumuongoza kuelekea katika meza ya chakula.Japokuwa mwanga ulikuwa hafifu lakini Patrick aliweza kulishuhudia vyema vazi la Savanna na kusisimka mwili kwani aliweza kuiona hadi nguo ya ndani aliyokuwa amevaa .Mapigo ya moyo wake yakaanza kumuenda kasi.Ni muda mrefu sasa umepita hajawahi kusisimkwa mwili.Savanna na Patrick wakaangaliana kwa sekunde kadhaa Savanna akauliza
“Mbona unaniangalia hivyo Patrick?
“You are so amazing tonight” akajibu Patrick
“Thank you” akajibu Savanna kisha wakaelekea katika meza iliyokuwa imesheheni vyakula vya aina mbali mbali walivyoviandaa
“Karibu chakula Patrick,chakula ambacho ni maalum kwetu.Just for tonight let us forget the world and enjoy the night.Let us make our own world ” Akasema Savanna.
Waliendelea kula taratibu huku wakisindikizwa na muziki laini.Kila Patrick alipomtazama Savanna alisisimka mwili wake kutokana na kuzishuhuhudia chuchu za kuvutia za Savanna ambazo zilikuwa zinaonekana kwa urahisi kutokana na vazi lile alilokuwa amevaa lililoonyesha kila kitu.Taratibu akahisi mtafaruku katika sehemu za ikulu ambazo zilikuwa zimechachamaa kupita maelezo.
“Gosh ! haya ni majaribu makubwa sana.Savanna ananiweka katika wakati mgumu mno.Ouh jamani nitafanya nini mimi? Akawaza Patrick huku akiendelea kumtazama Savanna ambaye alikuwa ameinamisha kichwa.Ghafla akainua kichwa na kugundua kwamba Patrick alikuwa anamuangalia akatabasamu
Baada ya kumaliza kula Savanna akamuomba Patrick waelekee katika sofa lililokuwa na meza ndogo pembeni iliyokuwa na chupa tatu za mvinyo pamoja na glasi mbili.
“Na tunywe kwa furaha huku tukitakiana maisha marefu” akasema Savanna huku akiisogelea glasi yake iliyokuwa na mvinyo karibu na Patrick wakagonganisha glasi.Waliendelea kunywa na kadiri muda ulivyozidi kusonga ndivyo maongezi na vicheko vilivyozidi.Walikumbushana mambo mengi na hasa nyakati zile walizokuwa wapenzi,Ulikuwa ni wakati wa furaha mno kwa wote.Maongezi yalikolea na kulikuwa na kila dalili kwamba walianza kulemewa na kilevi.Savanna akainuka pale alipokuwa amekaa na kuelekea katika redio akaweka muziki laini sana halafu akamfuata Patrick
“Patrick can we dance?
Bila ubishi Patrick akainuka akakumbatiana na Savanna wakaanza kucheza.Patrick akahisi kama chaji za umeme zinapita mwilini mwake pale kifua cha Savanna kilichobeba chuchu laini kilipokigusana na kifua chake.Kadiri muziki ulivyokuwa ukienda ndivyo walivyojikuta wakikumbatiana kwa nguvu zaidi.Muziki ulimalizika lakini bado waliendelea kukumbatiana kwa nguvu .Taratibu Savanna akaupeleka mkono wake wa kulia chini kidogo ya kiuno cha Patrick na kukutana na kitu kigumu kilichotuna.Taratibu na kwa ufundi Savanna akakishika kitu kile kilichotuna na kumfanya Patrick atoe mguno na kuhema kwa nguvu kisha akampiga Savanna busu zito lililomfanya aweweseke.Taratibu Patrick akausogeza mdomo wake karibu na Savanna na kuutoa ulimi wake na zoezi la kunyonyana ndimi likaanza huku wakishikana na kutomasana sehemu mbali mbali za mwili.Wote wawili walikuwa wakihema kwa nguvu na kila mmoja akiongea maneno ambayo mwenzie hakuweza kuyaelewa.
“Ouh,Ouh,ouh Patrick take ..m.me..to ..parr….r..paradise” akasema Savanna kwa sauti yenye kukwama kwama.Alikuwa hajiwezi tena kwa raha alizozisikia.Patrick akamuinua na kwenda naye chumbani.Kilichoendelea huko ni miguno na vilio vya utamu uliopitiliza
* * * *
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mlio wa saa ya ukutani ndio uliomstua Patrick akafumbua macho na kutazama ukutani kulikokuwa na saa kubwa.Ilikuwa ni saa mbili za asubuhi.Pembeni yake alikuwa amelala Savanna akiwa katika usingizi mzito.Patrick akamtazama na kutabasamu
“Gosh ! Usiku wa jana kamwe sintausahau katika maisha yangu.Sijawahi kuwa na usiku wa kipekee kama ule.Nilijihisi kama nimetoka kabisa katika ulimwengu huu.Ouh Savanna I didn’t know how much I still love you.Umenirudishia tena furaha yangu iliyopotea.” akawaza Patrick halafu akainama na kumbusu Savanna shavuni na mara Savanna akafumbua macho.
“Ouh Patrick thank you so much.You are so sweet” akasema Savanna
“Thank you for the wonderfull night.Sijawahi kuwa na usiku mzuri kama wa jana.Nimekuwa nikiuota usiku kama ule kwa miaka mingi.Ahsante sana Patrick..Ahsante sana” akasema Savanna akamvuta tena Patrick kwake na kumpa busu zito.Patrick akatabasamu na kusema
“Savanna you are wonderfull,you are amazing.Baada ya usiku wa jana,najiona mtu mpya.Savanna naomba nitamke kwamba najiona ni kama mfalme mwenye nguvu mwenye uwezo wa kufanya chochote nikiwa nawe.Umenipa nguvu na matumaini.Siku zote nitaendelea kumshukuru Mungu kwa kunikutanisha nawe.Nina uhakika mkubwa kwamba kukutana kwetu haikuwa kwa bahati mbaya.Mungu alikuwa na makusudi yake na ndiyo maana leo hii ninathubutu kutamka kwamba pamoja na kwamba tuliachana na kila mmoja akaendelea na maisha yake ,lakini bado moyoni mwangu una nafasi ya kipekee kabisa.Bado ninakupenda Savanna na hata siku moja upendo wangu kwako haujapungua.Sitaki kubishana na moyo wangu kwamba wewe ndiye mwanamke ambaye umeumbwa kwa ajili yangu.Savanna ninaombi moja kwako” Patrick akanyamaza akamtazama Savanna ambaye machozi yalikuwa yanamtoka
“Omba chochote Patrick nitakupatia” akasema Savanna huku akifuta machozi yale ya furaha
“Savanna pengine ombi langu kwako linaweza kuwa gumu hasa kutokana na matukio ambayo yamekuwa yananitokea lakini napenda kuwa wazi kwako kwamba ninaomba nafasi nyingine katika moyo wangu.Ninakubaliana na maneno uliyoniambia jana kwamba natakiwa kuufungua moyo wangu tena.Nimeufungua moyo wangu kwako na nina imani wewe ndiye pekee ambaye utaweza kunisahaulisha mambo yote yaliyopita na kunifanya niwe na maisha yenye furaha sana hapa duniani.Naomba uwe malkia wangu Savanna.” Patrick aliyasema maneno haya taratibu na kwa hisia kubwa.Mara tu alipomaliza kusema ya moyoni mwake,Savanna aliinuka kwa kasi na kulitupa shuka pembeni kisha akamkumbatia Patrick kwa nguvu.Alikuwa akiweweseka huku akimpiga Patrick mabusu mfululizo
“Patrick unataka kunipa uchizi.Kwa muda mrefu sana nimekuwa nikiota kuusikia mdomo wako ukitamka meneo haya mazito uliyonitamkia sasa hivi.Patrick nashukuru sana na sina cha kusema zaidi ya kukuhakikishia kwamba siku zote moyo wangu ulikuwa na nafasi kwa ajili yako pekee.Niliamini siku moja mimi na wewe tutakuwa pamoja hata kama si katika maisha haya basi katika maisha mengine baada ya kufa.Nimekuwa nikimuomba sana Mungu kwa jambo hili lakini hatimaye leo hii limekuwa kweli.Huu ni kama muujiza kwangu.Patrick nakukabidhi moyo wangu na kila kilicho changu.Naomba unitawale ee mfalme wangu.Niamuru chochote nitakutii” akasema Savanna kwa hisia kali huku akitokwa na machozi ya furaha.Ilikuwa ni kama ndoto.Hakuamini kama ile ndoto yake ya siku nyingi ya kuwa na Patrick leo hii imekuwa kweli.Walikumbatiana kwa furaha huku wakiepeana mabusu mfululizo na taratibu wakajikuta wakianza kuhama katika ulimwengu huu na kwenda katika ulimwengu uliojaa mahaba mazito.Migumo na mihemo ya kimahaba ndivyo vilitawala chumba hiki.Patrick akaufungua mpya wa mapenzi na Savanna.
Ukurasa mpya wa maisha ya Patrick umefunguliwa na tayari ni meneja wa kiwanda cha kusindika nyama.Maisha yake yanakwenda vizuri kwa sasa.Alinawiri na kupendeza sana.Alikiongoza kiwanda hiki cha kusindika nyama kwa ufanisi mkubwa na ndani ya kipindi kifupi kiwanda hiki kilikuwa ni moja kati ya viwanda bora kabisa nchini
Mizizi ya penzi imara kati yake na Savanna ilichomoza kwa kasi na kwa sasa penzi lao halikuwa la siri tena.Lilikuwa kwa ndugu jamaa na marafiki.Alimtambulisha rasmi Savanna kama mpenzi wake na kwa pamoja walikuwa na mipango mingi na ndoto nyingi za kutimiza katika maisha yao yajayo na kubwa likiwa ni kufunga ndoa mara tu kesi ya Patrick itakapomalizika.Bado kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili Patrick iliendelea kuunguruma mahakamani.Tayari upande wa mashitaka ulikwisha funga funga ushahidi wao hivyo kutoa nafasi kwa upande wa utetezi nao kuwaleta mahakamni mashahidi wanaomtetea Patrick.Upande wa utetezi ukiongozwa na Savanna uliitaka Mahakama kumuachia huru mteja wao kwa sababu alisababisha kifo wakati akijaribu kunyang’anya silaha mtu aliyekuwa ameishika silaha hiyo na aliyekuwa na dhamira ya kufanya mauaji.Baada ya Patrick kutoa ushahidi wake mahakamani ilifuata nafasi ya mashahidi kuanza kutoa ushahidi wao mbele ya mahakama.
Siku moja jioni Savanna alichelewa kurudi nyumbani na kukuta tayari Patrick amekwisha rejea toka kazini.Siku hii Savanna alionekana mchovu na mwenye mawazo mengi.Patrick aliligundua hilo na kumuuliza ni jambo gani lililokuwa limemsibu.Savanna hakujbu kitu akainuka pale sofani akajimiminia mvinyo katika glasi akanywa funda kubwa halafu akamtazama Patrick
“Savanna una tatizo gani leo mpenzi wangu? Si kawaida yako kuwa katika hali hii.Tafadhali niambie kama una tatizo lolote.” Akasema Patrick.Savanna akainama akafikiri kwa sekunde kadhaa na kusema
“Patrick nina tatizo mpenzi wangu.Kuna jambo linaniumiza kichwa changu sana.Nimekuwa nikilifikiria suala hili kwa muda mrefu sasa lakini nimeshindwa kulipatia ufumbuzi”
“Jambo gani hilo linakusumbua Savanna? Tafadhali niambie.Hakuna jambo lolote linaloweza kutushinda kulipatia ufumbuzi” akasema Patrick.Savanna akainamisha kichwa akafikiri kidogo na kusema
“Kuna tatizo kidogo katika kesi”
“Katika kesi? Patrick akastuka
“Ndiyo Patrick kuna tatizo dogo”
“Tatizo gani” akauliza Patrick ambaye tayari moyo wake ulianza kumwenda mbio
“Patrick nilishindwa kukutaarifu mapema kuhusu jambo hili kwa kuwa naamini ni jambo ambalo hutapenda kulisikia lakini naomba nikutaarifu kwamba katika orodha ya watu wanaotakiwa kutoa ushahidi wao mahakamani lipo pia jina la Happy”
Patrick kijasho kikamtoka .Alistushwa sana kwa taarifa ile
“Ou my God “ akasema kwa sauti ndogo huku akimkazia macho Savanna
“Happy kibaho? Akauliza Patrick
“Ndiyo.Happy Kibaho”
“Ouh my Gosh.! How could you do that Savanna?Tulikubaliana kwamba Happy hatahusika na chochote katika kesi hii,aliniacha nikisota gerezani kwa kosa ambalo sikulifanya,hakuona umuhimu wangu,kwake yeye hata kama nikifungwa gerezani hatajali,kwa nini basi tumtumie mtu kama huyu? Savanna Happy kibaho ni jina ambalo sitaki kulisikia tena katika masikio yangu.” Patrick akasimama
“Patrick hii ndiyo sababu sikutaka kukueleza mapema.Nilijua lazima ungeshtushwa sana na taarifa hiyo”
“Savanna tafadhali niko chini ya miguu yako naomba kama kuna uwezekano liondoe jina la Happy katika orodha ya mashahidi.Tunao mashahidi wengi ambao tutawatumia katika kesi hii.” Akasema Patrick.Savanna akamshika mabegani na kusema
“Patrick mpenzi wangu ninafahamu ni namna gani Happy alivyokuumiza na jinsi gani unavyomchukia.Nafahamu pia uhusika wa Happy katika kesi hii unavyokuumiza kwani utairudisha tena taswira ya mtu ambaye hutaki tena kumuona au kumsikia katika maisha yako.Hata mimi suala hili ni gumu sana kwangu lakini naomba niwe wazi kwako kwamba Happy ni mtu muhimu sana katika hatua hii tuliyofikia.Ushahidi wake una nguvu sana”
“Savanna mashahidi hawa wote tulionao hawatoshi hadi Happy naye ashirikishwe katika kutoa ushahidi? To be honest I hate her.Sitaki kuiona tena sura yake kutokana na mambo aliyonifanyia.” Akasema Patrick
“Ushahidi mzito tuliouwasilisha mahakamani pamoja na ule unaoendelea kutolewa na mashahidi unajitosheleza sana lakini katika ushahidi wote huo Happy ametajwa sana kwani yeye ndiye aliyekoswa na risasi iliyotoka katika bastora aliyokuwa ameishika Vero.Happy anatakiwa aieleze mahakama kila kitu kilichotokea jioni ile.Ni ushahidi muhimu mno ambao ninaamini ndio utakaoisaidia mahakama kuamua hatima ya kesi hii.Patrick nakuomba mpenzi wangu tumtafute Happy na kumuomba atoe ushahidi wake .Nafahamu kwamba unamchukia na hutaki kumuona tena lakini kwa hatua hii Happy ni mtu muhimu sana kwetu.Patrick we’re almost to the end now so we need to do everything we can to win.Ninamuomba sana Mungu atusaidie ili tuweze kulimaliza suala hii haraka na tuitimize ndoto yetu ya kufunga ndoa.Naomba uniruhusu mpenzi wangu nimtafute Happy ili aweze kuja kutoa ushahidi wake “ akasema Savanna.
Patrick akashika kichwa kwa mikono yake akainama na kuzama katika mawazo.Akainuka pale alipokuwa amekaa akaenda dirishani,akasimama na kuelekeza macho yake nje kana kwamba kuna kitu alikuwa anakiangalia
“Happy Kibaho !” akasema taratibu halafu akainama tena
“Nilimpenda kiasi ambacho siwezi kuelezea.Nilimpa kila kitu na kuamini kwamba yeye ndiye mwanamke pekee ambaye nimepangiwa niwe naye katika maisha yangu.Pamoja na kumuonyesha kila aina ya upendo lakini Happy bado alidiriki kufanya kitendo kichafu ambacho sikuwahi kutegemea au hata kuota kama msichana kama Happy anaweza akafanya.Aligundua kosa alilolitenda na akapotea moja kwa moja akiniacha nikiozea gerezani kwa kosa ambalo alilisababisha yeye mwenyewe.Je mtu wa namna hii aliyenisababishia majeraha makubwa ya moyo ninastahili kuonana naye tena ana kwa ana? Moyo wangu hautaki kabisa na hauko tayari kuonana tena na Happy lakini kwa kuwa hili ni ombi la Savanna itanibidi nikaze moyo na kukubali aje atoe ushahidi wake.” Akawaza Patrick halafu akamgeukia Savanna
“Unafahamu mahala aliko Happy kwa sasa? Savanna akainuka na kumfuata Patrick pale alipokuwa amesimama.
“Patrick kuna jambo lingine ambalo naomba ulifahamu”
“Jambo gani hilo Savanna?
“Happy hayupo hapa nchini”
“Hayupo hapa nchini?.How do you know that she’s not here? Akauliza Patrick kwa wasi wasi
“Samahani Patrick kwa kutokufahamisha suala hili toka mwanzo lakini naomba nikufahamishe kwamba mimi ndiye niliyemsaidia Happy kuondoka hapa nchini” akasema Savanna.Patrick akazidi kuchanganyikiwa
“Savanna unazidi kunichanganya akili yangu.Ulimsaidia Happy kuondoka hapa nchini? Kwa nini hukuniambia muda wote huu? Do you know where she is now?
“Patrick ni hadithi ndefu sana na sikutaka kukwambia mapema kwa sababu nilijua utaumia na mimi sitaki kukuona ukiumia.”
“Ok niambie nini kilitokea? Happy yuko wapi? Akauliza Patrick.Savanna akainama akafikiri kidogo halafu akasema
“Nilipigiwa simu usiku na mzee Kibaho baba mzazi wa Happy akaniuliza kama nina taarifa zozote kuhusiana na Happy kwani hakuwa ameonekana nyumbani kwao toka alipoondoka asubuhi.Sikujua mahala alipokuwa Happy na mara ya mwisho kuonana naye ilikuwa ni gerezani asubuhi.Hii ilikuwa ni siku ile nilipokuja gerezani na mama na tukamkuta Happy pale mama akamfokea sana.” Savanna akasema halafu akamtazama Patrick kisha akaendelea
“Asubuhi ya siku iliyofuata nikiwa najiandaa kuja gerezani ,alikuja mmoja wa wafanyakazi wangu akiwa na gazeti lililokuwa na picha chafu za Happy katika ukurasa wa mbele.Nilistuka sana baada ya kuziona picha zile na kama haitoshi mtumishi yule akainionyesha pia na video iliyokuwa mtandaoni.Ilinibidi nimpigie simu Margreth naye akanifahamisha kwamba Happy alikuwa amekunywa sumu kwa lengo la kujiua.Nilikwenda hadi katika hospitali ya Brahmaputra ambako Happy alikuwa amekimbizwa na kupatiwa huduma ya kuondolewa sumu mwilini.Nilishauriana na familia yake na tukakubaliana kwamba ili kumuepusha Happy na aibu kubwa aliyoipata itabidi kumpeleka mafichoni nje ya nchi sehemu ambako hakuna mtu anayemfahamu .Kama mchango wangu kwao nilijitolea usafiri wa kwenda Kigali Rwanda ambako tayari nilikwisha fanya mawasiliano na meneja wa hoteli moja kubwa mjini Kigali ambaye ni rafiki yangu na kumuomba Happy akae katika hoteli yake hadi hapo atakapopona kabisa .Mimi baba yake,mzee Kibaho pamoja na daktari mmoja tulielekea Kigali Rwanda na nilimuacha Happy kule akiwa na baba yake pamoja na daktari “ akasema Savanna.
“So she’s in Kigali now? Akauliza Patrick
“Alikuwa Kigali lakini kwa taarifa nilizozipata toka kwa rafiki yangu Christine ni kwamba Happy alitoweka pale hotelini na hakuna anayefahamu alikwenda wapi.” Akasema Savanna
“Ouh my God.Tumekwama tena” akasema Patrick
“Tukitaka kumpata Happy hatuna budi kuwasiliana na familia yake.Nina imani lazima watakuwa wanafahamu mahala alipo”
“Hilo nalo ni tatizo lingine.Sina hakika kama familia yake inaweza kutupa ushirikiano na kutuambia mahala aliko Happy” akasema Patrick
“Mimi ndiye nitakayekwenda kuonana nao.Nina imani msaada wangu hawataweza kuusahau kwa hiyo watanisaidia”
“Hata kama familia yake itakubali kushirikiana nasi ,vipi kuhusu Happy mwenyewe atakuwa tayari kurudi tena hapa Tanzania kutoa ushahidi wake baada ya mambo ya aibu kubwa aliyoyafanya? Sina hakika kama anaweza akakanyaga tena Tanzania hasa kutokana na aibu kubwa aliyoipata kutokana na uchafu mkubwa alioufanya.Sina hakika kama suala hili litafanikiwa Savanna,Naomba tusiumize vichwa vyetu kuhusu huyu mwanamke.Tutafute njia nyingine ya kutusaidia na si kumtegemea Happy” akasema Patrick akionyeaha kukata tamaa kabisa ya kumpata Happy
“Patrick mpenzi wangu laiti kama kungekuwa na njia nyingine ya kufanya nisingethubutu kukutajia jina la Happy lakini kwa hatua tuliyofikia ni lazima tumpate Happy.We’re almost to the end.Patrick naomba uniruhusu mimi nikaonane na familia ya Happy nitawalilia na kuwaomba wanisaidie.Mzee Kibaho ni mtu mwelewa sana na nina hakika atakuwa tayari kutusaidia”
Patrick akainama akafikiri kidogo na kusema
“Do what you have to do Savanna lakini moyo wangu haujapenda kuonana na Happy kabisa”
“Ahsante sana mpenzi wangu.Umefanya jambo la maana sana kwa kukubali.Najua si maamuzi mepesi lakini its for the best of us.I promise you that we’re going to finish this once and for all” akasema Savanna,Patrick hakujibu kitu
* * * *
Saa nne za asubuhi siku iliyofuata ilimkuta Savanna nje ya geti la nyumba ya akina Happy.Ni muda mrefu umepita toka alipokuja katika nyumba hii.Akiwa ndani ya gari lake ,alilitazama geti la nyumba ile na kuvuta pumzi ndefu
“Help me God.Laiti ningekuwa na namna nyingine ya kufanya katu nisingethubutu kuja tena katika nyumba hii.Sikutaka Happy aonane tena na Patrick hasa katika wakati ambao penzi letu limekwisha weka mizizi imara,lakini kwa hali halisi ilivyo ninalazimika kurejea tena katika nyumba hii kutafuta msaada” akawaza Savanna halafu akashuka na kwenda kubonyeza kengele ya getini
Baada ya dakika moja geti likafunguliwa.Alikuwa ni mama yake Happy.Savanna akaingiwa na woga kidogo lakini akakaza moyo akasalimiana na mama yake Happy na kukaribishwa ndani
“Savanna umepotea sana mwanangu.Habari za siku nyingi?
“Kazi zimekuwa nyingi mama na ndiyo maana sijafika hapa muda mrefu sijafika kuwatembelea.Habari za hapa?
“Habari za hapa nzuri Savanna.Karibu sana” akasema mama Happy kisha mtumishi wa ndani akawahudumia vinywaji
“Mama mna mawasiliano yoyote na Happy? Nilipigiwa simu na Christine yule rafiki yangu niliyemkabidhi amuhudumie kule Kigali kwamba Happy aliondoka katika hoteli ile aliyokuwa anakaa na mpaka sasa hajui alipo.Nimepata wasi wasi sana na nikaona ni bora nije kuuliza kama mnalifahamu jambo hili” akasema Savanna na mama yake Happy akaonyesha mstuko Fulani
“Savanna suala hili tumelisikia na hata sisi limetustua sana.Mpaka hivi sasa hatujui Happy yuko wapi na hatuna mawaliano naye yoyote.Tumeamua kumuachia Mungu na kumuomba amlinde na kumpa uzima kokote kule aliko.Tunaamini siku moja lazima atarejea nyumbani” akasema mama Happy
Savanna kijasho kikamtoka.Akavuta pumzi ndefu na kusema
“Ouh my gosh !
Kimya kikatanda mle sebuleni halafu Savanna akauliza
“Margreth naye yuko wapi?
“Margreth yuko kazini “
Savanna akainama na kufikiri kwa muda kisha akasema
“Mama mimi nakwenda.Tutaonana tena siku nyingine.Endapo mtapata mawasiliano yoyote ya Happy naomba mtanitaarifu “akasema Savanna huku akiinuka.Mama yake Happy akastuka
“Savanna kulikoni? Mbona ghafla hivyo?
“Utanisamehe mama nimekumbuka kwamba nina miadi na mtu wa muhimu sana muda mfupi ujao.Nitakuja tena kukusalimu siku nyingine” Akasema Savanna na kuonyesha kwamba hakutaka tena maongezi akaingia katika gari lake na kuondoka
“Kuna kitu nimekigundua toka kwa mama yake Happy. Alikuwa na wasi wasi mwingi.Inaonekana kuna jambo analifahamu kuhusu Happy na hakutaka kunieleza.Margreth au mzee Kibaho wanaweza wakanipa ukweli halisi.Ngoja kwanza nikaonane na Margreth” akawaza Savanna halafu akaegesha gari pembeni ya barabara akachukua simu yake na kumpigia Margreth
“Hallo Savanna.Habari za siku nyingi? Akasema Margreth baada ya kupokea simu
“Habari nzuri Margreth.Hatujaonana muda mrefu sana”
“Ni kweli Savanna.Mbona umekuwa kimya hivyo?
“Ni mihangaiko tu Margreth.Uko wapi sasa hivi?
“Sasa hivi niko kazini lakini niko mbioni kutoka nataka kwenda kuhudhuria mazishi ya rafiki yangu”
“Margreth,ninahitaji sana kuonana nawe.Kuna jambo muhimu nahitaji kuongea nawe.Tunaweza kuonana kabla hujaenda msibani?
“Hakuna tatizo Savanna.Tukutane wapi?
“Tuonane pale Lemina Café.Ninaelekea huko sasa hivi.Utanikuta pale”
“Sawa Savanna.Nakuja hapa muda si mrefu” akajibu Margreth na kukata simu.
* * * *
Habari za siku nyingi Margreth? Alianzisha mazungumzo Savanna baada ya kuonana na Margreth
“Habari nzuri Savanna.Umepotea sana dada yangu”
“Ni kweli Margreth ni muda mrefu sana hatujaonana.Hii inachangiwa na majukumu mengi ya kazi”
“Ni kweli kabisa Savanna” akajibu Margreth.
“ Patrick anaendeleaje? Kesi yake imefikia wapi?
“ Patrick anaendelea vizuri na kesi yake naendelea vizuri pia.Kwa hivi sasa kinachoendelea na kusikilizwa kwa mashahidi wa utetezi.Tutalimaliza suala hili” akasema Savanna
“ namuombea Mungu Patrick suala hili liishe na aendelee na maisha yake” akasema Margreth kisha kikapita kimya kifupi.Savanna akasema
“Margreth nimekuita hapa nina tatizo ambalo nahitaji sana msaada wako” akasema Savanna
“Usijali Savanna niko tayari kukusaidia kwa lolote”
“Ahsante sana.Tatizo langu ni kutaka kufahamu mahala aliko Happy.Nahitaji kuzungumza naye”
Margreth akastuka na kumuangalia Savanna
“Happy ..?!! akauliza Margreth.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ndiyo.Nina shida kubwa ya kuongea na Happy.”
“Happy yuko Kigali mahala ulikomuacha” akajibu Margreth na kumfanya Savanna acheke kidogo
“Happy hayuko Kigali.Aliondoka kule muda mrefu sana .Tafadhali naomba Margreth unisaidie nizungumze na Happy.” Akasema Savanna.Margreth akaona aibu kidogo na kutabasamu
“Samahani Savanna kwa kutaka kukudanganya lakini ukweli ni kwamba taarifa hiyo uliyonayo ndiyo hata sisi tunayo.Tulitaarifiwa kwamba Happy ameondoka katika hoteli aliyokuwa akikaa na haijulikani alielekea wapi.Tumejaribu sana kumtafuta bila mafanikio.Kwani kuna tatizo gani Savanna?
“Nina tatizo kubwa sana kumuona Happy.Tatizo ninalomtafutia Happy ni kwa sababu ya Patrick.”
“Patrick !!..” Margreth akashangaa
“Patrick anamtafutia nini Happy?
“Nadhani ulisikia kwamba Patrick alipata dhamana akatoka gerezani”
“Dada Savanna kwa kweli sihitaji kusikia au kufuatilia lolote linalohusiana na Patrick.Yeye ndiye chanzo cha dada yangu kuteseka na kupoteza mwelekeo mzima wa maisha yake.Kila anapokuwa karibu na Happy basi lazima kuna jambo baya linatokea.Kabla hajaonana na Patrick maisha ya Happy yalikuwa mazuri na yenye furaha lakini mara tu alipokutana na Patrick basi maisha yake yamebadilika ghafla na kupoteza kabisa mwelekeo mzima wa maisha yake.To be honest I hate that dude” akasema Margreth
“Nakuelewa sana Margreth lakini naomba nikukumbushe kwamba mara ya kwanza Patrick aliua bila kukusudia wakati akimuokoa dada yako asidhalilishwe na kundi la wahuni waliokuwa na lengo la kumbaka.Alifungwa gerezani na yakatokea yaliyotokea hadi walipokuja kukutana tena siku chache kabla ya kufunga ndoa.Kwa mapenzi makubwa waliyokuwa nayo na kwa ridhaa yao wenyewe waliamua kuachana na wapenzi wao ili waweze kutimiza ndoto yao ya kuwa pamoja.Katika ugomvi ule uliotokea na kupelekea kifo cha Vero na ni Happy ndiye aliyemsukuma Vero akajigonga ukutani na kufariki dunia.Kwa mapenzi makubwa aliyokuwa nayo Patrick wa Happy aliamua kuubeba mzigo wote wa kesi hii.Na kwa taarifa yako ni kwamba mimi ndiye niliyepambana na kumtoa Happy katika kesi ile kwa ombi la Patrick.Kwa maana hiyo hakuna sababu ya kumlaumu Patrick” akasema Savanna.Margreth hakusema kitu na kwa mbali macho yake yalionyesha kulengwa na machozi
“Kesi ya Patrick inaendeleaje? Akauliza Margreth
“Mashahidi wanaendelea kutoa ushahidi wao na wiki hii shahidi aliyebaki atatoa ushahidi wake na baada ya hapo atabaki shahidi mmoja tu katika orodha ya mashahidi upande wa uetetezi.Ni Happy.Yeye ndiye mtu wa mwisho kutoa ushahidi wake .Ushahidi wake una nguvu sana kwa sababu yeye ndiye anayeifahamu vyema historia yake na Patrick na kila kitu kilichotokea usiku ule.Kwa hiyo namuhitaji sana Happy.Nakuomba kama unafahamu mahala alipo niambie tafadhali”akasema Savanna.
“Sifahamu aliko Happy” akajibu Margreth.Savanna akamtazama kwa macho makali na kusema
“Margreth nafahamu kuna kitu ambacho unanificha”
“I don’t know anything Savanna” akasema Margreth
“Margreth mimi ni rafiki wa familia yenu.Nilimsaidia Happy kama ndugu yangu wakati alipokutwa na matatizo.Na mimi nimepatwa na tatizo na ninaomba mnisaidie kama ndugu yenu.Sina maana ya kwamba nataka Patrick na Happy warudiane tena la hasha.Ninachotaka mimi ni ushahidi tu tena teknolojia imeimarika sana siku hizi anaweza akatoa ushahidi wake huko huko mahala aliko na si lazima aje Tanzania” akasema Savanna
“Savanna nimekwisha kwambia kwamba sifahamu mahala aliko Happy,mbona hutaki kunielewa? Akafoka Savanna
“Ok! Ok! nimekuelewa Margreth.Hakuna yeyote kati yenu anayeiona thamani ya Patrick tena.Natumai nyote mnatamani kusikia Patrick amefungwa gerezani.I cant let Patrick go to jail after all that has sacrificed.He’s my friend and I’ll do anything to set him free.Nitakwenda kumtafuta Happy mimi mwenyewe kwa gharama zangu na kwa njia ninayoijua mimi.Kama bado yuko hai nakuhakikishia kwamba nitampata tu.Kesho nitakwenda Kigali na nitaanza kumtafuta Happy tokea pale.Nina marafiki wengi pale na watanisaidia kujua Happy alipo.Ahsante kwa kuitika mwito wangu.Tutazidi kuonana” akasema Savanna halafu akainuka akachukua mkoba wake na kuanza kuondoka.
“Savanna wait…!! akasema Margreth.Savanna akageuka ,akamtazama Margreth na kurejea pale mezani
“Unasemaje Margreth? akauliza Savanna
“Naomba ukae chini Savanna” akasema Margreth
“Savanna umenipa wakati mgumu sana.Nashindwa nifanye nini lakini naomba nikufahamishe kwamba ninafahamu mahala alipo Happy” akasema Margreth.Uso wa Savanna ukaonyesha tabasamu .
“Ahsante sana Margreth kwa kuwa muwazi.Happy yuko wapi?
“Happy aliondoka Kigali na kuelekea Marekani .Kwa sasa anashi Los angeles .Yeye binafsi hataki mtu yeyote zaidi ya familia yake afahamu mahala aliko.Hivi sasa maisha yake ni mazuri na yenye amani.Nimeamua kukueleza ukweli wa mahala alipo Happy kutokana na uzito wa suala unalomtafutia japo najua kutakuwa na mtafaruku kwa sababu nimevunja makubaliano yetu ya kutomweleza mtu yeyote mahala aliko” akasema Margreth
“Usihofu Margreth.Hakuna mwingine zaidi yangu atakayejua kuhusu jambo hili.Sasa nieleze nitampata vipi? Unaweza kunipatia mawasiliano yake?
“Its not that simple Savanna.Nitakachofanya mimi ndiye nitakayeongea naye kwanza ili tuone atatoa jibu gani.Naomba niwe wazi kwako kwamba Happy hataki mawasiliano na mtu yeyote sasa na hasa hasa wewe.Sijui ulimfanya kitu gani kwani aliweka wazi kwamba katika watu anaowachukia basi wewe ni mmoja wao.Naomba uniachie mimi hiyo kazi nitaongea naye halafu nitakwambia jibu atakalonipa” akasema Margreth
“Ahsante sana Margreth.Nakuomba ujitahidi kwa kadiri utakavyoweza umshawishi akubali.Mkumbushe kwamba hatima ya Patrick iko mikononi mwake.”
“Ni kazi ngumu Savanna lakini nitajitahidi” akajibu Margreth.
“Jitahidi Margreth.Hata kama italazimika kumtumia tiketi ya ndege ya kuja na kurudi mimi niko tayari kugharamia.Kitu kingine ambacho unapaswa kumkumbusha ni kwamba hakuna mtu mwenye lengo la kumshawishi arejeshe uhusiano wake na Patrick kwani najua tayari ana maisha yake yenye furaha halikadhalika Patrick naye ana maisha yake yenye furaha pia.Tunachohitaji sisi ni ushahidi tu ambao utamuweka huru Patrick “ akasema Savanna halafu akafungua pochi lake na kutoa bunda la noti akahesabu noti kumi na tano za elfu kumi kumi na kumkabidhi Margreth.
“Hizi ni kwa ajili ya mawasiliano na Happy” akasema Savanna.Margreth akazichukua fedha zile na kumrudishia
“Nashukuru sana Savanna lakini naomba uziweke pesa hizo utazitumia kwa kitu kingine.Nitafanya mawasiliano kwa gharama zangu.” Akasema Margreth .Savanna akazichukua fedha zile na kuweka mkobani wakaagana akaondoka
Baada ya Savanna kuondoka,bado Margreth aliendelea kubaki pale mezani akiwa na mawazo mengi
“Nimefanya kosa kubwa sana kuvunja makubaliano yangu na Happy . Kwa mdomo wake mwenyewe alitamka kwamba hataki tena kurudi Tanzania.Nitaanzaje kumwelezea kuhusiana na suala hili? Ouh my gosh ! nimekoroga mambo.Happy atanilaumu sana kwa jambo hili lakini kwa upande mwingine ana haki ya kufahamu kinachoendelea huku nyumbani.Ana kila sababu ya kuja kutoa ushahidi mahakamani na kumuepusha Patrick na adhabu yoyote anayoweza kuipata kwa kosa ambalo hakulitenda.” Akawaza Margreth halafu akainuka akachukua mkoba wake na kuondoka
Margreth alifika nyumbani kwao lakini kabla hajaingia chumbani kwake mama yake akatokea
“Margreth mbona umewahi kurudi leo?
“Ninakwenda kuhudhuria mazishi ya yule rafiki yangu aliyefariki juzi” akasema Margreth
“Maggie ,Savanna alifika hapa “
“Alikuwa anataka nini? Akauliza Margreth
“Kikubwa alichoniuliza ni kama tuna mawasiliano na Happy au kama tufahamu mahala aliko hivi sasa.”
“Ulimjibu nini?
“Nilimjibu kwamba hata sisi hatufahamu mahala aliko Happy.Baada ya jibu hilo akaondoka zake.Nina wasi wasi sana kwa kuamua kumtafuta Happy hivi sasa.Sitaki kabisa wafahamu mahala Happy alipo” akasema mama yake
“Mama nimeonana na Savanna.Alinipigia simu wakati nikitoka kazini na nikaonana naye.Ni kweli ana tatizo na ndiyo maana anamtafuta Happy.” Akasema Margreth
“Ana tatizo gani? Sitaki wamuhusishe tena mwanangu katika masuala yao.”
“Mama Savanna ana matatizo makubwa na ni lazima aonane au awasiliane naye”
“Ana tatizo gani?
“Ni kuhusiana na ile kesi ya Patrick”
“Kesi ya Patrick ?!!..mama yake akashangaa
“Ndiyo mama.Happy anatakiwa atoe ushahidi wake.”
“Margreth ..!!!! akasema mama yake
“Hapana Margreth.Mwanangu Happy kamwe sintaruhusu aje tena huku na kuonana tena na Yule kijana.Mambo aliyokumbana nayo yanatosha sitaki tena mwanangu aumie.Maisha yake ni mazuri kwa sasa na tayari amekwisha msahau Patrick.Sitaki aonane tena na yule kijana aliyejaa mabalaa mwili mzima”
“mama..!!! “ akasema Margreth
“Hapana Margreth.Siruhusu mwanangu kushiriki kwa namna yoyote katika kesi hii.Tayari maisha yake yametulia hivi sasa na sitaki apate tena matatizo mengine.”
“Mama kama Happy asipofanya hivyo kuna uwezekano Patrick akafungwa gerezani.”
“Itakuwa vyema kama akifungwa.Ninamchukia sana yule kijana na kama ningekuwa na uwezo ningemuondoa kabisa katika uso wa dunia” mama yake Happy akasema kwa ukali
“mama si sahihi kusema hivyo.Kumbuka Patrick alikubali kuubeba mzigo mzito wa kesi kwa kosa ambalo hakulitenda.Happy ndiye aliyeua na ndiye anayestahili kusimama mahakamani hivi sasa lakini Patrick ameliepusha hilo na amejitolea yeye mwenyewe kuubeba mzigo huu.Mama huoni kwamba Happy analazimika kuwa mstari wa mbele kumtetea Patrick? Ninajua kwa sasa amekwisha anza maisha mapya na hana mpango tena na Patrick wala kurejea nyumbani lakini pamoja na hayo bado ana wajibu wa kuja kumtolea ushahidi mwenzake.” Margreth akajitahidi kumuelewesha mama yake ambaye bado alionekana kutokubaliana kwa namna yoyote ile na hoja ile ya kumtaka Hapy atoe ushahidi kwa Patrick
“Pamoja na hayo,bado sitaki mwanangu arejee.Sitaki aumie tena.Margreth wewe mwenyewe unafahamu fika kwamba yule kijana sijui amempa nini Happy.Kitendo cha Happy kumuona tu basi huwa anasahu kila kitu na kumkimbilia yeye.Kwa sasa Happy amekwisha rudiana tena na Mike na maisha yake yana furaha sitaki aonane tena na yule kijana.“ mama Happy bado aliendelea kuushikilia msimamo wake
“Mama natambua Happy tayari ameamua kuendelea na maisha yake na hana tena mpango wa kuendelea na Patrick kwa hiyo usiogope hata kama wataonana hakuna kitakachotokea.Anachotakiwa kufanya yeye ni kutoa tu ushahidi wake halafu aondoke zake akaendelee na maisha yake.Isitoshe hata Patrick naye amekwisha endelea na maisha yake na hana tena mpango na Happy”
“Margreth nimekwisha kueleza kwamba hata unishawishi vipi Happy hatakuja tena na kuonana na Patrick.Neno langu mimi ni la mwisho na sitaki tena mjadala huu uendelee.” Akasema mama yake Happy huku akiondoka akiwa amekasirika sana.Margreth naye akaelekea chumbani kwake na kujitupa kitandani
“Sikubaliani na mama hata kidogo.Hatutatenda haki kama Happy hatatoa ushahidi wake mahakamani kumtetea Patrick mtu aliyeubeba mzigo wa mashtaka yaliyokuwa yanamkabili yeye.Lazima niwasiliane na Happy nisikie naye ana maoni gani kuhusu suala hili.Tukifanya mchezo Patrick anaweza akafungwa” Akawaza Margreth halafu akaichukua simu yake na kuzitafuta namba za Happy akapiga huku moyo wake ukimwenda mbio.Simu iliita na kukata.Akaangalia saa ya ukutani ilionyesha ni saa sita za mchana
“Yawezekana yuko katika usingizi mzito kwani mida hii huko kwao bado ni usiku.Ngoja nimpigie tena” Margreth akapiga tena
“Hallow “ simu ikapokelewa na sauti nzito ya kiume.Margreth akastuka na kudhani labda amekosea namba
“Halow naitwa Margreth,napiga simu toka Tanz…..” kabla hajamaliza,yule mwanaume aliyepokea simu akasema
“Margreth,Mike hapa naongea.Habari za Tanzania?Umekwisha isahau sauti yangu mara hii?
Margreth akavuta pumzi ndefu na kusema
“Mike !! nafurahi kuongea nawe tena.Ni muda mrefu umepita.Samahani kwa kukusumbua na kukuamsha usingizini.Nilikuwa Nahitaji kuongea na Happy”
“Happy niko naye hapa.Subiri kidogo nimuamshe” akasema Mike na baada ya muda sauti yenye usingizi ya Happy ikasikika
“Hallow Margreth”
“Happy.!! Samahani nimekuamsha”
“Usijali Margreth hata hivyo nimelala muda si mrefu sana.Mike amekuja leo hivyo tukaenda club,Habari za huko?
“Huku kwema Happy,tunaendelea vizuri isipokuwa yule rafiki yangu Salama amefariki dunia wakati akijifungua na leo tunamzika”
“Salama yule aliyeolewa na mzungu?
“Ndiyo huyo”
“Dah ! poleni sana.Habari nyingine?
“Habari nzuri Happy.” Akasema Margreth
“Maggie nilikuahidi kukutumia ile hela ya kununua gari,sijasau nitakutumia wiki ijayo,wiki hii nilikuwa nimetingwa sana na kazi”
“Ahsante sana Happy lakini sijakupigia kwa ajili ya suala hilo.Kuna suala linguine”
“Suala gani Maggie?
“Happy kuna tatizo limejitokeza”:
“Tatizo gani? akauliza Happy.Margreth akashusha pumzi na kusema
“Its about Patrick”
“Patrick ..!!!! “ Happy akastuka
“Ndiyo Happy.Nimeoanana na Savanna muda si mrefu na amenifahamisha kwamba Patrick alifanikiwa kupata dhamana na yuko huru lakini kesi yake inaendelea kusikilizwa na kinachoendelea hivi sasa ni mashahidi wa upande wa utetezi kutoa ushahidi wao.Savanna alitaka kufahamu mahala ulipo” akasema Margreth
“Ananitafuta mimi? Kwa nini? Akauliza Happy kwa wasi wasi
“Jina lako liko katika orodha ya watu wanaotakiwa kutoa ushahidi wao mahakamani kumtetea Patrick”
“No ! No ! no !!!..Thats impossible.Margreth no body should know where I am.” Akasema Happy
“Its too late Happy.Nimelazimika kumweleza ukweli Savanna kutokana na uzito wa suala lenyewe.”
“Ouh Margreth how on earth could you do such a thing? Tulikubaliana kwamba asiambiwe mtu mwingine yeyote mahala nilipo.Kwa nini lakini umefanaya hivyo? How could you betray me? Akalalama Happy
“Naomba unisamehe sana Happy kwa kilichotokea.Najua yalikuwa ni makubalianao yetu kwamba asifahamu mtu mwingine yeyote mahala ulipo lakini nimelazimika kumweleza Savanna na hakuna mtu mwingine yeyote anayelifahamu hilo zaidi yake.”
“Margreth siwezi kukuamini tena.Umeyafanya maisha yangu yawe magumu tena.Umenifanya nirudi tena katika kile ambacho nimekuwa nikikimbia kwa muda huu wote” akasema Happy
“Happy naomba unisikilize kwa makini.Nililazimika kumweleza Savanna mahala ulipo baada ya kuniweka wazi kwamba ushahidi wako una nguvu sana ya kumsaidia Patrick asihukumiwe kifungo.Happy hata mimi inaniuma sana kukukumbusha mambo ambayo unajitahidi kuyasahau lakini naomba niwe muwazi kwako kwamba you have to save Patrick.He saved you from going to jail and its your turn now to save him” akasema Margreth.Baada ya ukimya mfupi Happy akasema
“Margerth nimekuelewa lakini sina hakika kama nitaweza kufanya hivyo.Ninapambana hivi sasa kumsahau Patrick na kuendelea na maisha yangu mapya yenye furaha na siko tayari kuonana tena na Patrick ana kwa ana.” Akasema Happy
“Happy sina maana ya kwamba ukitoa ushahidi utarudiana tena na Patrick na wala sikushauri ufanye hivyo lakini nakukumbusha tu kwamba Patrick ameubeba mzigo mkubwa sana na endapo atafungwa kwa sababu tu ya kukosekana ushahidi wenye nguvu,nakuapia Happy hautakuwa na furaha hata siku moja katika maisha yako.Patrick’s shadow will haunt you forever” Akasema Margreth
“What can I do Margreth? Let it be.Look Margreth ,there is nothing I can do now to help him.I’m trying to pick up the pieces and arrange my life again so I cant go back to square one.Nilimtenda vibaya Mike na kumsababisia maumivu makali ya moyo lakini hivi sasa ndiye amekuwa msaada wangu mkubwa na ndiye anayenisaidia kusahau mambo yote yaliyopita.Ninaishi hapa Marekani kwa sababu yake.Amenitafutia nyumba,kazi na kila kitu.He loves me and I’m learning to love him so how could I tell him that I’m going back to Tanzania? Please Margreth,this conversation is over.” Akasema Happy
“Happy kabla hujakata simu naomba nikukumbushe kitu kimoja.Ulinitamkia wewe mwenyewe kwa mdomo wako kwamba Patrick hakusababisha kifo cha Vero bali ni wewe uliyemsukuma akajigonga ukutani na kufariki.Patrick kwa mapenzi makubwa aliyokuwa nayo kwako aliamua kujitwisha yeye mzigo wote .Ameteseka gerezani kwa kipindi kirefu na bado anaendelea na kesi.Nomba leo unitamkie neno moja tu kwa mdomo wako kwamba uko tayari Patrick afungwe gerezani kwa kosa ambalo hakulitenda? Nipe jibu moja tu na nitakuelewa” akasema Margreth.Happy machozi yakamtoka
“I don’t know Margreth.’ll call you later” akasema Happy na kukata simu.Machozi yalianza kumtoka na akaanza kulia kwa kwikwi.Mike aliyekuwa chumbani akatoka haraka aliposikia Happy akilia kwa kwikwi.
“Happy kuna nini? Mbona unalia? Kuna taarifa ambayo si nzuri? Akauliza Mike
Happy akamkumbatia Mike kwa nguvu huku akiendelea kulia
“Nyamaza kulia mpenzi wangu na uniambie nini kinakuliza.Kuna tatizo gani nyumbani? Akauliza Mike.Happy hakujibu kitu aliendelea kulia kwa kwikwi.Mike akamletea glasi ya maji akanywa
“Tafadhali niambie Happy una tatizo gani?
“Mike kuna tatizo limetokea”
“Niambie Happy ni tatizo gani ? Niko hapa kukusaidia”
“Si tatizo kubwa lakini linahusiana na kesi ya Patrick” akasema Happy na kumstua Mike
“Nini kimetokea katika hiyo kesi?
“Savanna wakili anayemtetea Patrick amefika nyumbani leo hii na kuulizia taarifa zangu na kuomba apatiwe mawasiliano yangu lakini kwa bahati mbaya amekutana na Margreth na akamueleza kila kitu kuhusu mimi”
“Ouh my gosh ! Kwa nini lakini amefanya hivyo wakati mlikwishakubaliana kwamba mtu yeyote asifahamu mahala ulipo?
“Kwa madai ya Margreth ni kwamba aliamua kumweleza ukweli Savanna kutokana na uzito wa suala hilo alilokuwa ananitafutia”
“Ni suala gani alilokuwa anakutafutia?
Happy akafikiri kidogo na kusema
“Natakiwa kutoa ushahidi wangu mahakamani kumtetea Patrick.”
Kimya kikatanda mle ndani.Kila mmoja alikuwa anawaza lake.Mike alionekana kuishiwa nguvu.
“Happy my angel tell me its not true and if true you wont do it” akasema Mike
“Its true Mike.Natakiwa mahakamani nikatoe ushahidi wangu.
“That’s impossible.You cant go back there” akasema Mike.Alistushwa sana na taarifa ile ya Happy
“Happy mpenzi naomba unihakikishie kwamba hutakwenda tena Tanzania.Hutakwenda kuonana tena na Patrick.Kama ingekuwa ni kesi inayomkabili mtu mwingine nisingekuwa na wasi wasi wowote lakini kukuacha ukaonane tena na Patrick hilo ni jambo ambalo siwezi kulifanya” akasema Mike huku amemshika Happy mabeganiCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mike kuna jambo ambalo ningependa ulifahamu” akasema Happy
“Jambo gani Happy ? Mbona unanipa wasi wasi mpenzi wangu? Akauliza Mike.Happy akavuta punzi ndefu na kusema
“Patrick hakumuua Vero”
Mike akastuka na kumtumbulia Happy macho.
“Sikuelewi unamaanisha nini Happy.Patrick anatuhumiwa kwa kusababisha kifo cha Vero.Kwa nini unasema kwamba si yeye aliyesababisha kifo cha Vero? Akauliza Mike.Happy akamtazama usoni na kusema
“Mimi ndiye nilisababisha kifo cha Vero.” Akasema Happy
Mike akastuka na kumuachia Happy mikono halafu akasimama na kumuangalia Happy kana kwamba ni mara ya kwanza anamuona
“That’s not true .Its not true…” akasema Mike
“Its true Mike.I killed her.Samahani kwa kutokwambia kuhusu suala hili kwa sababu hii ni sehemu moja ya maisha yangu ambayo ninapambana ili niisahau.”akasema Happy
“Sikuelewi mpenzi wangu.Kwa nini unifiche kitu kikubwa kama hiki?
“Nisamehe mpenzi wangu.Naomba unisamehe Mike na unielewe kwamba sikufanya makusudi kutokwambia kitu kama hiki.Naamini hata wewe ungekuwa katika nafasi yangu ungefanya kama nilivyofaya mimi yaani kuliweka jambo hili kuwa ni siri ya moyoni.Ni jambo ambalo kila nikilifikiria huwa linanipa wakati mgumu sana.I’ve been trying to forget that night but I cant..” akasema Happy huku akishindwa kujizuia na kutoa machozi.Mike akamsogelea na kumkumbatia
“Nyamaza mepnzi wangu.Nyamaza Happy.Naomba unieleze ni kitu gani kilitokea usiku huo na kwa nini Patrick ndiye anayetuhuiwa kwa kusababisha mauaji hayo? Akasema Mike.Happy akafuta machozi akafikri kidogio na kusema
“Tulikuwa hotelini mimi na wewe tukipata chakula nilipopigiwa simu na Patrick kwamba kuna matatizo yametokea na baba yake amelazwa katika hospitali kuu ya magonjwa ya moyo .Kama utakumbuka nilikuomba unirudishe nyumbani ambako nilichukua gari langu na kukimbia hospitali.Nilimkuta Patrick halafu tukapanda katika ghorofa ya juu ambayo bado ujenzi wake ulikuwa unaendelea na Patrick akaanza kunisimuilia kilichotokea.Ghafla akatokea Vero akiwa na bastora mkononi.Alikuwa amekasirika na sura yake ilionyesha kwamba alikuwa amedhamiria kufanya kitu kibaya.Nadhani nilikueleza kuhusiana na kitendo alichokifanya Patrick cha kuvunja uchumba na Vero kitendo ambacho kilimuumiza sana.Alituelekezea bastora ile huku akitoa vitisho vingi sana na kutishai kututoa uhai mimi na Patricki.Patrick alimsihi aache utani na silaha za moto na ndipo alipoonyesha kwamba hakuwa akitania pale alipoachia risasi iliyonikosa na kupiga nguzo.Nilihisi kama nimekufa nikaanguka chini.Kitendo kile kilimkasirisha Patrick ambaye bila kujali hatari iliyokuwepo akamfuata Vero na kuanza kumnyang’anya Vero ile silaha.Kitendo kile kiliniogopesha sana na nikajua Vero angeweza kumdhuru Patrick hivyo nikainuka na kwenda kumsukuma Vero ambaye alijigonga ukutani na kufariki dunia.Patrick hakutaka nihusishwe katika kesi ile kwa kuamua kuubeba mzigo wote wa kesi ya mauaji .Kila mtu anajua kwamba Patrick ndiye aliyesababisah kifo cha Vero.Alikubali kuubeba mzigo huu mzito wa kesi kubwa kama hii kwa ajili yangu kwa ajili yua kunikinga na kesi hii.”akasema Happy.Mike akamtazama kwa makini na kusema
“Ahsante Happy kwa kunieleza ukweli lakini pamoja na hayo ninataka kukuuliza jambo moja ”
“Uliza Mike”
“Do you still love him? Akauliza Mike
“Mike !! ..akasema Happy
“Just answer my question Happy.Do you have any feeling for him?
“Mike I’m with you now.Its you that I love now.Nimekuwa nikijitahidi kuifuta picha ya Patrick moyoni mwangu na hiyo inamaanisha kwamba sina hisia zozote kwake”
“Are you sure? Akauliza Mike
“Yes Mike I’m sure”
“Kama ni kweli hayo unayoniambia kwa nini ulikuwa unalia baada ya kuzipata taarifa hizi?
“Mike hata kama ungekuwa ni wewe lazima ungetoa machozi.Patrick naye ni binadamu na anakabiliwa na kesi kwa kosa ambalo hakulitenda .Nilishindwa namna ya kufanya hasa katika wakati huu ninaojitahidi kumsahau ndiyo maana nikashindwa kujizuia kulia” akasema Happy
“Its ok Happy.Forget about that.Umeshaamua kuyasahau yote ya nyuma kwa hiyo songa mbele.Mimi niko hapa na niko tayari kukusaida kwa kila namna nitakavyoweza ili uweze kusahau historia na matukio yote yaliyopita.Let him go”
“Mike ! How could you say that? Ingekuwa ni wewe uko katika nafasi yangu ungefanya nini? Ungemuacha mtu kama huyu afungwe gerezani? He saved me.He saved a woman you love.So that’s how you repay him? Akauliza Happy
“So what’s your decision? Akauliza Mike
“Nitakwenda Tanzania.Nitakwenda kutoa ushahidi wangu mahakamani.Siko tayari Patrick afungwe gerezani.Tafadhali Mike naomba uniruhusu niende Tanzania nikamtolee Patrick ushahidi.Lengo langu ni ili Patrick awe huru na aendelee na maisha yake.Najua unaogopa nini kitatokea endapo nitaonana naye lakini nakuhakikishia kwamba kitakachonipeleka huko ni kutoa tu huo ushahidi wangu na jambo lingine lolote.Me and him its over.” akasema Happy.Mike akazunguka zunguka mle ndani na kusema
“Laiti nisingekuwa na marufuku ya kukanyaga ardhi ya Tanzania nisingekubali uende peke yako.Ningekupeleka ukatoe ushahidi wako halafu turudi wote marekani.Sijui ni kwa nini ninakosa imani na Patrick.” Akasema Mike kwa masikitiko
“Kwa maana hiyo unaniruhusu niende Tanzania? Akaulza Happy
“Sina haja ya kukuruhusi kwani tayari umekwisha fanya maamuzi na siwezi kukukatalia.Ni kweli Patrick anastahili kutendewa wema kama alioutenda kwako.Lakini sijui kwa nini roho yangu bado inasita sana”
“Huniamni Mike?
“Nakuamini sana mpenzi wangu lakini nashindwa kujizuia kuwa na wasi wasi kuja kwamba unakwenda kuonana na Patrick tena.Patrick alifanya kitendo cha kijasiri sana ambacho hata mimi kimenigusa ,lakini naomba nikiri kwako mpenzi wangu kwamba siwezi kushindana na Patrick katika vita ya kukugombania .Nafahamu Patrick amekuwa moyoni mwako kwa miaka mingi sana .Nenda Tanzania mpenzi lakini ujue kwamba ninakuamini na kwamba hutafanya kitendo kama ulichonifanyia kipindi kile kwani sijui kama nitaweza kuyavumilia maumivu na mateso ya moyo kama niliyoyapata wakati ule.” Akasema Mike
“Mike naomba uniamini haya nikwambiayo kwamba kilichobaki kati yangu na Patrick ni historia tu.Kinachonisukuma kutaka kwenda kutoa ushahidi wangu ni kumsaidia ili kama ikiwezekana aweze kuachiwa huru.Alionyesha ubinadamu mkubwa kwangu kwa hiyo na mimi sina budi kumsaidia.After this I’m done with him.Patrick atakuwa huru na maisha yake na mimi nawe tutakuwa huru” akasema Happy
* * * *
Margreth akiwa msibani pamoja na waombolezaji wengine mara simu yake ikaita.Alikuwa ni Happy aliyempigia
“Hallo Happy” akasema Margreth baada ya kupokea simu
“Tayari umefika msibani?
“Ndiyo Happy.Tunajiandaa kwenda kuzika”
“Sawa Magreth,nimekupigia kukutaarifu kwamba ninakuja Tanzania kutoa ushahidi wangu halafu nitarejea tena marekani. Najua nitakabiliana na matatizo mengi lakini sina namna lazima nikabiliane na kila kitu.Naomba uongee na Savanna na akwambie ni lini ninahitajika mahakamani.”
“Ouh god thank you so much.Ahsante sana Happy kwa uamuzi huu.Nitamtaarifu Savanna halafu nitakufahamisha jibu atakalonipa” akasema Margreth na kukata simu halafu akamtafuta Savanna na kumtaarifu kuhusiana na jibu la Happy” .Hizi zilikuwa ni habari njema sana kwa Savanna japokuwa alishindwa kujizuia kuwa na wasi wasi nini kitatokea pale Patrick na Happy watakapokutana tena
“Sijui ni kwa nini ninakuwa na wasi wasi mwingi kuhusu Patrick kuonana na Happy.Labda ni kutokana na historia yao kwamba kila wakutanapo hushindwa kuzizuia furaha zao basi mapenzi yao huanza upya.Lakini sipaswi kuwa na wasi wasi wowote.Patrick ni wangu na hakuna yeyote mwenye uwezo wa kumnasua toka katika mikono yangu.Ni Happy pekee ndiye mwenye kunipa wasi wasi “akawaza Savanna akiwa ofisini kwake
Ndege ya shirika la ndege la afrika kusini iliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam saa mbili za usiku.Miongoni mwa abiria waliokuwemo katika ndege hii ni Happy Kibaho ambaye monekano wake ulikuwa umebadilika sana na alionekana mrembo zaidi ya alivyokuwa alipoondoka Tanzania miezi zaidi ya kumi iliyopita.Kama ungekutana naye ghafla ingekuwia ugumu kidogo kumtambua.
Baada ya kukamilisha taratibu alitoka nje na kulakiwa na familia yake yote.Kilikuwa ni kipindi cha furaha kubwa kwa familia hii kukutana tena na mtoto wao ambaye hawakuwa wametegemea kama wangeonana naye tena hivi karibuni.Wote waliustaajabia uzuri wa Happy na namna alivyokuwa amebadilika.Hakukuwa na mwandishi yeyote wa habari aliyekuapo pale uwanjani kwani ujio wa Happy ulikuwa ni wa siri kubwa
“Wow Happy umebadilika sana” akasema mzee Kibaho na kumkumbatia mwanae kwa mara ya pili
“Ouh Dady ! nililazimika kufanya mabadiliko kidogo katika muonekano wangu wa zamani.Nilitaka nibadilike na kuwa Happy wa tofauti na zamani”
“You look so wonderfull and amazing as always.You look more than an angel” akasema mzee Kibaho kisha wote wakaelekea katika gari lao na kurejea nyumbani.Waliwasili nyumbani ambako kuliandaliwa tafrija ndogo ya kumkaribisha tena nyumbani Happy.Baada ya chakula na maongezi Happy akapelekwa chumbani kwake kulala.
“Margreth naomba nikalale chumbani kwako.Sitaki kulala katika chumba change cha zamani.Kuna kumbukumbu nyingi za nyuma ambazo nimekwisha anza kuzisahau.” Akasema Happy na kuelekea katika chumba cha Margreth.Kabla ya kulala,Happy akamkumbusha Margreth amtaarifu Savanna kwamba tayari amekwisha wasili na kama ana nafasi waonane kesho .Margreth akazitafuta namba za simu za Savanna akapiga.
Kwa muda wa dakika kadhaa sasa Savanna alikuwa anamkodolea macho Patrick bila kuongea lolote
“C’mon my angel ! Mbona unanitazama namna hiyo? Akauliza Patrick
“Sijui ni kwa nini nimejikuta nikiwa hivi siku ya leo.Natamani niendelee kukuangalia usiku kucha.Patrick nakupenda sana.Nakupenda zaidi ya unavyoweza kufikiri.Naomba niwe wazi kwako kwamba sintaweza kuishi maisha yangu bila ya kuwa nawe.” Akasema Savanna kwa sauti laini yenye mahaba mazito.Patrick akamvuta kwake na kumbusu kisha akasema
“Savanna wewe ni malaika wangu.Naomba ufahamu kwamba nakupenda na nitakupenda daima.Nakuahidi mara tu mambo haya yatakapokwisha basi tutafunga ndoa na tutaishi sote hadi kifo kitakapotutenganisha.” Akasema Patrck
“Patrick my love kwa nini tusifunge ndoa hata kabla ya kesi hii kumalizika? Binafsi sioni kipingamizi chochote cha kutuzuia tusifunge ndoa mapema” akasema Savanna
“Hakuna kipingamizi chochote Savanna cha kutufanya mimi nawe tushindwe kufunga ndoa.Kitu pekee kinachonisukuma na kunifanya niamni kwamba ni vyema kama tutafunga ndoa baada ya kesi kumalizika ni kuogopa kuchanganya mambo.Ninafikiria ni bora kama tukaelekeza nguvu katika jambo moja kwanza na baada ya kulimaliza basi tuelekeze nguvu katika jambo lingine ambalo ni ndoa yetu”
“Nakubaliana nawe Patrick japokuwa nilipenda sana jambo hili tulifanye mapema.Hata hivyo wazo lako zuri ni la msingi sana.Hatuna budi kuelekeza nguvu zetu zote kwa sasa katika kesi na baadae tushughulike na ndoa.” Savanna akastushwa na mlio wa simu yake.Akausogeza mkono na kuichukua
“Ni Margreth” akasema Savanna
“Anataka nini usiku huu? Akauliza Patrick
“sijui ngoja nimsikilize” akasema Savanna na kubonyeza kitufe cha kupokelea
“Hallo Margreth”
“Hallo Savanna.Samahani kwa kukusumbua usiku huu”
“Bila samahani Margreth.Jisikie huru kunipigia wakati wowote”
“Ahsante sana.Savanna nimekupigia kukutaarifu kwamba Happy amekwisha wasili.Amefika usiku huu.Ameomba kesho muonane hapa nyumbani”
“Ouh ok.Thats good news.Mwambie nashukuru sana kwa kufika kwake .Amefanya jambo kubwa na la maana sana na kesho nitakuja kuonana naye” akasema Savanna
“Kitu kingine Savanna,utakapokuja kuonana na Happy please don’t bring Patrick with you.Make sure Patrick and Happy they wont see each other.”
“Usijali Margreth.Siwezi kuambatana na Patrick. “
“Thank you Savanna.Good night”
“Good night Margreth” akajibu Savanna na kukata simu halafu akamgeukia Patrick
“Happy amekwisha wasili”
Patrick akavuta pumzi ndefu kisha akasema
“Hizo ni habari njema sana.”
“Yah.Amefanya jambo la maana ” akasema Savanna kisha akamkazia macho Patrick
“Nini Savanna? Mbona unaniangalia hivyo?
“Kuna kitu ambacho nahitaji uhakika toka kwako”
“Kitu gani Savanna?
“Are you sure there will be no problem when you see Happy again?
Patrick akamtazama Savanna akavuta pumzi ndefu na kusema
“Usihofu Savanna,nakuhakikishia kwamba hakutakuwa na tatizo lolote.Siwezi kukuficha kwamba tayari nimekwisha mtoa Happy moyoni mwangu lakini bado nina donge kubwa limenikaa kooni la kutaka kufahamu ni kwa nini alitenda vile ? Kwa nini alifanya kitendo kile cha kupiga picha na video za utupu na kuzivujisha? Zaidi ya yote kwa nini aliamua kunitelekeza gerezani wakati akifahamu fika kwamba nilikuwa nimeubeba mzigo ambao ulimuhusu yeye? Ningefurahi sana kama ningepata nafasi ya kumuuliza na kupata majibu ya maswali yangu lakini sintaweza kufanya hivyo kwani sitaki kukumbuka mambo ya nyuma.Kitu cha msingi ninachoshukuru ni kwa kukubali kwake kuja kutoa ushahidi.Baada ya kumaliza kutoa ushahidi sintahitaji kumuona tena.Nataka niendelee na maisha yangu nikiwa na wewe mpenzi wangu ambaye unanipenda,unanijali na kunithamini.” Akasema Patrick na uso wa Savanna ukajenga tabasamu pana,akainama na kumbusu halafu wakakumbatiana.
* * * *
Ni Happy ndiye aliyemuamsha mdogo wake Margreth asubuhi ili ajiandae awahi kazini.Usiku wa kuamkia siku hiyo ulikuwa mrefu sana kwa Happy na hakuweza kupata kabisa usingizi.Picha za matukio yaliyotokea miezi zaidi ya kumi iliyopita zilikuwa zkimjia kila alipojaribu kufumba macho.Alikumbuka toka kipindi alichokutana na Patrick shuleni Malangali Iringa hadi muda huu.
“Happy leo hujalala kabisa” akasema Margreth kwa sauti iliyojaa usingizi.Happy akatabasamu
“Mimi ni kawaida yangu.Huwa nina muda mchache sana wa kulala,muda mwingi ninafanya kazi.Amka ujiandae uende kazini” akasema Happy
Margreth akaamka akajindaa na kuondoa zake kuelekea kazini.Happy naye akatoka na kuanza kuizunguka nyumba yao.
Saa nne za asubuhi ilimkuta Savanna katika geti la akina Happy.Akapiga honi na Pendo mfanyakazi wa ndani akamfungulia geti na kumkaribisha ndani
Mtu wa kwanza kusalimiana naye alikuwa ni mzee Kibaho.Kwa kuwa mzee KIbaho alikuwa na haraka ya kuwahi katika shughuli zake hakuongea sana na Savanna akaondoka na kumuacha Savanna akiongea na mama yake Happy hadi pale Happy alipojitokeza.Savanna alishindwa kujizuia kutoa tabasamu pana sana baada kumuona tena Happy na namna alivyobadilika na kuwa mzuri
“My gosh ! huyu ni Happy au ni mzimu wake? Gosh ! she’s so pretty.She’s amazing.Dah ! binti huyu amejaaliwa uzuri wa aina yake” akawaza Savanna
“Hallow Savanna” akasalimu Happy
“Hallow Happy” akajibu Savanna na kuinuka kisha wakakumbatiana
“karibu tena nyumbani Happy” akasema Savanna
“Ahsante Savanna,nimefurahi sana kurejea tena nyumbani.Poleni na matatizo ya kila siku”
“Tumekwisha poa Happy.” Akasema Savanna halafu mama yake Happy akainuka na kuwaacha peke yao pale sebuleni ili kuwapa nafasi nzuri ya kuongea mambo yao kwa uhuru.
“Savanna twende bustanini ,naona hapa sebuleni hapatufai kwa maongezi yetu” akasema Happy kisha wakainuka na kuelekea bustanini
“Karibu sana Savanna.Habari za siku? Akaanzisha mazungumzo Happy baada ya kufika bustanini
“Habari nzuri Happy.Nimefurahi tena kukuona.Umebadilika sana.Ouh my gosh you are so beautiful.You are mazing” akasema Savanna na Happy akatabasamu
“Thank you Savanna” akajibu Happy
“Vipi maisha yako kwa ujumla? Akauliza Savanna
“Namshukuru Mungu .Kwa kweli Mungu anaweza.Ukimuomba kwa dhati Mungu anajibu.Nilikwisha kata tamaa kabisa na maisha yangu.Nilimuomba Mungu nikamlilia anisaidie na kweli amenisaidia na hali yangu imebadilika kama unavyoniona” akasema Happy na kucheka kidogo
“Nilipatwa na wasi wasi mkubwa Christine aliponipigia simu na kunitaarifu kwamba umetoweka pale hotelini Kigali na hawajui mahala ulipo.” Akasema Savanna na kumfanya Happy acheke kidogo
“Savanna kwanza kabisa napenda nikushukuru wewe binafsi kwani msaada wako ulikuwa mkubwa mno na ambao siwezi kuulipa.Ulinisaidia sana kujitambua na kunifanya niamue kuishi tena.Baada ya kukaa kwa muda pale Kigali nilipata wazo la kuondoka .Niliamua niende Marekani .Nilijua ile ndiyo sehemu salama kwa mimi kuishi tofauti na pale Rwanda ambako ni karibu sana na Tanzania.Vile vile tayari taarifa zangu zilikwisha fika kule na tayari nilianza kufahamika.Mtu pekee aliyenisaidia nikarejea tena Marekani ni Mike.Ninamshukuru sana kwa msaada wake mkubwa.Kwa sasa ninaishi na kufanya kazi Los Angeles na maisha yangu yanakwenda vizuri.” Akasema HappyCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“So you are back together,you and Mike” akauliza Savanna
“I’m sorry to say this Savanna but yes ! we’re back together and deeply in love na tunategemea kufunga ndoa” akasema Happy huku akitabasamu kuona aibu kwa mbali
“Ouh ! Congraturations” akasema Savanna
“Thank you” akajibu Happy kisha kimya kifupi kikapita
“What a stupid woman..Yaani anadiriki kusema wazi wazi kwamba amerudiana na Mike na wanatarajia kufunga ndoa huku akisahau kwamba alimuacha Patrick akisota gerezani kwa kosa ambalo hakulitenda.” Akawaza Savanna.Happy akasema
“Savanna haikuwa rahisi kwangu kuamua kuja tena Tanzania.Niliapa kutokurudi tena Tanzania lakini kutokana na uzito wa suala lenyewe nimevunja kiapo changu ili na mimi niweze kutoa msaada wangu japo mdogo kwa Patrick ambaye alifanya jambo la kijasiri sana kuniokoa mimi nisikae gerezani kwa hiyo isingekuwa vyema kama ningekataa kuja kumtolea ushahidi .Nimekuita hapa ili unipe mwongozo wa kinachoendelea na ninachotakiwa kukisema mahakamani” akasema Happy
“Happy nimefurahi sana kusikia maendeleo yako na kukuona ukiwa ni mwenye furaha.Lakini kabla hatujaendelea na maongezi yetu aren’t you gonna ask?
“Ask what? Happy akashangaa
“How he’s doing”
“Savanna,Patrick ni mtu ambaye nilimpenda kwa moyo wangu wote.Sijawahi kupenda mtu kama nilivyompenda yeye.Amenifanyia mambo mengi ambayo hakuna mtu yeyote anaweza akanifanyia.Patrick made me a woman.Kuna mengi ambayo naweza kueleza kwa siku nzima kuhusu Patrick lakini naweza kusema kwamba maisha ni kitu cha ajabu sana.Pamoja na upendo wote na kila kitu alichonifanyia Patrick lakini hivi sasa I’m fighting to forget him.Its difficult but I thank God I’m doing fine without him.Ninaamini mimi na Patrick hatukupangwa tuwe pamoja.” Akasema Happy akanyamaza akameza mate na kuendelea
“Sijataka kumuulizia kwa sababu ninajua mimi ni mtu ambaye hataki kuniona tena katika maisha yake na ana hasira kubwa na mimi kwanza kwa kuziona picha zile na pili kwa kuondoka na kumuacha gerezani.Savanna moyo wangu unaniuma sana japokuwa hakuna anayeweza kulifahamu hilo.Bado kitendo kile cha kudhalilishwa kwa zile picha chafu hakijapona na kurudi kwangu tena Tanzania kumekitonesha kidonda change.Sina hakika kama ulimueleza Patrick ukweli halisi wa kilichotokea.Japo kwa ufupi unaweza ukanieleza anaendeleaje?
“Patrick is fine.He’s doing ok.Tuliibadili kesi na kuwa kesi ya kuua bila kukusudia na akapatiwa dhamana.Anaendelea vizuri na maisha yake mapya na kwa sasa ni meneja wa kiwanda cha kusindika nyama.” akasema Savanna
“Ouh that’s great.Is he married ? akauliza Happy huku akitabasamu.Savanna naye akatabasamu
“Not yet”
“Ouh Gosh ! what he’s waiting for? Is he still waiting for me?
“Tunasubiri mambo haya yamalizike ndipo tuanze taratibu za ndoa yetu” akasema Savanna huku akitabasamu
“We? are you two together? Akauliza Happy kwa mshangao.
“Yes ! we’re together now.We live together though not yet married” akasema Savanna
Happy akavuta pumzi ndefu na kumeza fundo la mate.Akapatwa na kigugumizi akakohoa kidogo na kusema
“Congraturations guys” akasema Happy na sura yake ilionyesha mabadiliko kidogo.
“Thank you “ akasema Savanna.Ni wazi maneno yale ya Savanna yalimchoma Happy.Savanna aliligundua hilo na hakutaka kuendeleza maongezi kuhusu mahusiano yake na Patrick na badala yake akaendelea kumweleza Happy kuhusiana na mwenendo wa kesi na namna atakavyotoa ushahidi wake.Baada ya maongezi marefu Savanna akaondoka zake.
* * * *
Ni alhamisi siku ambayo Happy alitakiwa kusimama kizimbani na kutoa ushahidi wake.Siku hii aliamka mapema sana asubuhi akaanza kujiandaa.Alikuwa mkimya na mwenye wasi wasi.Mpaka ilipotimu saa tatu za asubuhi tayari alikwisha jiandaa tayari kabisa kuelekea mahakamani .Familia nzima ilikuwa imejiandaa kuandamana naye mahakamani.
“Are you ready Happy? akauliza mzee Kibaho
“I’m ready dady though I’m a bit nervous” akajibu Happy
“Be strong .You can do it” akasema mzee Kibaho
“Yes Dady.I’ll be strong.I need to finish this”
“Tuko pamoja Happy usiogope” akasema Margreth kisha kwa pamoja wakaingia garini na safari ya kuelekea mahakamani ikaanza.
Mahakama ilifurika watu tofauti na siku za kawaida.Tetesi za Happy kuwepo mahakamani siku hii zilisambaa na kuwafanya watu wafurike mahakamani ili kumuona mrembo huyu ambaye aliviteka vyombo vya habari miezi zaidi ya kumi iliyopita kutokana na skendo zake mbali mbali na hasa ile ya mwisho ambapo picha na video zake za utupu vilisambaa katika magazeti na mitandao na kisha akatoweka ghafla bila kujulikana alielekea wapi.Wengi walikuwa na hamu ya kumuona tena.
Saa tano na dakika ishirini,Happy aliwasili mahakamani akiwa ameongozana na familia yake.Pale mahakamani alipokewa na Savanna na kuongozwa kuelekea ndani ya jengo la mahakama.Wengi hawakuweza kumtambua kwa haraka kutokana na namna alivyokuwa amebadilika.
“Nashukuru sana umekuja Happy.Naomba ondoa wasi wasi” akasema Savanna
“Usijali Savanna.I’ll do my best” akajibu Happy huku uso wake ukijilazimisha kutabasamu
Savanna aliingia ndani ya mahakama na Happy akaufungua mlango wa chumba kimoja mle mahakamani akaingia ndani na kumuomba Happy naye aingie.Mara tu alipoingia ndani ya chumba kile Happy akapatwa na mstuko mkubwa.Alitumbua macho kana kwamba ameona mzuka au kitu cha kushangaza.Alibaki amesimama huku akihisi mwili wake kuingiwa na baridi.Alikuwa anatazamana na Patrick ambaye naye alipatwa na mstuko .Chumba kikagubikwa na ukimya mzito.Savanna ambaye alisimama katikati yao akawaangalia wote na kisha akasema
“I’ll be outside.I’ll leave you guys alone so that you can great each other” akasema Savanna na kutoka mle chumbani.Patrick na Happy waliendelea kutazamana huku wote wakiwa bado wamesimama.Baada ya kama dakika mbili Patrick akakohoa kidogo na kusema
“Hallow …Ha..Happy”
“Hallo Patrick” akajibu Happy kwa sauti ndogo yenye kutetemeka.Kimya kidogo kikapita Patrick akasema
“Nimefurahi kukuona tena Happy”
“Hata mimi nimefurahi kukuona tena Patrick” akajibu Happy.Baada ya maneno hayo machache ukatanda ukimya mzito mle chumbani.Hakuna aliyemsemesha mwenzake.Patrick akaketi kitini na kuinama chini.Happy akamtazama kwa makini na kutaka kusema neno akafumbua midomo yake lakini sauti ikakwama.
“ouh my gosh ! Hiki ndicho nilichokuwa nakikwepa.Sikutaka kuonana tena na Patrick ana kwa ana.Kwa nini Savanna amenikutanisha naye wakati tulikubaliana kwamba sitaki kuonana na Patrick? Ouh gosh ! Nitafanya nini sasa? .akawaza Happy ,akaufunika uso wake kwa viganja vya mikono.Machozi yalikuwa yanamtoka
“God please help me.Niko katika wakati mgumu sana.Kumbu kumbu zote za nyuma zimerejea ghafla baada ya kumuona tena Patrick.I feel so guilty.I don’t know what to do anymore.” Akawaza Happy na mara mlango ukafunguliwa Savanna akaingia
“Are you guys ok? Akauliza Savanna
“Yes ! we’re ok” akajibu Happy.Macho yake yalionekana kujaa machozi.Savanna akamuuliza
“Are you ready Happy?
“Yes ! Yes !.I’m ready” akajibu Happy huku akifuta machozi
“Patrick ni muda sasa wa kuingia mahakamani.” Akasema Savanna Patrick akainuka na kuelekea katika chumba cha mahakama.
“Savanna kwa nini umefanya hivi? Kwa nini umenikutanisha na Patrick? Akauliza Happy
“Happy ni vigumu kukwepa kuonana na Patrick lakini hata hivyo tutaongea baadae lakini kwa sasa hebu tuelekeze mawazo yetu katika jambo lililotuleta hapa” akasema Savanna huku akikusanya mafaili yake
“Usiogope Happy.Ondoa hofu.You can do it” akasema Savanna na kisha akaongozana na Hapyy kuelekea katika chumba cha mahakama.Happy alikuwa anamulikwa na mianga ya kamera za waandishi wa habari waliofika kwa wingi mahakamani
* * * *
Saa nane za mchana Happy alimaliza kutoa ushahidi wake.Toka mashahidi wa upande wa utetezi walipoanza kutoa ushahidi wao haikuwahi kutokea siku ambayo Mahakama ilikumbwa na simanzi kama siku hii ya leo.Watu wote walikuwa kimya kabisa wakimsikiliza Happy
Happy ambaye alikuwa anaongea kwa hisia kubwa na wakati mwingine kulazimika kusimama na kufuta machozi,alianza kwa kuielezea mahakama historia fupi ya mahusiano yake na Patrick toka walipokutana shuleni,wakajenga mahusiano hadi walivyopotezana baada ya yeye kuondoka na kwenda masomoni Marekani.Aliielezea mahakama namna Veronika alivyotunga uongo na kuwatenganisha yeye na Patrick hadi walipokuja kuonana tena siku aliyoshinda taji la miss Tanzania.Aliendelea pia kuielezea mahakama juu ya maamuzi waliyoamua kuyachukua kwa pamoja yeye na Patrick ya kuachana na wapenzi wao na kuurejesha tena uhusiano wao kwani bado walikuwa wanapendana.Alikiri kumpenda Patrick zaidi ya anavyoweza kueleza na ndiyo maana alikuwa tayari kuachana na mpenzi wake Mike na kuurejesha uhusiano wa kimapenzi na Patrick.
Happy aliieleza makahama kilichotokea jioni ile na kusababisha kifo cha Vero.Sehemu hii ilikuwa ni sehemu ambayo iliwatoa machozi watu wengi akiwamo Patrick ambaye alishindwa kuyazuia machozi kumchuruzika mashavuni pale Happy alipotamka kwamba Vero aliteleza na kujigonga ukutani wakati akinyang’anyana silaha na Patrick ,silaha ambayo alitaka kuitumia kufanya mauaji
Baada ya kumaliza kutoa ushahidi wake na mahakama kuahirishwa,Happy alitoka huku ameinamisha kichwa.Bado machozi yaliendelea kumtoka.Familia yake ilikuwa pamoja naye wakiongozana kutoka nje ya jengo la mahakama.Waandishi wa habari na wapiga picha waliendelea kumfuata Happy na kumpiga picha nyingi.Ili kuwakwepa waandishi wa habari waliokuwa wakimsonga Happy,familia yake ikamuwahisha katika gari na kufunga milango kabla gari halijaondoka Happy akaomba wasubiri alitaka kuongea na Savanna.Margreth akampigia simu Savanna na kumfahamisha kwamba Happy anahitaji kuonana naye.Baada ya kama dakika tano Savanna akafika
“Thank you Happy.You did great” akasema Savanna.Happy akafuta machozi na kusema
“Nini kitaendelea baada ya hapa?
“Tayari tumefunga ushahidi kwa upande wetu.Nitakufahamisha baadae nini kitakachoendelea” akasema Savanna ,kisha wakaagana na kuondoka
Baada ya kuachana na akina Happy,Savanna naye akaingia garini na Patrick wakaondoka .Hawakutaka kupita sehemu yoyote na moja kwa moja wakaelekea nyumbani.Ndani ya gari ,Patrick alikuwa kimya sana
“Say something my love” akasema Savanna baada ya kuona kimya kimezidi mle garini
“I have nothing to say my love” akasema Patrick
“Still thinking about her?
“No ! She’s not in my thoughts anymore.Ninachowaza ni nini kinakwenda kutokea baada ya hapa”
“Usihofu Patrick.Niamini ninachokwambia kwamba mpaka hapa tumefanya vizuri sana na nina hakika tutashinda kesi hii.Ushahidi uliotolewa ni dhahiri unaendana na hoja tuliyoijenga ya kuitaka mahakama ikuache huru.” Akasema Savanna
“Nilihitaji sana kuonana na Happy ana kwa ana.Nina maswali mengi ambayo nataka anijibu lakini mara tu nilipomuona sikuweza tena kuwa na ujasiri wa kumuuliza chochote.” Akawaza Patrick
“Happy amebadilika sana.Uzuri wake umeongezeka maradufu.Inaonekana ameridhika na maisha anayoishi sasa.She’s already forgoten about me.Kweli dunia ina maajabu sana.Happy msichana ambaye nilimpenda kwa moyo wangu wote na tuliwekeana ahadi lukuki kwamba hatutaachana hadi kifo kitutenganishe lakini leo hii tumetazamana kama hatujuani,kama hatujawahi kuwa katika mahusiano.Nilipoteza kila kitu kwa ajili yake lakini pamoja na mambo yote aliyonitendea hakuthubutu hata kusema samahani kwa mambo aliyoyafanya.Inaonekana hajutii kabisa kitu alichokifanya.” Akawaza Patrick
“I was so stupid kuamua kuacha kila kitu kwa sababu yake nikiamini kwamba ndiye mwanamke ambaye ananifaa maishani.Nilikuwa na upofu wa fikra nikiamini kwamba hakuna mwanamke mwingine ambaye anafanana naye.Nilifanya kosa kubwa sana.Kwa sababu yake nimempoteza Vero mwanamke aliyenipenda kwa moyo wake wote,nimempoteza baba yangu,marafiki na nilipoteza hata dira na mwelekeo mzima wa maisha yangu na mwishowe na yeye mwenyewe akanikimbia na kuniacha nikiteseka gerezani.Anyway sitakiwi kuwaza sana kuhusu mambo haya.Yaliyopita yamepita na kinachotakiwa kwa sasa ni mimi kuelekeza nguvu na akili yangu katika kuyajenga maisha yangu na Savanna.Hata hivyo Happy amenifundisha kitu kimoja kikubwa.Amenisaida kumjua binadamu ni kiumbe wa namna gani.” akawaza Patrick halafu akageuza shingo yake na kumtazama Savanna ambaye naye aligeuza shingo yake wakatazamana na kutabasamu
“Why you are looking at me like that?
“Its nothing Savanna.” Akasema Patrick na kutabasamu halafu akaegemeza kichwa chake kitini.
“Namshukuru sana Mungu kwani pamoja na yote yaliyotokea lakini bado ameendelea kuwa upande wangu na ameniletea tena mwanamke mwingine ambaye ninaamini ndiye aliyeumbwa kwa ajili yangu.Savanna ananipenda kwa moyo wake wote .Amekuwa nami toka matatizo haya yalipotokea .Amenipigania kwa nguvu zake zote.Ananijali na kuniheshimu.Ni yeye ndiye aliyeokota vipande vya moyo wangu uliovunjwa vunjwa na Vero akaviunga na kunifanya nirejee tena katika maisha yangu ya kawaida.Yeye ni sababu ya mimi kuamua kupenda tena.Hakika huyu ndiye mwanamke ambaye nitampenda kwa moyo wangu wote na kwa siku zote za uhai wangu.Hata siku moja sintathubutu kumtoa chozi.Wanawake kama yeye ni nadra sana kuonekana zama hizi zilizojaa ulaghai.Najiona ni mtu mwenye bahati kubwa sana kuwa na Savanna na nitamuomba Mungu atujalie maisha mazuri na yenye furaha” akawaza Patrick halafu akamgeukia Savanna na kumtazama
“I love you Savanna.I love you so much.I just want you to know that you mean a lot to me” akasema Patrick na kumfanya Savanna atabasamu.akauchukua mkono wa kulia wa Patrick na kuubusu.
“I love you too Patrick more than words can say” akasema Savanna na safari ikaendelea
“Happy jitahidi ule walau kidogo.Nyamaza kulia” Margreth alikuwa anambembeleza Happy ambaye toka wamerejea amekuwa akilia
“Margreth ninajuta ni kwa nini nimerudi Tanzania” akasema Happy huku akifuta machozi.
“Usiseme hivyo Happy.Umefanya jambo la maana sana kuja kutoa ushahidi wako kwa Patrick”
“Nilidhani nimekwisha msahau Patrick na hayupo tena moyoni mwangu lakini nilikuwa najidanganya”
“kwa nini unasema hivyo Happy?
“Margreh sikufichi mara tu nilipoonana na Patrick moyo wangu ulistuka .Nilihisi kama moyo wangu unataka kusimama.Nilikosa kitu cha kuongea,midomo ilikuwa inanitetemeka .Mwili wote ulikuwa wa baridi.Ouh gosh !!” akasema Happy
“Pale mahakamani nilikuwa natoa ushahidi wangu huku machozi yananitoka kutokana na uchungu niliokuwa nao moyoni baada ya kuonana tena na Patrick.Historia nzima ya maisha yangu ya nyuma ilirudi tena .Niliona aibu kubwa ,nilijisikua uchungu mkubwa na kuutambua ujinga nilioufanya wa kuamua kuondoka na kumuacha Patrick akiteseka gerezani” akasema Happy akainama na kukishika kichwa chake.Margreth akamtazama na kusema
“Sasa utafanya nini Happy?
“I don’t know what to do Margreth.Nahisi kuchanganyikiwa kabisa.Sijui nifanye nini” akasema Happy
“Kwa nini usifanye mpango wa kuonana na Patrick ili muongee na muyaweke sawa mambo haya? Nadhani mkikaa na kuyaongea mambo haya na mkaombana msamaha nyote mtabaki na amani.Nina hakika hata yeye mwenyewe ana hamu ya kuongea na wewe.Nadhani ni wakati muafaka sasa wa Patrick kufahamu kilichotokea.Hata wewe mwenyewe umekuwa mgumu sana kueleza kuhusu tukio lile na hata sisi ndugu zako mpaka leo hii hatufahamu nini kilitokea na ni akina nani waliokutenda kitendo kile.Naona ni wakati muafaka sasa wa kuliweka wazi jambo hili.Nina hakika hata Patrick angependa kusikia sababu iiliyokufanya ukaondoka ghafla na kumuacha peke yake gerezani.” Akasema Margreth
“Margreth kwa mara ya kwanza najilaumu sana kwa jambo nililolifanya.Nimetambua kosa langu.Nilipaswa kusimama imara na kueleza kilichotokea.Sikupaswa kuikimbia nchi.Sikupaswa kumuacha Patrick peke yake gerezani.Kwa hivi sasa nimechelewa sana na hakuna ambaye ataniamini hata nikisema ukweli.Natamani nipate walau dakika hata mbili za kuongea na Patrick na kumfahamisha juu ya kilichotokea na kumuomba anisamehe.lakini….” Happy akasita
“lakini nini Happy?CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Patrick has moved on.Tayari yuko katika mahusiano na Savanna na wana mipango ya kufunga ndoa mara tu baada ya kumalizika kwa kesi” akasema Happy
“Tell me you are jocking.!!!! Margreth akashangaa
“Si utani Maggie.Haya ni maneno toka katika kinywa cha Savanna mwenyewe”
“Gosh .! akasema Margreth
“Hiyo ndiyo hali halisi.Maisha yana maajabu sana” akasema Happy kwa huzuni
“I think there must be ana explanation to this.Hainiingii akilini kabisa.Ninachofahamu ni kwamba Parick anakupenda sana na yuko tayari hata kufanya jambo lolote kwa ajili yako.Mambo aliyoyafanya Patrick kwako ni makubwa sana na yananifanya nisiwe mwepesi kuamini kama ni kweli Patrick anaweza akahamisha penzi lake kwa Savanna katika kipindi kifupi namna hii”akasema Margreth.Happy akamtazama mdogo wake na kusema
“Margreth bado kuna mambo mengi ambayo hujayafahamu bado lakini kitu kimoja ambacho napenda ufahamu ni kwamba I’m no longer in Patrick’s heart”
“Kwa nini unasema hivyo Happy? Una hakika na unachokisema?
“Mbona umelin’ang’ania sana suala la kutaka kuonana na Patrick ? Akauliza Happy
“Naomba usinielewe vibaya Happy.Lengo langu si kutaka wewe na Patrick mrudiane kwani hilo ni jambo ambalo haliwezekani kwa sasa kwani kila mmoja tayari amekwisha anza maisha mapya.Ninachokitaka mimi ni wewe na Patrick mkutane muongee na mzimalize tofauti zenu ili muishi kwa amani.Kama hutafanikiwa kuonana na Patrick na ukamfahamisha kilichotokea ,nina hakika hautakuwa na amani kwa maisha yako yote yaliyobakia kwa sababu ni wewe ndiye uliyeondoka bila kumtaarifu chochote Patrick.Kama alifanikiwa kuziona picha zile na jinsi ulivyoondoka ghafla bila taarifa yoyote ni wazi Patrick ataelewa kwamba ulifanya kitendo kile .Suluhisho hapa ni wewe kuonana na Patrick mkaongea na ukamueleza kila kitu bila kumficha.I swear to god you’ll be free “
“Margreth sikatai ushauri wako kwani hata mimi ninahitaji sana kupata nafasi ya kuonana na Patrick lakini laiti ungeuona uso wa Patrick leo mara tu niliponana naye ungekubaliana na ninachokisema kwamba siko tena katika moyo na akili yake.He hates me.I deserve all that for what I did to him.It hurt so much” akasema Happy na kushindwa kuvumilia kutokwa na machozi
“Usilie Happy.Kama kweli una nia ya dhati ya kuonana na Patrick ili muongee na kuyaweka sawa mambo haya basi tunatakiwa tutafute njia.”
“Nahitaji sana kuonana na Patrick lakini sijui ni kwa namna gani nitafanikiwa kwa hilo” akasema Happy
“Happy I‘m your sister and a friend too so tell me the truth” akasema Margreth
“What truth?
“Do you still love Patrick?
“Baada ya kurejesha uhusiano wangu na Mike niliamini kwamba Patrick amekwisha toka moyoni mwangu lakini baada ya kuonana naye leo nimegundua kitu kimoja” Happy akasita na kutazama chini.
“Umegundua kitu gani Happy? Akauliza Margreth
“I was so wrong.Patrick ni mtu ambaye siwezi kumfuta kirahisi katika moyo wangu.To answer your question Yes I still love him.” Maneno yale yakamfanya Margerth akae kimya kwa muda akamuangalia dada yake.
* * * *
Ni saa nne za usiku,Linah rafiki mkubwa wa Loniki alikuwa amejilaza katika sofa kubwa lililokuwa sebuleni.Kama ilivyokuwa kwa watu wengine wenye ukaribu na familia ya Vero,Linah naye alikuwepo mahahakani kusikiliza ushahidi wa Happy.Baada ya kutoka mahakamani alirejea moja kwa moja nyumbani kwake.Toka amerudi alikuwa amejilaza katika sofa hili akitazama runinga huku katika meza ndogo iliyokuwa pembeni kulikuwa na chupa kubwa ya mvinyo
“Leo nilipomuona Happy mahakamani moyo wangu ulistuka sana.Niliumia mno hasa nikikumbuka kitendo tulichomfanyia.Kwa nini nilikubali kushirikiana na Loniki kumfanyia Happy mambo yale? Najilaumu sana kwa jambo lile.Happy hastahili hata kidogo kufanyiwa ukatili wa namna ile.” akawaza Linah halafu akachukua glasi yake ya mvinyo na kupiga funda kubwa
“Maelezo aliyoyatoa mahakamani yalinitoa machozi.Aliongea kwa uchungu sana na kwa hisia kubwa.Wote tuliokuwa hatufahamu historia yake na Patrick leo tumeufahamu ukweli.Sioni sababu ya kuwalaumu Patrick na Happy kwa sababu aliyeanzisha haya yote ni Vero pale alipodiriki kutunga uongo na kuwatenganisha.Uongo wake umekuja kumuumbua na badala yake akataka kufanya mauaji.Stupid girl” akawaza Linah na kuchukua glasi yake ya mvinyo akanywa
“Naungana na yule wakili anayeongoza jopo la mawakili wanaomtetea Patrick kuitaka mahakama imuachie huru Patrick.Hakuna kesi ya maana hapa.Nasikitika niliingia kichwa kichwa katika jambo hili kabla sijaufahamu ukweli halisi.Sitaki tena kushirikiana na Loniki” akawaza Linah lakini ghafla akastuka
“Mhh !! Inabidi nitumie akili nyingi ili kuanza kumkwepa Loniki na kumfanya asiendelee na mipango yake ya kulipiza kisasi.Mpaka sasa lengo lake bado halijabadilika. Bado anataka Patrick auawe.Amekuwa akinitumia fedha nyingi ili niweze kusuka mipango ya kumuua Patrick.,fedha ambazo nimekuwa nikigawana na Khumalo.Iwapo atagundua kwamba nilikuwa namdanganya na kwamba hakuna mpango wowote wa kumuua Patrick basi lazima kutazuka vita kubwa sana kati yangu naye.Ngoja kwanza nimpigie simu nimpe taarifa za kilichotokea leo mahakamani” akawaza Linah na kuinuka akachukua simu yake akampigia Loniki.
“hallow Loniki,habari za London?
“London kwenda,habari za huko nyumbani?
“Huku nako ni kwema kabisa” akasema Linah na kuvuta pumzi.Sauti ya Loniki ilionyesha ni kama mtu ambaye hakuwa na furaha kama ilivyozoeleka
“Mama kanipigia simu na kuniambia kwamba Happy alikuwepo mahakamani leo na ametoa ushahidi wake” akasema Loniki
“Ndiyo Lonny,Happy ametokea mahakamani leo na ametoa ushahidi wake “ akajibu Linah
“Vipi kuhusu mwenendo mzima wa kesi? Akauliza Loniki
“Lonny pamoja na jitihada zote tulizozifanya,naomba niwe wazi kwako kwamba kutokana na ushahidi uliotolea mahakamani na upande wa utetezi na hasa huu ambao umetolewa leo na Happy,tuna kazi ngumu ya kufanya kuhakikisha kwamba Patrick anafungwa.Niliongea na mwanasheria mmoja wa serikali na akaniweka wazi kwamba ushahidi uliotolewa mahakamani ni mzito sana na unatosha kabisa kuishawishi mahakama kumuachia huru Patrick”
“Damn it !!..That wont happen..!! akaongea Loniki kwa ukali
“Linah nilikuachia kazi hii na ukanihakikishia kwamba utafanya kila uwezalo na kuhakikisha kwamba Patrick anauawa au anafungwa gerezani .Nimekuwa nakutumia fedha nyingi kwa ajili ya kufanikisha hayo sasa iweje leo unipe kauli yenye utata namna hiyo? Unataka kunihakikishia kwamba juhudi zote tulizofanya na mamilioni yote ambayo nimekuwa nakutumia wewe na Khumalo nimetwanga maji kwenye kinu? Akauliza Loniki
“Loniki wewe ni zaidi ya rafiki kwa hiyo naomba uniamini kile ninachokwambia.Ni kweli mipango ilifanyika na kama nilivyokueleza .Nimekwisha hakikishiwa na watu wazito mahakamani kwamba Patrick lazima afungwe hata kama kutatolewa ushahidi wa aina gani.Kwa hiyo usiwe na wasi wasi Loniki” Linah akamdanganya Loniki
“Sawa Linah.Naomba iwe hivyo lakini endapo itatokea vinginevyo sijui itakuaje kwa sababu tumepoteza fedha nyingi sana mpaka sasa na hakuna matunda yoyote.Lengo langu mimi lilikuwa kuwaua Patrick na Happy lakini ni wewe Na Khumalo ndio mliopinga jambo hilo kwa hiyo basi hakikisheni kwamba kwa vyovyote itakavyokuwa kama haitawezekana kumuua basi lazima Patrick afungwe gerezani.Endapo mtashindwa kulitekeleza hilo basi nitarudi mimi mwenyewe na safari hii sintakuwa na namna nyingine zaidi ya kutafuta watu wengine na kuwaua Patrick na Happy.Inaniuma sana kuwaona washenzi hawa wakiendelea kuvuta hewa hii safi wakati mdogo wangu waliyemkatili uhai wake anaoza kaburini.” Akasema Loniki kwa ukali
“Loniki naomba unisiklize vizuri.Suala hili si jepesi kama unavyolifikiri.Tulilipinga wazo lako la kutaka Patrick na Happy wauawe kutokana na athari ambazo zingeweza kujitokeza.Lakini kwa kuwa lengo lako lilikuwa ni kulipa kisasi ndiyo maana tukapendekeza kwamba badala ya kufanya mauaji basi tuyafanye maisha yako yawe magumu na Patrick afungwe kigerezani.Hicho ndicho nimekuwa na kifanya na Khumalo muda huu wote..” akasema Linah ambaye alikuwa ameukunja uso wake kwa hasira. Na mara simu ikakatwa
“Amekata simu Sitaki tena kujihusisha na mipango ya Loniki.Sitaki kutafuta mgogoro na vyombo vya dola kwa sababu ya hivi vimilioni alivyokuwa ananitumia.Ninayamudu maisha yangu mwenyewe.Biashara zangu zinaniingizia fedha nyingi na kunifanya niishi kama binti mfalme.Patrick na Happy hawana kosa lolote la kustahili kutendewa hivyo anavyotaka..Najua atakuwa amekasirika lakini simuogopi hata kidogo.Tena ngoja nimpigie simu Khumalo nimueleze kuhusiana na ujinga wa Lonny” akawaza Linah
* * * *
Saa nne za usiku Happy bado alikuwa amekaa kitandani.Alikuwa ameegemea kitanda macho yake yamemvimba
“Happy tafadhali usiendelee kulia.Toka umerudi umekuwa unalia.Tafadhali usilie tena.Inatosha sasa” akasema Margreh aliyekuwa pembeni ya dada yake
“let me cry Margreth.Nina uchungu mwingi sana na sijui nifanya nini.I’m confused” akasema Happy.Margreth akamtazama dada yake usoni akainuka na kuiendea meza ndogo akachukua simu
“Mpigie savanna sasa hivi na umwambie kwamba unahitaji kuonana na Patrick” akasema Margreth.Happy akamtazama na kusema
“Are you sure you want me to do this? Akauliza Happy
“Happy kama kweli una nia ya dhati ya kutaka akili yako itulie na maisha yako yawe na amani tafadhali ongea na Patrick”
“Nitamwambia kitu gani? Ninaogopa Margreth”
“Ukweli.Mweleze ukweli” akajibu Margreth na kuzitafuta namba za Savanna akapiga
“Hallow” akasema Savanna baada ya kupokea simu
“Hallow Margreth…!! Akasema tena Savanna.Happy akakohoa kidogo na kusema
“Savanna its me Happy”
“Ouh Happy.How are you my dear? Akasema Savanna
“I’m ok Savanna”
“Nafurahi kusikia kwamba unaendelea vizuri”
“Yah !..” akasema Happy
“Happy napenda nikushukuru sana kwa kitendo ulichokifanya leo.You did it so well” akasema Savanna
“Yah ! akajibu Happy na kumfanya Savanna astuke kidogo
“Happy are you ok? Akauliza Savanna.Happy hakujibu kitu
“Happy is there anything wrong? Akauliza tena Savanna
“Savanna I’m sorry to disturb you at this time” akasema Happy
“Usijali Happy.Hujanisumbua chochote.Muda wowote unaruhusiwa kunipigia simu.Una tatizo lolote Happy? Akauliza Savanna.Happy akasita kidogo kisha akasema
“Savanna unaweza kuniruhusu niongee na Patrick japo kwa dakika mbili? Akasema Happy.Savanna akasita kidogo na kusema
“Hakuna tatizo Happy.Patrick huyu hapa ongea naye” akasema Savanna na kumpatia Patrick simu
“Happy anahitaji kuongea nawe” akasema Savanna.Patrick akamtazama usoni
“Ongea naye”akasisitiza Savanna.Patrick akaiweka simu sikioni
“Hallow” akasema
“Hallow Patrick “ akajibu Happy
“Are you ok ? akauliza Happy
“I’m ok” akajibu Patrick kwa ufupi
“Savanna ameniambia kwamba unataka kuongea na mimi” akasema Patrick
“Ndiyo Patrick.Kwanza samahani sana kwa kukusumbua”
“Bila samahani Happy”
“Patrick sina hakika kama utakuwa tayari lakini nahitaji kukuona.Nina maongezi nawe ya maana sana”
“Maongezi na mimi?! Patrick akashangaa
“Ndiyo Patrick.Nina maongezi nawe kidogo”
“Unataka tuongee kuhusu nini Happy?
“Patrick kuna mambo ambayo nahitaji kukueleza.Kuna mambo ya maana sana ambayo unahitaji kuyafahamu”
“mambo hayo huwezi kunieleza simuni sasa hivi?
“hapana Patrick.hatuwezi kuongea simuni.Nahitaji sana kuonana nawe ana kwa ana” akasema Happy
“Sawa Happy niko tayari kuonana nawe ili unieleze hicho unachotaka kunieleza lakini nina sharti moja tu kwamba lazima na Savanna kipenzi cha roho yangu awepo.Yeye anastahili kufahamu kila kinachoendelea katika maisha yangu.Uko tayari kwa hilo? Akauliza Patrick lakini ghafla simu ikakatika ‘
“Amekata simu” akasema Patrick
“Mpigie pengine ni tatizo la kimawasiliano” akasema Savanna
“Hakuna sababu ya kumpigia.Isitoshe sina mpango na sihitaji kuonana naye sasa na katika maisha yangu yote yaliyobaki.Biashara ya mimi na yeye ilikwisha pale alipoamua kuondoka na kunitelekeza gerezani” akasema Patrick
“Pengine ana jambo la maana anataka kukwambia” akasema Savanna
“Hana tena jambo lolote la maana ambalo anaweza akanieleza.Ninachoshukuru ni yeye kukubali kuja kunitolea ushahidi na baada ya hapo mimi naye hatuna tena mahusiano.Mahusiano yangu naye yaliisha alipoondoka na kunitelekeza gerezani” akasema Patrick. Savanna akamuangalia na kuuliza
“Why are you avoiding her?
Patrick akamvuta Savanna karibu yake akambusu .
“It’s because I have you now.Sihitaji kuiumiza akili yangu kwa mambo yaliyokwisha pita.Ninachokiangalia hivi sasa ni maisha yangu na mbele nikiwa nawe malaika wangu.Nakupenda sana Savanna zaidi ya ninavyoweza kueleza” akasema Patrick na kumbusu tena Savanna mdomoni
Suala la Patrick kuweka sharti la kuongozana na Savanna lilimuumiza sana moyo Happy na kumfanya akate simu na kuitupa kitandani
“Damn you Patrick..How could you do that to me? Happy akahamaki
“Patrick kasemaje? Akauliza Margreth
“Amesema hawezi kuonana nami hadi aongozane na mpenzi wake Savanna.Margreth I’ve lost him..I’ve lost Patrick.” akasema Happy kwa uchungu
“Usiseme hivyo Happy.Kama kweli bado unampenda kwa dhati,tafuta namna utakayoweza kumtafuta mkakaa na kuliongea jambo hili.” Margreth akajaribu kumpa moyo dada yake
“No way Margreth.Nimeshampoteza Patrick.Tayari yuko katika mahusiano mengine na amekwisha nisahau.Sitaki tena kuingilia mahusiano yake kwani nimekwisha jifunza wakati ule wa Vero.Ni kosa langu na ninastahili kuteseka kwa maisha yangu yote.Sikupaswa kukimbia na kumuacha Patrick peke yake gerezani.Kitendo kile kimemfanya Patrick anichukie sana na hata nilipomtazama machoni niliona wazi kwamba ananichukia mno” akasema Happy
“Sasa utafanya nini Happy?
“Sina cha kufanya tena.Its my mistakes and I cant blame anybody”
“will you be ok?
“No ! I’ll never be ok in my life but I’m going to try living my life without him .Margreth my life will never be the same again.Patrick ndiye alikuwa ni kila kitu kwangu”
Margreth akamtazama dada yake kwa huruma na kusema
“Laiti ningekuwa na njia yoyote ya kuweza kufanya ili kuurejesha tena uhusiano wako na Patrick ningefanya hivyo lakini nasikitika sina namna yoyote ninayoweza kufanya kwa sasa.May be the best thing is to let him go for good” akasema Margreth
“May be that’s the best way for now. Its obvious me and Patric we’re finished.Patrick atabaki kuwa sehemu ya kumbu kumbu yangu .Pamoja na hayo sintaondoka Tanzania hadi hukumu yake itakapotolewa.Nataka niwepo siku hiyo ya hukumu.” Akasema Happy
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Abiria waliokuwa katika ndege ya shirika la ndege la British airways walianza kutoka nje ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.Miongoni mwao alikuwamo Loniki akitokea jijini London Uingereza anakoishi.Linah rafiki yake mkubwa alikuwepo uwanjani kumpokea.
“Karibu tena nyumbani Lonny” akasema Linah huku akikumbatiana na Loniki
“Ahsante sana Linah.Wow ! Unazidi kunawiri” akasema Loniki na wote wakacheka kisha wakaondoka pale uwanjani.
“Mambo yanakwendaje Linah? Akauliza Loniki wakiwa garini
“Mambo ni kama vile nilivyokwambia Lonny.Tunasubiri siku ya hukumu”
“Vizuri sana.Mambo yote umeyaweka sawa?
“Kwa mujibu wa mtu ambaye yuko ndani ya mahakama ambaye ndiye tunamtumia kurekebisha mambo ametuhakikihsia kwamba kila kitu kimewekwa sawa na kwamba Patrick lazima atafungwa.”
“Nafurahi kusikia hivyo.Khumalo ana taarifa kwamba ninakuja na tunakwenda kuonana naye usiku huu?
“Ndiyo.Nilimtaarifu mapema na amenielekeza mahala ambako tutamkuta”
“Ok thats good” akasema Lonny na safari ikaendelea
Ni siku tatu zimebaki kabla ya hukumu ya Patrick kutolewa.Hii ndiyo iliyomsukuma Loniki na kumlazimu aje mara moja ili kufanikisha mipango yake ya kuhakikisha kwamba Patrick anafungwa gerezani baada ya mipango ya kumuua kuonekana kugonga mwamba.
“Lonny ..!! akaita Linah.Loniki akageuka na kumtazama
“Itakuaje iwapo itatokea mahakama ikamuachia huru Patrick?
Loniki akatabasamu kidogo na kusema
“I will kill him myself.Hicho ndicho kitu ambacho kimenirejesha nyumbani.Kama mahakama itamuachia huru Patrick lazima afe.Sintakubali kumuona akiendelea kuishi kwa furaha wakati mdogo wangu ameoza kaburini.Lazima naye afe na ndiyo maana usiku huu nataka nikamtaarifu Khumalo ili alifahamu hilo.Kwa nini umeuliza?
“Never mind its nothing” akajibu Linah na safari ikaendelea kimya kimya hadi walipofika katika klabu moja ya usiku ambako ndiko Khumalo alikokuwa anastarehe.Waliingia pale klabuni na kuelekea moja kwa moja sehemu alipo Khumalo.Alikuwa amezungukwa na mabinti watatu wazuri waliovaa nusu utupu.Mara tu alipowaona Linah na Loniki akawaondoa wale mabinti na kuwakaribisha
“Pole na safari Lonny” akasema Khumalo
‘Nashukuru nimefika salama.Habari za huku?
“Habari za huku nzuri .maisha yanaendelea kama unavyoona” akasema Khumalo na kucheka kidogo halafu akatoa pakiti la sigara akatoa moja na kumrushia Lonny naye akatoa sigara moja akawasha na kuendela kuvuta
“Maisha ni mazuri na matamu.Sina sababu yoyote ya kulalamika” akasema Khumalo
“yah ! Hata mimi naona” akajibu Lonny huku akipuliza moshi mwingi hewani
“Linah alinitaarifu kwamba utafika jioni ya leo na kwamba ulihitaji kuonana nami.Nilistuka kidogo nikajua lazima una suala zito ambalo huwezi kulala bila kuniona”
“Ndiyo Khumalo.Nadhani unafahamu kilichonirejesha nyumbani”
“Nafahamu Loniki na hukuwa na sababu ya kuacha kupumzika na kuja kuniona.”
“Nisingeweza kupata usingizi bila kukuona.Kama unavyofahamu hukumu ni jumanne ijayo.Nataka Kujua mipango inaendaje.Mmejiandaa vipi?
“Kujiandaa kwa nini Lonny? Ninavyofahamu mimi ni kwamba tuliufuta mpango wa kumuua Patrick na tumekuwa tukifanya kila linalowezekana ili Patrick ahukumiwe kifungo kirefu gerezani.Hayo si ndiyo yalikuwa makubaliano yetu?
“Ndiyo Khumalo lakini kuna mambo mawili ambayo yanaweza yakatokea hapa.Patrick anaweza akafungwa au akachiwa huru.Endapo ikitokea akahukumiwa kifungo gerezani basi biashara na wewe itakuwa imekwisha lakini ikitokea kwamba ataachiwa huru na mahakama basi kazi bado itaendelea.Lazima Patrick auawe.Siko tayari kumuona Patrick akiendelea kutamba mtaani wakati alimuua mdogo wangu kwa makusudi kabisa” Loniki aliongea pasi na masihara
“Hilo ni suala ambalo halina tatizo.Kama ataachiwa huru na mahakama basi tutatekeleza huo mpango wako wa kumuua.Lakini naomba utambue kwamba kama ukitaka Patrick auawe itatulazimu tuongee biashara mpya”
Loniki akastuka sana baada ya kauli ile ya Khumalo
“Fedha !!...” akauliza Khumalo kwa mshangao.
“Ndiyo Lonny.Unatakiwa kuongeza fedha kwani itakuwa ni kazi nyingine.”
“You are kidding Khumalo.Nimekuwa nawatumia mamilioni ya fedha kwa ajili ya kazi hii.Mnataka tena niongeze fedha nyingine?
“Loniki pesa ulizokuwa unatuma zote tumezitumia katika kusuka mipango ili Patrick aweze kufungwa.Na kama unavyofahamu hii ni kama bahati nasibu.Mnaweza mkatumia fedha na mkashindwa vile vile kwa hiyo endapo itatokea Patrick ataachiwa huru na ukataka auawe basi itakulazimu kuongeza fedha.Kitu kingine naomba ufahamu kwamba mimi huwa sipendi kuzungumzia mambo ya biashara au kazi katika sehemu za sterehe.Nimewaheshimu sana na ndiyo maana nimekubali kuonana nanyi kati kati ya starehe zangu.Kwa hiyo sitaki tuendele kubishana.Naomba jibu moja kama utaongeza fedha au utatafuta mtu mwingine wa kukufanyia kazi yako? Akasema Khumalo.Loniki akaingiwa na woga kwa namna Khumalo alivyokuwa amebadilika
“Manataka niongeze shilingi ngapi? Akauliza Loniki huku ameukunja uso wake
“millioni arobaini” akajibu Khumalo.Lonny akasimama na kushika kiuno chake akamtazama Khumalo kwa jicho la kali.
“Milioni arobaini?
“Ndiyo.Si fedha nyingi kwa kazi kama hiyo unayoitaka ya kutoa uhai wa mtu.Kama utaona ni nyingi naomba utafute mtu mwingine.”
Loniki akainama akafikiri na kusema
“Nitaangalia namna ya kufanya.Tusubiri kwanza hukumu itolewe” akasema Loniki akiwa na hasira akamshika mkono Linah wakaondoka na kuelekea nyumbani kwa akina Loniki wakaagana na Linah akaanza safari ya kurejea kwake.
“Loniki ni mtu mwenye roho mbaya sana.Bado nia yake ya kumuua Patrick iko pale pale.Hapana siko tayari kumuacha afanikishe mipango yake hiyo.I have to do something to stop her.Ninachotakiwa kukifanya kwa sasa ni kuonana na Sarah.Kwa pamoja tunaweza kumzuia asifanye mpango wowote wa mauaji.Mimi peke yangu siwezi kumshauri aachane na mipango hiyo kwa sababu nimeshiriki kuanzia mwanzo na tayari nimekwisha tumia fedha zake nyingi nikimdanganya kwamba kuna mipango ninaisuka ili Patrick afungwe gerezani.Najua Sarah atataka kuufahamu ukweli wote lakini sina namna nyingine itabidi nimueleze kila kitu kuhusiana na uchafu wa Loniki” Akawaza Linah akapunguza mwendo wa gari na kuchukua simu yake akazitafuta namba za simu za Sarah na kumpigia.
“Hallow Sarah” akasema Linah baada ya Saraha kupokea simu
“Hallow Linah,habari yako? Nimestuka sana baada ya kuiona simu yako mida hii.Si kawaida yako kunipigia simu hasa kwa nyakati kama hizi’ akasema Sarah
“Samahani Sarah kwa kukusumbua.Ni kweli sijawahi kukupigia simu kwa muda kama huu lakini imenilazimu kufanya hivyo leo.Saraha nina shida na wewe ya muhimu sana.Nahitaji kuonana nawe usiku huu kuna jambo la muhimu mno nataka tuongee”
“Linah mbona unanipa wasi wasi? Kuna tatizo gani? akauliza Sarah kwa wasi wasi.
“Usihofu Sarah ni mambo ya kawaida tu ya kuelekezana.Uko wapi sasa hivi?
“Niko nyumbani kwangu.Wewe uko wapi?
“Niko barabarani,nimetoka kumpeleka Loniki nyumbani”
“Loniki !!!...Sarah akashangaa.
“Ndiyo .Ina maana huna taarifa kwamba Loniki anakuja leo?
“Hapana Linah.Sina taarifa yoyote ile kuhusu Lonny.Unajua mimi na dada yangu hatuna maelewano mazuri toka ulipotokea msiba wa Vero kwa hiyo mawasiliano kati yetu si mazuri”
“Yah ! nalifahamu hilo Sarah.Kwa hiyo tunaweza kuonana usiku huu?
“Unaweza ukaja nyumbani kwangu? Unajua siwezi kutoka usiku huu kwani mume wangu amerejea usiku huu kwa hiyo siwezi kuondoka na kumuacha peke yake”
“Nmekuelewa Sarah.Ninakuja hapo hapo nyumbani kwako.” Akajibu Linah na kukata simu
Ilimchukua zaidi ya dakika arobaini kufika nyumbani kwa Sarah.Akafunguliwa geti na kuingia ndani.
“Karibu sana Linah.” Akasema Sarah
“Ahsante sana Sarah.Ni muda mrefu hatujaonana”
“Kweli Linah.karibu sana”
“Nashukuru sana Sarah.Lakini nisingependa kukupotezea muda zaidi .Tunaweza tukaongea hapa nje?
“Hapana Linah.Twende tukaongelee ndani“ Sarah akamuongoza Linah hadi katika chumba cha maongezi
“Linah umenistua sana leo.Kuna tatizo gani? akauliza Sarah akiwa na shauku ya kutaka kufahamu kilichomleta Linah nyumbani kwake usiku ule
“Usiogope sarah.Nimelazimika kuja usiku huu kutokana na unyeti wa jambo lenyewe.Sarah kilichonileta hapa ni kuhusiana na Loniki”
“Loniki kafanya nini tena?! Saraha akashangaa
“Ni hadithi ndefu kidogo lakini nitajaribu kukuelezea kwa ufupi.Ni kwamba kwa muda mrefu sasa Loniki amekuwa katika mikakati ya kuhakikisha analipiza kisasi kwa wale waliosababisha kifo cha Vero,hapa anawalenga Patrick na Happy”
“Yah ! Nilijua toka mwanzo kwamba Lonny alikuwa na mpango wa kulipiza kisasi kwani aliwahi kunitamkia hata mimi kwamba ni lazima atalipiza kisasi kwa watu waliosababisha kifo cha Vero na hilo ndilo jambo ambalo limekuwa likituweka mbali mbali mimi nay eye kwani sioni mantiki ya kulipiza kisasi wakati tayari shauri hili liko katika vyombo vya maamuzi” akasema Sarah
“Kama aliwahi kukutamkia hivyo basi hakuwa anatania.Alimaanisha alichokuwa anakisema.Alinishirikisha mimi pia katika mipango yake kwa kuniomba nimsaidie kutafuta mtu au watu ambao watamsaidia kuifanya kazi hiyo.Nilimsaidia kumpata mtu mmoja ambaye alikuwa tayari kuifanya kazi hiyo.Niliwakutanisha wakaongea na kuelewana namna watakavyotekeleza mpango huo wa kulipa kisasi.Loniki alitaka Patrick na Happy wauawe.Khumalo alilipinga wazo hilo la kuwaua Patrick na Happy kwa haraka kama alivyokuwa anataka Lonny badala yake akashauri kwamba kwa kuwa wakati ule Patrick alikuwa gerezani basi nguvu ielekezwe kwa Happy lengo hapa likiwa ni kumfanyia udhalilishaji mkubwa ambao utapelekea uhusiano wake na Patrick kuvunjika.Khumalo na genge lake walifanikiwa kumteka Happy na kumpeleka mafichoni na huko alifanyiwa udhalilishaji mkubwa sana.Alifanyishwa ngono na vijana wawili huku akirekodiwa na kupigwa picha .Aliamriwa kufanya vile kwa kisingizio kwamba endapo angekataa basi Patrick angeuawa na kwa kuwa Happy anampenda sana Patrick alikubali kufanya vile ili kumuokoa Patrick” akasema Linah na kumtazama Sarah usoni ambaye alionyesha mstuko mkubwa
“My Gosh ! kumbe Lonny ndiye aliyemfanyia Happy kitendo kile?? Akauliza Sarah
“Ndiyo.Happy alifanyiwa udhalilishaji ule huku Loniki akishuhudia.Sarah kwa kweli lile lilikuwa ni tukio baya sana ambalo halitaweza kufutika moyoni mwangu.Ninalijutia sana kosa lile kwani hata mimi nilishiriki” akasema Linah kwa masikitiko halafu akaendelea
“Kilichofuata baada ya hapo ni kama tulivyoona katika magazeti na mitandao.” Linah akanyamaza,akamtazama Sarah na kuendelea
“Katika kipindi hiki ambacho amekuwa Uingereza bado ameendelea na mipango yake ya kuhakikisha kwamba Patrick anafungwa gerezani tena kifungo kirefu.Amekuja leo hii ili kufanikisha kile ambacho amekwisha kianza muda mrefu .Kikubwa zaidi kilichonifanya nikutafute usiku huu ni kwamba amedhamiria kumuua Patrick endapo mahakama itamuachia huru” akasema Linah.Sarah akasimama kwa hasira
“Why are you telling me all this now? Akauliza Sarah
“Because we have to stop her !! akasema Linah naye akasimama
“No Linah ! go away.Wewe na Happy lenu moja.Nyote mmeshiriki katika njama hizi.Linah how could you do that? How could you hurt Parick like that? .akauliza Sarah kwa uchungu
“Sarah please forgive me. Sikuwa nikiufahamu ukweli wa mambo na ndiyo maana nilikubali kushirikiana na Loniki.Kwa sasa baada ya kuufahamu ukweli ninajutia na tafadhali Sarah naomba tushirikiane sote tumuokoe Patrick “
“Go away Linah ! You and Lonny are both killers and tomorrow morning I’m going to report you ” akasema Sarah ambaye alikuwa amepandwa na hasira
“Tafadhali usifanye hivyo Sarah.Tunatakiwa tutafute namna ya kufanya ili kumzuia Lonny asitekeleze mipango yake bila kuwashirikisha polisi.Ukitoa taarifa hizi polisi Loniki anaweza akaenda gerezani.” Akasema Linah
Sarah akainama akafikiri kwa sekunde kadhaa halafu akainua kichwa akamuangalia Linah kwa macho makali.
“Bado siamini kama na wewe umekubali kuungana na Loniki.Nilikuheshimu sana kama dada yangu lakini kwa jambo hili ulilolifanya umenifanya nikutazame upya” akasema Sarah
“C’mon Sarah.Huu si wakati wa kuanzisha malumbano.Tunatakiwa kushirikiana katik…………….” Kabla hajamaliza sentensi yake Sarah akamzuia
“Hakuna njia nyingine zaidi ya kulifikisha suala hili katika vyombo vya dola.Wewe na rafiki yako mtakwenda kujieleza mbele ya vyombo vya sheria.” Akasema Sarah kwa ukali.Linah akamsogelea na kumshika bega
“Nisikilize vizuri Sarah.Najua wewe na Loniki hamna maelewano mazuri lakini yule ni dada yako,ni ndugu yako wa damu.Ukilifikisha suala hili polisi Loniki atakamatwa na anaweza akafungwa gerezani.So tell me are you sure you want to send your sister to jail?
Sarah akainama halafu akainua kichwa akamtazama Linah na kusema
“Unataka tufanye nini?
“Kwa sasa bado najaribu kuangalia namna tutakavyoweza kumzuia Lonny asitekeleze mpango wake.Leo nimeona nikufahamishe kinachoendelea.Nitakupugia simu kesho kukufahamisha mipango yake inavyoendelea na kwa pamoja tutaona namna ya kuweza kumzuia.Sitaki afahamu kama nina mawasiliano nawe kwa hiyo usinipigie simu mimi ndiye nitakayekupigia.Naomba vile vile unihakikishie kitu kimoja”
“kitu gani hicho Linah?
“Naomba haya tuliyoyaongea hapa yabaki kati yetu”
Sarah akamtazama Linah na kusema
“Sintamwambia mtu yeyote lakini naomba utafute haraka mpango wa kumzuia Loniki asiweze kutekeleza mpango huo wa kumuua Patrick” akasema Sarah
“Usihofu Sarah.Nitakufahamisha kila kitu namna tutakavyofanya” akasema Linah halafu akaagana na Sarah akaondoa zake.
“Kazi ya kwanza nimeimaliza.Japokuwa haikuwa rahisi lakini nashukuru Sarah amenielewa.Kinachofuata sasa ni kuongea na Khumalo.” Akawaza Linah akiwa garini akapunguza mwendo wa gari na kuliegesha pembeni ya bara bara akachukua simu yake na kumpigia Khumalo.
“hallo Linah´ akasema Khumalo
“Khumalo bado uko klabuni?
“Ndiyo Linah bado niko hapa klabuni na warembo wangu.Unasemaje?
“Ni kuhusu Lonny”
“Lonny kafanya nini tena? Si tumekwisha malizana naye?
“Nafahamu hilo Khumalo lakini kuna jambo ambalo nataka tulijadii.” Akasema Linah na kuliwasha gari akaliingiza barabarani.
“jambo gani hilo Linah?
“Ni kuhusu huu mpango wake wa kumuua Patrick”
“Kuna tatizo gani katika hilo?
“Are you real gonna do it? Akauliza Linah
“Do what ? khumalo naye akauliza
“Kill Patrick” akasema LInah.Khumalo akacheka kidogo na kusema
“Kwa nini unauliza hivyo Linah wakati unafahamu kabisa kwamba hakuna mpango wowote wa kumuua Patrick? Mimi na wewe tulikwishakubaliana kwamba tutakula fedha za Loniki lakini hatutakeleza mpango wake wowote.Tulichomfanyia Happy kinatosha sana.Siwezi kuendelea kuumiza tena watu wasio na hatia”
“Nimekeuelewa Khumalo lakini nina wazo moja”
“Wazo gani Linah?
“Ninaomba uondoke hapa Dar na usirudi hadi hapo nitakapokutaarifu.”
“Hata hivyo huo ndio ulikuwa mpango wangu.Kesho nilipanga niende Zanzibar kula raha na mpenzi wangu Sakina.Nasubiri milioni arobaini za mwisho toka kwa Lonny”
“Hilo ni jambo zuri sana Khumalo na nina imani endapo ikitokea mahakama ikamuachia huru Patrick Lonny atakutafuta na akikukosa basi hatakuwa na la kufanya tena zaidi ya kuahirisha mpango wake”
“usihofu Linah.Endapo kutakuwa na tatizo lolote na utahitaji msaada wangu utanitafuta na nitawatuma vijana wangu wakusaidie”
“Ahsante sana Khumalo” akasema Linah akaagana na Khumalo na kukata simu
“Sasa mambo yamekaa sawa.Nadhani huu ndio mwisho wa urafiki wangu na Loniki.Ni heri kuishi bila kuwa na rafiki kuliko kuishi na rafiki kama Lonny.” Akawaza Linah huku akielekea nyumbani kwake
* * * *
Siku mpya imeanza.Saa tatu za asubuhi ilimkuta Loniki mbele ya kaburi la Veronika. Kwa muda wa dakika kadhaa alikuwa amesimama akiliangalia kaburi hili huku michirizi ya machozi ikionekana mashavuni
“Vero mdogo wangu nilikuahidi kwamba lazima nikulipizie kisasi kwa wale wote waliokukatili na kusababisha kifo chako.Ule muda wa malipo umewadia.Kesho ni hukumu ya Patrick.Endapo mahakama itamuachia huru basi sintakuwa na njia nyingine zaidi ya kuhakikisha naye anauawa.Ni adhabu mbili tu anazostahili Patrick,kifungo gerezani au kifo.Yule mwanamke wake hali kadhalika naye anastahili adhabu ya kifo.Nitamsaka kokote aliko na kuhakikisha kwamba naye anakufa.Sintakuangusha mdogo wangu” akasema Loniki huku akitoa machozi.Akachukua maua aliyokuja nayo akayaweka juu ya kaburi na kuondoka
* * * *
Saa tatu za usiku,Patrick amejilaza kitandani.Pembeni yake alikuwepo mpenzi wake Savanna.Kutwa nzima ya leo Patrick alikuwa ni mtu mwenye mawazo mengi sana.
“Patrick mpenzi wangu,nimekwisha kuambia kwamba usiwe na mawazo wala wasiwasi.Kesi hii tumepambana nayo vya kutosha na nina uhakika mkubwa wa kushinda.I’ve done my best na ndiyo maana nina uhakika mkubwa wa kushinda kesi hii.Endapo itakuwa vnginevyo basi yatakuwa ni matakwa ya mahakama lakini hata kama ikiwa hivyo basi nitakata rufaa na kupambana tena.Kitu muhimu ni kuwa tayari kwa maamuzi yoyote yatakayotolewa na mahakama.” Akasema Savanna.Patrick ambaye alikuwa amejilalaza akainuka na kukaa halafu akamtazama Savanna kwa makini na kusema
“I’m scared.Sielewi kwa nini nina hofu kubwa.Sijawahi kuwa na hofu ya namna hii maishani mwangu.|” akasema Patrick huku akiupeleka mkono wake sehemu ya kifua unapokaa moyo
“Kitu gani kinakufanya uwe na hofu Patrick? Akauliza Savanna
“Nahofia iwapo nitahukumiwa kifungo maisha yangu ambayo kwa sasa tayari yameanza kwenda vizuri yataharibika na kila kitu kitapotea” Akasema PatrickCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Patrick,tumepambana vya kutosha na mimi kama wakili niliyeisimamia kesi hii ninauhakika mkubwa sana kwamba nimefanya kazi yangu ipasavyo kuishawishi mahakama ikuachie huru.Hoja tulizojenga na kuziwasilisha ni nzito na zina ushahidi wa kutosha.Lakini watoa hukumu nao ni binadamu na inawezekana wakaamua tofauti na tunavyotegemea sisi lakini hata kama ikitokea watakuhukumu kifungo tutakata rufaa.” Akasema Savanna na kumfanya Patrick atabasamu na kumvuta Savanna karibu akambusu
“Kila mara namshukuru sana Mungu kwa kunipa mwanamke ambaye ni jasiri na ambaye yuko tayari kufanya kila linalowezekana kwa ajili yangu.Endapo mahakama itaniachia huru basi ndani ya kipindi kifupi sana lazima tufunge ndoa.”
Uso wa Savanna ukajenga tabasamu pana
“Patrick mpenzi wangu ,Mungu aliyetukutanisha anafahamu ni namna gani ninakupenda.Ni Mungu huyu huyu ambaye atatusaidia ili tuweze kuitimiza ndoto yetu hii kubwa.Siku zote tunatakiwa tumuamini na kumtegemea yeye pekee.Kwa imani niliyonayo kwa Mungu huyu mmoja muumba wa mbingu na nchi nina imani tutashinda kesi na tutafanikiwa kuwa pamoja milele “ akasema Savanna huku amemkumbatia Patrick kwa nguvu
“Savanna endapo nitapewa adhabu ya kifungo gerezani tafadhali naomba usinitelekeze kama walivyofanya wengine.Naomba unisubiri hadi hadi hapo nitakapomaliza kifungo changu ili tuweze kuitimiza ndoto yetu ya kuwa pamoja.Will you wait for me darling?
“Patrick kwanza naomba ufahamu kwamba hutakwenda gerezani.Hata kama ikitokea kwamba utahukumiwa kifungo basi itapambana hadi nihakikishe ninakutoa.Kuhusu kukusubiri usitie shaka kuhusu hilo.Niko tayari hata kutumia muda wangu wote uliobaki hapa duniani kukusubiri wewe tu kwa hiyo usiwe na hofu hata kidogo na hilo.” Akasema Savanna kwa sauti laini
Waliongea mambo mengi sana usiku huo .Savanna alijitahidi kwa kila alivyoweza kumpa moyo Patrick kuhusu hukumu yake siku itakayofuata.Huu ulikuwa ni usiku mgumu sana kwa Patrick.Alitumia muda mwingi kusali na kumuomba Mungu amuepushe na kifungo
Familia nzima ya mzee Kibaho ilikuwa imekusanyika kwa ajili ya kusali sala ya jioni kama ilivyo kawaida yao kukutana na kusali pamoja kabla ya kwenda kulala.Siku hii ya leo kulikuwa na maombi maalum ya kumuombea Patrick ambaye hukumu yake ilitegemewa kutolewa siku inayofuata.Pamoja na maombi haya ya familia lakini Happy yeye alikuwa na maombi yake binafsi ya kufunga na kusali kwa muda wa siku tatu akimuomba Mungu amsaidie Patrick achiwe huru.
Baada ya kumaliza maombi yale ya jioni Happy na mdogo wake Margreth wakaenda chumbani kwao.
“Margreth I’m so nervous.Nahisi kama mwili wangu unatetemeka kila nikifkiria whats going to happen tomorrow.” Akasema Happy Margreth aliyekuwa anapanga nguo katika kabati lake akaacha kazi ile na kumfuata Happy
“Do you believe in God? Akauliza Margreth
“Ofcourse I do “ akajibu Happy
“Vizuri.Kama unamuamini Mungu muache atende kazi yake.Hana sababu ya kuogopa hata kidogo.Mtumaini yeye siku zote” akasema Margreth
“Margreth I believe in God lakini nashidwa kujizuia kuwa na wasiwasi.Sifahamu kitakachotokea kesho.Ouh Gosh! Akasema Happy
“Ilitakiwa mimi ndiye niwe nimesimama kizimbani siku ya kesho nikihukumiwa na si Patrick.Lakini Patrick ndiye anayehukumiwa badala yangu.Sijawahi kuona mtu mwenye upendo mkubwa na wa ajabu kama huyu.I’m so sorry I’ve lost him and I don’t know what to do to get him back.” Akasema Happy
“Happy tafadhali usiwaze sana kuhusu mambo hayo.Tusubiri kwanza hadi siku ya kesho tuone nini kitatokea na baada ya hapo tutajua nini cha kufanya” akasema Margreth
“Margret sina ujanja tena.Tayari nimekwisha mpoteza Patrick.” Akasema Happy na mara wote wakastushwa na mlio wa simu ya Margreth.Akaichukua na kutazama mpigani halafu akavuta pumzi ndefu
“Its mike” akasema
“Tell him I’m not around” akasema Happy
“Happy siku ya leo hii ni mara ya tatu anapiga simu na hutaki kuongea naye.Happy I dont want to lie anymore.Please talk to him” akasema Margreth
“Ouh My God I don’t know what to tell him” akasema Happy
“Tell him anything.Ana hamu sana ya kuongea nawe.Mike ni mchumba wako.Ukikataa kuongea naye unamuumiza sana na utamfanya ahisi kwamba huku mambo si shwari.Tafadhali ongea naye.” Akasema Margreth.Happy akachukua simu ile ambao bado iliendelea kuita akabonyeza kitufe cha kupokelea simu
“Hallow Mike” akasema Happy.Mara moja Mike akaitambua sauti ya Happy
“Hallo malaika wangu .” akasema Mike kwa furaha
“Unaendeleaje Mike? Akasema Happy
“Ninaendelea vizuri Happy.Nimefurahi sana kuisikia sauti yako.Unaendeleaje? akauliza Mike
“Naendelea vizuri Mike.”
“Nafurahi kusikia hivyo.I miss you a lot my angel” akasema Mike
“I miss you too” akajibu Hapy
”How’s Patrick? Akauliza Mike na kumfanya Happy asite kujibu
“Happy how’s Patrick? Uliniambia kwamba hukumu yake ni kesho?
“Ndiyo Mike hukumu yake ni kesho” akajibu Happy
“Utahudhuria mahakamani? Akauliza Mike
“Ndiyo Mike nitahudhuria kwani ndicho kitu pekee ambacho kimeniweka hapa hadi muda huu kwa hiyo siwezi kukosa mahakamani.” Akajibu Happy
“Are you guys talk often? Akauliza Mike
“Mike mbona una wasi wasi hivyo? Akauliza Happy
“Lazima niwe na wasi wasi mpenzi wangu kwa sababu nafahamu kwamba Patrick ana sehemu kubwa sana moyoni mwako kwa hiyo nashindwa kujizuia kuwa na wivu kila nikifikiria kwamba uko karibu naye na mnaweza mkaonana” akasema Mike
“Usihofu Mike.Mimi na Patrick kilichobaki ni historia tu kati yetu na hakuna chochote kinachoendelea.Tayari kila mmoja ameendelea na maisha yake.Tayari naye ana mchumba na wanategemea kufunga ndoa muda wowote.Kwa hiyo huna sababu ya kuhofu”
“Hizo ni habari njema sana.Kwa hiyo utarejea mara tu baada ya hukumu kutolewa?
“Ndiyo Mike.Ni hicho tu kilichokuwa kinaniweka hapa na baada ya siku ya kesho I’ll say goodbye to Tanzania and leave this blessed country for good.Mike kuna jambo nataka kukueleza” akajibu Happy
“Jambo gani Happy?
“Unakumbuka uliwahi kuniomba nifunge nawe ndoa na nikakwambia kwamba unisubiri hadi hapo nitakapokuwa tayari?
“Ndiyo Happy nakumbuka sana na sijawahi kukuuliza tena kuhusu suala lile kwa sababu nilitaka utafakari na kama ukiwa tayari basi unijibu”
“Mike naomba nikufahamishe kwamba tayari nimekwisha fanya maamuzi yangu na jibu langu ni ndiyo.Nitafunga ndoa nawe Mike” akasema Happy na Mike akaruka kwa furaha asiyaamini masikio yake.
“Ouh Happy kwa muda mrefu sana nimekuwa nikisubiri unitamkie maneno kama haya.Nimefurahi sana mpenzi wangu.Nitaanza maandalizi mara moja na kuwataarifu ndugu na jamaa kuhusu jambo hili jema.”
“Hapana Mike usimwambie mtu yeyote kwanza.Tutawaambia tutakapokuwa pamoja nitakaporudi”
“sawa malaika wangu.Chochote utakacho niamuru nitatii.Ninakupenda sana Happy.Ahsante sana”
“Hata mimi nakupenda sana Mike na ndiyo maana nahitaji kuwa nawe katika maisha yangu yote yaliyobaki hapa duniani” akasema Happy.Wakaagana na kukata simu
“Happy !! akaita Margreth
“Una hakika na hicho ulichokisema?
“Kitu gani Margreth?
“kwamba unataka kuolewa na Mike? Happy akainama na kusema
I don’t know Margreth but I think that’s the best way to do for now.”
“Happy kwa nini umemwambia Mike jambo ambalo huna uhakika nalo?
“Margreth I have to do this.I’ll learn to love Mike.” Akasema Happy.Margreth akainamisha kichwa akaonekana kusikitika
“Unasikitika nini Margreth?
“Ninasikitika kwa sababu you cant swallow back what you’ve promised Mike.Kwa maana hiyo basi unatakiwa usimame katika maneno yako.Lazima uolewe na Mike.Jitahidi usimuumize kama wakati ule.”
Happy akazama katika mawazo mengi na baada ya muda akasema
“Margrteh I’ve made my decision.I’ll marry Mike.Hakuna uwezekano tena wa kuwa na Patrick.I’ve lost him”
**********************
Ni dakika ya pili sasa toka alipoweka shingoni tai yake akitaka kuifunga.Alikuwa amesimama mbele ya kioo kikubwa cha kujtazamia .Sauti ndogo ya muziki ilikuwa inasikika.Patrick alikuwa anabubujikwa na machozi kutokana wimbo uliokuwa uitwao see you again wimbo ulioimbwa na Carrie underwood
I will see you again,woah
This is not where it ends
I will carry you with me oh
Till I see you again
Patrick akaimba kibwagizo cha wimbo ule na mara Savanna akaingia mle chumbani na kuuzima mziki ule
“Patrick mbona unajipa wakati mgumu namna hiyo? Kwa nini ujiumize moyo wako? Just relax.Everything will be fine.Stop torturing yourself.” Akasema Savanna huku akimfuta machozi
“Savanna malaika wangu I’m so scared .Nashindwa kujiuia kuwaza nini kitatokea endapo nitahukumiwa kifungo.Hii ni siku ngumu sana katika maisha yangu”
“Patrick usiwaze sana kuhusu nini kitatokea.Tujiandae kwa maamuzi yoyote yale yatakayotolewa na mahakama.I’ve done my level best as a lawyer lakini mahakama ndiyo yenye kutoa maamuzi.Endapo watatoa adhabu ya kifungo gerezani,tutakata rufaa kama nilivyokuahidi.I’m right here beside you ,you are not alone” akasema Savanna na kumbusu Patrick halafu akamfungia tai
“Now you look perfect.you are so handsome Patrick.I love you” akasema Savanna na kumbusu tena Patrick shavuni
Wakati Savanna akijiandaa Patrick alitoka mle chumbani na kwenda nje ya nyumba
“Ni katika nyumba hii furaha yangu ya maisha iliporejea tena.Endapo nitafungwa gerezani nitaikosa nyumba hii iliyojaa furaha amani na upendo.” Akawaza Patrick halafu akarejea ndani.Savanna alimaliza kujiandaa akajumuika na mpenzi wake mezani wakapata stafstahi
“Are you ready to go Patrick? Akauliza Savanna
“I’m ready” akajibu Patrick na kisha wakatoka wakaingia garini na kuondoka kuelekea mahakamani
* * * *
Saa tatu za asubuhi ilimkuta Sarah tayari amekwisha wasili mahakamani.Aliwahi sana kufika pale ili apate nafasi ya kuonana na Linah ambaye alimwahidi kumpigia simu na kumfahamisha kuhusiana na mpango wa namna watakavyoweza kumdhibiti Loniki asiweze kuutekeleza mpango wake wa kumdhuru Patrick endapo mahakama itamuachia huru,lakini toka walipoonana usiku ule Linah hakumpigia tena simu jambo lililoanza kumpa wasi wasi.Kilichompa wasiwasi zaidi simu ya Linah haikuwa ikipatikana na hakupafahamu mahala alipokuwa amehamia.Mtu pekee ambaye angeweza kumpa jibu la wapi alipo Linah ni Loniki lakini aliogopa kumuuliza chochote kutokana na mahusiano yao kutokuwa mazuri.Pale mahakamani alijaribu kuangaza huku na huko lakini hakumuona mtu yeyote wa familia yake.Akachukua simu na kumpigia mama yake.
“mama shikamoo’
“Marahaba Sarah.Hujambo?
“Sijambo mama”
“Uko wapi Sarah? Si unajua leo ni siku ya hukumu?
“Nafahamu mama.Tayari niko hapa mahakamani.”
“Mbona umewahi namna hiyo?
“Ndiyo mama nimeamua tu kuwahi.Unakuja mahakamani?
“Ndiyo ninakuja niko njiani”
“Uko na Loniki?
“Hapana.Loniki amekuja kuchukuliwa na rafiki yake asubuhi ya leo.Aliniaga kwamba kuna sehemu wanakwenda lakini hatachelewa kufika mahakamani”
“rafiki yake yupi unayemzungumzia? Akauliza Sarah
“Kwani Loniki ana rafiki mwingine zaidi ya Linah? Huyo ndiye aliyefika asubuhi na wakaondoka wote”
“Sawa mama.Mimi utanikuta hapa” akasema Sarah na kukata simu
“Kwa nini Linah hajawasiliana nami kama alivyoniahidi na simu yake haipatikani tena? Amekwenda wapi na Loniki asubuhi hii? Kuna kitu gani kinachoendelea? Inawezekana Linah akawa ameshindwa kupata njia ya kumdhibiti Loniki? Edapo sintakuwa nimeonana naye hadi hukumu itakapotolewa na mahakama ikamuachia huru Patrick basi sintakuwa na njia nyingine zaidi ya kulifikisha suala hili katika vyombo vya usalama.” Akawaza Sarah huku akijaribu kupiga tena namba za simu za Linah bila mafanikio
* * * *
“C’mon Khumalo what happened to you? “ akasema Loniki akiwa na simu mkononi akijaribu kupiga tena na tena namba za khumalo lakini kila alipopiga jibu lilikuwa moja tu
“Namba ya simu ya mteja unayempigia haipatikani kwa sasa.tafadhali jaribu tena baadae.”
“Damn it !!! “ akasema Loniki kwa hasira na kugonganisha mikono yake.Linah aliyekuwa katika usukani akamtazama bila kusema chochote akaendelea na kukanyaga mafuta
Loniki na Linah walikuwa wanaelekea nyumbani kwa Khumalo.Asubuhi na mapema Linah alimfuata Loniki nyumbani kwao na kumfahamisha kwamba Khumalo hakuwa anapatikana simuni,taarifa ambayo ilimstua sana Loniki na akaamuru wamfuate Khumalo nyumbani.Katika siku hii Loniki alimuhitaji sana Khumalo ili aweze kutekeleza mpango waliokuwa wameongea wa kumuua Patrick endapo mahakama ingemuachia huru.Linah alifuata kila alichokisema Loniki lakini moyoni alikuwa akifahamu wazi kwamba Khumalo hakuwepo na walipanga Khumalo atoweke baada ya kupokea fedha toka kwa Loniki.
“Huyu Khumalo mbona anaanza kunipa wasi wasi? Kwa nini hapatikani simuni wakati anajua fika kwamba leo ni siku ambayo Patrick anahukumiwa kwa hiyo lolote linaweza kutokea? Loniki akajiuliza maswali mfululizo.Linah ambaye siku hii ya leo alionekana kuwa mkimya na mwenye wasi wasi mwingi hakujibu chochote
“Say something Linah” akafoka Loniki
“Niseme nini Lonny? Khumalo hapatikani simuni .Tunachotakiwa ni kufika nyumbani kwake na kuangalia kama ana tatizo.Pengine labda simu yake ikawa na matatizo” akasema Linah
“What a stupid woman.Sihitaji tena urafiki na mjinga kama huyu.After today its over.Hanisaidii kitu chochote katika maisha yangu zaidi ya kuniingiza katika mambo ambayo yanaweza kuniletea matatizo.Amenishirikisha katika mipango yake ya visasi na kunisababishia dhambi kubwa .Kitendo cha kumdhalilisha Happy namna ile kinaniumiza sana hadi leo hii.Sitaki tena urafiki na huyu mjinga” akawaza Linah wakati wamekaribia kufika nyumbani kwa Khumalo
Walifika katika jumba la Khumalo.Linah akapiga honi ili wafunguliwe geti.Loniki baada ya kuona mlinzi anachelewa kutoka akafungua mlango wa gari na kushuka garini akaenda kubonyeza kengele ya getini.Baada ya muda kidogo mlango mdogo wa geti ukafunguliwa
“Habari yako? Akasema jamaa mnene aliyefungua geti
“Habari nzuri” akajibu Loniki
“Nikusaidie nini? Akauliza yule jamaa
“Nina shida na Khumalo.Ninaitwa Loniki na mwenzangu pale garini anaitwa Linah.Sisi ni marafiki zake na tuna biashara naye ya muhimu sana”
Una biashara gani na Khumalo?
“Kuna kazi nilikuwa nimeelewana naye aifanye ambayo anatakiwa aifanye leo lakini kitu cha kushangaza ni kwamba hapatikani katika simu hivyo tumeamua kuja hapa nyumbani kwake kuonana naye” akasema Loniki
“Samahani dada yangu.Khumalo hayupo amesafiri” akasema yule jamaa na kumfanya Loniki ahamaki
“Acha utani ndugu yangu.Khumalo amesafiri lini na bila kututaarifu?
“Khumalo hayupo dada amepatwa na safari ya ghafla na kuondoka usiku wa kuamkia leo.” Akasema yule kijana .
“Ouh gosh ! amesema atarudi lini? Akauliza Loniki ambaye alionekana kustushwa sana na jibu lile
“hakusema atarudi lini lakini mara nyingi huwa akisafiri humchukua hata zaidi ya miezi sita kurejea.” Akasema yule kijana na kuzidi kummaliza nguvu Loniki
“Hakuna namna ambayo tunaweza kumpata au kuwasiliana naye ili kama yeye hauypo basi vijana wake waifanye kazi tuliyokubaliana kwani tayari nimekwisha mlipa fedha zote alizozihitaji” akasema Loniki
“Khumalo akisafiri kumpata huwa ni kazi ngumu sana kwa sababu huwa hatulii katika sehemu moja”
Jibu lile likamnyong’onyeza kabisa Loniki akaegemea ukuta.Baada ya kutafakari akaagana na Yule kijana na kurejea tena garini
“ Damn it !!...akafoka Loniki baada ya kurejea garini.Alikuwa amekasirika sana na kijasho kilianza kumchuruzikaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“amesemaje yule kijana? Khumalo yuko wapi? Akauliza Linah ambaye alikuwa amebaki garini
“Khumalo amesafiri usiku wa kuamkia leo na haijulikani kama atarejea hivi karibuni” akasema Loniki
“ How could he do that? Kwa nini aondoke kimya kimya bila kututaarifu wakati alijua kabisa tuna mkataba naye na tayari fedha zote alizozihitaji nimeshampatia?Kwa nini ametufanyia hivi?.” Akalalamika Loniki
“kwa hiyo tutafanya nini? Akauliza Linah
“Sina hakika kama ni kweli Khumalo amesafiri .Najua atakuwa amejificha mle ndani.” Akasema Loniki
“Hapana Loniki.Kama umeambiwa kwamba Khumalo hayupo ni kweli atakuwa amesafiri.”
Loniki akageuka akamtazama Linah kwa muda kisha akasema
“How could you believe him so easily?
“Kwa sababu ninamfahamu vizuri Khumalo.Ni mtu ambaye huwa muwazi siku zote na kama imetokea amesafiri ghafla namna hii basi lazima kuna sababu ya msingi sana iliyomuondoa hapa nchini usiku .Inawezekana labda alikuwa anakimbia vyombo vya usalama kutokana na shughulio anazozifanya” Akasema Linah
“you failed me Linah.Wewe ndiye uliyeniambia nimuamini Khumalo.Unaona sasa kitu ambacho ametufanyia? Nini kitafuata iwapo mahakama itamuachia Patrick huru? Linah siwezi kukubali kumuona Patrick akiachiwa huru na akendelea kula raha na Malaya wake huku mdogo wangu akiwa ameoza kaburini.Endesha gari tuondoke” akasema Loniki kwa ukali
“Tunaelekea wapi?
“Turudi nyumbani”
“Lonny huoni kama tutachelewa mahakamani? Nyumbani tunaenda kufanya nini? Akauliza Linah
“Nimesema endesha gari tunarudi nyumbani? Akafoka Lonny.Linah akageuza gari na safari ya kurejea nyumbani ikaanza.
Waliwasili nyumbani kwa akina Loniki na kwa haraka akashuka garini akaelekea moja kwa moja chumbani kwa mama yake.Kabati kubwa la nguo halikuwa limefungwa na funguo,akalifungua na kifungua droo ndogo ndani ya lile kabati halafu akatabasamu
“Nilijua tu lazima itakuwepo,Baba alikuwa na bastora mbili kabla hajafariki.Moja ni ile aliyoitumia Vero kutaka kumtoa uhai yule shetani na nyingine ni hii hapa.Kama Vero alimkosa siku ile,mimi sintamkosa leo.Nimehitimu mafunzo ya kulenga shabaha kwa hiyo nina uhakika mkubwa wa kuufumua ubongo wake leo endapo mahakama itamuachia huru” akawaza Lonny halafu akaibusu bastora ile
“Don’t fail me my baby.Do as I tell you to do” akasema Lonny kisha akaiweka bastora ile katika mkoba wake akachukua funguo za gari lililokuwa la Vero akatoka
“Shuka katika gari hilo .Tutatumia hili hapa” Loniki akamuamuru Linah ambaye alishuka na kuingia katika gari lile alilolitaka Lonny
“Drive” akasema Lonny
“Tunakwenda wapi Lonny? Mahakamani? Akauliza Linah
“Stop asking questions Linah.Endesha gari.Ndiyo tunakwenda mahakamani” akasema Lonny kwa ukali.
“Loniki tafadhali naomba usiwe na hasira na mimi.Nilimuamini Khumalo kwa kuwa ni mtu niliyewahi kufanya naye kazi mara kadhaa” akasema Linah Loniki akamtazama kwa jicho kali na kusema
“Save your breath Linah.Nitamalizana nawe baadae.Kwa sasa niache nifikirie kuhusu plan B” akasema Lonny
“Plan B? akauliza Linah
“Yes Plan B.Wewe na shetani mwenzio Khumalo mmenifanyia jambo baya sana kwa hiyo nitawaonyesha kwamba hata mimi nina uwezo wa kufanya hizi kazi.” Akasema Loniki
“Loniki tafadhali naomba tuheshimiane na usirudie tena kuniita mimi shetani.Kama mimi nitakuwa shetani wewe utakuwa nani? Akasema Linah kwa ukali huku akitaka kulisimamisha gari.
“Shut up you bastard.Usinipandishe hasira zangu muda huu.Kuanzia sasa utafanya kile nitakachokuamuru” akafoka Loniki huku akimuelekezea Linah bastora.Linah akatetemeka
“Ouh gosh ! Kumbe ana bastora..mshenzi huyu amedhamiria kweli kumuua Patrick endapo ataachiwa huru na mahakama.Lazima nifanye jambo kumzuia asifanye anavyotaka kufanya.Nitatafuta namna ya kuwasiliana na Sarah.Najua hadi hivi sasa atakuwa anajiuliza sana ni kwa nini sijampigia simu kumtaarifu chochote kama nilivyokuwa nimemuahidi.Kutwa nzima ya jana nililazimika kutoitumia ile laini yangu ya kawaida kwa sababu nilikuwa na huyu shetani muda wote kwa hiyo niliogopa asije gundua kwamba nilikuwa nawasiliana na Sarah.”akawaza Linah
Kadiri muda ulivyokuwa unasonga ndivyo idadi ya watu ilivyokuwa inaongezeka mahakamani.Mpaka kufikia saa nne za asubuhi idadi ya watu ilikuwa kubwa.Sarah ambaye aliwahi sana kufika mahakamani macho yake hayakubanduka katika geti la kungilia akijaribu kuangaza kama atamuona Loniki na Linah
Akiwa bado ameyaelekeza macho yake katika geti la kuingilia mahakamani,aliziona gari tatu zikiingia.Alizifuatilia kwa macho hadi katika maegesho.Toka katika gari zile ikashuka familia ya Patrick ikiongozwa na mama yake,pamoja na ndugu wengine.Bila kupoteza muda Sarah apiga hatua na kuwafuata mahala walipo akawasabahi.Wakati akiongea na familia ya Patrick gari la mama yake likawasili pale mahakamni.Baada ya kuegeshwa mama yake Sarah akashuka garini akiongozana na akina mama wanne.Mahali alikoegesha gari si mbali sana na pale alipokuwa amesimama Sarah akiongea na familia ya Patrick.Mama yake Sarah akamuona mwanae na kumtazama kwa jicho kali bila kusema chochote .Tayari alikuwa katika uadui mkubwa na familia ya Patrick.Sarah akawaaga familia ya Patrick na kwenda kuungana na mama yake.
“Sarah unachokifanya si kitu kizuri hata kidogo” akasema mama yake kwa ukali
“Kwa nini mama?
“Kwa nini unadiriki kuungana na wale watu ambao unafahamu fika kwamba ni maadui zetu? Mtoto wao amemuua mdogo wako.Hupaswi kuandamana nao hata kidogo na hii ndiyo sababu inayokufanya wewe na dada yako Loniki msielewane”
“Mama mimi sipendezwi hata kidogo na tabia yenu hii ya kuichukia familia ya Patrick.Mambo yamekwisha tokea na tusubiri hukumu ya Mahakama muda mfupi ujao.Binafsi sina chuki yoyote na familia ile na ndiyo maana nashirikiana nao kwa moyo mkunjufu.” Akasema Sarah na mama yake akamtazama kwa jicho kali na kusonya halafu akapiga hatua kuondoa zake na wale akina mama aliokuwa ameambatana nao na kumuacha Sarah akiwa amesimama peke yake
Gari moja jeusi likaingia pale mahakamani na kuelekea sehemu ya maegesho.Ndani ya gari lile alikuwemo Happy Kibaho na familia yake.Wote wakaendelea kubaki ndani ya gari wakisubiri muda wa kusomwa hukumu ufike .Happy aliogopa kushuka garini kuwakwepa waandishi wa habari waliokuwa wakimtafuta usiku na mchana ili kumuhoji bila mafanikio.
Happy na familia yake wakiwa bado ndani ya gari,katika geti la kuingilia pale mahakamani likaingia gari moja la kifahari aina ya Mercedece benz s 320 CDI 4 MATIC ya rangi nyeusi na kwenda kuegesha si mbali sana na mahala walipokuwa wameegesha gari akina Happy.Baada ya sekunde kadhaa. Milango ya gari lile la kifahari sana ikafunguliwa akashuka Patrick na Savanna.Patrick alikuwa mevaa suti nyeusi iliyomkaa vyema na miwani myeusi kuyaziba macho yake.Savanna naye halikadhalika alivaa suti ya rangi nyeusi.Mara tu waliposhuka waandishi wa habari waliwazingira na kuanza kuwapiga picha.Hawakuwajali wakashikana mikono na kuelekea moja kwa moja ndani ya jengo la mahakama.
Akiwa ndani ya gari na familia yake Happy akawashuhudia Patrick na Savanna wakiingia mahakamani.Ni wazi alikuwa anaumia sana moyoni.Familia yote ilikuwa kimya kabisa.Hawakutaka kusema kwa kuogopa Happy asije umia zaidi
“Mimi ndiye niliyepaswa kumsindikiza Patrick mahakamani leo.Nasikitika sana kumpoteza Patrick” akawaza Happy
Nusu saa baadae watu wakaanza kuingia mahakamani kwani hukumu ilitarajiwa kuanza kusomwa muda wowote.Happy na familia yake wakashuka garini na kuungana na watu wengine waliokuwa wanaingia ndani ya mahakama.Wapiga picha bila kuchelewa wakaanza kumpiga picha Happy wakati akitembea kuingia ndani ya mahakama akiwa na familia yake.Ukumbi wa mahakama ulifurika watu
Saa tano na dakika kumi jopo la majaji watatu wa mahakama kuu wakiongozwa na Jaji Gregory Mkaga wakaingia mahakamani.Watu wote walikuwa kimya kabisa wakisilikiza.
Saa sita na dakika ishirini na saba Loniki na Linah wakawasili mahakamani.Walikuwa wamechelewa sana na tayari mahakama ilikuwa inaendelea.Loniki akaitoa bastora yake katika mkoba akaitazama kisha akairudisha mkobani.
“Twende tuingie mahakamani.” Akaamuru Loniki ,wakashuka na kuingia mahakamani huku mkoba uliokuwa na bastora ukibaki ndani ya gari
Hatimaye muda wa kusomwa hukumu ukawadia.Hiki kilikuwa ni kipindi kigumu sana kwa watu wote.Patrick alikuwa anatetemeka mwili huku akiomba kimoyo moyo Mungu amsaidie na amuepushe na kifungo.Happy alikuwa ameweka mkono wake wa kulia katika sehemu ya kifua mahala ulipo moyo.Alihisi mwili mzima kumtetemeka.Kila mtu pale mahakamani kiroho kilimdunda
“God please help Patrick and help me too.I don’t know what’s going to happen if Patrick will go to jail.” Happy akaomba kimya kimya.
Loniki ambaye alikuwa amesimama nyuma kabisa ya chumba cha mahakama kwa kukosa nafasi ya kukaa mikono yake ilikuwa inamtoka jasho
“Hiki ndicho kipindi cha kubaini nini kitatokea.I’m not scared to kill him if the court will set him free.I swear I’ll kill him today” akawaza Loniki huku moyo wake ukimwenda mbio sana.Linah ambaye naye aliokuwa amesimama pembeni ya Loniki miguu yake ilikuwa inamtetemeka.Alikua akitafuta njia ambayo angeitumia ili kumdhibiti Loniki asiweze kutimiza lengo lake la kumuua Patrick endapo angeachiwa huru na mahakama.Alifikiria kuwataarifu polisi kuhusu suala lile lakini akaogopa kwamba huenda hata naye lingemletea matatizo kwani alihusika kwa kiasi kikubwa katika mipango yote ya loniki
“Njia pekee hapa ni kuwasiliana na Sarah lakini nitawasiliana naye vipi wakati Loniki tayari amenibana? I Must find a way,ngoja kwanza hukumu itolewe” akawaza Linah
Savanna aliyekuwa amekaa mbele kabisa alikuwa kimya.Japokuwa anajiamini kwa kazi kubwa aliyoifanya akishirikiana na jopo la mawakili kutoka kampuni yake ya uwakili,alishindwa kujizuia kuogopa kwani hakujua nini kinakwenda kutokea muda mfupi unaokuja.
“Ee Mungu ,nakuachia wewe kila kitu.Nimeifanya kazi yangu ya kumtetea Parick kwa uwezo wangu wote ulionijalia lakini wewe ndiye mwamuzi wa yote.Kama ni kwa mapenzi yako Patrick aende gerezani sina tatizo lakini kama ikikupendeza naomba Patrick aachiwe huru.Hakutenda kosa hili na zaidi ya yote ninamuhitaji sana katika maisha yangu” Savanna naye alikuwa amefunga mikono yake kifuani akifanya maombi ya kimya kimya akisubiri hukumu..Huu ulikuwa ni wakati wa kila mtu kuomba kile alichokuwa anakitaka kitokee
Kwa mujibu wa kifungu cha 326(1) b cha sheria ya mwenendo wa mashtaka sura ya 20 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 mahakama kuu kanda ya Dar es salaam ilimuachia huru Patrick baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani na upande wa utetezi kwamba kifo cha Vero kilitokea kwa bahati mbaya kati kati ya purukushani za kunyang’anyana silaha ambayo Vero alitaka kuitumia katika kufanya mauaji.
“Yametimia.Twende tuondoke” Loniki akamuamuru Linah wakatoka nje na moja kwa moja wakaelekea katika gari lao.Baada ya kuingia garini Loniki akainama na kulia sana
“He killed my sister..!!! why they let him go??? Why???!!!!!!!...Loniki alilia kwa uchungu
“Vero nitakulipizia kisasi.Siwezi kukubali mtu aliyekukatili uhai wako aendelee kuwa hai.” Akasema Loniki kwa uchungu
“Pamoja na kutoa mamilioni ya fedha ili huyu shetani afungwe gerezani lakini bado imeshindikana.You failed me Linah..You failed me.I knew this would happen…!! Thank you” akasema Loniki.
“Lonny mimi si wa kulaumiwa hata kidogo haya ni maamuzi ya mahakama.Kazi yangu ilikuwa ni kusuka mipango ya kumfunga Patrick lakini kama majaji wameamua hivi na tayari wamekwisha kula hela yetu basi kuna kila ulazima wa kuwauliza kulikoni mambo yawe hivi? Akasema Linah
“Shut up Linah..! Hakuna haja ya kuwatafuta tena hao majaji.Tayari nimekwisha poteza mamilioni ya fedha ambazo hazitaweza kurudi na hakuna chochote kilichofanyika.” Akasema Loniki kwa ukali
Watu sasa walianza kutoka mahakamani.Mama yake Loniki naye alitoka mahakamani akiongozana na akina mama wanne waliokuwa wamemshikilia.Alikuwa analia,aliumizwa sana na maamuzi yale ya mahakama.Lonny akamtazama mama yake kwa uchungu akainama na kufuta machozi
“Nilijua toka mwanzo jambo kama hili linaweza kutokea na ndiyo maana sikutaka kusubiri hukumu ya mahakama.Hakuna hukumu ya haki itakayotendeka na ndiyo maana nikaamua kutafuta hukumu yangu mwenyewe lakini wewe Linah na Khumalo mkanizuia nisifanye nilivyokuwa natka kufanya..Umeona sasa kilichotokea? Muuaji wa mdogo wangu ameachiwa huru..” akasema Loniki kwa uchungu.
Watu sasa walikuwa wengi nje ya mahakama.Wengi hususani ndugu jamaa na rafiki wa Patrick walikuwa na furaha na walionekana wakipongezana.Waliifurahia hukumu ile na kuipongeza mahakama kwa kutenda haki.Happy naye alitoka mahakani akiongozana na familia yake. Uso wake ulikuwa umepambwa na tabasamu pana sana licha ya machozi kuendelea kumtiririka.Alikuwa analia kwa furaha ya Patrick kuachiwa huru.Ili kumuepusha Happy na maswali ya waandishi wa habari wakaelekea moja kwa moja katika gari lao lakini Happy akagoma kuingia
“Happy mambo yamekwisha hapa mahakamani.Ingia garini tuondoke” akasema mzee Kibaho
“No dady.!I have to talk to Patrick before I leave.May be its going to be my last talk to him” akasema Happy
Wakiwa ndani ya gari wakiangalia kilichokuwa kinaendela,Loniki na LInah wakamshuhudia Sarah akimpa mkono mama yake Patrick.Kiendo kile kikazidi kumuumiza Loniki
“ After Patrick,that bastard will be next.I must teach her a lesson.Simtambui tena Saraha kama ndugu yangu.I don’t know her anymore” akasema Loniki kwa hasira.Vicheko na kupongezana viliendelea nje ya mahakama na hatimaye baada ya muda Patrick naye akatoka akiwa ameongozana na Savanna.Watu walimpongeza na kumsifu Savanna kwa umahiri wake .Kwa mara nyingine tena alidhihirisha umahiri wake katika masuala ya sheria.
Wakati mambo haya yote yakiendelea,Happy alikuwa nyuma ya gari lao akiandika kitu katika kijitabu chake kidogo.alipomaliza akaichana ile karatasi na kuishika mkononi na kuanza kupiga hatua kuelekea katika umati ule wa watu alikokuwa Patrick bila kujali waandishio wa habair na wapiga picha waliokuwa wakimpiga picha katika kila hatua aliyopiga..Savanna ndiye aliyekuwa wa kwanza kumuona Happy karibu na mahala walipokuwa wamesimama
“Happy!” akasema Savanna na kumfuata Happy akamshika mkono akamkumbatia na kupiga piga mgongoni.
“Hongera sana Savanna.Nimeikubali kazi yako.Wewe ni mmoja kati ya wanasheria mahiri kabisa hapa nchini”
“Thank you” akajibu Savanna
“Namshukuru sana Mungu kwa kushinda kesi hii” Akasema Savanna na mara Patrick akatokea
“Happy ! akasema Patrick
“Patrick ! …akasema Happy halafu wakakumbatiana kwa furaha.Savanna ambaye alikuwa amesimama pembeni yao akatabasamu .Happy akasogeza mdomo wake hadi karibu na sikio la Parick akamnong’oneza jambo.
“Hongera sana Patrick.Thank you that you saved me,you saved my life.I’ll always be thankfull to you” akasema Happy halafu akatumbukiza kitu katika mfuko wa koti la Patrick.Taratibu huku machozi yakimtoka Happy akamuachia Patrick na kuanza kuondoka huku Savanna na Patrick wakimtazama
“dady its over now.Tunaweza kuondoka” akasema Happy baada ya kuingia garini
“Ahsante Mungu kwa kusikia kilio chetu na hatimaye Patrick yuko huru.Nina furaha na uchungu kwa wakati mmoja.Ninafuraha kwa kuwa Patrick ameachiwa huru kwa sababu hakutenda kosa lolote .Aliubeba mzigo wangu mimi.Ninalia kwa uchungu kwa sababu hivi sasa ningekuwa pembeni yake tunaufurahia ushindi huu kwa pamoja na pengine ungekuwa ni mwanzo wa kuelekea kutimiza ndoto zetu nyingi tulizokuwa nazo.Ouh gosh ! there will be no dreams anymore.There is no us.I’ve lost Patrick”akawaza Happy.
.Zaidi ya nusu saa bado zoezi la kupongzana liliendelea pale nje ya mahakama.
“Patrick tumekaa sana hapa.Sherehe hizi zinatakiwa zikaendelee nyumbani.Tunatakiwa tuandae sherehe ya kukupongeza.Leo nina furaha sana” akasema Alois kaka yake Patrick.Patrick akatabasamu halafu akamvuta Savanna karibu yake na kusema
“Nadhani yatubidi tuelekee nyumbani kwanza .Nataka nikapunzishe kichwa changu na kumshukuru malaika wangu huyu ambaye ameniwezesha leo niwe huru tena.Nina deni kubwa kwa Savanna.Amepambana kufa na kupona hadi nimeshinda kesi.Nadhani muda huu ni maalum kwa ajili yetu na jioni ya leo tutakuja nyumbani kwa ajili ya kuwashukuru familia nzima” akasema Patrick
“kama ni hivyo basi tutaandaa sherehe ndogo jioni ya leo.Tafadhali hakikisha hukosi kufika nyumbani jioni ya leo” akasema Alois
Patrick akamfuata mama yake aliyekuwa amezungukwa na akina mama wengine ,akamvuta pembeni
“mama mimi naondoka.Nimeongea na Alois nitakuja nyumbani jioni ya leo kwa ajili ya kutoa shukrani zangu kwenu kwa msaada wenu mkubwa katika kipindi chote hiki cha matatizo yangu.”
“Nilidhani tunaondoka wote na kwenda nyumbani? Tunahitaji sana kukaa kama familia leo ni siku yetu kubwa sana” akasema mama yake Patrick
“Ninafahamu hilo mama lakini kwa sasa nahitaji kupumzika kidogo na kumshukuru Mungu.Nitakuja jioni na tutajumuika pamoja” akasema Patrick halafu akaagana na mama yake akamshika mkono Savanna na kuingia katika gari lao na kuondokaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“washa gari.We follow them” akaamuru Loniki ambaye alikuwa garini na Linah .Bila ubishi Linah akawasha gari na kuanza kuwafuata akina Patrick
Sarah bado aliendelea kuangaza macho pale mahakami akitegemea kumuona Linah.Muda wote alikuwa roho juu kila alipokumbuka maneno ya Linah kwamba Loniki amedhamiria kufanya jambo baya endapo mahakama itamuachia huru Patrick.
“Inawezekana Linah alikuwa ananidanganya? Hapana ,Linah hakuwa ananidananya na katu hawezi kufanya hivyo.Ninaheshimiana naye sana na katu hawezi kuthubutu kucheza na akili yangu namna hii.Ninashawishika kuyaamini maneno yake.Lakini mbona hakunipigia simu kama alivyokuwa ameniahidi? Na simu yake kwa nini haipatikani tena?” akawaza Sarah huku akiangaza angaza na mara akawaona Patrick na Savanna wakiingia katika gari lao la kifahari wakaondoka pale mahakamani..Sarah akahisi kama nywele zinamsisimka.Alitamani awakimbilie na kumuonya Patrick kuhusu taarifa za kuwepo kwa mpango wa kumuua lakini akaogopa kwa kuwa hakuwa bado na ushahidi wa kutosha wa jambo hilo.Mtu pekee ambaye angeweza kulithibitisha hilo alikuwa ni Linah .
“Natamani nimweleze Patrick kuhusiana na mambo aliyonieleza Linah lakini naogopa.Linah yuko wapi ? akawaza Sarah na mara simu yake ikaita.Alikuwa ni shangazi yake.Sarah akaguna kidogo halafu akaipokea
“Hallow shangazi”
“Sarah uko wapi?
“Niko bado hapa mahakamani”
“Sarah njoo nyumbani mara moja.Hali ya mama yako si nzuri hata kidgo.Mtaarifu na Loniki kama utamuona kwa sababu ninajaribu kumpigia simu lakini simu yake haipatikani.Ulimuona mahakamani leo?
“Hapana sikumuona mahakamani na sina hakika kama alikuja”
“Hata mimi sikumuona sijui yuko wapi.Fanya haraka uje nyumbani” akasema shangazi yake Sarah.
“Sawa shangazi ninakuja sasa hivi” akasema Sarah na kwa haraka akaelekea katika gari lake.
* * * *
Savanna alikuwa anaendesha gari huku machozi yakimtoka
“Unalia nini malaika wangu? Akauliza Patrick
“Patrick machozi haya ya furaha yanatoka yenyewe na hasa nikikumbuka kazi kubwa iliyofanyika.To be honest haikuwa kesi rahisi.Ni moja kati ya kesi ambazo zimewahi kuniumiza kichwa change mno.Thanx God its over” akasema Savanna
“Savanna nina deni kubwa sana kwako na wale wote ambao mmepigana kufa na kupona kuhakikisha kwamba ninakuwa huru tena.Savanna umepambana vilivyo.Sioni kitu cha kukulipa mpenzi wangu.” Akasema Patrick
“Patrick ninaombi moja tu kwako”
“Omba chochote Savanna.”
“Katika watu ambao utawashukuru,usisaha kumshukuru pia Happy.Alifanya jambo kubwa sana..Ushahidi wake ulichangia sana kuipa nguvu hoja ya yetu na kuishawishi mahakama kukuacha huru”
Mara tu Savanna alipolitaja jina la Happy mara moja Patrick akakumbuka kitu.wakati akiwa wamekumbatiana Happy aliweka kitu fulani katika mfuko wake wa koti.Akaingiza mkono mfukoni na kutoa kikaratasi kidogo
“Whats that? Akauliza Savanna
“Ni karatasi Happy aliiweka mfukoni “akasema Patrick halafu akaikunjua karatasi ile na kuisoma.
Kwako Patrick
Nina kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa siku ya leo.Ninafuraha kubwa nisiyoweza kuielezea.Nashukuru mahakama kwa maamuzi yake.Namshukuru sana Savanna kwa kupambana hadi umeachiwa huru.
Patrick nimeamua kukuandikia maneno haya machache kwa sababu sintapata tena nafasi ya kuongea nawe ana kwa ana.This might be our last contact.Maneno machache ninayotaka kukueleza ni kwamba Patrick you are a great man.I’m proud of you.Ninafuraha kukutana na mtu kama wewe katika maisha yangu.
Patrick you saved me.You saved my life.Ninashukuru sana kwa upendo wako usioelezeka wala kupimika.Sina kitu cha kukulipa kwa wema ulionitendea na upendo ulionionyesha toka tulipoonana na kufahamiana.Ninaapa kwamba hatatokea mwanaume ambaye atanionyesha upendo kama ulinionyesha wewe .Nitakuombea siku zote kwa Mungu ili uwe na furaha katika maisha yako.I know Savanna will take a good care of you.You deserve someone better than me,you deserve her.
Patrick we had lots of dreams togeth.I want you to fullfil all the dreams we had.Get married to Savanna and you live a good and Happy life.
Mwisho kabisa ninaomba toka ndani ya moyo wako unisamehe kwa makosa yote niliyokukosea.
I will always miss you
Kiss and goodbye
Happy
Alimaliza kuisoma barua ile na kuirudia tena kwa mara ya pili halafu akaikunja na kuiweka mfukoni
“Anasemaje Happy? Akauliza Savanna.Patrick hakujibu kitu akaitoa barua ile na kumpatia
“utasoma mwenyewe alichokiandika”
Savanna hakuisoma barua ile kwa kuwa alikuwa anaendesha gari akaiweka pembeni kwa lengo la kuisoma baadae
Toka mahakamani Patrick na Loniki wakaelekea moja kwa moja makaburini ambako Patrick alitaka kuweka maua katika kaburi la Vero .Waliegesha gari na kushuka wakaelekea lilipo kaburi la Vero.Akiwa na maua mkononi,Patrick akasimama mbele ya kaburi la Vero.Akalitazama kaburi lile kwa makini halafu akapiga magoti na kuyaweka maua aliyokuja nayo.
Savanna alijisogeza pembeni na kumuacha Patrick peke yake pale kaburini
“He needs to be alone” akawaza Savanna na kusogea pembeni
Wakati Patrick akiwa amepiga magoti katika kaburi la Veronika,gari walilokuwamo Linah na Loniki nalo likawasili.Walikuwa wakiwafuata kwa nyuma akina Patrick.Loniki akaitoa bastora yake akaishika mkononi
“Stay in the car” akasema Loniki na kuufungua mlango lakini kabla hajashusha mguu chini akasikia sauti za watu wakiimba wakielekea kule makaburini
“Whats that ? You hear something? Akauliza Loniki
“Nasikia kama sauti za nyimbo” akajibu Linah mara ukatokea msafara wa watu waliokuwa wanakuja kuzika
“ouh gosh !! akasema Loniki kwa ghadhabu
“Mpango wote umeharibika”
“Damn ..!!!..akazidi kulalama Loniki.Msafara ule wa magari ukazidi kukaribia ,Loniki akafunga mlango wa gari.
Sauti zile za watu wakiimba zikamstua pia Patrick,akasitisha maombi yake na kuinuka
“Twende tuondoke Savanna” akasema Patrick wakaingia katika gari laona kuondoka pale makaburini.Loniki na Linah wakaendela kuwafuatilia kwa nyuma
“ Kama si watu hawa kunivuruga ningemtundika risasi Patick juu ya kaburi la mdogo wangu.Ana bahati sana lakini kabla jua halijazama jioni ya leo lazima niitoe roho yake” akasema Lonki.Linah hakujibu kitu alikuwa anatetemeka kwa ndani.Hakujua angewezaje kumuokoa Patrick kwani Loniki alikwisha dhamiria kufanya mauaji
Toka makaburini Patrick na Savanna wakaelekea moja kwa moja nyumbani .Patrick alikuwa na kazi kubwa ya kupokea simu nyingi nyingi za pongezi toka kwa watu mbalimbali kwa kesi ile kumalizika
“Itanichukua siku nzima ya leo kupokea salamu mbali mbali toka kwa watu.Nimefarijika sana kwa pongezi na pole nyingi toka kwa watu mbalimbali” akasema Patrick kwa furaha
“Bado pongezi zangu mimi” akasema Savanna na wote wakacheka .Waliendelea na safari yao bila kufahamu kwamba walikuwa wanafuatiliwa na akina Loniki
Walifika nyumbani kwao na kusimamisha gari nje ya geti wakisubiri geti lifunguliwe.
“Nahisi wamekuja nyumbani kwao.This is the time” akasema Loniki
Linah akasimamisha gari nyuma ya gari la akina Patrick waliokuwa wanasubiri kufunguliwa geti.
“Wait for me here.Dont do anything stupid to ruin my plan.” akasema Loniki halafu akaichukua bastora yake akaificha kiunoni na kuchomoa funguo ya gari akashuka.Akapiga hatua chache na kulifikia gari la akina Patrick.Akagonga kioo cha mbele upande aliokaa Patrick ambaye aligeuza kichwa na kupatwa na mstuko mkubwa.Aliitambua sura ya mtu aliyekuwa amesimama nje ya gari.
“Loniki ..!!! akasema Patrick kwa mshangao.Hakuwa ametegemea kumuona Loniki sehemu ile na kwa wakati ule.Ni muda mrefu hajawahi kuonana na Loniki.Savanna naye akageuka na kumtazama Loniki.Mara moja akaikumbuka sura ile.Alikumbuka kuiona sura ile katika msiba wa Vero.
“What is she doing here ? akajiuliza Loniki.
Patrick akafungua mlango wa gari na kushuka huku sura yake ikionyesha wasi wasi
“Hallow Patrick.How are you? Ite been a while “ akasema Loniki huku akilazimisha kutabasamu
“Kweli ni muda mrefu sana hatujaonana Loniki.Karibu sana” akasema Patrick.
Geti lilifunguliwa na Savanna akaliingiza gari ndani.Alipatwa na wasi wasi mwingi kuhusiana na ujio ule wa ghafla wa Loniki
“Karibu ndani Loniki” akasema Patrick na kumuongoza Loniki kuelekea ndani
“Ahsante sana” akajibu Loniki na kumfuata Patrick kuelekea ndani
“wow ! Patrick una nyumba nzuri sana.Hongera” akasema Loniki
“ahsante sana “ akajibu Patrick.Bado aliendelea kuwa na wasi wasi kuhusiana na ujio ule wa ghafla wa Loniki
“Hallow I’m Savanna” Savanna akamsalimu Loniki
“Ouh I’m glad to meet you Savanna.You are Patrick’s lawyer right?
“Yes ! “ akajibu Savanna
“Naitwa Loniki.Ni dada wa Veronika.Nimepita hapa mara moja kuwasalimu na kutoa pongezi zangu kwa Patrick na kuongea naye machache ili tuyamalize yaliyopita na tuanze maisha mapya.” Akasema Loniki na kumfanya Patrick atabasamu
Mara tu alipohakikisha kwamba Loniki ameingia ndani na akina Patrick,Linah akachukua simu yake akaiwasha na kuzitafuta namba za simu za Sarah
“ouh my God naomba nimpate Sarah.” Akawaza Linah huku akibonyeza kitufe cha kupigia simu na simu ikaanza kuita.Iliita mara ya kwanza na kukatika bila kupokelewa. Akapiga tena
“Ouh C’mon Sarah pick up the phone” akasema Linah na mara simu ikapokelewa.
“Hallow Linah.Umepotelea wapi?Nimekutafuta mahakamani sijakuona.Nini kinaendelea ? Mbona hatujawasiliana tena?
Huku akihema kwa nguvu Linah akasema
“Sikiliza Sarah hatuna muda wa kupoteza tena.Loniki yuko hapa nyumbani anakoishi Patrick na Savanna.Ana bastora ameificha na akina Patrick hawajui chochote.She’s going to kill Patrick.Tafadhali fanya kila unaloweza ufike hapa mara moja ila nakuomba tafadhali usipite polisi.Ukija na polisi mambo yanaweza kuwa mabaya zaidi.Tafadhali Sarah fanya haraka” akasema Lnah
“Ouh Mungu wangu ! hebu nielekeze mahala nyumba hiyo ilipo” akasema Sarah huku mwili ukimtetemeka.Linah akamuelekeza mahala nyumba ya Savanna ilipo
“Ahsante Linah nakuja sasa hivi.Na wewe unafanya nini hapo? Kwanini usikimbie kuyanusuru maisha yako?
“Natamani sana nikimbie lakini funguo ya gari anayo yeye na amenifungia ndani ya gari”
“C’mon Linah fanya unavyoweza na uondoke humo ndani ya gari.Lazima Loniki atakuua tu.”
“Siwezi kuondoka Sarah.Nataka nijue kila kinachoendelea hapa.” Akasema Linah
“Sawa Linah ninakuja hapo sasa hivi” akajibu Saraha na kukata simu.Akageuza gari na kuanza safari ya kuelekea mahala alikoelekezwa
Akiwa njiani kuelekea nyumbani kwa Savanna akachukua simu na kumpigia shangazi yake
“Shangazi naomba unisikilize vizuri.Muda huu Loniki yuko nyumbani kwa Patrick .Amekwenda kwa lengo la kumuua na sekunde yoyote kuanzia sasa anaweza akafanya hivyo.Ana bastora ameificha .Shangazi tunatakiwa tumzuie asifanye unyama huo anaotaka kuufanya”
“Hebu nielekeze mahala huko aliko Loniki,mbona anataka kutuletea matatizo mengine makubwa? Akasema shangazi yake kwa mstuko
Sarah akamuelekeza shangazi yake mahala nyumba ya Savanna ilipo.Mara tu alipomaliza kuongea na Sarah simuni mama yake Loniki ambaye alikuwa pembeni yake akamkazia macho na kumuuliza
“Nini kimetokea? Kuna tatizo gani?
“Loniki amekwenda nyumbani kwa Patrick .Anataka kumuua ana bastora”
Mama yake akastuka na kupata nguvu za ghafla akainuka na kuelekea chumbani kwake akafungua kabati lake kubwa la nguo na mara moyo wake ukaanza kwenda mbio
“Ouh Mungu wangu ! Loniki amechukua bastora iliyokuwa humu”
Baada ya kuongea na shangazi yake,Sarah akazitafuta namba za simu za Alois na kumpigia akamfahamisha juu ya tukio hilo
“Please Alois we have to save Patrick.Loniki ana silaha na muda wowote anaweza akamuua ” akasisitiza Sarah
“Sarah nakuja huko sasa hivi” akajibu Alois
* * * *
“Habari za siku nyingi Loniki? Akasema Patrick
“habari nzuri Patrick.Ni muda mrefu sana hatujaonana.Nimerudi juzi na kilichonirudisha ni kuhudhuria siku ya leo”.akasema Loniki halafu kimya kifupi kikatanda
“Patrick mimi si mkaaji sana.Nimeona kabla sijarudi London nipite hapa nikusalimu na kukupa pole kwa matatizo yaliyokupata.Pamoja na hayo….” Lonik akainuka na kuwatazama Patrick na Savanna
“Pamoja na hayo nimekuja pia kukuaga Patrick”
“Are you leaving so soon? Akauliza Patrick
“Yah ! soon I’ll be going but today its you who is going.Patrick I’vecome to kill you” akasema Loniki na kwa kasi ya aina yake akatoa bastora yake na kuwalenga Patrick na Savanna
“Loniki ..!! Unafanya nini? Akauliza Patrick kwa mstuko
“shut up !! akafoka Loniki kwa ukali
Patrick na Savanna wakaangaliana kwa woga.Wote walikuwa wanatetemeka .Macho ya Loniki hayakuonyesha masihara hata kidogo.
“Ouh Mungu wangu mambo gani haya yananitokea? Please help me God.Ee Mungu umekuwa unaniokoa katika kila ovu,naomba usiniache katika hili pia.” Patrick akaomba kimoyo moyo huku mwili ukitetemeka
Mara mtumishi wa ndani akaingia pale sebuleni kwa kasi na sinia la vinywaji bila kujua kilichokuwa kinaendelea,ghafla akastuka baada ya kumuona Loniki amewaelekezea Patrick na Savanna bastora ,sinia la vinywaji likamponyoka na kuanguka chini.Loniki akamgeukia
“Ukijaribu kukimbia nakupiga risasi.Kaa pale na ufanye vile nitakavyokuamuru” Loniki akamwambia kwa ukali yule mtumishi wa ndani ambaye alikuwa anatetemeka.
“Pigeni magoti wote” akaamuru Loniki.
“Loniki please don’t kill us.Nitakupa kiasi chochote cha pesa unachohitaji ….!! “ akasema Savanna huku akitetemeka .Machozi mengi yalikuwa yanamtoka
“Shut up !!..akafoka Loniki na kumtazama Yule mfanyakazi wa ndani
“wewe ! Kata ule waya wa umeme na uwafunge hawa mikono kwa nyuma.!! Loniki akamuamuru yule mfanyakazi ambaye kwa woga aliokuwa nao aliitekeleza amri ile kwa haraka.Akawafunga Patrick na Savanna mikono kwa nyuma kwa kutumia waya
“Loniki tafadali naomba usitudhuru.Tumekukosea kitu gani hadi utufanye hivi?” akaomba Patrick.Kauli ile ikaonyesha uzidi kumpandisha hasira Loniki
“Huna haya mshenzi wewe.Ulimuua mdogo wangu bila kosa.Niliapa kulipa kisasi kwa wale wote walioukatili uhai wa mdogo wangu.I loved her so much.Ni kwa sababu ya mapenzi yangu kwake ndiyo maana niliweka ahadi ya kulipa kisasi.Kifo chake kiliniuma sana.How could you kill her like that? Don’t you have a soul you bastard? She loved you with all her heart and in return you killed her.I cant let you walk again.Ndani ya sekunde kadhaa zijazo utaungana naye mbele za haki mshenzi wewe” akasema Loniki na kumtemea Patrick mate usoni.
“Loniki Patrick hakufanya lolote.Hakumua Veronika.Ngoja nkwambie ukw……” akasema Savanna lakini kabla hajamaliza sentensi yake ukasikika mlio wa risasi.Wote wakaanguka na kulala chini.Taratibu Patrick akafumbua macho ,pembeni yake alikuwa amelala Savanna na damu nyingi zikimtoka
“Savanna !! Savanna !! Savannaaaaa..!!!!! “ akaita Patrick huku akilia
“Hiyo ndiyo adhabu yako kuku wewe.Wewe ndiye uliyeishawishi Mahakama imuachie huru huyu mshenzi.Hii ndiyo hukumu yako” akasema Loniki huku akiusogelea mwili wa Savanna pale chini na kuupiga teke.Patrick alikuwa amelala sakafuni mikono yake imefungwa kwa nyuma hivyo hakuweza kufanya lolote.Pembeni yake mwanamke aliyempenda sana alikuwa amelalia dimbwi la damu.
“shetani wewe !! how could you do this? I’m going to kill you !! “ Patrick akasema ghadhabu.
“Usihofu Patrick.In few minutes you’ll join her” akasema Loniki
Mlio ule wa risasi ulimstua sana Linah aliyekuwa amefungiwa garini
“Ouh Mungu wangu tayari Lonny amemuua Patrick” akasema Linah na kuchukua simu yake akampigia Sarah
“Saraha umefika wapi?
“Tayari nimefika maeneo haya.Ndani ya dakika moja nitakuwa nimewasili hapo nyumbani”
“Hurry up ! Tayari risasi moja imelia ndani”
“Ouh my God ! ..akasema Sarah na kuongeza mwendo wa gari.Mikono yake ilikuwa inamtetemeka.
“Nilisikia uchungu sana kwa kifo cha Vero.Hakuna mtu niliyempenda kama yeye.Nataka ukamjibu ni kwa nini ulimsaliti? Kabla hujamuua aliumia sana moyo wake kwa usaliti uliomfanyia. Mateso na maumivu ya moyo aliyoyapata siku ile nataka uyapate nawe leo hii. You’ll die in agony ..! akasema Loniki
“Lonny ..!! Unafanya nini? Akasema kwa sauti Sarah.Loniki akastuka mno baada ya kumuona Sarah pale.Hasira zikampanda mara dufu
“Lonny please ! naomba tafadhali usimuue Patrick..Dont……!!!! akasema Sarah lakini Loniki akamkatisha
“imekuwa vizuri umekuja mwenyewe ushuhudie namna ninavyo mlipia Vero kisasi.Nataka ushuhudie namna Patrick anavyokufa kwa maumivu” akasema Loniki kwa hasira huku mkono wake ukimtetemeka.
“Loniki tafadhali usimuue Patrick.Please I beg you my sister don’t do that..!!! akaomba Sarah huku akipiga magoti
“Sarah sikutambui tena kama ndugu yangu.I don’t know you anymore.Kwa kitendo chako cha kushirikiana na huyu nguruwe wewe si ndugu yangu.Nakukana duniani na ahera.Nina kuchukia sana na baada ya Patrick itakuwa ni zamu yako wewe na Linah…She betrayed me…!!!!
Bila kusita Loniki akaachia risasi kumuelekea Patrick akaanguka chini pembeni ya Savanna.Mlio ule wa risasi ukawastua Linah na Sarah ambao walianguka chini.Baada ya sekunde kadhaa Sarah aliyekuwa anatetemeka mwili akainua kichwa.Hakuamini alichokiona.Patrick alikuwa ameanguka pembeni ya Savanna akiwa katika dimbwi la damu
“Ouh Mungu wangu ..Lonny umemuua Patrick.Umemuua Patrick.Lonny !!! “ akapiga ukelele Sarah na kuinuka akaanza kupiga hatua kumfuata Loniki.
“Sarah simama hapo hapo,usipige hata hatua moja.” Akasema Loniki kwa ukali
“Are you going to shoot me? Akasema Sarah huku akitembea kumuendea Loniki
“Sarah tafadhali naomba usipige hatua hata moja.I’ll shoot you..!!!!! akasema Loniki kwa ukali
“Sarah usijaribu kumsogelea atakupiga risasi ,anamaanisha anachokisema“ Linah aliyekuwa amejibanza pembeni ya mlango akamuonya Sarah
“Shoot me Lonny.Kama mimi si ndugu yako nipige risasi” akasema Sarah huku akipiga hatua kumuendea Patrick aliyekuwa amelala pale sakafuni
“Sarah don’t force me to kill you.Stay where you are” akasema tena Loniki kwa ukali
“Shoot me ..!!! akasema Sarah huku akiunyanyua mguu wake lakini kabla hajaushusha chini ukasikia tena mlio wa risasi.Sarah akaanguka chini.Alikuwa anavuja damu nyingi.Loniki akaushusha chini mkono wake uliokuwa na bastora.Alikuwa anatetemeka
“gosh !! nimemuua ndugu yangu..!! akasema Loniki na kuitupa chini bastora yake akamkimbilia Sarah aliyekuwa amelala chini damu nyingi ikimtoka
“Sarah..! Sarah..!!! Saraaaahhhh….!! Akaita Loniki kwa sauti kubwa huku akilia.Alimuinua mdogo wake na kumuweka magotini pake huku akilia kwa nguvu.
“Sarah !’m sorry ..!!!..I’m sorry sarah ..!! …Please forgive me ..!! ..Loniki aliendelea kulia kwa nguvu.Pembeni ya mlango Linah alikuwa ameanguka na kuzirai
Mara katika mlango mkubwa wa sebuleni akaingia Aloisi akiwa ameongozana na askari waliokuwa wamevalia fulana za kujikinga na risasi.Sebule yote ilikuwa imetapakaa damu.Watu watatu walikuwa wamelalia damu.Loniki bado aliendelea kulia kwa nguvu.Askari polisi wakaiokota bastora ile ya Loniki aliyokuwa ameitupa pembeni.
Magari mawili ya wagonjwa yakafika haraka sana .Patrick,Savanna,Sarah,Linah na msichana wa kazi wakapakiwa katika magari na kukimbizwa hospitali.Eneo lote lilitawaliwa na vilio wakati miili inatolewa ndani.Loniki alionekana kama mtu aliyechanganyikiwa.Alikuwa anaongea maneno mfululizo yasiyoeleweka.Polisi walifanya uchunguzi wao wa kina ndani ya ile nyumba na wakiwa katika harakati za uchunguzi mara akawasili mama yake Loniki lakini mara tu alipokutana na umati mkubwa wa watu pale nje akaanguka na kupoteza fahamu.
Baada ya kukamlisha uchunghuzi wao askari polisi wakaondoak na Loniki ambaye bado alionean kama my aliyechanganyikiwa.
* * * *
St Patrick hospital moja ya hospitali kubwa na mpya jijini Dar ambayo hivi karibuni serikali imeitangaza kuwa hospitali ya rufaa iligeuka uwanja wa heka heka baada ya majeruhi wa shambulio la risasi kufikishwa pale hospitalini.Haraka haraka walikimbiza katika chumba cha wagonjwa mahututi kwa ajili ya kuokoa maisha yao.Madaktari wote mabingwa wa upasuaji wakaitwa mara moja ili kuongeza nguvu katika kuokoa maisha ya majeruhi wale.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Vipimo vya awali vilibaini kwamba Savanna tayari amekwisha fariki dunia kabla ya kufikishwa pale hospitali.Patrick na Sarah ambao walionekana kuwa hai wakakimbizwa katika chumba cha upasuaji kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa dharura.Katika chumba kingine cha wagonjwa wa dharura ,Linah na mfanyakazi wa ndani wa Savanna walikuwa wanaendelea vizuri baada ya kuzimia kutokana na mstuko walioupata.Tayari walikuwa chini ya uangalizi wa polisi kwani ni watu pekee ambao walilishuhudia tukio zima lilivyotokea.
Taarifa za kutokea shambulio la risasi nyumbani kwa wakili maarufu Savanna Francis Kito zilisambaa kwa kasi na kusababisha idadi kubwa ya watu kumiminika St Patrick hospital ili kuhakikisha kuhusu taarifa hizo.Walinzi waliokuwepo getini walizuia watu kuingia hospitalini hapo isipokuwa wale wagonjwa wa dharura
Alois akiwa njiani kuelekea hospitali alipatwa na wazo la kuwapigia nyumbani kwao na kuwafahamisha kilichotokea.Akapunguza mwendo wa gari na kumpigia simu mama yake.
“Hallo Alois mbona umeondoka ghafla na hujaniaga unaelekea wapi?Tunahitaji chupa tatu za shampeni pamoja na bia za kopo.Naomba wakati unarudi ununue vitu hivyo uje navyo.” Akasema mama yale.Alois akavuta pumzi ndefu na kufikiri kwa muda
“Alois umesikia “ akauliza tena mama yake
“mama .!! akaita Alois
“Nini Alois? Kama hutaweza niambie ili nimtume mtu mwingne”
“Si hivyo ,mama ila kuna tatizo limetokea”
“Tatizo gani tena?
“mama hakutakuwa na sherehe yoyote tena” akasema Alois
“Alois mbona unanistua? Kwa nini kusiwe na sherehe?
“Patrick amepatwa na matatizo”
“matatizo ?? mama yake akashangaa
“Ndiyo mama”
“Matatizo gani? Akauliza mama yake kwa wasi wasi.Alois akavuta pumzi ndefu na kusema
“Patrick amepigwa risasi….”
“Ouh Mun………..” kabla hajamliza sentensi yake akaanguka ghafla na kupoteza fahamu
“mama .!! mama..!! mama..!!!!’ akaita Alois lakini hakujibiwa.Akaogopa na kukata simu akampigia mke wake akamuomba amuangalie mama yake.
“mama ameanguka ghafla na amepoteza fahamu.Hatujui tatizo ni nini lakini alionekana alikuwa anaongea na simu kwani simu yake imeanguka pembeni na imesambaratika.Uko wapi Alois? Akasema Sesilia mke wa Alois
“Sikiliza mke wangu” akasema alois
“Kuanzia sasa hivi sitisheni shughuli zote kuhusiana na sherehe mliyokuwa mnaiandaa.Hakutakuwa na sherehe tena.Kitu kingine nakuomba uendeshe gari na mumpeleke mama haraka katika hospitali ya karibu kwa Dr Khan ili apatiwe matibabu ya haraka”
“Alois wewe uko wapi? Akauliza Sesi kwa wasi wasi
“Siwezi kuja huko nyumbani sasa hivi.Kuna jambo limetokea nitakutaarifu baadae.Ukishafika hospitali tafadhali nipigie simu” akasema Alois na kukata simu.Mwili bado uliendelea kumtetemeka
“Mambo gani haya yanatupata katika familia yetu? Hata kabla machungu ya kuondokewa na baba hayajapoa ,tunapatwa na tatizo lingine.Ouh Mungu naomba umponye Patrick.Tafadhali usimchukue kwa wakati huu” akaomba Alois.
Mara tu alipofika hospitali alijitambulisha mapokezi na kuomba kuonana na daktari ili aweze kupatiwa taarifa za maendeleo ya mgonjwa wake lakini alitaarifiwa kwamba kwa muda ule asingeweza kumuona daktari kwa kuwa walikuwa katika chumba cha upasuaji wakijaribu kuokoa maisha ya Patrick na Sarah.Alois akapelekwa katika sehemu ya mapumziko katika ofisi ya mganga mkuu akimsubiri amalize upasuaji .Akiwa amepumzika katika sofa jeusi lililokuwa nje ya ofisi ya mganga mkuu simu yake ikaita.Alikuwa ni mke wake.
“Hallow Secy .Tayari mmefika hospitali?
“Ndiyo Alois tumefika lakini kuna tatizo lingine limejitokeza.Dr Khan amempima akagundua kwamba tatizo la mama ni zaidi ya kupoteza fahamu kwa hiyo ametuandikia tumpeleke katika hospitali ya rufaa ya jeshi pale wana wataalamu wazuri na vifaa na wanaweza wakabaini kwa haraka tatizo la mama.Hivi sasa tuko njiani tunaelekea huko hospitali”
“Ouh Mungu wangu ! kwa hiyo Dr Khan hajasema lolote kwamba linaweza kuwa ni tatizo gani?
“Hapana hajasema lolote isipokuwa ametuandikia makaratasi ya kwenda nayo huko na sijui kaandika nini”
“Unaionaje hali ya mama?
“hali yake haina mabadiliko yoyote”
“Uko na nani hapo karibu?
“Niko na ndugu wengine hapa .Wewe uko wapi? Njoo Alois hali hii mimi inaniogopesha sana” akasema Secilia
“Sesilia naomba uwe na ujasiri hasa kwa wakati huu .Mimi nitakuja lakini kwa sasa niko sehemu fulani.Ukifika hospitali nitaarifu kuna jambo nitakuelezea lakini nataka wakati uko peke yako”
“Alois nini kinaendelea?”
“Nitakwambia baadae.Ukifika hospitali nijulishe” akasema Alois na kukata simu.Jasho lilikuwa linamtiririka
Takribani masaa mawili yamekwisha pita sasa toka Alois alipofika hapa hospitali.Bado Patrick alikuwa katika chumba cha upasuaji.Madaktari walikuwa na kazi ngumu ya kujaribu kuokoa maisha yake na Sarah.Alois alishindwa kukaa akasimama na kuzunguka zunguka .Akiwa bado katika mawazo mengi simu yake ikaita
“Hallow Secy.Nipe habari za huko “ akasema Alois
“Tumemfikisha mama hapa hospitali na tayari madaktari wamempokea na wanaendelea kumfanyia uchunguzi.Hali ya mama si nzuri hata kidogo.Hapa nilipo ninatetemeka.Kwa jinsi anavyoonekana lolote linaweza likatokea.” Akasema Secilia
“Secy be strong my love.Tunapita katika kipindi kigumu sana. Sasa hivi.Just be strong Secy I’ll join you soon”
“Alois kuna jambo gani huko uliko kiasi kwamba huwezi kufika hapa hospitali? Uliniambia kuna jambo unataka kunieleza ni jambo gani hilo?
“Secy tafadhali naomba usipge ukulele wowote na kuwastua watu wengine.Kuna tukio limetokea.Patrick amepigwa risasi” akasema Alois
“Whaaat ….!!!!!!!! Sesilia akastuka na taratibu akaona nguvu zinamuisha akajikuta akikaa chini.Ilimchukua zaidi ya dakika moja Sesilia kuongea tena
“Kapigwa risasi na nani?
“kapigwa risasi na Loniki dada yake Vero.Yeye,Savanna na Sarah wote wamepigwa risasi”
“Ouh gosh..! anaendeleaje? Ni mzima?
Mpaka hivi sasa bado madaktari wanaendelea na upasuaji wakijaribu kuyaokoa maisha yao.Siwezi kusema chochote kwa sasa.Nitakujulisha baadae nini kinachoendelea hapa”
“Alois tafadhali naomba uniambie kama Patrick bado yuko hai” akasema Sesilia
“Sesi siwezi kusema lolote kwa sasa na ndiyo maana nimeogopa kumwambia mtu yeyote kwanza kuhofia yasije yakatokea kama yaliyotokea kwa mama”
“Ulimwambia mama? Akauliza Sesi
“Nilimpigia simu na kumpa taarifa hizi na ndiyo sababu ya kuanguka na kupoteza fahamu”
Sesi alisikika akili simuni na baada ya muda akasema
“promise me Alois that Patrick will be fine” Akasema Sesi
“I don’t know my love.I real don’t know.Tunachotakiwa kufanya kwa sasa ni kumuombea .Nitakupa taarifa zaidi baada ya kuonana na madaktari”
“Alois I’m coming there to join you .Nimepatwa na mstuko mkubwa sana” akasema Sesilia
“Hapana usije huku hospitali.Kaa hapo hapo hospitali baada tu ya kupata taarifa za huku nitakuja huko mara moja” akasema Alois
* * * *
Ni saa mbili za usiku.Happy alikuwa amejilaza sofani akiongeza sauti ya runinga ili aweze kutazama taarifa ya habari.Pamoja naye pale sebuleni alikuwepo mzee Kibaho, na Margreth.Mama yao alikuwa jikoni akisaidiana na Pendo mtumishi wa ndani kuandaa chakula cha jioni
“Pengine.Katika taarifa ya habari ya leo watatangaza maamuzi ya mahakama ya kumuachia huru Patrick” akasema Happy
“Kulikuwa na waandishi wengi wa habari pale mahakamani kwa hiyo nina uhakika mkubwa lazima hii itakuwa ni moja ya habari za leo” akasema Margreth huku akicheka kicheko kidogo
“Wakili maarufu nchini amefariki dunia kwa kupigwa risasi”
“Kenya yaongeza askari wake nchini Somalia”
Hivyo vilikuwa ni vichwa vya habari vilivyosomwa katika muhtasari wa habari.
“Wakili gani maarufu kapigwa risasi? Akauliza Happy na kukaa vizuri ili aitazame vizuri taarifa ile ya habari.
Baada ya muhtasari ule wa habari ikafuata habari kamili
“Wakili maarufu nchini Bi Savanna Francis Kito amefariki dunia kwa kupigwa risasi nyumbani kwake alasiri ya leo.Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi wa kanda maalum ya Dare s salaam,wakili Savanna amepigwa risasi muda mfupi baada ya kuwasili nyumbani kwake akitokea mahakamani ambako alikuwa akimtetea mtu ambaye anadaiwa ni mpenzi wake aliyekuwa anakabliwa na shitaka la kuua bila kukusudia na kumuwezesha kushinda kesi hiyo.Pamoja na Savanna watu wengine waliopigwa risasi na ambao hali zao zinasemekana ni tete ni mpenzi wake Patrick ,pamoja na mtu mwingine aliyejulikana kwa jina moja tu la Sarah.Jeshi la polisi linamshikilia mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina moja tu la Loniki kwa kuhusika na tukio hilo.Enzi za uhai wake,Savanna alikuwa anamiliki kampuni ya uwakili iliyojizolea sifa kemkem ndani na nje ya nchi kutokana n uamahiri wake wa kusimamia kesi kubwa kubwa.Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peoni Amina
Mara tu taarifa ile ilipomalizika,kila mtu pale sebuleni hakuamini alichokitazama.Ghafla kikasikika kishindo Happy alianguka na kupoteza fahamu.Kikaibuka kizaa zaa kingine pale sebuleni.Margreth alipiga kelele kubwa na kumstua mama yao aliyekuwa jikoni ,akatoka mbio na kuja sebuleni na kumkuta mwanae akiwa amelala chini hana fahamu.Mzee Kibaho akaendelea kumpatia huduma ya kwanza.Wote kwa pamoja wakashirikiana kumpatia Happy huduma ya kwanza ili azinduke.
Hatmaye baada ya jitihada kubwa za wote pale sebuleni Happy akazinduka.Mama yake akamkumbata kwa nguvu.
“Mama wamemuua Patrick….Patrick amepigwa risasi..!!.Ouh Patr…….” Happy akaangua kilio
“Usilie Happy.Nyamaza kulia .Patrick bado yuko hai,hajafa” akasema mzee Kibaho
“Patrick amekufa? Akauliza kwa mshangao mama yake Happy
“Patrick na Savanna wamepigwa risasi alasiri ya leo baada ya kufika nyumbani kwao wakitokea mahakamani.Savanna yule wakili wake amefariki dunia na Patrick hali yake inasemekena si nzuri.” Akasema mzee Kibaho.Mke wake akashika kichwa kwa mikono yake
“Ouh Jamani.! Nani amefanya ukatili wa namna hii? Savanna amekufa? Hata siamini” akasema mama yake Happy
“Mama nitampata wapi Patrick? Wamemuua mpemzi wangu.Wamemuua Patrick..why they killed him?...Happy akaendelea kulia
“Happy Patrick hajafa.” Akasema mzee Kibaho akijaribu kumtuliza mwanae
“Patrick is dead.They killed him.I need to die too…” akasema Happy
“Happy taarifa ile inasema kwamba aliyethibitishwa kufa mpaka sasa hivi ni Savanna lakini Patrick na mtu mwingine wao bado wazima ingawa hali zao si nzuri.Kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa Patrick akapona.Nyamaza kulia mwanangu na tumuombee Patrick” akasema mzee Kibaho ambaye hata naye alikuwa anatetemeka kwa ndani.Alisikia uchungu mkubwa sana.
“dady take me to hospital..I need to confirm this..” akasema Happy huku akiinuka.lakini miguu yake haikuwa na nguvu akaanguka .
“Pumzika Happy.Hali yako si nzuri .Naomba uniamini nikwambiayo,Patrick hajafa.Tulia na kesho asubuhi tutafuatilia taarifa hizi” akasema mzee Kibaho
Happy hakujibu tena.Aliendelea kulia.Familia nzima ilikuwa kimya na kila mmoja alikuwa anawaza lake.Taarifa ile iliwastua sana.Margreth alikuwa amekaa chini.Hakuweza kuongea lolote.Ni machozi tu ndiyo yalikuwa yanamtoka.Alimfahamu Patrick kwa muda mrefu sana.Alifahamu ni namna gani alivyokuwa mtu muhimu kwa dada yake Happy.Alivuta kumbu kumbu na kukumbuka sura ya Patrick pale mahakamni.Kila alipoikumbuka sura ya Patrick na Savanna machozi yalizidi kumtoka.Mama yao naye alikuwa amekaa sofani akitoa mchozi.
“Siku zote nilikuwa namsema vibaya sana Patrick.Nilimuona kama mtu mbaya aliyekuwa akimsababishia mabalaa mwanangu Happy.Masikini Patrick nani lakini aliyemfanyia unyama huu ? Alikuwa ni kijana mpole na asiye penda ugomvi na mtu.Alimpenda sana Happy hadi akaamua kukaa gerezani badala yake.Happy atakuwa katika wakati mgumu sana kwani najua pamoja na yote yaliyotokea lakini bado anampenda mno Patrick.Kama Patrick atafariki maisha yake hayatakuwa na furaha tena”
Akawaza mama yake Happy huku akimtazama mwanae Happy aliyekuwa amekaa juu ya zulia akiendelea kulia.Mzee Kibaho alijitahidi kutokuwaonyesha mstuko alioupata na kuendelea kuwapa moyo familia yake lakini kwa ndani alikuwa anatetemeka.Alitoka pale sebuleni na kuelekea chumbani kwake Akatoa kitambaa na kujifuta machozi.Alibaki amesimama kwa takribani dakika mbili akiangalia juu.Kichwa chake kilijaa mawazo mengi.
“Ouh Jamani nani huyu ambaye amemfanyia Patrick jambo baya kama hili ? nani huyu anayetaka kumuua Patrick.Namfahamu yule kijana hana ugomvi na mtu yeyote kwa nini basi afanyiwe kitendo cha kinyama kama hiki? Mungu wangu naomba umponye Patrick.Usimchukue sasa hivi” akawaza mzee Kibaho na kukumbuka kitu alichokuja kuchukua mle chumbani.Akafungua kabati lake dogo na kuchukua vidonge viwili vya usingizi na kurejea sebuleni akampatia Happy.Lengo lake lilikuwa kumsaidia Happy ili aweze kulala.Happy akazipokea dawa zile akameza na kisha mzee Kibaho akamshika mkono akampeleka chumbani kupumzika na kisha kurejea sebuleni.Mara simu ya Margreth ikaanza kuita.Aliitazama simu ile ikiita lakini hakuwa na nguvu za kuinuka mahala alipokaa na kwenda kuipokea .Mzee Kibaho akaichukua na kutazama mpigaji.Alikuwa ni Mike
“Hallow Mike” akasema mzee Kibaho
“Ouh kumbe ni wewe baba, shikamoo”
“marahaba Mike,habari za huko?
“Habari za huku nzuri.habari za Tanzania?
“Tanzania kwema tu”
“baba,Margreth uko naye karibu?
“Mike,Margreth yupo lakini ameshindwa kupokea simu yako muda huu.Kuna matatizo yametokea”
“matatizo gani baba? akauliza Mike kwa wasi wasi
“Ni kuhusu Patrick”
“Patrick amefanya nini? Happy aliniambia kwamba leo ilikuwa ni hukumu yake.Amehukumiwa kifungo?
“Patrick hajafungwa.Mahakama imemuachia huru “
“Hizo ni habari njema sana.Nini basi kimemtokea?
“Patrick amepigwa risasi” akasema mzee Kibaho.Kimya kikatanda simuni .Baada ya muda Mike ambaye sauti yake ilionyesha mstuko mkubwa akauliza
“Nani kafanya tukio hilo?Vipi hali yake?
“Mpaka sasa hivi kuna mtu mmoja ambaye anashikiliwa na polisi na inaaminika ndiye aliyefanya tukio hilo.Hali yake bado haijulikani lakini kwa kujibu wa taarifa iliyopatikana toka hospitali alikokimbizwa ni kwamba hali yake ni mahututi na madaktari wanajitahidi kujaribu kuokoa maisha yake.”
“Ouh Mungu wangu.!!!! Happy yuko wapi? Amekwisha zipata taarifa hizi?
“Ndiyo amezipata taarifa hizi .Alistuka na kupoteza fahamu.Hivi sasa nimempa dawa za usingizi amelala.Mike nadhani ingekuwa vyema kama tungewasiliana kesho kwa sababu kwa sasa watu wote bado tuko katika taharuki” akasema mzee Kibaho
“Ahsante baba.Nashukuru sana kwa taarifa.Poleni sana.Tafadhali naombeni mnitaarifu kila kinachoendelea na kama kuna kitu ninaweza kusaidia.Nimestushwa sana na taarifa hizi”
‘Usijali Mike tutakufahamisha” akasma mzee Kibaho na kukata simu
* * * *
Mlango wa chumba cha upasuaji ulifunguliwa na kitanda cha magurudumu kikatolewa na kupelekwa katika jingo la wagonjwa wa uangalizi maalum.Ilikuwa ni saa tatu na robo za usiku.Upasuaji aliofanyiwa Patrick ulichukua muda mrefu kukamilika
Alois bado alikuwa katika ofisi ya mganga mkuu akisubiri upasuaji umalizike ili ajue kinachoendelea.Akiwa bado amejiinamia akitafakari mara akatokea daktari mkuu akiwa ameongozana na maafisa watatu wa polisi.
“natumai utakuwa ndugu Alois” akasema daktari yule bingwa huku akimpa mkono Alois
“Ndiye mimi dokta” akajibu Alois.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nimepewa taarifa zako kule chini.Pole sana kwa kunisubiri kwa muda mrefu.Karibu ofisini” akasema daktari na Alois pamoja na wale maafisa wa polisi wakaingia ofisini
“Ndugu zangu huyu hapa ni Alois .Kwa taarifa nilizopewa ni kwamba yeye ni ndugu wa Patrick yule majeruhi tuliyemaliza kumshughulikia hivi punde.Alois hawa ni maafisa wa polisi wakiongozwa na mkaguzi Ernest Kengele” Dokta Ezekiel majala akafanya utambulisho mfupi halafu akaendelea
“Ndugu zangu nimewaiteni hapa kuwapeni taarifa ya awali ya maendeleo ya wagonjwa walioletwa hapa.Tulipokea watu watano watatu kati yao walikuwa wamejeruhiwa vibaya sana kwa risasi ,mmoja kati ya hao waliojeruhiwa alikuwa amekwisha fariki.Jina lake ni Savanna .Alifariki kabla hata ya kufikishwa hapa hospitali.Wagojwa wengine wawili hawakuwa na majeraha yoyote isipkuwa walikuwa wamepoteza fahamu kutokana na mstuko.Hawa tuliwapatia msaada na tayari wamekwisha zinduka na wanaisaidia polisi hivi sasa.” Akasema Dr Ezekiel akawatazama watu wote mle ofisini na kuendelea
“Wagonjwa wawili waliokuwa wamejeruhiwa vibaya sana kwa risasi tuliwafanyia upasuaji.Mmoja ambaye ni mwanamke alikuwa amepigwa risasi katika bega la kushoto. Kwa bahati nzuri haikuweza kuleta madhara makubwa.Patrick yeye ndiye aliyekuwa amejeruhiwa vibaya sana.Nadhani lengo la mtu aliyemshambulia lilikuwa ni kumuua kwani alilenga kuupiga moyo lakini kwa bahati nzuri risasi ilipita pembeni kidogo ya moyo na hivyo kujeruhi baadhi ya msihipa..Tunaendelea kumuangalia kwa karibu zaidi na endapo italazimika kufanya tena upasuaji mwingine basi tutafanya hivyo lakini kwa sasa siwezi kusema lolote kwani tumuweka katika mashine ya kumsaidia kupumua.Ninapenda kuwahakikishia kwamba tutafanya kila tuwezalo ili kuokoa maisha yake..” Akasema Dr Ezekiel.
* * * *
Baada ya kutoka hospitali alikolazwa Patrick,Alois akaeleka moja kwa moja katika hospitali ya jeshi alikopelekwa mama yake.Nje ya hospitali ile alikutana na kundi kubwa la akina mama na ndugu wengine waliofika pale baada ya kupata taarifa za kilichotokea.Wengi wao walikuwa wanatokwa na machozi.Alois akawasalimu na walitaka kujua kilichokuwa kinaendelae huko alikotoka kwani tayari taarifa zilikwisha sambaa kwamba Patrick amepigwa risasi.Aliwaeleza hali ya Patrick ilivyo na kuwapa moyo .
“Vipi maendeleo ya mama? Kuna taarifa zozote toka kwa madaktari?Alosi akamuuliza mke wake
“Mpaka mida hii bado hakuna taarifa zozote tulizopewa ,bado madaktari wanaendelea kumfanyia uchunguzi wa kina kujua tatizo lake na wametuomba tuwasubiri hapa” Akasema Secilia.Alois akainamisha kichwa.Alihisi kuchanganyikiwa.
“Alois ni nani aliyempiga Patrick risasi? Tayari amekamatwa? Akauliza Secilia
“Kwa mujibu wa polisi mpaka sasa hivi wanawashikilia watu watatu ambao walikutwa eneo la tukio lakini aliyefanya tukio hilo ni Loniki dada yake Vero.Nasikitika sikuwahi kufika mapema eneo la tukio pengine ningeweza kulizuia tukio hili lisitokee”
“Ulitaarifiwa kuhusu tukio hilo? Akauliza Secilia huku akionekana kushangaa
“Muda mfupi kabla ya tukio kutokea,Sarah alinipigia simu na kunitaarifu kwamba niende haraka nyumbani kwa Savanna kwani Loniki alikuwepo kule na alikuwa amedhamiria kumdhuru Patrick.Niliondoka nyumbani haraka bila kuaga au kumwamba mtu yeyote na nilipofika eneo la tukio tayari Loniki alikwisha fanya alichotaka kukifanya”
“Loniki mwenyewe amekamatwa? Akauliza Secilia huku akimuma meno kwa hasira
“Naye ni miongoni mwa watu wanaoshikiliwa na jeshi la polisi” akasema Alois halafu wote wakakaa kimya baada ya kutolea daktari ambaye aliwataka ndugu wa karibu wa mgonjwa wamfuate ofisini.Alois,Secilia na akina mama wengine wawili wakaongozana na daktari hadi ofisini kwake.
“Poleni sana ndugu zangu kwa matatizo” akaanzisha mazungumzo daktari
“Ndugu zangu nimewaiteni ili niwape taarifa kuhusu mgonjwa wenu.Tumempokea mgonjwa akiwa katika hali ya kutokujitambua na tumemfanyia uchunguzi ili kujua tatizo lake.Tumegundua kwamba mgonjwa wenu amepatwa na tatizo la kupooza upande wa kulia.”
“Ouh Mungu wangu …!! Alois akastuka na kushika kichwa chake.Hakuwa ametegemea taarifa ile.Secilia alishindwa kujizuia akaangua kilio.Mmoja wa akina mama akamtoa nje
“Poleni sana ndugu zangu lakini huu ni ugonjwa wa kawaida na unaweza kumpata mtu yeyote na hasa watu ambao umri wao ni mkubwa .Tayari tumekwisha muanzishia matibabu na msiwe na wasi wasi .Hapa tunao madaktari bingwa wa magonjwa haya na nina imani atapona na kurejea katika hali yake ya kawaida” akasema daktari.
* * * *
Saa kumi na mbili za asubuhi tayari Happy alikwisha amka.Alilala usingizi mzito kutokana na dawa za usingizi alizokuwa amepewa.Familia nzima ilikwisha amka mapema na kujiandaa kwa ajili ya kwenda hospitali kufuatilia hali ya Patrick.Walipokuwa tayari wakaingia garini na kuondoka kuelekea hospitali
“Ee Mungu naomba msaidie Patrick apone.Naomba usimchukue mapema .Ni mwanaume wa pekee kabisa hapa duniani.Bado tunamuhitaji mno katika maisha yetu.Please Lord help me,don’t take Patrick now”” Happy alikuwa anaomba kimya kimya wakati wakielekea hospitali
Waliwasili hospitali na kukuta kundi kubwa la watu waliokuwa wamekuja kuwaona ndugu zao waliolazwa hapo hospitalini.Hawakujua ni wapi wangeweza kupata taarifa za maendeleo ya Patrick.Mzee Kibaho akaenda mapokezi akaongea na wauguzi waliokuwapo pale na kuelekezwa katika jengo ambalo ni maalum kwa wagonjwa walio mahututi.Haraka haraka mzee Kibaho na familia yake wakaelekea upande ule.Kulikuwa na idadi kubwa ya watu ambao walikuwa wamesimama nje ya jengo lile.Wakiwa wamesimama pale nje mara Alois akatoka ndani ya lile jengo.Ndugu ,jamaa na marafiki waliokuwepo pale kufuatilia hali ya Patrick wakamzunguka.Alois alionekana kuwa na haraka.Aliwatuliza watu wale waliokuwa wamemzunguka na kuwaambia kwamba Patrick alikuwa anaendelea vizuri kisha akawaacha watu wale na kuanza kutembea kwa kasi.Happy akamkimbilia na kumuita
“Alois .!!!” alois akageuka na kukutana na sura iliyosawajika ya Happy
“ Happy ..!!! akasema Alois kwa mshangao.Mara moja familia nzima ya Happy ikamfuata.Alois akasalimiana nao wote
“Pole sana Alois “ akasema mzee Kibaho
“Tumekwisha poa mzee “ akajibu Alois
“Vipi maendeleo ya Patrick? Akauliza Happy
“Hali yake si mbaya sana kwa mujibu wa madkatari ingawa bado yuko katika mashine ya kumsaidia kupumia.” Akasema Alois
“My God please save him “akasema Happy huku akishindwa kujizuia kuangusha machozi
“Usihofu Happy.Tunatakiwa tumuombee sana” akasema alois
“Aliyefanya unyama huu tayari amekamatwa? Akauliza kwa hasira mzee Kbaho
“Ni Loniki dada yake Vero.Tayari anashikiliwa na jeshi la polisi pamoja na watu wengine wawili.” Akasema Alois na kuchukua namba za simu za mzee Kibaho kwa ajili ya mawasiliano.Kabla hajaondoka Happy akamuuliza
“Alois is there anything I can do to help? Akauliza Happy.Alois akasita kidogo halafu akajibu
“Happy nashukuru sana lakini kwa sasa naomba upumzike nitakapokuhitaji nitakutaarifu”
“Alosi I need to help.Patrick is my friend.He’s here ni my heart.Please let me do something for him” akasema Happy huku akilia
Alois akafikiri kidogo na kusema
“Ok Happy.Ahsante sana kwa msaada wako.Hivi tunavyoongea mama yetu amelazwa hospitali amepatwa na tatizo la kupooza upande mmoja baada ya kupata taarifa za Patrick kupigwa risasi.Naomba uende pale na usaidiane na wale akina mama wanaoendelea kumuuguza .I know you are strong woman.Wengi wao wanashindwa kuvumilia wakimuona mama.Ninaimani utawapa moyo na kuwatuliza.Pale utamkuta Secilia mke wangu mimi nitakuja baadae natakiwa kituo cha polisi” akasema Alois.Familia ya Happy wakaonekana kustushwa na taarifa ile ya ugonjwa wa mama yake Patrick
“Alois nashukuru sana kwa nafasi hii.Ninaelekea huko sasa hivi.As far as I’m doing this for Patrick I’l be strong” akasema Happy huku akifuta machozi
“Ahsante sana Happy.Nitampigia simu Secilia ambaye yuko kule toka alfajiri kumfahamisha.Utasaidiana naye kwani yeye ndiye niliyemkabidhi majukumu yote ya kule” akasema Alois na kumpatia Happy namba za simu za Secilia na kuodoka.Happy na familai yake nao wakaondoka
* * * *
Saa tatu za asubuhi Alois akawasili katika kituo cha polisi kama alivyokuwa ameombwa.Saa nne za asubuhi akaitwa katika ofisi ya upelelezi.
“Alois nimekuita hapa ili kukupa taarifa za awali kuhusiana na uchunguzi wa tukio la jana.Jeshi la polisi hadi hivi sasa linawashikilia watu watatu .Mmoja anaitwa Linah na mwingine ni Loniki na mwingine ni mfanyakazi wa ndani wa Savanna aitwaye Chiku.Linah na huyu mfanyakazi wa ndani wa Savanna ambao hali zao zinaendelea vizuri wataletwa hapa kwa ajili ya mahojiano.Loniki tunaendelea kumshkilia hapa kituoni toka jana ingawa anaonekana kama ni mtu aliyechanganyikiwa.Tunafanya utaratibu wa kumfanyia uchunguzi wa wa kina wa akili yake.Jeshi la polisi litampeleka katika hospitali kuu ya magonjwa ya akili .Pamoja na hayo bado tunandelea na uchunguzi wetu wa kina ili kubaini wale wote waliohusika katika tukio hili.Nashukuru sana kwa ushirikiano wako na endapo utakuwa na taarifa nyingine zaidi ambazo zitaweza kutusaidia tafadhali usisite kutufahamisha mara moja” akasema Inspekta Kengele na baada ya mahojiano kidogo Alois akaondoka
Saa saba za mchana katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere ndege ya shirika la ndege la Afrimerica linalofanya safari zake kati ya nchi za Amerika na Afrika ikatua.Miongoni mwa abiria walioshuka katika ndege hiyo ni bwana na bibi Francis serverine Kito wakiambatana na binti yao Maria.Hawa ni wazazi wa Savanna.Wote walikuwa na sura za majonzi sana
Familia ya mzee Francis Kito imekuwa ikiishi nchini Marekani kwa muda mrefu sasa ambako waanamiliki biashara kadhaa kubwa.
Kisha shuka ndegeni familia hii ililakiwa na vilio toka kwa ndugu na jamaa waliokuwepo pale uwanjani kuwapokea..Toka uwanja wa ndege msafara wa magari ukaelekea moja kwa moja nyumbani kwao Mbezi ambako ndiko kulikuwa na msiba wa Savanna.Watu walikuwa ni wengi sana.Savanna alifahamika na watu wengi katika kipindi kifupi alichofanya kazi yake ya uwakili.Alijizolea sifa kemkem ndani na je ya nchi kutokana na umahiri wake katika sheria.Baada ya kuwasili nyumbani kwao ,eneo lote lilitawaliwa na vilio.Watu wengi ilikuwa ni mara ya kwanza kuwaona wazazi wa Savanna.Wengi wa marafiki na hata watu wa karibu yake hawakufahamu kama wazazi wa Savanna wanaishi nchini Marekani na ni watu matajiri na wenye uwezo mkubwa .Siku zote Savanna kupenda kuweka wazi kuhusiana na familia yake.Hakupenda kujivuna kwa utajiri wa familia yake na siku zote alipambana ili apate mafanikio kuwa nguvu zake na kwa kiasi kikubwa alifanikiwa katika hilo.
Baaa ya vilio kupungua,kikaitishwa kikao cha ndugu kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mazishi.Mpaka wakati huo bado mwili wa Savanna haukuwa umekabidhiwa rasmi kwa familia yake Jeshi la polisi liliendelea na uchunguzi wake.
* * * *
Alois alikuwa amesimama huku mkono mmoja akiwa ameuegemeza katika nguzo.Kichwa chake alikuwa amekiinamisha chini.Alikuwa na mawazo mengi.
“Alois ..!! akaita mke wake aliyekuwa amekaa pembeni yake akiwa na Happy wakisubiri mgonjwa aliyekuwa katika chumba cha vipimo
“Alois ! akaita tena Secilia lakini Alois alionekana kuwa mbali sana kimawazo.Secy akamsogelea na kumshika bega.
“Usiwaze sana Alois.Mungu yupo atatusaidia na tutakivuka kipindi hiki kigumu
“Nashindwa kujizuia kuwaza Secy.Hali za mama na Patrick bado ni tete.Mimi ndiye mkubwa wa familia niliyebaki lazima kichwa kiniume lazima niwaze” akasema Alois.Mke wake akamtazama kwa macho ya huruma na kusema
“Alois nadhani ni vyema niende kwanza nyumbani nikawatazame watoto kwa sababu toka nilipoondoka asubuhi sijui wako katika hali gani.Utabaki hapa na Happy” akasema Secy
“Ahsante sana mke wangu .Nashukuru umekumbuka hata watoto.Kwa sasa mimi akili yangu yote inawaza wagonjwa wangu.Funguo hizi hapa za gari mimi nitatumia gari la Happy si amekuja nalo?
“Ndiyo amekuja na gari” akajibu Secy
“Endapo kutakuwa na mabadiliko yoyote sintakutaarifu mara moja” akasema Alois
Baada ya Secy kuondoka Alois akaenda kukaa katika sofa alilokuwa amekaa Happy ambaye michirizi ya machozi ilionekana mashavuni mwake.
“Happy usilie.Huu ni wakati ambao tunatakiwa kuwa majasiri na kumuomba sana Mungu ili wagonjwa wetu waweze kupata nafuu.” Akasema Alois
“Alois kuna nyakati ninashindwa kuvumilia kutokwa na machozi.Patrick ni mtu wangu wa muhimu sana japokuwa mambo mengi yametokea kati yetu lakini yeye bado ni mtu mwenye nafasi kubwa na ya pekee kabisa moyoni mwangu.He’s my first man to love na sijawahi kumpenda mtu mwingine yeyote kama ninavyompenda yeye.Naomba nikiri kwako Alois kwamba bado ninampenda sana Patrick kwa moyo wangu wote na ndiyo maana ninaumia sana moyoni kwani sikupata nafasi ya kukaa naye na kuongea mambo kuhusu mambo yaliyotokea kati yetu.Alois tell me Patrick wont die because I need to tell him the truth” akasema Happy na kuanza kulia
“Nyamaza kulia Happy.Patrick is strong and a fighter.He will fight this.He’ll live for us who love him so much.Ni ukweli gani unaotaka kumweleza?
Happy akafuta machozi na kusema
“Toka nimerudi nimekuwa nikitafuta nafasi ya kukutana naye ili nimweleze ukweli kuhusiana na kilichotokea kati yetu lakini imeshindikana kwa sisi kukutna tena kwa sababu Patrick ana hasira na mimi .Please Patrick fight for your life.I need you back.You need to hear the truth.” Akasema Happy
“Happy ni jambo gani hilo ambalo ulitaka kumweleza Patrick.You can tell me” akasema Alois
“Ni kuhusu zile picha zangu zilizosambazwa magazetini na mitandaoni ambazo ndizo chanzo cha mimi na Patrick kutengana tena”Alois akavuta pumzi ndefu na kusema
“ Kuna nini kuhusu zile picha?
Happy akafuta machozi na kusema
“Unakumbuka siku ile ambayo mlinikuta gerezani na mama akanitolea maneno ya ukali na akanifukuza?
“Ndiyo nakumbuka siku ile.Kitendo kile cha mama hata mimi sikukifurahia”
“Basi nilipondoka pale gerezani nikiwa katika daraja la Kigamboni nikirejea,nilitekwa na watu nisiowajua .Walinifunga kitambaa usoni na kunipeleka mahala nisipopajua.Waliniweka katika chumba kimoja kikubwa..Niliambiwa kwamba kuna mtu ambaye aliwatuma kufanya kazi ile na kwamba natakiwa nifanye anavyotaka mtu huyo ama sivyo Patrick angeuliwa .Walisema kwamba kuna mtu ambaye ameandaliwa gerezani na ana chakula chenye sumu kali na andapo ningekataa kufanya wanavyotaka basi Patrick angeuawa.Waliniambia ili nimuokoe Patrick asife kwa sumu lazima nifanye mapenzi na watu wawili.Sikuwa na namna nyingine ya kufanya zaidi ya kukubali kwa kuwa sikujua kama walikuwa wananiambia kweli au walikuwa wanatania.Nilifanya mapenzi na watu wale bila kujua kwamba walikuwa wananirekodi na kunipiga picha.Kesho yake picha zilitoka magazetini na video ile kusambazwa mitandaoni.Niliumia sana Alois.Nilifahamu kwamba lengo la watu wale lilikuwa kunidhalilisha.Nilifadhaika sana.Nilikata tamaa ya kuendelea kuishi nikaamua kunywa sumu ili niondoke duniani lakini haikuwa mipango ya Mungu nife mapema.Nilikimbizwa hospitali nikatibiwa na kupona.Namshukuru sana Savanna kwani ni yeye ambaye alinishauri niende kupumzika nje ya nchi ili kuiepuka aibu kubwa niliyoipata.Nilikubali na kuona ndiyo njia pekee kwa wakati ule.I was so stupid to run away and leave Patrick alone.Alinikodishia ndege hadi Rwanda pamoja na kulipia gharama zote za hoteli kubwa niliyokaa .Toka pale Kigali nilienda kuishi nchini Marekani ambako bado ninaishi hadi hivi sasa.Nimerudi Tanzania kwa lengo moja tu la kutoa ushahidi wangu katika kesi hii ya Patrick.Nimekuwa nikitafuta nafasi ya kuonana na Patrick ana kwa ana na kuongea iliniweze kumueleza ukweli ulivyo lakini imekuwa ngumu sana kuonana naye.Kinachonisikitisha zaidi ni kwamba tayari Patrick ananichukia sana kwa kudhani kwamba nilifanya kitendo kile kwa kukusudia .Ni kweli naweza kuwa nilifanya makosa kuondoka na kumuacha peke yake gerezani na kwa muda huu wote sijawahi hata kumtafuta na kumueleza ukweli halisi lakini najua sikufanya kitendo kile kwa makusudi.Nilifanya vile kwa ajili ya kumlinda yeye mwenyewe.Sikujua kama watu wale walioniteka na kuniamuru nifanye vile walikuwa wanatania au vipi.Mimi ni msichana ninayejiheshimu sana na katu siwezi kutenda matendo kama yale kwa hiari yangu. ” Akasema Happy na kumuacha Alois akishangaa
“Happy ! kwa nini hukusema toka mapema kuhusu jambo hili na umesubiri hadi hivi sasa? Kwa nini usingeweka wazi ili uchunguzi ufanyike mara moja na wahusika waweze kubainika na kufikishwa katika mikono ya sheria? Nikweli Patrick aliumia sana kwa kitendo kile na hasa ulipoondoka bila kutoa taarifa yoyote.Aliteseka mno na kukata tamaa ya kuishi tena baada ya kupelekewa picha zile gerezani.Ulifanya kosa kubwa kuondoka.Hivi ni visa toka kwa maadui zenu na ulipaswa usimame imara na upambane.Hukutakiwa kukimbia na kumuacha Patrick peke yake na kumfanya aamini kwamba ulifanya kitendo kile kwa makusudi kabisa.Kitendo cha kukimbia kimewapa ushindi maadui zenu ambao hawapendi kuwaona mkiwa pamoja.Lengo lao limefanikiwa na kwa hivi saa hamko pamoja tena.…Ouh gosh ..!!” akasema Alois
“Nilikuwa nafikiria sana kuhusu kusema ukweli lakini kila nilipofikiria kufanya hivyo nilishindwa kwa sababu siwafahamu watu hao waliofanya kitendo kile na nilidhani nisingeweza kuliweka wazi jambo hili kwa jamii ikanielewa hivyo nikaona ni bora niliache tu kama lilivyo.” Akasema Happy.Alois akatoa simu yake na kumpigia Inspekta KengeleCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hallow Alois” akasema Kengele baada ya kupokea simu
“Samahani kwa kukusumbua afande,kuna taarifa nimeipata sasa hivi toka kwa msichana mmoja aitwaye Happy Kibaho aliyewahi kuwa Miss Tanzania na mpenzi wa Patrick”
“Taarifa gani hiyo Alois?
“Amenieleza kwamba aliwahi kutekwa na watu wasiojulikana akapelekwa sehemu ambayo haifahamu na kulazimishwa kufanya mapenzi na watu wawili kwa madai kwamba asipofanya hivyo Patrick angeuawa.Ili kumnusuru Patrick ambaye kwa wakati huo alikuwa gerezani Happy alikubali kufanya walivyotaka hao watu na kumbe wakati akifanya mapenzi na watu hao walikuwa wakimrekodi na kumpiga picha na kisha kuzisambaza katika vyombo vya habari na kwenye mitandao ya kijamii.Nimeona nikupe taarifa hizi kuhusu jambo hili pengine waliomfanyia hivi Happy ndio hao hao waliotaka kumuua Patrick” akasema Alois
“Ahsante sana kwa taarifa Alois lakini hata sisi tayari tumeipata taarifa hiyo”
“Mmeipata taarifa hiyo? Alois akashangaa
“Ndiyo Alois.Kuna mwanamke mmoja anaitwa Linah ambaye tunamshikilia kuhusiana na tukio hili lililotokea.Huyu tulimkuta katika eneo la tukio akiwa hana fahamu.Baada ya mahojiano,Linah amekiri kwamba Loniki ndiye aliyehusika kuratibu mambo yote hayo na hata kutekwa kwa Happy na kufanyiwa kitendo hicho alichofanyiwa.Anekiri kwamba Loniki ndiye aliyemuua Savanna na kuwajeruhi Patrick na Sarah kwa risasi kwa lengo la kulipiza kisasi kwa kifo cha mdogo wake Vero.Hivi sasa tunamtafuta mtu mmoja anayefahamika kwa jina moja tu la Khumalo ambaye amekimbia na hajulikani alipo.Huyu inasemekana ni mfanyabiashara wa madawa ya kulevya na amekuwa akijihusisha vile vile na vitendo vya ujambazi pamoja na kuwachezesha mabinti wadogo filamu za ngono na kwenda kuziuza nje ya nchi.Khumalo ndiye aliyefanikisha kutekwa kwa Happy na kufanyiwa udhalilishaji ule mkubwa.Kwa sasa tunaelekeza nguvu zote kumtafuta yeye tukishirikiana na polisi wa kimataifa.Tutamuhitaji Happy baadae kwa ajili ya mahojiano ya kina kuhusiana na kilichotokea.” Akasema Inspekta Kengele
“Ahsante sana kwa taarifa hizo afande.Happy niko naye hapa nitakuja naye kituoni hapo baadae”
“Ahsante Alois.Tutazidi kufahamishana kama kuna jambo lolote litajitokeza” akasema Kengele na kukata simu.Alois akavuta pumzi ndefu
“ayari polisi wana taarifa hizo na wamekwisha mfahamu mtu aliyefanya kitendo kile” akasema Alois
“Wamemfahamu? Ni nani huyo shetani aliyenidhalilisha namna ile na kunitenganisha na Patrick ? Nani kawapa taarifa hizo? Akauliza Happy
“Kuna mwanamke mmoja anaitwa Linah ambaye naye alikutwa eneo la tukio akiwa amezimia.Baada ya kuhojiwa amekiri kwamba Loniki ndiye aliyeratibu mpango mzima wa kutaka kumuua Patrick na hata kutekwa kwako na kufanyiwa kitendo kile.Lengo lake likiwa ni kutaka kulipiza kisasi kwa kifo cha mdogo wake Vero”
“Ouh jamani kwa nini lakini afanye vile” akauliza Happy kwa hasira
“Alitaka kulipiza kisasi kwa kifo cha mdogo wake.Polisi pia wanamtafuta mtu mmoja aitwaye Khumalo ambaye ndiye aliyefanikisha mpango huo .Inasemekana Khumalo amekuwa akiwachezesha filamu za ngono wasichana wadogo na kwenda kuziuza nje ya nchi” akasema Alois na Happy akashindwa kujizuia kulia kwa nguvu
“Nyamaza kulia Happy.Tayari waliofanya kitendo kile wamekwisha bainika na watafikishwa katika mkono wa sheria.Lazima haki tendeke.Pole sana Happy.hakuna aliyekuwa akifahamu chochote kuhusiana na tukio lile.Wengi tulikulaani tulipozioan picha zile katika magazeti lakini hatukuufahamu ukweli halisi” akasema Alois
“Alois nina uchungu mwingi sana moyoni.Kwa nini wanitende vile? Hata kama wamejulikana lakini tayari wamekwisha niweka jeraha lisilopona moyoni.Tayari wamekwishaziharibu ndoto zangu zote za kuwa na Patrick .Hata kama wakifungwa lakini hawataweza kuliponya jeraha walilonisababishia moyoni labda kama wakiweza kunirejeshea tena Patrick.Walipofanya nikatengana naye waliyaharibu kabisa masha yangu.Alois ninampenda Patrick .Mimi na yeye tumetoka mbali tuna historia ndefu na ndiyo maana hata baada ya kutengana kwa muda mrefu tulipokutana tu tukajikuta tukiwa wapenzi tena.Kuna kitu kinaishi mioyoni mwetu na hakuna awezaye kukiondoa.Kuachana na wapenzi wetu na kurudiana tena halikuwa jambo rahisi hata kidogo.It was a huge sacrifice lakini tuliweza kufanya hivyo kwa sababu tunapendana .Inaniuma sana kuona yale yote tuliyoyafanya yamekuwa kazi bure.We cant be together anymore.It hurt ..it hurt so much” akasema Happy kwa uchungu
“ Pole sana Happy..Tumuombe Patrick apone ili aufahamu ukweli..Anahitaji kuufahamu ukweli halisi kuhusu nini kilichotokea.Pole sana kwa tukio lile baya kabisa ambalo lilisababisha jamii nzima ikuchukie na kukuhukumu bila kuujua ukweli” akasema Alois na mara akatokea daktari na kuwaita ofisini kwake
* * * *
Tayari jua limekwisha chwea na kiza kimeanza kutanda.Alois na Happy waliwaaga madaktari na wauguzi na kuondoka.Katika hospitali hii hairuhusiwi mtu ambaye si mgonjwa au mfanyakazi wa hospitali kuwepo hapa usiku.Waliingia katika gari la Happy na kuanza safari ya kuelekea katika hospitali alikolazwa Patrick.Safari ilikuwa ya kimya kmya hadi walipofika hospitali na kuonana na daktari wa zamu ambaye aliwafahamisha kwamba hali ya Patrick bado haikuwa na mabadiliko yoyote
“Tuzidi kumuombea Mungu amsaidie.Sisi hapa hospitali tunafanya kila tuwezalo kuhakikisha kwamba hali yake inarejea kuwa nzuri na kama litatokea la kutokea basi ni mapenzi yake Mungu lakini nina uhakika mkubwa kwamba Patrick atarejea katika hali yake ya kawaida hivi karibuni.Yule mwenzake Sarah anaendelea vizuri na tayari tumemuondoa toka katika wodi ya wagonjwa mahututi na tumemuhamishia katika chumba cha kawaida.Kwa siku ya leo ameweza hata kuongea na ndugu zake waliomtembelea.Hata Patrick nina uhakika mkubwa kwamba atapata nafuu muda si mrefu” akasema daktari yule ambaye kitambulisho alichovaa kilionyesha anaitwa Lomayaki Laiza
Toka katika jengo la wagonjwa mahututi Alois na Happy wakaelekea moja kwa moja hadi katika chumba alikohamishiwa Sarah ambako walikutana na ndugu zake wengine waliokuwapo ili kumuuguza.Happy aliogopa sna kuwepo mahala pale akamuacha Alois na kuelekea katika viti vya mapokezi.Alois alisita kuingia ndani kwani toka kilipotokea kifo cha Vero mahusiano ya familia zao hayakuwa mazuri hata kidogo.Mara mlango wa chumba ukafunguliwa na mama yake sarah akatoka
“karibu baba” akasema
“Ahsante sana mama,shikamoo”
“marahaba Alois.Pole sana kwa matatizo’
“ahsante mama .Poleni nanyi”
“Ahsante Alois.Vipi hali ya Patrick anaendelaje?
“Hali yake bado haina mabadiliko yoyote.Bado anasaidiwa kupumia kwa mashine.Lakini madaktari wanasema kwamba atapata nafuu hivi karibuni”
“Namuombea Patrick apone.Sijui ni shetani gani aliyezipitia familia zetu.Alois usinione ninaongea hivi lakini nina uchungu mkubwa sana.Nimelia sana kwa tukio hili.Nimenusurika kumpoteza tena mtoto mwingine.Alois nilitaka kupoteza maisha nilipopata taarifa hizi.Mpaka sasa sielewi ni ujasiri wa namna gani uliompelekea Loniki akafanya kitendo kama hiki.Najua alikuwa ameumizwa na kifo cha mdogo wake lakini sikutegemea kama siku moja angeweza kufanya kitendo cha kinyama kama hiki.” Akasema mama yake Sarah
“Hata mimi inanishanaza sana kwa nini Loniki aliamua kufanya vile.Sikutegemea kama Loniki angeweza kujenga chuki kubwa kama ile.Kifo cha Vero kilituumiza sote,ukiacha Vero hata sisi tulimpoteza baba yetu kwa hiyo hata sisi pia tulikuwa katika wakati mgumu sana. Na hatukutakiwa kuweka chuki kati yetu.Kitendo hiki cha Loniki kimepelekea mama yetu apatwe na mstuko na kupooza upande mmoja.”
“Ouh Jamani..!!! mama yake Loniki akastuka
“Amelazwa hospitali gani?
“amelazwa katika hospitali kuu ya jeshi”
“Vipi hali yake?
“hali yake bado ni tete.Hawezi kuongea au kufanya jambo lolote”
“Pole sana Alois.Najua uko katika wakati mgumu mno wa kuwauguza mama na ndugu yako.Mungu atakupa nguvu Alois na atatusaidia kuyashinda majaribu haya yanayozikumba familia zetu sasa hivi “
“Nashukuru mama .Mungu atatusaidia na watapona.Vipi Sarah anaendelaje?
“Maendeleo yake si mabaya na leo hii ameweza hata kuongea kidogo .Hivi sasa amelala.Namshukuru Mungu hali yake inaendelea vizuri kwa sasa’
“Tunashukuru sana kama hali yake inaendelea vizuri.Nitapita tena kumjulia hali kesho asubuhi”
“Nashukuru sana Alois kwa kutujulia hali”
“Usijali mama tuko pamoja katika wakati huu mgumu”
Alois akamfuata Happy wakaondoka
“ kesho asubuhi mimi nitawahi huku hospitali ili kufahamu maendelo ya Patrick halafuniende kujua hali ya mama.Kesho Cecy, atakwernda kazini kwao ili kona endapo ataweza kupatiwa ruhusa ya mwezi mmoja.”
“ Mimi nitawaho hospitali kumuona mama.Utanikuta kule” akasema Happy
“Happy usisumbuke sana.Unaweza ukapumzika hadimida ya mchana”
“ hapana Alois,nitawahi hospoitali kujua hai a mama.We’re together in this” akasema Happy
“ Ahsante sana Happy” akasema Alis
Kwa kuwa Alois hakuwa na gari ilimbidi Happy ampeleke kwanza nyumbani kwake halafu ndipo aendelee na safari yake ya kwenda nyumbani.
* * * *
Saa nne za asubuhi siku iliyofuata mwili wa Savanna ukakabidhiwa kwa familia yake kwa ajili ya kuendelea na taratibu za mazishi.Jackson Mkikwa mmoja kati ya mawakili wanaofanya kazi katika kampuni ya uwakili ya Savanna aliupokea mwili huo kwa niaba ya familia.Baada ya kukabidhiwa mwili wa Savanna toka jeshi la polisi,ukapelekwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili wa ajili ya kuhifadhiwa hadi hapo taratibu za mazishi zitakapokamilika.Alois alikuwa ni mmoja wa watu waliokuwepo wakati mwili wa Savanna ukikabidhiwa kwa famila na baada ya kushuhudia tukio lile akaondoka kuelekea hospitali ya jeshi alikolazwa mama yake.
“Patrick anaendeleaje? Akauliza Happy baada ya Alois kufika pale hospitali.Happy alikwisha fika pale hospitalini toka saa kumi na mbili za asubuhi
“Bado hali yake iko vile vile.Hakuna mabadilliko yoyote.Vipi hali ya mama? Akauliza Alois
“Mama naye anaendelea vizuri.Kuumekuwa na mabadiliko kidogo katika hali yake” akasema Happy
“eee Mungu tusaidie wagonjwa wetu waweze kupata nafuu ya haraka.” Alois akasema na kutaka kuelekea katika chumba cha mgonjwa lakini Happy akamzuia
“Tumeambiwa tusubiri nje wakati madaktari wanaendelea kumuhudumia mgojwa” akasema Happy.Kikapita kimya kifupi
“Ulimtembelea Sarah leo asubuhi? Happy akauliza
“sikuweza kupata nafasi ya kwenda kumuona.Baada ya kutoka kumuona Patrick nilikuwa na maafisa wa polisi hivyo sikuweza kufika chumbani kwa Sarah.” Akasema Alois
“Mungu atamsaidia na atapona sambamba na Patrick na mama.Kuna taarifa yoyote mpya toka polisi kuhusiana na Khumalo?
“Hapna sijapata taarifa zozote kuhusiana na Khumalo ila mwili wa Savanna umekabidhiwa kwa familia yake baada ya kumalizika kwa uchunguzi” akasema Alois
“Masikini Savanna.Umepata taarifa zozote kuhusiana na taratibu za mazishi?
“Taratibu zinaendelea na kwa mujibu wa Jackson ambaye ndiye aliyeupokea mwili huo kwa niaba ya famlia ,ratiba ya mazishi itatolewa leo baada ya kikao cha ndugu kwani hawakuwa wamepanga chochote kuhusiana na siku ya kumzika Savanna..Pamoja na hayo nina wazo moja”
“wazo gani?
“Ninafikiria kwamba itakuwa vyema iwapo tutakwenda kutoa pole kwa wazazi wa Savanna ambao tayari wamekwisha fika toka marekani wanakoishi.Savanna alikuwa ni mtu wetu wa karibu sana kwa hiyo pamoja na kwamba hata sisi tuko katika wakati mgumu lakini lazima tushiriki kikamilifu katika msiba wake”
“Ni weli Alois.Hilo ni wazo la msingi sana .Tunaweza kuutumia muda huu ambao madaktari wanaendelea na taratibu zao kwenda msibani” akasema Happy.Alois na Happy wakawaaga akina mama waliokuwapo pale hospitali kisha wakaondoka kuelekea nyumbani kwa wazazi wa Savanna ambako ndiko kulikuwa na msiba.Kifo hiki cha Savanna kilitangazwa sana na vyombo vya habari.Savanna alikuwa ni mtu aliyejizolea sifa nyingi kutokana na uwezo na umahiri wake mkubwa katika kusimamia kesi mbali mabli kubwa kubwa nchini.Kutokana na sifa hizo watu wengi walistushwa sana na kifo chake cha ghafla hivyo kupafanya nyumbani kwao pafurike watu
Alois na Happy walifika msibani wakashuka garini na kuingia ndani kwa lengo la kutoa pole kwa familia ya Savanna.Mara tu Happy alipoonekana pale msibani ,minong’ono ikaanza.Happy alikwisha izoea hali hii na haikumpa shida yoyote.Walijitambulisha kwa msimamizi wa shughuli za pale nyumbani ambaye aliwapeleka moja kwa moja katika chumba ambacho alikuwemo mama yake Savanna na mdogo wake Savanna aitwaye Maria.Alois na Happy wakatoa pole kwa wafiwa na baada ya hapo wakapelekwa bustanini ambako baba yake Savanna alikuwa amekaa na baadhi ya wazee.Alois na Happy wakatambulishwa kwake.
“karibuni sana vijana wangu.Nafurahi kuwaona.Kumbe wewe ndiye Happy?
“Ndiye mimi baba” akajibu Happy huku akishangaa ni wapi mzee yule alikomfahamia
“Nafurahi kukuona.Savanna aliwahi kunieleza kuhusu matatizo uliyoyapata na akaniomba ukakae katika hoteli yetu iliyoko Kigali.” Akasema baba yake Savanna na kumfanya Happy astuke.Hakuwa akifahamu kama hoteli ile aliyokuwa akikaa jijini Kigali ilikuwa ni ya akina Savanna
“Ndiyo baba.Niliwahi kupata matatizo makubwa wakati fulani na Savanna ndiye mtu pekee aliyenisaidia sana wakati ule.Msaada wake ulikuwa mkubwa na siku zote atabaki kuwa moyoni mwangu kutokana na moyo wake wa huruma “ akasema Happy
“Nimefarijika sana kwa ujio wenu vijana wangu.Nawapa pole vile vile kwa matatizo mliyoyapata na kufiwa na rafiki yenu.Tunamuombea Mungu Patrick aweze kupona na nina imani Mungu atamsaidia na atapona.Baada ya kumaliza taratibu za kumhifadhi mwanangu basi nitatafuta wasaa na kuja kuwatembelea wagonjwa wote”
“Ahsante sana mzee.Tunakuombea kwa Mungu vile vile akupe nguvu na ustahimilivu wewe na familia yako katika kipndi hiki kibumu.Ni wakati mgumu sana kwetu sote lakini Mungu yuko pamoja nasi” akasema Alois
“Ni kweli vijana wangu.Mimi na familia yangu tuko katika wakati mgumu sana.Kifo cha Savanna kimetuumiza mno na hasa kutokana na mazingira yake.Tulimpenda mno Savanna na tulikuwa na mipango mingi mizuri kwa ajili yake lakini ndiyo hivyo tena ,yameshatokea haya na kutokea,hatuna tena kitu cha kufanya.Haya yote ni mapenzi ya Mungu “ Akasma baba yake Savanna kisha wakaagana na kuondoka
“Savanna hakuwahi kunieleza kama hoteli ile niliyokuwa nakaa kule Kigali ni mali yao.Aliniambia kwamba anafahamiana na mmiliki wa hoteli ile.Ouh Savanna ! Siwezi kuusahau msada ule mkubwa alionisaidia wakati ule.Amekufa wakati ambao bado anahitajika sana.She was too young to die” akasema Happy na macho yake yakalengwa na machozi
“Nilimfahamu Savanna baada ya kuanza kuisimamia kesi ya Patrick.Alikuwa karibu na familia yetu katika kipindi chote cha kesi.Ametufanyia mambo mengi makubwa ambayo si rahis kuyalipa.Alikuwa ni mtu wa kipekee sana.Kitu kinachoinishangaza ni kwamba katikak umfahamu kote Savanna,hata siku moja sikuwahi kusikia akiongelea kuhusu uwezo mkubwa wa kifedha wa familia yake na wala sikufahamu kama alikuwa na mdogo wake ambaye wamefanana kama mapacha.Kwa kweli tumeondokewa na mtu muhimu sana.Katika uhai wake hakupenda kujikweza wala kujivuna” akasema alois wakiwa garini wakirejea toka nyumbani kwa akina Savanna
“Itamchukua Patrick muda mrefu kurejea katika hali yake ya kawaida baada ya kufahamu kamba Savanna amefariki dunia” akasema Alois
“Yah ! atakuwa na wakati mgumu sana.Alimpenda mno Savanna.” Akasema Happy.
Ni siku ya sita sasa toka lilipotokea shambulio la silaha na kusabisha kifo cha Savanna.Patrick alikwisha anza kupata nafuu na alikwisha ondolewa ile mashine iliyokuwa inamsaidia kupumua.Sarah naye alikuwa anaendelea vizuri na ilitegemewa muda wowote angeruhusiwa kurejea nyumbani
“Ni siku ya jumamosi,siku tulivu iliyotawaliwa na kijua kikali,siku ambayo wakili mashuhuri nchini,Savanna alikuwa anazikwa.Watu walikuwa ni wengi sana.Saa sita mchana mwili wa Savanna ukawasili nyumbani ukitokea hospitali ulikokuwa umehifadhiwa.Ulipokelewa kwa vilio toka kwa umati mkubwa wa watu waliokuwa wamekuja kuungana na familia katika kumsindikiza Savanna katika safari yake ya mwisho.Salamu za rambi rambi zilitolewa toka kwwa watu mbali mbali waliohudhuria,akiwemo waziri wa sheria na katiba aliyeiwakilisha serikali na ambaye alikuwa rafiki wa karibu wa Savanna.Baada ya salamu nyingi za rambi rambi toka kwa watu mbali mbali likafuata zoezi la kuuaga mwili wa marehemu.Wengi walipoteza fahamu katika zoezi hili.Zoezi la kuaga mwili lilipokamilika ibada ya kumuombea marehemu ikafanyika hapo hapo nyumbani na kisha mwili wa marehemu ukapakiwa garini na safari ya kumsindikiza Savanna katika nyumba yake ya milele ikaanza.Ulikuwa ni msafara mrefu wa magari kuelekea makaburini.Alois,mke wake Secilia,Happy pamoja na baadhi ya ndugu zao walikuwepo pia.
Hatimaye mwili wa Savanna ukashushwa kaburini.Watu wengi walipoteza fahamu katika hatua hii.Ilikuwa vigumu kuamini kama ni kweli Savanna hawatamuona tena.Kaburi likafunikwa na hatimaye watu mbali mbali wakaweka shada zao za maua juu ya kaburi.Shughuli za mazishi zilikamilika na watu wakatawanyika.Wengi wakarejea nyumbani kwa wafiwa na wengine wakaelekea makwao.Safari ya Savanna duniani ikaishia hapo
* * * *CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hali ya Patrick iliendelea kuimarika siku hadi siku na hatimaye akatolewa katika chumba cha wagonjwa mahututi na kuhamishiwa katika chumba cha wagonjwa wa kawaida.Sarah alikwisha ruhusiwa kurejea nyumbani baada ya hali yake kuwa nzuri
Watu wengi walikuwa wakimtembelea Patrick hospitali na kumjulia hali na kumtakia uponaji wa haraka.Happy alikuwa ni mtu wa kwanza kila siku kumtembelea na kumjulia hali na hakukosa asubuhi mchana na jioni.Chumba cha Patrick kilijaa maua na kadi za kumtakia uponaji wa haraka toka kwa watu mbali mbali waliokuwa wanamtembelea.
Toka amepata nafuu na kuhamishiwa katika chumba cha kawaida,Patrick amekuwa akitembelewa na watu wengi kila siku lakini katik watu wote waliomtembelea kuna watu wawili ambao hakuwaona .Ni mama yake pamoja na Savanna
“Kwa muda mrefu sasa sijamuona mama yangu yuko wapi? Hafahamu kama ninaumwa na nimelazwa hospiali? Kitu kingine kinachonishangaza hakuna mtu ambaye anataka kunieleza mpenzi wangu Savanna anaendeleaje kwa sababu kwa mujibu wa kumbu kumbu zangu,Loniki alimpiga risasi muda mfupi kabla hajanipiga mimi.Savanna anaendeleaje? Yuko wapi? Patrick akajiuliza maswali haya lakini akakosa jibu
“Nitamuuliza Alois” akasema Patrick
“Bado siamini kama Loniki angeweza kufanya kitendo kama kile.Itanichukua muda mrefu sana kuisahau ile siku.Mpaka hivi sasa naona ni kama muujiza mimi kuwa hai.Huu ni muujiza mkubwa Mungu amenitendea.Nilikiona kifo.Nilihisi tayari nimekufa.Nilisikia risasi ikinipenya mwilini .Hili ni tukio baya kabisa kuwahi kunitokea” akasema Patrick na kuuma meno kwa hasira.Mara picha ya Savanna akiwa amelala katika dimbwi la damu ikamjia
“Ouh Savanna ! Kwa nini Loniki alimpiga risasi? Kama alikuwa anataka kulipiza kisasi angenipiga mimi na si Savanna ambaye hahusiani chochote na kilichotokea kati yangu na Vero..I’ll never forgive Loniki for what she did to Savanna.I swear I’ll never forgive her.Amemuumiza mtu ambaye ninampenda na hastahili kabisa kuumizwa.Kama ni kisasi angelipiza kwangu mimi na Happy na si Savanna”
Mara tu alipolikumbuka jina la Happy akahisi kama mwili wote unamsimka
“Happy amekuwa akija kunitazama kila siku asubuhi mchana na jioni.Masikini Happy nimetoka naye mbali sana .Sikutegemea kama siku moja tungefikia hatua kama tuliyofikia ya kuishi kama hatujuani.Sikutegemea kama ingetokea siku ningemchukia Happy.Nilimpenda kwa moyo wangu wote lakini sielewi ni shetani gani alimwingia na kumfanya aamue kufanya ule uchafu na kwa aibu aliyoipata akatoweka bila hata kuniaga.Kila nikilikumbuka jambo hili naumia sana.Aliniacha nikiteseka peke yangu gerezani kwa kosa ambalo sikulitenda.Nikifikiria maumivu niliyoyapata najikuta nashindwa kabisa kumsamehe Happy.Mimi na yeye tuna historia ndefu na mapenzi yasiyoelezeka lakini vyote vilikwisha siku alipoamua kunitelekeza gerezani .Ni Savanna ndiye aliyekuwa nami kila sekunde na amepambana na mimi kuhakikisha ninashinda kesi.Aliiona thamani yangu kwake na ndiyo maana alikuwa radhi kufanya kila aliloweza kunisaidia.Savanna anastahili nafasi kubwa na ya pekee kabisa moyoni mwangu.Sina haja ya kuendelea kumuwaza Happy mtu ambaye aliamua kuniacha na kwenda kurudiana na mchumba wake Mike.Mimi na yeye tutaendelea kuwa marafiki tu.” Akawaza Patrick. Halafu akageuza shingo yake na kutazama pembeni kulikokuwa na lundo la maua aliyokuja nayo Happy.Patrick akanyoosha mkono na kuyavuta maua yale akaichukua kadi iliyokuwa imefungwa pamoja na yale maua.Ilikuwa na maneno matamu ya kumtakia uponaji wa haraka.Patrick akatabasmu na kuiweka pembeni.
* * * *
Siku zilizidi kusonga kwa kasi na hali ya Patrick iliendelea kuimarika siku hadi siku.Tayari alikwisha pewa taarifa kuhusiana na kifo cha Savanna.Alois alimweleza ukweli kwamba Savanna alifariki katika tukio lile Hii ilikuwa ni taarifa mbaya sana kwa Patrick kuwahi kuisikia.Ilimuumiza kupita kiasi na kumfanya apatwe na tatizo la kupoteza fahamu mara kwa mara kwa siku tatu mfululizo.Alionekana ni kama mtu ambaye alichanganyikiwa akili na madaktari walihofia pengine hali ile ingeweza kuathiri maendeleo ya afya yake kwa kiasi kikubwa.
Ilikuwa ni siku ya jumapili siku ambayo watu wengi huitumia kwa ajili ya kuwatembelea ndugu jamaa na marafiki walioko mahospitalini.Hospitali ya St Patrick ilikuwa na idadi kubwa ya watu waliokuja kuwatembelea wagonjwa wao.Chumba cha Patrick kilikuwa kimejaa watu waliokuja kumjulia hali.Ni kawaida ya chumba hiki kujaa watu kila siku wanaokuja kumpa pole Patrick. Lakini kwa siku hii ya leo idadi iliongezeka.Muda wa kuruhusiwa kuwatembelea wagonjwa ulimalizika na watu wakaombwa waondoke pale hospitali
Dakika kama arobaini toka muda uliopangwa kuwaona wagonjwa kumalizika Alois aliyekuwa amebaki na mgonjwa akapigiwa simu .Alikuwa ni mzee Francis Kito baba mzazi wa Savanna
“Shikamoo mzee” akasema Alois
“marahaba Alois hujambo?
“Sijambo mzee”
“Vipi mgonjwa anaendeleaje?
“Anaendelea vizuri sana”
“nafurahi kusikia hivyo. Alois nilikuahidi kwamba siku moja nitamtembelea mgonjwa hapo hospitalini.Sikuweza kufanya hivyo mapema kutokana na mambo kuwa mengi.Kwa kuwa leo nina nafasi nimeona nije nimtazame Patrick niongee naye kidogo.Niko hapa getini naomba uje unichukue” akasema mzee Kito.Kwa haraka Alois akaenda getini na kuichukua familia ya mzee Kito akawaongoza kuelekea katika chumba cha Patrick
Patrick alikuwa amejilaza kitandani kwake akizisoma baadhi ya kadi za kumtakia uponaji wa haraka alizoletewa na watu mbalimbali mara mlango ukafunguliwa na akaingia Alois akiwa ameongozana na familia ya mzee Francis.Patrick akastuka na mapigo ya moyo wake kumwenda mbio na kuhisi kama amemuona Savanna baada ya kugonganisha macho na Maria mdogo wake Savanna.
“Patrick kuna wageni wamekuja kukutembela.Huyu ni mzee Francisi Kito baba mzazi wa Savanna.Huyu ni mama yake mzazi Savanna na huyu hapa anaitwa Maria ni mdogo wake Savanna.Baba ,mama na Maria huyu ndiye Patrick na tunamshukuru Mungu kwa sasa hali yake inaendelea vizuri na kwa mujibu wa madaktari muda wowote anaweza akaruhusiwa kurejea nyumbani” Alois akafanya utambulisho Familia ya mzee Francis wakamsalimu Patrick na kumpa pole nyingi kwanza kwa tukio lililotokea na pili kwa kuondokewa na mpenzi wake Savanna
“Patrick utatusamehe sana kwa kutoweza kufika hapa mapema kukujulia hali.Hilo lilitokana na mambo kuwa mengi sana na hivyo kukosa kabisa nafasi ya kuja.Kilikuwa ni kipindi kigumu sana kwetu kama familia kwa kumpoteza mtoto wetu ,hata hivyo tulikuwa tunawasiliana na Alois ambaye alikuwa akitupa taarifa za maendeleo yako” akasema mzee Francis Kito
“Nafahamu baba.Nafahamu ni jinsi gani mlivyokuwa na wakati mgumu.” Akasema Patrick huku akijifuta jasho usoni
“Kama alivyotangulia kusema Alois,sisi ndiyo familia ya Savanna.Kwa muda mrefu sasa tunaishi nchini Marekani.Tuna miradi yetu kule na vile vile tumefanya uwekezaji kadhaa katika baadhi ya nchi za Afrika na asia.” Akasema mzee Kito
“Nashukuru sana kuwafahamu.Savanna aliniambia kwamba wazazi wake wanaishi Marekani lakini hakuwahi kunieleza wanaishi sehemu gani ya Marekani .Katika mipango yetu tulipanga baada ya kesi kumalizika tungefunga safari kuja Marekani kwa ajili ya utambulisho na kuomba Baraka zenu kabla ya kufunga ndoa,nasikitika kwamba hili halikuweza kufanikiwa”akasema Patrick kwa uchungu
“Pole sana Patrick.Haya ndiyo mambo ya dunia.Savanna hakupenda sana kuwa tegemezi.Siku zote alipenda kufanya kile ambacho alikipenda na ndiyo maana baada ya kumaliza masomo yake ya sheria alirejea nchini Tanzania na kuanza kufanya kazi ya uwakili.Alipenda sana kuwa mwanasheria na ndoto yake ilikuwa ni siku moja awe mwanasheria mkubwa Nadhani ndoto yake hii kwa kiasi fulani ilitimia.Savanna alipenda kuishi maisha anayoyataka yeye na siku zote aliithamini sana furaha ya moyo wake.Mara nyingi alikuwa akitupigia simu na kutueleza ni jinsi gani ulivyoweza kuyafanya maisha yake yawe na furaha.Hata sisi tulifurahi sana kumuona mtoto wetu akiwa na furaha kubwa namna ile.Mimi binafsi aliwahi kunielea namna gani alivyokuwa anakupenda na mipango yenu yote ya baadae,Nasikitika kwamba mipango yenu yote mliyoipanga imeishia njiani.Pamoja na Savanna kutokuwpo leo hii lakini maisha hayana budi kuendelea.Sote tutakufa na tuamini kwamba siku moja tutakutana naye katika makazi ya milele.” Akasema mzee Kibaho.Patrick machozi yalikuwa yanamtoka.Alikosa neno la kusema.Mzee Kito akasema
“Patrick..!
“Naam baba” akasema Patrick
“Utatuwia radhi sana kwa sababu siku ya leo tutakuwa tumekurejeshea machungu ya kuondokewa na mtu uliyempenda sana”
“usijali baba.Najaribu kuizoea hali hii lakini inaniwia vigumu sana.Nadhani itanichukua muda mrefu kuizoea” akasema Patrick.Mama yake Savanna akashindwa kujizuia akatokwa na machozi,akafungua mlango na kutoka mle chumbani
“Patrick pamoja na kukujulia hali,kuna jambo moja ambalo tumekuja kukueleza.Ni kwamba tunategemea kuondoka katika siku mbili zijazo kurejea Marekani.Tumekaa Tanzania kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa.Maisha hayana budi kuendelea.Patrick tunaomba ufahamu kwamba kwa sasa wewe ni mwanetu.Tunakuhesabu kama mmoja wa wanafamilia.Ulikuwa ni sehemu muhimu ya maisha ya mtoto wetu kwa hiyo hata baada ya yeye kutangulia mbele za haki lakini bado tutaendelea kuvienzi na kuvithamini vitu vyote vilivyokuwa na thamani kubwa kwake.Patrick tunakukabidhi mali zote za Savanna zilzoko hapa nchini na nje ya nchi.Hapa Tanzania alikuwa na nyumba tatu.Moja ni ile aliyokuwa akiishi na nyingine mbili amezipangisha kwa mashirika.Vile vile alikuwa na magari matatu,tunakukabidhi pia kampuni yake ya uwakili pamoja na kiwanda cha kusindika nyama na kile ambacho alikuwa katika mpango wa kukifungua cha kutengeneza maji ya kunywa.Vyote hivi ni mali yako na tunakuomba uviendeleze na uvitunze kama njia moja ya kumuenzi mtu aliyekuwa muhimu sana kwako.Wanasheria wetu wanaendelea kufuatilia mali zake nyingine zilizoko nje ya nchi ikiwa ni pamoja na fedha ambazo alikuwa akiweka katika mabenki kadhaa ya ndani na nje ya nchi na watakapokamilisha kazi hii tutakutaarifu.” Mzee Kito akanyamaza kidogo na kuendelea
“Tuna miradi ya uwekezaji ya familia ambayo kila mwaka hugawana kiasi cha faida inayopatikana katika uwekezaji huo.Kila mwanafamilia hupata mgao wao.Kuanzia sasa wewe ndiye utakayekuwa ukichukua fungu la Savanna.” Akasema mzee Kito .Patrick alikosa neno la kusema ni machozi tu yaliyokuwa yanamtoka.Akajitahidi akafuta machozi na kusema
“Baba,mama na Maria sipati neno zuri la kuweza kutoa shukrani zangu kwenu kwanza kwa kuja kunijulia hali.Pili nashukuru sana kwa maamuzi yenu ya kunitambua mimi kama mwanafamilia yenu.Ninayakubali na kuyapokea maamuzi hayo ya familia na ninawaahidi kwamba katika siku zote za maisha yangu nitamuenzi Savanna kama lulu ya pekee kabisa kuwahi kutokea katika maisha yangu.Mali zote nitazitunza na kuziheshimu na kuziendeleza.Ndoto zake zote nitajitahidi kuzitimiza na kulifanya jina la Savanna litukuke kila siku.Sina neno zaidi la kusema zaidi ya hayo machache.Ahsanteni sana na Mungu awabariki” akasema Patrick huku machozi yakimtoka
“Patrick tunakushukuru kwa maneno yako mazito ya shukrani.Tutakuwa tukiwasiliana nawe mara kwa mara kujua hali yako na endapo utakuwa na tatizo lolote usisite kutueleza.Sisi ni wazazi wako na tutakusadia.Kitu cha mwisho ambacho nataka kukueleza ni kwamba Savanna is gone.She’ll never come back.So you have to live your life.You have to move on with your life.Be Happy and enjoy life.That’s the best thing Savanna wants you to do now.” Akasema mzee Kito
“Nimekulewa baba na nitajitahdi kuyafanyia kazi hayo maneno uliyonieleza japokuwa ni vigumu sana.I’ll be Happy for her.I’ll live my life the way she wanted me to” akasema Patrick
Familia ya Franis kito ikaagana na Patrick na kisha wakaondoka na kumuacha akindelea kubujikwa na machozi .Ujio ule ulimkumbusha mambo mengi kuhusu mpenzi wake Savanna.
* * * *
Hatimaye Patrick akaruhusiwa kutoka hospitali.Hali yake ilikuwa nzuri sasa.Ndugu zake kadhaa walikuwepo hospitali pamoja na Happy wakati akiruhusiwa kurejea nyumbani.Wakati wakiondoka Alois alimtaka apande gari moja na Happy lakini kwa mshangao wa wengi,Patrick alikataa na kupanda gari la Alois
Toka hospitali waliekea moja kwa moja katika hospitali ya jeshi alikolazwa mama yake ambaye mpaka wakati huo hakuweza bado kuongea japokuwa hali yake ilikuwa inaendelea vizuri kutokana na mazoezi aliyokuwa akipewa .Patrick alilia machozi mengi kumuona mama yake akiwa katika hali ile
siku iliyofuata Alois na Happy wakampeleka Patrick katika kaburi la Savanna.Patrick alilia sana siku hii.Ilimbidi Alois atumie nguvu kumuondoa pale kaburini akamrudisha nyumbani kwani hakutaka kabisa kuondoka pale kaburini.Toka siku ile Patrick alipenda kuutumia muda mwingi akiwa mwenyewe.
Siku moja jumamosi Happy alifika nyumbani kwa akina Patrick akiwa na maua na kumfuata Patrick bustanini alikokuwa ametulia akisoma kitabu, akamsalimu na kumpatia yale maua.
“Happy kuna jambo nataka kukuuliza” akasema Patrick baada ya kuyapokea yale maua ya Happy
“Uliza usihofu”
“Why are you doing this to me? Kwa muda mrefu sasa umekuwa karibu kufuatilia hali yangu toka nikiwa hospitali na hata sasa.Nakushukuru sana kwa hilo lakini najiuliza ni kwa nini unayafanya haya sasa? Ni njia ya kutafuta msamaha wangu? Au unatafuta tena ukaribu na mimi? akauliza Patrick ambaye alionekana ni mwenye hasira.Happy alibabaika akashindwa ajibu nini
“Answer me Happy.what do you want from me? Akauliza tena Patrick
“Patrick I’m not doing this for you.I’m doing this for me.
“You feel guilty,isnt it? Akauliza Patrick kwa ukali
“You feel guilty for what you did to me,right? Happy machozi yakaanza kumtoka
“Patrick you are my friend.Pamoja na yote yaliyotokea lakini bado una thamani kubwa sana katika maisha yangu.Bado una nafasi ya peke ndani ya moyo wangu na ndiyo maana unaniona niko hapa leo.Its not easy for me to be here but I have to be here,I have to do this” Akasema Happy.Patrick akamtazama kwa jicho kali Happy akaendelea
“Patrick ninafahamu ni jinsi gani unavyoumia moyoni na hasa unaponiona hapa mbele yako.Patrick nisingeweza kuusogeza tena uso wangu mbele yako lakini kinachonifanya niwe hapa karibu yako ni moyo wangu ambao hauna furaha bila ya kukuona.Patrick kuna mambo mengi yametokea kati yetu na nimekuwa nikitafuta nafasi ya kukaa na kuongea nawe kuhusiana na kilichotokea kati yetu lakini umekataa kunipa hata hiyo hafasi ya kuongea nawe tena.Why do you hate me so much? Why don’t you listen to what I want to tell you? Don’t you have any feelings for me in your hear anymore?
Patrick aliyekuwa ameinamisha kichwa chini akainua kichwa na kumtazama Happy kwa hasira
“Feelings ???!!..you don’t have to talk about feelings because you dont know what it real means.You want to know what I feel inside me when I see you? It’s hate.I hate you Happy.I hate you so much.Happy nilikupenda sana nikawa tayari kuacha kila kitu kwa ajili yako,nikaubeba mzigo mzito wa kesi iliyokuwa ikukabili wewe, lakini ni kitu gani umenilipa kwa haya yote? Nothing .!!!!!!! Badala yake umepiga picha chafu na kuzisambaza na kama haitoshi ukaamua kunikimbia na kuniacha peke yangu nikiozea gerezani.Najua ulitegemea ningefungwa gerezani ili uendelee kula raha za dunia na mabwana zako lakini watu walioiona thamani yangu kwao wamenipigania na hatimaye leo hii niko huru tena.Kwa hayo yote hebu jiulize Happy una sababu yoyote ya kutaka kupata nafasi ya kuongea na mimi? You dont deserve even a second of my time.Ninashukuru kwa msaada wako mkubwa wakati ninaumwa lakini kwa sasa nimekwisha pona na ninakuomba kitu kimoja tu,leave me alone.I want to be alone.I don’t need you and I don’t love you anymore.You never loved me it was all lies” akasema Patrick kwa ukali
Happy machozi yalikuwa yanamtiririka.
“Patrick kwa nini unanifanyia hivi? Why are you doing this to me?
“Because you are a monster and you don’t deserve a second chance !! Tafadhali ondoka mbele ya macho yangu Malaya mkubwa wewe !!!!” akasema Partrik kwa ukali na kumfanya Happy azidi kulia kwa nguvu.
Patrick najua unanichukia na sitaki kukulazimisha kwamba unisamehe.Ahsante kwa matusi yote uliyonitukana.Nitaondoka Patrick kama ulivyoniamuru and this time it’ll be for good.You’ll never see me again in your life but before I leave please give me five minutes .Kuna jambo ambalo bado hujalifahamu.Please listen to me and then I’ll go and leave you alone …” akasema Happy.Patrick akamtazama kwa macho makali
“Happy tafadhali ondoka.Kuzidi kukaa hapa unazidi kunichafua.Ninakuchukia kama ninavyomchikia shetani.” Akafoka Patrick.Happy akampigia magoti na kuendelea kumlilia .Patrick kwa hasira akamsukuma akangukia katika majani.
“Patrick .!!!!!!.. akaita Alois ambaye alitokea ghafla
“Unafanya nini ?? akauliza Alois kisha akamfuata Happy pale chini alipokuwa ameanguka akilia.Akamuinua.
“Inuka Happy.Pole,sana” akasema Alois.Happy akafuta machozi na kumtazama Patrick aliyekuwa amefura kwa hasira
“Patrick I’m leaving.I’m so sorry for everything and I’ll never bother you again.You’ll never see me again in your life. Good bye Patick” akasema Happy na kuondoka kwa kasi.Alois akamuangalia Patrick kwa macho makali
:Patrick umefanya nini? Nilikuwa nimesimama nimesikia matusi yote uliyomtukana Happy.kwa nini ulifanya vile?Happy hakustahili matusi kashfa na maneno yale makali” akasema Alois.Huku akihema kwa kasi Patrick akajibu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Yule Malaya hastahili hata dakaka ya kuongea na mimi.Namchukia Happy.Namchukia sana na nikimuona tena hapa nitamfanyia kitu kibaya sana” akasema Patrick.Alois akamtazama kwa makini na kusema
“Patrick umefanya kosa kubwa ambalo utajilaumu sana.ulitakiwa umsikilize alitaka kukueleza kitu gani”
“Katika siku zote za maisha yangu nitasikitika sana kumpoteza Savanna mwanamke ambaye alinipenda kwa dhati na kunijali na si huyu chui mwenye ngozi ya kondoo”
“Patrick ulitakiwa umpe nafasi Happy ya kukueleza alichotaka kukueleza.Kuna kitu ambacho bado hukifahamu” akasema Alois
“Hana jambo lolote la kunieleza kahaba Yule.” Akasema Patrick kwa ukali.Alois akaonyesha kukasirishwa na kauli ile
“Tafadhali Patrick naomba iwe mwanzo na mwisho kumuita Happy Kahaba.Show her some respect.Toka matatizo haya yametokea amekuwa nasi bega kwa bega.Hakuna siku aliyopumzika.Hakuna rafiki yako hata mmoja ambaye amethubutu kufanya kazi kubwa kama aliyoifanya Happy.Ni mtu ambaye anahitaji shukrani za pekee badala ya matusi uliyomporomoshea.Zaidi ya yote unafahamu masahibu aliyokumbana nayo?? Unafahamu ????..akauliza Alois kwa ukali
“Sifahamu !! akajibu Patrick
“Kama hufahamu kwa nini basi hukumpa nafasi ya kumsikiliza? Alois akauliza kwa ukali.Patrick hakujibu kitu
“Kama hufahamu Happy alitaka kukwambia nini,basi nisikilize kwa makini halafu wewe mwenyewe utafanya maamuzi.” Akasema Alois na kuanza kumuelezea Patrick mkasa mzima uliompata Happy.Mpaka anamaliza kumuelezea Patrick alikuwa amejiinamia asijue la kufanya
“Ouh Mungu wangu,hayo yote unayoaniambia Alois ni ya kweli?
“Huo ni ukweli halisi”
“Savanna alifahamu kila kitu kwa nini hakuniambia ukweli? Ni kweli nilimchukia sana Happy na sikutaka tena kumuona katika maisha yangu.Sikuufahamu ukweli .Ulikuwa sahihi Alois I was wrong .I made a big mistake” akasema Patrick na kuinama chini.
“Nitafanya nini sasa? Akauliza Patrick.Alois akamtazama na kusema
“Naomba uniambie ukweli wa moyo wako .Ni kweli unamchukia Happy na hutaki kumuona tena katika maisha yako? Ni kweli yale mapenzi yote uliyokuwa nayo kwake yamekwisha kabisa? Be honest with me” akasema Alois
Patrick akainama akafikiri na kusema
“Alois pamoja na mambo yote yaliyotokea lakini siku zote Happy amekuwa moyoni mwangu.Nafasi yake bado ipo katika moyo wangu.Nilidhani tayari nimekwisha msahau Happy lakini baada ya kumuona mahakamani siku alipotoa ushahidi wake ndipo nilipogundua kwamba Happy bado ana nafasi kwangu lakini kutokana na mambo aliyoyafanya sikuwa na hamu hata ya kumuona tena” akasema Patrick
“Do you still love her? Akauliza Alois
“Alois what do you expect me to say? You know the answer.I still love her” akasema Patrick
“Nimepata nafasi ya kuwa karibu na Happy na amenieleza undani wake.Bado anakupenda sana.Ninaweza kukushauri kwamba kwa kuwa hivi sasa Savanna hayupo tena na kama bado hujampa nafasi yake mtu mwingine nakushauri umfikirie Happy.Ni mwanamke ambaye unahitaji kuwa naye katika maisha yako.Mmetoka mbali na mnafahamiana vizuri.Msamehe kwa alichokifanya na mfungue ukurasa mpya wa maisha yenu.You need to be Happy .Mtu pekee ambaye anaweza akakupa furaha ya maisha baada ya Savanna ni Happy” akasema Alois
“Nakubaliana nawe Alois.Mimi na Happy kamwe hatuwezi kutengana.Kila mara kuna nguvu ambayo inatutenganisha lakini kunatokea tena nguvu nyingine ambayo inatuunganisha tena.Ukianza kufuatilia matukio yaliyotokea toka nimefahamiana na Happy utakubaliana na haya nikwambiayo.Halafu kitu kingine kinacholeta ugumu ni kwamba tayari Happy amekwisha rudiana na Mike mchumba wake wa zamani kwa hiyo uwezekano wa kumpata tena ni mdogo sana” akasema Patrick
“Patrick unatakiwa umtafute Happy na uongee naye Nina imani mtayaweka sawa mambo haya”
“Alois tafadhali naomba unisaidie niweze kuongea tena na Happy.Please help me Alois” akasema Patrick
Alois hakujibu kitu akachukua simu yake na kuzitafuta namba za simu za Happy akapiga lakini simu yake haikupatikana tena.
“Simu yake haipatikani tena” akasema alois
“Namfuata nyumbani kwao.Tafadhali naomba uambatane nami.” akasema Patrick na kwa pamoja wakaingia katika gari la Alois wakaondoka kuelekea kwa akina Happy
“Alois nitahakikisha wale wote waliomfanyia Happy kitendo hiki cha udhalilishaji wanafungwa gerezani” akasema Patrick
“Usijali kuhusu hilo Patrick.Kuna taarifa nimezipata leo kwamba Khumalo amekamatwa na polisi wa kimataifa akijaribu kuingia nchini Afrika kusini.Anarudishwa nchini kujibu tuhuma zinazomkabili.Haki itatendeka na jina la Happy litasafishwa na hesima yake itarudi” akasema Alois
Kila aliyekuwepo ndani alistushwa na hali aliyorudi nayo Happy.Japokuwa alikuwa amevaa miwani myeusi lakini michirizi ya machozi ilionekana katika mashavu yake.Mama yake ambaye alikuwa wa kwanza kumuona wakati akishuka garini akastuka na kudhani labda kuna taarifa mbaya.
“Happy kuna nini? Akauliza
Happy hakujibu kitu akatembea kwa kasi kuelekea chumbani kwake,mama yake akamfuata
“Happy mbona umetustua namna hiyo? Kuna jambo gani huko utokako? Patrick mzima?
“Patrick mzima mama” akajibu Happy huku akifuta machozi
Mama yake akavuta pumzi ndefu baada ya kusikia kwamba Patrick ni mzima
“Ouh ahsante Mungu nilifikiri kuna tatizo limetokea.Sasa kinachokuliza kitu gani?
“Mama tutaongea baadae.I need to be alone “ akasema Happy,Mama yake akamtazama na kutoka mle chumbani.
Baada ya mama yake kutoka mle chumbani Happy akafunga mlango halafu akalifungua sanduku lake akatoa bahasha iliyokuwa na picha ya Patrick.Akaitazama picha ile kwa muda huku machozi yakimtoka.
“Patrick kwa nini kila mara ninateseka kwa ajili yako? Nimejitahidi kukusahau lakini nimeshindwa.Nimeendelea kuwa mtumwa wa penzi lako.Nimejaribu kuendelea na maisha yangu bila ya wewe lakini nimeshindwa kwa sababu kila ninapojaribu kupiga hatua ,wewe hutokea mbele yangu na kunirudisha nyuma.Hii ina maanisha kwamba nitaendelea kuteseka hadi mwisho wa maisha yangu.Patrick kama ungefahamu ni namna gani ninakupenda usingethubutu kunitamkia maneno yale makali.” Akasema Happy kwa sauti ndogo huku akiitazama ile picha.Akaiweka picha ile pembeni,na kufuta machozi
“You don’t deserve a second chance.!! Tafadhali ondoka mbele ya macho yangu Malaya mkubwa wewe.!!!
Maneno haya aliyotamka Parick yakajirudia tena kichwani kwake.Akafuta machozi
“Patrick midomo yako mizuri ambayo siku zote imekuwa ikinitamkia maneno matamu na kunifanya nijione malkia katika himaya ya mfalme lakini leo hii siamini kama imetamka maneno hayo mazito. Hata kama nilikosea,hukupaswa kunitamkia maneno kama yale” akasema Happy kwa uchungu
“I saw your eyes.May be you are right that I’ve to stay away from your life.” Akaendelea kusema Happy akaishika tena picha ile ya Patrick
“Pengine hii inaweza kuwa njia bora zaidi kwa mimi kuendelea na maisha yangu nikiwa na amani bila ya wewe.You are right I don’t deserve you.Kila mara unapokuwa nami lazima ukutane na matatizo.Ni wakati sasa wa kuachana nawe Patrick.Ni wakati wa kufungua ukurasa mpya wa maisha yangu.Bado wako watu wanaonipenda na kunijali.Nilimuahidi Mike kwamba nitakaporejea Marekani tutafunga ndoa.Nadhani hili ndilo jambo la msingi kwa sasa.Nitajifunza kumpenda Mike kwa moyo wangu wote kwa sababu naye ananijali na kunithamini na zaidi ya yote ananipenda sana.I have to let you go Patrick.It hurt but I have to do it and leave you alone.” Akasema Happy huku akiichana katikati picha ile ya Patrick
Wakati Happy akiwa chumbani kwake,nje ya nyumba yao ikasikika honi ya gari.Mama yake akaenda kufungua mlango na kustuka kwa kuiona sura ya Patrick .Mara moja akajua kuna jambo limetokea.
“Patrick !!..akasema kwa mshangao
“mama shikamoo” akasema Patrick
“Marahaba Patrick.Karibuni ndani” akasema mama yake Happy na kuwakaribisha Patrick na Alois ndani
“Habari za hapa ? akauliza Patrick
“Habari za hapa nzuri.Vipi unaendeleaje?Nimestuka sana nilipokuona” akasema mama Happy ambaye bado aliendela kuwa na mstuko kwa ujio ule wa Patrick
“Namshukuru Mungu ninaendelea vizuri.” Akajibu Patrick halafu kikapita kimya kifupi
“Mama Happy tumemkuta? Akauliza Patrick
“Happy yupo.Ngoja nikamute”
Mama Happy akainuka nakuelekea chumbani kwa Happy.Aligonga mlango na Happy akaufungua.Alistuka kwa hali aliyomkuta nayo.
“Happy una tatizo gani?
“Sina tatizo lolote mama.Tatizo langu limekwisha” akajibu Happy huku akifuta machozi
“Patrick amekuja,anahitaji kukuona”
Happy akastuka na kumuangalia mama yake
“Umemwambia kwamba nipo?
“Ndiyo Happy.Nimemweleza kwamba upo ndani”
“Mama naomba mwambie kwamba sitaki kuonana naye.Sina muda wa kuonana naye na aondoke zake“
“Happy ! ! mama yake akasangaa
“Nini kimetokea? Kwa nini hutaki kuonana na Patrick leo? Mmekorofishana ?
“Mama sitaki kuonana na Patrick.Mimi na yeye basi.Nashukuru yuko mzima na anaendelea vizuri sasa.Sitaki kusikia lolote kuhusiana na Patrick.It’s over between us.” akasema Happy.Mama yake akamsogelea na kumshika mkono
“Niambie Happy nini kimetokea? Kila siku unaondoka hapa na kwenda kwa Patrick lakini leo umerudi unalia.nini kimetokea huko ?
“Usihofu mama hakuna kitu chochote kibaya kilichotokea .Nimeamua tu sitaki kuonana na Patrick tena.Mwambie aondoke haraka hapa nyumbani” akasema Happy.mama yake akarejea tena sebuleni
“Patrick nini kimetokea ? Happy aliniaga kwamba anakuja kwako leo asubuhi lakini nikashangaa anarudi akiwa analia.Kila nikimuuliza hataki kunijibu.Nini kimetokea kati yenu? Mmegombana? Nimemweleza kwamba uko hapa na unahitaji kuonana naye lakini amekataa kata kata na amesema uondoke haraka sana wewe na yeye basi.Nini kimetokea? Tafadhalio naomba uniweke wazi”
“Mama ni kweli kuna jambo limetokea kati yangu na yeye na ndiyo maana nimekuja hapa ili tuweze kuliongea na kulimaliza.Naomba unisaidie mama niweze kuonana naye”
“Nashindwa nikusaidiaje mwanangu kwa sababu Happy amekataa kabisa kuonana nawe.”
Patrick akainama na kufikiri kisha akasema
“Mama naomba unipeleke chumbani kwa Happy nikaongee naye huko huko”
“Tafadhali baba naomba usiende huko.Naogopa kusijetokea matatizo”
“Hakuna tatizo lolote linaloweza kutokea.Naomba unipeleke mama” akasisitiza Patrick.Mama yake Happy akamuongoza Patrick hadi chumbani kwa Happy na kumkuta Happy akiwa amejiinamia kitandani akilia
“Mama kwa nini umemleta huyu chumbani kwangu ??Akauliza Happy ka ukali
“Happy naomba muongee na kumaliza tofauti zenu.Patrick amekuja hapa ili muongee na msawazishe kilichotokea.Tafadhali nawaombeni msigombane.Ongeeni mambo yenu na muelewane”
“Mama naomba mtoe huyu mtu nje.Sitaki kumuona tena katika maisha yangu” akasema Happy kwa ukali
“Mama naomba utuache wenyewe” akasema Patrick na mama yake Happy akatoka mle chumbani.Patrick akafunga mlango
“Patrick go out.Get out of my room” akasema Happy kwa ukali
“Happy naomba unisikilize .Nimekuja hapa kuongea na wewe.Nimekuja kuomba samahani kwa maneno niliyoyasema.Happy naomba unisamehe kwa maneno yote niliyoyasema.” Akasema Patrick
“ Patrick sihitaji kuongea nawe kitu chochote tena.tafadhali ondoka”
“Happy naomba unielewe.Sintaondoka humu chumbani mpaka pale utakaponisikiliza ninachotaka kukwambia.Tafadhali Happy usilifanye jambo hili kuwa gumu kwangu. Tafadhali naomba unisikilize malaika wangu.” Akasema Patrick huku akipiga magoti kumsihi Happy atulize hasira na wakae waongee
Happy akastuka ghafla na kumtazama Patrick usoni.
“what you’ve just said? Am I your angel ? No you are mistaken.Mimi ni mwanamke Malaya na siwezi kuwa malaika wako.Please Patrick stand up and go and don’t dare look for me again in your life.It’s over between us.It’s been all lies.You said yourself ” akasema Happy
“Happy tafadhali naomba unisikilize.Nilitamka maneno yale machafu kutokana hasira nilizokuwa nazo.Sikuwa naufahamu ukweli halisi.Nisamehe sana Happy”
“Now do you know the truth?
“Yes ! I know the truth.Alois told me everything”
“Do you believe what he told you?
“You tell me! Is all that true? Akauliza Patrick .Happy akainama chini akafuta machozi
“Yes..thats the truth”
“Ouh Happy ! Kwa nini hukunieleza mapema? Kwa nini ukaniacha nikiteseka muda huu wote na kujenga chuki juu yako? Nilitamani hata kujitoa uhai wangu kwa kitendo kile nikiamini ulikifanya kwa makusudi.Endapo ungekimbia na kunieleza ukweli mapema wala tusingefika hapa tulipofika sasa hivi.” akasema kwa uchungu Patrick
“Nilijua Savanna atakueleza ukweli wote kwa sababu yeye alifahamu kila kitu kilichotokea na yeye ndiye aliyeratibu safari ya mimi kuondoka hapa nchini kwenda Kigali Rwanda.” Akasema Happy
“Baada ya tukio lile nilipatwa na uchungu mkubwa sana nilikata tamaa hata ya kuendelea kuishi.Nilifanya jaribio la kujitoa uhai kwa kunywa sumu lakini niliwahishwa hospitali na wakayanusuru maisha yangu.Patrick naomba uelewe kwamba haikuwa dhamira yangu kuondoka na kukuacha peke yako ukiteseka kwa kosa ambalo nililitenda mimi lakini kutokana na tukio lile nililazimika kuondoka kuikwepa aibu kubwa niliyoipata.Nilikata tama kabisa ya kuendelea na mahusino yetu na niliamua kukukabidhi kwa Savanna .Niliamini anakupenda na wewe unampenda na kwake utakuwa katika mikono salama.Siku zote nilizokaa mbali nawe niliteseka sana na sikuwa na amani hata kidogo hadi nilipokuja kukuona tena .Patrick naomba unisamehe kwa matatizo yote niliyokusabishia.Nimekuwa chanzo cha matatizo mengi katika maisha yako.Nina imani pamoja na mateso na maumivu yote niliyokuletea utatafuta ndani ya moyo wako nafasi ya kunisamehe ili niweze kuishi kwa amani.Najua siwezi kuulipa wema wako wote ulionitendea na sijui nifaye nini ili niweze kuifuta taswira hii mbaya ambayo tayari imejengeka kichwani kwako. Nilichokifanya ni kitua mbacho hakisameheki japo sikuwa na namna nyingine ya kufanya.Niliamini ninafanya vile kuokoa maisha ya mwanaume nimpendaye.Nimekuumiza sana Patrick.” Happy akashindwa kuendelea akaanza kulia.Patrick akamfuata na kumkumbatia
“Please Happy forgive me for everything.Sikuwa naufahamu ukweli.” akasema Patrick
“Patrick ni mimi ndiye unayetakiwa kunisamehe kwa kuwa nimekukosea sana na kukusababishia mateso makubwa.Patrick I deserve any punishment from you and the best punishment is to stay away from you…” akasema HappyCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/-
“Shhhhhhhhhhh..!!!! Please Happy don’t say anything.Kamwe hustahili mateso au adhabu ya aina yoyote ile ila waliokutenda kitendo kile na kukusababishia mateso makubwa namna hii lazima wapate adhabu kali sana.” Akasema Patrick huku akiendelea kumkumbatia Happy kwa nguvu
“so have you forgiven me? Akauliza Happy
“Yes ! Yes ! I’ve forgiven you.Have you forgiven me? Akauliza Patrick
“Niliumia sana kwa maneno uliyonitamkia leo.Nimelia sana lakini mwisho wa siku pamoja na machungu yote bado nimejikuta nikiendelea kuwa mtumwa kwako.Nitaendelea kuwa mtumwa kwako kwa maisha yangu yote .Patrick kamwe siwezi kuwa na hasira au kinyongo kwako.You are forgiven” akasema Happy.Wakakumbatiana kwa nguvu zaidi
“Happy pamoja na yote yaliyotokea kati yetu lakini moyo wangu unashindwa kabisa kukusahau.Hata pale nilipoamini kwamba tayari umeamua kunikimbia na nikaamua kuwa na Savanna bado niliendelea kukukumbuka.Happy tumepitia matatizo mengi na kila pale tulipotenganishwa na nguvu za dunia lakini tunajikuta tumekutanishwa tena katika mazingira ya ajabu ajabu.Happy we’re meant to be together.Nothing than death can separate us in this world.” Akasema Patrick
“Patrick do I still have a place in your heart? Akauliza Happy
“Happy bado nafasi yako ni kubwa sana katika moyo wangu.Siku zote utaendelea kuwa na nafasi ya pekee kabisa ndani ya moyo wangu.Happy nakupenda sana na nitakupenda daima” akasema Patrick
“Ouh Patrick I love you so so so much” akasema Happy na kumbusu Patrick kisha wakakumbatiana kwa nguvu.
“After today nothing will separate us again” akasema Patrck.Happy machozi yakiwatoka wote wawili
“Nini kinakuliza Happy? Akauliza Patrick
“Huwezi kujua ni jinsi gani nilivyoteseka kwa ajili yako Patrick.Siamini kama leo hii niko nawe tena. Niliamini tayari nimekwisha kupoteza na sintakuona tena maishani mwangu lakini kwa nguvu za Mungu niko nawe tena .Nakubaliana nawe kwamba hakuna kitu kinachoweza kututenganisha zaidi ya kifo katika hii dunia.Tumeumbwa ili tuwe wawili” akasema Happy.Patrick akamuangalia usoni na kusema
“Niliambiwa na Savanna kwamba ulikuwa umerudiana na Mike.Ni kweli? Akauliza Patrick.Swali lile likamstua Happy akamuachia Patrick na kutazama chini.
“Ni kweli.Nilirudiana na Mike kwa sababu alinisaidia kuingia tena Marekani Alinishawishi nirudiane naye tena na kwa kuwa sikuwa na mategemeo ya kurejea tena Tanzania nilikubali kurudiana naye.Naomba unielewe Patrick kwamba nilirudiana na Mike si kwa ajili ya mapenzi bali kwa ajili ya kutafuta msaada .I lied to him.I’ll have to say sorry.Najua ataumia sana lakini sina namna nyingine.Siwezi tena kurejea Marekani na siwezi kuendelea kuwa naye tena.Nitaongea naye na atanielewa.Hawezi kunifuata Tanzania kwa sababu amepigwa marufuku asikanyage ardhi ya Tanzania” Akasema Happy.Patrick akaonyesha wasi wasi
“Patrick naomba unielewe kwamba katika dunia hii mwanaume nimpendaye ni wewe pekee na ambaye umejaa moyoni mwangu.Tafadhali naomba unipokee tena katika moyo wako.Naomba nafasi nyingine tena” akasema Happy
Patric akamvuta Happy karibu yake akamkumbatia
“Huna haja ya kuomba nafasi ndani ya moyo wangu.Siku zote nafasi yako ipo hapa ndani ya moyo wangu.Karibu tena ndani ya moyo wangu Happy” akasema Patrick na kumpa Happy busu zito kisha wakakumbatiana kwa nguvu.Ukurasa mpya ukafunguliwa tena kati ya Patrick na Happy
* * * *
“Mimi Patrick ,katika imani,uaminifu na upendo,nakuchukua wewe Happy Kibaho kuwa mke wangu wa ndoa,kushirikiana nawe mipango ya Mungu katika maisha yetu ya pamoja tukiunganishwa katika kristu,Kwa msaada wa Mungu naomba anipe nguvu niwe kiongozi imara wa kiroho katika maisha yetu,katika raha na shida,ugonjwa na afya,furaha na huzuni,mpaka kifo kitutenganishe.Ninakupa kila nilichonacho na mapenzi yangu yote katika jina la yesu kristu.Kwa pete hii ninafunga kiapo changu cha kukupenda wewe Happy Kibaho,Mungu anisaidie kukilinda kiapo hiki,kwa jina la baba na la mwana na la roho mtakatifu Amen.”
Kanisa zima lililokuwa limefurika watu likalipuka kwa kelele za shangwe na vigele gele vingi baada ya Patrick kula kiapo chake mbele ya kanisa huku akimvisha Happy pete ya ndoa.Hii ilikuwa ni siku yao kubwa sana ambayo waliiota kwa muda mrefu.Ni siku waliyofunga pingu za maisha.Miezi mitano imekwiwha pita toka walipokutana tena.Hakukuwa tena na kikwazo chochote cha kuwazuia kufunga ndoa hivyo taratibu zikafanyika ili kuwawezesha kufunga ndoa.
Baada ya kutoka kanisani,ilifuata sherehe iliyohudhuriwa na watu wachache akiwemo Sarah dada yake Veronika pamoja na wazazi wa Savanna.Sherehe hii ilihusisha baadhi ya ndugu wa karibu na marafiki wachache tu.Baada sherehe kumalizika walipanda ndege kuelekea kisiwani Zanzibar kwa ajili ya fungate.
MIEZI 12 BAADAE
Ni saa tatu za usiku katika hospitali ya St Theresa,watoto mapacha wa kike wanazaliwa.Furaha ya Happy ilikuwa haielezeki kwa kuwapata watoto hawa mapacha.Mumewe Patrick ambaye alikuwepo pale hospitali alikuwa pia na furaha iliyopitiliza.
“Wataitwa Babrah na Brenda” akasema Patrick akitaja majina ya watoto wake
Maisha yaliendea kuwa ya furaha kubwa kwa familia hii.Mwezi wa pili baada ya kujifungua ,Mahakama ilitoa hukumu kwa wale wote waliohusika na tukio lililosabisha kifo cha Savanna.Mahakama ilimtia hatiani Loniki kwa kosa la kuua kwa kukusudia na kumhukumu adhabu ya kifungo cha maisha jela.Khumalo ambaye naye alishiriki katika mipango ya Loniki ya kumteka na kumdhallisha Happy,pamoja na kujihusisha na biashara za madawa ya kulevya,ujambazi na kutengeneza filamu za ngono alihukumiwa kifungo cha miaka hamsini gerezani na kazi ngumu.Vijana sita ambao walikuwa wakishirikiana naye walifungwa miaka thelathini kila mmoja kwa kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya.Mahakama pia ilimtia hatiani Linah kwa kujihusiha na njama za kuteka na kudhalilisha na kumhukumu miaka mitano jela.
Baada ya adhabu ile kutolewa,vilifuata vilio toka kwa ndugu na jamaa wa washtakiwa.Mzee Francis Kito na familia yake ambao walikuwepo mahakamni walipeana mikono ya pongezi na Patrick
“haki imetendeka” akasema mzee Kito huku akimkumbatia mke wake
“mahakama imetenda haki” akajibu Patrick
“Siwezi kusema kwamba nimefurahi kwa adhabu hii kwa sababu bado haiwezi kunirejeshea mwanangu Savanna.Lakini hata hivyo hizi ni sheria za nchi na lazima zifuatwe.Kwa upande wangu mimi nimekwisha wasamehe wale wote waliomuua mwanangu na sina kinyongo nao tena” akasema mzee Francis Kito.
Wakati wakiendelea kupeana pongezi kwa hukumu ile ,mara akatokea Sarah ambaye macho yake yalikuwa mekundu.Alikuwa Amelia sana.
“Pole sana Sarah.Hata mimi namuonea huruma sana Loniki lakini hakuna namna nyingine ya kufanya ili kugeuza maamuzi haya ya mahakama.” Akasema Patrick
“Hakuna lolote tunaloweza kulifanya Patrick.Mahakama imefanya kazi yake.Loniki alitenda kitendo cha kikatili sana.Nikikumbuka siku ile ninasikia uchungu mkubwa sana alitaka kutuua sote wawili.Ninaumia moyoni kumuona ndugu yangu wa damu akienda kutumikia adhabu ya kifungo cha maisha gerezani lakini kwa upande wa pili anastahili adhabu ile kutokana na mambo aliyoyafanya.Siku zote nilikuwa nikimmuonya na kumkanya kuhusu mambo ya kulipiza kisasi lakini hakunisikia.” Akasema Sarah
“Binafsi nimekwisha msamehe kwa kosa alilolitenda.Sina kinyongo naye tena cha aina yoyote” akasema Patrick
“hata mimi nimekwisha msamehe muda mrefu” akasema Sarah huku akijifuta machozi
“Patrick nimekuja kukuaga.Ninaondoka nchini”
“Unaondoka nchini? Unakwenda wapi?
“Mume wanu amehamishiwa nchini Holland kikazi kwa hiyo na mimi sina budi kumfuata.Kilichoniweka hapa hadi muda huu ni kusubiri hukumu hii .Kwa sasa baada ya hukumu kutolewa sina tena kitu cha kuendelea kusubuiri.Yanibidi niondoke nikaungane na familia yangu.Nadhani itanisaidia pia kulisahau tukio lile lililotokea.Nilinusurika kuuawa na ndugu yangu wa damu.Tukio lile limeniathiri sana kisaikolojia.Nadhani nahitaji mapumziko na kutuliza akili yangu mbali na hapa nyumbani.Tutakuwa tukiwasiliana mara kwa mara” akasema Sarah
“Nakubaliana nawe Sarah.Tukio lile ni moja ya tukio baya kabisa na unahitaji mapumziko.Nakutakia kila la heri huko uendako.Tuzidi kuombeana na kuwasiliana.Nitakuwa nikimtembelea mama mara kwa mara.Bado ni mama yangu na kwa sasa ambapo Loniki na wewe nyote hampo anahitaji mtu wa kumfariji kwa hiyo nitachukua nafasi yenu.Kwa heri Sarah” akasema Patrick akakumbatiana na Sarah wakaagana akaondoka
Hakukuwa tena na kitu chochote cha kusubiri pale mahakamani Patric na mkewe Happy wakaingia garini na kuondoka.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
MWISHO…
0 comments:
Post a Comment