Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

SITAKI TENA - 2

 





    Simulizi : Sitaki Tena

    Sehemu Ya Pili (2)



    Ilipoishia asubuhi..

    “Levina wangu bado upo?”

    “nipo Gervas wangu.”

    Nilitoka kwa shangwe zote huku nikiamini kuwa atakuwa Gervas tena kwa mara hii ya pili atakuwa kaja peke yake hayupo tena na wale walinzi. Gervas bado alikuwa hajiamini amini kama kweli ni Levina mimi kutokana nakuwa na giza maeneo yale lakini sauti yangu ilikuwa jibu tosha kwa yeye kuniamini.

    “Twende mpaka hostel kwetu kulee”

    Songa nayo sasa…



    Tuliongoza moja kwa moja mpaka upande yalipo mabweni yao. wanafunzi wengi walikuwa wamejiachia nje nadhani kutokana na giza kutanda maeneo yale,tulipitiliza mpaka chumbani kwa Gervas na tulipofika nilimsimulia yote niliotendewa na marafiki zake,alikasirika sana na kuniahidi atadili na mmoja baada ya mwingine kwani wahuni hao ameshawatambua,Nilimwelezea Gervas nia yangu ya kuwa pale kuwa sina hata nauli ya kwenda Dar sina na hata nyumbani Dar nimeshapasahau hivyo anipe ramani ya kuweza kufika mpaka nyumbani kwetu.kwa upande wa Gervas hakuwa na hela kabisa zaidi ya kuniachia shilingi elfu kumi na tano kasha akaniandikia ramani yakuweza kufika kwa ndugu yake anayeishi morogoro anaitwa Baba Ali na ndio atanipatia pesa kidogo za kuweza kunifikisha mpaka nyumbani kwetu Dar,alinikabidhi ramani mbili ya kwanza ni yakufika mpaka eneo analoishi Baba Ali pale Morogoro na ya pili ni ramani ya kufika mpaka nyumbani kwetu kasha akanipatia tisheti na traki suti nyeupe kwani nguo zangu nillizokuwa nazo zilikuwa hazifai hata kuziangalia kwa macho,ndani ya muda mchache tayari tulikuwa njiani na Gervas tukitafuta eneo la pembezoni mwa ukuta ambalo kidogo linaweza kuruka,Gervas aliinama na kunipa mgongo kisha nikapanda nakuruka ukuta na nilipotua tu upande wan je Gervas naye alifanya hivyo hivyo lakini kwa bahati mbaya ile anaruka tu umeme ukawa umesharudi hivyo nikasikia sauti ya Gervas ikijibizana na walinzi waliokuwa tayari wameshaona tukio zima lililokuwa likiendelea,

    “Levina safari njema Mpenzi wangu we nenda tu”

    “Ahsante Gervas nakupenda sana”

    niliondoka zangu taratibu huku nikitafuta angalau gari yakuweza kunifikisha mpaka mjini,kwa bahati nzuri nikapata daladala ambayo ilinitoa pale mpaka mjini na tulipofika nilikata tiketi ya kunifikisha mpaka morogoro kwani niliweza kupata gari ndogo aina ya ‘Coastal’ kutokana na nauli yangu kuwa ndogo. Nilivumilia na ubaridi uliokuwepo pale mpaka ilipotimia alfajiri watu wakawa tayari wameshaanza kupanda ndani ya ile gari,ndani ya siti yangu ilitakiwa tukae watu watatu hivyo nikawa mimi na Baba mmoja akiwa na mke alikuwa anaonesha kuzidiwa sana nadhani alikuwa mgonjwa kwani alikuwa akilia sana mwenyewe na msaada mkubwa ulikuwa kwa mume wake.

    Safari ya kutokea pale Iringa na kuelekea Dodoma ilikuwa imetimia huku nikiamini kabisa nikifika Morogoro nitashuka na kuliacha gari likiendelea na safari yake ya kuelekea Dodoma.Safari ilivyokuwa inazidi kuendelea ndipo nilipoamini kuwa wale walikuwa ni wazazi wa marehemu Pendo kwani stori alizokuwa ananipigia Baba Yule dhahiri zilihamisha hisia zangu nakuamini moja kwa moja ni Baba Pendo na Yule Mama aliyekuwa akilia muda wote ule alikuwa ni Mama Pendo,alikuwa na uchungu sana na mwanaye na alitapika karibu njia nzima safarini,

    nilishikwa na aibu ikiambatana na hasira huku nikijikuta Napata moyo wa huruma nakuropoka,

    “mzee,mzee mimi ndio niliomuua Pendo”



    nilijikuta nimeropoka kila kitu huku kwa ghafla yule mzee akamuwahi kumshika mke wake kisha alinigeukia na kuniuliza tena.

    “binti ulikuwa unasema? samahani sana sijakusikia vizuri nilikuwa namuwekea karibu na mdomo mama yako mfuko aweze kutapika”

    aliongea yule mzee bila ya kuonyesha wasi wasi wowote kama kuna neno baya ambalo Levina mimi nimeropoka,

    “nilitaka kukupa mfuko huu hapa mkubwa nimeona huo mdogo hautatosha kwa maana mama anatapika sana..”

    nilimjibu kwa kuzuga huku macho nimeyaelekezea chini kwa aibu kubwa niliokuwa nayo pale, nilijifanya kihere here kwa kumpa maji yakunywa yule mama aliyekuwa anatapika ambaye ni mama yake na Pendo,

    Mzee alinishukuru sana kwa wema wangu japokuwa ukweli nilibaki nao moyoni,

    “Umesema binti unaelekea wapi?”

    Aliniuliza yule mzee na kwa mda ule tulikuwa tukiendelea kupiga story za kawaida kuhusiana na maisha njia nzima japo ukweli kuhusu pendo nilikuwa nao moyoni,

    “Naelekea Dar es salaam kutafuta kazi”

    “Kazi gani binti yangu?”

    “Naenda kutafuta kazi za ndani”

    nilimdanganya sana kuhusu maisha yangu kwa ujumla na aliweza kuniamini kwa asilimia kubwa kuwa anatokea Iringa naelekea Dar kutafuta kazi za ndani,

    ile roho ya kikatili,ilikuwa imeshaanza kunikabili kwani sikuwa hata na huruma ya aina yoyote,huku tukiwa tumeshasafiri mwendo wa kama masaa manne hivyo nikamwambia mzee kwakua gari ilikuwa inapitia Morogoro halafu ndo inaenda Dodoma ilinibidi nimwambie mzee kuwa tukifika morogoro anishtue kwa sababu nimeshapasahau sitapakumbuka vizuri.

    Ndani ya masaa kama sita huku kausingizi kakiinipitia mzee alinishtua na kuniambia kuwa tulikuwa tayari tupo maeneo ya mzumbe tukikaribia kuingia morogoro,hivyo niwe tayari nisilale tena, nilianza kujawa na furaha isiyotabirika huku furaha yangu zaidi nikiielekeza katika mifuko ya ile traki suti niliyokuwa nimeivaa na kuchomoa zile karatasi za ramani kisha nikazing'ang'ania mikononi mwangu nikisubiri niingie Morogoro.





    ***********





    Hatimaye tuliiingia ndani ya mkoa wa Morogoro,. Nilimuaga mzee pale lakini nilishindwa kumuaga Mama kwakuwa tayari alikuwa ameshapitiwa na usingizi.

    “usijali binti utafanikiwa nakutakia maisha mema na ubarikiwe upate kazi na uishi kwa amani huko uendako”

    yale maneno hayakuniingia akilini hata kidogo kwani hayakuwa na ukweli wa aina yoyote pale ila niliamua nimuitikie tu kwa kumridhisha yule mzee,

    “ahsante sana mzee na poleni sana kwa msiba uliowakuta”

    Nilimwambia huku nikionesha tabasamu la huruma la uongo. Nilimpa mkono kisha nikamuaga kuelekea stendi ya upande wa pili huku yule mzee akiamini kabisa kuwa nlikuwa naelekea dar kumbe naweka kwanza kituo.





    ************





    Muda ulikuwa umeshatimia kama saa nane mchana huku kukiwa na hali ya uvugu vugu iliyojawa na baridi lakini siyo kali sana kama la Iringa kwani manyunyu yalikuwa yakidondoka taaratibu kuashiria mvua inataka kunyesha. Huku nikiwa nimejikunyata mikono yangu niking'ang'ania zile ramani ndani ya mifuko ya suruali, niliweza kutoa na kufungua mojawapo ya ramani iliyokuwa inaelekeza kwa 'Baba Ali' huku nikiiongoza inavyoelekeza,

    “sasa, hapa ndio nimeambiwa panaitwa 'Boma Road' na ramani inaelekeza kota hizi hizi, embu ngoja nimuulizie huyu mtu.”

    “Samahani kaka, sijui unamfahamu 'Baba Ali'?”

    Nilimuuliza mpita njia niliyeamini kuwa atanisaidia kumpata mtu ninayemhitaji,

    "Baba Ali..Baba Ali.. Yeeah, nimemkumbuka anaishi maeneo ya paleee juu tena mnene hivii alikuwa anaishi na mke wake na watoto lakini sasa hivi anaishi peke yake?"

    “Ndio huyo huyo”

    Nilimuitikia tu huku nikiamini atakuwa ndo huyo huyo kutokana na maelezo aliyonipa Gervas,

    “Nyosha na hii barabara ukifika pale njia panda anza kuhesabu nyumba ya kwanza mpaka ya tatu ndo hapo hapo”

    “Ok, asante sana”

    furaha ilinizidia zaidi ya pale nilipokua naelekezwa sikutaka hata kugeuka nyuma akili yangu ikaelekea mpaka kwenye njia panda na nilipofika kwenye lile eneo nikaanza kuhesabu nyumba ya kwanza mpaka ya tatu, nikaingia ilikuwa ni nyumba kubwa iliyojaa wapangaji mbalimbali nilipofika nikapokelewa na majirani na kuwaulizia 'Baba Ali' kisha wakaninyoshea chumba anachoishi na kuanza kugonga hodi,

    “karibu karibu”

    ilisikika sauti yakiume niliyoamini ndio mwenyewe 'Baba Ali..'

    “Wewe ndio baba Ali?”

    “Ndio mimi karibu binti,”

    Niliingia ndani kwake japo alikuwa na chumba na sebule,ni kweli sikuona dalili yoyote ya mke wala watoto ,niliweza kumwelezea matatizo yangu yote kisa cha mimi kupelekwa gerezani na wema wote alionitendea mdogo wake ambaye ni Gervas, Misukosuko yote hadi nilivyokwenda kwa Gervas akanipa ramani mpaka nimefika hapa. Aliitikia kuwa ilikuwa ni kweli alikuwa akimfahamu Gervas kama ndugu na alikuwa akiishi na mkewe na watoto lakini wameshaachana na kuhusu kuelekea nyumbani kwetu nisijali kesho yake atanipeleka mpaka mlangoni kwetu, hivyo akanizidishia furaha na msisimko ndani ya mwili wangu zile ramani zikawa hazina tena maana kwangu nikampa akazichukuwa na kuzifinyanga kisha akaenda kuzitupa nje.

    Ilikuwa imeshatimia saa tatu za usiku hivyo aliniandalia maji ya kuoga nikaenda kuoga niliporudi nikakuta kashanunua chakula (chipsi mayai) hivyo tukakaa mezani na kula. Baada ya hapo alinielekeza chumba nitakacholala kisha taa zikazimwa nikamwacha akijilaza kwenye kochi pale sebuleni.



    Ulikuwa ni usiku wa manane nikiwa nimejifunika shuka sio zito sana huku nikiwa nimejikunja kwa kaubaridi kalichokuwa kakininyemelea nilianza kuhisi kama kuna mtu anahema mgongoni mwangu tena kwa pumzi ya hali ya juu,nilipaamini sana pale na pia nilivyomuheshimu 'Baba Ali' sikufikiria hata kidogo kama anaweza kunifanya chochote. Kadri muda ulivyokuwa unaenda ndivyo nilihisi kama mikono inapenya katika makwapa yangu kisha inashika na kutekenya matiti yangu huku ikiteleza kwa kunipapasa pasasa ikihamia taratibu katika sehemu zangu za siri na kuanza kuzitekenya, nilishtuka lakini kwa ujasiri niliokuwa nao sikutaka kupiga kelele kwanza mpaka nimjue ni nani anayenifanyia vile, sasa nikawa napapaswa maeneo ya mapajani kwangu huku yule mtu akigeukia upande wa mbele yangu.

    “Kohh..! Kohh..! Kohh..!”

    Nikakohoa kwa nguvu japo yule mtu ashtuke lakini hukutaka kuniachia,

    “Wewe nani? Naomba uniache..!”

    Niliamua kutoa sauti ya juu kidogo huku nikiwa na hasira kali na mishipa iliyonitanda usoni, lakini haikusaidia kwani kilichofuata nilihisi kama panga au kisu kikiumana na sakafu kisha haraka taa ikawashwa!

    “Heee Bab Ali..?”

    Sikutaka kuamini hata kidogo kwani ni kweli alikuwa 'Baba Ali' juu ya kifua changu, aliyejitambulisha na kunipa hifadhi hapa kwake ndo alikuwa akitaka kunibaka.

    “Shhh. Nani Baba Ali..?

    Tena ukome siku nyingine kuniita hivyo.Gervas mie simjui na huyo 'Baba Ali' unayedhania ni mimi siyo na huko kwenu sikujui malaya mkubwa we..!”

    Yale maneno yalinichoma sana sikuwa na jinsi kwakuwa alinishikia panga na kunilazimisha kufanya atakavyo hivyo akaniingilia kinyume na maumbile usiku kuchwa huku akinisababishia maumivu makali na damu nyingi kunitoka mwilini mwangu.

    Sikuweza kupata usingizi hata baada ya kunifanya atakavyo na kuniacha

    pale usiku uleKitandani nikiwa sijiwezi. Nilimshuhudia akichukuwa suruali yake na kutoa noti

    ya shilingi elfu moja na kunipatia..

    “We Malaya, chukuwa hii itakusaidia

    japo ukapate chai”

    “Nilijikuta napandwa na hasira kali, huku

    nikihema haraka haraka pale bila hatakuongea chochote. Nilichukua ti

    sheti yangu na ile traki suti nyeupe aliyoniachia Gervas kisha nilimgeukia

    na kumwambia...”

    “Ahsante sana kwa wema wako ulionitendea”

    Kisha nilitoka nje,kupitia kwenyekakorido ambapo pembeni kulikuwa na beseni la vyombo vichafu vya

    majirani kwa bahati nzuri nilikiona kisu katika vile vyombo hivyo halmashauri

    ya kichwa changu ilifanya kazi fasta.nilikichukuwa na kurudi ndani kwa

    kasi ya ajabu na kumkuta 'Baba Ali' akiwa kainama chini uku akifungakamba za viatu,nikamuwahi kabla

    hajageuka na kuinuka na kumchomakisu cha mgongoni kisha

    nilikichomoa haraka na kumuwahi

    tena kabla hajapiga kelele na kumchoma tena maeneo ya shingoni kisha nilichukuwa kitambaa na

    kumjaza mdomoni ,hivyo nikamshuhudia 'Baba Ali' akigala galapale chini huku akitoa macho na

    mishipa ya shingoni ikimlegea.Zoezi lililofuata ni kuingia mpaka chumbani kwake na kutafuta hela zilipo, nilitumia kama dakika tano bila ya mafanikio huku nikishuhudia kuona madawa ya kulevya pamoja na

    vitambulisho mbalimbali vya watu tofauti feki hivyo nikagundua kuwa'Baba Ali' alikuwa ni jambazi tena suguLililoshindikana tena lilikuwalikitafutwa, baada ya kutafuta hela bila

    ya mafanikio hatimaye nilifanikiwa kuzipata pesa nyingi sana kwenye kisanduku alichokuwa amekificha chini ya kitanda, lakini mimi nilikuwa nahtaji kama shilingi elfu hamsini tu hivyo nilizichomoa,

    “Liwalo na liwe..!”

    Nilijihisi kama yule stelingi wa muvi za

    kichina 'Jet Li', kwakuwa ilikuwa usiku

    sana kama mida ya saa kumi, niliweza kutoka pale bila hata ya kuonana na majirani wowote haraka haraka nikafuata ile njia niliokuja nayo nakuondoka kuelekea msamvu ambapo

    ndipo ilipo stendi ya mabasi ya mikoani.



    *********



    Nilikuwa tayari nimeshakata tiketi katika basi la ‘Abood’, safari ya kutoka

    Morogoro kuelekea Dar ilianza nilikuwapo ndani ya basi la kwanza

    kabisa lililotoka sa kumi na moja nanusu, na tangu nilipoingia katika basi sikuwa na wasiwasi wowote kwani moyo wa kishujaa na kijasiri ulikuwa umenitawala, lakini sasa takribani nusu

    ya watu kwenye lile basi walikuwa wakinishangaa huku wakiangaliana na

    kutikisa vichwa vyao, nilishindwa kujizuia nikajiangalia juu mpaka chini.

    “Mmmh...! M mmmh...!”

    Safari hii niliweza kuwahi kujiziba

    mdomo ili nisiropoke jambo lolote baya kwani traki suti yangu yote ilikuwa

    imejaa damu huku na mikono yangu ikitapakaa damu mpaka sehemu za

    usoni kitendo kilichofanya njia nzima abiria wanishangae kwa kuwa vile.

    Tukiwa tunakaribia kuingia chalinze, Basi letu likasimamishwa na trafiki

    wawili mmojawapo akiwa ni askari polisi,kwa mara nyingine moyo ukawa

    kama unawaka,nywele zilinisisimka huku mdomo ukinitetemeka kisha

    nikalitega sikio langu kwa upande wa nje kusikia maneno ya kondakta wa

    basi letu akiwa na trafiki.

    “Umesema mmepakiza abiria wangapi?”

    “Sitini na mbili tu”

    “Hakuna waliosimama?”

    “Hakuna”

    “Usiniambie hakuna wacha nipande

    niingie nijionee mwenyewe ndo uniambie hakuna sawa?”

    Maneno hayo yalinifanya nizidi kulegea kwani aliyekuwa anaongea na

    kondakta alikuwa hajavalia mavasi meupe bali alivalia mavazi ya kaki yale

    yenyewe ya polisi huku akiwa kashikilia bunduki akapanda ndani ya

    basi huku akiangaza siti moja baada yanyingine na alipofika kwangu..

    “We vipi tena Mmepata ajali wapi?”

    “Hatujapata ajali yoyote huyo kapanda

    basi hivyo hivyo..!”

    Aliropoka dereva wa basi huku akisaidiana na kondakta

    wake kunimaliza.

    “Haya shuka… Shuka upesi chini… We dereva endeleeni na safari yenu"

    Nilijikuta nipo mikononi mwa yule polisi haraka akiniwahi kwa kunifunga pingu baada kushushwa chini nakuacha basi likiendelea na safari.

    “Mungu wangu...! Mungu wangu...!

    mbona umeniacha..? Mbona wanitenda hivi....!”

    Nilijikuta nikiandamwa na mikosi na kumshushia lawama Mwenyezi Mungu

    alieniumba na kujiona sifai kuishi katika dunia hii, huku nikiwa chini ya

    ulinzi pale barabarani,Yule askari polisi akaniangalia juu mpaka chini akawa

    anatingisha kichwa huku akicheka kuashiria kama mtu anayenifahamu

    sana..

    “Levina..?”

    Sikuamini amini kama jina hilo atakuwa amelitaja yule askari au ameambiwa na

    mtu kuwa naitwa Levina, nilihisi kama moyo ukinipasuka ghafla, hivyo nikawa

    sina tena jinsi kwani nikawanimeshapatikana, lakini swali lililoniumiza kichwa ni kwamba nipo

    pale kwa kosa lipi la mauaji?

    “maskini isikute baba yake 'Pendo ndo kamtuma huyu polisi..? ....Au,

    nilivyomuua 'Baba Ali taarifa zimemfikia

    huyu polisi..?”



    Nikiwa bado najiuma uma pale huku akili ikiwa haifanyi kazi kabisa,ghafla

    nikamuona yule polisi kabadilika zaidi ya pale kwani sura yake ilikunjamana

    ghafla huku akinifokea.

    “Kwanini umeua Tena..?”

    Lile swali lilinifanya nilegee nakudondoka mpaka chini kwani

    nilikuwa sina nguvu tena ya kusimama huku nikishindwa kujua kipi cha

    kufanya pale chini.

    “Au unapenda kwenda tena gerezani,

    naona safari yako nyingine sasa

    imefika..?”

    “Hapana nisamehe afande sijakusudia nii...l...ii...piii...ti...wa..., tu..na shetani..?”

    Kabla sijamalizia kujitetea nilishangaa

    kuinuliwa kwa kushikwa shati kwanguvu kisha kilichofuata ni kupigwa

    vibao na mitama huku nikishindwa hata kujizuia kutokana na zile pingu nilizokuwa nimefungwa mikononi. “Kaka mkubwa, wacha nimpeleke

    kituoni Dar huyu mpumbavu ana kesi kubwa na nitampigia simu afande

    Geofrey aje msaidiane hapa..”

    Nilijihisi kama mtu asiye na bahati hapa duniani, maumivu aliyonisababishia

    'Baba Ali wakati akiniingilia kinyume namaumbile ukiongezea maumivu

    aliyonisababishia huyu polisi vilinifanya niumie sana moyoni, huku mwili wangu

    ukiwa hautamaniki kwa majeraha.

    “Ingia kwenye gari mpumbavu wee..!”

    Aliendelea kunikaripia yule polisi ambaye sikumfahamu kwa jina lakini lafudhi aliyokuwa akiongea ilinifanya niamini kabisa atakuwa ni muhaya tena yule wa kule Bukoba ndani ndani (Vijijini),Tukiwa ndani ya ile gari aina ya 'One Ten' huku nikiwa nyuma na askari mmoja na yule mwingine akiwa anaendesha gari, Ujasiri wangu feki niliuweka pembeni hivyo nikawa ni mtu wa kutoa machozi na kujiuguza sehemu zilizoonesha kuumizwa katika mwili wangu,njia nzima mpaka tunaingia Kibaha nilikuwa mtulivu bila kusemeshwa kitu chochote na yule polisi,Tulipofika maeneo 'Mbezi' yule polisi akafungua kinywa chake na kuniuliza”

    “Unasikia njaa..?”

    “Kimya….!”

    “Dereva embu pitia pale 'Mnama Restaurant' tupate chochote...”

    Maswali aliyoniuliza na maongezi aliyokuwa akiongea na dereva ndo kati ya vitu vilivyoanza kuuchanganya ubongo wangu.

    “Mbona kabadilika tena huyu polisi..? Asije kuwa wananifanyia njama kama Baba Ali..?”

    Kwanini wameniagizia chakula kama kweli nina hatia? Sijui nimuulize kosa langu ni lipi hapa hapa..?”

    Nikiwa bado nimekaa katika kiti cha mgawaha mmoja pale mbezi nikiwa mimi na polisi wawili mmojawapo ndo yule aliyekuwa akinishikia bunduki na ndo aliyenifunga pingu,

    “Wewe muuaji unakula nini?

    “Hapana..., Sili chochot..." kabla sijamalizia kusema nilishtukia napigwa na kitako cha bunduki na yule yule polisi.

    “Usitufanye siye wapumbavu, kuua uue..! Tunakuonea huruma japo na wewe upate chochote unatuletea 'usenge' au umeshazoea maharage ya Gerezani nini...?”

    Nilijikuta nanywea na kuwa mdogo na kukubali kula chakula kama walichoagizia wao ambapo walikuwa wakila wali nyama.

    Ndani ya nusu saa nikarudishwa tena kwenye lile gari lakini safari hii nilishangaa hawakunifunga tena pingu mikononi hivyo nikabaki na maswali mengi sana kichwani.



    Mawasiliano ya mimi na wale askari bado hayakuwa mazuri kwani hadi tunapita kimara hakuna hata mmoja aliyenisemesha zaidi ya yule mmoja kukaa karibu na mini nisiweze kutoroka huku mwingne akiwa dereva ndani ya ile gari.

    Mawazo yalitawala sana kichwa changu huku nikijiona si mtu tena wa kuonana na mama yangu wala Gervas.., Nikiwa bado niko kwenye dimbwi la mawazo huku tukiingia kwenye foleni ya mataa pale ubungo ghafla macho yangu yakaamia kwenye gari la pembeni yetu aina ya 'suzuki' hasira nilizoshikwa nazo ghafla ziliwafanya hata abiria waliokuwa ndani ya daladala ambayo ilikuwa nyuma ya ile gari niliokuwa nimeikodolea macho waweze kunishangaa, Hilo sikulijali kabisa maishani mwangu kwani Levina mimi aibu ilishanitokaga siku nyingi ukianzia pale shuleni kwa kina Gervas waliponigalagaza wale wanafunzi, pia katika basi nililokuwa nimeshushwa hvyo ukinishangaa mi ntakuona mtu wa ajabu sana,

    Akili na mawazo yakiwa bado ndani ya kale ka suzuki ambapo macho yangu yalikutana uso kwa uso na Mama ambaye sitakuja nimsahau hata nife, hakuwa mwingine bali ni yule mama aliyenipeleka polisi kwa mara ya kwanza na ndiyo aliyefanya maisha yangu yapo hivi mpaka sasa,

    “lazima nife mimi au wewe”

    Nilijisemea kimoyomoyo huku nikimtolea macho yalioambatana na mchozi ulioanza kuniteremka kwa ghadhabu niliyokuwanayo, Kilichofuata ni kuhema haraka haraka huku pua zangu zikianza kujaa makamasi kama mtu aliyepatwa na mafua ya ghafla.. Kama kawaida yangu sikutaka kuchelewesha muda.

    “Bunduki kitu gani wacha anifyatue tu lakini kwa huyu adui yangu siwezi kamwe kumuacha…”

    Nikatoka spidi katika lile gari nililokuwa huku nikimwacha yule askari akinilenga huku akinikimbilia lakini hilo sikulijari ndani ya sekunde chache nikawa nishafungua na kuingia kwenye ile suzuki na ku loki milango yote tayari kwa kumvagaa yule mama aliyekuwa akiendesha peke yake ndani ya kale kagari.

    Nilitumia kucha zangu na meno kama filamu zile za kutisha 'VAMPIRE' kuisambaratisha kwanza sura ya yule mama kisha nikachukuwa mtandio wake aliokuwa nao amejifunga mabegani na kuuvingirisha shingoni mwake tayari kwa kumnyonga, Akiwa bado anakurupuka na kutapatapa pale gari zilikuwa tayari zimeruhusiwa na trafiki na wale polisi niliokuwa nao tayari niliweza kuwaona wakiwa nje wanataka kuingia ndani nilipokuamo, Sikujua hata siku moja kuendesha gari lakini nilisikia kwa wenzangu tu kuwa kuna kitu kinaitwa gia kipo kama rungu pia kingine kinaitwa ‘krachi’ kipo miguuni, sikulielewa hilo lakini nilijikuta nimekanyaga chini bila kujua kama ndio breki au ndo hiyo krachi kisha nikalishikilia rungu na kulisogeza kisha nikashangaa kuona gari ikitoka tena kwa mwendo wa kasi pale,nikiwa huku nimekaza ule mtandio shingoni mwa yule mama huku upande mmoja nikishikilia msteringi nilijikuta nimevamia gari za watu wengine waliokuwa mbele yangu na kusababisha ajali mbaya pale huku umati wa watu ukifurika katika lile eneo kushuhudia ile ajari.

    Watu walikuwa ni wengi sana mpaka nikachanganyikiwa japokuwa nilijihisi mwili wote haufai kwa maumivu, ile gari niliokuwa nayo ilikuwa imeharibika vibaya baada ya mda mchache nilihisi kuna watu nje wanavunja vioo vya gari wanataka kuingia ndani katika kuangalia vizuri macho yakamwona yule polisi alionifikisha hapa nilipo..,

    “Levina...! Levina...! Jisalimishe mwenyewe unajitafutia matatizo”

    Yale maneno ya yule polisi aliyokuwa akiniambia, hayakuniingia akilini mwangu kabisa niliona kama anampigia mbuzi gitaa ili acheze.yule mama sikujua kama alikuwa amekufa ila nilimwacha pale akiwa anahema kwa kasi ya juu huku akiwa hajitambui wala hajiwezi hata kunyanyuka,haraka haraka nikafungua mlango upande wa nyuma kisha nikatoka spidi huku nikiuacha umati wa watu ukiwa haujui nini kinaendelea kutokana na lile tukio..

    Spidi niliyotoka nayo pale huku watu wachache wakinishangaa si kwasababu nimeponea chupuchupu kwenye ile ajali bali pia waliniona kama mtu aliyechanganyikiwa kwa jinsi nguo zangu zilivyokuwa hazitamaniki kwa uchafu tena ule uliokolea damu katika ile suruali aina ya trakisuti ilivyobadilika rangi nyekundu iliyokuwa imetapakaa damu na kuwa kama nyeusi nyeusi,

    Sikumuogopa hata mtu nilizidisha mbio huku nikielekea barabara ya kwenda mwenge, kelele za wapiga debe pale ubungo ziliongeza hisia zaidi ndani ya kichwa changu kwani kitendo cha kugeuka nyuma ilikuwa kosa kubwa sana kwangu kwani niliamini na kujua tu lazima umati mkubwa wa watu uwe unanikimbiza nyuma yangu huku, nikiwa nasonga mbele haijapita hata hatua ishirini mara kundi la watu wengine wakawa tayari wametanda mbele ya macho yangu.



    *********



    Baada ya yule polisi kunishika ndani ya basi akanifunga pingu baada ya pale akatikisa kichwa chake kuashiria kuwa ananifahamu akaniita na jina

    “Levina...!”

    “kwanini umeua tena?”

    “Au unapenda kwenda gerezani tena”

    Hayo ni kati ya maneno ninayoweza kuyakumbuka kwani yalinifanya niishiwe nguvu na kudondoka mpaka nikapoteza fahamu,ninachokumbuka nilishtuka na kushuhudia nikipepelewa na yule polisi huku nikiwa kwenye gari ambayo sikuitambua vizuri kwa nje kwani alikuwa amenilaza ndani ya lile gari na mikononi mwangu bado nilikuwa na pingu hivyo nilipopata usingizi akaendesha gari mpaka nakuja kushtuka tumeshafika Dar na nilikuwa nikiota ndoto tena matukio ya ajabu ajabu kama lile la kumuua yule Mama na kuharibu vibaya lile gari lake pia kufukuzwa na umati mkubwa wa watu pale ubungo.

    “Mungu wangu kumbe yote yale ilikuwa ni kama ndoto..!”

    Nilijikuta nausemea moyo huku nikishusha pumzi kubwa.

    “Uuhh...! Uuuhh...!”

    Taaratibu nikiendelea kuhema kwa nguvu na hasira kali,

    “hapa ni wapi?”

    Nilijikuta nikimuuliza swali yule polisi aliyenitoa kule Chalinze na ndiye alikuwa amenipakia baada ya kuzimia pale Chalinze.

    “Hupaswi kuja. Unapaona pale?”

    “Nikakaa kimya…”

    Huku nikiona kibao kimeandikwa mbele yangu.., 'CENTRAL POLICE'

    Nilitamani kutoroka pale lakini nisingeweza kwani mda wote nilikuwa na pingu mikononi.

    “Levina...! Embu niambie ukweli hizo damu katika hiyo suruali ilikuwaje?”

    Nikawa najiuma uma nashindwa nimpe jibu gani kwani ni kweli nimeua lakini nikisema ajue itanigharimu sana maishani mwangu.

    “Afande hizi ni damu za kawaida tu ambazo nilipitia buchani kuchukuwa nyama na kupeleka nyumbani nilipokuwa kule Morogoro..!”

    Nilijikuta namdanganya lakini kiukweli alionesha kuchekeshwa na mimi sana mpaka nikamshangaa.

    “Levina acha kunichekesha we mtoto...

    Mbona kule nilipokushusha kwenye basi nilikuuliza swali kama hili na ukaniambia kweli umeua ila kwa bahati mbaya..?”

    “Mi mi...?

    Labda utakuwa ulisikia vibaya afande....”

    Nilijitahidi sana kujikaza na kubadilika lakini yule askari hakuridhika na majibu yangu,na kwa safari hii hakuwa mkali wa kunipiga bali nilimshangaa pia kwa kuongea na mimi ndipo akataka kuniambia ukweli sababu kubwa ya kunichukuwa na kunileta mpaka maeneo haya kituo cha polisi endapo tu nitamjibu maswali yake kikamilifu, huku tukiwa tumeliangalia lango la kuingia polisi.

    “Sitapenda nikuingize tena pale polisi najua utateseka sana mpaka uje kutoka tena mdogo wangu,ila kitu kimoja ninachotaka kuongea na wewe ni unipe jibu moja tu ili niweze kukusaidia..

    “Huko ulipotoka umeua?

    “Sijaua na naogopa sana kuua maishani mwangu..!”

    Nilimjibu mara ya pili lakini kwa sasa nilianza kuonesha kauoga, Kwani nilianza kuingiwa na hofu huku nikitoka jasho jembamba mwilini mwangu na niliamini kabisa ntakuwa nategwa.

    “Mimi nataka kukusaidia Levina lakini unakuwa mbishi si ndio..?”

    Alianza kubadilika yule afande huku akinikodolea mijicho na kunionesha ufunguo wa zile pingu kuwa kama nitakuwa mkweli atanifungua pingu kisha nitakuwa huru na salama, Kitendo kile kikanifanya uzalendo uanze kunishinda na kujikuta namjibu anavyotaka,

    “ni kweli nimeua lakini si kwa kukusudia..”

    “Umeua..? ..Nani uliyemuua Levina?”

    “B...aa..a..a..b..a.. A...l..i..”

    Nilitaja jina kwa kujiuma uma pale pale yule afande akabadilika ghafla na kugeuza ile gari kisha safari ikaanza lakini sikuweza kujua ni wapi nilipokuwa napelekwa zaidi ya kushuhudia akitoka kwa mwendo wa kasi huku nikiwemo ndani ya lile gari lake.

    Mwendo wa kasi aliotoka nao yule afande haukuwa wa kawaida, kwani nilijikuta nabilingita ndani ya lile gari lake huku mikononi pingu zikinishika vilivyo.

    Nilichoweza kuambulia kujua ni pale tulipokatisha maeneo yalionesha kuwa na maduka mengi huku daladala nyingi zikiwa na mstari mwekundu katikati na maandishi yaliosomeka 'ubungo - k/koo, hvyo halmashauri yangu ya kichwa ikanituma moja kwa moja na kujua tayari nimeingia maeneo ya kariakoo,nikiwa ndani ya gari huku yule afande akiliendesha gari mithili ya mtu aliyeliiba lile gari au kuna mtu anamfukuzia nilishangaa pia kulipita tena kwa kasi eneo lile ambalo nilishawahi kukaa rumande kipindi kile cha kesi yangu si kwingine bali ni kituo cha polisi cha 'MSIMBAZI'

    Safari ilizidi kusonga mbele kwani tulikuwa maeneo kidogo ninayoweza kuyatambua

    Kama vile tulikuwa kiprefti cha kamata lakini maswali mengi kichwani mwangu yalinizidia bila ya kuwa na jibu.

    “Samahani afande..”

    “Samahani ya nini? Na unataka nini tena?”

    Majibu yake bado yakanifanya niishiwe nguvu.

    “Nahitaji kujua tunaelekea wapi?”

    “Nyamaaaazaa..! Tena kimya nisikusikie tena ukiongea..!”

    Ilinibidi niwe mpole huku nikishindwa kujielewa na kujiona sina umuhimu tena hapa duniani,na sasa nilikuwa tayari kwa lolote litakalonikuta mbeleni.

    “Bora hata akaniue nijue moja kuliko kuendelea kuteseka namna hii”

    Niliusemea moyo maneno ya ajabu, Muda wote moyo ulikuwa ukinienda tena kwa kasi ya ajabu huku kichwa kikiniuma sana nafikiri yote ni kwasababu ya kuwaza sana,Mara tukasimama eneo kama nilikuwa nalifahamu kisha yule afande akachukuwa funguo zake na kunifungua ile pingu,

    “Twende..”

    Mara nikashangaa kushuka naye huku kanishika mkono,lakini nikawa bado na wasiwasi kwani ile nyumba mbele yangu kama naifahamu japokuwa ilikuwa imepakwa rangi,niliendelea kumshangaa yule afande kunizungusha nyuma ya ile nyumba na kukutana na kaburi kubwa likiwa limeng'arishwa kwa kuezekwa marumaru nyeupe zilizong'aa mithili ya kioo,huku katikati kukiwa na picha kubwa..

    “Uuuuwiii..! Uuuuwiii...! Uuuuwiii...! Baaaba umeniacha...! Najua mimi ndio chanzo,nisamehe Baba yangu...! Baaaaaaaabaaaaaaa...!”

    Nililia sana na kwa sauti ya juu huku nikiamini ile picha ni ya baba yangu na pale tulikuwa eneo la nyumbani kwetu japokuwa hakukubadilika sana,sauti ya juu niliokuwa nikilia iliwafanya majirani kuja kushuhudia pale huku mlango wa nyuma ukifunguliwa..

    “Maaaamaa..! Maaamaa...! mnisamehe miiimi...”





    * * * * *



    ‘Afande Deus’ ndio jina lililokuwa likitambulika sana kazini alipolitumikia jeshi la polisi, weusi na urefu ukichangia kuwa na mwili mkubwa ni kati ya vitu vilivyomfanya kuogopeka katika jamii haswa ukizingatia ukali aliokuwa nao akiwa kazini, hakuwa na cheo sana lakini uonekano wake ulimfanya aonekane kama mtu mwenye cheo kikubwa, Kazi yake kubwa ilikuwa ni kusindikiza watuhumiwa wa kesi mbalimbali mpaka mahakamani na kuwarudisha tena rumande huku akisaidiana na mapolisi wenzake,

    Alianza ukaribu na Baba yake Levina toka kipindi kile cha kesi ya Levina na hii yote ni kufanya levina anakuwa huru,alijitahidi sana mpaka kuwashawishi wakubwa wake ili Levina awe huru lakini ilishindikana na matokeo yake alisimamishwa kazi kwa mda mrefu wakamfanyia upelelezi ikaonekana hakuna ukweli ndani yake hivyo baada ya mda mrefu kidogo akarudishwa tena kazini lakini haikuwa mwisho wa kuwa karibu na Baba Levina kwani hata alipofunga ndoa msimamizi wake alikuwa ni Baba yake Levina na alizawadia gari ndogo ya kutembelea, Tayari walikuwa kama familia moja na hata Baba Levina alipofariki afande Deus aliumia kweli kwani alifanyiwa mengi sana ikiwa ni pamoja na kununuliwa kiwanja na kusaidiwa pesa kidogo za kujenga.

    Afande Deus aliahidi hata siku Levina akiwa huru atamsaidia kwani ilikuwa ni vigumu kumfatilia tena Levina Gerezani akiwa kama afande anayejulikana na aliyewahi kusimamishwa kazi kwa kesi ya huyo huyo Levina.

    Akiwa bado kikazi na magwanda yake ya kipolisi na bunduki yake akitokea chalinze kuwasindikiza wazazi wake waliokuja kumtembelea Dar, alikutana na rafiki yake waliyewahi kusoma pamoja ambaye ni trafiki, kwa utani waliozoeana aliweza kukagua mabasi mawili ndipo akamgundua Levina alikuwepo kwenye basi moja wapo,lakini ili kuua soo ilimbidi ajifanye mkali ili aondoke naye kiulaini.





    ~ BAADA YA MIEZI TISA ~





    “Umesema kapanda basi lipi?”

    “Sijui vizuri lakini likizo zote huwa anapanda basi la 'HOOD'”

    Haraka haraka, Nikatoka mbio kuelekea nyumbani nikampita mama sebuleni akinishangaa ndani ya dakika tatu nikatoka nikiwa nimevalia kiblauzi cha mikanda cha pinki chini nikipigilia kipedo changu cha jinsi huku chini kabisa nikiwa nimevalia viatu vyeupe aina ya 'Makhirikhiri' usoni nikiwa na zile miwani kubwa za kuzuia jua na hivi kamwili kalikuwa kamesharudi,mtoto figa ninayo,makalio ndo usiseme, yaani daaah...! Natamani kama ungeniona hivi? Kwani sikuwa tena Levina yule mliokuwa mnamjua zamani,

    Nilijipenda sana na hii yote ni kufanya Gervas na jamii kwa ujumla inione si Levina yule waliyekuwa wanamjua kipindi kilee cha matatizo.

    Nikiwa ndani ya daladala iliyoukuwa inatokea kariakoo na kuelekea ubungo kumpokea Gervas aliyekuwa amemaliza masomo yake ya kidato cha Nne huko Iringa, nikiwa nimekaa siti ya pembeni na Mmama nisiyekuwa namfahamu nadhani ni kutokana na mavazi aliokuwa amevalia aina ya 'Baibui'.

    Tayari ilikuwa ni alasiri kwani hata saa yangu ya pinki aliyeninunulia afande Deus ilinionesha imeshatimia saa kumi na robo na Gervas alikuwa aingie mida ya saa kumi na mbili kwenye na nusu,

    nikiwa tayari nipo kwenye foleni maeneo ya manzese huku nikizubaa kwenye gari kutokana na kuwa na mawazo na shauku kubwa ya kumuona Gervas,

    “Hapo dada, hapo mjomba...”

    “Mama hapo...”

    Ilikuwa ni sauti ya kondakta akidai nauli za daladala.

    “kaka si nimeshakupa? Unataka nini sasa?”

    Alilalamika kwa konda yule mama aliyekuwa pembeni yangu huku akioneshwa kuchukizwa na kitendo cha konda kumdai nauli mara mbili mbili,

    Tukiwa ndo tunaingia ubungo niliweza kumshuhudia yule mama akitoa baibui yake katika paji la uso huku akisogeza simu yake karibu na sikio aweze kuzungumza na simu..

    “kumbe namfahamu..! Mshenzi mkubwa we unabahati sana...!”

    Alikuwa ndio yuleyule mama niliyowahi kumuota namnyonga na mtandio pia ndo yule aliyewahi kuniharibia maisha yangu enzi zile,

    Sikutaka tena ugomvi kabisaa kwani afande Deus alinisihi mambo mengi sana ya kujihadhari nayo ikiwemo ugomvi usiokuwa na maana.,Hasira na chuki zilinishika lakini sikuweza kukabiliana naye.

    Saa yangu ilikuwa tayari inaonyesha ni saa kumi na mbili kama na dakika ishirini,Nikiwa tayari nimeshaingia mule ubungo ndani ya stendi ya mabasi.

    Hatimaye basi la 'HOOD' likaingia, Watu ni wengi walioshuka, Kila walipokuwa wanashuka ndivyo mapigo ya moyo yalikuwa yakinienda mbio, ghafla nikahisi kama kuna mtu ananigusa mgongoni nikajikuta nageuka bila kuangalia na kumkumbatia….

    “…..waaaooo Gervas...!”

    Maskini aibu kubwa ilinishika watu wakabaki wakinishangaa kumbe hakuwa Gervas.,bali alikuwa ni Mama aliyejitambulisha kwa jina la 'Mama Ali' huku akiwa na mtoto wake 'Ali' na vijana wawili wakiume waliovalia miwani meusi huku wakizunguka zunguka kuashiria wanakuja kumpokea ndugu yao.

    “Samahani binti mimi si Gervas..”

    “Nimeshajua hata mimi nimekosea ila naomba nisamehe”

    “Hamna neno kwani huyo Gervas ndo unamsubiria..?”

    “Ndio mama..ni ndugu na pia jirani yangu wa siku nyingi..”

    Nikiwa bado namjibu yule Mama aliyejitambulisha kama 'Mama Ali' mara nikamuona Gervas akishuka bila kuchelewa nikamuwahi na kumkumbatia,kisha wale vijana wakamuwahi na kuonesha vitambulisho vya kazi zao kilichofuata nikumshuhudia Gervas akifungwa pingu mbele ya macho yangu.

    “Kafanya nini tena..?

    Muacheni jamani.., Muaaaaaaaaacheni...!”

    Nilihisi kama ndoto lakini ilikuwa kweli Gervas kafungwa pingu bila kujua kosa lake.

    “Geeervaaaaaas...!”



    ********



    Taarifa za juu ya kifo cha 'Baba Ali' zilienea sana ikiwa ni kuanzia Kwa majirani Mpaka kwenye vyombo vya habari, Siku ya Mazishi 'Mama Ali' alizimia mara mbili ikiwa ni pamoja na kupata pigo la kuachwa na mtoto ambaye ni Ali tena mdogo sana akiwa na miaka minne tu,

    Upelelezi juu ya kifo cha ‘Baba Ali’ ulifanyika kwa haraka zaidi na kuanzia usaidizi wa Majirani ambao walimshuhudia mtu wa mwisho aliyeingia ndani kwa ‘Baba Ali’ hakuwa mwingine bali ni Levina japo majirani walimtambua kwa sura tu na si kwa jina.

    Uchunguzi uliofanywa kwa kina ulibainika kukutwa na karatasi mbili mifukoni kwa Baba Ali ambazo zilifinyangwa sana na zilionesha ramani ya anapoishi Baba Ali ambaye si huyu aliyeuliwa,

    Polisi walifanikiwa kumkamata Baba Ali mwenyewe na kumuweka hatiani kisha akafanikisha mpaka jinsi ya kumpata Gervas, hivyo polisi kwa kusaidiana na Mama Ali wakawa tayari stendi ya ubungo wakimsubiri Gervas,ambapo ilisemekana ameshapanda basi aina ya 'HOOD' hivyo kuanzia saa kumi na mbili atakuwa ameshafika Mama ali akisaidiwa na mapolisi wawili huku akishikilia picha ya Gervas aliyopewa na Baba Ali waliyemuweka hatiani kule Morogoro,wakafanikiwa kumpata Gervas.





    ******

    Nikajikuta navua viatu vyangu na kuvishika mikononi huku nikiitupa ile miwani kwani niliona haina umuhimu tena kwangu,

    Nilijitahidi sana nisiweze kupiga makelele eneo lile, nikabaki nafuta mchozi tu huku nikiwafatilia polisi kwa nyuma nijue watampeleka wapi,nikawaona wakiingia kituo cha polisi pale pale ubungo,nikashusha pumzi,kisha nikatazama ni jinsi gani naweza kuongea na Gervas,nikiwa bado najifikiria pale ghafla nikapigwa kikumbo na Mama Ali.,

    “Na huyu hapa tumchukuwe aliniambia ni ndugu yake..!”

    “Nani..? Mimi...! hapana...!, aah...! aah..!”

    Nilijikuta namkana Kama Petro alivyomkana Yesu mara tatu, Huku nikijifanya kama simjui Gervas kwakuwa nilikuwa tayari nilishalikoroga nilipomwambia mwanzoni kuwa Gervas ni ndugu na jirani yangu,

    “We binti.? Embu potea hapa haraka...!”

    Aliongea kwa sauti ya juu askari mmoja pale huku kanikazia macho.

    “Hapa leo siendi popote kama kurudishwa gerezani wacha nirudishwe mie na sio Gervas ambaye hana hata hatia.”

    Nilijisemea kimoyo moyo huku naongoza njia ya kutokea,

    “Lakini haiwezekani narudi, aah...! aah...!”

    Nilijikuta narudi tena huku nikiangalia saa yangu ikinionesha ni saa mbili kasoro usiku, hilo sikulijali kikubwa ni jinsi gani nitamtoa Gervas, Nikajikuta halmashauri yangu ya kichwa inafanya kazi fasta na kuchukuwa simu yangu tayari kwa kumpigia 'Afande Deus'..,

    “Haloo... Shikamoo Baba Deus..! Nipo hapa polisi

    “Wapi...? Na umefanya nini tena Levina...?”

    “Nipo hapa kituo cha polisi ubungo ndani ya stendi ya basi...”

    Nikiwa bado naendelea kumuelekeza Afande Deus nilipo, Nikashangaa ananikatia simu..

    Nilizidi kuumia moyoni kwani mimi ndio nilikuwa mtu wa kumsaidia Gervas ili aweze kutoka pale.,

    Ilimchukuwa lisaa tu kwa afande Deus kuweza kufika eneo lile,nikamshuhudia akipitiliza na kuingia ndani kituoni nadhani hakuniona vizuri nilipo hivyo nikamfuatilia kwa nyuma,

    “Jambo afande”

    “Habari, kuna binti yangu yupo humu ndani..?”

    “Hakuna binti yeyote aliyeletwa leo humu....!”

    Wakiwa bado wanajibizana nikajitokeza kwa nyuma taaratibu huku nikinyata….

    “Mimi hapa Baba...!”

    “Twende nyumbani..!”

    Alinichukuwa kiaskari zaidi huku nikitetemeka na kuelekea upande aliokuwa amepaki gari yake,nikaingia na kupanda gari yake kabla hajaondoka nikamwambia ukweli,

    “Baba...!”

    “Unasemaje tena..?”

    “Aliyekuwa amewekwa ndani siyo Mimi..?”

    “Nani sasa.?”

    “Ni Gervas…..!”

    “Naaaaaaaaaaaaaaaan….!”



    * * * *



    Nikiwa nimetulia kwenye gari peke yangu huku nikimwacha Afande Deus akirudi tena kituoni kumalizana na mapolisi wenzake kuhusu kutoka kwa Gervas, Haikuchukuwa muda nikamwona anarudi peke yake huku akitingisha kichwa kuashiria kuwa kashindwa kumtoa Gervas,

    “Wamesemaje..?”

    Nilijikuta naropoka nikitaka kujua.

    ”Imeshindikana mpaka kesho kwani ni kesi kubwa sana..!”

    Miguu ilinilegea,mwili ukaingiwa na ganzi,kichwa kikawa kizito mda huohuo huku nisijue nini cha kufanya, Gari ikawashwa tayari kwa kwenda nyumbani.

    Baada ya nusu saa tukawa tumeshaingia nyumbani kwani njiani hakukuwa na foleni kabisa,tuliweza kuingia nyumbani kwakuwa afande Deus alikuwa na haraka akaniacha nje na kuniaga kwa kuniambia kuwa kesho asubuhi atadamkia kwa Gervas,nikamuitikia na kuingia ndani,

    Nilipoingia ndani nikakuta hali si shwari kwani Mama alikuwa akilia sana bila kujua nini tatizo,

    “Au kwasababu nimechelewa kurudi..?”

    Nilijikuta najipa maswali yasiyo na majibu,

    nilijaribu kumnyamazisha lakini ilinichukuwa mda mpaka akanyamaza na kwikwi ikamuisha kisha akanipa barua aliyokuwa ameshikilia,nikaichukuwa na kuanza kuisoma huku presha ikinipanda na kushuka, nikiwa natetemeka





    * * * *



    Niliendelea kuisoma ile barua huku nikihisi kichwa changu kizito,huku ganzi ikinijaa mwilini,kadri nilivyokuwa naendelea kusoma ndipo kizunguzungu kikanizidia..,

    “LEVINA CHRISTIAN”

    Unahitajika Mahakama ya mwanzo mkoani Mbeya haraka upatapo barua hii..

    Uchunguzi wa kina uliofanywa na jopo la Madaktari kutoka Iringa imebainika kuwa Marehemu ‘Pendo’ amefariki kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali na mwili wake kuokotwa porini huko Iringa,

    Na siku alioachiwa huru gerezani alikuwa na wewe Levina Christian ambao wote mlikuwa wafungwa, hivyo ukiwa kama mtu ambaye uliongozana naye kutoka gerezani mara ya mwisho unahitajika na mahakama haraka iwezekanavyo kwa ushahidi juu ya kifo cha Pendo Abel...”

    Nilipomaliza tu kuisoma nikamgeukia Mama nakuanza kwani alikuwa bado anaendelea kulia tena kwa sauti ya chininini, kichwa na akili yangu vikiwa havifanyikazi, nilijihisi kujiharishia huku nikiwahi kulibana tumbo langu lililokuwa linaunguruma kwa kasi kisha nikamtazama mama yangu.

    “Nani ameileta hii barua..?”

    “Vijana wawili waliovalia nguo za kiraia wakiwa na gari...”

    Sikuhitaji kujua la zaidi,nilichofanya ni kumuhadithia Mama yote yaliyonikuta kuhusiana na Gervas,

    “Mama haiwezekani,inanibidi leo leo tena sasa hivi nifanye juu chini tena kabla hata afande Deus hajajua kitu chochote niwe nimeshaondoka na kwenda kulimaliza hili tatizo najua kesho asubuh Gervas atatolewa kwahiyo Mama nakuomba Gervas usimwambie lolote juu yangu”

    “Mama nakuomba sana.,sana tena sana..,

    Hii barua na hata hizi taarifa asizijue afande Deus,atashindwa kunisaidia kumtoa Gervas..!”

    “Mwanangu kwanini ni wewe tu jamani..?

    .......Kwanini mikosi yote inakuja kwako tu..?”

    Aliongea kwa sauti ya kukwaruza kuonesha kwamba amelia sana na sauti inataka kumkauka..,

    “Mama Naumia na nitaendelea kuumia., Najua na wewe unaumia lakini ninachokuomba uwe na moyo wa subira nitarudi salama tu wala usihofu?

    “Sawa mwanangu..,ila chunga sana mwanangu..”

    Haraka bila kupoteza mda nikaingia chumbani kwangu na kuvaa suruali yangu ya jinsi,nikajivika tsheti yangu ya kijani iliyokuwa na maandishi makubwa kwa mbele yaliyosomeka 'YOTE MAISHA' chini nikadondoka na raba za rangi ya kijivu,kisha nikachukuwa kijibegi changu cha mgongoni, nikatoka sebuleni na kumuaga mama,

    “Chukuwa hii itakusaidia huko ukipatwa na matatizo itakuepusha nayo”

    Alinivulia cheni yake ya dhahabu kisha akanivalisha,

    “na hii nauli itakusaidia uko uendako”

    Akafungua upindo wa kanga yake na kunipa kiasi cha shilingi elfu sabini,

    Haikuwa na jinsi ilinibidi nichukuwe hivyo vitu kisha nikafanya ishara ya msalaba na kuondoka zangu huku nikimsisitizia Mama afanye juu chini Afande Deus asijue chochote na amdanganye vyovyote,

    Sikuhtaji Mama anisindikize kwa usiku ule kwani nilijua kabisa inaweza kutokea Afande Deus akaja pale usiku kwa kushtukiza,

    Nikiwa nje natoka naelekea stendi ya mabasi japo nikaambulie gari lolote,nikashangaa mwanga mkali wa gari ukinimulika machoni,nikiwa najaribu kujizuia na kulikwepa mara nikashuhudia likisimama mbele yangu..

    “Levina...! Levina...! Levina...!

    Unaenda wapi usiku huu..?

    Hapa huwezi kututoroka hata mara moja,Na tupo hapa nje tangu ulipoletwa na Afande Deus..!”

    Moyo ulilia paaah..! Kisha nikahisi kama mlango unafunguliwa nyumbani nilipotoka,

    “Kwani nyie wakina nani?”

    “Huitaji kujua ila utajua ukifika mahakamani kule mbeya”

    Nikashuhudia Afande mmoja akishuka kwenye gari kisha akanifuata na kunifunga pingu haraka akaniweka kwenye gari aina ya 'Toyota Land Cruiser' nyeupe.,

    Niliumia moyo,nguvu nilikuwa tena sina nilipojaribu kuangalia nyumbani macho yalikutana na Macho ya Mama yangu akiwa amesimama mlangoni huku macho yake yakionesha kuwa na simanzi tele,mara gari ikitoka pale kwa kasi ya ajabu.

    “Mwanaangu....!”

    Ndio neno la mwisho nililoweza kuambulia kwa Mama huku akiniliza na kunisisimua mwili wote kwani alinikumbusha aliniambia hivyo kipindi kile nahukumiwa mahakamani.





    * * * *





    Safari ilianza kuanzia Dar lakini tulipofika Morogoro nilijikuta Nalia sana kutokana na mauaji niliyoyafanya ila nikajipa moyo na tulipofika Iringa haswaa tulipofika kijiji cha 'Liamkena' machozi mengi yalinitoka huku nikilia kwa sauti ya chini chini na kwikwi kwa mbali kila nikikumbuka mateso niliyopata pale kwa wale wanafunzi,pia nilipomua rafiki yangu Pendo bila kukusudia, Nilipigwa na baridi lakini sikuweza kulisikia nadhani hii ni kutokana na kuchanganyikiwa kwanza ni kuwaza itakuwaje kwa Gervas asubuhi pili huko niendako kutoa ushahidi,

    Ilituchukuwa masaa kama kumi na moja mpaka kufika Mbeya,

    Tulifikia mahakamani moja kwa moja kwani kesho yake ndio kesi itasomwa ila nilishangaa kupelekwa pale mahakamani asubuhi asubuhi, Wale askari wakanichukuwa hadi kwenye ofisi nisiyoifahamu pale pale mahakamani, nikiwa nashangaa shangaa huku na kule ghafla nikashangaa nasemesha kwa upande wa nyuma yangu..

    “Hujambo binti..? Za masiku..?”

    Alikuwa ni baba yake na Pendo yule niliyomdanganya kipindi kile kuwa nafanya kazi za ndani na sasa alikuwa pale ofisini…

    “Ba..a..a..a..a..b..a...Pe..ndo...Mi sijamuua mtoto wako…….!!!!!!!!!”





    * * *******





    “Yuko wapi Gervas..?”

    Ndio neno nililoweza kulitoa baada ya kuzinduka pale hospitali huku nikishangaa nimetundikiwa dripu na kujua kuwa kumbe zile zote zilikuwa ni ndoto na hisia za ajabu eti mpaka napelekwa mahamakani, Nikakutana na 'Baba Pendo' na kuanza kumlilia kuwa sijaua,

    “Ooooohhh...! Uuuuuuuuhhh..!

    Mungu waaaaangu..!

    God forbid.....!”

    Nilijikuta nalitoa hilo neno la kiingereza japo sikuwa najua maana yake kwani nilimsikia mara nyingi Afande Deus analitumia anapokabiliwa na matatizo,huku kichomi kikinizidi kuniuma na kupumua haraka zaidi..

    Kucheki pembeni yangu nikamshuhudia Mama akiwa amenishikilia dripu tena akiwa bado machozi yakimlengalenga kuonesha kuwa bado analia huku akinitazama..

    “Mwanangu...! Nisamehe mimi...! Mwanangu...! Najua mimi ndio chanzo cha yote hayo...!

    “Najuta kukuonesha ile barua....!”

    “Hapana Mama kwani mbona mimi mzima tu....!”

    Nilimjibu Mama bila ya kuwa na wasiwasi wowote huku nikijiamini mimi ni mzima tu,

    “Usilie mama...." "Hapana mwanangu....

    Daktari amesema kuwa u...”

    Juhudi za afande Deus kumtoa Gervas katika kituo cha Polisi pale ubungo zilifanikiwa kwani alikuwa akiheshimika na kufahamika hivyo alijitahdi kumtetea Gervas kwa kila njia mpaka akafanikiwa lakini ilikuwa kwa masharti kuwa Gervas hatakiwi kabisa kuönekana Dar es salam na Tanzania kwa ujumla kwani kuonekana kwake kutamletea matatizo makubwa Levina ikiwa ni pamoja na kuwekwa Gerezani tena kwa mara ya pili,hivyo

    Afande Deus alichokifanya ni kumchukuwa Gervas moja kwa moja mpaka kwa wazazi wake kisha kuwapa masharti aliyopewa baada ya kuafikiana wazazi wa Gervas wakahaidi kumtorosha Gervas na kwenda kuendelea masomo yake nje ya nchi,

    Mwanzoni Gervas hakuliafiki kabisa na yote hiyo ni kotakana na kumpenda sana Levina kutoka moyoni,lakini baada ya wazazi wake kumsema sana ikabidi wakubaliane tena kishingo upande kuwa ataondoka tu haina jinsi,

    Walienda nyumbani kwa kina Levina asubuhi asubuhi lakini waliwakosa hivyo Afande Deus akampigia simu Mama Levina na kuambiwa kuwa Levina kalazwa na wapo hospitali ya 'Ocean Road……..'





    * * * *





    ……Kabla Mama hajamalizia kuongea Mara akaingia Afande Deus akiwa na Gervas pamoja na Wazazi wa Gervas.

    Nilijihisi nimepona pale kitandani lakini kila nikitaka kunyanyua mkono niinuke nilishindwa,

    “Nesi...! Nesi..! Nesi....!

    Msaada hapa....! Msaada Nesi...!”

    Ilikuwa ni sauti ya Mama iliyokuwa ikiomba msaada kwa Nesi aje kwangu kunisaidia.

    Nikashuhudia Nesi akija haraka kunihudumia huku akiniinua mgongo..,

    Kisha akamwambia kitu afande Deus na Mama.

    “Huyu mnyanyueni taratibu, kwani upande huu wote wa kushoto haufanyi kazi kabisa..,

    Hapo hapo Halmashauri yangu ya kichwa ikagundua moja kwa moja neno la mwisho alilokuwa anataka kuniambia Mama kabla afande Deus hajaingia ilikuwa ndio hilo kuwa nimepooza upande mmoja.

    Nilijikuta kama mtu asiye na bahati hapa duniani ikabidi nikabiliano nayo,

    “Pole Levina utapona usijali...”

    Sauti ya chinichini tulivu iliyopenyeza kwenye maskio yangu ikitokea kwa Gervas huku akionesha kuwa anahuzuni sana machoni,

    “Nakupenda Gervas....!”

    “Nakupenda pia Levina..!”

    Bila kuonesha woga wowote kutoka kwa wazazi wa Gervas na kwa kujiamini niliweza kuiona mikono ya Gervas ikinipapasa katika mkono wangu mmoja kwa kuteleza nikibaki namtolea jicho la aibu kisha akashika ile dripu huku akiugusa kwa kuupapasa ule mrija wa kupitishia damu na kuanza kutoa mchozi huku akiniangalia kwa huruma, Haraka pale nikashtuka kwa msisimko uliokuwa unaendelea kisha Nikabadilisha mada kwani afande Deus alikuwa akinitolea macho sana...

    “Vipi mmeshayamaliza huko Polisi….?”

    Kabla hajanijibu Gervas nikamwona Nesi ameshawasili kwenye wodi niliyolazwa na kuwafukuza watu lakini sura ya huyu Nesi haikuwa ngeni machoni mwangu ila sikuweza kuwa na kumbukumbu vizuri kutokana na fahamu kutonirudia vizuri na kwa haraka.

    “Jamani wapendwa muda wa kuona wagonjwa umeisha..., Tunawaomba muondoke sasa ni zamu ya daktari kuja kumtibia mgonjwa wenu..”

    Iliongea kwa ukali tena mara mbili mbili ile sauti ya Nesi wa zamu aliokuwa amevalia mavazi rangi ya machungwa.,

    “Levina..,Ugua pole, Jioni tutakuja tena kukutembelea na kukuletea chakula...”

    “Haya...,ahsanteni”

    Nikawajibu wazazi wa Gervas na afande Deus kwa sauti ya upole kwani hata na sauti yangu ilishindwa kabisa kutoka,

    kisha hao wakaondoka huku Mama akiwatoa nje na kuniahidi kuwa kesho asubuhi watakuja tena kunitembelea.



    * * * *





    Mpaka kufika saa Kumi na Mbili jioni hakuna mtu yoyote aliyekuja kututembelea hivyo Mama alinilazimisha kula chakula (mtori) kile cha mchana nilichokuwa nimewekewa katika hotpoti nikala na kupumzika,

    Sikuweza kupata usingizi kabisa,sauti tulivu za ndege kwa mbaaali na mlio wa maji ya bahari niliyokuwa naiskia kutoka nje ya hii hospitali ya 'Ocean Road' ndo kati ya vitu vilivyochochea hisia zangu za mimi kuanza kupata usingizi taaaaratibu,

    Hata hivyo ilipotimia saa saba za usiku usingizi ulikuwa tayari umeshaanza kunipitia huku Mama yangu akiwa amejiegesha upande wa pembeni yangu akiniangalia kwa msaada,

    Kitanda cha pembeni yangu kulikuwa na mgonjwa aliyekuwa analia sana huku akihitaji msaada wa Nesi,Punde yule Nesi aliwasili na ni yule niliyemwona mchana na ndiye aliyewaondoa kwa mara mwisho wakina Gervas hapa hospitalini,

    “Nimeshamkumbuka huyu mshenzi...! Nilishaweka ahadi na kuapa lazima nimteketeze huyu mtu...!”

    Hasira zilinijaa sana kwani sikuamini kuwa huyu Mama atakuwa Nesi?

    “Ina maana siku zote ni Nesi..? Mungu wangu nani aliyempa kazi...?”

    Ni kati ya maswali yaliyonishtua baada ya fahamu kunirudia vizur na kugundua kuwa huyu alikuwa ni yule Mama aliyenifanya mpaka nimekuwa hivi, yule ambaye nilikuwa namuota ovyo kwenye matukio mojawapo lile la kumnyonga na mtandio,na hata juzi nilivyoenda kumpokea Gervas tulipanda naye dalalada japo sikumgundua vizuri mpaka alipovua baibui yake tena kwa mbali ndo nikawa nimemgundua.

    Kila nikimwangalia pembeni yangu ndivyo hasira ilinizidi kuninyemelea akilini mwangu kwakuwa nilikuwa sina nguvu tena upande mmoja kwa kupooza nilijikuta naropoka kwa sauti ya chinichini bila yeye kusikia.

    “Unabahati sana nimepooza...kwani ilikuwa ni safari yako sa hivi...”

    Kisha nikajiegemeza taratibu kutafuta tena usingizi,

    **********



    ITAENDELEA













0 comments:

Post a Comment

Blog