Simulizi : Ndoa Ilivyoteteresha Imani Yangu
Sehemu Ya Nne (4)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Flora kuna kitu nataka ukione kuhusu mapenzi. Mapenzi yanajitosheleza. Mapenzi hayahitaji umbo wala sura wala rangi.. mapenzi hayahitaji pesa wala mali.Mapenzi yanahitaji mapenzi basi. Mapenzi yanahitaji kufurahia basi. NA FURAHA HIYO NDO KAMA MIMI NINAVYOJISIKIA. NIMEJISIKIA FURAHA SANA. NA NDIO MANA UNAONA WEWE NI MKE WA MTU NA SIJALI. NIMEACHA WASICHANA WENGI ILA NIMEONA PENZI LA KWELI KWAKO.. NA LINANIFURAHISHA. HAIJALISHI UKOJE ILA NASIKIA FAHARI SANA KUKUKUMBATIA. SITAKI KUKUFORCE. NATAKA UWE NA UHURU. KAMA NIKIKULAZIMISHA UTANITESA NA SITAFUEAHIA PENZI. LAKINI KAMA UTAACHIA MOYO WAKO UENDESHE MAPENZI BASI WOTE TUTAFURAHIA NA NINATAKA ULE USEMI WA SIWEZI KUISHI BILA MPENZI WANGU UFANYE KAZI KWAKO. KWANGU UNAFANYA KAZI NDO MAANA NASUMBUKA KAMA HIVI. NATAKA MOYO WAKO UENDESHE MAPENZI NA SIO AKILI. AKILI KAZI YAKE NI KUFAN YA KAZI KUSOMA NA KUTAFUTA MAISHA. MOYO KAZI YAKE NI KUPENDA TU BASI. HIVYO MAMII UWE HURU. NATAMANI SANA KUKUELEZA MIMI NI NANI LAKINI LEO SIO MAHALI PAKE. WEWE NI MALKIA.. WEWE NI LULU MAMA. SIJUI KAMA UNALIJUA HILO…. NIKUACHE UTAFSKARI KWA MOYO HAYA. KISHA SIKULAZIMISHI.. SITAKULAUMU WALA KUKUCHUKIA. NATAKA KESHO MAJIRA YA SAA SITA MCHANA WAKATI WA LUNCH TIME UNIPE JIBU MOJA TU. AIZA KUNIAMBIA MOYO WAKO UMELUBALI AMA AKILI YAKO IMEKATAA MAMII… OKAY?ALIMALIZA KUONGEA KISHA AKANIKISS KWENYE PAJI LA USO NA KUSEMA ONCE AGAIN SORRY SIO MIMI NI MOYO WANGU. ALINIAGA NA KUONDOKA.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
TANGU NIMEZALIWA NIMETOKA KENYE TUMBO LA MAMA YANGU SKUWAHI KUONA MTU MWENYE UPENDO WA NAMNA HIII, MWENYE UPEO KUHUSU MAPENZ KAMA HUYU NILIANZA KUFIKIRI AKILI NA MOYO,,, NILIJIPA KAZI MWENYEWE NA MITIHANI YA HARAKA HARAK,, NIKASEMA LAKINI KWELIEEE, AKILI IKICHOKA HUWA HUTAKI KABISA KUFIKIRI MAMBO YA MAPENZI, INAWEZEKANA TUNAJILAZIMISHA KUPENDA PASIPOPENDWA,,, NILIANZA KUJIULIZA MIAKA YOTE FRANSIS ALIKUWA WAPI ASINITAFUTE NA KUNIAMBIA MANENO HAYA,, NIKAJIULIZA NA KUJIJIBU ,,,,,,,,,, KISHA NIKSAME MWANAUME KAMA HUYU HAJAOA MPAKA LEO YAMKINI HE IS SMART NA NDIO MAANA HAJAOA KWANI ANATAKA KUJITENDEA HAKI,,, NIKASEMA HUYU ANAJUE MAANA YA MAPENZI,, NILIWAZA SANA KWA MUDA MREFU,, NILIANGALIA SAA YANGU YA MKONONI MUNGU WANGU,, NI SAA MBILI KASORO ROBO USIKU,, MAMA YANGU,, NILISHTUKA SANA,, NILITOKA NJE NA KUMKUTA MLINZI ANANISUBIRI AFUNGE GETI,, NILIMSALIMIA NA KUSEMA MAMA LEO VIPI SIO KAWAIDA YAKO,,, AKILI YANGU ILIWAZA NYUMBANI TU NA KUOMBA MUNGU NJIA NZIMA NISIMKUTE MUME WANGU NYUMBANI MAANA NDO NINGESHAAA, NILICHUKUA TAXI NA KUMWAMBIA DEREVA KIMBIZAGRI HARAKA NIPELEKE HOME,, DEREVA ALIFANYA HIVYO NA ALINIAMBIA USIJALI MR NIMEMUONA PALE MALAIKA PUP ANGONGA VITU..WALA USIJALI,, NILIMUULIZA KWELI? ALISEMA KWELI,, KISHA NIKAFARIJIKA,, NILIFIKA NYUMBANI NA KUINGIA NDANI NA KUKETI, NA KUANZA KUTAFAKARI KWANZA KWA UPYA.. NINI NINATAKA KUFANYA,, JE NIMJIBU MOYO UMEKUBALI AMA NIMJIBU AKILI IMEKATAAA? SIKUWA NA LA KUWAZA,, NILIHISI NI HABATI NIKAKUMBUKA ALISEMA HATA KUFA ATAKUFA KWA AJILI YANGU,, NIKAJIULIZA NAACHIAJE BAHATI KAMA HIII…. NIKAWAZA SANA NA KUOGOPA KUMKOSA FRANSIS… NILIJIULIZA MASWALI MENGI,, JIBU NILILOPAA NI WKAMBA MOYO HUPENDA MAHALI SAHIHI ILA AKILI HAIJUI KUPENDA,, LAKINI KWA NGUVU GU YA AJABU NIKASKIA AKILI IKINIAMBIA NDOA NA IHESHIMIWE NA WATU WOTE. NILIENDEA KUOGA NIKIWA NA JIBU TAYARI,, NA SASA NILIKUWA NASUBIRI KESHO YAKE SAA SITA IFIKE NIKATOE JIBU HILO.. AMBALO NILIJUA LITANISAIDIA MAISHANI MWANMWOTE. NA NIDINGEJUTIA JBU LANGU KWANI ALISHANIAMBAI HATANILAUMU KWA JIBU LOLOTE LILE.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
SIKUWA NA MUDA WA KUIKUMBUKA IMANI YANGU HATA KIDOGO, SIKUWEZA KUKUMBUKA CHOCHOTE NA HATA SIKUWA NATAKA KUKUMBUKA CHOCHOTE, NI KAMA NILIONA MUNGU HAWEZI KUNISAIDIA MUEA OTE NIMEKWUA MUAMINIFU MBONA ASINITENDEE MUUJIZA KWA MUME WANGU, KWA NINI,,,, USINGIZI ULIKUWA MTAMU SANA, MUME ALIRUDIA KAMA KAWAIDA MIDA YAKE, NILIMFUNGULIA NA ALIINGIA, HAA ALIPOTKA KUANZISHA UGOMVI SUTAKA KUMSIKILIZA, ALILALA NA ASBH NILIAMKA NA KUMUANDALIA CHAI NA NGUO ZA KUVAA KISHA NIKAMUAGA NA KUONDOKA,, WAKATI NATOKA MAMA KELLY ALINIPIGIS HONI NA KUNIAMBIA UKO TAYARI TWENDE,, NDI NIKO TAYRI,, NDIVYO NILIMJIBU.
88888888
Mama Kelly hakuwahi luwa rafiki yangu kabisa
Na sikiwahi kizoeana naye hata kidogo. Ila kwa nafasi ya jana yake na kisa nilichomueleza sasa aliniambia kwamba atakiwa akunipatoa lift kwenye gari yake kunipeleka ofcn nisijali. Alionekana mkarimu sana kwangu. TULIPAKIA GARI NA KUELEKEA OFCN. MAMA KELLY NI MWANAMKE AMBAYE HUPENDA KUVALIA NGUO ZA KUJOFUNIMA NA KUJITANDA SANA. NI MWANAMKE ALIYEKULIA PWANI YA MOMBASA. ALIJOPE DA SANA. NA ALIOLEWA NA MWANAUME WA KIKRISTO JAPO YEYE ALIKUWA MUISLAMU. ALIJIPENDA SANA NA WENGI WALIKUWA WAKIMUITA MPEMBA. HILO NDILO JINA LAKE MTAANI. LAKINI PIA ALIKUWA HODARI WA KUPIKA VITAFUNWA MTAANI NA ALIKUWA AKIJULIKANA KWA SIFA HIYO. LAFUDHI YAKE YA KIMOMBASA MOMBASA ILIKUWA HAIWEZI KUFUTIKA KABISA. NILIPOKETI GARINI TU ALINOAMBIA HAYA BIBI JINIGE MKANDA HUO. NILIACHIA TABASAMU KWA NENO JINIGE… KISHA AKACHEKA NA YEYE NA KUNIPIGA KOFI PAJANI HUKU AKONIAMBIA FLORA WEWE NI KIBOKO… AKAACHIA CHEKO HA HA HA AAAAA….. NILIJIA FIKA KINACHOMCHEKESHA ILA NIKAJOFANYA SIJUI CHOCHOTE. alinoambia haya ULE MTAMBO WA JANA WAKO A?NOLIENDELEA KUJIKAUSHA KISHA AKASEMA…
Nilitaka kushangaa uzuri wako wote unataka umwagikie chini…. huyo mumeo anajifanya kidume cha mtaa sasa na wewe shurutii uwe mtetea…. taga hata mayai ya khanga haaaa… kwani nini bwana?! Aliongea kwa lafuzi ya limombasa muda wote. Sikumjibu neno ila kucheka tu kwa namna aongeavyo. Alishuka akanifungulia mlango kisha akanikumbatia na kuniambia wewe ni Bonge la demu. Badae nataka hiyo agenda yako tukalie mahali tuijadili. Nilishuka na kuingia ofcn.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
8888888888888888
NILIINGIA OFCN. SIKU ILIKUWA YA TOFAUTI NA SIKU ZINGINE ZOTE. NAFSI YANGU ILIANZA TAKASIKA NA KUWA NA FURAHA KIASI. JAPO SI SANA LAKINI KWA KIASI. NILIFANYA KAZI ZANGU HUKU NIKISUBIRI SAA SITA IFILE NIZUNGUMZE NA FRANSIS. MUDA ULIENDELEA NA GHAFLA SAA SITA ILIWADIA. MOYO WANGU ULIANZA KUDUNDA KWA KASI NA MASHAVU YALIANZA KUPATA MOTO WA AJABU KWA HOFU YA KUTOA JIBU. NILITAZAMA SAA YANGU YA MKONONI ILIIAMBIA NI SAA SITA NA DAKIKA TATU. NILIISOGELEA SIMU YANGU YA MEZANI NA KUAMZA KUPIGA NAMBA YA FRANSIS. KISHA ILIITA MARA MBILI KISHA SAUTI YA FRANSIS ILIITIKA.. HALOOO FLORA..
HALOO FRANSIS.
KISHA ALIKAA KIMYA KWA SEKUMDE KADHAA NISIWEZE KUSEMA LOLOTE HUKU NAOGOPA SANA.
flora nakusikiliza. Sauti ya upole ya kiume ilizungumza. Frank aliongea kwa upole wa hali ya juu sana.
Nilivuta pumnzi nzito kisha nikasema Moyo wangu umekubali…
Aliniambia please rudia tena….
Nilisema moyo wangu umekubali…
Kisha akasema fine fine fine babe.. lets our heart talk… Aliniambia nitakuka kukuchukua kwa lunch time nahitaji nusu saa tu na wewe. Only 30 minutes mamiii.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alikata simu na kuniambia ni get ready. Niliendelea kufikiri uzuri na ukarimu wa fransis nisijue anataka kunifanya nini kwa hizo 30 mnts. Lakini kwa vile nolishajitolea basi sikuwa na mashaka niliamimi pendo lake la dhati kwangu na kutaka kuona mapenzi ni nini. Kwani niliamini nimefika ikulu ya mapenzi.
Muda uliwadia na alipogia simu na kuniambia nimduate chini yuko na gari nyekundu. Nilitoka na kukuta gari nyekundu nzuri ya kifahari. Nilipofika alinifumgulia mlango kwa kujivuta kisha akaniambia karibu mpenzi wangu. Nilikuwa ni a wasi wasi sana. Ndani ya gari nilipofika tu alinikaribisha ice cream. Aliola kisha akaniambia karibu mama.. feel at home… jisikie… nitume mapenzi nitakupatia…. kisha aliweka mziki na maneno niliyoyasikia kwenye mziki huo ni i will love you always…. na yeye alikuwa akiimba huku akiendesha gari. Na kisha alipiga honi na mlinzi alifungua geti na tukaingia ndani kisha geti likafungwa. Moja kwa moja alinipeleka sebuleni kwake akiwa kanishika kwa mikono yake na akisema ur mine am urs…. alinimetisha juu ya kochi huku akisema NAOGOPA… SIAMINI UMENIKUBALI FLORA… SIAMINI MAMA… NATETEMEKA SIJUI NIKWAMBIE NINI…alirudi na glass ameishikilia mkono wa kushoto na chupa ya champagne kaishikilia mkono wa kulia. Aliifungua na kumimina nusu kwenye glass kisha akaninywesha na kuniambia Nakuoenda sana mpenzi… lrts enjoy u.our love…. Alichukua mkono wangu wa kulia na kuzitazama pete zangu mbili… kisha alitoa pete kwenye kikasha na kusema nakuvalisha pete hii flora no mata what… ukitaka itupe ama vyovyote ila i love you mamiii. Alichukua kifole changu cha kati na kutumbukiza pete nzuri sana iliyokuwa inang’aa sana… Kisha alichukua mkono wangu na kubusu kidole cha pete ile na akanikumbatia na kisha akaanza kulia akisema i do not belive…Siamini umenithamini kiasi hiki…Nitakupenda.. nitakulinda… ilibifi kufa kwa ajili yako nitakufa.. kama kukupenda wewe ni dhambi acha nihukumiwe… i love you…. na mimk machozi yalinidondoka… sikujua ni ya huzuni wala furaha…
Kisha alinitazama na kuniambia Tunaweza ku kiss….Haimgekuwa rahisi kukataa… nisingeweza kwani tayari ufahamu ulitekwa na fransis.
Baada ya kukiss aliangalia saa yake ya mkononi na kuniambia ni saa nane na robo mamii naomba nikurudishe kazini.NAKUHITAJI SANA ILA NAOMBA NIKURUDOSHE KAZINI KISHA NITAKUAMBIA CHA KUFANYA…. tuliondoka na kurudi ofcn. Aliniacha nje na yeye akaondoka. Nilibaki namuwaza na kulia sana. Nililia kwa muda mrefu sana kisha nilinyamaza na kuendelea na kazi . Nilijiuliza kwa nini mwanaume mtanashati… mwenye mapenzi ya kweli hajaoa hadi sasa?nilijiuliza sana. Jibu nilipata kwamba hataki kupenda kwa akili ila kwa moyo.
88888888888
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alinieleza ndani ya siku mbili atasafiri safari ya wiki mbili. Na hivyo alitamani siku moja walau tukae pamoja kwa masaa hata mawili. Alikuwa kama sijui kanifanya nini. Hakuna nililoweza kubisha. Kila alichosema niliitika kama kondooo… Sawa.. ndio… haya… aliniburuza sana. Nilimpigia simu mama kelly na alifika kwa safari ya kurudi nyumbani.Ila aliniambia tupite mahali tukae tuzungumze. Haikuwa tabia tangu kukaa mahali mara baaada ya kutoka kazini. Ila sasa nilianza kuwa na safari za kutoka na kukaa bar. Na sikujali kabisa. Kipindi cha nyuma nilitoka ili niweze kwenda kanisani tena kwa speed ya ajabu. Ila sasa nakubali kabisa kukaa bar wala sijali. Mama kely aliitisha sod na mimi nikaotisha juice. Kisha soga zikanza. Nilishakuwa nimechetuliwa na fransis. Hivyo sikuona tatizo kumuelezea mama kelly juu ya fransis.
Mama kely nimepata rafikk ila simfahamu vizuri nataka uniambie je unamfaham Feansis?
Hapana simfahamu. Ila kumfahamu nipe tu siku mbili nakujia na jibu murua. Kwani jamaa ndo anakamua mashine?
Mama lkelly aliniuliza.. nilitabasamu na kumwambia huenda akakamua ila bado sijamjua vizuri..
Mama kelly aliachia cheko lake la kimombasa…. hahaha haaaaa… haloooo oo ya makamuzi… kisha akanipiga kibao mgongoni na kuamza kuzungumza.
Flora sikia. Yule jamaa lazima kadata
Sasa wewe zubaa ile kwako… hizi ndo bahati. Au wewe huoni?hapo kaacha wasichana kakufuata wewe… usimzubaishe.. mlobeshe fasta fasta kiutu uzima unichukulie change pale. Mtu mwenyewe matawi yule.. manake nimesikia ck…. anapumua ck..
Mama kelly alio gea kiswahili cha kihuni sana hata sikumuelewa…
Ck ndo nini?nilimuuliza…
Alicheka te a na akaniambia ck ni Celvin Klein… chata ya pesa ni perfum mama kwani pua zako hazinusi?kama anaweza kutumia perfum ya ghali vile si haba ni matawi.
Mh.. nilishangaa kidogo.
Mama kelly aliendelea kunipo geza. Kisha akaniambia sasa flora haya masketi yako na mavitenge yako sasa ndo uyaache. Anza kutoka ki ck. Wewe si unamuona kijana anavyowaka…. mpe mapigo ya ukweli. Mavitenge yako ngoja ukialikwa kwenye mikutano ya chama na serikali nfo uyavae. Niliendelea kumsikiliza mama kelly akiongea nisiweze kumjibu. Tulimaliza kunywa soda kisha nikamwambia Fransis anataka nikutane naye. Ila sijui naanzaje,,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mama kelly alimitazama na kusema unaanzaje aje?kwani mumeo huyo useme unakesha naye?sema unaumwa nenda hospital kisha unaenda kwa ck… ama hiyo imekaaje?
Nilitabasamu kisha nikaku aliaana na ushauri wa mama kelly. Na nikamwambia basi nitafanya hivyo. Akaniambia alafu nakuona jina la fransis linakukaa sana. Hembu mpe nick name isije kukuletea balaa mara ukamwita deus fransis. Nilicheka sana na nikajua kweli nilko na mtaalamu. Na kisha nikamwambia basi haina shida. Nitamuita ck. Tulicheka na kuondoka. Aliniacha nashuka kisha akaondoka.
88888888
Shetani alikuwa amejipanga bara bara. Kila kona nilikutana na jeshi lale limejipanga vyema. Na sikuweza kufurukuta. Nilikaa muda kidogo kisha mama mchungaji na mchungaji walikuja kunitembelea na kutaka kujua kulikoni sipatikani? NILIANZA KUJITETEA OO KAZI.. MAMBO MENGI KIOFISI NIMESHIKIKA SANA NA KUOANDISHWA CHEO MAJUKUMJ YAMEONHEZEKA. TAYARI NILIWEZA KUTUNGA UONGO MKUBWA NA WALIAMINI KABISA. WALINISIHI SANA HATA MARA MOJA KWA WIKK NIWE NAO . LAKINK NIKIWAHAMIMISHIA SIWEZI KUHUDHURIA KABISA KUTOKANA NA UBUSY
8888888888
Mama Kelly alitokea kunipenda gjafla. Alikuwa akowasiliana na mimk kila dakika kwa simu ya mezani na kuniita mama ck. Wakati huo hakikuwa na simu za mikononi na kama zilikuwepo basi ni kama walikuwepo wachache sana. Simu iliita na nilijua ni ck… ilienda kupokea kisha nikasiki…
Aa mama ck… sema.
Mh… niliguna kisha nikamwambia sina usemi.
Akaniambia.Sikia flora naomba anza sasa kujifunza kuvaa sio hayo masuti yako kama bibi kilimo…. nilicheka kwanza kwani alinichekesha kwa namna alovyoitamka. Nilishindwa kumuelewa kwa nini hataki nivae vile ili hali yeye anavalia vyema katila miondoko ya kipwani pwani. Aliniambia atanifumdisha kuvaa na aliniambia anakuja mara moja. Alikuja aliniambia naweza kuvalia sketi fulani yangu aijuayo na blauzi fulani. Nguo hizo sikuzipenda kutokana na kunibana sana . Ila yeye alisema hizi sasa ndo nguo za ki ck.. usiniangushe. Kesho va hizi. Anza kuumwa na sema utaenda hosptal na kazini omba ruhusa kisha take ur time ma ck.. sawa mama?
Mh… sawa. Niliitika na kisha akaondoka. Usiku ulikuwa mrefu. Nilitamani pakuche. Asbh mr nilimueleza naumwa na aliniambia pole kisha nikavaa na kuondoka. Mama kely aliponiona alisema saaafiiii … maneno hayo mwana…. alinisifia kupendwza sana. Aliniambia umbo lako hizi ndo nguo zako. Akanipa namba ya mdada mmoja miuza nguo na kumwambia huyi mpige pamba kama imelda… kisha akasema ataniletea nguo na tulakubaliana. Niliomba ruhusa kazini kwamba ni mgonjwa na kuondoka. Moja kwa moja nilielekea ofcn kwa ck na nilipofika nilizuiwa kwanza na kuambiwa mpaka apewe taarifa. Masecretary walikuwa wakibishana wakisema alisema leo hataki usumbufu na hana apoint ment yoyote. Niliwaambia wamwambie ni Flora na walisema hapana hatuwezi. Niliwaomba kuongea na simu na walisema hawafanyi hivyo. Niliwauliza huqa anatoka break kwa chai?walisema hapana. Lakini hutoka kufanya zoezi la kupanda nankushuka ngazi kila saa nne na mchana. Hivyo kaa hapo umsubiri akitoka akikuona atakutambua. Nilikaa pembeni nikiwa nasubiri Mr Ck atoke anione huo muda. Nikiwa nimekaa alipita binti na moja kwa moja aliruhusiwa kuingia kwa ck… nilijiuliza sana kulikoni?nilitamani kujua kwa nini huyo ameruhusiwa hata bila kuulizwa?moja kwa moja akili ikaniambia no mpenzi wake.. moyo ukaanza kuniuma… mh…. na baada ya dakika kama 30 hivi alitoka na kuondoka. Nilijiskia vibaya sana na kuamua kuondoka. Nilianza kuondoka na wale wadada waliniona na kuniambia madam anatoka usiondoke. Nilirejea na kweli nilimuona ck akitoka. Akiwa kavalia shati jeupe sana la mikono mirefu na kukunja mikono hiyo.. kisha suruali ya cadet iliyomkaa vyema… na akaniona ma kuniita Flora?is that you?
Nilimwambia ndio. Kisha mikawa kama namawazo na aliwaambia wale mabinti… huyu ni mwanamke wa muhimu sana. Tafadhali naomba sana akija ruksa kuingia hata kama sipo ofcn kwani ataanza kutumia ofc yangu nikiwa sipo. Nilianza kugarijika na kuona kama mpaka naruhusiwa kutumia ofc ya mtu who am i? Nilijipandisha chati. Akiwa kanikumbatia kabisa asijali lolote alinichukua mpaka ofcn kwake. Niliketi na aliniambia enhe..
Nilimueleza nimepata nafasi na hivyo naweza kuwa naye kwa muda aliouhitaji kwani nimeaga kwenda hospital. Alinifurahia sana kisha akasema anamaliza jambo tuondoke. Alinouliza ningependa kula nini ama kunywa nini nikiwa nawaza alisema ngojaa.. alichukua simu na kupiga na kusema naomba mixed juice mbili… ndani ya dakika 5 zilikuja juice mbili na akanikabidhi na yeye akainywa yakweke mara moja vaap… kisha akaendelea na kazi zake..
888888888
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alimaliza kufanya kazi zake na tukaondoka. Kama kawaida kwenye gari lake la kifahari. Huko aliniwekea nyimbo za kimapenzi zenye kunienzi. Alinipeleka mpaka nyumbani kwake kama kawaida. Nyumba yake kubwa… ya kifahari na safi sana. Alikuwa ni mwanaume anayejipenda sana. Aliniambia kuwa huru mamii…. akanichukua na kuanza kunitembeza.. alinionyesha chumba chake cha kulala na kusema this is our Bed room.. kisha akanitembeza vyumba vingine na kunionyesha jiko na stoo na kunionyesha libray yake na chumba cha kufanya mazoezi. Aliniambia anaipenda nyumba yake na ndiye rafiki yake… na aliniambia huwa hapendi kujidhalilisha na nyumba yake mimi ndiye mwanamke wa kwanza kuingia mume kama mpenzi. Ila ndugu tu ndo huingia humo.
Aliniambia anatamani kila chakula nitakachopima na aliniambia niseme nataka kupika nini akachukue. Nilimueleza aseme yeye mimi nitampikia. Alisema anatamani kula ugali na samaki . Nilimwambia sawa naweza kuandaa. Aliambia anakuka na kunionyesha jiko na kila kitu. Mh.. Sikuamini kwa namna alivyomithamini. Aliniambia flora nataka mimi na wewe tufurahie mapenzi yetu. Sioni sababu ya kutumia hotel kwani tutafaidiaha wengi. Ila hapa kwangu ni salama na pazuri. Tutapatumia hapa hapa mpenzi. Aliondoka kisha akarudi akiwa kanunua vitu vingi… Alinipatia khanga na kuniambia natamani uvalie khanga tu. Nilicheka na alisema wewe ni mke wangu mpenzi. Sikujali nilivalia kumfurahisha. Kisha nimaendelea kupika huku akiwa anatengeneza juice. Alinivutia sana. Nilijisikia niko peponi.
888888
OFCN WANAJUA NAUMWA. MR ANAJUA NAUMWA. ILA NIKO KWA CK. NINAJISIKIA FURAHA YA AJABU. NAJISIKIA NIKO PEPONI. NILIKUWA NAPIKA KWA UMAKINI WA HALI YA JUU. CK AKIENDELEA KUTENGENEZA JUICE KWA USTADI PIA. NILIKUWA NIKIMFUATILIA KWA UMAKINI WA HALI YA JUU. ALIMALIZA KISHA AKAENDA KUVALIA KAPTULA PANA NA KURIDI KIFUA WAZI. ALIWEKA MZIKI NYORORO. SIKUWAHI KUWA MJUZI WA MIZIKI KWANI NYIMBO ZANGU ZILIKUWA NI ZA ULYANKULU NA NYIMBO ZA KWAYA ZA AINA ZOTE. KWAYZ ZINGEIMBA NINGEWEZA KUKUAMBIA NI KWAYA GANI AMA MUIMBAJI GANI. NYIMBO ZA TENZI ZA ROHONI NILIZIJUA ZOTE LICHA YA MWIMBIENI BWANA. SASA NASIKIA NYIMBO LAINI NA ZENYE KUASHIRIA MAPENZI AMA KUMSIFU MPENZI. NILIELEWA KILA NENO LA NYIMBO HIZO LAKINI UNGENIAMBIA NI NANI KAIMBA AMA KWA HAKIMA SINGEKUWA NA JIBU. SEBULE YAKE NZURI SANA YENYE UTANASHATI WA HALI YA JUU. ALIANZA KUPANGA MEZA NA AKANIULIZA NAHITAJI NINI MEZANI. NILIMUEMEZA APANGE NIONE KAMA ANAJUA. ALICHEKA AKANIPIGA KIBAO CHA MAKALIO YANGU NA KIYAFINYA KWA VIDOLE VYAKE VYOTE VITANO KAMA ANAYESONDILIA KITU. KISHA ALINIBUSU KWENYE PAJI LA USO NA KUSEMA Am lucky so lucky… akamalizia kwa kunipiga kibao cha shavu na akaendelea na kupanga MEZA.
8888888888
YEYETO ANGEINGIA MULE NDANI NA KUTUONA ANGEWEZA KUJUA KWAMBA MIMK NA CK NI MKE NA MUME. TENA KWA NDOA CHANGA SANA. NILIANZA KUWAZA VIBAYA. NILIANZA KUMTAMANI CK AWE MUME WANGU. ALIJUA THAMANI YA MWANAMKE. ALIJUA MWANAMKE ANAHITAJI NINI. NI MUDA WA WIKI MBILI TU TANGU NIMFAHAMU LAKINI NAANZA KUOGOPA KUMKOSA. AMA KWELI MOYO KAZI YAKE KUPENDA NA AKILI KAZI YAKE KUSOMA NA KUFANYA KAZI. CK ALIUJAA MOYO WANGU. NILIJISIKIA RAHA YA AJABU
SIJUI NI USHAMBA AMA UGENI WA MAPENZI AMA NINI. LAKINK NILIJIONA MWENYE BAHATI KUBWA SANA. CHAKULA KILIKUWA TAYARI MEZANI. ALIPANGA MEZA KAMA HOTELINI. CK NI MSTARABH
.. MTANASHATI NA MWENYE KUJUA MAMBO MENGI. KWA NYUMBA YA MWANAUME ASIYE NA MKE KUWA NA VITU KAMA VILE NI LAZIMA NI MWANAUME MTANASHATI NA MWENYE KUJUA VITU. ALIVUTA KITI NA KUNUAMBIA KETI HAPA. KISHA NA YEYE AKAKETI TUKIWA TUNATAZAMANA. LOO… MACHO YAKE YALINITAZAMA SANA DIRECT KWENYE MACHO YANGU NA AKASEMA HUU NDIO MLO WA THAMANI KULIKO MILO NILIYOWAHI KUILA SIKU ZILIZOPITA. ALINIAMBIA WEWE NDIYE UMEFANYA MLO HUU UWE WA PEKEE. KUPIKIWA NA MWANAMKE NIMPENDAYE NI LAZIMA NIWE NA AFYA. ALINIANGALIA TENA NA KUSEMA…FLORA YOU KNOW WHAT? NITAFANIKIWA SANA. AKILI YANGU IMETULIA SANA. KUWA NA WEWE NI MWANZO WA MAFANIKIO YANGU SASA. NILIJIULIZA MAFANIKIO GANI ANAUOTAKA ZAIDI YA ALIYONAYO ILA NIKAJIZUIA KUULIZA.. KISHA AKASEMA NAHISI UNATAKA KUSEMA NENO.. HEMBU SEMA MAMA.. WAKATI HUO AKINICHAMBULIA SAMAKI NA KUNIWEKEA KWENYE SAHANI YANGU…. DAH… AMA KWELI CK NI MOTO WA KUOTEA MBALI.
8888888888888
TULIMALIZA KULA KISHA AKANIAMBIA NI NGEPENDA TUKAE WAPI ILI TUWEZE KUZUNGUMZA…. NILIMWAMBIA TUNGEKAA TU SEBULENI. ALINIAMBIA NYUMA KUNA SEHEMU KUBWA YENYE BWAWA LA KUOGELEA NA BUSTANI YA MAUA… KISHA AKANIULIZA UNAJUA KUOGELEA?.. HARAKA NILIMWAMBIA SIJUI… KISHA AKANIAMBIA GOOD. NITAKUWA MWALIMU WAKO. . NILIMWAMBIA NINGEPENDA KUONA BUSTANI HIYO. ALINIVHUKUA NA KWENDA KUNIONYESHA.. DAH.. AMA KWELI BONGE LA BUSTANJ NA BWAWA ZURI LA KUOGELEA. NILIPAPENDA KWA KWELI. NI PAZURI. NILIMWAMBIA NAHITAJI KUKAA BUSTANINI. ALIINGIA NDANI NA KUJA NA CHUPA AMBAYO SIKUJUA IMEBEBA POMBE GANI. ILA HAIKUWA JUICE WALA SODA WALA BIA.. ALISOGEZA CHUPA KARIBU NA NILIMWAMBIA SITUMII KILEVI.. HAKUSHANGAA SANA ALISEMA HAINA SHAKA MAMII AKANILETEA JUICE ILE ALIYOTENGENEZA YEYE. KISHA AKANIAMBIA NA MIMI SITAKUMYWA POMBE TENA KUANZIA LEO NIMEACHA RASMI. KAMA UTAKUNYWA NITAKUMYWA. KAMA HUTAKUMYWA SITAKUNYWA. KINACHOKUPA FIRAHA NITAKIFANYA. KINACHOKUKOSESHA FURAHA NITAKIACHA.. FLORA I LOVE YOU. TULIENDELEA KUMYWA JUICE HUKU AKINIELEZEA MAISHA YAKE.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
888888
NIMEZALIWA KWENYE FAMILIA YA WATOTO WAWILI TU. MIMI NA DADA YANGU. DADA YANGU ALIOLEWA NA MWARABU NA KUHAMIA UARABUNI MIAKA MINGI SANA. ALINICHUKUA MIMI NA MAMA NA TUKAISHI UARABUNI PIA. HUKO NILISOMA NA KUPATA ELIMU NZURI SANA YA BIASHARA. KISHA NILIFANYA KAZI KAMA MTUMWA NIKIWEKEZA ILI NIKIRUDI NYUMBANI NIWE NA KITU. MAMA YANGU UARABUNI ALIKUWA YAYA WA WATOTO WA KIARABU KWENYE FAMILIA MOJA MAARUFU SANA UARABUNI. ALIPENDWA MNO NA MZEE WA HIYO FAMILIA. HIVYO ALIKUWA AKIMPATIA PESA NYINGI SANA NA NILISOMA KWA PESA HIZO ZA MAMA. BAADA YA KUMALIZA KUSOMA MAMA ALINIAMBIA NIRUDI NYUMBANI KUTAFUTA SHAMBA . NILIFANIKIWA KUPATA SHAMBA HILI LA HEKA TATU. NA NIKALINUNUA KWA BEI RAHISI SANA MIAKA HIYO. KISHA NILIRUDI TENA UARABUNI AMBAKO NILIPATA KAZI KATIKA SHIRIKA LA NDEGE. SASA NILIWEZA KUSAFIRI NCHI MBALJ MBALI NA KUINGIZA PESA NA KUCHUNGUZA BIASHARA ZA KUFANYA. KWA VILE NILIKUWA NA UCHUNGU WA MAISHA SIKUCHEZEA PESA HATA KIDOGO ISIPOKUWA NI KUZIFANYIA VITU VYA MAANA. NILIONA KAZI KWENYE SHIRIKA LA NDEGE ZINANIBANA NA NIKAACHA NA KUANZA KUUZA SPEAR ZA MAGARI KUTOKA DUBAI KUJA TANZANIA. NILIKUWA NAWAPA WENYE MADUKA MIZIGO YANGU WANIUZIE NA WAO WACHUKUE PERCENT KIDOGO. NA WALIKUWA WAAMINIFU SANA. NILIFANIKIWA MNO NA KWA UBAHILI WANGU NILIWEZA KUJENGA HUU MJENGO UNAOUONA. NA KUWEKA KILA KITU. LAKINI HATA HIVYO BIASHARA ILIKUWA NZURI NA NIKAONA SINA SABABU YA KUISHI TANZANIA ILA NIENDELEE KUISHI UARABUNI KWA BIASHARA ZAIDI. HUKO NILIKAA SANA. NA NIKAWA NA MAHUSIANO NA MSICHANA WA KIARABU AMBAYE TULIPENDANA LAKINI SIO KWA MOYO ILA NI AKILI ILINISUKUMA NIMPENDE. NA BAADAE NILIKUWA SINA FURAHA NAYE NA NIKAAVHANA NAYE NA KURUDI TANZANIA KWANI KUKAA KULE NILIONA ANANISUMBUA SANA NA KUNIKERA. NILIRUDI TANZANIA MIAKA 3 ILIYOPITA. LAKINI KWA BAHATI MBAYA MAMA YANGU ALIFARIKI DUNIA NA TUMEMZIMA HUKU SHAMBANI.. KULEEEEE.. ALINJONYESHA KWA MKONO KUELEKEZA MAHALI AMEMZIKA MAMA YAKE. BAADA YA MAMA KUFARIKI NILIJIHISI MPWEKE NA HIVYO SASA NILIHITAJI MPENZI NA BADO SIKUPATA MOYO ULIPOPENDA. NILIPENDANA NA ZULEA LAKINI BADO ILIKUWA KIAKILI. HAKUNISIKILIZA WALA KUNIHESHIMU. NA NIKAAMUA KUACHANA NAYE NA AKAOLEWA. MILIMPENDA KWA DHATI SANA LAKINI PENDO LANGU ALILIDHARAU MNO NA KUNIONA MJINGA HATA KUTONISIKILIZA. NILIMNUNULIA GARI ZURI LA KIFAHARI NA ALIAMUA KULIUZA KITU KILICHONISIKITISHA SANA AKISEMA HAWEZI KUTUMIA GARI ILI HALI HANA BIASHARA. HIVYO ALIUZA GARI NA KUSEMA KAMA NILIMPA ZAWADI BASI ANA UHURU WA KUFANYA CHOCHOTE NA ZAWAFI YAKE. NA ALIZIDI KUNIMERA NIKAACHANA NAYE. NA NDIPO SIKU MOJA NILIKUONA UKIWA UMETOKA SOKONI KARIBU NA SALON MOJA YA KIUME NINYOAPO NA KWA NAMNA YA PEKEE SANA NILIVUTIWA NA WEWE NA KUANZA KUKUFUATILIA KWA UKARIBU SANA. ULIKUWA UMEVALIA KHANGA TU LAKINI NILIKUPENDA MNO. NA KUANZA LUKUFUATILIA. NILIJUA ULIPOINGIA… NIKAJUA UFANYIAPO KAZI. NILIUMIA NILIPOGUNDUA UMEOLEWA. ILA NILIPATA FARAJA NILIPOGUNDUA MUMEO NI LAZIMA MLIPENDANA KWA AKILI KWANI HANGEWEZA KUKUACHA HOME NA YEYE KUTOKA NA WANAWAKE KAMA MWENGE. NAMJUA SANA MUMEO. NISAMEHE ILA HAKUPENDI. NI AKILI ILIMSUKUMA AKUOE. ILA SIO MOYO. NILIANZA KUKUWAZIA KWA UMAKINI SANA NA NDIPO NIKAJITOSA KUJA KWAKO. THANKS GOD ULIACHIA MOYO WAKO UKAFANYA MAAAMUZI NA SIO AKILI.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
FLORA NAKUPENDA NA NIMEAMINI UNANIPENDA. NAOMBA ANGALIA SAA YAKO YA MKONONI….. NILIANGALIA SAA YANGU ILIKUWA NI SAA KUMI NA MOJA NA ROBO JIONI. ALINITAZAMA MA KUNIAMBIA UNANIPENDA?NILIMJIBU NDIO NAKUPENDA SANA. KISHA AKANIAMBIA NAOMBA UNIAMBIE UNATAKA NINI KWANGU…. HARAKA SANA NILIMWAMBIA NATAKA UNIPENDE TU BASI. ALINIAMBIA HILO UMEPATA. SEMA UNATAKA NIKUFANYIE NINI ZAIDI YA MAPENZI YANGU. SEMA MAMIII…. ALINIACHA NIKIWA NIMEKAA NA AKANYANYUKA… NIKIWA NAENDELEA KUTAFAKARI NIOMBE NINI HUKU NAKIULIZA NIOMBE GARI? NIOMBE SHAMBA AMA NIOMBE NINI?KABLA SIJAPATA JIBU ALIKUJA NA FUNGUO AMESHIKILIALANGONI. KISHA AKAITA HARUNA KAFUNGUE KULE GARAGE…. HARUNA ALIKUJA NA KUCHUKUA ZILE FUNGUO NA KUONDOKA. KISHA ALINICHUKUA NA KUNIAMBIA TWENDE HUKU. NILIANZA KUTEMBEA NAYE KUELEKEA ALIPOKUWA ANAELEKEA HARUNA. KISHA ALIFUNGUA GETI KUBWA NA NDANI KULIKUWA NA MAGARI ZAIDI YA NANE YAMEFUNIKWA. ALINIAMBIA NI GARI GANI UNAPENDA?ENZI HIZO GARI ZILIZOKUWA KWENYE CHART NI BALOON. NILIMJIBU NAPENDA BALÒON. KISHA ALIENDA MOJA KWA MOJA NA KUFUNUA GARI AINA YA BALOO YENYE RANGI YA SILVER METALIC…. GARI MPYA YENYE CHASIS NUMBER. AKANIAMBIA HIZI NI ZILIZOBAKI KWENYE SYOCK YANGU. ILA NAKUPA HII KWA VILE UMEIPENDA. LAKINI NITAKULETEA GARI YA CHOICE YANGU INAYOKUFANANIA KAMA MPENZI WA FRANSIS…. SAWA MAMIII… ALIMUAGIZA HARUNA ATOE ILE GARI.. NI KAMA NILIKUWA SIAMINK KINACHOENDELEA. NILIHISI NIKO NDOTONI.. SIJAWAHI KUHO GWA KITU CHA THAMANI KIRAHISI HIVYO. UWIII NILISHANGAA SANA. GARI YA MILIONI KAMA 6 HIVI MIAKA HIYO NI KAMA MAMILIONI SASA. TENA ISI GEKUWA MPYA VILE. TULIRUDI MPAKA NDANI NA AKANIAMBIA NIJIANDAE NA TUONDOKE NIWAHI NYUMBANI KISHA GARI NIKITAKA KUONDOKA NAYO FINE. NIKIAMUA KUPELEKEWA FINE. NILICHAMGANYIKIWA. NILITAMANI MUDA USISOGEE. KWA MARA YA MWWNZA KUTAMANI LISAA LIMOJA IWE NI DAKIKA MOJA.
888888888888
DEUSI ALISHAKUWA AMEZOELEA POMBE NA KUTONIJALI WALA KUJALI WANAWE. NILIRUDI NYUMBANI NA HAKUWEPO. NILIMPIGIA SIMU CK NA KUELEZA NIMEFIKA SALAMA NA SIJAMKUTA MR. HIVYO ANAWEZA KUNITUMIA GARI YANGU. LAKINI AMPE DILLER WAKE ANILETEE NA NDIYE ATAKAYESHUGHULIKIA MAMBO YA KUSAJILI GARI NA KILA KITU. ALINIAMBIA MAMA TEMBELEA CHASIS NUMBER HATA MWEZI. WEKA HESHIMA MJINI. UKISIMAMISHWA SEMA NI MIMI NIMEKUUZIA. MIMI NDIO BABA YAO MATRAFICK HAPA MJINI USIOGOPE LOLOTE. IN 1 HOUR GARI ITAKUWA GETINI NA FULL TANK DARLING. THE CAR IS URS SAWA MAMA?HUU NI MWANZO TU. UTASHANGAA. NAKUPENDA KWA KUMAANISHA. SITAKI UUMIE ILA NATAKA HATA KAMA NI KUFA UFE NA TASWIRA YANGU. AMA NIKIFA UBAKI NA LENGO LA MAISHA. ALIKATA SIMU NA ALINIAGA NA KUNITAKIA USIKU MWEMA.
888888
MUME ALIRUDI NA ALISHANGAA KUONA GARI. ALITAZAMA NA KUPUUZA. ALIKUWA KALEWA. ALIINGIA NA KUSEMA UMEAMUA KUNUNUA ILI USIWE OMBA OMBA EEE… GOOD. ALINIAMBIA HIVYO KWANI SIKU ZA NYUMA NILIMWAMBIA SITAKI KUOMBA OMBA NITANUNUA GARI YANGU. HAKUNIULIZA NAENDELWAJE WALA NINI. ALIINGIA NDANI NA KUOGA NA KULALA. KWA MARA YA KWANZA KUWAHI KURUDI TANGU TUMEKOROFISHANA. ASBH MAMA KELY ALINIPIGIA HONI. NILITOKA NA KUMWAMBIA NIMEPEWA GARI NA CK… NOOO NOOO FLORA NOOO
MAMA KELLY ALISHANGAA.
Alishuka garini na kushangaa ile gari haswaa. Mnoo. Alinionea wivu haswa. Akasema haya mama all the best. Ila natamani kuiendesha. Aliniambia anarudisha kupark yake kisba tutumie ile kwa kwenda kazini. Kwa vile alishakuwa rafiki nilimruhusu. Na alifanys hivyo. Alirudi na alinie desha mpama ofcn kwake kisha akaniacha nikaenda ofcn. Na kuniomba jioni nimpitie.
Ofcn kwa ck alisema nina uhuru wa kuruhusiwa kuingia wakati wowote. Hali kazalika nyumbani kwake niliambiwa wakati wowote.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilijiona malkia.
Cha kwanza kufanya ni kumpigia simu ck na kumshukuru sana. Aliniambia nisijali na nitakuwa nashukuru kila siku. Alisema hivi..
“Flora mpenzi wangu.. kama hujui kushukuru sasa ndo ujifunze.. maana utashukuru sana mpama ukose cha kusema. Huwa nakuambia sina maneno ya kukuambia nakupenda zaidi ya i love you. So na weee utanielewa kwa mimi kukupatia zawadi. Nataka uishiwe na maneno mamiii.
NILIMSHUKURU SANA KWA UKARIMU WAKE. ALINIELEZA ANAJIANDAA LUJIFUNGASHA NA ANAENDA BANK KUTRANSFEW PESA HIVYO ATARUDI HOME NA KUJIANDAA KUFLY USIKU HUO SAA TANO . ALINIAGA NA KUNITAKIA KUBAKI SALAMA. KISHA NA MIMI NIKAMTAKIA SAFARI NJEMA. NILIENDELEA NA KAZI KISHA NILATOKA LISAA LIMOJA KABLA YA KAZI NA KUELEKEA OFCN KWA MAMA KELY ILI KUONDOKA. ALIPONIONA ALIFURAHIA SANA NA ALIJJFUNGASHA NA TUKAONDOKA. NILIMSIMULIA KILA KIYU SIKUACHA HATA KIMOJA. MAMA KELY ALINIAMBIA HIYO NFO BAHATI SASA. NISHINDWE MWENYEWE. NILIMUELEZEA CK ANASAFIRI USIKU HUO. ALINIAMBIA FANYA JUU CHINI UKAMUAGE. USIACHE KABISA. FANYA JUU CHINI NA MAUA UMPELEKEE NA KADI YA KUSEMA UTAM MISS. NA MA LOVE KIBAO. NILIONA NI WAZO ZURI. TULIPITIA DUKANI TUKANUNUA MAUA KISHA KADI NA HAOOOO NIKAMUOMBA MAMA KELY ANISINDIKIZE KWA CK. KWA VILE NILIKUWA NA UHURU WA KUINGIA NILIAMUA KWENDA NA TULIFUMGULIWA GETI NA NILIINGIA. CK ALIKUWA HAJAKUJA BADO. MAMA KELY ALINIAMBIA SASA NDO UPIKE CHAI YA ILIKI NA PILI PILI MANGA KWA MBALI AKIJA MKARIBISHE NAYO BIBI WEWE.. SI NI MUMEO?TENA NDO UMSHIKE MKONO HADI CHUMBANI UKAMPATIE HUKO HUKO NA POLE KIBAO.. UNAFANYA MCHEZO EEE.. AMA BALOON NI MENO MWENZANGU USEME UKISHAFIKISHA EIGHTEE JINO LA 32 LAZIMA LIOTE?AKA… UKISHIKWA BIBI WEWE SHIKAMANA.
Niliona mama kely kanishauri la maana. Haraka nilifanya kama alivyoniagiza hakukuwa na karafuu ila tangawizi tu na tea masala. Niliingia jikoni na kuanza kupika
Wee flora wee?mama kely aliita..
Niliitika abeee..
Na sio uivhemshe hiyo chai kama dawa ya kutoa mimba eee mwana.. majani weka mwishoni ukiwa unaitia kwenye flask upo mama?
Nikacheka na kumwambia nipo.
Chai ilikuwa tayari na baada ya dakika kadhaa ck aliwsili. Ilikuwa ni bonge la suprise kwake. Nilimpokea hakuamini. Alinikumbatia na kunibus. Kisha nikampeleka chumbani na kumwambia apumzike nakuja. Nilichukua chai na kikombe na kumpelekea. Kisha nikaakaa naye akanywa kikombe kizima na kufurahia sana. Nilimtambulisha kwa mama kely na kumwambia ni best friend wangu
Walisalimiana na baada ya muda tuliondoka. Sikumpa maua wala ile kadi. Ila niliiweka kwenye libray yake nikijua nitakapofika nyumbani nitampigia simu aende library akaa ngalie kuna nini.
88888
NILIIITA FARAJA NA FURAHA. CK ALINIWEKA KWENYE SEHEMU NYIMGINE KABISA. MUME NILIANZA KUMZOEA. ILA SIO KWA KITOKERWA NA MAMBO YAKE. LA HASHA NI KWA VILE NILIKUWA NA FARAJA MAHALI. BAADA YA SIKU TATI ALIKUMA KIJANA ANAITWA MWARABU NA KUMIPATIA KADI YA GARI.. PLATE NUMBER.. NA KILA KILICBOHITAJIKA KWA AJILI YA GARI. NA CHA KUFURAHISHA ZAIDI KADI ILIANDIKWA JINA LANGU. WHAT A SUPRISE! MAISHA YALIENDELEA HUKU NIKIMKUMBUKA SANA CK. NA YEYE HALI KAZALIKA. ALINITUMIA PICHA KWA EMAIL NA KILA ALICHOFANYA. MILIMPENDA SANA KWA KWELI. NILISIKIA FURAHA SANA KUWA NA CK. A GREAT MAN. A MAN WITH TRUE ANA HEART LOVE.. HIVI NDIVYO NILIMUITA.MUDA ULIPITA SANA NA WIKI TATU ZIIISHA NA CK ALIREJEA NCHINI. NOLIJUA MITALETEWA MIZAWADI KEDE KEDE KUTOKA A NA SHAUKU YAKE NA MIMI. NILIANZA KUVAA KI CHEKI SISTER KWA AJILI YA CK. MAMA KELY ALINIVISHA. MAMBO YAKAWA SAWA KABISA. NA NILIFURAHIA SANA KWA MAVAZI HAYO. KILA ALIYENIONA ALINISIFIA SANA NA HATA BAADHI YA WANAUME SASA WALIANZA KUMITANIA NA KUNITONGOZA. NILIJUA NAOENDEZA SANA. KUMBE NILUSHAACHA KUMTUMIKIA MUNGU NA WAZINZI WAKAPATA NAFASI YA KUNITONGOZA. KITU AMBACHO HAPO MWANZO HAKUNA ALIYENIONA NA KUWAHI KUNITANIA. LICHA YA KUKAA KARIBU NA MIMI.
88888
MAPENZI YALIPAMBA MOTO. ILIKUWA SASA INAHITAJIKA USIKU MZIMA KATI YANGU MIMI NA CK. HAIKUWA TENA NI KUKUTANA LISAA WALA MASAA. SASA ALINISIHI ANAHITAJI USIKU MZIMA. NILISEMA LIWALO NA LIWE. NITAPAMBANA KUFA KUPONA KWA GHARAMA ZOZOTE ZILE. NILITAMANI SANA NIPATE NAFASI HII. NIYAIPATAJE?NINA MSHAURI. NILIMTAFUTA MAMA KELLY NA KUMUELEZA. ALINIAMBIA NI RAHISI SANA MWANA. ACHA UJINGA NA USHAMBA. AGA UMEPATA DHARURA… KAMA VIPI SEMA NIKUSINDIKIZE. ILA MCHONGO NAUTENGENEZA MIMI
MUME WANGU HANA NENO. UTANISINDIKIZA MAHALI. WEWE SEME UNANISINFIKIZA MIMI BASI. NILIONA NI KAZI NGUMU. ILA NILIMUAHIDI MAMA KELY NIKIFANIKIWA TU BASI. ALINIAMBIA LAZIMA UFANIKIWE. KWANI WEWE HUNA PETE YA NYOTA?MBONA KAMA UNAONEKANA MJANJA?MH PETE YA NYOTA NDO NINI NILIMUULIZA..
hujui?pete ya kukusafishia nyota. Kuna mzee hapa alimaarufu kwa shughuli hizo. Mambo yako yatakunyookea utashangaa. Na ninakubakikishia hata mumeo hatafurukuta.
Alinieleza mama kelly. Na alisisitiza sana na kuniambia yeye anaishi atakavyo. Kisha akaniambia sema unataka ck adate ama mumeo?chagua moja.
Mh.. nilikuwa kwenye wakati mgumu sana. Nisingeelewa kwa haraka. Kisha sijui ni woga ama ni nini nikamwambia nataka kuwa na nyota.
Aliniambia atanipeleka mahali kabla ya kuomba ruhusa.
Na baada ya siku mbili yulienda nje ya mji kwa mzee huyo ambaye alinituma pete na kuifanyia mambo zake. Kisha akaniambia naivaa tu siku ambayo ninataka kufanya mambo yangu. Ila siku sitaki kufanya napaswa kuiweke kwenye pochi.
Sikuona ni ajabu ila niliku aliaana na jambo hilo na nikarudi mjini. Baada ya siku tatu niliomba ruhusa ya kumsindimiza mama kely na haikuwa na maulizo mengi nikakubaliwa.
Ilikuwa furaha ya ajabu.
Nilimoatia ck taarifa na akakubaliana na mimi.
Siku ya kutoka nilojiandaa mapema sana. Kisha nikamueleza mama kely. Na yeye akanisindikiza kwa ck.
Tulifika mida ya asbh sana na mama kely aliniambia anatoka na atarudi usiku kwa kulala na kesho tuondoke. Sikujua anaenda wapi.
Aliondoka na kubaki na ck.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Tulikula yilikunywa.. niligunfishwa kuogelea na baada ya muda tulirudi ndani na kulala kama mtu na mkewe. Midaa ya saa nne mama kely alirejea na alipewa chumba chake akalala. Ulikuwa usiku wa kukumbukwa. Asbh akili yangu iliniambia nitapata zawadi nyingi sana. Na kweli ndivyo ilivyokuwa. Nilipewa begi zima la mazaga zaga. Nguo viatu.. perfum nk. Nilifurahia sana. Kisha tuliondoka na mama kely aliondoka na begi kwani nilihofia mume kuona vitu vya thamani ingenigharimu.
888888
TAYARI NIMEZINI…. TAYARI NIMEENDA KWA MGANGA… YATARI NASEMA UONGO WA HAJA… TAYARI KANISA NIMELIACHA. SASA NAVAA NGUO AMBAZO ZA KISHENZI SHENZI TU MARA MAPAJA WAZI MARA MATITI WAZI… NA NINANIFUNZA KUNYWA WINE NA SPRITE….. nimekuwa mbaya kuliko mwanzo. Lakini haya yote siyaoni. MIMI NA CK. CK NA MIMI. KILA WIKI TUNAKUTANA MARA MBILI MPAKA TATU. TUNAFURAHIANA. UZINZI UMENIKEA NAFANYA KAMA KUBUHU. KWA AKILI YA HALI YA JUU. MUME SIMJALI WALA KUMHURUMIA. WATU WA KANISANI WANANISHANGAA NA KUUMIA SANA. WAMEOMBA BILA SHAKA MPAKA BASI. MAMA YANGU MZAZI ALINIONA NIKIWA NIMEVALIA SKETI FUPI SABA NA BLAUZI OLIYOACHA KIFUA . ALIELEZWA HABARI ZANGU SIKU ZA NYUMA KWAMBA NIMEKUWA NA TABIA YA KUVALIA UCHI. HAKUAMINI. NA SASA ANATAKA KUNIONA KWA MACHO. ALIFANIKIWA KUNIONA LIVE. NIKIWA NAENDESHA GARI NA KISKETI KIFUPI SANA HAKUAMINI WAKATI NATEREMKA GARINI. flora ni wewe mwanangu ama nakufananisha?
NILIKUWA NIMENENEPA SANA NA KUNAWIRI HASWAA KUTOKANA NA CARE ZA CK. MAPAJA YALIKUWA MANONO NA MAKALIO YAKAWA MAKUBWA SANA. HIVYO NGUO NIKIVALIA HUPANDISHWA JUU NA MAKALIO PIA.
Nilijitetea niko kwenye gari.. nikajitetea nikifika ofcn sitoki…
Nilijitetea kwa kila hali lakini mama hakunielewa. Alinionya sana na kisha akaondoka nikimuahidi kubafilika. Aliia sana.
888888
NILIANZA KUTOKA NA KINA BITE MAMA KELY NA SARA MFANYAKAZI MWENZANGU. NA KWENDA KWENYE HOTELI ZA GHARAMA. HUKO NILIKUNYWA POMBE KWA SIRI MTU ASIJUE. ILA NILIYEKUWA NAO KWA WAKATI HUO. CK ALIKUJA NA KUKAA MA SISI KWA MUDA KISBA ALIONDOKA NA KUTUACHA. WANAUME WALIANZA KUTUTAMANI NA KUTUTONGOZA SANA. NILIOGOPA KUWA KARIBU NA MWANAUME. SI KWA VILE YA DEUS MUME WANGU LA HASHA. ILA KWA SABABU YA CK. BITE NA SARA NA MAMA KELY TULISHIBANA. ALIYEKUWA NA OESA ANGEMUITA MWENZAKE NA TUNGEENDA KWA NYAMA CHOMA NA SODA KILA TULIPOPENDA MARA BAADA YA KUTOKA KAZINI. PENZI LANGU NA CK LIKAWA TAMU NA LA MVUTO. KIASI HATA SARA BITE AMBAO NI SK GLE LADY WALIKUWA WAKINITAMANI. MUDA ULIENDA NA NILIJIHISI NI MJAMZITO. NILIENDA KUPIMA NA MUJIKUTA NI MJAMZITO. NILIANZA KUJIULIZA NIFANYEJE. NILIPATA AKILI NA KUSEMA HAPA NI LAZIMA NIZAE NIMZALIE CK. KAMA KAWAIDA NILIMUELEZA ALWATANI MAMA KELY NIKAMUELEZA KUHUSU UJAUZITO. ALINIELEZA NI LAZIMA NITOE HIYO MIMBA. MH… SIJAWAHI. ALINIAMBIA TENA HARAKA.
NILIAMUA KUFANYA HIVYO . NILIOGOPA SANA MWANZONI LAKINI NILIJIKAZA.
NILILAZWA NA NILIMUELEZA CK NAUMWA TU NA TUMBO LA UTU UXIMA NA AKAELEWA. NILIHOFU KUMUELEZA UKWELI. ALINIHUDUMIA MWANZO MWISHO. NILIRUHUSIWA NA NILIRUDI MYUMBANI.
888888
NI MIEZI TISA SASA IMEISHA TANGU NIMFSHAMU CK. SIKU YA SIKU KUU YAKE YA KUZALIWA NILIJIPANGA KUMFANYIA SUPRISE. NILIANDAA KEKI YA NGUVU. KISHA NIKAANDA CHAMPAGNE NA KUMNUNULIA SURUALI NA SHATI KAMA APENDAVYO KUVALIA. NILIANDAA KILA KITU NA KWENDA PALE KWAKE JIONI NIKAWA NAMSUBIRI. NILIWEKA ZAWADI ZAKE VYEMA KWA AJILI YA SUPRISE. KEKI.. KADI NA NGUO HIZO. KISHA NIKAENDELEA KUMSUBIRI.SAA MOJA IKAPITA.. SAA MBILI KISHA SAA TATU USIKU BADO HAJAKUJA. NIKAMUWAZIA SANA ATAKUWA WAPI?HIVYO NIKAONA NITACHELEWA NA KUAMUA KUONDOKA. LAKINI ASBH SANA NILISEMA NITARUDI ILI KUMSUPRISE..NILIJIANDAA KWA AJILI YA KWENDA KAZINI. NA SIKUELEKEA KAZINI MOJA KWA MONA ILA NIKAAMUA SASA KWENDA KWA CK. NILIFIKA NI MAJIRA YA SAA KUMI NA MBILI ASBH. NILIMKUTA HARUNA GETINI NA ALINIAMBIA CK HAYUPO. NILIONA GARI NDANI ASIJUE NIMEONA GARI. KISHA NIKAMWAMBI okay basi acha niingie. ali ikataza pia. Nilimgombeza sana tena kwa nguvu mno. Lakini bado alinikataza. NILIMWAMBIA NITAINGIA LAZIMA. KWA VILE NILIKUWA NATUMIA KELELE NYINGI NI KAMA NILIWASUMBUA WALIOKUWA NDANI HIVYO MLINZI ALINIAMBIA NI BORA NIEMDE NIRUDI BADAE. NILIUMIA SANA MOYO WANGU. NA AKILI IKAVURUGIKA SASA NIKAAMUA KWENDA OFCN KWAKE. NILIFIKA OFCN KWAKE NIKAINGIA KWANI NILIRUBUSIWA. NA NILIPIGA SIMU YA CK YA NYUMBANJ HAIKUPOLELEWA. LAKINI NIKAAMUA KUMPIGIA MSHAURI WANGU ANIPE USHAURI.
MARA GHAFLA NAMPIGIA MAMA KELY NAAMBIWA HAJAFIKA KAZINI. NIKAPUUZA NA KUAMUA KUELEKEA KAZINI KWANGU. NIKIWA OFCN KWANGU SARA ALINIFUATA NA KUNIAMBIA DA FLORA MIMI KUNA KITU KINANIUMA NATAKA KUKUAMBIA.
NILIMWAMBIA NI NINI?
ALINIAMBIA NI SIRI ILA UWE MSIRI. NILIMSILILIZA KWA MAKINI. KISHA AKANIAMBIA NAOMBA UVUMILIE NIKIKUAMBIA.
Je no siri gani sarah atamwambia Florah???
Tukijaliwa kesho tutaijua.
Muwe na usiku mwema.
88888CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
SARA ALIONEKANA ANASHAUKU YA KUNIELEZA NA ALIKUWA KAMA ANAONEKANA KUSIKITKA SANA,, NILIMWAMBIA ANIACHE NIFANYE JAMBO FULANI KAZINI KISHA TUTAZUNGUMZA, NILIKUWA NIKIKUWAZA CK KWA NIN HAPATIKANI, KWA NINI GARI LIKO NDANI NA HAYUPO NI MOJA YA SIKU AMBAZO PIA AKILI YANGU ILIKUWA INAVURUGIKIWA,, NIKIWA NIMESHAMALIZA KUFANYA KAZI YANGU, NILIMIUTA SARA NA TULITOKA NA KWENDA KUSIMAMA KWENYE VERANDA YA OFC, HUKO TULIONGEA SANA NA MAONGEZI YETU YALKUWA HIVI…
Yani da Flora kuna kitu kinaniuma sana. Na sipendi namna ambayo Bite anafanya. Amekuwa akitoka na mumeo kitu ambacho sikifurahii kabisa na ni ukweli haswa. Na ninalila kitu cha kukuhakikishia.
Moyo ulinilipuka. Nilimuuliza sara
Una uhakika?Sara aliniambia ana uhakika na hata kama nataka kuhakikisha yuko tayari kufanya nihakikishe.
Nilitokwa na machozi kwa nini Bite anifanyie hivyo. Niliumia sana na kama kawaida sina wa kumuomba ushauri zaidi ya Mama kelly.
Nilimuuliza sara nifanyeje sasa huku nikiwa nimechanganyikiwa…Sara aliniambia kaa naye mbali ila naomba usimwambie nimekuambia mimi nimeshindwa kuvumilia. Lakini pia flors kuwa msiri na mambo yako. Sio wote wanafurahia kuona unapenswa na ck. Moyo uliniuma sana. Bite nilimpenda kama mdogo wangu. Nilimheshimu sana. Kwa nini anifanyie hivi. Nilikasirika na sasa nilitamani hata sijui kumfanya nini.
888888
NILIONDOKA NIKIWA KAMA NIMEPANICK. NILIENDA MOJA KWA MOJA OFCN KWA MAMA KELY. NIKIWA NAMSUBIRI KWANI HAKUWEPO NA NILIAMBIWA ATAKUJA ALIKUWA MA DHARURA.
NILIKAA OFCN KWAKE NA MFANYAKAXI MWENZAKE NIKIWA NAMSUBIRI. MUNGU WANGU!
Naota ama ni kweli?Sikuamini nilichokiona. Ni mama kely kwenye gari ya ck. Ck anamshusha mama kely na anawasha gari na kuondoka… moyo ulinilipuka. Mapigo ya moyo yalidunda kwa kasi. Sikuweza kuongea ila nilikuwa natetemeka… kumbe wenye pressure husumbuka sana… Nilikuwa nahindwa kupumua ipasavyo. Ni kama niliyekimbizwa sana na kichoka kwa kuhema. Pumzi zangu hazitoki sawa sawa…. kicha kiliniuma kama mishipa ya damu imebast… no ndani ya sekunde kadhaa haya yalinipata…Mama kely hakujua niko ofcn kwake… alikuwa akicheka na kusalimiana na wenzake hukua akiwambia yeye ni Alwatani… hakuna anayeingia mjini asisign kwake… niliumia sana na kutoka na nilikutana naye kwenye korido na hakunisalimia wala hakuonekana kujali. Niliondoka kwa hasira nikiwa nalia sana. Nilijiuliza niende wapi?akili ilinivurugika… Niliumia sana. Kichwa kiliuma na macho kunivimba. Nilianza kuhisi miguu mizito na nilishindwa kuendesha gari. Haraka nilipaki pembeni kwani nilikuwa nikipigiwa honi nyingi na madereva wengine huku wakinitusi wasijue yaliyonisibu.
Mama mmoja alihisi nina tatizo kwani nilisimamisha gari kwa ghafla sana. Nilikuwa nimelegea… alikuja na kugonga kiyoo cha mlangoni kuniambia nifungue lakink sikuwa naweza nililalia staling ya gari. MILANGO ILIKUWA IMEJILOKU.aliiita watu na walipasua kiyoo cha gari na kutoa locku. Silumbuki ilikuwaje ila nilizinduka nikiwa hospital na nilimuona mama yangu mzazi akiniambia mawazo ni ya nini?
88888
Mama alinihoji sana na sikuwa naelewa. Nilianza kurudisha kumbu kumbu pole pole. Na nilianza kukumbuka kila kitu. Niligeukia ukutani na kuanza kulia kwa nini mama kely anitende vile. Mama aliondoka na sasa ni wafanyakazi waliokuwa wanakuja kunisalimia. Wengi walijua ni pressure za mume. Lakini ukweli ya mume hayakuniuma kama ya ck na mama kely. Na kama ingekuwa ni kwa wema kwa nini mama kely asinisalimie na kunipuuza?nililia sana huku hakuna aliyekuwa anaelewa mchezo mzima. Nikiwa nimekaa na Bibi mama tunayefanya naye kazi alinihoji sana na kuniambia ni lazima nitulie la sivyo nitachanganyikiwa kwani nielekeako si kuzuri. Nilitamani kumsimulia issue nzima lakini niliogopa kwani kulikuwa na watu wengine. Mume wangu alikuwa akija kunisalimia na mke wa kaka yake aliongozana naye. Mke wa kaka yake alikuwa akinihudumia kwa kila kitu. Sikumuona mama kely wala biye wala sara. Niliumia sana. Moyo ulijaa chuki na kisasi. Nilikaa hospital siku nne. Kisha niliruhusiwa kutoka na kwenda nyumbani. Nilimuomba bibi mara apatapo nafasi aje kunitembelea. Nyumbani walikuka wamama wenzangu wa kanisani kuniona. Waliomba pamoja na mimi. Walinisomea neno. Na waliondoka. Sikuwa ninabujasiri hata wa kuwatazama. Sikuwapenda sana. Waliondoka na kuniahidi watakuja kumisalimia tena.
88
NIKIWA NIMEPATA NAFUU KABISA NA KUJIONA NAWEZA KUFANYA KILA KITU. NILIMPIGIA BIBI SIMU NA KUMTAKA KUZUNGUMZA NAYE WALAU NIPATE AHUENI. BIBI ALIKUJA NA NILIMUELEZEA MAHUSIANO YANGU NA CK. NA MPAKA TULIPOFIKA. KISHA NIKAMUELEZEA MAHUSIANO YA BITE NA MUME WANGU. NA NILIMUELEZA KWAMBA SARA NDIYE ALIYENIELEZEA YOTE. BIBI ALISIKITIKA SANA NA KUNIAMBIA MWANANGU YOTE HAYA UMEYAPANDA MWENYEWE. NILIKUONYA MWANZO NA NILIKUAMBIA ANAYEPELEKWA NA MAJI HUFA AKICHEKA… SASA NDO WEWE. YOTE HAYA YANAKUPATA UKIWA UNACHEKELEA. UMECHEKELEA MARAFIKI WAPYA… UMECHEKELEA MALI ZA UZINZI NA SASA UNAKUFA NA PRESSURE TUKIKUONA.
ALIENDELEA KUSEMA…
FLora umekuwa mwanamke qa kushangaliwa sasa hivi. Nguo uvaazo ni kituko. Lakini hakuna anayekuambia. Sio kwamba watu wanakuona umependeza wana gamaza la hasha. Wanakuona kama umechamganyikiwa.Flora kwa macho yangu nimekushuhudia ukiwa unabadilisha nguo kwenye gari baada ya wewe kutoka kazini. Na ukavaa nusu uchi. Flora una akili kweli?
Any way nisikugombeze sana maana maji yameshamwagika. Isipokuwa uote yanayotokea sasa hivi hembu yapuuze. Achana na hao marafiki. Rudia tabia yako ya mwanzoni. Hii hali itaisha pole pole. Achana na ck. Achana na mama kely achana ma bite na hata sara achana naye. Fuata maisha yako. Penda kanisa kama zamani. La sivyo utaaibika zaidi. Hio ni negative bado picha. Ila ukichoma negativu hawatapata picha watu. Lakini ukitunza negative picha halisi itajulikana na aibu ya maisha.
BIBI ALIMALIZA KUZUNGUMZZA NA AKANIAMBIA ANAONDOKA. ALIPOONDOKA TU SARA NA BITE NAO WALIINGIA.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
888
Nilipowaona nilishindwa kujizuia. Nilianza kuropoka kama sina akili nzuri.
Wanafiki nyie mnanizunguka.. tokeni hapa kwangu malaya ninyi. Wewe bite huna aibu unatoka na mume wangu loo mbona huna haya?Na hata wewe sara mmbea na wewe lenu moja. Na hata mama Kely naye. Malaya nyie. Noliwatukana kwa maneno hayo tu. Sikuwa najua zaidi ya hapo. Waliondoka huku wakiwa wametahayari. Sara alioneka a kiumia na wakati wanaondoka walizozana. Na kila mmoja kuondoka na njia yake. Mama yangu mzazi alikuja kunisalimia na aliniambia mama mkwe wangu kamueleza maneno makali sana juu yangu kuwa na mahusiano na mwanaume.
Mama alianza hivi.
Florah mwanangu mbona unaniacba uchi wangu kila mmoja anione?
Niligutuka kidogo na kisha kung’aka.
Mama nimefanya nini?
Mama aliniambia usinifiche. Tafadhali nieleze ukweli nikusaidie.
Hembu niambie wewe ni wa kuwa na mabwana kweli mwanangu?utumishi wa Mungu umeuacha kwa nini?
Mama alidondosha machozi. Niliogopa kumficha ila kumwambia kweli sikuwa tayari. Alilia sana akinieleza wewe ni wa kwenda kwa waganga?wewe wa kulewa?wewe wa kutoa momba?wewe huyu Flora… ni nini kimekupata mwanangu?mbona umekuwa zaidi ya mmbwa?mbona hali yako imekuwa mbaya kuliko mwanzo?
Mama aliomboleza. Wakati analia mimi ninapata hasira na kuunda agenda mpya akilini juu ya ck na mama kely. Licha ya bite ambaye bado nina hasira naye.
Mama alinisihi nimueleze ukweli ila nilisema amenisingizia. Na mama aliniambia mama mkwe wako kasema kwa namna unavyomuaibisha wala hata hapa hatakuja kabisa.
Niliumia ila nilamwambia mama mbona asiseme mwanae anamuaibisha ili hali anajua tabia zake?
Mama aliniambia huu sjo muda wa kulumbana na kutaka kulipiza kisasi. Ni muda wako wa kujirekebisha. Hembu kumbuka mwanangu Mungu alivyokupigania siku za ujana wako ukamtumainie sasa.
Nilimkatalia mama katu katu kuhusu tuhuma alizonipatia.
Mama aliondoka akiwa hana furaha kabisa.
888888
SIKU ILIYOFUATA NILIENDA KAZINI. BIBI ALINIITA NA KUNIAMBIA KUWA MAKINI SANA. NILITAMANI KUMPIGIA CK SIMU KWANI NILIM MISS. NILIPIGA SIMU YAKE YA OFCN NA KWA BAHATO ALIPOKEA. HAKUONGEA KAMA AWALI. ILA ALIKUWA KAMA ANANIKEJELI. NILIMUULIZA MBONA HUNA RAHA?ALINIELEZA NINI UMENIFANYIA?NILIMUULIZA KWANI NI NINI?
ALINIAMBIA KITU CHA AJABU.
ALINIAMBIA HIVI. KAMA UNAWEZA KUJA HAPA OFCN MARA MOJA NJOO. SIWEZI KUONGEA MA WEWE KWA SIMU. TAFADHALI NJOO MARA MOJA.
HARAKA NILITOKA NA KUWASHA GARI NANKUMFUATA. NILIFIKA NA ALINIKARIBISHA OFCN KWAKE NA KISHA ALINIAMBIA HIVI.
Flora nimekupenda sana. Lakini iweje uniloge?yani unaenda kwa mganga anakupa pete ya kuniloga?na kisha anakuambia ubebe mimba na uue mtoto uli penzi langu kwako lisife. Flora wewe ni wa kunifanyia mimi hivyo?
Nilishangaa sana kajuaje nikajua tu mama kely kamwambia mpaka kajazia.
Aliniambia unabisha?sema ukweli nikusamehe mpenzi wangu. Alinisihi nimwambie ukweli.
888888
NIKIWA NIMEKAA NATAFAKRI NISIJUE NIFANYE NINI,
CK ALINIULIZA UTAKUNYWA NINI MAMII? NILITAFAKARI UZURI WAKE NA UPOLE WAKE, UPENDO WAKE NA SIKU ZOTE ALIVONIHURUMIA,, NILIONA NJIA PEKEE NI KUAMUA KUMUELEZA UKWELI,
NILIMUELEZA NITAKUNYWA JUICE, NA ALINIITISHIA JUICE NA KUNIPATIA. ALIONEKANA MPOLE SANA, NA KISHA ALINIAMBIA NIAMBIE UKWELI FLORA, WANADAMU HUKOSEA, KUTENDA KOSA SIO KOSA BALI KURUDIA KOSA,, NA ALINIONYESHA ZAWADI ZANGU KWENYE DROO YAKE, ALINONYESHA CHENI YA DHAHABU, ALINIONYESHA HERENI NZURI SANA AMBAZO ZILIKUWA KWENYE PARK NZURI SNA NA KUSEMA ALL THESE ARE URS,, NAKUPENDA FLORA, JUST TELL ME THE TRUTH .NIAMBIE HAYA MAMA NIAMBIE,, HAYA MAMII NIAMBIE UKWELI WAKO,, NIAMBIE MPENZI WANGU,, MIMI NA WEWE NI WAPENZI MWAKA SASA UNANIFICHA NINI?
NILIFURAHIA ALIVYONIKUMBATIA, NILIFURAHIA ALIVYONIBEMBELEZA NA AKILI YANGU IKANIAMBIA KWA NINI NIMDANGANYE, BORA NIMWAMBIE UKWELI ANISAMEHE YAISHE TUANZE MAISHA YETU MAPYA.
Flora mimi siamini uchawi na kamwe siwezi kulogeka, yani wala usijali kwani najua uchawi wako haujanidhuru… hivyo usijali kunieleza ukweli mamii.. aliishika shika mikono yangu na kisha akaniambia haya mami niambie.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment