Search This Blog

Friday, July 15, 2022

KICHAA - 4

 







    Simulizi : Kichaa

    Sehemu Ya Nne (4)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Ha! Sasa mbona unashangaa hivyo. Simaanishi malaika wa mbiguni. Mi namuongelea mtoto Neema. Yule ambae, akitoka Mama anaingia yeye. Hapo mtoto akanipa salamu, siunajua kuna kaugomvi kati yangu nayeye? Nikamwambia hayo yaishe, nae akasema kashapotezea, nikajisemea 'Yes, game over' namimi nikasema lazma nimtupie maswaga niliyopewa na Side. Mwanangu nikaanza kutupa maneno matamu hadi mwenyewe nayatamani. Nimemuimbisha wee hadi akatoa kikaratasi. Kuja kukisoma, mtoto amekubali. Nilipata shangwe, nikakimbia hadi home. Siunajua bimkubwa alivyo na kaunene ka aina? Sasa mie nilimbebelea juujuu. Huwezi amini kwafuraha tu. Hadi nilijikuta nataka kuropoka mbele ya bimkubwa. Ila nikavunga kiana" Aliongea Musa huku furaha ikiendelea kumjaa vilivyo mwilini na moyoni mwake.



    "ok, hatua nzuri. Sasa hapa chamsingi ni wewe kumvizia nyumbani kwao. Siunajua tena huyo dogo bado kabisa. Sasa anaweza kufikiria mara yapili na sumu yako akaifyonza yote. Tena nenda muda huuhuu. Kaongeze max. Siunajua huu ndio mtihani wa somo la mapenzi. Nenda kaufanye poa." Kitendo bila kuchelewa, Musa aliamua kuondoka na kwenda moja kwa moja hadi kwa kina Neema, alipofika. Hakuna aliyemkuta zaidi ya Neema pekee. Siku hiyo waliongea mengi na wakafungua rasmi ukurasa wa penzi lao."



    * ** *



    Jijini dar-es-salaam. Maeneo ya masaki. Moja kati ya nyumba zilizojengeka vilivyo kwa uimara na uzuri. Muheshimiwa, Pita Mwambe, anaendelea kufurahia na mke wake pamoja na watoto wake wawili ambao mmoja kati yao ni wakiume kwa jina la John, huku wapili akiwa ni wakike kwa jina la Esta. Mheshimiwa Pita, yeye alikuwa na maisha ya furaha siku zote. Alikuwa na kitambi laini kilichodhihirisha shibe yake. Huku, nguo nyadhifu zikiendelea kuwafanya watu wasiomfahamu. Kumuita tajiri, au kumvika cheo chochote kiendanacho na mavazi yake. Akiwa anaendelea kupiga soga kwa kukejeliana huku wakichekeshana na familia yake. Mara ghafla, alipigiwa simu. Kwa manjonjo na jeuri ya pesa, aliichukuwa simu yake na kuisoma kwenye kioo. Aliitambua kisha akaiweka sikioni.



    "Hello, Muheshimiwa!" Iliongea sauti ya upande wa pili wa simu yake.



    "Enhee! Nakusikia?."



    "Muheshimiwa.. Mimi ndio yule, mlezi wa watoto yatima kwenye kile kituo ulichotembelea jana. Nilikuwa tu. Nakukumbusha kuhusu ile ahadi yako, ya vyakula ulivyoahidi. Vipi? Maana bado hatujavipata."



    "Kuhusu jambo hilo, usijali.. Nilikuwa nimesahau tu. Ila muda si,mrefu vitakuwa hapo. Ngoja niongee na vijana wangu ili wavilete." Akashukuru, kisha simu ikakatwa. Nikawaida yake kuwasaidia wananchi wake pasina kujali matabaka. Ingawa amefunikwa na shuka zito tena jeusi la utajili, lakini hiyo haikumfanya yeye asiwaone masikini. Kila leo alitoa msaada na nikipenzi cha watu sana. Hakuna anae mchukia.



    . Alimuita Sam, kijana mwenye mwili uliyotengemaa kwa kuzoea mazoezi magumu afanyayo kila siku. Alipomuita akamuagiza kupeleka chakula kwenye kituo cha kulelea watoto yatima. Alipomaliza kutoa maagizo hapohapo Sam akachukuwa vijana kadhaa na kupanda nao kwenye gari moja kwa moja hadi super market wakanunua mahtaji kisha wakayaweka garini na moja kwa moja wakaelekea kwenye kituo kile cha kulelea watoto yatima. Walipofika wakaonana na uongozi wa kituo kile kisha wakatoa msaada.



    "Napenda kuchukua nafasi hii kutoa shukurani za dhati kwa niaba ya wahusika wa kituo hichi. Hatuna chakuwalipa bali maombi pekee ndio malipo yetu. Mwenyezi awabariki, azidishe kipato chenu na awaongezee umri mrefu ilimuendelee kutoa msaada kwa wenye shida. Hatuna ziada zaidi ya kuwaomba tu muendelee kuwa na moyo huohuo." Alitoa shukurani, Mlezi wa watoto wale ajulikanae kwa jina la Magrena. Ni mama wa makamu, mpole, mstaarabu, na mengineyo mengi yanayofanana na hayo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kushukuriwa kwa Kundi hilo la Muheshimiwa pita Mwambe, kwao ilikuwa ni kawaida. Hata sifa sasa walikuwa wameshazizoea hivyo walipomaliza kupewa shukurani, hawa kubweteka pale. Walirudi kwenye usafiri wao na kujirejesha moja kwa moja hadi maskani kwao. Walipofika walishuka huku wote kwa pamoja wakiwa wamevalia suti nyeusi, viatu, mpaka kofia. Walirejea katika sehemu zao na kuendelea kuweka ulinzi ndani ya nyumba hiyo kubwa na yenye kuvutia.



    Sam, alirejesha taarifa kwa Muheshimiwa baada ya haponae pia alienda kufanya ulinzi.



    Muheshimiwa Mwambe alikuwa akiendelea kufurahi na wanae huku akiwa sihi wasome kwa bidii. Hakika ni ukimuona utajua moja kwa moja kuwa ni mpenda maendeleo na mtu mwenyekupenda kusaidia wenzake.



    ..... .... ... ...



    Kila kichaa hutembelewa na ndugu rafiki pamoja na jamaa kila ifikapo siku ya kutembelewa isipokuwa Mavugo ambae nikama hakuwa na ndugu wala jamaa, nae hakuwa hata na muda wa kuhtaji kutembelewa. Kila siku za kutembelewa, yeye huwa bize na mambo yake. Hata maafande waliokuwa wa kimtembelea zamani. Waliacha baada ya kubaini umakini wa ugonjwa aliyonao mfungwa wao. Kwa mujibu wa sheria, walimuacha huru kwani waliamini uwezekano wa yeye kupona ni mdogo sana.



    "Mammaaa... Nipelekeni nyumbani.. Huku hakuna hata matope ya kuchezea. Kila siku sivui samaki japo nina tega kwenye bakuli langu. Mistaki kuchomwa sindano... Nirudisheni tuu" Ni kawaida ya vichaa kutoa visingizio vyao kwa ndugu zao ilimradi tu, waombe kutolewa pale na hiyo ilikuwa ni sauti ya kichaa mmoja aliyekuwa akijitetea mbele ya Mama yake.



    Kichaa mwingine yeye kila ndugu zake walipomuongelesha, hakuwajibu zaidi ya kuwacheka tu, huku mwingine akileta fujo na kuharibu haribu zawadi kitendo kinachopelekea achomwe sindano za usingizi tu. Kuna wale vichaa ambao kazi yao kubwa ni kutoa mate midomoni mwao muda wote pasina kujali kuwa robo tatu ya mwili wa binadamu ni maji.



    Ndugu msomaji, kama unampenda ndugu yako hebu tafuta tiba kwa hali na mali iliapone nasio kumpeleka kwenye hospitali ya vichaa. Hakika kule ni kumuongezea ukichaa tu. Nasio kumpatia tiba kuna kila aina ya vichaa na ukimpeleka nduguyo lazma uamini hilo hakika chozi halitosita kukutoka kama hauwezi kuvumilia mateso wayapatayo binadamu wenzako ambao wamerukwa na akili.



    "Mavugo, mbona umejiinamia tu. Unawaza nini?" Aliongea docta Endrew huku akimshika kichwa Kichaa Mavugo.



    "Najaribu kuwaza tu. Hivi, hii dunia kwanini kila inavyojizungusha ndivyo binadamu wanazidi kuchanganyikiwa. Hebu mtazame yule pale binadamu." Akasontesha mkono mbele ya Kichaa moja ambae yeye alikuwa anajiwasha makofi yanguvu muda wote huku akilia kutokana na maumivu aliyokuwa akiyapata, na pindi aliposhikwa mikono na nduguze waliyokuja kumuona. Alikuwa akikasirika na kujibadilishia adhabu. Kutoka kwenye kujiwasha makofi hadi kujibamiza kwenye meza. Hakika ni mateso makubwa aliyoendelea kujipa, si kwamba haumii. La. Bali anashindwa kujizuia na adhabu ile ya kujipa mwenyewe.



    Docta Endrew, alipotazama adhabu ile aliyoendelea kujipa kichaa yule, aliumia sana na kuchukua sindano ya usingizi iliakamchome na kumuondoa kwenye mateso yale kwa muda. Lakini Mavugo alimzuia na kumwambia kuwa, "Huwezi kukuwa bila kutazama matatizo." Hapo docta Endrew akapinga.



    "Lakini Mavugo, matatizo mengine hayavumiliki. Hebu ona anavyojiumiza. Dah! Mpaka nauhisi moyo wangu unaruka."



    "Docta.... Kila kifanyikapo ndani ya hii dunia. Nifunzo tosha... Usimchome sindano angali bado anatamani kuongea na ndugu zake. Sindano yako haina uwezo wa kuunda akili bali inamdhoofisha tu. Jaribu kufikilia hata kama ni wewe ungekuwa ukikubali kuchomwa sindano nyingi kiasi kile kwa siku? Basi muache, huenda ni somo bora la kitisho kwa ndugu zake. Na hapo ndipo Mungu anaonesha ufahari mbele ya waja wake."



    Docta Endrew huwa anamuheshimu kichaa Mavugo. Lakini si kila aongealo hulifuata. Hapo akatoka na kwenda kumchoma sindano za usingizi Kichaa yule aliyeendelea kujipa mateso.



    Alipomchoma sindano akasinzia moja kwa moja wakambeba na kumpeleka wodini. Alipotoka huko akarejea moja kwa moja hadi alipomuacha Mavugo. Alimkuta, wakacheka kwa pamoja kutokana na vituko ndani ya maongezi yao. Docta Endrew alijitahidi kumpeleleza Mavugo juu ya anachokumbuka maishani mwake lakini ni wazi kuwa Mavugo nikama alikuwa hakumbuki chochote zaidi alikuwa akiishikilia ile picha aliyopiga yeye, mtoto mmoja, mwanamke pamoja na keki tu.



    Kichaa mmoja aliwaita wenzake na kuwataka watoroke kwa siri kwani hawakupenda kukaa hospitali mule. Wenzake walimsikia na kufuata alichosema huku Mavugo yeye akiwapinga vilivyo walipogoma na kuhtaji waliloamua liwe ndipo akachukua chaki kishaaka chora mlango ubaoni,



    "Anhaa! Anatufungia mlango eti? Basi tunaubomoa huohuo." Aliongea kiongozi wavichaa wale wenye mpango wa kutoroka. Wote kwa pamoja wakajipanga na akili zao zikawa zinawatuma waendelee kubomoa ule mlango. Ungewaona walivyohangaika, mara kusukuma ubao ule uliochorwa mlango, mara kuupiga vichwa kwakuzani kuwa huenda wakaufungua mlango ule. Walihangaika huku Mavugo akiwaacha na kujua kuwa tayari amewakomesha.



    "Naona muda huu tumechoka. Hii inatokana na mlango kuwa mgumu sana kufunguka. Hivyo tunahitajika kwenda kupumzika na kesho mapema tuwahi na nguvu mpya kisha tuubomoe tena ilitutoroke. Tumechoka na manyanyaso." Alipomaliza kuongea mkubwa wao, wote walirudi na kujilaza.



    Hayo ndio maisha aliyoishi Mavugo hospitali hapo.



    Kila usiku ulipofika yeye alikuwa ni mtu wa kuingalia picha yake na kukumbuka tu ahadi za mwanae pindi alipokuwa akitoa ahadi ya uandishi wa habari. Hakuna kingine alichokumbuka, ingawa alikumbuka jambo hilo. Lakini nalo halikuweza kumsaidia kujitambua hata kidogo. Kila siku alilala kwa mateso makali ya kukumbuka jambo fulani maishani mwake.



    "Hivi docta Izack, we unadhani huyu Mavugo itakuwa rahisi kumponyesha?" Aliongea docta Endrew.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Kiukweli hapo sijui. Lakini kama vipimo vilivyosema, anahtajika kumuona mtu atakaemfanya akumbuke mambo yote na hapo ndipo akili zitakapomrejea. Lakini kinyume na hivyo. Hapo hakuna msaada wa aina yeyote. Kama unavyojua, kwa hapa hospital sivirahisi kumpata mtu ambae ni ndugu yake mwenye uwezo wa kurejesha kumbukumbu zote za Mavugo. Labda miningetoa wazo. Itafaa zaidi, endapo tukiiiba ile picha yake na kwenda kuitangaza kwenye media mbalimbali, huenda waliopo kwenye hiyo picha wakajitokeza na huo ndo ukawa msaada wakumsaidia yeye." Aliongea docta Izack.



    Wazo la docta Izack, lilichambuliwa na kuonekana lipo sawa. Wakakubaliana kuhusu kuiba picha ya Mavugo, lakini pia wakapinga suala la kutangaza picha ile kwenye media kwakuhofia usalama wa Mavugo.



    .... .... ....



    Siku zilipita, miezi, hatimae miaka kadhaa. Neema na Musa penzi lao lilinoga sana, na kwa wakati huo Musa alikuwa akijihusisha na kazi za mtaani kutokana na kushindwa kuendelea na kidato cha tano. Si kwamba alifeli, hapana. Bali ni majukumu tu, yalimbana. Mama yake kwa wakati huo hakuwa mwenye kujiweza hivyo ilimbidi yeye ayachukue majukumu yote ya familia akiwa na umri wa miaka ishirini kwa kipindi hicho, suala la Musa kuishia njiani, halikumfanya Neema amchukie wala asimjali. Zaidi aliongeza upendo, ingawa alikuwa akisoma kwenye moja kati ya shule za bweni hapo Mwanza lakini hakuacha kumuwaza mpenzi wake hata kidogo. Kila ilipofika likizo alienda kumtembelea Mama yake na Musa, na kumsaidia kazi ndogo ndogo. Mama Neema alilijua penzi la Musa na mwanae lakini alilistahi na kumsihi mwanae kuwa awe makini sana. Mawaidha ya Ma. Neema, ndio ukombozi wake kwani aliyasikiliza na kuyapa nafasi ya kumuathiri moyoni mwake, jambo lililopelekea kujihadhari na kufanya mapenzi na Mavugo, ahadi wakaweka kwamba. Watafanya tendo baada ya kuwa mke na mume. Hakuna kati yao aliepinga Musa aliendelea kujishughulisha mtaani huku Neema shuleni ilimradi tu mwisho wa siku wajenge familia njema.



    Hicho kidogo alichokipata mtaani, ndicho alichokula na mama yake nyumbani. Hali ya Mama Musa iliendelea kuwa mbaya kutokana na maisha magumu. Kwakuwa hakukuwa na pesa za kutosha kwa ajili ya kumpeleka hospitali iliatibu magonjwa yaliyoendelea kumtokea, aliamua kukaa nyumbani kana kwamba haumwi. Musa yeye ndio baba, pia ndio mama huku kazi anayoitegemea ni ya uoshaji magari wa kujitegemea. Yaani anasubiria gari lipack sehemu, akitoka mwenye gari, hapo Musa anajikimbiza na ndoo yake kwa haraka anachukua tambala na sabuni kisha anaosha, kazi hiyo ilikuwa na changamoto nyingi sana ikiwemo kufanyakazi bila malipo kwani hakukuwa na makubaliano baina ya muoshewa gari na muosha gari.



    Huku nako kwa Neema, alikiheshimu kitabu. Kilipoanguka, alikiokota na kukibusu, kisha akachukuwa kisomo. Miguu yake alikuwa akiiweka ndani ya karai lake dogo lenye maji iliajisomee na kuuepuka usingizi. Darasani alifanya vizuri huku kwenye upande wa michezo akifanya vizuri pia.



    Kiufupi Neema hakuujua usingizi kivile kwani ratiba yake ya masomo iliubana sana usingizi wake. Siku nzima aliimaliza darasani huku usiku wa siku hiyo akiumalizia kwenye kujisomea mwenyewe, ni zaidi ya adhabu aliyoamua kujipa huku akiamini kuwa lazma angekuja achana nayo.

    Wanafunzi wengi wa kiume walivutiwa na sura yake huku wengine wakivutiwa na maungo yake ambayo yalitanuka vilivyo. Kila walipomfuata waliishia kujilaumu tu kwani Neema ni kama hakuwa na muda wa kuwa na mvulana. Yeye zake ni masomo tu.



    "Hivi, Anna... We unadhani kweli, Neema atakuwa hana mshikaji kweli." Aliuliza mvulana mmoja kwa jina la brian. Kaka mkuu wa shule ile, pia ni mmoja kati ya wavulana ambao walishamfuata Neema lakini wasikubaliwe.



    "Nikweli, Neema hana mvulana mbona huamini? Kwani vipi. Na wewe umetolewa nje?" Alijibu Anna ambae ni rafiki wa karibu wa Neema.



    Brian huku akitoa misonyo ambayo haieleweki kama ni yakujilaumu au yakujidharau au yanini. Alijibu huku akikikuna kichwa chake kana kwamba kimejaa wadudu chungu. "Yaani Anna huwezi amini. Amenitolea nje pasina kuangalia skafu wala tai niloivaa. Minashangaa mpaka sasa, inamaana kuna mtanashati kama mimi kwenye shule hii anaemzuzua au ile amri ya kuwaruhusu wavulana wote wavaemashati ya mikono mirefu ndio imepelekea kila mtu awe kambale eti! Sasa we ngoja, siananichomolea mimi kilagia. Achanimuoneshe kwamba mimi ndio mwenye cheo kikubwa shuleni hapa. Yaani, naenda kuongea na kiongozi wa toi, nikitoka hapo naenda kwa stoo kipa, nikitokahapo naenda kwa dispilini prifekti. Huko kote naenda kumchafulia tu. Ilikila siku hapa shuleni aione chungu. Na kwa taarifa yako, lazma ajilete tena kwa kuomba msamaha. Allaaah! Mimi ndio brian mwingine toleo feki" Alipomaliza akanyanyuka darasani na kwenda kutekeleza yale aliyoongea mbele ya Anna.



    Neema alianza kupatiwa adhabu sikubaada ya siku huku akiambiwa kama akitaka kusamehewa basi amkubali kaka mkuu. Maskini Neema kila siku anadeki vyoo, anapanga vifaa store, anapewa makosa yakinidhamu na kupata adhabu. Afanye nini wakati hana cheo shuleni, amlalamikie kiongozi gani matatizo yake ilhali kiongozi mkubwa ndie atoaye amri ya mateso apewayo. Aliona bora apewe adhabu kulikokufungua ukurasa mwingine wa mapenzi ambao hata hakuwa na shidanao.



    Upande wa Musa, yeye aliendelea kuhangaika hivyohivyo kiume.



    Siku zote hakupata, hata siku alizolala njaa yeye, hakuweza kukubali na mama yake alale njaa. Alijipiga na hata kukopa ilimradi tu, mama ale.



    Hakuwahi kumjua, baba yake wala kufahamu chochote kuhusu baba yake. Yeye alichojua ni mama yake tu. Hakuwa na ndugu zaidi ya huyo. Alipouliza juu ya baba yake, mama aliishia kutoa chozi jambo lililomuumiza sana Musa. Alijiapiza kutomuuliza tena mama yake maswali ya kuita machozi ya mama yake.



    Kila likizo, Musa na Neema walikutana na kujadili maisha yao matarajiwa.



    .... ... .... ....



    Docta Endrew na docta Izack, walishafanikisha kupora picha ya Mavugo japo iliwachukua sana muda kupora picha hiyo. Wakaaitoa kopi kisha kila mmoja akawa na ya kwake wote kwa pamoja wakaanza kutembea mtaani kwa ajili ya kuwatafuta wale walioonekana kwenye picha ile. Hakuna walichopata wala kuambulia zaidi ya kupigwa na jua kali. Walifanyakazi hiyo bila mafanikio ya aina yoyote. Walitafuta hadi wakasema kuwa wamechoka. Wakaamua kuirejesha tu. Picha ile kwa Mavugo ambae anaamini aliipoteza kwa muda mrefu.



    .... ... .... ....CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Pita Mwambe, aliendelea kushukuriwa na wananchi kila siku kutokana na misaada aliyowapatia. Hakuwa anachagua, alitoa kwa masikini, watoto yatima, watoto wanaoishi mazingira hatarishi, alitoa pembe jeo kwa wakulima mbalimbali, barabara zilitengenezwa jimboni kwake. Sasa kwanini wananchi wa mchukie? Alitoa saidia mamia na maelfu ya watu pasina kujali matabaka yao. Hakuna mbuge aliejaribu kugombea kwenye jimbo la pita Mwambe nae akapita. Ni wazi kuwa wananchi walikuwa wameshamkabidhi kura zao kutokana na jinsi alivyowajali. Vyombo vya habari vyote vilimsifia huku vikiendelea kukuza jina lake kwa kutaja misaada mbalimbali aliyoendelea kutoa. Licha ya moyo wake, vilevile kule bungeni, mawaziri walipata tabu sana kwani hakuwa mtu wa kutania katika ujengaji hoja na hakuogopa yeyote yule.





    Baba Neema aliendelea kuchakalika kila siku kwa ajili ya familia yake. Alihakikisha kuwa, familia yake haikosi hata sumni.



    Kama kawaida ya Baba Neema, yeye kila siku atokapo kazini huwa anatabia ya kwenda kupombeka kisha anarejea nyumbani majira ya usiku.



    "Muhudumu... Mimi nimesema leta bia, wewe unanizuia. Hivi hela nizakwako auuu zaa kwangu. Nitamwambia bosi wako akufukuze kazi sasa hivi. We unajua mimi ni nani. Mimi ndio Devi. Allaaa, natumia pesa zangu nasio zako." Ni sauti ya kilevi iliyomtoka Baba Neema kwenye moja kati ya pub aliyoipenda sana. Sikwamba hakuwa akiudumiwa, bali nikawaida yake kuchangamka na kuleta utani pindi atoshekapo. Kama humjui unaweza kumuongeza bia, wengi wameshakula losi kwa kuyaamini maneno yake. Akiwa na rafiki yake ajulikanae kwa jina la Amos, walianza kujadili mambo yao ambayo kwao wanayathamini sana.



    "Hivi, Amosii... Unajua kuwa Mwamba, anaetimba popote hata kwenye miamba. Sasa amerudi." Aliongea Baba Neema.



    "Unamaanisha, Mwanao Neema au nini?" Aliongea Amosi.



    "aaah! Amosi,.. Usitake niambia huto tuchupa twa bia ulitokunywa tena kwa hela yangu ndio tuna kupelekea wewe uniulize upuuzi. Inamaana ni kisema Mwamba hunielewi. Hadi ulete maswali yasiyo na kichwa wala miguu hapa." Aliongea Baba Neema huku akiendelea kunywa.



    "Tatizo lako wewe ndio hilo, yaani ukininunulia pombe, mpaka uninyanyase.. Uninyanyase.. Weee.. Kwani mimi kuuliza nikosa?" Aliongea Amosi rafiki wa Baba Neema.



    Waliendelea kupiga soga za hapa na pale. Lakini zaidi wakuwa wakiisifia pombe tu. Walipomaliza walinyanyuka na wakaagana kila mmoja akaenda kwake. Baba Neema akiwa njiani, aliendelea kusindikizwa na nyimbo mbalimbali ambazo huzitunga pindi alewapo. Hatimae alifika kwake, kama kawaida hupokelewa vizuri na kupewa mahtaji yote ikiwemo chakula, maji ya kuoga na kadhalika. Siku hiyo ni ndani ya masiku ambayo Neema alikuwa likizo, na kwakuwa kwa muda huo alikuwa ni kama ameshakuwa. Aliona achukuwe nafasi ile kuuliza swali linalomtatanisha miaka yote toka yupo mdogo.



    "Baba.. Unampenda mama?" alijibu baba yake kuwa anampenda sana. Kisha Neema akageuza macho yake kwa mama yake. Nako akauliza hivyohivyo. Mama yake pia akajibu kuwa anampenda baba yake.



    "Nashukuru kusikia mnapendana kiasi hicho. Lakini... Mie kuna suala moja ambalo linanitatiza. Hivi ni kwanini toka nipo mdogo, baba huwa analala chumba chake na mama huwa analala chumba chake. Wakati nyie ni mume na mke?" Aliuliza Neema swali lililomfanya baba yake ahisi kama pombe imekata kichwani na sasa anaulizwa swali ambalo hanauwezo wa kulijibu pasina kulewa. Mama yake nae, alijikuta akipaliwa na maji aliyokuwa akiyanywa. Wakaangaliana wawili wale kwa nukta kadhaa huku alama za mshangao zikijichora usoni mwao. Neema alishuhudia jambo lile, lakini kwakuwa hakuwepo pale kwa ajili ya kushangaa. Alitulia ilikusikiliza atakachoambiwa na wazazi wake. Baba alikosa jibu, kisabuni mama akajikaza.



    "Haya ni mambo ya wakubwa. Hayakuhusu, tena usijikuze kiasi cha kudadisi vilivyo nje ya umri wako. Unanisikia wewe mtoto? Shika adabu yako. Nisisikie tena unahoji swali hilo." Alifoka Mama kisha akatoka hapohapo na kwenda hadi chumbani mwake, huku baba akifuatia nae pia alienda chumbani mwake na kwenye meza. Wakamuacha Neema pekee.



    Neema aliwaza sana akiwa mezani pale peke yake. Mwisho wa siku alijiona huenda yeye ndie mwenye makosa. Aliamua kwenda chumbani kwa mama yake bila hodi. Ile anaingia tu. Akamkuta mama yake anameza vidonge ambavyo nikama anavifahamu. Alipochunguza kwa umakini aligundua kuwa ni vidonge vya kuongeza siku. Alikumbwa na bumbuwazi la ghafla, hakutegemea jambo lile mama nae alipohisi kama kuna mtu ameingia ndani mwake akataka kuvificha lakini alipoangalia mbele tayari alikuwa amechelewa kwani mwanae tayari alisha viona.



    "Mama.. Unataka kunambia kuwa.. Kuwa... Huwa unaishi kwa kuongeza siku?" Aliuliza Neema.



    .... .... .....



    "Nimelikumbuka jalala. Nahtaji kwenda kukaa karibu yake, ninuse harufu nzuri itokayo jalalani. Huku nikiwaona watoto waliyoachwa na wazazi wao wanavyojituma kulisaka tonge jalalani huko. Nimekumbuka kuona vurugu za kugombania mabombonya na vyuma chakavu. Nahtaji kuwaona wanawake waliyofukuzwa makwao na kuwekwa wengine kisa walikosea kusuuza sahani. Wanawake majasiri wasioogopa ukali wa jua utuao utosini mwao.. Wanawake wanaoweza kuhimili kuishi na uchafu pasina kuugua, wanaoweza kula chakula ambacho kimelambwa na mbwa. Nimeukumbuka sana mtaa. Mtaa uliyona mafunzo tele juu ya maisha. Mtaa usio na huruma mbele ya watoto waliyozaliwa na wanawake. Nahtaji kurudi mtaani iliniendelee kujifunza somo zuri la maisha. Hakika mimi bado mwanafunzi. Vipi wewe Endrew ambae ndio kwanza hata robo tatu ya ujana haujaifikia ni vipi uniambie umeshasoma sana. Kama wewe ni msomi je, unaijua njaa... Ushawahi kumwagiwa maji ya moto na kuachiwa alama ya maisha? Je, ushawahi kuua kwa maneno?" Aliuliza Mavugo. Maswali yaliyozidi kumchanganya docta Endrew.





    Alibaki akimtumbulia macho Mavugo. Hakujibu wala kuongea chochote kwa dakika zaidi ya mbili. Docta Endrew alibaki kujiuliza maswali mengi sana juu ya Mavugo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kama kweli ni kichaa.. Mbona anajua mengi? Ni yapi hayo yaliyomkuta au aliyoyashuhudia mtaani? Mbona faili lake linaeleza kinyume na maneno yake?. Hayo ni baadhi ya maswali yaliyojijenga kichwani mwa docta Endrew, alihisi kama maswali menyewe yanakiwasha kichwa ndipo akaanza kukikuna.



    "Docta, vipi, mbona unakuna kichwa? Una mvi, chawa, kunguni, au sungusungu wamehamia kichwani?" Aliuliza Mavugo na kumpelekea Docta Endrew ajishtukie kisha akasema."Hapana Bwana Mavugo, najaribu tu kukuna akili. Siunajua tena.."



    "Docta, unajua mie natatizo moja." Alidakia Mavugo.



    "Tatizo? Lipi tena hilo Mavugo" Alihoji kwa mshangao docta Endrew.



    "Tatizo langu ni kuwaona nyie na minguo yenu ya hospitali. Siipendi sana. Kingine ni juu ya hawa machizi ninaoishinao. Kutwa hawawazi maendeleo wenyewe wakilala na kuamka, akili zao zinafanya ya jana tu. Sasa kunisaidia, nilikuwa naomba angalau unitoroshe hapa. Au uwe unanipeleka mtaani kisha jioni na rudi kupumzika maana sioni ninachofanya tafadhali nisaidie kwa hilo." Mavugo alipoweka nukta ya maneno yake. Huku Docta Endrew tayari tumbo lilianza kumsumbua huku akitetemeka kwa uoga wa maneno ya Mavugo.



    "We Mavugo wewe. Hivi kwa akili yako unadhani kuna ruhsa ya kumtoa kichaa akachanganyikane na raia? Aisee hapo mie siwezi. Japo wewe ni rafiki yangu." Alijibu Docta Endrew huku akimshika bega Mavugo.



    "Docta... Nadhani hutambui maana ya urafiki wewe. Hivi unadhani kuongea nami pekee kunaweza fanya niamini kuwa wewe ni rafiki yangu? Labda nikwambie kitu. Unaweza kunitoa hapa kama ukitaka, na hauwezi kunitoa kama hutaki.



    Kumbuka, kichaa huletwa hapa baada ya kukosa matunzo au tiba au labda usumbufu wake ulikuwa mkubwa huko uraiani. Nadhani unajua mie nipo hapa kwakuwa nimekosa matunzo tu. Sasa naomba unichukue na unitunze kama kweli wewe ni rafiki yangu wa damu. Kama kweli ulivyokuwa ukisema kuwa upo tayari kunisaidia ulisema ukweli basi nisaidie. Nahtaji nianze maisha mapya kupitia wema wako kwani hapa nilipo sina hata chembe yanijuacho kuhusu maisha yangu. Simjui baba, simjui mama. Sijui nimetoka wapi wala naelekea wapi nijuacho ni hapa nilipo labda na mambo niliyoyafanya baada ya kuharibika kwa kumbukumbu zangu za zamani. Tafadhali, nisaidie kunitoa hapa mie nitakubali kulelewa nawe. Sitokusumbua kama nifanyavyo kwa wengine kwakuwa wewe ni rafiki bora kwangu. Huu muda mfupi niliyokaa nawewe hapa hospitali umetosha kuniaminisha kuwa wewe ni kijana mwema na mtu anaependa kujifunza. Tafadhali ninahtaji kutoka humu nitoe." Ni maneno makali sana aliyoongea Mavugo. Kwanini chozi lisimtoke Docta Endrew? Hakika sikuchoka pekee bali moyo pia ulimuuma na kutengeneza huruma isiyo kifani. Alijifikiria juu ya tabia ya Mavugo, akafikiria juu ya maisha anayoishi na kujipajibu kuwa hayaendani hata kidogo na yeye. Akatupa jicho kiuwezo japo simkubwa lakini sihaba mpaka ashindwe kumsaidia bwana Mavugo. Aliendelea kuisumbua akili yake huku ukimya ukitawala si kwa Endrew pekee bali hata kwa Mavugo pia.



    "Lakini.. Japo kesi ilishakatwa ila naomba unipe ukweli ili hata kama nikikusaidia nijue jinsi ya kufanya. Sijui unaweza kuniruhusu nikuulize swali."



    "Uliza tu Docta. Toa shaka." Alikubali Mavugo.



    "Inasemekana miaka kumi na mitano iliyopita. Wewe ulifanya mauaji ya watu watatu na ukahukumiwa japo huku jitetea zaidi ulionesha kiburi lakini mwisho wasiku ndipo walipobaini kuwa wewe ni mgonjwa wa akili. Je, ni kweli wale watu uliwaua wewe. Tafadhali naomba jibu fasaha." Alihoji Docta Endrew na kutega sikio ilikupata mkanda mzima wa majibu.



    ..... ... ... ... ...



    Mama Neema alikosa la kumjibu mwanae akabaki kimya tu huku uso wake ameuweka chini.



    "Mamaa! Sinaongea nawewe... Inamaana hunisikii au?" Akauliza Neema kwa ghadhabu huku akiviendea vidonge vile ndipo alipohakikisha kuwa, Mama yake anatumia A.R.V. Neema alilia sana huku akimvutavuta mama yake kwa machungu.



    Aliwaza mengi sana Neema. Lakini alijikuta akizimia ghafla baada ya kukumbuka kuwa alishawahi kufanya mapenzi na Musa.



    Alizinduka baada ya kumwagiwa maji ya baridi, huku mbele ya macho yake akimuona Mama yake akimlilia. Akamuangalia kwa hasira sana na kuhisi kuwa huenda Mama yake anajiliza kinafki. Kilichokuwa kikimuumiza sana ni juu ya Mama yake kuutambua uhusiano kati ya yeye na Musa na mara kadhaa alishawapatia baraka lakini hakuwahi kumwambia hata siku moja kuwa yeye ni muathirika. Neema aliamini kuwa kama mama yake nimuathirika basi nae lazma atakuwa ameathirika. Na kwaharakaharaka alihisi kuwa ndio maana Baba yake hulala chumba tofauti na Mama yake.



    "Niache.!!! Usinishike. Kama unanipenda mbona ulinificha mpaka nimegundua mwenyewe. Ona nimemuambukiza mtoto wa watu pasina kujua." Alilalamika sana Neema huku Mama yake akishindwa aanze vipi kumuelezea kwani hakutaka kumpa hata nafasi ya kujielezea.



    . Neema akiwa analia alirudisha kumbukumbu nyuma na kuikumbuka vyema ile siku ya kwanza toka wapate likizo shuleni kwao na akaukumbuka kwa umakini zaidi usiku wa siku hiyo. Ndio angekumbuka nyota za angani au chakula alichokula usikuhuo lakini hakukumbuka hayo bali alichokumbuka ni vile vishawishi vya mpenzi wake Musa pale alipoomba waitengue amri ya sita ndani ya chumba anacholalia Musa. Kumbukumbu za Neema zinamkumbusha kuwa alikataakatakata na kumsisitiza Musa kuhusu ile ahadi yao ya kutofanya mapenzi kabla ya ndoa. Lakini Musa alibembeleza vilivyo tena kwa sauti iliyosindikizwa na machozi na ndipo hapo Neema aliporuhusu nguo zake kumshuka chini na kuzitupa pembezoni mwa kitanda kisha wote kwa pamoja wakashirikiana kuvunja ahadi yao. Kumbukumbu zile ziliendelea kumtesa zaidi Neema na kumfanya asahau kama alikuwa amelishika shati la mama yake huku akimvuta kwa hasira. Alikuja kukurupushwa na kofi moja lililompeleka hadi chini.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "We mtoto huna adabu wewe... Hivi unataka mie mama yako nikubembeleze vipi iliunisikilize ninachoongea? Allaaah! Sikia ni kwambie mwanangu. Mimi sio mjinga kukuficha yote hayo bali ninamaana yangu. Nimengi yaliyonikuta mpaka leo hapa nilipo. Nakupenda sana mwanangu.. Nakupenda." Hapo Mama Neema akavuta pumzi huku kamasi na machozi yakiendelea kumtoka, akafumba macho kwa sekunde kisha akayafumbua na kuyatazamisha kwa mwanae aliyekuwa chini kwa muda huo. Sura ya Neema ilionesha chuki ya wazi dhidi ya mama yake. Lakini mama hilo hakulijali akamshika mkono mwanae na kumketisha kitandani kishaakaanza kumpa hadithi ya maisha yake kwanzia pale walipotengana na wazazi wao pindi meli ya Mv bukoba ilipozama. Mpaka walipolifakamia jiji la Mwanza. Yeye pamoja na mdogo wake. Pia hakusita kumuhadithia sababu ya kifo cha mdogo wake na kisa cha yeye kubakwa na Afande Kipara. Aliihadithia vizuri ile siku aliyoenda kutoa damu katika hospitali ya Bugando na ndiko alikokupata habari ya ugonjwa wa Ukimwi. Alihadithia kiundani zaidi na hakuna alichoficha. Mpaka jinsi alivyojifungua kwa taabu mwanae huyo Neema. Alipofika hapo akasitakidogo kishaakamwambia kuwa, yeye aliamini kuwa Neema atakuwa na V.v.u lakini vipimo vilipinga hilo. Ndipo kwa mara ya kwanza akayaona maajabu ya dunia kwani aliamini kuwa, kama mama akiwa na V.v.u basi na mtoto lazma awe navyo, alihadithia vizuri zaidi mpaka hapo alipomaliza.



    Neema alijiona ni mkosaji sana kwani alimchukia mama yake bila kujua, alijikuta akifurahi huku akishangaa hapohapo, pia soni ilimjaa usoni huku akizilaumu fikra zake. Alishukuru sana kujua ukweli ambao ulijificha unaohusu maisha yake. Hapo akamfuta machozi mama yake na kumuhurumia sana pia alimsifu kwa ushupavu na kutamka wazi kuwa Mama yake ni shujaa wa kike. Mtoto na mama walifutana machozi na mpaka wote kwa pamoja walijikuta wakichukuliwa na usingizi huku wakiwa wamekumbatiana.



    ..... .... ......



    Ulikuwa usiku wa kipekee zaidi kwa Musa, usiku ambao hakutamani apatwe na usingizi hata kidogo, japo haikuwa kawaida yake kukaa macho hadi mida ya saa tatu usiku kwani hutoka mihangaikoni akiwa amechoka sana hivyo hula, kuoga na kulala tu. Lakini siku hiyo alikuwa macho huku akifikiria sana. Hakuwa anafikiria, mbingu wala viatu bali alifikiria kiumakini zaidi ile kazi aliyoahidiwa siku ijayo kutoka kwa mfanyabiashara maarufu jijini hapo. Anakumbuka kuwa chanzo cha yeye kuahidiwa kazi ni juu ya wema mdogo aliyoufanya, wema wa kuokota picha iliyomdondoka mfanyabiashara yule na kurejeshea.



    "mmmh! Yaani mtu kumuokotea picha yake tu. Tena picha iliyochakaa. Tayari anakuahidi kazi. Mmh! Hakika kila sifa anastahiki mwenyezi. Natamani kesho ifike iliaje kuongea na mama kwa ajili ya kunipatia kazi. Nitafurahi ile mbaya. Halafu watanikomaje? Ngoja tu, muda wa dharau unaelekea ukingoni. Sasa nadhani nitapajua hata dar-es-salaam live nasiokuishia kupaona kwenye tv tu." Alijisemea Musa huku akiendelea kupingana na usingizi uliyokuwa ukimnyemelea. Aliwaza lakini mwisho wa siku alipitiwa na usingizi tu.



    .... .... .....



    "Swali lako ni zur sana docta Endrew lakini hebu tazama saa yako. Usiku umeenda sana. Hata kama nikisema nikujibu, itachukuwa muda sana mpaka kukamilika kwa jibu. Istoshe umeshapitiliza hadi shifti. Ni usiku muda huu. We huoni hupaswi kuendelea kuwepo hapa. Hebu nakuomba nenda nyumbani kesho ukija nakuahidi jibu lako lakini unapaswa uwe makini sana maana nishakusihi kuwa mjinga huachwa na ujinga wake." Aliongea Mavugo na kumfanya docta Endrew agundue kuwa tayari muda ulishamuacha sana. Hakujutia kupoteza muda wake akiwa na Mavugo zaidi alijiona kuwa ni mwenye bahati kwani aliamini kila sentensi ya Mavugo kwake ni darasa tosha. Kwakuwa muda nikweli ulikuwa hauruhusu. Hapo docta Endrew akaondoka na kwenda kwake huku Mavugo nae akibaki hospitali hapo kama kawaida yake.



     Musa alikurupuka na kuiacha shuka baada ya kushindwa na miale ya jua la asubuhi iliyoingia ndani kupitia kwenye matundu yaliyokuwepo kwenye mabati ya chumba chake. Huwezi ukasema sababu ya Musa kuamka ni miale ya jua. La! Hasha. Mara ngapi Musa anachelewa kuamka ilhali jua lipo. Hapo hakuna kingine kilicho muamsha mapema namna ile zaidi ya furaha ya ahadi ya kazi. Alishukuru Mungu kuiona siku mpya, siku aliyoingoja kwa hamu na hata kuifanya ichelewe zaidi. Alienda kunawa pamoja na kupiga mswaki kisha akajirudisha tena ndani kwa akafungua kopo moja la mafuta ya kujipaka kopo dogo kabisa la bei ya chini ya kuanzia kuuza mafuta hayo kwenye duka lolote hapa nchini, akachovya kwani badala atoke na mafuta ya mgando kama yatokayo kwenye kopo la aina ile. Yeye akatoka na mafuta ya kula. Bila wasiwasi akapaka usoni huku akisahau kichwani na maeneo ya masikioni pamoja na shingoni. Akapaka mikono yote miwili huku akiishia mkabala na mabega kisha akamalizia miguuni. Naam, nisehemu ambazo huwa hazistiri kwa mavazi tu lakini sehemu kama kifua, tumbo na maeneo mengine ikiwemo yale ya faragha, menyewe hakuyapatia mafuta kisa huwa hayaonekani kwenye halaiki na hiyo ilikuwa namna moja ama nyingine ya kubana matumizi ya mafuta. Baada ya hapo aliyavua yale mavazi aliyolalanayo usiku wa siku hiyo na kuchukuwa mavazi nadhifu kabisa na kisha akayavaa.



    "Mwanangu mbona umeupara hivyo utadhani Muendeshaji wa harusi? Au unaenda kwenye harusi?" Alihoji Mama Musa na hiyo ni baada ya kujuliana hali na mwanae. Musa kusikia hivyo akacheka kidogo huku akimalizia kufunga nyuzi ya vile viatu vyake ambavyo huwa anavivaa kwenye sherehe au ahadi maalumu. "Mama nawe kwa kejeli! Kwahiyo unashindwa tu kuniambia kuwa sijapendeza hadi unifananishe na wale ma mc wa kwenye harusi. Wale wasiojua kuwa mkanda huvaliwa kiunoni na situmboni, acha basi Mama." Akajidhalilisha kiutani mbele ya Mama yake.



    Kama kawaida Mama yake akamsifia ilikurejesha hisia ya Mwanae nae ajihisi ni mtaalamu wa kuchagua nguo kama wafanyavyo vijana wenzake wa kileo.



    "Haya wasalimie huko uendako." Aliaga Mama.



    "Usijali. Badae Mama" Alipokeza Musa na moja kwa moja akaondoka. Hakuwa na baiskeli wala usafiri wowote wa haraka zaidi ya miguu yake. Mguu mosi, mguu pili kwa mwendo wa kuogopa vumbi na uchafu wa hiari, hukuakiiamini saa yake iliyosoma vyema mkononi. Aliiangalia kila baada ya dakika kadhaa. Alienda moja kwa moja hadi sehemu walipoahidiana wakutane na mfanyabiashara yule. Alipofika alisubiri kama Nusu saa tu. Baada ya hapo ilifika gari aliyoijua na kuifuata, haikumchukua muda kufikiria kuwa gari ile ndio ya yule mfanyabiashara bali ilimchukua muda kufikiria jinsi yakumuheshimu bwana yule kwa kumpa salamu ya kipekee. Kama kawaida alinyenyekea kwa dhati nae akaitikiwa. Waliongea kidogo maneno ya hapa na pale kisha Musa akaingia garini. Gari iliwashwa huku Musa akitoa maelekezo ya sehemu za kupitia na mwisho wa siku walifika nyumbani kwa kina Musa. Walipofika mfanyabiashara yule akasalimu na utambulisho mfupi ukafuata.



    "Mama huyu ndo, yule niliyekwambia jana. Kuhusu ahadi yake ya kuja hapa kuniomba angalau nifanyenae kazi." Alimtambulisha mgeni kwa mama yake.



    "Anhaa... Nashukuru kukufahamu. Karibu sana hapa ndio kwa kina Musa na mimi ndio mama ya..." Alisita kidogo baada ya kugundua kuwa aliongea maneno yale kabla ya mgeni kuketi kitini. "Samahani baba.. Naomba keti kwenye kigoda ilituweze kuongea kwa utulivu. We Musa, hebu niletee hilo sandalusi langu la kukalia." Akatoka Musa na kuingia ndani, hakukawai akarejea huku ameshikiria alichoagizwa alipofika akatandika kisha Mama yake akaketi.



    Maongezi mafupi ya utambuzi yaliisha ikiwa tayari walijuana hadi kabila, mpaka maeneo waliyozaliwa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Mgeni yule alieleza kiundani zaidi juu ya shida yake ya kumuhitaji Musa kwa ajili ya kumfanya awe anasaidiana nae kazi kutokana na kupenda hulka yake pamoja na moyo mwema aliyokuwanao Musa. Hakusita pia kuelezea wema uliyomfanya yeye ampende Musa na pia akatoa mifano kadhaa ya vijana ambao ameshafanyanao kazi lakini wakamzunguka hiyo nikutokana na uaminifu ziro wa vijana wale istoshe walimtafuta wenyewe ila kishawishi kingine kilichompelekea amuhtaji Musa ni baada ya Musa kujitambulisha kwamba yeye si mtoto wa mtaani bali anakwao kabisa na hata elimu anayo tena ya kiwango kizuri tu.



    Mama Musa kwakuwa anapenda maendeleo ya Mwanae. Hakuona kama kuna haja ya yeye kumzuia mwanae japo alijua kuwa ni lazma atengane nae kwani mwanae alihtajika kwenda kuuza duka kubwa la mfanyabiashara huyo lipatikanalo jijini Dar-es-salaam. Zaidi aliamini kuwa mafanikio ya Mwanae ni yake pia.



    Musa alifurahi sana baada ya Mama yake kuridhia na aliahidi palepale kwamba anaenda kufanyakazi iliamsaidie Mama yake yule ambae maradhi yalimpata kila siku kutokana na virusi vya umasikini ambavyo viliruhusu kila aina ya magonjwa ya njaa.





    Yule mfanyabiashara aliahidi kumuijia wiki kadhaa mbele kisha aliacha pesa ya kumfanya Mama Neema angalau apate kula na kubadili mwili wake. Kisha akaaga na kuondoka. Furaha iliyonakshiwa na machozi huku majonzi yakiipongeza kwa hiari. Hawakujua wanafurahi kwasababu ya kutengana au wanalia kwasababu ya kasi.



    Neema alipopelekewa taarifa za uondokaji wa mpenzi wake, aliumia sana kwani hakuwahi kuwaza kutengana nae namna ile.



    "Salio la uhai wangu umelibeba wewe... Jinsi utakavyolitunza ndivyo unavyoendelea kuokoa maisha yangu... Nipende kama unipendavyo na unilindie penzi langu... Ningekuwa nauwezo wa kutamka neno 'hapana' basi huu ungekuwa wasaa wake.. Lakini nitaanzaje kutamka ilhali ufuatacho ndicho cha muhimu. Kumbuka mimi ndio pekee kwako kisha ukumbuke kuwa huku pia umemuacha Mama halafu upige kazi kwa bidii... Nakupenda sana Musa lakini unapaswa kuniacha japo tumezoeana. Ila... Please and please hifadhi pendo langu na ulisome kama Msahafu kamwe usilibadili hata kidogo. Kama ukinicheat i swear to God takuua kwa mikono yangu dhaifu isiyoweza hata kushikiria kisu. Heshimu hisia zangu popote utakapokuwa." Aliongea Neema huku macho yake pamoja na maneno yakimtoka kwa hali ya kutisha zaidi.



    "Nashukuru kwa kunikumbusha japo natambua nanijukumu langu kutambua.. Napenda kufanya rejea ya maneno ya wahenga pale waliposema kuwa 'Jasiri haachi asili'. Mpenzi mimi ni jasiri na wewe kwangu ni kama asili, basi siwezi kukuacha hata kama nitanyooshewa bunduki kinywani au kuwekewa panga shingoni. Nataka kukuona kwenye sofa nataka kumuona mwanangu akichezea toi huku pembeni televisheni ndogo kwa ajili yake ikiendelea kuonesha Muvi zakitoto. Nahitaji kulala kwenye magodolo ya wale wanaojiita matajiri na hitaji niifutilie mbali hii lugha mbaya isiyojulikana pamoja na huu msamiti wa umasikini kisha ni andike upya msamiati wa mafanikio tena kwa kalamu ya kijani anayomiliki rais tu. Nakupenda nakuheshimu nakujali pia. Sina usemi hata nikitafuta sitopata, najua unajitambua penzini. Sina shaka na pendo lako."



    Waliendelea kutoleana maneno, mazito kwa mepesi. Yakuumiza na yakufurahisha lakini zaidi waliichukia dharau wapatiwayo kisa umasikini tu. Pia Musa hakusita kumuhimiza mpenzi wake kuwa anatakiwa kusoma kama hatosoma tena ilikufanikisha malengo yake.



    Siku zilitimia hatimae Musa alichukuliwa na yule mfanyabiashara. Moja kwa moja hadi Dar-es-salaam. Ni kama robo ya ndoto zake ilitimia ile tu kuuona mji ule. Alifurahi sana. Walipokelewa vizuri kwenye nyumba ya heshma kwanzia getini.



    "Jisikie upo nyumbani.. Hapa ni kwetu sote.. Naimani hutokuwa nauoga baada ya maneno hayo." Ni maneno ya mwisho mwisho aliyoyaongea Mfanyabiashara yule baada ya kumkaribisha Musa kwa maneno marefu kidogo. Musa alikaribia kwa heshima zote. Kwakuwa uchovu ulimtawala kwani hajawahi na wala simzoefu wa kusafiri safari ndefu. Aliomba aonyeshwe pahala pa kujipumzisha alichukuliwa na kupelekwa. Hakuwa na muda wakuongea bali wakulala tu. Hivyo alijiza na usingizi palepale ukamvaa.



    ..... .... ......



    Docta Endrew aliendelea kusumbuliwa na maneno ya Kichaa Mavugo. Kubwa zaidi lililomfanya mpaka kujipigapiga kichwa ofisini mwake kwa mkono wake wenye kalamu yake ni juu ya ukweli alioupata kutoka kwa Mavugo.



    Ina maana huyu Mavugo hakuua? Kumbe si Muuaji? Aaah! Miaka yote hiyo mahakama imemuweka ndani bila ushahidi.



    "This is unfair." Akajiropokea ofisini mwake huku akipiga meza kwa nguvu wala asiyajali maumivu.



    Hapo akasimama na mkono wake wa kulia akiushikisha mezani huku ule wa kushoto akiutumia kukizungusha kile kiti cha ofisini mwake. Akakereka zaidi akakiacha kiti na kuanza kukuna kichwa. Hapo napo akaona kama bado, akaanza kutembea tembea ndani ya ofisi yake Safiri isiyokuwa na mwisho.



    Kama hakuua yeye, basi amesingiziwa na kama amesingiziwa basi kuna jambo limejificha hapa. Mmmh! Jambo lipi? Je, Mavugo analijua? Hapana hawezi kulitambua kutokana na kufutika kwa kumbukumbu kichwani mwake. Na vipi kuhusu kumchukua. Je, nimchukue???



    Hayo ni mawazo yaliyokuwa yakiendelea kutalii kichwani mwa Docta Endrew.. Mawazo hayo tu ndio yaliyomtoa kitini na kumsimamisha mwisho wa siku kumzurulisha ofisini mule pasina kumsimamisha. Mara aende kulia mara kushoto, mara ashike kalamu mara aiweke mezani. Kumbe ni mawazo tu.



    Siku hiyo Docta Endrew aliomba ruhusa mapema na kurejea nyumbani kwake. Alipofika hakuhitaji stori wala nini. Moja kwa moja alipitiliza hadi chumbani na kujipumzisha baada ya kumeza dawa za kichwa alizonazo palepale kwake.



    Mke wa Docta Endrew ni mpenzi sana wa filamu hasa zile filamu ndefu zenye misimu. Hupenda kufanya hivyo kila siku amalizapo shughuli zote za pale nyumbani kwake. Haikuwa kawaida ya Mumewe kurejea mida kama ile tena huku akisahau kumjulia hali mke wake na kupitiliza hadi ndani.



    Inamaana hajaniona? Audharau tu? Ata!! Huyu atakuwa natatizo. Ngoja nimfuate. Nimawazo aliyowaza mkewe.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Mke wa Docta Endrew aliingia chumbani na kumkuta mumewe amejipumzisha huku macho yake mawili akiwa ameyaangalizisha juu. Alisita kidogo baada ya kumuona mumewe ametawaliwa na huzuni. Taratibu akamsogelea na kumshika begani.



    "Mume wangu... Kipi kimekusibu?" Alihoji mke wa Docta Endrew huku akiendelea kupitisha mkono wake kichwani mwa mmewe.



    "Hakuna kitu mke wangu. Sema niuchovu tu." Alijibu Docta Endrew huku akijiinua kitandani na kujikalisha.



    "Uchovu?? Aaah! Usinidanganye. Usiniaminishe kuwa uchovu pekee ndio umekupelekea kurudi nyumbani muda huu. Wala usiniambie eti. Hali uliyoingia nayo humu leo inauhusiano na uchovu. Mie staki ngonjera bali nahtaji kujua umepatwa nanini?" Maneno yalimtoka Mke wa Docta. Docta anajua mke wake akikazania jambo hupenda mpaka alijue ili ashiriki kwenye utatuzi. Kwakujua hilo ilibidi alete ubeberu ilikumuonyesha mkewake kuwa yeye ndie mwanamume.



    "Halafu we mwanamke usiniletee usumbufu.. Tena kama umeshindwa kuangalia televisheni heli ukaoshe vyombo. Niache nilale.. Kwanza huna adabu, Mumeo anafika badala ya kumuacha apumzike we... Unamuamsha tu. Hivyo ndivyo kwenu wamekufunza eti? Nakuuliza wewe... Kwenu huwa mko hivyo? Sasa kaendelee kazi yako niliyokukuta unaifanya. Ebo!" Maneno yale yalitosha zaidi kumvunja moyo mke wa Endrew. Hapo hakuwa na usemi kwani hapendi kumuudhi mumewe. Alilitambua kosa na kunyanyuka kwa kujivuta kama asiyejiskia taratibu akaondoka na kurejea sebuleni.



    Docta Endrew aliendelea kutembelewa na maswali yaliyomchekesha, mkejeli, na kumuhuzunisha. Alikaa na kufikiria siku hiyo nzima. Baada ya kufikiria kwa kina aliona ni kweli Mavugo si'wakukaa hospitalini pale bali angekuwa katika shirika fulani akifanya kazi zake. Siku hiyo iliisha huku tayari amepata jibu na siku iliyofuata akaanza taratibu za kumtoa mgonjwa yule wa akili.



    Docta Endrew ingawa alikabiliwa na changamoto nyingi lakini mwisho wa siku alikubaliwa kumchukua na kumpeleka kwake. Mavugo alifurahi sana baada ya kutoka hospitali na kupelekwa kwa Docta Endrew. Alitoa shukurani kama wafanyavyo wengine.

    ..... ... .....



    Likizo fupi ya Neema iliisha na yeye akarejea shule. Kama kawaida ya Neema yeye huwa bize na masomo huku akiamini lazma yatamtoa tu.



    "Hivi we Neema? Mbona huelimiki japo we nimsomi. Sjui nini kinachokupelekea hivyo.. Au kwenu bushi nini... We mtu gani usiyekuwa na boyfriend. Kila siku unatusumbua sisi tunapoongea na watu wetu. Mara ooh! Ongeeni taratibu mie nisome. Acha hizo shtuka hapa mjini afu shule ndio sehemu ya kuwa huru. Hivi we unawezaje kukaa hivyo hivyo tu tena kwa muda mrefu. Mie siwezi duh!" Aliongea rafiki yake kwa jina la Mishi. Hiyo ni baada ya Mishi kuombwa na Neema apunguze sauti ya aliyekuwa akiongea nae kwenye simu.



    "Labda mwambie nawewe shosti. Huenda akakuelewa maana. Mi kila siku lazma niseme. Lakini wallaaa hasikii. Anajifanya wakusoma sana." Aliongea Jesca ambae nae pia ni rafiki wa Neema pamoja na Mishi.



    "Hivi, niwaulize swali?" Alihoji Neema baada ya kuwaangalia marafiki zake kwa jicho la ukali kidogo.



    "Uliza shosti" Alijibu Jesca.



    "Mmekosa kazi ya kufanya?" Aliuliza Neema na kuwapelekea rafiki zake walikutazamana kisha wakakosa majibu. Swali la Neema lilikuwa ni moja kati ya maswali ambayo kama ukiulizwa bila kutaraji basi lazma uchukie au uumie moyoni. Na ndivyo ilivyokuwa kwa washauri wale ambao waliamua tu kujilaza na kufikiria ya kwao huku ya Neema wakimuachia mwenyewe.

    ... ... .......



    Ilikuwa ni siku moja kati ya masiku aliyopendelea kwenda sokoni Mama Neema. Siku hiyo alichukua kapu lake na kwenda kununua mahtaji ya nyumbani. Akiwa njiani kutoka sokoni alipita kona kadhaa na kutokea barabarani. Alinyoosha na kufika sehemu wanapokaa ombaomba kwakuwa ni mtu wa huruma. Alimfuata ombaomba mmoja aliyekuwa anaonesha dhahirikuwa anaugonjwa mkali sana. Ombaomba huyo alikuwa akikohoa kikohozi kigumu na kutema makohozi yaliyoambatana na chembechembe za damu. Huku mwili wake ukiwa umekonda maratatu ya wewe, macho yake yakiiacha ngozi iliyojikunja kunja kwa madonda yaliyokauka na kupona huku mengine ya kijitonesha. Nywele zake zilikuwa ni kama zimenyonyoka na kukosa rutba ya kuota kama zamani. Ndio, salawili yake ilioneshawazi kumshuka kama angesimama lakini natumai angesitahiwa na kamba ya katani aliyokuwa ameivaa kiunoni kama mkanda. Mama Neema alimtathmini mtu yule ambae kwaharaka hakujulikana kama ni mtoto alietaraji kuingia duniani au ni mzee wa miaka elfu moja na kuendelea. Mtu yule alinyenyekea zaidi mkono wa Neema uliyokuwa umeshikiria shilingi miatano na asimuangalie usoni kama wafanyavyo wengine. Haikuhitaji hadubini kuzigundua shida zilizomjaa mtu yule. Wala hakukuwa na haja ya kutumia darubini ilikutazama kubaini ugonjwa wa kisasa aliyokuwanao bwana yule. Naam, kuna waliyompita huku wakitema mate kwani alitoa harufu kutokana na kukosa matunzo, pia ombaomba wenzake walimtenga na kumuweka mbali kidogo na wao kwa kuwa kosesha wateja.





    Macho ya Mama Neema yaliendelea kuuangalia mwili wa mtu yule kwa umakini zaidi huku akili ikiendelea kupekuwa kwenye mafaili yake kwa ajili ya kujaribu huenda anajulikana.



    "Ki... Ki... Kiki... kibakuli?" Aliongea kwa mshangao huku akiruhusu kidole chake kisonte mwili wa mtu yule.



    Mawimbi ya sauti ya Mama Neema yalipiga vilivyo kwenye ngoma ya masikio ya mtu yule ambae kama ukimuita ombaomba ndio utakuwa umetaja jina la kazi yake. Sikwamba hakuisikia sauti iliyoita. Aliisikia vizuri tu lakini hakupata muda wa kuifikiria zaidi kwani katika maisha yake hakuwa na kumbukumbu kama alishasikia sauti ya aina ile ikimshangaa.



    Kwa udhaifu mkubwa akayachukuwa macho yake na kuyahamishia mwilini mwa Mama Neema.



    Mtu yule hakuamini alichokiona. Alihisi huenda ni jinamizi imemuijia mchana mchana. Alijikebehi kwa mshangao lakini alijiona mpuuzi baada ya kugundua kuwa giza lilikuwa halijaingia. Kwakuwa hakuwa na imani na macho yake, aliyapikicha kisha akaangalia tena lakini aliishia kuiona sura ileile.



    "Aishaaaa!!!!" Alishangaa sana ombaomba yule baada yakugundua kuwa kumbe macho yake yalimkutanisha na mwanamke anaemjua kwa jina la Aisha.



    "Ndio mimi Kibakuli wangu. Vipi mbona upo kwenye hali hii?" Alihoji Mama Neema huku akiangusha kapu lake chini "Yuko wapi Dada Aneth. Umefikajefikaje hapa?" Mama Neema hakuna alichojibiwa zaidi ya kuishia kuyaona machozi ya mtu yule.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kabla hajaongea, akakohoa kikohozi cha pumu, kisha akayameza makohozi yake kwa kujua kuwa endapo yakionekana basi na chembechembe za damu zingeonekana.



    Mama Neema hakuhitaji kuhangaika kufikiri ilikutambua kuwa mtu yule hakuwa na makazi. Haraka alikodi tax na kumpeleka moja kwa moja hadi kwake. Alikaa nae mpaka muda aliporejea mume wake. Alimuelezea kiufupi na kuomba wampeleke hospitali.



    Kwa ushirikiano wa Baba Neema na Mama Neema walimchukuwa mtu yule na kumpeleka hadi hospitali ya bugando. Alilazwa na matibabu yakaanza mara moja.



    Docta Endrew ni mfanyakazi katika hospitali ile lakini yeye huusika na vichaa tu. Kipindi anatoka kazini alipamiana kwa bahati mbaya na Mama Neema kitendo kilichopelekea adondoshe mafaili kadhaa aliyokuwa ameyashikiria.



    "Oooh! Samahani mdogo wangu." Aliongea Mama Neema baada ya kupamiana na Docta Endrew.



    "Bila samahani dada. Kawaida wala usijali." Wote kwa pamoja wakaokota makaratasi machache pale chini kwakusaidiana.



    "Ok, thanks.. Naitwa Endrew ni dacta na ninahusika na wagonjwa wa akili." Alishukuru Docta Endrew baada ya kukabidhiwa karatasi na Mama Neema. Kisha akajitambulisha.



    "Nimefurahi kutambua jina lako. Mimi naitwa Aisha Mapuya au zaidi unaweza ukaniita Mama Neema."



    "Oooh! Ok.. Bila shaka umeleta mgonjwa."



    "Ndio wala hujakosea."



    "Aaah! Ninani yako?"



    "mhh! Kaka tu"



    "Ok, kwasasa ninaharaka kidogo. Labda nikuachie business card yangu utanitafuta kwa msaada zaidi kuhusu mgonjwa."



    "Kaka unadhani wenzio tumesoma? Sasa hizo sjui bibinesi dadi tunapesa ya kuzinunua basi. Ndio kwanza mgonjwa yupo hospitali kwani zinauzwa hapa hapa?"



    Docta huku akitabasamu."hapana dada yangu. Business card sio dawa. Ok, basi tuachane na hayo. Una simu?" Mama Neema akatoa Simu kisha wakabadilishana namba na wakaachana.



    Docta Endrew alienda mpaka kwake na kukutana na Mavugo ambae kwa muda huo alikuwa nje ya nyumba ile huku ametulia.



    "Vipi mbona leo umechelewa kutoka?" Alihoji Mavugo baada ya kusalimiana na Docta Endrew.



    "Kuna mdada nilipamiana nae kwa bahati mbaya kipindi nakuja sasa nadhani yeye ndie kanichelewesha. Lakini hakuna kilichoharibika kwani nimechelewa kama dakika tano pekee."



    "Ok, pole kwa hilo. Lakini wakati mwingine unapaswa kuwa makini sana na muda iliusipoteze mambo yako ya muhimu. Kumbuka sekunde moja ikikupita nisawasawa na kupitwa na madili miliöni moja sasa vipi wewe upitwe na dakika tano zote halafu ulizike? Usikubali muda ukupite hata kwa dharula. Kumbuka laiti kama dunia ingekuwa haiyaheshimu masaa basi mambo yako yote yange goma. Hebu ona uaminifu wa dunia, kila siku inajizungusha katika muhimili wake kwa masaa 24 na kuzalisha usiku na mchana. Sasa kwanini wewe ukubali dharula ziingilie mipangilio yako? Usilaumu nchi jilaumu mwenyewe." Ni kawaida ya Mavugo kuchambua kila jambo liwe dogo au kubwa. Kwakuwa docta Endrew alikwisha mzoea, jambo hilo halikumsumbua sana. Alimuomba waingie ndani. Walikaribishwa kwa vizuri kama ilivyo kawaida ya mke wa Docta Endrew kumkaribisha mumewe pindi atokapo kazini.



    Upande wa hospitali Docta aliwaita mama neema na baba neema.



    "ok, inabidi tu mkubaliane na matokeo. Mgonjwa wenu ana Virusi vya ukimwi na inaonekana hakuwa akitumia hata A.R.V. Hivyo magonjwa mengi yamepata ruksa ya kumuingia kwa haraka zaidi na kumdhoofisha. Ina bidi abaki hapa hospital kwa muda wa wiki nzima ilituangalie hali yake itaendaje." Ni baadhi ya maneno aliyoongea Docta.



    Walikubaliana na maneno yale kisha wakaaga na kwenda kwao.





    . Wakiwa njiani kuelekea kwao. Baba Neema alihoji maswali mengi sana ikiwa ni kuhitaji kumjua huyo waliyekuwa wakimsaidia.



    "Baba Neema.. Subiri kwanza hali yamgonjwa iwe vizuri na hapo ndipo nitakapokujibu maswali yako kiusahihi zaidi." Majibu ya Mama Neema hayakuwa yakimridhisha Baba Neema hata kidogo. Kwakuwa kwa muda huo Mama Neema hakuwa sawa kiakili. Baba Neema hakuona haja ya kuendelea kumfyatulia maswali yenye majibu yasiyoridhisha.



    Walifika nyumbani na zoezi la upishi kwa Mama Neema likaanza. Alipomaliza kupika walikula.



    "Sasa.... Unajua leo umenitoa tu kazini kwa dharula."



    "Kwahiyo?" Alihoji Mama Neema.



    "Kwahiyo nini.. Sinahtaji niende zangu kwa wifi yako, pombe. Siunajua ndomida yenyewe hii." Aliongea Baba Neema huku mkono wake wa kushoto akiuangalizisha kulia na kutazama Saa yake.



    "Hivi... Hata kama ndo mapenzi ya dhati na hiyo pombe! Ndo uache matatizo hapa ya wagonjwa na wewe kwenda kupombeka." Akaongea Mama Neema huku ameweka mikono yake kiunoni mwake.



    Baba Neema hilo hakulijali sana akaanza safari ya kwenda kuisaka pombe. Mama Neema akajiweka mlangoni na kuziba njia ilikusudi Baba Neema au Devi asiondoke.



    "Mbona unanizuia?"



    "Kwasababu hutakikunielewa. We unadhani ukirudi umelewa hayo mawazo yakushauriana yatatokea wapi?" Alihoji Mama Neema. Hapo Devi ikabidi atumie utaalamu wake wa maneno. Akamlaghai Mama Neema mpaka akakubali kuiachia njia.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Devi alienda kwenye pombe kitendo kilichompelekea Mama Neema kuboeka kukaa peke yake ilhali anamawazo.



    Alikumbuka jambo. Akachukuwa simu yake na kuibonyeza kana kwamba kuna kitu anatafuta. Alipopata na kujiridhisha aliiweka simu ile kwenye sikio lake. Iliita na mwisho wa siku ilipokelewa.



    "Hello!" Sauti kutoka kwenye simu iliita. Mama Neema alijibu na kisha kujielezea.



    "Usijali.. Hatamie ulinipatia namba zako hivyo hakuna kilichoharibika hapo. Enhee vipi mgonjwa wenu anaendeleaje?" Alihoji mtu yule wa upande wa pili. Mama Neema alimjibu na kumpatia maelezo yote waliyopatiwa na Docta.



    Baada ya kupeana taarifa. Hakukuwa na ziada zaidi yakukata Simu.

    Mama Neema kila akifikiria, chozi lilizidi kumtoka. Alijitamania kufa kwa kuliko kuendelea kutatua matatizo yasiyo tatulika. Alijiona kila kosa lililoendelea.. Yeye ndio chanzo cha kosa hilo. Kwanini asiangue kilio ilikuiridhisha nafsi yake juu ya kipindi kigumu alichonacho? Aliuchukia uwepo wake na alijihisi yeye yupo duniani kwa ajili ya kuwaweka watu matatizoni.



    Alikumbuka ile siku aliyomuingiza matatizoni yule mtu aliejitambulisha kwa jina la Mavugo. Akakumbuka jinsi alivyo mharibia maisha Kibakuli kule kwa Aneth. Naam, yule Getiman ndio aliitwa Kibakuli. Alikumbuka zile siku zote alizoishi pale kwa Aneth akiwa kama mfanyakazi wa ndani. Alifumba macho na kuminya chozi kishalikaanguka chini.



    Ni mengi aliyoyawaza mpaka akahisi yeye amebeba maovu na uwepo wake utaendelea kutangaza maovu zaidi. Akatamani kujiua. Akakiendea Kisu huku baada ya kuandika maandishi ya kutokuhusishwa katika kesi ile kwa mtu yeyote. Kishaakashikiria kisu na kukiangalizisha tumboni. Akiwa anakipeleka tumboni aliwaza mengi sana, akakumbuka alivyomuhangaikia mwanae na pia akawaza maisha ya mwanae baada ya yeye kufariki. Akauona ugumu wa mwanae ataoupitia bila Mama. Pia akamfikiria kibakuli atavyoteseka. Hapohapo yakajirudia kichwani mwake yale maneno yenye busara aliyowahi kuambiwa siku aliyofanya mauaji. Alimkumbuka vilivyo huyo mtu aliejitambulisha kwa kipindi kile kwa jina la Mavugo. Akapata picha matatizo atakayo yaacha kwa Devi pindi maafande watakapo mng'ang'ania kama mshukiwa namba moja wa mauaji. Hapohapo akafumba macho yake mawili na kukitupa kisu kile chini.



    Aliamua kuichana ile karatasi na moja kwa moja akakimbilia chumbani mwake na kujibwaga kitandani huku akiendelea kulia.



    ..... .... ......



    Baada ya muda kupita, ulisikika wimbo uliyokuwa ukiimbwa kilevi. Wimbo ule ulikuwa ukiisifia bia tu na ulionekana ni mpya masikioni mwa kila aliyeusikia. Sauti ya wimbo ule ilisikika vyema sikioni mwa Mama Neema nae akaitambua sauti ile na mtunzi wa wimbo ule bila shaka alimtambua.



    Muimbaji alipofika mlangoni aligonga mlango na kufunguliwa na Mama Neema. Hata alipofika alianza ucheshi wake wa hapa na pale. Baadae alijitupa kwenye sofa na kupitiwa usingizi palepale. Huku Neema kwa muda huo nae akiwa amerejea kulala.





    Usiku wa siku hiyo ulipita. kulipo pambazuka Mama Neema aliamka na kwenda kufanya usafi wa mwili baada ya hapo alimuamsha Devi ambae alikuwa amelala sebuleni kutokana na pombe aliyo kunywa usiku wa kuamkia siku hiyo. Devi baada ya kuamka nae alifanya usafi wa mwili huku Mama Neema yeye akianza uwashaji jiko kwa ajili ya mapishi.



    ''Vipi kwani kuna haja ya mimi kwenda kumuona mgonjwa?'' Alihoji Baba Neema.



    ''Haina haja kwani kinachotakiwa hapa ni mimi kwenda kumpelekea chakula tu. Kwahiyo sidhani kama swala hilo lina weza kukufanya wewe uhangaike namna hiyo. Wewe nenda tu kazini, nitakupa habari'' Alijibu Mama Neema.



    ''Sawa haina shida achamie niende kazini manake kuna kazi za watu jana zime lala sasa naimani watakuja asubuhi kuziijia.'' Aliongea Baba Neema.



    Walitaniana kidogo kisha Baba Neema akaondoka nyumbani na kuelekea kazini. Alipofika alichukuwa vifaa nakuanza kupaka rangi kabati aliyoilaza jana, alipomaliza alihamia kwenye vitanda kadhaa ambavyo aliacha kuvipiga msasa siku iliyopita. Alifanya kazi zile na kuzimaliza saa moja kabla ya wale wahusika kuanza kuja. Hata walipofika walimlipa pesa yake nae akawapatia vitu vyao.



    ''We Marijani... Hebu nnjoo hapa mara moja'' Aliita Baba Neema kumuita mmoja kati ya wafanya kazi wake.



    ''Ndio nakusikiliza mkubwa'' Aliitikia wito kwa heshma.



    ''Nadhani unakumbuka vizuri kuhusiana na ile inshu ya kutengeneza madwati ya shule. Vipi unayafuata saa ngapi maana naona muda unazidi kwenda tu. Wakati tuna kazi nyingi.. Au we unapenda kila kitu hadi ukumbushwe?'' Alihoji Baba Neema.Na hapo ndipo Marjani akakumbuka kuhusu swala lile.



    ''Lakini Boss ile inshu ya shule simpaka saa tatu au nilisikia vibaya?''



    '' oooh... Shit!!!!! Hivi wewe Marijani huwa unatumia akili ya nani kufikiria?''



    ''Nani?? mimi??''



    ''Kumbe naongea nanani?"'



    '' Hahahahaha... Bosi bwana. Nilidhani unamuuliza mtu mwingine. Sasa bosi inamaana watu huwa wanatumia akili za kina nani kufikiria?''



    ''Sipendi maswali hebu nenda kafanye kazi'' Aliongea Baba Neema na Marjani akatii.



    Nikawaida ya Marjani kugombezwa na Bosi wake kwani nae nimmoja kati ya wale binadamu waliyopo kwa ajili ya masihara. Sasa mara nyingi Baba Neema si mpenzi wa masihara pindi awapo kazini. Lakini huwa ana vituko pindi tu aiwekapo pombe kinywani. Na hayo ndio maisha ya Baba Neema. Ufundi seremala ndio unamlisha yeye pamoja na familia yake, una msomesha Neema, na kupangilia mambo mengine ya kimaendeleo. Ni bora uchezee sehemu yoyote lakini si hiyo yake ya kazi.



    .............................. ...............................................CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Musa alianza kazi ya kuuza duka huko Dar-es-saalam. Duka lenyewe lilikuwa ni lile linalohusika na maswala ya ujenzi. Naam, lilikuwa kubwa sana kitendo kilichopelekea yeye kuongezwa pale na kuweka idadi ya wauzaji wawili maana haikuwa rahisi kwa muuzaji yule wa mwanzo kuwa ridhisha wateja wengi ambao waliyokuwa wakija pale na kununua vifaa. Wengi wao walikuwa wakikasirika na kuondoka kutokana na foleni huku wengine waki hudumiwa ilhali wana fyatua malalamiko. Naam, ujio wa Musa ulisaidia sana kwani wateja wengi walianza kupata haki zao na waliendelea kufurika kila leo kutokana na upatikanaji wa mahitaji yao kiurahisi.



    Musa aifanya kazi yake kwa bidii sana huku akifikiria jinsi maisha yao yalivyo magumu. Bahati nzuri ile kazi yao hawakuifanya hadi usiku bali waliifanya hadi mida ya saa kumi na nusu na kufunga duka lao kisha kurejea pale walipoishi wote kwa pamoja.



    ''Dah! leo nimechoka sana, siunajua wateja walivyokuwa wengi. Yaani sasa hivi naenda kulala kabisa maana duh!!'' Aliongea Musa kipindi anafanya harakati za kufunga pale.



    ''pole sana jamaa.. Ila wewe kaza tu. Siunajua mwanzo mgumu.... Sema nini? nakupa bigapu. unajitahidi sana mkali wangu. Mi... nilikuwa nakuchukulia mchumba tu. Kumbe kazi unaiweza mwanangu.'' Aliongea Paul au pal kama alivyojiita na kupenda watu wa muite. pal yeye ni mzoefu na ndio mfanyakazi mwenzie na Musa. Yeye Pal sikwamba aliokotwa au kuletwa kufanya kazi kwa msaada. la. huyu pal yeye ni mtoto wa dada yake na mwenye duka kabisa, yeye kwakuwa hakupenda kusoma. Aliamua kumuomba mjomba wake kazi ya dukani nae mjomba wake akampatia bila kinyongo cha aina yoyote.



    ....................... .................................................



    ''Mavugo acha mie niende nikamuone yule dada nilokwambia kuwa ni rafiki yangu.''



    ''Yupi huyo? aaaaaaaah kumbe yule ambae ulinambia ana mgonjwa''



    ''yes.. Huyohuyo. Kuna mambo anahitaji kunieleza sasa ameomba nikamsikilize kisha ni mshauri''



    '' Umshauri?'' akacheka Mavugo tena kwa kicheko cha dharau. Kisha akasema. ''Hivi wewe ndugu yangu, ushaona maji yakidanganywa hata siku moja?'' Hapo Docta Endrew nikama hakuelewa chochote ikabidi aulize.



    ''Sikia Endrew.. Usitake kunifanya mie mtoto sawa? unajua tokea elimu itolewe vichwani mwa watu na ikakusanywa kwenye vitabu iliwatu mjifunze. Matokeo yake mmeshinwa kujifunza na kuanza kutengeneza matabaka ya wasomi na mbumbumbu.'' Aliongea Mavugo na kumfanya Docta Endrew ajihisi vibaya.



    ''Aaaaaaah! Unajua Mavugo hapo unakosea sasa.. Kwani kuonana na rafiki yangu kuna uhusiano gani na elimu yangu?''



    ''Kijana kuwa uyaone. Mkubwa akikosea huwa haambiwi kwa namna hiyo. Kingine mimi nimekwambia hivyo kutokana na maneno yako yaliyo likosea heshima sikio langu. Huwezi kunidanganya kisa unadhani sijui.. Hivi toka lini mtu aliyepata matatizo akapatiwa ushauri? au ndio tuseme hujui hata maana ya ushauri eti?'' Aliongea Mavugo. Hapo Docta Endrew akatabasamu kidogo na kuiachia ile sura yake ya mikunjo aliyoanza kuitengeneza.



    ''Kweli.. Nilikuwa nimesahau ugonjwa wako. Kumbe bado unaumwa? Kwani wewe kwa akili zako unaweza kumshauri mtu wa aina gani kama unasema mwenye matatizo hashauriwi'' Alihoji Docta Endrew kwa mzaha.



    '''We.. naona shule ilikuharibu na si kukufunza. Hebu kabla hujaondoka na kwenda huko. Naomba nikufunze jambo'' Aliongea Mavugo na Docta Endrew akakaa ilikusikiliza utumbo wa Mavugo kama alivyodhania.





     '' Unajua ushauri huwa hautolewi baada ya tatizo bali hutolewa kabla ya tatizo lakini umetumia laghai zako tu kunidanganya kuwa unaenda kumpa ushauri mtu ambae tayari ana matatizo'' Aliongea Mavugo na kumpelekea Docta Endrew aangue kicheko chakujilazimisha ilikuibua dharau iliyo jificha moyoni mwake.

    ''Kweli wewe ni Kichaa.... Ina maana unatakakuniambia watu wote wanaopewa ushauri hua hawana matatizo? Hebu punguza kichaa bwana, kwani mimi ninapo kushauri wewe baada ya kukosea huo hauitwi ushauri? ahaaaa!!! acha hivyo bwana Mavugo kwanza unazidi kunilia muda wangu acha mie niende.'' Aliongea Endrew huku akianza kunza kuondoka.

    ''Subirii!!!'' Ilisikika sauti ya kukalipa iliyomfanya Endrew asimame, kisha Mavugo akamsogelea. ''Unajua wewe unajifanya umtaalamu sana wa mambo eti kisa umekabidhiwa kuhudumia wagonjwa wa akili. Hebu ngonja nikupe somo kabla hujaenda huko kwa huyo mtu wako.. Unajua kuna vitu viwili ambavyo umeshindwa kuvitofautisha na kujikuta ukijiona uko sawa kumbe unakosea.. Kuna kitu kina itwa ushauri na kuna kingine kinaitwa nasaha,'' Hapo Endrew akawa makini kusikiliza.

    '' Ushauri wenyewe hutolewa kama tahadhari kwa ajili ya jambo linalo sadikika kutokea au kinga ya jambo hilo.Halafu pia kuna kitu kina itwa nasaha, hichi hutolewa baada ya jambo fulani kumtokea mtu. Sasa wewe kwenye nasaha unaweka ushauri na kwenye ushauri unaweka nasaha na hapo ndipo kutokuelewana kwetu kunapoingia'' Aliongea Mavugo kisha akaanza kuondoka na kurejea ndani. Docta Endrew yeye akajikuta akipatwa na bumbuwazi kwani hakutaraji kabisa kama angekuwa na makosa. Hapo kwa mara nyingine akamuomba Mavugo msamaha na zaidi akapendekeza kama Mavugo ataweza basi aendenae kule alipohtaji kwenda.

    ''Hapana mie sijiskii kutoka acha nibaki tu. Wewe nenda wala usijali'' Alikataa Mavugo.

    ''Tafadhari naomba nawe uungane nami angalau ukampatie nasaha zako yule dadanakuomba'' Aliendelea kubembeleza lakini Mavugo alikataa katakata ndipo Endrew alipoamua kuondoka yeye mwenyewe.

    Alienda hadi eneo walilo ahidiana wakutane na Mama Neema, alipofika walisalimiana na maongezi ya kaanza.

    ''Unajua dokta mie nimekuita hapa ili uweze kunisaidia maana kuna mambo ambayo yanakisumbua sana kichwa changu'' Aliongea Mama Neema na Docta Endrew aiendelea kuonesha umakini katiika kusikiliza kile alichokuwa akihitaji kuambiwa.

    '' Dokta mie unavyoniona mpaka hapa ni muathirika wa virusi vya ukimwi na ninaishi navyo kwa zaidi ya miaka kumi na tisa illiyopita......'' Alihadithia yote yaliyompata katika maisha yake na hakuficha hata moja mbele ya Docta Endrew yaani alieleza mpaka ile siri iliyopo kati yake yeye na Baba Neema kwamba yeye na Baba Neema simke na Mume bali ni kaka na dada wa hiari lakini waliweka siri tu.

    Hapo Docta Endrew akapumua na kukosa hata aya yakuanzia, alibaki akilishangaa umbile dogo la mwana mama yule huku akitathmini mengi aliyo yapitia katika maisha yake alichoka. Jasho lilijikuta likimtoka ghafla bila yeye kukusudia huku akizidi kumuhurumia zaidi Mama yule.

    ''Ina maana unataka kuniambia ulishawahi hadi kuua?''CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ''Ndio Dokta''

    ''Sasa mbona serikali haijakuhukumu. na ilikuwaje hadi akahukumiwa mtu mwingine tena asiye na makosa wakati wewe muuaji ukibaki nje''

    ''Dokta!!! Nimesha kwambia kuwa yule aliye hukumiwa alihukumiwa kwaiaba ya kunisaidia tu. Nahakuna yeyote anaejua kuwa mimi nilishaua zaidi ya wewe niliyekuambia pamoja na Devi tu. Tafadhali nisaidie dokta kuhusu suala la huyu mbonjwa wangu muathirika ambae alisababishiwa uathirika na mimi. Nimfanmye nini maana kiukweli japo ni miaka kumi na tisa imepita lakini bado na mpenda. Istoshe mimi kwa sasa naishi na Devi toka miaka hiyo iliyopita pia nakumbuka kipindi nafukuzwa kule kwa Aneth mimi na mimba yangu. Kibakuli alihitaji kuondoka na mimi lakini nilimzuia tu, ila mpaka leo anajua kuwa ile mimba ilikuwa yake wakati, ni yayule mwana haramu aliyekufa miaka kadhaa kwa kifo alichostahili aliyeitwa afande Kipara. Tafadhali dokta nisaidie maana huyo mgonjwa akigundua kuwa mimi ndie nilyemuambukiza ukimwi basi atanichukia tena atanilaani kama nikimwambia kuwa Neema si mwanae wa kumzaa. Bora Neema ningekuwa sijampa historia ya maisha yangu lakini tayari hakuna asilolijua kuhusu mimi. Sasa we unadhani hapo mie nifanye nini. Tafadhali Dokta nisaidie, sihitaji kumpoteza kibakuli wangu''

    Hapo Dokta Endrew hakuwa najibu zaidi ya kukikuna kichwa chake tu. Alijaribu kufikiria mpaka mwisho wa akili zake lakini hakuna alichoweza kukiambulia ambacho kina weza kuwa msaada kwa Mama Neema.

    ''Dada nimekuelewa sana. lakini swala lako linahitaji ufikiri wa hali yajuu zaidi kwani yakifanyika makosa kwenye kufikiri. Basi kutatokea tatizo kubwa sana. Hivyo nilikuwa ninaomba unipe muda wa kufikiri. Lakini kwakuwa sasa hivi mwanao Neema yupo shule, basi mi sioni kama kuna ubaya wewe ukikaa na kaka yako huyo wa hiyari kisha umueleze jambo hilo ili huyo mpenzi wako akiruusiwa kusiwepo tena na mitafaruku ya hapa na pale. Akikuuliza kuhusu mtoto, wewe usimwambie kuwa si..wake bali mwambie kuwa ni wake na kwasasa yupo shule. Siku Neema akirejea hapo nadhani tayari cha kufanya kitakuwa kimesha fahamika.'' Aliongea Endrew na wote kwa pamoja wakaagana baada ya kumaliza maongezi yao. Kwa namna fulani Mama Neema aliridhika a ushauri ule hata alipofika nyumbani alifanya mambo yake huku akimtegea Devi arudi jioni.

    Siku hiyo Devi alirudi jioni huku kinywa chake kikiwa hainukii pombe, kwakuwa alijua kunauwezekano siku hiyo kukawa na kikao kati yake na Mama Neema maana hata yeye alikuwa na shida ya kufahamu mambo mengi kuhusuyule mtu waliyemsaidia kwani hakuwa akimfahamu hata kidogo.

    Baada ya kupata cha kula cha jioni ukurasa wa maongezi ulifungulwa kati yao na hiyo ni baada ya Devi kutaka kumjua yule mgonjwa waliyemsaidia



    'Mhhh!! dada yangu hapo una mtihani sana maana endapo mambo haya yakijulikana zaidi. Inaweza kuwa hatari sana na hata kukugharimu. Hapa unachotakiwa kufanya nikuacha nyuma ya pazia pabaki mamefungwa na kufanya usiri tu. Haina jinsi.

    Mdanganye kuwa mtoto ni wake ilikuokoa mengi, nibora atambue kuwa wewe ndie chanzo cha yeye kuwa hivyo ilhali anajua ana mtoto. Kuliko kujua ukweli. We fanya hivyo na imani mambo yataenda vyema tu na sir itaendelea kutunzwa.'' Aliongea Devi huku kwa wakati huo Aisha akizungusha mikono yake kichwani kwa kumaanisha kwamba kwa muda huo akili yake iikuwa inavuruga tu.

    ''Kaka usitake kuniambia kuwa kutunza siri kwa Kibakuli ndio suluhisho la matatizo,'' Aliongea Aisha kisha akavuta pumzi kidogo na kuendelea kusema.''Mpaka sasa tayari Neema anajua kuwa wewe si Baba yakke mzazi nami nilimwambia ukweli wa mimi na wewe japo sikumwambia kuwa wewe ni kama kaka yangu ila anajua kuwa wewe simzazi wake. Sasa we unadhani Neema anaweza kukubali kuishi na Baba nitae mletea na kumtambulisha kuwa ndio Baba yake? kumbuka anamchukia sana Baba yake japo sijawahi kumwambia kuwa hayupo duniani yule mwana haramu.'' Aliongea Aisha huku akionesha wazi kushindwa kuya vumilia aliyokuwa akiyaongea. Hapo Devi akashusha pumzi ya nguvu.

    Ati, anamjua Baba yake? Ati anatambua kuwa mimi si Baba yake? Toka lini?. Ni maswali yaliyoendelea kukizunguka kichwa cha Devi. Maswali hayo hayakuwa haba kiasi cha kumfanya kichwa chake kisimuume. Hapo akauchukua mkono wake wa kulia na kuanza kuutembeza kichwani mwake si kwa ajili ya kusafisha nywele zake! bali ni kukikunakuna tu na asielewe nini alipaswa kukifanya.

    Nikama kiti alichokalia kilikuwa na miba jinsi alivyo jitoa kwacho. Alisimama sasa na hapo akannza kutembea kwakuzunguka palepale huku paji lake la uso akiendelea kulisurubisha kwakutumia kiganja cha mkono wake ambao ulitoka punde tu kukuna kichwa chake.

    ''Kwahiyo unataka kunambia kuwa Neema tayari anajua kila kitu!!!!!???? kwanini ulimjuza mapema sana? kwanini??? ahhhhh!! sasa nini maana ya kutunza siri toka kipindi kile? ah! kama ulijua utafanya hivyo mbona ulikubali kutunza siri halafu kwa unafiki wako eti ukiwa nami unaniita mumeo. Sasa kumbe huwa una nifanyia unafki tu.'' Aliongea Devi huku akipiga piga ukuta baada ya kuliachia paji la uso wake. Akaona kama kuendelea kuendelea kuwa pale ni kama kero akaanza kuchukuliwa na miguu yake ilikupelekwa ndani lakini kabla hata hajavuka maeneo yale akadakwa mkono. Hapo ikabidi ajigeuze na kutazama nyuma ilikujiridhisha japo alitambua wazi kuwa aliyekuwa amemshika ni Aisha. Ndipo alipomuona aisha akiwa amemkaza mkono huku akiiruhusu miguu yake kusakiti eneo lili na kuyaruhusu magoti yake kutua chini kisha akaanza kuomba msamaha.

    Aliomba msamaha wakuridhisha sana na akaongezea kwakusema kuwa Neema bado anajua kuwa mimi na wewe ni mtu na mkewe isipokuwa tu ameshajua kuwa wewe si mzazi wake. Nilimueleza ukweli siku aliyonibana sana, siku hiyo sikuwa na jinsi zaidi ya ukweli tu Lakini haikuwa dhamira yangu, naomba unisamehe'' Msamaha aliupata baada ya kujieleza kiundani zaidi mpaka Devi akaridhika.

    Mama Neema alieleza mbinu aliyopewa na Docta Endrew na Devi akaridhika nayo.

    ''Ipo vyema.... Inafaa hiyo'' Alisema Devi baada ya kuulizwa kama waitumie au la.

    Siku hiyo waliagana huku wakiwa wamekubaliana kuifuata ile mbinu ya Docta Endrew.

    ............................. ....................................................... .................

    Musa yeye aliendelea kuangalia video usiku ule ilhali wenzake wakiwa wameondoka na kumuacha peke yake sebuleni. Naam, nikwakua vitu kama vile hakuwahi kuvipata akiwa nyumbani kwao ambapo si video tu. Bali hata umeme haukuwahi kuingia kwao.

    Alikuwa ameanza kuifuatilia tamthiia moja ya kikorea ijulikanayo kwajina la Dong yi. Kwakuwa alkuwa akiifahamu lugha ya kigeni, jambo hilo halikuweza kumtatiza sana kushindwa kuelewa mpaka tafsii za maneno zilizo kuwa zikipita kila wahusika walivyo kuwa wakiongea. Hakika aliifurahia tamthilai ile iliyosheheni masuala ya utawala wa kifalme huku ikitembea na dhamira ya mapenzi. Alimpenda sana Dong yi akamchukia Lady jung kama ambavyo alivyopatiwa roho ngumu kwenye hadithi ile Zaidi nile penzi tamu na la kipekee lililochorwa kati ya mfalme na Dong yi ndilo liliweza kumvutia zaidi na kumfanya ajihisi yupo na mpenzi wake Neema. Mawazo yalikitawala kichwa chake na kuanza kuingiza amri za kumbukumbu zilizomrudisha mbali kimawazo na hata kuikumbuka ile siku aliyotamkiwa wazi na Neema kuwa lazma atamuoa kwa hali yeyote ile pasina kujali msululu wa shida zilizomo katika familia yao.

    Kila alipo kumbuka bas aligundua kuwa amemkosa sana mpenzi wake yule, alitamani awe karibu nae lakini masomo ndio tatizo ila kwa upande mwingine aliona hata kama angekuwa karibu nae angemlishanini? angemlaza wapi? angempeleka wapi? Hapo ndipo hasira za kujituma katika kazi kwa bidii ziliendelea. Akalisaliti sofa na kuanza kujongea hadi chumbani kwake alipofika alifanya utaratibu wa kuchojoa mavazi ya juu na kubakiza yale ya ndani aliyoyateua kwa ajili ya kulalia akakiendea kitanda chake kilichokua hatua kadhaa mbele ya macho yake kisha akajibwaga na kuyaruhusu mawazo yamtawale kwa hiyari yake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alidhani huenda mawazo yange mrudisha kwenye ile fikra ya mpenzi wake Neema, badala yake yalimfanya amkumbuke Mama yake na akumbuke jinsi shida alivyo jaza utajiri nyumbani kwao. Hakika hakuipenda shida japo shida ilimng'ang'ania na hata kumvuta shati kila siku lakini alijitahidi juu chini kuikwepa na ndio maana alifanya kazi kwa bidii huku akiamini kuwa yale yaliyomo katika maisha yake kwa wakati huo yataja kuwa historia. Alipokumbuka kuwa kwa wakati ule Mama yake alikuwa na simu. Akaichukua simu na kubonyeza vitufe kadhaa kisha akaiweka sikioni. Simu iliita kama sekunde kumi tu na hapo hapo ikapokelewa, alimjulia hali Mama yake na kumuuliza juu ya upatikanaji wa chakula pamoja na mahitaji mengine muhimu. Mama yake alishukuru Mungu na kumwambia kuwa kila kitu anapata kwani mfanya biashara yule anampatia msaada wa kutosha kila aendapo Mwanza.

    Baada ya maongezi yale hapo kidogo roho ya Musa ikaridhika kwani huwa anapatwa na mashaka sana kila amkumbukapo Mama yake, akaichukua shuka na kujifunika hakuchukua muda sana tayari usingizi ukawa umemchukua.

    .............................. ......................................................



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog