Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

BLOOD DEAL - 5

 







    Simulizi : Blood Deal

    Sehemu  Ya Tano (5)





    ”Aliita kwa sauti ya juu sana iliyopelekea kila mmoja wao kumshangaa , hakuishia kuita tu bali alianza kupiga hatua ya kumfuata eneo alilokuwa amesimama

    “ unamfahamu huyu mwanangu ?”

    Mac Donald alimuuliza Poul mara baada ya kufika eneo hilo ,

    “ ndiyo , ni rafikiyangu sana ,tafadhali naomba umuachie nipo chini ya miguu yako “,

    alizungumza ,huku akipiga magoti ,uso wake tu uliashilia ukweli wa hali ya juu , japo aliufahamu uadui kati yake na baba wa binti huyo, lakini hakujali ,alichojali ni kumtetea Joan ,tayari alishamngundua MacDonald hakuwa Mtu wa msamaha kwa kiumbe yeyeto anayedriki kuivaimia ngome yake .CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Upande wa Mohammed alikuwa kimya kabisa , hakujua kama angeweza kutoka salama ndani ya ngome hiyo , yeye na MacDonald walikuwa maadui wa muda mrefu sana ,toka enzi za kutekwa kwa Poul miaka kadhaa iliyopita , na mara baada ya kumgundua mtu huyo aliamua kutomsaidia David zaidi ya kutoa pesa tu ! Alifanya hivyo kwa sababu David alikuwa akimuuzia madawa ya kulevya nchini kwake .

    “ okay sasa unataka nikusaidieje ?”

    “ nakuomba usimuue muache aende salama ,tambua tuna safari kwa leo usiku ?

    “ haina shida ,ila hawataondoka hapa hadi siye tufike Tanzania “

    kusikia Tanzania Mohammed alichanganyikiwa tayari alishangundua kipi kinaenda kutokea , alijihapiza kama atapata mwanya kidogo atoe taarifa kwa David .

    “ Tunaenda sote Poul “

    “hapana , huwezi ukaondoka kwenda huko , unatakiwa urudi nyumbani haraka iwezekanavyo “

    “ sirudi , nipo tayari kuyapoteza maisha yangu ,kuliko kurudi mikononi mwenu , hamfai kabisa ,nishangundua ub….”

    “shiiiiii!”

    Joan alikatizwa na Poul ,hakutaka mzozano , alichotaka yeye ni kwenda Tanzania mara moja , hasira aliyokuwa nayo dhidi ya David aliifahamu mwenyewe , alitamani kumuua kwa mkono wake , haraka iwezekanvyo . MacDonald hakutaka kupoteza muda alimchukua Mohammed na kumfungia ndani ya chumba, Joan alimpa nafasi ya kuongea na Poul , kila mtu alitoa machozi ya furaha , Poul alimshukuru sana Joan kwa moyo wake huo wa kujitolea kwa ajili yake , japo hakutoa pesa ,ama kitu chochote ,lakini kitendo cha yeye kusafiri hadi China ilikuwa ni moja ya upendo wa hali ya juu sana .

    ****





    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ****

    Ilikuwa ni taarifa yenye kupendeza masikioni mwa David alihisi ushindi wa hali ya juu sana , hakutaka kuamini kirahisi rahisi , alichaomu ni kumtafuta Deus

    “ kaka umesikia kilichotokea China?”

    “Ndiyo kaka nilikwambia Masoud ni mtu hatari sana “

    “ ujue siamini kabisa kama kauawa ?”

    “ Amini kaka ,leo ni kukesha bar tukibadili ,kilimanjaro, Tusker kwenda Ndovu ,kunywa mpaka ziishe kiwandani bwana mdogo ,ha ha ha! “

    Deus aliongea kwa mbwembwe, hakujua kama walikuwa ndani ya mtego , zile taarifa kutoka kwa Omar ziliyafurahisha masikoa yao , hakuna aliyeufahamu ukweli hilo lilibaki kuwa siri ya watu wawili tu .

    Omar na MacDonald walicheza mchezo wa hatari , mara baada ya kumuangamiza Masoud ,Omar alimpigia simu Deus kabla ya David akijifanya yeye ndiye Masoud ,jinsi alivyobarikiwa kuigiza sauti ilikuwa ni ngumu sana wao kuelewa ,kila kitu kilipangwa na wapi wangekutania ,hilo lilizidi kuwapa faraja sana watu hao ,

    “ Hapa ni kunywa kwenda mbele “

    “ umeona ?Nilikuwa na wasiwasi sana , maji y alifika kidevuni ,hapa nilikuwa na wazo la kutoroka tu ,maana kijana keshaufahamu ukweli wote “

    “ ha ha ha ha! Sifa ya mwanaume sio kukimbia sifa ya mwanaume ni kupambana tu , mlango ukifungwa wewe pitia hata dirishani , napo pakifungwa toboa hata ukuta ili mradi utoke “

    “ kweli bhana hapa sina wasiwasi kabisa , sasa naishi kama mfalme daaah!’

    “ hayo ndiyo maneno mjo….”

    Hakuweza kumalizia vyema ,sentensi yake baada yakungundua kuna mtu anawafuatili ,Deus hakujali sana aliendelea kuongea na kunywa ,lakini kila alipokutanisha macho na mtu huyo aliyekuwa meza ya tatu toka walipokaa wao ,mtu huyo alikwepesha macho ,hilo likaanza kumtia wasiwasi sana ,

    “ oyaaa yule fala namstukia “

    “ fala gani ?”

    “ meza ya tatu toka hapa ,hatulii nahisi anatuchukua maongezi , acha nimfuate “

    Deus alizungumza , huku akinyanyuka ,kabla ya kufika eneo hilo mwanamke aliyekuwa akimshuku naye alinyanyuka na kutoka ndani ya hoteli hiyo , kitendo hicho kilizidi kumchanganya David na rafiki yake , hata ile hali ya kulewa lewa ilianza kuwatoka , haraka walikimbia kuelekea nje rakini hawakufanikiwa kumkamata zaidi ya kupokea moshi wa pikipiki ,

    “ shitiii !” Tumfatilie “ papo hapo waliingia ndani ya gari la David ,lakini hakufanikiwa kumpata

    “sasa atakuwa nani ?”

    “ Hata mie sijui , mbaya zaidi ni mwanamke , anaonekana freshi , maana alivyoindoa pikipiki hiyo ,kama asingekuwa mtu wa mazoezi lazima angekula rami “

    “ kweli , sasa tufanyeje ?’

    “ Hakuna cha kufanya ,hapa turudi hotelini ,tukaendelee kuchafua meza , “

    “ sina hata hamu ujue ,acha nikupeleke kwako .”

    David alijikuta akipata woga wa hali ya juu , kitendo cha kufatiliwa ndani ya hoteli usiku huo kilizidi kumpa wasiwasi , alishajua kaupata ushindi sasa nani huyo tena? Japo walikuwa wawili yeye na rafiki yake lakini alijishuku mwenyewe , akili yake ilikosa utulivu kabisa, alimfikisha salama Deus nyumbani kwake kisha naye akaelekea kwake Pansias , akiwa njia aliiona ile pikipiki ikimfuatilia , hapo ndipo alipoaanza kuziamini hisia zake , kila alipopunguza mwendo ,pikipiki nayo ilipunguza mwendo , ikabidi asimama kwanza nayo ikasimama .

    “ Nani huyu ?”

    Alijiuliza peke yake ,lakini hakupata jibu , ghafla ilimpita kwa kasi ya ajabu ,naye aliifatilia ,lakini hakuweza kuipata , mwanamke huyo alikuwa akiendesha kwa kasi ya ajabu ,

    “ subiri nitampata tu , hawezi kunishinda demu mie ni mafia tena wa kimataifa nampa siku tatu .“

    Alizidi kuongea peke yake , dakika kumi alisimama mbele ya geti lake ,akiwa anasubiri lango kufunguliwa , kabla ya kuingiza ndani gari lake pikipiki ile ikapita tena karibu kabisa na gari lake , alihisi mkonjo ukitaka kumtoka , hata kulala ndani kwake aliogopa ,

    “ Yero funga geti ,siingizi gari ,mwambie mama ,nitampigia simu “,

    hakutaka tena kulala nyumbani hapo alichofanya ni kutafuta nyumba ya kulala wangeni , usiku mzima hakupata usingizi kabisa , akili yote ilikuwa kwa mwanamke huyo japo hakumfahamu .



    Alijihaisi mkosefu sana ndani ya nafsi yake , hakujua ni kwa njia ipi angeweza kulipa deni lililokuwa mbele yake , roho yake ilimuuma mkupita maelezo ,kila siku alijiona mkosefu ,hakutakiwa kuishi maisha mazuri na yenye furaha na amani bila kutoa msaada wake aliokuwa amejihapiza miaka kadhaa iliyopita , machozi na majonzi ndicho hasa kilikuwa chakula chake , japo alikuwa ameolewa tena na mwanaume tajiri huko Tarime ,lakini hakuufurahia utajiri huo kila alipokumbuka deni lake . Vero alizidi kugugumia kwa mawazo , kitu kilichomuumiza zaidi ni kumtelekeza Poul , hakujua yuko wapi , yuko hai ama la !

    “ Nastahili adhabu ,tena adhabu ya kuchinjwa kabisa , sikupaswa kumfanyia hivi Janiphar ,nimeishi kwake muda mrefu , alinilea kwa moyo mmoja tena we………….”.

    Alishindwa kuendelea kutokana na kuzidiwa na maumivu makali ndani ya mwili wake ,kila alipomkumbuka Janiphar alizidi kuumia zaidi , muda mwingine alitamani kwenda kaburini kuomba msamaha ,

    “ kwanini sikumweleza ukweli ? Ili hali kila kitu nilikifahamu ?, kweli natakiwa nifanye maamuzi ya lazima , naweza kumfurahisha huko aliko “,

    alizidi kuongea peke yake ndani ya chumba chake akiwa amesimama dirishani , huku mkononi akiwa ameshilia picha ya Janiphar wakiwa wote ,waliyokuwa wameipiga miaka kadhaa iliyopita , uso wake ulipabwa kwa machozi .CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alirudi taratibu hadi kitandani kwake , aliketi na kujiinamia , hakujua aanzie wapi , alipojitazama alikuwa mjamzito , hapo ndipo aliposhtuka.

    “ hapana lazima nifanye kitu , haiwezekani “,

    aliongea kwa hisia kali, na kunyanyuka , alivua khanga aliyokuwa amejifunga na kuvaa dela rangi ya kahawia , huku nywele zake zilizokuwa zimesukwa msuko wa twende kilioni alizifunga na kitambaa cha nguo hiyo , hakujua anakwenda wapi ,lakini moyo ulimtaka kutoka ndani ya nyumba hiyo ,

    “ Marwa natoka kidogo ,kaka yako akija mwambia nimekwenda saloon mara moja “

    “sawa shemu ,ila usichelewe “.

    Hakumjibu chochote zaidi ya kutoa tabasamu changa na kutoka nje , alitembea kama mgonjwa ,hakuja anaelekea wapi , lakini alizidi kusonga mbele , akiwa ndani ya mawazo ghafla alipitwa na msichana aliyeonekana mtu wa mazoezi sana , kwanza tembea yake tu ilifanani ,hapo ndipo moyo wake ulipomtuma kumsimamamisha msichana huyo ,

    “ samahani dada “,

    aliongea Vero huku akiongeza hatua kwani dada yule alikuwa amempita umbali kidogo

    “ dadaaaa !”,

    aliita kwa sauti ,kiasi hapo ndipo yule msichana alishtuka na kusimama bila kuangalia nyuma

    “ na …nashida nawewe kidogooooo”,

    alionngea huku akihema kutokana na hali yake ya ujauzito

    “ shida ngani ?”, Aliuliza kwa sauti ya kukwaruza kwaruza,

    “ aaaaah! Nikubwa kidogo sijui tunaweza tuakaenda kukaa sehemu nzuri ?”

    , Vero alisema huku akiutengeneza uso wake kwa tabasamu ,japo moyo haukuwa na tabasamu kabisa

    “ hapana nawahi seheemu muhimu nitafute kesho “

    , msichana yule ambaye hakumfahamu jina lake mara moja , aliongea huku akianza kuondoka ,hatua tatu alitupa kikaratasi mfano wa kitambulisho ,

    “ chukua hiyo ,kila kitu kitakuwa sawa “ ,

    ilibidi vero akiokote kile kitambulisho na kuanza kukisoma , macho yake yalipokea hali ya mshangao ,lakini hakutaka kujali alichotaka yeye ni kutekeleza adhima yake .

    “ Kama nilivyokueleza jana , kuna kazi naweza kukupatia ila siyo ngumu sana “

    “ mmmmh !”

    “ Nataka uelekee mwanza , kuna jamaa mmoja anaitwa David ………”,

    ilibidi Vero amsimlie kisa chote bila kubakisha hata chembe , muda mwingine alijikuta akitoa chozi ,

    “ huyo amekwisha nakuhakishia ushindi “,

    alijibu Ghati msichana aliyejiamini kupita maeleezo , kwanza alishawahi kuwa mwanajeshi kwa miaka mitatu ,kisha akafukuzwa kwa kosa la mauaji , kufukuzwa huko kulimpelekea yeye kuishi maisha hatarishi sana , Tarime nzima ilimfahamu alikuwa mtu mgomvi kupita maelezo , na muda mwingine alijihusisha katika ujambazi pindi alipofulia ,

    “ leo hii naanza kufanya mazoezi , hili jeshi la mtu mmoja , unachotakiwa wewe ni kunipa ramani yote , wapi anaishi ,na kipi anafanya “

    “ kwasasa sifahamu ila ukifika mwanza ,huwezi kumkosa ni mtu mmoja maarufu sana , ulizia ofisi za usafirishaji mtaa wa pamba, humkosi , ni mmnene kiasi , mfupi wa wastani na maji yakunde , anapenda sifa pia mnywaji mzuri wa pombe , aaah! Alikuwa anapendelea kwenda villa ni moja ya club maarufu sana hapo mwanza ,ipo kirumba , ama malaika beach huko ilemela , sehemu hizo humkosi , yeye anaishi Pansias soko jipya ,fanya hivyo mdogo wangu “

    “ mkubwa umemaliza , namchinja kama kuku ,kabla ya mtu yeyote hajatekeleza , ila naomba kitu kimoja unisaidie “

    “kipi?”

    “ nahitaji pikipiki aina ya Boxer “

    “ondoa shaka ,tukutane kesho kwa Matiku shop utachangua unayotaka “.

    Hivyo ndivyo ilivyokuwa , baada ya zoezi lote kukamilika , Ghati alisafiri hadi mwanza akiwa na pikipiki kisu mfukoni , hakuwa na kitu chochote , siku hiyo hiyo alianza kazi ya kumtafuta David kweli alibahatika kumpata na kuanza kumfuatilia bila yeye kujua chochote , Ghati alikuwa akiumia kila aliposikia maongezi kati ya marafiki hao wawili ,alipohakikisha amemaliza uchunguzi wake aliamua kujitokeza , hapo ndipo alipoamua kumfuatilia David hadi nyumbani kwake .





    ***

    “ Hatutakiwi kupoteza muda kila kitu nimeshakiweka sawa , nimeangalia hali ya usalama iko sawa , inatakiwa tuondoke mara moja “,

    MacDonald aliongea huku akipiga hatua kuwafuata wenzake , Poul kusikia maneno hayo hasira zake zilizidi kuongezeka , alitamani kupaa hadi Tanzania

    “ ondoka nami tafadhali “

    “Joan unatakiwa urudi nyumbani , huko hapakufai tafadhali nakuomba”,

    Poul aliongea huku akinyanyuka sehemu aliyokuwa ameketi , alianza kuingia chumbani kwake , lakini kabla hajaufikia mlango shati lake lilishikwa kwa nyuma ,hapo ndipo alipogeuka

    “ nakuomba tuondoke wote sitoweza kurudi Iran bila wewe , tambua nimetoka huko kwa ajili yako , leo hii nakupata tena unanikimbia ?”

    Joan aliongea kwa huzuni sana , sura yake tu iliashiria huzuni kubwa ilikuwa imeutawala uso wake

    “ na…nafahamu hilo Jo ,ila nakuomba uwe mvumilivu , nitarudi “

    “ hapanaaa !”,

    msichana yule alishindwa kuvumilia , aliona hatendewi haki , lakini Poul hakutaka kujali, yeye alitaka kufika Tanzania ili atekeleze kile alichokidhamiria kwa siku nyingi, maneno ya Joan kama angeyaendekeza yangesababisha mambo kuharibika , hakutaka tena kumsikiliza , alijitoa mikononi mwa msichana huyo na kuendelea na safari yake , Joan alijiona mkosefu , hakujua kwanini Poul alikuwa amebadilika hivyo , machozi na kamasi nyepesi nyepesi zilianza kutoka ,

    “ okay “,

    alitamka neno hilo na kuanza kuondoka eneo hilo akiwa anakimbia kutoka nje,

    “ kile kitoto kipo wapi ?’

    “ kimetoka sijui kilikoelekea “

    “ okaya hakituhusu , naombeni tutoke , Hassan hakikisha unamfungia huyo boya hadi nitakapokuambia”

    MacDonald alisema hayo huku , akiaendelea kukusanya baadhi ya vifaa alivyoona vinafaa katika kazi iliyoko mbele yake ,

    “ wewe utachukua nini ?’

    “ naomba hicho kisu chenye meno kwa nyuma “

    “ punguza utani Poul ,kisu? Cha nini , chukua hii bastola inakufaa “,

    aliongea huku mkono wake wa kushotao , ukinyoka kumpatia Poul siraha hiyo , lakini yeye aliendelea kukataa , alichotaka ni kisu peke yake ,

    “ okay , sawa uko tayari tuondoke ?”

    “ Ndiyo “

    , walianza kutembea kutoka ndani ya ngome hiyo , MacDonald mbele akiwa amebeba begi dogo la mgongoni aina ya Jansport rangi ya blue bahari , kichwa chake kikiwa kimenyolewa mtindo wa baroteli , akiwa amevaa jinsi yeusi pamoja na tsheti rangi nyeupe , hakuwa na tabia ya kuvaa viatu , ziadi alipendelea kuvaa sendozi , kwa upande wa Poul , yeye alivaa vazi la kijeshi kuanzia juu hadi chini , huku uso wake akiufunika kwa miwani ya jua .

    “Utaweza kuendesha ?” ,

    Macdonald alimuuliza Omar, akiwa anafungua mlango wa Toyota Landcruiser kutoka Japani , yenye rangi ya maziwa , gari aliyokuwa akiipenda kupita maelezo ,

    “ haina shinda , “

    “ inatakiwa tuwahi ndege ya saa tisa usiku , “

    “ kwa hapa ?’

    “ hapana , tunakwenda mjini Beijing “

    “ basi sawa “.

    Safari ya kuelekea Beijing ikaanza , hakuna aliyemuongelesha mwenzie , kila mtu alikuwa akiwaza yake ,hadi wanafika nje ya uwanja wa ndege wa Capital intanatinal Airport , uwanja mkubwa sana nchini China , kabla ya kushuka MaCDonald alimtafua mmoja wa vijana wake , alikuja kulichua gari hilo , na wao walielekea sehemu ya kupumzikia kabla ya kuingia ndani ya chumba cha kukaguliwa ,

    “ tumewahi kidogo ?’,

    Omar aliuliza huku , akifuta vumbi kiti hicho kwa mkono wake wa kushoto

    “ kiasi , bado kama dakika arobaini tu “.

    Dakika arobaini zilikatika mithili ya umeme wa Tanzania , hapo ndipo Poul alipoanza kuamini kama kweli alikuwa akielekea Tanzania , alianza kuhisi miguu ikikosa nguvu kabisa , hakujua kwanini hali hiyo ilikuwa ikimtokea , hata alipoanza kuingia kwenye chumba cha kukaguliwa alikuwa bado anatetemeka , sijui zilikuwa hasira ama nini ?

    “ Mbona hivyo ?’

    “ Hata siju “

    “ unatakiwa uwe jasili , ukianza kuleta woga hapo hakuna kitakachoenda kutokea , ni bora tukarudi na ukaendelee na mas…”

    “ shiti !, Ha..ha..hakuna..k..kit..u , kama ..hi..chooooo ! Lazima nimfurahishe baba yangu siwezi “.

    Poul alisema huku akiendelea kutetemeka , safari hii hadi midomo yake nayo ilikuwa ikitetemeka , haukuwa woga , bali zilikuwa ni hasira na hamasa za kufika salama Tanzania . Nusu saa ndege kutoka shirika la ndege dunia Delta ilianza kuseleleka taratibu ikizifuata njia zake , seleleka hiyo ilianza kuongezeka kila baada ya dakika na baadaye ilipaa na kuuacha uwanja huo wa China .

    ****

    Mohammed alizidi kuchanganyikiwa , yale maneno aliyoyasikia kutoka kwa MacDonald yalizidi kuivuruga akili yake , tayari taa nyekundu ilikuwa imeanza kuwaka ndani ya kichwa chake , hakuwa na uhakika kama kweli David atapona , sasa alikuwa na kazi moja tu, ya kumokoa ,ni kupiga simu ama kutuma ujumbe mfupi , kwa kuwa hakuwa amefungwa zaidi ya kufungiwa ndani ya chumba hicho , hakupata taabu kuichukua simu yake aina ya Tecno C8 , haraka bila kupoteza sekunde alikwenda upande wa majina na kulitafuta jina la David Tanzania, kisha alipiga na kuupeleka mkono wake wa kulia sikioni , dakika moja alibaki amesikiliza , lakini hakupata jibu lolote , aliitoa na kupiga tena safari hii aliweka sauti kabisa akawa anaitazama , ghafla ilikata bila kuita , akapiga tena , lakini mambo yalikuwa yaleyale ,CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “ ama niko sehemu mbaya ?” ,

    alijiuliza peke yake huku akinyanyuka sehemu hiyo , alitembea hadi usawa wa dirisha na kupiga lakini mambo yakawa yale yale , aliuma meno kwa hasira na kuambatanisha na mfyonzo wa hasira ,

    “ poa acha nimtafute upande wa WhatsApp”.

    Alifungua upande huo , lakini alipotaka kuandika pakamwandikia WhattsApp Erro , hapo ndipo alipozidi kuchanganyikiwa , hakuishia hapo alienda upande wa Facebook Messenger , napo hapakufunguka zaidi ya kupokea maneno Wainting for Network ,

    “ duuuuh!”

    Alisema neno hilo ,huku akiinama juu ya mbao ya dirisha , alihisi mwili wote kutweta kwa jasho , ilibidi avue kanzu yake na kubaki na bukta pekee ,

    “ eeeeh ! , Nadhani ujumbe wa kawaida utakwenda ?, acha nijaribu na huko “,

    alisema hayo huku anyosha mkono kuichukua simu yake , lakini kwa bahati mbaya aliishika vibaya ikamponyoka na kudondoka chini kwa mlio mkali sana , alibaki amepigwa bumbuwazi hakujua afanye kitu gani , alitumia kama dakika mbili akiwa katika hali hiyo hiyo , kisha alipata ujasiri wa kuichukua , alirudishia vitu vyake vizuri kisha aliiwasha , lakini ilipowaka tayari kioo chake kilikuwa kimevujia wino hivyo akawa amepata wakati mgumu sana , dakika tano baada ya kuwaka ilizima tena , alipoiwasha iliwaka lakini ikazima tema , ukawa kama mchezo wa kuwaka na kuzima .

    Nchini Tanzania mambo yalikwa magumu sana kwa upande wa mafia David , hakuweza kulala ndani ya Annex hoteli , hoteli iliyopo katikati ya jiji la mwanza karibu kabisa na stendi ya zamani ya mabasi yaendayo mikoani , japo alikuwa ndani ya hoteli kubwa na yenye hadhi , lakini alikuwa hana amani ndani ya moyo wake , msichana aliyemuona akimfuatilia kwa pikipiki masaa machache yaliyopita alizidi kuivuruga akili yake , kila aliposikia mlio uliofanania na ile pikipiki alishtuka,

    “ huyu ni nani ?”

    Alijiuliza peke yake akiwa kitandani , kitanda kikubwa kilichokuwa kimetandikwa kwa shuka nyeupe ,pamoja na mito yake nayo ilivikwa kava rangi hiyohiyo , kila alilojiuliza hakupata jibu , alibaki akiwaza na kuwazua bila kupata jibu , hadi inatimia saa tisa alikuwa macho , taratibu alinyanyuka na kuelekea chooni ,akiwa bado huko alisikia mlango wa chumba chake ukigongwa , mwanzo alihisi labda alisikia vibaya , lakini aliposikiliza vizuri aligundua ilikuwa kweli , hapo ndipo hofu ilipozidi kuongezeka

    “ nani huyu ?”,

    swali hilo lilitoka huku likiukatisha mkojo uliokuwa unatoka kwa fujo , kwa zile haraka na woga achilia mbali wasiwasi alijikuta akiumalizia mkojo huo kwenye boksa yake ,

    “ puuuuuh!” ,

    Alishusha pumzi ndefu na kuanza kutoka ndani ya choo hicho , huku akiwa anatetemeka ,

    “ nani ?”

    “ fungua “,

    sauti ya mwanamke ilipenya vyema ndani ya ngoma za masikio yake , hapo ndipo alipoyamini masikio yake na hisia zake, alitazama kulia na kushoto na kukutana na bastola yake , aliachia tabasamu huku akiwa anaikagua ,ghafla tabasamu hilo liliyeyuka na kurejewa tena na hali ya huzuni , baada ya kugundua kuwa haikuwa na risasi hata moja ,

    “ ngoo!, ngooo!”, mgongaji naye aliendelea kugonga huku aliomba mlango ufunguliwe .



    Ndege iliendelea kukata anga usiku huo , huku kila mtu ndani ya ndege hiyo akiwa kimya kabisa , wengine walikuwa wamesinzia na wengine walikuwa wakitafakari mambo tofauti tofauti ndani ya bongo zao , mtu aliyeonekana kuwaza zaidi alikuwa Poul , hakujua ni kipi kwanza angeweza kukiongea pindi atakapoutazama uso wa baba yake huyo mdogo , kila neno aliloweka akilini mwake aliona halina maana,

    “ nitaanzaje kuongea naye ama nisimuongeleshe , zaidi ya kumchana chana kmbavu zake ?”

    Alijiuliza peke yake , siyo swali la aina hiyo tu, bali aliwaza na kuwazua mambo mengi , kitu kilichomuuma zaidi ni kuuawa kwa baba yeke tena na mtu wa karibu kabisa , aliamini ni yeye pekee ndiye aliyeifahamu siri hiyo , je babu na bibi yake, achilia mbali shangazi yake Anginess , wote wakiyasikia maneno hayo watafanyaje ? Ulikuwa ni wakati mgumu sana kwake , lakini hakuwa na jinsi , ilikuwa ni lazima atekeleze kila alichokidhamiria , akiwa ndani ya mawazo hayo alijikuta akupitiwa na usingizi , usingizi uliokuwa mrefu kupita maelezo , zaidi ya masaa sita alikuwa amelala , alikuja kushtuka baada ya kufika Nairobi nchini Kenya .





    Taratibu zilipokamilika hapo Nairobi walianza safari ya kuimalizia safari yao , hapo ndipo kila mtu alizidi kupandwa na hasira dhidi ya David , nyuso zao tu ziliashiria hali hiyo , kila mtu alikunja makunyazi usoni , muda mwingine Poul aliweza kutoa machozi , walifika salama ndani ya uwanja wa ndege jiji mwanza majira ya saa tisa alasiri , wakitanguliwa na ndege toka commoro kama dakika kumi na tano tu . Baada ya taratibu zote kufanyika walitoka ndani ya uwanja huo wakiwa na hamasa ya kukutana na David ,

    “ Poul! “ ,

    ilikuwa ni sauti ya msichana iliyopenya vyema ndani ya ngoma za masikio ya Poul , aliyekuwa akifungua mlango wa kebu, iliyokuwa imepaki nje ya uwanja huo , aliigeuza haraka shingo yake na kukutana na sura ya msichana ambaye hakudhamiria kumuona sehemu hiyo , hakuweza kuyaamini macho yake , alibaki amepigwa na bumbuwazi huku wenzake wakiwa tayari wameshaingia ndani ya kebu hiyo ,

    “ Poul tunache…” ,

    MacDonald alisema huku akitoa kichwa chake ndani ya kebu hiyo , lakini naye alijikuta akistajabu , msichana aliyekuwa mbele yao alizidi kuwashangaza , hawakufahamu alifika saa ngapi eneo hilo , pia hawakutarajia kumuona kabisa nchini Tanzania ,

    “ Joan”,

    Poul aliita akiwa bado haamini kile kilichokuwa mbele yake ,

    “ binti ingia twende “

    ilibidi MacDonald akatishe mazungumzo hayo , ambayo yalikuwa yameanza kutokea kati ya marafiki hao ,

    “ kwanini umenifuata ?”

    Poul aliuza kwa lugha ya kichina ,kutompa nafasi dereva kebu , kuelewa kilichokuwa kikiendelea

    “ siyo mie , bali ni moyo “,

    Joan alisema kwa kujiamini na bila kujali , furaha aliyokuwa nayo aliifahamu peke yake .

    ****

    “ Sitaweza kukubali kirahisi hivi , lazima nifanye kitu cha haraka na chepesi zaidi ? ,

    Joan aliwaza ndani ya ubongo wake akiwa anaendelea kukimbia kutoka ndani ya ngome hiyo , muda mwingine aliweza kudondoka kutokana na urefu wa kiatu chake , lakini alinyanyuka na kuendelea na safari yake , kichwani mwake alidhamiria kufika Tanzania kwa namna yeyote , toka azaliwe hakuwahi kudhuru nchi yeyote ya Afrika zaidi ya China , Iran na Oman nyumbani kwa mama yake . Kitendo cha yeye kutaka kwenda Tanzania kilikuwa ni cha ajabu sana , lakini alijihapiza kufika nchi hiyo , bahati ilikuwa yake mara baada ya kutokea barabarani usiku huo alibahatika kupata treni iliyokuwa ikielekea Beijing usiku huo , alipanda na kuketi kimya , majira ya saa saba kasorobo, saa za huko alifika mjini humo , alishuka na kutafuta moja ya benki , alitoa kiasi kikubwa cha pesa alichodhani kitamtosha kwa safari yake , alichukua usafiri uliompeleka uwanja wa ndege wa Capital Intarnational Airport , bahati nzuri alibahatisha kupata ndege iliyokuwa ikielekea Commoro moja ya nchi inayopatikana Afrika .

    Baada ya kufuata taratibu zote safari ya kuelekea Commoro ilianza akiwa na tumaini la kufika Tanzania, iwe isiwe!

    “ Unaelekea wapi kaka ?” ,

    Joan alimuuliza abiria aliyekuwa ameketi naye siti moja , kwa lugha ya kingereza

    “ Nairobi , ila nikifika Commoro nitabadirisha ndege “

    “ aaaah ! Na Tanzania je ni mbali ukiwa hapo Commoro ?”

    “ Hahahaha! Tanzania iko ukanda wa Afrika mashariki ,ni moja ya nchi jirani na Kenya ambako ndiko naelekea “

    “wewe si umesema unaelekea Nairobi ?”

    “ Dada Nairobi ni mji mkuu wa Kenya “CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “ okay , sawa nimekuelewa ,je unaweza kunipeleka Tanzania ?, nitakulipa “

    “ Hapana , ila nitakusaidia kufika huko ,tukifika Kenya ,kwani unaelekea mkoa ngani ukifika Tanzania ?” , aliuliza kijana huyo aliyekuwa bize na simu yake ,japo alikuwa akizungumza na Joan

    “ aaah ! ni…ni ..Munza , yaani ule mji wenye ziwa Victoria “

    “ okay sio Munza ni Mwanza , napafahamu ,niliwahi kwenda huko miaka mitatu iliyopita ,kabla ya kuhamia China , ujue mie ni raia wa Kenya ila napenda sana kudhuru nchi mbalimbali duniani “

    “nashukuru kwa msaada wako , me naitwa Shamimu raia wa Iraq , sijui unaitwa nani ?

    Ilibidi Joan adanganye ,maana alikuwa bado na hofu ya kukamatwa

    “ naitwa Daniel Onyango “.

    Hapo ndipo urafiki wa watu hao ulipoanzia , waliendelea kuzungumza mengi sana , hakuna aliyeweza kulala ,hadi wanafika Commoro , kisha safari ya kuelekea Nairobi ilianza kupitia shirika hilo hilo .

    “ sasa ukifika Mwanza utaenda wapi ?

    “ Kuna mjomba wangu ananipokea “

    “ usahawasiliana naye ?”

    “ Ndiyo “.

    Japo Joan alijua ni uongo mtupu , lakini hakutakiwa kuweka wazi mambo yake , moyoni alijipa tumaini la kukutana na Poul , kweli walipofika Nairobi Daniel alifanya kama alivyoahidi na Joan akaanza safari yake ya kuelekea jijini mwanza nchini Tanzania , nchi amabayao hakuwahi kuiona na hata kuikanyanga toka azaliwe , kila kitu kilikuwa kigeni sana , ila ile hali yake ya uongeaji kiasi ilimsaidi . alishuka ndani ya uwanja huo hakutaka kutoka nje alihakikisha anabaki ndani ili kumsubili Poul , tayari alikuwa ameshaulizia kama kulikuwa kuna ndege inayotokea China , japo hakuwa na uhakika lakini alijiaminisha ndani ya moyo wake uwepo wa Poul eneo hilo muda mfupi , akiwa anashangaa shangaa mazingira ya hapo , ndege kubwa ilitua ndani ya uwanja huo , hapo ndipo alipozidisha umakini mara baada ya abiria kuanza kutoka .

    Moyo wake ulitaka kupasuka mara baada ya kumuona Poul aliwa ameongozana na wanaume wawili , hakutaka kujitokeza kwanza , alihakikisha wanampita kama hatua kadhaa ,ndipo naye alianza kuwafuata na kabla ya wao kuondoka alimuita Poul .

    ****

    Bado alikuwa haamini kama kweli bastola yake haikuwa na risasi , aliitzama zaidi ya mara tatu ,lakini hali ilikuwa ni ile ile , bastola haikuwa na risasi ,

    “ siwezi kufa kifala namna hii , cha msingi ni kutumia akili za kuzaliwa “

    . Aliwaza ndani ya akili yake huku akizunguka ndani ya chumba hicho ,taulo kiunoni ,

    “ hutaki kufunguaa”

    “ kwani wewe nani hasa ?”

    , David aliuliza huku akipiga hatua kuufuata mlango , lakini kabla ya kufungua aliinama kidogo na kuchungulia nje ya mlango huo kupitia kitundu cha funguo , hakufanikiwa kuona chochote ,

    “acha nimkomeshe “ ,

    aliwaza hayo huku akishika funguo na kuizungusha kwa haraka sana , mkono mwingine ulishika komeo , mlango ulipoanza kunfuguka ilibidi aufuate kule unakoelekea ,

    “ jamani mpenzii umenisimamisha muda mrefu hapo nje “ ,

    sauti ya mwanamke aliyeonekana kulewa kupita maelezo ,ilipenya vyema ndani ya masikio yake, alihisi kutua kitu flani ndani ya moyo wake , alianza kutoka nyuma ya mlango huo , alitumia kama dakika mbili kumtazama mwanamke aliyekuwa amelala juu ya kochi ,huku akianza kukoroma ,

    “ dada” aliita lakini hakupata ushirikiano ,

    “ watu wengine bagi kweli ,tena zile za Tarime , pombe gani hizi hadi unapotea chumba ? Wanawake wa namna hii hawafai kabisa “

    , maneno hayo aliyawaza huku akianza kupiga hatua za kumfuata mwanamke huyo ,

    “ oyaaa! Umekosea room , amka usepe “

    “acha kunizingua , mie nausingizi niache Maiko , ushanikera , niache mbwa wewe”

    , mwanamke huyo aliongea maneno hayo, huku akiwa bado amelala , David kuona hivyo alianza kumvuta kwa nguvu akimtoa nje , hakujali kelele za mwanamke huyo .

    “ Haaaa! Mijitu mingine haifai kabisa “,

    hakutaka tena kulala ,kila kitu kilikuwa kimeharibika , alielekea bafuni alioga na baada ya kuvaa alitoka ndani ya hoteli hiyo ,

    “ bora niende Villa nikapoteze mawazo “

    , huo ndio uamzi aliouamua , safari ya kuelekea Villa ikaanza, alipitia barabara ya Pamba road , alipofika makutano ya barabara ya kutoka nyegezi alikata kulia na kuikamata barabara ya Kinyyata road , alinyosha moja kwa moja hadi Mission , kisha alikunja kushoto kwake , kwa kuwa ilikuwa usiku na mji wa Mwanza huwa hauna foleni sana alijiuta akitumia dakika saba tu kufika hapo , alishuka na kuingia ndani ya Club hiyo, hadi kunapambazuka alikuwa bado yumo humo humo .

    “ Sihitaji usumbufu naomba nipumzike , mtu yeyote akija mwambie sipo “

    “ lakini baba Rebecca unatatizo gani , jana hujalala nyumbani ,nakuliza hunipi jibu ,nini tatizo mpenzi ?”

    , aliongea kwa huzuni mke wake , akiwa amekaa pembeni na mume wake , macho yake makubwa kiasi yalikuwa akimtazama mwanaume huyo

    “ sina tatizoa sema nimechoaka “

    “ sawa mpenzi , lakini samahani kwa maswali , hebu niambie jana ulikuwa na tatizo gani?”

    “ Nimekwambia sitaki usumbufu ,mbona hunielewi wewe Malaya ,hebu toka hapa”

    , aliongea kwa ukali, akitaka kumpiga mke wake , naye hakuwa na jinsi ilibidi atoke ndani ya chumba hicho , siku hiyo alishinda amelala hakutoka kabisa nyumbani hapo , siku iliyofuata ndipo alipoelekea ofisini kwake.,

    “ griiii,griiii griiii” ,

    ulikuwa ni mlio wa simu yake ya mezani , ikiita , haraka bila kuchelewa aliipoke

    “ nipo Tanzania naomba tuonane “

    “ wewe nani ?”

    “mie Masoud “

    “ ha ha ha ha !Kaka ulifika salama ?”

    “ Namshukuru mungu niko salama kabisa , mambo yalikwenda vyema kabisa “

    “ safi sana , sasa naomba uje ofisini kwangu , pia kuna kazi nyigine nataka kukupa , ushakuwa ndugu yangu , kwa hili ulilolifanya daaah! Unastahili pongezi sana , unajua huyo kijana alikuwa ananichanganya sana “,





    David aliongea bila kujua kama maneno hayo yalikuwa akipenya vizuri ndani ya masikio ya Poul , Joan na MacDonald , Omar alikuwa anaendelea kuigiza sauti ya Masoud na kujifanya yeye ndiye .

    “ Sasa tunaondoka “

    “ ndiyo , ila huyu binti abaki “

    , Joan hakuwa mbishi , alirudi kitandani na kuendelea kulala , dakika tatu walikuwa nje ya mwanza hoteli , hoteli waliyokuwa wamefikia jana yake , Poul aliyatazama mazingira hayo na kujikuta akitoa chozi , picha na kumbukumbu mbalimbali zilianza kupita ndani ya kichwa mfano maji ndani ya mto , alimkumbuka sana baba yake na mama yake waliokuwa wakipendelea kumleta eneo hilo nyakati za sikukuu kabla ya kumpeleka Salma Cone , sehemu pendwa kwa watoto na wakazi wa jiji hilo.

    “ tupeleke pamba karibu kabisa na posta ya zamani “,

    Poul alizungumza na dereva kebu , aliyekuwa amepaki mbele ya hoteli hiyo , kwa lugha ya Kiswahili ,

    “ msimbazi mjomba “

    “ haina shida “

    Wote watatu waliingia ndani ya kebu hiyo na safari ya kuelekea ofisi kwa David ikaanza , dakika saba kebu hiyo ilifunga breki mbele ya jingo hilo refu , na wote walishuka kisha walianza kupandisha ngazi .

    “ habari yako dada ?” ,

    Omar alimsalimia dada wa mapokezi ,kwa Kiswahili kibovu ,

    “ nzuri , sijui nikusaidie nini ?” ,

    alizungumza huku macho yake , yakiendelea kutazama kioo cha talakilishi ndogo ya mezani aina ya Dell,

    “ sijui mkurugezi tumemkuta ?”

    “ yupo , nimweleze nani ?”

    “ mwmbie Masoud”.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Papo hapo msichana yule aliyekuwa na sura pana yenye macho makubwa kiasi , huku rangi ya ngozi yake ikiwa nyeusi , alibonyeza namba flani katika simu yake ya mezani na baada ya dakika moja simu iliita

    “ kuna wageni wako hapa bosi “

    “toka wapi ?”

    , upande wa pili uliuza

    “ aaaah ! toka….toka ….sijui ila anaitwa Masoud “

    “ okay mwambie aingie “ ,

    alikata simu na kuwapatia taarifa hiyo , kila mtu alifurahi , Poul alihisi kuchanganyikiwa zaidi , alitamani akimbie hadi ofisini humo afike na kumtoboa na kisu kilichokuwa mfukoni mwa suruali yake ,

    “ mnaweza mkaenda , nyosheni na hili korido , mtakata kushoto chumba cha kwanza mkono wa kulia “

    “ ahsante sana !!!” ,

    Waliitikia kwa pamoja kisha walianza kuongoza njia , walipofika mbele ya chumba hicho kila mtu alisimama kwanza , na kutazamana machoni ,

    “ Poul ingia “,

    MacDonald aliongea na Poul aliitikia agizo hilo , kwa mkono wake wa kulia alishika komeo na kusukuma mlango huo nao ukafungua ,

    “ good day { siku njema }”,

    poul aliongea neno hilo mara baada kuingia ndani ya chumba hicho , sauti hiyo ilimfanya David ashtuke , aliunyanyua uso wake na kukutana ana kwa ana na kijana huyo aliyedhania kuwa alishakufa , alishindwa kuongea , kusimama na kufanya chochote zaidi ya kuendelea kukaa , huku akiwa anamtazama kwa macho ya wasiwasi

    “ pokea salamu kutoka kwa kaka yako Emanuel na Shemeji yako Janifahar , hawajambo “ ,

    alizidi kuongea , akiwa amemtazama machoni , alishindwa kuvumilia zaidi papo hapo alichomoa kisu chake kwa haraka sana alikichana kiganja chake,cha mkono wa kulia, mkono uliokuwa umeegemezwa juu ya meza , kabla haja mchoma cha pili , MacDonald aliingia akiambatana na Omar,

    “ Poul stop, stop we need to speak with him……….{ Poul acha , acha tunatakiwa kuongea naye ….}”,

    aliongea huku akimkamata Poul na kumtoa eneo hilo ,

    “ hapanaaaaa!Natakiwa nimuee kabla ya ……”

    Poul aliongea huku akilia , kitendo cha kukatishwa adhima yake kilimkera sana , tayari moyo wake ulishawaka kwa kazi hiyo ,

    “ huwezi kufanya mapema kiasi hicho nisikiliz e mwanangu “,

    aliongea huku akiwa amemshikilia , wakiwa bado wanarumbana , ghafla mlango ulifunguliwa , mtu aliyekuwa amevaa vazi refu rangi nyekundu juu hadi chini alisimama mbele yao , huku akiwatazama mmoja baada ya mwingine , mkononi akiwa ameshika bastola.



    Kila kitu kilikuwa kimekamilika ,kama uchunguzi alikuwa ameshaupata , kilichokuwa kimebaki ni kutekeleza kazi iliyokuwa mbele yake , alikuwa na masaa maachache tu , mbele yake kuikamilisha kazi hiyo , usiku alioamua kujitokeza ndio ulikuwa wa mwisho kwake , alipanga siku inayofuata ilikuwa ni kukamilisha kazi hiyo ,kisha angerejea Tarime . Ghati aliendelea kuzunguka na kumfuatilia David ,kila alikokwenda , alikuwa na uzoefu mzuri sana wa kuendesha pikipiki , muda mwingine alijishangaa hadi yeye mwenyewe jinsi alivyokuwa akiiendesha pikipiki hiyo na kumpita David .

    “ Ha ha ha ha! Huyu mbona mtoto sana , ndo anajiita mafia , ?

    Ghati aliwaza peke yake akiwa anamtazama David alivyokuwa anahaha ,

    “ acha nimuache kesho nitampeleka ahera mbuzi wa sikukuu huyu “

    , ilibidi aondoke na kurudi sehemu aliyofikia , huku kichwani mwake akilala na wazo la kumuangamiza David ,

    “ mkubwa kila kitu kipo sawa , na kesho majira ya saa nne kamili asubuhi nitamalizia kazi yako , na jioni nitakuwa Tarime “

    “ Ghati acha uongo , “

    “ siye ni watani ? Sipendi mtu asiyeamini ninachokisema kipo sahihi kabisa , naomba unielewe “

    “ nitashukuru sana “

    “ pamoja nikutakie usiku mwema , kiongozi “

    , Ghati alikata simu , aliichomeka chini ya mto , kisha alielekea bafuni , alipotoka alivaa, kisha alielekea moja kwa moja sehemmu ya chakula , ndani ya Kitwima hoteli , hoteli iliyopo barabara ya rufiji , mkabara na soko la mirongo jijini mwanza ,alijikuta akitumia zaidi ya dakika sabini kukumaliza chakula hicho , kisha alirejea ndani ya chumba chake kwa kuumalizia usiku uliokuwa umebakia .

    Toka afike mwanza hakuwahi kuvaa mavazi ya kike hata siku moja , ila siku hiyo alivaa mavazi hayo , alihakikisha amependeza kupita maelezo , ile hali yake ya kiume ume siku hiyo haikuwepo , baada ya kumaliza kujiandaa , alichukua kisu chake na bastola vyote alivichomeka ndani ya mkoba , akiambatanisha na mavazi mekundu mfano yale ya wacheza kufuu ,

    “ hapa lazima niingie tu “,

    aliwaza huku akikikagua kitambulisho alichokuwa amekichongesha kikifanania na vile vya wafanyakazi mojawapo kati ya kampuni alizokuwa akizimiliki David ,

    “ halooo ! Miss habari za leo “,,

    Ghati alimsalimia dada wa mapokezi ,mara baada ya kufika ofisini hapo majira ya saa tatu na dakika arobaini asubuhi , salamu hiyo ilitoka kwa sauti ya ushawishi pamoja na tabasamu usoni mwake ,

    “ nzuri “ ,

    alijibu kwa mkato msichana huyo, huku akiendelea na shughuli zake ,

    “ naitwa Isabella, katibu mwenezi ,Imaraseko supermarket, nashida ya kuonana na mkurungezi “

    , aliongea huku akimkabidhi kitabulisho hicho ,

    “ aaah ! Una miadi naye ?”

    “ Hapana ni shida ya dharula , nisaidie tafadhali “

    “ lakini anawageni , subiri hapo , wakitoka utaingia “

    “mpig…”, alikatishwa ,

    “kila ofisi ina utaratibu wake , naomba ufuate “.

    Ilibidi Ghati afuate mashariti , aliviendea vitu vilivyokuwa mkono wa kushoto na kuketi , dakika tatu alinyanyuka ,

    “ dada unaweza ukanionyesha msalani ,na…”

    “ okay nyosha moja kwa moja usikate “

    “ahsante “

    ,alianza kuondoka eneo hilo, kichwani akipanga kuingia ndani ya ofisi ya David , kabla hajafika uwani alikutana na mmoja wa mfanyakazi ,

    “ naulizia ofisi ya mkurugezi nimepotea “

    , aliongea bila kusalimia,

    “okay , rudi nyuma ukate mkono wa kushoto , chumba cha kwanza “

    “ahsante “,

    alijihisi ushindi wa hali ya juu , alichokifanya ni kuingia uwani ,alibadili nguo kwa haraka sana , kisha alitoka kwa tahadhali sana , alinyosha moja kwa moja hadi mbele ya ofisi hiyo, akiwa na bastola pamoja na kisu ,kilichokuwa kiunoni , hakutaka kupoteza muda alifungua mlango, na kuingia ,macho yake yalipokelewa na zaidi ya watu wawili , waliokuwa wanazozana .

    *****



    Poul hakutaka kukubaliana na maneno ya MacDonald , aliona hafanyiwi haki , kwa jinsi alivyokuwa amewaka kwa hasira ilikuwa ni ngumu sana kumuelewesha ,

    “ nyie mbona mnazozana ndani ya ofisi za watu ?,

    Mtu aliyekuwa amesimama na bastola aliongea kwa lugha ya Kiswahili, akiwa anamtazama mmoja baada ya mwingine

    “Poul nisa..mehe mwa..nangu …ni..nisam..ehe ta…”

    “ funga kopo lako haraka , sihitaji ngojera zako hapa “,

    mtu yule aliongea huku alivua kitambaa alichokuwa amejifunika usoni , lahaulla ! Alikuwa Ghati , alinyosha mkono wake sawasawa na uso wa David , mkono uliokuwa umeshikilia bastola , tayari kwa kumuua , CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “ sina muda wa kupoteza , rest in peace {pumzika kwa amani }paaaa!”

    Maneno hayo aliyasindikiza kwa risasi , lakini risasi hiyo ilipiga talakilishi , mara baada ya mkono huo kupigwa teke na Omar ,

    “ uyataka faya nini? This is our person , who send you?{ Huyu ni mtu wetu , nani kakutuma ?}, aliuliza Omar kwa Kiswahili kibovu , akiwa amemkamata vyema Ghati ,

    “ hutakiwi kujua , ila tabua , mtu huyu hatakiwi kuishi , natekeleza agizo kutoka kwa boss “

    “ boss! Who is your boss?[boss! Nani boss wako] ?”,

    Poul naye aliyaingilia mazungumzo hayo , muda wote huo David alikuwa kimya ,kabisa ,moyoni aliomba miujiza itokee , ila kwa dalili zilizokuwepo mbele yake , ilikuwa ni ngumu sana kutokea hilo , mwili wote ulitweta kwa jasho , hakuwa akisikia hata maumivu ya kuchanwa kiganja chake , japo damu zilikuwa zikiendelea kutoka ,

    “ binti usipousema ukweli utakufa “,

    MacDonald aliongea huku akimuachia Poul na kumsogelea Ghati , alimkaba shingo yake kwa mkono wa kushoto , akiwa ameyatoa macho , mdomo wa bastola ukiwa usoni kwa Ghati,

    “ semaaa”

    “ sawa niachie “,

    japo alikuwa amekabwa kwa nguvu lakini , hakudiriki kutetemeka , ilibidi asimulie nusu ya kisa , Poul kusikia jina la Vero , alijikuta akitoa chozi, picha na kumbukumbu zote zilirejea, alimkumbuka msichana huyo aliyekuwa akimlea vizuri , akimpeleka shule na kumfuata , akimchekesha pindi alipokwazika ,kila kitu kilirejea ndani ya akili yake .

    “ Baba muachie , ni mtu mzuri sana “

    “ kweli ?’

    “ Ndiyo “

    Ghati alipoachiwa alimfuata David , alimpiga ngumi ya kifua hali iliyopelekea kuinama kidogo , kwa jinsi alivyokuwa amenywea hata hakupata wazo la kuchukua bastola yake , alikuwa mdogo mithili ya pilitoni , kitu alichokuwa akikiwaza ni miujiza tu , alitamani kupiga kelele lakini hakuweza,

    “ anatakiwa apelekwe sehemu nzuri kwa mahojiano zaidi “,

    Ghati aliongea , huku akiwatazama wenzake , mawazo hayo yalionekana kufaa sana , ilibidi wampe somo la kujikaza pindi atakapotoka nje , na kama angeleta usumbufu kifo kilikuwa halali yake , hakuwa na ubishi alijikaza na kuanza kuongoza njia mbele akitanguliwa na Omar pamoja na Ghati aliyekuwa bado na mavazi yake yale yale mekundu , hakujali kama angeweza kushitukiwa , kisha alifuta Poul na nyuma kabisa alikuwa MacDonald ,

    “ Linda nakuja “

    “ sawa boss “,

    msichana wa mapokezi alijibu huku akiwa amemkazia macho boss wake huyo , hakujua kipi kilikuwa kinaendelea , hadi wanatoka nje ya jengo hilo hakuna mtu aliye fahamu , japo walinzi toka shirika la Kk security walikuwa eneo hilo ,lakini hawakufahamu nini kilikuwa kikiendelea .

    Baada ya kumuingiza ndani ya gari lake aina ya Prando hapo ndipo walipomfunga uso kwa kitambaa cheusi safari ya kuelekea Geita ndani ya pori la matete ilianza , Omar ndiye alikuwa dereva , aliendesha gari hadi kigongo feri ,kwa muongozo wa Ghati pamoja na Poul , akipitia barabara ya Shinyanga , walifuata utaratibu wote hapo kivukoni kisha waliendelea na safari yao .

    Majira ya saa kumi jioni walikuwa ndani ya pori hilo ,walimshusha na kuanza kumvuta kuingia ndani zaidi ,

    “unachotakiwa ni kuongea ukweli , ukifanya hivyo utakuwa umejiwekea uwezekano wa wewe kuendelea kuishi “,

    Poul aliongea huku akimchanja chanja na ncha ya kisu chake , mgongoni, chanja chanja hiyo ilipelekea shati lake uchanika chanika , japo alikuwa akimuomba msamaha ,lakini Poul hakuwa na roho ya kutoa msamaha huo ,

    “ mpe hii karatasi aandike sababu ya kuua”,

    MacDonald aliongea huku akitoa kipande cha karatasi na kumpatia Poul ,naye alikifikisha moja kwa moja kwa David ,

    “ andika ukweli wote , ukipindisha , kifo halali yako, pia orodhesha mali zote na unirithishe mimi “

    “zote !”

    “ Ndiyo ?”

    “ Ha..ha..hapana mwanagu ,mie nitaishije lakini ?”

    “ kwani mali zako? , Jasho la baba yangu ,ama hufahamu hilo paaaa!”

    Aliongea kwa hasira , kitendo cha David kukataa kumrithisha mali ,kilimkera sana , ilibidi ampinge makofi ya usoni ili kumuweka sawa , makofi hayo hayakubadili nia ya David aliendelea kukataa tu ! Hapo ndipo msichana Ghati alipopandwa na hasira alimsukuma Poul na kumsogerea David ,

    “ Omar nipatie huo mkasi , anaona tunacheka .“

    Baada ya kupewa alianza kumbana kila sehemu ya mwili , muda mwingine alidriki kutoka na kiasi kidogo cha nyama , japo aliumia na kutoa machozi lakini msimamo ulikiuwa ule ule , mali hakutaka kuachia ,

    “ sasa nakufanyia kitu mbaya , nakuoa meno bila ganzi “,

    MacDonald aliongea kwa kichina , lugha ambayo ilikuwa ngeni kwa David na Ghati pekee yao , alimtoa Ghati na kumpiga ngumi moja tu iliyopelekea meno yake mawili ya mbele kutoka , yakiacha damu zikichuruzika ,

    “ bado unagoma ?’

    “ Naaaandikaaaa”,

    aliongea kwa maumivu makali sana, ilibidi akubali , hali aliyokuwa nayo ilimtisha , tayari alishatambua nia ya watu hao , kukataa kwake kungepelekea hata kifo .

    *****

    “ Huu ndi…o.. ukw…eliiiiii, na..kuomba…usiniue …mwana..ngu”,

    alizungumza kwa taabu sana ,kutokana na maumivu makali aliyokuwa akiyasikia , Poul alishindwa kuvumilia pindi alipoyasoma maamdishi hayo ,ilikuwa kama katoneshwa donda alilia sana ,

    “ ahsante , kwa ukweli wako ila tambua sitakuacha hai “

    “ ha.pa..na .. nisa..mehe ..nai..acha ..fami..lia…yang..na..nani?”

    “ Hahahaha! Ulipowaua wazazi wangu ulitegemea nitaishi na nani ?, Unastahili kufa, nitawasaidia mie “,

    Poul hakutaka tena kuongea alianza kumchana chana kila sehemu ya mwili , jinsi alivyokuwa amevimba kwa hasira na uchungu ilikuwa ngumu mtu yeyote kumkataza , hakuishia kumchana chana tu, alianza kumkata kidole kimoja baada ya kingine , David alilia kama mtoto mdogo , maumivu aliyokuwa akiyasikia aliyafahamu mwenye ,

    “ hadi unakufa nakukata kiungo kimoja baada ya kingine , jinsi unavyoumia na kuhangahika kwa maumivu makali na machungu tambua hata wao walihangaika vivyo , waliumia vivyo “ ,

    aliongea huku akihamia vidole vya miguuni nako alikata kimoja baada ya kingine kwa kutumia kisu chake , muda wote huo wenzake walikuwa kimya wakikitazama kitendo hicho , hakuna aliyeweza kumuonea huruma David ,

    “ sasa zamu ya kukata masikio , pua na mdomo “

    “ boraaa un..iue..tu ..kuliko ..ku.ni..fa..ny..ia..hiviiiiiiiiiiiii”

    “ hahahah !” Poul alicheka kwa dharau iliyochanganyikana na hasira , hakujali maneno yake alimkata sikio la kushoto na kuliweka pembeni , na la kushoto alifanya vivyo hivyo , alihakikisha kila kiungo amekitoa katika mwili huo ,

    “ hebu mmalizie tuondoke “

    “ sawa “ ,

    papo hapo alimchoma kisu cha tumboni kama mara tatu , akichoma na kuchomoa , hakuna kilichosika zaidi ya kilio cha maumivu kisha David alipoteza maisha papo hapo ,

    “ tunamzika ?”

    “ Hana haja ya kuzikwa , baba yangu alilala barabarani usiku mzima akiwa amekufa , atakuwa chakula cha fisi , tuondokeni “.

    Poul alihisi kutua kitu flani kizito ndani ya mwili wake , alijihisi mwepesi kabisa , kitu kilichokuwepo mbele yake ni kufikisha ujumbe huo kwa babu na bibi yake ambao sasa walikuwa wakiishi katika nyumba ya wazazi wake hapo Bugando . Walisafiri hadi mwanza jioni hiyo hiyo , majira ya saa nne usiku walikuwa kivuko cha kigongo feri , walisubili kwa muda wa dakika kumi na tano , ndipo feri hiyo ilifika , waliingiza gari lao ambalo lilikuwa la marehemu David , na baada ya dakika kumi na tano walikuwa upande wa pili , dakika arobaini na tano tayari walikuwa ndani ya jiji la mwanza ,

    “ sasa mie nasepa “CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “ wapi tena ?”

    “ Kitwima hoteli , kesho asubuhi ya saa kumi na moja naingia Tarime “

    “ hapana dada Ghati , naomba kesho twende sote nyumbani kwetu aghalau ukawaone wazee wangu ,nadhani watafurahi sana kukuona , na utanisaidia kuwaelewesha “

    “ nini haraka , ila kwa kuwa umeongea wewe nitakuwa bega kwa bega nawe “ ,

    yalikuwa maongezi kati Vero na Poul wakiwa nje ya mwanza hoteli usiku huo .Vero aliagana nao kisha akaondoka , kwa miadi ya kukutana siku ilifuata .

    ****





    “Khogoo! Khogoo!Khogooo!” ,

    Ilikuwa ni sauti ya geti likigongwa , sauti hiyo haikufika mapema masikioni pa wakazi wa nyumba hiyo , kutokana na hali ya mvua ya rasha rasha ,iliyokuwa ikinyesha , asubuhi hiyo , wanaume watatu na mwanamke mmoja walikuwa wamesimama mbele ya geti hilo waliendelea kugonga bila kuchoka ,

    “ bibi nasikia kuna mtu anagonga geti “

    “ nenda kamtazame , yawezekana atakuwa shangazi yako , jana alisema anakuja “,

    aliongea mwanamke aliyekuwa ameketi juu ya kitanda chake , huku mwili wake akiwa ameufunika kwa nguo nzito ili kulikabili baridi la siku hiyo , hakuwa na kawaida ya kuamka mapema, lakini siku hiyo alikuwa ameshaamka na tayari alikuwa ameshaoga , msichana wa kazi alipoelekea getini akiwa amejifunika na mwavuli kuzuia maji ya mvua yasiulowanishe mwili wake ,naye alitoka chumbani kwake akijikokota taratibu ,

    “ kumbe uko huku babu “

    “ ndiyo bibi , sikutaka kukuamsha ,harafu leo usiku nimeota ndoto mbaya sana “,

    aliongea mzee Poul huku akijitengeneza vizuri , macho yake tu yaliashilia kile alichokiongea

    “ babu umeota nini ?

    Mke wake ambaye walizoeana kuitana babu na bibi, wakifatisha tabia za wajukuu zao , alimuuliza huku akiwa amemkazia macho yake madogo kiasi , ya kizee

    “ nimeota mwanangu Emanuel akimpiga sana mdogo wake David , na hata amepelekea kumuua , sijui ndoto gani hiyo “

    “mmmmh ! Unasema ?”,

    Bibi alijikuta akiuliza swali hilo kana kwamba hakuwa amesikia kile kilicho zungumzwa , kabla mzee huyo hajazungumza , watu watano walisimama katikati ya sebule yake , Jesca ambaye ni msichana wa kazi aliwakaribisha kwa heshima,

    “ shikamoo babu “,

    Poul alimsalimia babu yake huku akinyosha mkono wake wa kulia , mzee huyo aliupokea kwa furaha , huku uso wake wa kizee ukiweka tabasamu na shangwa za kumuona mjuu wake huyo aliyekuwa kipenzi chake ,toka utoto ,

    Umekuja lini ?Mume wangu ?” ,

    Bibi yake naye alimuuliza , huku akinyanyuka kwenye kiti na kumfuata mjukuu huyo , alimkumbatia katika kifua chake , huku akitoa machozi ya furaha sana , japo ulikuwa muda mfupi tu toka wametengana , lakini kwake aliona kama miaka kumi iliyopita , baada ya salamu hizo , wote walikaa na utambulisho uliendelea ,muda ulipowadia , Poul aliwasimulia kila kitu kilichokuwa kimetokea , hali iliyopelekea hata wao kushtuka sana na kushangaa , japo ilikuwa ngumu kuamini ,ila maneno yaliyokuwa yameandikwa kwenye karatasi yalizidi kuwaaminisha sana . Ilikuwa kama msiba ndani ya nyumba hiyo , wazee hao walimlilia mtoto wao Emanuel na mkwe wao Janiphar , huku wakiendelea kumtupia laana na lawama David , hawakusta kutoa shukurani za dhati kwa MacDonald aliyejitolea kwa moyo wake wa dhati na mapenzi ya kweli , ya kumtetea mjukuu wao hadi hapo , zaidi na zaidi walimshukuru pia Ghati na Vero kwa kazi waliyokuwa wameifanya , pia walimomba Ghati akirejea Tarime asiste kumsalimia sana msichana huyo na kumtaka afike nyumbani hapo , sasa walimchukulia kama mtoto wao wa kuzaa .

    Taarifa hizo pia zilifika kwa shangazi yake Poul aliyekuwa Daktari wa Bugando kwa muda huo , aliumia sana , naye alimulaani kaka yake huyo mdogo , kwa kuwa alikuwa akizifahamu tabia zake toka wakiwa wadogo hakusta kumuamini Poul.

    *****

    “ Mwanao atakuja tu , naomba nipumzike tafadhali “,

    aliongea Mohamed mara baada ya kufika Iran , akitokea China , mke wake alizidi kulalama japo alikuwaa ameshaambiwa ukweli wote na kuombwa amuache mtoto aendelea na maisha yake ,lakini hakukubaliana naye , alichotaka ni uwepo wa Joan nyumbani hapo , maisha yake bila binti huyo hayakuwa yamekamilika kabisa

    “ sasa unategemea ningefanyaje ?’

    “ wewe ulishindwa kumkamata kwa nguvu ?”

    “ Wewe si unamjua MacDonald , yule mtambo , naomba tuwaache waendele na maisha yao , watoto wamependana basi “

    “ huna akili Mohammed , nani akubali mwanangu awe na mtu mweusi tena kafiri “

    “ wewe ulichanguliwa mume ?”

    “ Hapana “

    “basi muache Joan afanye mambo yake , cha msingi ni kuwashauri wasijihusishe na mapenzi katika umri mdogo , hilo linaweza pelekea kuharibu masomo yao “

    , mwanaume huyo alijitahidi kumshauri mke wake , hadi alikubali , kilichokuwa kimebaki ni kuwaombea dua njema watoto hao , ambao hawakujua wako wapi , lakini waliamini wapo salama .

    Wiki moja baadaye Poul na wenzake walisafiri hadi China walikaa nyumbani kwa MacDonald kwa muda wa siku tatu kisha walielekea Iran nyumbani kwao Joan , walipokelewa kwa furaha , hata wao walishangaa mapokezi hayo , siku hiyo wazazi hao, walitoa ruhsa kwa marafi hao na kuwasistizia zaidi kusoma , Joan alijihisi kunenepa kila kitu alikiona kipya ndani ya masikio yake , siku tano kulifanyika tafirija kubwa nyumbani hapo iliyohudhuliwa na idadi kubwa ya watu , tena wale walioheshimia ndani ya Iran na Oman , baada ya sherehe hiyo watoto hao walilejea China kwa ajili ya masomo yao , huku wakiwa na shangwe ndani ya mioyo yao.Siku hazikuganda hatimaye Poul alihitimu masomo yake yote ,hadi yale ya chuo na kulejea nyumbani kwao Tanzania kuziendeleza mali za baba yake ambazo kwa muda huo zilikuwa chini ya usimamizi wa shangazi yake na mke wa David ambaye hakuwa na roho mbaya kama ya mume wake , aliwashukuru kwa kusimamia vyema, mali hizo .

    ****

    Ilikuwa ni harusi kubwa sana nchini Tanzania ambayo haijawahi kutokea , ni zaidi ya miezi miwili ndoa hiyo ilikuwa ikitangazwa katika vyombo mbalimabali vya habari , kila mtu alijihapiza kuhudhulia sherehe hiyo , ambayo ilikuwa ya kihistoria . Tarehe 03/02/2008, siku hiyo ilikuwa ikisubiliwa kwa hamu sana , mji wa mwanza ulikuwa umefurika idadi kubwa ya watu , japo ilikuwa siku ya mvua ya rasharasha, lakini watu hawakujali mvua hiyo , toka saa kumi na mbili asubuhi watu walijaa ndani uwanja wa furahisha kirumba, kungojea tukio hilo , hakuna kanisa ambalo lingeweza kutosha kuchukua idadi ya watu hao .

    Majira ya saa nne asubuhi magari ya viogozi mbalimbali wa serikali yalianza kuingia ndani ya uwanja huo , siyo ya serikali pekee yake, bali hata ya watu mashuhuri nje ya Tanzania , saa moja mbele , zilisikika kelele na ndelemo toka kila kona ya uwanja huo , mwanamke mwenye asili ya kiarabu alikuwa ndani ya shela , akikokotwa na farasi mweupe toka uingereza , farasi huyo alipita katikati ya uwanja huo , hali iliyopelekea kila mtu kusimama na kushangilia , kabla hajafika mbele , bwana harusi alitokea , kitendo kilichozidi kuwashangaza watu hao ,ambao hawakufahamu ni muda gani alifika eneo hilo ,wazazi wa Joan pamoja na ndugu toka Iran na Oman hawakuwa nyuma kutoa tabasamu zao .

    “ umependeza mpenzi “

    “ ahsante , siamini kama leo naolewa na wewe”

    “ amini “ ,

    waliongea kwa furaha huku wakitembea kwenda mbele , mshereheshaji aliongea mawili matatu ,kisha Padri Nikodemu alifungisha ndoa hiyo , hali iliyopelekea shangwa za hali ya juu , wengi wao walitoa machozi ya furaha , mtu aliyekuwa akilia bila kunyamaza alikuwa shangazi yake Poul , kumbukumbu za ndoa ya kaka yake Emanuel zilikuwa zimelejea , alimuona Poul kama kaka yake kwa jinsi walivyofanana. Tukio hilo lilipokamilika watu walitawanyika wakisubili jioni kwenda ukumbini .

    “ ujue siamini kama kweli nimekuoa “

    “ kwanini?”CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “ Misukosuko iliyokuwa mbele yetu ilikuwa inanitisha “

    “kweli , ila yalishapita cha msingi tuangalie mbele , jana daima haitatusaidia “

    “ umeongea la maana , eeeeh ! Hebu niambie utanizalia watoto wangapi ?”

    “ Mmoja “, aliogea Joan huku akitabasamu .

    “ acha masihala mie msukuma nataka watoto kumi , hujui natakiwa kutengeneza ukoo “

    “ kumi , hawatoshi , nakuzalia kumi na tano , timu ya mpira , pamoja na viongozi wake “

    “ hahahaha!”

    Walicheka kwa furaha kisha walijifunika shuka gubi gubi , kuumalizia usiku huo , wakiwa ndani ya Goldcrest hotel , wakisubili siku inayofuata waelekee Marekani kwa ajili ya fungate lao.



    MWISHO.



0 comments:

Post a Comment

Blog