Simulizi : Usilie Nadia
Sehemu Ya Nne (4)
Danny amekufa akinitetea, sijui kuhusu mama mwenye upendo uliopitiliza mama aliyenipenda hata bila kuniona!!...Desmund, Desmund mapenzi yangu yooote niliyokupa umenitenda hivi Desmund….kweli umeamua kunifanya niwe mkimbizi kiasi hiki Desmund ambaye sijawahi hata kukutukana sijawahi kukulaumu Desmund, Des niliyekunyenyekea licha ya kuwa nakuzidi kwa kila kitu…leo unaniita Chokoraa na nisiyefaa katyika jamii, unawatuma watu waniue mimi Desmund!!” kikafuata kilio kikuu huenda kupita vyote, Nadia alilia sana, alilia akiomboleza juu ya kifo cha Danny na kuhusu mama asiyejua kama alikufa ama la!! Lakini Nadia aliamini kuwa walimuua. Nadia alilia kinyakyusa!! Alilia huku akilaani katika namna ya kuimba!!
“Nadia, mimi nipo upende wako na sitakusaliti, ni mimi na wewe tunajua wapi tulipokutana amini kuwa …”
“Shhhhhhh!!!! Wote ninyi ni wale wale..” alinikaripia. Nikatambua kuwa hii ni hasira iliyopitiliza. Nikaamua kumuacha Nadia alie akimaliza apumzike na huenda anaweza kusema nami tena, maana kwa hali aliyokuwanayo angeweza kunipiga hata makofi!!
HAIKUWA kama nilivyodhani kuwa Nadia alitakiwa kupumzika ili hasira zake zipungue, niliamua kuondoka kimyakimya bila kumuaga Nadia ambaye bado alikuwa anatetemeka.
“Unaenda wapi Gerlad!!” kwa mara ya kwanza aliniita kwa jina langu halisi. Nikakosa cha kujibu lakini sikuendelea zaidi nikalazimika kugeuka.
“Unaondoka kwa chuki kisa nimekueleza ukweli sivyo? Kisa nimesema kuwa nyie wote ni walewale. Kisa nimewasema sivyo!! Ulitaka nisiuseme ukweli ama, mwandishi hutakiwi kuchukia eti kisa tu wewe ni mwanaume. Haya basi tuseme kuwa nyinyi hamfanani, mbona nilipotoka pale nyumbani kwa Danny nikazidi kukutana na akina nyie n matatizo yenu yaleyale. Hivi kwani nyie wanaume huwa mnawaza nini? Ama labda niseme hivi nyie huwa mna cha huyu mbaya huyu mzuri!! Hamna mashaka kabisa kuwa mwingine anaweza kuwa jini. Hebu ‘imagine’ na hali yangu ile ya kutokea rumande, nimechakaa haswa, nimekonda na nina kidonda kibichi, jenga picha kuwa bado nikakutana na wanaume wanajifanya kunitamani. Huruma yenu ipo wapi? Nilikwambia kuwa nakiri kuwa wema hufa mapema, Jadida na Danny waliondoka mapema sana, ni hawa walikuwa wema kwangu na wakaondoka nikiwa nawahitaji. Tazama Danny amekufa bila hata kuniambia kwa nini Desmund alikuwa akiwachukia watu weupe, jibu ambalo nilikuwa nalitafuta siku zote” Nadia akatabasamu kidogo kisha akaendelea, “Ujue mwandishi labda nina hasira sana ama labda ni kwa sababu nasema kweli nd’o maana wanishangaa, ndio lazima unishangae maana si ndio zenu kuuchukia kweli, lakini amini kuwa hakuna kitu kizuri kama ukweli katika maisha haya, ni kweli kabisa kuwa ukweli unaumiza sana lakini unakuta mtu nimemwambia kabisa kuwa mimi sina cha kupoteza awe mkweli tu lakini bado anadanganya. Baada ya kuwa nimeondoka nyumbani kwa Danny aliyekuwa marehemu tayari huku sijui lolote kuhusu mama yake mzazi sikuwa na pa kwenda mjini Musoma. Nilitamani kumkabili Desmnd lakini nikagundua kuwa sijajipanga na mwisho wa siku nitarejea kulekule rumande na safari hii asingepatikana Danny mwingine kuweza kunikomboa, nikaingia mtaani, nikapata pikipiki ambayo nilitaka inipeleke moja kwa moja kituo cha mabasi.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Unaenda kupanda basi muda huu dada ama!” mazoea yetu yalianzia hapa na huyu bwana ambaye uso wake nilipoutazama alionyesha kuwa mkarimu lakini sikutilia maanani maana hata Desmund alikuwa hivyo hivyo.
Nilikubali kuwa nahitaji kusafiri kuelekea Mwanza. Na hapa akanipinga sana kuwa hakuna mabasi muda huo na kwa pale Musoma mabasi hayana utaratibu wa kulazwa humo Stendi.
Kweli tulipofika hapakuwa na mabasi, na ni kama alinisoma akili yangu kuwa nilikuwa nina hofu lakini kuna jambo kama alishindwa kuniambia hata nilipomlipa pesa yake aliipokea kwa kinyongo. Alitamani sana kusema nami zaidi lakini sikuwa nikimpa ushirikiano. Akawasha pikipiki yake na kutoweka.
Alipoondoka ndipo hofu ikazidi kunitawala maana niligundua kuwa nimebaki katika upweke mwingine mpya. Katika kituo cha mabasi huku nyuma nikiwa nimeacha maiti katika chumba cha Danny. Na ni Danny alikuwa ameuwawa.
Nikiwa bado katika tafakari, upepo ukipuliza na baridi ikipenyeza katika mwili wangu nikapata wageni wa ghafla waliokuja kunighasi. Huenda ni jambo hili lilimtia hofu yule dereva wa pikipiki. Walikuwa ni vibaka!!
Wakanighasi huku na kule wakinilazimisha niwape pesa, katika kunitikisa mara simu ikadondoka wakaitwaa, wakaendelea kunibughudhi na hapo likatokea jambo jingine lililonifanya nistaajabu. Nilisikia kelele za mwanaume akiwafukuza wezi wale huku, nilipogeuka alikuwa ni dereva wa pikipiki akiwa na panga mkononi akielekea pale nilipokuwa, waler vibaka wakatoweka na ile simu.
Uzuri ni kwamba hawakunijeruhi.
“Nilijua nikikwambia mapema kuwa kuna vibaka maeneo haya ungeweza kunihisi vibaya sana maana hukuwa na ushirikiano katika mazungumzo yetu” aliniambia yule mwanaume huku akinishika mkono. Sasa nilifuata alichokuwa akiniambia, hofu ilikuwa imetanda upya, alikuwa ameninusuru kutoka katika mikono mibaya ya vibaka.
Akanipeleka katika pikipiki yake aliyokuwa ameiegesha mahali.
Akanichukua hadi nyumbani kwake!!!
Akalala chini akaniachia kitanda!!
Huu ukawa mwanzo wa kufahamiana na Christian.
Asubuhi aliniamsha mapema sana ili niwahi basi la kwenda Mwanza!! Lakini sikuitamani ardhi ya Mwanza ambayo ilishuhudia nikilawitiwa na haikusema chochote.
Chris akanisoma akili yangu na kuamua kuhoji! Lakini sikuwa tayari kumweleza lolote kuhusiana na mimi, lakini sikuitaka safari ya Mwanza. Nikahitaji hifadhi walau kwa siku mbili tatu niweze walau kumkabili Desmund ana kwa ana tena, kwa silaha yoyote nimwondoe duniani kisha nikamatwe nifungwe ama ninyongwe niende kumwomba msamaha mama yangu aliyeniachia laana hiyo.
Naam!! Sikutakiwa kuondoka katika mji huo!!
“Chriss…”
Alinitazama nami nikaendelea, “Sikufahamu hata kidogo nawe haunifahamu na bado umekuwa mwema kwangu. Asante sana kwa yote…..”
“Lakini unaonekana unatawaliwa na hofu!!...halafu kama nakuja vile” aliniambia huku akinitazama kwa makini.
“Sidhani kama unanijua lakini.”
“Ni kweli huenda mmefanana si unajua tena duniani wawiliwawili.”
“Wewe ni mwenyeji sana hapa Musoma.”
“Mi mwenyeji nimekulia hapahapa na hata kielimu changu kidogo nimechukulia hapahapa” alinijibu kwa ufasaha huku alkienda kuiwasha pikipiki ili anipeleke stendi.
“Inapendeza sana unapofanana na mke wa mheshimiwa bwana.” Alisema neno ambalo lilinishtua.
“Mheshimiwa gani tena jamani.”
“Diwani wetu aliwahi kuwa na mke kama wewe ila alitoweka kimyakimya si unajua tena waheshimiwa huenda alimpeleka kusoma ulaya”
“Diwani yupi? Nami kidogo mwenyeji hapa.”
“Huyu aliyeingia baada ya Kenyigo kuuwawa kwa risasi wanamuita Desmund!” alinijibu, moyo ukapasuka kusikia habari hiyo. Yaani Desmund ni diwani?? Tena anaitwa mheshimiwa!!
Desmund alimuua Kenyigo!!! Niliwaza, maana sijui tu kwanini niliwaza. Lakini nilihisi jambo hilo Desmund alimuua Kenyigo ili apate nafasi ya udiwani, alaa!! Ni hivyo maana miaka mitano ilikuwa haijapita bado ya kuweza kugombea udiwani.
“Vipi unamfahamu mheshimiwa?” aliniuliza huku akiendelea na mambo yake.
“Chriss, hebu njoo kidogo. Namfahamu Desmund namfahamu vyema.”
“Kivipi?”
“Nilikuwa mkewe.” Nikamjibu, akaacha yote aliyokuwa anafanya akanitazama kwa mshangao huku akiwa haamini hata kidogo.
“Chriss kama nilivyosema kuwa wewe hunijui nami sikujui na hata unastaajabu kwa nini sihitaji tena hiyo safari ya Mwanza, kama nitakuwa najipalia makaa ya moto na yaache yaniunguze lakini kama ni sahihi na iwe hivyo. Chriss kwa uliyonitendea usiku wa jana naamini wewe ni mtu unayejali. Naomba nikushirikishe kidogo juu yangu”….nikamuhadithia Chris dhuluma ambayo ananifanyia huyo mtu wanayemuita mheshimiwa. Nikamweleza asilimia hamsini kuhusu mimi, kisha nikamweleza juu ya mauaji yaliyofanyika usiku huo na hatimaye nikakutana naye akanipeleka mjini.
Chriss alistushwa sana na habari hiyo niliyomsimulia lakini sikuwa na namna nililazimika kutapatapa kama naweza kupata wa kuungana nami katika harakati hizo. Chriss alionekana kuwa mwelewa sana jambo lililonifariji sana.
Safari ikahairishwa, nikabaki nyumbani kwa Chriss huku nikiwa nimejitoa mhanga kwa lolote litakalotokea, na kwa mara nyingine nikakumbuka kumtukuza Mungu kwa yote anayonitendea huku nikiamini kuwa bado yupo upande wangu. Licha ya magumu yote ambayo nilikuwa napitia bado aliniunganisha na watu ambao walikuwa upande wangu.
Sikutakiwa kutoka nje kabisa wakati wa mchana, hivyo mambo yangu yote ya faragha nilifanya katika kiza kinene.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa muda wa juma moja kilitokea ambacho nilitaraji, nikageuka kuwa mke wa Chriss kwa hiari yangu maana hakunibaka. Ni Chriss aliyekuwa ananipa habari zote zilizokuwa zinaendelea mtaani, nia yangu ilikuwa hali itulie ili niweze kutimiza azma yangu.
Usiku mmoja nilimuuliza Chriss swali moja tu ambalo lilinifanya niendelee kuwaona wanaume kuwa wote hawapendi kuwa wakweli. Nilimuuliza iwapo ana mke!! Akanijibu kuwa hajaoa na kama ikiwezekana atanioa mimi. Nilirudia swali hilo mara tatu na jibu likabakia kuwa lile la mwanzo.
Macho yake yaling’ara kabisa kwa nuru ya upendo. Alikuwa anaongea kwa hisia kali sana za kimapenzi.
Mwanzoni nilikuwa kama mtumwa tu wa mapenzi yake, yaani nilikuwa nafanya ilimradi tu kwa kuwa nafanya. Lakini taratibu nikawa nakolea na kujikuta nikimkaribisha Chriss katika moyo wangu.
Niliponyoa nywele zangu kichwani hakika nilibadilika, mavazi ya baibui yakanifanya sasa niwe huru kuwa natoka nje mara moja moja. Chriss ambaye alikuwa akifanya shughuli ya bodaboda alikuwa anatoka asubuhi akiwa amenichemshia chai ya maziwa na kuniwekea katika chupa, mchana alileta aidha chakula kikiwa tayari ama mboga nami ninapika akirudi jioni anapata chakula nyumbani. Uzuri pale hapakuwa na majirani maeneo ya karibu ambao wangeweza kuhoji chochote.
Licha ya kuwa anafanya shughuli za bodaboda alikuwa amejipanga kiasi chake, chumba na sebule vilikuwa vimesheheni haswa. Nami nikawa mama mwenye nyumba.
Mapenzi huondoa chuki, mapenzi hushinda vita, mapenjzi huweza kuisimamisha dunia kwa dakika kadhaa. Mapenzi ni kitu cha ajabu sana!!
Nimtafutie nini Desmund iwapo Chriss alikuwa akinipa mapenzi ya dhati, Desmund alinipenda kwa sababu nilikuwa nina pesa, lakini Chriss alinipenda kama nilivyo!! Hiyo ilikuwa tofauti kubwa sana kati ya wanaume hao.
Moyo wangu ukajifunza kusamehe, nikaamini huenda mama yangu ameifuta ile laana aliyonipa. Kama mama yangu amenifutia laana ni kwanini mimi nakuwa na kisasi moyoni mwangu? Nilijiuliza siku ambayo nilijipanga rasmi kwenda kumvamia mkewe Desmund katika mkutano wa kisiasa na kummaliza ikiwezekana.
Nilihudhuria mkutano ule huku nikiwa na silaha ya kisu kikali.
Lakini moyo ukawa mzito, na nikahisi kuwa huyu mama hana kosa, mbaya wangu mimi alikuwa ni Desmund. Ni huyo alifaa kuitumikia adhabu niliyokuwa nimeipanga!!
Nikajiuliza kuwa iwapo nitamujeruhi yule mama na kisha nikakamatwa, hiyo inamaanisha kuwa Desmund atabaki kuwa huru na akinicheka nikiwa jele!!
Hapana!! Nikahairisha nikaamua kujipa moyo kuwa nitampata Desmund! Ni huyu wa kunieleza jambo ambalo Danny alitaka kuniambia lakini wakamuua kabla hajanieleza. Nilimuhitaji Desmund anipe jibu hilo kabla sijaamua kumuua ama kumsamehe!!
Mwandishi katika haya maisha huwa tunapata shule kila siku na masomo ni mapya kila leo na waalimu pia ni wapya. Nililokutana nalo kwa Chriss ulikuwa mzigo hakika, mzigo mzito kutua….ewe moyo ulaaniwe!!
Ilikuwa saa sita usiku. Mimi sinahili wala lile nilikuwa natazama tamthilia za kifilipino sikuwa na mashaka juu ya Chriss ambaye alikuwa katika mihangaiko yake, haikuwa mara ya kwanza kwake kuchelewa nyumbani. Nikasikia mlango ukigongwa, nikaendakufungua huku nikiamini kuwa ni Chris ambaye nilikuwa namuita mume wangu kwa kipindi kile.
Mara!! Uso kwa uso kwa na mwnamke mnene mfupi rangi ya chokleti.
Nikamkaribisha lakini akaonekana kusita, akamuulizia Chriss. Nikamjibu kuwa hajatoka kazini na hapo pepo la wivu likanishawishi kumuuliza swali kuwa yeye ni nani.
“Ni rafiki yake tu!! Nitarudi baadaye.” Alinijibu kisha akaondoka akiniachia mchomo mkali wa wivu!! Ina maana Chriss ana wanawake nje!!
Nikazihifadhi hasira ili Chriss akirejea nimweleze.
Nilidhani atarejea Chriss kabla ya balaa lililotokea baada ya nusu saa. Mlango uligongwa tena, nikatambua kuwa atakuwa Chriss nikaufungua mlango kwa fujo!! Na hasira ikinitawala.
Uso wa uso na yule mama mfupi. Lakini sasa hakuwa mwenyewe alikuwa na wengine wanne, wote wakiwa na miili iliyoshiba haswa.
“Kwani wewe ni nani yake?” aliniuliza, nami nikapata fursa ya kumtambia kama yeye ni kimada basi mimi ni mke.
“Mimi ni mkewe…mama mwenye nyumba hii.” Niliwajibu.
Sikujua kama nimefanya kosa!! Nilisikia kauli moja tu..’unamchelewesha huyu Malaya!!’..kauli ambayo Desmund aliwahi kunieleza. Na hapo nikajikuta nimesukumwa nikaangukia katika kochi nikajigonga mgongo, nikiwa sijayahimili maumivu yale, yule mwanamke kibonge mfupi akanirukia na kuniangusha chini vizuri, akaanza kunikwangua na yale makucha yao marefu!! Neno Malaya likijirudia mara kwa mara.
Hadi wakati Chriss anafika nilikuwa hoi nikivuja damu na bado nilikuwa sijaelewa nini kinaendelea.
“We mpuuzi unataka upewe nini wewe…yaani kitanda changu, unalala na changudoa anajiita mama mwenye nyumba. Christian sihitaji kujua wala kusikia lolote kutoka kwako kabla hujafanya maamuzi kati ya haya mawili. Nikabidhi pikipiki yangu, utoke katika nyumba hii na usinijue tena, ama huyu Malaya wako aondoke hapa nd’o uzungumze na mimi vizuri.” Ilikuwa sauti ya amri kutoka kwa yule mwanamke huku wenzake wakiishabikia.
Naam!! Chriss akawa mdogo, alikuwa anatetemeka…..Chriss ambaye nilikuwa nimempa nafasi katika moyo wangu huku nikiamini ni kiumbe pekee anayeweza kunipa faraja, sasa nasikia akiambiwa kufanya maamuzi. Chriss hakunitazama nilivyokuwa navuja damu, Chriss hakukumbuka hata machungu yangu yote niliyomweleza hapo kabla na mbaya zaidi hakukumbuka kuwa niliwahi kumuuliza swali kama ana mke ama la!! Hivi hakujua maana yangu, angenambia tu ukweli, kwani wanaume wangapi wamenitumia hovyohovyo, kwani wangapi wamenidanganya?? Ni dunia nzima ilikuwa imenigeuka si mbaya naye angekuwa muwazi kwani nilikuwa na thamani gani tena, eeh nilikuwa na jipya gani mimi. Haya yote aliyapuuzia, kumbe alikuwa anacheza na hisia zangu tena!! Alikuwa anacheza na moyo uliopondeka naye akazidi kuuponda….
Kisha akapiga nyundo ya mwisho….Chriss akatoa kauli kwa kinywa chake, taa ikiwa inawaka na jicho langu likimtazama.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Isabela mke wangu nisamehe!!” alitamka, nikasikia mapigo ya moyo kama yanataka kukatisha safari yake.
“Chris baba nimekwambia chukua maamuzi kwanza.”
“Nadia chukua nguo zako na uiache nyuma hii. Huyu ni mke wangu na kila kitu kwangu” alisema Chris kwa sauti yenye kitetemeshi, bila shaka moyo ulikuwa unamsuta!!.
Wanawake wanne na mwanaume mmoja wakawa wananipinga mimi!! Unadhani ningejiteteaje? Nilikuwa pake yangu katika hii dunia!!
Na hapo nikaulaani moyo wangu!! Moyo uliodanganyika, uliodanganywa na mwanaume. Mwandishi bado nakuambia nyie wote ni sawa unakataa, unapata chuki unataka kuondoka chumbani bila kuaga unaleta hasira kwa kuambiwa ukweli. Unakataa nini sasa unakataa nini nakwambia nyie wote ni walewale!! Haya ondoka, endelea na hasira hizohizo, endelea ondoka mlango upo wazi, niache nilie mwenyewe, nenda hata Desmund alienda, hata Chriss aliniacha, Danny naye aliniacha, Jadida aliniacha, mama alinikataa akanilaani, baba na ndugu zangu wote walienda na wewe nenda…nenda si nd’o ulichoamua…niache!!.....ne…ee…” hakuweza kuendelea Nadia. Maneno yake yakanichoma, sikuweza kujizuia kulia, nikamkimbilia Nadia na nikaweka uandishi pembeni nikalazimika kumuomba msamaha Nadia. Haikuwa kazi ndogo!!
NADIA alilia sana kwa sauti ya juu huku machozi yake yakiishia katika bega langu, niliendelea kumkumbatia labda ndo faraja pekee aliyokuwa anahitaji kwa wakati ule. Sikujua nini nimwambie maana alikuwa kama ananihukumu mimi pia kwani nilikuwa mwanaume pia. Mara nikajikuta nauchukia sana uanaume japo sikutamani kuzaliwa mwanamke kisha kuteseka kama Nadia.
Hatimaye Nadia alinyamaza kulia lakini hakutaka hicho kilichomkaba kooni kiishie hapo!!
Aliketi akanitazama usoni!!
Ama!! Alikuwa amevimba macho yake haswa!! Na yalikuwa mekundu, kama ilikuwa mara ya kwanza kumuona lazima utetereke na uhisi kuwa huenda ni mgonjwa mahututi!!
“Mwandishi, nilisimama wima nikataka kutembea niondoke zangu bila kumtazama Chriss machoni lakini kizunguzungu kilinishika, nikaanguka chini kama mzigo, ule mwili uliokuwa umepigwa sana sasa nikawa nimejitonesha tena!!
Chris alinisogelea lakini nikasikia akipewa onyo kali sana kutoka kwa yule mama. Ni hapo nilipogundua kuwa Chriss alikuwa anawekwa kinyumba na yule mama nd’o maana alitakiwa kutii kila alichokuwa anaambiwa!!
“Mletee chochote kilichokuwa chake atoke humu ndani.” Sauti ya mwanamke iliamuru.
Kimya kikatanda kisha nikaisikia tena ile sauti, “Hizo nguo amezinunua yeye ama umemnunulia.” Nikawa nimetega masikio nimsikie Chriss.
“Amezinunua yeye, sikuwahi kumnunulia chochote!! Naapa.” Alidanganya Chriss bila shaka alifanya vile kwa sababu ya masalia ya upendo aliokuwanao kwangu. Yule mama akasonya, Chriss akanifikishia lile begi pale chini kisha akaninong’oneza jambo Fulani.
Nikasimama tena sasa nikajikongoja nikatoka nje.
Nilipogeuka kumtazama Chriss kwa mara ya mwisho, ukungu wa machozi ulikuwa umenitanda sikuweza kujua kama alikuwa anatabasamu ama alikuwa ananisikitikia.
Lakini nilichoweza kukiona kwa uhakika, ni saa ya ukutani.
Ilikuwa saa kumi kasorobo usiku!!
Naenda wapi mimi Nadia!! Nilijiuliza sana na sikuyapata majibu, nilitarajia walau wale wanawake wenzangu watapatwa na huruma na kuniita walau nilale hadi asubuhi lakini haikuwa hivyo hakuna aliyenionea huruma hata kidogo.
Nilikuwa nimetengwa tena na dunia!! Chriss aliyekuwa kila kitu kwangu alikuwa amenisaliti.
Naam!! Nikayafuta rasmi yale mawazo kuwa huenda mama yangu alikuwa ameifuta ile laana aliyonipa akiwa Saudi Arabia, ile laana ilikuwa inaishi bado!!
Nilikuwa nimelaaniwa!!
Kutoka pale Kariakoo ya Musoma hadi barabara ya lami hapakuwa na umbali sana, nilijikongoja taratibu hadi nikaifikia barabara huku nikiwa sijui nini cha kufanya. Na magari yalikuwa yameipumzisha lami!! Kimya kikuu!!
Hakika Chriss alikuwa ameninunulia nguo nyingi, ni kama kuna kitu fulani alikuwa akiwaza juu yangu, labda kuwa mkewe siku moja ama kuwa nami milele. Lakini sasa sikuhitaji kujua hayo. Zile nguo zikaniwia nzito sana, ukiongezea na yale maumivu makali katika mwili wangu lile begi lilikuwa adhabu!! Nikaamua kulitua chini. Nikajisogeza katika kichaka kidogo nikaliweka hapo!! Kisha nikaondoka peke yangu hadi barabara ya lami!!
Hapo sasa uoga ukaanza tena!! Uoga mkuu. Nikahofia watu wabaya wangeweza kunidhuru usiku ule.
Ni hapo ndipo nikayakumbuka maneno ambayo Chriss alininong’oneza wakati akinipatia lile begi. “Kwenye zipu ya kushoto!!”…naam aliniambia juu ya zipu ya kushoto.
Nikatimua mbio huku nikichechemea kurejea kule ambapo niliacha lile begi.
Dakika kadhaa nilizotoweka pale hazikuleta tofauti. Nikalikuta lipo salama, upesi nikapekua katika zipu ya kushoto.
Pesa!! Nikakutana na burungutu la pesa!!
Machozi ambayo sikujua kama ni ya uchungu ama furaha yakanitoka huku nikijikuta nakosa maamuzi sahihi juu ya hukumu gani alikuwa anastahili Chriss, je? Nimsamehe ama ni lipi la kufanya!! Nikaamua kumsahau Chriss huku nafsi ikisema nami kuwa Chriss alikuwa ananipenda lakini tatizo alikuwa chini ya uongozi wa mwanamke.
Chris alikuwa amewekwa kinyumba!!!
Nguvu zikarejea tena, nikalitwaa lile begi, pesa nikazisunda katika kifua changu. Nikajikongoja hadi katika nyumba ya kulala wageni.
Nikapata chumba pale!!
Nikapumzika!!!
Ulikuwa usiku wa aina yake ambao hakika sikuutarajia, kutoka katika penzi mwanana na kuangukia katika ukimbizi tena.” Nadia akasita kisha akaniambia kwa upole, “Mwandishi haya maisha hayana ramani….na kama ipo basi Nadia mimi siwezi kuisoma ramani vizuri.” Akasita kisha akaendelea, “ningeweza vipi kukubali kubaki Musoma wakati nilikuwa nimetengwa tayari…ningekubali vipi huruma ya wananchi wakati niliamini kuwa huruma hizo zimeniponza na moyo wangu mwepesi umenigharimu!! Nilikuwa mjinga sana kubakia Musoma, lakini si mjinga wa mwisho labda hata Desmund naye alikuwa mjinga vilevile. Cha muhimu ninachoweza kusema kwa asilimia kadhaa kubaki kule kulinisaidia lakini kosa kubwa nililofanya ni kuhitaji huruma kutoka kwa wananchi wa ardhi ambayo ilikuwa imenisaliti. Mwisho wa jina la Nadia na kuzaliwa kwa jina la Mariam kulinisaidia kidogo, lakini afadhali yale magumu aliyoyapitia Nadia kuliko huu mkasa ambao Mariam alikumbana nao!!!” Nadia akanitazama akanikonyeza kisha akasema, “Yeah ni hivyo ule ulikuwa mwisho wa u Nadia nikabadilika kuwa Mariam. Lakini kubadilika kwa jina hakukumaanisha kuwa ule ulikuwa mwisho wa mateso yangu wala haikumaanisha mimi kuwa Mariam ilimaanisha mama Nadia ataifuta laana….laana ile ingefutika iwapo tu kama Nadia ningeuwawa. Naam asingekuwepo wa kunirithi mateso yangu. Lakini sasa ningekufa vipi iwapo kuna mtu namdai mali zangu, nife vipi wakati Desmund anaishi??” kauli za Nadia ziliniacha njia panda, nikashangaa sana maana kweli siku ya kwanza aliniambia anaitwa Mariam tulipokutana katika mazingira tatanishi, nikatambua kuwa ni mambo ya wasichana tu kupenda kudanganya majina lakini sasa nilikuwa nimelipata jibu lakini halikuwa jibu sahihi. Kivipi sasa anaitwa Mariam wakati alikuwa akiitwa Nadia??CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kwa hiyo wewe ni Maria mama Nadia?” hatimaye nikajikuta namuuliza swali kwa mara ya kwanza kabisa tangu nianze utafiti wa kisa hiki cha aina yake.
Badala ya kunijibu aliniangalia kwa makini kama anayeisoma akili yangu. Kisha akaanza kusimulia kwa sauti ya chini.
“Ilifikia kipindi nikakimbilia vituo vya watoto yatima wakanambia kuwa hairuhusiwi na hawapokei mtu juu ya miaka kumi na nane nikakataliwa, nikakimbia huku na kule kama kichaa. Mwisho nikakimbilia katika shule ya sekondari ya wasichana Songe! Sijui unaijua??.....shule moja hivi Musoma ni ya wasichana, nikalazimika kuwa napita mchana wakati wa chakula cha mchana na majira ya jioni kuokota mabaki ya ugali na maharage wanayobakiza, mwanzoni walinishangaa lakini mwisho wakanizoea nami wakaniunganisha katika kundi maarufu kwa jina la ‘waloko’. Hayo yakawa maisha yangu!!
Naam! Nilikuwa katika kutimiza lile neno alilosema Desmund kuwa mimi ni chokoraa. Tena chokoraa mzoefu.
Nilikula mabaki na kulala popote!! Sasa nikakibariki rasmi kifo changu maana nilijua lazima nitakufa tu!! Nikaamini kuwa laana ni kitu kimoja kibaya sana, laana ya mzazi haikwepeki. Nilikonda sana na mwili kuwa kama motto mdogo, sikuwa na nywele kichwani. Hakika nilikuwa nimekongoroka!!
Nilikuwa nalia moyoni nikiwaona wasichana waliokuwa wanasoma shule ile wakitoroka na kuchukuliwa na wanaume wenye pesa zao huku wengine wakichukuliwa na wanafunzi wenzao wa shule jirani ya Musoma ufundi. Nilitamani kuwahadithia maisha yangu ili wajifunze kitu lakini ningeanzia wapi mimi!! Nikabaki kuwasikitikia tu bila kuwaambia lolote. Na maisha yakaendelea.
Nilidumu pale kwa miezi kadhaa huku nikiwa nimeizoea ile hali na hatimaye nikasahau kile kisa matata kilichonifanya mimi kupoteza ramani na kujikuta nikiangukia katika uchokoraa rasmi!! Nikiwa sina ndugu wala rafiki!!.......hatimaye ukafika ule muda wa kupata rafiki mpya aliyesababisha nibadilike kutoka katika u Nadia na kuingia katika u Mariam.”
Akasita akatwaa maji na kunywa kisha akaendelea!! “Kipindi cha mitihani hakuna asiyekijua, kipindi hicho kila mwanafunzi hutingwa na mambo yake akijaribu kujikwamua aweze kufaulu. Kila mtu huwa na mbinu zake za ufaulu lakini mbinu maarufu ni kuangaliziana ama kuingia na majibu katika chumba cha mitihani, siku hiyo mchana kama kawaida tulikuwa tunarandaranda huku na kule katika ile shule, tukingojea muda wa chakula cha mchana ufike. Ndipo nilipokutana na Jesca, niliwahi kuwa mwanafunzi hivyo nilijua kila kitu, Jesca hakuwa na nia ya kuja chooni lakini nia yake ilikuwa kufuata majibu aliyokuwa ameyahifadhi chooni, nilimuona alipoyahifadhi na hata alipoenda kuyachukua nilimuona pia. Lakini licha ya kumuona yeye pia kuna kitu nilikigundua, kuwa kuna mwalimu alikuwa ameyaona yale majibu na alikuwa anategea amwone aliyeyaweka, nilimtambua mwalimu Temba maana alikuwa anaogopwa sana na kuna wakati alikuwa akitugeuzia kibao hata sisi ambao aliamini tunaokota mabaki ya chakula kile kwa ajili ya bata nyumbani, hakujua mimi nilikuwa nakula chakula kile.
Yule binti alivyotoka darasani nami nikasimama ilimradi tu nipishane naye, nikajifanya namuulizia kitu, akanitazama kwa hasira kali. Bila shaka hakuvutiwa na ombi langu!! Sikutaka apige hatua mbele zaidi, “dada mwalimu Temba amekutegea ameyaona majibu yako!! Usiende!” nilimwambia na kuhakikisha amesikia kisha nikachukua hamsini zangu nay eye nikamwacha bila kumtazama tena……sikujua nini kiliendelea lakini jioni Jesca alinitafuta!! Huo ukawa mwanzo wa urafiki wetu, urafiki ulioniingiza katika jina jipya na MATESO MAPYA!!
MATESO MATAKATIFU!!! MATESO NISIYOTAKA KUYAKUMBUKA!!.....Usiku mwema Gerlad!!” Nadia alinikatisha ghafla wakati nilikuwa nimejiweka makini sasa kusikiliza ni kitu gani kilitokea.
Kukatishwa huko kukaniacha katika njia panda. Nikabaki na maswali ambayo hata ungekuwa wewe lazima ungejiuliza.
MOJA: Nadia alilala gesti siku alipofukuzwa nini kilijiri sasa?
MBILI: Nadia akabadilika kuwa MARIAM…nini chanzo.
TATU: JESCA anahusika vipi katika mkasa huu?
NNE: Nadia anadai mateso ya MARIAM ni makali kuliko haya ya NADIA…..inawezekana vipi? Na ilikuwaje?
TANO: Nini hatma ya Desmund maana Nadia hajawahi kumsamehe!!
Ni maswali hayo yaliyoniumiza kichwa lakini sikuwa na jinsi nikalazimika kumjibu Nadia, “USIKU MWEMA PIA”…kisha nikaondoka na kuufunga mlango!!!
Ndipo nilipokutana na Jesca, niliwahi kuwa mwanafunzi hivyo nilijua kila kitu, Jesca hakuwa na nia ya kuja chooni lakini nia yake ilikuwa kufuata majibu aliyokuwa ameyahifadhi chooni, nilimuona alipoyahifadhi na hata alipoenda kuyachukua nilimuona pia. Lakini licha ya kumuona yeye pia kuna kitu nilikigundua, kuwa kuna mwalimu alikuwa ameyaona yale majibu na alikuwa anategea amwone aliyeyaweka, nilimtambua mwalimu Temba maana alikuwa anaogopwa sana na kuna wakati alikuwa akitugeuzia kibao hata sisi ambao aliamini tunaokota mabaki ya chakula kile kwa ajili ya bata nyumbani, hakujua mimi nilikuwa nakula chakula kile.
Yule binti alivyotoka darasani nami nikasimama ilimradi tu nipishane naye, nikajifanya namuulizia kitu, akanitazama kwa hasira kali. Bila shaka hakuvutiwa na ombi langu!! Sikutaka apige hatua mbele zaidi, “dada mwalimu Temba amekutegea ameyaona majibu yako!! Usiende!” nilimwambia na kuhakikisha amesikia kisha nikachukua hamsini zangu nay eye nikamwacha bila kumtazama tena……sikujua nini kiliendelea lakini jioni Jesca alinitafuta!! Huo ukawa mwanzo wa urafiki wetu, urafiki ulioniingiza katika jina jipya na MATESO MAPYA!!
MATESO MATAKATIFU!!!”
USIKU ulikuwa mrefu sana nikijiuliza ni nini kilimsibu Nadia hadi kufikia hatua ya kuitwa Mariam. Hakika nilijaribu kuumiza kichwa lakini hata kubabia nini kimemsibu nilishindwa.
Nikatwaa dawa za maumivu na kujidunga kisha nijilaza kitandani na kupitiwa na usingizi.
Asubuhi niliwahi sana kuamka nikajiandaa kisha nikaenda chumbani kwa Nadia, siku hii niliamua kumfuata katika namna ya kuanzia pale tulipoishia usiku uliopita, niliamua kukiuka kila ambacho nilikuwa nimejipangia katika kuandaa maandiko haya kutoka katika maisha ya Nadia.
Nilifika na kugonga mlango ukafunguliwa, Nadia alikuwa amechanuka na tabasamu jepesi usoni.
Nikamjulia hali, naye kanijulia hali yangu!!
Nikaketi, kisha nikanyanyua mkonga wa simu na kuwapigia wahusika wa hoteli ile tayari kwa kutuandalia kifungua kinywa.
“Nimewaambia tayari kama ni chai au kuna jingine.” Alinikatisha baada ya kuigundua nia yangu.
Nikamtazama akanikonyeza!!CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Silali fofofo kama wewe….”aliniambia na hapo mlango ukagongwa akaenda kufungua.
Kwa mara nyingine tena ilikuwa ni kapuchino!!
Vikombe viwili!! Sijui alijuaje kama nami ningefika kwa wakati.
Kila mmoja akatwaa kikombe chake!! Kimya kikatanda wakati tukifungua kinywa!!
Nadia alipoona kimya kimetanda sana alichukua rimoti na kuwasha luninga. Akakutana na muziki akaacha katika chaneli hiyohiyo. Mara muziki ukamalizika kikafuata kipindi kingine, Nadia hakujishughulisha kubadili chaneli badala yake akatabasamu akitazama ile luninga nami nikatazama nini kinamfanya atabasamu!!
Kilikuwa ni kipindi cha kawaida tu!! Basi nikajiongeza kuwa alikuwa na lake la ziada. Mara akatua kikombe chini akanitazama.
“Hivi na wewe umewahi kuingia studio?” aliniuliza. Nami nikakitua kikombe changu chini. Kisha kwa kujiamini kabisa nikamjibu, “Yaani mwandishi mzima kama mimi hadi leo niwe sijaingia studio?”
“Umenijibu ama umeniuliza swali?” aliniambia, mara tukajikuta tumecheka wote kwa pamoja.
“Nimewahi kuingia mara kwa mara Nadia.” Nilijirekebisha hatimaye.
“Mwenzangu, yaani namuangalia huyu mdada hapa hajiamini kabisa sijui ni mara yake ya kwanza kuingia studio huyu?...maana dah! Mi mwenyewe mara ya kwanza kuingia studio nilikuwa natetemeka kweli, yaani studio bwana haijalishi wewe una degree wala nini yaani unaweza kuaibika. Mara ya kwanza niliingia katika studio ya redio moja hapo Musoma inaitwa Victoria FM ebwana wee mimi nilimwambia Jesca ukweli kuwa sijawahi kuingia studio, akalazimisha kweli hadi tukaenda, sema hakuwa na nia mbaya, aliamua kunisaidia kutokana na ukarimu wangu kwake. Maana aliniapia kuwa laity kama angekamatwa anaangalizia kwenye ule mtihani angewekewa sifuri kisha angefukuzwa shule na kutakiwa kurudi na mzazi wake shuleni baada ya adhabu atakayokuwa amepewa kumalizika. Ni katika maongezi hayo Jesca akanieleza kuwa anasomeshwa na mjomba wake na ni mkali sana huku shangazi yake akiwa hampendi hata kidogo. Jesca akataka kujua kidogo kuhusu mimi pia, hakuamini hata kidogo kuwa nimemaliza chuo kikuu, akajiroga na kuanza kuzungumza nami kiingereza hapo nikampoteza vibaya. Yaani alipotea kweli maana alikuwa na kiingereza cha kuungaunga huku mimi nikiifurahia lugha ile.” Hapa Nafia akasita kisha akatabasamu, bila shaka aklifurahia sana kumbukumbu ile. Kisha akaendelea, “nilimweleza mengi sana kuhusiana na masomo, naam Jesca akaniona mimi kuwa wa muhimu kwake, akaniunganisha kwa rafiki yake mtaani nikaanza kuishi hapo huku akinipatia shilingi kama elfu kumi na tano hivi na vifaa kadha wa kadha nikaanza kuuza mihogo ya kukaanga. Hakika lilikuwa jambo jema, nilikuwa makini sana na yule niliyeishi naye pia nilikuwa makini nisiropoke lolote zito kwa Jesca asije kuwa kama waliotangulia, waliishia kunijua tu lakini mwisho wakanitenda. Nilivuta subira hadi nilipomzoea kisha nikamwamini Jesca ndipo nikaanza kumshirikisha mambo yangu, na nilifanya hivyo kwa sababu tu alikuwa mtu wa kutafiti sana, alikuwa akiniuliza maswali mengi na mara nyingine ni kama alikuwa akinirudisha darasani kwani aliniomba nimsaidie mambo kadha wa kadha, nilipoweza nikasaidia na niliposhindwa nikamweleza. Jesca akawa rafiki mwema!!
Swali lake gumu nililoshindwa kulijibu ni moja tu!! Kwanini nipo hivyo wakati nimesoma hadi chuo kikuu??
Nilipomjibu kuwa baba yangu alichoma vyeti vyangu na sasa sikuwa na ushahidi wowote wa elimu yangu likazaliwa swali jingine la kwanini ilikuwa hivyo nikamweleza tena sababu moja baada ya nyingine, na hatimaye nikajikuta nimemweleza juu ya Desmund!!
Simulizi ya maisha yangu ikambamba na kumliza Jesca, akaamua kutafuta namna ya kunisaidia na mwisho akakutana na Abraham Swea, mtangazaji wa redio Victoria katika vipindi mbalimbali kimojawapo kikiwemo MAPITO.
Siku moja Jesca akanieleza kuwa Abraham alikuwa akihitaji kufanya kipindi na mimi. Kipindi ambacho kitaniwezesha kupata msaada wowote ule kwani yeye Jesca alikuwa anakaribia kumaliza shule hivyo lazima ningeteseka sana. Hakika alikuwa amesema jambo la maana, nikakubaliana naye lakini nikamweleza kuwa jina la Nadia ni jina chafu tayari linaweza kuniingiza matatani. Sipo tayari kulitumia na watu walifahamu!! Sikutaka kumweleza kiundani juu ya kesi ya mauaji niliyoamini kuwa inanikabili. Lakini alinielewa, akazungusha kichwa huku na kule na mara akaanguka na jina ‘MARIAM’ akaniambia kuwa nitumie jina la hilo badala ya Nadia.
“Ni jina la marehemu mama yangu!! Nilimpenda sana, japo sikuwahi kumwona na siiikumbuki sura yake lakini niliambiwa na jamaa zake kuwa nililia siku tatu mfululizo baada ya kufariki kwake.” Jesca alinipa sababu ya kulitumia jina lile. Kwa sababu zake zile sikuweza kumpinga. Nikakubali kuwa Mariam.
Siku mbili baadaye nikaingia studio kwa mara ya kwanza, katika kipindi cha mapito. Kipindi ambacho kiliibadilisha tena historia ya maisha yangu. Nilijieleza kwa umakini sana huku nikikwepa kulitaja jina la Desmund, nikayaelezea magumu niliyopitiakatika jiji la Mwanza nikamtaja Jadida kama dada yangu wa kuzaliwa, nikasimulia juu ya utata wa Musoma vijijini nilipotaka kubakwa na akina Mwita. Hata kabla sijamaliza kusimulia Abraham alikuwa anatokwa na machozi, waliopiga simu wote walikuwa wanalia. Hapo sasa nikagundua kuwa mambo ambayo nilikuwa nimeyapitia hakutakiwa kuyapitia mwanadamu wa kawaida. Huenda Nadia mimi sikuwa wa kawaida!!!
Nilipata misaada mbalimbali, lakini msaada moja mkubwa ulikuwa ni kazi! Mzee mmoja alipiga simu akajitambulisha kama mzee Matata, alikuwa ananingoja nitoke studio aweze kuonana nami aangalie uwezekano wa kunipa ajira baada ya usaili. Maana nilisema kuwa eleimu yangu ni ya chuo kikuu lakini vyeti vyangu viliungua katika ajali ya moto ambayo iliondoka na uhai wa wazazi wangu wote wawili. Mzee Matata akawa ameguswa.
Nikiwa palepale studio nilipata msaada wa takribani shilingi laki moja. Jambo jema kabisa.
Nilipotoka nje nilimkuta Jesca akiwa analia kwa furaha na huzuni, alikuwa kikifuatilia kipindi kile moja kwa moja katika redio ndogo aliyokuwa amekuja nayo.
Wakati nazungumza na Jesca, ndipo nikaitwa katika gari moja ya kifahari kiasi. Aliyeniita alikuwa mzee Matata. Alikuwa na sura iliyojaa majonzi tele! Akajitambulisha nami nikajitambulisha, mara akafika Abraham tukaungana katika maongezi, maongezi juu ya ajira. Baada ya mazungumzo akanipatia namba zake za simu, akanisihi nimpigie simu siku inayofuata.
Siku iliyofuata nikafanya kama alivyoagiza, akanielekeza ofisi yake ilipokuwa, maeneo ya Mwisenge nje kidogo ya mji wa Musoma. Ilikuwa ofisi iliyojishughulisha na mambo ya usafirishaji, nikawekwa kama mwanafunzi wa majuma mawili nikawa mwepesi wa kuelewa na baada ya hapo nikahamishiwa katika ofisi zilizokuwa maeneo ya Nyasho!!
Huku nikaanza kufanya kazi, huku kila siku nikiamini kuwa kuna jambo sijalitimiza. Nilikuwa nadaiwa suala la kumkomoa Desmund!! Nikaliweka kiporo hili huku kila siku nikiombea nisikutane naye, yeye wala mkewe.
Ilikuwa kazi nzuri iliyonilipa vyema, mkurugenzi alinipatia chumba katika nyumba yake, huko nikawa naishi na msichana wake wa kazi. Yeye alikuwa akiishi nyumba kubwa pamoja na familia yake.
Nilichezwa machale tangu mwanzo kuwa nikianza kula vizuri tu nitapendeza, na hapo matatizo yataanza tena. Naam ukafikia ule wakati wa Nadia ambaye wakati huo niliitwa Mariam kuanza kuumiza akili yangu.
Bosi alikuwa akinitaka kimapenzi!
Haya yalianza baada ya kuniandalia safari ya kikazi kwenda Mwanza kwa ajili ya kuwafundisha kazi katika ofisi ya usafirishaji jijini huko. Akanipangia hoteli nzuri, na baada ya siku mbili alifika usiku kunijulia hali. Kwa sababu alikuwa mtu mzima sana mimi nilimkaribisha chumbani kwangu. Huko akapata nafasi ya kunitamkia kuwa alihitaji kunioa.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilipepesa macho huku na kule na kutamani atoweke mbele yangu, lakini alikuwa akingoja jibu langu.
Nikamtazama na bila kusita NIKAMKATAA!!
Hakuniaga akaondoka kisha akanitumia ujumbe kuwa nifikirie mara mbili!! Lakini sikuwa na haja ya kufikiria mara mbili wala kuhoji juu ya familia yake italichukuliaje jambo hilo, nilikuwa nimesimamia hapo hapo kuwa SIMTAKI!!!
Hilo lilikuwa kosa klililonitupa katika kinywa kingine kisichokuwa na huruma!!
Lakini labda kosa hilo lilikuwa dogo sana, nikafanya dhambi kwake nikamweleza mfanyakazi mwenzangu juu ya jambo hilo, sidhani kama nilifanya jambo sahihi.
Juma moja baadaye akanitumia ujumbe “NASIKIA UMEWATANGAZIA WATU KUWA UMENIKATAA”….Nikajua yule mfanyakazi mwenzangu amewasambazia watu wengine jambo hilo, ni mimi nilitakiwa kujilaumu.
Nilimpigia simu Jesca na kumweleza kila kitu, akanitoa hofu na kunambia kuwa mzee yule ni mtu wa watu sana na anaheshimika kutokana na moyo wake wa kujitolea, hawezi kunifanyia jambo lolote baya kitu cha msingi nilitakiwa kumwomba msamaha!!!
Msamaha?? Nikajiuliza, msamaha kwa lipi sasa, yaani amenitongoza nimemkataa nimwombe msamaha looh!….nikaamua kupuuzia. Huku nikimdangaya Jesca kuwa nitamuomba msamaha mzee Matata.
Ni heri ningejifanya mjinga nimwombe msamaha kuliko ukaidi nilioufanya!!!!
Usiku wa siku hiyo nikavamiwa pale chumbani, sikuchukua dakika nikakutana na giza nene!! Bila shaka waliniwekea madawa wanayojua wao!!
Nilipokuja kufumbua macho nikajikuta katika chumba kikubwa sana na sikuwa peke yangu, tulikuwa wengi lakini ni mimi pekee nilikuwa na afya tele. Wenzangu walikuwa wamekonda na walikuwa uchi wa mnyama, hawakuwa wakijiweza hata kidogo japo macho yao wengine yalikuwa wazi na wengine walikuwa wamesinzia. Hakuna aliyejishughulisha na mimi, chumba kilikuwa kina mwanga lakini ni kama hawakuwa wakiona lolote.
Nilipogeuka kushoto nikakutana na kikaratasi.
“WAULIZE WENZAKO NINI KILIWASIBU…KISHA UJIANDAE NA WEWE”
Mwandishi nilichanganyikiwa ujue yaani muda mfupi uliopita nilikuwa katika chumba cha hoteli jijini Mwanza, sasa nipo katika chumba cha ajabu sana na watu nisowafahamu tena wakiwa katika hali ya utatanishi! Uchi wa mnyama!!, nilichanganyikiwa sana. Nikasimama niweze kutafuta pa kutokea, nikajikuta nimekanyanga mkono wa mtu, sijui ulivunjika ule!! Alilia sana..alilia na hakuwa na la kufanya, kama alidhani kuwa alinipiga basi alikuwa amenipapasa tu!!
Nikahaha huku na kule!
Sikuupata mlango hata nilipofanikiwa kuzurura kila kona!!!
MARA KIZA !! NILIPAGAWA
Niliita jina la Jesca, ni huyu aliyekuwa ndugu wa pekee katika himaya yangu kwa wakati ule, ningeweza kuita mama lakini mama huyo alikuwa amenimwagia laana tayari, mzee Matata ambaye alikuwa ameniajiri sijui kama ndo huyu alikuwa ameniweka katika himaya hii ya kutisha ama vipi? Nilikosa majibu mara nikauona mkoba wangu upesi nikaupapasa na kukutana na simu yangu ya mkononi, nikaichukua upesi nikataka kupiga, nikakutana na neno ‘insert sim card’, nikajiuliza ni muda gani niliitoa kadi yangu ya simu!! Sikukumbuka hata kidogo!!....mwandishi kuna wakati niliwahi kuombea kifo lakini hapa nilikiogopa sana, kifo cha kufa kimateso namna ile, haikutamanisha hata kidogo kuwatazama watu wale waliokuwa kando yangu!! Bila shaka kabla ya kuwa vile walipitia magumu sana!!!........” Nadia akanyamaza kisha akaangaza huku na kule. Kisha akaniambia, “Tutelemke chini tukanunue maji nina kiu sana.”
Nikavaa makubadhi yangu nay eye akajitanda kiremba chake tukafunga chumba na kutelemka chini!!! Huku nikiwa nina wahka wa kujua nini kilijiri???
Nilimshika mkono Nadia tukakiacha chumba na kuteremsha chini ambapo nia yetu ilikuwa kununua maji ya kunywa. Nadia alikuwa mchangamfu sana tofauti na siku nyingine. Tukakifikia kibanda kidogo maalumu kwa huduma hizo tukanunua chupa mbili za maji ya baridi. Nikafanya malipo tukarejea tena juu.
“Hivi keshokutwa nd’o safari eeh.” Aliniuliza.
“Duh unakumbukumbu wewe, mi nilishaanza kunogewa na kanda ya ziwa. Yah! Keshokutwa ndani ya basi tena Dar es salaam hiyo, umepamis eeh!!” nilimjibu huku nikimtazama usoni ataipokea vipi ile hali. Niliamini anatamani sana kufika Dar es salaam maana mazungumzo yetu ya awali kabisa hadi kufikia hapo Mwanza kulikuwa na mazuri mengi sana tuliyoyataegemea jijini Dar es salaam. Jiji hilo ungekuwa mwanzo wa kuungana tena na familia yake iliyobakia. Nilikuwa nimemuhakikishia hilo, nami nilikuwa nimehakikishiwa na watu waliokuwa wameniagiza.
“Dar es salaam, Dar es salaam, Dar Dar es salaam.” Nadia akawa kama anayeimba kwa sauti ya chini, furaha ikapotea usoni mwake na macho yake yakabadilika na kuwa mekundu tena, yakang’ara kwa ishara ya machozi muda wowote.
Tukaufikia mlango wa chumba changu nikaufungua, Nadia akatangulia kuingia na kujirusha kitandani. Mimi nikaweka vifaa vyangu vya kurekodia sawasawia ili kama lipo neno kuhusiana na Dar es saalam ama chochote kile aweze kunieleza nami nirekodi.
“Dar es salaam, dah marafiki zangu enzi hizo wal;ikuwa wananitamani sana nilipowaambia kuwa naishi Dar es saalam, mimi pamoja na wao tuliiona Dar kama paradise na mahali ambapo pana kila aina ya starehe.
Lakini tukasahau kuwa hata mateso pia yanaweza kuwepo, lakini utayafahamu vipi mateso kama wewe mwenyewe hujawahi kuteseka. Shida ikukumbe wewe nd’o utaweza kuhadithia vizuri, hata wewe mwandishi najua unanisikiliza lakini huwezi kujua uchungu nilionao nikikwambia niliteseka.
Dar es salaam si mahali sahihi na niliingia huko nikiitwa Mariam.
Jina hili sijui kama lilikuwa sahihi kutoka kwa Jesca maana liliniiingiza pabaya. Baada ya kutekwa na watu nisiowajua na kisha kutupwa katika kile chumba cha watu ambao ni sahihi kuwaita wafu, aah!! Mzee Mwaijande jamani…” alisita akaanza kulia kidogo kisha akaendelea.
“Kila wema upande wa Nadia hawadumu, yaani yule mzee angeishi walau siku mbili hakika yasingenikuta yale yaliyonikuta, mzee wa watu akajifia!! Na walimuua kwa mateso wale. Ni mzee Mwaijande alikuwa walau na uwezo kidogo wa kuzungumza akanieleza kuwa nijipe pole kwani nipo katika tundu baya tayari, tundu la kifo!! Sikumuelewa nikaendelea kumuhoji, akanieleza kuwa kwa sababu mimi nina nguvu ningeweza kulikwepa japo ni hatari kuthubutu kutoroka. Akaendelea kwa shida kuzungumza akaniambia kuwa yeye alikuwa katika ugomvi na mtu akajikuta yumo humo ndani baada ya kuonekana ule ugomvi wa kuwania kiwanja alikuwa akielekea kuushinda. Nayeye akawa kama mimi akashindwa kukiri kuwa yule mpinzani wake ndiye aliyemtupa humo ndani.
“Kwani wewe uligombana na nani.”
“Na mzee Makorani wa hapo hivi Area C”
“Area C wapi tena mzee wangu.”
“Si hapa Dodoma ama wewe si mwenyeji!!” alinijibu bila wasiwasi. Hapo sasa nikapagawa, mimi nilikuwa Mwanza, sasa naambiwa Dodoma. Nikiwa katika hamaniko mara mwanamke mwingine akadai hapo tulipokuwa ni Singida, mwingine akajikaza kazungumza kuwa tupo Mugumu Serengeti. Hapo sasa nikatambua fika kuwa hakuna ajuaye ni wapi tulipo kila mmoja aliletwa bila kujitambua.
Mzee Mwaijande akaendelea kuniambia kuwa humo kuna mawili ama matatu kama yapo, lakini kubwa zaidi ni biashara ya madawa ya kulevya.
“Watakupasua tumbo lako na kuweka madawa yao, si unawaona wenzako hao wote wamesafiri mara kadhaa.” Mwili ukanisisimka kusikia jambo lile. Nilikuwa naona tu katika luninga mambo kama hayo ya mtu kupasuliwa tumbo na kisha kuhifadhi madawa ya kulevya, sasa naambiwa kuwa na mimi nitakuwa mmoja wao.
“Kama wewe ni mrembo wataanza na wewe kwanza kuwafurahisha na baada ya hapo utawatumikia katika biashara yao. Wenzako hao wamekuja humu ndani wakiwa warembo sasa wamejiishia. Mwingine anasema alikuwa Miss wapi sijui, miss Upareni.” Aliposema hivyo nikazifdi kusisimka, kumbe miss Upareni hakufa mwandishi, wala hakupotea katika mazingira ya kutatanisha alitekwa na kisha nafasi yake ikachukuliwa na mtu mwingine. Niliduwaa kwa sababu niliwahi kusoma katika gazeti tukio hilo.
“Lakini wewe unaweza kutoka hai humu ndani. Zipo njia zao mimi kama mkongwe ninazifahamu. Hivi huu ni mwaka gani kwani?” aliniuliza.
Nikamtajia mwaka ambao nilifahamu tupo.
“Doh! Nimekaa miaka mitano humu sasa. Jitahidi utoke binti, ukitoka wewe unaweza kutukomboa na sisi.” Alinisihi na mara milango ikafunguliwa. Wakavutwa watu kadhaa wenye nguvu kiasi. Mimi wakaniacha, nikiwa naduwaa mara wakarejea mara ya pili wakanichukua.
Nikakutana na mwili wa mzee Mwaijande ukiwa mfu tayari. Niliwasikia wakipiga simu na kuwaeleza watu wao kuwa mzee alikuwa amechoka tayari.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Naam simulizi yake ikaishia pale huku akiniacha bila kuijua njia.
Kutoijua njia kukanisababisha nifike Dar es salaam, walinisafirisha katika namna ileile ya kwanza. Sijui sasa kutoka katika nyumba ile hadi Dar ni muda gani lakini pale Dar nikafikishwa katika hospitali ambayo nimeisahau jina lakini inajulikana tu. Tukifika Dar nitakuonyesha. Mwandishi nikiisikia Dar najisikia uchungu, yaani natamani isingekuwepo ama nisingefahamu pale nilipokuwa ni wapi, lakini nilipafahamu na huyo Daktari niliwahi kumwona hapo kabla. Daktari akanichoma sindano ya ganzi hapo nikiwa namuona, wamenifunga kamba ngumu. Bora wangefanya hivyo nikiwa najaribu kujifungua mtoto lakini wao walifanya vile kwa lengo lao la kunibebesha madawa ya kulevya.
Sijui ni kitu gani nilikuwa nimewakosea, nakumbuka nilipiga kelele sana, lakini macho na midomo ikawa mizito. Nikasinzia.
Nilizindukia katika hospitali nyingine, huku sasa walikuwa ni madaktari wengine wazungu. Nikajikuta nimeshonwa tumboni.
Bila shaka walikuwa wamenitumia tayari.
Nilijilaani na kukitamani kifo, lakini kila nilipotamani kufa nikawa namkumbuka Desmund!! Sikutakiwa kufa, nikaamini hivyo.
Baada ya hapo nilipoteza fahamu tena na nikaibukia tena katika kile chumba katika mji tusioujua wote kwa pamoja.
Ule usemi wa kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza ulichukua nafasi yake baadaye kidogo. Nilikuwa napewa huduma nzuri sana, nikafanyishwa mazoezi na mara nikawa nalazwa kitandani, sikuchanganyika tena na wale wenzangu, sikujua wana nia gani mpya, nikaendelea kuvumilia. Hadi nilipopona kabisa ndipo nikakutana na mzee wa kiarabu.
Mkutano wetu wa kwanza ulikuwa chumbani tukiwa wawili pekee. Nikiwa uchi wa mnyama. Yeye alikuwa na taulo tu.
Mara akanisemesha kiarabu, nikaambulia baadhi ya maneno maana nilijifunza kutoka kwa baba yangu enzi hizo lakini sikumjibu. Mara akanisogelea na kuanza kunipapasa. Nikajua yale maneno ya Mwaijande yanatimia. Unadhani ningefanya nini na ningekimbilia wapi? Akazidi kunipapasa. Hapo nikanyanyua kinywa changu nikasema nisamehe kwa kiarabu. Akashtuka akaniangalia na kukoma kunipapasa.
“Wewe unatoka wapi?” aliniuliza kwa kiarabu, hilo nalo nikalinasa lakini kujibu ikawa kazi ngumu. Lakini nikajikakamua na kumjibu niwezavyo, “Familia ya Barghash.” Nikajibu
Akaendelea kuzungumza harakaharaka nikamwambia simwelewi, akajaribu kusema Kiswahili, naam Kiswahili kibovu kabisa.
Lakini afadhali nilinasa mawili matatu.
Akanieleza kuwa kama nikiwa mpenzi wake atanisaidia. Ningeanza vipi kumkatalia wakati nilimkatalia mzee Matata na sasa nipo katika matata.
Uhusiano ukaanza siku ile!!
Uhusiano wa kujilazimisha ilimradi kama kweli ataweza anisaidie nitoroke. Nilifanikiwa kujua kuwa yeye hakuwa na sauti ya mwisho, kwani kuna mzee mmoja alikuwa akiamrisha na yeye anatii. Hapo nikajua kuwa kazi ipo.
Jicho la yule mzee mkuu zaidi sijui kama lilikuwa halijawahi kuniona ama vipi, maana siku ambayo nilonana naye alikuwa kama zezeta anayetazama nzi arukavyo na kutua. Akanipandiosha na kunishusha.
Baadaye akahitaji kuonana nami tukiwa wawili tu. Bahati nzuri alikuwa anajua kiingereza na mimi hapo palikuwa nyumbani.
Tulizungumza mengi, na baada ya kutoka hapo nilikuwa na cheo. Cheo katika taasisi nisiyoijua na mbaya zaidi hata sikujua ni nani amesababisha nitupwe hapo na sikujua hata ni nchi gani.
Nikaanza kukitumikia kile cheo, jukumu langu likiwa kuhesabu kila siku ni akina nani wapo hai na wangapi wamekufa! Hivyo tu, kila mmoja alikuwa amefungwa namba mkononi ambayo ilikuwa haivuliwi hadi pale unapofariki.
Mwanzoni nilikuwa muoga sana kushuhudia mtu anavyokufa lakini baadaye na hata sasa ua mtu mbele yangu na wala sitatikisa hata mkono. Nilibadilishwa roho yangu na kuwa ya kinyama sana. Nikawa nawahesabu wenzangu, kila siku lazima mmoja alikufa nikiwa naona. Kila walivyokuwa wanakufa nikawa natamani kushuhudia kifo cha Desmund kwa macho yangu kwa mambo haya magumu aliyonisababishia.
Lakini sikujua hata nilipokuwa.
Baadaye mkuu akanitaka kimapenzi na wakati huo Barakat alikuwa mpenzi wangu. Sikumkataa na yeye nikamwachia anachotaka, sikuwa na thamani mwandishi, thamani yangu ipo wapi? Kama sina uhuru ni kitu gani cha kunilinda? Hakikuwepo….
Nilidhani mkuu yule waliyezoea kumuita masta alinitaka kimapenzi tu kisha basi ajiondokee zake lakini mara akaniganda, kila baada ya juma moja ananivamia na kunitaka kimapenzi.
Siku ya siku ambayo sikuwa naijua hata jina lake baada ya kuishi kwa muda katika mazingira yale. Siku iliyonihamishia katika ukimbizi mwingine.
Mwandishi yule masta alinifumania na Barakat, tulikuwa tumekumbatiana tu kimahaba. Aisee mimi nilijifanya nimezoea kuona watu wakiwa wafu ama wamekufa, kumbe kuna wenzangu wanajua kuua.
Masta alirusha sijui kitu gani kile kikauparaza mkono wa Barakati ukawa kama unataka kukatika, Barakati naye akajitutumua akachomoa jambia akarusha likapasua bega la masta. Hapo sasa wakavaana kimya kimya, mimi nikajua yeyote yule atakayepona ataniua mimi..hapo nikaamua kutimua mbio, kuelekea popote pale ambapo ningeweza kufikia tamati yangu.
Nilikimbia sana na huku nyuma nikasikia sauti ikiita jina langu kwa namna, maana walizoea kuniita 105 (one zero Five)…nikaibaini ile sauti kuwa ni ya yule masta, sikutaka kugeka maana kwa vyovyote vile nilikuwa nakufa. Asingenipa muda wa kujieleza. Mara taa zikazimwa, giza kali na sikujua naelekea wapi tena, lakini sikuacha kukimbia, nilizidi kupenya huku na kule, mara nianguke nasimama tena, sikuwa na uhakika hata asilimia moja kuwa huko mbele kuna njia maana sikuwahi kufika huko. Sauti ya masta sasa niliisikia kwa mbali sana. Nikaendelea mbele, nikafikia vyuma nikajibamiza nakuanguka chini, nikaisikia damu ikivuja kutoka katika midomo yangu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nikatulia pale huku nikikisikia kifua changu kikipiga filimbi kila nilivyokuwa napumua. Giza tu ndo macho yangu yaliweza kuona. Nilibaki kushika vyuma vile nikisubiri wafike na kuniua. Maana miguu ilikuwa inavuta sana na sikuwa na nguvu za kuendelea kukimbia na hata ningekuwanazo ningekimbia kwenda wapi??
Nikakumbuka kufanya sala ili M<ungu anichukue kabla hawajanifikia ikibidi. Wakati nasali sauti ya masta nayo ikazidi kusogea karibu na masikio yangu.
Alikuwa anatukana matusi ya kiingereza, hakika alikuwa amekasirika maana aliweka na kiapo kuwa akinikamata ananikata vipandevipande. Mwandishi hata sala sikuweza kuimaliza, nikakisubiri kifo changu.
“Nakulaani Desmund na damu hii inayoenda kumwagika, roho hii inayohukumiwa bila hatia Desmund popote ulipo, isiondoke roho hii kabla haijakusulubisha wewe na ukoo wote na kizazi chako chote, Desmund nakufa mimi…nakufa d’o kitu ulichokuwa unataka, lakini nakuaminisha kuwa upendo wangu ulioulipa kwa mabaya haya utakusulubu maisha yako yote, na damu hii haitakauaka kabla haujajutia….” Nilizungumza huku nikiisikia sauti yangu ikijirudiarudia.
Badala ya kusikia jibu kutoka kwa Desmund mara nikasikia nikikamatwa mguu wangu!!
“Mpumbavu, Malaya mkubwa wewe.” Masta alikoroma kiingereza.
Nadia nilikuwa nimekamatika.
Hilo likawa neno lake la mwisho kwa kiingereza akaanza kuzungumza kiarabu cha ndani kabisa. Alinivuta lakini sikutaka kumfuata. Niliendelea kung’ang’ania vyuma nilivyokuwa nimeshikilia. Lakini nilijua tu ni mfa maji haishi kutapatapa…….” Akasita kisha akaendelea, “Yaani nimesema maji nd’o nakumbuka tumenunua maji na hadi sasa hatujanywa!! Duh yasije yakawa ya moto tena.” Alisema Nadia kisha akachukua maji nami nikatwaa yangu, hakika makoo yalikuwa yamekaua haswaa!!
“Mpumbavu, Malaya mkubwa wewe.” Masta alikoroma kiingereza.
Nadia nilikuwa nimekamatika.
Hilo likawa neno lake la mwisho kwa kiingereza akaanza kuzungumza kiarabu cha ndani kabisa. Alinivuta lakini sikutaka kumfuata. Niliendelea kung’ang’ania vyuma nilivyokuwa nimeshikilia. Lakini nilijua tu ni mfa maji haishi kutapatapa…….” Akasita kisha akaendelea, “Yaani nimesema maji nd’o nakumbuka tumenunua maji na hadi sasa hatujanywa!! Duh yasije yakawa ya moto tena.” Alisema Nadia kisha akachukua maji nami nikatwaa yangu, hakika makoo yalikuwa yamekaua haswaa!!
“Katika maisha wanadamu huwa ni wagumu sana kuamini kuwa Mungu yupo hasahasa wakati wa shida ama tatizo kubwa. Mungu hukumbukwa wakati wa raha tu. Utawasikia maharusi wakimshukuru Mungu kwa kuwafanikishia jambo hilo walilolingoja kwa muda mrefu lakini ni nadra sana kuwasikia wafiwa wakimshukuru Mungu waziwazi kwa kumtwaa mojawapo kati ya wapendwa wao!! Wanadamu sisi watu wa ajabu sana!! Nawakumbuka rafiki zangu wengi tu walivyofeli masomo yao hawakumwambia Mungu asante kama walivyofanya baada ya kufaulu!!” Nadia alinieleza maneno yale baada ya kuwa amekunywa nusu chupa ya yale maji. Nami nikatikisa kichwa kumuunga mkono.
“Hata mimi ni mmojawao, mmoja kati ya wasiomkumbuka na kumuamini Mungu wawapo katika shida ngumu. Badala yake kutarajia miujiza ya kidunia. Maana katika giza lile ambalo nilikuwa kisha yule muuaji akanikamata miguu sikutarajia lolote linaweza kufanyika kwa muujiza wa Mungu na badala yake niliendelea kuamini kuwa ni mimi pekee wa kuweza kuiokoa nafsi yangu. Niliendelea kutapatapa huku na kule nikiling’ang’ania chuma ambalo lilibaki kuwa muhimili wangu mkuu, na yeye aliendelea kunivuta huku akizidi kuweka viapo vikali vya kuniua kwa kunikatakata. Labda ulikuwa wakati wa kujikabidhi kwa Mungu lakini ningeanza vipi kuamini kuwa Mungu alikuwa upande wangu wakati kila baya linalotokea aliwashindia maadui zangu na akiniacha mimi katika majeraha? Nikajiaminisha kuwa yule hakuwa Mungu wangu bali Mungu wa maadui zangu.
Naam!! Huenda aliisikia sauti yangu, labda alingoja niwe katika wakati mgumu kama ule nd’o aweze kujionyesha kwangu!! Lile chuma ambalo nilikuwa nalitegemea sasa lilianza kulegea kutokana na kuvutwa sana na yule mzee wa kiarabu tuliyezoea kumuita masta. Hapo sasa nikakata tamaa, nikataka kujiachia lakini nafsi ikagoma kukata tamaa nikaendelea kushikilia japo nilikuwa nazidi kulisikia likisogea na mimi.
Mara likafyatuka!!
Nilichoweza kukisikia ni yowe la hofu kutoka kwa yule mwarabu, na baada ya hapo maji yalitusomba kwa nguvu mno na kisha kuanza kusdafiri nasi, ni hapo ndipo nikatambua kuwa chuma niliyokuwa nimeshikilia ilikuwa ni ufunguo wa aidha tanki la maji ama chochote kile. Lakini ajabu ni uwingi wa maji yale, nikajishukuru kwa kutokuwa mvivu kujifunza kuogelea enzi hizo nikitumikia uvuvi nyumbani kwao Desmund, nilikata maji kwa mwendo mkali, hofu ikiwa imetanda hasahasa lile giza nene, giza likiwa limetawala. Nilijigonga huku na kule lakini sikubadili azma yangu ya kutapatapa kama nitakufa nife nikiwa najaribu!! Baada ya kuogelea kwa dakika kadhaa hatimaye niliweza kuona mwanga. Hapakuwa na giza tena, niliangaza kushoto na kulia baada ya kunyanyua kichwa changu, nikawaona watu kwa mbali, hivyo nikatambua kuwa sikuwa mbali sana kutoka katika ufukwe. Hofu nyingine ilikuwa juu ya nchi ambayo ningeweza kuwepo na watu wa pale ufukweni, isijekuwa ni walewakle waliokuwa wametuteka wakanikamata tena. Nikazama tena majini na kuanza kupiga mbizi. Na nilipoibuka tena ndipo nilipokutana na maajabu makubwa ambayo sikuyatarajia hata kidogo!!
Nikaona PANTONI…..lilelile la Kigamboni!!
Kwa hiyo pale tulikuwa Dar esa salaam!!
Nilistaajabu huku nikiendelea kukata maji, sikujua hata ni wapi nilitokea hadi kufika pale nilipokuwa, lakini nilitilia mashaka maggorofa kadhaa yaliyokuwa kandokando na bahari ya hindi. Nikaufikia ufukwe, mavazi yangu yakiwa tepetepe, ubize wa watu jijini Dar es salaam ukanisaidia sana, hakuna aliyekuwa na habari na mwenzake katika ufukwe ule. Nilijituliza huku nikitafakari ni kipi kinafuata katika maisha yangu baada ya Mungu kuniepusha na mauti yale?
Hakika ni Mungu tu, maana kwa uweza wangu hakuna ambalo ningeweza kufanya.
Jua likapiga na upepo ukapuliza mavazi yangu yakapata hali ya ukavu kiasi!!
Na akili nayo ikachangamka na kutambua kuwa kuna uwezekano mkubwa sana wale watu watakuwa wakinitafuta. Na iwapo wakinikamata wataniua maana kuna siri tayari nilikuwa nimezijua, utumwa katika nchi huru, tena utumwa wenye adhabu nzito ndani yake. Uuzaji wa madawa ya kulevya!!
Nikasimama wima, walau nilikuwa katika jiji ambalo nilikuwa nalifahamu, lakini ni jiji ambalo bila kuwa na pesa hauna maana ya kuwa hapo nadhani unalijua vyema, nami sikuwa na nauli wala mtu ninayemfahamu pale. Nikiwa wima nikajiuliza niende wapi, mwisho nikaamua kuelekea Vijibweni, ni huku tuliwahi kuishi na familia yangu kabla sijaamua kuasi na kuungana na Desmund katika mahusiano ya mashaka, mateso na karaha tupu huku yakiichafua historia yangu jumla. Nilipiga hatua moja baada ya nyingine, kutoka kivukoni hadi Kibada si karibu hata kidogo nililazimika kutembea sana. Hatimaye nikaifikia ile nyumba ambayo zamani nilikuwa nikikohoa kidogo tu nasikilizwa, nyumba ambayo mlinzi alikuwa akiniogopa na kuniheshimu zaidi ya mbwa mkali. Nyumba ambayo familia yenye upendo na amani iliishi humo. Nikainama chini na kujitazama, sikuwa na viatu na nguo niliyovaa ilikuwa imechakaa, nikajifikiria jinsi kichwa changu kisichokuwa na nywele nyingi jinsi kisivyotamanisha hata kukitazama. Kwa unyonge kabisa nikapiga hatua tena nikalifikia geti.
Nikajipa moyo kuwa labda habari za kwenda Saudi Arabia ni uongo mtupu familia yangu itakuwepo.
Labda hata habari za mama kufariki ni uongo vilevile alikuwa hai na wote walikuwa ndani, labda hata mlinzi aitwaye Hamduni nitamkuta na ataniheshimu tena.
Wakati naduwaa mara geti lilifunguliwa ghafla, akatoka mlinzi akiwa na bunduki aina ya gobole mkononi. Alikuwa ameikunja sura yake akinitazama mimi.
“Wewe ni nani ana unataka nini hapa?” alinikoromea! Nilikuwa katika mshtuko bado nikabaki kumwangalia badala ya kumjibu, akanirukia na kunikwida na kisha kurudia swali lilelile
“Naitwa Mariam!” nilimjibu.
“Sijakuuliza jina kichaa wewe, unafanya nini hapa muda huu?” aliniuliza kwa jazba. Kabla sijajibu akaendelea, “Hapa haturuhusu hayo mambo yenu ya kuombaomba sijui” alisema lakini mara akanikazia macho katika kifua changu!! Nami nikajitazama, nilikuwa natokwa damu.
“Umekuwaje binti!!” sasa aliniuliza kwa upole.
“Naitwa Mariam, wazazi wangu wanaishi katika nyumba hii”
“Wazazi wako?...maskini madawa ya kulevya kila siku wanakataza maskini. Binti mzuri kama huyu na yeye yamemwathiri looh!! Kijana taifa la kesho huu usemi ufutwe sasa.” Alilalamika peke yake, nikajua anahisi mimi nimeathirika na madawa.
“Mzee Barghash ni baba yangu.” Niliongezea.
“Binti….njia ile pale waweza kwenda zako mbali na hapa.”
“Babu sijachanganyikiwa, situmii madawa ya kulevya, nina akili zangu timamu, niulize lolote nami nitakujibu!! Tafadhali nisaidie nionane nao.”
“Binti leo tarehe ngapi mwezi wa ngapi? Na ni mwaka gani huu achana na tarehe kwanza.” Aliniuliza kama kunipima akili. Hakika alikuwa amenipata vilivyo, sikujua hata huo ulikuwa mwaka gani na sikujua hata nimekaa kule mafichoni kwa muda gani. Lakini nikajitahidi niweze kujibu ili aweze kuniamini.
Nikajiaminisha kuwa huenda hata mwaka mmoja haujaisha tangu nitupwe kule. Nikaamua kukadiria kuwa ulipita mwaka
“Mwaka 2010…”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Yesu wangu weee!! Binti toka na upotee mbele yangu mara moja nasema.”
“Babu nipe nafasi ya mwisho. Nisikilize tafadhali.”
Wakati anataka kunitishia bunduki mara mtu mmoja akatokea getini, na kumshangaa yule mzee.
“Kababu huyu ni nani? Bona chafu chafu tu navaa uchi hapa” sauti ya mama wa kihindi. Ikakoroma huku akinitazama kwa sekunde moja huku sekunde nyingine akimtazama mlinzi. Ile hali ya kuhangaika kuzungumza Kiswahili ikanipa upenyo wa kujaribu bahati yangu ya kuuthibitishia umma kuwa sikuwa kichaa.
“Excuse me madame! Can I talk to you..pleasee!!” nilimsihi kwa lugha ya kiingereza, hapo akashtuka na kisha kuniuliza kwa kiingereza huku akiwa na wasiwasi na mlinzi naye akinishangaa.
“Wewe ni nani.’ Akaniuliza, nikajieleza vyema ubin wangu.
“Ooooh!! Baba yako alituuzia nyumba hii miaka mingi sasa hadi leo 2010 ni muda sana. Kumbe wewe ni mtoto wake, nini kimekutokea?” alinieleza na ni hapo nikatambua kuwa nimekaa kule sirini kwa miaka miwili tangu 2009 na huo mwaka ulikuwa 2011. Nikabaki kinywa wazi. Hapakuwa na jipya nikajaribu kuulizia kuhusu majirani, mama yule hakuwa akimfahamu hata mmoja.
Kisha akaamuru geti likafungwa!!
Nikatakiwa kupotea eneo lile.
Nikatii lakini nikamwomba mlinzi kidogo anisikilize.
“Jizungushe pita baada ya dakika kumi apotee.” Aliniambia, nikajiondokea. Nikapita huku na kule kama nitakuta wale majirani wa miaka hiyo lakini haikuwa hivyo, palikuwa na watu wagenmi tu!!
Baada ya dakika kumi nikarejea. Nikamwomba mlinzi aniazime simu yake nipige. Aliniangalia kwa mashaka nami nikagundua hofu yake.
“Nikutajie namba unipigie hizo namba tafadhali nakuomba.” Nilimsihi, akanielewa.
Nikajaribu kuvuta kumbukumbu, nikataja na kungoja majibu.
Simu ikaanza kuita!! Mara ya kwanza haikupokelewa!!
Mara ya pili ikapokelewa na mwanaume, jambo ambalo sikulitarajia.
Mlinzi akaniamini akanipa simu nizungumze huku akiiweka sawa bunduki yake, bila shaka kitisho nisikimbie na simu yake.
“Samahani, naomba kuongea na nani huyu? Naomba kuongea na mwenye simu kakangu.” Nilijikuta nasema.
“Mimi ndiye mwenye simu aisee.” Alinijibu kwa jeuri.
Nikaishiwa usemi lakini mara nikamsikia akisema maneno chinichini na hatimaye akaanza kuongea msichana.
“Halo! Samahani nikumbushe jina lako tafadhali.”
“Yaani wewe unapiga na hujui unayempigia.”
“Samahani wewe ni Jesca.”
“Kwani wewe unampigia nani?” aliniuliza na mlinzi naye alikunja sura akionyesha kujutia pesa ilivyokuwa inateketea katika simu yake.
“Nampigia Jesca tafadhali.” Nilisihi.
“Ni mimi nini shida na nani mwenzangu?”
“Jesca mimi Mariam, mimi Nadia Jesca!!! Jesca kama ni wewe kweli tambua kuwa nipo katika shida kubwa.”
“Nadiaaaa!!! Nadiaaaa!!!” alihamanika huko alipokuwa.
Simu nayo ikakatika!!
Mlinzi akaanza kulaumu, mara simu ikaita kwa namba mpya tofauti na ya Jesca, mlinzi akapokea.
Alikuwa Jesca.
“Nadia nilijua haujafa, nilijua wamekusingizia Nadia, nilijua ni njama….nililia Nadia, nililia sana lakini sikuwa tayari kusema ulazwe pema peponi, sikuwa tayari Nadia. Sauti yako ipo hai Nadia, nakupenda Nadia wangu, upo wapi Nadia.” Aliongea kwa hisia kali Jesca, machozi yakaanza kunibubujika.
“Nipo kama sipo, nipo kama mzimu, sina nguo za kuvaa, sina chakula, sina mahali pa kuishi. Ni afadhali ningekuwa katika kambi za wakimbizi. Jesca labda ni bora ningekuwa nimekufa, lakini ninayopitia ni zaidi ya mahangaiko. Jesca nakupenda sana na namba yako haikufutika katika kichwa changu kamwe. Nilikwambia ni wewe pekee ndugu yangu katika dunia hii. “
“Mtanimalizia chaji yangu!!” alilalamika mlinzi.
‘Jesca upo wapi kwani.”
“Nipo mlimani mpenzi. Nipo huku chuoni.”
“Jesca jamani!!! Hadi umefika chuo, mimi nipo huku Kibada, kama nilivyokwambia sina hali.”
“Kibada ni wapi??”
“Kigamboni…” nilimjibu nikamsikia akimuuliza yule mvulana aliyepokera simu mara ya kwanza.
“Baby Kibada unapajua”..kisha baada ya dakika kadhaa akaniambia, “tunakuja huko muda si mrefu eti utungojee Kigamboni huohuo upande wa pili..”
“Jesca natamani ungepewa macho, unione nilivyovimba miguu, upewe na tumbo langu uisikie hii njaa kali inayioishi humu, Jesca sitaweza kufika Kigamboni. Nitafia njiani!!” nilimnweleza. Nikamsikia akilia kwa kwikwi kutoka upande wa pili.
“Basi tunakuja hadi huko!! Usijali.” Aliniambia.
“Sawa mtatumia namba hii babu ataniambia.” Nilihitimisha.
Kisha nikazungumza na babu akakubaliana na mimi, nikaahidi kuwa wakifika nitampa chochote kitu atie mfukoni. Hapo nikamteka.
Nikaondoka pale na kujiweka mbali kidogo, nilipokaa chini nikakumbuka kumshukuru Mungu wangu!!! Alikuwa akinionyesha miujiza.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya masaa mawili na nusu hatimaye nikaona gari likisimama kwa mbali, babu akanipungia mkono. Nikakimbia mbio kwenda alipokuwa.
“Wapo ndani ya gari ile, usisahau chochote kitu!!”
Hapo hapo nikatimua mbio, mara mlango wa gari ukafunguliwa haraka akatoka binti akiwa amevaa kisasa sana, sketi fupi mno na viatu virefu. Akaweka urembo wake kando akavua viatu na kuanza kutimua mbio.
Harufu ya upendo ikasafiri na kuzifikia pua zangu, macho yanayomaanisha yanachotazama yakanieleza kuwa yule alikuwa Jesca. Naam! Hatimaye tukakutana ana kwa ana tukarukiana na kukumbatiana kwa nguvu, hiyo haikutosha Jesca akajisahau kuwa mimi nina njaa akanirukia tukaanguka chini lakini furaha haikupotea hata kidogo!!
Jesca alikuwa analia na machozi yake yaliangukia katika mabega yangu!!
Alikuwa amekuwa mdada mkubwa tena wa kisasa!!
Baada ya kusalimiana nikamkumbuka babu, Jesca akanipatia noti mbili nyekundu nikampelekea, mzee hakuamini lakini nadhani alitambua kuwa wema wake na imani yake kwangu vilikuwa vikubwa sana!!
“Bryan….anaitwa Mariam ni dada yangu. Na…Mariam huyu anaitwa Bryan ni mchumba wangu. Mengi tutayafahamu mbele kwa mbele.” Alitambulisha Jesca. Kisha nikapakizwa ndani ya gari tukaondoka!!
Wanasema kuwa baada ya dhiki ni faraja lakini kwa Nadia mimi kila baada ya dhiki ilikuwa inakuja dhiki nyingine inayofanana na faraja kisha inanisulubu. Hata hapa nilipokuwa sikutaka kujidanganya kuwa nimefika katika kikomo cha mateso!! Lakini walau nilikuwa katika mikono ya Jesca, na hapo niliweza tena ku….” Nadia akanitazama kisha akatabasamu!! Nikaelewa alikuwa anamaanisha nini kuikatisha ile kauli.
“Hee!! Yaani kumbe unanisikiliza tu hata kusema Nadia twende kula muda umefika aa mwanaume mbaya wewe dah!! Mwone!! Mi nina njaa mwenzako sio siri, ile kapuchino yote imamemalizika tumboni…”
“Niwapigie simu walete huku ama..”
“Hamna hawa wakileta huku huwa wanapunja sana. Twende hukohuko yaani wakinipunja tu naenda jikoni mwenyewe kujipakulia.” Alitania Nadia, tukajikuta tunacheka wote.
“Haya basi nipishe nibadili nguo mwenzako.’ Aliniomba, nami nikatoka nje ya chumba chake na kwenda katika chumba changu.
Huko chumbani wakati na mimi nabadili nguo nilikuwa nahangaika na utata wa simulizi hiyo yenye maswali mengi!!
Sasa Jesa na Nadia wamekutana Dar!! Hivi huu ndo mwisho wa simulizi ama? Lakini haiwezi kuisha maana hali niliyomkuta nayo Nadia Musoma haikuwa ya kawaida hata kidogo sasa alirudi lini Musoma na ni kwanini nilimkuta katika hali ile??
Baada ya dakika zipatazo kumi mlango wangu uligongwa nami wakati huo nilikuwa namalizia kufunga kishikizo katika shati langu.
Nikauendea mlango huku nikijua kuwa lazima atakuwa Nadia, na sikuwa nimekosea alikuwa ni yeye.
Nikaufunga mlango kisha kwa mara nyingine tukaenda chini kupata chakula.
Nadia akaagiza nami nikaagiza, baada ya muhudumu kuondoka nikamtazama Nadia na hapo nikapata cha kuanzia maongezi maana tulikuwa kimya sana.
“Yaani macho yako dah! Yamekuwa mekundu, ukiongezea huo weupe na kilio ndo umetisha kabisa.”
“Duh nimejaribu kunawa, bado yanaonekana mekundu?” akanijibu. Nikamweleza kuwa si tu mekundu bali yamevimba pia. Kisha nikaongezea neno ambalo lilizua simulizi nyingine kutoka kwa Nadia.
“Aisee kama yangekuwepo mashindano ya kulia duniani ungejitwalia tunzo.” Nadia akanitazama kwa makini kama vile hakusikia vyema nilichomweleza.
“Katika hayo mashindano labda kama Jesca asingeshiriki. Lakini kama angeshiriki basi tena kila mashindano yanapofika angeshinda yeye, aisee kuna watu wanajua kulia duniani, sema heri yake yeye ni mweusi hata hawi mwekundu, tatizo moja tu akilia mwache hadi anyamaze hataki kubembelezwa na mbaya zaidi anaweza hata kukutusi ukijifanya kumbembeleza, dah Jesca!! Lakini alikuwa na sababu ya kulia, na ni Jesca anayenifanya nizidi kuamini wanaume wote ni sawa tu hakuna cha wewe mwandishi wala raisi wa nchi wote hamna maana kabisa, yaani ujue siku ya kwanza namwona Bryan nilimwona tu kama vile kuna jambo analificha, niliona kabisa tabasamu la kinafiki kutoka katika uso wake, nami nikampa tabasamu la kinafiki maisha yakaendelea. Wakanifiokisha hadi mahali walipokuwa wanaishi, aisee nitakuwa mnafiki nikisema Bryan nalikuwa hajajipanga, kiukweli alikuwa amekamilisha kila kitu kinachofaa kuwa ndani ya nyumba, na Jesca alikuwa mama mwenye nyumba ile.
Nilipofika pale mida ya jioni nikatambua kuwa jumla ndani tulikuwa watu hai watano, Jesca na mchumba wake, msichana wa kazi na kitoto kidogo, na mimi. Jesca akanieleza kuwa alizaa kabla ya kuingia chuo. Sikutaka kumuhoji sana lakini ni kama alikuwa na simulizi nyingine nzito nyuma yake. Nikaandaliwa chakula nikala na hapo nikapata nguvu mwilini.
Siku iliyofuata nilibaki mimi na msichana wa kazi na mtoto, Jesca alienda chuo na mchumba wake alienda alipojua yeye. Hakika siku hiyo nilivuta hewa safi na kujisikia nipo nyumbani kabisa, siku ya pili na hatimaye majuma mawili nikiwa nakula milo mitatu kwa siku.
Ndipo ikafikia siku ya kupata majibu yangu!! Siku hii Jesca alichelewa sana kutoka chumbani mwake, na hata alipotoka alikuwa amevaa hijabu.
“Jesca wewe na hijabu wapi na wapi na tangu lini?” nikamuuliza. Badala ya kujibu akacheka tu!! Nikajua anapotezea kujibu swali langu, kiherehere kikanishika nikaendelea kuuliza.
“Mwenzangu, mara moja moja huwa navaa…” alinijibu kwa sauti ya chini na hapo hapo nikaona kitu cha kustua sana.
Damu!! Damu katika hijabu nyeupe ya Jesca.
“Jesca, na hiyo damu hapo!!”
“Wapi eeh!! Damu.” Akaweweseka nami nikamkazia macho. Sikumjibu weweseko lake nikamngoja aseme kitu.
Mara akaanza kulia!! Si nilikwambia kuna watu wanajua kulia mwandishi, alilia akakimbilia chumbani kwangu!! Nami nikamfuata.
Nikamkuta ameondoa hijabu na kichwa kimebaki wazi na alikuwa amejiinamia. Nikamtikisa, alikuwa analia tu!!
Mara akaunyanyua uso wake, mwandishi mimi najua nilishapigwa sana hata mara nya kwanza kuonana na wewe ulinikuta na majeraha lakini ni mara chache sana niliwahi kuona mtu amepigwa akapigika.
Jesca alikuwa hatamaniki kumtazama! Alikuwa na manundu usoni na katika paji la uso na alikuwa na michubuko kadhaa.
“Jesca ni nini ntena hiki?’ nilimuuliza lakini hakujibu bali alikuwa analia kama mtoto mdogo, alilia sana kila akijaribu kusema neno inashindikana anaambulia kutoa kamasi tu, kisha kilio upya, halafu analia kwa sauti ya juu sasa. Nikamwacha akalia kwa takribani nusu saa. Hapo sasa kidogo aliweza kusema neno la kwanza kuhusiana na uso wake.
“Bryan amenipiga Mariam, amenipiga sana jana usiku!!” sitaisahau sauti hii jinsi ilivyonichoma na kuniumiza moyo wangu. Chozi likanitoka nikawahi kulidaka kwa kutumia kitambaa cha mkononi, Jesca hakuona.
Jesca akanieleza juu ya maisha yake kwa miaka miwili nyuma. Akanieleza juu ya mjomba wake kushindwa kuendelea kumlipia ada kutokana na shinikizo la mkewe, kabla matokeo hayajatoka Jesca akazurura huku na kule na mwisho kukutana na Bryan, mwanaume ambaye alimpa sharti moja tu kuwa naye katika mapenzi kumzalia mtoto na kisha atamfanyia kila kitu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa sababu Jesca alipenda kusoma akakubaliana na hali, akabeba mimba akiwa nyumbani, baadaye Bryan akamtorosha kwenda Dar es salaam, ni huko ambapo alimzaa mtoto wake wa kwanza akiwa mwaka wa kwanza chuoni. Mapenzi yaliendelea vyema lakini unyanyasaji ukaanza taratibu kisha kukolea, Bryan akamfanya Jesca kama mtoto mdogo, hatakiwi kuulizia lolote ambalo atakuwa na mashaka nalo, hakuruhusiwa kujua Bryan anafanya kazi gani na wapi. Na baadaye vipigo pasipo na sababu vikaanza, Jesca akavumilia tu! Siku nyingine Bryan harudi siku tatu, akirudi siku ya nne asikute chakula mezani inakuwa tiketi ya kumpiga Jesca. Jesca hakuwa na la kufanya kwa sababu alikuwa mtumwa tu na alimtegemea Bryan kwa kila kitu, akipigwa anajikausha, akitukanwa hajibu kitu, nia yake ikiwa kumaliza masomo ya chuo kikuu na kutafuta kazi yake.
Kama hiyo haitoshi Bryan akaanza tabia mbaya kabisa, tabia ambayo baada ya kukataliwa nd’o ikanogesha kichapo kila siku. Yaani acha tu Mariam naishi kimateso sana hapa. Nd’o kama hivi akinipiga navaa hijabu naenda chuo, ipo siku nitatimiza ndoto zangu dada Mariam ipo siku na Mungu ninayemuamini ananisimamia”
“Jesca kuna jambo gani jingine la zaidi.” Nilimuuliza baada ya kuona maelezo yake yana walakini.
“Nikitoka chuo basi dadangu.” Akanijibu, akavaa hijabu nyingine, akaondoka!!
Mwandishi niliyapima yale maelezo ya Jesca lakini hayakuniingia akilini, niliamini kuwa lazima kuna jambo la ziada linasababisha haya, haiwezekani mwanaume akutoe kijijini huko akulete mjini akubali umzalie, akutafutie mfanyakazi akuweke katika nyumba kubwa mwisho aanze tu kukupiga, akili ikagoma.
Nikajiahidi kuwa akitoka chuo nitambana nijue alimkosea nini Bryan, nikahisi huenda hata aliwahi kumsaliti ama ana kimwanachuo kingine huko anarusha shutuma kwa Bryan!! Nikaingoja mida ifike.
Jioni ile akarejea akiongozana na mchumba wake!! Wakaenda chumabni moja kwa moja.
“Jesca mwambie Naomi asituwekee chakula tumekuja nacho sawa eeh!!” Bryan aliniambia kwa sauti tulivu, nikaitikia kwa kichwa.
Nikajua wapendanao wamepatana tayari!! Na nikaamini kuwa nimeikosa nafasi ya kujua nini kinamsibu Jesca.
Usilolijua mwandishi ni sawa na usiku wa giza……” akasita kidogo akatazama mahali nami nikatazama, muhudumu alikuwa analeta chakula.
“Vipi atupelekee chumbani ama vipi?” nilimuuliza Nadia.
“Yaani kama ulikuwa kichwani mwangu!!” alinijibu, nami nikachukua jukumu la kumweleza muhudumu nia yetu! Akatii.
Tukaenda chumbani!!
Tulikifunika kile chakula, Nadia akaendelea kuzungumza.
“Yaani sijui ni ule moyo wa Jadida bado ulikuwa ukikitawala kifua changu ama vipi, yaani sikuwa na amani hata kidogo, hadi majira ya saa tano usiku nilikuwa sijalala. Nilikuwa nikitafakari uhuni wa wanaume hawa. Nikajikuta nahisi nipo katika nyumba moja na Desmund!! Kwa aliyonisimulia Jesca nikamwona Bryan kama Desmund. Na hapo nikaanza kuwafananisha lakini nikashtushwa na kishindo kikubwa.
Ule ulikuwa usiku hivyo kishindo hata kama ni kidogo lazima ukisikia vyema, vipi kuhusu kishindo kikubwa.
Hapo nikavamiwa na akili ambayo naweza kuiita ya kitoto. Sikuwa nimebanwa mkojo lakini ile hali ya kujua kuwa njia ya kwenda chooni ni lazima upite mbele ya chumba cha Jesca na mchumba wake. Nikaamua kutoka kwenda chooni nikijisemea kuwa huenda ni Jesca amepigwa!!
He! Ujue ilikuwa kama masihara, napita mbele ya kile chumba nikawa nasikia mabishano, hakika yalikuwa mabishano makubwa!!
Jesca alisikika akilia, na Bryan alikuwa anakoroma akilazimisha jambo.
“Jessy nitakuua ujue, nitakuua nasema….si wewe huwa unakataa halafu nikienda kwa watu wengine unaleta kidomodomo. Si uwe unakaa kimya!! Sasa nasemaje leo ni utake usitake.” Kauli ikakatika kisha ikasikika kelele mithili ya mikanda, Jesca alikuwa anachapwa maana nilimsikia akilia sana na hapo akasema neno.
“Bryan we niue tu lakini mi sitaki hayo mambo sitaki Bryan mbona unakuwa huniheshimu?? Eeh!! Bryan mi sitakiiiiii…..” alilalamika . Hapo kiherehere changu kikanivuta kuchungulia kama inawezekana. Nikatazama kushoto na kulia, hakuna mtu!! Nikausogelea mlango, uzuri waliacha taa inawaka, kupitia kitasa nikakuta kitundu kidogo, nikajivika ujasiri na kuchungulia kidogo, kisha nikatoka kwa kunyata hadi chumba cha mfanyakazi nikamkuta anakoroma nikafunga kwa njue ili akibanwa mkojo na kutaka kutoka nje asiweze kunifumania, nikarudi tena kuchungulia.
Jesca alikuwa akilazimisha kuishika chupi yake, Bryan akawa anaivuta huku akimchapa kwa kutumia ule mkanda. Jesca alikuwa amechakaa vibaya kutokana na kipigo.
“Bryan mwanao anakuangalia ujue, kuwa na aibu Bryan unachotaka kufanya si Mungu wala mwanao anakipenda…acha Bryan acha!!” Jesca alizidi kusisitiza. Bryan akageuza jicho akatazama kitanda cha mtoto wao ambaye alikuwa amelala. Kisha akapuuza. Hapo sasa akatumia nguvu zaidi!!
Mimi nilikuwa sijapata jibu, Jesca ni kipi anachokataa.
Nikaendelea kuangalia filamu hiyo ya kutisha. Mara Bryan akafanikiwa kuitoa nguo pekee iliyobaki akatika mwili wa Jesca, mara akaitoa bukta yake!! Ningekuwa Nadia wa miaka ile ningeweza kustuka lakini Nadia huyu wa kuitwa Mariam hata sikutetemeka nikaendelea kuangalia. Na baada ya sekunde kadhaa nikapata jibu na hapo nikageuka Nadia mtata.
Maneno ya Jesca sitayasahau hata kidogo, ni haya yaliyonibadilisha ghafla usiku ule na kujikuta katika chuki isiyosemekana na kisha kunisukumia kufanya jambo ambalo lilinirudisha shimoni. Shimo la mateso.
“Bryan haujalewa na una akili zako timamu, sina nguvu za kukabiliana na wewe na unanifanyia haya mbele ya mtoto wako, kama nikidhurika Bryan mwanao pekee ndo shahidi kuwa si mimi niliyetaka bali umenilazimisha kuniingilia kinyume na maumbile!! Ni yeye atakayekuhukumu.” Jesca alimaliza kisha akamwacha Bryan afanye lolote lile ambalo alikuwa anataka kulifanya.
Ningekuwa mpumbavu kushuhudia haya!! Nilikuwa nimekula na nimeshiba, sikumwogopa tena Bryan. Na ili nimkabili vyema nikambatiza jina nikamuita Desmund!!
Bryan bila haya akachukua mafuta fulani mkononi na kumsogelea Jesca!!
Nikafanya jaribio!!
Jaribio lililofanikiwa, nikakishusha kitasa, mlango ukafunguka!!
Ana kwa na ana mtu na mpenzi wake wakiwa uchi wa mnyama!!
“We Mariam!!..we…” kigugumizi kikamshika Bryan.
“Endelea unachotaka kufanya Desmund!!” nikamwita kwa jina hilo ili nijitie hasira zaidi.
“We Mariam unaota ama nani Desmund hapa.” Jesca alijiongelesha kama vile hakuna ambalo lilitaka kutokea.
Bryan akajaribu kunisogelea na hapo ndipo nikatambua kuwa tabu nilizopitia zilinikomaza, nilimrukia Bryan nikambamiza kwa kutumia goti langu katika korodani zake. Nikaiona sura ya Desmund machoni pake!! Jesca akanisogelea nikamsukuma huko akaanguka, sasa nikaanza kumchapa na ule mkanda, akajaribu kusimama nikamkanyaga teke la tumboni. Akaanguka chini akatoa kilio nikasikia sauti kama ya Desmund!! Nikazidi kucharuka nikachukua chupa ya soda akataka kujitetea nikawa nimeirusha tayari ikambamiza kichwani, akarudi chini na kuiangukia sakafu kisha akatulia.
“Anataka kukudhalilisha na unataka kumtetea…unaijua thamani yako Jesca?? Unaijua??” nilimuhoji akawa anatetemeka badala ya kunijibu.
“Sasa unasimama muda huu na unaondoka hapa leo hii hii…”
“Lakini ni usiku …”
“Shhhh!! Nasema Jesca unaondoka hapa ama niondoke mimi na usije ukasema uliwahi kukutana na mimi katika maisha yako. Wewe ni mwanamke, unatakiwa kujitambua…unataka kuuchekea huu upuuzi!! Mwanao ataiiga nini kwako, unamuandaa kuwa shoga?” nilimuuliza kwa ghadhabu kuu….Jesca akawa mpole.
“Vipi sasa chuo?”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Vyote vya shetani ni batili!! Bryan ni shetani mkubwa.” Nilimjibu!! Hapa sasa akanielewa.
“Si9 unazo pesa kidogo.”
“Zipo…”
“Tunaondoka hapa sasa hivi na mtoto. Aisga akiamka antakutana na mfanyakazi wake ama akifa jumla wazazi wake watakisia nini kilichomuua ama hao wanawake wake wajinga wajinga ambao huwa wanamtegemea mi*** yao watatoa taarifa kwa polisi.” Niliongea kwa ghadhabu sana na nilitukana, nadhani unanisamehe mwandishi maana nasema kilichotokea!!” Nadia aliniambia nikakubali kwa kichwa kisha akaendelea.
Ilikuwa saa sita usiku, nikambeba mtoto wa Jesca,tukatoka nje, jiji lilikuwa halijatulia bado. Tukapata taksi tukaondoka na kwenda kulala nyumba za kulala wageni huko Ubungo!!
Huu ukawa usiku wa namna yake mwandishi, usiku ambao niliamua kwa kauli moja tu, Mungu ananionyesha mabalaa haya, Mungu ananiepusha na kifo akiwa na maksudi nami, halafu ni kama nilikuwa nalaza damu.
Jesca alinieleza kuwa alikuwa na kiasi cha laki saba katika akaunti yake. Hii ilikuwa inatosha sana, ilikuwa ni wakati muafaka wa kumkabili Desmund ili nimpe salamu kutoka katika ile kuzimu ya baharini ambayo nilikuwa na kisha ikazushwa kuwa nimekufa.
Mzee Matata angeongoza mbio hizi za kunieleza ni nanji huyo alitaka kuniua kabla sijaonana na Desmund mume wangu, kila ambaye angenipa jibu hyakika angekuwa amenisaidia sana. Jesca na mwanaye walisinzia lakini mimi nilichelewa sana kulala.
Mwisho nikalala nikiwa na kauli mbiu, nipo hai ili Desmund akome!....mh!! we G wewe yaani ukinogewaga kusikiliza hata kula hunikumbushi au ndo unataka vidonda vya tumbo visimame hapa tuanze kukimbizana hospitali tena” alisema Nadia hapo nami nikakumbuka kuwa kulikuwa na chakula mbele yetu, nikakifunua.
Ewalaa!! Mapaja mawili ya kuku wa kienyeji, wali mweupe na vidikodiko vingine.
Nadia sahani yake na mimi yangu!!!
Kila mtu kwa mwendo wake akaanza kula!!
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment