Simulizi : Kichaa
Sehemu Ya Tatu (3)
. "da.. Poa mwana usiongee sana mie nimekuelewa. Lakini lazma nimwambie kuwa alichofanya sio. " Aliongea Side.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Nitashukuru kama hautomzingua. Nakujua wewe sekunde moja na kofi. Usimpige please. Siunajua japo naumia kwa yeye kunidhalilisha lakini bado nampenda?"
"poa. Usijali, achamie nirudi darasani kuandika,andika notes za kingereza. Siunajua jana sikuja skul, nilikuwa namishemishe home. Sasa teacher akikuta hujaandika Notes yeye hatakikujua."
"poa side. Achamie niendelee kuvumilia."
Waliagana marafiki wale. Side akaenda kuandika notes huku Musa akiendelea kubaki darasani. Haukupita muda kengele ya kurejea madarasani ikagongwa. Wanafunzi wote wakaanza kukimbizana kuyawahi madarasa. Wale waliyokuwa wakinunua misuba, walikimbia huku wengine wakiacha chenji zao kwa mama muuza. Ungepata muda wakuwaona, nadhani hapo ndipo ungeamini jinsi wanafunzi wanavyojua kuheshimu kengele. Wale waliyochelewa walipigishwa magoti na viöngozi wao. Kwakuwa hata viongozi wa wanafunzi hupokea rushwa hivyo mwenye shilingi mia au miambili yeye aliachwa na kwenda darasani huku wale wasio na pesa wakirukishwa vichura kupelekwa ofisini kwa ajili ya kupata adhabu.
Mwalimu kibalaghashia alikuwa na kipindi baada ya mapumziko kwenye darasa la kina Musa. Hivyo alichukuwa kitabu chake cha hesabu huku mkono mwingine ameshikiria fimbo na kwenda moja kwa moja hadi darasani mwa kina Musa.
"Motto" Aliropoka mmoja kati ya wanafunzi wa darasa lile. Kisha wanafunzi wote wakakaa kimya huku wale waliyokuwa wamekaa vibaya wakijirekebisha haraka na macho yao yote wakayaelekeza maeneo ya mlangoni. Wote kwa pamoja wakasimama..
"Elimu ni ufunguo wa maisha. Shikamoo mwalimu." Walisalimu na kutulia kimya utadhani maji mtungini.
"Mar-habaa. Hamjamboo?" Aliitikia salamu ya wanafunzi kisha akawauliza hali zao.
"Hatujambo.." Waliitikia wote kwa pamoja. Hata Musa nae aliitika ilhali alikuwa ni mgonjwa wa mawazo.
"OK, kama ilivyokawaida yetu. Atakaejibu swali ndie atakae kaa sawa?" wakaitikia wanafunzi baadhi. Huku wale wagonjwa wa hesabu wakikasirika na kuzidisha chuki kwa mwalimu wao.
Mwalimu aliuliza maswali na wote waliyojibu wakakaa. Kicha akafundisha na alivyomaliza alitoa zoezi kishaakaondoka.
Wakati wote huo Musa alikuwa akikumbuka viboko vingi alivyochapwa na walimu wake, kishaakawa akiyaangalia majiraha ambayo bado hayajapona. Hakuona haja ya kukaa darasani akaona bora atoroke maana shuleni paliendelea kumboa.
Alitoroka na kwenda kwa rafiki yake mchoraji ajulikanae kwajina la Macho.
"Oy, macho niaje."
"Shwari Musa. Vipi mbona mapema? Au umekuja kunivunja goti la chai. Nini"
"Aaaah! Hapana Macho. Mie nimekuja kusikilizia. Siunajua tena huko skul. Miyeyusho sana. Nimeona bora kuja huku kibandani kwako."
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwakuwa Macho. Alikuwa ni mmoja kati ya wale ambao swala la Elimu lilisha wapita kushoto. Alifurahia uwepo wa Musa muda ule ambao musa angefaa kuwa darasani.
Usihangaike kumjua macho.. Labda kiufupi... Macho ni mtoto wa Mzee Sadick, kabila la baba yake ni msukuma. Macho hakuwa na Mama kwasababu Mama yake alifariki kipindi Macho anazaliwa. Hivyo alilazimika kulelewa kigumu na baba yake. Kipaji cha kuchora kilijionesha pindi tu. Macho alivyojua kushikilia kalamu. Baba yake alimpeleka shule, lakini macho hakupenda shule. Aliwahi kurudia Darasa la nne kwa muda wa miaka minne. Kwakuwa alijua kumjumlisha na kutoa, pamoja na kuandika na kusoma vizuri. Hivyo aliona ni bora aachane na shule kishaakamuomba baba yake amfungulie kijiwe iliaanze kazi kupitia fani aliyonayo. Baba alimuelewa na kumfungulia. Mpaka muda huo Macho anamiaka saba kwenye kazi ile. Nailikuwa ikimlipa kama kawaida. Na hiyo ndio historia fupi ya Macho.
Mudi alimuelezea matatizo yake rafiki yake huyo. Nakwakuwa marafiki hao walipendana. Macho alimuhurumia sana Musa kwakuwa anayajua mapenzi kutokana na yeye kupitia hukohuko. Hakuona ajabu kumshauri rafiki yake huyo ambae alimzidi miaka tisa nyuma ya kuzaliwa.
"Hapa chamsingi ni kwenda kwa mganga ilikumfanya. Neema ajilete mwenyewe." Alishauri Macho.
"Hee! Wewe Macho. Waganga kazi yao sikutibu wagonjwa na kuwapa dawa. Sasa kwani mimi ni mgonjwa?" Alishangaa Musa.
"Ndio, wewe ni mgonjwa. Tena mgonjwa wa mapenzi.. Hivyo ni vyema kwenda kwa mganga iliakatupatie dawa za mapenzi."
"Inamaana unataka kunambia kuwa kuna dawa za mapenzi"
"Haa! We utajulia wapi mtoto wa juzi wewe... Kama kuna dawa ya malaria, ugonjwa unaoua. Ije Mapenzi tu," Akacheka Macho kisha akaendelea kusema, "Tena huyo msichana. Atajileta mwenyewe.. Hata kama alikuwa anakuchukia."
"weewee..! Macho tafadhali nipeleke sasa hivi. Siunajua tena. Na hamu yakuwa nae."
"Wewe usijali. Ngoja nimalizie hapa kazi za watu. Halafu nitakupeleka. Chamuhimu wewe nenda hom kabadili nguo. Kishaugeuze halafu twende sasa kwa mganga mahili asiyeshindwa hata siku moja."
palepale, Musa akaaga na kwenda kwao kubadili nguo. Alipofika alimsalimu mama yake na kupata chakula.
Alipomaliza kula, hapohapo akatoka mbio na kwenda moja kwa moja hadi kwa rafiki yake Macho. Alipofika akamkuta macho bado anafanyakazi. Akaendelea kumsubiri.
* * * *
Saa tisa na dakika ishirini ndio muda ambao hugongwa kengele ya mapumziko kabla ya kugongwa ile ya kutanyishwa. Ilivyogongwa kengele hiyo kila mwanafunzi alijiandaa, wale wana michezo wao waliwaza kwenda kushindana, wale walioanzisha dhambi ya mahusiano wao pia waliwaza kukutana, hata watorokaji pia hawakuwa nyuma huku wasiyopenda kusoma wakiona hicho ndicho kipindi bora kwao na zaidi walikuwa wakiomba kila siku wasisome bali wacheze tu.
"Neema twende tuwahi. Siunajua leo hatuna mazoezi bali tunacheza tu."
"ndio najua. Nyie fanyeni kutangulia mie namalizia kuweka madaftari yangu kwenye mfuko halafu nakuja huko."
"poa. Acha sie tutangulie."
Hayo yalikuwa ni majibizano kati ya Neema na marafiki zake. Neema aliachwa akiweka madaftari kwenye mfuko wake kisha wenzie wakatangulia. Alipomaliza akatoka nje na kuanza kuitafuta njia ya kwenda uwanjani.
Akiwa anaendelea kutembea huku akiwahi, mara akasikia anaitwa. Kugeuka nyuma, akamuona Side rafiki yake na Musa. Kwakuwa alimjua, hivyo hakuwa na haja ya kuendelea na safari bali alimsubiri.
"Mambo, Side?"
"Mabaya"
"mmh! Kwanini?"
"Inamaana unajifanya hujui kuwa kuna mtu ameumia, mwili na moyo kwa ajili yako? Unajifanya hujui kuwa kuna mtu mpaka sasa anaona aibu kutokana na wewe kumdhalilisha. Hebu fikiria, akitembea anahisi yupo uchi, anapopita watu wanamsontesheana mikono halafu eti unanishangaa kukwambia Mambo mabaya."
"Mbona sikuelewi Side. Kwani ninani huyo ambae nimemfanyia hivyo jamani?" hapo Neema akaanza kupata hamu ya kudadisi zaidi.
"Nani mwingine zaidi ya Musa.."
"Haa! Kumbe Musa. Huyo hatasinahuruma nae. Kwanza nilikuwa na muheshimu sana ila alichonifanyia.. Sihitaji hatakumuona."
"Kipi hicho alichokufanyia hadi usihitaji kumuona? Kipi Neema. Au kukwambia Anakupenda?"
"Kumbe, jibu unalo. Pigia msitari. Yaani bila hata aibu ananiletea barua. Mara, ooh nikilala nakuota, mara ooh, naomba ukubali kuwa namimi. Hivi kweli hata kama niwewe ungefanya nini. Kwakuwa alijifanya anajua kudhalilisha watu.. Nami nikaamua kumsema kwa mwalimu, halafu zaidi nikamchamba iliaelewe kuwa sikupenda."
"Kwahiyo Neema. Kosa la Musa hapo ninini?"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Side, usitake kujifanya hujui kosa hapo. Mbona lipo wazi. Kosa ni kunitumia hiyo sijui barua yake ya ujingaujinga" Akajibu Neema huku akibetua mdomo wake ilikukazia kauli yake.
"Kwahiyo. Kukutumia barua ndio kosa, sindio?" akauliza Side.
"Pigia msitari" Akajibu Neema kwa ufupi.
"Anhaa! Je, angekufuata mwenyewe bila barua?" Akauliza tena swali jingine.
"Angenifata. Ili...?" alibwata Neema.
"Iliakwambie kile alichokuwa amekiandika."
"Usinichekeshe.. Ina maana wewe huoni kama hayo maneno, ni yakijingajinga. Sasa ananipenda, kwani nani kamwambia anipende." Aliongea Neema, huku akijihami iliasijiweke kwenye kosa.
"Neema. Hujajibu swali, bali umeelezea tu jambo ambalo hata halina maana. Ok, hebu nijibu inamaana unataka kunambia kuwa mtu akisema anakupenda wewe unahisi nikosa eti?" Aliuliza Side.
"Ndio.. Ni kosa."Alijibu Neema. Alipohisi maelezo yake haya ridhishi hapo akaongeza, "Kwani we Side. Unataka kunambia hujui kama Neno hilo hutumiwa na wakubwa. Au unauliza nini hasa." Side alicheka kidogo kicheko chadharau, kisha akasema; "kwani Neema. Wewe haumpendi mama yako? Au baba yako? Je, ukiwaambia kuwa unawapenda nikosa? Hebu acha utoto..." Side ni kama alimchokonoa Neema. Neema hapendi kuambiwa kuwa afanyacho ni utoto. Hapo akafura kwa hasira, sura yake ikabadilika, macho yakawakilisha kuwa amani imetoweka.
"Vipi mrembo! Umechukia kuambiwa uache utoto?. Ndio.. Acha utoto, we unadhani mtu mkubwa na akili zake timamu anaweza kumdhalilisha mwenzie eti kisa amemwambia anampenda. Mimi nilikuwa nakuona umekuwa kumbe bado unamambo ya kitoto. Hebu angalia umefaidika nini. Kumtukana Mtu eti kisa kakwambia anakupenda, öna umemfanya apigwe kisa anakupenda. Je unajua majiraha amekandwa nanani? Au ulikuwa tu unamsababishia majiraha eti. Haya umeona haitoshi sasa umemtangaza kila sehemu. We huoni huo ni utoto?" Maneno ya Side yalimuingia vilivyo Neema. Palepale akajiona mwenye makosa sana. Akaondoka bila hata kuaga huku akikimbia, aliusahau tena uwanja. Na hapo akaanza kushika njia ya kuelekea kwao. Njiani hakutaka kusemeshana na mtu.
"Vipi mwanangu mböna unakataa kula." Aliuliza mama Neema.
"Hapana mama. Sijisikii tu. Kula." Alijibu Neema huku akijitoa kwenye sofa na kuanza kuelekea chumbani.
"Au.. Unaumwa?" Aliuliza tena Mama Neema.
"Hapana. Siumwi wala nini mama."
Akaingia chumbani kisha akajifunika shuka gubigubi na kuendelea kujionea aibu. Alihisi dunia nzima imemuona kuwa yeye ni mtesaji wa viumbe. Aliumia sana kila alipofikiria jinsi alivyokuwa akimshushua Musa. Alijiona ni mwenye makosa sana.
Mawazo yakaanza kumuadhibu, huruma ikaanza kuumiza moyo.
Yaani nimemsema kwa mwalimu! Mtoto wa watu ameadhibiwa! Kadhalilishwa kwa kuvuliwa uniform zake mbele yangu!! Nimemfanya ashindwe kusoma.. Nimemtangaza kwa watu. Pia nimemfuata na kumuaibisha..! Haa!. Masikini naona aibu mie. Sijui nitaanzaje kumuomba msamaha. Ni baadhi ya mawazo yaliyoendelea kukisumbua kichwa chake.
Mama Neema alishindwa kuelewa kwasababu haikuwa kawaida kwa mwanae kurudi shule majira ya saa tisa tena hataki kula. Amefikia ndani na kujifungia. Aliwaza sana lakini hakutaka kumfatilia sana mwanae. Alihisi huenda wamepishana kauli huko shuleni.
..... ..... ... ....
"Karibuni.. Karibuni.. Najua mmekuja na matatizo sana. Semeni matatizo yenu ilimtatuliwe mbele ya mganga Ngulu.. Mganga wa waganga.. Hahahahaha...hahahahaha.." Ni sauti ya kuogfya iliyomtoka mganga Ngulu baada ya kuwakaribisha kina Musa ndani ya kijumba chake kidogo kilicho zungushiwa majani kwanzia juu hadi chini. Huku ndani ya kijumba hicho kukiwa na makolokolo mbalimbali. Vibuyu vidogo vidogo vilienea juu ya shuka jekundi lililotandikwa chini huku vichupa mbalimbali vikiwa vimejaa dawa zisizoeleweka. Si tu sauti ya mganga ngulu au mganga wa waganga iliyoogofya. Vilevile kitambaa cheusi alichojifunga mfungo wa lubega, huku akipitisha chekundu ilikuwianisha na kutengeneza vazi pamoja na kile kitambaa cheupe alichokifunga kichwani huku uso wake akiwa ameuchafua chafua kwa ungaunga wa madawa yake ndivyo vilimfanya aonekane kwenye muonekano wa kutisha na kuogofya zaidi.
Alichukuwa kibuyu chake kidogo kisha akakisogeza puani na kukinusa. "Chchaaa! Chchaaa! Chaaa!" Alipiga chafia tatu mfululizo kisha akasema, "Naitwa Makata, nimetoka pande za mashariki maghalibi, kusini kaskazini mwa saudiarabia. Nimekuja hapa kwasababu nimeitwa na wanadamu wenye shida. Tafadhali ongeeni shida zenu wala msiogope nami nitawatatulia." Ni sauti ya tofauti na ile ya kwanza aliyokuwa akiitoa mganga Ngulu. Sauti hii ya sasa ilimfanya Musa aogope zaidi na kujikuta akitetemeka tu lakini Macho yeye hakuwa kwenye uoga kwani ni mzoefu na kwa imani yake aliamini kuwa yule waliyokuwa wakimsikia si, mganga Ngulu bali ni jini lamganga ngulu.
"Sisi, tunashida.. Mlimwengu huyu anateseka sana. Kuna binti ametokea kumpenda sana. Kama unavyomuona Mlimwengu amefanya kila njia lakini ameshndwa ndio maana tumeamua kuja kwako iliangalau utusaidie." Alieleza matatizo Macho.
"Ni sikia matatizo yake. Mlimwengu hebu nipatie mkono wako." Akaambiwa Musa kisha Musa akamshika mkono mganga yule japo alikuwa anamuogopa. Baada ya mganga kushikana mkon na Musa akamwambia kuwa kila jambo atalosema sharti Musa aseme 'tawile' kama lipo sahihi.
"Je, unahitaji awe anakuwazia muda wote?"
"Tawile"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ha.ha.ha.ha. Sasa mlimwengu hapa umefika. Ha.ha.ha.ha.ha. Nakupa dawa. Dawa hii uwende ukajifukize. Kadri moshi utavyotoka ndivyo wewe unatakiwa utaje jina la huyo binti. Ha.ha.ha.ha.ha. Lakini dawa hii inamasharti. Masharti yenyewe, hautakiwi uiweke kwenye mkaa bali kwenye ukuni ilimoto unapofuka ufuke na ule wa ukuni."
"Tawile."
"Haya mie naondoka. Chamuhimu wewe fuata masharti. Lakini pia usiache kutoa Elfu tano kwa ajili ya kiti."
"Tawile."
Hapo mganga akajigeuza geuza shingo kwa nguvu kisha akajibwaga chini kwa dakika moja halafu baada ya hapo akawa kama fahamu zimemuijia na kuonesha kuwa hakuwa anajua chochote kilichokuwa kikiendelea maeneo yale.
Walitoa pesa na wakaaga kisha wakaondoka. Wakiwa njiani Musa hakusita kuulizia juu ya maajabu aliyoyaona kule kwa mganga na pia aliielezea hali yake ya uoga ambayo ilimpata. Yote kwa yote, Macho alimsihi Musa kuwa atimize masharti ilidawa ifanye kazi. Hatimae walifika sehemu na kuachana. Macho akaelekea kwao na Musa akaelekea kwao. Alipofika akachoma ile dawa kwenye ukuni kisha akaanza kujifukiza moshi huku akilitaja zaidi jina la Neema. Nakumuita. Ati Neema ndio amfuate Musa. Kitendo ambacho si rahisi.
... ... ... ...
Ilikuwa majira ya saa kumi na mbili jioni. Musa alikuwa chumbani mwake akijisomeasomea huku Mama Musa yeye akihangaika nje na kuwasha Moto kwa ajili ya maandalizi ya mapishi ya usiku. Muda huo, anaonekana Neema akiwa amevalia viatu vyenye uwezo wa kugonga nyoka, huku mwili wake ukiwa umefunikwa na gauni refu lililooana na kitambaa cheusi alichojitanda pamoja na mawani meusi. Neema safari yake ilikomea pale nje kwa kina Musa. Akasalimia kisha akauliza kama Musa yupo. Mama Musa alimjibu kuwa yumo na kumuelekeza chumba cha Musa.
"Hodi.." Aliongea baada ya kugonga mlango mara tatu kwa kutumia mkono wake wakulia. Ilikuwa ajabu sana kwa Musa kusikia sauti ya kike ambyo haifanani na ile ya Ma.yake. Alishazoea kusikia sauti ya rafiki zake wa kiume kama kina Side. Lakini siku hiyo alishangaa sana kusikia sauti yakike.
"Karibu.. Pita ndani" Aliongea Musa huku akijitengeneza kwa ajili ya kumpokea mgeni huyo asiye mjua.
"Ahsante." Aliitikia Nèema kisha akaanza kufungua mikanda ya viatu vyake na kuvivua.
Neema alipomaliza kuvua viatu vyake aliingia moja kwa moja hadi ndani. Alipoingia tu, aibu ikamjaa akashindwa hata kumtazama Musa.
Kimoyomoyo, Musa alifurahi na kuamini kuwa huenda dawa ya mganga itakuwa imefanya kazi. Hapo akatabasamu rohoni huku uso wake ameukunja kuashiria kuchukizwa na jambo alilotendewa na Neema.
"Enhee! Nambie umefuata nini nyumbani kwetu? Au nd'o umekuja kuniua kabisa eti?" Aliongea Musa.
"Hapana Musa usiseme hivyo.." kabla hata Neema hajamalizia maneno yake. Musa akadakia.
"Kumbe nisemeje.. Neema. Umenidhalilisha kisa na kupenda, umenifanya niadhibiwe pia. Halafu unakuja eti unanambia nisiseme hivyo. Tafadhali toka kwetu usije kuniua bure!" Akatulia kidogo. Hapo alipotulia ndipo Neema alipopatumia.
"Nia yangu sio kukuua wala kukuumiza. Bali nikukuomba msamaha. Samahani sana kwakukuumiza. Najua umeumia sana na mpaka sasa huna amani kisa mimi. Najua unashindwa hata kusoma kwa raha kisa mimi. Tafadhali naomba unisamehe mie sikujua kama kutatokea mambo yote hayo." Aliongea Neema huku machozi yakimchuruzika.
"Eti, Tafadhali naomba unisamehe mie sikujua kama yatatokea mambo hayo." Musa akanukuu kwa dharau maneno ya Neema kisha akaendelea. "Inamaana unataka kunambia, kipindi unaichukua hiyo miguu yako na kuipeleka stafu. Hukujua kama ukinisema nitaadhibiwa? Au unataka kunambia kuwa hukusoma mwisho wa barua pale nilipokuomba kuwa iwe siri yako? Sasa haukujua kama kitatokea kitu gani. Au umekuja kunikashfu eti?" Hapo Neema akaongeza kilio chake cha kwikwi huku moko wake wa kushoto akiutumia kujifutia machozi yaliyokuwa yakimtoka. Hakuwa na jinsi, akashuka hadi chini na kuishikiria miguu ya Musa huku yeye akiwa amepiga magoti kisha akaendelea kuomba msamaha, "Ni kweli.. Ni kweli kabisa Musa. Nilikufanyia yote hayo. Nimekusema kwa mwalimu ukaadhibiwa tena mbele ya macho yangu kwa udhalilishaji wa hali ya juu. Lakini mpaka sasa nimetambua kosa. Na sitorudia tena kufanya hivyo. Naomba unisamehe nipochini ya miguu yako." Hapo Musa alikuwa si mwenye kujali maombi ya Neema bali aliendelea kufurahia ile hali ya kunyenyekewa na msichana anaempenda. Aliendelea kufurahi moyoni huku akijiaminisha kuwa, ile dawa ya mganga ndio iliyomuita Neema. Kwakuwa lengo lake ni kukubaliwa nasio kuombwa msamaha. Hapo sasa akaanza kutumia sayansi ya ulimi ilikuvumbua upendo wake uliyojificha moyoni mwa Neema.
Alijitahidi sana kutupa maneno yenye uwezo wa kumdhoofisha Neema. Lakini Neema alionesha kupinga vikali tena kwa mifano bayana.
"Mi, siwezi kuwa na mpenzi. Bado mdogo sana. Umri wangu haujafikia kiwango chakumiliki mvulana. Halafu labda nikupe ushauri kaka yangu... Wewe bado upo mdogo. Yanini uyawahi? Mapenzi yapo tu. Subiri umri wako utafika utayapitia hadi utayachoka. Hebu tusome acha hizo tabia mbaya. Mie sipendi rafiki mwenye tabia mbaya." Hayo ni baadhi tu ya maneno yaliyomtoka Neema baada tu yakuachiwa upenyo wa kuongea. Ni kama Musa alifanya kosa kumsamehe Neema kwani hapo alikutana na ushauri hadi akaanza kuona aibu. Mwisho wa siku waliachana bila kufikia muafaka. Neema alikumbatia msimamo wake huku Musa akimuomba akajaribu kufikiria tena.
Usiku wa siku hiyo Musa alimtembelea rafiki yake macho na kumueleza mafanikio ya ile dawa waliyopewa na mganga. Macho alifurahi na kumsihi rafiki yake kuwa asikate tamaa kwani mwanzo huwa ni mgumu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Walipomaliza maongezi yao, Musa akaaga kishaakaenda kwao kula. Siku hiyo alikuwa na furaha hadi mama yake akamshangaa.
Alipomaliza kula akamuaga mama yake kishaakaenda kwa rafiki yake Side usiku huohuo.
Alimkuta side ameshaanza kuupata usingizi. Lakini hakukubali maneno yake yalale. Akamuamsha kishaakaanza kumpa stori. "Unajua Side, mi nauhakika ile dawa ya mganga niliyojifukiza ndiyo iliyosababisha yote yale. Maana huwezi amini mtoto mwenyewe akajileta. Minilidhani labda amekuja kuniharibia hadi kwa mama. Ila chakushangaza mtoto akaanza kuomba msamaha. Hadi machozi yakamtoka. Mimi nikasema Yes! Dawa inafanya kazi.. Hapo nikaanza kujishaua shaua. Mara nikatae mara nafsi ikubali. Mtoto akashndwa kuvumilia. Mwennyewe akashuka chini. Ooh, nisamehe, sijui sikutegemea kufanya hivyo. Basi mie nikamkazia utadhani nimekasirika kweli. Ila mwisho wa siku nikamsamehe kwakudhani huenda labda.. Labda mwenyewe amenikubali. Chakushangaza nilipoanza kumuingzia swaga za mapenzi. Dogo akazingua kinyama. Halafu akajifanya mama ushauri yaani.. Leo nimepewa ushauri we acha tu."
"We unauhakika gani kama huyo mganga ndio kakusaidia? Afu acha inshu zako nawewe. Mie dogo nimemuita skul nikampa mabango hadi akaona aibu. Amekuja kukuomba msamaha kisa mimi na siyo madawa ya mganga wako. Halafu huenda angekubali kuwa nawe sema ujinga wako tu. Wakutumia madawa ndio umekuharibia bwege wewe." Akasema Side na kumfanya Musa abakikwenye mshangao.
"Ku..ku..kumbe ni wewe uliyeøngea nae?" Aliuliza Musa huku akiwa amejawa na kigugumizi mdomoni kwani hakutaraji habari ile kutoka kwa Side.
.. "Kumbe ulijua ni hayo madawa ya mganga wako. Afu nilikuwa nakukaushia tu kipindi unamsifia,sifia huyo mganga wako. Lakini poa tu kwasababu we ni mkali wangu ila angekuwa mwingine tungezenguana mie inshu za kuamini waganga sifagilii. Mwanamume hatongozei wanawake kwa dawa. Bali hutumia maneno matamu yenye ladha isiyomithilika."
"Poa Side nashukuru sana kunisaidia. Lakini... Kwa jinsi ni mjuavyo Neema si mrahisi namna ile. Nadhani hata wewe nishahidi. Neema alishawahi kunipiga shiti mbele ya darasa, ila mwanangu.. Wewe ni noma. Hebu namimi nipe kanuni uliyotumia hadi kumkokotoa mtoto anaejifanya mgumu kama swali la hesabu." Aliongea Musa kisha akajiweka sawa kusikiliza. Huku kwa muda huo rafiki yake Side akitoa kicheko cha kebehi.
"Sikia mwanangu. Hawa mademu huwa hawana kanuni ila hushindwa kulingana na maneno yao.
Unajua hakuna kiumbe dhaifu kama mwanamke. Yaani ni waoga, wapole, watu wanaopenda amani siku zote. Ila hujifanya wakali, hawaogopi, eti wanashushua wanaume mbele ya watu. Kiukweli wanawake wote ni waoga. Ukiwa kama mwanamume. Unanjia nyingi za kumfanya msichana akuelewe. Labda utake tu mwenyewe." Akakohoa kidogo side kishaakaendelea, "Hakuna kanuni ya mwanamke hata ukijaribu kumtafutia kanuni utaishia kuumia. Wewe njia ya kukuokoa mbele yao ni kuutumia udhaifu wao ilikuwapata. Kwamfano, Mwanamke akiwa anajifanya anajua kuongea sana ujue huo ndio udhaifu wake. Sasa kujua hivyo tayari utamshinda kwani utakuwa umeingia vitani huku umemsoma adui wako. Pia kuna wale wanawake wenye dharau.. Yaani unaweza ukamuita akakutukana, au ukamuomba kuongea nae yeye akawa anajifanya hana muda. Sasa hao nao pia huo ndio udhaifu wao sasa nijukumu lako wewe kuutumia udhaifu wao iliuwashinde. Amini wanawake ni waoga kama unabisha hebu chukua hata kadudu halafu kaweke kwenye shati au kichwa au sehemu yeyote kwa msichana unaehisi huyo ni jasiri kisha muoneshe uone jinsi atakavyohangaika kwa uoga na makelele. Sasa ule ukelele ndio tofauti ya wewe na yeye hivyo wanawake ni waoga. Tena nikupe siri nyingine. Hujifanya hawana huruma kumbe wao ndio wenye huruma kuliko chochote dunia hii. Sasa huruma ni udhaifu, tumia huruma yao kuwateka akili na mioyo yao. Ni maneno, na vitendo pamoja na hisia pekee ndivyo vitu vitavyokufanya uweze kupata utakacho kwa Neema wala siyo Imani. Imani haina msaada kwako pindi utongozapo tena usilete maongezi ya imani maana utajiharibia kumbuka, kutongoza ni sayansi au sanaa ya ushawishi. Mshawishi yeyote hutegemea lugha ilikufanikiwa. Lugha ndio kiungo pekee kitakachokufanya ufanikiwe. Ukitumia lugha ya chooni Neema atakufananisha na choo, ukitumia lugha ya sokoni Neema atakufananisha na Soko lakini ukitumia lugha ya kiume lazma ufananishwe na mwanamume. Mimi nilitumia lugha ya kiume ndio maana Neema alinielewa na kujakukuomba msamaha." Aliongea Side maneno ambayo kwa Musa yalikuwa ni zaidi ya elimu kwani hakuwahi kuyajua hapo kabla. Musa alimshukuru sana rafiki yake na kumuahidi kuwa ataachana na masuala ya waganga. Kwakuwa usiku ulikuwa umezidi, hakuwa na laziada hapo alimuaga rafiki yake na kurudi kwao kulala.
.... ... ...
Ilikuwa ni majira ya saa saba usiku kama ilivyosoma saa iliyokuwa ukutani mwa chumba anacholala Neema. Muda huo mama Neema alikuwa akikoroma tu. Upande mwingine wakitanda huku upande aliyopo Neema akiendelea kushindana na mawazo yaliyomsumbua kichwani. Alilazimisha kulala lakini mawazo yaliendelea kumlazimisha asilale. Kila akifumba macho ilikuzalisha usingizi. Utasa wa macho yake ulijionesha na usingizi wake ni kama ulipeperuka na kwenda asipopajua. Alibaki amefumbua macho huku akilazimishwa na mawazo kumuwaza kijana aliyemfanyia matukio ya ajabu.
"Wewe Moyo wangu. Hebu usiniumbue mwenzio. Nakuomba usimuweke mtu, tafadhali nakusihi. Mama alisema mapenzi ndio muharibifu wa maisha, sasa mbona wewe Moyo unaishara za kupenda? Nakuuliza wewe.. Unajifanya hunisikii eti? Kwani sio wewe uliyeshauriana na akili huko nyuma na kuahidi kupenda masomo? Sasa mbona najihisi mapenzi,mapenzi tu. Aaah! Usijifanye huijui ilekauli ya baba. Mimi ni mwamba, popote na timba tu." Ni baadhi tu ya mashtaka aliyoyatoa Neema kuupatia Moyo wake. Alijilaumu kujikuta amependa lakini pia alifurahia jinsi mapenzi yalivyompeleka.
Kesho yake alienda shule baada ya kufanya mazoezi kwenye chumba chake cha mazoezi.
... .. ...
Siku hiyo Mama Neema aliamka vizuri na kufanya usafi kama kawaida. Alipomaliza kazi aliamua kwenda kwa rafiki yake kwa ajili ya kupiga stori maana hakuwa na kazi ya kufanya kwa muda huo. Huko kwa rafiki yake waliteta wakiwa kwenye maongezi yao mara ghafla alipita Kichaa mmoja aliyekuwa ameshikilia mfuniko wa ndoo huku mdomo wake akiutumia kama sauti ya gari. Alipiga sauti za honi kwa mdomo huku akitumia mfuniko kama usukani wa gari yake. Alifika hadi maeneo waliyokuwepo kina Mama Neema.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Wewe.. Mwehu wewe. Hebu toka hapa nyie ndio waleta nuksi." Ni sauti ya rafiki yake na Mama Neema iliyofoka.
"Jamaniii... Sio vizuri hivyo dada Suzi..." Alidakia Mama Neema baada ya kumsikia shoga yake akiendelea kumfokea yule kichaa.
"Kumbe vizuri niaje Mama Neema!.. We unadhani hiyo harufu ya jalala anayonuka nani wa kuivumilia." Alidakia shoga yake mama Neema ajulikanae kwa jina la Suzi.
"Ni kweli, ananuka.. Lakini ungemwambia tu vizuri. Nasiyo kumfokea kama hivyo."
"Ma. Neema.. Mimi siyokuwafokea tu. Hata maji ya moto huwa nawamwagia kabisa. Hawana adabu wala heshima. Hebu lione hapo nimelitukana ilabado linajichekelesha. Licheki na miudende yake inalitoka tu mdomoni hadi kinyaa." Akatema mate chini kisha akafoka, "We mwehu inamaana bado husikii eti?" Akachukua kikombe cha maji kilichokuwa karibu na mguu wa Ma'Neema. Akampondea mwehu yule.
"Jamaani... Mungu hapendi hivyo da'Suzi. Hebu jiulize hata kama ungekuwa wewe au ndugu yako anafanyiwa hivyo ungejisikiaje. Sio vi..."
"E..eee.. Ma'Neema usinichefue... Kama unatetea wehu kivyako. Mimi siwezi hurumia mwehu tena niache tusije tukakosana. Ohooo, kwanza toka.. Sitaki kukuona hata hapa kwangu." Suzi alisema maneno yale baada ya kudakia kauli ya mama Neema. Hapo akajiinua kwenye mkeka alipokuwa ameyatunza makaliyo yake. Kisha akavaa viatu na kujiingiza ndani mwake huku amefura.
Mama Neema. Alibaki pale nje akimshuhudia Mwehu yule ambae kwa muda huo alikuwa akiendesha gari lake la mfuniko wa ndoo. Alimuhurumia sana lakini asimsaidie.
Hakuwa najinsi zaidi ya kuchukuliwa na miguu yake kwa hiyari na kupelekwa moja kwa moja hadi ndani ya nyumbani kwake alipofika alijibwaga kwenye sofa huku akili yake akiirudisha kwa Suzi ambae alionekana kutokuwa na huruma hata kidogo. Kitendo kile kilimfanya akumbuke kesi ambayo ingemfanya aingize shingo yake kwenye kitanzi au ahukumiwe kifungo cha maisha. Alimkumbuka sana yule mtu aliyemsaidia kuepuka kesi ile. Mtu aliyeonekana kama kichaa. Akakumbuka ushauri wa kichaa yule kipindi anamnyanganya kile kisu alichokitumia kuuchomoa uhai wa Afande Kipara. Akakumbuka kuwa, Kichaa yule aliyemuokoa na kesi ya mauaji ndie aliyemfanya awaheshimu watu wote wanaotembea jalalani na mitaani huku miili yao wameivika madaso yaliyooza, midomo yao muda wote ikiropoka pasina kujali muktadha. Hapo tena akamfikilia huyo shoga yake suzi ambae bila haya alimtukana Mwehu kwa kosa tu lakupita pembezoni mwa mkeka waliyokuwa wamewekea makalio na miguu yao.
"Eee Mungu.. Najua yule kichaa wa watu aliejitolea kifo kwa ajili ya kunihurumia. Kwa sasa atakuwa yupo mbele ya haki. Nakuomba msamehe madhambi yake na umpatie uzima na faraja ya roho huko aliko." Alijitamkia Mama Neema huku akimkumbuka kichaa yule aliyejitambulisha kwa jina la Mavugo, huku akiamini kabisa.. Kichaa yule hatokuwa duniani kwa muda ule kwani ni miaka mingi imeshapita toka waachane siku ile ambayo mama Neema hatoisahau ingawa kwa kipindi kile hakuwa anaitwa Mama Neema bali Aisha Mapuya. Alipitiwa na usingizi palepale kwenye sofa.
.... ...
Siku hiyo Neema hakuwa na raha kabisa hasa kila alipotupa jicho upande wa nyuma kule kwenye madawati ya mwisho na kuiona sura ya upole aliyoivaa Musa. Muda wote Neema alijihisi aibu. Musa na Neema waliendelea kukatana macho kwa mavizio ya zamu. Mwalimu akigeuka kuandika Neema aligeuza shingo yake na kuyatupa macho yake usoni mwa Musa ambae kwa muda huo yeye aliyatupa chini ya dawati ilikuyasitili. Kwa upande wa Musa yeye aliyatupa Macho yake mwilini mwa neema pindi ambapo mwalimu alikuwa bize kwenye maongezi. Waliendelea na kamchezo kao kakutupiana macho na wakati mwingine walipata ajali za kugongana uso kwa uso lakini wote kwa pamoja walijishtukia na kuyainamisha chini macho yao ilimradi tu aibu aibu.
Ulipoisha muda wa vipindi, Neema alienda kwenye dawati la Musa na kuwaomba wale marafiki wa musa wa mpishe kidogo kwani alikuwa na maongezi kidogo na Musa.
Rafiki wa Musa pamoja na wanafunzi wengine walishangazwa sana na kitendo kile maana wanajua wazi kuwa Neema na Musa si marafiki kwani walitukanana na kupelekana hadi kwa walimu. Wale wanafunzi wenye midomo walianza minong'ong'ono ya chini,chini. Huku vichwa vya habari vyao vikiwa ni Neema na Musa.
"vipi Musa bado umenikasirikia?" Aliuliza Neema baada ya kujuliana hali na kupeana salamu.
"Hapana Neema. Mbona nipo fresh tu."
"Anhaa.. Poa."
"Ok. Usijali."
Ukazuka ukimya wa muda kati yao. Huku wote wawili wakipatwa nauoga uliopelekea hata sauti zao kujawa na mitetemiko ya hapa na pale.
Musa akajitutumua na kuuliza,"Vipi.. Unamishe yeyote mbona backbench?" hapo Neema akaanza kujing'atang'ata kutafuta maneno. Huku jasho likianza kumtoka kwapani.
"Nn..nili...nilii.. Hapana. Nilitaka tu kukuomba unifunze alichofundisha mwalimu maana sikumuelewa kabisa." Alijibu Neema huku akiikanyagakanyaga miguu yake.
. "Kwanini hujamuelewa mwalimu? Au haukuwa makini, e?" Alihoji Musa.
"Hapana nilikuwa makini lakini sijamuelewa. Ufundishaji wake sijui haukuwa mzuri?" Alijitetea Neema.
"Mmmh! Mbona ameeleweka tu. Ok, na mbona alipotoa ruhusa ya wanafunzi ambao hawajaelewa kunyoosha mkono. Wewe hauku nyoosha wakati haukuelewa." Musa aliendelea kutengeneza hoja mbalimbali ilikumfanya Neema azidi kujitetea zaidi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mwisho wa siku Musa aliamua kumuelekeza yale aliyofundisha mwalimu. Alimsihi kuwa awe makini sana pindi mwalimu awamo darasani na kumwambia kuwa kuna mambo ambayo huwa ni ya siri sana yamtokayo mwalimu pindi afundishapo jambo fulani hivyo nijukumu lake kuwa msikivu na mtulivu. Neema aliinua kichwa chake kuonesha amekubali yaliyosemwa na Musa.
Siku hiyo Neema alikuwa muda wote yupo na Musa kwanzia ndani na hata nje ya darasa jambo lililopelekea walimu na wanafunzi hasa wanaofahamu ugomvi wa wawili hao kupata hofu.
"Neema... Umenisindikiza hadi huku halafu ushindwe kuingia home. Kweli?"
"Usijali, acha niende nyumbani kwanza huwa sipendi kupitia kwenye nyumba yeyote kabla ya kupitia kwetu."
"Kwanini, hupendi? Au ukipita huwa unakaukiwa damu?" Alipohoji swali lile Musa ni kama alimtekenya Neema. Hapo akaanza kucheka. Kishaakasema," Yaani wewe unavituko." Akawa makini kidogo na kuendelea, "Hapana.. Hapana hayo ni maisha yangu na sheria zangu binafsi." Maneno yake yaka sababisha mshangao wa hiari kutoka kwa Musa.
"Kumbe sheria tu!! Mi nilidhani labda una sababu ile yamsingi au labda ushachanjiwa dawa kumbe sheria tu. Twende bana.. Sheria zinatenguliwaga tu. Siunajua sheria si, Msahafu eti hazitotenguliwa. Fanya hivyo." Akamaliza maneno yake na kumshika mkono Neema. Neema hakutaka kuelewa somo hata kidogo. Akaendelea kugoma mpaka Musa akaishiwa maneno ya kuongea..
"Sawa.. Umeshinda. Hebu tuachane na hayo. Vipi, ulilikiria kwa mara ya pili ombi langu?" Aliuliza huku nafsi yake ikivuka ujasiri na kuanza kuleta uoga.
"Hivi, Musa.. Ina maana tuseme wewe huwa kichwa ngumu eti! Yaani mimi niache kufanya mambo yangu nianze kukufikilia wewe sindio?" Neema alibadilika na kuongea sauti ya juu. Tena ile ya kuogofya, sauti ile ikazidisha uoga kwa Musa na kuhisi huenda akizidisha king'ang'anizi hata uo urafiki utakufa akose yote.
"Basi... Yaishe, lakini sio vizuri hivyo."
"Kumbe, vizuri niaje Musa. Acha mie niende." Akaondoka. Musa ile furaha yake ya siku nzima ikaisha ghafla. Alipofika nyumbani kwake kitandani hapo akaanza kutalii ndani ya bahari lile la mawazo. Mawazo yalimshinda na kuamua angalau amtafute rafiki yake amshauri.
.... ...
"Afya.. Eee. E.e. Afya ni kitu bora. Ya kwanza mchicha ya pili mayai. Na maharage pia.." Ni sauti ya Baba Neema. Alikuwa akiimba moja kati ya nyimbo azipendazo pindi awapo kwenye akili ya pombe.
"We.. Neema? Wewe Mwanangu." Aliita huku akigonga mlango kwa hodi. Neema aliisikia sauti ya Baba yake kipenzi na kwenda kufungua mlango.
"Karibu baba."Alimkaribisha Baada ya kumsalimu na kumjulia hali.
"Ahsante sana mwamba, popote unatimba.. Eee nakutegemea wewe. Uje urithi hadi pombe sawa mwanangu." Neema alimuitikia Baba yake kwa kila alichosema kwakuwa anamjua baba yake pindi anukiapo pombe kinywani huwaje.
Mzee alimpigisha mwanae hadithi mbili tatu kishaakakaribishwa chakula na mke wake. Alienda na kula chakula kile. Waliagana na kila mmoja akaenda kulala.
Upande wa Musa. Yeye alikuwa kwa rafiki yake akipata ushauri.
"Unajua wewe Musa. Uache ushamba wako. Elimika, oohooo. We jifanye domo zege. Labda ni kwambie kitu. Mwanamke kama nilivyokwisha kwambia, huwa anatabia ya kujifanya anamaamuzi ya mdomo. Wewe kama mwanamume unachotakiwa sio kushughulika na utatuzi wa maamuzi yake ya mdomo bali shughulika na moyo wake tu." Aliongea Side na kumfanya Musa aendelee kujenga maswali mengi kichwani.
"Sawa nimekusikia mzee wa mipango. Samahani natakaniulize ila usinicheke.. Umesema kuwa mwanamke akiongea mimi nisijali maneno ya mdomo wake bali niongee na Moyo wake." akaitikia Side kumaanisha kuwa alitamka jambo lile. Kisha Musa akaendelea, "Sasa ndugu yangu.. Hebu nielekeze jinsi ya kuongea na Moyo wa mwanamke. Maana labda hilo ndilo kosa langu kubwa." Aliomba msaada wa elimu kwa rafiki yake.
"Usijali, wewe ni rafiki yangu kwahiyo mambo kama haya ni muhimu na unapaswa kuyatambua. Unajua binadamu ni kama gari na mwili wake nio ulitumika kama mfano wa gari. Kwakuwa gari huwa na gia boksi basi binadamu huwa na ubongo kama gia boksi. Basi kwenye gari kuna kitu cha muhimu sana kinaitwa injini, nadhani unafahamu umuhimu wa injini na kazi kubwa ya injini. Nako pia kwa binadamu kuna kiungo kinaitwa Moyo. Kiungo hicho hufanya kazi za muhimu sana ndani ya mwili. Sina muda wa kukuelezea kazi zote ila natumai ukirejea kwenye kitabu cha Sayansi darasani utazipata. Huo moyo ndio umebeba kitu cha muhimu sana kiitwacho hisia na hiyo ndio siri ya moyo kuona hata kama macho yako hayana nuru, kusikia hata kama masikio yako hayaruhusu kupenya kwa sauti. Moyo unauwezo wa kufanya kazi zote za milango yafahamu pasina kuihusisha na hiyo yote inatokana na uwepo wa hisia. Unajua kuwa moyo ukichafuka na kutoa hamu ya chakula, binadamu hawezi kula hata kama ana midomo mingi? Je, unajua kuwa hisia za moyo zikikupeleka sehemu fulani lazma uende hata kama pana ogopesha na kutisha? Je, unajua kuwa hisia zina uwezo wa kuagiza chozi na kulitoa kupitia macho? Je, unajua kuwa hisia ndio huufanya mwili wa binadamu usisimke na kuhisi jambo pindi uguswapo?. Basi tangu leo elewa hisia ndio sababu ya yote. Mdomo hupenda kuongopea yaliyomo moyoni kwasababu unajua kabisa hisia ni mbaya, hata macho hupenda kuongopea yaliyomo kwenye hisia. Sasa wewe kama mtafutaji unajikuta unakatishwa tamaa kwa kusikiliza maneno ya kinywa bila kutambua maneno ya Moyo. Kuna njia ya kuteka hisia. Njia hizo ni mbili tu. Yaani njia ya Maneno na njia ya matendo. Ninaposema maneno yaani nikuyatamka yali yasemwayo na moyo wako pasina uoga au uongezaji chumvi kwani lugha ya moyo huwa tamu sana. Huleta chozi, huleta tabasamu, huleta maumivu pia.. Usije ukadanganywa na mdomo. Siku zote mdomo huwa kinyume na moyo. Pindi akutukanapo wewe usidhani Moyo ndio umetukana. Moyo huwa unaheshma tu. Unachopaswa kufanya sio kubishana na mdomo wake bali moyo wake kupitia maneno au vitendo vyako, lengo ni kuteka hisia zake tu. Mtu yeyote hata kama mfalme au rais, ukimteka hisia tu. Unauwezo wa kumfanya akafanya chochote kwa ajili yako. Mi nakusihi fanya hayo." Alimaliza kutoa elimu kisha akaruhusu swali. Hapo Musa hakuwa na swali bali kushangaa na kutoamini elimu aliyoipata.
"Labda na swali la uzushi."CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ha.ha.ha.ha. Uliza tu."
"Hivi... Yote hayo wewe uliyajulia wapi?"
"Mimi hayo yote nilijifunza kwa marehemu babu yangu. Alikuwa akinifunza mengi sana mpaka alipofariki."
"Haa! Hivi kumbe hata tuzee tunayajua mapenzi?"
"Babu alikuwa akiniambia kuwa vijana wa siku hizi hatujui mapenzi. Sasa wewe Musa.. Hebu fanya tuchonge kesho maana hapa nimechoka ile mbaya."
"poa mwana.."
Wakaagana kisha Musa akaondoka na kurudi kwao.
Upande wa Neema yeye alibaki akiulaumu mdomo wake kwa utoaji wa maneno ambayo hayapo hata Moyoni.
"Lakini.. Mimi niliongea vile sikwamba sikutaka kwenda kwa kina Musa. Bali nilikuwa nahtaji aendelee kunibembeleza kwa maneno matamu. Siwezi kukubali hata siku moja kuamrishwa na maneno yasiyo na ladha. Mie hadi nipate ladha hapo ndipo utaniona na nyanyuka na kumtumikia mtu fulani. Kwa hilo naomba Moyo unisamehe maana ni kazi yangu kuongea nikiwa kama mdomo." Hayo ni baadhi ya majibu yaliyojibiwa na mdomo wa Neema pindi alipokuwa akiulizwa na kulaumiwa na Moyo.
Ndugu msomaji, kumbe hata viungo vya mwili navyopia hukoseana, hulaumiana, na husameheana. Amini usiamini ndivyo ilivyo na ndio maana unaweza kujikuta unadhulika pasina kutarajia, kwa mfano; Mokono unaweza taka kushika moto, halafu ngozi ikakataa, au akili ikakataa kutokana na kuyajua madhara ya Moto, ila mkono ukawa mbishi na kushika Moto. Hapo madhara yanaweza kutokea na lawama zitapelekwa kwa Mkono. Kwahiyo kumbe tunapoteua viongozi wa nchi tusisahau na kuteua viongozi wa miili yetu ilikuhakikisha usalama.
Siku hiyo ilipita, siku iliyofuata ndio siku ambayo Musa alijiapisha kuwa lazma akaongee ya moyoni na siyo ya mdomoni pasina kujali mahali watakapo kuwa.
Huku Neema nae akiwaza jinsi ya kumzungusha Musa kwa maneno.
Siku hiyo Musa alichelewa shule, hivyo aliadhibiwa na walimu kisha akapewa adhabu ya kuchimba shimo dogo la kutupia taka kabla hazijachomwa.
Neema hakuwa na raha kumkosa Musa darasani, hakuwa na jinsi aliamua kutoka kinyonge na kuelekea chooni na hiyo ni baada ya kuomba ruhusa kwa mwalimu aliyekuwa akifundisha. Ukweli Neema hakuwa anaenda chooni kwa ajili ya haja. Bali kuwaza tu.
Akiwa nyuma ya madarasa na kukiendea choo. Pembezoni mwa miti mingi mingi alimuona kijana mmoja ambae kwa muda huo alikuwa amevua shati na kubakiza flana. Kijana yule alikuwa bize na uchimbaji. Neema aliumaliza muda wake kumuangalia kijana yule mpaka hapo alipogundua kuwa kijana yule amevaa sura kama ya Musa usoni mwake. Aliamua kuahirisha safari ya chooni na kuelekea maeneo aliyokuwapo kijana yule.
Endelea.... Hakuna lugha ngumu kama ile iongelewayo na macho. Macho hupata tabu sana kuuaminisha moyo kuwa, chaguo sahihi ndilo ulitazamalo. Kwa lugha ya mdomo inayotegemea sana muktadha, yenyewe huongea tu hata kama yatokayo kinywani haya husiani na yaonekanayo machoni.
Naam, alipofika akamuona Musa akiwa bize na uchimbaji wa shimo lile la taka. Hakusita kumuita, walisalimiana kwa furaha huku wote kwa pamoja wakizisahau karaha walizokuwa nazo muda mfupi.
"Masikini.. Vipi, mbona umepewa adhabu ngumu hivi?" Aliuliza Neema kwa roho ya huruma.
Musa, huku akicheka kidogo utadhani haumizwi na kazi ile., "Kawaida tu Neema. Siunajua tena masuala ya uchelewaji. We usijali au sio?"
"Lazma, nijali. Hebu tazama walivyokuchosha, jasho linakumwagika tu. Ona.. Ona.. Pote hapa umechimba wewe tu. Hapana Musa huu ni uonevu." Aliongea Neema huku akipatwa na huzuni.
"Sasa unadhani utafanyanini? Hapa shuleni mwanafunzi asiye na cheo yeye huruhusiwa kuyaonja maumivu makali, endapo tu hana chenji. Lakini yule mwenye chochote mfukoni yeye huheshimiwa na ahongapo huachishwa kazi yake na kupewa mwingine. Kwahiyo tumeshazoea we usijali." Neema aliendelea kuumia zaidi. Hapo akaomba jembe na yeye kujichanganya iliangalau atumikie adhabu ile wakiwa pamoja.
Walifanya kazi ile pasina kujali wanafunzi wenzao waliyowapita wala walimu waliowatazama na kuwahoji maswali ya hapa na pale. Hatimae majira ya saa nane, walimaliza kabisa kazi ile na kupeleka taarifa.
Wakiwa njiani wakielekea kwenye moja kati ya miti mizuri ya shuleni pale. Mara Neema akapandiliwa na jani. Kwa uoga aliruka na kumvaa Musa iliampatie msaada. Kwakuwa Musa hakuwa na taarifa ya ujio wa mwili wa Neema. Hapo akapitiwa na kuanguka chini. Kwa bahati nzuri alianguka vizuri, huku Neema akiwa juu ya kifua chake. Wote kwa pamoja hawakuamini kama kweli wapo chini tena wamelaliana. Naam, ni chuchu ambazo zilikuwa ndio kwanza zinaanza kulitafuta jua la adhuhuri. Wanaziita chuchu saa sita, ndizo zilizomchoma vilivyo Musa na kumpelekea asiikumbuke ajali waliyoipata na kuanza kuzalisha wazo jingine. Aliwaza kuwa amemuoa Neema na hapo wapo kwenye fungate ya harusi yao. Musa alikuja kukurupushwa na kibao kilichotoka mkononi mwa Neema na ndipo alipokumbuka kuwa, kumbe alikuwa ameanza kumtomasa kwenye maeneo ya faragha pasina idhini.
Naam, wanasema kibao cha mpenzi hakiumizi.. Ndivyo ilivyokuwa kwa Musa ambae aligeuza shavu jingine na kuomba azidishiwe vibao.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Samahani sana Neema kwakukushika bila ridhaa yako. Labda nakuomba usitoe hukumu yako mbele ya mwili wangu, kumbuka sikufanya hivyo kwa kupenda bali nilikuwa mawazoni. Nakuomba usinichukie tafadhali. Rudi basi." Alibaki akiongea peke yake huku Neema akikimbia na kwenda hadi maeneo ya vyoo vya kike huku akilia. Neema hakuhtaji kusikia chochote kutoka kwa Musa alichojua ni kuondoka eneo lile.
"Mimi ni mjinga sana. Hivi nilishindwa kujizuia hadi nikaanza kumshika Neema? Ona sasa, nimeshindwa kuvuta subira sasa nimevuta majanga. Sidhani kama Neema atanisamehe Side. Yaani alitoka amechukia halafu kama hajielewi hivi? Mi sikufichi hapa nimeshamkosa Neema wangu kwa ujinga." Alikuwa akijilaumu mbele ya rafiki yake Side ambae walitafutana muda wa saa tina, ule muda wa michezo. Musa hakukomea hapo... Aliendelea kujilaumu, zaidi na zaidi mbele ya rafiki yake huyo.
"Musa? Umefanya vizuri sana. Na hapo umeongea na moyo wa mtu kwa vitendo pasina wewe kujijua. Neema alikunasa kibao ilikutetea jinsi yake tu natumai ni baada ya kukumbuka maneno ya mama yake juu ya wanamume. Neema kama kweli angekuwa hakupendi, basi angekukabili palepale. Ila alionesha udhaifu wa uoga wa mapenzi tu, na jambo hilo hufanya wengi waliopenda bila kutamani kwa mara ya kwanza. Hawezi kukufikiria uwapo mbele yake na ndio maana akakuondokea iliakakufikirie zaidi. Hakuna mtu anaechukia kukumbatiwa, wala hakuna anaechukiwa kuambiwa anapendwa. Nina uhakika asilimia zote Neema ameangukia kwenye mapenzi. Na aliyemuangukia ni wewe tu." kupitia maneno yenye ukweli wa utatuzi kutoka kwa Side, yaliweza kumfumbua Musa na kuirejesha theluthi ya furaha yake ambayo ilikuwa imepotea. Hapo Musa akakili wazi kuwa anajivunia kupata rafiki kama Side.
... ....
"Unajua huyu kichaa Mavugo. Yupo tofauti sana na wenzake. Sawa yeye hajielewi lakini hufikia muda akili zake hurudi kwa dakika kadhaa tena hutoweka, tumejaribu kila njia ya kurejesha kumbukumbu. Kwani tatizolimsumbualo ni kutojielewa. Lakini tumeishia kufeli tu. Kama shoti tumeshampiga sana ila nikama tunamuumiza tu na hakuna kumbukumbu yoyote inayomrejea. Ila ni kichaa mzuri, anatambua hatari na kuzikwepa, hapa labda tufanye uchunguzi zaidi juu yake."
"Ni kweli kabisa dokta Endrew.. Lakini pia Mavugo anaonekana kuwa na mengi sana kichwani mwake. Ukichaa wake si..wa bure. Nahisi ni msomi. Ngoja tufanye uchunguzi kwanza. Enhee, hivi unamuonaje huyu mgonjwa aliyeletwa leo. Anavituko sana."
"Ha.ha.ha. Kumbe huyo anaelilia kunyonya?"
"hapana si,huyo."
. "Kama si, huyo. Kumbe ni yupi docta izack." Alihoji docta Endrew huku akichezea kalamu yake kwenye meza.
"Ni yule aliyekuwa analilia apelekwe studio akatoe albamu." Aliongea dokta Izak huku akijibadili mkao wake kwenye kiti.
Docta Endrew alikumbuka kishaakajikuta akicheka kila alipokumbuka vituko vya kichaa yule mpya. "Sasa... Docta, achamie nikuache kidogo. Weendelea na kazi." Aliongea docta Endrew kisha akajitoa kitini.
"wapi sasa?" Aliuliza docta Izack huku akipekuapekua makaratasi kadhaa mezani pale.
"Naenda kumchoma sindano ya usingizi yule kichaa anaekula nyama yake mwenyewe. Nahisi atakuwa ameshaamka, ngoja nimuwahi asije kujibebena mwili mzima."
"anhaa.. Upo sahihi. Wewe nenda kamshughulikie." Akatoka docta Endrew kishaakaelekea kwenye chumba ambacho wamemuhifadhi kichaa yule ambae yeye maisha yake kila leo hujiadhibu tu. Alipofika alimkuta bado amelala akamkadiria muda kishaakatoka. Docta Endrew aliona bora ajipitishe angalau kwenye uwanja waliyopo vichaa.
Kuna kichaa mmoja yeye ni wamakamu lakini muda wote amuonapo mtu hupenda kupiga goti na kusalimia. Kichaa huyo ni msumbufu lakini si mkorofi. Kwakuwa docta endrew anawafahamu vichaa wale jambo hilo halikuwa tabu alimuitikia na kuendelea na safari yake.
Kufika sehemu akakuta vichaa kadhaa wamesimama na kutulia kimya. Huku mmoja wao akiwa mbele na vile vitabu vya watoto ambavyo huchorwa midoli, "Hili andiko linasema, mama mwenye nyumba hulipwa deni lake kila adaipo. Vilevile tukifungua hukumu za kisasa aya ya kwanza msitari wa pili hadi watatu unasema; Tuwaheshimu wazee wetu kwa kuwa shika videvu vyao na tuwatii kwakusikiliza hadithi zao japo ni zauongo." Ni kichaa mmoja aliyekuwa bize huku akiwahubiria wenzake mambo ambayo ni kama waliyaelewa wenyewe tu. Hapo docta Endrew akacheka sana baada ya kutazama umakini wa vichaa wale wengine waliyo kaa kama wasikilizaji, akawakejeli kimoyomoyo huku akisogea mahali walipo.
"Mwalimu... Umesema kuwa, wototo wadogo wanapaswa wapelekwe shule wakiwa migongoni mwa mama zao. Je, watu wazima wapelekwe shule wakiwa wapi?" Ni swali kutoka kwa mmoja kati ya vichaa wasikilizaji. Kichaa yule aliyeongoza mahubiri akanuna kidogo kishaakafungua kitabu chake na kutoa majibu. Docta Endrew aliona kuendlea kukaa pale ni kama kupoteza muda, akajivuta na kuondoka taratibu. Akiwa njiani alifanikiwa kumtazama kichaa mmoja aliyekuwa bize kuandikaandika chini. Aliamua kumsogelea na hapo ndipo alipomkuta kichaa ambae kwake anamthamini na kumtofautisha na vichaa wengine. Kichaa huyo ana umri kati ya miaka arobaini na moja hadi arobaini na nne. Aliletwa hospitali hapo miaka kumi na tano iliyopita baada ya kubainika kuwa anaugonjwa wa akili hivyo gereza si haki yake. Naam, ndio yuleyule aliyefungwa kwa kesi ya mauaji ya watu watatu kwenye mazingira tofauti anaitwa, Mavugo. Docta alimsogelea na kwenda kukaa nae kwani anampenda sana.
.... ... ...
Neema alitumia muda wake mwingi kumuwazia Musa. Zaidi alikuwa akijipa picha ya kumbukumbu jinsi yeye na Musa walivyoanguka kwa pamoja. Alitamani angalau wangechukuliwa hadi picha iliawe analitazama pozi tamu alilokuwa ameliweka mwilini mwa Musa. Kila akikumbuka jinsi Musa alivyomkosea adabu anacheka kimoyomoyo baada ya kubaini kuwa alimuadhibu kwa kofi. Hisia za utamu zilimjaa na kumpatia raha muda wote. Alijicheka na kujinunisha muda huohuo huku akizikebehi zile hasira zake za kinafki.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Side na rafiki yake Musa, wao walikuwa wameshakwenda kucheza mpira maana walikuwa wanamechi za mikondo.
Timu ya Musa ilikuwa ni tofauti na ile ya Side kwakuwa mikondo yao haikuwa sawa. Musa hucheza kama kiungo mchezeshaji ndani ya timu yake ya mkondo huku kwenye timu ya shule akiwa kama kiraka. Yaani yeye niwakupachika namba yeyote ile anacheza. Upande wa Side yeye ni namba tisa mzuri tu. Mechi hiyoilikuwa tamu sana si tu kwa waliyobahatika kuitazama bali hadi kwa wachezaji wenyewe. Hawa kucheza kwa kuzimiliki dakika tisini bali waliishia robo yake kutokana na kulia kwa kengele ya kutawanywa.
Wanafunzi wote waliposikia kengele hiyo ya kutawanywa waliichukuwa miguu yao huku wakiwa wamevuta vyema pumzi zao na kukimbia vilivyo hadi paredi kwa ajili ya kusikiliza matangazo.
Walipomaliza kutangaziwa, walitawanyishwa na kila mmoja kwenda kwao.
"Musa..! Musa..!" Ni sauti ya Neema aliyoita jina hilo huku mwenye jina akiambiwa na ubongo wake uliopata taarifa kutoka kwenye sikio kuwa ageuke. Akageuka kuja kuhamaki. Uso kwa uso na Neema. Hakuyaamini macho yake akayafumba na kuyafumbua lakini aliendlea kumuona Neema. Hapo akaanza kuvuta picha jinsi walivyozinguana muda mchache uliyopita, akaendelea kutokujiamini. Akahisi macho yana muongopea. Akaamua kutumia sauti yake kumuita huyo Neema iliaamini kupitia masikio.
"Neema.. Kumbe niwewe?" Aliita Musa na hapo ndipo alipoamini kwamba kumbe aliyemuwazia ndie. Alimfuata kwa kasi, akamshika mkono na kumtoa kwenye msongamano ule wa wanafunzi wenzao. Kisha wakajibakiza nyuma na kuanza kuongea. Neema aliomba msamaha kwa kosa la kumuadhibu Musa kwa kibao, kwakuwa Musa alitambua wazi kuwa ile ilikuwa ni haki ya Neema kufanya vile. Akajifanya kumsamehe wakati hata moyoni mwake hakuwa amekosewa. Hatimai hayo yakaisha wakaendelea kupiga soga za hapa na pale. Neema alipoishiwa maneno alileta umbea na kwapamoja wakashirikiana kuteta.
"Neema. Hebu tuachane na hayo. Hayatuhusu, siunajua tena." Aliongea Musa huku akimpiga Neema ngumi isiyoumiza begani.
"kumbe tupige stori zipi?" alihoji.
"Zozote," Alijibu, alipomuona Neema yupo kimya. Alijua huenda hajaridhika na jibu lake ikabidi aseme tena, "Hata za movie, au za nyumbani, za maisha, hata za mapenzi kama zipo." Neema alipopangiwa listi hiyo akajichekelesha kidogo. Hakukurupuka kwenye uteuzi japo alikuwa na moja ambayo alishaiteua.
"ok, minimeonelea tupige stori za nyumbani." Ni kinyume na matarajio ya Musa kwani yeye aliiweka mada ile kwenye listi kwa kudhani huenda haitotajwa.
Neema akaanza kumsimulia Musa vituko vya baba yake. Kiukweli vilikuwa vinafurahisha lakini Musa hakutoa walau tabasamu hata moja. Muda wote alijawa na hasira alikuwa amebadilika sura na kutengeneza uso wake wa kukasirikia lakini alijitahidi sana kuung'ang'aniza uwe na furaha ya lazma.
"Oy, Neema eee. Nimechoka na maneno maneno yako ambayo hayana kichwa wala miguu. Mimi nakupenda na wewe hilo unalijua, sasa swala lililopo ni wewe kuniambia jibu ulilofikiria na sio kuchengesha mada hapa." Ni matokeo ya Musa kushindwa uvumilivu ndipo alipojikuta akiropoka maneno yale ya hasira pasina kuyazuia. Palepale Neema nae akajikasirisha na hasira zisije, akauchukua mkono wake na kuingiza ndani ya begi lake la shule, alipoutoa ukatoka na kikaratasi kidogo alichokifunga na kamba.
"Shika.." Alisema huku akimpatia kikaratasi kile. Alipochukua, Neema akaongeza, "Nakuomba usifungue hadi mimi nitokomee" Musa akakubali japokuwa alikuwa na maswali mengi ambayo alijua majibu yake yatakuja muda mfupi.
Neema alitokomea na kumuacha Musa aliyekuwa akingoja kusoma kikaratasi kile. Alipoona Neema ametokomea, akaanza kufungua kamba ile kwa ajili ya kutazama kilichomo ndani. Alikuta kikaratasi kingine kidogo zaidi ya kile chajuu. Kikaratasi kile kilikuwa na neno moja tu. Musa alidhani huenda maneno yangekuwa mengi lakini alipoishika karatasi ilionesha neno moja. Akalisoma, kwanza hakuamini, ikabidi amshirikishe mtu mmoja aliyepita maeneo yale kwa uhakika zaidi kwani alidhani huenda kisomo chake kimemdanganya.
"Imeandikwa 'NAKUPENDA'" alisoma mtu yule.
Furaha isiyokifani ilimpata Musa aliamua akimbie hadi kwao iliakaipatie haki furaha yake.
.... ... ....
"Bwana Mavugo.. Shikamoo...." Alisalimu Docta Endrew baada ya kumfikia kichaa yule aliyekuwa bize na kuandika andika.
"Hivi, wewe Endrew? Nani kakwambia anashida na kunyenyekewa. Hebu nitolee salamu za dhalimu mkubwa mbele ya masikio yangu." Hapo Endrew akatabasamu kiaina kwa kujua lazma ajifunze kitu kupitia kwa kichaa yule aliyejawa na mengi. Akajiulizisha iliapate kujua jambo.
"Waliotutawala pasina ridhaa yetu karne kadhaa zilizopita. Ndio waliyoleta salamu hii ya utumwa. Walifanya hivyo nia na madhumuni ni kutufanya tuwanyenyekee wao utadhani ndio waliyoiumba dunia. Salamu hiyo haikutolewa kama udhaniavyo wewe bali wenzetu walipga magoti na kunyenyekea kisha wakaitoa." Endrew akabisha kishaakasema. "Kama ni kweli, hebu niambie salamu sahihi ni ipi?"
"Safi sana Endrew.. Najua umetumia miaka yako mingi masomoni iliangalau uweze kupunguza ujinga. Lakini nasikitika umeambulia kuishi na vichaa tu. Labda nikuulize jambo. Hivi.. Unaweza kuniambia neno, Shikamoo linatafsiriwa vipi katika lugha yeyote ile ya kigeni au hata ya kibantu," docta Endrew akaishia kukuna kichwa lakini asipate maana. "Sio unakunakuna kichwa tu. Sema usaidiwe." alisema Kichaa Mavugo. Kwa aibu docta endrew akakubali kuomba msaada kwa kichaa. Hapo Mavugo akajikuna kidogo kidevuni kwa mbwembwe kisha akasema..
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Unajua sisi binadamu matendo yetu yanategemea majira, hivyo hata salamu zetu hutoka kwa kufuata mfumo huo wa muda. Hebu funguka kifikra wewe, waingereza husalimiana kwa majira, waarabu, hata wa bantu, si hivyo tu, dunia nzima inategemea majira. Lengo la salamu ni kutakiana amani baada ya kujuliana hali nasi kunyenyekeana kana kwamba kuna muumba kati yetu. Mimi kwakuwa nafuata majira, asubuhi nitakujulia hali, mchana na hata usiku. Rudi shule Endrew, ukajifunze salamu na sio kukurupuka tu."
Endrew huku akicheka akasema "Unajua Mavugo wewe huwa nakushangaa sana. Sijui mwenzangu unayatolea wapi yote haya. Hapo kidogo umeniacha, naomba kuuliza. Hivi hili neno salamu kwanza linamaana gani? Manake mie sijui, huwa nawambia tu watoto wanisalimie tu lakini kiukweli wakinihoji maana yake sijui. Nisaidie bwana Mavugo." Alitega sikio tena ilikusikiliza majibu kutoka kwa Mavugo.
"Sikia docta Endrew, wajinga huachwa na ujinga wao. Ingetosha nikakuacha lakini kwakuwa wewe ni rafiki yangu, hebu achanikuambie jambo. Penda kuishi kwa kujifunza iliuwe mwanafunzi bora.
Ok, neno 'Salamu' chimbuko lake sio kiswahili bali nineno la kiarabu. Neno hili linatumiwa tu kwakiswahili kwasababu lilitoholewa kutoka lugha ya kiarabu hadi kiswahili. Lakini sikwamba walilitohowa neno hilo kwakukosa msamiati wake la, hasha! Msamiati wake upo. Nao ni 'Amani' hivyo Salamu kwa kiswahili ni Amani. Kumbe sasa huwa tunasalimiana kwalengo lakutakiana Amani na sio kunyenyekeana. Nadhani umenipata." Mavugo akaendelea kuandika.
"Mmmh! Hapo nimekupata. Wala sina swali. Labda tu nikuulize, hivi unaweza niambia labda kabla hujapatwa na hali hii ya ukichaa ulikuwa na kazi gani?"
"Mbona Endrew huwa hunielewi? Mimi sio kichaa. Ebo! Vichaa ni wale kule wanachezacheza kichizi. Tena usitake kunikera hapa."
"Sawa bwana Mavugo. Samahani sana, labda nimekosea kukuuliza tu. Lakini lengo langu halikuwa baya. Nauliza tu zamani ulikuwa na kazi gani?"
"Swala la kazi mie sijui hata kidogo. Kwanza hata mie mwenyewe sijielewi mbona nyie madocta wasumbufu ah! Kwanza naomba unipishe niladhani umeanza kupata akili kumbe bado hazimo."
Docta Endrew alipofukuzwa na Mavugo ndipo alipokumbuka ile kazi yake ya kwenda kumchoma sindano ya usingizi yule kichaa aliyekuwa akifanyakazi yakujitafuna mwenyewe. Akatoka kishaakaenda kumchoma baada ya kumkuta macho, alipomaliza akarudi kwa docta mwenzie kishaakamuhadithia yote kwa pamoja wakacheka, huku Mavugo yeye akiendelea kuandika mambo yasiyofahamika.
"Unajua nimejaribu kupitiapitia hapa habari za Mavugo inaonesha aliletwa hapa miaka kumi na tano iliyopita na..."
"Kumbe ni wakitambo humu!!" Alidakia docta Endrew hata kabla mwenzie hajamaliza.
"Lakini pia nimegundua, kumbe huyu Mavugo hata kama tukisema tumpige shoti vipi haitosaidia. Kumbe anatatizo kubwa sana, na hakuna njia yeyote ile ya kumrejesha kwenye hali yake ya kawaida ila atarejea endapo atamuona mtu aliyewahi kuishinae au kuwa rafiki yake kabla ya hayo matatizo hapo ndipo kumbukumbu zitamkaa sawa na akili yake itatulia. Si unajua huwa anauwezo wa kukumbuka kidogo na hata anapokumbuka anapata kazi sana kwani huumia kichwa tu wala asielewe kama akikumbukacho ndicho." docta Endrew huruma ikazidi kumjaa baada yakung'amua jambo juu ya hali ya Mavugo.
Atapona vipi na kurudi timamu wakati yupo hospitali? Atawaona vipi hao wataomkumbusha? Au nd'o ataishi hivyohivyo milele?. Hayo ni baadhi kati ya maswali aliyoendlea kujiuliza docta yule ambae ingawa anamiezi miwili na robo toka ahamishiwe Bugando hosipatal. Lakini alikuwa ametengeneza urafiki na kuvutiwa sana na mambo ya Kichaa Mavugo, zaidi aliamini kuwa huenda Mavugo aliwahi kuwa na cheo fulani katika nchi hii lakini alikuwa akilikebehi wazo lake baada ya kugundua kuwa mtu yeyote mwenye cheo asingeachanizwa namna ile.
Lazma nijue nini hatma ya Mavugo. Alijisemea huku akizungushwa na kiti cha ofisini mwake.
..... .... .....
"Utaniumiza mwanangu... Mama yako nimeshajiishia hapa." Aliongea Mama Musa baada ya Musa kumkwapua na kumbeba juujuu kwa furaha.
"Mama leo nina furaha sana?" Aliongea Musa huku akimtua Mama yake ambae sasa alianza kulalamika kwa kubebwa juujuu.
"Furaha gani tena Mwanangu? Halafu mbona michirizi ya jasho na nguo inauchafu wa udongo. Umepigana?"
"Hapana mama.. Sema leo tulikuwa na kijikazi shuleni ndio maana unaona hivi"
"sawa, nambie namimi nijue unachofurahia mwanangu manake leo upo tofauti sana."
Musa akaona aibu,
"Hapana mama.. Nafurahia tu kumuelewa mwalimu."
"haa! Hicho ndicho kimekufanya uje kunisumbua hivyo. Mmmh! Haya bhana, jitahidi mwanangu siunajua mimi nakutegemea wewe."
"Natambua hilo mama."
Musa akatoka kishaakakimbilia chumbani mwake, alipofika akajitupia kitandani hivyohivyo na nguo zake za shule. Akakitoa kile kikaratasi na taratibu akaanza kukipitia utadhani anajisomea.
Musa akiwa kitandani pale huku akiendelea kutabasamu, mawazo yalimvaa na kumrudisha nyuma akaanza kukumbuka kipindi anamuhangaikia Neema, mpaka anafikia hadi kuadhibiwa kisa yeye, baada ya kumbukumbu hiyo iliyoambatana na machozi ya furaha. Alibadili nguo na palepale alijiinua moja kwa moja hadi kwa rafiki yake Side.
"Aiseeee!! Side umenisaidia sana." Aliongea kabla hata ya salamu. Kwa muda huo rafiki yake alikuwa bize na kuchota maji. Lakini alipomuona Side, akaamua kuahirisha kazi yake nakusikiliza ujio wa rafiki yake.
"Unamaanisha nini kusema hivyo. Halafu kwanza tuheshimiane sawa?" Aliongea Side huku akisontesha kidole chake kwenye paji la uso wa Musa.
"Kwani hatuheshmiani? Au umeanza talalila zako hapa." Alijibu Musa huku uso wake ukionesha furaha na kuendelea tanguliza utani mbele.
"Mi najua kuwa sina hadhi ya mbwa. Mbona unakuja na kufurahi bila salamu. Hivi unajua umuhimu wa salamu wewe? Huijui hali yangu? Unakuja tu namifuraha yako hapa hujui tupoje. Pengine labda tupo kwenye huzuni. Sasa we unadhani utajuaje. Waafrika tumefunzwa kutoa salamu. Allaaaa! Sio kufika nakuelezeana tu raha wala karaha zetu. Kwani utajua vipi kama mie sinafuraha bila kunijulia hali. Acha pigo zako kijana." Alilalamika Side huku akikemea vilivyo tabia ya rafiki yake.
"Ok, ni kweli... Nisamehe mkali, vipi, mambo yanasemaje?"
"dah! Mdogomdogo tu. Sijui huko kwenu."
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Huku sisi tunamshukuru Mungu tu."
"ndio, hicho ndicho chamsingi. Siunajua hata hapa akapenda anazichukua pumzi zake alizotuazima. Lakini ameziacha tu. Hivyo, hatuna budi kumshukuru. Yeye ndie kila kitu. Enhee! Leta stori"
"Mwana... Basi si tumetawanishwa skuli. Nikiwa naenda hom, mara nikasikia naitwa. Nikajiuliza, nani tena anaeniita. Kugeuka nikakutana na malaika..." Hapo Side akashangaa kidogo kusikia neno malaika.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment