Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

NOTHING WITHOUT YOU (SI KITU BILA WEWE) - 3

 





    Simulizi : Nothing Without You (Si Kitu Bila Wewe)

    Sehemu Ya Tatu (3)





    Ilipoishia





    Siku ziliendelea kukatika. Hidifonce hakuweza kumuona tena Maria ingawa moyo wake ulikuwa na hamu kubwa ya kumuona. Majukumu kazini yalikuwa yamembana kupita kiasi. Kila siku muda wake wa kurudi nyumbani ulikuwa usiku.

    “Nitamtafuta tu, nimetokea kumpenda sana binti huyu” Hidifonce alijisemea.





    Songa nayo sasa...









    Maria hakujisikia vizuri moyoni, mvulana ambaye alikuwa amemuona katika kipindi kichache kilichopita alionekana kumchanganya. Ni kweli alikuwa amewaona wavulana wengi na kutongozwa na wavulana wengi lakini mvulana ambaye alikuwa amemuona katika kipindi kichache kilichopita alionekana kumchanganya.

    Akajilaza kitandani na kuanza kumfikiria. Akili yake haikutulia kabisa, moyo wake ulionekana kuhisi kitu fulani ambacho kilikuwa kigeni sana maishani mwake. Akaanza kujisikia kupenda na kuitaji. Mapenzi makubwa aliyokuwa nayo moyoni, alitaka kumpatia Hidifonce ambaye alikuwa amemuona nje.

    Hakuwa akimfahamu kwa jina na hiyo ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kumuona machoni mwake. Bado aliendelea kukihisi kile kitu kizito moyoni mwake. Hakutaka tena kuendelea kubaki ndani, akatoka nje ili kwenda kumwangalia Hidifonce kwa mara nyingine.

    Hidifonce hakuwa pamoja na vijana wale, alikuwa ameondoka na kuelekea chumbani mwake. Maria akaonekan kuwa mpweke, moyo wake ukaanza kummisi mvulana ambaye ilikuwa mara yake ya kwanza kumuona machoni mwake.

    Akaanza kurudi nyumbani kwao ambako akaingia getini na kuelekea chumbani kwake. Maria hakulala, muda wote alikuwa akimfikiria Hidifonce. Kitandani hakukulaloka, alibaki akijigeuza huku na kule. Maria akasahau kabisa kama alikuwa mtoto wa mchungaji wala hakufahamu kama alikuwa katika kikundi cha Uimbaji kanisani, kwa kipindi hicho kitu alichokijali ni kuwa pamoja na Hidifonce tu.

    Wiki moja ilipita, Hidifonce hakuonekana machoni mwake, siku zote hizo Maria alikuwa akionekana kuwa na mawazo juu ya Hidifonce. Muda mwingi Maria alikuwa akimfikira Hidifonce kiasi ambacho alishindwa kabisa kujisomea nyumbani.

    Maria akaonekana kutokukubali kabisa kuuacha moyo wake uwe na mawazo juu ya Hidifonce. Kitu alichokifanya ni kwenda katika sehemu ile ambay alimuona Hidifonce akiwa amekaa paoja na vijana wengine. Maria akaamuulizia Hidifonce mahali pale.

    Kila kijana ambaye alikuwa mahali pale alibaki akishangaa, hawakujua Maria na Hidifonce walikuwa wamefahamiana vipi kwani Maria aliuliza kana kwamba alikuwa akimfahamu Hidifonce. Akaelekezwa nyumba ambayo Hidifonce alikuwa akiishi na moja kwa moja kuanza kwenda huko.

    “Ni vigumu kumpata mchana. Muda mwingi huwa anashinda ofisini” Msichana mmoja aliyekuwa akikaa katika nyumba ile, Shania alimwambia Maria.

    Maria akaonekana kuchoka, maneno ambayo aliambiwa yalionekana kumuumiza, alihitaji sana kuonana na Hidifonce kwa wakati huo, maneno ambayo aliambiwa kuwa usiku ndio ulikuwa muda wa kuonana nae ulionekana kumuumiza.

    Hakuwa na uhakika kama angeruhusiwa kwenda sehemu yoyote usiku. Alijiona kuwa na bahati mbaya, akamwangalia Shania huku akioekana kuhuzunika, alionekana kukosa raha kabisa.

    “Akirudi mwambie namtafuta” Maria alimwambia Shania na kuondoka.

    Shania akabaki akiwa na mshangao, hakuamini msichana mrembo kama Maria angefika nyumbani hapo na kumuulizia Hidifonce. Alimuona Maria kama msichana ambaye alitakiwa kukaa nyumbai na kumsubiri mvulana na si yeye kwenda kumuulizia mvulana.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ********







    Mitumbwi zaidi ya elfu tatu ilikuwa ikiingia katika ziwa Viktoria kila siku usiku. Wavuvi walikuwa wakivua samaki usiku mpaka alfajiri muda ambao walikuwa wakirudi katika makazi yao na kuwauza.

    Biashara ile ilionekana kubadilisha maisha ya wakazi wengi kwa wananchi ambao walikuwa wakizunguka ziwa la Viktroria, yaani kuanzia Uganda, Kenya mpaka Tanzania. Samaki halikuonekana kuwa tatizo kwa upande wa sehemu hizo tatu, kila siku samaki wengi walikuwa wakivuliwa, hasa katika usiku ambao hakukuwa na mwezi.

    Kati ya wavuvi ambao walikuwa wakifanya kazi ya uvuvi alikuwepo mzee Mshana ambaye mara kwa mara alikuwa akiingia ziwani pamoja na vijana wake kufanya kazi hiyo ya uvuvi. Kila siku walikuwa wakiingia ziwani usiku pamoja na chemri zao.

    Kazi kubwa ya chemri zao ilikuwa ni mwanga. Ziwani hakukuwa na mwanga hali ambayo mara samaki walipokuwa wakiuona mwanga wa Chemri, walikuwa wakija juu hali iliyofanya kuvuliwa kwa urahisi zaidi. Kutokana na hali hii, kazi ya uvuvi ilionekana kuwa ngumu katika kipindi ambacho kulikuwa na mbaramwezi, katika kipindi hicho, samaki hawakuwa wakija juu kwani mwanga wa mbaramwezi ulikuwa ukiwatosha.

    Mzee Mshana pamoja na vijana wake walikuwa wakiendelea na kazi zao za uvuvi kama kawaida. Walikuwa katikati ya ziwa huku wakijaribu kushusha nyavu zao kujaribu kama wangeweza kupata samaki wowote. Kipindi hicho kilionekana kuwa kipindi kigumu kutokana na mwezi kuangaza angani.

    Walijaribu kushusha nyavu zao katika kila kona lakini hawakupata samaki wengi, kila mmoja alionekana kuchanganyikiwa. Mara kwa mara walikuwa wakiuangalia mwezi kwa nyuso zilizojaa hasira. Hawakuupenda mwezi katika maisha yao kwani upatikanaji wake ulikuwa ukiyafanya maisha yao kuwa magumu.

    “Kuna boti ile inaondoka...ilikuwa imesimama mahali pale. Kwa nini tusiende pale na sisi tukajaribu?” Fikiri aliwaambia wavuvi wenzake akiwepo mzee Mshana .

    “Hakuna kitu pale. Hivi kama kungekuwa na kitu wale wangeondoka na mtumbwi wao?” Mzee Mshana alimwambia Fikiri.

    Mvutano ukaanzia mahali hapo. Fikiri alikuwa wakitaka kuelekea katika eneo lile kwa ajili ya kuhakikisha kama kweli hakukuwa na samaki. Tayari Fikiri akaonekana kuwa na wasiwasi na mtumbwi ule ambao ulikuwa umeondoka kwa kasi mahali pale.

    Kila alipotaka kulipotezea jambo hilo, moyoni alisikia sauti ambayo ilimwambia kuwa ni lazima waende mahali pale. Fikiri alijaibu kubishana na sauti ile lakini sauti ile ikaonekana kuwa kero moyoni mwake. Hakujua kama sauti ile ilikuwa ni mawazo yake mwenyewe, sauti ya Malaika au sauti ya Roho chafu iliyokuwa ikimtaka awashawishi wenzake waende pale ili wazame na kupotea.

    Akaupiga moyo wake konde na moja kwa moja kuwang’ang’aniza wavuvi wenzake waende mahali pale. Fikiri alionekana kuwa mbishi hali ambayo iliwafanya kukubaliana nae kwa shingo upande. Wakaanza kupiga kasia mpaka katika eneo lile ambapo wakachukua nyavu na kushusha majini.

    Wala hawakuchukua muda mrefu, mara wakasikia kitu kizito kikiwa kinaivuta vuta nyavu yao. Wakajitahidi kuvuta nyavu zao lakini wala hawakufanikiwa kitu ambacho kiliwapelekea kumwambia Fikiri kuingia chini ya Ziwa kwa ajili ya kumtoa samaki huyo mkubwa ambaye alikuwa amenasa katika nyavu zao.

    Fikiri hakuwa na la kujifikiria mara mbili mbili, moja kwa moja akajitosa majini huku akiwa na kisu chake mkononi pamoja na tochi ambayo ilikuwa na uwezo wa kutokupitisha maji. Alikuwa akielekea chini kabisa ambako kulikuwa na kina kirefu zaidi ya maghorofa kumi na mbili.

    Baada ya kufika chini ya maji, akaanza kumulika mulika katika kila kona majini mule hasa katika nyavu yao ambayo walikuwa wameishusha. Aliendelea kuangalia zaidi na zaidi, ni samaki wachache ndio ambao walikuwa wamenasa katika nyavu zao.

    Fikiri akajaribu kuivuta tena nyavu ile, ilionekana kuwa nzito kuja juu hali iliyomfanya kugundua kuwa kulikuwa na kitu majini, hasa kule chini kabisa. Kwa sababu bado alikuwa amebakisha pumzi za kutosha, akaendelea kwenda chini huku akimulika mulika.

    Fikiri hakuamini macho yake, alibaki akitetemeka huku akiuhisi mwili wake ukifa ganzi majini. Kitu alichokiona hakuwa akiamini kama ndicho kilikuwa kile alichokuwa akikiona au kilikuwa tofauti na kile. Alitamani apige mbizi kwenda juu, lakini akaupiga moyo wake kondo na kuelekea kule alipomuona binadamu huku akikiweka vizuri kisu chake.

    Ulikuwa ni mwili wa binadamu ambao uilikuwa umelegea kupita kiasi. Akaushika mkono na kuanza kurudi kwa juu. Wavuvi mbao walikuwa mtumbwini walikuwa wakimsubiria Fikiri kwa furaha zote kwani waliamini kuwa ni lazima angerudi mtumbwini hapo akiwa na samaki mkubwa ambaye allikuwa amenasa katika nyavu yao.

    Fikiri akaibuka na kuomba msaada wa kumvuta kutoka majini. Hakukuwa na mtu ambaye alikuwa akiamini kile ambacho alikuwa akikiona mahali pale. Fikiri alikuwa amekuja na kitu kingine ambacho kilikuwa na tofauti na matarajio yao.

    “Binadamu....!” Mzee Mshana alisema huku akionekana kuogopa.

    “Hebu muwekeni hapo kwanza” Fikiri aliwaambia wavuvi wenzake na kumvuta Patrick na kumuweka katika mtumbwi wao.

    Kila mmoja alikuwa akimwangalia Patrick kwa mshangao, kila walipojaribu kumuuliza Fikiri kwa kile ambacho kilikuwa kimetokea ziwani mule, hakuongea kitu, alikuwa amekaa pembeni akihema kwa nguvu kutokana na kutokuvuta pumzi muda mrefu majini.

    “Hivi anapumua?” Mzee Mshana aliuliza hali iliyompelekea mvuvi mmoja kusikiliza mapigo ya moyo.

    “Mhhh!! Kwa mbali sana....yaani sana” Kijana yule mvuvi alimjibu.

    Hakukuwa na mtu ambaye alikuwa na hamu ya kuendelea na uvuvi, walichokifanya ni kuanza safri ya kuelekea katika kisiwa cha Ukerewe ambacho walikuwa wakiishi. Muda wote walikuwa wakijitahidi kumtoa maji Patrick tumboni, hakuwa akijitambua kabisa pale alipokuwa na wala hakujua ni kitu gani kilikuwa kinaendelea.

    Walichukua masaa mawili mpaka katika kisiwa cha Ukerewe ambako wakauweka mtumbwi wao na kisha kuanza kuelekea katika nyumba yao huku saa ikiwaonyesha kuwa saa kumi na robo alfajiri.

    Patrick akawekwa katika chumba ambacho hakikuwa na kitu chochote kile kwa ajili ya kupata hewa safi. Masaa yaliendelea kukatika, ilipofika saa nne asubuhi, Patrick akafumbua macho. Akaanza kuangalia huku na kule, uso wake ulijawa na mshangao kupita kiasi.

    Akainuka kutoka pale kitandani na kuanza kuelekea nje, maeneo ya eneo lile yalionekana kumchanganya kupita kiasi. Akaanza kuvuta kumbukumbu zake, alikumbuka mara ya mwisho alikuwa katika mtumbwi pamoja na wavuvi wengine na kisha kutoswa majini. Alikumbuka kila kitu, alipoanza kutapatapa mpaka kuona giza mbele yake.

    Akaangalia vizuri sehemu ile, wavuvi wanne wakaonekana wakiwa katika mtumbwi uliokuwa karibu na ufukwe wakichambua samaki. Patrick akaanza kupiga hatua kuwafuata mtumbwini mule. Kila mtu akaanza kumwangalia Patrick huku nyuso zao zikionekana kujawa na tabasamu.

    “Unaendelea vipi?” Fikiri alimuuliza Patrick.

    ‘Naendelea vizuri. Hivi ni nini kilitokea?” Patrick aliuliza hali iliyowafanya wavuvi wale kuanza kumuelezea kila kitu ambacho kilitokea.

    Katika kisiwa hicho cha Ukerewe ndipo ambapo Patrick alipoanza maisha mapya. Kila siku alikuwa akibaki nyumbani pamoja na Fikiri huku wavuvi wakiendelea na kazi zao za uvuvi. Patrick alionekana mpweke, baridi lililokuwa kisiwani kule lilionekana kumsumbua kupita kiasi.

    Muda mwingi alikuwa akimfikiria Azizi, hakujua ni kitu gani ambacho kilikuwa kimetokea kwa Azizi, kila siku maisha yake yalikuwa na huzuni, akili yake ilijua fika kwamba Azizi alikuwa ametoswa majini kama vile ambavyo ilitokea kwake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hakujua kama Azizi alikuwa amenusurika kama ambavyo alinusurika yeye. Kila siku mawazo juu ya Azizi yalikuwa yakimsumbua, wakati mwingine alikuwa akitoa machozi, alijiona kumpoteza tu muhimu maishani mwake ambaye aliamini kuwa angekuwa pamoja nae hadi pale ambapo maisha yake yangekuwa salama.

    Kila siku Patrick alikuwa na wazo moja tu, la kuondoka kisiwani hapo na kuelekea Mwanza mjini ambako huko angejua ni wapi ambapo angetakiwa kwenda. Hakutaka kabisa kuishi kisiwani hapo, kila siku alikuwa akipanga namna yya kutoroka kisiwani hapo.

    Mwezi ulikatika, bado Patrick alikuwa kisiwani hapo huku akiwa amezoeana na watu wengi ambao walikuwa wakiishi kisiwani hapo. Patrick alikuwa akisaidiana nao kazi japokuwa akili yake ilikuwa ikitafuta namna ya kutoroka mahali hapo.

    Siku ziliendelea kukatika, kila njia ambayo alikuwa akiifikiria aliiona kutokufaa kabisa. Kitu alichokifanya kwa wakati huo ni kujenga urafiki mkubwa na Fikiri ambaye wakatokea kuzoeana kama ambavyo alizoeana na Azizi ambaye hadi wakati huo hakujua alikuwa mahali gani.

    “Nataka kujifunza kuvua samaki” Patrick alimwambia Fikiri asubuhi moja ambapo hakukuwa na watu wengi kisiwani hapo.

    “Mbona asubuhi namna hiyo, wewe unafikiri utapata samaki kweli?” Fikiri aliuliza.

    “Nitapata tu. Kama ambavyo Petro alivyopata wakati walipokwenda kuvua” Patrick alimwambia Fikiri.

    Fikiri hakuwa na jinsi, kwa kuwa alikuwa amemzoea sana Patrick, akaona kuwa kusingekuwa na tatizo kama ambavyo alivyofikiria. Akamkabidhi Patick mtumbwi mmoja na kisha kuingia nao majini. Akili ya Patrick ilikuwa ikifikiria kuondoka kisiwani hapo ambapo aliyaona maisha kuwa magumu kwake.

    Akaanza kupiga kasi kwa kasi, hakuttaka kuchelewa sana kufika Mwanza mjini. Aliendelea kupiga kasia zaidi na zaidi, alikuwa akipishana na mitumbwi kadhalika ziwani mule. Mikono yake ilikuwa imechoka kupita kiasi lakini hakutaka kusimama njiani, bado alitaka kufika Mwanza mapema.

    Alichukua masaa matatu mpaka kufika Mwanza mjini. Mitumbwi ilikuwa mingi ziwani na wala hakukuwa na mtu aliyehofia kwa mtu mwenye umri kama wake kutumia mtumbwi ziwani. Mara baada ya kufika karibu na nchi kavu, akauegesha mtumwi pembeni na kisha kuteremka.

    Akaanza kupiga hatua kuelekea mjini huku akiangalia huku na kule. Njaa kali ilikuwa imemkamata kiasi ambacho wakati mwingine alikuwa akijihisi kusikia kizunguzungu. Patric alitembea kwa haraka sana, maghorofa yalikuwa yakionekana machoni mwake, akaanza kuangalia huku na kule, macho yake yakamuona dereva Taksi ambaye alikuwa amesimama nje ya gari lake.

    “Naomba unisaidie” Patrick alimwambia dereva yule.

    “Nikusaidie nini?”

    “Mia tano. Nasikia njaa kaka yangu” Patric alimwambia dereva yule kwa sauti ya chini ambayo ilionyesha ni kwa kiasi gani alikuwa na njaa kwa wakati ule.

    “Umeniona mimi ni benki? Au kituo cha kutoa msaada kwa watoto wa mitaani?” Dereva yule aliuliza huku akinekana kukasirika kutokana na kuwa mahali hapo kwa masaa manne pasipo kupata abiria yeyote.

    “Naomba unisaidie kaka yangu” Patrick alimwambia dereva yule.

    “Sikiliza. Unaliona gari lile, wafuate na uwaombe msaada, watakusaidia. Wao wanawajali watoto lakini si mimi” Dereva yule alimwambia Patrick.

    Patrick akaliangalia gari lile ambalo alikuwa ameambiwa. Maneno makubwa yaliyosomeka THOMAS LYARUU TOURISM COMPANY yalikuwa yakionekana katika gari moja aina ya Harrier. Patrick akaanza kupiga htua za haraka haraka kuelekea katika gari lile.

    Alipofika nyuma ya gari lile, akaanza kuangalia nyuma ya gari lile. Kreti tano za soda pamoja na mikate ilikuwa ikionekana vizuri machoni mwake. Akajaribu kuufungua mlango ule wa nyuma kabisa, mlango ukafungua na kisha kuingia. Kutokana na njaa kali aliyokuwa nayo, akaanza kunywa soda zile na kula mikate ile kwa kasi kubwa.

    Alikula na kunywa, ghafla akasikia mlango wa mbele ya gari ukifunguliwa. Kwa kasi akajifunika shuka kubwa lililokuwa nyuma ya gari lile sehemu ya kubebea mzigo na kujifunika. Patrick akasikia gari lile likiwashwa na kisha kuondoka mahali pale huku akiwa garini.

    “Ni lazima tuwahi. Tunajua kuwa kule tutakutana na wazungu wengi ambao tutawachukua na kuwapeleka wanapopataka” Sauti ya kijana mmoja ilisikika.

    “Ila si kuna magari mengine ya kampuni hii yataelekea kule?”

    “Ndio”

    Gari lile la watalii lilikuwa likiendelea na safari ya kuelekea Musoma katika kijiji cha Butiama kwa ajili ya kukumbukwa kwa Hayati Mwalimu Nyerere. Wazungu wengi walikuwa wakitarajiwa kukusanyika mahali kule kwa ajili ya kuangalia kaburi la kiongozi huyo ambaye alikuwa ameipa Tanganyika uhuru.

    Siku hiyo ilionekana kuwa maalumu kwa Watanzania, wafanyaazi hawakwenda kazini na wala wanafunzi hawakwenda shuleni. Idadi ya watu zaidi ya elfu tano iltarajiwa kukusanyika katika kijiji hicho, kila mtu alitamani kuliona kaburi hilo ambalo lilikuwa likitangazwa sana katika vyombo vya habari hasa mara baada ya kufanyiwa matengenezo na kuwa tofauti na jinsi lilivyokuwa kabla.

    Patrick hakujua alikuwa akipelekwa wapi ila kitu ambacho alikuwa akikitaka ni kuondoka na kuelekea sehemu yoyote ile ili tu akaanze maisha mapya. Vumbi lilikuwa likiingia katika shuka lile lakini Patrick hakuonekana kujali, bado alikuwa akitaka kufika mwisho wa safari ile ambayo hakujua ingekuwa mahali gani.

    Patrick alionekana kuchoka na maisha, alijitolea aishi sehemu yoyote ambayo aliiona kuwa na utulivu na salama katika maisha yake. Kila siku alikuwa akijifikiria ni kwa jinsi gani angefanikiwa katika maisha yake na kurudi kijijini Itilima kwa ajili ya kumuoa Siwema ambaye bado alikuwa akimpenda kuliko msichana yeyote.

    Gari lile lilitembea kwa masaa matatu, Patrick alilihisi likisimama, akafungua shuka na kuanza kuchungulia kwa nje. Milango ya gari lile ikafunguliwa na wale watu ambao walikuwa katika gari lile kuteremka. Sauti za watu zilikuwa zikisikika mahali pale.

    “Kachukue vinywaji kule nyuma ya gari” Sauti ya kijana mmoja ilisikika.

    Patrick akaonekana kushtuka, hakujua ni kitu gani ambacho alitakiwa kukifanya kwa wakati ule. Alisikia vishindo vya mtu akija kule ambako alikuwepo. Patrick akaanza kutetemeka kwa hofu, wasiwasi ulikuwa umemjaa kupita kiasi, tayari alijiona kukamatwa na mtu yule ambaye alikuwa akija kule kuchukua vinywaji.



    ****************************************







    Hidifonce alijikuta akichanganyikiwa kupita kiasi. Kitendo cha Maria kuja nyumbani na kumuulizia kilionekana kumchanganya sana. Akaanza kumfikiria msichana huyo, uzuri wake na hadi kila kitu ambacho alikuwa nacho.

    Hakujiona kujiamini kabisa, Maria kwake alionekana kuwa msichana mzuri ambaye wala hakutakiwa kuwa na mwanamume kama yeye. Mwanaume ambaye alihitajika kuwa na Maria ni yule ambaye alikuwa na usafiri utakaomfanya Maria kutokutembea kwa miguu kwa ajili ya kuuchosha mwili wake.

    Alimwangalia Shania mara mbili mbili, hakuonekana kutokuamini kile ambacho alikuwa amemwambia. Kitendo cha Maria kuja nyumbani pale kilionekana kumfanya kutokuamini kabisa. Akaingia chumbani kwake na kujipumzisha kitandani mwake.

    Akili yake ikaanza kumfikiria Maria toka siku ile ambayo alikuwa amemuona na kuangaliana kupita kiasi. Hidifonce akaanza kujiona mtu mwenye bahati sana, kitendo cha kuuliziwa na Maria, msichana ambaye alikuwa na uzuri wa kipekee, kilionekana kuwa kitendo kilichokuwa na bahati kubwa.

    Hidifonce hakutaka kabisa kuonana na Maria kitendo ambacho kilimfanya kuchelewa kurudi nyumbani. Kila sik alipokuwa akirudi nyumbani alikutana na malalamiko kadhaa kutoka kwa Maria ambayo alikuwa ameyaacha kwa Shania.

    Maria alionekana kumuhitaji Hidifonce ambaye wala hakuonekana kujali kutokana na woga ambao alikuwa nao. Malalamiko yaliendelea kuzidi kila siku lakini wala hakukuwa na mabadiliko ambayo yalikuwa yametokea, bado Hidifonce hakutaka kuonana na Maria.

    “Ameleta bahasha” Shania alimwambia Hidifonce huku akimkabidhi bahasha ile.

    Hidifonce akaichukua bahasha ile kubwa ya kaki na kuingia ndani. Akaanza kuifngua, macho yake yakakutana na maua kadhaa pamoja na kadi. Tabasamu kubwa likautawala uso wake. Akaendelea kuangalia zaidi, macho yake yakakutana na albamu ndogo ambayo akaichukua na kuanza kuangalia picha zilizokuwa katika albamu ile.

    Hidifonce akaonekana kushtuka, mapigo ya moyo yakaanza kumdunda kwa kasi, hakuamini kile ambacho alikua akikiona katika albamu ile. Picha kadhaa za Maria ambazo alikuwa amezipiga nusu uchi zilikuwa zikionekana vizuri machoni mwake.

    Hidifonce akajiona kuhisi hali ya tofauti mwiini mwake. Hamu ya kufanya mapenzi ikaanza kumkumba. Kila alipozidi kuziangala picha zile na ndivyo ambavyo alizidi kuchanganyikiwa na hali ile kumshika zaidi. Alipomaliza kuzingalia picha zile, akajilaza kitandani huku albamu ikiwa pembeni yake.

    Tayari akaona ni kwa jinsi gani Maria aikuwa akimpenda, moyo wake akauhisi kuanza kuingia katika uhitaji wa kuwa pamoja na Maria. Mpaka kufikia hatua ile, hakuona sababu ya kumpotezea Maria, alijua ni kwa jinsi gani moyo wa msichana yule ulikuwa ukimuuma kila alipokuwa akija nyumbani na kumkosa.

    “Ni lazima niongee nae kesho” Hidifonce alisema.

    Siku iliyofuata ilikuwa jumamosi ambayo wala Hidifonce hakuwa akielekea kazini. Alibaki nyumbani huku akiiona siku hiyo kuwa maalumu ya yeye kuwa pamoja na Maria na kuongea. Alianza kufanya kazi zake kama kawaida na alipomaliza, akaandaa chakula na kuanza kula.

    Alitaka kupata maandalizi makubwa zaidi kwa ajili ya kuongea na msichana yule ambaye kila siku sifa za uzuri wake zilikuwa zikizidi kusikika kutoka kwa watu mbalimbali mtaani pale. Hidifonce alifanya kila kitu, alipomaliza, akamfuata Shania.

    “Unaweza kwenda kumuita?”

    “Nani?”

    “Maria”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Shania akachomoka mahali pale na kuelekea nyumbani kwa mchungaji Christopher kwa ajili ya kumuita Shania. Shania hakuonekana kuamini kama kweli Hidfonce ndiye ambaye alikuwa akimuita kwa wakati huo. Kwa kuwa alikuwa amekwishaoga, akaanza kujiandaa kwa kujipulizia pafyumu kadhaa na kisha kuanza kwenda kumuona Hidifonce. Kadri alivyozidi kupiga hatua kuelekea katika nyumba aliyokuwa akiishi Hidifonce na ndivyo ambavyo mapigo yake ya moyo yalivyozidi kumdunda.

    “Naomba unisindikize Shania” Maria alimwambia Shania huku akionekana kuogopa kuingia peke yake.

    “Inga tu. Kama unaogopa basi rudi” Shania alimwambia Maria ambaye akaingia ndani.

    Hidifonce alikuwa ametulia kitini huku akionekana kuukunja uso wake kama mtu ambaye alikuwa amekasirika. Maria akaonekana kuogopa, akamwangalia Hidifonce mara mbili mbili huku kadri muda ulivyozidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo hofu ilivyompata zaidi.

    Kwa sababu hakukuwa na viti chumbani pale, Maria akakaa kitandani, macho yake yalikuwa yakiangalia chini huku kwa mbali akionekana kutetemeka. Hidifonce alibaki akimwangalia Maria, tayari alikwishauona woga ambao alikuwa nao Maria, akaanza kumsogelea kwa karibu.

    “Mbona umefanya ujinga huu Maria?” Hidifonce aliuliza huku akimwangalia Maria. Maria hakujibu kitu.

    “Yaani unanitumia picha ulizopiga nusu uchi. Unafikiri nikiziangalia ndio nitakuona wewe mzuri? Sikiliza Maria, kama mbaya ni mbaya tu, hata ungeniletea picha za utupu kabisa, ungeendelea kubaki hivyo hivyo, yaani wala usingenisisimua” Hidifonce alimwambia Maria.

    Ghafla Maria akaanza kubadilika. Kwikwi ikaanza na hatimae machozi kuanza kumtoka. Maneno aliyoyaongea Hidifonce yalionekana kumuumiza kupita kiasi. Akasimama na kuanza kuufuata mlango. Hakutaka kumwangalia Hidifonce usoni, tayari machozi yake yalikuwa yameloanisha mashavu yake. Akatoka ndani ya chumba kile na kuufunga mlango kwa kuubamiza hali iliyoonyesha ni kwa jinsi gani alikuwa na hasira.





    *****







    “Au acha. Tutachukua tukirudi” Sauti ilisikika masikioni mwa Patrick.

    Mwanaume yule ambaye alitaka kuufungua mlango wa nyuma kwa ajili ya kuchukua vinywaji akauacha mlango ule na kisha kuondoka kuelekea ndani ya eneo lililokuwa kaburi lile. Patrick akaanza kushukuru Mungu, hakuamini kama kweli alikuwa amenusurika kuonwa na mwanaume yule ambaye wala hakuwa amemuona.

    Patrick akalifungua shuka na kisha kutoka. Mwili mzima ulikuwa umejaa mavumbi ambayo yalikuwa yakipenya taratibu mpaka mule alipokuwa amejifunika kwa shuka. Akaanza kupiga hatua kulekea kule ambako watu walikuwa wakielekea.

    Watu zaidi ya elfu tano kutoka katika nchi mbalimbali walikuwa wamekusanyika katika kijiji hicho kwa ajili ya kuangalia kaburi alilozikwa rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere. Wazungu kutoka Marekani, Uingereza na nchi nyingine nyingi walikuwa mahali hapo katika siku hiyo ambayo ilionekana kuwa muhimu katika maisha yao.

    Kila mtu alikuwa akimwangalia Patrick ambaye alikuwa mchafu kupitiliza. Walinzi ambao walikuwa wakisimama katika geti la kuingilia eneo la kaburi wakamzuia Patrick. Patrick akaanza kupiga hatua kurudi nyuma hadi kule kulipokuwa na sehemu ya kuegeshea magari na kutulia chini.

    Bado kichwa chake kilikuwa kikimfikiria Azizi ambaye hadi kufikia kipindi hicho hakuwa akifahamu sehemu ambayo rafiki yake huyo alipokuwa. Hakuwa na uhakika kama alikuwa hai au alikuwa amekufa baada ya kutoswa majini, kila alipokuwa akifikiria kuhusu Azizi, alikosa raha kabisa.

    Masaa yalizidi kusogea huku. Jioni ikaingia, muda ambao watu wakaanza kuingia katika magari yao na kisha kuanza safari ya kuelekea nyumbani kwao na katika hoteli ambazo walikuwa wamepanga. Patrick akasimama kutoka pale alipokuwa na moja kwa moja kupiga hatua kuelekea katika sehemu moja ambayo ilikuwa na magari kadhaa.

    Patrick akajaribu kufungua mlango wa buti a gari moja aina ndogo aina ya Chesa mayai. Mlango haukuwa umefungwa kwa ufunguo jambo ambalo lilionekana kumfurahisha Patrick ambaye akaingia ndani kwa haraka haraka na kuufunga.

    Zilipita dakika kumi, mara wamiliki wa lile gari wakasikika wakiingia garini na kuliwasha gari lile. Patrick aliendelea kubaki katika buti lile, vumbi likaanza kuingia katika buti lile lililomfanya mara kwa mara kukohoa.

    “Thirty kilometres left before we get in Serengeti hotel (Tuna kilometa thelathini hata kabla hatujaingia katika hoteli ya Serengeti)” Mtu mmoja alisikika. Patrick akaisikiliza lafudhi ambayo ilikuwa imetolewa katika uongeaji wa lugha ile, lafudhi ilisikika kuwa ni ya mtu mweusi aliyekulia Afrika.

    “Ok! We have to get rooms (Tutatakiwa kuchukua vyuma)” Sauti ya mwanaue mmoja mzungu ilisikika.

    Gari liliendeshwa kwa mwendo wa kasi japokuwa barabara haikuwa nzuri. Ndani ya gari hilo kulikuwa na watu wawili, mwanaume mmoja wa kiafrika pamoja na mzungu mmoja. Katika gari jingne ambalo lilikuwa likiongozana na gari hilo, kulikuwa na watu watatu, mwanamke mmoja mzungu, mwanamke mmoja wa kiafrika pamoja na mtoto mmoja wa kike wa kizungu.

    Magari yale yalikuwa yakiendelea kukata mbuga mpaka kufika katika hoteli ya Serengeti ambako wakayapaki magari yale na kisha kuanza kuelekea katiika jengo la hoteli ile.

    “Jesus Christ! I’ve forgot my laptop. Lydia, go and get my laptop (Nimesahau laptop yangu. Lydia, kanichukulie laptop yangu) Mwanaume yule mzungu alimwambia binti yake ambaye kwa haraka haraka akarudi katika gari lile.

    Akaanza kuitafuta laptop ya baba yake, Bwana Smith lakini hakuweza kuiona. Wazo likamjia kwamba mara kwa mara alikuwa akiiweka katika buti la gari. Akaanza kupiga hatua kulekea katika buti la gari ambako akalifungua na kuingiza mono moja kwa moja bila kuangalia.

    Lidya akaonekana kushtuka, akalifungua vizuri boneti lile la gari na kuangalia, macho yake yakakutana na mwili wa mtu, akabaki akitetemeka huku akiuhisi mwili wake kufa ganzi.

    Lydia akaanza kipiga kelele huku akikimbia kuelekea katika jengo la hoteli ile. Walinzi wakatokea na kuanza kumfuata Lydia kwa mwendo wa kasi. Mara Bwana Smith ambaye alikuwa kaunta pamoja na wenzake wakaanza kuelekea nje ambako wakakutana na Lydia ambaye bado alikuwa akilia kwa woga.

    “Lydia..what happened? (Lydia...nini kimetokea?)

    “A ghost...a ghost...a ghost dad )Mzimu...mzimu...mzimu baba)” Lydia alimwambia baba yake, Bwana Smith

    “A ghost? Where is it? (Mzimu? Uko wapi?)” Mzee Smith alimuuliza Lydia

    “In the car (Garini)” Lydia alijibu hali iliyowafanya wote kuanza kuelekea garini huku wakiongozana na walinzi.



    ****************************************







    Hali ya Siwema ilikuwa mbaya kupita kiasi. Kila siku macho yake yalikuwa yamefumba, hakufumbua macho, alitulia kitandani kimya kana kwamba alikuwa amekufa. Udundaji wa moyo wake ndio ambao uliwafanya madaktari na manesi kujua kwamba bado Siwema alikuwa hai.

    Mwili wake bado ulikuwa vilevile, micharazo pamoja na alama za mapanga bado zilikuwa zikionekana vizuri japokuwa vidonda vyake vilikuwa vimesafishwa na kupakwa dawa. Siwema aliendelea kubaki kimya kila siku, madaktari na manesi hawakuwa na uhakika kama kuna siku Siwema angefumbua macho na kurudi katika hali yake ya kawaida.

    Hakukuwa na mtu ambaye alifika mahali hapo kumuona Siwema, hata wale watu ambao walikuwa wamemleta hospitalini pale hawakuonekana tena. Kila nesi alikuwa akimuonea huruma Siwema ambaye hali yake ilizidi kuwa mbaya.

    Madaktari wakafanya kazi ya ziada katika kuhakikisha wanampa Siwema huduma bora. Ndani ya wiki moja, hali yake ikaanza kuonekana kurudi katika hali ya kawaida jambo ambalo lilileta matumaini kwa kila aliyemwangalia.

    Tiba iliendelea zaidi na zaidi, Siwema akaonekana kupata nguvu na hata macho yake alikuwa akiyafumbua kama kawaida. Tatizo lilibaki kuwa moja, Siwema hakuwa akiongea. Kila siku alikuwa akiwaangalia manesi ambao walikuja katika chumba chake na kumjulia hali pasipo kuongea chochote kile.

    Kila nesi alikuwa akimuonea huruma Siwema ambaye alikuwa ametelekezwa hospitalini hapo. Chakula cha kila siku kilikuwa kikiletwa na wauguzi hao ambao walitokea kumpenda Siwema kuliko mgonjwa yeyote hospitalini hapo.

    Miezi miwili ikakatika, Siwema akarudi katika hali yake ya kawaida ambapo akaanza kuwaelezea manesi na madaktari kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea katika maisha yake. Kila mtu alionekana kumuonea huruma Siwema ambaye alionekana mdogo sana kupitia matatizo kama yale.

    Kila mtu alimshauri kurudi kijijini kwao lakini Siwema hakuonekana kuelewa, hakutaka tena kurudi kijijini. Alimuogopa sana baba yake, hakujua angefanywa nini kama tu angerudi kijijini na kuingia mikononi mwa baba yake ambaye hakuwa na mchezo hata mara moja.

    Kwa kuwa Siwema hakuwa na pa kwenda kwa wakati huo, nesi Getrude akaamua kwenda kukaa nae nyumbani mpaka hapo mambo yake binafsi yatakapokuwa salama. Siwema hakuwa na kipingamizi chochote kile, moja kwa moja akaamia nyumbani kwa Getrude ambaye alikuwa amepanga vyumba viwili hapo hapo Nzega.

    Kila siku mawazo yake yalikuwa kwa Patrick ambaye hadi wakati huo hakuwa akijua mahali ambapo alipokuwa. Siwema aliumia sana moyoni kila alipokuwa akimfikiria Patrick. Kamwe hakutaka kutengana nae, alikuwa akizidi kumhitaji kila siku.

    Siwema alizikumbuka picha zake nyingi ambazo alikuwa akichorwa katika kipindi ambacho alikuwa kijijini. Alimkumbuka Patrick kwa kila kitu katika maisha yake, kwa kifupi, hakutaka kuwa na mwanaume yeyote zaidi ya Patrick.

    Kama kawaida, wavulana hawakutaka kuwa nyuma, kila siku walikuwa wakimtaka Siwema ambaye alikuwa akivutia kadri siku zilivyozidi kwenda mbele. Siwema hakuonekana kuwa kushawishika kirahisi, kila siku alikuwa akitunza uaminifu wake kwa Patrick ambaye alimhesabia kuwa mume wake wa baadae.

    Getrude akamtafutia Siwema kazi ya kufagia katika ofisi moja ya Usafiri. Siwema alionekana kutisha katika uzuri wake. Watu wengi ambao walikuwa wakifika katika ofisi hizo kwa ajili ya kukata tiketi za kuelekea Dar es Salaam, Mwanza na mikoa mingine, walionekana kuvutiwa sana na Siwema.

    Siwema hakuonekana kukubaliana na mvulana yeyote ambaye alikuwa akimwambia kile ambacho kilikuwa moyoni mwake, hakuamini kama kulikuwa na mwanaume ambaye alikuwa akimpenda zaidi ya Patrick. Aliuapiza moyo wake kwamba isingewezekana kwake kumsaliti Patrick japokuwa hakuwa karibu nae.

    Bosi wa kampuni hiyo ya mabasi ya SARAFINA TRANSPORT hakuwa mbali. Fedha zake ndizo zilikuwa fimbo za kuwakamatia wasichana ambao walionekana kumsumbua. Alimjaribu Siwema kwa fedha zake lakini Siwema hauonekana kukubali, bado alikuwa akiitunza ahadi ya kutokumsaliti Patrick.

    Msimamo wa Siwema ukamfanya bosi Nhiga kukata tamaa. Hakumfuatilia tena Siwema zaidi ya kuanza kuchunguza ni mvulana gani ambaye alikuwa akimchanganya Siwema mpaka kumkatalia. Kila siku alifanya uchunguzi lakini hakumpata mvulana yeyote yule. Hakuonekana kukata tamaa, bado alikuwa akiendelea na uchunguzi wake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/









    *****











    Maria alionekana kuumia kupita kiasi, maneno ambayo aliambiwa na Hidifonce yalionekana kumuumiza kupita kawaida. Alirudi nyumbani huku machozi yakizidi kumtoka. Maria alionekana kubadilika, kila mtu ambaye alikuwa akimwangalia, alimuonea huruma japokuwa hawakujua ni kitu gani kilikuwa kinaendelea kwa wakati huo.

    Maria aliendelea kupiga hatua hadi nyumbani kwao ambapo akaingia ndani ya eneo la nyumba yao. Moja kwa moja akaelekea katika kibaraza cha nyumba yao na kutulia. Maneno ya Hidifonce yalikuwa yakijirudia rudia kichwani mwake, maumivu yaliogezeka zaidi na zaidi.

    Ingawa alikuwa hajawahi kutembea na mvulana yeyote lakini jina ‘malaya’ ndilo ambalo lilikuwa likijirudia kichwani mwake. Alijiona kama alikuwa msichana malaya kutokana na kile ambacho alikuwa amekifanya kwa Hidifonce

    Alijua kwamba alikuwa na haki zote za kupenda na kuhitaji kwa kuwa alikuwa na moyo wa nyama kama wengine, sasa kwa nini hakupewa nafasi ya kusikilizwa zaidi? Kila alichokuwa akikifikiria mahali hapo, bado alijiona kuumia kupita kiasi, moyo wake ulikuwa katika maumivu makali hata zaidi ya kupigwa na msumari wa moto moyoni.

    “Kwa nini hautaki kunielewa Hidifonce? Kwa nini unauumiza moyo wangu namna hii?” Maria alijiuliza lakini alikosa jibu.

    Akainuka mahali hapo na kuelekea ndani huku akionekana kuwa mpweke kupita kawaida. Ndani hakukukalika vizuri, kila wakati alikuwa akishika kalamu yake na kuandika jina la Hidifonce kiganjani. Moyo wake ulikuwa katika mapenzi makubwa ambayo hakujua kama kulikuwa na mtu ambaye alikuwa na mapenzi kama aliyokuwa nayo yeye.

    Akatamani kumpigia simu Hidifonce lakini hakuwa na namba yake jambo lililomfanya kutulia huku akiiangalia simu yake.

    “Naomba uwe wangu Hidifonce.....naomba uwe pamoja nami” Maria alijisemea huku machozi yakianza tena kumlenga.











    ******









    Alijulikana kwa jina la Gabriel Smith, mchungaji ambaye alikuwa akitokea katika nchi ya Marekani ndani ya jiji la New York. Mchunngaji Smith alikuwa na kanisa kubwa kuliko kanisa lolote katika jiji la New York. Kila siku kazi yake ilikuwa ni kuhubiri Injili katika sehemu mbalimbali duniani.

    Hakuwa akitulia kanisani kwake, mara kwa mara alikuwa akisafiri kuelekea katika nchi mbalimbali kuhubiri Injili. Katika kila nchi ambayo alikuwa akienda, wagonjwa waliponywa na hata wenye shida mbalimbali waliombewa.

    Jina lake likawa kubwa miongoni mwa wachungaji wakubwa duniani kama Benni Hinni, Td Jakes na wahubiri wengine. Miujiza mbalimbali ambayo ilikuwa ikifanyika katika mikutano mbalimbali aliyokuwa akihubiri ndio ambayo ilimfanya kujulikana zaidi.

    Katika maisha yake alibahatika kupata watoto watatu tu, wa kwanza alikuwa James ambaye alikuwa mwanasheria wa kujitegemea na ambaye alianzisha kampuni yake mwenyewe nchini Marekani. Wa pili alikuwa Mickey ambaye alikuwa akicheza mchezo wa kikapu katika timu ya Heart nchini Marekani na wa mwisho alikuwa Lydia ambaye bado alikuwa akiishi nae.

    Katika maisha yake yote, mchungaji Smith alikuwa na mke mmoja ambaye alipata nae watoto hao wote, mwanamke huyu aliitwa Elizabeth.

    Elizabeth alionekana kuwa kila kitu katika maisha yake, alimpenda mwanamke huyu kuliko mwanamke yeyote katika dunia hii kwani yeye ndiye ambaye alikuwa akimpa furaha kila siku na kujiona mtu muhimu katika dunia hii.

    Kila alipokuwa akisafiri kuelekea katika mikutano mbalimbali ya kimataifa, mchungaji Smith alikuwa akienda sambamba na mkewe, Elizabeth. Ingawa walikuwa na umri mkubwa lakini mapenzi yao bado yalikuwa yakionekana kuwa makubwa tofauti na wale watu ambao walikuwa wameanza uhusiano katika siku chache zilizopita.

    Ukarabati wa eneo la kaburi la Nyerere ulikuwa umetangazwa katika vituo mbalimbali duniani. Kaburi lile lilikuwa limefanyiwa ukarabati na kuwa sehemu mojawapo ya kufanyia utalii kwa ajili ya kumbukumbu ya kumuenzi Baba wa Taifa.

    Mchungaji Smith hakutaka kubaki nchini Marekani, nae akatamani kwenda huko kuangalia ukarabati huo ambao ulikuwa umefanyika.

    Kwa kipindi kirefu sana alikuwa akimfahamu vilivyo marehemu Nyerere. Alipokuwa shuleni hasa chuoni miaka ishirini iliyopita, alikuwa akisoma mambo mengi kuhusu mtu huyo. Aliimpenda sana hasa na moyo mkubwa wa kujitoa aliokuwa nao katika kuutafuta uhuru wa nchi ya Tanganyika pamoja na nchi nyingine za jirani.

    Mchungaji Smith akajiona kuwa na umuhimu wa kwenda Tanzania kwa ajili ya kuona kile ambacho kilikuwa kimetangazwa na ambacho kilitakiwa kufanyika katika siku ya tarehe 14 mwezi wa 10 mwaka 2000.

    Kwa kuwa binti yake, Lydia alikuwa nyumbani, akaamua kusafiri nae na kuelekea katika nae nchini Tanzania pamoja na mkewe. Akaanza kupiga simu kwa rafiki yake ambaye walikuwa wamezoeana kwa kipindi kirefu, mtanzania Gibson ambaye mara kwa mara alikuwa akimpokea kila alipokuwa akielekea nchini Tanzania.

    Mara baada ya kufika nchini Tanzania kisiri pasipo watu wa makanisa kujua kama yuko nchini Tanzania, safari ya kuelekea mkoani Musoma katika kijiji cha Butiama kuanza. Hawakutaka kupanda ndege, walitaka kusafiri kwa kutumia gari kwani walitaka kupitia katika mbuga kubwa ya wanyama ambapo hapo wangechukua vyumba na kisha kuendelea na safari yao na baadae kurudi katika hoteli hiyo.









    *****







    Mchungaji Smith, mkewe, Lydia na walinzi walikuwa wakiendelea kupiga hatua kulekea kule ambapo Lydia alikuwa akidai kwamba alimwona mzimu. Walitembea kwa hatua za haraka haraka huku mchungaji Smith akiwa na hamu ya kuuona mzimu wenyewe ambao Lydia alikuwa ameuona.

    Walifika katika gari lile, boneti la gari lilikuwa wazi. Lydia hakusogea zaidi ya kunyooshea gari lile kidole. Gibson na mkewe, Beatrice wakafika mahali hapo na kutaka kujua ni kitu gani kilichokuwa kinaendelea. Mchungaji Smith akaanza kupiga hatua kuelekea kule kulipokuwa na gari lile, alipofika akachukua tochi yake na kumulika garini.

    Patrick alikuwa akionekana amelala garini huku akionekana kutokujitambua kabisa. Mchungaji Smith akasogea karibu zaidi na zaidi na kuupeleka mkono wake ndani ya boneti lile la gari na kumgusa Patrick huku akijaribu kumtingisha lakini Patrick hakushtuka.

    Mchungaji Smith akalifungua vizuri boneti lile la gari na kisha kujaribu kumtoa Patrick. Gibson akaja na kusaidiana nae. Mwili mzima wa Patrick ulikuwa umejaa mavumbi, alionekana kutisha kupita kawaida. Walinzi waliokuwa mahali pale wakambeba Patrick mpaka katika sakafu na kuanza kupepea.

    Patrick alikuwa kimya, alionekana kupoteza fahamu kutokana na vumbi alilokuwa amelipata pamoja na udogo wa hewa ambao alikuwa akiupata. Wakaanza kumpa huduma ya kwanza huku mchungaji Smith akiomba Mungu Patrick afumbue macho yake na kuangalia tena.

    Kama Patrick angekufa kwa wakati huo, tayari alijiona kuwa katika wakati mgumu kwa kuwa kusingekuwa na uthibitisho wowote kama Patrick alikuwa ameingia mwenyewe katika boneti lile. Watanzania wote wangeamini mchungaji Smith ndiye ambaye alkuwa amemuweka Patrick katika boneti lile.

    “Hivi kuna hospitali hapa?” Gibson aliwauliza walinzi.

    “Hospitali! Hospitali mbugani! Wala hakuna” Mlinzi mmoja alijibu.

    “Kwa hiyo hakuna?”

    “Ndio. Labda mpite mbuga kwa mbuga mpaka Arusha” Mlinzi aliwaambia.

    Baada ya kumpa Patrick huduma ya kwanza, moja kwa moja safari ya kuelekea jijini Arusha ikaanza. Safari ilikuwa ni mbuga kwa mbuga lakini gari lilikuwa likiendeshwa kwa mwendo wa kasi pasipo kujali mashimo ambayo yalikuwa katika barabara hiyo ya vumbi.

    Bado Patrick alikuwa hajafungua macho, aliendelea kulala katika usingizi wa kifo. Vumbi jingi lilikuwa limeingia katika mapafu yake, hewa ndogo ambayo alikuwa akiipata kule katika boneti la gari ndilo ambayo ilikuwa imempa hali mbaya zaidi.

    Mpaka wanafika Arusha, tayari ilikuwa imetimia saa kumi alfajiri. Moja kwa moja wakaanza kuelekea mjini mpaka katika hospitali ya Kilutheri ya Selian ambako Patrick anapelekwa hadi katika chumba cha peke yake na kupewa huduma.

    Ndani ya masaa mawili, Patrick anarudiwa na fahamu. Kila mmoja akaonekana kufurahia, hawakuamini kama Patrick angeweza kurudiwa na fahau kwa haraka namna ile.

    “Tunamshukuru Mungu” Mchungaji Smith alisema.

    Wote wakashikana mikono na kuanza kumshukuru Mungu. Sala ya shukrani iliendelea mahali hapo kwa dakika kadhaa. Muda wote huo Patrick hakuwa akielewa ni kitu gani kilikuwa kinaendelea mahali hapo, akabaki akishangaa tu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya kuulizwa ni kitu gani ambacho kilikuwa kimetokea, Patrick anaanza kueleza kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea katika maisha yake. Kila mtu hakuamini kile ambacho alikuwa amekisikia kutoka kwa Patrick. Bi Rachel hakuweza kuvumilia, akabaki akilia tu.

    “Inasikitisha” Mchungaji Smith aliwaambia.

    “Lakini ni kijana mdogo sana”

    “Ndio. Ni lazima tumsaidie. Ni lazima uondoke nae Gibson. Ishi pamoja nae ili asiwe katika hali hii ya mawazo kwani kichwa chake naamini hakiko sawa. Jaribu kumfariji kila siku. Mimi na mke wangu tunaahidi kumsaidia katika kipindi ambacho atakuwa kwako” Mchungaji Smith aliwaambia.

    “Sawa mchungaj. Hakuna wasiwasi” Gibson alisema.

    Mchungaji Smith hakuendelea kukaa mahali hapo. Safari ya kuelekea nchini Marekani ikaanza. Walichukua ndege kutoka Arusha ambayo iliwapeleka mpaka Dar es Salaam ambako wakachukua ndege ya shirika la Emirates na kuelekea Marekani ambako kulikuwa na mkutano mkubwa katika jiji la Los Angels.

    Ndani ya ndege bado walikuwa wakikumbuka historia ya maisha ya Patrick ambayo aliwaambia, kila mmoja akaonekana kuguswa na historia ya maisha ya Patrick. Wakaiahidi mioyo yao kumsaidia Patrick katika hali yoyote watakayokuwa nayo.

    “Ni lazima tumsaidie. Ni lazima tutume dola elfu tano kila mwezi kwa ajili yake” Mchungaji Smith alimwambia mkewe.

    “Kweli kabisa. Ni lazima tufanye hivyo. Najua Mungu ana makusudi na maisha yake” Bi Rachel alisema.

    Kiasi ambacho kilikuwa kimetajwa kwa ajili ya kummsaidia Patrick kilikuwa kiasi kikubwa cha fedha hasa kama kingewekwa katika thamani ya fedha ya kitanzania.

    Kiasi cha zaidi ya shilingi milioni tano ndicho ambacho kilikuwa kimepangwa kwa ajili ya kumsaidia Patrick ambaye alitakiwa kuishi nyumbani kwa Gibson jijini Dar es Salaam. Mchungaji Smith na mkewe, Rachel walikuwa wakiendelea na safari yao huku mioyo yao ikijua kwamba huku Tanzania kulikuwa na mtu ambaye waliahidi kwa mioyo yao yote kumsaidia.



    **********************************************************





    Hidifonce alitulia kitandani, hakuonekana kufurahishwa na kile ambacho alikuwa amemfanyia Maria. Alijua fika kuwa moyo wa binti huyo ulikuwa katika mapenzi mazito juu yake. Akaanza kuyajutia maneno ambayo alikuwa ameongea mbele ya Maria, hata yeye hakuonekana kufurahishwa nayo.

    Hidifonce akainuka na kuanza kutembea tembea chumbani kwake huku akionekana kuwa na mawazo juu ya Maria. Muda wote alikuwa akipigapiga mikono yake huku macho yake yakiangalia darini. Alikuwa katika hali ile kwa muda fulani, akarudi tena kitandani.

    “Haiwezekani, ni lazima nimuite” Hidifonce alisema na kisha kutoka nje ya chumba kile.

    Moja kwa moja akamtafuta Shania na kisha kumtuma kwenda kumuita Maria. Shania akaondoka mahali pale na kuelekea nyumbani kwa mchungaji Christopher ambako baada ya dakika kumi, akarudi pamoja na Maria ambaye alikuwa katika hali iliyojaa furaha.

    Moja kwa moja akaingia katika chumba cha Hidifonce na kutulia. Macho yake yalikuwa yakiangalia chini kama kawaida yake, alikuwa akijisikia aibu kiasi ambacho hakuweza kukutanisha macho na Hidifonce. Hidifonce alikuwa ametulia huku macho yake yakiendelea kumwangalia Maria, akaanza kujisogeza karibu nae.

    Mkono wake akaupeleka shavuni mwa Maria na kuanza kulishika shika shavu lake. Maria akaanza kusisimka, mguso wa Hidifonce ukaonekana kuanza kumletea hali ya tofauti mwilini mwake. Hidifonce akaonekana kugundua hali ile, akazidi kusogea karibu zaidi. Akamgeuzia Maria upande wake na kuanza kumwangalia vizuri usoni.

    Hidifonce akaanza kuusogeza uso wake karibu na uso wa Maria, kwa kiasi fulani Maria akatamani kuurudisha nyuma uso wake lakini akashindwa kutokana na Hidifonce kumvutia kwake zaidi. Maria akashtukia lipsi za Hidifonce zikiwa karibu na lipsi zake.

    Mapigo ya moyo yakaanza kumdunda, mzunguko wa damu ukaongezeka mwilini mwake, woga ukaanza kumwingia. Pumzi ambayo ilikuwa ikitoka kwa Hidifoce tayari ilikuwa ikimpata vilivyo. Ghafla akashtukia mikono yake ikishikwa na Hidifonce, Maria akaonekana kulegea kupita kiasi hali iliyomfanya Hidifonce kuanza kumlaza kitandani.

    Ghafla kinywa cha Hidifonce kikawa kinywani mwa Maria na kitendo cha kubadilishana mate kuanza mara moja. Kadri muda ulivyokuwa ukizidi kwenda na kitendo kile kuzidi kuchukua nafasi, Maria akajikuta akianza kutoa miguno ambayo alikuwa na uhakika kwamba hakuwahi kuitoa kabla maishani mwake.

    Hidifonce akaanza kuipitisha mikono yake mwilini mwa Maria ambaye alihisi vijidudu vikianza kumtembelea mwilini. Maria akaonekana kuchoka pasipo kukimbia, akaonekana kuwa tayari kwa kitu chochote ambacho kilikuwa kikitaka kuchukua nafasi mahali hapo.

    Hidifonce akaanza kumchojoa Maria nguo zake. Akaanza na sketi ambayo alikuwa ameivaa, Maria akabaki na skin tight tu. Hidifonce akaanza utundu wake wa kuyachezea mapaja ya Maria ambaye alibaki akilalamika kwa raha. Hidifonce hakutaka kuacha, aliendelea zaidi na zaidi na kuanza kuamia juu.

    Blauzi ambayo alikuwa ameivaa ikaanza kufunguliwa vifungo, nguo yake ya ndani ambayo ilikuwa imeyaziba matiti yake ndio ambayo ilikuwa imebakia. Hidifonce akaanza kuipandisha nguo nguo ile, tumbo laini lililokuwa linavutia lilikuwa linaonekana vizuri.

    Hidifonce akaanza utundu wake katika tumbo hilo mpaka akakisifikia kitov na kuanza kukichezea alivyotaka. Kelele za mahaba zikazidi kusikika kutoka kwa Maria, muda wote alikuwa akikunja kunja vidole vyake vya miguuni huku akilivuta vuta shuka lililokuwa limetandikwa.

    Katika kipindi hicho hakukumbuka kama alikuwa mwanakwaya kanisani kwao wala kukumbuka kama alikuwa mtoto wa mchungaji. Utundu ambao alikuwa akiufanya Hidifonce mwilini mwake ulionekana kumsahalisha yote ambayo yalikuwa yakimhusu.

    Maria akalegea kabisa kana kwamba mtu ambaye alikuwa amepoteza fahamu. Hidifonce hakuonekana kuwa na haraka, aliendelea kumchezea Maria alivyotaka. Maria akabakia mtupu hali iliyompelekea nae Hidifonce kuvua nguo zake katika kasi ambayo hata yeye mwenyewe ilikuwa ikimshangaza.

    “Niacheeeeeeee.....” Maria alimwambia Hidifonce kwa sauti ya chini iliyojaa mahaba.

    “Niacheeeeee” Maria aliendelea kumwambia Hidifonce.

    Maria alitaka aachwe lakini matendo yake kitandani hapo hayakumaanisha kabisa juu ya kile ambacho alikuwa akikisema. Alikuwa akimvutia Hidifonce kwake zaidi huku akitamani Hidifonce aendelee kufanya kile ambacho alikuwa akikifanya.

    “Mamaaaaa...Unaniumi....” Maria alijikuta akipiga kelele mara baada ya kusikia maumivu chini ya kitovu.

    Damu zilikuwa zinamtoka na kuanza kuchirizika katika mapaja yake. Akaanza kukuruka na kujaribu kumsukuma Hidifonce lakini Hidifonce hakutaka kutoka. Bado alikuwa akiendelea kupiga pushapu hali ambayo ilimfanya Maria kupiga kelele zaidi.

    Ingawa mwanzo alikuwa akimsukuma Hidifonce, ghafla hali ikaonekana kuanza kubadilika, akaanza kumvutia Hidifonce kwake huku akiizungusha mikono yake mgongoni mwa Hidifonce.

    Hiyo ndio ilikuwa siku iliyobadilisha kila kitu, hapo ndipo maisha ya Maria yakaonekana kubadilika na kuigia katika mapenzi makubwa na Hidifonce. Akatokea kumpenda Hidifonce kuliko mwanaume yeyote maishani mwake. Maria akawa haambiwi wala hasikii mbele ya Hidifonce. Mara kwa mara alikuwa akivuiwa chupi yake na kufanyiwa mchezo ule ambao ulikuwa ukimbadilisha kupita kiasi.

    Umbo lake ambalo lilikuwa likionekana kuvutia likabadilika na kuvutia zaidi. Hipsi zake zikaongezeka na hata tumbo lake kujipanga vilivyo. Maria akaanza maringo, hakujiona kuwa tofauti na wasichana wengine ambao walikuwa wameuanza mchezo ule kitambo. Kila siku alikuwa chumbani kwa Hidifonce huku akimpikia, na kila Hidifonce aliporudi, ngono ilikuwa ikiendelea kama kawaida.

    *****

    Mara baada ya Patrick kujisikia nafuu, akaruhusiwa kutoka hospitalini ambako Gibson na mkewe wakamchukua na kwenda nae jijini Dar es Salaam. Gibson na mkewe walitaka kumpa Patrick kila kitu ambacho alikuwa akikihitaji katika maisha yake.

    Kila mwezi mchungaji Smith pamoja na mkewe, Bi Rachel walikuwa wakimtumia fedha Gibson kiasi cha zaidi ya shilingi milioni saba kwa ajili ya kumtunza Patrick ambaye kadri siku zilivyozidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo alizidi kubadilika.

    Patrick akaonekana kuwa na afya tena, mwili wake ulikuwa umeongezeka kupita kiasi. Japokuwa alikuwa na mawazo juu ya baba yake na mama yake lakini Patrick alijitahidi kukaa na vijana wenzie kwa ajili ya kuongea mambo tofauti tofauti hali iliyomtoa katika msongo mkubwa wa mawazo.

    Siku ya Krismasi ilipofikia, matokeo ya darasa la saba yakatolewa. Patrick alikuwa amefanya vizuri kuliko wote katika shule ambayo alikuwa amemalizia elimu ya msingi. Alama zake nyingi alizozipata ndizo ambazo zilimfanya kujiunga na shule ya Sekondari ya wavulana ya Kibaha.

    Kila siku Patrick alionekana kuwa na furaha, hatua ya yeye kuchaguliwa na kujiunga na shule hiyo kulionekana kumpa furaha kupita kawaida. Kila siku aliziona ndoto zake za kuwa mwanasheria zikianza kutimia. Ila pamoja na hayo yote, alitamani baba yake na mama yake wawe mahali hapo kwa ajili ya kuyaona mafanikio yake.

    Maandalizi yakaanza kufanyika, Patrick akanunuliwa kila kitu ambacho kilikuwa kikihitajika shuleni. Mavazi mazuri, begi kubwa languo pamoja na mahitaji yake mengine yalikuwa ymewekwa tayari kwa ajili ya kwenda shule na kuanza kidato cha kwanza.

    Masomo yalipoanza, Patrick alionekana kuwa tofauti na wanafunzi wengine. Shuleni alikuwa akionekana mpweke kupita kawaida. Kusoma kwake likawa ni jambo gumu ambalo lilipelekea kufeli masomo yake kuliko mwanafunzi yeyote aliyekuwa akisoma shuleni hapo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Muda mwingi Patrick alikuwa akiutumia kwa kuchora pica mbalimbali za viongozi wa nchi hii. Uchoraji wa Patrick ukaonekana kumsisimua kila mtu ambaye alikuwa akiziangalia picha zake. Hakukuwa na utofauti wowote kama ungeonyeshwa picha ambayo ilipigwa na kamera na picha ambayo aliichora Patrickk.

    Patrick alionekana kuwa na uwezo mkubwa sana wa uchoraji ambao aliiwakilisha shule yake katika kila mashindano ya uchoraji yalipofanyika. Jina lake likaanza kujulikana katika shule zote, kipaji chake cha uchoraji kilionekana kumvutia kila mtu.

    Waandishi wa habari wakaanza kumiminika katika shule ya Sekondari ya Kibaha kwa ajili ya kuziangalia picha ambazo zilikuwa zimechorwa na Patrick. Kila mwandishi alitaka Patrick afanye kazi pamoja nao kwa ajili ya kuchora picha mbalimbali ambazo zingekuwa zikichapishwa magazetini.

    Waandishi wa habari kwa kuyawakilisha magazeti yao, wakaamua kuweka mikataba na Patrick ya kuchora picha kadhaa na kuzichapa katika magazeti yao. Kila mtu ambaye aliyanunua magazeti yale na kuziangalia picha zile, alishindwa kuamini kama picha zile zilikuwa zimechorwa.

    Jina a Patrick likaaanza kukua, akaanza kushika kiasi kikubwa cha fedha mkononi mwake. Masomo akawa ameyasahau kabisa hali iliyomfanya kufeli kupita kawaida. Kila mtihani ambao ulikuwa ukifayika shuleni, Patrick alifeli vibaya.

    “Kwa hiyo tumfanye nini?” Mwalimu wa Taaluma aliwauliza walimu wenzake katika mkutano wa walimu uliofanyika suleni hapo.

    “Tumuiteni na kumuonya. Najua atabadilika” Mwalimu Mkuu aliwaambia.

    Patrick aliitwa na kuonywa kutokana na kile ambacho kilikuwa kikiendelea. Aliambiwa asome sana na mambo ya kuchora ayafanye baadae. Patrick alionekana kukubali lakini hakukuwa na mabadiliko yoyote ambayo yalitokea. Kila siku Patrick alikuwa akiendelea kuchora zaidi na zaidi huku picha zake akiziuza katika magazeti mbalimbali.

    “Haina jinsi. Ni lazima tumsimamishe shule” Mwalimu wa Taaluma alisema.

    Hiyo ndio ilikuwa hatua ambayo ilichukuliwa, Patrick akasimamishwa shule. Patrick alijiona kupewa uhuru mkubwa zaidi. Kila siku nyumbani alikuwa akichora picha, hakuonekana kuijali elimu hata mara moja japokuwa alikuwa amewekewa kiasi kikubwa cha fedha katika akaunti yake na kiasi hicho kilikuwa kikiongezeka kadri miezi ilivyokuwa ikisonga mbele.

    Baada ya mwezi kumalizika, Patrick akaruhusiwa tena kurudi shuleni. Patrick hakuonekana kuwa na mabadiliko yoyote yale, bado alikuwa akiendelea kchora, tena wakati huu alikuwa ameongeza kasi zaidi.

    Aliwachora walimu mbalimbali shuleni hapo, picha ambazo walimu hao walizichukua na kuziweka katika flemu na kuzitundika ukutani. Picha zile zilionekana kuwa na uhalisia kabisa, hazikuonekana kuwa na utofauti wowote na zile za kupigwa kwa kamera.

    Bado maendeleo yalikuwa mabaya. Patrick hakuwahi kupata alama zaidi ya kumi katika mitihani yake yote. Kitu ambacho alikuwa akiking’ang’ania katika maisha yake kilikuwa ni kipaji cha uchoraji ambacho aliamini kuwa kingeweza kumtoa katika maisha yake.

    “Ni lazima tumfukuze shule. Ni kweli anaipa shule zawadi mbalimbali za uchoraji, ila hapa amekuja kusoma na si kuchora. Kwa sababu maendeleo yake hayaridhishi, basi ni lazima tumfukuze shule” Mwalimu mkuu aliwaambia walimu wenzake.

    Hivyo ndivyo ilivyokubaliwa. Patrick akafukuzwa shuleni hapo. Gibson na Beatrice hawakutaka kumsema Patrck kutokana na maisha ambayo alikuwa amepitia. Kutokana na kutotaka kusoma na badala yake kutaka kuchora, Gibson akaamua kumpigia simu mchungaji Smith ambaye aionekana kusikitishwa na kile ambacho kilikuwa kimetokea katika maiaha ya Patick.

    “Unasema kweli amefukuzwa shule?”

    “Ndio”

    Mchungaji Smith na mkewe hawakuwa na jinsi, wakaanza kuyakabidhi maisha ya Patrick mikononi mwa Mungu. Tayari wakaona roho ya kutotaka maendeleo ilikuwa imemkumba Patrick hali iliyompelekea kutotaka kusoma kabisa. Kila siku walikuwa wakifanya maombi ili Mungu Ambadilishe Patrick na kuigeukia Elimu.



    *********************************************************



    “Hali imeongezeka mchungaji. Patrick bado anaendelea kuchora na si kusoma. Yaani tunashindwa kujua tufanye nini” Sauti ya Gibson ilisikika simuni.

    Patrick alionekana kushindikana kabisa. Kila siku alikuwa mtu wa kuchora tu, hakutaka kusoma kabisa. Maisha ya nyuma ambayo alikuwa amepitia ndio ambayo yalikuwa yameondoa hamu yake ya kusoma kabisa. Hakuona kama kulikuwa na sababu ya kuendelea kusoma na wakati alikuwa akiishi katika hali ya mawazo mengi.

    Waandishi wa habari wakazidi kumiminika zaidi. Picha alizokuwa akizichora Patrick zilionekana kumchanganya kila aliyekuwa akiziangalia. Patrick akawa na jina kubwa kwa watu wote ambao walikuwa wakimzunguka, katika vyombo vingi vya habari hasa vya magazeti, Patrick alikuwa akijulikana vilivyo.

    “Kwa hiyo hataki kusoma kabisa?” Mchungaji Smith aliuliza.

    “Ndio”

    “Nakuja Tanzania kwa ajili yake. Nitamchukua na kumleta huku ili nimpeleke katika shule yenye vipaji mbalimbali” Mchungaji Smith alimwambia Gibson na simu kukatwa.

    Moja kwa moja Gibson akampa taarifa zile Patrick. Patrick akaonekana kufurahia sana. Hakufurahi kwa sababu alikuwa akielekea Marekani siku si nyingi, bali alikuwa akifurahi kwa sababu alikuwa akipelekwa katika shule ya kukuza vipaji, huko hakukuwa na masomo tena kama jinsi ambavyo ilivyokuwa Tanzania.

    Baada ya wiki moja mchungaji Smith akaingia nchini Tanzania. Akapata muda wa kuongea na Patrick huku Gibson akiwa mkalimani wake. Mipango ya Patrick kusafirishwa ikaanza. Kila kitu kilipokuwa tayari, Patrick alikuwa katika ndege ya shirika la American Airlines wakielekea Marekani.

    Kitendo cha kupanda ndege kilimpa faraja kupita kiasi. Hakuamini kama muda huo alikuwa amepanda ndege, usafiri ambao hakuwa akiufikiria hata siku moja kuwa angeutumia. Moyo wake ulikuwa na furaha kupita kawaida, ila kila alipokuwa akimfikiria Siwema, furaha ikatoweka kwani alijua kwamba alikuwa akienda kuishi mbali na Siwema.

    Walitumia zaidi ya masaa kumi na nane angani pamoja na kubadilisha ndege jijini Uholanzi na ndipo ndege ikaanza kutua katika uwanja wa ndege wa JFK yaani John F. Kennedy uliokuwa katika jimbo kubwa la kibiashara la New York.

    Mara baada ya ndege kusimama, abiria wakaanza kuteremka. Patrick alibaki akiangalia majengo marefu ambayo yalikuwa yakionekana vizuri machoni mwake. Baridi ambalo lilikuwa likimpiga ndilo ambalo lilimfanya kuanza kupiga hatua kuelekea kule katika jengo la uwanja ule.

    Kila kitu ambacho Patrick alikuwa akikiangalia kwa wakati huo alibaki akishangaa tu. Idadi kubwa ya majengo marefu pamoja na usafi mkubwa uliokuwa ukinekana ulimfanya Patrick kubaki na mshangao. Kila wakati alikuwa akiangalia katika kila kona, hakuonekana kujisikia huru kabisa, alionekana kuogopa kupita kiasi.

    Mara baada ya mizigo kukaguliwa, moja kwa moja wakaanza kutoka nje ya jengo lile ambako Bi Rachel alikuwa uwanjani pale na kuwapokea.

    Wote wakaingia garini na dereva kushikilia usukani. Muda wote Patrick alikuwa akiagalia nje dirishani. Bado mambo mengi mageni yalikuwa yakionekana machoni mwake.

    Moja kwa moja dereva akachukua barabara ya St’ Johnson 23 ambayo ilikuwa ikielekea katika upande wa magharibi wa jimbo hilo huku lengo lae likiwa ni kufika katika jiji la Brookyn, jiji mojawapo lililokuwa likikaliwa na watu matajiri katika jimbo hilo.

    Baada ya kufika umbali wa kilometa moja, dereva akakata kona kushoto na kuchukua barabara ya Alexander 35 ambayo bado ilikuwa ikiendelea na uboreshaji wa kuongeza barabara ya njia saba. Maneno makubwa yaliyosomeka ‘WELCOME IN BROOKLYN CITY’ yalikuwa yakionekana katika bango kubwa lililokuwa mbele katika njia kubwa lililokuwa limewekwa katika maghorofa makubwa mawili.

    Safari yao iliendelea zaidi na zaidi, barabara nyingi zilikuwa zikionekana njiani ambako wakaamua kuchukua barabara moja ambayo ilikuwa ikiwapeleka mpaka katika mji mdogo wa Port Elizabeth. Baada ya dakika kadhaa, gari likasimama nje ya nyumba moja kubwa na ya kifahari.

    Nyumba ilionekana kuwa kubwa sana. Geti likajifungua na gari kuingia. Magari zaidi ya kumi na mbili yalikuwa yakionekana yakiwa yamepakiwa pembeni. Bwawa kubwa la kuogelea lilikuwa likionekana machoni mwa Patrick.

    Patrick alibaki akishangaa, hakuamini kama duniani kulikuwa na nyumba kubwa namna ile. Sanamu kubwa ya Yesu akiwa msalabani ilikuwa ikionekana pembeni kabisa na nyumba ile. Akaanza kukazia macho katika eneo moja ambalo lilikuwa na miti kadhaa, wanyama walikuwa wakionekana huku neno ‘Zoo’ likionekana vizuri.

    Wote wakateremka, Patrick akakaribishwa katika nyumba hiyo, maneno mbalimbali yalikuwa yakionekana yakiwa yameandikwa ukutani. Maneno hayo yote yalikuwa ni mistari kadhaa ambayo ilikuwa imeandikwa katika Biblia. Patrick akashtuka mara baada ya kuangalia huku na kule na kugundua kwamba kulikuwa na kamera katika maeneo mengi ya nyumba ile.

    Hapo ndipo ambapo maisha ya Patrick yalipoanza kwa mara nyingine. Taratibu akaanza kujifunza lugha ngeni ya kingereza na baada ya mwezi mmoja, akaweza kuifahamu lugha hiyo. Patrick akazoeleka na kila mtu katika nyumba hiyo, muda wote alikuwa akionekana kuwa na furaha kupita kiasi.

    Mwezi mwingine ulipofikia, Patrick akaandikishwa katika shule ambayo ilikuwa ikikuza vipaji mbalimbali iliyoitwa Vanguard ambayo ilikuwa katika jiji la Florida. Mara ya kwanza alikuwa mgeni kabisa, kila mtu kwake alionekana mpya.

    Kila siku alikuwa akikaa peke yake mpaka pale msichana wa kizungu, Vanessa alipoanza urafiki nae. Kila siku Vanessa alikuwa karibu na Patrick, walisoma wote huku hata wakati wa mapumziko wakienda kula chakula pamoja.

    Kutokana na umaarufu aliokuwa nao mchungaji wa Kimataifa, Smith, Patrick alikuwa akiheshimiwa sana shuleni hapo. Patrick alionekana kuwa mchangamfu sana kwa Vanessa hali ambayo ilimfanya kupata marafiki wengi ambao walisikia juu ya uchangamfu wa Patrick kutoka kwa Vanessa.

    Kila mwanafunzi shuleni hapo alikuwa akitaka kukaa karibu na Patrick huku wengine wakijiuliza juu ya kipaji ambacho alikuwa nacho kilichomfanya kuletwa katika shule hiyo. Hakuwa akielekea katika vikundi vya nyimbo wala michezo yoyote, muda wote alikuwa darasani tu.

    “What is your talent, Patrick? (Kipaji chako ni nini, Patrick?)” Vanessa alimuuliza Patrick ambaye hakujibu kitu zaidi ya kutbasamu tu.

    “What do u think? (Unafikiria nini?)”

    “Nothing. Are you a singer? Actor? Pleaseee Patrick..tell me (Sifikirii kitu. Wewe ni muimbaji? Muigizaji? Tafadhari Patrick..naomba uniambie)” Vanessa alimwambia Patrick.

    “Do you real want to know Van? (Kweli unataka kujua Van?)” Patrick aliuliza huku akimwangalia Vanessa kwa uso uliojaa tabasamu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Yeah” Vanessa alijibu.

    Patrick akachukua begi lake ambalo lilikuwa na madaftari kadhaa na kuliweka mezani. Akalifungua huku Vanessa akitaka kujua Patick alitaka kumuonyeshea kitu gani. Patrick akatoa bahasha moja na kisha kumkabidhi Vanessa.

    Vanessa akaifungua bahasha ile, akakutana na karatasi kubwa ambayo akaitoa na macho yake kutua katika picha moja. Vanessa akaonekana kushtuka, macho yake yakaongezeka kwa ukubwa kutokana na kuwa na mshangao mkubwa.

    “Where did u get my picture? (Umeipata wapi picha yangu?)” Vanessa aliuliza huku akishangaa. Maswali yakaanza kumiminika kichwani mwake, kamwe hakuwahi kumuonyeshea wala kumpa Patrick picha yoyote ile, kitendo cha Patrick kuwa na picha yake kilionekana kumshtua.

    “I drew it (Niliichora)” Patrick alitoa jibu lililomshangaza Vanessa.

    “What......? “

    “I drew it yesterday (Niliichora jana)” Vanessa akabaki kuwa na mshangao, hakuamini hata kidogo kama picha ile ilikuwa imechorwa.

    Mara akainuka kutoka katika kiti kile na kuanza kuelekea nje huku akiruka ruka. Kila mwanafunzi alibaki akimshangaa Vanessa ambaye akaanza kuipitisha picha ile kwa kila mwanafunzi ambaye alikutana nae huku jina la Patrick likitajwa mara kwa mara kutoka kichwani mwake.

    Ni ndani ya dakika thelathini, kila mwanafunzi alikuwa amejua ni kitu gani ambacho alikuwa amekifanya Patrick. Kwa wanafunzi ambao hawakuwa wakimfahamu Patrick kwa kumwangalia zaidi ya kumsikia wakataka kumuona kwa macho yao. Picha ambayo alikuwa ameichora ilionekana kumdatisha kila mtu. Hakukuwa na mtu ambaye aliamni kama picha ile ilikuwa imechorwa.

    Wanafunzi wengi pamoja na walimu wakaanza kuelekea katika darasa lile huku wakiongozana na Vanessa ambaye alionekana kuwa na furaha kupita kiasi. Walipofika darasani, Patrick hakuwepo, alikuwa amekwishaondoka.

    “Where is Patric? (Patrick yuko wapi?)” Mwalimu mmoja kati ya walimu wanne waliokuja darasani mule pamoja na wanafunzi wasiopungua hamsini aliwauliza wanafunzi ambao waliwakuta katika darasa lile.

    “He left (Aliondoka)” Mwanafunzi mmoja alijibu.







    *****









    Mapenzi kati ya Hidifonce na Maria yalikuwa moto moto. Kila siku walikuwa pamoja na kufanya mambo tofauti tofauti yaliyokuwa yakihusu mahaba. Maria ndiye ambaye alionekana kuchanganyikiwa zaidi, kasi kubwa ya mapenzi ilikuwa imemkamata.

    Darasani hakusoma kabisa kwani muda mwingi alikuwa akimfikiria Hidifonce hali iliyomplekea kutofanya vizuri katika masomo yake. Alipoingia kidato cha nne, bado akili yake ilikuwa ikifikiria mapenzi zaidi hali iliyompelekea kufeli mitihani yake ya mwisho.

    Matokeo yale yalimfanya kutokuendelea na kisato cha tano, mchungaji Christopher na mkewe wakaamua kumuanzisha katika chuo kimoja ambako huko alikwenda kusomea kompyuta. Muda mwingi Maria bado alikuwa akiutumia kumfikiria Hidifonce, mapenzi bado yalikuwa yakiendelea kumchanganya.

    Japokuwa bado alikuwa akisomea kozi ya kompyuta lakini bado Maria hakuonekana kutulia kabisa, bado mapenzi yalikuwa yakiendelea kumchanganya kila siku. Alichukua muda wa miezi miwili, kutokana na kuwa na alama zilizokuwa zikiridhisha, akapelekwa katika chuo cha uwalimu katika wilaya ya Kasuru Mkoani Kigoma.

    Huko kidogo akaonekana kusoma, mawazo juu ya Hidifonce yalikuwa yakiendelea japokuwa hayakuwa kama kipindi ambacho alikuwa Dar es Salaam. Kila siku walikuwa wakiaidiana mambo mengi kuhusu maisha yao ya baadae, kila mmoja alitamani kuwa na mwenzake.

    Hali ikaanza kubadilika, mabadiliko ya mwili yakaanza kumtia wasiwasi Maria. Muda mwingi alikuwa akijisikia kichefuchefu hali iliyompelekea kupenda sana kula vitu vichachu. Maria alijua ni kitu gani ambacho kilikuwa kinaendelea mwilini mwake, tayari akajijua kwamba alikuwa mjauzito.

    Ingawa bado alikuwa akiendelea kuwa katika hali hiyo, alijitahidi sana kusoma kwani aliamini kama angefanikiwa basi mtoto wake ambaye alikuwa tumboni ni lazima angeishi maisha ambayo alitaka aishi. Taarifa za ujauzito wake akaamua kumpa Hidifonce ambaye akaonekana kushtuka kupita kiasi.

    “Mbona umeshtuka sasa?” Maria alimuuliza Hidifonce simuni.

    “Kulea. Unajua kuna kazi fulani nimeanza kuifanya, nimewaeleza ukweli kama sina mke wala mtoto” Hidifonce alimwambia Maria.

    “Sasa unafikiri tutafanyaje mpenzi?”

    “Nitaishi nawe ila kwanza acha nikamilishe hii kazi ambayo nimepewa”

    “Kazi gani mpenzi?”

    “Ya kawaida tu. Usijali. Nitakutaarifu” Hidifonce alimwambia Maria.

    Huo ndio ukawa mwisho wa kuongea na Hidifonce mwaka huo. Kila alipokuwa akimpigia simu, hakuwa akipatikana. Jambo hilo lilionekana kumuumiza sana Maria lakini hakuonekana kujali kitu chochote kile. Bado akili yake akaiweka katika kusoma.

    Baada ya miezi tisa, Maria akajifungua mtoto mzuri wa kike ambaye alimpa jina la Natalia. Natalia alionekana kuchukua kila kitu kutoka kwa mama yake. Sura yake iikuwa ikimvutia kila mtu ambaye alikuwa akimwangalia. Uzuri wa Natalia ukawapelekea watu kuona kuwa mtoto huyo angekuja kutisha sana katika miaka ya baadae.

    Alipomaliza masomo yake, akachaguliwa kufundisha katika shule ya msingi ya Kigoma. Kutokana na kuingiza fedha za kutosha kila mwisho wa mwezi, Maria akaanza kuyatengeza maisha yake na ya mwanae. Akapanga nyumba nzima maeneo ya Mji Mwema.

    Nyumba ilikuwa kubwa lakini ni watu wawili tu ndio ambao walikuwa wakiishi humo. Kila siku Maria alijitahidi kumlea Natalia katika maisha ambayo mtoto alitakiwa kulelewa. Baada ya kuona kwamba kazi zilikuwa nyingi, akaamua kumuajiri msichana ambaye akaanza kumsaidia kazi pale nyumbani kwake.

    Bosi wa shirika la Umoja wa Mataifa ambaye alikuwa akiishi karibu na nyumba aliyopanga Maria akatokea kumpenda Maria. Kila siku bosi huyo, Jonas alikuwa akijitahidi kuwasiliana na Maria huku lengo lake kubwa likiwa ni kuweka mazoea makubwa ambayo yangepelekea kumtaka uhusiano.

    Mara ya kwanza Maria alikuwa akiona usumbufu kupokea simu zaidi ya kumi na tano kutoka kwa Jonas lakini baadae akaonekana kuzoea, hakuona tena usumbufu wowote ule. Jonas alijitahidi kupiga hatua moja mpaka nyingine.

    Hapo akaanza kumuomba Maria watoke chakula cha usiku ombi ambalo Maria wala hakukataa hata kidogo. Mara kwa mara walikuwa wakitoka mitoko ya kwenda hotelini lakini wala Jonas hakutamka kitu chochote kile, bado alikuwa akijipanga zaidi.

    Kwanza alitaka kumsoma Maria, alitaka kujua mwanamke huyo alikwa akipendelea nini zaidi maishani mwake na vitu gani ambavyo hakuwa akivipendelea. Kumsoma Maria halikuwa jambo dogo, lilimchukua miezi miwili, akaonekana kujua mengi kutoka kwa Maria.

    “Kwa nini mara kwa mara unaonekana mpweke?” Jonas alimuuliza Maria.

    “Mawazo Jonas...”

    “Mawazo ya nini tena? Au kazi unayoifanya hauitaki?” Jonas alimuuliza Maria.

    Maria hakujibu chochote kile, alibaki kimya. Jonas hakutaka kuendelea kuuliza maswali zaidi, akaamua kuanzisha stori nyingine.

    Bado Maria hakuwa sawa kiakili, kila siku alikuwa akimuwaza Hidifonce, moyo wake ulikuwa ukimuuma kupita kawaida mara baada ya kuona kwamba Hidifonce alikuwa amebadilisha namba ya simu. Muda mrefu uipita toka mara ya mwisho kuongea na Hidifonce, moyo wake haukuwa na furaha kabisa.

    “Kuna kitu nataka kukwambia Maria” Jonas alimwambia Maria siku moja baada ya kutoka chakula cha usiku.

    “Kitu gani?” Maria aliuliza.

    “Kuna kazi nimekutafutia. Nimekutafutia kazi katika shirika la Umoja wa Mataifa” Jonas alimwambia.

    Maria akaonekana kushtuka kupita kiasi. Hakuonekana kuamini kile ambacho alikuwa amekisikia kutoka kwa Jonas. Kufanya kazi katika shirika la Umoja wa Mataifa kulionekana kumchangaya kupita kiasi. Alilijua fika shirika hilo, lilikuwa moja ya mashirika makubwa duniani ambayo yalikuwa yamegawanyika katika vitengo vingi. Alimwangalia Jonas mara mbili mbili huku akionekana kutokuamini.

    “Unasemaje?”

    “Ndio hivyo Maria. Nimefanya hivyo kwa sababu ya kitu kimoja tu” Jonas alimwambia Maria.

    “Kitu gani?”

    Jonas hakutaka kujibu kwa haraka haraka, alibaki kimya kwa muda akimwangalia Maria. Uzuri wake ulionekana kumvutia kupita kawaida, akajisogeza kwa karibu zaidi. Akaupeleka mkono wake na kuushika mkono wa Maria.

    “Nakupenda Maria. Mapenzi makubwa ambayo nimekuwa nayo juu yako ndiyo ambayo yamenifanya kkufanyia hivi. Nakupenda Maria, ninahitaji kuwa nawe, ninahitaji kukuoa na tuwe na familia yetu” Jonas alimwambia Maria.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Maria alibaki kimya. Maneno yae yaliirudisha akili yake nyuma kabisa, akaanza kumfikiria Hidifonce. Moyo wake ulikuwa kwa Hidifonce japokuwa kwa asilimia fulani Jonas alikuwa ameanza kuingia. Alimwangalia Jonas, picha ya Hidifonce ikawa ikijirudia mara kwa mara kichwani mwake.

    “Haiwezekani Jonas” Maria alimwambia Jonas ambaye akashusha pumzi ndefu.

    “Unasemaje?”

    “Najua haukutegemea kulisikia hili Jonas”

    “Tatizo nini Maria. Tatizo liko wapi kama nimamua kujitolea maisha yangu kwa ajili yako. Ninakupenda Maria. Ninajitahidi kufanya kila niwezapo kukufanya ufurahie maishani mwako” Jonas alimwambia Maria ambaye akaanza kulia.

    “HIDIFONCE’ Lilikuwa jina ambalo lilikuwa lijirudia kichwani mwa Maria.



    ************************************************







    **** Je huo ndio mwanzo wa mafanikio ya Patrick nchini Marekani?





    ****Je Maria ataweza kumkubalia Jonas kuwa nae? Na Bi Anna ataweza kufunga ndoa na Bwana Mayemba?





    ***** ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog