Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

SITAKI TENA - 4

 







    Simulizi : Sitaki Tena

    Sehemu Ya Nne (4)





    Ilipoishia jana usiku..



    Akachomoa kitambulisho chake cha kazi na kunioneshea. Maskini kumbe alikuwa haitwi Mage, jina lake ni Gracia.

    ‘’Ooooh! My God! Nimekwisha Levina mimi nateketea sasa,

    alichukuwa pingu zake na kunifunga?

    “Twende Polisi mbwa wee. Damu nzito kuliko Maji na leo ndio utaeleza Mauaji yako ulioyafanya?’’

    Maskini kumbe alikuwa haitwi Mage,jina lake ni Gracia.



    Songa nayo sasa…



    ‘’Ooooh! My God! Nimekwisha Levina mimi nateketea sasa,

    alichukuwa pingu zake na kunifunga?

    Nilijihisi mimba inataka kunitoka kwani tayari nilikuwa nimefungwa pingu mikononi mwangu huku tunatoka nje.

    ‘’Dada Mage niachie nakuomba sana Dada?’’

    ‘’Nimeshakwambia siitwi 'Mage' na Mie siyo Dada yako mpumbavu nini, uunaakili kweli wewe?’’

    Nilijikuta naishiwa nguvu huku nikipata uchungu ghafla wa hii mimba yangu.

    ‘’Nakuomba unionee huruma jamani Afande!’’

    ‘’Ulivyoua hukuona huruma? Then unataka leo mimi ndio nikuonee huruma wewe Mpumbavu sana tena sana we Levina....!’’

    Yale maneno yaliingia moja kwa moja kichwani mpaka nikajihisi kizungu zungu huku nikimtolea macho,

    Akiwa anahangaika kufungua mlango ule wa kutokea. Nilifura kwa hasira nikajikuta naivaa ile sura yangu ya kikatili pale pale na kuachana na ulokole kwa muda, Nilimvizia afungue tu ule mlango, Mungu si Athuman punde alishikilia kitasa ili afungue mlango ile tunataka tu kutoka papo hapo nikajiangusha chini huku nikiacha wazi eneo langu lote la kuanzia mapajani, kiufupi lile gauni langu lilinifunika kiasi kwamba tumbo langu lote likawa wazi hivyo dhahiri kama mwanamke kweli atanionea huruma na ile mimba niliyokuwa nayo.

    ‘’Mamaa yangu tumboo! Tumboo langu afande!’’

    ‘’Tuuuumbo? Embu twende huko na utakoma huko nitahakikisha unajifungulia gerezani! Au unataka nikutoe hiyo mimba eeennhh?’’

    ‘’Hapana Afande fungua tu huo mlango unipeleke unapotaka.’’

    Aliongea kwa hasira lakini hazikunitisha, nikajifanya mjinga ili nimpime nijue atanipeleka kweli au la.! kitendo cha kuinama na kunivuta nisimame juu huku nikiwa na pingu hapo hapo nilimvaa na zile pingu shingoni mwake nikamkaba nazo mithili ya yule mwanamieleka 'undertaker' akizidisha nguvu zake lakini mimi sikujali kwani niliamini kichwani mwake ni lazima atakuwa anajua kweli tumbo lilikuwa likiniuma, kumbe kwangu mie ilikuwa ni mbinu tu!

    ‘’....una...a...ta...k...a…… ku....nifanya ni....ni...?’’

    Aliongea kwa sauti ya kujiuma uma kwani tayari nilikuwa nimemthibiti vilivyo, kitendo cha yeye kuachia mikono na kutafuta bastola yake pembeni ya suruali ilikuwa kosa kwani pale pale zile pingu zikawa tayari zinamalizia kazi yake maana zilikuwa zimeumana na koo lake na kung'ang'ania kwa nguvu zote.

    ‘’...Un...aaa...n..iu..aaaa ……Leeee...vinaaaaa...!’’

    ‘’Kufa tu wewe si umesema sio Dada yangu..? kwanini unataka kunikatishia ndoto zangu..? shwaiin mkubwa we....!’’

    Niliongea kwa sauti ya kikatili na ubabe huku yule afande akitapatapa mbele ya macho yangu huku na kule kuonesha kwamba anakata roho. Alifurukuta kwa nguvu halafu akaanza kulegea huku macho yake yakibadilika rangi na kuwa mekundu na mishipa ikimtoka eneo la shingo yake hakika sikuogopa kwani nilishazoea kuua. Pale pale nikachukua ile bastola pembeni ya mfuko wa suruali yake, nikaichomoa na kuikoki kisha nikamuingizia mdomoni mwake na kuifyatua. Nilijitenga mbali sana na damu kwani ingekuwa rahisi kushikwa endapo ningekutwa na damu kwenye nguo. Nikahakikisha amekufa kabisa, haraka haraka nikamsachi mifukoni mwake na kuupata ufunguo, nikauchukua na kujifungua pingu kisha nikachukuwa tiketi yangu na pasipoti ambavyo tayari alikuwa ameshanipora.

    Niliuchukuwa ule mwili wake na kuuweka chini ya kameza mule mule ndani kisha nikaufunikia na maboksi, nilipomaliza nikatoka nje na kufunga ule mlango kwa ufunguo kisha nikauweka mfukoni na kuondoka.







    * * * * *





    ‘’Najua sijachelewa sana lakini mie nilishakuwa mtoto wa mjini hivyo njia zote nazijua!’’

    Nilitoka kwa majigambo huku nikijiamini safari yangu bado ipo. Nilipokaribia lile eneo la kuchekiwa pasipoti mara nikamwona askari mwingine ndio alikuwa anamalizia kufunga mlango kuonesha kuwa watu wamekwisha na muda wowote ndege inaondoka, pale pale nikabadilisha mwendo na kutembea mwendo kama kumsindikiza bi harusi akiwa kanisani au akiingia ukumbini huku nimeshikilia tumbo langu taaaaratibu.

    ‘’askariii! Askariiii! mnaniacha jamani!’’

    ‘’Ulikuwa wapi muda wote we binti?’’

    Tumbooo...! Tumbo! linanisumbua na hii mimba ndio kabisaaa..?

    ‘’Haya embu fanya fanya haraka, pasipoti yako imeshachekiwa pale?’’

    ‘’Ndio afande’’

    ‘’Na tiketi?’’

    ‘’Nayo pia vyote hivi hapa na mizigo yangu tayari wameshapakia’’

    Niliongea kwa kujiamini huku nikiamini asilimia mia yule askari hafahamu lolote pia mda ule tulioondoka na yule askari yeye hakuwepo,

    ‘’'Host'! bado usifunge huo mlango wa ndege kuna binti anamimba huyu hapa amechelewa kidogo!’’

    Yule askari akawa anamwambia mhudumu wa ndege anisubirie.

    Mpaka napanda ngazi kwenye ndege bado nikawa sijiamini amini haswa kwa kitendo cha kumuua yule askari pale pale uwanja wa ndege.

    "Mpumbavu sana wewe na bora tungekuacha tu!"

    Ilisikika sauti pembeni yangu nilipoingia tu ndani ya ndege huku nikiwa nimemkabidhi tiketi ya ndege yule mhudumu wa ndege,

    ‘’Utakaa hapa!’’

    ‘’Ahsante sana’’

    Nilijikuta peke yangu kwenye ile siti, sikutaka kuuliza chochote zaidi ya kukaa kimya peke yangu nikishusha pumzi.

    ‘’Ulikuwa wapi we mshenzi enh!’’

    "nilikuwa ch…’’

    ‘’Sasa kama hapa tu unaonesha uvivu wako je ukifika huko? Mwanangu Gervas si atakuwa analala na njaa?’’

    Alikuwa ni Mama Gervas akitokea lango la chooni akiwa amefura kwa hasira huku abiria wote wakimshangaa kwa maneno anayotoa. Sikumjibisha hata neno nikakaa kimya, safari ikaanza ya kuondoka katika ardhi ya Tanzania na kuelekea Marekani.





    * * * *





    Mpaka tunaingia Dubai bado nilikuwa sijiamini amini kama kweli ndio naelekea kwa Gervas au la! Mawazo mengi yalinitawala nilijisalia kimyakimya ndani ya ndege huku nikitubu makosa niliotenda,

    "Hakika kwa Mungu kuna utukufu! Eeeh Mungu wangu weza kunifungulia njia zote! Baba weza kuniondolea mikosi yote inayonikumba. Kwa jina lako nasema. Amen!’’

    Ni kati ya sala nilizokuwa nikisali kimyakimya bila hata ya Mama Gervas kujua chochote. Mara kitu kikadondoka eneo la chini yangu kikitokea kwenye gauni niliokuwa nimevaa, haraka haraka nikaangalia kwanza pembeni yangu na kumuona Mama Gervas akiwa kajifunika kitambaa kwenye paji la uso akionesha kupitiwa na usingizi,

    Nikalipenyeza jicho langu fasta eneo la chini kuangalia.

    ‘’Mungu wangu si ule ufunguo wa kulee uwanja wa ndege huu?’’

    Hofu ikaanza kunitanda kwani ni kweli nilipomuua yule askari pale uwanja wa ndege nilimfungia na ufunguo nikauweka mfukoni.

    ‘’ayaiya...! iyaaa...! iyaaaa...! iyaaaaa!’’

    Nikauvuta na kuuchukuwa kisha nikaukagua vizuri, ulikuwa si kama funguo za kawaida bali ulikuwa tofauti kwani hata maandishi yake yalikuwa yameandikwa 'TZ ARPT 06' kila nikiyasoma yale maandishi nazidi kuchanganyikiwa lakini halmashauri yangu ya kichwa ikafanya kazi fasta kuwa niende chooni nikaitupe sikuchelewesha muda.

    ‘’where is toilet?’’

    Sikutaka kuonekana wakuja hata, palepale mhudumu akanielekeza na kuingia huku nikimwacha Mama Gervas akiwa kapitiwa na usingizi, nilipofika tu chooni kabla sijautupa ule ufunguo nikawa natetemeka huku namuomba Mungu atende miujiza usije onekana tena,

    Kwa haraka niliyoingia nayo mule chooni nilijikuta najisahau hata kufunga mlango hivyo nikaufunga ile naumalizia kuufunga nasikia kama kuna mtu ananiita.

    "Levinaaa! Levinaaaa"

    ‘’abee Mama!’’

    Sauti ya Mama Gervas ilikuwa ikiniita kwani hakuna abiria yeyote aliyekuwa analijua jina langu zaidi ya Mama Gervas mule ndani ya ndege.

    ‘’Hiiivi we mtoto? Kwanini unaniaibisha kiasi hiki? Hiyo mimba yako ndo inakufanya hivyo?"

    ‘’Kwani nini tena Mama?’’

    ‘’Unadhani hii ndege ya marehemu Baba yako? Eeenh....! Twende ukaone upuuzi ulioufanya?’’

    Sikudhania kama Mama Gervas anaweza kuja chooni na kunitoa tena akiwa ananivuta nywele zangu mputa mputa ndani ya ndege mpaka abiria wote wakawa wananishangaa mimi na Mama Gervas,

    ‘’Hapana...! Hapana....! Hapana...! Hapana wala siyo mimi...!’’

    Maskini ni ile siti niliokuwa nimekalia ilikuwa imetapakaa damu nilivyokuwa nimeegemea, kwa mshangao niliokuwa nao nilijikuta ule ufunguo unadondoka pale pale kisha kwa haraka Mama Gervas akauwahi kuuokota.

    ‘’Na huu funguo wa nani’’

    ‘’Wakwangu Mama!’’

    Akauchukuwa nakuanza kuukagua kagua, kisha nikamwona kama ameshtuka ghafla.

    "Umesema funguo ya nani?’’

    ‘’Ya kwangu Mama?’’

    ‘’Mbona imeandikwa 'TZ ARPT 06'?’’

    Aliposema hilo neno tu haraka haraka yule mhudumu wa ndege nikahisi kama ameshajua kila kitu kwani aliposikia tu Mama Gervas akitamka namba za ile funguo akatoka kasi na kuelekea kwa marubani sikumwelewa ameenda kufanyaje.

    ‘’We mtoto utakuwa jambazi wewe..! Hiivi kale kanyumba kenu ndo muwe na funguo kama huu uliotengenezea 'material' adimu hivi?’’

    Nikamyamazia aongee mpaka basi huku akili yangu yote nikiielekezea kwa yule mhudumu.





    * * * *





    Ilituchukuwa kama Masaa saba kutokea Dubai mpaka uwanja mkubwa wa kubadilishia ndege pale ‘Amsterdam’ Uholanzi, Ule ufunguo tayari ulikuwa mikononi mwa Mama Gervas, tulishuka salama bila hata kuulizwa kitu chochote kutoka kwa yule mhudumu wa ndege, na sasa tulihitajika kupumzika kwa siku moja hotelini kisha kesho yake tutapanda ndege nyingine lakini ya shirika hili hili la 'Emirates'.

    Tukiwa lango la kutokea huku kila mmoja wetu akisubiria mizigo nilishangaa mizigo yetu ya mimi na Mama Gervas kuzuiliwa na Askari wa usalama kama watatu huku wakiwa na bunduki zao pembeni,

    hofu ikanijaa tena Moyoni, walionesha kama sura za kukasirishwa na kitu, wakanifanya nikose Amani na kuanza kusingizia tumbo linaniuma.

    ‘’Oooh Jesus! My stomach uuuh! Uuuh! Mummy pliz help me!’’

    ‘’shut up! Tena ukome kunililia hapa who is your mother?’’

    Tayari Mama Gervas akawa amenigeuka pale pale kisha nikamshuhudia akitoa ufunguo na kuwakabidhi wale askari, wakauangalia mara mbili mbili kisha wakamruhusu Mama Gervas aende ila mimi nibaki,

    ‘’Eeeh Mwenyezi mungu why me? Why me? why me?’’

    Nilianza kutoa machozi huku nikimshuhudia Mama Gervas akiondoka kwa kunizomea.





    ***********





    Nikaanza kutetemeka nisijue nitaambiwa nini pale, wakatizamana kisha nikawaona wakiongea kwa sauti ya chini chini huku wakitingisha vichwa vyao.

    ‘’Ok! You can go!’’

    Sikuamini yale maneno nilioambiwa kwani niliambulia neno 'go' tu kisha wakanikabidhi ule ufunguo wangu, nadhani hawakuwa wanaelewa maana ya yale maandishi,

    Nikatoka pale spidi huku nikimfuatilia Mama Gervas kujua kakatizia wapi, Mara nikamwona akiwa na Wasaidizi wakimbebea mizigo yake huku wakiingia jumba kubwa lilioandikwa mbele kwa maandishi makubwa,

    'VAN LANTEER HOTEL' sikutaka hata kujua maana kwani neno 'hotel' lilitosha kwangu kujua pale ni wapi, taratibu nikajongea mpaka mapokezi na kuonesha tiketi yangu ya ndege na Pasipoti kisha yule muhudumu akawaita wenzake wakachukuwa kibegi changu na kuniongoza mpaka chumbani.

    ‘’Umenusurika we mbwaa eenh? Na unabahati mi nilitaka urudishwe Tanzania kabisa kuliko kufuatana na wewe Malaya mchafu!’’

    ‘’Mama elewa kuwa nami ni binadamu na nina haki zote!’’

    ‘’Haki! Unahaki gani wewe zaidi ya kufanya umalaya wako uende ukamuambukize mwanangu magonjwa yako ya ajabu ajabu?’’

    Alinipokea kwa matusi mpaka kufanya wale wahudumu wa pale hotelini wamshangae kwa maneno yake japo hawakumuelewa lugha anayozungumza.

    Kilikuwa ni chumba kikubwa cha vitanda viwili ndani yake kukiwa na kila kitu,

    sikuwa mtu wa amani mda wote wa usiku niliolala pale hotelini na Mama Gervas, alizidi kuwa mkali kama mbogo mpaka nikatamani asubuhi ifike haraka tuendelee na safari yetu.

    ‘’Zima hiyo taa nimesema? Mda wote umekaa na hilo li Biblia lako unajifanya eti umeokoka! Wakuokoka utakuwa malaya wewe eenh’’

    Nilizima ile taa kuepusha lawama ikanibidi nipige magoti na kuanza kusali kwa sauti ya chini chini,

    ‘’Eee Mungu Baba ahsante kwa wema wako wote ulionitendea, Baba nakuja mbele yako nikitanguliza maombi yangu kwako. Weza kuniokoa na kuniepusha kwa mabaya yote yanayo’’

    Nikiwa naendelea kuomba pale chini nikamshuhudia Mama gervas akiamka na kuwasha taa.

    ‘’Hivi we mpumbavu? We ndo wakuninyima usingizi kwa mikelele yako? Eeennh?’’

    Nilimshuhudia akiwa amefura hasira huku mishipa ya usoni ikimsimama,kisha akanivua ile nguo niliyokuwa nimeivaa (night dress) nikabaki utupu kama nilivyozaliwa, Mama Gervas alikuwa kabadilika sasa kwani aliniburuta usiku ule mpaka bafuni na kunilaza kwenye 'karo' la kuogea kisha akafungulia maji akatoka zake nje, akiwa anatoka tu nilimsemesha,

    ‘’Nimekufanya nini Mama Gervas....! Nisamehe kama nimetenda kosa kwako!’’

    Akiwa kaniacha bafuni pale kwenye 'karo' la kuogea Mara akarudi na kijikaratasi kisha akafungua na kutoa vitu kama unga unga. Nilikuwa naskia kwa watu tu lakini sikuwahi kuwekewa, ulikuwa ni 'upupu' ule unaowasha mwili mzima na sasa ulikuwa umechanganyika na maji niliyokuwemo ndani yake.

    ‘’Mamaaa ....Maaamaa Gervas nawashwa!!! Nawashwaaa!!! nawashwaa Mamaaa!!!’’

    ‘’Na hapa bado nilishakwambia Malaya kama wewe huwezi ukawa na mwanangu, na hiyo ni trela tu bado picha lenyewe’’

    Niliwashwa sana huku nikipiga makelele yasiyo na faida kwani kile chumba kilikuwa hakitoi makelele ya aina yoyote, nililia sana kwa kuwashwa mpaka nikajihisi mimba yangu inataka kutoka,

    ‘’Haya chukua uendelee kusali sasa mie naenda kulala!’’

    Alirudi Mara ya pili mule bafuni na safari hii alirudi na Biblia yangu kisha akaitupia kwenye 'karo' niliokuwamo, nguvu zilikuwa zimeniisha, niliwashwa mpaka mwili ukavimba na kujiona umezoea ule muwasho, huku nikiliegemea lile 'karo' na kuitazama Biblia yangu ambayo tayari ilikuwa imelowa sana na yale maji.

    Ilipofika asubuhi na mapema nikiwa nimepitiwa na usingizi kwenye yale maji niliweza kutoka pale kwenye karo la kuogea mpaka chumbani huku nikimshuhudia Mama Gervas akiwa anajiandaa haraka haraka,

    ‘’Fanya haraka uko nakuacha mie!’’

    Sikumjibu chochote zaidi ya kufungua kibegi changu na kuchukuwa 'dera' langu na kuvaa, kisha nikarudi bafuni kuchukuwa Biblia yangu kwenye 'karo' huku ikiwa imelowa chapa chapa, nikaichukuwa na kuipakia kwenye kibegi changu hivyo hivyo.



    ********





    Safari ya kwenda uwanja wa ndege ilikuwa imetimia, Wahudumu ndo walikuwa watu wakwanza kutugongea wakitaka mizigo yetu, walituchukuwa mpaka uwanja wa ndege lakini mda wote nilikuwa kimya sikutaka kumsemesha Mama Gervas lolote kwani nilikuwa na hasira naye sana kwa kitendo alichonifanyia jana usiku.

    Ndege ya shirika lile lile la 'Emirates' ndio ilikuwa ikitusubiria kila mtu alikuwa kwenye siti yake tayari kwa safari ya kutoka pale uholanzi na kuelekea Marekani tukipitia kusini mwa Canada.

    Safari hii nilishangaa sana kwani tulichukuwa mda mchache kama masaa matano au sita kuingia mji wa Maryland.

    Watu walikuwa ni wengi wakiwasubiria ndugu na marafiki zao,

    ‘’Umemuona Gervas yulee!’’

    Alijiongelesha Mama Gervas kwa kujifanya amesahau vitendo anavyonifanyia sikumjibu chochote zaidi ya kukaa kimya nikimuangalia huyo Gervas kwa mbali akitufata eneo tulipokuwa.

    ‘’Shikamoo Mama! Za huko utokako?’’

    Gervas alimkumbatia kwanza Mama yake na kisha akanigeukia nilishangaa Gervas kutonionyesha furaha ya aina yoyote kwani hakunikumbatia,

    ‘’Mambo Levina?’’

    Salam ile ilinifanya nianze kuchanganyikiwa na kuhisi mengi kichwani mwangu lakini halmashauri yangu ya kichwa ikafanya kazi fasta na kujua kuwa itakuwa ni uchochezi unaofanywa na Mama yake nisiendelee kuwa na Gervas.

    ‘’twendeni Mama twende ingieni kwenye gari!’’

    Tukatoka pale na kukatisha kitongoji cha Baltimore kisha tukautafuta Mji wa Detroit ambao ndio alikuwa akiishi Gervas na kufanya kazi huko.

    Tulipofika tu tulikuta kumeshaandaliwa vyakula Mezani japo hatukumuona mtu yoyote aliyeandaa,Mda wote sikuwa na raha kwani nilimkuta si Gervas niliyemtegemea,alikuwa kabadilika sana huku mda wote akionesha kuwa karibu na Mama yake. Sikwenda kuoga mda ule ila Mama alienda kuoga na aliporudi,

    ‘’Mama tukaribie tule jamani chakula nilichokitengeneza mwenyewe!’’

    Gervas alitukaribisha pale sebuleni tupate chakula lakini sikuwa na hamu kabisa ya kile chakula hivyo nikapakua kidogo sana kumridhisha tu.

    Ulipofika mda wa usiku nilishuhudia Mama akielekezwa chumba cha kulala kisha Mimi nikaingia chumba anacholala Gervas na kulala naye,Niliingia bafuni na kumuacha Gervas akiwa pale chumbani anaangalia Tv.

    Nilipotoka nikamkuta bado hajalala hivyo nikachukua nguo yangu ya kulalia tayari kwa kulala, nikaomba sala fupi kimya kimya kisha nikachukua shuka nakuanza kujifunika,

    ‘’Gervas mpenzi!’’

    ‘’mmhh!’’

    ‘’Mi ndio nalala hivyo, lakini kabla sijalala nahtaji kujua kwanini leo hujachangamka mpenzi wangu eenh!’’

    ‘’Levina!’’

    ‘’Abeeh.!’’

    ‘’...Utaacha lini kuua....?’’

    Hilo swali lilinitatiza nisijue nianzie wapi kumjibu,

    ‘’kwani nimemuua nani tena?’’

    Akaangalia kwa pembeni kisha akanitolea mafaili akidai kuwa katumiwa kwa njia ya 'Fax' jana.

    ‘’Levina, umemuua askari uwanja wa ndege kisha ukamfungia ndani humo humo na ushahidi huu hapa unatafutwa kuanzia hivi sasa!’’

    Nilitetemeka na kushindwa kujua nianzie wapi huku machozi yakinilenga lenga.

    ‘’Levina !Nakupenda na ndio Mana nipo na wewe mpaka sasa!’’

    ‘’Asante Gervas nakupenda na wewe pia, ila kitu kimoja nakuomba usimwambie Mama pliz! Kwasababu si unajua Wamama? Anaweza kumwambia Mama yangu akachanganyikiwa!’’

    Nilimdanganya Gervas ili asije akamwambia Mama yake kwani angenibadilikia.

    Moyo wa upendo kwa Gervas ukazidi kunitawala katika nafsi yangu, nilipata usingizi wa raha sana usiku kwani nilijikuta nikichukuwa mikono yangu nakupenyeza katika kifua chake kilichojaa nywele, taratibu nikizishika shika kwa kuteleza mpaka mabegani mwake, hakika Gervas alikuwa ana mwili mzuri, nilijikuta nikilegea huku nikijigeuza geuza huku na kule kumwachia Gervas mwili wangu wote aufanye anavyotaka, kwa kifupi niliufurahia usiku mpaka inafika alfajiri Gervas alikuwa bado hoi na anataka tuendelee.

    ‘’Sweetie mi nipo kwa ajili yako, nenda kajiandae tu uende kazini!’’

    ‘’Ok! Wacha nijimwagie maji fasta fasta niende!’’

    Aliingia bafuni na kujimwagia maji, kisha nikakimbia jikoni kumwandalia chai angalau kikombe kimoja na alipotoka nikasaidia kumvalisha nguo kisha akanywa ile chai haraka haraka nikamsindikiza mpaka nje na kuondoka zake, nilipoingia ndani nikapitiliza na kuingia jikoni nikamkuta Mama Gervas akiosha vyombo huku akitengeneza kitu kama chai..

    ‘’Mama shikamoo!’’

    Hakuitikia akanitolea macho kisha akapekuwa haraka haraka kwenye eneo lililokuwa na vyombo na kuchomoa kisu chenye ncha kali na kunifuata huku akiongea kwa ukali

    ‘’Sali sala zako za Mwisho malaya mkubwa we unaetaka kuniulia mwanangu kwa ukimwi uliotoka nao Tanzania’’.



    Nilipoingia ndani nikapitiliza na kuingia jikoni nikamkuta Mama Gervas akiosha vyombo huku akitengeneza kitu kama chai.

    ‘’Mama shikamoo!’’

    Hakuitikia akanitolea macho kisha akapekuwa haraka haraka kwenye eneo lililokuwa na vyombo na kuchomoa kisu chenye ncha kali na kunifuata huku akiongea kwa ukali.

    ‘’Sali sala zako za Mwisho malaya mkubwa wewe unaetaka kuniulia mwanangu kwa ukimwi uliotoka nao Tanzania!’’

    ‘’Baba katika jina la Yesu! Nakemea mapepo yanayomuandama huyu Mama. Yehova Baba fungua njia zote na umponye huyu Mama, mtenganishe na shetani anayemuandama!’’

    Nilimkemea mapepo Mama Gervas mpaka akaanguka mbele yangu kabla hajanifikia na kile kisu chake,

    ‘’Eeeh Jehova Ire kwa jina la uwezo wako nasema ahsante Baba, ahsante nakushukuru kwa matendo yako Ameni....’’

    Mama Gervas aligaa gaa mwisho akaanza kutoa mapovu mdomoni mwake mithili ya mtu mwenye kifafa, Nikaitoa mikono yangu kichwani mwake na kumshika mkono wake huku nikimwinua asimame,

    Kisha nikamtuliza kwenye kiti kilichokuwa pale jikoni nakumshuhudia akifumbua macho na kuniangalia kwa huruma huku akihema haraka haraka,

    ‘’Mwanangu Levina?’’

    ‘’Abeee Mama!’’

    ‘’Mwanangu Gervas yuko wapi?’’

    ‘’Kashaenda Kazini’’

    ‘’Uhhh...! Uhhh...! Bwana Yesu asifiwe sana Levina....!’’

    ‘’....Ameni....!’’

    Nilimuitikia lakini hakika nimeamini kwa Mungu hakuna lisiloshindikana, sasa Mama Gervas akawa ameokoka na hata alivyorudi Gervas tulikuwa na furaha sana kwani siku hiyo chakula alitengeneza Mama Gervas kisha akakiombea mwenyewe na hata ulipofika mda wa kulala aliniomba ile Biblia aliyoitupa katika karo la maji kipindi kile kule hotelini ili achambue Neno la Mungu asome.

    ‘’Bwana wetu Asifiwe!’’

    ‘’Ameni!’’

    Ilikuwa ni salamu ya Mama Gervas kila alipokuwa anaamka, Alinipenda sana tena ninaweza kusema alinipenda zaidi ya Mtoto wake Gervas.

    ‘’Leo Mwanangu tutakula nini?’’

    ‘’sijui Mama lakini mie nimekumbuka vyakula vya Tanzania, Tungepika chipsi mayai, Viazi si vipo stoo?’’

    ‘’Hapo mwanangu umenena hata Gervas akivikuta atafurahi sana’’.

    Nilipendana sana na Mama Gervas kwani tuliweza kushirikiana kwa kila kitu na hata ilipofika siku ya Jumapili tuliweza kwenda kanisani wote ikiwa ni pamoja na Gervas hakika sasa familia ilikuwa ya kilokole naweza kusema.





    * * * * BAADA YA MWAKA * * * *





    Hakika Neema ya Bwana Yesu kristu ilikuwa imetawala maisha yangu kwani hata nilipopata uchungu siku zangu za kujifungua Mama Gervas alikuwa mtu wa kwanza kunichukuwa na kunipeleka hospitali kujifungua, Gervas alifurahi sana mpaka ikaniuma kwani mtoto alikuwa si wake bali ni wa mtu nisiyemfahamu.

    Haikuwa shida kwa Gervas kwani mtoto alipofikisha umri wa miezi Nane alichukuliwa na kwenda kulelewa na shirika la kulelea watoto la ‘TAPKIDS CARE’S’. Huku gharama zote zikiwa juu ya Gervas, Nilisomeshwa lugha ya kiingereza mpaka nikakielewa kiufasaha, nilijifunza kuendesha gari mpaka nikajua na nilikuwa huru muda wote kwani ilifika kipindi naenda kanisani kila siku jioni huku upendo wangu nikiuelekezea kwa wachungaji na baadhi ya waumini wenzangu kwani nilikuwa mmoja kati ya wanakwaya katika kanisa la ‘ST.JOHN’S EPISCOPAL CHURCH’ pale pale Detroit.

    Kitu kikubwa nachoweza kusema ni kwamba hadi nilipoanza kumtumia Mama hela nyumbani (Tanzania) bado Gervas alikuwa bega kwa bega na mimi, Sikuweza kuamini lakini ilinibidi niamini kwani ‘Jammy’ alikuwa mtu tofauti na nilivyodhania, aliishi na Mama yangu vizuri sana,

    Sikusikia habari yeyote kuhusiana na yale mauaji niliyofanya kipindi cha nyuma.





    * * * *





    Ni asubuhi na mapema ambapo nilipanga na Mama Gervas twende wote ‘supermarket’ lakini yeye alidai amechoka sana kwani ni kweli jana yake usiku tulikuwa na maombi sana mpaka Gervas akatangulia kwenda kulala ili leo awahi kazini hivyo akaniacha mimi na Mama tukiendelea.

    ‘’Bwana wetu asifiwe Mama!’’

    ‘’Ameni Mwanangu umeamka salama?’’

    ‘’Ndio Mama wacha nielekee supermarket nikatafute chochote cha kuweka stoo siunajua tena akiba imetuishia?’’

    ‘’Haya Mwanangu wewe nenda tu leo mimi nimejichokea! Usijali chakula nitapika mwenyewe’’

    Niliagana na Mama kisha nikaondoka huku nikijitahidi niwahi kurudi,

    ilinichukuwa kama lisaa tu nikawa nimerudi kwani hakukuwa mbali sana na nilikuwa nikiendesha gari mwenyewe, niliporudi nilipokelewa vizuri tu na Mama na hata mizigo tulisaidiana naye kushusha.

    Lakini nilipofika chumbani kwangu nilijihisi mzito huku kichwa kikinijaa kwa mawazo.

    ‘’Mwanangu unamatatizo gani tena?’’

    ‘’Hapana Mama sijisikii vizuri ghafla!’’

    ‘’Haya pumzika tu Mwanangu na ukiamka ndio utakula sawa Mwanangu?’’

    Mama alikuwa tayari ameshaniandalia chakula lakini kwa jinsi hali yangu ilivyokuwa tete ilinibidi nipumzike kwanza alafu nikishahamka ndo nitakula.

    ‘’Vipi Levina mpenzi wangu unaumwa?’’

    ‘’Ooh, karibu Mume wangu!, Nimepitiwa tu na usingizi, pole na kazi!’’.

    Nilijikuta nimepitiwa na usingizi mzito na hata usiku ulipotimia ni Gervas alinishtua niamke kwani alikuwa tayari kesharudi kutoka ofisini.

    Sikuweza kula kabisa zaidi ya kuchukuwa Biblia yangu na kuchambua neno la Mungu na baada ya hapo nikachukuwa simu na kupiga nyumbani kuwajulia hali, lakini wote walikuwa wazima hivyo nikapunguza wasiwasi na kumuomba Mungu anibariki.

    Usiku wote nililala kwa shida sana, na hata nilipoamka Mama naye hakuwa katika hali nzuri kwani nilihisi kabadilika kidogo.

    ‘’Mwanangu mbona mvivu hivyo toka jana?’’

    ‘’Mama inanibidi leo unisindikize twende hospitali!’’

    ‘’Leo hakuna cha hospitali wala kanisani, muda wowote Watu wa usafi wanakuja kusafisha jumba lote! Hivyo hutakiwi kuondoka kuanzia sasa...!’’

    Sikuwa na jinsi zaidi ya kumsikiliza Mama Gervas, haikuwa mda tangu Gervas aelekee ofisini, hao watu takribani kumi na tano huku wakiwa na gari lao spesho waliingia ndani na kuanza usafi wa kutoa kila kitu nje kuanzia sebuleni mpaka chumbani kisha wapulizie dawa.

    ‘’Unajifanya unaumwa umwa eeh? Huyo ni shetani tu Mwanangu kakufanya hivyo? Au umeshatembea na mtu tofauti na Gervas?’’

    ‘’Ushindwe tena na ulegee kabisa Mama’’

    Nilijikuta hasira zikinipanda japo siku nyingi sijawahi kugombana na Mama toka niokoke.

    ‘’Unaniambiaje Levina? Sasa leo tutaona kati ya mimi na wewe nani kaokoka?

    Sikutaka kumjibiza tena chochote zaidi ya kumwacha aongee akichoka ataacha, Nikachukuwa Biblia yangu iliyokuwa tayari imeshatolewa nje.

    Ndani ya nusu saa jumba lote lilikuwa limeshatolewa kila kitu nje huku wale wafanyakazi wakiendelea kupuliza dawa mbali mbali, na walipomaliza wakaanza kurudisha kitu kimoja kimoja, kwasababu walikuwa wengi haikuwachukuwa mda mrefu wakawa wamemaliza tena walimalizia chumbani kwangu,

    ‘’Ooh Jesus...! Nini tena hiki hapa?’’

    Maskini nilishasahau habari za mikosi kwa mda mrefu sana na sasa hivi niliona kama miujiza kwani wale watu wa usafi walivyomaliza kuingiza vitu, niliingia chumbani kwangu, nikiwa nakagua kagua usafi walioufanya mpaka chini ya kitanda, macho yangu yalikutana uso kwa uso na vitu vyeusi vyeusi vilivyofungwa kwa kitambaa lakini halmashauri yangu ya kichwa ikafanya kazi na kugundua kuwa zile ni hirizi, nikiwa bado nashangaa pale mara Mama Gervas akaingia ghafla chumbani.

    ‘’Nini tena Mwanangu!’’

    ‘’Mama sijui nani kaweka hizi hirizi chumbani kwangu?’’

    ‘’Najua tu utakuwa wewe mchawi unajifanya umeokoka. Mimi nakuangaliaga tu siku nyingi nadhani mda wako wa kurudi Tanzania umefika sasa mpumbavu mkubwa weeeee!

    ‘’Mama mi sijui kwakweli!’’

    ‘’Hapana wewe ndiye unaenirogea mwanangu kila siku asikuache na hii mi hirizi yako eenh? Ngoja nimpigie simu aje ashuhudie unavyomroga kila siku mchawi mkubwa we?’’

    ‘’Hapana Mama usifanye hivyo! Siyo mimi Mama!’’



    Nililia sana lakini haikusaidia mpaka pale Gervas alipokuja na alipofika tu Mama Gervas akawa tayari kazitoa zile hirizi na kumuonesha.

    ‘’Levinaaaaaa?’’

    ‘’Abee Mme wangu!’’

    ‘’Nani Mmeo! Nauliza ni wewe ndio uliofanya uchafu huu?’’

    Huku akinioneshea zile hirizi.

    ‘’Hapana sio mimi!’’

    ‘’Nani sasa? Kwahiyo ni Mama yangu eenh? Si nakuuliza wewe?’’

    ‘’Nisamehe Gervas kama nimekosea!’’

    Neno hilo lilimkera sana Gervas hadi kufikia hatua ya kunipiga kibao,

    ‘’Gervas mpenzi rudi! Nakuomba rudi, Usiondoke....!’’

    ‘’....Niache hukoooo....! Aliongea kwa ukali huku nikiling'ang'ania shati lake asiweze kuondoka lakini haikuwezekana kwani alichukuwa ufunguo wa gari, akaliwasha na kuondoka zake. Nilinyosha mikono miwili juu huku nikimlaumu mwenyezi Mungu.

    ‘’Mungu wangu.....!Mungu wangu....! mbona umeniacha....! Kwanini wajitenga mbali nami....?’’

    Niliendelea kulia pale bila msaada wowote huku Mama Gervas akiendelea kunisakama kwa maneno.

    ‘’Embu tuondolee upumbavu wako hapa.... Wewe unadhani Mwanangu anaweza kuendelea kuwa na wewe Mwaka mzima bila ya hata mtoto? Na lazima utakuwa mgumba weeee!"

    Aliendelea kuniambia Maneno ambayo yaliutesa sana moyo wangu.

    Mara simu ya Mama Gervas ikaita, haraka haraka akaipokea na kuanza kuongea, nikabaki namtolea macho huku nikiwa bado na uchungu kwa kile kilichonikuta.

    ‘’..Hallo...!

    .....Aaah, Mwanangu Gervas...! Enh..,.nipo naye bado huyu mwanaizaya... Haya ongea naye...!’’

    ‘’...Hallow Levina...!’’

    ‘’.....Eenh Mme wangu....!’’

    ‘’Nimeshakwambia Mimi siyo Mumeo kuanzia sasa...?, Na tena kusanya kilicho chako, Ukamchukue na Mwanao alafu upitie nauli hapa ‘MARRIOTT HOTEL’ urudi zako Tanzania nimekuchoka Levina! Umeniskia? Ole wako nirudi nikukute utanijua vizuri na huo uchawi wako mpumbavu sana!’’

    Sikuwa na lazaidi ya kamasi kunitoka, macho kuwa mekundu, mwili kunilegea huku sauti ikikatika na kichwa kunigonga kikiambatana na kizungu zungu.

    ‘’Eeh Mungu Baba kama uliteswa na kufa pia ukafufuka! Weza nami kuniokoa katika mikosi hii! Sina mtetezi aliyebaki zaidi yako Baba muumba wa mbingu na nchi....!’’

    Nilipomaliza sala ghafla nikahisi Neema ya ajabu imenitembelea mwilini mwangu kwani nilisisimka nakuhisi kama Maombi yangu yamekubaliwa hivyo halmashauri yangu ya kichwa ikanituma moja kwa moja nielekee kwa Mchungaji kanisani pale ninaposali, haikuwa mbali sana na wala sikuhitaji kutembea na gari kwani niliamini itazua tena ugomvi mwingine hivyo nikajikongoja hadi kanisani ambapo pembeni yake lilikuwa limejengwa jumba kubwa la kuishi wachungaji.

    ‘’Bwana wetu asifiwe!’’

    ‘’Ameni!!!!’’

    ‘’Baba niko hapa mbele yako kwanza kukupa taarifa juu ya kutoelewana na Mme wangu, Hivyo nikiwa kama muumini wako nakuomba sana Baba unisaidie kwa hilo!’’

    Yule mchungaji niliyomkuta alinielewa kwani amenizoea sana kipindi ninachokuja kwenye kwaya, alinichukuwa na kunipandisha katika gari yake kisha safari ya kurudi nyumbani kwa Gervas ikaanza.

    Ilikuwa imeshatimu kama mida ya jioni sana kwani nakagiza kalianza kutokeza tayari tulikuwa katika geti la nyumbani kwa Gervas tukipiga hodi.

    Geti likafunguliwa,

    ‘’Bwana wetu asifiwe’’

    ‘’Washenzi wakubwa nyie! Yani Levina umeamua kumleta na huyu Mchawi mwenzako mwingine siyo?’’

    ‘’Gervaaaaaaaaas?’’

    Ilikuwa ni sauti ya Mama Gervas baada tu ya kufungua mlango akaanza kutushambulia kwa maneno huku akimwita mwanaye Gervas aje,

    ‘’Haya Mwanangu embu waone hawa wachawi sijui wamefuata nini hapa?’’

    ‘’Levina!’’

    ‘’Abee!’’

    ‘’Haya ingia ndani sasa hivi tena haraka!’’

    Sikuamini maneno ya Gervas kwani ni kweli alionesha moyo wa huruma hadi Mama Gervas akashangaa kwa kauli aliyotoa mwanaye.

    ‘’Mchungaji huyu kafika, Ahsante kwa kumrudisha wewe rudi kaendelee na shughuli zako kanisani!

    ‘’Eeh Baba yetu uliye mbingu!,Nasema ahsante Baba kwa kuweza kuwabadilisha Gervas na Mama yake, Nakuomba Baba waishi na waendelee kuwa na Amani, Na moyo wa huruma maishani mwao!’’

    ‘’Ameni kwaheri mchungaji!’’

    ‘’Haya jamani Amani ya Bwana iwe nanyi, Bwana wetu Asifiwe sana!’’

    Niliingia ndani huku nikimwacha Gervas akiagana na yule mchungaji.

    Nilipoingia tu ndani nilichokutana nacho naweza kusema sitakuja kusahau maishani Mwangu na ndiyo maana nasema kuwa ‘Sitaki Tena' bora nife!’ kwani mama Gervas alikuwa ameshikilia waya wa moto huku akimwita mwanaye aje kunifunua nguo ili waanze kunichoma choma eneo lote la mwili, naye Gervas alipoingia ndani akanishikilia mikono yangu miwili kwa nguvu.

    ‘’Mchome kabisa mpaka iingie ndani? Choma na li uso lake akawange vizuri!’’

    ‘’Nimekosa nini jamani? Nisameheni! Gervas nisamehe! Mama nisamehe!’’

    Niliumia sana na nikaomba bora nife tu kuliko mateso ninayoendelea kuyapata, Ndani ya nusu saa walikuwa wameshanichoma choma karibu mwili mzima, mara mama gervas akaenda chumbani kwake nakutoka na viwembe, alianza kuninyoa upara kuanzia kichwani mpaka sehemu zangu za siri huku Gervas akiwa msaidizi kwa kunipiga vibao kila ninapopiga kelele, niliumia sana mwili wote ulikuwa wamoto ukiambatana na sakafu ambayo tayari ilikuwa imetapakaa damu yangu.

    ‘’Naombeni mniache niondoke zangu jamani kama mnaniua niueni tu! Leteni kisu mniue kabisa! Niueni nasema niueniiiiiiii!’’



    *********





    ‘’Hapa leo mpaka tuhakikishe umekufa tunakuona halafu tunachukuwa mwili wako na kuuchoma moto! Umezidi uchawi! Kila siku kutuwangia tu?’’

    ‘’Mwanangu Gervas embu endelea kumshika hivyo hivyo ngoja niende nikachemshe maji ya kumwangamiza huyu mchawi wetu, Ndiyo dawa yao hawa!’’

    Nilizidi kulia huku nikiwa sina tena mtetezi kwani hata Gervas alikuwa tayari kitu kimoja na Mama yake, haikuchukuwa mda Mama Gervas akawa na sufuria lililokuwa linatoa mvuke likiashiria kuna kitu ndani yake tena cha moto sana, hakika yalikuwa maji ya moto.

    ‘’Mama usinichome pliiiz! Mamaaaa! Mamaaaa! Mama Gervas pliiiiiiz! Aiiyaa iyaaa yayaaaa yaaaaaa! Gervas Mwambie Mama yako asinichome jamani!’’

    ‘’Mchawi mkubwa wee embu Mama limwagie hayo maji haraka libabuke tukalichome moto?’’

    Gervas alikuwa akimshinikiza Mama yake animwagie yale maji ya moto lakini kabla hayajanifikia tayari miguu yangu ilikuwa imeshasalimiana na miguu yake Mama Gervas hivyo nikamtegua akateleza na sufuria lake kwa nyuma huku lile sufuria likimfunika kwa juu yake

    ‘’Mamaaa...! Mamaaa....!’’

    Gervas aliita kwa hasira huku akiniachia na kumuwahi mama yake ambaye tayari alikuwa ameanguka chini huku nikiamini kama hajafa basi atakuwa nusu mfu.

    Bila kupoteza muda ndio ikawa nafasi yangu ya kutoroka pale pale nikavuta pochi ya Gervas aliyokuwa ameiweka mezani pale sebuleni na kukimbia nje, huku nikimwacha Gervas akimshika na kumlilia Mama yake kwa uchungu pale chini.

    Nilivyofika nje nilitetemeka na kujibanza kwenye kauchochoro ka kutokea nje huku nikiangalia kama Gervas atatoka nje, Haijachukuwa mda Gervas akatoka nje.

    ‘’Levinaaaa....! Levinaaaa.....! Levinaaaa....! Levinaaaa.....!’’

    Nilikaa kimya kwani alionesha kutoka kwa hasira kali huku mkononi kashikilia kisu, niliamini kabisa itakuwa alitaka kuniua, Mara akarudi ndani na kutoka tena nje kwa Mara ya pili huku akimbeba Mama yake nadhani huenda alikuwa amezidiwa au amekufa kabisa, alipotoka pale nje gari yake ilikuwepo moja tu nyingine sikuweza kujua kaiacha wapi. Mara akamlaza mama yake pale nje ya gari kisha akajisachi mifukoni akionekana kuna kitu kakisahau. Akarudi ndani tena dakika chache akatoka huku akiönekana kuzidi kuchanganyikiwa, nikaanza kuingiwa na roho ya huruma huku nikijiangalia majeraha yangu waliyonidhuru, kisha nikaangalia mikononi mwangu..

    ‘’Ooh my God!’’

    Kumbe nilivyochukua ile pochi ya Gervas nilichukuwa pamoja na funguo za gari bila kujijua kwa kuchanganyikiwa

    ‘’Sijui nimrudishie funguo yake tu!’’

    Nilizidi kuingiwa wasiwasi huku Moyo wa huruma ukinitawala kila nikiendelea kumuona Gervas akihangaika kujisachi pale. Nikasimama nakuanza kujitokeza na kuelekea lile eneo aliopo Gervas kwa nia ya kumrudishia ufunguo na pochi yake, lakini kabla sijafika tu lile eneo nikahisi nafsi inapingana na mimi kwa kile kitendo cha kurudisha ule ufunguo..

    Hivyo nilichokifanya nilirudi haraka kwenye lile eneo ambalo nilikuwa nimejificha na kuanza kuita kwa sauti ya juu.

    “Gervaaas....! Gervaaas.....!”

    Alianza kugeuka huku na huku asielewe anaitwa na nani, pale pale nikatumia nafasi hiyo kuutupia ule ufunguo eneo alilokuwepo Gervas,

    “Levinaaa....! Levinaaa...! njöoooo....!”

    Aliuokota ule ufunguo na kunishuhudia nikikimbia huku akibaki kuniita nirudi.

    ‘’Mlivyoniumiza na kunitesa inatosha!”

    Nilijisemea kimoyo moyo huku nikikimbia zangu kuelekea sehemu isiyojulikana na kumuacha Gervas pale nje kwake.

    Sikumuogopa mtu yeyote kwa jinsi nilivyokuwa nimeharibika mwili wangu kwa makovu, chini nilikuwa peku huku kichwani nikiwa na upara tena ule uliokuwa na damu damu kwa sababu ya kunyolewa ovyo na Mama Gervas. Nikiwa bado nipo njiani huku nikitembea nisijue naelekea wapi ghafla..





    * * * *





    “Niko wapi hapa?”

    Heey! Calm dawn! Calm dawn Lady!”

    “who ar u!”

    Niliuliza kwa sauti ya ukali.

    “Em Dactar Stan, fram 'Detroit hospital'

    Nilijikuta nikiwa tayari hospitali huku maumivu ya mgongo yakinizidia, nilijitahidi kuvuta kumbukumbu nijue imekuwaje nipo hapa lakini kitu nilichoweza kukumbuka ni pale nilipogongwa na gari ya Gervas usiku nje kidogo na maeneo ya kwake,

    “Gervas alitaka kuniua?”

    Nilikuwa nabadilishwa dripu huku nikijiuliza mara mbili mbili.Niliwekwa katika wodi ya wagonjwa wasiojiweza (mahtuti) huku nikiwa wodi moja na mtu ambaye sikumgundua vizuri nadhani ni kutokana na maumivu aliyonayo, pia alikuwa amezungushiwa bandeji mwili wote kuanzia kichwani mpaka miguuni huku sehemu ya macho ikiwa wazi.

    “Kweli nimeamini kuna watu wanamatatizo na wanateseka na kuumia zaidi yangu! Embu mcheki huyu mtu, inatia huruma jamani!”

    Nilijikuta namuonea huruma mgonjwa ambaye tayari alikuwa kitanda cha pembeni yangu huku dokta akimbadilisha dripu.

    “Eeh Mungu niepushe na mikosi! Nisije kuwa kama huyu jirani yangu, pia Mponye na huyu Mama aliokuwa pembeni yangu!”

    Nilijisalia kimoyomoyo huku nikishindwa kabisa kuamka pale kwenye kitanda kutokana na maumivu ya mgongo, na kichwa.

    Nikiwa bado namshangaa yule Mama ghafla nikamuona Gervas kwa macho yangu akiwa anaingia na Nesi katika wodi niliokuwamo,

    “Yesu wangu! Nani aliyemwambia nipo hapa? Au yeye ndo aliyenileta?”

    Ni kati ya maswali yaliyonichanganya kichwa huku nikimwangalia Gervas aliyekuwa akikaribia eneo nililopo, nilitamani ardhi ipasuke nidumbukie, kila nikijiangalia mwili wangu ulikuwa bado una makovu kovu na maumivu yakinizidia yakiambatana na hasira kila nikiendelea kumtolea macho Gervas, aliponifikia karibu yangu nikageuza kichwa changu upande wa pili kisha nikatumia mkono ule mmoja kujifunika kichwa haraka haraka,

    Mara nikasikia kimya kisha nikaisikia sauti ya Gervas kwa mbaaali.

    “Unaendeleaje Mama!”

    “Pole sana Mama yangu utapona tu!”

    Nilishtuka na mwili kunilegea ‘then’ halmashauri yangu ya kichwa ikafanya kazi fasta na kujua kuwa yule ni Mama yake Gervas.Nikaendelea kutega sikio kuwasikia mazungumzo yao.

    “Vipi Mwanangu yule mwanaizaya Levina ulimpata?”

    “Mama wakati nakukimbiza hospitali nikiwa njiani na gari nilimuona, nikamgonga ‘then’ sikuangalia tena, lakini kwa jinsi nilivyompitia hawezi kupona pale!”

    Yale maneno aliyokuwa akizungumza Gervas kwa Mama yake yalizidi kunitia hasira na kumchukia kabisa Gervas.

    Nilichokifanya nikuvua ulokole wangu kwa muda nakuhakikisha nimewaua wote wawili haijalishi nimepona au bado naumwa.







    * * * *





    Ilipofika mda wa usiku, ni nesi mmoja tu ambaye kila baada ya dakika tano hadi kumi, alikuwa ndani ya wodi yetu akituangalia kama kuna mtu anahitaji msaada wowote. Mwili wangu ulikuwa haujiwezi kwa lolote na hata chakula cha mchana nilikula kidogo lakini gharama zote zilikuwa ni kwa hospitali,

    “Yani leo simuachi, nitahakikisha nimemuua kwa mkono wangu mpumbavu mkubwa aliyetaka kuharibu maisha yangu yeye na mtoto wake”

    Sasa hasira zilikuwa zimefika mwisho huku kwikwi ikinibana,taratibu nikaanza kuichomoa mirija ya dripu niliyokuwa nimewekewa, nilipomaliza nilijiangusha mpaka chini kwakuwa nilikuwa na maumivu mgongoni si sana niliweza kujiburuza mpaka kitanda cha Mama Gervas, nilipofikia pale nikaangaza pembeni yake nikakutana na boksi likiwa lina picha za sindano, haraka haraka nikafungua nakuchomoa sindano kisha nikavuta dawa kwenye kikopo, sikuhitaji hata kulijua jina lake wala matumizi yake, kisha nikamwamsha.

    “Mama Gervas?”

    “Heee! Mwanangu Levina? Unafanyaje huku sasa hivi?”

    “Nipo kwa ajili yako!”

    Nikaivuta ile dawa iingie kwenye sindano kwa wingi kisha nikamshika kwa nguvu kichwani akawa anataka kupiga kelele, nikaivuta ile dripu yake na kumnywesha maji ya dripu kisha nikamjaza na mirija ya ile dripu yote mdomoni mwake baada ya hapo tena nikachukuwa shuka lake na kumsokomeza nalo mdomoni,Sasa kilichofuatia nikuanza kumtoboa macho yake nikitumia sindano,

    "Kufa kabisa mshenzi kabisa!!!"

    Kwa hasira niliyoendelea kuwa nayo nilijikuta namfunua nguo yake ya ndani (Chupi), kisha nikaingiza mkono na kupenyeza ile sindano na kuimwaga dawa ndani yake, sikutaka kumshuhudia akikata roho ila niliamini hawezi kupona hata kidogo,

    “Mungu akulaze pahali pema peponi....! Amina...!”

    Nilimalizia kwa sala huku nikichechemea kutoka nje,

    Kulikuwa kimya sana, sikuweza kukutana na Nesi wala dokta katika korido yote lakini niliamini kabisa kamera zinafanya kazi hivyo niliongeza spidi mpaka eneo la nje nikajificha eneo la kupaki magari huku nikiwaangalia jinsi ya kuwatoka wale walinzi waliokuwa wamejiweka kwenye kijumba kwa chini pale getini.

    “Hili hili naondoka nalo!”

    Lilikuwa ni gari jeusi aina ya 'Toyota Spacio' ilikuwa haijafungwa milango, nikaingia ndani yake na kujificha eneo la siti za nyuma ya lile gari kimya.

    Haikupita mda nikasikia kelele za watu wakijibizana, mara wakaingia katika gari nililokuwamo.

    “Geofrey nakwambia kweli, nimemuuliza na Dokta kaniambia kuwa kuna binti aligongwa na gari ndio aliyekuwa amelazwa pembeni na Mama!”

    “Sasa we utajuaje kama ndio huyo aliyemuua Mama yako?”

    “Sikiliza Geofrey, nilivyoelezewa kuwa yule binti alikuwa na makovu mwili mzima na ana upara uliokuwa umetapakaa vidonda donda vya damu, mimi nakwambia huyo atakuwa ni Levina tu!”

    “Levina yupi? Yule Mke waaa...?”

    ‘’....Enhee....!, Huyo... huyo..! yule aliyekuwa Mke wangu! Nipo radhi kumtafuta na nikimkosa basi Mama yake atakuwa halali yangu!"

    Yale maneno waliyokuwa wanaongea Gervas na rafiki yake yalinitisha nikajikuta naropoka kwa hofu niliyokuwa nayo pale.

    “Ukamuue nani? Na bado wewe?”

    Pale pale nikafungua mlango nakujitupa nje na kubiringita mpaka uvunguni mwa gari lingine la pembeni yangu,

    “Criminal! Criminal! please help em!”

    Sikutaka kabisa kugeuka nyuma wala kujua kama wananifuata au la. Nilipofikia gari la tatu nikafungua mlango na kuingia kisha nikakaa kimyaa huku nikisikilizia itakuwaje pale.

    “Oh..!, My God..!, Bwana niokoe...,Yesu niokoe...!!!!!,

    Nikasali kimoyo moyo

    Mara nikaona gari la kina Gervas hiloo linatoka nje ya geti haraka haraka namimi nikapata wazo la kuongozana naye kujua ataenda wapi?

    “Ooooh maskini Levina mimi....! Ona sasa hamna ufunguo!”

    Nililegea mwili mzima baada ya kugundua pale hakuna ufunguo,Haraka haraka halmashauri yangu ya kichwa ikafanya kazi fasta na kugundua ile njia inayofanywa mara nyingi na vijana wa kihuni wanapoiba magari,

    Nikainama chini na kuanza kuzivuta nyaya zilizokuwa zinaelekea maeneo ya kwenye `msteringi` japo sikuwa najua wanafanyeje fanyeje,

    “Yap..., yap.... Yeeeeees....!”

    Furaha ilinijaa tele moyoni baada ya kufanikiwa kuziunganisha zile nyaya kisha nikashuhudia gari kuwaka, sikutaka kupoteza muda nilitoka spidi mpaka getini huku nikiwa nimefunga vioo vya ile gari ambavyo vilikuwa na 'Tintedi' .Nilishangaa nilipopita getini bila kuzuiliwa lakini nilikuja kujigundua kuwa itakuwa ni gari hata ya Dokta au mtu anayefahamika sana.

    “Sasaaaa, mungu wangu! Watakuwa wameelekea wapi hawa?”

    Hilo swali lilinisumbua sana kichwa huku nisijue nielekee wapi, lakini haikuchukuwa muda nikawa tayari nimeshapata jibu na kuongoza moja kwa moja mpaka 'TAPKID'S CARE'S kwenda kumchukuwa mtoto wangu ‘Jelly’, lakini nilipofika tu pale nje moyo ulipasuka ghafla.

    ‘’Wanampeleka wapi? Na kwanini Gervas ananifanyia hivi jamani?”

    Nilijikuta naishiwa nguvu huku nisielewe nini cha kufanya huku nikiwa namuangalia Gervas akiwa kambeba mwanangu 'Jelly' na akiwa anampakiza kwenye ile gari niliowaacha nayo toka pale hospitali.

    "Ama zangu, ama zao....!, niwe hai au waniue lakini mpaka nihakikishe mtoto wangu anakuwa mikononi mwangu”

    Nikawatolea macho mpaka nilipohakikisha wanatoka pale nami nikawa nyuma yao nawafuatilia taratibu, tulitembea mwendo mrefu kidogo wakakata kona nakupaki gari lao eneo la ‘Supermarket` ya 'Honey Bee La Colmena'..,

    Nami nikapaki maeneo ya karibu yao nakuangalia nini kitaendelea pale, mara akashuka Gervas peke yake na kukimbia kuelekea ndani pale ‘Supermaket’,

    “Hii ndio nafasi yangu siwezi kuichezea hata kidogo”

    Nikaangaza pembeni ya lile gari lakini sikuweza kuona chochote zaidi ya kuuona waya mwembamba, nikauchukuwa hivyo hivyo na kwenda mpaka eneo la lile gari sikutaka kupoteza muda nikafungua mlango wa nyuma taratibu, nakuanza kumnyemelea na nilipomfikia karibu nilimvisha ule waya kwa nguvu zote kisha nikauzungurushia pale pale kwenye kiti chake, mpaka nilipohakikisha yupo kimya, nikajua lazima keshakufa kwani ule waya ulimpitia hadi eneo la kohoni mwake mpaka nikahisi nimevunja mishipa ya koromeo lake ndipo nikamwachia,

    “Twende Mwanangu hawa si watu wazuri”

    Nikambeba mwanangu na kukimbia naye mpaka kwenye gari,nikiwa ndo namuweka tu vizuri kabla hata ya mimi sijapanda mara nikasikia sauti pembeni yangu.

    “Levinaaa, Levinaaa mrudishe huyo mtoto nimesema?”

    “Kama ni damu yako atarudi, na kama si damu yako sitomrudisha!!!!”

    Hayo maneno yalimkera sana Gervas mpaka akavitupa vile vitu alivyokuwa amevishika toka supermarket na kuanza kunifuata bila hata kujua ndani ya gari lake kama tayari kuna maiti, bila kupoteza muda nikaingia ndani ya gari langu kisha nikaanza kuzigusisha zile nyaya ili liwake, kila nikijaribu gari inakataa, nikasachi kwa pembeni pembeni kwenye zile ndroo za gari labda naweza kupata ufunguo wa akiba,sikupata zaidi ya kuambulia kijibastola tu,huku nikimwangalia Gervas ndo anakaribia kunifikia,

    “Nimesema Gervas toka!, Tokaaa!, rudi ulipotoka nimesema?”

    Nikaikoki ile bastola tayari kwa kumfyatua.

    “Simtaki mtoto ninachotaka ni hiyo roho yako tu Levina!”

    Gervas aliongea kwa ghadhabu na kunichochea hisia zangu za kumfyatua,

    “Gervas nakupenda lakini imenibidi,”

    pale pale nikafyatua miguu yake yote miwili,

    maskini Gervas akabaki anatapatapa pale chini huku watu wakinitolea macho kwa kitendo nilichokifanya.

    “...Ingekuwa Bongo kwetu nisingenusurika...”

    Niliusemea moyo huku nikimfuata Gervas aliyekuwa tayari kadondoka chini na damu zikimtiririka kupitia magotini mwake, huku nikiingiliwa na moyo wa huruma, nilipomfikia karibu Gervas alikuwa kalegea hana nguvu yoyote.



    ********



    “Levinaa..? Levinaaa? Umemuua Mama yangu na mie unaniua siyo?”

    “Gervas pole! Ilinibidi nifanye vile sina jinsi kwa mlivyokuwa tayari mmenifanyia pale kwako!”

    Nilimjibu kwa hasira huku nikimburuza kuelekea eneo nilipokuwa nimepaki gari langu nikamnyanyua nakumpakiza ndani ya gari, kisha nikajaribu tena kwa mara ya pili kuliwasha gari kwa ajili ya kumuwahisha Gervas hospitali,

    Nikiwa ndani ya gari bado nahangaika kuliwasha mara Polisi na gari zao wakawa tayari wameshafika lile eneo huku wakiingia kwenye lile gari nilipokuwa nimemuua rafiki yake Gervas, nikashuhudia wakiutoa ule mwili wa yule mtu niliyomuua huku watu waliokuwa lile eneo wakiwaelekeza askari sehemu niliyopo,

    Woga ulianza kunitanda huku nikishindwa nifanyaje, Gari limeshindwa kuwaka pembeni yangu Gervas akinililia kwa maumivu aliyonayo,

    Nilijikuta natoka nje huku nikimwacha mwanangu na gervas ndani ya gari, kisha wale askari kabla hawajanifikia karibu nikainua mikono yangu miwili juu nakujisalimisha mbele yao,

    Ile askari wakiwa wanakaribia kunifikia tu mara nikasikia sauti inatoka ndani ya gari,

    “Mummy! Mummy! Mummy!”

    Kugeuka nyuma namuona Gervas akimnyonga Mwanangu ndani ya gari.

    “Gervaaaas...? Stoooooop....!”

    ********



    ‘’Tax! Tax! Tax!”

    Gervas alikuwa tayari anaita teksi kwa upande wa pili huku mwanangu akiwa kamkwida ubavuni mwake hali ile ilinifanya nidhani anataka kumyonga kumbe siyo, lakini alikuwa hawezi kushuka kutokana na miguu yake yote kuingiwa na risasi,,

    “Liwalo na liwe! Polisi kitu gani?”

    Nikageuka nyuma na kumuwahi mtoto wangu kwa Gervas na kumpora, nikampakiza kwenye teksi ile ile aliyoiita Gervas kisha nikasaidiana na yule dereva teksi haraka haraka bila kujali kama polisi watafyatua risasi au la, Tukambeba Gervas na kumpakiza ndani ya ile teksi.

    “Please driver! Gooo...! Gooo....! Gooo.....!”

    “where are we Going?”

    “Atheneum Suite hotel!”

    Nikaona kama ananichelewesha huku nachezea kifo kwani tayari askari walikuwa bado kidogo sana watufikie, nikamsukuma yule dereva teksi kwa nje kisha nikaligeuza gari la lake kwa kasi ya ajabu na kutokomea huku nikiwaacha wale polisi wengine wakiwa wanafyatua risasi huku wengine wakiligeukia gari lao tayari kwa kunifukuza, nilijitahidi kuendesha kwa kasi huku nikikimbiza gari na kukatiza hata maeneo mengine sikuyajua vizuri lakini Mungu alinyoosha njia, nikapita kona kona na kuingia kichochoro nisichokijua kisha nikacheki 'saiti mila' yangu sikuona gari yoyote ya polisi iliyokuwa inanifuatilia kwa nyuma, nikapunguza mwendo, huku nikipumua taratibu mara,

    “Nimekupata sasa, Nakuua hapa hapa!”

    Alikuwa ni Gervas ambaye tayari alikuwa kaiwahi ile bastola niliyokuwa nayo na tayari alikuwa ameniwekea kichwani huku akitaka kunifyatua.

    “Gervas usiniue pliiz?”

    “Umeniumiza sana na kunisaidia sana, lakini kwanini umemuua Mama yangu?”

    Ilo swali lilinifanya nianze kutetemeka, na kuanza kuhisi haja ndogo ikijipenyeza taaratibu kwenye nguo yangu ya ndani, nikiwa bado naendelea kutetemeka mara mlio wa gari la polisi tukaanza kuusikia.

    “Kimbiza gari hadi ofisini kwangu haraka?”

    Aliniamrisha Gervas huku akiwa bado kaniwekea

    Ile bastola kichwani mwangu, Nilikimbiza ile gari mpaka karibu na ofisi yake nikalisimamisha kisha halmashauri yangu ya kichwa ikafanya kazi fasta,

    “Gervas nakuomba sana na niko tayari kukuacha na mtoto lakini usimfanye lolote pliiz!, naomba unipe pesa kidogo niingie pale!”

    “Ya nini? na Kufanya nini?”

    “Nahitaji kukununulia kibaiskeli cha kutembelea kwa muda”

    “Shilingi ngapi?”

    “Dola 95!”

    “Chukuwa hapa mfukoni”

    Nikamsachi mfukoni na kuchukuwa fasta nikaingia pale dukani na kutoka na kibaiskeli nikakiweka nyuma ya gari.

    “Levina?”

    “Abeeh!”

    “Nakupenda!”

    Yale maneno yalinisisimua kutokea kwenye nywele kupitia mapajani mwangu mpaka kwenye unyayo, kisha nikamwangalia mwanangu nakumbusu, nikamkumbatia na Gervas nikampa’ denda’ takribani kama dakika mbili nzima.

    “Gervas Mme wangu? Nakupenda sana sana sana tena sana.....!”

    “Ok...!,Levina...., Twende ofisini kwangu mara moja tukaangalie utaratibu unakuwaje.....”

    Nikaliwasha gari na kuelekea ofisini kwa Gervas huku moyo wangu ukiwa na amani iliyotawaliwa na furaha tele ndani yake, sikuamini kama nitakuja kuendelea na Gervas, ni kweli Gervas bado amenikaa akilini na kumuacha sintoweza hata siku moja, nampenda sana tu,

    Ndani ya kama dakika Tano tukawa tayari ofisini kwa Gervas, nikashusha kile kibaiskeli nakukifungua kisha nikamfuata Gervas nakumbeba na kumpakiza kwenye kile kibaiskeli baada ya hapo nikamchukuwa na mwanangu nikambeba mgongoni na kuanza kumsukuma Gervas kuelekea ofisini kwake,

    Wafanyakazi wenzake wengi walikuwa wakimshangaa na kumpa pole huku wengine wakitaka kujua imekuwaje lakini Gervas aliwadanganya amepata ajali, moja kwa moja mpaka tukaingia kwenye mlango ulioandikwa 'CEO' lakini kwa sasa nilikuwa msomi tena mjanja hivyo hilo neno halikunichanganya hata kidogo akili yangu, kwani nilijua tu itakuwa ni ofisi ya mkubwa wao tena mkurugenzi na lile neno linamaanisha 'CHIEF EXECUTIVE OFFICER' tukaingia mpaka ndani Gervas akaanza kuongea na bosi wake pale huku akimdanganya kwa maneno mengi akimtaka aache kazi kutokana na matatizo aliyoyapata na kudai kuwa anakwenda kujitibia Tanzania.

    “Sign here! Be carefully please !”

    Ni kati ya maneno waliokuwa wanaafikiana na baada ya hapo tukatoka na Gervas huku akiwa kashikilia karatasi kubwa kuelekea ofisi ya mhasibu.

    Tukatoka nje huku nikimsaidia Gervas kushika burungutu la mapesa yaliowekwa kwenye mfuko wa kaki yakiambatana na hundi 'Cheque' nyingine ya pesa zilizobaki, na kuelekea hospitali nyingine tofauti na ile ya kwanza, yenyewe iliitwa 'Henry Ford Hospital' hapa hapa Detroit, ndani ya masaa manne tayari gervas alikuwa keshatolewa risasi lakini itamchukuwa muda kidogo mpaka aje kuweza kutembea mwenyewe bila ya kutumia kibaiskeli cha kubebea wagonjwa.





    * * * * * ** *





    Safari ya kurudi nyumbani anapoishi Gervas ikaanza, mwanangu ‘Jelly’ alikuwa mdogo sana kwani alikuwa na umri wa miaka miwili na siku sabini tu.

    “Levinaa? Sahau yote yaliyopita na jiskie uko nyumbani!”

    “Ahsante sana Mme wangu Gervas!”

    Tukaingia nyumbani,Kulikuwa bado ni kuchafu sana tangu kipindi kile huenda Gervas alikuwa halali mule, nikafikia kufanya usafi wa nguvu kisha baada ya hapo nikapiga simu nyumbani kuwajulia hali kwani ni muda mrefu kidogo sikuwasiliana nao.

    Hakika ulikuwa ni usiku wa furaha sana kwangu kwa mara nyingine, niliweza kuyafurahia maisha tena nikiwa na Gervas, mpaka ilipofika asubuhi yake nikaingia jikoni kwa ajili ya kuandaa kifungua kinywa mara nikasikia sauti za gari la polisi zikiingia pale nyumbani, haraka haraka nikamkimbilia Gervas kumwambia kisha nikamfuata mwanangu ‘Jelly’ na kumbeba nikajificha huku nikimwacha Gervas akijikongoja kwa kibaiskeli,

    ‘Is diz ur house?”

    “Yes of course!”

    Muda wote nilikuwa nimeyapenyeza maskio yangu huku nikitaka kujua nini kinaendelea,Mara moyo ukaripuka ghafla baada ya kusikia wale mapolisi wakimwambia Gervas kuwa Mama yake hajafa ila ni kipofu na anahitaji kumuona, na wenyewe wako pale wakisaidiana na madokta kumtafuta binti anayeitwa Levina kwani ndio aliyetaka kumuua Mama yake Gervas na akatoroka hospitalini na Gari ya Dokta, kwa mujibu wa kamera zilivyoonesha tukio lote, hivyo anatafutwa kwa makosa matatu, la kwanza, kumchoma sindano za ganzi machoni mwa Mama Gervas, la pili kutoroka bila ruhusa yeyote na tatu kuiba gari la dokta na kutoroka nalo,

    “Mungu wangu itakuwaje sasa? Mungu saidia Gervas asinibadilikie!”

    Nilisali kimoyo moyo huku nikitetemeka kwani tayari mikono yangu ilikuwa imejaa jasho sana hivyo nikamshusha mtoto wangu ‘Jelly’ chini kisha nikaendelea kusikilizia itakuwaje.

    Mara nikashangaa wanampakiza Gervas kwenye Gari lile la polisi na kuondoka naye.

    Ilibaki kidogo niropoke kwa sauti, lakini roho ya kiujasiri ikanijaa na kunyamaza kimya huku nikimwamgalia Gervas akitokomea na lile gari, nikageuza kichwa na kubaki kumwangalia mwanangu pale chini.

    “Jelly Mwanangu! Jelly nakupendaeeh !mwaaah!”

    Ilinibidi nipotezee mawazo kwa mwanangu ‘Jelly’ kwani kiukweli mchozi ulikuwa karibu kunitoka.

    “Sasa jamani watakuwa wamempeleka wapi Gervas wangu....?”

    Nilizidi kuumia kila nikiwaza walivyomchukuwa Gervas, nikajikuta nachanganya juice kwenye uji wa Jelly.

    “Oooh...! My God...!, hii yote ni kwa ajili ya kumuwaza huyu Gervas wangu jamani aaah!”

    Nilikaa sina amani kuanzia asubuhi mpaka jioni huku nisielewe kama Gervas atakuwa wapi? Na atarudi saa ngapi?

    Ilipotimu usiku wa saa mbili nikaanza kuhisi kama mlio wa gari nje,sikutaka kuchungulia wala nini, haraka haraka nikamweka kwenye kitanda chake mwanangu vizuri kisha nikaenda hadi sebuleni nikahakikisha milango yote imefungwa, Nikarudi chumbani nakujifunika shuka tayari kwa kulala,huku nikiwa naendelea kusikiliza kwa mbaali sauti kutoka nje,

    Mara kimya kikatanda kwa muda halafu nikasikia sauti ya kiume inajibizana na mwanamke,

    “Umemwacha wapi? Humu ndani?”

    “Yupo humu ndani lakini Mama mi naomba muishi kwa amani tu, na Imani atakusaidia kwani amebadilika kwa sasa!”

    Haraka haraka fikra zangu zikanituma moja kwa moja atakuwa ni Gervas na Mama yake. Nikatoka nje kwenda kuwafungulia mlango

    “Ooh....! Mama Mamaa...!”

    Nilijigeuza nakujifanya mtoto huku nikimkumbatia Mama Gervas na mwanae Gervas akishuhudia kwa tabasamu kali, maskini najutia nilichomfanyia kwani mama Gervas sasa alikuwa hana tena uwezo wa kuona maishani mwake mwote, nikamshika mkono nakuingia naye ndani,

    “Levina na Gervas wanangu?”

    “Naam Mama, Abee Mama!”

    “Nawaombeni muishi pamoja milele kwani naamini mmetoka mbali mpaka kufikia hapa.

    Alikuwa akiongea Mama Gervas hadi akanifanya nitoe mchozi kwani mimi ndio niliowafanya wawe walemavu vile.

    “Gervas na Levina wanangu! Nawaombeni sana mnisamehe sitakuja kurudia tena maishani mwangu...!

    .....Tangu tukiwa Dar es salaam nilikuwa nikimchukia sana Levina na hadi kuna kipindi tuliposafiri kuja huku tukiwa hotelini pale Uholanzi, nilimwekea Levina ‘Upupu’ kwenye maji akawashwa mwili mzima mpaka asubuhi,’’

    “Mamaa...? Mamaaa....?”

    Gervas akaita kwa sauti ya juu huku mishipa ikimtoka kwa hasira.

    “Subiri nimalizie Gervas, haikuishha hapo tu kwani hata tulivyofika hapa bado niliendelea kumnyanyasa na kumtesa na hata lile suala la kukutwa na ‘hirizi’ chumbani kwako ni mimi ndio niliziweka ili wewe umfukuze Levina”

    “Ooooh! My God! Mama? Mama?”

    Gervas akaanza kulia kwa hasira hadi kunichochea na mimi kuanza kulia palepale

    “Mama mimi nimeshakusamehe na Gervas pia tulisha sameeheana na kwa sasa nawaombeni tuishi tu kwa amani na upendo!”

    Kuanzia hapo tukaanzisha maisha mapya huku mimi nikiwa karibu sana na watu watatu,

    Ilinilazimu nimhudumie Jelly, Gervas na Mama yake kwa kila kitu, niliteseka sana lakini ilinibidi kwani nilimpenda sana Gervas.

    Gervas hakuwa na kazi tena na Mama yake nilimsaidia kumuongoza kwa kila alichokuwa anakitaka.

    Siku moja nikamshauri Gervas turudi Tanzania kwani haya maisha tunayoendelea nayo yakutumia pesa bila kuingiza chochote ipo siku tutaishiwa hadi nauli ya kurudi kwetu Tanzania na hata tukirudi tutakuwa hatuna kitu,Tukakubaliana tufanye mpango tuondoke na kuelekea kwetu Tanzania.



    ~ BAADA YA MIEZI MIWILI ~







    Asubuhi na mapema nikiwa mimi na Mwanangu Jelly pamoja na Gervas ndani ya teksi tukielekea uwanja wa ndege wa 'Bay Bridge' pale Marlyland jimbo la Detroit, ndani ya masaa kama sita tulikuwa tumeshafika, tuliweza kukuta zile ndege za tripu fupi fupi nyingi zikiwa zinaelekea Canada, Mexico na hata nyingine afrika ya kusini,

    Lengo letu lilikuwa kupata ndege ya kwenda Afrika ya kusini then tukifika tutachukuwa basi nakula boda kwani kama tungepanda Ndege kubwa tungekamatwa kirahisi na mapolisi, hakukuwa na haja ya (kukata tiketi kabla ya safari) kufanya ‘Booking’ hivyo tiketi tulikatia pale pale na safari ya kuelekea Afrika ya kusini ikaanza.



    * * * * **





    Baridi kali lililokuwa linaeendelea katika jiji la 'Johhanesburg' lilifanya Gervas aendelee kuumia sana haswa upande wa magoti iliyokuwa na makovu yaliofanyiwa operesheni baada ya Mimi kumpiga risasi, huku mwanangu 'Jelly' nikimfunikia minguo mingi asipatwe na ubaridi kwa upande wa Mama Gervas tulimnunulia miwani mikubwa meusi aivae japo hakuweza kuona chochote zaidi ya kusikia tu tena kwa mbaali,

    Bila ya kupoteza muda tukatafuta sehemu ya kulala na kupata 'African sun Hotel' iliyokuwa umbali wa kama kilometa kumi kutokea uwanja wa ndege wa ‘Johhanesburg’ uitwao 'Tambo' ambapo ilitakiwa tulale na kesho yake safari ya kwenda nyumbani kwetu Tanzania.

    “Mama. Wewe itabidi tulale wote then Gervas atalala na Mwanangu Jelly!”

    Huwezi amini tulilala na Mama Gervas vizuri mpaka asubuhi, na kulipokucha tulipata basi la kutupeleka mpaka 'Harare Zimbabwe' huku tukiitafuta Zambia kwa kupitia boda ya 'Chirundu' kisha tukapapita 'Bulawayo' na baada ya hapo usiku sana tukapita nchi ya 'Botswana' pembezoni mwa feri ya 'kazungula' karibu na 'Livingstone.

    Lakini ilipofika alfajiri sana tukawa tunakaribia kufika Zambia. Kwa bahati nzuri tukakuta treni ya kuelekea Tanzania bado inanafasi tena kubwa sana hivyo tukakata tiketi na kuendelea na safari.

    Mpaka tunatoka nchi ya Zambia wote tulikuwa hoi, Gervas alichoka sana, mtoto wangu Jelly naye alikuwa kapitiwa na usingizi mzito,

    “Mama....! Mama.....! Mama.....! Gervas.....!”

    Nilianza kutetemeka huku nikiwa sijui nini kimemtokea Mama Gervas kwani nilipomvua miwani,macho yake yalikuwa yanatoa kitu kama usaa na alikuwa kalala huku kaachia mdomo wake wazi uliofanya harufu kali itoke kinywani mwake.

    “Mungu wangu.....! Mama.....! Mama.....!”

    Nikaendelea kumwamsha huku woga ukianza kunitawala kwani Gervas alikuwa bado kapitiwa na usingizi, halmashauri yangu ya kichwa ikafanya kazi fasta na kugundua kuwa nilisahau kumpa Mama Gervas zile dawa alizoandikiwa na Dokta ambazo huwa zinamsaidia kuzuia uchafu sana sana usaa au maji maji yasitoke machoni,

    “My God.....! Mungu saidia......!”

    Nikiwa bado natetemeka nisijue nini cha kufanya mara Gervas akashtuka kutoka usingizini.

    “Vipi Levina mbona upo hivyo.....?”

    “...Hapana Gervas....!”

    Nikamjibu kwa woga tena kwa kutetemeka huku nikimuangalia Mama yake kwa masikitiko makubwa.

    “Gervas.....?”

    “Eeeh....!, Unasemaje Levina wangu.....!”

    “.....Ujue Mama mpaka sasa hali yake siyo nzuri kabisaa....!”

    “Ni.....i.....i.....i......i......i......i......ni......?”



    ******







    “Kweli Gervas.., embu mwangalie Macho yake yalivyokuwa.....?”

    “Mama....? Mama....?”

    Gervas hakuamini hata kidogo alihakikisha kwa kumtingisha Mama yake pale mpaka abiria waliokuwa karibu yetu wote wakamshangaa pale.

    “Levina umemfanyaje tena Mama yangu....?”

    “Nielewe Gervas.., sijamfanya kitu chochote jamani....!”

    “Mbona haongei......?”

    “Ulimpa anywe dawa zake alizopewa na dokta.....?”

    “Hapana Gervas..., nilipitiwa na kujisahau kumpa....!”

    “Levinaaaaaaaaaaaaaaaa......? Unampenda kweli Mama yangu....?”

    Gervas sasa alikuwa ameshabadilika huku mishipa ya usoni mwake ikimkakamaa kwani ni kweli Mama Gervas anaweza akawa amekufa kwa hali ile aliyokuwa nayo pale,

    “Levina......! Ahsante kwa kuniulia Mama yangu.., ubarikiwe na Bwana.....!”

    “Nooo........!, Gervas usiseme hivyo.......!”

    “Au kwasababu ulimwona kipofu.....? Na mimi sijiwezi....? Haya niuwe na mimi sasa....? Niueeeee Levina si ndio ulivyokuwa unataka....?”

    Gervas hasira zilimjaa huku kwikwi ikimshika kwa uchungu mpaka kunifanya na mimi mchozi uanze kunidondoka, huku abiria wasijue nini kinaendelea pale,

    “Nilijua tu Levina siku moja utakuja kumuua Mama yangu......!”

    Treni bado ilikuwa katika kasi, abiria wengi walianza kusogea karibu kwenye siti zetu huku wakisikiliza majibizano kati yangu na Gervas kuhusu Mama yake huku Gervas akiwa kavimba uso kwa hasira kali aliyokuwa nayo.

    “Mama amka! Mama!”

    Gervas akawa bado haamini chochote kuhusu Mama yake, akamtingisha tena kwa mara ya pili kisha akamgusa eneo la kifuani japo asikie mapigo ya moyo bila mafanikio yoyote.

    “Mama kwanini umekufa Mama? Sina tena Mama! Aiyaaaaa.., Iyaaaaaaa.., Iyaaaaaaaa.., Iyaaaaaaaaa.....!”

    Gervas alizidi kulia kwa uchungu pale mpaka akadondoka kwenye kibaiskeli chake cha kubebea wagonjwa alichokuwa amekikalia kisha akaanza kugala gala pale chini huku watu wakimuwahi.

    “Niacheni....?, Nimesema niacheni....!, sina tena umuhimu na sababu ya kuendelea kuishi hapa Duniani.....!”

    “Nooooo......! Gervas Mme wangu usifanye hivyo......!”

    Tayari gervas akawa amechomoa bastola ya Askari Polisi wa treni aliyekuja kusuluhisha pale, haraka haraka Gervas akajinyoshea kichwani mwake huku akitaka kujiua pale pale nikamrukia na kumuwahi kuishika ile bastola..., kabla hajajiua, maskini ile namzuia tu nilipoishika ile bastola tayari mkono wa Gervas ukawa umenizidia nguvu na kufanya ile bastola kugeuka na kumfyatua mwanangu Jelly eneo la kichwani pale pale alipokuwa amesinzia,

    “Jelly Mwanangu? Jellllyyyyy”

    Nikamwacha Gervas na kumuwahi mwanangu na kumkumbatia, huku watu wote kwenye treni wakipiga makelele na Mapolisi wakawa tayari wamemuwahi Gervas na kumfunga pingu.

    Kutokana na kuchanganyikiwa kupita kiasi na kitendo cha kumshuhudia Gervas akiwa hatiani, Nikajikuta nimetoka na Mwanangu kupitia dirishani na kudondoka mpaka chini nikisalimiana na ardhi huku treni ikiendelea na safari kwa mwendo wa kasi sana..

    Nilibiringita sana huku nikiendelea kumkumbatia marehemu Mwanangu kwa nguvu zote huku kichwa chake kikimeguka vipande vipande baada ya kupigwa ile risasi na Gervas kwa bahati mbaya,Nadhani itakuwa kwa sababu kuwa na ubongo ambao hukukomaa vizuri ndio maana kuanzia usoni hakutamaniki.





    * * * * * *







    Nilibaki naitolea macho treni ambayo ilikuwa mwendo kasi ikitomekea huku nikiwa na machungu sana juu ya kufariki kwa mwanangu Jelly, mwili wangu wote na nguo zilikuwa zimejaa damu tapa tapa, maskini Jelly hakuwa na kichwa tena zaidi ya kumshuhudia akibakiwa na shingo peke yake kutokana na nilivyomshika vibaya kipindi nimebiringita kutoka kwenye ile treni,

    Ilikuwa ni jioni na eneo lile ambalo tayari tulikuwa tumeipita Zambia lakini sikujua vizuri yalikuwa ni maeneo gani, kwani kulikuwa kama jangwa hakukuwa na miti mingi zaidi ya kujaa michanga na vumbi tupu kutawala.

    "Kwaheri Mwanangu Jelly.....! Sijakuua mwanangu ni bahati mbaya imetokea, msamehe Gervas....! Ona sasa umekufa bila hata ya kumjua baba yako......!”

    Nilikuwa kama nimechanganyikiwa kwani nilimweka mwanangu chini huku nikifukua mchanga tayari kwa kumfukia Jelly wangu....,

    “Roho yanguuuuu.....! Na ikuimbieee.... Jinsi weewee.... Uliivyoo mkuuu.....!”

    Nilizidi kuchanganyikiwa hadi nikajikuta naimba nyimbo za dini huku nikiwa namweka Mwanangu ‘Jelly’ kwenye kashimo nilichokachimba kwa mikono na vijiti...

    “Jelly mwanangu.....! Pumzika kwa amani....”

    Nikamfukia na ule mchanga kisha nikatengeneza kakitu kama kamsalaba, nilipomaliza nikaondoka zangu,

    Baridi lilikuwa kali sana likanifanya nijikunyate sana huku nikitembea taratibu nisijue naelekea wapi? Giza nalo likaanza kutawala huku njaa ikinishika nisijue nini chakula....

    Hakika ni mateso juu ya mateso kwani sikutembea mwendo mrefu sana, nikakutana na kaeneo kama ka msitu kadogo pale pale nikachuma majani nakuyalaza kwa kuyapanga chini kisha nikajikunyata hivyo hivyo japo nipate usingizi, nilipata shida sana mpaka kuja kuupata usingizi, kwani baridi lilikuwa kali sana mpaka kunifanya mdomo kutetemeka huku kiu ya maji ikinishika lakini baada ya kama masaa mawili nikawa tayari nimeshapitiwa na usingizi na kitu kilichokuja kunishtua usiku sana ni baridi na upepo uliozidi kupita kiasi na sauti za ndege,Wanyama wakali eneo lile, mara nikaanza kuhisi kama kitu kinateleza miguuni mwangu huku kikiwa cha ubaridi, haraka haraka nikavuta majani nakupiga kelele,

    “Niaaaaache ukooooo.....?”

    Kisha nikakitolea macho ili kujua ni kitu gani....?

    “Oooooh Mungu wangu... Nakufaaaaa.....!”

    Alikuwa ni Fisi, yule mnyama anayeogopewa na kila mtu kwa kula mizoga,Na sasa tayari alikuwa ameukamata mguu wangu wa kulia kwa nguvu huku akiniburuta na wenzake wakiwa wananijalia lile eneo lile.

    Kitu kilichokuja kuniokoa pale ni 'Bundi' wale wa usiku ambao nao walijua mimi ni mzoga wakaja kwa dhumuni la kunila nyama, wale fisi wote wakakimbia na kujitanda kwa mbali huku wakinitazama.

    Ilikuwa ni rahisi sana kuwafukuza bundi kuliko ule umati wa fisi, ndani ya sekunde kadhaa bila hata ya kupata usingizi Levina mimi nikawa nimeshajiokoa lile eneo na kujikongoja moja kwa moja mpaka eneo la mbele kidogo huku njaa ikinizidia pamoja na usingizi mkali hivyo nikakata vimiti miti vidogo kisha nikapanda juu ya mti na kuvitandika na kupata usingizi.

    Ilipofika asubuhi njaa ilinizidia iliyochanganyika na kiu ya maji, lakini nikajipa moyo nikashuka pale mtini na kuendelea na safari yangu tena kwa kuitafuta ile njia ya reli..

    Nilitembea kwa muda mrefu jua lilitoka tena likawa kali sana,

    Kwa mwendo niliotembea nadhani inaweza kuwa kama siyo kilometa ishirini na tano au na saba hivi bila ya kukutana na mtu yeyote huko nilipotoka na tayari ilikuwa imeingia jioni kwani kale kaubaridi kalianza tena kunitawala mwilini mwangu,

    miguu ilinivimba sana huku jua likiwa limeninyong'onesha mwili wote na kuwa kama mtu aliyepigwa na ganzi.

    “Aaaah! Nimechoka sana!”

    Nikajikuta naongea peke yangu huku nimekaa chini ya mti na siwezi kuendelea tena na safari.

    Nikiwa bado nimetulia pale chini mara wakapita kinadada waliovalia nguo za kawaida tu lakini zile za kuisha isha wanazovaa watu wa vijijini mara nyingi huku wakiwa wamebebelea kama mitungi ya maji na wengine wakiwa na madebe mfano wa ndoo vichwani mwao,

    Hapo hapo halmashauri yangu ya kichwa ikafanya kazi fasta na kujua watakuwa wametoka au wanaelekea kisimani,

    “Ila mbona kama wanaongea kiswahili?”

    Walikuwa wakibishana kitu kwa lugha yetu ya kiswahili iliyochanganywa na lugha ambayo sikuielewa vizuri, hivyo wakanichochea hisia zangu akilini niweze kuachama mdomo wangu na kuwaita,

    “Jamani! Samahani!”

    Waliposikia sauti yangu waligeuka kuniangalia kisha kwa hofu zao wakadondosha chini ile mitungi yao ya maji na kukimbia walipotokea.

    “Busanso Afwa! Busanso Afwa!”

    Sikuwaelewa vizuri wanachoongea kwa sasa lakini ikanibidi niangalie nyuma yangu,hakuna kitu nikajiangalia na mimi mara mbili mbili,

    Maskini Levina mimi nilikuwa sitamaniki kwa zile nguo kwani damu nyingi ilikuwa imekaukia kwenye nguo huku nikionekana kupauka na kuchafuka sana kutokana na vumbi la maeneo yale,nikajua lazima waliniona kama mtu tofauti kwao, nilichokifanya nikuinuka pale na kuongoza moja kwa moja kuelekea ile njia waliokimbilia wale wadada.,

    Ilikuwa kagiza ndio kanaingia kwa mbaali huku nikiwa ndio naanza kuondoka pale mara nikasikia mlio kama wa treni unalia...

    Furaha ikanirudia moyoni nguvu zikanijaa kwa ghafla kwani ni kweli kwa mbaali saaaana, katikati mwa reli kulikuwa na taa kubwa zinawaka hivyo nikajua kama siyo majumba ya watu wanaishi huenda ile treni iliharibikia eneo lile hivyo nikazidisha nguvu na kukimbia mpaka maeneo ya karibu na pale.

    “Mungu wangu....! Ahsante sana.... Ahsante Baba....!”

    Nilisisimka mwili wote kwani ni kweli ilikuwa ni treni na pale palikuwa ni mpakani kabisa mwa Zambia na Malawi, giza tayari lilikuwa limeingia pale huku baadhi ya abiria wakiwa nje wengine ndani wakisubiri sijui ndio matengenezo au la...

    Nikawa tayari nimeshaifikia ile treni huku watu wengi wakiwa nje na wengine wakiwa ndani wanalalamika na kulaani kwa kitendo cha kuharibika ile treni..

    “Ona sasa na ile maiti ya yule mama aliouliwa na yule mdada itaozea humu humu ndani...Achana na hiyo maiti bado yule mlemavu naye miguu yake imeanza kutoa wadudu kama mafunza? Yani haya matreni kila mwaka hawayatengenezi vizuri!”

    Sauti za baadhi ya abiria waliokuwa wakiongea ndani ya ile treni walinifanya mchozi unitoke lakini nikajipa moyo wa kijasiri, hapo hapo na haraka haraka nikanyata na kujificha karibu na ile treni huku nikifikiria ni jinsi gani nitaingia mule ndani kwani walishanifahamu nilivyokimbia kupitia dirishani na tayari wanajua kama mimi ndio nimemuua Mama Gervas.

    Mara nikamuona mzee mmoja akiwa amevalia kofia nyeusi na koti akiwa anatafuta eneo akojoe akawa anasogelea eneo nililopo,

    Mungu wangu nikamshuhudia akifungua zipu yake na kuanza kunikojolea usoni bila ya yeye kujua lolote kama kuna mtu pale chini. Hasira zikazidi kunipanda nikavuta jiwe kubwa kisha nikainuka na kumuwahi mdomo, pale pale kabla hajaongea chochote nikampiga na lile jiwe utosini mwake kama mara mbili akawa amekufa,nikamburuta kwenye giza sana nakuanza kumvua lile koti lake na kumfunikia halafu nikamvua ile shati yake ya ndani pamoja na suruali yake nikavivaa kisha nikachukua kofia yake nakuigeuza nje ndani na kuivaa kujifunika sura yangu nikawa si Levina tena unayemjua.

    Nikajitokeza kwenye mwanga nje ya ile treni bila woga wowote huku nikilitafua behewa alilokuwa amepanda Gervas.

    “Nakumbuka kama ilikuwa ni H. 03 au 04”

    Lakini kabla sijalifikia nikasikia sauti ya mdada ananiita nyuma yangu..

    “We dadaaah! We dadaaah!?”

    Nikageuka kumuangalia, sikuweza kumfahamu hata kidogo hivyo nikamuuliza kwa kujiamini zaidi.

    “...Unasemaje...?”

    “Baba yangu alikuwa hapa hapa nje yuko wapi? Hizi nguo zake na hiyo ni kofia yake yuko wapi? Si nakuuliza wewe?”

    Alikuwa akiongea kwa sauti kubwa tena kwa uchungu na hasira huku nikibaki namwangalia tu, akanipiga kofi kwa nguvu likafanya watu wote kwenye treni wanitolee macho huku ile kofia ikinidondoka chini.

    “Haaaa...! Hujafa...? Si wewe ndio uliomuu...”

    Maskini akawa ameshanitambua baada ya ile kofia kunidondoka na kuachia sura yangu iliojawa na makovu.

    Mara nikawaona askari kama Wanne tena ni wale wale wa treni wakiwa wanakuja kwa mbali eneo tulipokuwa na yule mdada.



    ********



    “Uhh...! uhh....! Uhh....! Uhh....! Uhh...!”

    Tayari kijasho chembamba kilikuwa kikinitoka pamoja na kuwa na kaubaridi pale chini ya mti nilipokuwa nimepitiwa na usingizi mzito baada ya wale wadada walipodondosha mitungi yao ya maji na kunikimbia,

    “Mungu wangu! Kwanini tena jamani naendelea kuziota hizi ndoto za mauaji mimi?”

    Nilijikuta nikiilaumu nafsi yangu kwani ni kweli nilikuwa nikiota ndoto za ajabu ajabu, Eti nimeliona treni limeharibika mpaka nikamuua Mzee wa watu na kumvua nguo na kuzivaa mbaya zaidi eti nikaota nimekamatwa na yule mtoto wa huyo Mzee Mhhh!,

    “Eeeh mwenyezi Mungu niondolee ndoto chafu hizi zisiniandame tena....?”

    Nikasali kimoyomoyo kisha nikainuka pale chini ya ule mti niliokuwa nimepitiwa na usingizi kisha nikaenda hadi pale wadada walipondondosha ile mitungi yao ya maji na kuanza kukombeleza japo niweze kupata vijimaji kidogo.

    Jua la Asubuhi likiwa tayari limeshachomoza kabisa na mpaka kufikia leo nilikuwa natimiza siku ya pili bila kupata chochote tumboni zaidi ya hivi vijimaji.

    Nilikuwa sina jinsi yoyote zaidi ya kuendelea na safari huku nikiwa sijitambui ninapoelekea,Nilitembea tena umbali wa kama kilometa sita hivi ndipo nilipokutana na vinyumba vidogo vidogo.

    Furaha ikanijaa zaidi moyoni mwangu pale nilipowaona watu.

    “...Wale wadada walionikimbia kulee, mmoja wapo yulee ngoja nimuwahi nimuulize kitu!”

    Nikatembea fasta mpaka alipo na nikajua tu hajui Kiswahili wala Kiingereza kwa hiyo hapa nikutumia njia ya vitendo atanielewa,

    Safari hii yule dada hakuonesha woga wowote akanipeleka mpaka nyumbani kwao nikakutana na wazazi wao wakanipokea vizuri tu huku wakiongea wenyewe kwa lugha yao.

    “Lengula... Pela ine.....!”

    “Isa kuno....!”

    Yule mzee akatoka nje na kurudi na wazee wenzake wakiwa na shauku ya kutaka kunijua kiundani zaidi.

    “Lengula Mweni.....!”

    “Pela ine Cilyo!”

    Mara nikashangaa wameleta chakula pamoja na kombe kubwa la maji hivyo nikaanza kuambulia maneno nikajua

    “Kumbe 'Cilyo' inamaana ya chakula!”

    Sikukiweza kula kile chakula kwani ilikuwa kama maugali ugali ambayo hayajaiva vizuri yaliyochanganywa na mimboga ya majani iliyoungwa ovyo ovyo tu, sema kutokana na njaa ya siku mbili niliyokuwa nayo,nilijikuta nafakamia hivyo hivyo na kushushia na yale maji..

    “Naomba niongezeni tena maji ya kunywa....”

    Huku nikioneshea kwa vitendo kuwa nahitaji niongezewe maji,

    “Pela ine I majie!”

    Yule Mzee akamuamlisha mtoto wake aniletee, aliponiletea nikayanywa kisha nikamsikia akimtuma tena kwa mara ya pili yule mtoto.

    “Ya Na Ubwite Bane Nsansa”

    Akatoka halafu baada ya muda akarudi na Dada mmoja mweupe aliyeonekana kama mtu tofauti na wao kuanzia mavazi hadi nywele zake alivyozitengeneza,

    “How are you....?”

    “Am fine., who are u....?”

    Nikajua nimeshapata mtetezi wangu kuwa yule dada alikuwa akijua Kiingereza lakini nilijiuliza sana ametokea wapi na amejuaje kiingereza maeneo haya, Nilijiuliza mara mbili mbili bila ya kupata jibu,

    “Where are u came from?”

    “Am from South Africa to Tanzania..!”

    Nikamdanganya huku nikiangalia kwa pembeni kwani woga na aibu vilikuwa vimeshakuwa vimenitanda mule ndani huku wale wazee wakitusikiliza kwa ukaribu japokuwa hawakujua chochote pale.

    “Are u Tanzanian....?”

    “Yes of course...”

    "Waaaooh...! Do u knw how to speak swahili language.....?”

    “Ndio.....”

    Nikamjibu kwa Kiswahili mpaka akashangaa na hakuweza kuamini ndipo nilipoanza kujitambua kuanzia sehemu niliyopo.

    “Hapa tupo kusini Magharibi mwa Zambia na siyo mbali sana na mpakani mwa Malawi”

    “Ulisema unaitwa nani...?”

    " Brendah BreBre...."

    Nikamdanganya nikijua kuwa siku akijua kuwa naitwa Levina inaweza ikaleta matatizo yoyote.

    “Unaskia Brendah...”

    “Abee...!”

    “....Hiki kijiji kinaitwa 'Nakonde' ni maarufu sana hapa Zambia na hizi lugha wanazoongea huku ni ki 'Bemba' na ki, 'Njanja' ndicho wanachozungumza sana lakini ki 'Bemba' ndicho tunachozungumza sana,na nadhani umeshakisikia kabla sijaingia hapa...”

    “Happy..., Nafurahi sana kukufahamu....!”

    “Hata mimi nafurahi sana Brendah...!”

    Baada ya pale tukakumbatiana na kutoka na huyo dada anayeitwa 'Happy' na kuongozana naye mpaka kwenye kijumba chao,



    **********



    Jioni ilikuwa imeshatimia huku nakajua nako kakitaka kuzama, Nikiwa tayari na ninayemwamini ni mtetezi wangu, nilipewa maji ya kuoga nikajisafisha damu zote zilizogandia mwilini na baada ya hapo alinipa nguo zake nivae kisha akanipa chakula cha usiku,

    “Kwahiyo Happy...?unasoma au....?”

    “Hapana Brendah, Mimi nafanya kazi kulee 'Custom' (Mpakani) Mwa Zambia na Malawi tena ni mbali kidogo na hapa huwa nakuja kuchukuliwa na Gari asubuhi sana...!”

    huku tukiendelea kupiga naye stori nyingi za maisha huku zangu nikizificha ficha asizijue hata kidogo,Ilipotimia tena muda wa kulala alinipa shuka na kulala naye katika kitanda chake.

    Kwa mara nyingine nikafurahia maisha kwani ilipofika asubuhi niliamka kwa furaha zote huku mwili wangu ukisisimka mara kwa mara nadhani ni kutojiamini na mazingira niliyokuwa nayo,

    Nilivyoamka sikumkuta Happy bali niliambulia kikaratasi kilichoandikwa ujumbe pembeni yangu,

    Nikakichukuwa na kukisoma.

    “NAELEKEA OFISINI SAMAHANI SANA BRENDAH KWA KUTOKUAGA.,NISINGEWEZA KUKUAMSHA LAKINI USIHOFU MCHANA NITARUDI TUTAKUWA PAMOJA..UTAJIPIKIA CHAKULA NA MTAKULA HAPO NYUMBANI.

    Wako Mpendwa HAPPY.’

    Nilipomaliza kusoma nilijikuta nasisimka mara mbili mbili, Nikatoka nje na kukata mjiti kisha nikachukuwa kikombe cha maji nakuanza kupiga mswaki.



    ***********



    Kama kawaida yangu nilipomaliza nikaingia jikoni na kutengeneza chai ya rangi kisha nikaingia tena chumbani kupumzisha akili,

    Mwili wangu sasa ulikuwa umechangamka japokuwa akili haikuwa sawa hata kidogo kwani nilikuwa njia panda kwa vitu viwili, kwanza ni mawasiliano ya wazazi wangu na hofu kubwa ikiwa kama Gervas akienda kumwambia Mama kuwa mimi ndio niliyemuua Mama yake wakati sivyo, pili ni hatma yangu ya kukaa hapa,

    “Nitakaa mpaka lini hapa?”

    Hilo swali ndilo linalonisumbua sana kichwa changu haswaa.

    Nikiwa pale chumbani kwa Happy nikizubaa huku nakagua huku na kule nikaiona albamu ya picha zake nikavuta na kuanza kuziangalia moja moja,

    “Daaah kumbe Happy alishaolewa? Natamani na mimi ningekuwa nimefunga ndoa?”

    Nilizidi kujiumiza sana moyoni, nikaona ile albamu haina tena umuhimu kwangu nikaitupia pembeni na kuanza kupekua pekua mule ndani japo nimjue Happy kiundani zaidi.

    “...Waaaooh....! Mungu mkubwa kumbe anasimu ya akiba....”

    Sikuweza kuamini mara moja kwani ni kweli nilishuhudia simu ya ku 'slide' aina ya nokia n95, Haraka haraka nikaiwasha nakuanza kupiga namba ya 'Jammy' anayeishi na mama yangu Tanzania,

    “....Nakumbuka ni +255713133633 au na 4 mwishoni kama sikosei....”

    Nikapiga lakini ikawa haipatikani, Nkarudia mara mbili mbili bado ikawa vile vile, Nikajikuta nimelegea na nguvu kuniisha haraka haraka halmashauri yangu ikafanya kazi fasta nikafungua sehemu ya ‘internate’ ili nimtafute Jammy kupitia mtandao wa kijamii wa ‘facebook’,

    “Oooh... My God..! Why!!! Why!!! Why???”

    Maskini simu ikakatika chaji nikabaki natafuta sehemu ya kuchajia lakini pale hakukuwa na chaji ya kuchajia japokuwa palikuwa na umeme ule wa Jua,kwahiyo ikanibidi niiweke simu pembeni na kupumzika.

    “Brendah.... Brendah..... Brendah.....!”

    “Ooooh....! Happy....!”

    Alikuwa ni Happy amerudi toka ofisini na ndiye aliyeniamsha kutoka usingizini pale.

    “Amka mpendwa...! Vipi ushakula....?”

    “Hapana Happy..., Nilikunywa chai tu nikatengeneza na mihogo kidogo nikala ile asubuhi nimeshiba sana tu mpaka sasa”

    “Ngoja nibadili nguo basi niingie jikoni nipike fasta fasta.....!”

    “Hapana wala usijisumbue Happy mwenzako nimeshiba kweli ile mihogo na chai...”

    Akabadilisha nguo zake za ofisini na kuvaa za kawaida lakini swala la kupika akawa ameshaghairi tena kupika kwani kiukweli nilikuwa nimeshiba sana.

    “Leo nina habari njema kwako Brendah!”

    “Ipi tena hiyo Happy?”

    “kutoka ofisini ninapofanyia kazi!”

    Nilihisi kama moyo unataka kupasuka kwa furaha ya ajabu niliyokuwa nayo,

    “Eenhh...Nimejaribu kuongea na mchumba wangu wa zamani ambaye tunafanya naye kazi 'custom' (mpakani) na amekukubali kuwa mwanzoni mwa mwezi ujao ujiandae uanze kazi”

    “Kazi gani tena hiyo jamani!”

    “Brendah,ni kazi nzuri na ya kawaida mojawapo ni ya upishi pale ofisini au u 'mesenja' kwakuwa unajua kiingereza itakufaa sana”,

    “Ni sawa ahsante sana Happy kwa kuonesha unanijali kama rafiki wa karibu....”

    “Usijali Brendah na ukijituma zaidi unaweza ukabadilishwa kitengo na kupewa chochote kikubwa pale ofisini!”

    Nilijihisi si mtu wa mikosi tena bali ni mwenye bahati ile ya mtende,

    Niliishi na Happy vizuri sana kama ndugu na rafiki yangu wa karibu,alikuwa akiishi peke yake lakini majirani waliokuwa wamemzunguka aliishi nao vizuri kama ndugu na ndicho kitu nilichojifunza kutoka kwa Happy kuishi na jamii.





    ~ BAADA YA WIKI TATU~





    Siku ya kwenda kuanza kazi ilifika huku nikiwa sijulikani tena kwa jina la Levina pale mtaani bali ni Brendah BreBre,

    Ilikuwa ni asubuhi sana kwenye saa kumi na moja, Happy akiwa amenipa nguo zake za ziada za kazini, zilizonipendezesha mwili wangu vizuri na ka mwili kidoogo kalikuwa kanaanza kurudi, kichwani nywele zilianza kuniota kwa mbaali hivyo nikazichana huku yale makovu yakinipungua mwilini kwa kuweka poda nyingi na mdomo wangu nikiupendezesha kwa kuupaka lipsi ya rangi ya pinki na mguuni nikivalia kiatu si kirefu sana, kiukweli ni muda mrefu sikuvaa hivi vitu hivyo ikanifanya nijione tofauti na hata mwenyewe Happy anione mtu tofauti.

    “Brendah.,kiukweli umependezaa!”

    “Ahsante happy”

    Tayari mlio wa honi ulikuwa ukipigwa kutokea nje ukiashiria gari limeshafika.

    “Brendah si upo tayari!”

    “Tayari nakusikiliza wewe tu!”

    “Haya twende zetu gari ndo hiyo imeshafika”

    Tukatoka nje huku nikijiweka vizuri nguo yangu, nakuingia ndani ya gari tayari kwa kuanza safari

    Furaha ilinizidi na kusababisha mwili wangu kunisisimka mara kwa mara huku tukipiga story na kujiona kama vile ni ndoto lakini ilikuwa ni kweli kabisa.

    “Mnama...!, Huyu hapa ni rafiki yangu na ni kama ndugu yangu anaitwa Brendah niliyokuambia kipindi cha nyuma, Anaenda kuanza kazi na sisi leo!”

    “Aaaa ahaa! Brendah!”

    “Nafurahi kusikia kuwa tupo pamoja mrembo!”

    Aliongea kwa utani yule dereva 'Mnama' aliyeonesha kuwa mcheshi sana huku akiendelea kuendesha gari.

    Ilituchukuwa kama lisaa moja na nusu kufika pale custom (mpakani) mwa Zambia na Malawi (LUBA), wafanyakazi walikuwa wamevalia sare za nyeusi na nyeupe kama niliokuwa nimevalia,

    "Haya Brendah hapa ndipo kazini kwetu na mpaka uko upande ulee!"

    Tuliposhuka tu Happy akawa ananionesha mazingira ya pale huku tukiwa tunaelekea kwenye nyumba ambazo zimekaa kama ofisi zipo tatu tukaingia mojawapo kisha happy akagonga hodi..

    Tulipoingia tu ndani tukamkuta Bosi wa lile eneo keshafika hivyo bila kupoteza mda Happy akaongea naye.

    “Poka lunda Kumbwa....!”

    “....Imimonokele..,Pela ine Brendah....!”

    Akiwa bado Happy anaendelea kuongea na Bosi huku woga ukiwa bado umenijaa na hofu kubwa ikinitanda kutokana na kutojiamini kwamba ndio naelekea kufanya kazi kweli.

    "Sanguka Brendah!”

    Sikumwelewa Bosi anachosema mpaka Happy aliponielewesha kwa 'Sanguka' inamaanisha karibu kwa ki 'Bemba'.





    ¤ ¤ ¤ ¤ ¤ ¤





    Ndani ya masaa kama mawili nikawa tayari nimeshazoea mazingira ya pale na kitengo kikubwa nilichokuwa nimepangiwa ni u 'Mesenja' na siyo tena usafi kama ilivyotakiwa hapo mwanzo,

    Nilifanya kazi kwa kujituma zaidi huku malengo yangu nikiyatuliza akilini mwangu,

    Ilipokaribia muda wa mchana Bosi akawa ametoka na hapo hapo nikapata mwanya wa kuingia tena ofisini mwake nikafunga mlango kwa ufunguo haraka haraka nikaiwahi ile simu ya mezani na kuanza kupiga simu nyumbani,

    “Yes! Inaita! Inaita! Uhh! Thanx God!”

    “Hallow....! Hallow....!”

    Sauti ya kike ikapokea haraka haraka nikajua tu si mwingine atakuwa ni 'Jammy' tu.



    “Levina hapa anaongea, haya niambie fasta fasta mnaendeleaje huko?”

    "Wote wazima...? Mama mzima tu...! Tena tupo tunaishi na Gervas hapa nyumbani....!”

    “Whaaaat?”

    Nilishangaa kwa mshangao mpaka nikajikuta natetemeka na kizungu zungu kikanishika ghafla,

    Nikiwa bado najishangaa kwa ile simu mara nikasikia hodi inapigwa, Nikaanza kunyong'onyea huku nikihisi kama mkojo unajipenyeza kwenye zile sare zangu huku ukitaka kunitoka taratibu, Nikakata haraka ile simu na kuelekea mpaka kwenye mlango kuufungua taratibu huku nikiendelea kutetemeka,

    “Mhh Brendah....!

    Nilikuwa nakutafuta sana kumbe bado uko huku....?”

    “Nipo rafiki tu yangu, nimeachiwa kazi ya kupanga panga haya mafaili ndio namalizia....!”

    Nikamdanganya bila hata ya yeye kunigundua nilichokuwa nikikifanya huku nikishusha pumzi taratibu, Nikawa katika hali ya kawaida baada ya kuufungua ule mlango na kumkuta ni Happy.

    “Sasaaaa....! Muda umekwisha na gari ipo tayari twenzetu home....!”

    “Ok, Poa poa....!”

    Nikajiweka sawa sawa japokuwa sikuridhika kabisa kutomalizia maongezi yangu kwenye simu.

    Safari ya kuelekea nyumbani ikaanza na dereva wetu 'Mnama' akaturudisha, nilijitahidi sana kuonesha ninafuraha ili Happy asigundue chochote, Nikawa na story nyingi ndani ya gari mpaka kumfanya Dereva Mnama kucheka sana njia yote.



    ¤ ¤ ¤ ¤ ¤ ¤





    Hatimaye tulikuwa tumeshafika nyumbani, jua kali lilikuwa limetawala nikiwa mimi na Happy tukashuka ndani ya gari na kuongöza mpaka ndani kisha nikabadili nguo na kuelekea kuoga.

    Nilipotoka Happy naye akaenda kuoga na aliporudi nikaanza kumdodosa kwa maneno.

    “Happy hivi kuna simu kama niliona humu ndani jana?”

    “Aaaa haaa, Eeeh nimekumbuka Brendah si ya Nokia?”

    “Ndio!!”

    “Aaah...., Si unaona sa hivi natumia hii Samsung..., Ile situmii tena ipo tu”

    Akaingia kwenye droo na kunipatia.

    “Ooh! Thanx sana Happy!”

    Nilimshukuru sana na kumkumbatia nikionesha upendo wa hali ya juu kwake”

    “Lakini hapa huwa hakuna sehemu ya kuchaji mpaka ofisini ndio huwa nachaji simu zangu kwa hiyo kesho tukienda uikumbuke twende nayo!”

    Nilifurahi sana kupata simu huku nikitamani usiku ufike mapema na kukuchwe fasta ili niweze kufika ofisini nikiwa akili yangu yote nikiielekezea ofisini.

    “Mhh...! Jammy kanitisha kweli kwenye simu., Sasa imekuwaje tena Gervas aishi nyumbani kwetu?”

    Hilo ni kati ya maswali yaliokuwa yakiniumiza sana kichwa usiku kuchwa bila hata kupata lepe la usingizi huku nikiwa sijui nini kimetokea na kinachoendelea nyumbani.





    ¤ ¤ ¤ ¤ ¤ ¤ ¤



    Alfajiri tulivu ilikuwa imeshafika huku nikiwa nafuraha, safari hii nilijikuta naamka mapema na kumuamsha Happy aweze kujiandaa.

    “Haya Happy! Happy Amka kumekucha mpendwa! Amka mtu wangu!”

    Ndani ya dakika chache akawa kesha amka,

    Nikaanza kuandaa nguo za kuvaa na kitu cha kwanza kabisa kukumbuka ilikuwa ni simu niliyoachiwa na Happy na kuipaki vizuri kwenye kibegi changu na kuingia bafuni.

    Safari ya kuelekea ofisini ilikuwa imeshawadia huku nikiwa mstari wa mbele kuwahi ofisini pale baada ya kushuka tu.

    Breki ya kwanza ilikuwa ni kajumba cha mlinzi ambacho huwa kanaifadhiwa mizigo ya watu wale wanaokuwa wamesafirisha vitu vyao kwa njia ya magendo.

    Haraka haraka nikaiweka chaji na kuelekea ofisini kwa Bosi tayari kwa kuanza kazi.

    Nilishangaa kumkuta bosi hajafika lakini hilo halikunipa wasiwasi wowote na hata hivyo safari hii sikuwa na hamu tena ya kutumia ile simu ya mezani kwani niliamini tu yangu itajaa chaji na nitaongea na nyumbani muda wowote baadaye..

    Nilipomaliza tu kupanga vizuri mafaili kwa Bosi haraka haraka nikatoka na kuelekea kuchukua simu kwenye chaji lakini kabla sijafika eneo lile nikamuona mtu kama Happy akiongea kutumia ile simu yangu niliyoicha kwenye chaji, Hofu ikanitawala tena, Bila kupoteza muda nikaongeza spidi huku nikimuwahi nisije umbuka, Lakini kabla sijamfikia nikahisi kama kuna mtu ananiita nyuma yangu,

    “Levinaaa....! Levinaaa....! Levinaaa....!

    Isa kuno....! Isa kuno....!”



    *********





    Nikajikuta nimedondoka chini huku nikiwa sijielewi kwa kile kilichotokea, Kwani nikiwa bado nipo pale chini huku nikiendelea kumuangalia Bosi, maara nikashangaa Mdada mmoja aliyevalia sare kama yangu akimfuata huku akiwa kashika mafaili mkononi.

    “Aahaa...! Uenda alikuwa anamuita yule Mdada anayeenda pale...!, Lakiiini....!, Mbona wakati anaita alikuwa ananitazama sana kama ananiita mimi....? Kwanza mimi siitwi Levina naitwa Brendah....!”

    Nilijisemea kimoyo moyo huku nikiinuka pale chini kwa ujasiri na ukakamavu wa hali ya juu na kuanza kumfuata Happy eneo alipokuwa.

    “Brendah vipi tena nikakuona umeanguka pale chini....?”

    “Hapana nilijikwaa tu jamani....!”

    “Pole sana angalia vizuri huku kuna kokoto nyingi!”

    Nilimsikiliza tu na kumjibu huku yale maneno yake yakipita sikio la huku nakutokea kule..,

    “Kumbe maskini, Happy alikuwa akitumia simu yake ya samsung kuongea na watu...!”

    Nikabaki nafsi inanishuta baada ya kuona kufuli kubwa pale kwenye mlango nilipoiacha simu yangu.

    “Happy..., huyu mlinzi yuko wapi....?”

    Nilimuuliza Happy kwa jazba huku nikiamini labda mlinzi anaweza hata akawa ameichukuwa ile simu.

    “Kwani nini Brendah....?”

    “Niliacha ile simu humu ndani kwenye chaji...!”

    “Basi atakuwa katoka kidogo lakini atakuwa maeneo haya haya wala usijali!”

    Happy akanijibu kisha akaondoka na kwenda kuendelea na kazi zake.

    Nilikaa pale pale nikimsubiri mlinzi mpaka pake alipokuja na haraka haraka nikaiwahi simu na kuiwasha kisha ndani ya sekunde kadhaa nikakutana na meseji kama tatu zote zikitokea kwa Jammy 'Tanzania.

    “UPO WAPI LEVINA...? FANYA HARAKA URUDI AU UTUME PESA SISI HALI ZETU MBAYA HUKU....!”

    Sikutaka kabisa kuiamini ile meseji zaidi ya kuifuta pale kisha nikanyanyua simu na kupiga.

    “Hallow Jammy....!”

    “Eeehh.., Levina...? Umepata meseji zangu....?”

    “Ndio nimezipata,uko na Gervas karibu....?”

    “Nipo naye ngoja nimpe simu uongee naye....!”

    “Haya nipe niongee naye....”

    “Hallow Gervas...?”

    “Levina Mpenzi wangu upo wapiiiiii....?”

    Nilijikuta machozi yakinitoka niliposikia sauti ya Gervas, ikanibidi nianze kuamini kuwa ninaye ongea naye ni Gervas.

    “Mimi nipo mzima tu mpenzi wangu Gervas, embu niambie ilikuwaje tangu nilipokuacha pale kwenye treni?”

    “Levina? Niliteseka na kuumia sana, tulipofika tu Tanzania huku bado nikiwa katika ulinzi mkali na wale mapolisi wa treni kwa kosa la kufyatua risasi ndani ya treni, tukapitia hospitali kwa ajili ya uchunguzi juu ya kifo cha Mama yangu., Ikajulikana kuwa alikufa kwa maumivu makali ya kutokuzingatia dozi za dawa alizopewa, Ndipo nikaachiwa huru kwa matatizo yaliyonikuta,

    Nikauleta mwili wake mpaka nyumbani, hivyo tumemzika na sasa mi nimebaki Yatimaaaaa! Yatimaa, yatimaa Levina....? Sina Mama wala Baba....!”

    “Pole sana Gervas kwa yaliyokukuta....!”

    “Levina. Hapa nilipo sina hata pesa niliibiwa zote kwenye treni, sina kazi na mtetezi wangu aliyebaki ni rafiki yako Jammy...”

    “Mama yangu yuko wapi....?”

    “Mama yako yupo na hawezi hata kuongea zaidi ya kutoa macho muda wote, Lakini naye amepooza mwili wote, Na mimi sasa naelekea kufa kwani miguu yote imeshaoza na inatoa funza wale wakubwa, Jammy kila siku ananiosha na kunipaka dawa lakini haisaidii naendelea kunuka tu, Jammy ni kila kitu yeye ndiye anayemuhudumia Mama yako kwa kila kitu hata pale anapojisaidia hapo hapo, Na yeye hana kazi ila tunaishi kwa misaada ya watu, Tena wengine wameshatuchoka, Nanuka tu Levina, Nanuka mimi Gervas...? Kuna kipindi nilitaka kujiua lakini Jammy ndiye aliyeniona na kuniokoa.”

    Nilikata simu kwa hasira, kisha nikaibamiza chini kwa huku nikielekea ofisini kwa bosi nikiwa na akili tofauti...



    *********



    “What's wrong wit u Brendah....?”

    Nilipoingia tu nikakutana na maswali kutoka kwa Bosi,

    ‘’Nothin.....!’

    Nikamjibu kioga huku nikijiuma uma na kuonesha kuchanganyikiwa fulani,

    ‘’Brendah..? I love u...!’’

    Sikumshangaa hata siku moja Bosi wetu tangu nimeanza kazi hapa alikuwa akinitaka kimapenzi nikawa namkatalia,

    Nikatoka zangu nje na kuzunguka zunguka huku na kule huku nikiwa sijielewi elewi kutokana na hali ya nyumbani.

    ‘’Brendah...?, Unafanya nini tena hapa.....?’’

    Ilikuwa ni sauti ya Happy akiniinua kutoka pale chini nilipokuwa nimekaa huku miguu ikinilegea na kukosa nguvu kabisa.

    ‘’Happy...., Nashindwa kujielewa kabisa yani......!’’

    ‘’kwani vipi....?, Embu niambie imekuaje tena.....?’’

    ‘’Ni ile simu yako Happy....?’’

    ‘’Imefanyaje tena....?’’

    ‘’Nimejikuta kwa bahati mbaya nimeidondosha na kuharibika papo hapo..., Ona sasa ilivyokuwa.....’’

    Nikamuonesha simu yake ilivyokuwa huku nikamdanganya Happy ili asiweze kujua ukweli wowote kuwa ninachowaza ni nyumbani..,

    ‘’Pole...Na wala hata usiwaze Brendah.., Tutanunua nyingine kwa muda utumie....!’’

    Nikarudi katika hali yangu ya uchangamfu kasha nikaendelea na kazi kama kawaida.





    *****************



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog