Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

PAINFUL MEMORIES - 4

 





    Simulizi : Painful Memories

    Sehemu Ya Nne (4)



    Edmund aliuhisi mwili wake ukitetemeka kupita kawaida, miguu yake akaihisi ikianza kukosa nguvu. Mapigo yake ya moyo yakaanza kudunda kwa kasi isiyokuwa ya kawaida. Macho yake yalikuwa yakiangalia shuka ambalo lilikuwa limemfunika Eric. Shuka zima lilikuwa limetapakaa damu.

    Edmund akazidi kupiga hatua kukifuata kitanda kile huku dokta Patel akiwa nyuma yake akimfuata. Alipokifikia kitanda kile, akalifunua shuka lile. Edmund hakuamini kile ambacho alikuwa akikiona mbele yake. Kifua cha Eric kilikuwa kimetobolewa mara tatu na vitu ambavyo vilionekana kuwa visu.

    Eric alikuwa kimya pale kitandani. Edmund akajikuta akikosa nguvu, akakaa chini huku akilia kama mtoto na huku akiliita jina la Eric. Dokta Patel akashtuka, hakuamini kile ambacho alikuwa akikiona mahali pale. Alichokifanya kwa wakati huo ni kumwangalia vizuri Eric, alikuwa ameauawa pale kitandani.

    Alichokifanya dokta Patel ni kuondoka chumbani hapo na kisha kuelekea kuwaita Polisi ambao walikuwa sehemu ya mapokezi. Polisi wote walionekana kushtuka, hawakuamini kile ambacho walikuwa wakikiona kitandani pale. Hapo hapo bila kuchelewa mawasiliano na kituo cha polisi yakaanza kufanyika.

    Kilio cha Edmund ndicho ambacho kiliwavuta watu mahali pale. Kila nesi ambaye alifika ndani ya chumba kile na kuona kile ambacho kilikuwa kimetokea alibaki akiwa na mshtuko. Edmund hakuweza kukaa kimya, kile ambacho alikuwa amekiona kilionekana kumuumiza kupita kawaida. Edmund akachukuliwa na kisha kupelekwa katika ofisi ya dokta mkuu na kisha kutulia.

    Mwili wake ulikuwa ukizidi kutetemeka kwa hasira, hakujua ni mtu gani ambaye alikuwa akiyafanya yale yote. Alibaki ofisini pale huku akiendelea kulia kwa hasira. Akili yake ilikuwa imechanganyikiwa kupita kawaida. Hakuamini kama katika kipindi hicho alikuwa amempoteza mtoto wake, Eric ambaye alikuwa akiendelea kupata ahueni kitandani pale.

    Baada ya muda dokta Patel akaingia ndani ya ofisi ile na kisha kuanza kuongea na Edmund. Ingawa dokta Patel alikuwa akijitahidi sana kumbembeleza Edmund lakini hiyo wala haikusaidia kabisa, bado Edmund alikuwa akiendelea kulia kupita kawaida. Moyo wake ulikuwa umeumia kupita kawaida na kila alivyozidi kumfikiria mtoto wake, maumivu yalizidi kuongezeka zaidi na zaidi.

    Polisi wakaingia ndani ya ofisi ile na kisha kuanza kuongea pamoja nae huku wakimhoji baadhi ya maswali ambayo alitakiwa kuyajibu. Katika kila swali ambalo alikuwa akiulizwa mahali pale yalionekana kuwa magumu kwake. Hakumjua muuaji na wala hakujua maana halisi ya neno BINADAMU ambalo lilikuwa likiandikwa katika kila tukio la mauaji au ajali ambalo lilikuwa likifanyika.

    Maswali yaliendelea zaidi na zaidi mpaka pale ambapo Polisi hao walipotaka kuongea na mke wake pia. Edmund akaonekana kukumbuka kitu. Japokuwa tayari alikuwa amekubaliana na hali ambayo ilikuwa imetokea lakini hakumtaarifu mke wake. Hapo ndipo alipokumbuka kwamba alitakiwa kumwambia mke wake kitu ambacho kilikuwa kimetokea hospitalini.

    Hakujua mke wake angejisikiaje kama angemwambia kuhusu mauaji ambayo yalikuwa yametokea hospitalini pale. Akachukua simu yake na kutaka kumpigia kwa kutumia simu ya mezani chumbani mule lakini akasita. Hakutaka mke wake apate matatizo yoyote yale, aliona kulikuwa na uafadhali kama angekwenda na kuongea nae ana kwa ana.

    “Did you tell your wife about this? (Ulimwambia mke wako kuhusu hili?)” Polisi alimuuliza katika lafudhi ya Kihindi.

    “No! (Hapana)”

    “Where is she? (Yupo wapi?)”

    “In hotel room (Chumbani hotelini):

    “We have to see her too and ask her several questions (Inatubidi tumuone na kumuuliza baadhi ya maswali)” Polisi mmoja alimwambia.

    “Ok! Should I make a call to her? (Sawa! Nimpigie simu?)” Edmund aliuliza.

    “No! You dont have to do such a thing. We have to see her face to face....right? (Hapana! Hautakiwi kufanya kitu kama hicho. Itatubidi tuonane nae uso kwa uso....sawa?)”

    “Right! (Sawa)” Edmund alijibu.

    Hawakuwa na muda wa kupoteza mahali hapo, walichokifanya ni kuanza kuondoka kuelekea hotelini huku Edmund akionekana kuwa kwenye uso uliojaa majonzi tele. Kichwa chake kilikuwa kikimfikiria mtoto wake tu, Eric ambaye katika kipindi hicho alikuwa ameuawa kwa kuchomwa visu viwili kifuani mwake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alijua fika mapenzi ambayo mke wake, Uki alikuwa nayo kwa watoto wake, hakujua ni kwa jinsi gani Uki angeumia mara ambapo angemwambia ukweli kwamba mtoto wao, Eric alikuwa ameuawa kikatili juu ya kitanda ambacho alikuwa amelalia pale hotelini. Katika kipindi hicho, Edmund alikuwa katika hali mbaya kupita kawaida, hakujua ni kitu gani kingeendelea katika maisha yake mara tu ambapo angemfahamu mtu ambaye alikuwa amehusika katika mipango hiyo.

    Mara baada ya kufika hotelini, moja kwa moja akaingia ndani ya lifti na Polisi watatu na kisha kuelekea katika ghorofa ya tano na kuanza kuufuata mlango wa chumba kile walichokuwa wamechukua huku tayari ikiwa ni saa tisa usiku. Walipiga hatua zaidi na zaidi huku Edmund akiendelea kufikiria ni kwa mnamna gani angeweza kumfikishia mke wake, Uki taarifa ile ambayo ilikuwa ni taarifa iliyojaa maumivu makubwa.

    Wakaufikia mlango wa kuingilia ndani ya chumba kile. Edmund akashtuka, akaanza kuuangalia mlango ule, maneno yaliyoandikwa kwa herufi kubwa ambayo yalisomeka ‘BINADAMU’ yalikuwa yakionekana yakiwa yameandikwa katika mlango ule. Edmund akashtuka kupita kawaida, mshtuko ule ambao aliuonyesha mahali hapo ukawafanya Polisi wote kumuangalia.

    “They killed her too (Wamemuua pia)” Edmund alisema hata kabla hajaufungua mlango huku akiwa anayaangalia maneno yale yaliyoandikwa mlangoni.

    “What? (Nini?)” Polisi mmoja aliuliza kwa mshtuko.

    Edmund hakutaka kuufungua mlango, tayari alikwishajjua ni kitu gani kilikuwa kimeendelea ndani ya chumba kile. Akakaa chini pale pale mlangoni na kisha kuanza kulia. Moyo wake uliumia kupita kawaida, japokuwa hakuwa ameingia ndani lakini tayari alikwishajua kwamba mke wake mpendwa, Uki alikuwa ameuawa.

    Polisi mmoja akakishika kitasa cha mlango ule na kisha kuufungua mlango. Hapo hapo Polisi wote wakaingia ndani huku Edmund akiendelea kubaki pale mlangoni huku akilia kama mtoto. Polisi walikaa ndani ya chumba kile kwa dakika kadhaa, polisi mmoja akatoka nje ya chumba kile na kisha kumwangalia Edmund ambaye alikuwa akiendelea kulia kama mtoto mpaka kuwafanya wapangaji wengine kutoka nje.

    “She has been murdered (Ameuawa)” Polisi yule alimwambia Edmund ambaye akaongeza sauti ya kilio chake.

    ***

    Taarifa zikasambazwa nchini Tanzania. Kila mtu ambaye alizisikia alionekana kushtuka. Mauaji ambayo yalikuwa yamefanyika nchini India yalionekana kutawala sana katika vyombo vya habari nchini Tanzania. Watu hawakuamini kama kweli yule Edmund, tajiri mkubwa ndiye ambaye alikuwa akipitia katika wakati mgumu namna hiyo.

    Waliokuwa na mioyo laini wakajikuta wakianza kulia, mauaji yale yalionekana kuwa ni ya kupanga. Kila mmoja alikuwa na swali kichwani mwake, kila mmoja alitaka kufahamu maana halisi ya neno BINADAMU ambalo lilikuwa likiandikwa katika kila mauaji ambayo yalikuwa yakifanyika hasa yaliyokuwa yakiihusu familia ya Edmund.

    Wapelelezi nchini Tanzania bado walikuwa wakiendelea kupeleleza juu ya muuaji huyo ambaye alikuwa akiandika maneno hayo lakini mpaka kipindi hicho hakukuwa na mafanikio yoyote yale na hata dalili za kumpata muuaji hazikuwa zikionekana. Wananchi walikuwa wakiwalalamikia Polisi kwamba katika kipindi chote hicho walikuwa wameshindwa kumkamata muuaji ambaye alizidi kuua zaidi na zaidi.

    Habari za mauaji hayo ndizo ambazo zilikuwa zikivuma sana nchini Tanzania, katika kila kona watu walikuwa wakizungumza kuhusiana na mauaji hayo. Habari za mauaji hayo ndizo ambazo zilikuwa zikivuma sana katika vyombo mbalimbali vya habari kiasi ambacho ziliifanya kuenea zaidi na zaidi.

    Katika kipindi hicho ndicho ambacho Edmund alikuwa akijiandaa kurudi nchini Tanzania. Muda mwingi alikuwa mtu wa kulia tu, hakuamini kama safari yake ya kwenda India ndio ambayo ilikuwa imemletea mambo yale yote ambayo yalikuwa yamemuumiza kupita kawaida. Hakuamini moyoni mwake kama kweli alikuwa amempoteza mke wake, Uki ambaye alikuwa akimpenda sana pamoja na mtoto wake, Eric ambaye alikuwa ameanza kupata nafuu.

    Katika kipindi hicho, Edmund alikuwa na hasira kupita kawaida. Muda mwingi alikuwa akitetemeka kwa hasira, kiu yake yote ilikuwa ni kutaka kumfahamu mtu ambaye alikuwa amemsababishia maumivu yale aliyokuwa akiyasikia moyoni mwake. Muda wote Edmund alikuwa akionekana kuwa na mawazo kupita kawaida.

    Safari ya kurudi nchini Tanzania ikapangwa, ndege ya kukodi ikaandaliwa na miili yote miwili kuingizwa kwenye ndege hiyo na kuhifadhiwa vizuri. Safari hiyo ilionekana kuwa mbaya kwa Edmund, muda mwingi alikuwa kwenye kiti akilia tu. Mawazo yake yalikuwa yakimfikiria marehemu mke wake pamoja na mtoto wake, Eric. Hakujua angemueleza nini Erica ambaye alikuwa kwenye mapenzi mazito na kaka yake, Eric pamoja na mama yake, Uki.

    Ndege ilichukua muda wa masaa tisa ikaanza kuingia katika ardhi ya nchi ya Tanzania. Waandishi mbalimbali wa habari walikuwa wamekusanyika mahali hapo kwa ajili ya kupiga picha na kuzungumzia hali ambayo ilikuwa ikiendelea mahali hapo. Idadi ya wananchi elfu tatu walikuwa wamekusanyika uwanjani hapo pia huku lengo lao likiwa ni kumpa pole Edmund ambaye alionekana kuwa kwenye wakati mgumu.

    Ndege ilipokuwa ikitua, watu wakaanza kujikusanya huku wakiwa pamoja na waziri mkuu Bwana Hamadi Shimpoli. Edmund akaanza kushuka ndani ya ndege na kisha miili ya mke wake pamoja na mtoto wake kuteremshwa. Vilio vikaanza kusikika kutoka katika umati ule wa watu, kitendo cha kuona miili ikiteremshwa kilionekana kuwauma watu wengi ambao walikuwa wakiingalia.

    “Pole Edmund” Bwana Msantu alimwambia Edmund huku akimkumbatia.

    Edmund hakusema kitu chochote kile, aliwakumbatia wote huku akizidi kulia kama mtoto. Bado moyo wake ulikuwa ukizidi kumuuma kadri muda ulivyozidi kwenda mbele. Miili ile ikapakizwa ndani ya gari na kisha kuondoka mahali hapo huku Edmund akiwa amekwishaongea na Waziri Mkuu Bwana Shimpoli.

    Safari kwa wakati huo ilikuwa ni kwenda katika Hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya kuiandaa miili ile kwa ajili ya mazishi. Ilitakiwa kuandaliwa vilivyo, ipelekwe kanisani na kisha kufanyiwa ibada hata kabla ya kupelekwa nyumbani kuagwa na kisha kupelekwa makaburini kwa ajili ya mazishi.

    Huku safari ikiendelea zaidi na zaidi kuelekea Muhimbili, mara simu ya Edmund ikalia mlio wa kuingia meseji. Alichokifanya ni kuichukua simu yake kutoka mfukoni na kisha kuifungua meseji ile. Edmund akapigwa na mshtuko, mapigo yake ya moyo yakaaanza kudunda kwa kasi isiyo ya kawaida. Alipoisoma tu ile meseji, akamgeukia Bwana Msantu.

    “Erica yupo wapi?” Eric alimuuliza huku akionekana kuwa na hofu.

    “Yupo nyumbani”

    “Mmemuacha?” Edmund aliuliza kwa mshtuko.

    “Ndio. SI ulituambia tumuache ili asije hapa kwa sababu angelia sana” Bwana Msantu alimwambia Edmund.

    “Mungu wangu!”

    “Kuna nini?”

    “Wamemuua” Edmund alimwambia Bwana Msantu maneno ambayo yalionekana kumshtua kila mtu.

    Bwana Msantu akaichukua simu ile ya edmund na kisha kuiangalia meseji ile na kisha kuanza kuisoma. Meseji haikuwa na maneno mengi, ilikuwa imeandikwa jina moja tu lililosomeka ‘ERICA’. Edmund hakutaka kubaki ndani ya gari hio ambalo lilikuw likiendeshwa kuelekea hospitalini, alichokifanya ni kumuarisha dereva asimamishe gari na kisha kutoka garini na kuanza kukimbia.

    Edmund alionekana kuwa kama mtu ambaye alichanganyikiwa kwa wakati huo. Alikuwa akikimbia kwa kasi kuelekea Masaki alipokuwa akiishi Bwana Msantu. Tayari alikuwa na uhakika kwamba muuaji yule ambaye alikuwa amewaua mkewe, Uki pamoja na mtoto wake, Eric ndiye ambaye alikuwa amemuua Erica ambaye alikuwa ameachwa nyumbani.

    Alikimbia kwa mwendo wa kasi mpaka alipofika Magomeni ambako akakodi bajaji na kisha kuanza kuelekea Masaki huku muda wote akimuharakisha dereva aendeshe gari kwa kasi zaidi na zaidi kuelekea Masaki. Bado Edmund alikuwa amechanganyikiwa zaidi na zaidi, hakuamini kama kile kitu ambacho kilikuwa kimetokea kilikuwa ni halisi au ilikuwa ndoto mbaya na ya kutisha ambayo baada ya muda angeamka kutoka katika usingizi mzito.

    Bajaji haikuchukua muda mrefu wakawa wamekwishafika Masaki ambapo Edmund akateremka na kisha kuanza kuifuata nyumba ile ya kifahari. Alipofika getini tu, maneno makubwa ambayo yaliandikwa ‘BINADAMU’ yalikuwa yakionekana getini pale. Edmund akaonekana kushtuka kupita kawaida, mwili wake ukaanza kutetemeka tena.

    “Wamemuua” Edmund alisema huku akilishika lile geti na kulifungua huku dereva wa bajaji akionekana kumshangaa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Edmund akaonekana kuchanganyikiwa kupita kawaida. Tayari alikuwa akilia kama mtoto. Kitendo cha kuyaona maneno yale getini kwake tayari yakaonekana kwamba kulikuwa na mauaji ambayo yalikuwa yamefanyika ndani ya nyumba yake. Katika maisha yake, kwa wakati huo alikuwa amembakisha mtu mmoja tu, mtu ambaye aliamini kwamba ndiye ambaye angempa furaha moyoni mwake, Erica ambaye katika kipindi hicho alikuwa na uhakika kwamba mtu huyo alikuwa ameuawa.

    Edmund akafungua geti na kisha kuingia ndani. Kwanza mlinzi hakuwepo getini jambo ambalo lilionekana kumshangaza kupita kawaida. Alichokifanya ni akaufuata mlango wa kijumba kidogo cha mlinzi na kisha kuufungua. Mlinzia alikuwa amelala chini huku akiwa amefungwa kamba katika miko yake kwa nyuma pamoja na miguu yake huku mdomo akiwa amewekewa vitambaa kadhaa.

    Alichokifanya Edmund ni kuanza kumfungua kamba zile na kisha kumtoa vitambaa vile. Mlinzi akabaki akihema kwa nguvu huku akionekana kutokuamini kabisa kile ambacho kilikuwa kimeendelea.

    “Vipi? Kuna nini kimetokea?” Edmund alimuuliza mlinzi.

    “Kuna watu walikuja kunifunga kamba na kuniwekea vitambaa mdomoni” Mlinzi alijisemea.

    “Watu gani?” Edmund alimuuliza.

    “Siwajui. Sura zao ngeni machoni mwangu” Mlinzi alijibu.

    “Waliingia ndani?”

    “Ndio”

    Edmund hakutaka kubaki mahali hapo, alichokifanya ni kutoka mahali hapo na kuelekea ndani, Akaufungua mlango wa sebuleni na kisha kuingia ndani. Kitu cha kwanza alichokifanya ni kuanza kumuita mfanyakazi wa ndani ambaye akafika mahali hapo.

    “Kuna mtu aliingia ndani?” Edmund alimuuliza mfanyakazi wa ndani, Pamela.

    “Hapana” Pamela alijibu.

    “Erica yupo wapi?” Edmund alimuuliza.

    “Yupo ndani amelala” Pamela alijibu.

    “Una uhakika?”

    “Ndio” Pamela alijibu.

    Alichokifanya Edmund mahali hapo ni kuondoka na kisha kuufuata mlango wa chumba ambacho alikuwa akilala Erica. Maandishi yaliyosomeka ‘BINADAMU’ yalikuwa yakionekana katika mlango ule. Moyo wa Edmund ukapigwa ganzi huku miguu ikikosa nguvu na kukaa chini. Ni kilio ndicho ambacho kikaanza kusikika mahali hapo.

    Tayari alikwishajua kwamba ni mauaji ndio ambayo yalikuwa yamefanyika ndani ya chumba kile. Pamela alibaki akiwa amesimama huku akimwangalia Edmund ambaye alikuwa akilia kama mtoto mdogo huku akilitaja jina la Erica.

    “Kuna nini?” Pamela aliuliza huku akionekana kumshangaa.

    “Wamemuua”

    “Wamemuua! Nani tena?” Pamela aliuliza.

    “Wamemuua Erica wangu” Edmund alijibu.

    Pamela akaonekana kumshangaa Edmund, hakujua maneno yale ambayo alikuwa akiyaongea yalikuwa yakimaanisha nini. Halikuonekana kuwa jambo la kawaida Edmund kusema kwamba Erica alikuwa ameauwa na wakati hata ndani hakuwa ameingia na kumjulia hali Erica.

    Alichokifanya Pamela ni kuufungua mlango ule na kisha kuingia ndani. Uyowe mkubwa ukasikika kutoka kwa Pamela. Damu zilikuwa zikionekana katika shuka lililokuwa juu ya kitanda huku Erica akiwa pembeni ameuawa kikatili. Picha ambayo ilionekana machoni mwa Pamela ilionekana kutisha kupita kawaida.

    Pamela hakuongea kitu chochote kile, alibaki akilia huku Edmund akiendelea kuwa pale chini alipokuwa amekaa. Hiyo ndio hali ambayo ilikuwa imetokea. Edmund akampoteza kila mtu katika maisha yake. Watoto wake ambao alikuwa akiwapenda walikuwa wameuawa na mtu ambaye alikuwa akijiita ‘BINADAMU’.

    Si watoto peke yao ambao walikuwa wameuawa bali hata mke wake mpendwa, Uki alikuwa ameuawa kikatili. Maisha yake ya mbeleni yakaonekana kujaa giza, hakuona dalili zozote za kuweza kumpata muuaji ambaye alisababisha hayo yote.

    Polisi wakafika katika nyumba hiyo na kisha kufanya kile ambacho walitakiwa kukifanya likiwepo lile la kuupiga picha mwili wa Erica. Hali ilionekana kutisha na kusikitisha kupita kawaida. Waandishi wa habari hawakuchukua muda mrefu wakawa wamekwishafika katika nyumba hiyo.

    Matukio hayo mfululizo ya mauaji ambayo yalitoke ndani ya siku tatu ndio ambayo yalionekana kumchanganya sana Edmund. Muda mwingi alikuwa akionekana kuwa kama chizi, aliongea peke yake, kwa kumuangalia, alionekana dhahiri kukaribia kuwa chizi.

    Bwana Msantu ndiye ambaye alikuwa akimfariji katika kipindi hicho cha tabu. Kila alipokuwa akiyaangalia makaburi ya familia yake ambayo yalikuwa karibu karibu yalionekana kumuumiza kupita kawaida. Akili yake katika kipindi hicho ilikuwa ikifikiria kitu kimoja tu, kumtafuta mtu ambaye aliiangamiza familia yake kwa kujitambulisha kuwa alikuwa akiitwa ‘BINADAMU’.

    Saikolojia ya Edmund ikaonekana kutokuwa sawa jambo ambalo lilimfanya Bwana Msantu kumuita mtaalamu wa Saikolojia na kuanza kuongea na Edmund huku akijaribu kumuweka sawa. Kwa Edmund, kila kitu kikaonekana kutokwenda sawa. Japokuwa Mwanasaikolojia alikuwa amejitahidi kwa kiasi kikubwa sana kuirekebisha akili na mawazo ya Edmund lakini hakukuonekana kuwa na mafanikio yoyote yale.

    “Hali yake bado mbaya sana” Mwanasaikolojia, Fonce alimwambia Bwana Msantu.

    “Ila itakubidi wewe ndiye ushuhurike nae. Unafikiri ukishindwa wewe sisi tutaweza kweli?” Bana Msantu alimuuliza

    “Nipeni muda zaidi. Itanibidi kukaa nae kwa kipindi kirefu sana” Fonce alimwambia Bwana Msantu.

    Bado muda ulizidi kwenda mbele zaidi na zaidi. Hali ya Edmund ikazidi kuwa mbaya zaidi na zaidi. Uchizi ndio ambao ulikuwa umemuingia akilini mwake. Mwanzo alianza kuongea peke yake ila mwisho wa siku akaanza kuvua nguo zake na kisha kutembea huku akiwa mtupu ndani ya chumba ambacho alikuwa akikitumia.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Bwana Msantu, Bi Husna na Bi Nasra walionekana kuumia kupita kawaida, hali ambayo alikuwa nayo Edmund ikaonekana kuwaumiza kupita kawaida. Mauaji yale ambayo yalikuwa yametokea katika familia yake tayari yalikuwa yameharibu maisha yake. 

    Hakukuwa na mtu ambaye aliruhusiwa kuonana na Edmund kutokana na fujo mbalimbali ambazo alikuwa akizifanya kwa kila mtu ambaye alikuwa akitaka kumuona. Magazeti bado yalikuwa yakiendelea kuandika kila kitu ambacho kilikuwa kikiendelea katika maisha yake. Watu walionekana kukilaani kitendo kile kuliko vitendo vyote ambavyo vilikuwa vimewahi kutokea katika nchi ya Tanzania.

    Serikali ikatakiwa kufanya juu chini kwa ajili ya kuhakikisha muuaji anapatikana na kupelekwa katika vyombo vya sheria. Wapelelezi walikuwa wakiendelea kufanya kazi usiku na mchana lakini hakukuonekana kuwa na dalili zozote zile ambazo zingewaonyeshea kwamba muuaji alikuwa sehemu fulani.

    Mwezi wa kwanza ukapita, mwezi wa pili, wa tatu na wa nne lakini hakukuwa na dalili zozote zile. Huku wapelelezi wakiendelea kufanya upelelezi juu ya kumfahamu mtu ambaye alikuwa amefanya mauaji, Edmund bado alikuwa katika hali ile ile, alikuwa chizi kwa kiasi kikubwa sana, mawazo juu ya familia yake ndio ambayo yalikuwa yamemfanya kuwa katika hali ile.

    ***

    Hali ambayo alikuwa nayo Edmund ilionekana kumshangaza kila mtu, alikuwa amechanganyikiwa kwa asilimia mia moja. Kila alipokuwa katika eneo la hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikuwa akifungwa kamba, kila alipokuwa akiachiliwa, alikuwa akileta fujo huku muda mwingi akiliita jina la mke wake, Uki pamoja na majina ya watoto wake, Eric na Erica.

    Hali ile ilionekana kutokuamini kwa baadhi ya watu ambao walikuwa wakimfahamu sana Edmund. Edmund alikuwa mtu tajiri sana ambaye alikuwa na akili zake timamu lakini kile kitendo cha kuwapoteza watoto wake pamoja na mke wake kilionekana kumchanganya sana. Maswali mengi yalikuwa yakimiminika vichwani mwa watu mbalimbali nchini Tanzania lakini hakukuwa na mtu ambaye alikuwa na majibu juu ya maswali yale.

    Bwana Msantu, Bi Nasra na Bi Husna walikuwa wakifika hospitalini hapo kila siku kwa ajili ya kumuona Edmund ambaye hakuwa hata na nafuu. Akili yake ilikuwa imechanganyikiwa vile vile. Mwili wake ulipungua sana kutokana na kukataa kula kila alipokuwa akiletewa chakula. Hali ambayo alikuwa nayo Edmund ndio ambayo ikamfanya Bwana Msantu kumuajiri dokta ambaye alikuwa na uzoefu wa magonjwa ya akili ya binadamu kutoka nchini Kenya, dokta Oliech.

    Edmund akatolewa hospitalini na kisha kuanza kupewa matibabu nyumbani kwake huku akiwa chiniya uangalizi wa dokta Oliecha ambaye muda mwingi sana alikuwa akimtibu huku akimpa baadhi ya dawa. Dokta Oliecha alionekana kuwa dokta mzuri sana kwani japokuwa Edmund alikuwa mtu wa fujo lakini alikuwa na utulivu mkubwa sana kila alipokuwa na dokta Oliech.

    Matibabu yalikuwa yakiendelea zaidi na zaidi, Edmund akaanza kulishwa sana vyakula ambavyo vilikuwa na sukari kwa kuaminika sana kwa kuleta mabadiliko katika mishipa yake yote ambayo ilisababisha hali hiyo. Tiba iliendelea zaidi na zaidi huku dokta Oliecha akitumia hadi dawa nyingine za asili kama magamba ya mti wa Memeku ambao ulikuwa ukipatikana sana nchini Kenya.

    Magamba ya mti ule kwa kiasi fulani yakaanza kuonyesha mabadiliko katika afya ya Edmund. Picha ambazo mara kwa mara alikuwa akionyeshewa na dokta Oliech zikaanza kuonyesha mabadiliko. Waandishi wa habari hawakuwa nyuma, mara kwa maera walikuwa wakifika mahali hapo na kumjulia hali Edmund huku wakitoa taarifa magazetini juu ya afya ambayo alikuwa nayo Edmund.

    Kutokana na kulipwa kiasi kikubwa sana ambacho hakuwahi kulipwa toka aanze kazi, dokta Oliech alifanya kazi zaidi ya mara mbili. Baada ya muda wa miezi miwili mingine kukatika, Edmund akaanza kurudiwa na akili zake. Kwa kipindi hiki kidogo akawa na uwezo wa kumtambua huyu alikuwa nani na alifanya nini kabla ya hapo.

    Dokta Oliech aliona hiyo kutokutosha, akamuongezea tiba ya magamba ya mti wa Memeku zaidi na zaidi, mwezi mmoja ulipokatika, Edmund akafanikiwa kurudi katika hali yake. Alichokifanya Bwana Msantu ni kumlipa fedha zaidi dokta Oliech na kisha kumchukua Edmund na kumpeleka kwa mtu ambaye alikuwa bingwa wa Mambo ya Saikolojia katika hospitali ya Muhimbili, Bwana Emmanuel Kihampa.

    Kila siku kazi kubwa ya Bwana Kihampa ilikuwa ni kuongea na Edmund na kujitahidi kumrudisha katika hali ambayo alikuwa nayo kabla. Haliile ikaonekana kumsaidi sana, kwani baada ya wiki mbili, akawa amerudi katika hali yake kama kawaida. Ingawa alikuwa akikumbuka sana kuhusiana na mauaji ambayo yalikuwa yametokea lakini kwake hakuonekana kujali sana japokuwa alikuwa akitaka kupata mambo mengi kutoka kwa Polisi ambao walikuwa wakiangaika kumfahamu muuaji.

    Polisi kwa wakati huo wakaonekana kuchemka kabisa japokuwa hawakutaka kueleza ukweli, dalili za kumpata muuaji wala hazikuonekana kabisa. Walikuwa wakijizungusha huku na kule bila kutoa taarifa ambazo zilikuwa zimeshiba.

    “Nini kinaendelea? Mmefikia wapi?” Edmund alimuuliza mkuu wa polisi, Kamanda Idrisa.

    “Bado upelelezi unaendelea” Kamanda Idrisa alimwambia Edmund.

    “Huo upelelezi utakamilika lini?” Edmund alimuuliza huku akionekana kuanza kukasirika.

    “Bado kidogo”

    Edmund hakutaka kukaa ndani ya ofisi hiyo, alichokifanya mahali hapo ni kutoka nje na kisha kuondoka kuelekea nyumbani kwake. Mwili wake ulikuwa ukimtetemeka kwa hasira sana, kitu ambacho alikuwa akikitaka mahali hapo ni kumfahamu muuaji na kisha kumuua kwa kifo ambacho kingejaa maumivu sana.

    Akafika nyumbani kwake na kisha kujilaza kochini. Macho yake yalikuwa yakiangalia darini tu. Wala hazikupita dakika nyingi, mara simu yake ikaanza kuita, alipoangalia kioo cha simu yake, mpigaji alikuwa Ester, rafiki mkubwa wa marehemu mke wake. Edmund akaipokea simu ile.

    “Upo wapi?” Lilikuwa swali la kwanza alilouliza Ester hata kabla ya salamu.

    “Nyumbani” Edmund alijibu.

    “Unaweza kuja nyumbani sasa hivi?” Ester alimuuliza.

    “Kuna nini?”

    “Polisi wamemjua muuaji?” Ester aliuliza.

    “Hapana. Wananizingua tu” Edmund alijibu.

    “Njoo. Kuna vitu nimevihisi. Nimehisi kwamba muuaji atakuwa ni mtu fulani. Maneno yake ndio yamenifanya nimuhisi kwamba ni yeye” Ester alimwambia Edmund.

    Edmund akaonekana kushtuka, akaiweka vizuri simu yake sikioni huku akionekana kutokuamini kile ambacho alikuwa amekisikia. Kwa kipindi hicho alikuwa na kiu kubwa ya kumfahamu muuaji ambaye alikuwa amemsababishia kumbumbuku ambazo zilikuwa na maumivu makali moyoni mwake.

    “Ni nani?” Edmund alimuuliza Ester.

    “Njoo kwanza nyumbani. Neno BINADAMU ambalo linatumika linaonekana kunitia wasiwasi wa kumfahamu muuaji” Ester alisema.

    Edmund hakutaka kuchelewa, huku akiwa kama mtu ambaye alichanganyikiwa, akatoka sebuleni hapo na kisha kulifuata gari lake na kuondoka nyumbani hapo. Njiani hakutaka kuendesha gari lake kwa mwendo wa taratibu, alikuwa akiendesha kwa mwendo wa kasi huku akijiona kuchelewa kufika Kinondoni alipokuwa akiishi Ester,

    Mara baada ya kufika nyumbani hapo, kwa haraka sana akateremka na kuanza kuufuata mlango wa kuingia ndani ya nyumba ile na kisha kuanza kuugonga, mlango ukafunguliwa na mfanyakazi wa ndani na kuingia ndani. Breki ya kwanza ilikuwa kochini, akakaa hapo na kuanza kumsubiria Ester ambaye alikuwa bafuni akioga.

    Edmund alisubiri kwa muda wa dakika kdhaa, Ester akatokea mahali hapo ambapo wakaanza kuongea mambo mbalimbali huku akimpa pole kwa kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea katika maisha yake likiwepo lile la kuipoteza familia yake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Naomba uniambie” Edmund alimwambia Ester.

    “Muuaji wala simfahamu kabisa” Ester alimwambia Edmund.

    “Wewe si ulisema unamfahamu?”

    “Ndio. Ila hisia zangu zinanifanya nimuhisi mpenzi wa zamani wa marehemu mke wako, Uki” Ester alimwambia Edmund.

    “Huyo ndiye atakuwa amefanya hayo?” Edmund aliuliza.

    “Nahisi hivyo”

    “Anaitwa nani huyo? Na anakaa wapi?” Edmund aliuliza.

    “Anaitwa Rahman. Kwa sasa anaishi Afrika Kusini” Ester alijibu.

    “Bado unanichanganya sana. Sasa nitajua vipi kama amehusika? Na nini maana ya neno ‘BINADAMU” ambalo amekuwa akiliandika kila afanyapo mauaji’?” Edmund aliuliza.

    “Hilo neno ndilo hasa lililonifanya nimhisi kwamba ni yeye” Ester alimwambia Edmund.

    “Kivipi?”

    “BINADAMU”

    “Limekufanya nini kuhisi kwamba ni yeye?”

    “Ligawanye jina hilo mara mbili”

    “Bado sijakupata”

    “Unaonaje kama tukiliweka BIN ADAMU?” Ester aliuliza.

    “Bado sijakupata”

    Katika kila neno ambalo Ester aliongea mahali hapo Edmund hakuonekana kuelewa kitu chochote kile, bado akili yake ilikuwa ikichanganyikiwa kupita kawaida. Maneno ambayo aliongea Ester kwake yalionekana kuwa kama mafumbo ambayo alihitaji kufumbuliwa na hatimae kuambia jina la mtu ambaye alikuwa amehusika katika kumsababishia kumbukumbu zenye maumivu moyoni mwake.

    “Mtu mwenyewe anaitwa Rahman Adamu” Ester alimwambia Edmund na kuendelea.

    “Rahman Adamu?” Edmund aliuliza kwa mshtuko.

    “Ndio. Hapo alijaribu kuandika kwa kifupi tu. Kwa kuwa jina lake ni Rahman Adamu, yeye ameamua kuweka na kusomeka BINADAMU, akimaanisha Bin Adamu” Ester alimwambia Edmund ambaye alikuwa akimfahamu Adamu kuwa mwanaume ambaye alikuwa na mke wake, Uki hata kabla hajakutana nae.

    Edmund akaonekana kushtuka kupita kawaida, neno ambalo aliongea Ester na kisha kulifafanua lilionekana kuwa sahihi kabisa. Hapo hapo bila kutarajia, machozi yakaanza kumtoka, akasimama huku akionekana kuwa na hasira sana.

    “Ni yeye. Ni yeye huyo huyo Rahman Bin Adamu” Rahman alisema huku akitetemeka kwa hasira.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog