Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

NDOA ILIVYOTETERESHA IMANI YANGU - 3

 





    Simulizi : Ndoa Ilivyoteteresha Imani Yangu

    Sehemu Ya Tatu (3)



    FLORA ANAANGUKA DHAMBINI.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baba aliondoka na kuniacha. Nilimaliza kazi zangu na kuanza kufunga ofisi. Nilipomaliza kufunga ofisi nilitoka nje ili kuelekea kituoni kuwahi staff bus ambalo hucbukua kwanza watu wa ofisi fulani headnoffice na kutufuata sisi wa branch office. Nilipotoka nje ilikuwa ni ajabu. Kumbe nilichelewa sana. Na sikuwahi basi. Nikiwa naangalia ustarabu mwingine mwanaume mmoja mweusi mrefu alinisalimia.Hujambo Flora?niligeuka kumtazama. Ni mwanaume nisiyemfahamu. Ila nilishangaa amenitambuaje?alisema tena wewe si mrs Deusi?niliitika ndio. Akaniambia pole umechelewa bus. Nilishukuru. Kisha aliniaga na kuniachia business card yake. Aliondoka na kwenda kupakia gari la kifahari sana. Gari jeusi. Na alipooanza kuondoka alinipungia mkono. Na aliondoka. Na mimi nilipunga pia. Nilifika ngumbani na wazo la kumsamehe mume. Alipofika mume nilikuta mtoto mgonjwa. Nilimuangalia mtoto na kumuandaa. Kisha nikamueleza mr kumpeleka mtoto hospital. Mr kama hakuona umuhimu. Aliniambia anapitia mahali hivyo dereva taxi anakuja kunipeleka. Nilimwambia Deusi ni wewe ama umelogwa?huoni mtoto mgonjwa wewebjamani?pepo gani hilo linakusumbua lakini wewe mwanaume? Hasira sijui ziliyoka wapi. Taxii aliyoita ilikuja na sikuipakia. Kisha nikaitisha taxii yangu na kuondoka. Tulipata matibabu na kurudi nyumbani. Kuwa na mawazo mengi kuninifanya nikasahau jambo muhimu sana kanisani. Nilisahau kikao cha mkutano mkuu wa uwt. Hivyo nilifuatwa asbh saa nne nikiwa nimekaa na mtoto na kuambiwa mwenyekiti unasubiriwa kikao kianze. Nilishtuka. Na kusahau kama kuna mkutano. Niliwaomba waahirishe mkutano ninauguliwa. Na hivyo tufanye kipindi kijacho. Ilikuwa ni mkutano wa wenyekiti wote wa uwt wa kanda. Na walikuwa wanatafuta mwenyekiti ama raisi wa uwt taifa. Na jina langu lilipendekezwa. Nilisahau jambo hilo. Hivyo mkutano huo mkubwa na wa heshima kwa kazi ya Mungu nikaupuuza kwa ajili ya UJINGA.



    Aliyetumwa aliondoka. Na nilijiona niko sahihi. Baada ya lisaa limoja nilipigiwa simu na kuelezwa ofcn kuna mgeni. Anaomba kuzungumza na mimi. Niliuliza ni nani?secretary alisema hamjui. Kisha niliongea naye kwa simu ya mezani ya nyumbani. Alisema anaitwa Fransis . Mh.. sikuwa namfahamu. Alijitambulisha sana. Na mwisho akasema ngoja nikurahisishie. Mimi ni likuona jana. Nimepita kukusalimia tu. Sasa nilimkumbuka. Ni mwanaume niliyemuona jana. Aliniambia nilikuona kama huna furaha nikasema nikuache ila leo nimekuja kukujulia hali. Nilimueleza ninauguliwa ma mtoto hivyo sitakuwa kazini mpaka jumatatu. Alinipa pole sana na kuniambia angependa kujua mtoto anaendeleaje na kama sitajali naweza kumpigia kwa namba zake alizonipatia kwa simu. Mh… nilishangaa kwa upendo wake. Alikata simu na niliendelea na shughuli zangu. Jioni Mume alikuja kama kawaida kinuno kiliendelea kushika hatamu. Mwanaume gani asiyejali afya ya mtoto. Nilimchukia. Na kama kawaida aliondoka na kwenda tena bar. Kiliniuma sana. Nilijilaza kitandani na mwanangu. Nikiwa naugulia kupuuzwa. Na mara msichana aliniita na kuniambia kuna simu. Niliuliza kutoka wapi akasema mjomba kapiga. Niliamka na kufuata simu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilifuata simu ambayo dada aliiweka pembeni na kuja kuniita. Nilifika na kuinua simu. Akili iliniambia ni kaka yangu kwani ndiye huwa tunamuita mjomba. Haloo?upande wa pili ukiita na sasa niliweza kujua ni sauti ambayo naweza kuikumbuka..

    Haloo. Nani mwenzangu? Niliuliza japo sauti niliihisi.

    Flora mtoto anaendeleaje? Alilitaja jina langu kwa ustadi wa hali ya juu. Nilimueleza mtoto hajambo anaendelwea vizuri.

    Aliniambia nimepewa dawa gani ?

    Nilishangaa anawezaje kujali hivyo. Milimueleza dawa nilizopewa na akaniambia ni vyema nikae na mtoto karibu na kumpatia maji mengi na matumda fresh especial machungwa.

    Kipindi hicho kulikuwa na uhaba wa machungwa.

    Nilimueleza machungwa upatikanaji wake ni mgumu sana. Kisha akaniambia…

    Please flora.. be serious. Hata kama hayapatikani tutayatafuta. Mtoto ni bora sana. Tafadhali kesho nijulishe naweA kukupataje nikupatie machungwa. Tutayapata tu hakuna tatizo.

    Nilimshukuru sana .

    Asante Flora kuzumgymza na mimi nawatakia usiku mwema wewe na wanao. Mwambie anko i love her.

    Kisha alikata simu.

    Kwa dakika kadhaa niliendelea kuishikilia simu ile. Nilimtafakari sana na kumuona ni mwanaume wa ajabu. Mwenyevupendo na kujali sana. Alizumgumza kwa upole wa hali ya juu. Kwa huruma sana. Muda huo ilikuwa jioni sana. Nilifurahia na kujikuta napata faraja ya hali ya juu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tulikula na wanangu. Kisha tukaelekea kulala. Baada ya muda nilisikia mlio wa gari nankisha likazima. Sikulisikia tena. Niliamka na kuchungulia. Alikuwa ni mume wangu. Nilimtazama akiwa analumbana na mwanamke. Kisha nilizima taa za nje na kuziwasha tena. Bado waliendelea kulumbana. Nilisikiliza sana mazungumzo yao na ilikuwa ni kulumbana kwamba kwa nini ametoka kimapenzi na rafiki yake. Nilishangaa sana. Mume wangu anapiganiwa na wanawake? Kiliniuma. Nilitoka nje ili kuona kama naota ama ni ukweli . Nilikutana na mwanamke ninayemjua kwa Jina la mwenge. Mwanamke huyu ni moja ya wanawake makubuhu mtaani. Alikuwa akimshutumu Deusi kutoka na rafiki yake ili hali ni mpenzi wake. Kiliniuma sana. Nilipotoka mwanamke huyo aliondoka na mimi nikafungua gati mr aingie. Aliingia na nilifumga geti. Sikumsemesha maana ni mwepesi wa kupiga. Nilinyamaza na nikasema nitaongea naye asbh. Tulilala kwa kiburi. Nikiwa na hasira na akiwa kalewa. Niliumia sana. Mume hajali mimi wala mtoto mgonjwa. Kiliniuma sana. Nililala kwa hasira na kuota mambo mengi. Kisha nilishtuka saa nane na sikulala tena mpaka saa kumi na mbili asbh. Niliamka na kukaaa sebuleni. Ilikuwa ni majira ya saa tati asbh. Deusi aliniambia anaenda buchani anataka kupikiwa mtori. Nilimpuuza. Kisha akaondoka. Baada ya dakima kadhaa simu iliita na niliifuata. Alikuwa ni rafiki yangu amabye alionyesha kunijali. Aliniambia kwambaachungwa anayo. Nitayapataje?nilimwambia naweza kuyafuata aseme alipo. Aliniambia alipo na haraka nilivalia track suite yangu na kufunga khanga na kuondoka. Nilifika alipo. Niliona gari yake. Kwa woga niliangalia kushoto na kuliakisha nilamsogelea na kumsalimia. Asante sana. Nilimshukuru.

    Hapana u deserve better service.. ur such a beautfull woman.. nashangaa Deusi anavyokutreet. Hajui thamani yako flora. Nilishtuka na kumuuliza unamfahamu?alisema ndio. Ninamfahamu. Naona siku hizi amakuwa kijana wa ajabu sana. Anatoka na kila mwanamke. Atakuua mamiii… take care of ur self….

    Mh… nilipata hasira na uchungu. Kisha machozi yakanitoka.

    Do not cry baby…. usilie Flora. Usilie. Nilizidi kulia na kuo a dunia inanicheka.

    Kwa upendo aliniambia hembu ingia garini. Niliingia na aliondoa gari mahali pale kisha akawasha kiyoyozi na kunipatia maji akaniambia kunywa tuliza hasira. Aliendesha gari lake mpaka mahali kwenye ngumba kunwa sana ya kifahari. Na kumuamuru mlinzi afumgue gate. Kisha tukaingia humo. Aliniambia samahani kukuleta huku. Nilihisi pale sio mahali salama. Ila sikutaka pia uende nyumbani ukilia. So please dry ur tears then get fit and i will give you a ride. Alikuwa akizunguka zunguka kwenye mjengo huo. Nilikuwa nashangaa sana mjengo huo mzuri wenye unadhifu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Zilipita dakika kadhaa kisha akaniambia naweza kukupeleka sasa. Niliogopa sana. Hofu ilinijia. Wazo la lwamba ananitaka kimapenzi nilikuwa nalo kutokana na muonekano wake. Alihisi naogopa.

    Flora usiwe na wasi wasi. Unahitaji kuoendwa. Kubembelezwa na kujaliwa. Wewe ni mwanamke mrembo sana. Usiyestahili mateso. Nilikupenda sana siku ya kwanza nilipokuona. Moyo wangu ulilipuka mamii. Isipokuwa sikulazimishi. Na sihitaji jibu la mdomoni mwako. lets our heart talk. Unaweza kukataa ila moyo ukakubali. Unaweza kukubali ila moyo ukakataa. Mapenzi ni miyoyo na nafsi mamii. Usijilazimishe. Just relax baby…

    Fransis aliongea kwa style ambayo tangu nizaliwe sijawahi kusikia maneno hayo na namna yanavyotamkwa. Moyo ulidunda mbio na sura kunibadika. Nilishindwa kuongea na kuanza kutetemeka na maneno kunitoka kwa kugugumia kama mwenye kugugumizi.

    Fransis alinitazama tena kisha akasema… Flora ur the best woman ever…. a woman of my dream…

    Kisha akanipakiza garini na kuondoka.

    Nilihofu naweza kukutana na mr. Alinihakikishia usalama wangu. Aliniambia i will never do a mistake. Namjua Deus ni jeuri. Usijali. Nitakulinda. Nilifika nyumbani na mawazo tele. Upendo wa Fransis ulikuwa wa hali ya juu. Nilimhudumia mtoto na kisha nikajibwaga kitandani kusubiri mume arejee. Mume hakurejea. Japo aliondoka na pensi na tishirt kama mwanaume ajaye nyumba i mapema. Tulimsubiri sana bila mafanikio. Jioni iliingia. Kisha nikasema sitakuwa na fadhila kama sitamshukuru Fransis kwa upendo wake kunipatia machungwa.

    Niliiendea simu na kumpigia.Ilikuwa simu ya nyumbani kwake. Hakupokea. Iliita sana. Kisha nikajisikia vibaya. Baadae kidogo nilipiga tena. Alipokea. Na aliposikia ni sauti yangu alionyesha mufurahia sana



    Ooo… is that you inocent woman?

    Yes.. nilijibu.

    Kisha nilimwambia asante sana kwa machungwa. Nashukuru mno. Yamemfaa mtoto.

    Fransis alisema do not mention… its a minor thing mamaa. U deserve the best.

    Aligugumia kidogo kisha akaniambia mamii nikuache upumzike. Lala salama. Kesho nitakuwa ofisini kwa shughuli zangu nyeti nitakucheki endapo utakuwa free. Ama ukipata nafasi nipigie saa nane mchana. Bye . Aliniaga na nikaenda kukaa kwenye kochi nikimuwaza Fransis.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku iliyofuata ilikuwa ni jumapili. Nilijiandaa kwenda kanisani. Nilikuwa mzito sana. Na mwenye hasira nyingi sana. Tuliongozana na mr. Njiani tulilumbana vibaya mno. Na kugombana haswa. Niliona ubaya wake haswaa kwa ukubwa mnoooo. Tuligombana na akasema haendi kanisani tayari ni nuksi. Na mimi nilimwambia hivyo hivyo. Kisha nikashuka garini na kurudi nyumbani. Aliondoka na hakutaka hata kukaa hata myumbani. Nilifika nyumbani na kujilaza kitandani nikilia sana. Sikutoka kabisa chumbani hadi niliposikia hodi saa tisa mchana. Walikuwa ni wanawake wa kanisani. Walikuja kunisalimia. Niliwakaribisha na tulaanza kuzungumza. Walinitia moyo na kuniambia yatapita ni mapito tu. Ma wakaniambia shauku yao ilivyo kuu na wanavyoniombea nipate mafasi ya uwenyekiti taifa. Mimi nilijaribu kuwaeleza ugumu wake na jinsi nilivyobanwa. Waliniambia kwamba nikishughulika ma mambo ya Mungu na Mungu atashughulika na mambo yangu.

    Sikuwa tena habari ya maombi. Na wala sikuwa naona umuhumu tena wa kanisa. Makwazo ya deusi ndiyo yalitawala akili yangu kisha Fransis aliiyeka akili yangu haswaaaa.



    Wakati tukiwa tunaendelea kuzungumza simu iliita. Alikuwa ni Fransis kwa uhakika. Nilipokea simu.

    Haloo Flora..

    Haloo Fransis habari?

    Nzuri sana mamii. Nimesubiri sana simu yako nini mbaya?

    Hapana nimepata ugeni tafadhali tuzungumze badae.

    Please please Florah usiache kunipigia please. Sawa mamii..

    Ndio nitafanya hivyo.

    Okay mamii. Unanivutia sana na moyo wangu unateseka sasa. One thing…. please let our heart talk..

    Bye mamii.

    Alikata simu na niliduwaa kwa dakika moja. Kisha nikarudi kuzungumza na wanawake wale.



    Waliendelea kunisihi nikubali kugombea. Ila nilikataa kata kata. Walishangaa jinsi nimebadilika. Tuliomba pamoja na waliondoka.

    Ni kama nilikuwa natamani waondoke nizungumze na Fransis. Roho ya kuchukia kazi ya Mungu iliniingia kwa kasi ya ajabu.

    Wakati nikiwa najiandaa kuongea na simu rafiki yangu aliingia kunisalimia. Ni mfanyakazi mwenzangu tuliyependana na kusaidiana sana. Alijua habari zangu. Alinihurumia sana. Na aliniambia flora wewe ni mrembo sioni kwa nini uumizwe. Aliniambia kwamba amekuwa kwenye shida ya ndoa ila kilichsaidia ni kupuuza matatizo na kusonga mbele. Alikuwa akiniamini kwa maombi sana. Na alikuwa akiniogopa. Hivyo hakuwa akinieleza upuizi wowote. Baada ya muda niliamua kumpigia simu fransis kwani niliona Beti haondoki.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Fransis aliniambia anasafiri nje ya nchi ndani ya simu tatu kufuata mzigo wake. Hivyo angetamani kuon5gea na mimi nfipo asafiri. Aliniambia angetamani kusafiri akiwa na jambo jipya maishani mwake. Nilisisimkwa mwili kwa namna alivyokuwa akiongea. Niliohopa sana kwa hofu. Kisha nilimueleza kwamba nitamjibu kesho nikifika ofcn. Tulikubaliana na kuagana. Beti alihisi jambo. Ila anijuavyo alisita kuniuliza na aliogopa kuhisi ndivyo sivyo. Tuliagana na Beti na nilienda kulala. Nilianza kusikia hali ya tofauti kidogo. Hasira zilipungua. Uchungu nao ulianza kuisha. Nilihitaji faraja. Na niliiona kwa Fransis.



    nilifarijika sana kwa kuona kwamba kuna mtu ambaye anaweza kunisikiliza na kunihurumia, nilihesabu ni heshima sana, na kuanza kuwaza endapo sitatatufa muda wa kuonana naye basi nitakuwa sina shukrani, nilimfikiri sana fransis na kuanza kuwaza ni mwanaume wa wapi mbona sijawahi kumuona siku za nyuma ni nani huyu? ni msomi , ni mtanashati, ni mwanaume ambaye anaonekana anajua upendo na upole, je ana familia? niliwaza sana na kuanza kumuona mke wake ni mwanamke ambaye ana bahati sana . nilikumbuka aliniambia utanifahamu tu flora utanifahamuu… niliyakumbuka maneno yake haya na sasa shauku ya kmfahamu zaidi niliihitaji, niliamini yeye ananifahamu sana, sikutaka kuajua kanifahamuje lakini niliamini annifhamau kwani kwa namna ambavyo alikuwa akimuelezea deusi niliona ni mwanaume anayenifahamu fika. nilihama kwa fransis na kuhamia kwa deusi,, nilikumbuka alivhyokuwa akizozana na mwenge,, mwanamke ambaye hana thamani na aliyeishusha thamani yangu kwa mume wangu vilivyo, nilijiuliza kwa nini mume angu awe na mahusiano na mwanamke yule wa ajabu kiasi kile? niliona mume kanizalilisha vya kutosha, na kuniona sifai. mume alirejea na hakukuwa na maelewano mazuri kabisa, niliumia kumuona na alivyonizalilisha, nilimtazama aliavyovalia alivyochoka asivyojipenda,, nilimuhurumia kwa siku chache tu lakini alibadilika kabisa,, kisha nikamwambia siku hizi hata huendi salon? alinitazama na kuniambia ndio siendi nenda wewe kwani si una kichwa chako.. nilicheka kwa kejeli na hapo alirusha mkono wake kutaka kupiga na niliukwepa. aliendela kunisuka suka lakini nilimkwepa kisha akanifukuza ndani na kuniambia toka nje mshenzi wewe,, niikaa nje ya geti nikitafakari, niliumia sana,ilikuwa ni majira ya saa sita usiku,, nilikumbuka kitu..

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/akili yangu moja kwa moja iliniambia muda huo huo niende kwa rafiki yake ambaye ni majiran zetu, niligonga na kuwaeleza ugomvi wote, mume na mke wa hapo nilpofikia walinihurumia sana na kwanza waliniambia nipumzike kisha wakamfuata, wote walimfuata na kwenda kwa pamoja. waligonga mlango na kumsihi afungue,, kwa aibu alifungua na walimuelez kwamba niko kwao kwa vile amenifukuza, muda huo huo mke wa rafiki alikuja kunichukua na kurudi nyumbani,, sasa walitaka kutusuluhisha na kutuuliza kulikoni,, hapo ilikuwa ni muda mzuri wa kuzngumza,, mume alielezwa asema nini tatizo,, hakuna na chakusema zaidi ya kusema huyu mwanamke anajiskia sana na kujiona mzuri , ni hivyo tu alisema, na aliouliza je hakuheshimu? alisema heshima ni ya kinafiki anajifanyamama wa kanisani lakini ni mnafiki,, aliulizwa je anakunafikia wapi hakusema lolote,, majirani walimsihi aache tabia hiyo kwani anaweza kusabbisha ndoa kutetereka na kuvunjika, alisema hana pa kwenda atakaa hapa hapa nani amtake,,, nilipoulizwa nini tatizo nilieleza kwamba amekuwa mlevei na hakuwa anaakunywa hapo awali,, pia amekuwa na mahusiano ya mapenzi na mwenge,, niliposema mwenge kila mmoja alihamaki na mumejirani alimtazama deusi na kumwambia sasa unavuka mipaka kwa nini umekuwa mzembe hivyo mpaka unamzalilisha mkeo aliongea sana kumuonya na mume alisema amekbali kuonyeska na hatarudia tena na mambo yaishe, tulishikishwa mikono nikiamini walau sasa mambo yatakuwa mazuri kidogo .baada ya majiani hakuongea lolote, kwa muda wa siku hizo chache sikuweza kumuandalia chochote kwa ujeuri wake na kunifanya niwe na mawazo na hasira, niligundua hana viatu visafi, hana nguo nzuri za kazini, ilikuwa ni majira ya saa nane na robo usiku,,, nilijahidi kuamka mapame kumuandaaa. na haraka sana saa kumi na moja na nusu nilishaamka na nakumuandalia yeye kisha nikajiandaa mimi. nilimsalimia na kumueleza akaoge,,lakini hakunijibu badala yake aliniambia usifikiri nitakupeleka kazini na gari,, utaende na dala dala.. nilishangaa na nikaona anafikiri huduma yangu inahitaji malipo,, kumbe nilikuwa nafanya kama wajibu wangu.. niliondoka na yeye aliamka na kuondoka, alinipita nimesimama kituo cha dala dala nasuiri usafiri,, machozi ya uchungu yalindondoka,, kwani mbele kidogo alipakiza watu kuwapatia lift, nilijiuliza hao watu wananielewaje na walinipita kunisalimia,, nikiwa naendelea kulia yule mwanamke aliyenishauri jana yake akiwa na mumewe alipita na garni na kuniona na kusimamisha garni kisha kunipatia lift,, nilikuwa nalia sana na kwenye gari nilimsimulia kisa kizima,, alinihurumia na kuniambia acha kujitesa mama,, raha jipe mwenyewe unalia nini sasa? leo ndo umejua anatoka na mwenge? mbona ndio story mtaani unalia nini? wewe si unaomba omba mungu kisha akacheka na kuniambia atanitafuta tuongee zaidi kwani tulikuwa tumeshafika , nilishuka na aliondoka. na kukubaliana jioni tukutane tena ajekunifuata.



    FLORA NA PENZI JIPYA.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    SIKU NZIMA SIKUWA NA RAHA OFCN. MAMA MTU MXIMA AMBAYE TUMEZOEA KUMUITA BIBI KWA UZOEFU WA UTU UZIMA ALINITAZAMA NA KUJUA NINA TATIZO. LAKINI PIA HABARI ZA MWENGE ZILISHAENEA SANA NA KUFANYA KILA MTU SASA ATAKE KUNIJUA MIMI NA KUJIULIZA HOW MUME ANATOKA NA KAHABA ILI HALI ANA MKE MREMBO KIASI KILE. NILIAMUA KUFUNGUKA KWA BIBI NA KUMUELEZA KILA KITU. NILILIA SANA. BIBI ALINIAMBIA HUNA KASORO YOYOTE ILE. WEWE NI MWANAMKE MREMBO BADO. MA HATA KAMA MUME ANAKUWA NA TABIA MBOVU MSAMEHE ANGALIA FAMILIA YAKO. NILIMUELEZA BIBI KWAMBA PIA ANANIPIGA SANA. BIBI ALINIAMBIA UMEKUWA MSICHANA MREMBO MUAMINIFU SANA MAISHA YAKO YOTE. NA UMEKUWA MKE MWEMA NA MCHA MUNGU. HIVYO SHETANI ANAKUJARIBU MWANANGU. USILIE NYAMAZA. WAKATI NAENDELEA KUONGEA NA BIBI MARA SIMU YANGU ILIITA NA NILIPOPOKEA BIBI ALINIASHIRIA NISILIE ILI NIWEZE KUONGEA NA SIMU.

    Haloo mamii?Fransis hapa.

    MOYO ULIPATA BURUDIKO LA GHAFLA. LAKINI PIA NA MACHOZI YANINICHURUZIKA NIKIJIULIZA DEUSI HAWEZI KUFANYA HIVI?

    Haloo fransis habari? Huku nikiwa napiga kwikwi za kilio.

    Flora!whats wrong?are you okay mamii?

    Yes am okay… nilijibu huku nikiwa nalia bado.

    Noooo… big noooo… okay okay…. are you safe so that i can come and see you just now?

    SIKUJALI LOLOTE LILE. HARAKA SANA NILIJIBU YES AM OKAY.

    NA AKASEMA OKAY AM COMING.

    Nilikata simu kisha nikawa naendelea kutafakari. Na ndani ya dakika 20 sijui aliwezaje kuendesha gari haraka hivyo kwani najua umbali wa ofc zake na mahali ofc zangu zipo ni kama km 30 hivi.Dakika chache alisukuma mlango wa ofc yangu na nilimuona akiingia……

    Nilishtuka na machozi yalinibubujika zaidi…

    Alisimama kidogo kisha akasema naweza kukukumbatia?

    Sikuweza kutoa jibu. Na alisema Florah relax please let our heart talk…

    Flora naomba utambue kwamba moyp huwa hauoni kwa kukosea. Hufuata hisia zake na kuangukia mahali salama. Usiruhusu akili yako ifanye kazi. Bali achia moyp wako. Mimi moyo wangu unanisukuma sana kuwa na wewe. Moyo wangu unanisumbua na kunipelekesha. Akili yangu inajua wewe ni mke wa mtu ila moyo wangu unakataa baby… please lets our heart talk.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MANENO HAYO YALISABABISHA SIJUI NINI KITOKEE NA MWENYEWE NILIJIKUTA NIMESOGEA MPAMA MAHALI ALIPO NA KUJIKUMBATISHA NA KUJOLAZA JUU YA KIFUA CHAKE… NA HUKU NIKILIA…

    noooo nooo dont cry….. usilie flora. Usilie. Moyo wako sasa utulize. Umelia sana ila sasa imetosha. Dry ur tear… just smile i want to see you happy darling… ur a woman of my life. Nakupenda. Naongeakutoka moyoni na si akilini. Akili ifanye kazi ila moyo ufanye mapenzi… aliendelea kunikumbatia kwa dakika tano kisha akanisogeza hadi kwenye kiti changu na kuniketisha na kusema baby i love you. Take care anf talk to you soon. Bye for now. ALIFUNGUA MLANGO NA KUONDOKA NA KUNIACHA KAMA NIMECHANGANYIKIWA NIKIMTAMANI AENDELEE KUONGEA.. NIKIWA NAENDELEA KUTAFAKARI NISIJUE WALA KUMUONA BIBI.. SAUTI YA BIBI ILINIAMBIA flora flora flora… NILISHTUKA NA MAWAZO YAKARUDI OFCN.

    BIBI ALINISOGELEA NA KUNITAZAMA. ALINIAMBIA FLORA MIMI NI MTU MXIMA. UNACHOTAKA KUFANYA SIO SULUHISHO LA NDOA YAKO. ILA NI TATIZO JUU YA TATIZO. KUMBUKA HUYO UNAMPENDA KWA VILE UNATATIZO ILA SI KWA VILE UNAMPENDA. LINDA HESHIMA YAKO MWANANGU. MBONA RAHISI?

    SASA AKILI IKAWA INATAKA KUJITETEA NA KUANZA KUMUELEZA BIBI KWAMBA MUME HANITENDEI HAKI. AMENIONAJE.. MBONA ANATOKA NA MWENGE NA NIMEMUACHA TU?BIBI ALIJARIBU KUNIELEZEA LAKINI NILIONA NAONEWA SANA. NA BIBI AKANIAMBIA NAONA LEO AKILI SI YAKO MWANANGU. KESHO NITAONGEA NA WEWE. KISHA AKACHEKA. NA MIMI NIKACHEKA. ALIPIGA HATUA MBILI ZA KUONDOKA NA KISHA AKARUDI NA KUMISOGELEA KABISA MEZANI AKAINAMA NA KUNIAMBIA” flora anayepelekwa na maji mengi hufa akicheka”



    SIKUWA NA HAJA YA KUTAFAKARI MAELEZO YA BIBI ILA NILICHOKUWA NAWAZA NI HUG YA FRANSIS NA MANENO YAKE YENYE NGUVU NA UPENDO NA AKILI SANA. NILIJIULIZA KWELI AKILI YANGU HAITAKI. ILA MBONA MOYO UNATAKA?KISHA NIKASEMA LETS OUR HEART TALK… NA NIKAJIKUTA NINA FURAHA YA AJABU SANA NA AMANI TELE KABISA. NA KUANZA SURA MPYA KABISA. NILIKAA NA KUENDELEA NA KAZI KISHA MAJIRA YA JIONI KABLA MKE WA JIRANI HAJANIPITIA KAMA ALIVYOSEMA NIKAAMUA KUPIGA SIMU KWA FRANSIS KUMSALIMIA NA KUMUELEZA ASANTE KWA KUJA KUNITEMBELEA. ALIPOKEA SIMU NA KUNIELWZA KIDOGO YUKO BUSY NA MAMBO YA KIOFISI ILA ANAOMBA NIMPE NUSU SAA TU KISHA ATAKUJA KABISA KUNICHUKUA TUKAZUNGUMZE KWANI ANATAMANI KUZUNGUMZA NA MIMI. NILIKUWA TAYARI NA KISHA NIKAWA NAJIANDAA KUFUNGA OFSI. HAMADI Mama kely huyu hapa. Mke wa jirani.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alinitazama na nikaachia tabasamu la haja. Aliniambia ooo.. afadhali unacheka jirani yangu. Ama umepiga sala? Niliendelea kutabasamu. Aliniambia kama niko tayari nimwambie na tuondoke. Nilishindwa kumwambia nina ugeni. Na hivho nikamwambia kuna shuhguli naisubiri kuifanya toka kwa boss hivyo aondoke kwani boss anaweza niletea shida na tutaonana nyumbani nikifima namfuata. aliridhika na kuondoka. wakati anashuka ngazi mara fransis naye alikuwa akiingia na kupishana na mama kely na mama kelly aligeuka kumtazama. bila shaka alivutiwa naye. na mara niliingia ofcn kwangu na fransis alinifuata na kunikumbatia kwa uhuru sana. na kusema anasikia connection ya ajabu ambayo hajawahi kuisikia kabla. binafsi na mimi nilijikuta niki feel the same. aliniambia flora i love you thats all. i cant explain. ila i love you. and is not from my brain. this is from my heart. akaniambia flora anayekupenda hajali. ila ukimpenda mtu kwa akili huwa akili ikichoka unamchukia na kumsahau. lakini moyo huwa hauchoki na hausahau. ukichoka ni siku ya kufa tu. na ndio maana ndoa nyingi zinachokana kwa sababu ya kupe dana kiakili akili.. lakini mkipendana kimoyoni haina kuchoka mpaka kifo.. nisamehe kama hukuliona hili mpenzi. ila i love you mama. wewe ni mwanamke wa maisha yangu. nilikuwa nasubiri kwa hamu kumpenda mtu na sasa nimeingia mahali sahihi. sijutii kukupenda hata kama ni mke wa mtu. ikinipasa kufa acha nife ila this is love… the love i feel baby.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog