Simulizi : Sitaki Tena
Sehemu Ya Tatu (3)
Ilipoishia jana..
Kila nikimwangalia pembeni yangu ndivyo hasira ilinizidi kuninyemelea akilini mwangu kwakuwa nilikuwa sina nguvu tena upande mmoja kwa kupooza nilijikuta naropoka kwa sauti ya chinichini bila yeye kusikia.
“Unabahati sana nimepooza...kwani ilikuwa ni safari yako sa hivi...”
Kisha nikajiegemeza taratibu kutafuta tena usingizi,
Songa nayo sasa…
Baada kama ya nusu saa usingizi ukawa umenipitia na kilichokuja kunishtua ni Mkojo uliokuwa umenibana ukiambatana na haja kubwa pia nilikuwa najisikia kizungu zungu sana huku kichefuchefu kikinishika niliweza kumwamsha Mama na kumuelezea ikabidi amuite Nesi....,
Alitoka na kwenda mbio na kumuita Nesi, Punde akarudi naye,
“Hata kama naumwa....,lazima nikumalize..., Mmbeya mkubwa wee...!”
Niliongea taratibu na kuachia fyonyo kali huku nikimwacha yule Nesi pamoja na Mama wakishtuka na kushangaa wasielewe imekuwaje pale,
kilichofuatwa yule Nesi alichukuwa kibaiskeli cha kupakizia wagonjwa na kunichukuwa tukatoka wote kwa pamoja na Mama lakini tulipofika mlango wa chooni nilimsikia yule Nesi akimwambia kitu Mama...
“Mama...! Mama....! wewe usisumbuke huyu wacha niingie naye nimhudumie mimi tu..!”
“Hapana Mama twende wote...!”
“Levina acha ubishi..! Hata huyo atakusaidia tu kama mimi..!”
Nilimbishia Mama kwani niliamini kabisa yule Nesi tayari alikuwa ni adui yangu na anaweza kunidhuru.
Basi tukaingia chooni kisha yule Nesi akafunga mlango kwa ndani kwa kutumia ufunguo huku tukimuacha Mama nje akitusubiria.
“Wewe muuaji upo..? !...Umetoka gerezani lini..?”
Alianza kuongea kwa dharau huku akinibenulia mdomo wake lakini mimi
Nilikaa kimya huku nikimwangalia yule Nesi akichomoa dripu ili aweze kuniinamisha choöni niweze kujisaidia…
“.....Kama uko gerezani walikuacha leo mi sikuachi......!”
“....kwani nimefanyaje...?”
“…Ssshhhh...! We si Levina yule muuaji aliyewekwa gerezani miaka kama sita au saba iliyopita...?”
“Aaaahhh....! Aaaaaahh....!
Si...o..o..o.. mi..m..i..”
Nilimjibu kwa kujiuma uma kisha nikashangaa kitendo kilichofanyika pale kwani alichukuwa kichwa changu akaniinamisha kwenye tundu la choo tena kile choo cha kuflashi kwa mda mrefu.
Nilishindwa kuongea chochote kwani sura yote ilikuwa imeinama kwenye tundu la choo, sikuwa na nguvu kwani upande wangu mmoja ulikuwa umeshapooza,kwa lile tukio nilijikuta natoa haja kubwa na ndogo papo hapo...
“Nyoooooo...! Ushajinyea enhh..? Maana harufu ya kinyesi chako kishaanza kunuka tena sanaaaaaa.”
Aliongea kwa sauti ya chini chini ambayo mtu yeyote hawezi kuisikia kisha akanivua nguo yangu ya ndani ambayo ilikuwa tayari na kinyesi na kuitupia kwenye tundu la chooni likawa limetapakaa kile kinyesi changu kisha kabla hajaflashi akinikamata shingo tena kwa nguvu na kuniinamisha tena kwa mara ya pili chooni, maskini Levina mimi nilijikuta nakutana na kinyesi changu,huku nikikosa pumzi nilijikuta naachia mdomo wazi hivyo mdomo wangu ukakutana na kinyesi changu mwenyewe,nilikuwa sina jinsi zaidi ya kujikuta nikikimeza,
Alinifanya atakavyo kisha akaflashi kile choo huku kichwa changu kikiwa bado mule ndani ya choo,nilitapika sana,maskio yaliziba kwa mda na macho yakawa kama kipofu kwani sikuweza tena kuona mbele kwa mda ule zaidi ya kuhisi bado nimekabwa shingoni,
“bado hujafa tu....!”
“Utakufa wewe......! Sio mimi....!”
Nilimjibu kwa hasira ya hali ya juu huku nikizidi kumchochea na kumjaza hasira tena yule Nesi akiendelea kunitolea mimacho.
“..Unajifanya mbishi enh...? ...Hapa nakutoa maiti tu nampa Mama yako akakuzike muuaji mkubwa wee..."
Ghafla nikamshuhudia yule Nesi akiingiza mkono kwenye mfuko wa gauni lake na kuchomoa vile Visu vidogo vikali vya kufanyia operesheni na kuanza kukata kata mirija ya ile dripu ikaanza kuvuja kisha akaniangalia usoni,
“embu niambie wewe Muuaji nikuanze wapi...? Halafu uanze kusali sala zako za mwisho hapahapa...!”
“Tuuuhhh.....! Tuuuuhh...! Nikamtemea mate usoni mwake kwani nilikuwa sina nguvu za kumpiga, akakasiria na kunitoa kwenye kile kigari.
“Haya simama tupigane sasa...! Simama wewee..!”
Alinitoa kwenye kibaiskeli kile cha wagonjwa akinitaka nisimame, Sikuweza kusimama kwakuwa nilipooza upande mmoja hivyo nikadondoka moja kwa moja mpaka chini huku nikiwa uchi wa mnyama.
Alichoanza kukifanya ni kuchukuwa miguu yangu miwili na kuitanua,kisha akiwa kashikilia viwembe vyake tayari alikuwa amenishika matiti yangu na kutaka kuyakatakata.
Akiwa anataka kunikatakata na vile viwembe mara Mama akaanza kugongo hodi kwa nje.
“Nesi...! Nesi...! Nesi...!Bado hamjamaliza tu..! Levina....! Levina...! Levina....! Mwanangu...!”
Nilitamani niitike lakini tayari vile viwembe vilikuwa mdomoni mwangu,
“ole wako uitike...! Nakuchana chana sasa hivi..!”
*********
“....Namvalisha Mama tunatoka sasa hivi...!”
Aliongea kinafiki yule Nesi huku akinivalisha haraka haraka kisha vile viwembe akavitupa kwenye tundu la choo naku ‘flashi..’
Alinitoa pale nikiwa sijielewi ila ninachoweza ni kutoa macho na kusikia sauti kwa mbaaali sana, huku yule Nesi akinikokota na Mama mpaka wodi yangu wakanilaza,
Baada ya muda kidogo nikaanza kusikia sauti kwa mbali ya minong'ono nilihisi tu atakuwa ni Mama na Nesi wakizungumza.
“Yani Mama, mtoto wako alinisumbua sana kule chooni..! Haswa pale alipohtaji kujisaidia kwani ilikuwa ndo mara yake ya kwanza ndo mana tukawa tumechelewa kutoka..!"
“Usijali mwanangu...Ahsante kwa msaada wako Mungu atakubariki...Kaendelee na kazi tu...!”
Nilitamani niropoke pale pale lakini sikuweza kumuonesha wazi Mama kama namchukia sana huyu Nesi pia kwa vitendo alivyonifanyia.
Sikuweza kupata usingizi kabisa zaidi ya kutoa macho mpaka alfajiri kulipopambazuka na kumshuhudia Gervas akiwa mtu wa kwanza akiingia pale wodini.
“Shikamoo Mama..!”
“Marahaba mwanangu Mama na Baba umewaacha wazima..?”
“Wazima tu Mama”
Taratibu Gervas akaweka ule mfuko aliokuja nao ukiwa na chupa ya chai na ki hotpoti kidogo japo sikujua ndani yake kunanini.., kisha Gervas akanisogelea kitandani na kuongea na mimi huku akitokwa na machozi.
“vipi unajiskiaje Levina toka tulipokuacha...!”
Sikuweza kumjibu kwani sauti ilikauka nikabaki machozi yakinichururuzika mithili ya maji ya sabuni yakiteleza mwilini,
“Levina...! Levina....! Naomba japo nisikie sauti yako jamani...!”
Nilipenda sana nimuitikie Gervas nakuongea naye lakini ilishindikana kwani kitendo alichokuwa amenifanyia yule nesi kilinifanya nishindwe kufanya lolote.
~ NYUMBANI KWA KINA GERVAS ~
Wazazi wa Gervas hawakulala walifanya juu chini kuhakikisha Gervas anaondoka, mchana wa jana yake uleule waliotoka hospitalini walianza kufanya mipango na watu wa uhamiaji kwa ajili ya kumhangaikia pasipoti yeye Gervas na Baba yake,kwahiyo leo watachukuwa pasipoti zao na ndani ya siku mbili watakuwa wameshapata Viza ya kuingia Marekani.
Gervas alijitahidi sana kufanya kila liwezekanalo awe amemuweka Levina wazi lakini haikuwezekana kutokana na hali aliyomkuta nayo Levina.
~ HOSPITALINI ~
Kweli hujafa hujaumbika mpaka leo siku ya pili na sasa hivi jua linaelekea kuzama hakuna hata ndugu yeyote aliyekuja kunitembelea zaidi ya Gervas na Mke wa Afande Deus kuja kuniletea chakula.Nilijiona tangu matatizo yangu ya jela ukiongezea na haya yamenifanya nitengwe na ndugu mpaka baadhi ya Majirani.
“Kwanini ni mimi na mama yangu tu....! Kwanini wanatunyanyapaa kama wagonjwa wa ukimwi....?”
Hayo maswali niliojiuliza yalinifanya hata nishindwe kupata chakula kwani hasira iliniongezeka maradufu na kubaki namuangalia Mama huku mchozi ukinidondoka taratibu.
“Kula basi mwanangu upate nguvu....!”
Niliitikia kwa kutikisa kichwa nikimaanisha siwezi kula kwa mda ule lakini alinielewa.
“Kunywa basi angalau uji wa ulezi umechanganywa na maziwa ni mtamu sana mwanangu....!”
Nilikubali aninyweshe ule uji,nilikunywa japo taratibu sana,mara nikatapika uji wote,niliumia sana kwani Nilimuona yule Nesi mbaya wangu na ndio aliyenifanya nitapike,haraka haraka akaja.
“Ooohh...! Pole mgonjwa enhh...! Mama embu lete huo uji nimmnyweshe mwenyewe...!”
“Chukuwa mwanangu labda wewe kwakuwa Nesi atakubali kunywa bila hata kutapika....!”
Kila nilipotingisha kichwa nikionesha kukataa Mama hakunielewa, Akamkabidhi yule Nesi kibakuli cha uji kikiwa na kijiko aninyweshe.
“Nesi...! Nesi...! Ngoja niende uwani nikajisaidie, Nakuomba uendelee kumlisha huyu...
“....Usijali Mama....! Haya Levina kunywa uji basi...!”
Nilijikuta nakunywa ghafla nikamtapikia yule Nesi kwa makusudi huku akibaki kakunja sura yake.
“Unajifanya mjanja siyo....?”
Akaingia kwenye mfuko wa gauni lake na kuchomoa sindano kisha nikamuona akiichanganya kwenye kichupa kidogo kilichokuwa na dawa.
Nilikuwa niko tayari kwa lolote, Sikuweza kufanya chochote huku nikibaki nguvu zikizidi kuniishia.
“Haya chagua sasa nikuchome wapi wewe muuaji...!”
Nilibaki kimya, Mara nikasikia sauti...
“……nichome mimi tafadhali..!”
Alidakia yule mgonjwa aliyekuwa amelazwa pembeni yangu na yeye hakuwa na msaidizi nadhani alikuwa katoka au hayupo kabisa, lakini sikujua kwanini amesema vile.
“Huyo hana hatia...Njoo kwangu unichome nife...! Njoo...! Njoo...!”
Kabla hajamalizia kusema nilishuhudia yule Nesi akimrukia yule mgonjwa na kumchoma sindano ya shingoni halafu akamfunika mpaka usoni.
* * * *
Haikuchukuwa muda mrefu Mama akawa amerejea pale huku akimkuta yule Nesi anajiandaa kwa ajili ya kuondoka,
“Mgonjwa wako mwenyewe kagoma kunywa uji...!”
Akiwa anageuza na kuondoka zake yule Nesi mara...
“Nesi...! Nesi..! Nesi...!
“Samahani msaada pale kwenye kile kitanda yule mgonjwa pale anaonekana anatapatapa ‘Pliz’ kamsaidie Nesi....!”
Haraka haraka yule Nesi akamfata na kumshika kifuani kisha akafunika mwili wote.
“Hatunaye tena...! Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi Amina...!”
Aliongea yule Nesi huku akikimbia eneo lakutokea na baada ya mda nikamwona akirejea na wenzake huku wakibeba kitanda cha kubebea maiti wakaichukuwa ile maiti na kuondoka nayo.
“Maskini mimi Levina...Ilikuwa mimi ndio nife..!”
Nilijisemea kimoyomoyo huku nikimwangalia Mama yangu akimwaga mchozi kwa kumlilia yule mtu aliyekufa.
Niliogopa sana ilipofika usiku tena kila nikijifikiria kuhusiana na yule Nesi kwa jinsi alivyomkatili,
Hatimaye usiku ukawa, kwa kuhisi ingeweza kuwa imeshafika kwenye saa Nne kwani mama alianza kujikunyata kuashiria ananisubiria nilale naye apate japo kausingizi.
Nikiwa na mawazo tele huku nikimuangalia Mama akiwa kachoka sana nami nilijikuta napitiwa na usingizi., Kitu kilichokuja tena kunishtua usiku ule ni kama mtu niliyemhisi kama ananyata,niliogopa sana na kila nilipojitahidi kuvuta mkono wangu wa kulia japo Mama ashtuke haikuwa hivyo kwani Mama alikuwa amelala fofofo,yule mtu alipofika karibu yangu akaninong'oneza karibu na sikio langu la kulia.
“Nimekuja kukuua wewe...!”
“Hivi nimekufanya nini we Mwanamke...?”
Kwa mara nyingine nilijikuta sauti yangu imeweza kutoka.
Mara yule Nesi akavuta mto niliokuwa nimejiegemeza nao na kuuchukuwa kisha akanifunika usoni kwa nguvu akaniziba usoni huku akinibana kwa nguvu zake zote...
Nilijihisi vichomi mwili mzima vilivyoambatana na mafua ya ghafla kutokana na kukosa pumzi...Nilitapatapa japo upande mmoja ndo ulikuwa mzima, Nilitumia upande wa kulia ambao ulikuwa haujapooza,mpaka nikafanikiwa kudondosha dripu ndipo Mama akashtuka.
“Vipi tena Nesi...!”
“Hapana Mama namsaidia kumwekea dripu sawa kwani iliachia hivyo ikawa haitembei...!"
“...Ooohh Mungu wangu...! Ahsante sana Nesi kwani nilipitiwa na kausingizi kabisa, Nisamehe kwa hilo...!”
“...Usijali Mama na wala usiwe na wasiwasi nipo kwa ajili ya kazi hiyo...!”
Maneno waliokuwa wanaongea kati ya Mama na yule Nesi hayakuniingia akilini hata kidogo kwani baada ya Nesi tu kuondoka.
“Mama pliz...! Iwe isiwe..! Utake usitake...! Nakuomba asubuhi nirudi nyumbani hapa hakunifai Mama...! Nitakufa Mama sio kuzuri hapa kabisaa Mama...!”
~ SAFARI YA NYUMBANI ~
Alfajiri na Mapema Mama hakutaka kupoteza mda akafanya njia zote nikakubaliwa kutoka pale hospitali lakini ilinibidi nitoke na kigari cha wagonjwa na kwenda kumalizia kutibiwa nyumbani kwa kuwa nilikuwa nimepooza tu pia kuwa na gharama kubwa ambazo Mama asingeziweza nazo zilichangia mimi kutoka pale hospitali haraka...
Mama alikodi taxi yakutupeleka nyumbani na kabla hatujaingia maeneo ya nyumbani hofu ilianza kunitanda na kila nikimwangalia Mama naye alikuwa anatetemeka huku akifungua pochi na kumlipa dereva teksi shilingi elfu kumi….
“Mungu wangu nini tena hiki...”
“Kwani ni nini Mama..?”
“Levina....! Tumekwisha Levina....! Tumekwisha mwanangu...! Na hatuna mtetezi kwa hili tena...! .....Levina Mwananguuuuuuuuuu....!”
************
“Kwani ni nini Mama.?”
“Nyumba yetu imebomolewa mwanangu...! Ona sasa yani sisi ni watu wa mikosi tu kila siku...! Uuuuwii..! Uuuuuuwiii..! Levina tutaishi wapi tena Mwanangu..! Tutakuwa wageni wanani sisi...!”
Uchungu aliokuwa nao Mama ulinifanya na mimi niweze kutoa sauti lakini Dereva wa ile teksi alikuwa ameshatufikisha nyumbani hivyo kazi kubwa ilikuwa ni kunipakiza kwenye kibaiskeli cha wagonjwa alichopewa Mama pale hospitalini.
Ndani ya sekunde chache nikawa tayari mimeshashuswa na Mama ndio alikuwa akinikokota kuelekea nyumbani ambapo kulikuwa kumebomolewa vibaya,
kadri tulivyojuwa tunapasogelea nyumbani ndivyo akili na nguvu nikawa sina...tulipofika tu Mama aliniacha ghafla kisha akakimbilia ile sehemu kulipokuwa na kaburi la Baba ile marumaru iliyonakshiwa ikawa hamna tena,vumbi tupu ndo lilitawala eneo lile, Mara Mama akajilaza pale na kuanza kutapatapa pale.
“Ni nani aliyefanya hiivi....! Mamaaa.....! Mamaaaa....! Jamani nakufaaaaa....! Aiiyaaaa...! Uuuuuuh....!”
Nilijikuta nadondoka pale kutoka kwenye kibaiskeli na kuanza na mimi kutapata tapa tena kwa upande ule uliokuwa umepooza, Sikujihisi maumivu kwa mda ule... Nililia sana huku nywele zikinivurugika kwa kuchafuka na vumbi la pale chini.., Majirani walijitahidi japo kutuzuia lakini ilishindikana.., Mama akanivuta mkono kwa kuniburuza huku tukielekea sehemu kulipokuwa na kile kibaiskeli lakini kabla hatujafika pale ghafla
nilishangaa Mama akiniacha na kukimbia ndani kwenye ile nyumba yetu iliyokuwa haitamaniki kwa matofali yaliobaki bila kuwa na mpangilio, Nyufa tu ndo zilikuwa zikionekana huku paa likiwa kama linataka kupepea.. Akili na macho yangu yalikuwa kwa Mama nimuone amekimbilia nini mule., Nilijitahdi japo nitambae upande upande lakini haikuwezekana hivyo nikabaki natoa macho,nikamuona mama alipofika kwenye mlango akafungua pindo ya kanga yake haraka haraka na kuchomoa ufunguo kisha akafungua mlango mara nikashangaa akinikimbilia eneo nililopo.
“Pole mwanangu kwa kukuacha Mwenyewe....!”
“Usijali Mama nipo pamoja nawe...!”
“Nimechanganyikiwa mwanangu usinione hivi...!”
Akanipakiza kwenye kibaiskeli tayari kwa kuingia ndani.,nilisikitika hatukuwa na sebule tena zaidi ya vyumba viwili vilivyokuwa vimesalia,sikuweza kuona hata kijiko wala sahani mule ndani kwani hata upande wa jikoni sikuweza kuutambua vizuri wala upande wa kutokea na kuingilia.
******
“Kwanini nateseka hivi..? Nani wa kulaumiwa...?” Levina mimi mkosaji nisiye na hatia ndio nilikuwa nimeketi kwenye kibaiskeli cha wagonjwa chumbani huku nikiwa na mawazo yaliochanganyikana na maswali yasiyo na majibu.
“Lakiiiini...! Kumbe Kipindi chote ambacho afande Deus hakuonekana hospitali alikuwa akitetea nyumba yetu isiweze kubomolewa, alijitahidi sana lakini ramani ndo ilikuwa lazima ibomolewe hivyo wakabomoa vyumba viwili, choo, jiko na sebule nakutuachia vyumba viwili tu.Usiku wa siku ile tuliowasili nyumbani ndiyo Afande Deus alikuja kutupa taarifa juu ya bomoa bomoa na ilikuwa tena kilio kwangu na Mama.,
Ilipotimia asubuh nayo sikuweza kumuona tena Gervas zaidi ya kuja kuletewa taarifa na Mama yake kuwa ameshasafiri kama ilivyopangwa ili kulinda usalama wangu.
Nikawa kama mtu aliyepigwa ganzi nakusubiria iishe mwilini apate maumivu.
Kwanini Gervas hakuniaga.....?”
Niliumia moyo sana lakini haikuwa na jinsi zaidi ya kuwa na subira na kuamini iko siku nitamwona tena japokuwa sikupata kabisa nafasi ya kukaa na Gervas.
~ BAADA YA MIEZI 4 ~
Maisha kwetu yakawa ni ya kimaskini sana huku msaada mkubwa kwetu tukiuelekeza kwa Afande Deus, na mara moja moja tulikuwa tukipata msaada kwa wazazi wa Gervas kwani Mama hakuwa na kazi yeyote yakumuingizia kipato, mazoezi ya kusimama peke yangu ambayo nilikuwa napewa na Mama yalionesha matumaini makubwa kwangu kwani niliamini mda si mrefu nami nitaanza kutembea kama wengine,ilipungua sana hata na Mama pia.
“Levina mwanangu..!”
“Abee Mama..!”
“Leo nimechoka embu jaribu kutembea na kibaiskeli mwenyewe..., Utaweza tu mwanangu.....!”
Ni kweli ilifika kipindi Mama akawa anachoka lakini kwa sasa nilikuwa ninauwezo wa kusimama peke yangu huku nikitembea kwa mtindo wa kukikokota kile kibaiskeli taratibu huku nikitembea kwa mwendo mrefu kidogo na kurudi nyumbani.
Ilipofika usiku wa kama saa tano nikiwa na kauchovu kidogo kwa kuzunguka mda mrefu,Mama alikuwa ameshalala ghafla nikasikia sauti za watu nje zikipiga kelele,mwanzoni nilipuuzia lakini kadri nilivyotulia bado ile sauti ilizidi kupaza kwenye masikio yangu ikitokea kule nje,
nikafungua pazia na kutoa jicho taaratibu kujua ni kitu gani,sikuweza kuambulia kitu zaidi ya kuona watu wa mtaani wakiwa wake kwa waume wakimshambulia mtu kwa matusi na wengine wakimpiga kwa mawe na fimbo,nilipuuzia kwani sikuwa nawafahamu pale mtaani zaidi ya jirani yetu tu ambaye ni wazazi wa Gervas.
Nikiwa bado naangaza vizuri mara nikaliona gari la Afande deus lakini nilishangaa kuliona limepaki pale.
“Mmmhh.....! Atakuwa ni yeye kweli..?”
Nilijikuta naguna mwenyewe na kujiuliza bila ya majibu, haraka haraka bila hata ya kumwamsha Mama nikafungua mlango taaratibu huku nikiwa na kibaiskeli changu nikajikokota mpaka nje kushuhudia ni nini..
“Samahani ‘anti’….!”
“bila samahani..!”
“Eti pale kuna nini usiku huu...!”
“kuna kijiaskari kimoja huwa kinajifanya kimbeya na pia huwa kinatabia za kuchukuwa wake za watu..,sasa leo wamekikomesha na lazima kife pale...!"
“Samahani tena...! ......unaweza labda ukawa unamjua jina lake....?”
“Heee....! We dada vipi au na we alikuwa mpenzi wako....? Haya gari yake anayoendeshaga ile palee wanaiponda ponda...! Nenda kamsaidie..!”
Alinijibu kwa nyodo mpaka nikajuta kwanini nilimuuliza. Nikaondoka na kumwacha pale akiendelea kubwatuka.
“Looo..! Kamezidi sana kwa wake za watu leo atakoma lazima aisome namba...!
Sikuwa na hamu tena ya kumsikiliza yule dada niliyomuuliza, Hapohapo halmashauri yangu ya kichwa ikafanya kazi fasta na kugundua lile ni gari la Afande Deus lakini nani atakuwa alikuwa anaendesha..?
Nikaanza kukaribia lile eneo latukio huku nikiendesha kibaiskeli changu kwa kutumia mkono mmoja ule wa kulia uliokuwa mzima, Kadri nilivyokaribia moyo ulizidi kunipasuka na kwenda mbio.,kila nikilitazama gari lililokuwa likipondwa linafanana kabisa na la Afande Deus,
“Nilipolisogelea lile gari kweli lilikuwa la Afande Deus nilianza kuhisi ugonjwa unaanza tena kwani kwa sasa mwili wote ulikuwa haufanyi kazi.
“Mamaaa...mama uko wapi mamaa....! Afande Deus wanamuua huku..!
Nililia kwa uchungu na kwa sauti kali iliyowafanya wale watu waache kumpiga yule mtu na kuniangalia. Kuangalia nyuma yangu mama alikuwa anakuja kwa kunikimbilia nikatumia mwanya huohuo wa mimi na kibaiskeli changu kuudondokea ule mwili wa yule mtu aliyekuwa akipigwa pale chini.
“Niueni mimi! Kwanini mnampiga…? Kawafanya nini..?”
Yale maneno yalichochea hisia za wale watu waliokuwa na hasira kali, wakaendeleza kipigo kwangu bila ya kujali naumwa.
“Nakufaaa....! Nakufaaa..! Uuuuhh...! Uuuuh...! Niueni..! Niueni...! Nimalizieni nife..!”
~HOSPITALI TENA~
Mwili wangu ulikuwa tayari umeshajawa na plasta kwa kipigo nilichokipata, ni wazazi wa Gervas ndo walionileta wakisaidiana na Mama, nilivimba sana haswaa maeneo ya usoni, sasa idadi ya dawa za kumeza zilizokuwa zinatuliza maumivu zilizidi mara tatu yake..,
“Mama kwani Afande Deus alikufa..?”
“....Mwanangu...! Nitakuelezea tukifika nyumbani..!”
Japokuwa niliumia siyo sana, Wazazi wa Gervas wakishilikiana na Mama walipendekeza niendelee kutibiwa nyumbani tu.
Akili na hofu kubwa ilikuwa ni kwa afande Deus.
“Jamani hivi ninamikosi gani..? .....Isikute naenda kushuhudia kaburi..?”
Nilijiuliza kimoyo moyo huku nikiwa sijui nini kinachoendelea kuhusiana na Afande Deus,
* * * *
Ndani ya lisaa nikiwa mimi na wazazi wa Gervas tayari tulikuwa nyumbani kwetu wakitushusha na kuelekea kwao huku nikiona Mama wakimpatia pesa kidogo.
“Levina! Ugua pole na kuwa mwangalifu mama eenh!”
“Haya! Ahsanteni sana!”
Niliwaitikia tu ilimradi waondoke kwani alichoongea kilipitia upande huu nakutokea upande ule,hao tukaingia ndani huku nikikokotwa kwenye kibaiskeli cha wagonjwa nikiwa na shauku kubwa ya kutaka kujua kilchotokea jana yake.
”Enhee Mama niambie basi imekuwaje? Aunayeye Afande Deus mlimkimbiza hospitali?”
“Hapana mwanangu yule hakuwa Afande Deusi tunayemjua?”
“Niiiini? Alikuwa nani sasa? Mama acha kunificha mi namjua Afande Deus ni yeye mwenyewe alikuwa?”
“Hapana Levina!!!”
“Ni yeye Mama!!!”
“Hapaaaaaaaaaana!!!”
Kwa mara ya kwanza nilimshuhudia Mama akikasirika na kunijia juu kwani baadaye alikuja kuniweka wazi nikaamini.
Aliniambia kuwa lile gari la usiku lililokuwa likipondwa pondwa ni kweli la Afande Deus na kwa usiku ule Afande Deus alikuwa amekamatwa na kutekwa na majambazi na hajulikani aliko mpaka sasa na inasemekana kuwa hata wakati Mama alipompigia simu Afande Deus jana usiku hakuipokea yeye bali walipokea polisi wa zamu waliofanikiwa kumkamata Mama mmoja akiwa na mtoto mmoja aliyetambulika kama 'Mama Ali' pamoja na simu ya Afande Deus,na uchunguzi unaendelea juu ya kumpata Afande Deus aliko.
“Umesikia Mwanangu? Hata kama unajifanyia vijizoezi vyako vya kutembea uwe makini sana!!!”
“Sawa Mama nimekuelewa!!”
Nilimwitikia tu Mama huku nikiamini kabisa kuwa akili yangu haikuwa pale kwani nilijiuliza sana huyo Mama Ali lazima atakuwa amenitaja tu,halafu wakinipata na sina cha shahidi wala mtetezi itakuwaje?
Kila nikimfikiria Afande Deus kwa jinsi anavyotusaidia hapa nyumbani ndo kwanza nachanganyikiwa kabisaa.
* * * *
Taarifa juu ya kuokotwa
Kwa maiti kwenye daraja la sarenda ziliwafikia polisi haraka wakaenda kulithibitisha hilo na kuliwakilisha panapohusika, maiti iliweza kutambulika kirahisi kutokana na kufahamika kwake kwa mapolisi wenzake.
Vilio vingi vilitawala nyumbani kwa Afande Deus.Tukiwa kama watu wakaribu na marehemu kwa kushirikiana na Mama Deus tulikuwa tayari tumetinga mavazi yetu meusi na sasa ilikuwa muda wa kutupia mchanga.Nikiwa kwenye kibaiskeli changu huku nikishikwa na watu niliweza kuvumilia kwa mda kidogo tu.
“Baaaaba! Kweli umeniacha? Nitaenda tena wapi Baaaba?”
Nikachotewa mchanga tayari kwa kuuchukua kidogo na kuutupia kwenye kaburi.
“Baaaaba! Kweli umekwendaaaa? Baba Deus! kwanini? Nani aliyekuuuua?”
~ BAADA YA MIEZI 3 ~
Siku zilizidi kukatika nilianza kumsahau Afande Deus maishani mwangu, ila kitu ambacho kinaniuma mpaka leo hii ni Gervas. Hakuna hata siku niliyoambiwa na Mama yake kama amepiga simu au amenisalimia!
“Yani kweli miezi saba yote hiyo hata barua? Au alikuwa hanipendi kuniona na sasa yuko mbali na mimi ndo kanyamaza kabisaaa?
Laaaaaakini asije akawa na demu mwingine anayemchanganya?”
Nilikuwa najiuliza peke yangu na kujijibu huku nikimpikia Mama chakula kwani Levina mimi si Levina yule uliokuwa ukimjua tena. Mazoezi yalinisaidia saana japokuwa sikuwa nimepooza upande mkubwa,
Tofauti n kipindi kile sasa nikawa levina mpya asiyetembea na kibaiskeli cha wagonjwa,
Kupitia vyama vyao vya kusaidiana sasa Mama akapata kamkopo kalichomfanya afungue kagenge kadogo kwa ajili ya mimi na yeye kujikimu na maisha kwani hakukuwa na msaada mwingine tena maishani.
Sikuwahi kutembea na mwanaume yoyote maishani mwangu zaidi ya kuambulia kubakwa mara mbili,moja nikiwa kule gerezani na mara nyingine nikiwa Morogoro nyumbani kwa marehemu 'Baba Ali'.
Nilipenda sana siku moja Gervas aje kuwa Mme wangu wa ndoa kutokana na yeye kuwa kimya nikawa tayari nimeshakata tamaa.
Kuna kipindi Mama aliugua sana kwani alikuwa akisumbuliwa na kisukari nilipata shida sana kumuuguza kwani hela ya kumtibia ilikuwa shida na sikuwa na elimu yoyote zaidi ya kuishia kidato cha kwanza tena Mwanzoni kabisa na ndicho kipindi nilichowekwa gerezani,
kutokana na ugumu wa maisha na kuugua sana kwa Mama, Genge likafilisika kutokana na kutokuwa na sehemu nyingine ya kutuingizia kipato,
Tangu Mama alipoanza kuugua wazazi wa Gervas wakatutenga hakuna cha msaada tena.
* * * *
“Sema kaka?”
“Unaniambiaje sasa?”
“Wewe tu..,kulala elfu kumi cha fasta fasta buku tano!”
Ndiyo ilikuwa lugha yangu ya kazini, kwani ukinikuta mawindoni mida ya usiku huwezi amini.,
Kwanza kabisa jina la Levina nilikuwa nikilitumia mchana tu,na usiku naitwa 'Vina', Mwili ulikuwa umenirudi japo si sana,Ila makalio yangu bado yalikuwa ni makubwa na chuchu zilikuwa ndogo sana.
"Sikulazimishi kakaaa kama umeshindwa hapa...! Nenda kwa wengine wasiojua kukatikia sawa?"
Ni kati ya maneno yaliokuwa yakiwachanganya sana wanaume..,Na kujikuta wakining'ang'ania, kutokana na kuanza kuishi kwa uafadhali kulimfanya Mama asifanye jambo lolote na kutokana na kuniunga mkono juu ya kujiuza mwili kulinifanya nitembee na wanaume huku wengine waume za watu haijalishi ni mchana au usiku we twende tu.
Ndani ya Mwezi tu mtaa mzima ukawa umeshajua kazi yangu,kutembea na wanaume sita hadi nane kwa siku lilikuwa ni jambo dogo sana kwangu.
Siku moja nikiwa mawindoni usiku.
“Oyaaa Sista vipi kinaeleweka?”
“Vipi fasta fasta au kulala?”
“Aaaah Vina..... Leo unataka kunibania enhh...? Mimi wa kulala bhanaa vipi..!”
Aliongea kijana Mmoja mnene hivi japo sikumtambua kwani nina wateja wengi ila nilijikuta namkubalia kwenda kulala kwa tamaa ya pesa.
“Tulipane kabisaa.., nipe changu mapemaaaaa....!”
Hakuwa mtata hata kidogo yule jamaa akatoa burungutu la pesa na kuchomoa noti ya shilingi elfu kumi na kunipatia.
“Jammy...nishikie kesho nitakuja kuchukuwa kwako”
Kwa kawaida huwa nikipata wateja wa kulala nao sipendi kutembea na hela hivyo Jamila alikuwa rafiki yangu anayenichukulia pesa na mara nyingi.
Nikiwa nimevalia kimini kifupi kilichoachia mapaja yangu wazi huku ndani nikiwa mtupu kabisa kutokana na biashara zetu zinavyoruhusu.Tayari tukawa tumeshaelewana na yule Jamaa,nikawa ndani ya gari lake kuelekea hotelini au gesti yeyote kwa ajili ya kumpatia anachotaka huku akiendesha gari pia simu yake ikiita mara kwa mara naye akikata.
Hapakuwa mbali sana kwani ndani ya muda mfupi tayari alikuwa akiipaki gari kwenye hotel niliyokuwa sihifahamu vizuri akacheki simu yake pale.
Kama kawaida yangu huwa sipendi kuchelewesha muda tulipoingia chumbani tu.
“Chooni wapi?”
“Ingia humo!”
Nikachukuwa taulo la pale hotelini, Nikachukuwa na pochi kisha nikaingia bafuni,
nilijisafisha vizuri kwani tayari mteja nilimuona ana hela ya kutosha tangu alipochomoa burungutu la hela na kunipa elfu kumi kwahiyo ni kumpa mavitu mpaka mwenyewe aniongezee hela zaidi..
Nikajifungia mule chooni na kuchomoa sabuni yangu ya 'DETTOIL' nikachanganya na cream ya 'SPOT' ni kati ya vitu vinavyonifanya maumbile yangu ya ndani yanakuwa madogo (Samahani sana msomaji kama utakerwa na mimi,nisameheni sana kwa hapa)
Nikatoka huku sina hata lile taulo na kujitupa kitandani.
“Vipi unaenda kuoga au”
“Hapana nipe kwanza cha fasta nikaoge!”
Tukaingia pale kitandani na kumpatia anachokihitaji, Nilimchanganya sana kwa viuno nilivyomkatikia
“Inaatosha! Inaatoshaaa! Wacha nikaoge kwanza”
Akatoka spidi na kwenda kujimwagia maji huku akiniacha nimeduwaa pale kitandani,nikainuka kwenda kuzima taa lakini kabla sijafikia kibonyezeo cha kuzimia taa suruali ya yule mtu ikadondoka kutoka pale karibu na kakabati spesho kwa kuweka nguo, Ikanibidi niikote nakuirudishia ndipo nizime taa.
Ile nainua tu ile suruali macho yangu yakakutana na picha imedondoka ikimuonesha Afande Deus akiwa enzi zake akiwa hai.
Hofu ikaanza kunitanda nikaona nitakuwa nimemfananisha, wazo likanijia kutafuta mifukoni kwa haraka zaidi kabla hajatoka nikakutana na nyingine Nne zikiwa zinamuonesha Afande Deus akiwa ametekwa na kufungwa mdomo kwa plasta huku macho yakiwa yamejaa damu nilihisi watakuwa walimtoboa macho..,
“Mungu wangu! Kumbe niko na muuaji?”
Kwa haraka zaidi nikazichukuwa zile picha na kuzifungasha pamoja na nguo yangu ya ndani niliokuwa nimeibadilisha mda ule. Nikiwa namalizia kuweka zile picha mara simu ya yule mtu ikaingia ujumbe mfupi (meseji) Haraka haraka kabla hajatoka bafuni nikaichukuwa na kuisoma.
“UMESEMA JINA LAKE ANAITWA LEVINA? NAKUAMINIA FANYA JUU CHINI TUMUWEKE HATIANI,SI UNAJUA NI MUDA MREFU TUMEMSAKA?"
****
Ile namalizia kusoma nikaiweka ile simu haraka haraka na yule jamaa akawa ndio anatoka bafuni hivyo nikabaki sina tena ujanja wowote wa kukimbia zaidi ya kukubali kulala,
Nikawa namtaimu apate usingizi tu nisepe,Haijapita muda akawa amepitiwa na usingizi japo sidhani kama ulikuwa ni usingizi sana kwani alinikumbatia huku akikohoa mara kwa mara kuashiria yuko macho na hata simu yake inapoingia meseji alikuwa fasta kuipokea na kurudisha majibu kisha kujilaza tena.
“Nimekwisha Levina mimi? lazima nijikatae mbele yake kwanza mi siitwi Levina naitwa 'Vina'. Hata kina jammy wanalijua hilo!”
Nilijipa moyo huku nikiamini asilimia kubwa sitaweza kushikwa pale.
Taaratibu bila kupoteza mda nikamnyemelea akiwa kashapitiwa na usingizi nikamsogeza mikono yake aliokuwa amenikumbatia,nikavuta simu yake na funguo za gari,na lile burungutu lote ile simu nikaizima na kuitumbukiza kwenye pochi yangu kisha nikavaa nguo zangu fasta fasta tayari kwa kuondoka,ile nafungua kitasa tu nikamsikia akikohoa kuashiria kama mtu aliyeshtuka... sikutaka kuchelewesha mda kabisa nikatoka spidi mpaka kwenye gari yake na kuingia, Sikuwa najua kuendesha gari na nakubali hilo ni kosa kubwa sana kwangu, kwani nia kubwa ya kuchukuwa huu ufunguo ilikuwa ni kutafuta undani wa huyu mtu hivyo nikawa ndani gari yake nikipekua makaratasi yake.
Ndani ya sekunde chache nikawa nimeshayapata baadhi pamoja na pingu alizokuwa kaweka kwenye gari, nikazichukuwa na kutaka kugeuza kwenda kumfunga pingu.
“Aaaaah lakini acha tu niende nyumbani!”
Nilijikuta naghairi kurudi hivyo nikazichukuwa zile pingu na makaratasi na funguo niliziacha palepale kwenye gari lake nikaondoka zangu na kuelekea nje huku nikitafuta taksi niweze kwenda nyumbani usiku ule.
Pale getini hapakuwa na wakunizuia kwa jinsi nilivyokuwa nimevaa dhahiri walishajua tu mi ni malaya hivyo muda wowote natoka na kuingia.
* * * * *
Nikiwa nyumbani nimejipumzikia nyumbani huku nikipekuwa zile karatasi,
"Aaah!!! Sasa nimeshaanza kuzielewa kumbe yule alikuwa ni askari mpelelezi!!!! Lakiini kwanini alikuwa ananitafuta mimi?"
Ni kati ya maswali yaliyokuwa yananichanganya juu ya yule mtu niliyomtoroka hotelini, ikanibidi nimkabidhi Mama zile picha pia nimuelezee kilichonikuta mama hakuwa na la zaidi ya kuniambia niachane na hiyo biashara kwa mda wa usiku.
Sasa nikawa Levina kamili na siyo Vina tena kutokana na Biashara yangu kuifanya mchana
Na siyo usiku tena.
Mawindo yangu ni kwa waume za watu kwani niliamini ndo walikuwa wakinilipa vizuri,nilitokea kuchukiwa na kila mtu hapa mtaani lakini hilo sikulijali.
* * * *
Hali ya Mama ikazidi kubadilika kwani hakuwa anaumwa kisukari peke yake pia alikuwa na presha ya kupanda jambo lililoniwia vigumu maishani mwangu kwani msaada mkubwa ulijuwa ukitoka kwangu.
“Niongeze elfu kumi tena nikupe na nyuma kabisa!”
Ilinibidi wakati mwingine nikubali tu kuingiliwa kinyume na maumbile hii yote ni kuhakikisha Mama yangu anapona.
Ilifika kipindi Mama alishikwa na kisukari mpaka miguu ikamvimba na vidonda vikamtoka miguuni sana,hali hiyo ililichanganya sana lakini sikukata tamaa ya maisha nilichokifanya kwangu nikuendelea kufanya kazi yangu ya kujiuza mwili mpaka hapo Mama yangu atakapopona, kuna mda mwingine nilikuwa nikidhulumiwa na wanaume niliokuwa nikitembea nao,kipindi kingine nawakubali kufanya nao mapenzi hadi wanaume wawili mpaka watatu kwa mara moja,Nilijihisi kama mtu aliyechanganyikiwa na maisha..
“Leo twende tukalale kwangu! Ntakuongeza pesa!”
“Sawa tu!”
Nilikuwa radhi nikalale na mwanaume kisha mama nimuache akijiuguza nyumbani peke yake.
* * * *
“Leo nakuongeza dau! Kamata kwanza elfu ishirini kisha ukimaliza kazi nakupa na ishirini”
“Levina, Levina, Levina,nasikitika kuwa bado naipenda kazi yangu,na kila mara nilikuwa nikikutoa mimba hata kwa buku kumi na tano nakukubalia.”
“Ndio Dokta,ni kweli?”
“sasa basi! leo nasema NO!”
“Dokta pliz Dokta nitoe Dokta nitakupa chochote Dokta nitoe!”
“Nimesema NOOOOO!”
“Endapo nitakutoa hii mimba lazima uhatarishe maisha yako, kwani nitaharibu kizazi chako pengine usiweze kuzaa tena Maishani mwako! umeshawahi kuskia wanawake wagumba Levina?”
“Ndio”
“kwahiyo unapenda kuwa mgumba?”
“Hapana!
“Haya potea fasta”
Nilinywea nakujihisi nimekuwa mdogo kama kidonge cha piliton.,Nikabaki nalia huku Nisielewe mimba ni ya nani.
“Nitamlea hata kama atakuwa hana Baba”
Nilijisemea kwa sauti ya chini chini huku nikitafuta njia ya kutokea pale zahanati.
* * * *
Umati wa watu uliokuwa umefurika pale nyumbani kwetu ndo ulikuwa umenishtua asubuh asubuhi nikiwa nimetoka kwenye biashara zangu.
“Mbona kunanitisha hivi kweli kutakuwa na Msiba pale?”
Nilijikuta nikijiuliza mwenyewe huku nimejibanza kwenye kona,nguo nilizokuwa nimevaa zilikuwa fupi sana na nilikuwa nimechelewa kurudi nyumbani kwani kawaida yangu nikurudi alfajiri kwenye mida ya saa kumi usiku.
“Daah leo Levina mi nimeumbuka?
Lakini mbona kumetundikwa maturubai na Mapolisi wanazunguka zunguka..?”
Nilishindwa kujitambua kabisa mpaka alipopita mpita njia.
“Samahani kaka! Pale kuna nini?”
“kuna Msiba!”
“Maaamaa siamini Mama yangu amekufaa!”
“dada kwani vipi.?”
“Hapana hapana Mama yangu ndo nimeshampotezaaa!”
“lakini Dada!”
“Hakuna chanini Embu niache.Nenda zako tu kaka...Ooooh Mama! Mama! Mama! Mamaaa!"
“Sista Msiba haupo nyumba ile pale!”
“Uko wapi sasa?”
“Uko nyumba ya tatu kutoka pale, kwani yule mzee alikuwa mtu Maarufu sana na watu wanazidi kumiminika ndo Mana wameweka turubai refu kiasi kile!”
“Inamaana aliyekufa ni Baba Gervas?”
“yeah ! ndo huyo huyo na mi niko njia moja kuelekea pale.
Kila nikipiga akili ni jinsi gani nitaingia nyumbani sipati jibu…. haraka haraka halmashauri yangu ya kichwa ikafanya kazi fasta.
“'Enewei' hii pesa niliyotaka kumpa yule Dokta wacha niinunulie kanga nivae!”
Njia hii niliyotumia ndo ilikuwa sahihi kwani niliweza kuvaa kanga na kujifunika mpaka eneo la usoni na kuacha kijisehemu kidogo tu cha kutolea macho,
Watu walikuwa ni wengi sana eneo lile nilijipenyeza mpaka kwenye mlango wetu nakuingia ndani,nikamkuta Mama akiwa hoi pale kitandani.
“Mama vipi bado tu umelala!”
“Ndio mwanangu nitaenda wapi na hali yangu kama unavyoniona!”
“Unajua Nje kuna Msiba”
Nitajulia wapi tena mwanangu kama unavyoniona miguu imenijaa vidonda na ndo inavimba kila mda...kwani msiba wa nani?”
“Mama! Baba Gervas hatunaye tena!”
“Levina unasemaaa?”
Maskini sikujua kama ile taarifa niliyompa juu ya msiba itamletea madhara kwani nilishangaa Mama akianza kujiuma uma meno kisha akatapa tapa nakutoa mapovu mdomoni kana kwamba anaugua kifafa,baada ya mda tena nikamwona akinyong'onyea huku anavuta pumzi kwa tabu pale pale nikamuwahi na kuukutanisha mdomo wake na wangu kisha nikaanza kumpuliza ili naye apate pumzi kidogo.
Baada ya mda akarudi katika hali yake kisha,
“Levina nipe maji?”
“Pumzika kwanza Mama.!”
“Naskia kiu Mwanangu nipe hayo Maji?”
Nikawa mbishi kumpa maji kwani daktari alishaniambia Ninapomuona Mama katika hali ile nisithubutu kumpa kitu chochote mpaka baada ya masaa.
~ BAADA YA MIEZI 4 ~
Tayari tulikuwa tumeshasahau habari za msiba wa Baba Gervas,kwani mpaka msiba unaisha sikuweza kuiona hata sura ya Gervas,
“au pengine alibanwa na shule au... aliogopa kuja kwasababu anatafutwa na Mapolisi...?”
Ila kwa upande wa Mama yangu, hali yake bado ilikuwa ikibadilika siku baada ya siku, Mpaka mimba inamiezi minne bado niliendelea na biashara yangu ya kujiuza mwili kwani sikupata njia nyingine mbadala wa kujikimu na maisha, mtaa wote kila mtu alikuwa akikerwa na tabia yangu ya kutembea na waume za watu na hata Mama yake na Gervas alikuwa mmojawapo aliyenichukia sana na hata baada ya mumewe kufariki.
Ndipo nikapata wazo la kumrudia Mungu.
“Bwana Yesu asifiwe!”
“Amina karibu binti!”
“Mchungaji! nipo hapa mbele yako kutubu zambi zangu zote..!”
“Unaitwa nani Binti?”
“Levina!”
“Sogeza kichwa chako karibu,fumba macho!”
“Baba katika jina la Yesu! Weza kumfungulia binti huyu njia ,Muachanishe na nguvu zote za ajabu zitakazompinga..,Baba Mwenye majina Mengi Yehova Baba, Masiha...kwa nguvu na utukufu wako nakemea Mapepo wote wanaomzunguka...kwa jina la Yesu..!”
“AMINA!”
Baada ya hapo mwili wote ukasisimka na sikuamini maishani mwangu kama ipo siku ntakuwa vile,nikawa mlokole safi asiyemjua mwanaume,mara kwa mara Mchungaji alikuwa akija nyumbani kumuombea Mama,mpaka ikafika kipindi akapata nafuu kidogo naye akawa anaweza kutembea japo kidogo.
“Oya unamnyaka yule Malaya wa pale.?”
“Si yule aliyekuwa anatembea na waume za watu.?”
“aaahaa unasemea Levina?”
“Exactly!”
“Enhee kwani amefanya nini..?”
“Si kameokoka eti!”
“Oya kausha! kausha! Acha kunivunja mbavu mwana!”
Nilidharauliwa kila kona niliyopita, kwani ni kweli nilikuwa nime'change' kuanzia Mavazi,nilikuwa
Levina mimi wa kutembea na Biblia mda wote kuhubiri neno la Mungu mtaa kwa mtaa,
“ushindwe katika jina la Yesu!”
Nilikuwa mkali kukemea mapepo pale wanaume walipokuwa wakinitaka kimapenzi.
* * * *
“Hodi! Hodi!”
“Karibu... Levina embu nenda kafungue mlango naskia kama mtu anabisha hodi..!”
Ile nafungua tu mlango nakutana uso kwa uso na sura niliyokuwa nikiifahamu,kwani alikuwa amevalia kisasa, suruali ya jeans inayong'aa, tisheti nyeupe iliyoandikwa kwa herufi kubwa 'BACK FROM US',huku mwili wake uking'aa kwa cheni alizojizungushia kuanzia mikononi,shingoni mpaka pembeni mwa mifuko ya kwenye suruali yake,hakika alipendeza,
“oooh! Gervas!”
“Levinaaa! c'om n hug em'!”
Sikumuelewa vizuri alichoongea ila kwa vitendo alivyoonesha viliingia kwenye hisia zangu nakutambua kuwa anahitaji nimkumbatie,
“oooh...baby..! baby..! baby..! R u aukey..! Haw abau ua Mama!”
Niliambulia kusikia neno Mama lakini nikamwelewa anamzungumzia Mama.
“Mmmh yule pale sebuleni mzima tu! Pole kwa msiba!”
“Naaah Naaah usijali Levy, t was da past!”
“Unasema?”
Nilimuuliza kwani sikuwa namuelewa kabisa anachozungumza kwani alikuwa akichanganya lugha, nikamwacha pale akiongea na Mama kisha nikakimbia chumbani kwenda kubadilisha nguo
“Shikamoo Mama!”
"Marahaba Mwanangu Gervas mzima wewe?”
“Mimi mzima tu sijui nyie mnaendeleaje!”
“Tunamshukuru Mungu!”
“kumebadilika sana hapa hata na kwetu pia kidogo nilishapasahau...Mama nilishindwa kuja kwenye msiba kwani nilikatazwa na ndugu kutokana na ilee kesi ya Levina”
“Aaaaahhh ok, ok, ni kweli!” “Hata hivyo hakuna kilichoharibika nimekuja kuangalia kaburi la Baba pia nimeomba misa kesho asubuhi tutasali pale nyumbani!”
Nilivyorudi nikamkuta bado Gervas anaongea na Mama,
Baada ya mda Mama akaelekea chumbani na kuniacha pale na Gervas.
“Enhee! Niambie Gervas za kutususa tangu ulivyoondoka?”
“Hapana Levina mimi sijawasusa ila tangu nilivyoondoka na mzee kipindi kilee sikuweza kupata njia yoyote ya mawasiliano na wewe, niliumia sana moyo japo hutaniamini kwa hilo!”
“enhee nakusikiliza!”
“Baba akaniacha na kurudi huku bongo, nilikaa miezi mitano bila ya kuwa na mawasiliano yoyote na nyumbani, sikuweza kuwa na mchumba yeyote kwani niliamini wewe ndo wangu wa ndoa,"
“Ya kweli hayo Gervas?”
“Kweli Levy ilifika kipindi nikapata kazi katika kampuni moja huko ya kutengeneza pombe kali aina ya 'HAMMIER WHISKY' nikawa nafanyakazi huku najisomesha,kila siku nilijitahidi sana angalau nipate kusikia sauti yako lakini ilishindikana!”
“Kwanini ilishindikana?”
“Levy kila nikiwapigia simu wazazi wangu japo nipate kuongea na wewe wananiambia nikuache haunifai na nisiwe na wewe tena kwani umebadilika sana na unatembea na kila mtu hapa mtaani..!”
Nikashusha pumzi huku machozi yakinilengalenga kwa huruma nikaendelea kumsikiliza Gervas,
“enhee ikawaje?”
“Mimi na wewe Levy tumetoka mbali na elewa kuwa nakupenda na nitazidi kukupenda milele, sijataka kuwasikia wazazi wangu hata pale waliponiambia kuwa umebadilika, Baba yangu alifariki akiwa bado anakuchukia, Mama yangu pia mpaka sasa anakuchukia kwani nilivyomwambia kuwa nahtaji kukuona leo alinijia juu na kuchukia sana! Levy…. embu niambie kweli unanipenda?”
Nilikaa kimya huku naitazama mimba yangu na mwili kunisisimka na ulokole wangu kuuweka pembeni kwa mda.
“Levy hata kama mimba sio yangu mimi niko tayari kwenda kuishi na wewe huko Marekani, hiyo mimba mimi nitailea....elewa kuwa bado nakupenda”
“S...a..a..a..wa..! Na Mama je?”
“Kwani Hamna ndugu wa kumuacha na Mama yako?”
“kama unavyoniona Mimi ndo kila kitu kwa Mama!”
“Kwahiyo hutaki kwenda kuishi na mimi au hunipendi?”
Alianza kuzungumza kwa sauti ya ukali Gervas akanifanya nitetemeke na kujikuta nikitoa jibu haraka haraka.
“Sawa Gervas nimekuelewa na nitajitahidi tutakuwa pamoja!”
Hakuna mwanaume ambaye amekaa moyoni mwangu kama Gervas na hata kama angekaa miaka Mia ndo akarudi bado tu ningempenda kwa dhati, Juhudi nyingi alizonionesha toka kipindi niko Gerezani mpaka nilipo ni jambo la kumshukuru Mungu kwakweli,nilimalizana na Gervas kisha alichoniambia kuwa kesho yake atakuja kuniaga kwani Ofisi ilimpa ruhusa ya siku tano tu za kukaa hapa.
**********
Asubuhi na Mapema nikiwa nafanya usafi wa hapa na pale huku Mama nikimwacha sebuleni akizubaa mwenyewe,Nilifanya usafi fasta fasta kisha nikaingia ndani kumuogesha Mama yangu na baada ya hapo nikaingia bafuni,na kutoka nikiwa safi kisha nikavalia gauni langu refu huku pembeni nikiwa na Biblia na kalamu nikilichambua Neno la Mungu.Nikiwa bado naendelea kusoma Biblia Mara nikasikia hodi inapigwa mlangoni.
“Karibu! Aaaaah! Gervas karibu mpaka ndani!”
“Hata siyo mkaaji kwani nina mda mchache na hapa Naelekea Mjini kidogo nikamfanyie 'Shopping' Mama kisha nitarudi jioni sana!”
“Kwani safari ni lini?”
“Yani hapa unaponiona Tiketi nilishakata zamani ya 'go an return' kwahiyo usiku kwenye saa Nane leo hii ndio nitaondoka!”
“aaah sasa”
Kabla sijamaliza kumuuliza akadakia na kuendelea kuzungumza,
“wacha nimuage Mama then utanisindikiza ndio utajua kila kitu!”
Akaingia mpaka sebuleni akakaa kisha nikaenda chumbani kumuitia Mama aje amuage.
“Mama kwaheri mimi usiku wa leo narudi Marekani!”
“Mbona haraka haraka Mwanangu,mi nikajua upo hapa hata kamwezi kamoja ndio urudi!”
“Hapana Mama natakiwa haraka sana Shuleni pia Kazini ninapofanya kazi wananihtaji sana!”
“Haya Baba safari Njema huko uendako pia usitusahau Mwanangu uwe unatukumbuka”
“Sawa Mama usijali ntaendelea kuwakumbuka huko niendake Mama!”
Najua Gervas aliongea kwa makusudi ili Mama asiweze kujua mpango wetu wa mimi na Gervas.Tulitoka pale moja kwa tukawa tunaekea nyumbani kwao,
“Hapana Gervas mi sifiki kwenu Mama yako namuogopa sana!”
“Niiiiiiiiiini?”
“Gervas nielewe kwa hilo pia usijali Mama yako niko naye pamoja!”
“Levy ninachotaka ni twende nikakukabidhi kwa Mama sababu leo hii natangulia Mimi then nitawaachia Mipango yote ya kuja we na Mama yangu si ndio?”
“Sawa Gerva lakiini!”
“Hakuna cha Lakini, si umeshajua Mama yako mtu wa kumwacha naye?”
“Ndio nimeshajua!”
Nikamuitikia kwa woga huku nikiwa sijitambui nitamwacha vipi Mama yangu.
* * * *
Ni Wiki moja imeshapita tangu Gervas aondoke na kuniacha, Nilijutia kumdanganya hata Mama yake Gervas kuwa sipo na Mama yangu naishi peke yangu,Mpaka sasa Mama Gervas anajua kuwa Mama yangu aliugua sana nikamsafirisha Moshi nyumbani na kwa bahati mbaya akafia hukohuko hivyo sasa hivi naishi peke yangu., Siku aliyoondoka Gervas alinipatia Dola thelathini pamoja na simu huku akinisisitizia tufanye haraka mimi na Mama yake tuwe tumeshaondoka.
Namkubali Mungu na nipo naye Daima lakini kila nikimfikiria Gervas nakuwa katika wakati mgumu,kwani Mama yake Gervas hanipendi kabisa na mimi niko tayari hata nimuache Mama niondoke na Mama Gervas nikaishi na Mpenzi wangu Gervas.,Siku moja tukiwa katika pilika pilika za kuhangaikia Viza ya kusafiria pale ubalozi wa Marekani.
“Hivi wewe Levina na tumbo lako na umalaya wako unaenda kwa nani?”
“Mama,siku hizi nimeokoka na nimemrudia Bwana Yesu hivyo mi si Levina yule wa zamani!”
“eti Si Levina wazamani nyooooooooooooooo...na huko tuendako? Walahi nitahakikisha unarudi huku huku Malaya mkubwa wee 'x@sh@hhzzzzzshhh'....”
Aliachia sonyo kali mpaka kila mtu aliyekuwepo pale alishangaa, Sikuweza kumrudishia zaidi ya kumwachia Mungu na kuendelea kuvumilia kwani ndoto yangu ni kuishi na Gervas maishani mwangu.
~ BAADA YA WIKI MOJA ~
Furaha ilinitawala moyoni kwani tayari tulikuwa tumeshapata Viza na tiketi tukawa tumeshaweka booking, Ndege ya shirika la 'EMIRATES' ndo tuliotarajia kwenda nayo ikianzia safari yake hapa kisha kupitia 'Kenya' na kituo cha pili kitakuwa 'Dubai' kwa ajili ya kubadilisha ndege itakayotupeleka mpaka 'Stockhom' halafu itaelekea uwanja wa 'Amsterdam' pale Uholanzi kubadilisha tena ndege ya kuelekea moja kwa moja mpaka 'Maryland' ikipitia kusini mwa 'Canada' na huko ndo tutajua ni jinsi gani tutafika kwa Gervas ambaye anaishi jimbo la 'Detroit..'
Si furaha tu niliyokuwa nayo bali pia na huzuni huku nikiwa sijitambui Mama yangu nitamwacha na nani?
Gervas alikuwa akinipigia simu karibu kila siku huku akinisisitizia kuwa nikienda huko sirudi kwani ndo tunaanza maisha,sikuweza kuihofia mimba niliyokuwanayo kwani alishaniahidi kumlea mtoto nitakayemzaa.
Safari hii halmashauri yangu ya kichwa ilinituma vibaya kwani nilijikuta nikitupa ulokole wangu pembeni na kuanza kufanya mambo kinyume na yale ambayo yasiyompendeza Mwenyezi Mungu.
* * * *
Siku zilizidi kupungua hadi ikafikia siku Nne zimebaki huku nikiwa sijielewi kama safari kweli ipo au la !,nikawa kama mtu aliyechanganyikiwa kwani hali ya Mama yangu ilikuwa inabadilika badilika sana haipiti siku bila miguu yake kumvimba na ndio hapo hapo presha inamuanza na kuzidia lakini roho ya kikatili ikanitawala kuna kipindi Nilithubutu hata kumshindisha Mama yangu njaa karibu kila siku hiyo yote ni kuhangaikia safari, Mama yake Gervas bado aliendelea kunichukia lakini hilo sikulijali zaidi ya kumvumilia nakuona ipo siku atabadilika huko tuendako.
Roho ya kikatili iliendelea kunirudia tena kila mda na kila siku tena nilikuwa na roho mbaya kama ile ya kule msituni nilipomuua 'Pendo' na ile ya Morogoro pale Nilipomuua 'Baba Ali'
Mama yangu nikawa simpikii chakula zaidi ya kumnunulia vijichipsi vikavu siku nyingine nampa chai iliyokorogewa chumvi na hamna wala kitafunwa cha aina yoyote ili mradi tu ajaze tumbo siku ipite.
Mara zikasalia siku mbili ikabidi nijipendekeze kwenda kwa Mama Gervas kujua safari itakuwaje hiyo keshokutwa ikifika,
“Shikamoo!”
“Sihitaji shikamoo yako kama chakula ile, enh upo tayari we malaya usio na hata chembe ya aibu?”
“Nipo tayari ila”
“ila nini?”
“Safari si keshokutwa mchana Mama?”
Nilijikuta nambadilishia mada bila ya yeye kujitambua kisha nikamuaga akiwa amefura kwa hasira, huku akinisindikiza kwa fyonyo kali kuonesha kuwa hanipendi kabisaa.
“Na hapa usije, tutakutana 'Airport' hiyo keshokutwa we malaya.!”
Akaniaga huku Moyoni nikiwa sina raha ya vitu vitatu,kwanza nitawezaje kuishi naye huyu Mama Gervas huko niendako? Pili itakuwaje hii mimba kwani ndio kwanza ina miezi minne na nusu, tatu nitamwacha mwacha vipi Mama yangu na hali yake ile?
“aah liwalo na liwe”
nikajisemea kimoyo moyo huku nikijongea nyumbani kwetu, safari hii nilimuonea huruma kidogo Mama kwani ilipofika usiku tu nilimtengenezea uji tena ule wa ulezi hadi akanishangaa, alipomaliza kunywa tu,
“Ahsante sana Mwanangu uji mtamu, umenikumbusha mbali mno!”
“Usijali Mama nakupenda”
Nilimjibu kinafki huku nikilitambua kuwa sasa simpendi Mama hata kidogo na hii yote ni kwasababu ya safari.
Ulipofika mda wa kulala Nilimwacha Mama akiwa amejiegemeza kwenye kochi tena akiwa amepitiwa na usingizi, nilishangilia ushindi kimoyo moyo huku nikiamini mpaka kesho itakuwa imesalia siku moja tu.
Nikaingia chumbani kwangu tena kwa kunyata nikafungua Biblia yangu na kuanza kuomba,
“Eeeh Mwenyezi Mungu nakuomba unisamehe sana kwa kitendo nitakachofanya hivi punde! Kisha nikamaliza kwa kufanya ishara ya msalaba”
Nikafunika ile Biblia,kilichofuata nikachukua panga na kamba nene ndefu na kurudi tena sebuleni kwa kunyata lakini nilipofika tu sebuleni sikumkuta Mama pale nilipomuacha,hofu ikaanza kunitanda,nikahisi moyo wangu umepasuka huku na kule nikitoa macho kumtafuta Mara nikaona karatasi pale Mezani imefunikwa kwa hofu niliyokuwa nayo nikaiwahi haraka haraka kwenda kuichukua lakini kabla sijafika pale ndo nakaribia tu mara nikasikia kama sauti ya mtu anabisha hodi,haraka haraka nikaikodolea saa yetu ya ukutani ikanionesha ni saa tisa na robo usiku, nikawa najiuliza.
‘’Huyu ni nani anayebisha hodi sa hivi!’’
Sikuitikia ile hodi nilichokifanya nikaichukuwa ile karatasi na kuanza kuisoma.
"MWANANGU WA PEKEE LEVINA, KWANINI UNATAKA KUNIUA BILA YA KOSA LOLOTE…? NIMEHANGAIKIA MAISHA YAKO KWA MUDA MREFU MPAKA SASA.,NIMESIKITIKA SANA KUKUTA TIKETI YA NDEGE CHUMBANI KWAKO NA SAFARI NI KESHO,BILA HATA KUNIAMBIA CHOCHOTE MWANANGU.? MPAKA NIKAAMUA KUCHUKUWA UAMUZI HUU WA KUJIUA NITANGULIE MBELE YA HAKI,
NAKUTAKIA MAISHA MEMA,
Mimi MAMA YAKO,
Mama Levina.’’
"No.! No.! No! Mama.! Kwanini umewahi kufanya hiivyooo!"
Nikajikuta nauvua moyo wa kikatili na kuanza kumuonea huruma tena Mama huku nikielekea mlangoni kwa yule mtu aliyekuwa anabisha hodi,
‘’Hapa mezani nimekuta kikopo cha sumu ya panya na hii karatasi, yeye Mama atakuwa wapi sasa?’’
Kabla sijaufungua mlango nikalipenyeza jicho langu kwenye tobo la kuwekea ufunguo.
‘’Mungu mkubwa,huyu ni Mama yangu kabisa, ona na kanga nilizomnunulia kipindi kileee ni hizi hizi!’’
Sikutaka hata kuuliza ni nani kwani sauti nilikuwa siiskii lakini kwanilivyokuwa nimemchungulia dhahiri atakuwa ni Mama yangu,
‘’itakuwa alienda chooni kipindi kile nilivyoenda chumbani? Lakini ile sumu na barua kwanini aliamua kuandika vile? Inamaana anajua picha lote litakavyokuwa?’’
Ni kati ya maswali niliokuwa nikijiuliza bila kupata majibu kwani ni kweli choo chetu kimejengwa nje ya nyumba na yule niliyemchungulia ni Mama yangu kabisa.
Nikachukuwa vile vitu nilivyokuwa nimeshika ambavyo ni kamba kubwa nene pamoja na Panga kisha nikavitupia uvunguni mwa kochi ili Mama asijue lolote kisha nikarudi pale kwa ajili ya kumfungulia, kadri nilivyokuwa nashika kitasa ndivyo nilikuwa naona mlango unazidi kuwa mgumu nikausukuma kwanguvu kuelekea ndani nilipo, mara nikasikia kishindo cha mtu amedondoka mbele yangu,
‘’Mamaa! Mamaa! Ni wewe Mama!’’
Niliugeuza ule mwili nakuanza kuutingisha maskini ni kweli alikuwa Mama japo Mwili ulikuwa umeshabadilika na kuwa mweusi kama mkaa, huku damu yake ikibadilika na kuwa maji kama kamasi ikiteleza kutokea masikioni,puani na Mdomoni, ngozi yake ilijikunja sana lakini halmashauri yangu ya kichwa ikafanya kazi fasta na kujua kuwa huenda alikunywa ile sumu kidogo halafu akaenda chooni wakati anarudi ikamzidia.
Bila kupoteza muda nikauvuta ule mwili nakufunga mlango kwa ufunguo halafu nikamburuza mpaka sebuleni kisha nikaingia chumbani na kutoa Biblia.
‘’Eeeh Mungu Baba muweza wa yote!!! Natubu mbele za haki najua kama mimi ni Mwana mkosefu kwa kitendo nilichofanya na nitakachoendelea kukifanya ila naomba kusamehewa Amina.’’
Nilipomaliza nikaingia chumbani kwangu na kuchukua Gunia kubwa na koleo kisha nikalipitia lile panga pale uvunguni sebuleni na kuuburuta ule mwili kuelekea nje ya nyumba yetu, nawaombeni sana wasomaji mnisamehe kwa nilichokifanya mbeleni,
Nikauburuta ule mwili mpaka karibu na eneo lilipokuwa na kaburi la Baba, nikaulaza na kuchukuwa panga langu kisha nikaanza kutenganisha upande mmoja mmoja nikianzia na mikono,shingo na miguu yote miwili hakika sikuwa levina yule mlokole bali nilikuwa Levina Mkatili tena mnyama kama simba Dume tena yule anayoogopewa na kila mtu duniani. Nilichana kitambaa cha nguo yangu na kujifunika usoni kisha nikaanza kumkatakata Mama eneo la usoni ili nipoteze ushahidi kama ikija kujulikana, nahisi damu ilikuwa imeganda kwani sikushuhudia hata chembe ya damu ikimtoka.
Nilipomaliza nikachukuwa viwiliwili nikaanza kudumbukiza kwenye ule mfuko kisha
Nikachukuwa koleo nakuanza kuchimba kashimo kadogo kwa ajili ya kumfukia ili niendelee kupoteze ushahidi kabisa, nikiwa ndio namalizia kuchimba mara simu yangu ikaita,
********
‘’haloo..! aaah Gervas’’
‘’eenh Mmefikia wapi?’’
‘’Mama tayari nimemwacha na mtu na keshokutwa safari itakuwepo usijali mpenzi wangu..!’’
‘’Okey, msalimie sana Mama yako mwambie bado namkumbuka na kuna zawadi yake tayari nimemwandalia’’
‘’Usijali Gerva,amekusikia!’’
Nikakata simu nakumalizia kuchimba pale fasta fasta nilipomaliza nikashindilia na kokoto zilizokuwa karibu, kisha nikaingia ndani kwa mbwembwe.
‘’Zoezi la kwanza limeisha na bado Mama yake Gervas, atanitambua huko tunapoenda!’’
Nilijisemea kimoyo moyo huku nikijiamini kwa kile nilichokifanya muda si mrefu nilipofika sebuleni nikapiga magoti na kuomba tena.
‘’Najua jamii yote itachukizwa nami, lakini mtetezi wangu ni wewe Baba uliye juu mbinguni,
eeeh mwenyezi Mungu mlaze Mama yangu Mahala pema peponi, amina.’’
Nilipomaliza kusali tu ghafla nikaanza kujihisi mabadiliko makubwa kwenye mwili wangu sana sana eneo la tumbo, niliumia sana, nilijikaza bado ikawa haisaidii uchungu ulinizidia mpaka nikajihisi mimba inataka kuchomoka, nilishindwa kuvumilia nikaanza kugala gala pale chini lakini nikawa kama ndio nalichochea tumbo liendelee kuuma, miguu ikavimba kwa haraka nikawa najiburuza sasa kuelekea chumbani, kwa maumivu yaliokuwa yamenizidia mpaka nikajikuta nimeingia chumba cha Mama yangu ambaye tayari nimeshamuua, kwa kujikokota taaratibu mpaka eneo la 'dressing tebo' huku nikitafuta dawa yeyote ya kutuliza maumivu, nikajishikiza kwa mkono mmoja huku mkono mwingine ukiwa unafungua droo za lile 'dressing tebo'
‘’Mamaaaaaaa..! Mamaaaaaa...! Mamaaaaa...! Mi sijakuua Mama ulikunywa sumu mwenyewe Mama!’’
Sura yangu ilikuwa imekutana na kioo cha ile 'dressing tebo' ghafla ikatokea sura ya Mama katika kile kioo, nilichanganyikiwa na kujiona zaidi ya kichaa kwani usiku ule ule nilitokomea kusikojulikana huku nikiwa mtupu nimevalia 'Nguo ya kulalia' na nywele zikinivuruga,.
Kulipokucha asubuhi kila mtu alikuwa akinishangaa kwani nilikuwa tayari majalalani nikiokoteza vyakula vichafu, ukinisogelea utakuwa unatafuta balaa na Mimi nikawa si Levina tena.
‘’Ng'aaam! Ng'aaam! Piiiiiipi! Pipiiii! Oya pisha njia gari inakasi hiyo we fala nini? Embu pisha nitakuitia Mama yangu aje akugonge?’’
Nilikuwa tayari chizi kwani mikononi nilikuwa nimeshika mifuniko ya ndoo huku nikiendesha kama gari nazunguka zunguka wapita njia wakinishangaa
‘’Gervas panda twende wewe konda wadai nauli haoo!’’
Uchizi wangu uliendelea na ilipofika muda wa usiku sana, vijana kama sita hivi nafikiri walikuwa ni majambazi kwani walikuwa na makoti makubwa huku wamekunja sura zao walipita eneo nililokuwa nimejibanza na kujikunyata pale jalalani.
‘’Oyaa masela eenh!’’
‘’washikaji huyu chizi vipi, embu mchekini!’’
‘’Oyaa hapa si Marekani?’’
‘’Fala nini?’’
‘’Masela mi nina nyege sana kama vipi njooni basi!’’
Niliwaita wakanifanya kitendo kibaya wote wale huku nikifurahia kwa kile kitendo.
‘’kama vipi na kesho mje basi..! Au siyo masela?’’
Nikatoka eneo lile nikiwa na mimba yangu huku nikijitembelea kusiko julikana usiku ule, hata nilipowaona polisi sikuogopa kabisa,
‘’We binti chizi nini? Unafuata nini hapa Polisi?
Nilijikuta nimeingia kituo cha polisi huku nikiwa sina hata chembe ya woga!
‘’Kwani masela nyie vipi? Mi muuaji Mmesikia? Mimi ndio niliomuua Baba Ali, pendo na hata Mama yangu nimemuua mimi!’’
‘’Afande John, unarisikia hiri ritoto rinavyoropoka? Binti unaitwaga rinani?’’
‘’Mi naitwa Levina, oyaa kwanza nipe bangi nitoe stimu..!’’
"Haroo hiri siro ri revina tunaroritafutaga?’’
‘’Hamuwezi kunitafuta nyie mabwege labda mumtafute Afande Deus!’’
‘’Nani? Embu riingize rokapu ritatusaidia kumpata huyo revina, nakujua juu ya rimkuu riafande Deus!’’
*************
‘’Mamaaa nakufaaaaa! maama! Uuuuh! Uuuh!”
Nilishtuka kitandani nikiwa sijielewi na siamini kwa kilichonitokea kama kweli ni ndoto au la!..,jasho jembamba lilikuwa likinitiririka, nikawa mzito kuamka, nikaanza kupapasa papasa kitanda changu, nikaivuta saa yangu fasta ikawa inanionesha kuwa imetimia kama saa mbili na dakika ishirini asubuhi, sikuamini macho yangu mpaka pale nilipofungua dirisha ndio nikajua kuwa ni kweli asubuhi, nikatoka spidi mpaka sebuleni huku nikiwa nahema juu juu nikamkuta Mama akiwa amelala pale pale sebuleni nilipomuacha jana usiku baada ya kumpa uji wa ulezi, nikamwangalia huku machozi yakinitoka,
‘’Mama? Mama?’’
Akashtuka pale kutoka usingizini,
‘’mwanangu Levina vipi tena mbona unalia mwenyewe?"
Nikampa mikono ishara kuwa asimame kisha nikamkumbatia kwa nguvu huku nikiwa na hisia kali nyingi moyoni,
‘’nakupenda sana Mama yangu!’’
‘’Mbona hata na mie nakupenda pia mwanangu!’’
Nikatoka pale nakurudi tena chumbani huku nikitetemeka na kutojiamini kama kweli niliokuwa namkumbatia na kumsemesha ni Mama kweli au la!
‘’Hiiiiiivi Kwanini huwa naandamwa na ndoto za ajabu ajabu hivi? Eeh Mungu weza kuniepusha na ndoto mbaya kama ya leo usiku!’’
Nikachukuwa Biblia yangu na kalamu kisha nikaanza kulichambua Neno la Mungu taratibu.
Ndani ya lisaa nikawa nimeshamaliza kulichambua hivyo nikamtengenezea Mama uji wa ulezi kisha nikamwekea.
‘’Mama utakunywa uji upo pale kwenye chupa, Mi naelekea kumchukua rafiki yangu Jammy tutakuja naye baadaye!"
‘’Sawa Mwanangu uwahi kurudi tu!’’
‘’Hilo tu! Wala usijali kabisa Mama yangu.
Nikavaa nguo fasta kisha safari ya kumtafuta Jammy ikaanza.
Jammy au kwa jina lake kamili ni Jamila yule ambaye zamani sana alikuwa rafiki yangu kipindi kile nafanya biashara ya kujiuza mwili na ndiye aliyekuwa akinishikia pesa zangu. Nilimkuta nikamwelezea matatizo yangu na sababu kubwa ya kusafiri na kumuacha yeye na Mama yangu, kwakuwa Jammy hakuwa na sehemu maalumu ya kuishi hivyo nikamwomba sana aishi na Mama yangu na ipo siku nitakuja kuwachukuwa acha kwanza niende kuandaa Mazingira huko Marekani.
‘’Mama nakimbia Morogoro nitakaa kama wiki Moja nitarudi, kwa hiyo utakuwa na huyu rafiki yangu Jammy!’’
‘’Kuna nini tena Mwanangu huko Morogoro?’’
‘’Mama kuna dili nono hilo we subiri nikirudi nitakufanyia maajabu mpaka ushangae!’’
‘’Haya Mwanangu usisahau zawadi!’’
‘’Sema kingine Mama hilo tu?’’
Kamwe sitakuja kumuua Mama yangu nampenda sana, inanibidi nguvu zote nizielekezee kwa Mungu ili aniepushe kabisaa na ndoto za ajabu kama ya leo usiku niliyoota.
Nikaingia ndani na kutoka na kijibegi changu huku nikimwambia Jammy anisindikize, nikamfata Mama na kumkumbatia,
‘’Byee Mama!’’
Nikatoka pale huku namsihi Jammy anisaidie sana kuishi na Mama yangu pia ahamishe vitu vyake vyote na ahamie nyumbani kwetu leo leo.
* * * *
Tayari ilikuwa imetimia saa sita kama na dakika arobaini nikiwa njiani na Jammy akinisindikiza mpaka uwanja wa ndege. Ndege ilikuwa inaondoka saa tisa na nusu, nikawa na hofu kweli ya kuchelewa,
‘’Tukodishe teksi nini Jammy? Maana naona kama foleni inasumbua?
‘’Ni sawa tu Levina!’’
Tukashuka kwenye Dala Dala fasta na kuchukuwa teksi iliyotutoa kutokea pale Tazara mpaka uwanja wa ndege, kidogo tusingewahi kwani saa Nane kamili imetugongea ndio tunaingia uwanja wa ndege..
‘’Chukua pesa yako hii hapa fasta fasta!’’
Nikamlipa yule dereva teksi pesa yake na kukimbia sehemu ya kuingilia, ile tunafika tu tunakuta wanaosafiri ndio wanaweka mizigo yao kwenye lifti ya mizigo huku pembeni wakichekiwa passpoti zao, haraka haraka nikajisachi nakutoa pasipoti yangu kisha nikaishika mkononi, nikamwachia simu Jammy na vijihela kidogo kisha nikaagana naye akarudi zake.
"Kwa heri Jammy, take care sweety!"
Nilijikuta naongea kiingereza cha kujiuma uma pale mbele za watu na mimi nisijeonekana mshamba eneo lile.
Kwa mbali nikamwona Mama Gervas ndio anapita kukaguliwa na tayari alikuwa anaelekea sehemu ndege ilipo, sikuwa na wasiwasi wowote kwani tulikuwa tumeandikiwa kukaa siti moja wote kwenye tiketi, nikiwa na shauku ya kuingia ndani ya ndege, hatimaye ile foleni ikasogea na sasa ikafika zamu yangu kutoa ile pasipoti, yule mtu aliyenihudumia akaanza kama kuweka wasiwasi kwangu, akawa ananiangalia mara mbili mbili huku anatingisha kichwa chake kuonesha kuna kitu kinamtatiza juu yangu,
‘’Unaitwa nani?’’
‘’Levina Christian’’
Nilimjibu bila kuonesha woga wowote.
‘’Hii picha hapa kwenye Pasipoti ni yako?’’
‘’Ndio ni mimi kwani vipi mkubwa’’
‘’Embu kaa kwanza pembeni nimalize kuwahudumia hawa nina wasiwasi na wewe, nimekutafuta muda mrefu sana bila ya kukupata!’’
Mwili wote ukawa kama umepigwa ganzi, ghafla nikajikuta haja ndogo ikitaka kunitoka pale pale nikajihisi kama nina mkosi hapa duniani, nilitamani nichukue Biblia niombe pale pembeni lakini ikashindikana kwani nilishaipaki ndani ya begi na begi langu lilikuwa tayari limeshapitishwa hivyo nikawa nipo tayari kupelekwa popote, huku nikijiamini mtetezi wangu yu hai na anaweza yote kwa yule amuaminiaye.
Yule mhudumu aliendelea kuhudumia wengine huku akinitia gadhabu na kushindwa kujua nitoroke pale au?
‘’sijui nimkimbie? Lakini kama ninakosa mbona hawajanifunga chochote mikononi au hakuna wa kunilinda?’’
Alipowabakiza watu wachache yule mhudumu aliyekuwa amevalia mavazi ya kiaskari lakini yalikuwa katika rangi ya bluu kama wale askari wa uhamiaji, akamwomba mwenzake awamalizie huku akinifuata taratibu eneo nililokuwa nimetulia namsubiria.
‘’Twende paleee Mara moja Levina!’’
Nilishangaa napelekwa sehemu nisiyoifahamu kisha tukaingia chumba kidogo kilichokuwa hakina hata mtu, akaiweka bastola na pingu zake vizuri, kisha akafunga ule mlango na ufunguo kwa nguvu akanigeukia huku amekunja sura.
‘’Nimekwishaa Levina mimi leo isikute ana undugu na Baba ali au Baba Pendo?"
‘’Levina Christian?’’
‘’Naam ndio mimi!’’
Nilimjibu bila kuonesha woga wowote lakini moyo ulikuwa hauna nguvu huku mdomo ukinitetemeka kwa hofu.
‘’Kwanza samahani sana kwa kukupotezea muda. Lakini bado kuna dakika thelathini ndio ndege iondoke usijali kwa hilo utaondoka tu!’’
Nikashusha pumzi na kuwa na uhakika wa safari sasa nikajiweka sawa huku nikishika shika kitumbo changu kilichokuwa na mimba kama ya miezi minne na nusu hivi.
‘’Mimi ni askari mpelelezi siku nyingi na mara nyingi huwa napewa kazi ya kukagua pasipoti za watu hapa! Pasipoti yako kwanza imenitisha sana na nimekuwa na wasiwasi mkubwa juu ya hilo!"
Akazidi kunichanganya huku akiniacha nisielewe anamaanisha nini?
‘’Niambie ukweli wako kutoka moyoni nami nitaweza kukusaidia!’’
‘’Ukweli gani huo tena?’’
‘’Ulishawahi kufungwa gerezani Levina?’’
Aliposema hivyo nikaanza kuingiwa na woga zaidi lakini nikajiamini..!"
‘’Ndio wakati mtoto nilihukumiwa kifungo!’’
‘’...Hapo hapo nikashangaa yule askari akinikumbatia na kisha akatoa Machozi.
‘’...Nakupenda sana mdogo wangu, mimi naitwa Magdalena Christian au Mage kama walivyonizoea hapa, na mimi ni Dada yako kabisa wa damu japo Mama alinitelekeza nikiwa mdogo sana nikiwa na miaka minne tu, niliokotwa na wasamalia wema na kunipeleka kituo cha Watoto yatima (Mam`s orphans) hadi nilipofikia miaka saba nikampata mtu wa kunisomesha na kuniendeleza nililelewa na kusomeshwa na Mzungu ( Mark Lowlery ) anayeishi hukoo Canada kwa sasa lakini amenisaidia na anaendelea kunisaidia na huwa nawasiliana naye karibu kila siku mpaka hivi sasa, na hata Canada huwa naenda kila baada ya miezi miwili na yeye huwa anakuja hapa. Nilijitahdi kusoma mpaka nikapata kazi hii,
"Aaaaaaah My God! Kumbe nina Dada?"
"Yeah, ndio mimi Dada yako 'Mage' kupitia kazi niliyonayo nilikutafuta kwa muda mrefu bila ya mafanikio Mpaka niliposikia ulikuwa Jela, bado nikawa siamini kama ni wewe."
‘’Nilikuwa ni Mimi Dada!’’
‘’Jamani marehemu Baba tulishamzika siku nyingi sana! Vipi Mama yangu mzima uko?’’
Huku akitoa machozi yalionifanya nisisimke na mchozi kuanza kudondoka taratibu.,
‘’Mama mzima yupo nimemuacha na rafiki yangu Jammy!’’
"Nilisikia kuwa ulitoka pale gerezani na rafiki yako sijui anaitwa 'Pendo'?
‘’Ndio Dada nilitoka naye tukapata lifti then tulitekwa tukakimbilia msituni tukapoteana.
‘’Pole sana mdogo wangu vipi na Morogoro ulifuata nini tena?”
“ Morogoro nilienda kwa ndugu yake na Rafiki yangu anaitwa Baba Ali”
“ulishawahi kulala pale?’’
Sikuwa na wasiwasi wowote kwani nilijivunia niko na Dada yangu tena wa damu hivyo nilimjibu vyovyote kwa kujiamini.
“Nililala pale kwa 'Baba Ali' kesho yake nikaondoka nakuja Dar’’.
‘’Levina mdogo wangu?’’
‘’Abeee Dada Mage!"
‘’Poleee sana nasasa ndio unaelekea kuozea gerezani!
Nakuomba tena haraka sana unipe tiketi na Pasipoti yako na kuanzia sasa upo chini ya ulinzi"
‘’Vipi tena Dada Mage? Si umesema wewe ni Dada yangu wadamu?"
“Unahadhi ya kuwa na Dada kama mimi? Embu angalia!"
Akachomoa kitambulisho chake cha kazi na kunioneshea. Maskini kumbe alikuwa haitwi Mage, jina lake ni Gracia.
‘’Ooooh! My God! Nimekwisha Levina mimi nateketea sasa,
alichukuwa pingu zake na kunifunga?
“Twende Polisi mbwa wee. Damu nzito kuliko Maji na leo ndio utaeleza Mauaji yako ulioyafanya?’’
Maskini kumbe alikuwa haitwi Mage,jina lake ni Gracia.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment