Search This Blog

Friday, July 15, 2022

KICHAA - 1

 







    IMEANDIKWA NA : ZUBERY R. MAVUGO



    *********************************************************************************



    Simulizi : Kichaa

    Sehemu Ya Kwanza (1)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Njaa, iliendelea kulisumbua tumbo lake na kumpelekea kuanza kujipitisha maeneo ya ma'ntilie, huku akiamini kuwa shibe yake ipo mikononi mwao.



    "mmh, mmh, mmh, puu. Lalalalala. Toka! Hebu tutolee kichefu chefu hapa," Ni baada ya mtu huyo kufika kwenye moja kati ya migahawa ipatikanayo maeneo ya Igoma ndani ya jiji la Mwanza, sauti moja ya mwanamama muuza mgahawa ndio iliyatoa maneno hayo yenye kuonesha kukereka kwa uwepo wa mtu fulani maeneo yale.



    "Bado hunisikii. Eti, eee," Alibwata tena, huku mate yake yakishindwa kujizuia kubakia mdomoni na kujikuta yaki mwaga cheche zilizokuwa zikimfuata kijana ambae maneno hayo yalimuhusu yeye. Kijana yule ni kama hakuwa mwenye kusikia maneno yale, si.. Kwamba hana masikio. Laa! Hasha, bali pindi yalipomfikia yalipita sikio moja na kuelekea jingine.



    "We.. Kichaa, unajifanya hausikii, si,ndio? Mnatoka huko makwenu mmefanya uchawi au kuiba mmelogwa halafu mnakuja mjini kuwa kero kwetu. Hebu toka, kabla sijakufanyia kitu kibaya." Mama yule aliendelea kumfukuza yule kijana kwa maneno lakini ndio kwanza kijana yule aliendelea kutabasamu huku meno yake machafu yakipata ruksa ya kuonekana maeneo yale.



    "Anhaa! Kumbe unanicheka eti ee! Kwahiyo hapa nafanya upuuzi. Ngoja nikuoneshe," Aliongea mama yule huku miko yake akiwa ameiweka kwenye kiuno chake ambacho amekipiga kanga nzuri yenye maandishi ya bezo.



    "Asia?," Aliita mama yule na baada ya yule muitwaji kuitika. Akasema, "Niletee hilo sufuria lenye maji ya moto hapa. Nataka ni muoneshe huyu mbwa," Asia, alitii amri na kuleta sufuria hilo. Kwa kuwa lilikuwa la moto, alishindwa kulibeba bila kuweka kitu cha kuzuia hali ile. Aliamua kuchana boksi na kulitengeneza vizuri kisha akalishikamanisha na sufuria lile, baada ya hapo akaliinua na kumpelekea Mama yule.



    "Mwanaharamu mkubwa wewe. Unataka kuleta gundu mida hii.. Mbwa wewe." Alitamka maneno yale, kisha akayasindikiza maneno yake na maji ya moto yaliyompata vilivyo kijana yule.



    Masikini, kijana yule, aliangua kilio kama cha mbwa mwizi. Sasa alishindwa kustahimili maumivu aliyonayo na kujikuta akikimbia hovyo mfano wa mbwa aliepigwa jiwe la kichwa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Hicho ndicho chakula chako. Mbwa mkubwa we... Na bado, allaaa!! Ukichaa peleka milembe, mjini kila mtu yupo timamu bwana." Maneno yale ya bila huruma ya ubinadamu yaliendelea kutoka mdomoni kwa mama yule bila hata haya. Aliendelea kujisifu kwa kuhisi amemkomesha binadamu mwenzake na kusema.



    "Hatorudia tena. Wewe mbwa mwenyewe ukimwagia maji kiasi hicho, harudi tena. Ije yeye binadamu? Na akirudi basi atakuwa na roho ya paka. Halo, halo. Analeta ujiwe mbele ya nyundo. He,he,he,he. Ndo.. Basi tena." Baada ya kutamba kwa maneno yake pamoja na vidole vyake alivyovichezesha huku mkono mmoja akiwa kauweka kiunoni. Alirudi na sufuria lake ndani ya mgahawa huo, kisha akateka maji ya mengine na kuyachemsha.



    "Mamaaa! Mammaaa! Nakufa! Nakufaaa. Yalaaaa!" Kijana yule alipiga kelele za uchungu wa maumivu huku akiendelea kukimbia hovyo bila kujielewa. Ingawa alikuwa na minywele mingi iliyochakaa, ngozi yenye ukurutu uliokomaa nakuwa kama machacha, ngozi hiyo ilifunikwa na madaso ambayo zamani yalikuwa nguo. Madaso hayo, yalichanika kila mahali, kwa harakaharaka usingeshindwa kumuita kichaa mtu yule, maana hata usowake, ulipambwa na poda ya jalala aina ya majivu, pamoja na mafuta ya oil.



    Naam, alikuwa ni kichaa. Nadhani hata mama yule aliempa adhabu hiyo ya maji ya moto. Alimpa kwa sababu alijua kijana yule ni kichaa. Akashtaki wapi wakati Mahakama yake ni jalala? Akamlilie nani wakati wazazi wake ni mbwa wapatikanao mtaani? Nani wakumsaidia kijana huyo ambae hata hatathamani.



    Ni njaa pekee ndiyo iliyompelekea kufanyiwa hivyo. Wakati wewe ukisikia njaa unakimbia mapema nyumbani kwako na kupata chakula, au unaenda mgahawani. Kumbe kuna wengine wanapata adhabu ya kuunguzwa na kutengenezewa majiraha kisa njaa zao.



    Masikini, kijana yule aliendelea kukimbia huku maji yale yakiwa yameachia hatamu ya umoto na kusababisha maumivu yasiyo mithilika. Hapohapo jiraha kubwa lililoambatana na uvimbe kutokana na kuunguzwa kwa maji lilijijenga kuanzia, mkono wakushoto, ubavuni hadi mguuni. Aliendelea kukimbia hivyohivyo huku akiita neno 'MAMAA' na wala mama yake asije.



    Wengi waliomuöna barabarani walimzomea wengine wa kimcheka na kumthihaki, huku wachache wakimtumia kwenye mada zao. Hakuna hata mmoja aliemsaidia kichaa yule japokuwa alikuwa akiomba msaada.



    Alikimbia na kwenda kujitupa jalalani. Hakuwa na mahala pengine pakujisitili zaidi ya jalalani. Huko akakutana na watoto ambao nao walivalia madaso kama yeye huku wakiokota vyuma chakavu, pamoja na kina mama waliochafuka kwa kutafuta chakula ambacho hutupwa jalalani hapo. Watu wale masikini ndio walikuwa msaada wake, walimfuata na kumbeba, ingawa kila walipomvuta nguo, waliishia kubakiwa na kipande cha nguo hiyo kutokana na kuisha kwake. Lakini hilo halikuwafanya waache kumbeba na kumsogeza pembezoni mwa jalala lile.



    Walipomsogeza pembeni, mapema tu wakaanza kumpatia huduma ya kwanza ya kishamba. Bora wangekuwa na asali ilikumpaka huenda ingesaidia, hawakuwa na dawa yeyote zaidi ya mchanga uliopatikana maeneo yale ya jalala. Walimpakaa mchanga ule wenye chembechembe za uchafu kisha wakamuhitaji apumzike iliasiendelee kuyahisi zaidi maumivu.



    "Mpumzishe kwa lazima." Aliongea mama mmoja aliekuwa amesimama huku akiendelea kukiadhibu kichwa chake kwa kukikuta kutokana na muwasho aliokuwa akiupata;muwasho wa mmba pamoja na chawa katili.



    "Sawa, maana inabidi apumzike tu." Alijibu mama mwingine ambae yeye alikuwa bize na kufukuza inzi maeneo ya kidonda. Kisha mama yule akaiacha kazi ile kwa nukta, na kupeleka mkono wake hadi kwa maeneo ya shingoni mwa kichaa yule ambae sasa alikuwa akipiga mikono yake chini pamoja na paji lake ilikupolea maumivu kama alivyodhani. Mama yule, aliigusa gusu shingo ya kichaa yule iliyojaaliwa ukurutu mgumu, na nikama alikuwa akitafuta mshipa fulani. Hata alipoupata aliuzimisha kiustadi wa hali ya juu na palepale kichaa yule alipoteza fahamu.



    Ingawa njia ile ina madhara, lakini ndio njia pekee iliyopatikana kwao. Hawakuweza kumpeleka mgonjwa hosipitali akachomwe sindano ya ganzi iliasihisi uchungu au sindano ya usingizi kutokana na kutokuwa na pesa. Walilitambua hilo na walijua wazi hata kama wangempeleka hospitali, asingepata msaada wa aina yoyote ile zaidi ya kuangaliwa kwenye benchi kwa kebehi kama inzi mla mavi. Kwao, waliona njia pekee ya kutuliza maumivu ni kumfanya mgonjwa azimie kwa muda. Kumbe wakati wewe unapopata jiraha na kupigwa ganzi, au sindano ya usingizi. Kuna wengine ambao hata hiyo sindano hawaipati badala yake wanapata nyenzo za hatari.



    "...we mama, leta hiyo siso kabla sijakuharibia hapa." Ni sauti ya ukali iliyotoka kinywani mwa mtoto mwenye umri wa miaka kumi na nne, maeneo ya jalala hilo. Sauti hiyo isiyojali utofauti wa miaka iliendelea kukoroma. Mama alieambiwa atoe chuma chakavu, alionesha kama kutosikia sauti ile ya dharau tena ukizingatia mtoaji wa sauti ile ni mtoto ambae anauwezo mkubwa sana wa kumzaa. Alifikiria endapo atampa chuma kile chakavu basi ataikosa pesa il-hali nae anashida chungu nzima, hivyo aliona uamuzi wa yeye kuwa nunda ndio pekee utamsaidia mbele ya mtoto yule.



    "..we maza nunda sio? Nakwambia leta hapa hiyo siso." Aliendelea kutoa amri mtoto yule utadhani anaongea na mtoto mwenzake kumbe ni mama mzima. Mtoto yule alikuwa ana ngozi chafu iliyojaa ukurutu;ngozi ambayo hakuivika shati kutokana na ukosekanaji wa mashati juu ya hali duni aliyonayo. Huku chini akiwa amevaa kaptula iliyotoboka na kupelekea makalio yake yaliyopauka na kupata sugu kutokana na kukaliwa bila heshima yaonekane vilivyo pasina uficho.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "We... Mtoto wa mbwa, hebu kuwa na adabu pamoja na heshma. Wakubwa husalimiwa mjinga wewe, na sio kutolewa amri za siso tu." Aliongea mama yule kauli iliyohifadhi hasira za wazi juu ya kuchukia amri za mtoto yule mdogo ambae kwa kumuangalia tu. Anashindwa hata kumfananisha na watoto wake kutokana na umri mdogo alionao.



    "Afu.. We, maza takuharibia sasa hivi. We sema kama hutaki kunipa hiyo siso uone kama siichukui kwa nguvu. Heshima unaijua wewe? Kama ungekuwa na heshima ungekuja huku jalalani? Acha ujinga. Wenye heshima na adabu wapo majumbani kwao wakipikia waume zao na kuosha watoto wao. Wewe upo huku jalalani halafu unaitaji heshima, sijui adabu. Hebu lete hiyo siso, mpuuzi mkubwa."



    Mtoto yule alimkwapua mama kile chuma chakavu, kwa kuwa mama yule hakukubaliana na ile hali ya kunyakuliwa kirahisi chuma ambacho angekiuza na kupata pesa. Ndipo alipoamua kumvaa mtoto yule na kumng'ata vilivyo maeneo ya tumboni kwa kutumia meno yake yasioujua mswaki badala yake yanakijua chakula chajalala. Chakula ambacho kina bakteria waliojificha na wanaoonekana bila hata hadubini.



    "Unaning'ata. Ayaah! Niachie mbwa wewe." Alibwata mtoto yule baada ya meno ya mama kuzama vilivyo kwenye ngozi yatumbo lake. Mama yule alisikia kilio cha mtoto yule, lakini hakini hakuhtaji kumuachia mpaka hapo atakapo hakikisha karejeshewa chuma chake iliakauze na kupata pesa.

    Hapo mtoto yule akajihami kwa kumpiga mama yule na kile chuma kichwani. Kitendo kile kilimpelekea yule mama kuanguka chini huku damu nyingi zikimtoka na palepale alipoteza maisha.



    Hakuna aliebaki maeneo ya jalala lile. Si, wakinamama waliokuwa wakimsaidia kichaa pembezoni mwa jalala, wala machokoraa waliokuwa wakijitafutia riziki. Wote walikimbia ilikuepuka kubambikiziwa kesi na maafande. Hata yule mtoto nae alitimka. Hapo ulibaki mwili wa mama yule. Pamoja na kichaa aliekuwa pembezoni.



    Masaa kadhaa yalipita, hatimae yule kichaa alizinduka, kumbe muda huo ndio maafande walikuwa wanafika kwenye eneo la tukio. Walimbeba mama yule na kumbwaga kwenye gari kisha wakamchukua yule kichaa yule na kumsukumia ndani ya gari bila kujali jeraha lake.



    "Afande, huyu mjinga ndio tuna mbebesha kesi ya mauaji." Aliongea afande mmoja.





    "Huyu lazma itaijibu serikali, kwanini ameua." Alipokeza afande mwingine. Kisha maafande hao wakaingia wote kwa pamoja ndani ya gari.



    Yule kichaa alisikilizia maumivu maradufu ya alivyo yapata kabla, kusukumwa na maafande wale kulimpelekea yeye kutonesha jeraha lake na kuyahisi maumivu makali yasiyo na ganzi. Alipiga ukelele kila maumivu yalivyozidi kuongezeka.



    Maafande wale walipata kero kutokana na makelele ya kichaa yule kufuatia maumivu aliyokuwa akiyapata. Hakuna kati yao aliyoyajali maumivu yake pamoja na ndonda ambalolilianza kutoa majimaji na damu, bali waliishia kukereka na sauti ya maumivu ya kichaa yule.



    "Kimya! Allaaa! Nani unaemuimbia huo wimbo wako?" ni sauti kutoka kwa afande. Sauti iliyoambatana na rungu kali lililotua kwenye ugoko wa kichaa yule. Hakika aliyahisi maumivu mengine ambayo hakuwahi kuyawazia.



    Badala apunguze kilio, hapo aliongeza na kupigwa rungu la kwenye goti, alipolia tena alishushiwa moja la kichwa na hapohapo akazimia.



    Maafande wale wasio na huruma walianza kujipongeza kwa kazi ya kudhibiti ukelele wa kichaa kwa kumpiga hadi akazimia. Kisha kwa mbwembwe wakawasha gari lao na kuianza safari ya kuelekea kituoni.



    Ni barabara ya buzuruga. Gari moja kubwa la mizigo lilionekana kukatiza eneo lile, kutoka maeneo ya mabatini na kuelekea maeneo ya igoma. Maafande wale ambao hawakuwa makini katika uendeshaji wao waliweza kukumbana nalo mbele hatua kadhaa. Kabla hawajagongana dereva wa maafande alilipiga kona gari lake na kulielekeza upande wa raia waliotembea kwa miguu, ileanatafuta breki kabla hata hajapiga alimgonga mpita njia mmoja na kumsababishia kifo palepale. Breki zilikubali huku damu za mpita njia huyo zikikipamba kioo cha gari la maafande.



    Raia wenye hasira kali waliifuata gari hiyo na kuiadhibu kwa mawe. Huku wakihitaji kuwashusha maafande waliokuwamo ndani ya gari lile.



    Walifanikiwa kuwatoa maafande wale na kuwaadhibu huku nyuma nako walimvuta yule kichaa na kumjumuisha kwenye mkumbo huo wa kipigo. Hazikupita hata dakika tano gari jingine la maafande lilifika maeneo yale na walioshuka walitawanya raia kwa kupiga risasi juu. Kisha kuwaokoa waliokuwa wakipigwa na raia wenye hasira kali.



    Walimchukua tena kichaa yule nakumpeleka hosipitali pamoja na wale maafande wengine kufuatia kipigo cha raia.



    "Hakikisheni mnafanya juhudi zenu zote ili huyo kichaa apone."



    "Usijali, tupo kwa ajili hiyo. Chamsingi ni nyie kutulia tu."



    "yaani, dokta hakikisha unatumia uwezo wa hali ya juu maana serikali ina muhitaji sana huyo, na ndio mtuhumiwa wa kesi ya mauaji ya watu wawili."



    "Usijali."



    walikaa kusubiria hali ya kichaa yule ilivyoendelea na hiyo ni baada ya maiti ya yule mama pamoja na yule aliegongwa gari na maafande kupelekwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti kwa ajili ya upelelezi. Waliendelea kusubiri huku wakiomba kichaa yule apone.



    "Huyu, inabidi tujitahidi hata kuhonga iliatibiwe kwa taaluma ya juu maana akifa tu. Hakuna muda wa kuanza kupeleleza wahalifu, chamsingi huyu tunampa kesi za mauaji ya watu wawili." aliongea afande kipara huku akisikilizwa kwa umakini na wenzake watatu.

    Palepale maafande wale walihamaki, na hiyo nibaada ya mlango aliyomo kichaa yule kufunguliwa na kutoka daktari.



    "Dokta, anaendel..."



    "Njooni ofisini."



    walimfuata huku pumzi zao zikiwa juu juu na mapigo ya moyo kuwaenda kasi utadhani wamepewa taarifa za msiba.



    Dokta aliwaambia kuwa mgonjwa wao, hali yake bado tete na mpaka muda huo hakuwa amezinduka. Akawapa ruhusa wakaendelee na kazi kisha watarudi jioni.



    Waliafiki kisha wakarejea kituoni kwao pamoja na wale maafande ambao walipata majiraha lakini hawakuumia kufuatia hasira za wananchi.



    Walipofika tu. Cha kwanza walifungua faili la kesi ya mauaji.



    "Huyo mpuuzi lazma ashughulikie kesi zote. Chamuhimu ni yeye kupona tu. Sisi ndio maasikari wa nchi hii. Naipenda nchi yangu kwa sababu inanipa uhuru wa kukaa juu ya sheria hata kama na makosa. Sawa nyie ndio mmegonga hadi mkaua ila kesi lazma imuangukie huyo mjinga, hata yule sijui mama aliekufa kwa jalala, mjinga huyu ndie atatueleza kwanini amemuua. Lazma akubali labda kama sina kofia ya uafande nja gwanda la uafande." Aliongea afande kipara huku akimsimamia yule mwenye jukumu la kuandika faili la kesi.



    "Mtu mwenyewe hana muelekeo wa kimaisha. Bora tumuokoe kwa kwenda kunyongwa au kufungwa kifungo cha maisha. Ale bure alale bure, avae bure, tena bila kufanya kazi ngumu. Huoni kama tumemuokoa na maisha ya jalalani." Aliongea afande Dani na kuwafanya wenzake kuangua kicheko.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Raia waliishia kunong'ona juu ya uonevu waliofanyiwa na kulalamikia jeshi la polisi lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa zaidi ya jambo hilo kuongelewa rediöni tena mara moja tu.



    Ilipofika majira ya saa moja usiku. Wale maafande walirudi hosipitali kwa ajili ya kujua hali ya mtuhumiwa.



    kama hakuna uthibitisho basi yule aliekamatwa huitwa mshukiwa. Lakini maafande hawa walimpa jina la mtuhumiwa.



    . Walionana na daktari kisha akawapatia maendeleo ya mgonjwa wao na kuwahitaji waendelee kuwa na subra. Hawakuwa na jinsi maafande wale zaidi ya kuondoka, lakini walimsihi daktari ajitahidi kuhakikisha mgonjwa anapona kwa gharama yeyote ile.



    Walirudi mpaka kwenye kituo chao, baadhi yao walilala humohumo. Huku wengine wakiendelea kuburudika na vileo pasina kujali kofia na mikanda ya jamuhuri.



    "Afande.. Afande.. Naombeni msaada. Wanamuua mdogo wangu." Ni sauti ya binti mmoja mwenye umri wa miaka kumi na sita, sauti hiyo iliambatana na nukta za mihemo kutokana na mbio alizotoka nazo binti yule. Ukimuangalia, hutotamani kurudia tena kutokana na uchafu uliomjaa kwanzia usoni hadi kwenye mafundo ya miguu. Kuachilia mbali nguo zake ambazo zilitia kinyaa kutokana na kuanguka mara kadhaa kwenye mitaro ya maji machafu na kuzalisha harufu kali,lililoshindwa kustahimili pua za maafande. Vilevile, binti yule alinuka jasho pamoja na uchafu wa kike kutokana na kushindwa kujitunza. Si kwasababu hapendi, bali ni kutokana na kukosa matunzo. Kama usipoisikia sauti yake basi lazma uwe na mashaka usijue huyo binti ni msichana au mvulana.



    "Wewe chokoraa! Hebu kuwa naadabu."



    "Hapana, afande. Mdogo wangu wanamuua tafadhali naombeni msaada." Aliongea binti yule kwa sauti kavu, ambayo hata kutoka ilitoka kwa shida. Maafande wale kwao waliona ni kama kero kwani walikuwa bize na mambo yao. Halafu ukizingatia binti yule alikuwa ni chokoraa.



    Binti yule hakuchoka aliendelea kuomba. Sasa alishuka hadi chini na kupiga magoti huku akiishikiria yunifomu ya afande kipara na kumuomba.



    "Hebu toa uchafu hapaa! Mwanaharamu mkubwa. Nenda kamshike mama ako mavazi yake nasio kunichafulia gwanda langu la jamuhuri kwa harufu yako." Alifoka afande kipara huku kauli yake akiisindikiza na msukumo wa mguu uliomtoa binti yule na kumtupa pembeni.



    Masikini, binti yule chokoraa, alivyosukumwa kumbe alijibamiza. Tayari damu zikawa zinamchuruzika. Alianza kulia na kukata tamaa. Lakini alipokumbuka kuwa msaada pekee ni mapolisi. Hakuishia hapo, aliendelea kuwaomba hivyohivyo. Sasa afande kipara alichukia zaidi na kufungua mkanda wake kisha akamsogelea binti yule. Palepale akautua maungoni mwa binti yule. Kujigaragaza na kutoa ukelele wa majonzi ndivyo vilivyoashiria maumivu ya binti yule. Hapo kipara akamvutashati binti yule nakujikuta akibakiwa na kipande cha daso kutokana na kuisha kwa nguo ya yule binti.



    "Haa! Kumbe wewe ni wakike?" Alishangaa kwa swali kichaa yule. Nahiyo nibaada ya shati labinti kuchanika na kuzifanya chuchu zake zilizosimama kuonekana machoni mwa kipara. Hapo yule binti akaona aibu nakuanza kuficha maeneo ya maungo yake, lakini tayari alichelewa kwani maafande wote tayari walishayaona maungo yake mazuri na yenye kupendeza.



    "Yaani. Mie, nihangaike usiku kutoa pesa kwa malaya wakati nyie wa bure mpo! Tena mnafaa kuliko hata wale malaya." Aliongea afande kipara. Bila hata aibu kwa binti yule ambae asingeshindwa kumtofautisha na mwanae, huku wenzake wakimpongeza na kumpa hongera kwa mbuzi kufia buchani.



    Alitoa, amri binti yule abebwe na kuingizwa sero kisha akamfuata humo humo na kumuingilia binti yule bila hata kujali picha ya raisi wa jamuhuri ambayo ilikuwa juu ya ukuta wa kituo. Alimtoa ubikira binti yule, na kumfanyia yale yote ilhali anajua wazi kuwa yeye ni muathirika wa virusi vya ukimwi. Ambavyo alivipata miaka kadhaa iliyopita.



    Binti yule alishindwa kuvumilia aibu ile, alishindwa afiche damu, afiche sura, au chuchu zake iliaendelee kujenga mjengo waheshima. Kutokana na kuingiliwa bila ridhaa yake alijikuta akiumia sana na kichwa kilimgonga hadi kuzimia. Maafande wale walimchukua na kumuweka kwenye gari lao ambalo wamelipewa na serikali kutokana na makato ya mishahara ya wananchi walipiao kodi. Bila kujali hilo, waliyatumia mafuta ya gari lile, mafuta ambayo ukiyatathmini ni pesa za wananchi wa kipato cha chini, na kisha wakaenda kumtupa binti yule pembezoni mwa mto wa mchafu kuoga. Masikini binti yule, alifanyiwa yale kutokana na kudhani haki ipo kituoni. Sasa hakujua kama mdogo wake atakuwa hai au ameshauawa.



    Maafande wale, walimuacha yule binti maeneo ya hatari kama yale, kisha moja kwa moja wakarejea kituoni kwao na kuendeleza mambo yao. Wakasahau hitaji la binti yule, wakasahau shtaka lake, na maumivu aliyokuja nayo.



    Kipara alianza kuwahadithia wenzake utamu alioupata, kipindi anafanya ufirauni wake na wenzake walicheka kila alipoweka nukta. Waliendelea kujadili juu ya upuuzi wao mbele ya picha kubwa iliyokuwa maeneo yale. Picha ya rais wa Tanzania.



    Huku nako binti yule waliomtupa, alipatafahamu na kuhtaji kuinuka kwenda kumsaidia ndugu yake lakini alijishangaa baada ya kukabiliwa na maumivu ya kichwa, aliendelea kujikaza kila alipokumbuka adha aipatayo mdogo wake. Lakini alikumbana na mkinzano wa maumivu makali sehemu zote za mwili wake hasa sehemu zake za siri. Ndipo aliporudisha kumbukumbu kuwa alikuwa amebakwa.



    . Binti yule, hakuwa na uwezo wa kuamka kutokana na maumivu aliyo yapata. Alitamani apate msaada wa kwake, lakini hakuna aliemjali. Kila alipomkumbuka mdogo wake, akakumbuka unyama wa mapolisi. Aliishia kuendelea kulia.



    Nyanyuka nenda kapambane, hata ukikaa na kulia hakuna msaada utakaokuijia. Jikaze wewe ni mwanamke wa shoka. Ni sauti iliyomuijia binti yule ndani ya nafsi yake na kumpa ujasiri wa hali ya juu. Aliinuka kwa kujipepesua hivyohivyo, taratibu akajisogeza kwenye mto ule ujulikanao kama mchafu kuoga. Mto upatikanao maeneo ya buzuruga. Akanawa uso wake, na akavua madaso yake kisha akaoga maji yale machafu, ilikuondoa damu zilizomuenea kisha akayafua madaso yake na kuyavaa kwa mara nyingine. Hapo sasa akaanza kutembea kutokea buzuruga mpaka maeneo ya mabatini kwa ndani ndani. Ndipo alipokatiza sehemu na kukuta watu wamejaa. Nywele zilimsisimka na kuingiwa na uoga. Aliamua kwenda kutazama nini kilichowajaza watu wale. Hakuyaamini macho yake baada ya kukuta mwili wa mtoto umefunikwa shuka jeupe na kuachiwa maeneo ya kichwani kwa ajili ya kutambuliwa.



    Aliangua kilio cha hasira lakini hakuwa na jinsi mdogo wake tayari alikuwa amekwisha fariki. Wananchi walimsaidia na kwapamoja wakazika.



    Upande wa hosipitali mgonjwa aliendelea vizuri na hata zilipopita wiki mbili. Hapo maafande walipatiwa mtuhumiwa wao na kumpeleka moja kwa moja, mahabusu.



    Masikini, walimuadhibu kichaa yule pasina kujali hali aliyokuwa nayo. Walichukuwa plaizi na kumfinya sehemu mbalimbali za mwili wake huku wakimng'ang'aniza akili kufanya mauaji.

    Kichaa yule alishindwa kuvumilia maumivu makali kama yale. Aliamua kukubali kuwa yeye ndie aliemuua yule mama kule jalalani, na yeye ndie aliemgonga yule mtu na gari, hali yakuwa ukweli unajulikana kuwa mapolisi ndio walimgonga na gari yule mtu.



    Alipokubali kukili ndipo wakamrudisha mahabusu ilikusubiria siku ya kesi mahakamani.



    Upande wa yule binti, hali yake ilizidi kuwa dhoofu. Kila alipopita hakuwa na msaada na wala hakutamani kuomba msaada. Upungufu wa damu katika hospitali ya bugando ndio ulimfanya nae akajitolee damu iliangalau apate kuokoa maisha ya watu kutokana na kushindwa kuokoa ya ndugu yake. Hakuiona thamani yake katika hii dunia, alitamani ardhi ipasuke na aingie ndani yake lakini kwa muda huo ardhi haikufanya alichohtaji.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Samahani dada. Damu yako inaonesha wazi kuwa wewe ni muathirika wa virusi vya ukimwi. Hivyo haiwezekani kuwekwa katika mwili wa binadamu mwenzako." Ni maneno ya daktari aliewachukuwa vipimo wote walioenda kujitolea kwa hiyari damu zao.



    Binti, alichoka. Palepale alianguka chini na kuzimia. Alikaa masaa kadhaa ndipo alipozinduka.



    Aliwakumbuka wazazi wake walivyo mpenda yeye na mdogo wake, akaikumbuka ajali ya M.V, bukoba iliyowatenganisha wao na wazazi wao. Akakumbuka jinsi walivyolifakamia jiji la mwanza kama watoto wa mtaani kutokana na kukosa msaada. Akakumbuka siku ambayo alivamiwa na watoto wa wakoma na kuhtaji kumuingilia kwa lazma. Siku hiyo inamuuma sana maana ndiyo iliyomfanya ampoteze mdogo wake wapekee pale mdogo wake alipoingilia ilikumkinga dada yake asibakwe. Watoto wa wakoma walimuacha kwanza dada mtu na kumfuata mdogo mtu na kuanza kumshushia kipigo pamoja na kumshambulia kwa nyembe zao.



    Akakumbuka pia pale alipopata akili ya kwenda kutafuta msaada kituoni. Palepale alinyanyuka kwa hasira. Ingawa alikuwa na maumivu, lakini alitembea utadhani hana maumivu. Alipita sehemu na kukutana na muuzaji wa genge. Aliazima kisu kisha akaenda moja kwa moja hadi kituoni.



    Alimkuta afande kipara peke yake. Pamoja na yule mtu asiejielewa(Kichaa). Alipofika, alipokelewa kwa dharau na maneno ya kashfa. Kitendo bila kupoteza muda alimchoma kisu Afande kipara. Alimtoboa toboa mara kadhaa, kiasi cha yeye kujawa na damu. Maeneo yote ya mwili.



    "Dada, umeua?" Ni sauti ya kichaa yule.



    "Ndio, nimeua naninahitaji kufia gerezani. Sioni haja ya kukaa na mateso ambayo hayana hukumu. Bora nikahukumiwe huko na nife kifo kizuri cha kunyongwa. Nahitaji kufa, nifunge pingu na uniweke mahabusu, usihofu. Mahakamani nitakili ufanyaji wa tukio hili na wewe sitokufanya chochote bali utakuwa shahidi wa kesi hii ya mauaji." Aliongea binti yule maneno ya ukali. Huku akidhihirisha wazi kutokuogopa lolote litakalomkuta.



    "Una umri mdogo sana. Hufai kufungwa. Nenda kimbia kabisa wala usiwahi onekana machoni mwangu. Bado unahitaji kukamilisha ndoto zako. Usinione kichaa ukadhani sipo timamu. Leta hicho kisu kisha utoweke maeneo haya kabla haujakutwa hapa." Aliongea kichaa yule, maneno yaliyomfanya hadi binti yule ashangae sana.



    "Hapana, nilipouhitaji msaada, haukuja. Leo, siuhitaji ndio ujilete. Kaka umechelewa kunisaidia, nimedharirika, nimenyanyasika. Hadi nimeambukizwa virusi vya ukimwi. Ndugu yangu amefariki kisa haki yangu, mimi nimeharibiwa maisha kisa kutafuta haki. Sioni haja ya kuishi bora nikanyongwe iliniende huko haki ilipo. Sitaki nikuingize kwenye matatizo kaka yangu." Aliongea binti yule.





     Binti yule aliendelea kulalamika na alichohtaji kwa mda huo ni kunyongwa tu.



    "Dada yangu, hii dunia imebeba mengi na yenyekujificha machoni mwa watoto wa dogo. Kadri unavyozidi kukuwa ndivyo unavyozidi kuyaona. Huna haja ya kuamua maamuzi ya mbali wakati hauyajui hata ya kesho. Bado unahaja ya kuyaona ya duniani iliupate kujifunza, nakuomba nipatie hicho kisu kisha utoweke hapa." Aliongea kichaa huku akipeleka mkono wake kupokea kisu ambacho kimeng'ang'aniwa na dada yule.



    "Kaka, yadunia yanaumiza sana. Yameshanichosha. Bora nife, dunia gani hii iliyojivika ngozi ya simba, dunia inayomuwinda masikini utadhani swala porini. Hata kama nikiendelea kuishi nitaenda wapi mimi? Hakuna! Hakuna! Mama, baba, mdogo wangu wamesha tangulia kule haki ilipo. Na uhakika wameniandalia makazi mema na sasa wako wananisubiri."



    "Usiwe mdhaifu hali yakuwa wewe ni msichana. Wanawake huvumilia magumu na mepesi, mengi na machache. Na wako radhi wavuke mabonde na milima ya shida. Hautokuwa mwanamke jasiri kama unaogopa yaliyomo kwenye hii dunia. Naitwa MAVUGO." Aliongea maneno yale yaliyomfanya yule binti akose nguvu za kukishikiria kisu na hapo ndipo kichaa yule alipokinyakua.



    "Nashukuru sana kwa kuniokoa. Nitakukumbuka milele, sitoacha kulitaja jina lako. Mimi naitwa.. Aisha Mapuya. Nashukuru sana kaka yangu." Aliongea binti yule huku machozi yakimtoka.



    "Milima inatabia ya kukaa sehemu moja, lakini binadamu hana tabia hiyo. Ndio maana wanasema 'Milima haikutani binadamu huk..."Kabla hata hajamalizia kauli yake, ving'ora vilisikika kwa mbali na wakagundua wazi kuwa maafande wanakuja.



    "Kimbia.. Pita huku.. Mungu akuongoze." Ni sauti ya kichaa yule aliejitambulisha kwa jina la Mavugo.



    Binti yule, alimuangalia sana kichaa yule na alikalili alama kutoka kwa kichaa yule kisha akamuaga na kutimka.



    Ile ameondoka tu. Palepale maafande wakawa wamefika. Hawakuamini baada ya kumkuta mkubwa wao amelala chini huku majiraha yaliyoonekana vizuri kwenye mwili wake. Yakiwachekea na kuwadhihaki. Walipo tupa macho yao pembeni walimuona kichaa ameshikiria kisu chenye damu.



    Walijiuliza maswali mengi ya siyo na majibu kuhusu kichaa yule alipopatia kisu kile, na alitokaje mahabusu hadi kuua.



    Alipoona wamemkodolea sana macho, alikitupa kisu kile na kunyoosha mikono juu kamaishara ya kujisalimisha mbele ya maafande wale.



    Walimpokea, na kumdunda vilivyoutadhani hukumu imeshatolewa mahakamani.



    Hapo sasa kichaa yule akawa na kesi tatu za mauaji. Alipelekwa mahakamani na kesi yake ilikuwa ngumu sana. Alipopewa muda wa kujitetea hakuna alichosema zaidi ya kuihtaji hukumu yake.



    "Hakimu, ndio nimeua. Hili swala halihtaji ushahidi wowote, nimekili mwenyewe na ninahitaji hukumu. Naombeni msipoteze muda nihukumuni." Ni kauli alizotoa pale alipopewa fursa ya kujitetea. Hakika alishangaza sana mtuhumiwa huyo asieogopa hukumu kali itayomfuata.



    "Kiukweli mtukufu hakimu. Hakuna sababu iliyonifanya niue. Lakini niliamua kuua kwasababu nilijisikia kuua tu. Nilimuua yule mama kule jalalani, nikamgonga na gari yule kijana njiani, na mimi huyohuyo nilimchoma visu yule Afande tena ndani ya kituo chake. Naombeni hukumu kabla sijajisikia tena kuua. Tafadhali." Kichaa yule alizidi kuitikisa mahakama ile kwa majibu yakujiamini kiasi kile.

    Kesi ile ilikuwa na mashahidi wa kugushi, ambao walisisitiza kuwa wao walishuhudia mauaji ya Kichaa yule.



    Mwisho wa siku kichaa alihukumiwa kifungo cha maisha jela, hakupewa adhabu ya kazi ngumu kama wengine kutokana sijui na kifungu gani cha sheria alichokidokeza hakimu mahakamani pale.



    "Hakimu.. Nataka hukumu ya kunyongwa! Mbona hujanipa hukumu, badala yake umenipa raha? Hata huko gerezani nikijisikia kuua nitaua tu." Alibwata kichaa yule. Kipindi anatolewa kwa ajili ya kwenda kutumikia hukumu yake. Hakimu alibaki ameduwaa na hapo ndipo akaanza kuwa na wasiwasi na akili za mtu yule. Lakini hakuwa na jinsi kwakuwa tayari hukumu imeshapita.



    + + + + +



    Aisha mapuya, alijiegesha chini ya mti mmoja huku akitafakari jinsi ambavyo ameokolewa kwenye kesi ya mauaji tena na mtu asiyemjua. Alikumbuka jinsi mtu yule alivyokuwa akimsihi kutokukata tamaa. Lakini alibakiwa na mawazo mengi sana yaliyoendelea kutembea kichwani mwake. Akiwa katika mawazo yale, kichefuchefu kilimuijia ghafla na kujihisi kutapika.



    Mmh! Mbona sina ugonjwa?, au mimba? Lakini kama mimba..! Mbona sijatembea na mwanamume yeyote. Hii itakuwa malaria tu, au uchovu. Alijiuliza na kujijibu maswali mfululizo aliyoyatengeneza kichwani mwenyewe.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/





    Kichefu chefu kile kiliambatana na kizunguzungu kilichomfanya aione dunia jinsi ambavyo hutumia masaa ishirini na nne kukamilisha mzunguko wake. Alikishika kichwa lakini hiyo haikuwa msaada kwake. Hapo akapatahamu ya kutapika na kabla hata ya kuhitaji matapishi yakatoka kwa makusudi. Alilala chini ya mti ule na baada ya kuamka ndipo alipogundua maumivu ya kichwa aliyonayo. Alifikiria kwa nukta kadhaa, kilichomfanya aumie kichwa namna ile nakung'amua kizunguzungu alichokuwa nacho masaa kadhaa. Alipokumbuka kichefuchefu na kutapika ndipo alamu ya hatari ikagonga kichwani mwake na kuanza kumwambia kuwa, zile dalili alizozisoma kipindi kile anasoma shule za kuhusu mimba ndizo alizo nazo. Lakini aliendelea kuidharau alamu ile kwa jikosoa nakujiona kuwa hajawahi kufanya mapenzi kwa hiyari bali alifanya kwa lazma hivyo asingeweza kudhurika. Alihisi huenda atakuwa na malaria maana pia hizo ni dalili za malaria.



    Baada ya kufikiri kwa muda kadhaa, akajinyanyua na kusimama kwa ajili ya kuondoka maeneo yale. Aliposimama akili ilikosa pakumpeleka, kila alipopawazia aliona hakutakuwa na msaada kwake. Bila hiyari yake alijikuta akichukuliwa na miguu moja kwa moja ikaanza kumuongoza maeneo ya Igoma, alipofika. Wazo la kuomba kazi lilimwijia nakuona nibora akaombe kazi tu tena za ndani.



    Alifika nyumba moja na kufunguliwa na mlinda geti la nyumba hiyo.



    "Unashida gani?"



    "shikamoo..."



    "Sina shida nayo. Kuwa nawewe utazipata nyingi tu hadi utazichoka baada ya kugundua zinasumbua akili bila faida. ...we sema shida yako tu."



    "Samahani kaka yangu kama nimekukwaza. Mimi ninaomba kazi."



    "Kwa mimi naajili msichana wa kukaa nami muda wote katika geti hili, msichana wa kunitengea maji yakuoga, msichana wa kunipikia chakula na msichana wakuni... Wakuni..." Akasita kidogo baada ya kuona bosi wake akijongea maeneo yale kutoka ndani. Kishaakaendelea. "tuachane na hayo. Pia bosi wangu nae anatoa ajira muda huo huo. Anaajiri mfanyakazi wa kuosha vyombo, kusafisha ndani, kufuanguo zake na za mmewe, na mengineyo. Sasa chaguo ni lako kati ya kuajiriwa na mimi au na bosi wangu."



    Hapo, Aisha akatabasamu, kidogo baada ya kugundua vituko vya mlinda geti yule. Muda huohuo akafika yule bosi.



    "Shikamoo dada.."



    "Marahaba. Unashida gani?" Aliuliza baada tu yakuitikia salamu. Huku kwa muda huo mlinzi wa geti akiwa amenywea na kuendelea kuliadhibu rungu lake, kwa uoga wa bosi.



    Sijui ni mwambie nahitaji kazi au nimuombe msaada tu. Mmmh! Nikimuomba msaada hauwezi kunisaidia, hata hii kazi kweli nitaifanya kwa hali hii?.



    "We binti ni kiziwi?" Aliuliza yule bosi na hapo ndipo Aisha akagutuka kutoka mawazoni ghafla bila kufikiria akaropoka.



    "Hapana. Mi sijaua." Jibu lake lilikuwa na maana iliyojificha japo aliropoka kutokana na mawazo tu. Alimpelekea bosi amuhisi binti aliyerukwa na akili. Huku mlinzi wageti akipatia upenyo wa kucheka hadi akaanguka chini.



    "Nawe.. Kibakuli, uo wehu utakuisha lini? Hilo jibu limekuchekesha kiasi hicho. Badala hata ungehuzunika. Punguza wehu. Mdogo wangu hebu nifate tukaongee vizuri unaonekana hauko sawa kiakili wewe." Aliongea ma'mwenye nyumba kisha wakafatana hadi ndani. Walipofika wakaketi kwenye masofa na yule mama akaomba aelezwe shida ya binti yule.



    "Dada, nimekuja hapa kwako kwa ajili ya kuomba kazi. Naomba unisaidie dada yangu." Aliongea shida yake kiufupi. Ma'yule alimuuliza maswali kadhaa. Nakumpa tahadhali lakini pia aligusia suala la machokoraa jinsi walivyo na tabia mbovu. Kisha akamuomba historia ya maisha yake na anapotokea ilihatakama likitokea tatizo wajue jinsi yakulitatua mapema. Alitoa historia japo ilikuwa ya uongo. Dada yule alimkaribisha na kumpeleka pahala kwa ajili ya kuoga kisha akamuonesha chumba cha kupumzikia.



    Ilikuwa ni zaidi ya furaha kwa Aisha. Alishukuru sana Mungu, huku akimuombea kichaa yule apumzishwe huko alipo.



    * * * *



    Mavugo baada ya kupelekwa gerezani. Ndipo alipogundua kumbe ingawa gereza ni pahala pakufundishia adabu vilevile nisehemu pakufundishia uharifu.



    Siku ya kwanza tu anaingia hivi. Alikaribishwa yeye nawenzie watatu ambao waliingia wote kwa pamoja siku hiyo. Wale waliowakaribisha walikuwa na maneno yasiyo na heshma hata kidogo.



    "Wakezetu.. Karibuni. Tutawaoa.. Karibuni." Ni maneno baadhi katika wimbo wa kuwakaribisha. Wimbo uliofanana na kwaya lakini ulitumia mikono kama kifaa pekee cha muziki maeneo yale. Wimbo ule ambao ulikosa kwaya masta pekee uliendelea kuimbwa ndani ya gereza. Huku wafungwa wale wapya wakiipelekwa sehemu na maaskali jela waliowapokea.



    Hapo.. Matumbo yawafungwa wale wapya yakaanza kupata joto kutokana na wimbo ule uliokuwa na maneno makali na yenye lugha chafu. Sijui mtunzi wa nyimbo ile kipindi yupo uraiani alikuwa akiimba nyimbo za aina gani au labda aliwaza nini mpaka akatunga wimbo wa kukaribisha wafungwa. Tena wenye vitisho namna ile.





    Wafungwa wale wapya waliendelea kuusikia wimbo huo bila kificho. Walifikishwa mpaka kwenye vyumba vyao maalumu kulingana na namba zao.



    Ingizo jipya alikuwemo Mavugo, mwenye kesi ya mauaji ya watu watatu. Alikuwemo Moshi. Kesi yake ilikuwa ni yakuua mtu mmoja. Huku Salmini yeye akikabiliwa na kesi ya kumuua mke wake pamoja na mtoto wake.



    Kwakuwa waliingia pamoja hivyo muda wa chakula walitafutana haraka na kuonana, kisha wakaenda kupanga foleni kama maagizo yanavyosema.



    Mavugo, aliendelea kushangaa baada yakugundua kuwa kumbe hata wapishi nao ni wafungwa. Alijiuliza jinsi wanavyopata malipo yao lakini hakupata jibu. Ilipofika zamu yake kwenye foleni. Alienda na kupatiwa chakula kichache tofauti na waliomtangulia. Hata marafiki zake walipata hivyohivyo.



    Hawakuwa na jinsi waliamua kwenda kukaa kwa ajili ya kula na ndipo alipokuja jamaa mmoja aliepanda hewani. Huku nyama za mwili wake zikiwa zimejikata mapingili na kukomaa kila mahali. Jamaa yule alifanana na wanyanyua vyuma wazoefu.



    "Wapuuzi nyie. Mnakulakula tu. Mmelipia hapa?" Aliongea jamaa yule na hiyo nibaada ya kuipiga meza waliyokuwa wamewekea chakula wafungwa wale. Hapo, hakuna alieongea kila mmoja alinywea na hapohapo jamaa yule bila hata uoga wa nyampala aliyekuwa maeneo yale. Akaamrisha. Ati wachukuliwe wafungwa wale iliwaende kukaribishwa na hata kama wakila chakula, wawe wanakula kiuhalali. Sio kula bila kukilipia. Hapohapo alichukuliwa Salmin na kwenda kulawitiwa na wafuasi wa jamaa yule ajulikanae kwa jina la Tripple B. Kisha wakamchukuwa Moshi japo alipambana lakini walimshinda na kumfanyia yale waliyoyafanya kwa Salmin. Hapo wakamchukuwa Mavugo kwa ajili ya kumfanyia vile. Walianza kumtolea nguo zake alizokuwa amezivaa. Wakiwa kwenye harakati za kumfanyia ujinga wao huku akijitetea bila mafanikio. Hapo ndipo alipoingilia mtu mmoja nakutoa msaada kwa kuwatembezea judo wote walioonesha kuwashambulia wafungwa wale.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mtu huyo alimchukua Mavugo na kumpeleka moja kwa moja pahali pazuri. Huku wale wafuasi wa Tripple pamoja na Tripple wote wakinywea kutokana na kutembezewa kichapo cha adabu.



    "Kwa majina naitwa. Emanueli Zakayo. Nimeagizwa na serikali kwa ajili yako. Ingawa umepewa hukumu ya kifungo cha maisha lakini ushahidi haukuweza kuridhisha na hata kuwa namashaka na akili zako kutokana na maneno uliyokuwa ukiyaongea. Najua, utakuwa na sababu ya kuhitaji kunyongwa na ndiomaana ulitamani kunyongwa sana. Sasa labda ningependa kujua kwanini unahitaji kifo kuliko hata kuishi?" Aliongea mtu yule aliejitambulisha kwajina la Emanuel.



    "Mnanichunguza ee. Hivi nyie wapelelezi!! Mara ngapi nimeshawambia kuwa. Mimi sijui nilipotoka, yaani hata jina langu silijui. Au mnashida gani tofauti na hiyo. Kama shida ni kunipeleleza. Basi mniache, msidhani kisa mimi kichaa ndio mnaweza kujanipeleleza nakuwasaidia chochote. Kwanza achaneni na mimi. Au nawewe unataka kufa? Sema! Msipende kuwa wambea namna hiyo." Aliongea Mavugo na kumfanya Emma abadilishe pozi lake.



    "Mavugo. Tunashida na historia yako. Natunaihitaji zaidi ilikuhakikishatunaamua uamuzi sahihi. Unajua mpaka leo wanaendelea kuishi nawe unaendelea kuteseka. Je, unajisikia furaha kila siku kujitumbukiza kwenye matatizo huku ukijipa kauli mbiu ya Maumivu ndio haki yako. Hivi. Wewe niwakujifanya kichaa na kukubali kuangamia kisa vitu vya nyuma. Hebu angalia wapitumetoka. Shida yangu mimi nikukusaidia wewe na si vinginevyo. Nakuomba tafadhali elezea nami nitaichukua kama ushahidi. Ushahidi utakaokuweka huru na haya uliyoyafakamia bila kufikiri. Tafadhali usikubali kupotea hivihivi. Yaani, haki uloitafuta mwenyewe. Leo nd'0 imekufanyia hivi?" Aliongea Ema. Nakimaneno tu. Alionesha kumjua zaidi na kuwa na ukaribu fulani na anamfahamu sana Mavugo.



    "Ema, ukitaka niongee. Mlete mke wangu, mlete mtoto wangu pia. Hapo ndipo nitaongea. Lakini kama wao wamekosa haki, basi mimi sioni haja yakuitafuta hiyo haki ambayo imewaondoa wao." Aliongea Mavugo kwa ghadhabu kisha akaongeza. "Maisha ya ukichaa. Hayakuhusu. Bora uniache naukichaa wangu nami naufurahia kwasababu napata muda wa kuyaepuka ya dunia kwa kuwa mjinga." Aliongea. Kwa upole huku akiwa kama ni mwenye kumnong'oneza Ema. Wala hakushangaa kuiona sura ya Ema ndani ya gereza.





    . Baada ya mavugo kumnong'oneza Ema. Aliamua kuondoka na moja kwa moja kurudi hadi kwenye chumba chao. Alipofika, aliwaza sana na kuwazua. Kisha alifunua mchago na kuchukua picha moja kati ya tatu alizokuwa amezihifadhi chini ya mchago huo.



    Aliziangalia mara kadhaa, kiasi chakutokwa na machozi.

    Ni picha ya muhimu sana kwake. Kwenye picha hiyo kulikuwa na sura ya Mwanamke mmoja ambae ukimuangalia kwa wasiwasi wawezadhani ni mwarabu kumbe ni kutokana na uzuri wake wa asili. Mwanamke huyo alionesha tabasamu lililomfanya awe mzuri zaidi, alikuwa kushoto mwa picha hiyo huku katikati akionekana mtoto ambae ukimkadilia ni chini ya miaka kumi. Kuanzia sura, hadi mavazi basi usingeshindwa kugundua kuwa mtoto huyo ni wakiume. Kulia kwa mtoto huyo alionekana mwanamume ambae nae kama wengine aliashiria tabasamu. Huku mbele ya wote watatu hao kukipambwa na keki iliyokuwa kwenye meza maalumu kabisa. Na kwa muda huo ungegundua kuwa ni muda wa kuzima mishumaa yakeki hiyo kutokana na mtoto yule kuonesha ishara ya kupuliza mishumaa iliyokuwa ikiwaka.



    Mke wangu, nakupenda sana. Najua kuwa nawe unanipenda. Hata huko uliko huwa unaniombea na kutamani angalauuungane nami. Lakini inakuwa ngumu.

    Natambuwa wazi kuwa haupotena kwenye hii dunia. Lakini roho yako ipo pamoja nami.. Na unasikia kila ninachoongea kwa muda huu. Hakika umeondoka kwa kudhalilika sana. Naomba utambue kuwa, mimi kama mume bora nilipata pigo kubwa sana na sitokaa nisahau kamwe. Alijisemea Mavugo huku akiwa amekaza jicho lake upande wa mwanamke wa kwenye picha ile aliyokuwa akiiangalia. Kisha akayachukuwa macho yake kwa hali ya unyonge usio mithilika na kuyabwaga kwa mtoto aliyeonekana kwenye picha ile.



    Kumbukumbu zikamrudisha miaka kadhaa nyuma..



    * * * *



    "Mwanao Sufiani anapenda sana kusoma magazeti. Sijui naye anataka akikuwa awe Muandishi kama wewe Baba yake?" Ni sauti nyororo kutoka kwa Bi. Chiku au Ma. Sufiani kutokana nakujaaliwa mtoto wa kiume mwenye jina hilo. Sauti hiyo ilikuwa imeambatana na mikono ambayoiliendelea kupapasa,papasa maeneo ya uso wa mumewe huku mume wake nae akiipokeza kwa kuishika kuizuia isiendelee kumtekenya tekenya.



    "Eee, mtoto wa kiume lazma amrithi baba yake. We unataka mwanangu apende kuwa daktari iliakahangaike na vidonda huko, kama wewe Mama yake. Mwanangu ni Muandishi wa habari, na atafichua siri za uovu pamoja na kuwasaidia watu kwakufikisha matatizo yao mbele ya uongozi. Mwanangu hatokula rushwa ya kutoa Mimba, mwanangu hatoangalia watu wakifia hospitali na kuwafunikia kisha kuwaingiza mochwari. Bali mwanangu atawaanika madaktari wanao kula rushwa, atawafanya madaktari waingie gerezani kwa kosa la kusababisha vifo kisa uzembe. Hayo yote atayafanya kupitia Magazeti atakayoandika huko mbeleni. Na ndiomaana anapenda sana kusoma magazeti na sio kuuguza vidonda kama ufanyavyo wewe mama yake."



    "Umeanza tayari mambo yako. Mimi kila siku nakwambia Baba Sufiani. Bila mimi kumzalisha Mama yako wewe usingekuwepo hadi leo. Usimdharau daktari yeyote, sawa mimi ni mkeo lakini ukiugua nakutibu tu."



    " Astaghafirullah.. we mwanamke wewe... Acha uongo. Utapata dhambi bure. Nani aliyekudanganya. Mama Mavugo alimzaa Mavugo hospitali. Mimi sikuwa mzembe kiasi hicho. Nimezaliwa zangu nyumbani swaafi. Na sio huko hosipitali. Halafu ukome kumfunza mwanangu hayo ma microscope yako hayo. Sijui ma silinji. Sitaki mwanangu umuambukize udaktari. Dume langu lazma lifichue maovu na kuiandikia jamii mambo yaliyo jificha bwana. Alaaa!"



    Waliendelea na mjadala wao na mwisho wa siku waka kosa maelewano ikabidi wa muite mwana wao na wamuulizie anachopenda kati ya udaktari au Uandishi.



    "Baba.." aliita mtoto.



    "Naam, mwanangu" aliitikia Mavugo. Kisha mtoto akamuangalia mama yake na kumuita. Hivyohivyo kama kwa baba yake aliitika Mama. Kisha mtoto akaongea..



    "Ikiwa kama kunaulazima wa mimi kuiandikia jamii. Basi kushika kalamu ni jukumu langu. Lakini pia kama jamii itaugua basi nitashika sindano yenye dawa na kumchoma mgonjwa hadi apone ndipo niikamate tena kalamu." Majibu yale ya mwanawao huyo mdogo ambae alikuwa na umri wa miaka nane pekee. Yaliwafurahisha sana wazazi wake.



    * * * *



    Kengele ya kuwaamrisha wafungwa wote kulala. Ndiyo iliyakata mawazo yote ya Mavugo, na harakaharaka akafuta machozi. Kishaakairejesha picha ile mchagoni ilikufanya wafungwa wenzie wasiione.



    "Amka uoge kisha twende shoping kwa ajili ya kuchukuwa mavazi yako ya kuvaa maana huna kabisa nguo" Ni sauti ya Bosi wa Aisha aliyekuwa akimuamsha Aisha mara kadhaa hapo kabla.



    "Sawa dada." Aliamka Aisha. Nakuoga kisha akavaa nguo za dada yule ambazo zilimfanya aonekane wa tofauti kidogo. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Wakachukuwana hadi kwenye gari iliyokuwa sehemu ya kuhifadhia magari kwenye uwanja wa dada yule. Kisha wakapanda moja kati ya magari manne yaliyokuwepo pale.



    Mlio wa honi ndio ulio muamsha Kibakuli. Nakwenda kufungua geti kisha bosi wake pamoja na Aisha wakaondoka.





    Wakiwa ndani ya gari Aisha na bosi wake. Hawakuwa hivi hivi bali walizungumza mawili matatu huku gari hilo likienda.



    "Mmmh! Hapana Aisha, mie sipo hivyo. Kwanza samahani nilisahau kukujuza kuwa. Nimeolewa, na lakini kwa sasa mume wangu yupo dar-es-laam kuna mambo kaenda kufanya."



    "Waoo. Hongera sana bosi wangu."



    "Aisha. Nimekukataza mara ngapi kuhusu hilo jina la kuniita bosi. Wewe niite dada tu, sawa?"



    "Samahani dada yangu. Nimazoea tu."



    " usijali mdogo wangu."



    Hayo ni baadhi ya maongezi waliyokuwa wakiyaongea njiani. Hatimae walifika kwenye maduka ya nguo kisha wakachagua nguo nzuri na zakisasa kabisa. Umbo zuri alilojaaliwa Aisha ndilo lilizifanya nguo nyingi kumpendeza. Karibu kila kizuri cha dukani kwake kilifaa. Walinunua nguo na kuamua kurudi nyumbani kwao. Kama ilivyo kawaida walifunguliwa geti na kuingia ndani.



    Walipofika hatua ya kwanza ilikuwa ni kuoga kutokana na uchovu kisha Aisha akaelekea jikoni kwa ajili ya mapishi, huku Dada yake yeye akitazama moja kati ya seasöns za kikorea.



    Dada yule alijulikana kwa jina la Aneth. Aneth akiwa anaendelea kutazama Seasön mara ghafla simu yake ya mkononi iliita. Alipoiangalia kwenye kioo ilisomeka 'My husband'. Akaipokea na kuiweka sikioni.



    "Hello sweety" Ni sauti kutoka upande wa pili. Sauti ngumu iliyoonesha kujilazimisha kulainika.



    "Hello, darling" Ni sauti ya majibu kutoka kwa Aneth. Sauti nyororo yenye kutia hamu kuisikia tena pindi upatapo nafasi ya kuongea nayo.



    "Baby. Nimepata taarifa kuwa Mama amezidiwa na ule ugonjwa wake wa Moyo. Si unajua mimi nipo mbali? Nakuagiza wewe uende kahama kwa ajili ya kumuangalia si unajua huko nyumbani hakuna wa kumuangalia." Aliongea Wilson. Mume wa Aneth.



    "Haa! Masikini... Ameanza lini?" Aliuliza aneth. Kisha mumewe akamjibu kwa haraka.



    "Basi sawa mme wangu. Leo najiandaa kesho asubuhi nitaenda huko." Baada ya kupeana taarifa za hapa na pale simu ilikatwa na aneth akaendelea kuangalia video.



    Mmhmh! Hapa lazma ni mwambie dada kuhusu hii Mimba. Lakini.. Akiniuliza juu ya nilipoitolea nitamjibu nini?.. Je, nimwambie ukweli kuwa nilibakwa na maafande?. Hapana, siwezi. Nikimwambia hivyo tayari nitakuwa nimejiharibia kwa sababu historia ya maisha yangu nilompa haitoendana na mwisho ataniona muongo. Sasa nifanye nini wakati hali inazidi kuniwia ngumu. Au niitoe tu. Ndio, hapa chamuhimu nikuitoa ilinisipoteze kazi. Lakini...! Kutoa mimba ni dhambi kubwa na huleta madhara! Mimi kesho kutwa lazma ni mwambie dada najua atanisaidia anaonekana ni mwenye huruma. Ni mawazo yaliyokuwa yakimzunguka kichwani mwake Aisha pindi yupo jikoni na hiyo ni baada ya kupatwa na kichefuchefu cha ghafla.



    Hatimae muda wa chakula ulifika na wote kwa pamoja wakakutana mezani na kupata chakula. Kisha wakaongea machache, lakini Aisha hakugusia swala lake la mimba kwakuwa alipanga kumjuza dada yake swala hilo kesho kutwa.



    Haya, hatimae usiku uliingia na muda wa chakula chausiku ulipofika. Ndipo Aneth alipomuachia Aisha majukumu na kumpatia matumizi kisha akamjuza kuhusu safari ya yeye kwenda kahama kumuuguza mama mkwe. Hapo Aisha akapumua nakujua kuwa itakuwa ngumu sana kwa Aneth kuelewa kuwa yeye anamimba. Hivyo akaamua kuweka siri moyoni kama kawaida.



    Siku ya pili yake ilipofika. Aneth aliondoka na kwenda hadi kahama. Alipofika, alimkuta mama mkwe wake kwenye hosipitali ya goverment pale wilayani kahama, kishaakaanza kumuuguza.



    Huku nyuma Aisha alijiona yupo huru, na hakupata uoga tena kila alipobanwa kutapika alikimbia na kutapika. Tumbo lilipomuuma alitumia dawa. Kila alipomaliza kazi za nyumbani na kuwa huru. Alipenda sana kutoka nje na kuzurura zurura, lakini alifanya hivyo kwa tahadhali sana.



    Siku ziliendelea kusonga hatimae ikapita wiki nzima na hapo akawa ameizoea kabisa nyumba ile. Mimba nayoiliendelea kumsumbua ingawa bado ilikuwa haijaanza kujifichua. Hapo akawa mvivu kupika, kufanya usafi hata kusababisha migogoro kila siku kati yake na mfungua geti.



    Huwezi juwa lililomo moyoni mwa mtu. Siku moja mfungua geti aliingia ndani na kumkuta Aisha kajilaza kwenye masofa kutokana na uchovu. Alipofika ndani mule yeye moja kwa moja akahitaji kumjua Aisha kwa nguvu, japo kuwa Aisha alipinga. Lakini hakuwa na ubavu wa kukinzana na getimani yule, hivyo akafanikiwa kumjua Aisha.



    "Sasa, ulikuwa unanibania nini. We mwenyewe umefaudu utamu. Kaone, ulikuwa unajikatisha raha bure!" Ni baadhi ya maneno aliyoyatoa getimani yule. Huku akimfuta machozi Aisha ambae kwa muda huo alikuwa akitoa machozi.



    Masikini Aisha alikuwa akilia kwa kumuhurumia kijana wa watu ambae amejisababishia ukimwi bila kujua. Lakini hakutaka kumwambia maana alijua endapo atamwambia basi atamfanya kijana wa watu asiishi kwa amani. Lakini pia aliona kijana yule ameumia kutokana na tamaa zake.



    Hakuwa na jinsi na hapo akaamua kuliamisha penzi lake kwa geti mani. Kila siku usiku wakawa wanavunja amri ya sita, ndani ya nyumb ya bosi wao Aneth.



     Siku zilienda hatimae Mimba ya Aisha ikajidhìhirisha machoni mwa getimani.



    "sawa, minimekubaliana na hiyo mimba. Lakini nakuomba tunza siri." Masikini getimani alijikuta akikubali mzigo usio kuwa wake. Na hakuwa na kipingamizi kwa sababu yeye ndie mwanaume pekee wa Aisha. Hapo Aisha akawa amepata wa kumbambikizia mimba na ukimwi juu. Waliendelea na mapenzi yao hadi aliporudi Aneth na kukuta Aisha tayari ana mimba. Kwakuwa Aisha alimficha, Aneth toka mwanzo. Hivyo aneth alijua huo utakuwa ni umalaya wa Aisha na kuwaza kuwa huenda kipindi ambacho yeye hayupo ndicho Aisha alichokitumia kufanyia umalaya wake.



    "Aisha, ulikuja kuomba kazi nami nikakupa. Hakuna nilichokunyima kwanzia chakula, mavazi, na hata malazi. Nilikupa uhuru na kukuchukulia kama mdogo wangu. Lakini wewe leo umepoteza heshima. Hivi, we unadhani nani ana muda na kulea hiyo mimba yako humu ndani. Kiukweli sina msaada kwako, chamuhimu ni wewe kwenda kwa mahawala zako waliyokupa hiyo mimba." Hata Aisha alipojaribu kujitetea, hakuna kilichobadilika. Alipewa usiku mmoja tu wa siku hiyo kwa ajili ya hifadhi na kutakapo kucha aondoke ndani ya nyumba ile.



    Alichoka, kila akiukumbuka mtaa, akikumbuka shida za mtaa, akikumbuka uovu wa mtaa. Kisha akiwianisha jinsi alivyopokelewa na Aneth na kuanza kuishi pale. Pasina kusema kuwa anamimba na mimba yenyewe hakuipata hivihivi bali alibakwa tu bila ridhaa yake. Alibaki kujilaumu na kuwaza huenda angemtaarifu Aneth mapema kuwa alikuwa na mimba. Yote hayo yasingetokea. Alijiinamia kwa muda huku akiendelea kuwaza mawazo yasiyo wazuka.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alilaani kitendo cha kumpatia geti mani mwili wake na kumsababishia ukimwi. Pia alikumbuka kuwa yeye ndie aliyesababisha getimani amfuate kufuatia mitego aliyompa, lengo lake ilikuwa si. Kumuambukiza Ukimwi bali kumbambikizia kesi ya mimba kwa kudhani huenda kupitia getimani yeye asingefukuzwa. Masikini, Aisha anaishia kukinzana na migogoro ya nafsi na kuishia kujiona mwenye makosa. Soni ilimjaa, na hata kushindwa kuinua uso wake japo alikuwa ndani ya chumba alichopewa kwa ajili ya kupumzikia lakini alijionea aibu mwenyewe.



    Tumbo limemjaa, Aisha ameharibika. Ukimuangalia uso wake wakutisha huwezi tamani kurudia tena. Ingawa alikuwa akitumia vidonge vya kuongeza siku lakini hakuweza kukabiliana na mimba aliyokuwa nayo.



    Alitamani kujiua lakini kila alipoangaza vifaa vya kutolea uhai wake hakuona hata kimoja, alitamani atoke nje na kwenda kununua sumu dukani lakini hakuwa na pesa. Bora hata angekuwa na kanga huenda angeifunga juu ya paa nakujining'iniza lakini nguo zote alizokuwanazo alinyang'anywa na Aneth kwa sababu alinunuliwa na sio kwamba alijinunulia yeye. Labda nguo alizobakiziwa ni zile alizokuwa amezivaa kwa siku hiyo.



    Ingawa alipewa hifadhi ya kulala kwa siku hiyo lakini hakuweza kuvumilia kulala kwenye nyumba hiyo iliyojaza aibu yake. Taratibu bila hata kuaga aliichukuliwa na miguu yake na kupelekwa hadi getini. Alipofika alifunguliwa geti na mpenzi wake kibakuli au geti mani kwa jina la nyadhifa yake. Waliagana kwa majonzi na kwa muda wote huo getimani hakuwa ameanza kuadhirika zaidi na virusi vya ukimwi hiyo ilibaki kuwa siri ya Aisha pekee.



    Masikini, hapo sasa Aisha akaanza kutangatanga mtaani mida ile ya usiku huku baridi kali likiendelea kumuadhibu na kile kinguo chake cha mikono wazi kilichoishia juu kidogo ya magoti. Baridi hilo liliendelea kumpiga na kumfanya ayaadhibu meno yake kwa kuyagonganisha muda wote. Alipita kwenye vichochoro vya igoma utadhani yeye ni jasiri sana kumbe kutafuta pa kulala tu. Alifika sehemu yenye duka na kuchukua maboksi kisha akayachana kiustadi na kujitengenezea sehemu ya kulalia. Alipomaliza aliuweka mwili wake juu ya maboksi yale hakuwa na shuka hivyo alijifunika ngumi.



    "Oyaa. Mwanangu leo mie sijapata hata mtu wa kupiga ngeta. Daah! Bisu langu halijafanya kazi kabisa." Ni sauti ya Vijana wawili wa mtaani. Vijana ambao ukiwaona tu utawafananisha na vibaka waliyoshindikana kutokana na makovu yaliyowaenea.



    "Bora, wewe... Mimi mwenzio hapa. Nilipitia mitaa ya makoroboi, nikapitwa wembe na wale watoto wakule. Yaani hata sijafanya kazi." Aliongea kijana yule wa pili kwa sauti ya unyonge.



    "weeweeee! Acha basi. Kwahiyo jemedari unataka kusema wale watoto wa mama wa huko kati nd'o wamekupita wembe wako."



    "Nd'o hivyo mwanangu. Ila nimewakalili." Aliongea kijana yule aliyekuwa akilalamika. Safari ya vijana wale wawili. Iligota pale walipofika maeneo ya kibaraza cha duka ambapo ndipo alipokuwa amelala Aisha.



    Walinong'onezana kwa sauti. Kishawakamkurupua Aisha ambae kwa muda huo hakuwa anajielewa kama yupo macho au amelala.



    "oyaa. We manzi unazingua. Nani kakwambia ulale sehemu yangu." Aliongea mmoja kati ya vijana wale. Aisha nae alikuwa mgumu kuelewa. Aliendelea kujibizana na vijana wale. Ndipo walipochukuwa jukumu la kumpiga palepale mateke ya tumbo bila kujali mimba aliyokuwa nayo kisha wakamkimbia.





    Ilikuwa ni zaidi ya maumivu kwa binti Aisha, tena kwa bahati nzuri au mbaya mimba yake ilikuwa imefikisha miezi tisa timilifu hakuna ilichosubiria zaidi ya uchungu tu. Kama uchungu basi hapo aliupata tena wakutosha kiasi kwamba akawa hajielewi kabisa kutokana na maumivu. Hapohapo nje ya duka hilo mida hiyohiyo ya usiku.



    "Jikaze.. Jikaze.. Haya sukuma.. Sukumaa.." Ni sauti ya mama mmoja msamalia mwema. Mama ambae nae kama Aisha ni mlala nje. Alikuwa amelala na kina mama wengine kwenye kibaraza cha jirani lakini alienda kumsaidia Aisha baada ya kugundua kuwa anamimba. Muda wote huo Aisha aliendelea kujikema kwa nguvu utadhani ni mwenye kutoa haja kubwa. Zoezi hilo lilichukuwa muda kidogo mpaka kukamirika.



    Yule mama aliyekuwa amevalia mifuko ya nailoni kutokana na kukosa vifaa maalumu kwa ajili ya zoezi lile. Nikama aliongozwa na Mungu pale alipokata na kufunga kwa upesi kitovu cha mtoto yule wa kiume ambae ndio kwanza amezaliwa na kwa bahati alichapwa makofi kadhaa akaanza kulia.



    Naam. Inawezekana na hilo halina ubishi hata wanasayansi wa kale na wasasa wote wanakubali kuwa. Mtoto anaweza kuzaliwa bila virusi vya ukimwi ilhali mzazi wake anavyo. Najua utakuwa na maswali mengi lakini hiyo ni siri ya Mwenyezi Mungu pekee. Unaambiwa pale kwenye kumkata ule mrija unaemuunganisha Mama na mtoto. Basi hapo ndipo panaweza kumfanya mtoto akapata na virusi au asipate. Aisee., tumuacheni Mungu aitwe Mungu tu. Wala tusijadili zaidi uwezo wake maana tutajikuta wenye kukufuru pasipo kutarajia.



    "ng'aaaa... ng'aaaa...ng'aaaa...." Ni sauti ya mtoto yule ambae ndio kwanza ameingia duniani. Kwa muda huo Aisha alikuwa amezimia kutokana na shughuli pevu aliyoimaliza. Hapo Mama yule mwenye huruma akambeba mtoto yule na kwenda hadi maeneo ya mto kishaakachukuwa maji na kumsafisha. Maji mengine aliyoyabeba kwenye madumu ya dasani aliyatumia kumsafishia Aisha huku mikono yake akiwa ameifunga kiustadi.



    "Mwanangu. Hakuna maji yakukukandia. Hakuna dawa ya kutuliza maumivu. Ila nimekuchumia dawa ya kukata damu japo kidogo. Lakini yote kwa yote naomba umshukuru Mungu kwa kukujaalia neema ya kupata mtoto katika kipindi hiki kigumu ulichonacho. Ni wachache sana wapatao neema hizi, hii ni baraka mwenyezi ameamua kukuruzuku. Huwezi juwa labda kupitia mtoto huyu, wewe utapata kivuli na kuondokana na jua hili la utosini ulilonalo. Hapa chamuhimu wewe ondoka. Najua unamaumivu lakini haina jinsi hapa simahala pazuri kwako. Toka maana ukikutwa umezalia hapa kwenye duka la watu, wao hawatoelewa shida zako bali watajua ni wewe kuwapelekea nuksi." Aliongea mama yule mwenye huruma. Mama ambae ukimtazama waweza kumdharau kutokana na uchakavu wa nguo zake unaopelekea aonekane hana thamani lakini miaka ya nyuma mama huyo alikuwa daktari mzuri tu. Ila ni historia ndefu iliyompelekea kuwa maeneo yale.



    Labda kwa ufupi... Huko nyuma kabla ya kuujua mtaa. Aliitwa beatrice wanyika. Beatrice alikuwa mrefu kidogo, mwembamba kiasi. Sura iliyopambwa na macho maregevu huku kope zake zikiashiria kuhitaji kusinzia muda wote. Nyusi za asili ambazo hazihitaji haja ya wanja, huku shavu dodo lenye kuruhusu machozi ya furaha na huzuni yapite bila mkwaruzo wowote. Hivyo na vingine ndivyo vilivyompelekea Beatrice kuwa mzuri zaidi na hata kufatwa na wanamume. Lakini mara zote aliwakataa, kutokana na kutohitaji kujihusisha na maswala ya mapenzi. Hakika alikuwa na msimamo, kuachilia mbali kazi yake ya udaktari vilevile kwao walikuwa na uwezo hivyo hakuna kilichomshinda. Baada ya wazazi wake kufariki kwa ajali, na yeye kunusurika. Ndipo mjomba pamoja na ndugu kadhaa walipowahi mali za wazazi wake na kumzulumu. Kwakuwa alikuwa na haki ndipo alipoamua kufungua kesi mahakamani lakini sheria ni upanga na sio msumeno. Ilikata upande mmoja na yeye kuswekwa gerezani ati kwa kesi ya kuwaua wazazi wake. Wakati ni wazi kuwa wazazi wake walikufa kwa ajali ambayo haijatengenezwa na binadamu. Aliingia ndani na ndipo alipogundua kumbe hata kwenye magereza huwa kuna ubabe. Kwanza alipofika, alikutana na mfugwa mmoja kwa jina la Annastazia. Yeye alikuwa ni mfungwa aliyehukumiwa maisha yote gerezani na kwa muda huo Anna alikuwa na miaka ishirini toka aingie gerezani mule. Alikuwa katili kuliko hata wanamume, alikuwa jasiri na kila mfungwa mpya. Yeyme alimchukulia kama mke wake kwa hiyo hata alipofika kule Beatrice naye aliolewa na mwanamama huyo. Hayo ni mafupi kati ya mengi yaliyompata beatrice ambae kwa sasa ni mama anae ishi mtaani. Alitoka gerezani kufuatia msamaha wa rais. Hakuwa na pa kwenda zaidi ya mtaani tu.



    Haya tuendelee..CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Nashukuru sana Mama angu kwa msaada wako. Sina chakukulipa ila nakuombea kwa Mungu akulinde. Hakika wewe umeokoa maisha yangu na maisha ya mwanangu. Kwakuwa umesema mtoto huyu nimemzaa katika kipindi kigumu ila kwa neema za Mungu ameingia duniani," Aliongea Aisha kisha akakohowa kidogo kikohozi kigumu na kuendelea.





     "Angekuwa mtoto wa kiume basi ningemuita Baraka. Kutokana na misukosuko pamoja na changamoto hasi na chanya alizozipitia kipindi yuko tumboni. Lakini kwakuwa ni wakike acha na muita rehema. Hakika hii ni rehma ya Mungu pekee. Nakushukuru sana kwakunisaidia." Aliongea Aisha na kuanza kumuaga Mama yule kwa heshma zote kisha akaondoka maeneo yale. Aisha aliendelea kuzurura usiku ule yeye mtoto pamoja na maumivu yaliyotokana na taabu ya kujifungua. Kwakweli alipata taabu sana usiku huo.

    Alipita sehemu kwenye kiuchochoro kichafu na kuamua kujituliza hapo ilikupumzisha mwili wake ambao kwa muda huo ulikuwa taabani.



    " Mimi nalewa, nitaendelea kulewa hadi siku ya mwisho. Labda tuitwe walevi wote duniani na kuzuiwa, hapo sasa ndipo nitakapo anzakujifunza kuzoea. Lakini wewe pombe, nakupenda, nakujali, na ninakuhtaji sana maisha yangu yote. Hakika wewe ndio mke wangu wa maisha, sitokuacha hata kama wakikupiga vita kiasi gani. Nafurahi unanitoa mawazo, nazisahau shida niwapo na wewe. Mwaah! Nakupenda sana pombe." Ni sauti ya mlevi mmoja aliyekuwa akipita maeneo yale mkabala kabisa na Aisha, alikuwa akiongea maneno yake huku mkononi ameshikiria chupa ya bia. Alipofika kwenye kichochoro alifungua zipu kisha akaanza kukujoa pasina kuangalia mbele kutokana na ulevi aliyonao.



    Laahaullah.. Kumbe mkojo wake wa kilevi aliokuwa akiumwaga maeneo yale uliwamwagikia kina Aisha. Hapo sasa aisha akashindwa kuvumilia.



    "Kaka.. Usitufanyie hivyo. Mbona unatukojolea." Ni sauti iliyomtoka Aisha katika hali ya unyonge zaidi. Mlevi yule alipatwa na mshituko ghafla na kuhisi huenda maajabu yameamua kumpata. Lakini akajitutumua kilevi na kuendelea kukojoa tena.



    Sauti nyingine ya lawama ndiyo iliyomfanya mlevi yule agundue kumbe kuna mtu na mtoto maeneo yale. Na hiyo ni baada ya kichocheo cha kilio cha mtoto yule mchanga kwa jina la rehema.



    Ingawa mtu yule alikuwa mlevi, lakini hakunyimwa roho ya huruma. Alimchukuwa Aisha kisha akampeleka nyumbani kwake.



    Ni chumba chakupanga. Chumba ambacho hakiujui umeme, iwe mchana au usiku. Chumba hicho ndicho kilikuwa sebure na mahali pakulalia. Buibui, na wadudu wengine watambaao pamoja na baadhi warukao walijisweka ndani ya nyumba ile na kuishi kana kwamba wao ndio wapangaji. Naam. Kulikuwa kuna godoro dogo, kitanda kidogo na kilichotumika miaka mingi kabla, waweza sema ni cha urithi. Hakika ungefanikisha kutupa jicho ndani ya chumba hicho. Basi usingeshindwa kupaita stoo kwa jinsi ambavyo makolokolo yamejazana ndani mule.



    Ingawa chumba kile hakikuwa kisafi lakini aisha alionesha kukifurahia na moja kwa moja alikaribishwa kwenye kitanda kile na mlevi kisha aisha akalala yeye pamoja na mtoto wake. Lakini mlevi kwa heshma alichukuwa shuka na kulala chini.



    Japokuwa kitanda kile kilijawa na kunguni, lakini Aisha hakuonesha kuathirika na chochote mara zote yeye alifurahia tu na kumshukuru Mungu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mlevi hawezi kulala bila kuisifia pombe. Vivyo hivyo kwa mlevi yule, aliimba nyimbo kadhaa alizozitunga palepale na kisha akapitiwa na usingizi.



    Pilikapilika za wakazi wa jiji la Mwanza pamoja na makelele ya hapa na pale huku jua likianza kupenyeza ndani ya nyumba ile kufuatia matundu makubwa makumbwa yaliyomo ndani, ndivyo vilivyo muamsha mlevi yule na kuanza kujiandaa kwa kuoga na kupiga mswaki, baada ya hapo aliingiza mkono ndani ya suruali yake na kutoa shilingi elfu mbili na mia tatu. Akamuamsha Aisha na kumpatia pesa hiyo kisha akaondoka na kumwambia kuwa wataongea baadae kiundani zaidi.



    ... ... ... ....



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog