Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

PAINFUL MEMORIES - 2

 





    Simulizi : Painful Memories

    Sehemu Ya Pili (2)



    Miezi sita ilikuwa imepita tangu Edmund na Uki waingie kwenye uhusiano wa kimapenzi. Uhusiano ule ulionekana kuwaumiza vichwa watu wengi ambao walikuwa wakiufahamu. Ni kweli kwamba Edmund alikuwa na sura yenye mvuto kwa wasichana wengi ambao walikuwa wakimwangalia lakini hiyo haikuwa sababu ambayo ilimfanya Uki aingie katika mahusiano pamoja na Edmund.

    Uki alikuwa mtoto wa tajiri huku Edmund akiwa kijana masikini ambaye maisha yake yalikuwa yakitegemea kazi moja tu. Watu wengi walikuwa wakiudharau uhusino ule lakini hawakuwa na cha kufanya. 

    Magazeti mbalimbali yalikuwa yakiandika kuhusu uhusiano huo. Edmund akajikuta akianza kupata umaarufu jijini Dar es Salaam. Kazi ya usafi ambayo alikuwa akiifanya katika kipindi hicho alikuwa amekwishaachana nayo na katika kipindi hicho alikuwa akifanya kazi kama msimamizi wa bidhaa katika kampuni ya kutengeneza vinywaji ya BAVARIAN, kampuni ambayo ilikuwa ikimilikiwa na Bwana Msantu.

    Bwana Msantu na mkewe, Bi Nasra hawakuwa na cha kufanya juu ya uhusiano huo kwani binti yao ndiye ambaye alikuwa ameamua kuwa pamoja na Edmund. Kadri uhusiano ule ulivyokuwa ukizidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo ulizidi kuchanua zaidi na zaidi.

    Edmund hakuishi Tandale tena, kwa wakati huo alikuwa amepangiwa nyumba kubwa na ya kifahari iliyokuwa Mikocheni B. Uki hakutaka Edmund aishi peke yake ndani ya nyumba hiyo, aliogopa kumpoteza katika maisha yake jambo ambalo lilimfanya kwenda kuishi pamoja nae.

    Maisha yao yakawa kama mke na mume huku wakifanya kila kitu ambacho wanandoa walitakiwa kufanya mara wanapooana. Maisha kwao yakaonekana kuwa ya raha, hawakugombana, walipendana na kujaliana. Kila mmoja alikuwa akimthamini mwenzake kupita kawaida.

    Miezi sita mingine ikapita, Uki akapata ujauzito. Dalili zikaanza kujionyesha dhahiri, mara kwa mara alikuwa akijisikia kichefu chefu na kizunguzungu. Ingawa Edmund alikuwa bize na kazi yake lakini bado alikuwa karibu na Uki. Alimpenda kupita kawaida.

    Alikuwa akimhudumia kwa kila kitu, kwa wakati huo, mapenzi yao yalikuwa makubwa tofauti na kipindi kilichopita. Edmund hakutaka Uki afanye kazi yoyote ile japokuwa ujauzito ule ulikuwa mdogo sana, akamwajiri mfanyakazi wa ndani ambaye alikuwa akimhudumia Uki kwa kila kitu.

    “Kuna kitu nimekifikiria mpenzi” Uki alimwambia Edmund huku akiwa amemlalia kifuani mwake.

    “Kitu gani tena mpenzi?” Edmund alimuuliza Uki.

    “Ningependa tufunge ndoa, tuwe mume na mke” Uki alimwambia Edmund.

    “Hata mimi pia nilikuwa nikilifikiria hilo hilo. Sasa ni wakati wa sisi kufunga ndoa lakini hapa nilipo kuna suala moja linanitatiza” Edmund alimwambia Uki.

    “Suala gani?” Uki aliuliza.

    “Dini. Mimi ni Muislamu na wewe Mkristo. Itakuwa vipi hapo?”

    “Hakuna tatizo hata tukifunga ndoa kanisani. Kitu ninachokihitaji ni kuwa pamoja nawe tu” Uki alimwambia Edmund.

    Kama ambavyo walivyokuwa wamepanga na ndivyo ambavyo ilitarajiwa kufanyika. Uki alipoamua kuwaeleza wazazi wake kuhusu mpango ambao walikuwa wameupanga hakukuwa na mtu yeyote ambaye alionekana kubisha au kuweka pingamizi lolote lile.

    Hakuonekana kujali kama Uki angebadilisha dini na kuwa mkristo au la. Kwao dini hawakuipa nafasi kabisa kwa sababu hawakuwahi kwenda msikitini kwa zaidi ya miaka ishirini, walijiona kuwa kama wapagani. Mipango ya harusi ikaanza kufanyika tena kwa haraka sana. Kiasi cha shilingi milioni themanini kikawekwa tayari kwa ajili ya harusi hiyo ambayo ilitarajiwa kutikisa nchini Tanzania.

    Watu mbalimbali walikuwa wakitumiwa kadi za mialiko kwa ajili ya kuhudhuria harusi hiyo. Viongozi mbalimbali wa nchi wakaahidi kuhudhuria harusi hiyo ambayo ilianza kutangazwa katika vyombo mbalimbali vya habari huku ikiwa imebakia miezi mitatu kabla ya harusi hiyo kufanyika.

    Kutokana na jina lake kuwa kubwa katika ulimwengu wa biashara, Bwana Msantu akaamua kuwatumia kadi za mialiko wafanyabiashara wenzake wote kutoka nchi za mbali kama Dubai, Marekani na nchi nyingine nyingi. Kila mtu akawa na shauku ya kutaka kuishudia harusi hiyo ambayo mpaka hapo ilionekana kuwa harusi ya kifahari ambayo ingeweza kufunja rekodi na kuweka historia nchini Tanzania na Afrika Mashariki nzima.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Vuta picha itakuwaje” Edmund alimwambia Uki.

    “Sipati picha mpenzi. Sipati picha kabisa” Uki alijibu huku akionekana kuwa na furaha tele.

    “Nitakuwa na furaha zaidi mpaka pale ambapo mchungaji atasema kwamba tumekuwa mume na mke. Hapo ndipo nitakapokuwa na furaha zaidi” Edmund alimwambia Uki na kisha kumbusu shavuni.

    Kadri siku ya harusi ilivyokuwa ikizidi kukaribia na ndivyo ambavyo mapenzi yao yalipozidi kuchanua zaidi na zaidi. Kila mmoja alikuwa akimpenda mwenzake, moyo wake ulikuwa tayari kufanya kila linalowezekana kumfanya mwenzake kuwa na furaha.

    Edmund hakuwa akichelewa kurudi nyumbani. Kila siku saa moja usiku alikuwa akifika nyumbani na kutumia muda wake kukaa na mpenzi wake, Uki. Maisha yao yakaonekana kuwa ya raha, upendo wao ukawa mkubwa kupita kiasi mioyoni mwao.

    “Siku ngapi zimebaki?” Edmund aliuliza huku akitabasamu.

    “Siku thelathini mpenzi. Ila naziona kuwa kama miaka kumi kwa jinsi nilivyokuwa na hamu ya kuitwa mke wako” Uki alimwambia Edmund huku akionekana dhahiri kuona siku zikikawia kukatika.

    “Usijali. Tutafunga ndoa na kukuita mke wangu” Edmund alimwambia Uki na kisha kulibusu tumbo lake.

    “Linaanza kuwa kubwa ingawa bado ni mapema sana mpaka nashangaa” Uki alimwambia Edmund huku akilishika tumbo lake.

    “Ni miujiza. Mungu ameubariki huu ujauzito wako. Natumaini atatoka mtoto mzuri sana ambaye atafanana na sisi wote” Edmund alimwambia Uki.

    ******

    Tangu aachane na Uki, Rahman akawa mtu wa kupenda starehe, zile starehe ambazo alikuwa akizifanya siku za nyuma zikaongezeka zaidi na zaidi. Kwake, kutembea na wasichana na kulala nao katika hoteli mbalimbali za kifahari ndio ikawa sehemu ya maisha yake. Moyoni mwake hakumkumbuka Uki kabisa, alimsahau kabisa huku akiwa hakumbuki kama alikwishawahi kuwa na msichana aliyekuwa na jina hilo.

    Siku zikaendelea kukatika. Asilimia kubwa ya wasichana maarufu nchini Tanzania akawa amekwishatembea nao. Moyo wake haukuwa na mapenzi na msichana yeyote, alikuwa akitembea nao na kisha kuwaacha. Maisha yake yaliendelea zaidi na zaidi mpaka pale ambapo akampata binti wa tajiri Godson, Susan.

    Kutokana na tabia zake ambazo zilikuwa zikijulikana kwa kuchukua wasichana mbalimbali, mzee Godson hakuonekana kukubali. Akawaandaa vijana wake ambao aliwapa kazi moja tu ya kumkamata Rahman na kisha kumpeleka katika mikono yake.

    Mpango ule wa mzee Godson ukaonekana kuvuja jambo ambalo mzee Adamu, baba yake Rahman amsafirishe kijana wake kuelekea nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kuanza maisha huko. Hiyo ikaonekana kuwa afadhali katika maisha yake kwani kama angeendelea kubaki nchini Tanzania basi ilikuwa ni lazima kuuawa na mzee Godson.

    Starehe za Rahman ziliendelea mpaka nchini Afrika Kusini. Kila siku alikuwa akilala na wanawake mbalimbali hasa wa Kizulu ambao walikuwa wakionekana kuwa na mvuto kupita kawaida. Alinunua magari ya kifahari huku akiishi katika nyumba kubwa na ya kifahari ambayo alinunuliwa na baba yake nchini humo.

    Kila siku alikuwa akitumia kiasi kikubwa cha fedha lakini fedha hazikuonekana kupungua hata kidogo, kila siku zilikuwa zikizidi kuongezeka zaidi na zaidi. Maisha kwake yalionekana kuwa na amani kwa kuwa alipata kila kitu ambacho alikuwa akikitaka kwa wakati huo.

    Miezi ikakatika zaidi na zaidi. Kama starehe tayari alikuwa amekwishafanya starehe nyingi lakini wala maisha yake hayakubadilika. Kama kutembea na wasichana, alitembea na wasichana wa kila aina, wanene, wembamba, weupe na weusi lakini bado hali yake ilikuwa ile ile, haikubadilika.

    Kwa sasa aliamua kutulia, alichokifanya kwa wakati huo ni kujiaza kitandani na kisha kuanza kuwafikiria wanawake ambao alikuwa ametembea nao. Alihitaji kumchagua mwanamke mmoja ambaye huyo ndiye ambaye angeamua kumuoa. Kila msichana ambaye alikuwa akimfikiria kwa wakati huo alionekana kutokustahili, mwisho wa kila kitu, jina la msichana Uki likamjia kichwani mwake.

    Kwa haraka haraka akainuka kutoka kitandani na kisha kuifungua laptop yake. Lengo lake kwa wakati huo lilikuwa ni kutaka kuwasiliana na Uki kwa kupitia mitandao mbalimbali kwa ajili ya kumuomba msamaha, wapate muda wa kukaa chini na kuongea na kisha kuelewana kuhusu kufunga ndoa.

    Mpaka katika kipindi hicho hakuwa akifahamu kitu chochote kama Uki kama alikuwa kwenye mipango kabambe ya kufunga ndoa na Edmund. Alichokifanya mara baada ya kukosa mawasiliano nae ni kuamua kuja nchini Tanzania tu.

    Alikuja kimya kimya huku akiwa hataki mtu yeyote afahamu kama alikuwa ameingia nchini Tanzania. Moyo wake ulikuwa ukimuogopa sana mzee Godson ambaye bado alikuwa akimtafuta kwa udi na uvumba. Alipofika ndani ya jiji la Dar es salaam, safari yake ya kuelekea Masaki alipokua akiishi Uki, kwa wazazi wake kuanza.

    Jibu alilopewa na mlinzi lilionekana kumchanganya, hakuamini kama yule mwanamke ambaye alikuwa akimhitaji kwa wakati huo alikuwa kwenye maandalizi ya kufunga ndoa na mwanaume ambaye wala hakuwa akimfahamu. Alichokitaka Rahman ni kutaka kupafahamu mahali ambapo Uki na Edmund walipokuwa wakiishi na kuelekezwa.

    Akaingia ndani ya gari lake na safari ya kuelekea Mikocheni B kuanza. Mawazo yake katika kipindi hicho yalikuwa yakimfikiria Uki tu, aliuona moyo wake kurudi katika mapenzi ya msichana yule na katika kipindi kile alikuwa akimhitaji kuliko msichana yeyote katika maisha yake.

    Hakuwa radhi kumuona Uki akiolewa na mvulana mwingine, yeye ndiye ambaye alijiona kustahili kumuoa msichana yule mrembo. Tayari akaonekana kusahau kama yeye ndiye ambaye alikuwa amemuacha Uki katika hali mbaya, hakukumbuka kama alikuwa ameuumiza sana moyo wa Uki katika kipindi ambacho alikuwa ameamua kumuacha kwa sababu ya kuwafuata wasichana wengine.

    Hakuonekana kufahamu ni kwa namna gani Uki alikuwa ameumia moyoni mwake hasa mara baada ya kumuacha. Kitu ambacho alikuwa akikifikiria kwa wakati huo ni kumtaka Uki arudi tena mikononi mwake na hatimae wafunge ndoa na kuishi pamoja kama mume na mke.

    Alitumia dakika ishirini mpaka kufika Mikocheni B na kulisimamisha gari lake nje ya nyumba kubwa ya kifahari. Akapiga honi kadhaa na geti dogo kufunguliwa na mlinzi kutoka nje. Mlinzi akaanza kupiga hatua kulifuata gari lile na kuinama dirishani.

    “Nikusaidie nini?” Mlinzi aliuliza mara baada ya salamu.

    “Nahitaji kumuona Uki” Rahman alimwambia mlinzi.

    Mlinzi hakutaka kuhoji maswali zaidi, alichokifanya ni kwenda moja kwa moja ndani na kisha kumuita Uki. Wala hazikupita sekunde nyingi, Uki akatokea mahali hapo huku akiwa amevalia vazi lake refu aina ya Dela huku kwa mbali ujauzito wake ukionekana.

    Alipotoka nje ya geti, macho yake yakatua usoni mwa Rahman ambaye alikuwa ndani ya gari lake. Uki akaanza kumfuata Rahman na kisha kusimama nje ya gari lile huku uso wake ukionekana dhahiri kuwa na hasira.

    “Nikusaudie nini?” Uki alimuuliza Rahman.

    “Mbona unaonekana kuwa mkali. Au ni makosa kwa mtu kuja kumuona mpenzi wake?” Rahman alimuuliza huku akiufungua mlango wa gari lake na kutoka nje.

    “Nimekuuliza nikusaidie nini?”

    “Nimekuja kukuona kwa sababu kuna kitu ningependa kuongea nawe” Rahman alimwambia Uki.

    “Kuongea na mimi! Usinichekeshe! Kuna kitu umesahau kwangu nikupatie?” Uki aliuliza huku akitoa kicheko cha dhihaka.

    “Nisikilize Uki. Sijasahau kitu chochote kile. Nimekuja kwa ajili ya kusuluhisha kila kitu kilichotokea kwetu, hasa katika kipindi cha nyuma” Rahman alimwambia Uki.

    “Hivi umechanganyikiwa au?” Uki alimuuliza Rahman.

    “Nina akili timamu Uki. Nina akili zangu timamu kama nilizokuwa nazo siku zote” Rahman alijibu.

    “Hapana. Nahisi utakuwa umechanganyikiwa” Uki alimwambia Rahman na kisha kuanza kuondoka.

    Rahman hakutaka kuchelewa, hapo hapo akaanza kumfuata Uki na kisha kumshika mkono na kupiga magoti. Kitu cha kwanza ambacho alikifanya mahali hapo ni kuanza kumuomba Uki msamaha. Uki hakuonekana kumuelewa hata kidogo, kadri alivyokuwa akiendelea kukaa mahali pale na kumwangalia Rahman na ndivyo ambavyo hasira zake zilivyozidi kuongezeka zaidi na zaidi.

    “Nimejua nilipokosea. Naomba unisamehe Uki” Rahman alimwambia Uki.

    “Naomba uniachie mkono wangu”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hapana Uki. Nitakuachia endapo utaniambia kwamba umenisamehe” Rahman alimwambia Uki huku akimshilia vizuri mkono ule.

    “Nimesema niachieeeeeeeee” Uki alisema kwa sauati kubwa ambayo ilimfanya mlinzi kutoka nje.

    “Kuna nini tena?” Mlinzi aliuliza huku akiwaangalia.

    “Hayakuhusu kijana. Haya ni mambo ya wapendanao” Rahman alimjibu mlinzi.

    “Athumani, hebu njoo uutoe huu mkono wake katika mkono wangu” Uki alimwambia mlinzi.

    Hapo hapo Athumani akaanza kuwafuata na kisha kuushika mkono wa Rahman na kuanza kuubinya kiasi ambacho kilimpelekea Rahman kuuachia mkono wa Uki. Rahman alionekana kukasirika, mdomo wake ukaanza kuchezacheza kwa hasira, alikuwa akimwangalia Athumani huku akionekana kutaka kupigana nae.

    “Unataka kupigana? Utaweza mtoto wa mama?” Athumani alimuuliza Rahman ambaye alionekana kukasirika.

    “Nitarudi. Nitarudi kwa mara ya pili” Rahman alisema kwa sauti kubwa ambayo ilisikika vyema masikioni mwa Uki.

    “Nitakurudia Uki. Nitarudi kwako tena. Nitakaporudi, sitorudi kama nilivyo sasa, nitarudi huku nikiwa na shari moyoni mwangu. Nitarudi nikiwa na sura nyingine, sura iliyojaa maumivu, sura ambayo haitotaka maongezi ya amani” Rahman alimwambia Uki ambaye alikuwa amesimama na kisha kuingia ndani ya gari na Uki kuingia ndani ya eneo la nyumba yake.

    Muda wote Rahman alikuwa akionekana kuwa na hasira, hakuamini kama msichana ambaye alikuwa akimtaka kwa wakati huo alikuwa amekataa kuwa nae. Hakukumbuka kwamba yeye ndiye alikuwa chanzo ya hayo yote, hakukumbuka kitu chochote ambacho alikuwa amemfanyia Uki katika kipindi cha nyuma.

    Kwa wakati huo alikuwa na hasira moyoni, kitu ambacho alikuwa amekifikiria kwa wakati huo ni kumuua Uki kama kisasi cha kile ambacho alikuwa amemfanyia kwa wakati huo. Muda mwingi alikuwa akipiga usukani kwa hasira. Mwili wake ulikuwa ukimtetemeka kwa hasira kupita kawaida.

    Rahman hakutaka kuendelea kukaa nchini Tanzania kwa kuhofia kwamba mzee Godson angeweza kufahamu alipokuwa na hatimae kumuua. Alichokifanya ni kukata tiketi ya ndege na kisha kurudi Afrika Kusini huku akijiahidi kurudi tena nchini Tanzania kwa ajili ya kufanya kazi moja tu, kumuua Uki na mwanaume ambaye angekuja kumuoa.

    ****

    Mipango ya harusi bado ilikuwa ikiendelea kufanyika kama kawaida. Wanakamati walikuwa bize wakiangalia gharama za kila kitu ambacho kilitakiwa kutumika katika harusi hiyo ambayo ilishika sana vichwa vya watu nchini Tanzania. Gharama za ukumbi tayari zilikuwa zimekwishawekwa pembeni huku kiasi cha zaidi ya shilingi milioni nane kikiwekwa kwa ajili ya ukumbi.

    Gharama za vyakula na vinywaji nayo ikawekwa pembeni, kila kitu ambacho kilikuwa kikitakiwa kutumika katika harusi hiyo kilikuwa kimewekwa tayari. Siku ziliendelea kukatika mpaka siku mbili kabla ya harusi hiyo kufika. Wageni mbalimbali ambao walikuwa wamealikwa kuhudhuria harusi hiyo wakaanza kuingia ndani ya jiji la Dar es Salaam.

    Katika kipindi hicho, Uki hakuwa pamoja na mpenzi wake, Edmund, yeye alikuwa kwa wazazi wake huku mawasiliano yao yakiwa yanafanyika kwa njia ya simu tu. Kila mmoja alionekana kuwa na presha ya tukio la harusi hiyo. Kila walipokuwa wakiongea, walikuwa wakiongea kwa furaha huku wakishindwa kuzificha furaha zao za kutamani tukio la harusi lifanyike haraka sana.

    Masaa yalikatika na hatimae siku ambayo watu walikuwa wakiisubiria kwa hamu kufika. Magazeti mengi yalikuwa yameitangaza harusi hiyo huku watu wengi wakitakiwa kwenda kuhudhuria harusi hiyo ambayo ilionekana kuvuta hisia za watu. Kanisa ambalo lilitakiwa kutumika katika ufungaji wa ndoa hiyo likawekwa vizuri kwa kupambwa kwa aina ya mapambo mbalimbali.

    Mchungaji Thomas Lyaruu akajiandaa vilivyo kwa ajili ya kufungisha ndoa hiyo katika siku hiyo. Ibada ya harusi ilikuwa ikianza saa sita mchana lakini kuanzia saa mbili asubuhi, tayari kanisa lilikuwa limekwishajaa huku watu wengine wakizidi kuongezeka kanisani hapo jambo ambalo lilionekana kuwa harusi hiyo ingejaza watu wengi sana siku hiyo.

    Saa tano na nusu, rais wa nchi hii, Baraka Kyomo pamoja na rais wa Angola, Vonso Almeida walikuwa wakiingia ndani ya kanisa hilo huku wakiwa wamesindikizana na wake zao kwa ajili ya kuhudhuria harusi hiyo. Wote wakaanza kutembea kuelekea viti vya mbele huku watu wote kanisani wakiwa wamesimama kama kuonyesha heshima.

    Bwana Msantu, mkewe, Bi Nasra nao walikuwa viti vya mbele huku pembeni yao akiwa amekaa Bi Husna ambaye alikuwa akiwakilisha kama mzazi wa Edmund kanisani hapo. Kwaya mbalimbali zilikuwa zikiendelea kuimba kanisani huku muda ukizidi kwenda mbele. Ilipofika saa tano na dakika arobaini, gari la bwana harusi, Edmund likaingia katika eneo la kanisa hilo ambapo akashuka na kuanza kuelekea kanisani.

    Watu wote wakaanza kukipiga kelele za shangwe, Edmund alikuwa akionekana kupendeza sana, suti yake nyeusi, shati jeupe pamoja na tai ya bluu vilionekana kumpendezesha kupita kawaida. Edmund akaanza kupiga hatua pamoja na mpambe wake mpaka mbele ya kanisa na kisha kusimama. Wala hazikupita dakika nyingi, gari la bibi harusi, Uki likaingia ndani ya kanisa hilo ambapo akaanza kutembea na kutakiwa kusimama mlangoni.

    Shela jeupe ambalo lilikuwa liking’aa sana lilikuwa likionekana kumpendezesha sana uki ambaye alikuwa amepambwa kwa mapambo mengine mengi. Edmund pamoja na mpambe wake wakatakiwa kuelekea mlangoni na kisha kuanza kurudi mbele ya kanisa huku wakiwa wameongozana na bibi harusi, Uki pamoja na mpambe wake.

    Vigelegele vikaanza kupigwa kanisani hapo, watu wote walikuwa wamesimama, watoto wawili ambao walikuwa wameshika vikapu vidogo vilivyokuwa na maua walikuwa mbele huku wakimwaga maua yale sakafuni katika kila sehemu ambayo maharusi walitakiwa kukanyaga. Wazazi wote wa pande mbili walikuwa wakionekana kuwa na furaha kwa wakati huo, walikuwa wakiwaangalia watoto wao mpaka pale ambapo walipofika mbele ya kanisa na kutakiwa kusimama.

    Mchungaji Thomas Lyaruu akaanza kuhubiri Neno la Mungu ambalo lilihusiana na ndoa na baada ya kumaliza kutaka pete ziletwe mahali pale. Kila kitu ambacho kilikuwa kikitakiwa kufanyika kwa wakati huo kilifanyika na hatimae wawili hao kufunga ndoa ambayo ilionekana kuwa na baraka zote.

    Sherehe ya kuwapongeza ikafanyika katika ukumbi mkubwa uliokuwa katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam na kisha siku iliyofuata maharusi kuelekea katika visiwa vya Hawaii kwa ajili ya fungate yao huku gharama zote zikiwa chini ya Bwana Msantu ambaye alionekana kuwa na furaha kupita kawaida.

    “Unajisikiaje mke wangu?” Edmund alimuuliza Uki.

    “Siwezi kuelezea. Acha nipumzike mume wangu. Naweza kufa kwa jinsi nilivyokuwa na furaha” Uki alimwambia Edmund na kisha kumkumbatia huku wote wakionekana kuchoka.

    Walikaa katika visiwa vya Hawaii kwa muda wa mwezi mmoja na kisha kurudi nchini Tanzania ambako wakayaanza maisha kama mume na mke huku ujauzito wa Uki ukionekana waziwazi. Walichokifanya kwa wakati huo ni kuanza kuelekea hospitalini ambako vipimo vikafanyika.

    “Watoto mapacha” Uki alimwambia wazazi wake simuni.

    “Ni furaha yetu. Ni furaha kwetu kutarajia kupata wajukuu mapacha” Bi Nasra alisikika.

    “Hata sisi tuna furaha pia” Uki alimwambia mama yake.

    “Wote ni wa kike au wa kiume?” Bwana Msantu aliuliza huku akionekana kuwa na furaha.

    “Mmoja wa kiume na mmoja ni wa kike” Uki alijibu.

    “Mmewaandalia majina gani mpaka sasa hivi? Kama hamna majina semeni niwapatie majina” Bwana Msantu alimwambia Uki.

    “Baba yao ameamua kuwapa majina ambayo yanaonekana kuwafaa”

    “Majina gani?”

    “Wa kiume ataitwa Eric na wa kike ataitwa Erica” Uki alijibu.

    “Majina mazuri. Tumeyapenda sana” Bwana Msantu alimwambia.

    *********CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku ziliendelea kukatika huku tumbo la Uki likizidi kuwa kubwa. Kila wakati Uki alikuwa akionekana kuwa na furaha kupita kawaida. Mara kwa mara marafiki zake walikuwa wakifika nyumbani kwake na kumpongeza kwa kufanikisha kila kitu akiwepo rafiki yake mpendwa, Esta. 

    Kila siku Esta ndiye ambaye alikuwa akifika mahali hapo na kisha kuelekea kliniki pamoja jambo ambalo liliendelea kuukomaza urafiki wao. Wote walikuwa wakionekana kuwa na furaha kupita kawaida, Uki alikuwa akiijali hali yake ambayo alikuwa nayo kupita kawaida. Kila siku alikuwa akila kila kitu ambacho alikuwa akitakiwa kula hali ambayo ilikuwa ikiijenga afya yake kupita kawaida.

    “Njoo unisindikize kliniki” Uki alikuwa akimwambia Esta simuni.

    “Nakuja. Nipo huku Mlimani City. Nitakuja ndani ya dakika arobaini. Wewe jiandae tu” Sauti ya Esta ilisikika simuni.

    Uki akaanza kujiandaa huku kila wakati akiwasiliana na mume wake, Edmund. Muda ulizidi kwenda na hatimae ndani ya dakika arobaini, Esta akaingia ndani ya eneo la nyumba hiyo na kisha kuingia ndani ya gari la Uki na kuanza kuelekea katika hospitali ya Ocean Road. Walipofika hospitalini hapo, wote wakaelekea katika sehemu husika na kisha kuhudumiwa. Walichukua dakika hamsini na ndipo wakatoka katika hospitali hiyo, wakaingia ndani ya gari na kisha kuondoka.

    Gari likaingia katika barabara ya Ally Hassani Mwinyi na kisha kuanza kuelekea upande wa Morroko huku lengo lao kwa wakati huo likiwa ni kutaka kuelekea Mwenge kwa wakati huo. Barabarani hakukuwa na magari mengi kabisa jambo ambalo lilimfanya Uki kukanyaga mafuta kwa sana.

    Walipokuwa wakikaribia katika mataa ya daraja la Salenda, kwa mbali taa nyekundu zikaonekana kuwaka jambo ambalo liliwataka kusimama katika mataa hayo. Huku wakiwa katika mwendo mkali, Uki akajitahidi kukanyaga breki kwa ajili ya kulisimamisha gari hilo. Breki ikaonekana kukataa hali ambayo ilionekana kumshangaza kila mtu.

    “Vipi?” Esta aliuliza.

    “Breki inakataa” Uki alijibu.

    “Mungu wangu! Breki inakataa?” Esta aliuliza huku akionekana kushtuka.

    “Ndio. Najaribu kufunga breki lakini inakataa” Uki alimwambia Esta huku akiendelea zaidi na zaidi kufunga breki, kifaa cha kufunga breki kilikuwa kikibonyezeka lakini breki wala haikuwa ikifanya kazi jambo ambalo lilikuwa likiwashagaza.

    Gari bado lilikuwa likienda kwa mwendo wa kasi, lilipofika katika mataa ya Salenda likashindwa kusimama, likapitiliza. Ghafla, huku bahati mbaya ikiwa upande wao, gari moja kubwa aina ya lori lilikuwa kikipita kati mataa hayo kutokea katika njia iliyounganisha mpaka Al Muntazir. Kwa kuwa nalo lori lilikuwa kwenye mwendo wa kasi, dereva akashindwa kusimamisha lori lile na hivyo kulifuata gari ile alilokuwepo Uki na Esta ambalo nalo lilikuwa kwenye mwendo wa kasi na kuligonga ubavuni.

    Mlio mkubwa ukasikika mahali hapo, lori likasimama lakini gari alilokuwepo Uki na Esta likarushwa juu, likazungka juu mara nne na kisha kuanguka chini karibu kabisa na kituo cha polisi cha daraja la Salenda. Gari ile ilipotua chini, lilianguka huku mataili yakiwa juu. Watu wote ambao waliiona ajali ile wakashika vichwa vyao, ajali ile ilionekana kuwa mbaya sana katika uwepo wa macho yao. Wanawake wakapiga uyowe kwa woga, kwa jinsi ajali ilivyoonekana, hakukuwa na dalili kama kungekuwa na mtu amenusurika katika ajali ile.

    Watu wakaanza kukusanyika mahali pale na kisha kufanya juhudi zao kutaka kuwatoa watu ambao walikuwa ndani ya gari lile. Matairi yalikuwa juu, huku likiwa limebondeka kupita kawaida. Damu zilikuwa zimeanza kutapakaa mahali hapo, kwa jinsi hali ilivyoonekana, ajali ile ilionekana kuwa mbaya kuliko zote ambazo zilitokea katika barabara ya Ally Hassani Mwinyi jijini Dar se Salaam.



    Hakukuwa na haja ya kusubiria gari la wagonjwa lifike mahali hapo, baadhi ya watu ambao walikuwa na utu wakayaweka magari yao tayari kwa kuwabeba watu ambao walikuwa wamejeruhiwa vibaya katika ajali hiyo. Milango haikuweza kufunguliwa, ikang’olewa na kisha kuanza kujitahidi kuwatoa majeruhi.

    Damu zilikuwa nyingi ndani ya gari lile huku nyingine zikiendelea kutapakaa mpaka barabarani. Watu ambao walikuwa na simu zao zenye kamera wakaanza kulipiga picha gari lile ambalo lilikuwa limebondeka kupita kawaida.

    Kuwatoa majeruhi haikuwa kazi rahisi kabisa, miili ya majeruhi ilikuwa imebanwa na mabati ya gari lile. Si Uki wala Esta ambaye alikuwa akijitambua kwa watai huo, wote walikuwa wamepoteza fahamu kabisa na wala hawakujua ni kitu gani ambacho kilikuwa kinaendelea mahali hapo.

    Wananchi wa kawaida kushirikiana na mapolisi wa kituo cha daraja la Salenda walichukua takribani dakika thelathi ndipo wakafanikiwa kuwatoa Uki na Esta. Kila mtu ambaye alikuwa akiwaangalia alishika kichwa chake huku wengine wakiziba midomo yao, hakukuonekana kuwa na mtu yeyote ambaye alionekana kunusurika katika ajali ile.

    Watu walizidi kuumizwa zaidi mioyoni mwao hasa mara baada ya kumwangalia Uki na kuona kwamba alikuwa mwanamke mjauzito. Ingawa Uki alikuwa mtu maarufu lakini kwa wakati ule hakukuwa na mtu yeyote ambaye alikuwa amemgundua kutokana na uso wake wote kutapakaa damu.

    Wote wakapakizwa ndani ya gari aina ya Double Keabin na kisha safari ya kuelekea katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuanza. Gari lilikuwa likiendeshwa kwa mwendo wa kasi, kwa wakati huo kila mtu alikuwa akitamani kuingia ndani ya hospitali hiyo hata kabla majeruhi wale hawakupata matatizo zaidi.

    Walichukua dakika chache wakawa wamekwishafika katika eneo la hospitali hiyo ambako moja kwa moja machela zikaletwa na majeruhi wale kupelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ambako huduma zikaanza kutolewa. Kila daktari ambaye alikuwa akiwaangalia Uki na Esta alibaki kinywa wazi, hakuamini kama ajali ile ilikuwa ni ya gari na wala haikuwa ya ndege.

    “Hapana bwana. Hii ajali kweli balaa” Dokta Ibrahim aliwaambia manesi huku majeruhi wale wakipelekwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi.

    “Inatisha dokta”

    “Hii ajali ni ya gari au ajali ya kitu gani?”

    “Ajali ya gari”

    “Mmh! Basi itakuwa balaa. Sidhani kama hilo gari litaweza kutengenezwa” Dokta Ibrahim alisema huku wakiwaingiza katika chumba cha wagonjwa mahututi na kisha kuanza kuwapa huduma ya kwanza kabla ya kuendelea na matibabu mengine.

    ********

    Edmund alikuwa akiendelea na kazi zake kama kawaida. Muda mwingi alikuwa akionekana kuwa na furaha kupita kawaida, maisha ambayo alikuwa akiishi katika kipindi hicho yalionekana kuwa kama muujiza kwake, muda mwingi alikuwa alimshukuru Mungu kwa kumfanya kuwa na kiasi kikubwa cha fedha huku kila siku akizidi kuingiza fedha.

    Mara kwa mara alikuwa akikaa kimya na kuanza kuyafikiria maisha yake ambayo alikuwa akiishi kabla ya kupata kazi yoyote ile, akaanza kukumbuka katika kipindi kile ambacho alikuwa akifanya kazi ya kubeba magunia katika soko la Tandale, kila alipokuwa akifikiria, alibaki akimshukuru Mungu kwa kumuinua katika kipindi hicho na kumuweka juu.

    Dakika chache zilizopita alikuwa ametoka kuongea na mke wake kwamba ndio walikuwa wakitoka hospitalini tayari kwa ajili ya kuelekea nyumbani. Furaha yake ilikuwa ikikua maradufu katika kila kipindi ambacho alikuwa akimfikiria mke wake, Uki. Hakuamini kama baada ya siku kadhaa nae angekwenda kuitwa baba, tena baba wa watoto mapacha.

    Aliendelea na kazi zake kama kawaida, ghafla moyo wake ukawa mzito, furaha ambayo alikuwa nayo ikaanza kutoweka jambo ambalo likaonekana kuanza kumtia wasiwasi. Hakujua ni kitu gani kilikuwa kinaendelea kwa wakati huo. Akainuka kutoka kitini na kisha kuanza kuchungulia nje kwa kupitia dirisha la kioo.

    Kadri muda ulivyozidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo hali ile ilivyozidi kuongezeka zaidi na zaidi. Hapo hapo akachukua simu yake na kuanza kumpigia mke wake. Simu ikaanza kuita, iliita zaidi na zaidi lakini wala haikuweza kupokelewa jambo ambalo likamfanya kuwa na wasiwasi zaidi na zaidi.

    Edmund hakutaka kuishia hapo, alichokifanya ni kuanza kumpigia tena. Kama ilivyokuwa mara ya kwanza na ndivyo ilivyotokea tena, simu ilikuwa ikiita tu bila kupokelewa. Tayari wasiwasi ukazidi kumuingia na kujua kwamba kulikuwa na tatizo ambalo lilikuwa limetokea. Hakutaka tena kukaa ofisini, alichokifanya ni kuchukua koti lake la suti na kisha kutoka nje ya ofisi ile.

    “Mtu yeyote akija kuniulizia mwambie sipo” Edmund alimwambia Sekretari wake.

    “Niwaambie wakusubirie au?”

    “No! Waambie waje kesho” CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Na kama wakis.......” Sekretari aliuliza lakini hata kabla hajamalizia swali lake, tayari Edmund alikuwa ametoweka mbele ya macho yake.

    Edmund akalifuata gari lake, akaingia na kuondoka mahali hapo. Bado alikuwa na wasiwasi, alijaribu kumpigia simu mke wake zaidi na zaidi lakini hali bado ilikuwa vile vile, simu haikupokelewa hadi ikakatika. Edmund alikuwa akiendesha gari kwa kasi kuelekea nyumbani. Kutokana na mwendo ambao alikuwa nao, alitumia dakika kumi na kufika nyumbani ambako akateremka na kuanza kumfuata mlinzi.

    “Mke wangu yupo wapi?” Edmund alimuuliza mlinzi.

    “Alikwenda hospitalini”

    “Hajarudi hadi sasa hivi?”

    “Bado”

    “Aliondoka na Esta kama kawaida yake?”

    “Ndio”

    Hapo hapo Edmund akachukua simu yake na kuanza kumpigia tena mkewe, alipoona simu haipokelewi, akaanza kumpigia Esta. Kama ilivyokuwa kwa mke wake na ndivyo ambavyo iivyotokea kwa Esta, simu ilikuwa ikiita mpaka kukatika lakini waa haikupokelewa jambo ambalo lilikuwa likimuweka kwenye wasiwasi mkubwa kupita kawaida.

    Alichokifanya kwa wakati huo ni kuwapigia wazazi wake Uki. Tayari alikuwa amekwishahisi kwamba Uki alikuwa amekwenda kuwaona wazazi wake. Hisia zake hizo wala hakuzipa nafasi kubwa moyoni mwake, lakini kwa sababu ndicho alichokuwa akikihisi, hakuwa na budi kuwapigia.

    “Huku hajafika” Sauti ya Bi Nasra iliskika.

    “Mungu wangu! Sasa atakuwa wapi?” Edmund aliuliza.

    “Kwani nyumbani hayupo?”

    “Hayupo mama”

    “Mara ya mwisho alisema anakwenda wapi?”

    “Hospitalini?”

    “Hospitali gani?”

    “Huwa anakwenda Ocean Road”

    “Labda ungekwenda huko kumuangalia” Bi Nasra alimwambia Edmund.

    “Sawa. Ngoja nijaribu mama. Yaani unaponiambia kwamba hata uko hayupo ndio nachanganyikiwa kabisa” Edmund alisema na kisha kukata simu.

    Hakutaka kuchelewa, hapo hapo akaanza kulifuata gari lak na kisha kuanza safari ya kuelekea katika hospitali ya Ocean Road. Kichwa chake hakikutulia, moyo wake bado ulikuwa ukimuwaza mke wake tu. Tayari moyo wake ulikuwa na uhakika kwamba kulikuwa na jambo baya ambalo lilikuwa limetokea.

    Huku akiwa anaelekea hospitalini mara akasikia simu yake ikianza kuita. Alichokifanya ni kuingiza mkono mfukoni na kisha kuitoa simu ile na kuanza kukiangalia kioo cha simu ile. Alipoliona jina la mke wake, kwa haraka haraka akaipeleka sikioni.

    “Upo wapi mke wangu? Umenitia wasiwasi mpenzi. U mzima hapo ulipo?” Edmund aliuliza maswali mawili mfululizo.

    “Samahani kaka. Hapa ni kituo cha polisi cha Salenda” Sauti ya kiume ilijibu upande wa pili hali iliyomfanya Edmund kulipeleka gari pembeni na kulisimamisha.

    “Mke wangu amefanya nini mpaka kuwa kituoni?” Edmund aliuliza.

    “Upo wapi kwa sasa?”

    “Nimefika hapa Morroko”

    “Unaweza kufika hapa kituoni?” Sauti ya upande wa pili iliuliza.

    “Nipe dakika kadhaa” Edmund alijibu na kisha kuanza kuelekea katika kituo hicho cha polisi.

    Mwendo wake ulikuwa ni wa kasi, katika kipindi hicho, maswali mfululizo tayari yakaanza kumiminika kichwani mwake juu ya sababu ambayo ilimfanya mke wake kuwa katika kituo cha polisi. Kila kitu ambacho alikuwa akijiuliza mahali hapo, alikosa jibu kabisa.

    Alichukua dakika tatu tu akawa amekwishafika katika kituo hicho ambako akalipaki gari lake na kisha kuelekea mpaka kaunta ambako akajitambulisha. Polisi mmoja ambaye alikuwa ndani ya chumba kidogo akatokea mahali hapo, alipogongana macho yake na Edmund, akaonekana kushtuka. 

    “Kumbe yule ni shemeji yetu!” Polisi yule alisema huku akionekana kushtuka.

    “Mke wangu yupo wapi?” Edmund aliuliza hata kabla ya salamu.

    “Njoo hapa ndani mara moja” Polisi yule alimwambia Edmund na kisha kuingia ndani ya chumba kile.

    “Afande naomba uniambie kuna tatizo gani” Edmund alimwambia polisi yule huku wenzake wakianza kuingia ndani ya chumba kile.

    “Mkeo amepata ajali Edmund” Polisi yule alimwambia Edmund.

    “Unasemaje?”

    “Mkeo amepata ajali. Gari lake liligongwa na lori la mchanga”

    “Yupo wapi?”

    “Amewahishwa hospitalini”

    “Hospitali gani?”

    “Muhimb....”

    Edmund hakutaka kujua ni neno gani lingemaliziwa, tayari akaonekana kuifahamu hospitali hiyo, alichokifanya ni kutoka ndani ya kituo kile cha polisi na kisha kuingia ndani ya gari lake na kuondoka mahali hapo kwa kasi. Mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidunda kwa kasi kupita kawaida. Hofu kubwa ya kumpoteza mke wake ikawa imemuingia moyoni mwake.

    Aliendesha gari kwa kasi, hakujali mataa ya barabarani, hata pale ambapo yalikuwa yakimtaka yasimame, hakutii, alipita kwa kasi huku akili yake ikiwa inamuwaza mke wake tu. Hakujali kama angepata ajali au la, kitu ambacho alikuwa akikijali kwa wakati huo ni kuwahi hospitali kumuona mke wake tu. Hakutumia muda mwingi akawa amekwishafika katika hospitali hiyo ambapo akaanza kuelekea katika sehemu ya mapokezi na kisha kuanza kumuulizia mke wake.

    “Watu waliopata ajali ambao wameletwa katika hospitali hii hadi muda huu ni watu wawili tu” Mwanamke wa mapokezini alimwambia Edmund ambaye alionekana kuwa na wasiwasi.

    “Wako vipi hao?”

    “Wanawake wawili”

    “Wamepelekwa wapi?”

    “Watakuwa wamewachukua kuwaepeleka katika chumba cha wagonjwa mahututi” Mwanamke yule alijibu.

    Edmund hakutaka kusubiria kupewa maelezo mengine, alichokifanya kwa wakati huo ni kuanza kuondoka kuelekea mahali ambapo kilikuwepo chumba hicho. Alipofika, alitakiwa kukaa benchini mpaka pale ambapo kila kitu kingekamilika. Edmund alisubiri kwa muda wa dakika zaidi ya arobaini, chumba kile hakikufunguliwa hali ambayo kwa kiasi fulani ikaanza kumuingizia wasiwasi.

    “Mungu wangu! Mke wangu atakuwa amefariki! Mungu naomba umuokoe, Mungu naomba umponye” Edmund alisema huku machozi yakianza kumtoka.

    Dakika ziliendelea kukatika, yalipopita masaa mawili, mlango ukafunguliwa na dokta Ibrahim kutoka nje. Edmund hakutaka kuendelea kukaa benchini, alichokifanya ni kuanza kumfuata dokta Ibrahim.

    “Niambie kuhusu mke wangu” Edmund alimwambia dokta Ibrahim.

    “Mkeo yupi?”

    “Aliyepata ajali”

    “Ni miongoni mwa wanawake hawa wawili?”

    “Ndio”

    “Mmmh!” Dokta Ibrahim alitoa mguno ambao ukamfanya Edmund kushtuka na kujawa na hofu zaidi ya hofu ambayo alikuwa nayo kabla.

    “Niambie kuna nini! Amefariki?” Edmund aliuliza huku akimshika dokta Ibrahim koti lake huku machozi yakimtoka mfululizo.

    *********

    Kukataliwa na Uki kilikuwa ni kitendo ambacho kilimuumiza sana Rahman, wiki nzima hakuonekana kuwa kwenye hali ya kawaida jambo ambalo lilianzisha maswali kwa baadhi ya marafiki zake ambao alikuwa akiishi nao ndani ya nyumba aliyonunuliwa nchini Afrika Kusini. Mapenzi yakaonekana kumuumiza, maumivu makali ya mapenzi yalikuwa yameupata moyo wake.

    Japokuwa Rahman alikuwa amewazoea sana wasichana lakini katika kipindi hicho akaanza kulia, mapenzi yakaanza kumtoa machozi. Kuna wakati alikuwa akikumbuka kwamba yeye ndiye alikuwa chanzo cha kila kitu lakini kuna wakati mwingine alikataa kukubaliana na ukweli kwamba yeye ndiye alikuwa chanzo cha yale yote.

    Amani haikuwepo kabisa moyoni mwake, taratibu akaanza kumchukia Uki pamoja na mwanaume ambaye hakuwa akimfahamu. Rahman akaanza kuiridhisha roho yake kwa kuanza kutembea tena na wasichana wengine kwa nia ya kukipooza kidonda chake lakini wala kidonda hakikupata nafuu, bado kilikuwa kikiendelea kuuma moyoni mwake.

    Katika kipindi hicho alikuwa akimtaka Uki tu ambaye alikuwa na kiu kubwa ya kumuoa na kuwa mume na mke. Kila kitu tayari kikaonekana kushindikana, yule Uki ambaye alikuwa akimhitaji sana kwa kipindi hicho wala hakuwa nae, alikuwa na mwanaume mwingine ambaye alitarajia kufunga nae ndoa takatifu kanisani.

    Miezi ikakatika mpaka pale ambapo aliliona tangazo kwenye mtandao kwamba mtoto wa kitajiri, Uki alikuwa akienda kufunga ndoa na mwanaume ambaye alijulikana kwa jina la Edmund. Tangazo lile likaonekana kuwa kama msumari wa moto ambao ulichoma kidonda chake cha moyoni, akaonekana kuumia zaidi na zaidi.

    Akaanza kuisoma habari ile, kadri alivyokuwa akiisoma na ndivyo ambavyo aliumia zaidi na zaidi mpaka kufika kipindi kuwa na hasira kupita kawaida. Alichokifanya ni kuangalia tarehe ya harusi ile na kisha kuizima kompyuta yake. Tayari akaona kwamba kulikuwa na uhitaji wa kufanya jambo moja, kumuua Uki ili yeye pamoja na Edmund wakose wote.

    Kwa wakati huo wala hakutaka kufanya vitu vyake haraka haraka, alijiona kuwa na uhitaji wa kufanya mambo yake taratibu sana. Kwanza alitaka kuwaacha wafunge ndoa, waishi kwa muda fulani ndani ya ndoa na ndipo hapo aanze kufanya mambo yake kwa kumuua Uki. Siku ya harusi ikafika na harusi kufungwa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kitu alichokifanya Rahman kwa wakati huo ni kuwasiliana na mtu ambaye alikuwa akimuamini sana ambaye alikuwa nchini Tanzania kwa ajili ya kuwaandalia vijana ambao wangefanya kazi moja ambayo ilikuwa ni muhimu sana. Mawasiliano yakafanyika haraka sana na kisha kutakiwa kuelekea nchini Tanzania kwa lengo la kuonana na vijana hao ambao tayari walikuwa wamekwishaandaliwa.

    Rahman hakuwa na jinsi, alichokifanya ni kusafiri mpaka Tanzania kisiri na kisha kuonana na hao vijana na kisha kuwaambia kile ambacho alikuwa akikihitaji kwa wakati huo. Hakukuwa na mtu yeyote ambaye alionekana kuushangaa mpango ambao ulikuwa umepangwa kwa wakati huo, wote wakakubali na kuwa tayari kwa kuanza kazi.

    “Kwa nini asiuawe kama kawaida tu?” Rafiki yake, Omari alimuuliza.

    “Hapo itaweza kugundulika kwa urahisi sana. Yaani ninataka kumuua katika kifo ambacho hakutokuwa na mtu yeyote ambaye ataweza kugundua kama ni mpango kabambe ulipangwa” Rahman alimwambia Omari.

    “Kwa hiyo vijana umewaambia wamuue katika aina gani ya kifo?”

    “Walegeze breki za gari lake tu”

    “Halafu itakuwaje?

    “Wakilegeza, kila atakapotaka kufunga breki, ishindikane, mwisho wa siku akiwa kwenye mwendo wa kasi, agonge gari lolote mbele yake. Baada ya hapo, anarushwa nje ya gari kupitia kwenye kioo cha mbele na huo kuwa mwisho wake. Umeuonaje hapo?” Rahman alimwambia Omari ambaye alitikisa kichwa juu na chini kuonyesha kwamba alikuwa amemuelewa na kukubaliana na mpango ule.

    “Sasa hiyo kazi itafanyika lini?” Omari aliuliza.

    “Kwanza warudi kutoka huko walipokwenda kwa ajili ya fungate na kisha ndio kazi ifanyike” Rahman alimwambia Omari.

    “Basi poa. Nakutakia mafanikio mema”

    “Shukrani sana”

    Rahman hakutaka kuondoka nchini Tanzania, aliendelea kubaki huku akiendelea kuwasiliana na vijana wale huku akiwasisitiza kwa kukamilisha kazi ile ile. Katika kipindi hicho, kila siku ambayo alikuwa akikutana nao na kuongea alikuwa akiwagawia kiasi fulani cha fedha kama kuwahamasisha katika kazi ile ambayo walitakiwa kuifanya kwa wati huo.

    Mpaka Uki na Edmund wanarudi nchini Tanzania, kila kitu kilikuwa kimekwishapangwa na kukamilika kwa asilimia mia moja. Kazi ambayo waliifanya vijana ni kuanza kufuatilia ratiba nzima ya Uki, yaani kutoka kwenda kliniki na kurudi. Baada ya wiki, ratiba nzima walikuwa nayo.

    “Leo ndio siku yenyewe” Mmoja wa vijana wale, Osca alimwambia Rahman.

    “Atatoka leo?”

    “Ndio bosi. Atatoka kuelekea kliniki ila hatujajua muda gani” Osca alijibu.

    “Kwa hiyo mtajua vipi muda wa kutoka?”

    “Tunakwenda kumsubiria karibu na nyumba yake, atakapotoka tutamfuatilia hadi hospitalini na kisha kazi nzima kufanyika” Osca alijibu.

    “Sawa. Itakuwa vizuri sana” Rahman alijibu.

    Osca pamoja na mwenzake, Sefu wakajiandaa siku hiyo kwa ajili ya kwenda nyumbani kwa Edmund tayari kwa kufanya kile ambacho walikuwa wamekipanga. Walilisimmisha gari lao mbali kidogo na nyumba ya Edmund ambapo baada ya masaa matatu, gari la Uki likaonekana likianza kutoka ndani ya eneo la nyumba ile.

    Hawakutaka kuchelewa, walichokifanya ni kuanza kulifuatilia. Tayari lengo ambalo walikuwa wamelipanga lilikuwa kichwani mwao na kwa wakati huo walikuwa wakisubiria kuona gari hio likipakiwa na kisha kwenda kufanya kazi yao. Walizidi kulifuata lile gari mpaka lilipoingia ndani ya eneo la hospitali ya Ocean Road.

    “Umekumbuka kubeba spea?” Osca alimuuliza Sefu.

    “Kila kitu”

    “Kwa hiyo tushuke wote au unashuka wewe peke yako?”

    “Ngoja niende mimi peke yangu” Sefu alisema na kisha kuteremka garini.

    Sefu akateremka kutoka ndani ya gari lile na kisha kuelekea ndani ya eneo la hospitali ile ambapo akaanza kulifuata gari lile alilokuja nalo Uki pamoja na Esta. Kutokana na kuwa na idadi kubwa ya magari hospitalini pale, haikuwa rahisi kwa Sefu kuonekana kabisa. Mara alipolifikia, kwa haraka sana akaingia chini ya uvungu wa gari na kisha kuanza kuilegeza breki ya gari ile kwa kiasi kikubwa sana na kisha kuondoka huku akiwa ametumia dakika tano tu.

    “Vipi?” Osca alimuuliza Sefu.

    “Tayari”

    “Kuna haja ya kuendelea kuwafuatilia hadi watakapopata ajali?”

    “Hakuna haja. Wewe jua kwamba kazi yangu imefanyika na mpango utakamilika. Cha msingi, tuondoke tu” Sefu alimwambia Osca na kisha kuondoka mahali hapo huku wote wakiwa na uhakika wa kumsababishia ajali Uki.



    Mguno wa dokta Ibrahim ndio ambao ulikuwa umemtia wasiwasi zaidi kiasi ambacho mpaka wakati alikuwa akilia kama mtoto mdogo. Akili yake aliihisi kuchanganyikiwa kabisa, hakuwa akiamini kama kweli mke wake ambaye alikuwa mjauzito wa watoto wawili mapacha ndiye alikuwa amepata ajali hiyo mbaya.

    Bado Edmund alikuwa akiendelea kumshika koti dokta Ibrahim huku akiendelea kulia jambo ambalo liliwafanya watu ambao walikuwa wakipita mahali hapo kusimama na kuanza kuwaangalia. Alichokifanya dokta Ibrahim ni kumtaka Edmund aondoke nae na kuelekea nae kwenye ofisi yake na kisha kuanza kuongea nae.

    Kwanza kitu cha kwanza akaanza kumpa poe Edmund kwa kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea katika ajali ile mbaya ambayo ilionekana kutokuamini kama majeruhi wale ambao walikuwa wameletwa walikuwa wazima.

    “Mke wangu vipi dokta?” Edmund alimuuliza dokta Ibrahim ambaye alionekana akiongea maneno mengi.

    “Wanaendelea vizuri japokuwa hali zao bado hazijakaa sawa” Dokta Ibrahim alijibu.

    “Kwa hiyo watapona wote wawili?” Edmund aliuliza. 

    “Kupona wanaweza kupona japokuwa watachukua muda mrefu sana kitandani” Dokta alitoa jibu lililoonekana kumchosha Edmund.

    Muda uizidi kusogea zaidi na zaidi, kadri dakika zilivyozidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo Edmund alivyozidi kuumia zaidi na zaidi. Kitu alichokifanya mara baada ya kutoka katika ofisi ya dokta ni kuwapigia simu wazazi wake Uki na kisha kuwataarifu juu ya ajali mbaya ambayo ilikuwa imetokea na kumfanya Uki pamoja na Esta kuwa kitandani huku wakionekana kutokujitambua.

    Bwana Msantu pamoja na mkewe, Bi Nasra wakafika hospitalini hapo mara moja huku wote wakionekana kuchanganyikiwa. Taarifa ambayo walipewa na Edmund ilionekana kuwachanganya kupita kawaida. Moja kwa moja wakaanza kuelekea katika sehemu iliyokuwa na chumba kile cha wagonjwa mahututi ambapo wakamkuta Edmund nje akiwasubiri.

    “Kitu gani kimetokea. Tuambie kitu gani kimetokea” Bi Nasra alimwambia Edmund ambaye macho yake yalikuwa mekundu kwa sababu ya kulia sana.

    “Ajali mama. Mke wangu amepata ajali” Edmund alimwambia.

    Uwepo wa wazazi wale ukamfanya Edmund kuanza kulia tena. Moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makali kupita kawaida, muda wote huo alikuwa akilia tu. Mpaka kufikia hatua hiyo, hakukuwa na mtu ambaye alikuwa akifikiria kama Rahman alikuwa nyuma ya tukio zima ambalo lilikuwa limetokea.

    Wakakaa hospitalini hapo kwa muda wa zaidi ya masaa nane lakini bado hawakuruhusiwa kumuona Uki ambaye alionekana kuwa kwenye hali mbaya. Kitu ambacho Edmund alikuwa amekikumbuka kwa wakati huo ni kuwasiliana na ndugu zake Esta na kisha kuwaelezea kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea, baada ya dakika thelathini, baadhi ya ndugu zake Esta wakafika mahali pale na kisha Edmund kuanza kuwaelezea kila kitu.

    Vilio vikaonekana kuanza kutawala mahali pale. Kwa jinsi ambavyo ndugu zake Esta walivyokuwa wakilia na ndivyo ambavyo Edmund pamoja na wazazi wa Uki walipozidi kulia zaidi na zaidi kiasi ambacho hakukuwa na mtu ambaye alikuwa na uwezo wa kumbembeleza mwenzake.

    Hali ile iliendelea mpaka dakika ishirini zilizopita na ndipo kila mmoja akaonekana kutulia. Maongezi mengine yakafuatia mahali hapo na hivyo wote kutakiwa kumuomba Mungu kuwaponya watu wao ambao walikuwa ndani ya chumba kile ambacho kilionekana kutisha kupita kawaida. 

    Matibabu yaliendelea zaidi na zaidi. Ilipofikia saa tatu na robo usiku, mlango wa chumba kile ukafunguliwa na daktari Ibrahim pamoja na manesi kutoka kitu kilichowafanya wote kuanza kumfuata dokta Ibrahim na kumzunguka.

    “Wagonjwa wetu wanaendeleaje?” Lilikuwa ni swali lililotoka kwa Edmund.

    “Wanaendelea vizuri. Tulikuwa tukiwasafisha na kuwatibu vidonga vingine walivyovipata pamoja na kuwaandaa kwa ajili ya kuwaona” Dokta Ibrahim alijibu.

    “Kwa hiyo tunaweza kuingia kuwaona?” 

    “Hapana. Hamtakiwi kuingia kuwaona ndani ya chumba hiki. Watapelekwa katika chumba kingine, humo ndipo ambapo mtaweza kuwaona” Dokta Ibrahim aliwaambia.

    “Sawa” Wote waliitikia na kuendelea kusubiri.

    Ilipofika saa nne na nusu, Uki na Esta wakaanza kutolewa ndani ya chumba kile. Vilio vikaanza kusikika tena mahali pale. Kwa jinsi walivyokuwa wakiwaangalia Uki na Esta walijiona kama kuangalia maiti ambazo zilikuwa zimetoka kusafishwa mochwari na zilikuwa tayari kw ajili ya kuzikwa.

    Walipofikishwa katika chumba kile na ndipo hapo wote wakaitwa na kuingia. Uki na Esta walikuwa kimya vitandani huku miili yao ikiwa imepata majeraha makubwa kupita kawaida. Kila mmoja alikuwa akiwaangalia kwa uso uliojaa huzuni, kwa jinsi waliyokuwa wakionekana, hakukuwa na dalili zozote ambazo zingewafanya watu wale kuamka kwa mara nyingine tena.

    Uki ndiye ambaye alionekana kuhuzunisha zaidi. Hali ya ujauzito ambayo alikuwa nao pamoja na kupata ajali ile, tayari watu wakaona kwamba mimba ile ilikuwa imekwishaharibika. Tumbo lake lilikuwa limejaa mikwaruzo pamoja na vidonda jambo ambalo lilikuwa likisababisha bandeji zote alizokuwa amefungwa tumboni kuloanishwa na damu zilizokuwa zinatoka mara kwa mara japokuwa alikuwa amekwisapakwa dawa.

    “Mke wangu! Mke wangu! Uki mpenzi!” Edmund aliita huku akishindwa kuyazuia machozi yake yasimtoke.

    “Usilie Edmund. Atapona tu” Bwana Msantu alimwambia Edmund huku akimpigapiga begani.

    “Inaniuma sana. Naona kama Mungu ameamua kunikomesha katika hili” Edmund alimwambia Bwana Msantu.

    “Usiseme hivyo. Usitake kumkufuru Mungu”

    “Unafikiri nitasemaje. Yaani hata miezi miwili ya ndoa yetu haijafika, tayari amepata tatizo kama hili. Yaani naona kama kila kitu kimepangwa kutokea katika maisha yangu. Nafikiri imepangwa kwamba sitakiwi kuyafurahia maisha ya ndoa yangu” Edmund alisema huku akilia.

    “Usiseme hivyo Edmund. Uki atapona tu”

    “Atapona lini? Atafumbua macho yake lini? Nitaliona tena tabasamu lake lini?” Edmund aliuliza maswali mfululizo.

    “Cha msingi tumuombe Mungu tu”

    “Inaniuma. Mungu ndiye aliyepanga haya yatokee, kama alitaka niishi na mke wangu kwa furaha sidhani kama haya yangetokea. Kwa nini hakutaka kumuepushia kifo hiki mke wangu? Kwa nini hakutaka kunifaya kuwa na furaha?” Edmund aliuliza.

    “Uki hajafa Edmund”

    “Amekuwa nusu mfu. Hajafumbua macho yake kuniangalia japokuwa nimemuita mara kwa mara. Anapumulia mashine kuonyesha kwamba kwa hali ambayo anayo hata hewa hii ya kawaida haimtoshi. Namuona kuwa kama mfu ambaye anasubiri muujiza wa Mungu kutembea tena” Edmund alimwambia.

    Maneno yote ambayo alikuwa akiyaongea yalionekana kumuumiza kila mtu ambaye alikuwa ameyasikia. Kwa wakati huo, Edmund alionekana kama mtu ambaye alichanganyikiwa kutokana na tukio lile la ajali ambalo lilikuwa limetokea katika kipindi kile. Moyoni mwake hakuwa na tumaini kama mke wake, Uki angeweza kufumbua macho yake tena na kuongea pamoja nae, jakuwa na uhakika kabisa kama Uki angeweza kujifungua watoto wake salama na wakati hakuwa amerudiwa na fahamu zake.

    *******CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku ziliendelea kukatika zaidi na zaidi lakini bado hali iliendelea kuwa vile vile bila mabadiliko yoyote yale. Si Uki wa Esta ambaye alikuwa amerudiwa na fahamu katika kipindi hicho. Maisha ya kulia ndio yalikuwa sehemu ya maisha aliyokuwa akiishi Edmund, kila siku alikuwa akilia huku akimlaumu Mungu kwamba alikuwa mwanzo ya kila kitu kwa sababu alikuwa na uwezo wa kuizuia ajali ile isitokee.

    Watu wengi ambao walikuwa wakimiminika hospitalini pale walikuwa wakiendelea kumpa pole Edmund kwa kile ambacho kilikuwa kimetokea lakini wala pole zile hazikuonekana kubadilisha kitu chochote zaidi ya kumuongezea uchungu moyoni mwake. Kila siku alikuwa akimuomba Mungu amnusuru mke wake ili asifariki na hata ajifungue salama viumbe ambavyo alikuwa navyo tumboni.

    Taarifa juu ya kupata ajali kwa Uki ikatangazwa katika vyombo mbalimbali vya ajali huku Polisi kwa wakati huo wakifanya uchunguzi ili kuona chanzo cha ajali ile ambayo ilikuwa mbaya sana hata kuelezeka. Kila mtu ambaye alikuwa akiisoma habari juu ya ajali ile ambayo ilitokea ilionekana kumshtua.

    Katika kipindi cha kwanza idadi ya watu wengi walijua fika kwamba Rahman alikuwa nyuma ya tukio lile lakini walipokuwa wamesikia kwamba ilikuwa ni ajali basi wasiwasi wao juu ya Rahman ukaonekana kuanz kupotea. Idadi kubwa ya watu walikuwa wakimiminika hospitalini hapo na kumpa pole Edmund ambaye katika kipindi hicho alionekana kuwa kama mtu ambaye alichanganyikiwa kabisa kutokana na kile ambacho kilikuwa kimetokea.

    Edmund akawa mtu wa kulala hospitalini, hakutaka kutoka hospitalini, kila siku alikuwa akilala katika chumba alicholazwa Uki pamoja na Esta. Hakujali kuhusu kiti ambacho kwake alikuwa akikigeuza na kuwa kitanda, kitu ambacho alikuwa akikijali kwa wakati huo kilikuwa ni kukaa karibu na mke wake tu ambaye alikuwa akimpenda kupita kawaida.

    Mara kwa mara Edmund alikuwa akiyafikiria maisha aliyoishi zamani hata kabla hakukutana na Uki. Maisha yale kwake yalikuwa maisha magumu ambayo yalionekana kumtesa kila siku. Alipokuja kumpa Uki na kisha kumuoa, alijiona kwamba huko mbeleni kusingekuwa na huzuni tena, kitu ambacho alikitegemea kukipata hapo baadae ni furaha ambayo ingemfanya kufurahia maisha yake yote.

    Mategemeo na matumaini yake tayari yakaonekana kubadilika, kile ambacho alikuwa akikifikiria kilionekana kuwa kinyume kabisa. Furaha ambayo alikuwa akitarajia kuipata katika kipindi chote cha maisha ya ndoa ikawa imepotea kabisa. Kwa kipindi hicho, huzuni ikarudi tena, kwa wakati huu huzuni hii haikuja kama ilivyokuwa kabla, ilikuwa imekuja pamoja na maumivu makali moyoni.

    Edmund alikuwa akitumia muda mwingi sana kuwa macho zaidi ya kulala. Kila siku muda wake wa kulala ulikuwa saa tisa usiku na kuamka saa kumi na mbili alfajiri huku akiwa ndani ya chumba kile ambacho aliruhusiwa na dokta mkuu wa hospitali hiyo kulala humo bila kuwasumbua wagonjwa waliokuwa ndani ya chumba kile.

    “Uki wangu atapona kweli?” Edmund alikuwa akijiuliza swali hili mara kwa mara huku akionekana kukata tamaa kabisa.

    “Muda unazidi kwenda lakini bado anaonekana kuwa hivi hivi bila ya mabadiliko yoyote yale. Kwa nini Mungu umeamua kunifanyia hivi? Kwa nini mimi? Yaani kila siku mimi tu” Edmund alisema kwa sauti ya chini huku machozi yakianza tena kumtoka.

    Maisha yake ya kulia bado yalikuwa yakiendelea kama kawaida, tabasamu, kwake halikuonekana tena, majonzi ndicho kilikuwa kitu pekee ambacho kilikuwa kimeukumba moyo wake. Kidonda kikubwa akakihisi kikiwa kimeanza ndani ya moyo wake, kidonda ambacho kilikuwa na maumivu makali ambayo wala hayakuweza kuelezeka.

    Watu walikuwa wakiingia na kutoka lakini Edmund hakupata hata muda wa kutoka ndani ya chumba kile. Moyo wake kwa wakati huo tayari ukaanza kutengeneza hisia mbaya kwa kuona kwamba endapo angetoka ndani ya chumba kile basi mke wake, Uki angeweza kufariki. Edmund hakutaka kuliona jambo hilo likitokea, kitu ambacho alikuwa akitaka kukiona ni kufuatilia maendeleo yote ya mke wake, hatua kwa hatua hadi mwisho.

    Siku ziliendelea kukatika. Siku ya kumi na saba tangu ajali itokee, Esta akarudiwa na fahamu jambo ambalo lilionekana kuwa faraja kwa ndugu zake ambao mara kwa mara walikuwa wakifika hospitalini hapo kumuona. Kila mtu ambaye alimuona Esta akiyapepesa macho yake alikuwa akifurahi kupita kawaida.

    Kwa Uki bado mambo yalikuwa yale yale, hakukuwa na mabadiliko yoyote yale, bado alikuwa akiendelea kuwa katika usingizi wa kifo. Siku zikaendelea kwenda mbele huku Edmund akiendelea kumuomba Mungu amponye mke wake na hatimae afumbue macho tena. Siku nane baadae, Uki nae akaweza kuyafumbua macho yake jambo ambalo lilionekana kuwa kama ndoto kwa Edmund.

    “Nahisi nipo ndotoni” Edmund alisema huku akimwangalia mke wake.

    Asilimia kubwa ya miili yao ilikuwa na vidonda ambavyo kwa wakati huo vilikuwa vikiendelea kupona zaidi na zaidi. Uki akaonekana kushangaa, mahali ambapo alipokuwa kwa wakati huo kukaonekana kumshangaza.

    “Nipo wapi?” Uki aliuliza kwa sauti ndogo.

    Dokta Ibrahim hakutaka mtu yeyote aongee kitu chochote kile zaidi ya kuwataka watu wote watoke ndani ya chumba kile huku yeye akibaki na manesi ambao walikuwa wakiendelea kuwashughulikia Uki na Esta. Walichukua masaa mawili na ndipo waliporuhusiwa kuingia ndani huku wakitakiwa kutokuongea maneno yoyote yatakayowasababishia wagonjwa kulia kutokana na kutotakiwa kuzifumua nyuzi ambazo walikuwa wameshonwa miilini mwao.

    “Nipo wapi Edmund?” Uki alimuuliza Edmund kwa sauti ya chini.

    “Upo hospitalini” Edmund alijibu huku akiwa amemshika Uki mkono.

    “Nimefanya nini tena? Mbona nipo hivi?” Uki aliuliza huku akionekana kujishangaa japokuwa alionekana kutokuwa na nguvu kabisa.

    Edmund akakaa kimya kwa muda. Swali ambalo aliuliza Uki lilionekana kuwa gumu kujibika kwani alijua kwamba kama angempa jibu la ukweli basi Uki angeanza kulia jambo ambalo lingemsababishia matatizo zaidi na zaidi.

    “Namshukuru Mungu u mzima wa afya njema mpenzi” Edmund alimwambia Uki.

    Siku ziliendelea kukatika zaidi na zaidi. Mwezi wa kwanza ukapita, mwezi wa pili ukapita na hatimae mwezi wa tatu kuingia. Katika kipindi hicho Uki na Esta walikuwa wakiendelea vizuri kabisa. Walikuwa na uwezo wa kula wenyewe na kuongea kama kawaida japokuwa miili yao haikuwa na nguvu kabisa.

    “Naanza kusikia uchungu mpenzi” Uki alimwambia Edmund ambaye alikuwa pembeni yake huku akilishika tumbo lake.

    “Uchungu umeanza?” Edmund aliuliza huku akionekana kushtuka.

    “Ndio. Uchungu mpenzi” Uki alimwambia Edmund ambaye kwa haraka haraka alitoka ndani ya kile chumba na kuanza kumuita daktari.

    Edmund alikuwa akipiga kelele za kumuita daktari yeyote ambaye alikuwa akiisikia sauti yake. Hatimae madaktari watatu wakatokea mbele yake na kuanza kuongea nae.

    “Kuna nini tena mbona unapiga kelele hospitalini?” Dokta mmoja aliuliza.

    “Mke wangu”

    “Amefanya nini?”

    “Ameanza kusikia uchungu” Edmund alisema huku akianza kuelekea katika chumba kile na madaktari kuanza kumfuata.

    Madaktari wakaingia pamoja na Edmund ndani ya chumba kile. Macho yao yakatua kwa Uki ambaye alikuwa akiugulia uchungu wa kutaka kujifungua. Mara dokta Ibrahim akaingia ndani ya chumba kile huku akihema kwa nguvu. Kitu walichokifanya ni kumtoa Uki ndani ya chumba kile na kumpeleka katika chumba maalumu cha kujifungulia ambako Edmund alitakiwa kubaki nje.

    Madaktari pamoja na manesi wakaingia ndani ya chumba kile, wakakaa huko kwa dakika kadhaa, mlango ukafunguliwa na dokta Ibrahim kutoka na kuanza kumfuata Edmund ambaye alikuwa amesimama.

    “Kuna nini tena? Kuna tatizo lolote?” Edmund aliuliza huku akionekana kuwa na wasiwasi.

    “Ndio. Ila si kubwa sana” Dokta Ibrahim alijibu.

    “Tatizo gani?” Edmund aliuliza huku akionekana kuzidi kuwa na wasiwasi.

    “Mkeo hana nguvu za kuwasukuma watoto. Hivyo tumeona bora tumfanyie oparesheni kuwatoa watoto” Dokta alimwambia edmund ambaye alionekana kuwa na wasiwasi.

    “Mumfanyie oparesheni?”

    “Ndio”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mungu wangu!”

    “Usihofu Edmund, mkeo atajifungua salama tu” Dokta Ibrahim alimwambia Edmund.

    “Nina wasiwasi”

    “Wa nini tena?”

    “Hali yake”

    “Usihofu. Jikaze kila kitu kitakwenda salama”

    “Mmmh! Sawa” Edmund aliitikia na dokta Ibrahim kurudi ndani ya chumba kile.

    Hapo hapo Edmund akachukua simu na kisha kumpigia Bwana Msantu ambaye baada ya dakika kadhaa akafika hapo akiwa ametangulizana na mkewe, Bi Nasra. Edmund akawaelezea kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea, wote wakakaa benchini kusikilizia kitu gani kingeendelea. Kwa wakati huo kila mtu alikuwa akiomba sala yake kimoyo moyo kumuomba Mungu amnusuru Uki na ajifungue salama.

    ********

    Ukimya ulikuwa umetewala huku kila mtu akifikiria lake. Kwa wakati huo, kila mmoja alikuwa akijitahidi kusali sala ya kumuombea Uki ajifungue salama. Edmund alikuwa akionekana kuwa mpole kupita kawaida, uso wake haukuonekana kuwa na amani kabisa. Bado alikuwa akionekana kuwa na wasiwasi, hakujua kama mke wake angejifungua salama au la.

    Waliendelea kusubiri zaidi na zaidi, baada ya dakik arobaini na tano, mlango ukafunguliwa na dokta Ibrahim kutoka huku tabasamu pana likionekana usoni mwake. Wote wakajikuta wakisimama na kuanza kumfuata dokta Ibrahim.

    “Tuambie” Edmund alimwambia dokta Ibrahim huku akionekana kuwa na wasiwasi.

    “Mkeo amejifungua sala. Yeye ni mzima na watoto wako ni wazima pia” Dokta Ibrahim alimwambia Edmund ambaye akaanza kurukaruka kwa furaha huku akimkumbatia kila mtu.

    “Asante Yesu” Edmund alisema kwa sauti kubwa.

    Kwa kipindi hicho hawakutakiwa kwenda kumuangalia Uki kwa sababu alikuwa akihitaji muda refu wa mapumziko kutokana na oparesheni ambayo alikuwa amefanyiwa. Baada ya saa moja, wakaruhusiwa kuingia ndani ya chumba kile na kuwafuata watoto hao mapacha ambao walikuwa wamezaliwa muda si mrefu.

    “Wa kwanza kuzaliwa yupi hapa?” Edmund alimuuliza dokta Ibrahim.

    “Wa kiume”

    “Kwa hiyo mtoto wangu wa kwanza ni mvulana. Kama ilivyopangwa, huyu ataitwa Eric na huyu ataitwa Erica” Ibrahim alisema huku akimnyanyua Eric.

    Huo ndio ukawa mwanzo wa furaha yao. Watoto ambao walizaliwa wakawafanya wawili hao kupendana zaidi na zaidi. Mapenzi yao yalikuwa makubwa kupita kawaida, watoto wao wakawaonganisha na kuzidi kuwaweka pamoja zaidi na zaidi. Baada ya miezi miwili kupita, Uki pamoja na Esta wakaruhusiwa kurudi nyumbani huku wakiwa wametumia muda wa miezi mitano kuwa hospitalini.

    Maisha yakaendelea zaidi na zaidi. Kila siku Edmund akawa mtu wa kurudi nyumbani mapema huku akiwa na hamu ya kukaa karibu na watoto wake. Hakutaka kabisa kuwa mbali nao, alihitaji kuwapa mapenzi ya dhati na malezi bora kama mzazi bora ambaye alitakiwa kuwafanyia watoto wake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog