Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

PAINFUL MEMORIES - 3

 





    Simulizi : Painful Memories

    Sehemu Ya Tatu (3)



    Miaka mitano ikawa imepita huku familia hiyo ikiendelea kuwa karibu zaidi na zaidi. Mapenzi yao yalikuwa makubwa kiasi ambacho kiliwafanya kila siku kuyaona maisha yao kuwa na furaha. Katika kipindi hicho, Eric pamoja na Erica walikuwa wakisoma katika shule ya chekechea ya St Patricia ambayo ilimgharimu Edmund kulipia kiasi cha shilingi milioni tano kwa kila mtoto wake kwa mwaka.

    Kwa wakati huo Edmund hakutaka kuangalia gharama zozote zile, kiasi cha fedha ambacho alikuwa akiingiza, makampuni makubwa ambayo alikuwa akimiliki yalikuwa yakimfanya kumgharimu kiasi kikubwa cha fedha katika kuhakikisha kwamba watoto wake wanapata Elimu bora na kuishi maisha ya kifahari.

    Edmund alikuwa amenunua gari la kifahari kwa ajili ya kuwapeleka watoto wake shuleni pamoja na kumuajiri mtu ambaye alikuwa dereva ambaye kazi yake kubwa ilikuwa ni kuwaendesha Eric na Erica kuelekea shuleni. Kila siku kazi ya dereva huyo ilikuwa ni kuwapeleka na kuwarudisha nyumbani huku akilipwa mshahara mkubwa na wa kutosha.

    Maisha ya Edmund na Uki kwa wakati huu yalikuwa ni maisha ya kitajiri, utajiri mkubwa ambao walikuwa wakiumiliki ulikuwa umeongezeka kwa kiasi kikubwa sana. Kwa wakati huo walikuwa wakimiliki vituo vya mafuta nchini Tanzania ambavyo viliitwa Eroil Total, walikuwa wakimiliki mabasi makubwa ambayo yalikuwa yakifanya safari zake kuelekea Zambia, Zimbabwe, Malawi, Kongo, Burundi, Rwanda, Kenya na Uganda. 

    Hiyo kwao ikaonekana kutokutosha kiasi ambacho kikawafanya kununua boti nne kubwa ambazo zikaanza safari yake kutoka Dar es Salaam kuelekea Zanzibar. Utajiri wao ulionekana kuongezeka zaidi na zaidi, wakafungua kampuni kuwa ya kutengeneza magazeti pamoja huku wakifungua vituo viwili vya televisheni.

    Maisha yao yalikuwa ya juu, walikuwa wamekwishajenga nyumba kubwa na ya kifahari ambayo ilikuwa na kila kitu ndani huku ikiwa na ukubwa wa eneo la mita tisini kwa upana na themanini kwa urefu. Kutoka na Edmund kuwa mjasiriamali mkubwa katika kipindi hicho, mara kwa mara alikuwa akiongeza biashara nyingine nyingi ambazo zilikuwa zikiwaingizia fedha nyingi sana.

    **********CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Maisha ya kitajiri yalikuwa yakiendelea kila siku. Edmund akafahamiana na wafanyabiashara wengi wakubwa ambao wakaanza kusaidiana katika vitu mbalimbali katika maisha yao. Kutokana na kumiliki biashara nyingi na kubwa, Edmund akajikuta akianza kuingia katika ugomvi na wafanyabiashara wawili, Bwana Pawasa ambaye nae alikuwa akimiliki vituo kadhaa vya mafuta pamoja na Bwana Tim ambaye alikuwa akimiliki mabasi mbalimbali yaliyokuwa yakielekea nje ya nchi hapa Afrika.

    Kila siku yalikuwa yakiongelewa maneno mengi yalikuwa yakiongelewa. Ugomvi ukaanza kutokota kati ya Edumnd pamoja na matajiri hao ambao walionekana kuanza kupoteza umaarufu wa biashara zao hasa mara baada ya Edmund kuanza kuingia kiasi kikubwa zaidi ya wao. Ugomvi wa chini chini ulikuwa ukitokota kila siku jambo ambalo lilipelekea waziri mkuu kuwaita kisiri na kuanza kuongea nao.

    Ugomvi ule ulionekana kuwa kama ungetokea waziwazi basi ungeweza kuleta matatizo katika nchu ya Tanzania kutokana na wote hao kuisaidia Tanzania katika kuipatia kiasi fulani cha fedha kadri mambo yalipokuwa yakienda ndivyo sivyo. 

    Waziri mkuu akawaweka chini na kuongea pamoja nao kwamba hakukutakiwa kutokea ugomvi wowote ule kwani wote walikuwa watu muhimu sana katika nchi hii. Mkataba wa amani wa siri wa maneno ukasainiwa usiku huo jambo ambalo likawafanya kuwa marafiki kama kawaida japokuwa kila mmoja kichwani mwake akiwa akifikiria kitu.

    Chuki dhidi ya Edmund zilikuwa zikiendelea kila siku, katika vikao vingi vya wafanyabiashara wakubwa hakuwa akiitwa jambo ambalo lilionekana kumuumiza kupita kawaida. Utajiri ambao alikuwa akimiliki katika kipindi hicho tayari ukaonekana kutishia amani kwa kuwafilisi matajiri wengine ambao walionekana kuwa na chuki za waziwazi katika kutotaka kuona Edmund akiingiza kiasi kikubwa cha fedha.

    Chuki zile ambazo zilikuwa zimejengeka vichwani mwa matajiri ndizo ambazo zilimfanya Edmund kuanza kufuatilia sana na watu wa TRA ambao walikuwa wakitaka kuona vibali vyake vingi kuhusu biashara zake alizokuwa akizifanya. Kwa sababu rushwa ilikuwa imetolewa, biashara za Edmund zikaonekana kuwa na kasoro nyingi.

    Barabarani, mabasi yake yalikuwa yakikamatwa hovyo kwa kuonekana kwamba yalikuwa na matatizo mengi, boti zake zilikuwa zikikatazwa kufanya kazi kwa sababu zilikuwa na kasoro nyingi ambazo wala hazikuwa zikijulikana kabisa. Vituo vyake vya mafuta vikaanza kutibuliwa pia, skendo za uchakachuaji wa mafuta ukaanza kuzungumzwa juu ya vituo vyake kiasi ambacho kikafikia kipindi vikafungwa vyote.

    Kila kitu ambacho kilikuwa kikiendelea katika kipindi hicho kilikuwa kikifanyika chini ya watu wawili ambao walikuwa matajiri wakubwa, Bwana Tim pamoja na Bwana Pawasa. Hali ile ikaonekana kuanza kumuumiza sana Edmund kiasi ambacho akaamua kulifikisha suala hilo katika vyombo vya sheria kuangalia kama vile vilivyokuwa vikiongelewa juu ya biashara zake vilikuwa vya kweli au vilikuwa vya uongo.

    Kazi haikuwa ndogo kabisa. Kitu alichokifanya Edmund ni kuwafungulia kesi waarabu wa Saudi Arabia kwa kumuuzia mafuta ambayo yalikuwa yamechakachuliwa. Kesi hiyo ikaonekana kuwa kubwa jambo ambalo ikaamuliwa ifikishwe mahakamani. Vyombo vingi vya habari vikaanza kuielezea kesi ile ambayo ilionekana kuwa kubwa kuwahi kutokea nchini Tanzania ambayo ilikuwa ikimhusisha tajiri mkubwa.

    Katika kipindi hicho Bwana Tim na Bwana Pawasa wakaonekana kufurahia kile ambacho kilikuwa kimetokea, kitendo cha kumuona Edmund akianza kukorofishana na waarabu kilinekana kuwafurahisha. Kitu walichokifanya kwa wakati huo nao kuanza kuifuatilia kesi hiyo ambayo ilikuwa ikiandikwa katika vyombo mbalimbali vya habari.

    Huku kesi hiyo ikiwa inaendelea, Edmund akaanza kufungua kesi juu ya kampuni ya Marcopolo ambayo ilikuwa ikimuuzia mabasi makubwa ya abiria. Kesi mbili kwa pamoja zilikuwa zikiendelea kama kawaida. Huku kesi hizo zikiwa zimepamba moto, Edmund akafungua kesi na kampuni ya Kimarekani ambayo ilikuwa ikimuuzia boti ambazo alikuwa akizitumia kusafirisha abiria kuwapeleka Zanzibar na kuwarudisha Dar es Salaam.

    Kesi tatu kwa pamoja zilikuwa zikiendelea, kwa wakati huo Edmund alikuwa akionekana kuwa kama mtu ambaye alichanganyikiwa, alionekana kufanya kitu ambacho hakuwa akikielewa kilikuwa na madhara gani katika maisha yake. Mara kwa watu mbalimbali, viongozi wa nchi pamoja na matajiri wengine waliopenda maendeleo yake walikuwa wakimfuata na kumwambia kuachana na kesi zile lakini Edmund hakutaka kuelewa kabisa.

    “Nitaendelea kuhakikisha kesi zinaendelea” Edmund alimwambia mke wake, Uki.

    “Hilo linaweza kuwa tatizo mume wangu. Achana nao” 

    “Haiwezekani. Yaani hapa kuna mpango mmoja mkubwa sana ambao nimeupanga” Edmund alimwambia mke wake.

    “Mpango gani?”

    “Wewe subiri. Yaani hawa wamenichezea mimi Genius. Sasa nataka kuwaonyeshea kwamba nina akili zaidi yao” Edmund alimwambia Uki.

    “Mmmh! Mbona sikuelewi umemaanisha nini”

    “Usijali. Mwisho wa siku, utakuja kunielewa. Ila jua kwamba nina akili zaidi yao” Edmund alimwambia Uki huku akitabasamu.

    “Mmmh! Aya”

    Japokuwa jambo lile lilionekana kutaka kumyumbisha Edmund lakini kwake akaonekana kuwa na furaha. Kufuangua kesi kule kulionekana kufanyika makusudi ili mwisho wa siku kuanze kuleta kitu cha tofauti, kitu ambacho kingemuingizia fedha fedha zaidi ya zile ambazo zilikuwa zinatakiwa kuingia.

    Hakukuwa na mtu ambaye alikuwa akiufahamu mpango ambao Edmund alikuwa ameuweka, mpango ule ulikuwa ukijulikana na yeye tu, hakutaka mtu yeyote aufahamu, alitaka aufahamu yeye tu. Mpango ule kwake ukaonekana kuwa kiboko, mpango ule kwake ukaonekana kumuingizia fedha hapo baadae. 

    “Nina akili zaidi yao” Hayo ndio maneno ambayo alikuwa akiongea Edmund mara kwa mara huku watu wote wakiona kwamba alikuwa njiani kufilisika.

    *********CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kesi bado zilikuwa zikiendelea. Kitu alichokifanya Edmund ni kumchukua mwanasheria wake, Bwana Idrisa Kavishe ambaye ndiye alikuwa akisimamia kesi ile kwa upande wake. Magazeti pamoja na vyombo mbalimbali vya habari vilikuwa vikitangaza kuhusu kesi ile ambayo mpaka katika kipindi hicho, tayari Edmund alionekana kuanza kuzidiwa na hatimae baadae kufilisika.

    Kila gazeti ambalo lilikuwa likiandika kuhusiana na kesi ile lilikuwa likinunuliwa sana kupita kawaida kiasi ambacho kiliwafanya waandishi wa magazeti kuendelea kuitangaza habari ile zaidi na zaidi. Kila siku Edmund alikuwa akionekana kuwa na furaha, tayari mipango yake ilikuwa ikionekana kukamilika.

    Bwana Msantu ndiye ambaye alikuwa akikaa sana na Edmund na kisha kuongea nae. Mzee huyo hakuonekana kuwa na furaha, kwake, mali ambazo alikuwa akizimiliki Edmund zilikuwa kama mali zake pia. Hakutaka kuona Edmund akipatwa na matatizo kuhusiana na biashara zake. Mara kwa mara alikuwa akimsisitiza Edmund kuachana na kesi zile ambazo alikuwa amewashitaki Wamarekani na Waarabu lakini edmund hakuonekana kukubali hata kidogo, bado alikuwa aking’ang’ania tu.

    Siku ya kesi ikafika na kisha kesi kusikilizwa, nusu ya Watanzania walikuwa wametegesha masikio yao kuisikiliza kesi hiyo huku mahakamani kukiwa na idadi kubwa ya watu ambao walikuwa wamekwenda kuhudhuria kesi hiyo ambayo ilizidi kuvuma zaidi na zaidi. Mwanasheria, Kavishe alikuwa amesimama kama kawaida yake. Kadri kesi zilivyozidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo alikuwa akilitangaza jina lake zaidi na zaidi.

    “Nawashitaki kwa sababu wameniuzia mafuta ambayo yamechakachuliwa” Edmund aliiambia mahakama huku kila mtu akiwa kimya kumsikiliza.

    “Nimefanya nao biashara kwa kipindi kirefu sana, mwisho wa siku wameamua kuniuzia mafuta ambayo yamechakachuliwa” Edmund alimwambia hakimu.

    Kesi bado ilikuwa ikisikilizwa zaidi na zaidi huku waarabu wale wakijitetea kwamba mafuta ambayo walimuuzia Edmund hayakuwa yamechakachuliwa. Kitu ambacho walikitaka waarabu wale ni kuomba kwenda kuyaangalia mafuta hayo ambayo yalikuwa yamebaki katika visima vya vituo vya mafuta vya Eroil Total.

    Siku hiyo hiyo, kesi nyingine ikaendelea. Kama kawaida yake Edmund akasimama na kisha kuanza kuwashitaki Wajerumani ambao walikuwa wamemuuzia mabasi mabovu ambayo vifaa vyake havikuwa imara. Ile ikaonekana kuwa kama shutuma kwao, Wajerumani wakajitahidi kujitetea kwamba mabasi ya kampuni ya Marcopolo ambayo walikuwa wamemuuzia Edmund yalikuwa mazuri na hayakuwa na kifaa chocote kibovu.

    Hali haikuishia hapo. Baada ya kesi hiyo kuisha, ikaaingia kesi nyingine huku Edmund akiwashitaki Wamarekani kwa kumuuzia boti ambazo zilikuwa mbovu. Kama ilivyokuwa kwa wengine, nao Wamarekani wakaonekana kupinga kupita kawaida kwa kudai kwamba boti ambazo walikuwa wakimuuzia Edmund zilikuwa imara na wala hazikuwa na matatizo yoyote yale.

    Kitu kilichofanyika kwa wakati huo ni washitakiwa kuwaita watu wao kwa ajili ya kuchunguza vitu vyote ambavyo walikuwa wamemuuzia Edmund. Kitu cha kwanza, Waarabu wakawaita wataalamu wao na kisha kuyaangalia mafuta yale kuona kama yalikuwa yamechakachuliwa au la. Mafuta yakaonekana kuwa mazuri na wala hayakuwa yamechakachuliwa hata kidogo.

    Wamarekani nao wakawaita wataalamu wao na kisha kuanza kuchunguza vifaa vya meli zao ambazo zilisemekana kuwa na vifaa vibovu, hakukuonekana kuwa na tatizo lolote lile jambo ambalo liliacha maswali juu ya sababu ya Edmund kuwafungulia kesi.

    Wajerumani nao hawakutaka kukubali. Nao wakawaita wataalamu wao na kisha kuwataka kuangalia vifaa vya mabasi yale, kila kifaa kilikuwa kizima. Tayari mambo yakaonekana kwenda ndivyo sivyo, kwa kipindi hicho, Edmund akaanzisha kesi kuishitaki serikali ambayo ilikuwa imedai kwamba mafuta yake yalikuwa yaechakachuliwa na hivyo vito vyake kufungwa, mabasi yake pamoja na boti zake kutokufanya kazi kwa sababu zilikuwa na vifaa vibofu.

    “Mmmmh! Mbona inachanganya hapa!” Mwanaume mmoja alimwambia mwenzake huku akionekana kushangaa.

    “Ndio hivyo. Jamaa kaamua kuishitaki serikali” 

    Hapo ndipo vuguvugu lilipoanza. Mpaka kesi juu ya Waarabu, Wajerumani na Wamarekani inaisha na kuonekana kutokuwa na hatia, kesi ikawa juu ya Serikali. Kila siku Edmund alikuwa akilalamika kwamba serikali ilikuwa imemfanyia mchezo mchafu wa kutaka kumfilisi na ndio maana waliamua kuzusha maneno mengi.

    Kesi ikaonekana kuwa kubwa. Watu wote ambao walikuwa nyuma ya tukio lile wakaitwa mahakamani. Kwa sababu kulikuwa na myororo mkubwa wa watu ambao walikuwa wamehusika, watu wengi wakaachishwa kazi na hivyo kufikishwa mahakamani. Kesi ya Edmund haikuangalia mtu mmoja mmoja, yeye alikuwa akiishitaki serikali tu.

    Hapo ndipo hali ilipoonekana kuwa mbaya kwa serikali ya Tanzania, kwa jinsi kesi ilivyokuwa kubwa, tayari wakaonekana kushindwa. Mara kwa mara Edmund alikuwa akipigiwa simu na viongozi mbalimbali wa serikali kwa ajili ya kumuomba msamaha juu ya yale ambayo yalikuwa yametokea lakini edmund hakuonekana kukubali, tayari alikuwa amepoteza kiasi kikubwa cha fedha.

    Kesi iliendelea mpaka pale ambapo serikali ikatakiwa kumlipa Edmund kiasi cha shilingi trilioni mbili kama fidia juu ya kile ambacho kilikuwa kimetokea. Serikali ikaonekana kutikisika, kiasi cha fedha ambacho kilitakiwa kulipwa kama fidia kilikuwa kikubwa sana

    Bwana Tim pamoja na Pawasa wakaonekana kuwa kwenye hali mbaya, tayari mambo yakaonekana kuwageukia. Watu ambao walikuwa wamewapa rushwa tayari wakaonekana kutokuwa wavumilivu na hivyo kuwataja. Hiyo ilikuwa moja ya skendo kubwa nchini Tanzania, bwana Tim pamoja na Pawasa wakaitwa mahakamani na hivyo kufunguliwa kesi ikiwa pamoja na kutoa rushwa.

    Serikali haikuwa na uezo wa kutoa kiasi kikubwa cha fidia ambacho kilitakiwa kutoa, mpaka kipindi hicho, serikali iliahidi kutoa robo ya fidia ile huku ikijaribu kumuita Edmund na kumuomba kwamba alitakiwa kuwasamehe kwa kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea. Edmund hakukubali kirahisi, tayari aikuwa amepoteza muda wake wote na fedha nyingi ambazo alitakiwa kupokea.

    Kuanzia hapo, serikali ikaamua kumsamehe kodi zote ambazo alitakiwa kukatwa kwa muda wa miaka hamsini. Hiyo ilikuwa ni furaha kubwa kwa Edmund. Akalipwa kiasi cha bilioni mia tano na kisha kusamehewa kodi hizo. Hilo lilionekana kuwa kama pigo kwa serikali lakini katika kipindi hicho ilitakiwa kukubaliana na kila kitu.

    “Kwa hiki kilichotokea. Hakikisheni Tim na Pawasa wanashitakiwa ipasavyo” Waziri mkuu aliwaambia wahusika.

    Tayari kiasi kikubwa cha fedha kilikuwa kimetoka katika mfuko wa serikali, ujinga wa watu wachache ambao ulikuwa umefanyika ndi ambao ulikuwa umewaingiza katika matatizo hayo makubwa. Watu woteambao walihusika katika fitina zile wakapelekwa mahakamani na hukumu kutolewa. 

    Hukumu ya kifungo cha miaka kumi jela ndicho kilichowakuta Bwana Tim na Pawasa. Kila kitu katika maisha yao kikaonekana kubadilika, maisha ya gerezani ndio ambayo yalikuwa yakienda kuanza kwa wakati huo. Pamoja na kuwekwa jela, lakini bado walikuwa na kisasi mioyoni mwao, walitaka kufanya kitu ambacho kingemfanya Edmund kutokuwasahau katika maisha yake yote.

    ****

    Maisha yalikuwa yakiendelea kama kawaida. Edmund alikuwa amekwishaonekana kuwa mshindi kwa kile ambacho kilikuwa kikimuandama kwa muda mrefu sana. Robo ya malipo yake yalikuwa yaekwishafanyika na hivyo kuanzia hapo hakutakiwa kukatwa kodi ya biashara zake kwa muda wa miaka hamsini.

    Boti zake tayari zilikuwa zikiendelea kufanya kazi kama kawaida na kumuingizia kiasi kikubwa cha fedha. Vituo vyake vya mafuta navyo vilikuwa vikiendelea kuuza mafuta kama kawaida huku kwa wakati huu wateja wengi wakiwa wameongezeka. Pamoja na hayo yote, hata mabasi yake ya kwenda nchi za nje nayo yalikuwa yaikendelea na kazi zake kama kawaida.

    Kwa wakati huu mafanikio yake yakaonekana kuwa makubwa sana hata zaidi ya alivyokuwa akiyapata katika kipindi kile cha kabla ya kesi zile. Fedha zilikuwa zikimiminika katika akaunti yake kila siku jambo ambalo lilimfanya kupata mafanikio makubwa sana huku akishika namba tatu ya matajiri wote nchini Tanzania.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Bado mapenzi yake kwa familia yake yalikuwa makubwa sana, alikuwa akiipenda familia yake kuliko kitu chochote kile, aliithamini familia yake huku akitengeneza upendo mkubwa kwa watoto wake ambao kwa kipindi hicho walikuwa wakisoma chekechea katika shule ya St’ Patricia iliyokuwa Masaki jijini Dar es Salaam.

    Miezi iliendelea kukatika mpaka mwaka mmoja kumalizika na hatimae kuwaanzisha watoto wake darasa la kwanza katika shule ya St’ Marry jijini Dar es Salaam. Maisha bado yalikuwa yakiendelea kuwa ya furaha na upendo mkubwa. Mara kwa mara Edmund alikuwa akirudi nyumbani mapema na kukaa na familia yake ambayo ilikuwa ikimhitaji kila siku.

    Maendeleo ya watoto wake shuleni yalikuwa mazuri kupita kawaida. Walifahamu kusoma kwa haraka sana katika kipindi kile walichokuwa chekechea. Erica akawa mwanafunzi ambaye alipendelea sana masomo ya Sayansi lakini Eric alikuwa mwanafunzi ambaye alipendelea sana somo la hesabu.

    Vichwa vyao vikaonekana kuwa vyepesi kuelewa na vigumu kusahau jambo ambalo hata pale ambapo walikuwa darasa la kwanza, walimu walibaki wakiwashangaa. Mapacha hawa walikuwa kama mapacha wengine ambao walikuwa wamezaliwa katika familia yingine nyingine. Muda wote walikuwawakitaka kuwa pamoja tu.

    Darasani walikuwa wakikaa katika viti vilivyokuwa karibu karibu sana. Walikuwa wakivaa sare mpaka nyumbani huku muda mwingi wakitaka kuwa pamoja. Upendo wao ambao ulitengenezwa na wazazi wao ndio ambao uliwafanya kuwa karibu kupita kawaida. Lilipokuwa linatokea jambo lolote ambalo lilimfanya mmoja wao kulia, wote walikuwa wakilia, au hata mmoja wao kucheka, wote walikuwa wakicheka.

    Uwezo wao wa darasani ulikuwa ukionekana kuwaogopesha sana walimu, walikuwa wakionekana kuwa na akili za tofauti zaidi ya wanafunzi wengine wa shule hiyo. Mitihani yao walikuwa wakiifanya vizuri na kupata alama za juu zaidi ya wanafunzi wote jambo ambalo liliwapa sana furaha wazazi wao ambao mara kwa mara walikuwa wakiwanunulia zawadi mbalimbali kama kuwapongeza.

    Miezi ikaendelea kukatika na hatimae mwaka mwingine kuingia. Uwezo wao wa darasani wala haukupungua, ulizidi kuongezeka zaidi na zaidi kila siku. Walipoingia darasa la pili, uwezo wao ukawa mkubwa zaidi na wanafunzi ambao waliokuwa nao jambo liliowafanya walimu kuwapandisha darasa na kuwa darasa la tatu. Uwezo wao ulionekaa kuwa wa ajabu sana.

    Japokuwa walikuwa wamepandishwa darasa na kuwa darasa la tatu lakini bado waliendelea kuwakimbiza wanafunzi wenzao wa darasa la tatu kitu ambacho kilionekana kuwa kama muujiza. Mara kwa mara walimu walipokuwa wakiweka kikao, walikuwa wakipenda kuwazungumzia Eric na Erica ambao walikuwa juu sana kielimu.

    “Kwa hiyo tuwafanye nini sasa? Au tuwapeleke levo ya mwisho kabisa?” Mwalimu mkuu wa shule hiyo aliwauliza walimu.

    “Kuwapeleka grade seven?”

    “Ndio”

    “Mimi naona tusifanye hivyo. Hapa hapa tuendeleeni nao” Mwalimu Christopher aliwaambia.

    Bado akili za watoto hao zilionekana kuwa za ajabu, Edmund na Uki walikuwa wakiitwa mara kwa mara shuleni pale na kuambiwa maendeleo ya watoto wao jambo ambalo liliwafurahisha zaidi na zaidi na kuendelea kuwanunulia zawadi zaidi na zaidi kama namna moja wapo ya kuwahamasisha kufanya kile ambacho walikuwa wakiendelea kukifanya.

    Mwaka mwingine ukakatika na hatimae mwaka mwingine kuingia na kuwa darasa la nne. Makali yao hayakupungua jambo ambalo liliendelea kuwafariji wazazi wao na muda wa likizo ulipofika kuamua kwenda nchini Marekani kwa ajili ya kupumzisha akili zao. Walichukua muda wa mwezi mmoja kukaa nchini Marekani na ndipo hapo walipoamua kurudi nchini Tanzania kuendelea na shughuli zao kama kawaida.

    “Kichwa kinauma” Erica alimwambia Uki, mama yake alipokuwa akiamshwa kuelekea shuleni.

    “Kimeanza lini?” Uki aliuliza huku akionekana kuogopa kwani hakupenda watoto wake waumwe ugonjwa wowote ule.

    “Jana usiku” Erica alijibu.

    Uki akamuinua Erica na kisha kuelekea jikoni ambako akafungua kabati la vyombo sehemu ambayo ilikuwa ikihifadhiwa dawa na kisha kutoa vidonge na kisha kumywesha Erica. Uki hakutaka kuipuuzia hali ile, alichokifanya ni kumchukua Erica na kumpeleka hospitalini huku akimuagiza dereva amachukue Eric ambaye muda mwingi alikuwa akilia kutokana na Erica kuumwa na kumpeleka shuleni.

    “Usijali Eric. Mdogo wako atapona” Uki alimwambia Eric simuni.

    “Sawa mama” Eric alimwambia mama yake, Uki.

    Siku hiyo haikuonekana kuwa siku ya furaha kwa Eric, muda wote alikuwa akionekana kuwa na majonzi mno. Kuumwa kwa dada yake, Erica kulikuwa kumemuumiza kupita kawaida. Darasani, hakukusomeka kabisa, muda mwingi Eric alikuwa akionekana mgonjwa huku akiia tu. Alimpenda sana dada yake kuliko mtu yeyote katika maisha yake, hakutaka kumuona akipata matatizo ya aina yoyote ile.

    Eric alikuwa akiombea muda uende harakaharaka ili aondoke na kuelekea nyumbani kwa ajili ya kumuona dada yake na kujua hali yake ilivyokuwa ikiendelea kwa wakati huo. Muda wa kuondoka nyumbani ulipofika, dereva akamfuata na kisha kuingia garini na kuanza kuondoka kuelekea nyumbani.

    “Nataka kumuona dada” Eric alimwambia dereva ambaye alikuwa bize akiendesha gari.

    “Usijali. Tutafika sasa hivi” Dereva alijibu katika kipindi ambacho walikuwa wakikaribia kufika General Tyre Msasani.

    Gari liliendelea kwenda kwa mwendo wa kawaida. Kwa mbali mbele likaanza kuonekana gari kubwa aina ya lori ambalo lilikuwa limebeba matofari likija kwa kasi huku watu wakisikika wakipiga kelele. Dereva aliliona lori lile, alichokifanya ni kuanza kupunguza mwendo. Lori lile lilionekana kwenda upande mwingine lakini lilipokuwa likiwafikia, likabadilisha muelekeo na kuanza kulifuata gari lao.

    Dereva akaonekana kushtuka, alichokifanya ni kufunga breki na kutaka kulirudisha gari nyuma. Hali hiyo ikashindikana kufanyika kwa sababu nyuma ya gari lao kulikuwa na gari jingine huku mbele yao kukiwa na tuta.

    Dereva akaonekana kuchanganyikiwa, alichokifanya kwa wakati huo ni kutaka kuufungua mlango na kutoka nje ya gari lile. Kwa sababu akili yake ilikuwa imechanganyikiwa, akajikuta hata ile batani ya kuuachia mkanda akiwa haioni. Hali hiyo haikuwa kwake peke yake, hata kwa Eric ambaye alikuwa siti ya mbele ilikuwa vile vile.

    Lori lile likawa limekwishafika karibu yao kabisa huku likiwa kwenye mwendo wa kasi, lilipofika katika lile tuta, likaenda kwa juu na kisha kulivamia gari lile kwenye usawa wa kioo cha mbele, kilichotokea hapo ni kusikika mlio mkubwa. Taili la mbele la lori lile likawa limemfikia dereva kifuani na kumuua pale pale taili jingine likiwa limemmfikia Eric kifuani na kumbana vilivyo.

    Ingawa wote walikuwa wamebanwa na mataili lakini kwa Eric ikaonekana kumsaidia kwa sababu alikuwa amekisogeza kiti kwa nyuma. Taili likawa limembana kifuani, damu nyingi zilikuwa zikimtoka puani huku akichezacheza pale kwenye kiti kama mtu ambaye alikuwa akikata roho. Vipande vya vioo vya kioo kile cha mbele vilikuwa vimechanachana kichwani hali ambayo ilisababisha fuvu lake la kichwa kuonekana katika kila sehemu ambayo vioo vile vilikuwa vimechana.

    Watu wote waliokuwa wameshuhudua ajali ile wakaonekana kushika vichwa vyao kwa huzuni huku watu wengine wakianza kuelekea kule kulipotokea ajali ile. Kitu ambacho kilimshangaza kila mtu ni kwamba dereva wa lile lori tayari alikuwa amekwishakimbia katika eneo lile. Vijana watatu wakalisogelea gari lile na kuufungua mlango na kumtoa Eric na kisha kuanza kumpandisha Eric katika gari lao na kisha kuanza kumpeleka hospitalini huku damu zikiendelea kumtoka na huku akiendelea kuutisngishatingisha mwili wake kama mtu ambaye muda wowote ule angekata roho.

    “Mmmh! Hadi fuvu linaonekana” Kijana mmoja alisema kwa mshtuko huku akikiangalia kichwa cha Eric ambacho kilikuwa kimechanwachanwa na vipande vya kioo kile.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Gari lilikuwa likiendelea kwenda kwa mwendo wa kasi kuwahi hospitalini kwa ajili ya kumfikisha Eric hata kabla mambo hayajawa mabaya kabisa. Muda wote Eric bado alikuwa akiendelea kuuchezeshachezesha mwili wake kama mtu ambaye alikuwa akienda kukata roho muda wowote ule.

    Baada ya dakika chache tayari walikuwa wamekwishaingia katika eneo la hospitali ya Muhimbili ambako Eric akashushwa na kuingizwa kwenye moja ya machela ambazo zilikuwa nje katika eneo la hospitali ile. Gari lote lilikuwa limetapakaa damu, kila mtu ambaye alikuwa akimwangalia eric kwa namna alivyokuwa amejeruhiwa, alibaki kuwa na mshtuko moyoni.

    Machela ikaanza kusukumwa kuelekea ndani ya chumba cha upasuaji na kisha madaktari wote kuanza kufanya kazi zao kama kawaida huku wakijaribu kila njia kuokoa maisha ya Eric ambaye mwili wake ulikuwa ukiendelea kuchezacheza tu. Kazi haikuwa ndogo hata kidogo, madaktari waliendelea na kazi yao kwa muda wa saa moja, kidogo hali ikaonekana kuwa nafuu.

    Vipande vyote vya chupa ambavyo vilikuwa vimezama mwilini mwa Eric hasa katika sehemu ya uso pamoja na kichwani wakaviondoa na kisha kuanza kumsafisha na kisha kumuwekea dawa na kumpa muda wa kupumzika huku wakiwasubiria ndugu zake.

    ****

    Polisi walifika katika eneo la tukio, gari lilikuwa limegongwa vibaya na lori lile ambalo lilikuwa juu ya gari ile ndogo. Mwili ambao ulikuwa ukionekana katika kipindi hicho ambacho walikuwa wamefika ulikuwa mmoja tu. Polisi huku wakisaidiana na wananchi wengine wakaanza kuutoa mwili ule ambao ulikuwa umebanwa na taili katika kiti kile cha mbele kabisa.

    “Sasa kwa nini wameondoka na mwili mmoja?” Polisi mmoja aliuliza huku akionekana kushangaa.

    “Nadhani kwa sababu yule mtoto alikuwa mzima japokuwa alikuwa akielekea kukata roho muda wowote ule. Kwa namna moja au nyingine waliamua kumuwaisha hospitali kwa sababu huyu hapa tayari alikuwa amekwishafariki” Kijana mmoja ambaye walikuwa wakisaidiana nae alimwambia polisi yule.

    Mwili wa dereva haukuwa rahisi kutoka katika sehemu ile kitu ambacho kiliwafanya kukivuta kiti kwa nyuma na ndipo walipofanikiwa kuutoa. Damu zilikuwa zimetapakaa ndani ya gari lile, kifua cha dereva kilikuwa kimepasuka katikati. Kadri muda ulivyozidi kuongezeka mahali hapo na ndivyo ambavyo watu walivyozidi kuongezeka zaidi na zaidi huku hata waandishi wa habari wakiwa wamekwishafika katika eneo la ajali ile.

    “Hebu upekueni huo mwili mifukoni mwake kama kutakuwa na simu” Polisi mmoja alisema na hapo hapo kuanza kuupekea mwili ule katika mifuko ya suruali na kisha kutoa simu.

    Alichokifanya polisi yule mara baada ya kuichukua simu ile ni kuanza kutafuta namba fulani za watu wa karibu ambao alijua fika kwamba walikuwa wakiwafahamu watu wale ambao walikuwa wamepata ajali. Majina yalikuwa mengi simuni lakini walipofika katika jina lililoandikwa ‘Bosi’ hapo hapo akapiga namba ile na simu kupokelewa.

    “Umemrudisha salama Eric?” Sauti ya Edmund iliskika.

    “Samahani kidogo” Polisi yule alimwambia Edmund.

    “Wewe nani?” Edmund aliuliza huku akionekana kufahamu kwamba sauti ile haikuwa ya dereva ambaye alikuwa akiwaendesha watoto wake.

    “Unaongea na sajenti Edward hapa” Polisi yule alijibu.

    “Mungu wangu! Kuna nini tena? Gari langu limekamatwa?” Edmund aliuliza.

    “Hapana. Kuna ajali imetokea” Polisi yule alijibu.

    “Kuna ajali imetokea?”

    “Ndio”

    “Imetokea wapi?”

    “Hapa Msasani. Gari yako si hii yenye namba T113 NMC?” Polisi yule aliuliza.

    “Ndio”

    “Imepata ajali. Imegonga na lori lililobeba matofali” Polisi yule alimwambia Edmund.

    “Unasemaje?” Edmund aliuliza huku akionekana kuchanganyikiwa.

    “Ndio hivyo. Miili imepelekwa hospitalini sasa hivi”

    “Kwa hiyo una maana wote wamekufa? Unamaanisha mwanangu Eric amekufa?” Edmund aliuliza huku akisikika kama mtu aliyekuwa akitaka kulia.

    “Hapana. Ni dereva ndiye aliyekufa”

    “Na vipi kuhusu mtoto wangu?”

    “Hali yake haikuwa nzuri kabisa. Yaani ilikuwa mbaya sana. Cha msingi hebu tukutane Muhimbili” Polisi yule alijibu na kisha kukata simu.

    *****

    Edmund alionekana kuchanganyikiwa kupita kawaida. Taarifa ambayo alipewa na polisi ilionekana kumchanganya sana. Alichokifanya mahali hapo ni kumpigia simu mke wake ambaye bado alikuwa hospitalini na kutaka kuonana nae hapo hapo hospitalini alipokuwa hata kabla hawajakwenda katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

    Edmund hakutaka kumwambia Uki kile ambacho kilikuwa kimetokea lakini kwa namna ambayo Edmund alikuwa ameongea na mke wake, Uki tayari hali ikaonekana kumtia wasiwasi kupita kawaida. Alichokifanya Edmund ni kutoka ofisini huku akiwa amechaganyikiwa kupita kawaida kiasi ambacho hakutaka kumuaga hata sekretari wake.

    Edmund alikuwa akiendesha gari lake kwa mwendo wa kasi kuelekea katika hospitali ya Agha Khan kwa ajili ya kumchukua mke wake. Mara baada ya kufika hospitalini akamkuta mke wake, Uki nje akiwa pamoja na Erica na kisha kuteremka.

    “Kuna nini mume wangu?” Uki aliuliza huku akionekana kuchanganyikiwa.

    “Pandeni ndani ya gari kwanza”

    “Lakini nimekuja na gari langu”

    “Achana nalo kwanza. Ingia ndani ya gari hili. Kla kitu utajua mbele ya safari” Edmund alimwambia Uki ambaye akaingia ndani ya gari lile pamoja na Erica.

    “Kuna nini mume wangu?”

    “Eric amepata ajali” Edmund alitoa jibu ambalo liliufanya moyo wa Uki kupigwa ganzi.

    “Unasemaje?”

    “Ndio hivyo. Dereva amekufa hapohapo” Edmund alimwambia Uki.

    “Na Eric?” Uki aliuliza.

    “Hajafa ila hali yake si nzuri kabisa”

    “Mungu wangu!” Uki alisema na kuanza kulia.

    Walitumia muda wa dakika kadhaa mpaka kufika katika hospitali ya Muhimbili ambapo wakateremka na kuanza kuelekea sehemu ya mapokezi huku kila mmoja akionekana kuchanganyikiwa. Walipofika mapokezini, wakaanza kuulizia, wala hawakupata tabu, wakaelekezwa sehemu ya kwenda.

    “Karibu” Dokta Ibrahim aliwakaribisha huku akiwafahamu.

    “Tuambie kuhusu mtoto wetu” Edmund alimwambia dokta Ibrahim.

    “Subirini kwanza. Kaeni hapo kwenye benchi” Dokta Ibrahim aliwaambia na kisha kuingia katika chumba cha oparesheni.

    Hakukuwa na mtu ambaye alikuwa radhi kukaa benchini, wote walibaki wakiwa wamesimama wima huku wakimsikilizia dokta ambaye aliingia ndani ya chumba kile. Kila mmoja kwa wakati huo alikuwa na wasiwasi, muda wote Uki alikuwa akilia kama mtoto. Ni Edmund pekee andiye ambaye alikuwa akimfariji kwa wakati huo mgumu.

    *******CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Lilionekana kuwa janga kubwa na baya sana kuwahi kutokea katika familia hii ambayo ilikuwa ikiishi katika mapenzi makubwa pamoja na upendo wa hali ya juu. Ajali ambayo ilikuwa imetokea ilionekana kuishtua sana familia hii. Wote walikuwa kwenye wakati mgumu katika kipindi hicho, si Edmund, si Uki na wala si Erica, wote walikuwa wakilia kwa uchungu.

    Madaktari walionekana kuwa bize kwa wakati huo wakimshugulikia Eric ambaye alikuwa hoi kitandani kutokana na kupata ajali mbaya ambayo imetishia maisha yake. Muonekano wa daktari Ibrahim tayari ulikuwa umewaongezea wasiwasi mkubwa. Ni kweli kwamba dokta Ibrahim alikuwa akiongea kwa tabasamu la mbali lakini katika macho ya Edmund na Uki tabasamu lile lilionekana kuwa kama unafiki.

    Hakukuwa na mtu ambaye alikuwa na uhakika kwamba Eric alikuwa hai ndani ya chumba kile. Walichokifanya kwa wakati huo ni kushikana mikono kama ishara ya upendo huku wakimuomba Mungu amsaidie Eric ambaye alikuwa kwenye hali mbaya ndani ya chumba cha upasuaji.

    Baada ya masaa mawili, mlango ukafunguliwa na kisha dokta Ibrahim kutoka ndani ya chumba kile huku akionekana kuchoka kupita kawaida. Alichokifanya mahali hapo ni kuwataka kumfuata ndani ya ofisi yake kwa ajili ya kuongea nao na kuwaelezea jinsi hali ilivyokuwa juu ya mtoto wao, Eric.

    Wote wakaanza kumfuata mpaka ndani ya ofisi ile na kisha kuanza kuongea nao. Dokta hakuonekana kuwa katika hali ya kawaida, tabasamu lile la kinafiki ambalo alikuwa amewaonyeshea katika kipindi cha nyuma kwa wakati huu halikuonekana tena usoni mwake hali iliyoonyesha kwamba kulikuwa na dalili kwamba hali ya Eric haikuwa nzuri kabisa.

    “Poleni sana kwa hali iliyowakuta” Dokta Ibrahim aliwaambia.

    “Asante dokta” Wote waliitikia kiunyonge.

    “Hali ya mtoto wenu si nzuri sana. Mwili wake umepata majeraha makubwa sana kiasi ambacho kimeonekana hata kutushangaza sisi wenyewe” Dokta alisema huku akionekana kuwa na huzuni kubwa moyoni mwake.

    “Mungu wangu! Eric ataweza kupona?” Edmund aliuliza kwa sauti iliyojaa majonzi.

    “Kupona ataweza kupona ila itabidi tufanye kazi ya zaida sana. Kichwa chake kimepata majeraha makubwa, mbavu zake mbili zimevunjika, nadhani hii ni kwa sababu kulikuwa na kitu kizito ambacho kilikuwa kimembana” Dokta Ibrahim aliwaambia maneno ambayo yalionekana kuwakatisha tamaa.

    “Ila atapona?” Edmund aliuliza.

    “Atapona japokuwa anaweza kuchukua muda mrefu. Itatupasa tuendelee kumshughulikia kila siku” Dokta Ibrahim aliwaambia.

    “Hatuwezi kumuona kwa sasa?” Edmund aliuliza huku muda wote Uki akiwa analia tu.

    “Kwa leo haiwezekani kabisa. Inawezekana kesho kutwa ndio mkaruhusiwa kumuona” Dokta Ibrahim aliwaambia.

    “Tunakuomba dokta. Tunahitaji kumuona Eric” Edmund alimwambia dokta.

    “Haiwezekani. Hiyo ni kwa sababu ambazo zipo nje ya uwezo wetu” Dokta aliwaambia.

    Majonzi yakaonekana kuongezeka mioyoni mwao, tayari matumaini yote ambayo walikuwa nayo yakaonekana kupotea katika mioyo yao. Kwa wakati huo, walijiona kuwa katika kipindi kigumu kuliko vipindi vyote walivyokuwa wamepitia kama familia. 

    “Kuna kitu unaonekana kutuficha” Edmund alimwambia dokta ambaye alionekana kuwa kwenye hali fulani isiyo ya kawaida.

    “Hapana. Hakuna kitu cha kuwaficha” Dokta Ibrahim alijibu.

    “Kuna kitu. Naomba utuambie kuna nini kinaendelea”

    Dokta akakaa kimya kwa muda, akayainamisha macho yake chini na kisha kuyarudisha nyusoni mwao. Dokta Ibrahim alionekana kuwa na dukuduku la kutaka kuwaambia kwa wakati huo. Wote wakabaki kimya huku wakimwangalia dokta ambaye alionekana kuwa na wasiwasi. Hapo hapo akainiza mkono wake mfukoni na kisha kuwatolea kipande cha karatasi na kisha kuwagawia.

    Edmund akakichukua kile kikaratasi, akakikunjua na kisha kuanza kukisoma. Kikaratasi kile kilikuwa kimeandikwa maneno machache tu tena yaliyoandikwa kwa herufi kubwa ambayo yalisomeka ‘BINADAMU’. Edmund akaonekana kushtuka, akakirudia kukisoma kile kikaratasi zaidi na zaidi. 

    Akili yake ikaonekana kuchanganyikiwa kupita kawaida, mtu ambaye alikuwa ameandika kikaratasi kile hakuonekana kumfahamu. Kila alipokuwa akitaka kumfahamu mwandishi wa kile kikaratasi hakuonekana kumuelewa, mbaya zaidi hakujua dokta alikitoa wapi.

    “Hiki kikaratasi ni cha nini?” Edmund aliuliza.

    “Nimekikuta kwenye shati la mtoto wako?” Dokta Ibrahim alijibu.

    “Nani alikiandika?”

    “Hatujui. Ila inawezekana kuwa mtoto wako mwenyewe”

    “Hapana. Mtoto wangu hana mwandiko huu” Edmund alijibu.

    “Sasa unafikiri nani atakuwa amekiandika?”

    “Mmmh! Sifahamu. Ila ni nani aliyemleta hospitalini hapa?” Edmund aliuliza.

    “Kuna vijana walimleta wakiwa na gari”

    “Kuna uwezekano kwamba hao vijana ndio waliomuwekea kikaratasi hiki. Lakini neno hili linamaanisha nini?” Edmund aliuliza huku akiendendelea kukiangalia kikaratasi kile.

    “Sijui”

    Wala hazikuchukua dakika nyingi, Polisi wakafika mahali hapo huku wakiongozana na mkuu wa kituo cha polisi cha Msasani na kisha kuwapa pole. Edmund akaanza kumuelezea kamanda Idrisa juu ya kile kikaratasi pamoja na maneno ambayo yalikuwa yameandikwa katika karatasi ile jambo ambalo lilimfanya Edmund kuitwa katika kituo cha polisi kwa ajili ya kutoa baadhi ya maelezo.

    “Kwa hiyo haumfahamu kabisa?” Kamanda Idrisa aliuliza.

    “Ndio”

    “Kuna mtu yeyote ambaye una ugomvi nae?” Kamanda Idrisa aliuliza swali lililomfanya Edmund kuanza kufikiria.

    “Mmmh! Zamani sana. Nadhani unajua kuhusu ule ugomvi uliotokea na wafanyabiashara wenzangu” Edmund alisema.

    “Sasa unafikiri kwamba mmoja wao au wote wale watakuwa wamehusika katika hili?” Kamanda Idrisa alimuuliza.

    “Siwezi kujua. Yaani hapo sifahamu. Sidhani kama watakuwa na ugomvi nami japokuwa wamefungwa gerezani” Edmund alijibu.

    “Sawa. Cha msingi nenda, kazi hii tuachie sisi tutaifanyia kazi” Kamanda alimwambia na Edmund kuondoka huku akikiacha kikaratasi kile katika kituo kile cha poisi.

    Akili yake ilizidi kuchanganyikiwa, hakumfahamu ni mtu gani ambaye alikuwa amefanya tukio lile ambalo lilionekana kumuumiza kupita kawaida. Alichokifanya edmund mara baada ya kufika nyumbani kwake ni kuwapigia simu Bwana Msantu na mkewe, Bi Nasra na kisha kuta wafike nyumbani hapo.

    Wote wakafika na kuanza kuwaelezea kuhusu tukio lile. Hiyo ikaonekana kuwa taarifa mbaya ambayo ilimshtua kila mmoja, bila kupenda, machozi yakaanza kuwatoka. Hilo ndilo lilikuwa tukio ambalo liliandikwa sana kwenye magazeti mengi nchini, hilo ndio tukio ambalo lilimfanya kila mtu kumuonea huruma Edmund pamoja na Uki, hilo ndio tukio ambalo lilimuumiza sana Edmund. Hilo ndio lilikuwa tukio la kwanza kuitokea familia hiyo bila kujua kwamba kuna matukio mengi yangetokea katika maisha yake ya mbele pamoja na familia yake. Matukio hayo ndio ambayo yalimfanya kuwa na KUMBUKUMBU ZENYE KUUMIZA katika maisha yake ya baadae.

    ********CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hali ilionekana kutokubadilika kabisa. Eric bado alikuwa kwenye usingizi wa kifo jambo ambalo lilikuwa likimhuzunisha kila mmoja. Tayari Polisi wakaanza kuweka ulinzi mahali hapo kwa kuona kwamba kulikuwa na mtu au watu ambao walikuwa wakiiandama familia hiyo. Zaidi ya Polisi wawili waliokuwa na bunduki walikuwa wakikaa nje ya chumba kile.

    Siku ziliendelea kukatika zaidi na zaidi, Uki alikuwa akilia kama mtoto kila alipokuwa akimuona mtoto wake akiwa kitandani mahututi. Hakufumbua mdomo wala hakufumbua macho yake, ni mashine ya oksijeni ndio ambayo ilikuwa ikimsaidia kumpa hewa safi katika kipindi hicho.

    Madaktari walijitahidi kwa nguvu zao zote kutaka kumpa ahueni Eric lakini hali ilionekana kuwa ngumu sana. Bado Eric alikuwa amelala kitandani kimya. Ubongo wake ulikuwa katika hali mbaya sana, fuvu la kichwa chake lilikuwa limeharibiwa kutokana na chupa ambazo zilikuwa zimelichoma fuvu hilo.

    Kutokana na mtikisiko mkubwa wa fuvu lake, muda mwingi damu zilikuwa zikimtoka puani na hivyo madaktari kuwa na kazi ya kuzifuta muda wote. Tiba ya kumpatia ilikuwa ikihitaji kiasi kikubwa cha fedha na hivyo Edmund kulipia fedha zote lakini wala hakukuwa na unafuu wowote ule, Eric alikuwa akiendelea kuwa kimya pale kitandani.

    Kikao cha dharura cha madaktari kikafanyika mahali hapo kumzungumzia Eric ambaye hali yake iliendelea kuwa mbaya zaidi na zaidi. Madaktari walionekana kuchanganyikiwa, hawakujua ni kitu gani ambacho walitakiwa kukifanya ili kumrudisha Eric katika hali yake ya kawaida. Kikao kile kiliendelea kwa zaidi ya masaa matatu na ndipo uamuzi ukatolewa kwamba ilikuwa ni lazima Eric asafirishwe na kupelekwa nchini India kwa matibau zaidi.

    Hakukuwa na kupinga wala kuhitahji ushauri mahali hapo, kitu kile ambacho kilikuwa kimekubaliwa ndicho ambacho kilitakiwa kufanyika mahali hapo. Edmund pamoja na Uki wakaitwa na dokta Ibrahim na kuelezewa juu ya uamuzi ambao ulikuwa umefikiwa na nmadaktari, wote wakakubaliana nao.

    Mawasiliano kati ya hospitali ya Muhimbili na Hindu Mandal ya nchini India yakaanza kufanyika na kuwaelezea kwamba kulikuwa na mgonjwa ambaye alikuwa akitakiwa kupewa matibabu haraka iwezekanavyo. Ripoti juu ya magonjwa ambayo yalikuwa yakimsumbua Eric ikaandikwa na kisha kusafirishwa kwa njia ya fax kupelekwa nchini India.

    Vyombo vya habari havikubaki nyuma, kwa kila kitu ambacho kilikuwa kikiendelea kilikuwa kikiripotiwa na kuandikwa. Wananchi walikuwa wakihuzunika kupita kawaida, tayari wakawaona wale wazee matajiri ambao walikuwa wamefungwa gerezani kuhusika na kila kitu kilichoendelea.

    Maoni mbalimbali yalikuwa yakitolewa na wananchi, wapo waliotaka wale wazee wauawe lakini pia wapo walioitaka serikali kuwa makini kupeleleza kwa kina juu ya kile ambacho kilikuwa kikiendelea kwa wakati huo.

    Siku ya safari ikapangwa na hivyo Eric kusafirishwa kupelekwa nchini India. Ndani ya ndege, Edmund na Uki walionekana kuwa na huzuni kupita kawaida. Hawakuamini kama kwa wakati huo walikuwa ndani ya ndege kuelekea nchini India kumpatia Eric matibabu.

    Safari ilionekana kuwa ya huzuni kuliko safari zote, muda mwingi walikuwa wakimuomba Mungu amponye Eric ambaye bado alikuwa kimya kitandani. Walichukua masaa kumi wakawa wamekwishafika katika jiji la Mumbai nchini India. Kitanda alichokuwa amelazwa Eric kikatolewa na kisha kupakizwa ndani ya gari la wagonjwa a hospitali ya Hindu Mandal na kisha kuanza safari ya kuelekea hospitalini.

    Safari hiyo iliwachukua muda wa dakika kumi wakawa wamekwishafika katika hospitali hiyo ambapo moja kwa moja machela ikatolewa na kisha kuanza kusukumwa kuelekea ndani ya hospitali hiyo huku Eric akiwa juu ya machela hiyo. Machela ikaingizwa ndani ya chumba cha upasuaji, kila kitu ambacho kilifanyika katika hospitali ya Muhimbili kilitakiwa kufanyika tena ndani ya hospitali hiyo tena kwa uangalifu na umakini mkubwa zaidi.

    Edmund hakutaka kubaki hospitalini hapo, alichokifanya ni kumuaga Uki na kisha kuelekea mitaani ambapo akachukua chumba kimoja katika hoteli moja kubwa ya nyota tano ya Bhangra Pur ambayo ilikuwa hapo hapo jijini Mumbai. Alipoona kwamba amekamilisha kila kitu, akaanza tena kurudi hospitalini kuuangana na mke wake.

    Hapo ndipo matibabu yalipoanza tena huku madaktari zaidi ya wawili wakiwa wanampatia matibabu. Matibabu yaliendelea zaidi na zaidi mpaka pale wiki moja ilipokatika. Hali ya Eric ikaanza kuonekana kuwa na mafanikio, fahamu zake zikaanza kumrudia huku madaktari wakiwa wameshughulika kwa kiasi kikubwa sana mpaka kuliweka sawa fuvu lake pamoja na kulitibia katika sehemu ambazo zilikuwa zimechubuliwa na vipande vya vioo.

    “Hali inanihuzunisha sana” Uki alimwambia Edmund huku wakiwa wamekumbatiana tu.

    “Tuombe Mungu. Najua ana makusudi na maisha yetu” Edmund alimwambia Uki.

    “Ila inahuzunisha sana. Kwa nini Mungu ameamua kutupa majaribu haya? Mioyo yetu imeumia sana. Sijui kwa nini hili linatokea kwetu tu” Edmund alimwambia Uki huku kwa mbali machozi yakianza kumlenga.

    Hayo ndio yalikuwa maisha yao, kila siku walikuwa wakielekea hospitalini hapo na kurudi hotelini kulala. Majonzi bado yalikuwa yakiendelea zaidi na zaidi, hawakuwa na furaha hata mara moja nchini India. Hata pale ambapo Eric aliporudiwa na fahamu, hawakuwa na furaha ipasavyo, walichokuwa wakikitaka kwa wakati huo ni kumuona Eric akianza kuongea na hatimae kurudiwa na hali yake ya kawaida.

    Nchini Tanzania bado upelelezi ulikuwa ukiendelea. Neno ‘BINADAMU’ ndilo ambalo lilikuwa likiwachanganya Polisi hasa waliokuwa katika kitengo cha upelelezi. Neno lile lilionekana kuwa gumu kugundulika kwa mhusika ambaye alikuwa amesababisha yale yote. Upelelezi uliendelea kwa zaidi ya mwezi mmoja huku Edmund na Uki wakiwa nchini India lakini hakukuwa na mafanikio yoyote yale.

    “Ni lazima tujitahidi. Mhusika ni lazima apatikane kwa namna yoyote ile” Inspekta Pawasa aliwaambia Polisi wake waliokuwa katika kitengo cha upelelezi.

    ****

    Pacha, Erica hakuonekana kuwa na raha kabisa, muda wote alikuwa na uso ulikuwa na huzuni. Muda mwingi alikuwa akilia, maumivu ambayo alikuwa akiyasikia moyoni mwake yalikuwa makubwa. Kitendo cha kaka yake, Eric kupata ajali na kuwa hoi mahututi kitandani kilimnyima raha kabisa.

    Kila siku alikuwa mtu wa kulia tu, shuleni hakuwa akienda kabisa, bibi yake na babu yake ndio ambao walikuwa wakimfariji kwa wakati huo mgumu. Maisha yake bila Eric hayakuonekana kuwa na kitu kabisa. Katika kipindi ambacho Eric alikuwa akipelekwa nchni India kwa ajili ya matibabu, Erica alikuwa akitamani kwenda pamoja nao lakini ikashindikana kabisa kwa sababu bado alikuwa akihitajika shuleni.

    Siku hiyo alilia sana, hakula kitu chochote kile, alijifungia chumbani tu huku akilia. Kila alipokuwa akiambiwa ale chakula hakutaka kula kabisa. Mtu wa muhimu maishani mwake alikuwa ameondoka. Bwana Msantu na mkewe, Bi Nasra walikuwa wakipata tabu kila siku kumlazimisha Erica ale chakula cha kutosha lakini wala hakula chochote kile.

    Wakajitahidi kumnunulia vitu mbalimbali vya kuchezea lakini havikubadilisha kitu chochote kile. Alipokuwa akipelekwa shuleni, hakusoma kama ilivyo kawaida yake. Kila alipokuwa akikiangalia kitu alichokuwa akikitumia Eric darasani pale Erica alikuwa akilia tu.

    Mara kwa mara alipokuwa akirudishwa nyumbani alikuwa akiongea na wazazi wake ambao kila siku walikuwa wakimwambia kwamba Eric alikuwa akiendelea vizuri na mzima wa afya. Maneno yale kwa kiasi fulani yalikuwa yakimpa ahueni moyoni mwake lakini hayakuweza kumpa furaha kabisa. Kitu ambacho alikuwa akikihitaji katika kipindi hicho ni kumuona kaka yake akirudishwa nyumbani, waongee kama ilivyokuwa zamani na hata kwenda shuleni pamoja.

    Siku ziliendelea kukatika zaidi na zaidi lakini wala Eric hakurudishwa nyumbani. Jambo hilo lilimuweka Erica katika majonzi makubwa kupita kawaida. Kwa sababu alikuwa akikaa katika hali ya mawazo kwa kipindi kirefu, hata afya yake ikaanza kudhoofika. 

    “Babu, Eric atarudi lini?” Hilo dilo lilikuwa swali ambalo mara kwa mara Erica alikuwa akimuuliza Bwana Msantu.

    “Atarudi hivi karibuni. Anaendelea vizuri sasa hivi” Bwana Msantu alimwambia erica.

    ********CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mwezi mmoja ukakatika na wa pili kuingia, bado hali ilikuwa vile vile tu bila kuwa na mabadiliko yoyote zaidi ya Eric kurudiwa na fahamu zake tu. Kwa wakati huu macho yake alikuwa akiyafumbua lakini hakuwa akiongea kitu chochote kile. Aliwaangalia wazazi wake, tabasamu lake halikuonekana kabisa usoni mwake.

    Maisha yake ya pale kitandani yalionekana kuwa ya tabu kupita kawaida. Mara kwa mara wazazi wake walikuwa wakifika hospitalini pale na kumjulia hali. Madaktari bado walikuwa wakiendelea kumpatia matibabu kama kawaida. Baada ya miezi mitatu kupita, kidogo mabadiliko yakaanza kuonekana katika afya yake.

    Eric akaanza kuongea japokuwa aliongea kwa tabu sana. Jambo hili liliwapa furaha wazazi wake kiasi ambacho mara kwa mara walikuwa wakikumbatiana kwa furaha kubwa. Shukrani zao walimpa Mwenyezi Mungu kwa kumuwezesha Eric kufumbua mdomo wake na kuongea tena. Alichokifanya Edmund kwa wakati huo ni kuwapigia simu Bwana Msantu na Bi Nasra na kisha kuwaambia kuhusiana na maendeleo ambayo yalikuwa yametokea nchini India juu ya afya ya Eric.

    Matibabu yalizidi kuendelea zaidi na zaidi, fuvu lake la kichwa tayari lilikuwa limekwisharekebishwa. Picha za X ray zilipopigwa tena, fuvu lilikuwa limerudi katika hali ya kawaida huku mikwaruzo ambayo ilikuwa imesababishwa na vipande vya chupa ikiwa imepotea katika fuvu lile.

    Uso wake ukawa umewekwa vizuri na kurudishwa katika hali ya kawaida. Mbavu zake zilikuwa zimerekebishwa vizuri kabisa jambo ambalo lilionekana kuwa mafanikio makubwa sana katika afya yake. Siku zikakatika zaidi na zaidi, hapo hapo Eric akaanza kupewa mazoezi ya kutembea kwa ajili ya kuirudisha afya yake zaidi na zaidi.

    “Mungu atamsaidia tu” Edmund alimwambia mke wake, Uki katika kipindia ambacho walikuwa wakirudi hotelini huku ikiwa imetimia saa tano usiku.

    Walipofika chumbani, hawakulala, walibaki wakiongea kama kawaida huku wakiendelea kumshukuru Mungu kama kawaida yao. Siku hiyo waliongea mengi sana juu ya afya ya Eric huku kila wakati wakizidi kumuomba Mungu amrudishe katika afya yake ya kawaida. Ilipofika saa saba, wakapitiwa na usingizi.

    *******

    Saa nane na dakika kumi usiku, simu ya mezani ya pale chumbani ikaanza kuita kwa sauti kubwa. Wote wakashtuka kutoka usingizini. Kwanza wakaanza kuangaliana, hakujua ni mtu gani ambaye alikuwa akiwapigia simu kwa wakati huo na wakati walikuwa wamelala. Namba ya chumbani mule haikuwa ikijulikana na watu wengine zaidi ya wafanyakazi wa pale hotelini tena ambao walikuwa wakifanya kazi katika sehemu ya mapokezini tu.

    Waliangaliana kwa sekunde chache, Edmund akainuka na kuanza kuifuata simu ile ya mezani kwa mwendo wa kichovu huku akiwa amevaa bukta ndogo tu. Alipoifikia, akaichukua na kisha kuipelekea masikioni.

    “Hallow” Edmund aliita.

    “Eric” Sauti ya upande wa pili iliitikia na kisha simu kukatwa.

    Edmund akashtuka, akaanza kuita zaidi na zaidi lakini hakukuwa na mtu ambaye aliitikia. Edmund akapigwa na mshutuko, hakujua ni kitu gani ambacho kilimpelekea mpigaji wa simu ile kulitajajina la Eric na kisha kukata simu.

    Baada ya kubaki akiwa ameduwaa kwa muda wa sekunde kadhaa, hapo hapo akauachia mkonga wa simu ile na kisha kusimama kama mtu ambaye alipigwa ganzi kwa muda. Edmund akashtuka, akaguka nyuma na kisha kuchukua fulana yake ambayo ilikuwa kwenye mbao ya kutundikia nguo nguo.

    “Kuna nini?” Uki alimuuliza Edmund ambaye wala hakujibu kitu zaidi ya kuanza kuvaa fulana ile haraka haraka kama mtu ambaye alichanganyikiwa.

    Edmund hakutaka kuongea kitu chochote kile, hakujali kama alikuwa amevaa bukta tu, kitu alichokifanya mahali hapo ni kuanza kutoka nje ya chumba kile na kukimbia. Hakuona umuhimu wa lifti, kwake, hasa katika kipindi hicho lifti ilionekana kama kumchelewesha endapo angeipanda, akaanza kushuka ngazi kwa haraka haraka.

    Simu ile ikaonekana kumtia wasiwasi mkubwa, alichokuwa akikitaka mahali hapo ni kufika hospitali na kutaka kumuona mtoto wake tu. Kutokana na kasi aliyokuwa nayo katika kipindi hicho, alitumia sekunde thelathini kutoka kwenye ghorofa ya tano mpaka kufika chini. Mapokezini, hakukuwa na mtu yeyote yule zaidi ya wahudumu ambao walikuwa wakimwangalia tu.

    Akatoka nje ya hoteli ile kwa kasi na kisha kuanza kuifuata bajaji ambayo ilikuwa imepakiwa pembeni ya hoteli ile. Alipoifikia, hakutaka kumuulizia dereva, akakalia kiti cha mbele tayari kwa kuendesha bajaji ile. Akaanza kupapasa sehemu ya ufunguo, haukuwepo mahali pale. Kwa sababu dereva wa bajaji alikuwa karibu an bajaji ile, akaanza kuifuata huku akili ikimtuma kwamba Edmund alikuwa mwizi ambaye alitaka kuiiba bajaji yake.

    “What are you doing in my bajaj? (Unafanya nini ndani ya bajaji yangu?)” Dereva yule alimuuliza Edmund kwa lugha ya Kingereza ambacho kilijaa lafudhi ya Kihindi.

    “I want to see my son (Nataka kumuona kijana wangu)” Edmund alisema huku akionekana kuchanganyikiwa.

    “Where is he? (Yupo wapi?)” 

    “In the hospital (Hospitalini)” Edmund alijibu huku akiendelea kupapasa sehemu iliyokuwa ikitakiwa kuwa na ufunguo.

    “Which hospital? Mangradesh or somewhere else? (Hospitali ipi? Mangradesh au mahali pengine?)” Dereva yule alimuuliza.

    “Hindu Mandal” Edmund alijibu.

    Hapo hapo dereva wa bajaji akamtaka Edmund atoke kwenye kiti chake na kisha yeye kuushikilia usukani na kuiwasha na kuelekea katika hospitali hiyo. Muda wote edmund alikuwa akimtaka dereva wa bajaji ile aendeshe kwa kasi ili aweze kufika haraka katika hospitali ile. Kwa wakati huo tayari akaonekana kuwa na wasiwasi kupita kawaida.

    Simu ambayo ilikuwa imeingia huku mpigaji akilitaja jina la mtoto wake ilionekana kumtia wasiwasi kupita kawaida. Wala hawakuchukua muda mrefu wakawa wamekwishafika katika hospitali ile. Kwa haraka sana Edmund akateremka kutoka kwenye bajaji na kisha kuanza kulifuata jengo la hospitali ile.

    “Where is my money? (Fedha yangu iko wapi?)” Dereva wa bajaji alimuita Edmund na kumuuliza lakini Edmund hakugeuka nyuma.

    Akili yake kwa kipindi hicho ilikuwa imechanganyikiwa kupita kawaida. Alipofika sehemu ya mapokezi, hakutaka kubaki hapo, akapitiliza na kuanza kupandisha ghorofa ya juu. Polisi ambao walikuwa nje ya hospitali ile wakaonekana kuwa na wasiwasi, wakaanza kumfuatilia huku wakiwa na bunduki zao. Alipishana na madaktari pamoja na manesi ambao walikuwa wakimshangaa kupita kawaida. Walitamani kumuuliza ni kitu gani kilikuwa kikiendelea lakini hawakuweza kufanya hivyo kutokana na kasi ambayo alikuwa nayo Edmund.

    Alipofika kwenye ghorofa ya tatu, moja kwa moja akaanza kuelekea katika chumba ambacho alikuwa amelazwa Eric. Mwendo wake ulikuwa wa haraka haraka sana, Polisi ambao walikuwa nje ya jengo lile la hospitali tayari walikuwa wakiendelea kumfuatilia mpaka pale walipomfikia, hatua kumi kabla ya kuufikia mlango wa chumba alicholazwa Eric.

    “Who are you? (Wewe ni nani?)” Lilikuwa swali la kwanza ambalo aliulizwa na mmoja wa Polisi wale.

    “Pleaaseee! I want to see my son )Tafadhali! Nataka kumuona kijana wangu)” Edmund aliwaambia Polisi wale ambao walikuwa wamemshika.

    Edmund alikuwa akitaka kuachiwa ili aelekee katika chumba kile kwa ajili ya kumuona kijana wake, Eric lakini Polisi wale hawakutaka kumuacha, walikuwa wamemshika vilivyo kama kitendo kimoja cha kumzuia. Huku wakiwa wanabishana, mmoja wa madaktari ambao walikuwa wakimhudumia Eric akatokea mahali hapo, alipoona kwamba mtu aliyeshikwa alikuwa Edmund, akawaomba kumuachia.

    Alipoachiwa tu, Edmund akaanza kupiga hatua za haraka haraka kuufuata mlango ule huku dokta yule akimfuata kwa nyuma. Alipoufikia mlango wa kuingia ndani ya chumba kile, Edmund akakutana na maneno ambayo yalikuwa yameandikwa mlangoni kwa kutumia rangi nyekundu ambayo yalisomeka ‘BINADAMU’.

    “Mungu wangu!” Edmund alijisemea huku kumbukumbu zake zikiwa zimerudi nyuma kwa haraka sana kwamba neno lile lile lilikuwa limeandikwa katika kikaratasi ambacho kilikutwa katika mfuko wa shati la Eric. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Edmund akaonekana kuwa na wasiwasi, tayari neno lile ambalo alilikuta mlangoni pale likamtia wasiwasi kupita kawaida. Akakishika kitasa cha mlango ule na kisha kuanza kuingia ndani huku akili yake ikimwambia kwamba Eric alikuwa ameuawa ndani ya chumba kile na mtu ambaye alidhamiria kumuangamiza kwa wakati huo.

    Dokta yule nae hakutaka kubaki nje, akaingia pamoja na Edmund ndani ya chumba kile ambacho kwa Edmund kikaonekana kuwa kama chumba kilichojaa maumivu katika maisha yake.

    “Eric...!” Edmund aliita mara baada ya kuingia ndani ya chumba kile, alichokiona kitandani, hakuweza kukubaliana nacho, mwili wake ukaanza kutetemeka na kijasho kumtoka, akaanza kububujikwa na machozi.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog