Simulizi : Blood Deal
Sehemu Ya Nne (4)
Hali ya Joan ilibadilika ghafla , alihisi moyo wake ukimuuma bila kufahamu chanzo cha yote hayo , ile furaha na raha iliyokuwa imeutanda moyo wake sasa iligeuka na kuwa karaha , hakutaka tena kuendelea kukaa eneo hilo , akili yake ilimtuma kwenda kuongea na Poul ,
“Chunchang Poul yuko wapi “ aliuliza huku akiwa amemkazia macho kijana huyo wa kichina aliekuwa rafiki mkubwa wa Poul toka wakiwa wadogo ,
“hata sijui “
“kweli ?”
“ndio “
Hakutaka kuyaamini maneno ya kijana huyo kirahisi rahisi hivyo , alianza kuzunguka huku na huko , huku akiwauliza watu lakini jibu lilikuwa ni hilo hilo Poul hafahamiki alikokwenda , akiwa katika hali ya kukata tamaa , ghafla shule yao ilivamiwa na askari waliowaamru walimu wote , kufunga kikao hicho mara moja pamoja na kuwaruhusu wanafunzi wote kurejea majumbani , pia tarifa ya kupotea na kutekwa kwa mmoja wa mwanafunzi nayo ilitolewa .Hapo ndipo huzuni kwa Joan ilizidi kuongezeka
“nitamtafuta kwa akili zangu acha nikazungumze na baba nadhani atanisaidi “ Joan aliwaza ndani ya kichwa chake ,akiwa ndani ya ndege ndogo akielekea Iran , masaa kadhaa alishuka ndani ya uwanja mdogo wa nchi hiyo na kuchukuwa tax zilizokuwa zimepaki nje ya uwanja huo , safari ya kuelekea nyumabani ikaanza , huku kichwani akiwa na mzingo wa mawazo .
“mama nahitaji msaada wako ?” Joan alisema mara baada ya kufika nyumani kwao
“siku hizi unavuta bangi ama ?”
“Bangi !Hapana kwani vipi?”
“Kwanza umeingia kwa kasi kama unafukuzwa ,pili salamu hakuna ,na tatu kwanini umetoka shule bila taarifa “ maama yake aliongea kwa jazba sana , huku akiwa amesimama katikati ya subulehiyo ,
“ kunatatizo “
“lipi?”
“Shule imefungwa kwa muda mfupi ,mara baada ya kutokea kwa mapingano kando ya shule , na mwanfunzi mmoja kapotea “ Joan aliongea kwa unyonge sana , pindi alipomkumbuka rafiki yake Poul alihisi kuumwa
“Nasra kapotea ?”
“Bora angepotea yeye “
“kumbe nani?" Mama yake aliuliza kwa hamasa kubwa , maneno ya binti yake yalikuwa yanaendelea kumchanganya zaidi ,
“Poul"
Mzazi huyo hakutaka kuogea chochote ,zaidi ya kumkata jicho la hasira na kuondoka sebuleni hapo , akiwa chumbani alianza kuwasiliana na mume wake , naye alishtuka sana kusikia habari ya kupotea kwa Poul , moja kwa moja aliwasiliana na rafiki yake kipenzi David aliyeyapokea maneno hayo kwa furaha sana .
“Nitaondoka , siwezi ishi bila Poul “ Joan aliwaza peke yake ndani ya chumba chake ,usiku wa siku hiyo ,hadi kunapambazuka hakuwa amepata hata lepe la usingizi.
Homayoun alizidi kuchangnyikiwa zaidi , kila alichokifanya kilionekana kigumu , picha na matukio aliyokuwa akiyaona kupitia kompyuta ndongo ya mezani yalimtisha , alitamani kuwazuia ila alishindwa , kila alipojaribu kupiga simu ilikuwa haitoki kabisa, muda mwingine iliandika, emergency call , hivyo akawa wa kuzunguka zunguka ,huku na huko ndani ya ofisi hiyo kubwa na ya kisasa ,mara arudishe nywele zake ndefu shingoni , achilia mbali kutoa misonyo ya hasira , muda mwingine akidiriki kuiziba komyuta hiyo kwa viganja vyake vya mikono ili tu asiendelee kuliona tukio hilo ,jinsi mitambo ya MacDonald ilivyokuwa imara na bora zaidi uwezekano wa vijana hao kupona uliwa mdogo sana , na mbaya zaidi mitambo hiyo ilikuwa na uwezo wa kukata mawasiliano pindi uingiaapo ndani ya ngome ya MacDonald , hivyo ndivyo ilivyokuwa , baada ya vijana hao saba kuikanyanga ngome hiyo mawasiliano kati yao na Hamoyoun yalipotea .
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“nitafanya nini ?” alizidi kujiuliza huku akiendelea kutembea huku na huko , jasho jembamba likiendelea kulowanisha nguo zake , uso nao ulibadilika na kuwa mwekundu mithili ya nyanya ya Tanga, hakuja angesema kipi kwa David , hakujua pesa iliyopotea angeitoa wapi , kila alichokiwaza aliona hakifai.
“Nitajua cha kufanya “ aliwaza maneno hayo huku akifungua mlango wa ofisi hiyo ndogo , alitembea kwa kasi kuelekea stafu , huko nako alikuta kila mtu akiwa amebadilika kwa muonekano wa haraka haraka tu ,
“nisikilizeni “ alianza kuongea mara baada ya kuwatazama mmoja baada ya mwingine “ tunatakiwa tupambane kufa na kupona la sivyo maisha yetu yako hatari MacDonald sio mtu wa kuchezewa !”
“ndo nani ?”
“huyo ndie aliemtorosha Poul , ni mtu hatari , mbaya zaidi ana mitandao duniani kote , pili anakifaa cha kusikia mazungumzo zaidi ya kilometa mia tano, ana uwezo wa kukata masiliano pindi umkaribiapo na mwisho anamiliki mitandao yote ya simu duniani , swali je tukizembea tutamweza ?”
“hapana !!!!!!” wote walijibu kwa pamoja , huku macho yao yakiendelea kumtazama Homayoun kwa wasiwasi , hata wao walikuwa wameanza kuingiwa na hofu ndani ya mioyo yao , kila neno lillilokuwa likitoka mdomoni mwa kiongozi wao ,
“sasa tunafanyaje ?”
“hilo ndilo la kujiuliza sasa , “
“mie nadhani tumshirikishe boos “
“ataelewa ?”
“lazima aelewe tu ?”
****
Simu haikutoka mkononi ,kila mara alikuwa akiikagua ,kama kungekuwa na ujumbe wowote kutoka china , hakuweza kutulia dani ya ofisi yake , alinyanyuka na kutoka safari yake iliishia ofisini kwa Deus , huko nako hakukaa , kila aliloshauliwa aliona ni upuuzi tu , hadi inaingia jioni hakuwa amepata ujumbe wowote , hali hiyo ilizidi kumtisha , moyo wake ulikuwa na hamasa ya kufahamu kille kilichotoke china , hasa hasa alitaka kujua kipi kilimsibu Poul ,
“hawa vijana wanataka kunichezea ?” aliendelea kuwaza ndani ya kichwa chake , akiwa ndani ya gari lake ndogo akielekea nyumbani kwake ,
“tinti tinti tinti “ ulikuwa ni mlio wa ujumbe mfupi ndani ya simu yake , haraka alinyosha mkono wake na kuichukua simu iliyokuwa ndani ya mfuko wake wa shati , na kuelekea upande wa kiboksi cha ujumbe mfupi ,
“ hali tete boos , kijana hajapatikana “ hayo ndio yalikuwa maneno toka kwa Homayoun , japo yalikuwa mafupi lakini yalimtisha sana , taratibu alianza kupunguza mwendo wa gari hilo , huku akitafuta sehemu ya kupaki , mwili wote ulianza kumtetemeka mithili ya mtu alienyeshewa na mvua iliyoambana na baridi kali , hakuamini kama kweli Poul alikuwa hai , hakujua kipi kilisababisha kijana huyo aendelee kuwa hai , kama vijana wenye nguvu na uwezo alikuwa nao! Pesa ilikuwepo ya kutosha tena kutoka kwa watu zaidi ya wawili , je kwanini Poul awashinde ?Hakika alikuwa ndani ya mawazo sana , kila alichokiwaza hakikupata jibu sahihi .
“ Acha nimpigie “ papo hapo alianza kulitafuta jina la kijana huyo ndani ya simu yake , na baada ya kulipata alibonyeza kidude cha kijani kisha simu akaiweka sikioni , dakika moja ilianza kuita , akawa na hamasa ya kuongaea na kijana huyo , lakini simu hiyo haikupokelewa iliita hadi ikakatika , na alipopiga kwa mara ya pili simu haikupatikana hapo ndipo alipozidi kuchanganyikiwa zaidi , alitamani kulia lakini haikuwezekana , alihisi haja ndogo ikianza kutoka ,
“nitajua cha kufanya “ aliwasha gari na kuondoka , hakutaka tena kwenda nyumbani , aligeuza gari na kuifuata barabara la kwenda shinyanga , hakujali usiku huo ila alichodhamilia yeyea ni kuelekea kigoma usiku huo huo , ilikuwa kama kichekesho , lakini alidhamilia alichoamua , alipofika busagala alikata kulia na kuiacha barabara ya kwenda shinyanga , dakika kumi akawa amefika kingongo feri , bahati ilikuwa yake , aliikuta meli ndo imefika , alitulia kidogo ndani ya gari lake akisubiri abiria washuke ndani ya meli hiyo ,dakika kadhaa abiria walianza kuingia ndani ya melia hiyo , huku wakipita kando kando ya dirisha dogo kwa ajili ya kulipia nauli .Katika magari , gari la David lilikuwa la kwanza kuingia ndani ya feli hiyo , nusu saa baadae walikuwa upande wa pili tayari kwa safari ya kuelekea kigoma ,upande wa david,
“ nitawapoza hawa mafigisu figisu endapo nitakutana nao njiani “ aliwaza maneno hayo mara baada ya kuanza safari hiyo .Hadi inatimia saa kumi na moja alfajiri David alikuwa bado njia , japo alikuwa amechoka lakini hakutaka kukata tamaa , saa saba mchana ndipo aliikanyanga aridhi ya m zee Songoro huko ujiji Kigoma .
“ Babu kama nilivyokueleza nipo mashakani kabisa “
“mmmmh! Acha tujaribu , ila naona mtu alie ni hatari sana , anatumia dawa za kichina “
“ babu tuma hata radi tu, wewe hutakiwi kumuangamiza yule mchina hatuhusu “
“ acha tujaribu radi , “ alizungumza huku akimalizia kutengeneza radi hiyo , dakika kadhaa alianza kuirusha hewani , kitu mfano wa mpira wa tenesi kilianza kutoka ndani ya kibuyu , kikisambaa angani na kupotelea , lakini dakika kumi mzee Songoro alianza kushika koo lake kabla ya kuanza kutoka ndamu puani na mdomoni , kisha alidondoka .
“ Lazima niondoke tena usiku huu siwezi kuendelea kula raha ingali sijui hali ya Poul , je ni mzima ama la! Nampenda sana Poul , yeye ndiye kila kitu kwangu , furaha ndani ya moyo wangu , faraja pindi nihuzunikapo , joto langu wakati wa baridi , pia ni baridi kipindi cha joto …….no siwezi , nitamtafuta kwa gharama yeyote ilimrandi apatikane , iko wapi ahadi yangu ya kumpenda milele ? Yako wapi maneno yangu ya kumlinda milele! Tu….tuliahidiana kusaidiana wakati wa shida,na raha je msaada wangu kwake uko wapi ?” .
Yalikuwa ni maneno makali na ya kuhuzunisha ndani ya moyo wa msichana mdogo, wa kiarabu, ndani ya kasiri la mzee Mohammed mjini kerman kusini mashariki mwa Iran , Joan alizungumza huku macho yake madogo na yenye kuhisi usingizi singizi yakiitazama picha ndogo,aliyokuwa ameishikilia mkono wake wa kushoto, picha hiyo walipiga na Poul ,mwaka mmoja uliopita , mboni zake za macho zilizokuwa ndefu kiasi zilifunikwa na machozi yaliyokuwa yakitiririka kutoka ndani ya macho hayo , roho yake nayo haikuwa nyuma kumsindikiza katika safari yake hiyo ya uchungu .
“Ndio mie ni mwanamke , ila sitakiwi kuwa legelege napambana hadi nihakikishe Poul anapatikana tena akiwa hai “ Joan alizidi kuongae peke yake , hakutaka tena kuendelea kulala , alinyanyuka na kuiendea swichi iliyokuwa ukutani,karibu kabisa na mlango , aliwasha taa , kisha alirudi haraka hadi mezani , meza ndogo aliyokuwa akiitumia kwa matumizi yake ya kujisomea , hapo alinyosha mkono wake wa kushoto ,hadi alipoikamata saa yake ndogo ya mkononi ,
“ ooooh!Bado mapema sana , nitaondoka tu “ aliipeleka hadi mkono wake wa kulia na kuivalisha ndani ya mkono wa kushoto ,kisha alichukua simu yake akaingiza namba za siri kuangalia salio lililokuwa ndani ya mfuko wake wa benki ,
“aaaah! Zitatosha sana , “
aliwaza hayo huku akirudisha simu mezani , zilikuwa ni pesa nyingi sana ambazo alikuwa na uwezo wa kuzunguka dunia nzima tena kila siku! Bila kupumzika ,na pesa hizo zingebaki tu! Hakutaka kupoteza muda alianza kukusunya kila kitu , alichokiona ni cha muhimu sana , kisha alianza kutoka chumbani humo huku akinyata taratibu , begi lake likiwa mgongoni , kwa tahadhali aliweza kuufungua mlango na kufanikiwa kutoka nje , lakini kabla hajaondoka mlangoni hapo alirudi tena sebuleni , moja kwa moja aliiendea kamera iliyokuwa imefungwa sebuleni hapo na kuiharibu , Joan alitoa tabasamu la furaha baadaya kufanikisha zoezi hilo ,
“kweheri mama , kwaheri baba ….naenda kumtafuta kipenzi changu , mniombee mwaaaaaaaah!” Maneno hayo aliyazungumza akiwa ameshikilia picha ndogo iliyokuwa ndani ya moto{ flame} , huku akiiambatanisha na busu , hakuweza kuyazuia machozi , lakini hakuwa na jinsi ilibidi aondoke eneo hilo haraka iwezekanavyo .
“Nitatokaje “ alianza kuwaza tena , kasiri la baba yake lilikuwa na mageti matatau na kila geti kulikuwa na walinzi watatu ,
“ Abudull ni rafiki yangu sana , sasa namtumia yeye kunitoa ndani “ hakupoteza muda alianza kumfuata kijana huyo mwenye asili ya kisomali kwa mama yake , huku baba yake akiwa mwarabu wa nchi hiyo , hakuwa na elimu zaidi ya darasa la nne , huku akiwa yatima katika umri wake huo wa miaka ishirini , bibi yake ndiye alikuwa msaada toka akiwa mdogo , waliishi ndani ya eneo lenye watu masikini sana , wakiwa na kijumba kidogao tena cha tope , huku bibi yake akiwa muuzaji mzuri wa tende toka Oman.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ Abuu amkaaaaaaa”Joan alimuamsha kwa kumtikisa tikisa,
“eeeeh !”
“Shiiii!” Joan alimzuia kwa kidole chake cha shahada ,baada ya kushtuka kwa kupiga kelele
“ nataka kutoka Abuu “
“ nini muda huu wa saa saba usiku ?” Abudull alimuuliza Joan kwa mshangao huku akiwa haamini kile alichokisikia , kwa msichana mdogo kama yeye hakutakiwa kutoka nje usiku huo ,
“ utaniletea maatatizo dada “
“ yapi ?”
“ kwanza tabua hapa tunaonekana , pili ukipata matatizo mie nafia jela , tazama bibi yangu kikongwe msaada wake ni mie , na….nakuomba tafadhali usifanye hivyo rafiki yangu “ Abudull alisema kwa huzuni , huku akimpigia magoti Joan aliyeonekana kutojali chochote ,alichotaka yeye ni kutoka salama ndani ya jumba hilo .
“ sikia Abuu , kwanza hapa hatuonekani mambo yote nishamaliza , nitakupa kiasi chochote cha pesa utakacho ili unitoe humu ndani usiku huu “
“ ha…hapa..na Jo……Joan ….siwezi naipenda kazi yangu , tafadhali usiondoke nakuomba “
Abudull alisema akiwa bado pale pale chini , moyo wake haukuwa radhi kufanya kile alichotaka binti huyo mdogo wa miaka kumi na tatu tu ! Moyo nao ulianza kutoa machozi , aliipenda kazi yake ,na mbaya zaidi alimpenda bibi yake , tamaa ya pesa ingeweza kuhatarisha maisha yake ,
“ kwanza toa machozi , unanichuria Abuu , pili mbona hauko kama mwanaume! Sikia hofu yako nini ? Kama pesa naweza kukupa na hata ukaondoka nchini , muda mwingine usipende kuruhusu machozi kuonekana mbele za watu , hasahasa kwa watoto kwa kike , ok niambie nini unachoogopa rafiki yangu ?”
alizungumza Joan huku akiwa anapiga hatua kumfuata Abudull , kwa mkono wake wa kushoto alimvuta kutoka chini na kumkalisha katika kiti chake ,kisha nae akapiga magoti akimtazama uso wake , mikono yake yote miwili akiiegemeza mapajani mwa kijana huyo .
“Nakupenda sana , pia nayapenda maisha yako na ya bibi yako , sifanyi haya kwa kupenda nasukumwa na penzi la dhati kwa kijana niliekueleza leo mchana , maisha yangu hayatakamilika endapo nitaishi bila uwepo wa kijana huyu , Abuu nipo radhi kuyapoteza maisha yangu kwanza, ndiyo naye ayapoteze , ila sipo radhi kuishi kifalme na kimalkia , kwa umbo la nje , huku umbo la ndani linateketea kwa maumivu , ulishawahi kupenda ?”
Joan aliuliza swali hilo huku akimtazama kijana huyo machoni , Abudull hakuweza kujibu kwa maneno zaidi ya kuitikia kwa kutikisa kichwa kuashilia, kukubali swali hilo, alikuwa kama mgonjwa .
“ Basi kama ni hivyo nipe nafasi ya kuitafuta furaha yangu , na nikiipata zawadi yake kamwe hutoisahau milele “
“lakini mai…..maisha yangu Joan “
“ Abuu hutodhurika naomba niondoke tafadhali “ alisema hayo , huku akinyanyuka sehemu hiyo ,hakika alimpa wakati mugumu kijana wa watu , hakujua afanye nini naye alijikuta alidhamiria kumsaidia binti huyo , kama kazi alikuwa radhi kupoteza , na kama ni jela napo angeenda .hawakutaka kupoteza muda tena walichokifanya ni kuanza kuondoka eneo hilo , mita chache walisimama .
“Sikia Joan , inatakiwa uwe jasili , kama simba, je utaweza kukubali kukaa ndani ya takataka?”
“Ndio”.
“Haya ingia humu” Abudul alimuonyesha Joan pipa la uchafu ambao alipewa mchana yake kwenda kuutupa , lakini alijikuta akisahau na alipanga asubuhi yake afanye zoezi hilo , kabla ya mama mwenye nyumba kuamka , uwepo wa uchafu huo ukawa njia tosha kwa binti huyo kutoka ,
“ mwanangu mbona taka usiku huu ?”
“ Nilisahau , si unajua bi mkubwa !”
“ Kweli mwanangu “ hivyo ndivyo alivyofanikisha kupita geti la kwanza na la pili , Joan hakuamini kama kweli alifaniksha kupita salama sehemu zote hizo , aliendelea kuomba na geti la tatu watoke salama , kweli bahati ilikuwa yake waliweza kuvuka salama na safari ya kuelekea dampo ikaaza ,
“ nakutakia maisha mema Jaon “
“nawe ubaki salama , sawa ?”
Abudull alijibu kwa kutikisa kichwa, kisha Joan alianza kuondoka huku akikimbia , akiifuata barabara ya mkono wake wa kushoto , kitu cha kwanza kukifanya , aliielekea moja kwa moja benki , uzuri wa benki za huko zilikuwa zikifanya kazi masaa ishirini na nne , hivyo uwezekano wa y eye kupata huduma hiyo ulikuwepo tena kwa asilimia kubwa sana, alichofanya baada ya kufika benki hapo alifungua mfuko mwingine , na kuzihamisha pesa hizo, pia alichukua kiasi kikubwa cha pesa , kisha alianza kuondoka eneo hilo , hakujua aanzie wapi ila alichotaka ni kutoka ndani ya nchi hiyo kabla ya siku mpya kuwadia ,ilibidi atafute usafiri uliompeleka hadi stendi ya magari yatokayo ndani ya nchi hiyo nyakati za usiku , bahati ilikuwa yake , dakika tatu tu kufika hapo aliweza fanikisha kupata basi lililokuwa likielekea china , usiku huo , hakutaka kukaa nje mara baada ya kulipia alipanda ndani ya basi hilo ,na kuketi bila kuongea na mtu yeyote , hadi safari inaanza alikuwa kimya sana .akihofia watu kumfahamu.
****
David aliyatoa macho , mithili ya mjusi aliyebanwa nyuma ya mlango , hakujua afanye nini , msaada aliokuwa akiutegemea ulionekana kuanza kukwama , alishindwa kunyanyuka pahali hapo zaidi ya kujivuta kwa matako , kama mtoto mdogo , hakujali kuichafua suruali yake nyeupe na vumbi hilo jekundu la mkoa wa kigoma , alichowaza yeye ni kuyaokoa maisha yake , hali ya mzee Songoro ilimtisha sana , dalili ya kupona haikuonekana hata kidogo , alizidi kujinyonga nyonga na mikono yake shingoni , huku damu zikiendelea kutoka ndani ya pua na mdomo wake , dakika tano alitulia huku macho yakiwa juu, tayari mzee Songoro alikuwa amefarik! David kuona hivyo alianza kukimbia kama mwehu , kuelekea usawa alikopaki gari lake ,alikimbia huku akitazama nyuma ,utadhani alikuwa akikimbizwa , roho wa woga alikuwa amemkabili sana , hakujua alifikaje ndani ya gari hilo , aliwasha na kuanza kutoka eneo hilo kwa kasi sana , tumaini lake lilikuwa ni kutoka ndani ya mji huo akiwa salama , kabisa .
“Sasa nitafanya nini ?” alianza kuongea peke yake , akiwa ndani ya gari lake safari ya kuelekea mwanza ilianza, huku akiwa hajafanikisha zoezi lake .Aliumia sana .
****
Japo MacDonald alikuwa jambazi sana , pia alikuwa yuko mbele katika maswala ya jadi , hakuiamini dunia hata siku moja ,aliweza kutumia pia dawa za kienyeji endapo adui yeyote angemkabili kwa njia hiyo , alikuwa na dawa nyingi sana ndani ya chumba chake ,na chumba hicho hakuruhusiwa kuingia mtu yeyote zaidi ya yeye mwenyewe , si ya kichina ama ya kiarabu kote huko alipita nusu ya mwili wake ulijaa chale ,utafikiri aliwahi pitia mashindao ya chale! Chale hizo zilikuwa na uwezo pia wa kumfahamisha baya lolote , siku mzee Songoro alipojaribu kumtupia Poul radi yake ya kishirikiana chale za MacDonald zilitoa taarifa hiyo ,hivyo alilazimu kumtoa Poul sehemu aliyokuwa ameketi na kumhifadhi sehemu salama , ngome yake nayo ilikuwa imetengenezwa kwa nguvu hizo , hivyo madawa hayo yalijikuta yakimrudia yeye mwenyewe .
Prado ilizidi kuongeza mwendo zaidi ya uwezo wake , muda mwingine ilinesanesa na hata kujaribu kuruka baadhi ya vibonde , ilionekana mtu aliyekuwa ndani yake alikuwa na haraka sana , kweli ! David alionekana kuchanganyikiwa sana , hakutaka kuamini kama kweli mzee Songoro alikuwa amekufa! Kweli alikuwa na haja ya kuchanganyikiwa ,kwa msaada aliokuwa amempatia kwa muda mrefu na hata kufanikisha baadhi ya mambo yake , alikuwa na haki ya kuumia achilia mbali kuchanganyikiwa , machozi yalianza kutiririka taratibu yakichora barabara juu ya ngozi yake ya mashavu , muda mwingine alitamani kufa ,lakini roho wa uvumilivu alimkataza tena , akiwa ndani ya mawazo ghafla simu yake ilianza kuiita , bila kupoteza muda aliichukua haraka-haraka ,kitu cha kwanza kabla ya kupokea alitazama jina la mpigaji ,
“ mmmmh! “ Aliguna kwanza , mguno uliyokuwa umechanganyikana na uchungu , wasiwasi na hata hasira dhidi ya mpigaji huyo,
“ atanikoma mjinga sana “,CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
alijisemea ndani ya nafsi yake huku akibonyeza sehemu ya kupokelea , kisha aliupeleka mkono huo sikioni .
“ kwanza samahani sa……….”
“ Homayoun ,kama huwezi kazi sema , humuwezi kukaa kimya muda wote huo , hamjui kipi kilichonipata ?”
Aliongea David kwa hasira ,huku uso wake ukikunja ndita , povu nalo mdomoni lilitoka , mfano wa povu la bia ndani ya birauli.
“ unatakiwa utusikilize ,sio kulalamika , ok fine kama unaona tunazembea basi fanya wewe , na kuanzia sasa mie usinishirikishe katika mambo yako sawa?”
Homayoun nae alijikuta akipandisha hasira , hakujali kama David alikuwa boss wake , matatizo aliyokuwa nayo aliyafahamu yeye!
“ Usifike huko , ta…tafadhali! Bado nakuhitaji zaidi ya unavyofikiria, nakuomba sana , sana “
“ kwanza kabla ya yote ,vijana wako wote toka Tanzania wameuawa , pili ninavyoongea nawe uwezekano wa kumkamata kijana huyo ni mudogo sana , anasaidiwa na MacDonald tajiri wa nguvu zote, anatumia mitandao mirefu , na ana mbinu nyingi za kivita , naomba tuachane nae “
“ hujui unachokizungumza , wewe mwarabu koko, mjinga sana , kwa lipi atuzidi ?
“ Humfahamu ndo maana, ila ukweli ndio huo ,sawa kila kitakachoendelea nitakujuza sawa? “
“ poa”
Aliitikia kwa unyonge , siku zote hakutaka moyo wake upate karaha yeyote , jinsi alivyomjua Poul uhakika wa kumuacha hai haukuwepo,
“ siku nikimfahamu aliyemuua baba yangu nahakikisha namchoma kisu cha tumbo “
“kwanini Poul?”
David alihoji huku akimkazia macho kijana huyo ,
“amenifanya nikawa yatima, amenitesa vya kutosha , na mbaya zaidi ameniliza kwa muda mrefu , wallah ba mdogo namuua acha nikue “
“mmmh!” David aliishia kuguna tu, mara baada ya kuyakumbuka mazungumzoa kati yake na kijana huyo ,miaka kadhaa iliyopita , alihisi kuchanganyikiwa ,muda mwingine alijilaumu kuumuacha hai muda wote huo .
“ lakini nashindwaje ?”
Aliendelea kujiuliza mawazo yenye mfumo wa swali ,lakini hakupata jibu sahihi , zaidi ya kuongeza mawazo .
Hadi anafika nyumbani kwake majira ya saa sita usiku ,hakuwa amepata jibu lolote , zaidi ya kuendelea kuchanganyikiwa , hakutaka kuongea na mtu , kujitupa kitandani tena bila kuoga ,mkewe alipouliza hakupata jibu sahihi zaidi ya maeno makali tena yenye kuudhi sana .Saa kumi na mbili asubuhi alidamka na kuelekea bafuni alitoka bila kuongea na mtu yeyote ,zaidi ya salamu tu , hali hiyo ilimkwaza sana mkewe , hakujua kipi kilimsibu mumewe , kwanza hakuwa nyumbani hapo usiku mzima na mchana yake , bila taarifa yeyote ,na mbaya zaidi simu alizima zote , pili karudi bila kuzungumza chochote zaidi ya maneno ya karaha ,vyote hivyo vilimchanganya sana mwanamke huyo ,lakini hakuwa na cha kufanya .
“Kaka maji yamefika shingoni ukisikia aibu ,sasa ndio hiyo yaja ujue “
“kiaje David ?”
Deus alihoji huku akikigeuza kiti chake cha kuzunguka , na kumtazama David, aliyeonekana mnyonge kupita maelezo,uso wake tu ulionyesha hali hiyo ,achilia mbali midomo kukauka ,mithili ya mgonjwa wa maralia !
“Dogo anachosha kichwa changu ,kaka sipati usingizi , na mbaya zaidi nimetoka kwa babu a……….”
“ safi sana ,mtumie babu amuagamize , kwanini unachelewa ?”
David hakujibu mapema swali hilo ,zaidi ya kukaa kimya kama dakika tatu ,kisha alinyanyua shingo na kumtazama Deus kwa macho ya kukata tamaa,
“Babu kafariki “,
“nini? Na…nani kakwambia wewe ?”
Deus aliuliza kwa mshangao wa hali ya juu ,hakutaka kuyaamini maneno ya David kirahisi hivyo ,kifo cha mzee huyo kilikuwa pigo hata kwake ,
“hebu niambie kinaga ubaga ,”
aliongea huku akiwa katika hali hiyo hiyo , ilibidi David amsimlie kila kitu ,bila kuficha hata tone la mambo yote ,
“ ndiyo hivyo ,hapa nilipo sijielewi ,sina moja wala mbili ,nimechanganyikiwa kaka “
“ sikia kuna rafiki yangu toka Somalia atapambana nae najua lazima atamkamata tu “
“kweli? ,Maana mtu mwenyewe mtambo ,tena mtambo kweli kweli! Nimafia wa kimataifa tena aliyebobea , China nzima inamuogopa ,sijui kama tutamkamata ,hapa mie naona niuze kila kitu nisepe Tanzania hainifai kaka “
“ha ha ha ha ! Kaka maji ukiyavulia nguo shariti uyaoge , cha msingi hapa ni kutafuta njia nyingine si kukimbia ,na tambua kukimbia tatizo si kulitatua ,bali ni kujiongezea matatizo mengine ,umo ndani ya blood deal cha muhimu ni kukaa humo humo , “
“kweli ila kuna mengine yanakuwa magumu Deus “
“nisikilize mie , nimeanza kuona jua kabla yako, Masoud namuaminia sana hashindwi ,kama aliweza kulipua chuo kikuu cha Gharisa huko Kenya na kufanya matukio mengi na makubwa sana duniani , atamshindwa huyo sijui Donaldmac wako huyo? “
Deus aliongea kwa kujiamini kupita maelezo , kwa jinsi alivyomuamini Masoud ,kumkamata MacDonal kilikuwa ni kitendo kidogo sana na chepesi kwake .
“nakutegemea sana kaka “
“ondoa wasiwasi ,tena namtafuta sasa hivi “ ,
papo hapo Deus aliwasha tarakilishi yake ndogo ya menzani na kuanza kumtafuta Masoud ,bahati ilikuwa yake alimkuta akiwa mtandaoni , walianza kuwasiliana , Deus alimuomba afike mara moja Tanzania , kwakuwa masoud alikuwa kipesa zaidi hakukataa wito huo ,na aliahidi siku mbili angekuwa Tanzania .
****
Joan aliendelea kuwa kimya ndani ya basi hilo, bila kuongea na mtu yeyote ,akili yake yote ilikuwa ikiwaza jinsi ya kumpata Poul , China aliifahamu tena sana ,ila hakufahamu wapi alikokuwa Poul ,
“nitafanya nini ?’
Alianza tena kuwaza , muda mwingine alijikuta akiongea kwa sauti ,hali iliyopelekea hata kijana aliyekuwa amekaa pembeni yake kumsikia .
“Dada mambo? ,Naitwa Sharifu , mwanafunzi wa Nanjing Normal University,mwaka wa kwanza , nachukua e……..”
“eeeeeh! Sijakuuliza ,tafadhali “
Joan hakutaka kusikiliza ngojera za kijana huyo , aliyeonekana muongeaji sana , naye kuona hivyo ilibidi atulie na kuendelea kufanya mambo yake ,hadi basi hilo linaingia mjini Beijing mtaa wa Yaojiayuan ,katikati ya jiji hilo ,majira ya saa saba mchana saa za huko ,hakuna aliethubutu kuongea na mwenzake . Alitoka nje ya kituo hicho na kuelekea usawa uliokuwa umepaki kebu.
“ nipeleke Yi” Joan aliongea kwa kichina ,
“ sawa keti “,
safari ya kuelekea mjini Yi ilianza , mita chache kutoka kituoni hapo , Joan alishangaa kuona picha yake ikiwa imebadikwa kila pahali ikiwa na ujumbe wa kumtafuta ,si ukutani ama kwenye miti ,alishtuka sana , mshtuko huo ulimfanya hata dereva nae kushtuka ndipo alipmtazama vyema Joan .
“ unafanana sana na binti anayetafutwa “
“ pacha wangu ,hapa nilipo na elekea huko kutoa matangazo , sijui tutampata ?
“ kweli? Sio wewe ?
“ Pacha wangu , mbona mbishi lakini !“
“ basi yaishe “
Bwana Dong hakutaka kuyaamini maneno ya binti huyo hata kidogo , roho yake ilimweleza kuwa huyo ndiye , hakutaka kupoteza bahati hiyo , ahadi ya zawadi iliyokuwa imetolewa na baba yake , aliitamani sana ,kiasi hicho cha pesa kingesaidia kuyabadiri maisha yake kwa kiasi kikubwa , na hata kazi ya udereva kebu angeuacha ,
“siwezi lazima nimpeleke kituo cha polisi ,siwezi nikawa mjinga kiasi hicho ,yaani napiga teke gunia la pesa ? Ha ha ha ha ! Nitakuwa mjinga tena namba moja duniani ,yawezekana hii ni moja ya bahati yangu “,
Bwana Dong aliwaza peke yake , huku akiwaza kituo kipi angempeleka binti huyo , kwa upande wa Joan alihisi mambo kuanza kubadirika , hakutaka kurudi mikononi mwa wazazi wake akiwa bado hajafanikiwa kumpata Poul , haraka kama mbio za swala alianza kutafuta mbinu za kutoroka kabla ya kufika mjini Yi , akiwa bado hajafanikiwa kupata jawabu sahihi alishangaa , dereva huyo akikata njia ya kuelekea kituo cha polisi , hapo ndipo taa nyekundu iliwaka ndani ya kichwa chake .
“Binti nisubili hapa nakuja “,
Bwana Dong aliongea huku akifungua mlango wa kebu hiyo na kutoka mbio ,
“ sawa “,
Alijibu kwa haraka sana , huku akijitengeneza tengeneza . Dakika tatu bwana Dong alilejea huku akiwa ameambatana na askari watatu , mmoja wa kiume na wengine wa kike , jinsi walivyokuwa wakitembea kwa kasi , huku wakiongea ilionekana walikuwa na hasira sana .
“ Sasa yuko wapi ?”
Askari wa kike ,mnene kupita wote alihoji huku akimtazama ,bwana Dong , aliyekuwa bado haamini kama kweli Joan hakuwemo ndani ya gari hilo dogo ,
“ ongea , acha kutumbua macho , mtu mzima kama wew unadriki kudanganya jeshi la polisi? Unaifahamu kweli sheria ?”CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ kweli nimekuja naye “ ,
alijitetea ,lakini hakuna aliyedriki kumuamini,
“ basi acha ukae kwanza ndani ,nadhani akili yako itakaa sawa ,“
papo hapo askari hao walimkamata bwana Dong na kurudi nae ndani ya kituo cha polisi , akilia kama mtoto mdogo ,kitu kilichomuumiza zaidi ni hali ya mkewe aliyekuwa amelazwa hospitali kwa ajili ya uzazi. Na mbaya zaidi hakuwa na mtu wa kumsaidia zaidi ya yeye mwenyewe.
****
Hakuna kitu kilichowaumiza wazazi hao kama kuondokewa kwa mtoto wao wa pekee , uwepo wa Joan maishani mwao ulitosha kabisa kuyafurahia maisha hayo ya utajiri wa kupindukia,walimpenda sana binti huyo wapekee ,na hawakuwa tayari kumpoteza kwa namna yeyote ile , walikuwa tayari kupoteza pesa zote lakini si kumpoteza Joan . Alikuwa wa thamani sana kupita maelezo ,
“ namhitaji mwanangu Mohammed , wewe ndiye chanzo cha yeye kuondoka “ ,
mama yake Joan alisema huku akilia kilio cha uchungu , mapenzi aliyokuwa nayo kwa binti yake huyo aliyajua mwenyewe ,
“ mama Joan huu si muda wa kulalamikiana ,cha muhimu ni kutafuta njia mbadala ya kumpata , sio kulia “
“ hujui ulisemalo wewe , uchungu wake naufahamu , siku namleta duniani nilikuwa peke yangu , maumivu na adha zake nazijua mwenyewe , nakuomba ukamtafute tafadhali “,
aliendelea kulalamika mwanamama huyo wa kiarabu , hakulalamika pekee ,bali hata makofi madogo madogo ya kike kike yalitua mgongoni kwa mumewe , aliyekuwa ameketi mwanzo mwa kitanda, uso wake uliitazama sakafu , japo alionekana kimya ,lakini moyo ulimuuma sana kutomuona mwanae , hakujua kama yuko hai ama la! .
“ Nakuja “,
“na ukiingia humu ingia na Joan “,
Salma aliendelea kufyata, bila kujali kama maneno hayo yalikuwa mwiba kifuani mwa mwanaume huyo , hakutaka kumjibu chochote alitoka hadi nje alikokwenda kuitisha kikao kifupi na walinzi wote . Hakuna aliyeweza kufahamu ni wapi Joan alienda zaidi ya Abudull ,
“ naomba tukatoe taarifa kituo cha polisi ,vituo vya habari na kwingineko ,nadhani tunaweza kupata msaada wa haraka zaidi”,
mmoja wa walinzi hao alitao wazo ,na kupitishwa haraka sana .
Papo hapo Mohammed alirudi ndani , huko alielekea bafuni ,na baada ya kutoka alivaa kanzu rangi ya ugoro, akiongeza na balagashia alitoka nje , alikomkuta dereva wake akimsubiri , safari ya kuelekea kituo cha polisi ilianza , aliandikisha kila kitu , pamoja na kuacha picha ya Joan ,kisha alielekea vituo vya habari . siku hiyo mji ulizizima kwa habari hiyo ,kila mtu alikuwa na kazi ya kumtafuta binti huyo , kiasi cha pesa kilichokuwa kimetolewa kiliwachanganya watu , wengine walidriki kuelekea nchi jilani ,kama china na zinginezo ,ili mradi Joan apatikane .
Majengo na kuta mbalimbali zilijazwa picha za msichana huyo , askari nao hawakuwa nyuma kuranda randa mitaani kumtafuta Joan ,lakini hadi inafika jioni hakuna walichoambulia .
“ haloo “
“ naitwa bwana Dong toka china , binti yako leo , mchana ameonekana ndani ya mji wa Beijing akielekea Yi”
ulizungumza upande wa pili ,mara baada ya simu kupokelewa , taarifa hiyo ilimshtua sana Mohammed, aliyekuwa amejilaza chali juu ya kitanda ,pembeni yake aliketi mkewe akimlaumu .
“ Naelekea China sasa hivi “
“ ndiko alikokwenda ?”
“ Ndiyo huyu jamaa kadai yuko huko”,
jinsi alivyompenda mwanae hakutaka kupoteza muda ,wala kubadili nguo , alichukua passport,kadi ya benki ,pamoja na pesa kiasi ,kisha alielekea uwanja wa ndege ,kuiwahi ndege ya saa tano na dakika arobaini na tano usiku .
Mohammed aliona kama ndege haiendi mwendo aliotaka yeye , alitamani sana kufika mjini Beijing kisha mjini Yi , muda mwingine alizungumza peke yake , akili haikuwa yake , kila alichowaza alikiona hakipo sawa , alitamani kumuona binti yake haraka iwezekanavyo na kurejea nae nyumbani , kurudi nyumbani bila ,binti huyo lingekuwa tatizo jingine , muda mwingine alijilaumu kumkalipia , aliuchukia ulimi wake ,
“ sijui nitampata ?” ,
Alizungumza peke yake , hadi ndege inatua ndani ya uwanja wa ndege mjini Beijing hakuwa amepata usingizi , alishuka na kufuata taratibu zote kabla ya kutoka nje ya uwanja huo ,
“ naelekea Yi “
“ kwenda Yi kwa leo haiwezekani ?”
“ kwanini ?”
“ Daraja la Qzyong limevunjika kwa sababau ya mvua kubwa iliyonyesha usiku wa leo , serikali imetangaza watu kutovuka kabisa, naomba uondoke kesha “,
Dereva kebu, raia wa nchi hiyo alisema hayo huku akiendelea kufuta vumbi gari lake
“ acha utani bwana mdogo !”
“Kweli !Kwani wewe hujasikia taarifa hiyo ?”
“ Hapana “
“basi ndiyo hivyo “.
Mohammed alijikuta akinywea kabisa , taarifa hiyo hakutamani kuisikia masikioni mwake ,alichotaka yeye ni kumpata binti yake .
“Nitakodi helkopita “,
alijisemea hayo ,huku akianza kupiga hatua kutoka eneo hilo , jinsi alivyokuwa akitamani kumuona mwanae ,hakutaka kusikia habari zozote , kwa gharama yeyote alidhamiria kumpata mwanae kipenzi , kwa kuwa aliifahamu China hakusumbuka sana ,kupata helkopita ,alilipia kisha safari ya kuelekea mjini Yi ilianza , walifanikiwa kuingia salama mjini Yi ,majira ya saa tano asubuhi , macho yake yalishangazwa sana na mji huo , kila sehemu picha ya Joan ilikuwa imebandikwa , hali hiyo kiasi ilianza kumpa tumaini la kumpata mwanae , lakini hadi inaingia jioni hakuwa amefanikiwa kumpata mwanae ,hali hiyo ilianza kumpa wasiwasi .
****
Homayoun alizidi kuchanganyikiwa zaidi , ile idadi ya vijana wake kuuawa ilizidi kumtisha zaidi , moyoni hakuwa na imani kabisa ya kuendelea kuishi tena China , alichofanya ni kuamua kuuza kila kitu alichoona ni cha muhimu kisha alipanga kukimbilia kwao Afghanistani ambatane na rafiki yake kipenzi Murtazar , aliyapenda maisha yake , pia aliyachukia maisha ya ujambazi , umwangaji wa damu zisizo na hatia , kama pesa alikuwa nazo za kutosha, tena za kuishi maisha mazuri . Hakupenda tena kuishi maisha ya udigidigi ,alitamani kuwa raia mwema ,tena mwenye kumjua mungu ,atoe sadaka iliyo bora na akiri makosa yake ,kuangukia mikononi kwa MacDonald hakukuhitaji tena .
“ Nimeamua kuacha kazi hii ya ujambazi , ujue kaka nimeua watu wengi sana , si wakubwa na hata watoto wadogo tena wasio na hatia , damu zao zinanilia ,tafadhali David niache “
“unaongea pumba gani we koko la kiarabu? Hivi unaweza ukanibadiri ,mawazo yangu kirahisi rahisi kama unavyodhani ?”
“Siko radhi kukutumikia tena , haya si maisha ,naishi kwa kujificha ndani ya nchi yangu , nimsema sitaki , niache na maisha yangu “
“ okay sawa , nakutakia maisha mema”
David alikata simu haraka –haraka , kisha alitafuta jina la mmoja wa vijana aliowaamini na kuwapa kazi ya kwenda kumuangamiza Homayoun na rafiki yake kabla ya kufika Afghanistan , kweli vijana hao walianza kuwafuatilia kuanzia siku hiyo , kila walikokwenda walikuwa nao, na baada ya siku tatu waliuawa kwa kulishwa sumu ,ndani ya hoteli ikipenyezwa kwa mmoja wa wafanyakazi wa hoteli hiyo ,kisha nae walimua akiwa anarejea nyumbani kwake majira ya saa tisa usiku saa za huko ,walifanya hayo ili kuficha ukweli , kwani waliamini dunia haina siri .
****CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
David alianza kuhisi ushindi mpya ndani ya moyo wake ,maneno ya Deus alimjenga tena upya ,ile hofu ya kushindwa ilitoweka ghafla ,alitamani saa zikimbie mithili ya maji mto ,ili tu Masoud afike Tanzania , siku hiyo hata chai aliweza kunywa , tena ilishuka mara baada ya kupokea taarifa ya kuuawa kwa Homayoun na rafiki yake Murtazar , aliwapongeza sana vijana hao na kuahidi kuwazaongeza malipo ,kweli hilo alilitekeleza mapema sana.
Ndege toka shrike la ndege dunian Delta ilionekana ikitafuta uwelekeo mzuri wa kutoka ndani ya uwanja wa ndege mjini Mogadishu Samalia . Kila abiria alikuwa kimya kabisa , wapo walioswali ama kusali ili waweze kufika salama walikokuwa wakienda , miongoni mwa abiria hao alikuwemo Masoud .
Masoud alikuwa kimya kabisa muda wote , akili yake iliwaza kufika Tanzania mara moja , bado hakuwa akifahamu kinaga ubaga kipi aliitiwa Tanzania ,aliketi siti ya tatu toka mwisho , japo alikuwa mafia aliyetukuka ndani na nje ya Somalia , lakini alifanikiwa kuingia salama ndani ya uwanja huo na hata kuanza safari bila kukamatwa , ama kushukiwa na kitu chochote , hakutaka kuongea na mtu yeyote maana alifahamu kufanya hivyo kungechangia hadithi kubadirika,hadi anaingia Tanzania hakuwa amefungua kinywa chake , taratibu alianza kushuka ndani ya ndege hiyo, huku macho yake yakiwa yamefunikwa na miwani mikubwa ya jua , kichwa kikivalishwa kofia rangi yeusi kampuni ya Jordan , mwili wake aliufunika kwa koti kubwa jeusi ,huku miguu yake akiivalisha kiatu rangi ya kaki ,aina ya Timberland shingo ndefu .
Mara baada ya kukamilisha zoezi la ukanguzi na hata ugongwaji wa passport alianza kutoka ndani ya uwanja mkuu wa mkoa wa mwanza ,huku macho yake yakiwa makini na kila mmoja aliyekuwa eneo hilo ,dakika tatu alifanikiwa kumuona Deus akiwa na David , hapo ndipo alipoachia tabasamu lake la kwanza .
“ Karibu sana kaka”,
Deus aliongea huku akinyosha mkono wake wa kulia, kumsalimia Masoud , naye aliupokea na kuufumbata vyema , walisalimiana huku wakikumbatiana kwa furaha , kisha David alisalimiana naye .
“pole sana kwa uchovu kaka ?:
“ Ahsante , nishapoa , naona Tanzania njema sana , watu wakarimu tofauti na mataifa mengine “
“huo ndio uzuri wa Tanzania , tunaishi kwa upendo kama ndugu wa baba mmoja”.
David alizungumza ,huku akimfungulia mlango mgeni huyo, japo alijidai kujiongelesha lakini macho yake na mawazo yake vyote vilikuwa vikimchunguza Masoud , kwa asilimia kubwa alianza sasa kuyasadiki maneno ya Deus kwa vitendo .Safari yao iliishia ndani ya Wande hoteli iliyoko mtaa wa uhuru , karibu kabisa na Mount Meru University , siku zote Masoud hakupenda kukaa ndani ya hoteli kubwa na zenye hadhi ya nyota tano , aliamini kukaa ndani ya hoteli za chini humsaida kufanya mambo yake kiurahisi bila kushtukiwa na mtu yeyeote .Askari ama vyombo vyovyote vya dola huwa havina akili ya haraka –haraka ya kuchunguza mapema sehemu hizo , hadi wapate wazo hilo tayari Masoud alishatoroka .
“Sitaki kupoteza muda , je mnaweza mkaaniambia kitu mlichoniitia ili nikalala,nilale na wazo “ Masoud alizungumza hayo ,huku akiendelea kujifuta maji na taulo ,mara baada ya kutoka bafuni ,
“huyu rafiki yangu anatatizo “,
Deus alizungumza huku akimtazama mmoja baada ya mwingine , ilibidi David amsimlie kisa chote cha yeye kumtaka Poul , pia hakusita kumueleza mtu aliemteka kijana huyo .
“hakuna shinda , acha nitumie muda huu kumtafuta “
“ ahsante sana ,”
David na Deus waliondoka ndani ya hoteli hiyo , wakiwa na furaha ndani ya mioyo yao ,hasa hasa David, alitamani kumbeba rafiki yake huyo , kwa msaada alliompatia , hakika alistahili pongezi .
Masoud hakutaka kupoteza muda aliwasha talakilishi yake ndogo aina ya Apple , na kuanza kuitafuta China , baada ya kuisoma kwa usahihi , aliutafuta mji wa Beijing ,alijifunza kila kitu , kuanzia barabara , hoteli , vituo vya polisi , maadaraja na n.k , kufanya vile humasidia kupata maficho endapo lingetokea la kutoke , hata baada ya kukaribishwa Tanzania kitu cha kwanza alijifunza kwanza mazigira ya Tanzania tena mikoa yote aliifahamu !, Hakuishia hapo tu aliutafuta mji wa Yi pomoja na kijiji cha Anhui , hapo ndipo alipofanikiwa kuiona ngome ya MackDonald , japo aliona kwa uzuri zaidi lakini alishindwa kuelewa chochote , mazigira ya ngome hiyo yalimpoteza kabisa .
“ He is realy dengerous guy { kweli ni mtu hatari }”,
alizungumza peke yake ,baada ya kusumbuka kumpata mwanaume huyo , zaidi ya masaa matatu aliyamaliza lakini hakuweza kufanikiwa kwa lolote, aliuma meno kwa hasira , siku zote alifanya kazi kwa wepesi lakini siku hiyo ilikuwa ngumu sana kwake .
“pati wani imekataa nitatumia , pati tu “ .
alizungumza peke yake , huku akianza kumkumbuka Cindy .
Cindy alikuwa binti wa miaka ishirini na sita , alizaliwa ndani ya hospitali ya Temeke jijini Dar es salaam nchini Tanzania ,tena kwa bahati mbaya! Mama yake alikuwa raia wa Sudani ya kusini ,huku baba yake alikuwa raia wa Somalia , Husna ambaye ni mama yake Cindy alijikuta akishikwa uchungu wa kuzaa usiku wa saa sita , akiwa njiani kuelekea nyumbani kwake Tandika kitunda, mara baada ya kutoka kwenye mkesha wa pasaka huko mbagala ndani ya klabu ya Dar Live. Tabia yake chafu ya kupenda vileo na disko ilimfanya akawa sugu , hakuijali afya yake . Mara baada ya kujifungua mtoto wa kike Husna alitoroka siku mbili baada ya kujifungua na kumuacha binti yake mchanga ndani ya chumba chake ,hakutaka tena kuishi Tanzania alilejea nyumbani kwao . Cindy alibaki peke yake ndani ya chumba hicho zaidi ya masaa mawili ndipo rafiki wa mama yake alipokuja kumchukua baadaa ya kupata taarifa hizo toka kwa majirani wa Husna .
Naye kama mama yake Cindy aliondoka Tanzania akiwa na mtoto huyo ,hadi nchini kwao Somalia , japo alikuwa mlevi , muuza mwili na kila raha ya dunia aliifanya ,lakini alimlea Cindy kama mototo wake , miaka saba Cindy alianza shule hadi alipohitimu elimu ya sekondari , hapo ndipo alipoanza umcharuko , hakushikika ,akawa kiguu na njia ,mama yake kuona vile alilazimu kumfukuza nyumbani .Hakukosa pa kwenda ,uzuri wake tu wa sura na umbo, ulikuwa mtaji tosha wa yeye kupata hifadhi ,disko likawa lake , huko ndiko alikojikuta akiangukia mikononi mwa Masoud na wenzake akiwa na miaka kumi na sita .
Walimutumia Cindy kama mtaji wa wao kupata faida , kwanza walihakikisha anapendeza , anakula vizuri na kumiliki pesa , maisha hayo ya kifahari yalimfanya Cindy kupendeza na kuvutia ,hakuna mwanaume aliyemkwepa Cindy hata kama alikuwa mgumu mithili ya chuma ! Lakini kwa Cindy alirainika tu!.
“ Halooo !”
Sauti nyororo mithili ya kilio cha mtoto mchanga ilisikika ikipenya vyema ndani ya spika za simu ya Masoud , aliyekuwa amelala chali , mkono wake wa kulia ukishilia simu ,huku mwingine ukikipapasa kifua chake kikubwa kilichokuwa kimetunukiwa nywele nzuri na za kuvutia .
“ Vipi umeshalala? Kichuna changu “
“ wapi ,nipo na Omar tunamfuatilia mbuzi mmoja hapo , ila mugumu lakini atakamatwa tu “
“ ndiyo yule wa serikali ?”
“ Haswaa “
“ hakikisheni mnamuua , usiku huu huu ,pia unatakiwa uje Tanzania haraka iwezekanavyo ,nataka nikutume china kuna ng’ombe wa kiarabu anajidai mjaja “
“hata sie mpango wetu ni huo , poa nitafika hapo majira ya saa mbili usiku “
“poa “ Masoud alikata simu ,kisha alishusha pumzi ndefu , kwa jinsi alivyomfahamu Cindy aliamini MacDonald angekamatika kirahisi sana .
Siku tano baadae Cindy , Masoud na Omar walisafiri hadi China , kwa kuwa waliingia jioni na walikuwa wamechoka sana ,hawakutaka kusafiri tena , walilala ndani ya Beijing na kesho yake asubuhi walisafiri hadi Yi ndani ya kijiji cha Ahnui , karibu kabisa na ngome ya MacDonal ,walipata chumba na kumuacha Cindy akiiendea ngome ya MacDonald , siku hiyo alihakikisha anapendeza kupita maelezo , dhumuni la kufanya vile ilikuwa ni kumkamata gaidi huyo .
Alifanikiwa kuingia ndani ya ngome hiyo , na kukutana ana kwa ana na run snake aliyejikuta akitetemeka moyo ,pindi alipomtazama Cindy .Baada ya salamu aliomba apelekwe kwa MacDonald , naye hakufanya hiyana alimuongoza hadi sebuleni alikokutana na MacDonald , ayempokea kwa moyo wake wote .
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Akili ya Joan ilikuwa na uwezo wa kufanya kazi tofauti na umri wake ,tayari alikuwa ameshamsoma dereva huyo , kitendo cha yeye kuondoka ndani ya kebu hiyo kilimfurahisha sana . Hakutaka kupoteza muda alifungua mlango na kutoka , alitazama huku na huko kisha alizama ndani ya kijimgahawa kidogo kilichokuwepo eneo hilo ,alipitiliza moja kwa moja hadi chooni ,hakujali kusoma kama chumba alichoingia ni cha kike ama cha kiume , alichojua yeye ni kuingia ndani ya chumba cha choo.
“ Puuuuuuh!”,
Alishusha pumzi ndefu ,mithili ya mtu aliyetoka kukimbia mbio ndefu , kwa kiganja chake cha mkono wake wa kushoto aliufuta uso wake, macho nayo yaliutazama uso wa kioo ,kwa jinsi alivyokuwa amebadirika hata yeye alijishangaa,
“sirudi nyuma , cha msingi hapa ni kuubadili muonekano wangu tu “ ,
aliongea huku akifungua zipu ya begi lake , alitoa baibui jeusi ,alivaa kisha alikifunika kichwa chake na kitambaa kilichobakiza macho tu , na ili kujipoteza zaidi alivaa na miwani ya juu ,chini alivaa kiatu kirefu.
“ Hakuna wa kunitambua hapo “,
alisema hayo huku akitoka ndani ya choo hicho ,akiwa mlangoni alikutana na mwanaume , lakini hakujali alizidi kunyosha bila kuangalia nyuma , macho yake yaliiona kebu ya bwana Dong mara baada ya kutoka nje ,hakutaka kushughurika nayo ,yeye alichojali ni kutoka salama ndani ya jiji hili la Beijing.
“kaka mambo ?”
“ poa ,nimbie ? Dereva kebu aliongea huku akipiga hatua kumfuata mteja huyo
“naelekea Ahnui huko Yi”
“ poa ,wewe tena, hata bure, “
hakutaka kuongea zaidi ,alifungua mlango wa kebu hiyo upande wa nyuma na kuketi kimya , njia nzima hakuongea alijifanya kusinzia ili kutompa nasafi dereva kebu kumhoji hoji , kitu kilichokuwa kichwani mwake ni kufika huko tu, tena salama , hadi wanafika hakuwa amezungumza chochote ,alilipa kiasi cha pesa kilichohitajika kisha alianza kutembea tembea ,hakujua aanzie wapi ,zaidi ya lisaa limoja alikuwa bado akizurula huku na huko , alihisi kuchoka ,lakini hakutaka kukata tamaa ,aliendelea kuzurula huku akionyesha picha ya Poul napo hakupata jibu .
“Nirudi nyumbani ?” ,Alisema peke yake ,jioni hiyo ,
“ama niendelee kumtafuta ,lakini nitampataje “.
yalikuwa maswali yasiyokuwa na majibu , yakipita ndani ya kichwa cha msichana huyo , hakujua afanye kitu gani ,akili ilichoka kupita maelezo , kwa kuwa alikuwa amechoka sana ,hakutaka tena kuendelea kumtafuta ,alichofanya ni kutafuta hoteli , kesho yake alidamka mapema na kuanza kuzunguka mtaani lakini hakufanikiwa kabisa kumpata ,alirudi hotelini akiwa amechoka, siyo mwili pekee bali hata akili nayo ilichoka , alijihisi mkosefu sana , kumuacha Poul aendelee kuishi maisha hatarishi , muda mwingine alimlaani na kumlaumu mtu aliyemteka , masikini Joan alilia kilio kisicho nyamazika , picha na kumbukumbu wakiwa na Poul zilizidi kupenyeza ndani ya kichwa chake , hadi kunapambazuka siku ya tatu hakuwa amefanikiwa kufanya lolote . Siku hiyo moyo ulisita kutoka nje kabisa , alichokifanya ni kubaki ndani ya hoteli hiyo , alishuka chini ya heteli hiyo kwa lengo la kupata kifungua kinywa ,lakini akiwa njiani kuelekea eneo husika alinasa mazungumzo kati ya wanaume wawili , japo hakuwa mzuri sana katika lugha ya Kiswahili lakini alijikuta akinasa baadhii ya maneno, uwepo wa Poul maishani mwake ulimfanya akaelewa baadhi ya maneno ya Kiswahili .
“ Ndiyo binti ameshaingia ndani ya ngome toka jana , na tunawasiliana naye ,aaaaah! Mambo yako vizuri leo hii jioni tutakamilisha kila kitu ,kwani si anatakiwa kijana tu? “
“ Ndiyo, Poul ndo wa muhimu zaidi , hilo koko la kiarabu achaneni nalo ,ila likileta ubishi liuweni kabisa,”
aliongea David kwa kujiamini kupita maelezo , maneno hayo yalipenya vyema ndani ya ngoma za masikio ya Joan ,maana simu ilikuwa imewekwa kwenye round spika , yeye alikuwa amesimama karibu kabisa na Masoud ,ambaye hakujua kama kulikuwa na mtu mwingine aliyekuwa akisikia Kiswahili tena kwa ufasaha , Joan alihisi moyo ukipasuka ,alitamani kulia kwa sauti lakini alishindwa kufanya vile ,zaidi ya kubaki kimya mithili ya maji ndani ya mtungi , pia alijihapiza kuwafuatilia kila watakokwenda , hakujali kama angeweza kuingia matatizo ama hata kupoteza maisha yake .
****
Hakuna kitu ambacho MacDonald hakukifahamu , kila mipango aliyopanga David aliifahamu ,kuanzia Somalia alikopewa taarifa na kijana wake Omar ambaye pia ni kijana wa Masoud ,Omar alimpenda sana MacDonald kuzidi Masoud , kilichomfanya ampende ni ile roho yake ya upole , kupenda watoto hivyo vilimvutia sana , japo wote walikuwa majambazi lakini walitofautia MacDonalid hakupenda kudhuru watoto tofauti na Masoud ambaye hakujali ,yeye aliwaza pesa tu ,
“Kesho ndiyo tutakuja “
“poa , nawagoja tena acha niachie mitandao ili asishtukie , waendelee kuwasiliana , “
“ fanya nilivyokuambia ,ukombozi wa kijana huyo umewadia “
“ mie tena , anakamatwa kama kuku bandani “
“ ha ha ha ha !”
Walicheka kwa pamoja , kisha simu zikakatwa , MacDonald alibaki na hamu achilia mbali shauku ya kumuona Cindy mrembo aliyesifika kila kona ya Somalia , hakutaka kuwaeleza chochote vijana wake zaidi ya kutunza siri hiyo ndani ya moyo wake ,alibaki akimuhurumia Poul , alizidi kumchukia David kupita maelezo , hakujua ni adhabu ipi ingemfaa ,kila kifo alichokiwaza alikiona hakimfai , alitoa machozi ya hasira , alinyanyuka na kumuacha Poul bustanini , hakutaka chozi lake lionekane mbele ya kijana huyo aliyekuwa akihitaji msaada toka kwake .
Alielekea moja kwa moja chumbani kwake , kitu cha kwanza aliwasha mitambo yake yote ya ulinzi , mawasiliano na kila kitu ,kisha alifungulia mitandao yote ,alibaki akiyatumbua macho yake mbele ya runinga ,kila kitu aliweza kukiona . Omari hakuwa nyuma kumpatia kila taarifa . Aliendelea kuyauma meno kwa hasira huku mawazo yakipita ndani ya kichwa chake , muda mwingine alijilaumu kuchelewa kupambana naye mapema , aliona subira yake ingeweza kuleta madhara kwa kijana huyo .
“ Subiri kupambazuke nitawakomesha washenzi sana , kifo ni halali yake , mipango yake ya damu sasa imefika mwisho , hawezi kuichezea dunia kiasi hiki nami nipo “ .
Alisema peke yake ,kisha alijitupa kitandani na kulala , siku iliyofuata alidamka mapema sana ,kitu cha kwanza alichokifanya ni kufuatilia kila kitu kilichoendelea usiku wa jana , aliweza kuona jinsi walivyoingia ndani ya mgahawa huo , na hata maongezi yote aliweza kuayasikia ,hapo ndipo alipoachia tabasamu mara baada ya kumuona Masoud , mwanzo alidhani ni pande la mtu kama yeye .
“ Hiki kitoto ?,Acha tuone , yawezekana ni njoka la mapangoni “,
Aliongea peke yake , majira ya saa saba mchana alisikia mlango ukingongwa hakuwa na wasiwasi kila kitu alikifahamu , papo hapo alimtoa Poul ,hakutaka aonekane kwa mwanamke huyo , maana alishagundua alikuwa na siraha , sumu kali iliyokuwa na uwezo wa kuua ndani ya dakika mbili , pia alikuwa amevaa kifaa maarumu cha kuzuia risasi mwili mzima ,
“ shenzi taipu atanikoma “ ,
Cindy aliwaza ndani ya moyo wake , hakujua kama kila kitu kilkuiwa kipo wazo , alitembea taratibu huku akiendelea kuwasiliana na Masoud , kupitia kifaa kidogo alichokuwa amekipachika ndani ya sikio lake la kulia , Masoud naye alipeleka taarifa hizo kwa David .
“ Karibu malkia “,
MacDonald alimkaribisha ,mara baada ya Cindy kuikanyanga sebule yake , karibisha hiyo iliambatana na mkono ambao, Cindy aliukwepa kuupoke alihisi kitu japo mara moja hakukifahamu,
“ nashukuru sana “,
aliongea huku akiketi , macho yake yakawa na kazi ya kuikangua nyumba hiyo ,kwa jinsi iliyokuwa imejengwa hakuweza kuambulia kupata chochote zaidi ya kungundua kamera ya CCTV basi ,
“ sijui nikusaidie nini ?”
“ Naitwa Husna natokea Tanzania ni mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite ,nilikuwa natafuta soko ndani ya china ,sasa nimeelekezwa wewe ni dalali “ ,
aliongea kwa lugha ya kingereza ,
“ yaaaah! Ndiyooo……….ila kwa sasa ……….nita…………” ,
MacDonald alishindwa kuongea vizuri baada ya kumuona Cindy akipeleka muguu wake wa kushoto upande wa kamera hiyo iliyokuwa imefungwa chini ya kiti alichokuwa amekalia .
“ Stop {acha} unach…………”
“ usilete ujinga tulia vivyo hivyo wewe koko la kiarabu ,ulijua mie fala ,nakutafuta kwa muda mrefu sana ,yuko wapi Poul ?“
Cindy aliongea, huku akiwa amesimama , mikono yake yote ikiwa na bastola tena zikiwa tayari kwa kazi , jinsi alivyosimama kwa haraka , hata mwenyeji wake alikiri moyoni kuwa mdada huyo hakuwa mtu wa kuchezea , ilibidi aachia tabasamu la kumpumbaza , huku akiwa amekaa , alitumia dakika moja kumsoma , moyo wake haukuwa na wasiwasi kabisa , kwani hayo aliyatengemea toka mapema , hata hiyo kamera aliitegesha makusudi eneo hilo , pia alipanga kiti hicho ndicho Cindy angekalia .
“ Naongea na wewe yuko wapi , nina dakika tatu tu za kuendelea kukaa humu , ukileta ujinga nitakifumua kichwa chako , han*** wa kiume “.
Hakuna kitu kilichomuuma MacDonald kama kuitwa jina hilo ,tena na msichana mdogo , aliyauma meno kwa hasira,
,” sasa nakuonesha uhan*** wangu nina watoto saba leo unaniita hivyo mshenzi mkubwa “.
Aliongea kimoyo moyo ,maneno hayo nyenye uchungu ndani yake .
Hakutaka kukurupuka alichofanya ni kunyosha mikono juu kama alivyokuwa ameamriwa na Cindy ,
“tangulia “,CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
alianza kutembea huku akiwa vivyo hivyo , hatua tano alisimama ghafla na kuzungusha mguu wake wa kushoto uliopelekea Cindy kupokea teke la mbavu , risasi zaidi ya tano zilifyatuka hovyo ,bastola zote zikitoka mikononi mwake , akiwa bado anashangaa alijikuta akiangukia mikononi mwa MacDonald , mikono iliyokuwa na sugu achilia mbali nguvu .
“ Nieleze nani aliyekutuma ?”
“ Jamani mpenzi mwaaaah!”
Badala ya kujibu swali alianza kumbusu hovyo hovyo mwanaume huyo , alijua kufanya vile kungepelekea yeye kufanikisha adhima yake ,lakini alijikuta akipokea makofi makali sana ,
“ nawajua ninyi ni nyoka ,tena nyoka wenye sumu kali , usinifikilie mie ni fala kama mafala hao , sasa utajuta kunifahamu “.
Alimyanyua juu juu na kumfungia ndani ya chumba kilichokuwa na joto kali sana , kisha alilejea kwa Poul ,
“ naomba ujifiche kule kwenye mashine , usitoke wewe endelea kufatilia kila kinachoendelea , baba yako katuma tena watu “
“ sawa ila kwanini usiniruhusu niende kumuua kwa mkono wangu baba ?”
“ kuwa na subira ,wakati ukifika utafanya hivyo ,nakupenda sana “.
Hakuta kupoteza muda alichofanya ni kuondoka eneo hilo ,
“ naomba ufuate nitakachokueleza ,ukileta ubishi nakuangamiza sasa hivi , ongea na mbwa wenzio waje hapa mara moja “,
alimuamru Cindy mara baada ya kurudi tena ndani ya chumba
“ sitaki “
“ hunijui .“
Alipiga hatua tatu ya nne ilikuwa ngumi kali sana ,ngumi hiyo iliupasua vyema mdoma wa Cindy , toka aanze kazi hiyo miaka kumi iliyopita hakuwahi kukutana na mtu mwenye ngumi nzito na kali kiasi kile , alihisi nyota nyota ndani ya macho yake ,
“ sina utani ,nakukata kiungo kimoja baada ya kingine , sina huruma hata kidogo , nilifanyiwa upasuaji wa kutoa mishipa ya huruma ndani ya mwili wangu ,hivyo usidhani sijui hao wako wapi ,wamo ndani ya xchun “.
Kwa muonekano tu wa sura na macho , hakuwa akitania alichokizungumza ,
Cindy kusikia jina la hoteli alishaangaa sana , hapo ndipo alipoanza kuayaamini maneno ya watu , alitamani kukimbia lakini kamba alizokuwa amefungwa zilimzuia , pia alihofia kuangukia ndani ya tindikali .
“ unaona pipa hilo ?”,
Alisema huku akliisonta usawa wa pipa hilo, kwa kidole chake cha shahada ,pipi lililokuwa limejaa tindikali
“ ndi …yoo”
“ utazikwa humo endapo utaendelea kunizungusha , ongea na mbwa hao haraka “.
Kwa jinsi alivyokuwa akiteseka kwa maumivu hakuwa mbishi , alianza kuongea na Masoud pamoja na Omar akiwataka wafike eneo hilo kwani alikuwa amefanikiwa kumkamata MacDonald , Masoud alihisi ushindi wa hatari , alishangilia shangwe zisizo pimika , papo hapo aliongea na David ,huku akimsistiza kuandaa idadi ya pesa waliyokuwa wamekubaliana .
“ Mashikaji mambo safi “
“ Kweli ?”
“ Aaaaah ! Unacheza na Cindy namba nyingine hiyo “
“ aiseeee! Safi sana , kwahiyo twende mida hii ?”
“ Hapana twenda usiku , sitaki China ifahamu chochote , tunachinja na kurejea nyumbani usiku huo huo “
“ poa , tena itakuwa guda sana “.
Waliendelea kunywa kwa furaha ,huku kila mtu akiwaza yake , Omar alijifanya mtu mwema sana kwa Masoud lakini kila kitu alimjuza MacDonald ,hilo lilizidi kumpa tumaini MaCDonald , naye alijipanga kwa ujio huo , ujio huo pia aliutolea taarifa kwa vijana wake Hassan na Run snake .
Ilikuwa saa mbili na dakika kumi za usiku, ngome ya MacDonald ilivamiwa , wanaume wawili waliokuwa wamevalia mavazi ya kininja walikuwa wakitambaa taratibu nje ya ngome hiyo ,mithili ya mwendo wa nyoka , kwa jinsi walivyonekana wakitambaa hakika walionekana wataramu sana , walipolifikia lango kubwa walijikata Masoud alitangulia huku Omar akibaki nyuma , hiyo yote ilikuwa mipango ya Omar, kwa kuwa hakuifahamu ngome hiyo alijikuta akiangukia mikononi mwa Run snake aliyeanza kumshambulia kwa ngumi , naye kuona hivyo alianza kumshambulia kwa risasi na bahati mbaya Snake Run alipingwa risasi ya kifua iliyopelekea apoteze maisha yake .
“ Kaua kijana wako mmoja “
“ nini ?”
“ Rubani wako ameuawa “
“ Astaghfirullah! Kafa Snake wangu ?’
“ Ndiyo “
“ namfuata sasa hivi “
“ pitia geti la tatu ,yupo karibu na mchikichi ,kule kwenye giza ,fanya haraka sana “.
Yalikuwa ni mazungumzo kati ya Omar na MacDonad ,yaliyofanyika kwa siri sana , kabla ya kutoka alihakikisha mawasiliano yote anayazima , hivyo Masoud alishindwa kuwasiliana na Omar wala Cindy , pia alimficha Poul chini ya handaki ,na taa zote alizizima hali hiyo ilimtisha sana Masoud , hakujua ampatie wapi Omar,
“hapo sawa , tuma kijana wako aje anikamate , na ahakikishe ananipiga risasi hata mbili za miguuni ili tupoteze ushahidi , kisha nawe ukamkamate bado anahah a”
, mpango huo ulizidi kumfurahisha sana MacDOonald , na hakutaka kupoteza muda ,Hassan alipatiwa taarifa hizo naye alitekeleza mara moja , alitambaa taratibu hadi eneo hilo na alipolikaribia alimweleza Poul kuwasha taa , taa zilipowaka tu MacDonald alijitokeza mbele ya Masoud ,
“ paaaa!Paaaaa! “
Zilikuwa ni sauti za makofi zikimpongeza Masoud ,
“ bwana mdogo karibu kaburini , nadhani umechoka kuishi duniani nami sioni haja ya kukupeleka pahali unapopataka “
MacDonald alisema , huku akipiga hatua kumfuata Masoud ,kabla hajamfikia alishangaa kumuona akiruka sarakasi kisha alitua kifuani kwake ,kidogo MacDonald aanguke ,lakini alijiwahi na kunyanyuka , alirudi nyuma kama nusu mita na aliporudi alirudi kama mwendo wa umeme , na kutua kifuani kwa Masoud , moja kwa moja aliangukia mtaloni ,
“ sitaki kukuua kirahisi hivi ,naomba nikuonyeshe kazi kwanza , “
jinsi alivyokuwa na hasira alianza kumshambulia kwa kila aina ya pigo , japo naye alijaribu kujibu lakini alijikuta akizidiwa nguvu .
“ Nielezeni nani aliyewatuma ?
Aliwauliza wote , mara baada ya kuwakusanya sehemu moja , kwa jinsi Omar alivyojiweka ilikuwa ngumu sana mwenzake kumtambua , siri hiyo ilikuwa yake na MacDonald,
“ hakuna mtu “
“ kweli ?”
“ Ndiyo , “
Masoud alijibu kwa nyodo , hakutaka kumnyenyekea mwanaume mwenzake , alikuwa radhi kufa kuliko kuongea , japo alipigwa kipigo cha mbwa lakini hakudhubutu kuongea chochote , hadi anapoteza maisha hakuweza kumtaja David .
“ Sasa tuonaondo kwenda Tanzania mida hii , Hassan naomba ukamtupie ndani ya pipa huyu boya ,pia na yule demu muunganishe humo humo ,usisahau kuja na Poul “
Hassan alitekeleza hayo ,dakika saba alilejea akiwa na Poul aliyekuwa akilia ,kilio cha hasira , hakuja kwanini ,baba yake mdogo alikuwa akiendelea kumfuatilia , wakiwa bado wanajadili namna ya kusafiri walisikia sauti ya nyayo za mtu akitembea wote walishtuka, hakuna aliyeweza kumfahamu mtu huyo.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Joan alihakikisha anafuatilia kila nyendo za wanaume hao , aliamini kufanya vile kungemrahisishia kumpata Poul, japo alijua ni watu hatari , lakini hakutaka kukata tamaa, alikuwa radhi kuyapoteza maisha yake lakini ampate Poul , hata chai hakutaka kunywa tena , alibaki amesimama eneo hilo macho yake akimkangua mmoja baada ya mwingine , muda mwingine alitamani kuongea nao ,lakini alijikuta akipata woga , alipoona wameelekea chumbani kwao aliwafuatilia kwa nyuma ,hadi alipohakikisha anakifahamu chumba cha wanaume hao ,
“ naomba chai “ ,
alipiga simu sehemu husika
“ sawa “ ,
dakika tano mlango wa chumba chake uligongwa , kwa kuwa ulikuwa wazi hakuhangaika kunyanyuka alichofanya ni kumuomba muhudumu huyo kuingia mara moja .
“ sijui unaweza kunisaidia kitu dada ?”
“Kitu! Gani ?’
“ Aaaah ! Kuna wanaume wawili wapo chumba namba 453, naomba wakitoka unijuze “
“ hiyo siyo kazi yetu , siye tupo kwa ajili ya kuwahudumia ninnyi, na siyo kuchunga ka…”
“ dada usipende kuongea sana , kwani bei gani ?”
Joan aliongea, huku akiwa amemtazama machoni msichana huyo, aliyekuwa amestajabishwa na maneno ya msichana huyo mdogo , hakujua ujasiri huo kaliutoa wapi, kiumri kalikuwa kadogo sana , hata hakakustahili kuwa kaongeaji kiasi hicho ,
“ unaweza ukanipa kiasi gani labda ?”
Aliongea kwa nyodo za hali ya juu ,msichana huyo wa kichina , macho yake tu yaliashiria umaringo wa hali ya juu ,lakini hilo Joan hakulijali ,alichojali yeye ni kufanyiwa kazi yake , alijifunika vizuri sura yake ,kisha alichuku kipochi chake kidogo na kufungua , alitao idadi nyingi za noti na kuzitupia miguuni mwa msichana huyo ,aliyeyatoa macho yake mithili ya mwizi aliyekamatwa ,kwa picha ya haraka –haraka zilikuwa ni pesa nyingi sana,
“ okay nakuhakikishia ushindi “
“ fanya kweli , “
“poa “.
Alitoka akiwa haamini ,kama kitoto kile kingeweza kuwa na pesa zote hizo , hata alipozihesabu ilikuwa mishara yake ya miezi mitatu , na ili kuzifanyia kazi pesa hizo alikuwa makini kupita maelezo , usiku wa saa moja alimpatia taarifa ya kuondoka kwa wanaume hao ndani ya hoteli hiyo ,alitoka haraka sana na kuanza kuwafuatilia kila walikopita alikuwa nyuma yao , hadi wanaikaribia ngome ya MacDonald . Alitembea kwa tahadhali sana huku akiwa amejificha ficha , hakutaka kukurupuka sana alichofanya ni kutulia kwanza nje ,sehemu aliyoiona inamfaa zaidi , akiwa bado amesimama eneo hilo ghafla walitokea wanaume wawili mmoja alifanania na baba yake ,japo kulikuwa na giza ,lakini aliweza kumtambu vyema , alihisi moyo kumpasuka, alitembea taratibu kuelekea usawa uliokuwa na giza zaidi ,akawa anasikiliza kile kilichokuwa kikiendelea .
“ kweli umemuona akielekea huku?”Alimuuliza kwa lugha ya kichina ,
“ ndiyo , tena alikuwa anawafuatilia wanaume wawili “
“ unauhakika na ulisemalo ?”
“ Mjomba mie ndiye Shayyu , sikosei kazi yangu ,nimezaliwa China ,na nimekulia China, kila kitu nakifanya kwa akili , binti yako yuko hapa hapa, wewe nitoe changu ,handasi zinazidi “
, kijana aliyekuwa amejitolea kumsaidia baba yake Joan toka alipoingia ndani ya mji huo , mara nyingi kazi zake alizifanyia ndani ya hoteli , kwani aliamini humo ndimo watu hujificha , japo hakuwa na uhakika na binti huyo alipomuona kwa mara ya kwanza akitoka ndani ya hoteli , lakini alijiaminisha kuwa ndiye! Kweli alipatia, Mohammed hakuyaamini maneno ya kijana huyo ,mara moja kutokana na muonekano wake wa uteja teja ,lakini alijikuta akiyaamini japo kwa asilimia ndogo sana , ilibidi amtoe kiasi kidogo cha pesa na kuahidi kumuongeza kiasi kilichobaki mara baada ya kufanikisha zoezi yake .
Alianza kutembea taratibu kuingia ndani ya ngome hiyo ,iliyokuwa ikiyatisha macho yake , hatua chache aliuona mwili wa Run Snake ukiwa umetapakaa damu ,hapo ndipo alipoamua kuwa makini , alitoa sirasha yake ndani ya suruali na kuishika mkononi , jinsi alivyokuwa akinyanta ilionyesha alipitia mazoezi flaani ,baada ya kutembea umbali wa hatua kadhaa alisikia mabishano , kidogo alitulia kusikliza ,akiwa bado haja kaa vizuri masikio yake alipokea milio mitatu ya risasi , kisha kikasikika kilio cha mtu na baadaye kimya kikatawala , mara moja hakufahamu kikilichokuwa kiendelea ,
“ Kweli mwanangu yumo humu ?”
Alijiuliza peke yake , akiwa bado amesimama eneo hilo kwa tahadhali ya hali ya juu , dakiaka tano alisikia tena mazungumzo ,hapo ndipo alipoamu kutembea kwa kuvuruta miguu yake , aliona afanye hivyo ili kuwapa nafasi watu hao kumsikia yeye , ghafla taa zilizimwa ,alishituka sana ,macho yake yakapokelewa na giza tororo , akiwa bado hajapata jawabu la mazingira hayo ,kwa mbali aliona kivuli mfano wa mtu kikija eneo hilo , hakutaka kukimbia alichokifanya ni kupiga hatua kukifuata .
“ mikono juu “
Alitoa amri ambayo haikutekelezwa na kiumbe hicho ,zaidi kilizidi kusogea eneo alilokuwa amesimama,
“ukileta ubishi naku,,,,,,,,,,,,,”
“nawe nyosha mikono juu “
Mohammed alijikuta akikatishwa sentensi yake ,na pande la mtu , mara moja hakuweza kumfahamu mtu huyo ila baada ya taa kuwaka alijikuta akitetemeka mwili mzima , hakuamini kama siku hiyo angeweza kuangukia mikononi mwa MacDonald , alimfahamu toka zamani , hakuweza kufanya chochote zaidi ya kutekeleza kile alichoambiwa ,
“ unatafuta nini hapa ?”
“ Na…namf…uata mwanagu “
“ mwanao?”
MacDonald aliuliza kwa mshangao , hakujua ni mtoto yupi aliyekuwa anatafutwa ,wakati alikuwa na Poul tu ndani ya nyumba hiyo ,
“ nimetokea Iran … nimeambiwa mwanangu yumo humu tafadhali nipe mwanagu “.
Alizidi kujitete ,huku mikono yake akiwa ameikunyanta kwa mbele ,kwa jinsi alivyoonekana, usingeweza kuamini kama alikuwa mtu mkubwa, na aliye heshimika ndani na nje ya Iran ,
“ anaitwa nani ?”
“Joannnnnnn!”CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sauti nyororo na yenye utoto ndani yake ilipenya vyema ndani ya ngoma za masikio ya watu hao , wote walibaki wakistajabu , msichana aliyekuwa amejifunika mwili mzima alisimama mbele yao .
“ Joan mwanagu um……….”
“kimya !Unatafuta nini hapa binti ?”
MacDonald aliuliza huku akimfuata msichana huyo aliyekuwa umbali kidogo , Joan aliamua kujificha mara baada ya kumuona MacDonald akimfuata baba yake , ambaye alikuwa amempa mgongo mwanaume huyo . Ila baada ya kumuona baba yake akitaka kuingia matatizo aliamua kujitokeza angalau aweze kujaribu kuyaokoa maisha ya mzee wake .
“Hassan kamata hao na ufunge kamba ,wapeleke gerezani “,
alitoa amri na ilitekelezwa mara moja , lakini wakiwa wanaelekea huku Poul aliweza kumuona Joan ,
“Joannnn!!!!
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment